You are on page 1of 92

SHUHUDA ZA JASUSI

NDANI YA IDARA

UCHUNGUZI WA MLIPUKO WA BOMU KATIKA


UBALOZI WA MAREKANI DAR ES SALAAM –
TANZANIA

GODWIN CHILEWA
GOSTCH Publishers
Sponsored By Veritas Gospel Ministries
www.veritasgospel.org
Houston, Texas
© 2020 by Godwin Chilewa. All rights reserved.
Haki zote zimehifadhiwa. Hairuhusiwi kunakili, kuiga, kuchapa, kuchapisha sehemu
ya kitabu hiki katika mtandao, au kutumia sehemu yoyote ya kitabu hiki kibiashara
bila kupata ruhusa ya maandishi kutoka kwa mwandishi, kama inavyoagizwa na
sheria ya haki miliki. Hata hivyo inaruhusiwa kutumia nukuu za mafundisho
yaliyomo kuwaelimisha watu wengine neno la mungu, kuwafariji waliopatwa na
matatizo, na kutangaza habari njema za ufalme wa Mungu bila kudai malipo.
Maandiko matakatifu yamenukuliwa kutoka
Biblia takatifu –Swahili SUV na KJV

Published by GOSTCH Publishers


Kwa manunuzi wasiliana nasi
gostchil@gmail.com

© 2020 by Godwin Chilewa. All rights reserved.


No part of this book may be reproduced in any written, electronic, recording, or
photocopying without written permission of the author. The exception would be in
the case of brief quotations embodied in the critical articles or reviews and pages
where permission is specifically granted by the publisher or author.
Although every precaution has been taken to verify the accuracy of the information
contained herein, the author and publisher assume no responsibility for any errors
or omissions. No liability is assumed for damages that may result from the use of
information contained within.

GOSTCH Publishers
ISBN:
TUKUZO
Uinuliwe mwenyezi Mungu wetu mfalme Jehova – El-Shaddai
muumba wa mbingu na nchi, kwa wingi wa neema,
rehema, na Fadhili zako kwetu.
Hakika unastahili kuabudiwa.
YALIYOMO

UTANGULIZI .................................................................................................................... 1
BOMU UBALOZINI ........................................................................................................ 5
IDARA (TISS)…………………………………………………………..…..…43
KIKOSI KAZI (TANBOMB)........................................................................................ 55
FUNUNU ........................................................................................................................... 80
BEGA KWA BEGA NA FBI ....................................... Error! Bookmark not defined.
26 FEDERAL PLAZA NEW YORK ........................ Error! Bookmark not defined.
MBELE YA GAIDI........................................................ Error! Bookmark not defined.
JASUSI................................................................................ Error! Bookmark not defined.
WITO.................................................................................. Error! Bookmark not defined.
USHUHUDA WANGU NI AMINI ......................... Error! Bookmark not defined.
MAREJEO ........................................................................ Error! Bookmark not defined.
FALIHISI .......................................................................... Error! Bookmark not defined.
SHUKRANI

Kwa mzee Benedict Michael Kimwaga, wa Kibamba, Dar es Salaam,


na Gilbert Lameck Chilewa, wa Uzunguni, Dodoma,
Kwa msaada wao mkubwa katika kufanikisha yangu.
Mungu awabariki sawasawa na wingi wa
rehema na fadhili zake.

i
GO DW IN C H IL EWA | ii
SHUHUDA ZA JASUSI

NDANI YA IDARA

UCHUNGUZI WA MLIPUKO WA BOMU KATIKA


UBALOZI WA MAREKANI DAR ES SALAAM –
TANZANIA

GODWIN CHILEWA
GOSTCH Publishers
Sponsored By Veritas Gospel Ministries
www.veritasgospel.org
Houston, Texas
GO DW IN C H IL EWA | iv
UTANGULIZI

_______________

Mimi Godwin Chilewa wa Kinondoni, Dar es Salaam


Nathibitisha kwamba, yote niliyoyaandika katika
Kitabu hiki ni kweli tupu, kwa kadri ya
Utashi na kumbukumbu zangu.
_____________

