You are on page 1of 3

3Yohana

Utangulizi
Waraka wa tatu wa Yohana anaandikiwa Gayo, ambaye yawezekana alikuwa na wajibu wa kichungaji au
inawezekana alikuwa kiongozi muhimu katika kanisa. Anaelekezwa kuwasaidia na kuwahudumia wale wanaokuja
kama wajumbe wa Mungu. Pia anapewa onyo kuhusu Deotrefe, juu ya tabia yake ya kukosa ushirikiano. Yohana
anaeleza tarajio lake la kuja na kushughulikia tatizo hili yeye mwenyewe.

Wazo Kuu
Wajibu wa binafsi kuhusu watumishi wa kweli na wa uongo.

Tarehe
Waraka huu uliandikwa 90 B.K.

Mahali
Efeso.

Mgawanyiko
• Salamu (1:1- 4)
• Kutiwa moyo kwa Gayo (1: 5 – 8)
• Kukemewa kwa Deotrefe (1: 9 – 10)
• Kusifiwa kwa Demetrio (1: 11 – 12)
• Hitimisho (1:13 – 15)

1
3Yohana
Wasalimu hao rafiki zetu walioko huko, kila
Salamu mmoja kwa jina lake.
1Mzee,

Kwa Gayo mpenzi, nimpendaye katika


kweli.

Gayo Anasifiwa Kwa Ajili Ya Ukarimu Wake


2Mpenzi, naomba ufanikiwe katika mambo

yote na kuwa na afya yako kama vile roho yako


ifanikiwavyo. 3Ilinifurahisha sana baadhi ya
ndugu walipokuja na kutueleza juu ya uaminifu
wako katika kweli na jinsi unavyoendelea
kuenenda katika hiyo kweli. 4Sina furaha kubwa
kuliko hii, kusikia kwamba watoto wangu
wanaenenda katika kweli.
5Mpenzi, wewe ni mwaminifu kwa yale

unayowatendea ndugu, ingawa wao ni wageni


kwako. 6Wameshuhudia kuhusu upendo wako
mbele ya kanisa. Utafanya vema ukiwasafirisha
kama inavyostahili kwa Mungu. 7Ilikuwa ni kwa
ajili ya hilo Jina waliondoka, bila kukubali
kupokea msaada wo wote kutoka kwa watu
wasioamini. 8Kwa hiyo imetupasa sisi
kuonyesha ukarimu kwa watu kama hao ili
tuweze kutenda kazi pamoja kwa ajili ya kweli.

Deotrefe Na Demetrio
9Nililiandikia kanisa, lakini Deotrefe yeye

apendaye kujifanya wa kwanza, hakubali


mamlaka yetu. 10Hivyo kama nikija,
nitakumbuka matendo yake atendayo,
akitusingizia kwa maneno ya hila. Wala
hatosheki na hayo anayotusingizia,bali pia
hukataa kuwakaribisha ndugu na hata huwazuia
wale walio tayari kufanya hivyo na kuwafukuza
watoke kanisani.
11Mpenzi, usiige lile lililo baya bali lile lililo

jema. Ye yote atendaye mema atoka kwa


Mungu, atendaye mabaya hakumwona Mungu.

Salamu Za Mwisho
12Kila mtu ameshuhudia mema kuhusu

Demetrio, vivyo hivyo hata na hiyo kweli


yenyewe. Sisi pia twashuhudia mema juu yake,
nanyi mwajua kwamba ushuhuda wetu ni kweli.
13Ninayo mambo mengi ya kukuandikia,

lakini sipendi kuandika kwa kalamu na wino.


14Badala yake, nataraji kukuona upesi, nasi

tutaongea pamoja ana kwa ana.

Amani iwe kwako. Rafiki zetu walioko hapa


wanakusalimu.

2
3Yohana

You might also like