You are on page 1of 2

OCTOBER,2019.

UMOJA WA VIJANA SITA V6,

S.L.P.

DAR ES SALAAM.

YAH: KUSIMAMISHWA UANACHAMA KWA KIPINDI CHA MUDA USIOJULIKANA.

Husika na kichwa cha habari hapo juu.

Kulingana na mrejesho wakikao cha dharura kilichofanyika tarehe 29/09/2019, kanisani kuanzia saa
04:57 hadi saa 06:15 ambapo wajumbe wakiongozwa na kamati kuu ilitoa taarifa kuhusu mwenendo
mzima na utendaji kazi wa mjumbe Walter John na taarifa hiyo ilikuwa kama ifuatavyo:

1. Kushidwa kulipa faini ya 50,000/= kwa wakati bila kuwa na taarifa yoyote, ambayo ilikuwa ni
baada ya kusimamishwa katika chama kwa muda wa miezi miwili (2) na Hivyo kikao cha tarehe
06/01/2019 kiliamua mjumbe upigwe faini hiyo.
2. Kwenda nje ya mkataba wa makabidhiano ya mradi wa juice ambapo mpaka sasa bado
unadaiwa kiasi cha shilingi 26,000/= deni la sukari na 25,000/= deni la kuitumia ofisi nusu mwezi.
3. Kushinwa kulinda au kutetea mali za chama. Mfano; simu ya ofisi aina ya BONTEL kupotea
pamoja na laini zake mbili (TIGO NA AIRTEL) ambayo ilikuwa inatumika kwa mawasiliano yote ya
chama.
4. Kufungua mradi wako nje ya chama bila taarifa au kushirikisha wanachama wenzako ambapo ni
kinyume na katiba ya chama.
5. Kushindwa kutizima wajibu kulingana na katiba na sheria za chama

Hivyo basi kamati tendaji kwa niaba ya wanachama wa UMOJA WA VIJANA SITA (V6) kwenye kikao
walichokaa tarehe 06/10/2019 tumeamua kukusimamisha uanachama mjumbe WALTER JOHN kwa
muda usiojulikana mpaka pale uongozi utakapo toa tamko tena. Hivyo basi mjumbe Walter
hatashirikishwa taarifa yoyote ihusuyo chama wala kushiriki kazi yoyote katika mradi wowote wa chama.

Na pindi utakaporudi utatakiwa kulipa madeni yako yote ndani ya mwezi mmoja, kinyume na
makubaliano hayo utakuwa umejifukuzisha uanachama mwenyewe.

Tafadhari rejea viambatanishi kuhusu taarifa ya madeni yakuhusuyo mjumbe Walter na taarifa ya
thamani ya chama kwa sasa tangu ilipoanza tarehe 01/01/2018.

Wako katika ujenzi wa Taifa,

UMOJA WA VIJANA SITA (V6)

MRATIBU KATIBU
DENI LA MJUMBE WALTER JOHN MPAKA KUFIKIA …………………..

ADA…………………………………………………….75,000/=

FAINI………………………………………………….…50,000/=

SUKARI…………………………………………………26,000/=

MAREJESHO YA NUSU MWEZI………….....25,000/=

176,000/=

THAMANI YA CHAMA MPAKA KUFIKIA………………….

Chama kilianza mnamo tarehe 01/01/2018 kwa thamani ya 180,000/= ikiwa ni makusanyo ya kiingilio
cha 30,000/= kila mwanachama.

Ambapo mpaka sasa chama kina miradi miwili amabayo ni Mradi wa SABUNI na Mradi wa JUICE yenye
thamani ya Shilingi 2,129,550/=.

You might also like