M
aneno yaliyoandikwa hapo juu kwa kawaida hutumiwa na
mahakama, ofisi za serikali, na taasisi nyingine zinazotoa
huduma za kisheria kama kiapo cha kusema kweli. Kimsingi
mtu anayeapa mbele ya hakimu au afisa yeyote wa serikali
hujifunga kusema ukweli mtupu, pasipo kupindisha maneno. Kama
baadaye ikibainika kuwa maelezo yaliyotolewa na muhusika baada ya
kuapa ni ya uongo, mamlaka husika huweza kuchukua hatua za kisheria
dhidi yake ikiwa pamoja na kumfungulia mashitaka ya jinai, kumnyima
stahiki alizoomba, kumpiga faini, au kumtupa gerezani.
Ingawa kitabu hiki si nyaraka ya serikali inayonifunga kula kiapo
kabla ya kutoa maelezo yangu, na wala mimi siamini katika kuapa
(Yakobo 5:12), nimeona vema kuanza kutoa shuhuda zangu kwa ahadi
hiyo kwa sababu kuu tatu: Kwanza kwa kuwa nataka kusimulia
matendo makuu ambayo Mungu amenitendea katika maisha yangu.
Yamkini kila mtu mwenye imani huyaona matendo makuu ya Mungu
kwa namna yake, na kuyapokea kivyake. Lakini mlolongo wa matukio
na miujiza niliyopitia katika maisha yangu ni ya kipekee, ya
kushangaza, na kusisimua mno. Nina hakika kama matukio hayo
yangetengenezwa filamu, bila shaka ingeweza kushinda tuzo la Oscar
la nchini Marekani.

1
GO DW IN C H IL EWA |2

Kwa sababu ya msisimko huo, si ajabu watu wengi wakapata


mashaka kuhusu uhalisia wake, au wakashindwa kuamini kabisa kuwa
matukio hayo ni ya kweli. Kwa ahadi hiyo hapo juu, nataka kila mtu
asomaye kitabu hiki awe na hakika ya asilimia mia moja, kwamba yote
yaliyoandikwa humu ni ukweli mtupu, na wala si simulizi za kutunga
kama riwaya za Elvis Musiba, hekaya za Abunuwasi, au hadithi za Alif
lela u lela.
Sababu ya pili ni aina ya shuhuda ninazozieleza. Nakuhakikishia
kuwa shuhuda zilizomo kitabuni humu ni za kipekee sana. Ninaamini
zitakufundisha mengi, zitakuburudisha, zitakufunulia siri nyingi
ulizokuwa umefichwa, na kwa imani zitakusogeza karibu zaidi na
uwepo wa Mungu. Tofauti na shuhuda nyingine ulizopata kuzisikia, au
kusoma katika vitabu vingine, humu hakuna mambo ya kwenda
kuzimu, kula meza moja na shetani, au mambo mengine ya kufikirika
ambayo mtu wa kawaida hawezi kuyathibitisha. Shuhuda zilizomo
humu zinahusu maisha halisi ya jasusi aliyeitwa na Mungu
kumtumikia. Hakika Mungu huwahurumia watu wa kila taifa, kabila na
lugha. Huwaita walio wema na waovu; huwaongoza wanyonge katika
vita na kuwashindia, na ikimpendeza huwapa neema na kibali cha
kufanya mambo makuu japokuwa hawastahili. Haya yote Mungu
huyafanya kwa ajili ya utukufu wake, ili akili za waovu zifunguliwe,
wapate kumjua, kumgeukia na kumwabudu.
Binafsi nimemuona Mungu akitembea nami nikiwa jasusi wa
idara ya Usalama wa Taifa ya Tanzania (TISS), kazi niliyoifanya kwa
miaka zaidi ya ishirini. Nimemuona Mungu akipigana vita upande
wangu nikiwa katika mapambano na magaidi wa RENAMO wa
Msumbiji nikishirikiana na makomando wengine wa jeshi la wananchi
wa Tanzania (JWTZ) kutoka kikosi namba 92 Ngerengere (92 KJ).
Tena nimeuona mkono wa Mungu wenye nguvu ukiniinua wakati
nikifanya kazi na idara ya upelelezi (ukachelo) ya Marekani (Federal
Bureau of Investigation) katika kutafuta ufumbuzi wa kesi kubwa
zilizotingisha dunia. Pamoja na kutokuwa na elimu ya kutisha au
mafunzo ya ajabu, Mungu alinitumia sana kupata ufumbuzi wa maswali
yaliyowasumbua wataalam nguli wa ujasusi duniani.
Si hivyo tu, bali pia nimeuona mkono wa Mungu ukiniinua baada
ya kuanguka, kuniokoa kutoka katika makucha ya ibilisi, na kuniongoza
katika njia iliyonyooka ili niweze kumtumikia yeye. Kila
ninapoyatazama mapito haya huziona upya nguvu za Mungu
zinazoendelea kujidhihirisha kwangu kupitia maono na miujiza mingi
3 | SH U HU DA Z A J A SU SI – NDA NI YA IDAR A

katika kila hatua ninayokanyaga.


