You are on page 1of 1

SI MTUME WA FUJO (HE IS NOT A PRO PHET OF VIOLENCE)

Ni ahsanul khaliqini, Mtume wetu nabiya,

Rasuli mpewa dini, aweze kutuleteya,

Ndi swadiqul-amini, rehema aloshushiwa,

Sie mtume wa fujo, ni mtume wa Amani.

Ni mtume wa Amani, aliyepewa hidaya

Hidaya njema ya dini, huda kwa walobakiya,

Walobaki duniani, pia wanofuatiya,

Sie mtume wa fujo, ni mtume wa Amani.

Kapigana jihadini, si kwa kutaka ngamiya,

Ni kwa kutetea dini, ya sawa isilamiya,

Watu wasiwe shidani, wakitaka abudiya,

Sie mtume wa fujo, ni mtume wa Amani.

Nimekwenda vitabuni, Siraye kujisomeya,

Lile nililobaini, vita hakushadidiya,

Ni makafiri yakini, waliosababishiya,

Sie mtume wa fujo, ni rasuli wa Amani.

Rahimu kwa waumini, ilahi kamsifiya,

Habagui insani, wote kwake ni sawiya

Bora kwake muumini, si kabila, jinsiya

Sio mtume wa fujo, ni rasuli wa Amani.

You might also like