You are on page 1of 6

KUSIMAMA IMARA KATIKA NYAKATI Luka 18:1-8

NGUMU
KUSIMAMA IMARA
Inamaanisha kuwa madhubuti na kutoteteleka katika
maamuzi yako , mipango yako Imani yako na kila
ambacho Mungu ameweka ndani yako.
Nyakati Ngumu ni pamoja na kufiwa, Kutopatakazi ,
ugonjwa, kupata changamoto mbali mbali za maisha
ambazo kwa namna moja au nyingine huleta msongo wa
mawazo unaopelekea hisia za kukata tamaa au kuacha
umadhubuti wako wote.
SABABU ZINAZOPELEKEA KUKATA TAMAA
1. Kuwa na wasiwasi juu ya jambo uliloombea/Kutaka majibu ya aina Fulani na
kuachia fursa kwa jambo hilo kukupa jakamoyo na msongo wa mawazo : Kuruhusu
Hofu itawale , Kuona hustahili ,hufai , kuhairisha jambo kila wakati Wafilipi 4:6
Msijisumbue kwa neno lolote bali katika kila neno kwa kusali na kuomba ,pamoja na
kushukuru haja zenu na zijulikane kwa bwana
2. Kutokusubiri/Kuchukua hatua mwenyewe na kufanya kulingana na unavyo inafaa
Mithali 5: Mtumanini Bwana kwa moyo wako wote wala usizitegemee akili zako
mwenyewe ,katika njia zako zote mkiri yeye naye atanyoonya mapito yako ,Usiwe
mwenye hekima machoni pako ,mche Bwana ukajiepushe na ouvu
3. Kulaumu Wakati wa Changamoto Marko 4: 38 – Sikitu kwako kwamba
tunaangamia!! na kuona Mungu hafanyi kwa wakati wako
KWANINI USIKATE TAMAA
1. Upendo na Ahadi za Mungu ni hakika na kweli , hujibu kwa wakati sahihi-Hili
ndilo pendo ,si kwamba sisi tulimpenda Mungu bali kwamba yeye alitupenda sisi
akamtuma mwanawe kuwa kipatanisho kwa dhambi zetu 1Yohana 4:10 -Isaya
55:11 Ndivyo litakavyokuwa neon langu,litokalo katika kinywa change
halitanirudia bure bali litatimiza mapenzi yake yangu ,nalo litafanikiwa katika
mambo yale niliyolituma
2. Mjaribu yuko kazini na hasinziii mpaka akuangushe -Mithali 4:16 Maana
hawalali isipokuwa wametenda madhara, huondolewa usingizi ikiwa
hawakumwangusha mtu !!
3. Jua wewe ni nani katika ufalme wa Mungu ( Who are you , ? Wewe ni ukoo
gani , unanini na dhamani yako ni ipi? -Efeso 1:11 na ndani yake sisi nasi
tulifanywa urithi huku tukichaguliwa tangu awali sawa sawa na kusudi lake yeye
ambaye hufanya mambo yote kwa shauri la mapenzi yake
CHA KUFANYA ILI KUSIMAMA IMARA
1. Dhamiria ndani ya moyo wako kutokata tamaa -Luke 18 : 3 – alikuwa akimwendea
endea kadhi maana alidhamiria ndani ya moyo wake kwamba changamoto aliyokuwa
nayo hata ifumbia macho atakaza kwa bidi yote kutafuta haki yake (Usisite site)
2. Dhamiria kuomba bila kukoma : ( Kuwa Kero , make fuss, put tantrums as a toddler )
1. Luka 11:8 Nawaambia ya kwamba ijapokuwa haondoki ampe kwa kuwa ni rafiki yake
,lakini kwa vile asivyoacha kumwomba ,ataondoka na kumpa kadiri ya haja yake !
2. Luka 18:5 Lakini kwa kuwa mjane huyu ananiudhi,nitampatia haki yake asije akainichosha
kwa kunijia daima .
3. Dhamiria Kusubiri ukiwa na Tumaini kuu ! – Kwa Imani dhabiti ukijua yeye Mungu
atafanya –
1. Zaburi 46:10 Acheni Mjue ya kuwa mimi ni Mungu ,nitakuzwa katika mataifa ,nitakuzwa
katika nchi
2. Zaburi 27:10 Umngoje Bwana uwe hodari ,upige moyo konde naam umngoje Bwana
HITIMISHO
Subiri ! Mtafute Bwana maaadamu anapatikani . Mungu hujibu kwa wakati
Jazwa tumaaini Kuu huku ukisubiri maana bwana atatenda , maana amaesema
tutalipwa tusipozimia moyo ! Usizimie Moyo !!

You might also like