You are on page 1of 5

Ilisahihishwa 12/18/2020

Nini cha kufanya ikiwa utapimwa na kugundulika kuwa una COVID-19


Kujitenga ni wakati watu walio na maambukizi ya COVID-19 wanakaa nyumbani na mbali na watu
wengine, hadi wakati wanapopona. Hii ni kwa ajili ya kuzuia kuenea zaidi kwa virusi hivyo.

Kujitenga nyumbani:
Watu wengi walio na homa isiyo kali wanaweza kupata nafuu wakiwa nyumbani. Ingawa hakuna
matibabu mahsusi ya COVID-19, unapaswa kupata mapumziko mengi, kunywa vimiminika kwa
wingi, na kutumia dawa ya kupunguza homa endapo itahitajika.

• Kaa nyumbani, isipokuwa kwa huduma ya matibabu ya dharura au ikiwa unahisi hupo
salama ukiwa nyumbani. Vaa barakoa unapotaka kuondoka nyumbani.
• Piga simu kabla ya kutembelea mtoa huduma ya afya au idara ya dharura na uwaeleze
kuwa unajitenga kwa sababu una COVID-19.
• Kadri inavyowezekana, kaa kwenye chumba mahususi nyumbani kwako na tumia bafu
tofauti.
• Kaa angalau futi sita (au mita mbili) mbali na wengine nyumbani kwako wakati wote.
• Vaa barakoa ikiwa uko kwenye chumba chochote pamoja na watu wengine, isipokuwa
kama una matatizo ya kupumua. Usichangie vifaa vya nyumbani.
• Tafuta mtu mwingine wa kuwatunza wanyama wako kipenzi. Idadi ndogo ya wanyama
kipenzi imeripotiwa kuugua COVID-19. Watu walio na virusi wanapaswa kuepuka kuwa
karibu na wanyama hadi maelezo zaidi yatakapopatikana. Ikiwa unahitaji kumtunza
mnyama wako, vaa barakoa na unawe mikono kabla na baada ya kumtunza.
• Endelea kuwasiliana na wengine kwa kutumia teknolojia ili kuwasiliana na marafiki na
familia.
Tafuta cha kufanya ikiwa huwezi kuepuka kutangamana kwa karibu na mtu unayemtunza au na
mtu anayekutunza.
Angalia mwenendo wa muda kutoka wakati ulipokuwa katika hatari ya kuambukizwa ha di wakati
unapoweza kumaliza karantini ikiwa ulikuwa na dalili au hukuwa na dalili.

Usafishaji na uoshaji wa kila siku:


• Safisha na utumie kemikali kuua viini vya maradhi katika chumba chako na bafu tofauti.
Tafuta mtu mwingine asafishe maeneo mengine ya nyumba yako.
• Osha vyema vifaa vya nyumbani, kama vile vyombo, baada ya kuvitumia.
• Nawa mikono yako mara kwa mara kwa sabuni na maji kwa angalau sekunde 20. Tumia
kitakasa mikono chenye kileo ikiwa sabuni na maji havipatikani.

Wakati wa kupata huduma ya matibabu mara moja:


Ikiwa una matatizo ya kupumua, maumivu ya kifua, kuchanganyikiwa, au mabadiliko ya rangi
kwenye midomo yako, fizi, usoni, karibu na macho, au kucha, tafuta huduma za matibabu mara

Swahili
Ilisahihishwa 12/18/2020

moja. Mweleze mtoa huduma wako wa afya au 9-1-1 kuwa una COVID-19 na unajitenga
nyumbani.

Watu waliotangamana nawe kwa karibu watalazimika kukaa karantini:


Watu ambao walitangamana nawe kwa karibu wakati wa kipindi chako cha kuambukizana
watahitaji kujiweka karantini kwa siku 14 kwa kufuata hatua zilizopo kwenye Nini cha kufanya
ikiwa umetangamana kwa karibu na mtu aliye na COVID-19.

• Kutangamana kwa karibu kunamaanisha kuwa karibu chini ya futi sita (au mita mbili), kwa
jumla ya dakika 15 au zaidi kwa kipindi cha saa 24, na mtu aliye na COVID -19 wakati wa
kipindi chake cha kuambukizana. Kutangamana kwa karibu hakumaanishi kuwa mbali
zaidi ya futi sita katika mazingira yale yale ya ndani kwa muda mfupi, kutembea karibu, au
kwa muda mfupi kuwa kwenye chumba kimoja na mtu.
• Kipindi cha kuambukizana huanza siku mbili kabla ya dalili zako zozote zilipoanza – au
ikiwa hukuwa na dalili zozote, siku mbili kabla ya siku uliyopimwa – na kinaendelea hadi
wakati utakapopona.
• Watu waliotangamana nawe kwa karibu wanalazimika kupimwa haraka
iwezekanavyo. Ikiwa wana dalili za COVID-19, watahitaji kuzungumza na mtoa huduma
wao wa afya kuhusu mahali pa kupimwa. Hawana budi kukaa karantini na kufuata
mwongozo uliotolewa na Idara ya Afya hata kama matokeo ya kipimo chao ni hasi.
• Ikiwa mtu alitangamana kwa karibu na mtu mwingine aliyetangamana nawe kwa karibu,
hawahitaji kufuata mwongozo, isipokuwa kama wataonyesha dalili.

