You are on page 1of 3

Mambo Matano Yanayodhoofisha Upinzani Wetu Afrika!

Denis Mpagaze

Kazi ya upinzani si kusifu na kuabudu brother, kazi ya upinzani ni kutia mashaka kwa kila jambo
na kukosoa sana ili mambo yaendelee kuwa mazuri kwa sababu mpika pombe akisifiwa kesho
ataongeza maji, kazi ya upinzani si kuunga mkono juhudi kwa jina la handshake maana siasa
siyo harusi, kazi ya upinzani ni kutengeneza changamoto nyingi zaidi ili wenye mamlaka
waongeze juhudi zaidi, kazi ya upinzani si kuzila na kususia kama mke mwenza, kazi ya
upinzani ni kukomaa hadi kieleweke; upinzani si lele mama brother, upinzani ni kazi ya kufa na
kupona maana ni sawa unakwenda vitani kupigana na mtu mwenye mwenye mkuki na mishale
wewe una rungu tu!

Afrika tumepishana na maana hii ya upinzani, badala yake tumechukulia upinzani kama adui,
mchochezi, mhalifu, mshenzi, mtishia amani na hivyo tunawekeza nguvu nyingi katika
kupambana na wapinzani badala ya kupambana na yale wanayoyapigia kelele. Lakini pia
kusema serikali fulani haijafanya lolote kabisa siyo kazi ya upinzani tunayoijua sisi, hiyo ni kazi
ya ktafutana ubaya. Mpinzani wa kweli atakwambia umefanya tumeona lakini ulichokifanya
hakiendani na matarajio yetu, ongeza bidii au ondoka wenye uwezo wakusaidie! Hapo sijua
kama naeleweka! Sasa haya ndo tunayakosa Afrika! Badala yake upinzani wetu umeharibiwa na
mambo sita.

Moja: Upinzani wetu Afrika umekuwa kimbilio la wakosefu na ondoleo la dhambi!

Walioharibu kwenye vyama vyao hukimbilia vyama vya upinzani na kupokelewa kama
mashujaa walikosa adabu huko walikotoka, kisha wanaondolewa dhambi zao zote na kupewa
nafasi za juu ndani ya vyama bila kuwafanyia hata vetting! Yaani ni sawa na mtoto ameiba
mboga mama anamtandika viboko halafu anakimbilia kwa baba kubembelezwa. Hapo baba
anakosea! Baba mwenye akili atamuongezea viboko. Kitendo cha mgeni kupewa hadhi ya kula
na kunywea madhabahuni na wakati waliotoka jasho kujenga vyama hivyo wakibaki na hadhi
makarai yaliyotumika kujengea nyumba ya mfalme hupelekea makarai yanayojielewa kuasi
vyama vyo na kupelekea siri kwa adui! Hili hufanya upinzani Afrika kukosa heshima na hivyo
kutukanwa hadi na vichaa!
Mbili: Upinzani wetu Afrika umebaki wa ukimwaga mboga namwaga ugali, yaani niguse
ninuke!

Kuna watu wakiishaingia upinzani hawataki kugusa, kukosolewa kupewa onyo pale
wanapokwenda kinyume na taratibu za vyama vyao! Ukimgusa tu anakimbia na kwenda
kuongea shit kuhusu chama. Ohh chama kinatukata mishahara, ooh chama kinatunyanyasa,
mbona hukusema yote hayo kabla hujatimuliwa? Hizi tabia za niguse ninuke zimedhoofisha sana
upinzani hadi kila mtu kudhani ndani ya upinzani wamejaa madikteta! Kwa tabia hizi upinzani
hauwezi kupata heshima ya kusaidini nchi zaidi ya kuvuana nguo na kuchora vyama vya
upinzani kama ndoa za mitala tu. Thamani ya ndoa za mitaala ni wake kumlisha mume wao! Mtu
anaoa kama sehemu ya kitegauchumi. Sasa mnapolalamika kwamba wenyeviti wa vyama
wanawakata mishahara yenu si ndo yale yale ya wake kuwalisha wame zao? Turudisheni
heshima ya vyama vya siasa Afrika kwa manufaa ya maendeleo yetu wenyewe.

Tatu: Upinzani wetu Afrika umekuwa wa kugombania fito kwenda kujenga nyumba moja!

Upinzania wa Afrika unachosha sana. Yaani unakuna nchi moja inavyama vya upinzania hadi 15
vikishindana na chama tawala, kuna wakati Congo ilikuwa na vyama vya upinzani 42, sasa huo
ni upinzani au mbio za mwenge? Hivi watu 42 mnashindanaje na mtu mmoja mkamshinda?
Yaani pamoja na kuambiwa umoja ni nguvu utengano ni udhaifu bado hatuelewi! Naamini
Afrika kila nchi ikiwa na vyama viwili tu, vinavyoshindana lazima vingebadilishana serikali na
maendeleo tungeyaona. Hii ya kila chama kuja na staili yake ni kuvinufaisha vyama tawala.
Akumulikaye mchana, Usiku atakuchoma moto.

Nne: Upinzani Afrika umejengwa katika utamaduni wa asiyekubali kushindwa si mshindani


ndo maana katika chaguzi zote za Afrika kuna matokeo ya kuibiwa kura na kuiba kura tu,
hakuna anayeshindwa. Tabia hii inapoteza maana ya ushindani na mwisho wa siku tunajikuta
katika mabifu ya kunyimana chumvi!

Tano: Upinzani wa Afrika umejengeka katika misingi ya ubinafsi na ukabila. Mwalimu mmoja
aliwaambia wanafunzi wake kila mtu achukue karatasi na aandike anatamani nini maishani
mwake. Kila mtu aliandika anatamani kupata mafanikio binafsi hakuna aliyetamani jamii yake
au rafiki yake kupata mafanikio kuonyesha ubinafsi ni hulka ya mwanadamu! Sasa unapoingia
upinzani sharti ujikane mwenyewe kwa manufaa ya nchi! Mpinzani namfananisha na mchunga
ng’ombe na kiboko mkononi, ng’ombe akienda pembeni anatandikwa kiboko, serikali
ikijichanganya tandika kiboko lakini kumbuka it is very dangerous to be right when your
government is wrong!
Nimalizie kwa kusema upinzani ni ya kushona nguo za bendera za vyama na kuzivaa kwa
mbwembwe mitaani. Paka hawi mzuri kwa sababu ya rangi yake...hapana uzuri wa paka ni
kukamata panya. Upinzani mzuri ni wa kufichua yaliyojificha, kuwafanya wavivu waongeze
mbio kama! Hizi tabia za asubuhi wewe ni ndege, usiku wewe ni bata hazitakiwi katika upinzao
utakakaoikomboa Afrika!

You might also like