You are on page 1of 5

Kanisa la Pentekoste Kijitonyama

Parishi ya Mwananyamala

Kuhesabiwa Haki- Msamaha, kusafishwa/kuondolewa kwa makosa na hatia yangu


yote pamoja na hukumu niliyostahili kwa dhambi nilizozitenda, kwa njia ya Imani
katika Yesu Kristo, aliyechukua adhabu ya dhambi zangu na kulipa gharama kwa
kufa msalabani badala yangu.
Galatia 2:16 “hali tukijua ya kuwa mwanadamu hahesabiwi haki kwa matendo ya
sharia, bali kwa Imani ya Kristo Yesu, sisi tulimwani Kristo YEsu ili tuhesabiwe haki
kwa Imani ya Kristo, wala si kwa matendo ya sharia; maana kwa matendo ya sharia
hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki”
Hii inatuletea WOKOVU
Wokovu – Kuokolewa kutoka katika adhabu ya dhambi nilizozitenda, lakini kubwa
Zaidi ni kutoka katika mzizi wa dhambi, kutoka katika utumwa niliokuwa nao wa
mwili wa dhambi.
Waebrania 7:19, 25 “(Kwa maana ile sharia haikukamilisha neno); na pamoja na
hayo kuliingizwa matumaini yaliyo mazuri Zaidi, ambayo kwa hayo twamkaribia
Mungu… Naye kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa
yeye; maana yu hai sikuzote ili awaombee”
Roho Mtakatifu anakuja kuishi ndani yangu na kutenda kazi ndani yangu,
akiniongoza ili kuishinda dhambi kabla sijaitenda. Nimeokolewa kutoka katika
ulazima wa kutenda dhambi, kwa sababu tu nina mwili ulio dhafu.
Hii inatupeleka kwenye UTAKASO
Utakaso – ni matokeo ya wokovu, kuokolewa, kuokoka. Ni mabadiliko yakutoka
katika asili ya kibinadamu na kuingia au kuwa na asili ya Mungu.
2Petro 1:2-4 “Neema na iwe kwenu na Amani iongezwe katika kumjua Mungu na
Yesu Bwana wetu. Kwa kuwa uweza wa Uungu umetukirimia vitu vyote vipasavyo
uzima na utauwa (utakatifu), kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na
wema wake mwenyewe. Tena kwa hayo ametukirimia ahadi kubwa mno, za
thamani, ili kwamba kwa hizo mpate kuwa washirika wa tabia ya Uungu,
mkiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa”
1Petro 1:15-16, Mathayo 5:48.
Kutakaswa. Huu ni mchakato ambao ninaupitia kwa maisha yangu yote niwapo
hapa duniani, kwa kadri ninavyoendelea kumtii Roho Mtakatifu na neno, na
kuendelea kuyavua matendo ya mwili na kuzaa/vaa tunda la Roho. Galatia 5: 16-25

Tofauti kati ya kuwa na Dhambi (1Yohana 1:8-9) na Kutenda dhambi


(1Yohana 1:10, 2:1,3:6)
1
Kanisa la Pentekoste Kijitonyama
Parishi ya Mwananyamala
Anguko

Dhambi iliingia dunia kupitia kwa Adamu na Eva, ambao waliasi kwa kutomtii
Mungu. Kwa sababu ya Kuasi kwao (kutokutii) Adamu na Eva walianguka na
kuchafuka na dhambi na miili yao, asili yao ya kibinadamu ikafanyika kuwa na
dhambi (Mwanzo 3:1-6, Rumi5:12).
Dhambi ni kitu chochote kinachofanywa au fanyika kinyume na Mungu au mapenzi
yake na sheria zake. Kutenda dhambi ni kuvunja au kutokutii sheria au mapenzi ya
Mungu.

Kuwa na Dhambi – Majaribu/Jaribu/kujaribiwa

Wanadamu wote wanazaliwa wakiwa na asili ya dhambi au dhambi katika miili


yao. Hii ndiyo sababu Yohana anasema Kila mmoja ana dhambi. 1 Yohana 1:8
“Tukisema hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu”
Huwa tunapatwa na hali hii ya kuhisi tuna dhambi tunapojaribiwa Rejea kilio cha
Mtume Paulo kwenye Rumi 7.

Yakobo 1:14-15 inafafanua wazo hili vizuri, “Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa
yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa. Halafu ile tamaaikiisha
kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambiikiisha kukomaa huzaa mauti”

Kumbuka: Kujaribiwa kufanya dhambi si sawa na kufanya dhambi. Hata hivyo


iwapo kwa hiari yetu tunaamua kujiachia na kutii tamaa zetu, dhambi inazaliwa.
Hili hutokea pale ufahamu wetu unapoamua kukubalia na tamaa zetu za dhambi
zilizo katika miili hii ya kibinadamu.

Kutenda dhambi; kuanguka dhambini

Kuna tofauti kubwa sana kati ya kuwa na dhambi ( asili ya dhambi) na kutenda
dhambi. Wale wanaotenda dhambi ni wale walio amua kwa hiari yao kufanya
dhambi - hawako tayari kuacha dhambi.

1 Yohana 3:8 “atendaye dhambi ni wa Ibilisi, kwa kuwa ibilisi hutenda dhambi
tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi
za Ibilisi.”