Utakapokuwa umepona na unaweza kumaliza kujitenga nyumbani:


Unaweza kuacha kujitenga nyumbani wakati umepona, jambo ambalo linamaanisha kuwa
umekidhi yafuatayo:
Ikiwa ulikuwa na dalili, unaweza kuondoka nyumbani na kutangamana na wengine baada ya
mambo haya matatu kutokea (isipokuwa kama umeelekezwa vinginevyo na mtoa huduma wako
wa afya):
• hukuwa na homa kwa angalau saa 24 bila kutumia dawa za hupunguza homa na
• dalili zingine zimepata nafuu (kwa mfano, wakati kikohozi chako au upungufu wa pumzi
umepata nafuu) na
• angalau siku 10 zimepita tangu dalili zako zionekane kwa mara ya kwanza.
Ikiwa hukuwa na dalili yoyote, unaweza kuondoka nyumbani na kutangamana na wengine baada
ya:
• Siku 10 zimepita tangu tarehe uliyopimwa na kupatikana na maambukizi (isipokuwa kama
umeelekezwa vinginevyo na mtoa huduma wako wa afya).
Uamuzi wa kuacha kujitenga nyumbani unapaswa kufanywa kwa mashauriano na mtoa huduma
wako wa afya na Idara ya Afya.

Swahili
Ilisahihishwa 12/18/2020

Watu wengi hawahitaji kupimwa ili kubaini ni lini wanaweza kuwa karibu na watu wengine tena.
Hata hivyo, ikiwa mtoa huduma wako wa afya anapendekeza upimwe, atakujulisha ni wakati gani
unaweza kuanza tena kuwa karibu na wengine kulingana na matokeo ya kipimo chako.
Ithibati ya kipimo hasi haipaswi kuhitajika kutoka kwa mwajiri wako ili uweze kurudi kazini. Idara
ya Afya haitoi barua zinazoonyesha kuwa unaweza kurudi kazini. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi
ya kurudi kazini salama.
Pata maelezo zaidi kuhusu nini cha kufanya ikiwa una COVID-19 .

Swahili
Rev. 12/18/2020

What to do if you test positive for COVID-19


Isolation is when people with COVID-19 stay home and away from other people, until they
have recovered. This is to prevent further spread of the virus.

Isolate at home:
Most people with mild illness can recover at home. While there is no specific treatment for COVID -
19, you should get plenty of rest, drink plenty of fluids, and take fever-reducing medication if
needed.

• Stay home, except for urgent medical care or if you feel unsafe at home. Wear a wear a
face mask if you need to leave home.
• Call ahead before visiting a health care provider or emergency department and tell them
you are isolating because you have COVID-19.
• As much as possible, stay in a specific room in your home and use a separate bathroom.
• Stay at least six feet (or two meters) away from others in your home at all times.
• Wear a mask if you’re in any room with other people, unless you have trouble breathing.
Don’t share household items.
• Have someone else care for your pets. A small number of pets have been reported to be
sick with COVID-19. People with the virus should limit contact with animals until more
information is known. If you need to care for your pet, wear a mask and wash your hands
before and after.
• Stay connected with others by using technology to communicate with friends and family.
Find out what to do if you cannot avoid close contact with someone you take care of or with
someone who takes care of you.
See the timeline from when you were exposed to when you can end isolation if you had
symptoms or did not have symptoms.

Daily cleaning and washing:


• Clean and disinfect surfaces in your separate room and bathroom. Have someone else
clean the other areas of your home.
• Thoroughly wash household items, like utensils, after using them.
• Wash your hands often with soap and water for at least 20 seconds. Use alcohol-based
hand sanitizer if soap and water aren’t available.

When to get medical care immediately:


If you have difficulty breathing, chest pain, confusion, or changes in color on your lips, gums, face,
around the eyes, or nails, seek medical care immediately. Tell your health care provider or 9 -1-1
that you have COVID-19 and are isolating at home.

English
Rev. 12/18/2020

Your close contacts will need to quarantine:


People who were in close contact with you during your infectious period will need to quarantine for
14 days by following the steps in What to do if you are a close contact of someone with COVID-19.

• Close contact means being within six feet (or two meters), for a total of 15 minutes or more
over a 24-hour period, of someone with COVID-19 during their infectious period. Close
contact does not mean being more than six feet away in the same indoor environment for
a short period of time, walking by, or briefly being in the same room with someone.
• An infectious period starts two days before your symptoms began – or if you did not have
any symptoms, two days before the day you got tested – and continues until you are
recovered.
• Your close contacts will need to get tested as soon as they can. If they have symptoms of
COVID-19, they’ll need to talk to their health care provider about where to get tested. They
must quarantine and follow guidance provided by the Health Department even if this test is
negative.
• If someone was a close contact of your close contact, they do not need to follow the
guidelines, unless they have symptoms.

When you have recovered and can end home isolation:


You can stop home isolation when you have recovered, which means you have met the following:
If you had symptoms, you can leave home and be with others after these three things have
happened (unless otherwise instructed by your health care provider):
• you have had no fever for at least 24 hours without the use of medicine that reduces
fevers and
• other symptoms have improved (for example, when your cough or shortness of breath have
improved) and
• at least 10 days have passed since your symptoms first appeared.
If you did not have any symptoms, you can leave home and be with others after:
• 10 days have passed since the date you had your positive test (unless otherwise instructed
by your health care provider).
The decision to stop home isolation should be made in consultation with your health care provider
and the Health Department.
Most people do not need a test to determine when they can be around others again. However, if
your health care provider recommends testing, they will let you know when you can resume being
around others based on your test results.
Proof of a negative test should not be required from your employer to return to work. The Health
Department does not provide letters indicating that you can return to work. Find out more about
returning to work safely.
Find out more about what to do if you have COVID-19.

English

You might also like