You are on page 1of 6

MAKUBALIANO YA MAKABIDHIANO YA BIASHARA YA PIKIPIKI

MAKUBALIANO haya yanafanyika leo tarehe …… Mwezi ………. 2013 kati


ya ndugu SOMOE HEMED MKWACHU wa Dar Es salaam (ambaye katika
mkataba huu atajulikana kama “Mmiliki”) kwa upande mmoja.

NA

RAMADHANI MOHAMED BARUTI wa Dar es Salaam (ambaye katika mkataba


huu atajulikana kama “Mwendeshaji”) kwa upande mwingine.

KWAKUWA Mmiliki ni mmilikaji halali wa PIKIPIKI NA. T526 CPE-BAJAJ-


BOXER 150Cc ambayo imesajiliwa kwa ajili ya biashara ya usafirishaji wa
abiria jijini Dar Es Salaam (“pikipiki”)

KWAKUWA Mmiliki yuko radhi kumkabidhi Mwendeshaji pikipiki kwa


makubaliano na masharti yanayoainishwa hapa chini.

KWA HIYO BASI PANDE ZOTE MBILI WAMEKUBALIANA NA MKATABA


HUU UNASHUHUDIA KAMA IFUATAVYO.

1. Kwa mujibu wa masharti yaliyomo katika makabidhiano haya


Mmiliki anamkabidhi Mwendeshaji pikipiki kwa kipindi cha miezi
kumi na mbili kuanzia tarehe ya utiaji wa saini katika Mkataba huu.

2. Mwendeshaji ataitumia pikipiki katika biashara ya usafirishaji wa


abiria jijini Dar Es Salaam.
3. Mwendeshaji atapaswa kuwakilisha mapato ya shilingi 70,000/= kwa
wiki.

4. Mwendeshaji atawajibika kwa gharama zote za matengenezo ya


pikipiki.

5. Jukumu la usalama wa pikipiki litakuwa juu ya Mwendeshaji.

6. Gharama zote zitakazotokana na uvunjaji wa sheria za usalama


barabarani pamoja na matumizi ya leseni za usafirishaji zitakuwa juu
ya Mwendeshaji.

7. Endapo Mkataba huu utaisha kwa kufikia ukomo wake uliotajwa


katika kifungu cha 1 cha Mkataba huu pikipiki itakuwa mali ya
Mwendeshaji.

8. Endapo, kwa sababu yoyote, Mkataba huu utakoma kabla ya kufika


muda wa ukomo uliotajwa katika kifungu cha 1 cha Mkataba huu
pikipiki itakuwa ni mali ya Mmiliki na Mwendeshaji ataikikabidhi
katika hali nzuri mara moja kwa Mmiliki.

9. Mwendeshaji hataruhusiwa katika kipindi chote cha Mkataba huu


kukabidhi pikipiki kwa dereva mwingine au mtu mwingine awaye
yeyote.

KWA KUTHIBITISHA HAYA YOTE pande zote mbili wameweka sahihi zao
kwa namna na tarehe kama inavyoonyeshwa hapa chini:-

IMEWEKWA SAHIHI na KUTOLEWA


hapa Dar es salaam na FAIZER MOHAMED
YUFUF ambaye ninamfahamu … ________________
Binafsi leo tarehe…Mwezi…………..2013 FAIZER MOHAMED YUSUF
Jina: ………………………………..
Sahihi: ………………………………..
Anuani: ………………………………
Wadhifa: ………………………………

IMEWEKWA SAHIHI na KUTOLEWA


hapa Dar es salaam na Ramadhani Mohamed
Baruti ambaye ametambulishwa ________________
Kwangu na Somoe Mkwachu ambaye
Namfahamu binafsi leo…..Mwezi………..2013 Ramadhani Mohamed
Baruti

Jina: ………………………………..
Sahihi: ………………………………..
Anuani: ………………………………

Umetayarishwa na
MJ Diamond Advocates,

NIC Investment House,

2nd Floor, Wing "A",

P.O. Box 2494,

Dar es Salaam.
MAKUBALIANO YA MAKABIDHIANO YA BIASHARA YA PIKIPIKI

MAKUBALIANO haya yanafanyika leo tarehe …… Mwezi ………. 2013 kati


ya ndugu FAIZER MOHAMED YUSUF wa Dar Es salaam (ambaye katika
mkataba huu atajulikana kama “Mmiliki”) kwa upande mmoja.

