Professional Documents
Culture Documents
COVID 19 If You Are Diagnosed With COVID 19 Swahili+Eng
COVID 19 If You Are Diagnosed With COVID 19 Swahili+Eng
Kujitenga nyumbani:
Watu wengi walio na homa isiyo kali wanaweza kupata nafuu wakiwa nyumbani. Ingawa hakuna
matibabu mahsusi ya COVID-19, unapaswa kupata mapumziko mengi, kunywa vimiminika kwa
wingi, na kutumia dawa ya kupunguza homa endapo itahitajika.
• Kaa nyumbani, isipokuwa kwa huduma ya matibabu ya dharura au ikiwa unahisi hupo
salama ukiwa nyumbani. Vaa barakoa unapotaka kuondoka nyumbani.
• Piga simu kabla ya kutembelea mtoa huduma ya afya au idara ya dharura na uwaeleze
kuwa unajitenga kwa sababu una COVID-19.
• Kadri inavyowezekana, kaa kwenye chumba mahususi nyumbani kwako na tumia bafu
tofauti.
• Kaa angalau futi sita (au mita mbili) mbali na wengine nyumbani kwako wakati wote.
• Vaa barakoa ikiwa uko kwenye chumba chochote pamoja na watu wengine, isipokuwa
kama una matatizo ya kupumua. Usichangie vifaa vya nyumbani.
• Tafuta mtu mwingine wa kuwatunza wanyama wako kipenzi. Idadi ndogo ya wanyama
kipenzi imeripotiwa kuugua COVID-19. Watu walio na virusi wanapaswa kuepuka kuwa
karibu na wanyama hadi maelezo zaidi yatakapopatikana. Ikiwa unahitaji kumtunza
mnyama wako, vaa barakoa na unawe mikono kabla na baada ya kumtunza.
• Endelea kuwasiliana na wengine kwa kutumia teknolojia ili kuwasiliana na marafiki na
familia.
Tafuta cha kufanya ikiwa huwezi kuepuka kutangamana kwa karibu na mtu unayemtunza au na
mtu anayekutunza.
Angalia mwenendo wa muda kutoka wakati ulipokuwa katika hatari ya kuambukizwa ha di wakati
unapoweza kumaliza karantini ikiwa ulikuwa na dalili au hukuwa na dalili.
Swahili
Ilisahihishwa 12/18/2020
moja. Mweleze mtoa huduma wako wa afya au 9-1-1 kuwa una COVID-19 na unajitenga
nyumbani.
• Kutangamana kwa karibu kunamaanisha kuwa karibu chini ya futi sita (au mita mbili), kwa
jumla ya dakika 15 au zaidi kwa kipindi cha saa 24, na mtu aliye na COVID -19 wakati wa
kipindi chake cha kuambukizana. Kutangamana kwa karibu hakumaanishi kuwa mbali
zaidi ya futi sita katika mazingira yale yale ya ndani kwa muda mfupi, kutembea karibu, au
kwa muda mfupi kuwa kwenye chumba kimoja na mtu.
• Kipindi cha kuambukizana huanza siku mbili kabla ya dalili zako zozote zilipoanza – au
ikiwa hukuwa na dalili zozote, siku mbili kabla ya siku uliyopimwa – na kinaendelea hadi
wakati utakapopona.
• Watu waliotangamana nawe kwa karibu wanalazimika kupimwa haraka
iwezekanavyo. Ikiwa wana dalili za COVID-19, watahitaji kuzungumza na mtoa huduma
wao wa afya kuhusu mahali pa kupimwa. Hawana budi kukaa karantini na kufuata
mwongozo uliotolewa na Idara ya Afya hata kama matokeo ya kipimo chao ni hasi.
• Ikiwa mtu alitangamana kwa karibu na mtu mwingine aliyetangamana nawe kwa karibu,
hawahitaji kufuata mwongozo, isipokuwa kama wataonyesha dalili.
Swahili
Ilisahihishwa 12/18/2020
Watu wengi hawahitaji kupimwa ili kubaini ni lini wanaweza kuwa karibu na watu wengine tena.
Hata hivyo, ikiwa mtoa huduma wako wa afya anapendekeza upimwe, atakujulisha ni wakati gani
unaweza kuanza tena kuwa karibu na wengine kulingana na matokeo ya kipimo chako.
Ithibati ya kipimo hasi haipaswi kuhitajika kutoka kwa mwajiri wako ili uweze kurudi kazini. Idara
ya Afya haitoi barua zinazoonyesha kuwa unaweza kurudi kazini. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi
ya kurudi kazini salama.
Pata maelezo zaidi kuhusu nini cha kufanya ikiwa una COVID-19 .
Swahili
Rev. 12/18/2020
Isolate at home:
Most people with mild illness can recover at home. While there is no specific treatment for COVID -
19, you should get plenty of rest, drink plenty of fluids, and take fever-reducing medication if
needed.
• Stay home, except for urgent medical care or if you feel unsafe at home. Wear a wear a
face mask if you need to leave home.
• Call ahead before visiting a health care provider or emergency department and tell them
you are isolating because you have COVID-19.
• As much as possible, stay in a specific room in your home and use a separate bathroom.
• Stay at least six feet (or two meters) away from others in your home at all times.
• Wear a mask if you’re in any room with other people, unless you have trouble breathing.
Don’t share household items.
• Have someone else care for your pets. A small number of pets have been reported to be
sick with COVID-19. People with the virus should limit contact with animals until more
information is known. If you need to care for your pet, wear a mask and wash your hands
before and after.
• Stay connected with others by using technology to communicate with friends and family.
Find out what to do if you cannot avoid close contact with someone you take care of or with
someone who takes care of you.
See the timeline from when you were exposed to when you can end isolation if you had
symptoms or did not have symptoms.
English
Rev. 12/18/2020
• Close contact means being within six feet (or two meters), for a total of 15 minutes or more
over a 24-hour period, of someone with COVID-19 during their infectious period. Close
contact does not mean being more than six feet away in the same indoor environment for
a short period of time, walking by, or briefly being in the same room with someone.
• An infectious period starts two days before your symptoms began – or if you did not have
any symptoms, two days before the day you got tested – and continues until you are
recovered.
• Your close contacts will need to get tested as soon as they can. If they have symptoms of
COVID-19, they’ll need to talk to their health care provider about where to get tested. They
must quarantine and follow guidance provided by the Health Department even if this test is
negative.
• If someone was a close contact of your close contact, they do not need to follow the
guidelines, unless they have symptoms.
English