... na dhambi, ikiisha kukomaa, huzaa mauti

2
Kanisa la Pentekoste Kijitonyama
Parishi ya Mwananyamala
Yakobo 1:15 “halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile
dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti”

Hapa mauti inayotajwa ni mauti ya kiroho, kutengwa na Mungu. Rejea Mfano wa


Tajiri na Lazaro ( Luka 16:19 – 31). Mungu, hawezi kuwa na ushirika na mtu ambaye
hayuko tayari kuacha dhambi.

Tunapoyatoa maisha yetu kwa Yesu, tunaanza kutmbea kama yeye alivyotembea.
Tunakuwa tumejitoa na kuamua kwa hiari kuanza kuyafanya mapenzi ya Mungu na
kuacha kufanya au kuishi maisha ya dhambi. Tunakuwa tumetangaza vita dhidi ya
dhambi na kuanza kuishi maisha mapya ndani ya Yesu (2Korintho 5:17)
Ebrania 4:15 “Kwa kuwa hakuna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika
mambo yetu ya udhaifu; bali alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila
kufanya dhambi”
1 Petro 2:21 “ Kwa sababu ndio mlioitiwa; maana Kristo naye aliteswa kwa ajili
yenu, akawaachia kielelezo, mfuate nyayo zake”

Usitende dhambi!

“Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi. Na kama
mtu akitenda dhambi tunaye mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki”

Kutotenda dhambi ni jambo linalowezekana kabisa kwani limeandikwa kwa uwazi


kabisa katika neno la Mungu.

Ebrania 4:15 “Kwa kuwa hakuna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika
mambo yetu ya udhaifu; bali alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila
kufanya dhambi”
Rumi 8:3-4 “Maana yale yasiyowezekana kwa sheria, kwa vile ilivyokuwa dhaifu
kwa sababu ya mwili, Mungu kwa kumtuma mwananwe mwenyewe katika mfano
wa mwili ulio wa dhambi, na kwa sababu ya dhambi, aliihukumu dhambi katika
mwili; ili maagizo ya torati yatimizwe ndani yetu sisi tusioenenda kwa kufuata
mambo ya mwili, bali mambo ya roho”.
Rumi 12:2 “Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa
upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya
kumpendeza na ukamilifu”.

DHAMBI
Kufanya Dhambi ni kufanya jambo au kitu kisichompendeza Mungu.

3
Kanisa la Pentekoste Kijitonyama
Parishi ya Mwananyamala
Kila mtu anayezaliwa Duniani ni mwenye Dhammbi. Zaburi 51:5.
Maisha ya kawaida bila Yesu ni ya Dhambi kwa sababu yamejaa ubinafsi. Mfano
Mtoto mdogo.
Matokeo ya Dhambi.
1. Ina mchukiza Mungu. Mwanzo 6:5-7.
2. Inaleta hatia. Zaburi 51:1-3.
3. Inaleta utumwa. Rumi 6:17.
4. Upofu wa kiroho. 2kor 4:4.
5. Kifo cha Roho. Efeso 2:1
6. Inaondoa Tumaini. Efeso 2:12.
7. Tito 1:15, Yakobo 5:12.
Maneno kadhaa katika biblia yenye maana ya Dhambi.
Biblia inatumia zaidi ya neno moja kuieleza na kufafanua dhambi.
Kuacha njia au kuwa tofauti na kiwango:
Chattah kutolenga shabaha au kwenda kinyume. Waamuzi 20:16, Zaburi 51:4
Avon Kupinda au kupotosha. Hii ina maana ya kuamua kufanya kwa makusudi lile
ambalo si sahihi. Ayubu 33:27.
Shagah kukosea au kupotoka. Ayubu 19:4. Lawi 4:13.
Parabasis Kuiacha njia iliyonyooka, kuvuka mpaka au kwenda kinyume na mpaka.
Rumi 4:15, Galatia 3:15.
Harmatia kutolenga shabaha. Mathayo 1:21, Rumi 6:23.
Paraptoma Kuchukua hatua isiyo sahihi, kukosea. Kolosai 2:12, Efeso 2:5.
Kuelezea hali, hii ni hali ya jinsi mwanadamu alivyo:
Rasha mwovu. Zaburi 1:6, Zaburi 37:28
Asham kuwa na hatia kukosea. Mwanzo 26:10, Lawi 5 :15-16.
Uasi wa makusudi
Hii ni hali ambyo watu wanadhani wanaweza kuendelea na kufanya mambo yao
bila kumhitaji Mungu.
Persha kumpiga ngumi Mungu. Isaya 1:2, 1Falme 12:19.
Anomia kutokuwa na sheria ukaidi uasi. 2Kor 6:14,IYohana 3:4.
Matendo maouvu au dhamira mbaya.

4
Kanisa la Pentekoste Kijitonyama
Parishi ya Mwananyamala
Marah mkaidi, Zaburi 78:8
Ra’ah kuwa mwovu kufanya tendo mahsusi la uovu. Mwanzo 19:7.
Wazo la dhambi linaambatana na uhalisi na ukweli kwamba kuna kitu fulani
kimepotea, potoshwa au haribiwa.
Dhambi inatutenga na kutuweka mbali na Mungu, inasababisha matatizo kati ya
watu na hatimaye humharibu mtu binafsi.
Wajibu wetu.
Rumi 14:12., Ezekieli 18:20-23,Yohana 3:5-7.
Maswali ya kujadili
1. Kutokuwa na shabaha au kutoweza kulenga shabaha ni maana sahihi ya
Dhambi. Jadili
2. Kwanini Mungu alimpa mwanadamu hiari wakati alifahamu kwamba
mwanadamu atatenda dhambi?
3. Kwanini kujisikia hatia ni tatizo la watu wengi

You might also like