NA

OMARI SALUM OMARI wa Dar es Salaam (ambaye katika mkataba huu


atajulikana kama “Mwendeshaji”) kwa upande mwingine.

KWAMBA Mmiliki ni mmiliki halali wa PIKIPIKI NA. T495 CAV-SANLG-


125Cc ambayo imesajiliwa kwa ajili ya biashara ya usafirishaji wa abiria
jijini Dar Es Salaam (“pikipiki”)

KWAMBA Mmiliki yuko radhi kumkabidhi Mwendeshaji pikipiki kwa


makubaliano na masharti yanayoainishwa hapa chini.

KWA HIYO BASI PANDE ZOTE MBILI WAMEKUBALIANA NA MKATABA


HUU UNASHUHUDIA KAMA IFUATAVYO.

1. Kwa mujibu wa masharti yaliyomo katika makabidhiano haya


Mmiliki anamkabidhi Mwendeshaji pikipiki kwa kipindi cha miezi
kumi na mbili kuanzia tarehe ya utiaji wa saini katika Mkataba huu.

2. Mwendeshaji ataitumia pikipiki katika biashara ya usafirishaji wa


abiria jijini Dar Es Salaam.

3. Mwendeshaji atapaswa kuzalisha mapato ya shilingi 120,000/= kwa


wiki.
4. Mwendeshaji atalipwa ujira wa shilingi laki mbili (TZS 200,000/=)
kwa mwezi.

5. Matumizi kwa ajili ya matengenezo ya pikipiki kwa mwezi hayatazidi


Shilingi 100,000/=. Endapo gharama za matengenezo zitazidi kiwango
kilichotajwa hapo juu, Mwendeshaji atawajibika kuzifidia.

6. Jukumu la usalama wa pikipiki litakuwa juu ya Mwendeshaji.

7. Gharama zote zitakazotokana na uvunjwaji wa sheria za usalama


barabarani pamoja na matumizi ya leseni za usafirishaji zitakuwa juu
ya Mwendeshaji.

8. Mwendeshaji hataruhisiwa kuitumia pikipiki zaidi ya saa tano usiku.

9. Wakati wa kuanza Mkataba huu, Mmiliki atajaza mafuta katika tenki


ya pikipiki. Baada ya hapo jukumu la kujaza mafuta katika pikipiki
litakuwa juu ya Mwendeshaji.

10. Mwendeshaji hataruhusiwa katika kipindi chote cha Mkataba


huu kukabidhi pikipiki kwa dereva mwingine au mtu mwingine awaye
yeyote.

11. Mara baada ya kumalizika au kuvunjwa kwa mkataba huu,


Mwendeshaji atalazimika kukabidhi pikipiki kwa Mmiliki ikiwa
imejazwa mafuta na ikiwa katika hali nzuri.

KWA KUTHIBITISHA HAYA YOTE pande zote mbili wameweka sahihi zao
kwa namna na tarehe kama inavyoonyeshwa hapa chini:-

IMEWEKWA SAHIHI na KUTOLEWA


hapa Dar es salaam na FAIZER MOHAMED
YUSUF ambaye ninamfahamu … ________________
Binafsi leo tarehe…Mwezi…………..2013 FAIZER MOHAMED YUSUF

Jina: ………………………………..
Sahihi: ………………………………..
Anuani: ………………………………
Wadhifa: ………………………………

IMEWEKWA SAHIHI na KUTOLEWA


hapa Dar es salaam na OMARI SALUM
OMARI ambaye ametambulishwa … ________________
Kwangu na FAIZER YUSUF ambaye
Namfahamu binafsi leo..Mwezi…………..2013 OMARI SALUM OMARI

Jina: ………………………………..
Sahihi: ………………………………..
Anuani: ………………………………

Umetayarishwa na
MJ Diamond Advocates,

NIC Investment House,

2nd Floor, Wing "A",

P.O. Box 2494,

Dar es Salaam.

You might also like