Sababu ya tatu, nataka msomaji wangu usikie ushuhuda ulio
wazi, na wenye maelezo ya kina kiasi cha kuweza kuufanyia uchunguzi
wa kuthibitisha ukweli wake. Katika maisha yangu nimeshasikia
shuhuda nyingi, na za ajabu sana. Hata hivyo umuhimu wa shuhuda
hizo haukudumu moyoni mwangu kwa muda mrefu kwa sababu kuu
mbili: Kwanza, sikuwa na hakika na maelezo ya watoa shuhuda hizo
kwa sababu ya mkanganyiko wa maelezo yao. Pili sikuwa na njia au
fununu (lead) yoyote ya kuniwezesha kuchunguza shuhuda hizo ili
kuthibitisha ukweli wake, zaidi ya kuzipima katika mizani ya imani.
Bila shaka wewe pia katika maisha yako umeshakutana na hali kama
hiyo, inayokufanya utilie mashaka kila ushuhuda unaousikia. Ni kwa
sababu hiyo katika kitabu hiki nimejitahidi kulielezea kila tukio kwa
kina. Nikitaja mahali lilipotokea, muda - tarehe, mwezi na mwaka
husika. Pamoja na hilo, pia nimejitahidi kadri iwezekanavyo kutaja
majina halisi ya watu waliohusika, nyadhifa zao, na vitu vingine
vinavyoweza kukusaidia kufanya uchunguzi wa tukio hilo (kama
ukipenda) ili kupata habari zaidi, na kuthibitisha ukweli.
Hata hivyo, kwa vile matukio mengi niliyoyaeleza yametokea
wakati nikiwa mtumishi wa idara ya Usalama wa Taifa (TISS)
nimelazimika kutaja majina kamili ya maafisa Usalama wa Taifa wa
wazi (Overty operatives) tu hususan wakurugenzi, maafisa usalama wa
kitengo cha serikali (Government Security Officers), maafisa usalama wa
Taifa wa wilaya (District Security Officers), maafisa usalama wa Taifa wa
mikoa (Regional Security Officers) na maafisa wengine ambao kwa
nyadhifa na majukumu yao wanaruhusiwa kutajwa hadharani pasipo
kuhatarisha usalama au utendaji wao. Sambamba na hilo nimelazimika
kutumia majina bandia na au herufi kama SBM, GBC au X1 kwa
maafisa wa kificho - Coverty operatives (Ghost) ambao kisheria
hawaruhusiwi kutajwa hadharani - Rejea sheria namba 15 ya Idara ya
Usalama wa Taifa ya mwaka 1996.
Ni matumaini yangu kuwa ushuhuda huu utakujenga kiimani,
utakukutia moyo pale ulipokata tamaa, na kukusaidia kuziona nguvu za
Mungu katika maisha yako ya kila siku. Nakuombea sana, Mungu azidi
kukuimarisha kimwili, kiroho na kiakili, ili upate kumwamini na
kumwabudu katika roho na kweli siku zote za maisha yako.
Mungu akubariki
Godwin Chilewa
JASUSI
SURA YA KWANZA

