You are on page 1of 2

AKILI ZA KIUME

Kuna sababu juu ya kila kitu chini ya jua.


Kuna sababu nyuma ya uumbaji wa Mungu juu ya uumbaji wake.
Kuna sababu juu ya utofauti wa jinsia uliopo juu yetu.
Utofauti wa jinsia unaenda zaidi ya sababu za kibaiolojia, unaenda mbali zaidi hadi
kwenye sababu za kiutendaji.
Utofauti wetu kijinsia unatafsiri pia utofauti wetu katika utendaji na majukumu.
Hivyo, akili zetu na nia zetu lazima zitengenezwe ili ziendane na nafasi za
kiutendaji na kimajukumu zinazoendana na jinsia zetu.
Katika muktadha wa familia, inafahamika kwamba mwanamume ndiye kichwa cha
mwanamke na kiongozi wa familia au kaya.
1Wakorintho 11:2
Lakini nataka mjue ya kuwa kichwa cha kila mwanamume ni Kristo, na kichwa cha
mwanamke ni mwanamume, na kichwa cha Kristo ni Mungu

Mwanzo 18:17-19
17 BWANA akasema, Je! Nimfiche Abrahamu jambo ambalo ninataka kulifanya, 18 ikiwa
Abrahamu atakuwa taifa kuu, hodari, na katika yeye mataifa yote ya dunia watabarikiwa?
19 Kwa maana nimemchagua ili awaamuru wanawe na vizazi vyake baada yake
wadumishe njia ya BWANA, kwa kuwa wenye haki na kweli, ili BWANA naye
akamtimizie Abrahamu ahadi zake.

Yoshua 24:15
Nanyi kama mkiona ni vibaya kumtumikia BWANA, chagueni hivi leo mtakayemtumikia;
kwamba ni miungu ile ambayo baba zenu waliitumikia ng'ambo ya Mto, au kwamba ni
miungu ya wale Waamori ambao mnakaa katika nchi yao; lakini mimi na nyumba yangu
tutamtumikia BWANA.
Proverbs 17:16
Wana wa wana ndio taji la wazee, Na utukufu wa watoto ni baba zao.
Kama vichwa, na kama viongozi kuna namna fikra zetu na nia zetu zinapaswa kuwa.
Nia na fikra hizi hatuzipati kutoka kwetu wenyewe, bali kutoka kwa Yeye aliye
kichwa kwetu.
Biblia imesema, kichwa cha mwanamume ni Kristo, hivyo tunajifunza kutoka kwa
Kristo namna ya kuenenda kama vichwa.

1Wakorintho 11:1
Mniige mimi kama mimi ninavyomwiga Kristo

Mtume Paulo anawaagiza Wakorintho wamuige yeye kama vile yeye anavyomuiga
Kristo.
Je, ni katika yapi mtume Paulo anamuiga Kristo
Sura ya 10 ya Wakorintho wa kwanza imeleezea hayo.
1Wakorintho 10:23-24; 31-33
23 Vitu vyote ni halali; bali si vitu vyote vifaavyo. Vitu vyote ni halali; bali si vitu vyote
vijengavyo. 24 Mtu asitafute faida yake mwenyewe, bali ya mwenzake.
31 Basi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lolote, fanyeni yote kwa utukufu wa
Mungu. 32 Msiwakoseshe Wayahudi wala Wagiriki wala kanisa la Mungu, 33 vile vile
kama mimi niwapendezavyo watu wote katika mambo yote, nisitake faida yangu
mwenyewe, ila faida yao walio wengi, wapate kuokolewa.
Mojawapo ya jambo ambalo Paulo amelizungumzia kwa msisitizo katika sura hii ni
mtu kufanya mambo kwa ajili ya faida yaw engine.
Hii ndiyo akili iliyokuwa ndani ya Kristo pia, hakufikiria faida yake kwanza, bali
faida ya watu wengine.
Wafilipi 2:3-8; Yohana 15:13
Akili aliyokuwa nayo Kristo ni ya kutanguliza faida yaw engine kwanza.
Hii ni akili ambayo kama wanaume tunapaswa kuibeba, kwa sababu sisi ni
viongozi.
Anakoelekea mwanaume, ndiko familia na jamii inakoelekea
Katika unayoyafanya, je ni kwa kiasi gani umetanguliza faida ya wengine?
Je, unapotaka kuingia kwenye mahusiano ni kwa kiasi gani umetanguliza faida kwa
huyo binti?
Je, unapofanya biashara ni kwa kiasi gani umetanguliza faida kwa wateja wako?
Je katika taasisi unayofanyia kazi, ni kwa kiasi gani umetanguliza faida za taasisi?

Akili za kiume ni akili zinazofikiria faida za watu wengine kabla ya faida binafsi.

You might also like