You are on page 1of 2

Filemoni

Utangulizi
Waraka huu mfupi uliandikwa na Paulo kutoka Rumi nao umeainishwa na ule wa Waefeso, Wakolosai na
Wafilipi kama mojawapo ya nyaraka zake za gerezani. Ameandikiwa Filemoni, kwa Afia mwanamke mkristo, (
huenda alikuwa mkewe Filemoni ), kwa Arkipo (Kol.4:17) na kwa kanisa lililokuwa likikusanyika nyumbani kwa
Filemoni.
Bila shaka Onesmo alikuwa ametoroka kutoka kwa Filemoni huko Kolosai kwenda Rumi, ambako aliongoka
na kushirikiana na Paulo. Kama mtumwa, alikuwa mali ya Filemoni kisheria. Zaidi ya hayo inawezekana Onesmo
alikuwa anadaiwa vitu fulani fulani na Filemoni.
Kwa barua hii Paulo anamtuma Onesmo kwa Filemoni, akisisitiza kwamba mwenendo wa kikristo ungepaswa
utawale katika uhusiano wao. Paulo anaomba msamaha kwa ajili ya Onesmo, akiomba akubaliwe kama ndugu
mkristo. Ombi hilo limeandikwa kwa maarifa na waraka huu umepangwa kwa namna ambayo ungejenga
kusikilizana, kushawishi nia na kuamsha hisia.

Mwandishi
Mwandishi waraka huu ni Mtume Paulo.

Tarehe
Huu ni mojawapo wa waraka wa gerezani

Mgawanyo
• Salamu (1:1- 3)
• Kuhusika kwa Paulo na upendo (1:4 – 7)
• Paulo kumwombea Onesmo (1:8 – 22)
• Kuagana (1:23 – 25)

1
Filemoni
Salamu nipate faida kwako katika Bwana, uuburudisha
1Paulo, mfungwa wa Kristo Yesu, pamoja moyo wangu katika Kristo. 21Nikiwa na hakika
na Timotheo ndugu yetu, ya utii wako, nakuandikia, nikijua kwamba
utafanya hata zaidi ya yale nisemayo.
Kwa Filemoni rafiki yetu mpendwa na 22Jambo moja zaidi: Niandalie chumba cha

mtenda kazi mwenzetu, 2kwa dada yetu wageni, kwa kuwa nataraji kurudishwa kwenu
mpendwa Afia, kwa Arkipo askari mwenzetu na kama jibu la maombi yenu.
kwa kanisa lile likutanalo nyumbani mwako:
Salamu Za Mwisho Na Dua Ya Kuwatakia
3Neema iwe nanyi na amani itokayo kwa Heri
Mungu Baba yetu na Bwana Yesu Kristo. 23Epafra, aliye mfungwa mwenzangu katika

Kristo Yesu, anakusalimu. 24Vivyo hivyo Marko,


Shukrani Na Maombi Aristarko, Dema na Luka, watenda kazi
4Sikuzote ninamshukuru Mungu wenzangu wanakusalimu.
ninapokukumbuka katika maombi yangu, 5kwa 25Neema ya Bwana Yesu Kristo iwe pamoja

sababu ninasikia juu ya imani yako katika na roho zenu. Amen.


Bwana Yesu na upendo wako kwa watakatifu
wote. 6Naomba utiwe nguvu katika kuishuhudia
imani yako, ili upate kuwa na ufahamu mkamilifu
juu ya kila kitu chema tulicho nacho ndani ya
Kristo. 7Upendo wako umenifurahisha mno na
kunitia moyo, kwa sababu wewe ndugu,
umeiburudisha mioyo ya watakatifu.

Maombi Ya Paulo Ya Kumtetea Onesmo


8Hata hivyo, ingawa katika Kristo ningeweza

kuwa na ujasiri na kukuagiza yale yakupasayo


kutenda, 9lakini ninakuomba kwa upendo, mimi
Paulo, mzee na pia sasa nikiwa mfungwa wa
Kristo Yesu, 10nakuomba kwa ajili ya mwanangu
Onesmo, aliyefanyika mwanangu nilipokuwa
kwenye minyororo. 11Mwanzoni alikuwa hakufai,
lakini sasa anakufaa sana wewe na mimi pia.
12Namtuma kwako, yeye aliye moyo wangu

hasa.13Ningependa nikae naye ili ashike nafasi


yako ya kunisaidia wakati huu nikiwa kifungoni
kwa ajili ya Injili. 14Lakini sikutaka kufanya lo lote
bila idhini yako, ili wema wo wote uufanyao
usiwe wa lazima, bali wa hiari. 15Huenda sababu
ya yeye kutengwa nawe kwa kitambo kidogo ni
ili uwe naye daima. 16Si kama mtumwa, bali
bora kuliko mtumwa, kama ndugu mpendwa.
Yeye ni mpendwa sana kwangu na hata kwako
zaidi, yeye kama mwanadamu na kama ndugu
katika Bwana.
17Hivyo kama unanihesabu mimi kuwa

mshirika wako, mkaribishe kama vile


ungenikaribisha mimi mwenyewe. 18Kama
amekukosea lo lote au kama unamdai cho
chote, nidai mimi. 19Mimi Paulo, ninaandika
waraka huu kwa mkono wangu mwenyewe,
mimi nitalipa. Si kwamba ninakudai hata nafsi
yako mwenyewe. 20Ndugu yangu, natamani

You might also like