BOMU UBALOZINI

I
likuwa siku ya ijumaa, tarehe 7 August 1998 saa moja na nusu
asubuhi, eneo la Ilala Boma, Dar es salaam. Mimi pamoja na
maafisa wenzangu kumi na wawili tulikuwa tumekusanyika ndani
ya chumba namba 102, kilichokuwa kwenye jengo la ofisi ya mkuu
wa mkoa wa Dar es salaam kwa ajili ya kikao cha dharula. Chumba hiki
kilikuwa mojawapo ya ofisi nyingi za idara ya usalama wa Taifa
zilizozagaa jijini Dar es salaam na mikoa yote ya Tanzania.
Kikao kilikuwa kimeitishwa na mama Inviolata Murusuli, ambaye
wakati huo alikuwa ndiye mkuu wa usalama wa Taifa wilaya (District
Security Officer) Ilala, mkoa wa Dar es salaam. Wakati huo mambo ya
‘Kanda maalum za kipolisi’ yalikuwa hayajaanza. Mama huyu alikuwa
akiheshimika mno kwa uwezo wake mkubwa wa kusimamia
operesheni, kuhamasisha maafisa walio chini yake kufanya kazi kwa
bidii na weledi, na kutoa ushauri bora kwa viongozi wa juu. Sifa hizo
pamoja na nyingine nyingi ndizo zilizofanya akabidhiwe dhamana ya
kusimamia usalama wa wilaya maarufu, na ngumu kuliko zote nchini.
Kama ungekutana na mama Murusuli mitaani wakati ule, bila shaka
usingeamini kuwa ni mmoja wa watu muhimu mno katika idara ya
usalama wa Taifa. Sura yake nzuri, iliyoambatana na urefu wake wa futi
tano inchi nane, na umbo lake la kuvutia, iliwafanya wanaume wengi
kumuona kama mfanya biashara tajiri, muhadhili wa chuo kikuu, au
mwanasiasa maarufu wa taifa kubwa. Mama Murusuli alizitumia vema
sifa hizi katika kutekeleza majukumu yake ya kila siku, akiiwakilisha
vema idara ya usalama wa Taifa kila mahali alipokwenda.

5
GO DW IN C H IL EWA |6

Pamoja nami katika kikao hicho alikuwepo afisa mwandamizi


Coleta Ijagala ambaye mwaka 2006 aliteuliwa kuwa mkuu wa usalama
wa Taifa (DSO) wilaya ya Ubungo, afisa mwandamizi Mary (KIT),
afisa mwandamizi GM tuliyezoea tukimuita kwa jina la utani Morgan,
afisa mwandamizi Bakari Magani aliyefariki kwa shinikizo la damu
mwaka 2005, maafisa Edward (EL), Hamisi (HF) na John Fulela
aliyefariki mwaka 2001 baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Dhumuni la kikao hicho lilikuwa kupashana taarifa za kiitelejensia
(Situation report) kuhusu ya hali ya ulinzi na usalama nchini, na kupanga
mikakati ya kukamilisha malengo ya kazi zilizokuwa zikitukabili.
Mzungumzaji mkuu alikuwa kiongozi wetu, mama Murusuli ambaye
kutokana na wadhifa wake, na kwa mujibu wa chain of command ndiye
aliyekuwa akipokea maagizo kutoka makao makuu kupitia channel
husika, kutupa maelekezo na kusimamia utekelezaji.
Kama ilivyokuwa kawaida yake, siku hiyo mama Murusuli
alitugawia majukumu mapya, kisha akasisitiza umuhimu wa kila afisa
kukamilisha kazi zake kwa wakati, na kwa kuzingatia maadili na miiko
ya idara katika kila hatua ya utendaji kazi. Miaka hiyo ilikuwa mwiko
kwa maafisa wa idara (TISS), Polisi, Jeshi la wananchi (JWTZ) na
watendaji wengine wa serikali kujihusisha moja kwa moja na shughuli
za vyama vya siasa, kuonesha upendeleo kwa chama chochote, na au
kutumia jina la idara kwa manufaa binafsi. Miiko hii ilisaidia sana
kujenga jina nzuri la idara kiasi cha kuifanya iaminiwe na wananchi na
kuwa kimbilio la mwisho la wanyonge.
Ilimchukua mama Murusuli kiasi cha nusu saa hivi kutupa
muhtasali wa madokezo mbalimbali. Alipomaliza alitoa maagizo ya
jumla, kisha akatupa nafasi ya kujadili agizo moja moja, na kuuliza
maswali kwa mambo yaliyokuwa hayaeleweki vema. Binafsi nilikuwa
nikivutiwa sana na vikao vya aina hii, kwani vilinisaidia sana kujua
matukio yaliyokuwa yakiendelea duniani hususan kiuchumi, kisiasa, na
kijamii. Pamoja na hilo, vikao hivi pia vilinisaidia mno kujifunza mbinu
mpya za kukabiliana na changamoto za kazi ya uafisa usalama wa Taifa;
kazi niliyokuwa nikiipenda na kuithamini kuliko kitu kingine chochote,
ukiacha imani yangu kwa Mungu aliyeziumba mbingu na nchi.
Kikao kilichukua muda wa dakika sitini tu. Tulipokaribia kumaliza
mama Murusuli alimkabidhi kila mmoja wetu hati za maagizo ya kazi
aliyotakiwa kuishughulikia kama alivyokuwa ameelekeza. Hati hizo
tulizokuwa tukiziita ‘SIMU’ zilikuwa zikiletwa kwa mfuko maalum
(privet bag) kutoka makao makuu, na au kupokelewa kwa vyombo vya

6
7 | SH U HU DA Z A J A SU SI – NDA NI YA IDAR A

kijasusi zikiwa zimefungwa katika mafumbo (codes). Utaratibu huu ni


wa kawaida na hutumiwa na idara nyingi za kijasusi duniani.
Hati niliyopewa haikuwa mpya, bali muendelezo wa kazi tuliyokuwa
tukiifanya. Tofauti na hati nyingine, hati yangu ilikuwa na maagizo
maalum niliyopaswa kuyafuata ili kufanikisha kazi moja ngumu,
iliyokuwa ikiniumiza kichwa kwa zaidi ya wiki tatu. Katika utekelezaji
wa kazi za idara mara nyingine afisa hulazimika kupata kibali maalum
kutoka kwa mkurugenzi mkuu ili kufanya mambo fulani ambayo kama
akiyafanya bila ruhusa anaweza kujitia matatani.
Wakati tukiinuka ili kila mtu akaendelee na majukumu aliyopewa,
mama Murusuli akatutaka mimi, Morgan na Edward (EL) tubaki ofisini
kwake kwa dakika chache ili atupe maelezo ya ziada. Wenzetu
walipokwishatoka, mama Murusuli akatupa maelekezo ya kazi nyingine
ya dharula tuliyotakiwa kwenda kuifanya. Kwa kifupi, siku hiyo saa
tatu na nusu asubuhi kulikuwa na sherehe kubwa ya kimkoa
iliyopangwa kufanyika katika viwanja vya mnazi mmoja. Ingawa
shughuli hiyo haikuwa na wageni wengi wa kitaifa, ilitarajiwa kuwa na
maelfu ya wahudhuriaji kutoka maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es
salaam, na vitongoji vyake. Kwa sababu hiyo, mama Murusuli aliona
vyema kupeleka maafisa wake kuangalia usalama wa shughuli nzima.
Pamoja na wingi wa kazi zilizokuwa zikitukabili, agizo hilo
halikunishangaza. Mojawapo ya mambo muhimu niliyojifunza katika
mafunzo ya kijeshi ni kuwa tayari muda wote, kwa kazi yoyote na hali
yoyote. Mafunzo hayo yalinikaa vema na kunifanya nisilalamike wala
kuchukia kila nilipoongezewa majukumu. Hivyo baada ya maandalizi
ya hapa na pale mimi na wenzangu Edward (EL) na Morgan tukatoka
kuelekea viwanja vya Mnazi mmoja.
Ilituchukua dakika kumi tu kutoka Ilala Boma hadi kufika Mnazi
mmoja. Mimi na Morgan tulitumia pikipiki yangu aina ya Yamaha DT
125 ya rangi nyeupe na bluu, niliyopewa na idara. Mwenzetu Edward
(EL) alitumia gari ya DSO aina ya Mitsubishi Pajero, iliyokuwa na rangi
ya kijani mgomba. Uwanjani hapo tulikuta maelfu ya wananchi wa
wakiwa wameshajaa tele ingawa mambo yalikuwa hayajaanza.
Shughuli ilianza rasmi saa tatu na nusu kama ilivyokuwa imepangwa.
Vikundi mbalimbali vya ngoma, kwaya, na maigizo vilikuwepo
kutumbuiza hali iliyofanya uwanja kufurika kama tulivyokuwa
tumetarajia. Kila kikundi kilijitahidi kwa kadri ya uwezo wake kutoa
burudani ya hali ya juu kwa lengo la kupata mashabiki wengi zaidi. Kwa
siye wazoefu wa shughuli za aina hii tulijua fika, lengo la burudani hizo

7
GO DW IN C H IL EWA |8

ilikuwa kuwavutia wananchi kufika mahali hapo kwa wingi ili hatimae
waweze kusikiliza hotuba za viongozi zilizojaa maagizo ya utekelezaji
wa sera za chama na serikali yake.
Ilipofika saa tatu na nusu hivi mheshimiwa Yusuf Makamba
(aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam wakati huo) akawasili na
kupokelewa kwa shangwe na vifijo. Wakati huo Mimi na maafisa
wenzangu tulikuwa tumeshalivinjali eneo la uwanja wote kwa muda wa
kutosha, na hatukuona dalili zozote za maandalizi ya vitendo vya kiadui
au uvunjifu wa amani. Hali ilikuwa shwari.
Wakati sherehe zikiendelea ghafla ukasikika mshindo wa mlipuko
mkubwa mno upande wa kaskazini mashariki ya mahali tulipokuwa.
Mshindo huo ulikuwa haufanani kabisa na kishindo cha kupasuka kwa
tairi ya gari, bunduki, au muungurumo wa radi. Ulikuwa mshindo
mkubwa na mzito kuliko muungurumo wa Rocket Propelled Grenade
(RPG), silaha inayotumiwa na wanajeshi kulipua vifaru vya adui vitani.
Ingawa eneo tulilokuwepo lilikuwa na kelele nyingi na za kila aina, kila
mtu aliweza kusikia mlipuko huo kwani ulitikisa kila mahali.
Bila kupoteza muda nikainua mkono wangu wa kushoto kuitazama
saa niliyokuwa nimeivaa. Mishale ya saa hiyo ilinionesha ilikuwa
imetimia saa nne na nusu (juu ya alama) asubuhi. Mojawapo ya mambo
muhimu anayopaswa kufanya afisa usalama wa Taifa anapokuwa
kazini, ni kujua na kutunza muda sahihi wa kila tukio linalotokea.
Kufanya hivyo husaidia sana katika uchunguzi utakaofanywa baadae,
hususan katika kuunganisha nukta, kujumlisha moja na moja kupata
mbili, kupunguza idadi ya watuhumiwa, na hata kutambua sababu na
lengo lililopelekea tukio husika kutokea au kufanywa katika muda huo.
Huku nikiendelea kutafakari mshindo wa mlipuko huo, nikatembea
haraka haraka kumfuata Morgan aliyekuwa upande wa pili wa uwanja
akizungukia mkusanyiko wa watu. Ingawa umati wa watu ulikuwa
mkubwa mno sikuwa na shaka yoyote ya kutomuona kwani nilijua
atakuwa ameshafika kwenye kituo, yaani mahali tulipokubaliana
kukutana kama ikitokea dhalula. Utaratibu huu ambao ni wa kawaida
kwa maafisa wa idara husaidia sana kujipanga upya inapotokea dharula
ya kuwafanya mpotezane.
Wakati nikikaribia kituoni, kwa mbali nikamuona Edward (EL)
akiwa ameshafika. Macho yetu yalipogongana nikanyanyua mkono
wangu wa kushoto na kugusa upande wa kulia wa ncha ya kola ya shati
niliyokuwa nimeivaa kumuashiria kuwa mambo si shwari. Bila kusita
naye akanijibu kwa kugusa sikio lake la kushoto kuashiria kuwa hata

8
9 | SH U HU DA Z A J A SU SI – NDA NI YA IDAR A

yeye anaona hivyo. Sekunde therathini hivi baada ya mimi kuungana na


Edward, tukamuona mzee Morgan naye akija kwa kasi. Sote tulikuwa
katika hali ya tahadhari kubwa kwani hatukujua lililotokea.
“Mmesikia huo mlipuko” Morgan alituuliza kwa sauti kavu kidogo.
“Tumesikia, nadhani ni tanker la mafuta limelipuka” Edward alijibu
kwa sauti kavu.
“Hapana, hilo ni bomu” Nilimkatiza
“Hata mimi nadhani hivyo” Morgan aliniunga mkono.
“Kama ni bomu itakuwa ni hapo Upanga, makao makuu ya JWTZ”
Nilieleza huku sauti yangu ikiwa na mitetemo kidogo.
“Sidhani kama ni MMJ kwa jinsi nilivyousikia huo mlipuko inaelekea
umetokea mbali zaidi” Morgan alinirekebisha. Edward alitaka kusema
neno lakini akakatishwa na sauti ya radio ya mawasiliano aliyokuwa
ameivaa kiunoni na kuifunika kwa koti la suti aliyokuwa ameivaa.
“Tano Eko Nne Tano” (5E45) radio hiyo aina ya Telefunken iliita
kwa mara ya pili.
Katika hali ya kawaida maafisa usalama wa Taifa huwa hatufurahii
kutumia radio za mawasiliano kwa sababu mbalimbali. Kwanza radio
zinazofanana na hizi hutumiwa na maafisa wa polisi, askari wa usalama
barabarani, maaskari wa kikosi cha upelelezi wa makosa ya jinai, na hata
FFU. Kwa hiyo miaka ile mtu yeyote aliyeonekana ameshika radio za
aina hii watu walimuona ni polisi au shushushu, na hivyo kuanza
kumuepuka au kumtangaza vibaya.
Pili radio hizi huwa hazina siri. Zinaweza kukuumbua muda
wowote ule, bila kujali kama uko kwenye mawindo au la! jambo pekee
unaloweza kufanya kuepusha chokochoko ni kuifunga, au kuiacha
kwenye gari. Tatizo ukifanya hivyo halafu ikatokea dharula, ukatafutwa
usipatikane, unaweza kujikuta umezua balaa jingine. Idara humtaka
afisa aweze kupatikana muda wote anapohitajika kikazi, isipokuwa
kama ameagizwa au amelazimika kuwa mzimu (ghost).) tu. Jambo pekee
lililotufanya tuzipende radio hizi, ni uwezo wake mkubwa wa kukamata
mawasiliano, hasa ya jeshi la polisi. Kwa vile miaka hiyo matumizi ya
simu za mkononi yalikuwa aghali, na hayajaenea sana, ilikuwa rahisi
kwa maafisa wa idara (walioruhusiwa) kuingilia mawasiliano ya polisi ili
kujua mambo yanayoendelea, kufuatilia usalama wa misafara ya
viongozi, misako ya majambazi, na mambo mengine nyeti.
“Tano Eko Nne Tano”(5E45) radio hiyo iliita tena kwa sauti ya chini
kama Edward alivyokuwa ameitegesha.

9
GO DW IN C H IL EWA | 10

“Tayari wameanza kuita, huwenda wanafikiri tukio limetokea hapa”


Edward (EL) alieleza kwa sauti ya umakini.
Yamkini sisi sote tulikuwa tumeshaelewa maana ya code iliyokuwa
ikitumika kutuita, kwani kila mmoja wetu alikuwa akitumia radio hizo
inapolazimu. Hii ndiyo sababu iliyofanya idara kuweka codes za jumla,
zilizokuwa zikitumiwa na ofisi nzima, na codes maalum, zilizotumiwa na
watu wachache, katika operesheni maalum tu. Codes hizi zilikuwa
zikibadilika kila mara kadri watumiaji walivyoona inafaa kulinda usiri
sambamba wa kazi husika.
Maneno Tano Eko Nne Tano yaliyosikika kwenye radio ya Edward
(EL) siku hiyo, yalitujulisha kuwa mkuu wetu wa kazi (E45) alikuwa
akimuita kwa dharula Edward (EL) ambaye ni namba 5 ili aseme naye.
Kwa kawaida herufi E hutamkwa Eko ili iweze kusikika kwa ufasaha.
“Chilewa, chukua pikipiki yako, mara moja kimbia makao makuu ya
jeshi ukaangalie kilichotokea. Kama ukikuta hapo hali ni shwari, tafuta
mahali lilipotokea, jua tatizo ni nini, na ulete taarifa kamili”
Morgan, aliyekuwa afisa mwandamizi kwetu (SSO) aliniagiza.
“Timamu” Nilimjibu kwa sauti ya kujiamini.
Bila kupoteza muda nikaifuata pikipiki yangu niliyokuwa
nimeiegesha karibu na mahali tuliposimama na kuirukia, nikaipiga kiki
na kuondoka kwa kasi. Mita chache tu kutoka mahali hapo nikakata
kushoto na kuingia katika barabara kuu, kisha nikaongeza mwendo.
Mbele kidogo nikakata kona kuingia barabara ya Bibi titi Mohammed
iliyokuwa ikiniongoza kuelekea maeneo ya upanga yalikokuwa makao
makuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ). Lakini, kabla sijafika
mahali nilikokuwa nimepanga kukata kona, mbele yangu nikaona
wingu kubwa la moshi mweupe ukipaa angani. Mara moja
nikayakumbuka maneno ya Edward (EL), kwamba mshindo ule
huenda ulisababishwa na mlipuko wa tenka la mafuta. Uzito wa moshi
na rangi yake ulionesha wazi ulikuwa ukitoka katika moto mkubwa
kuliko kawaida. Bila kujishauri nikaongeza mwendo wa pikipiki kufuata
mahali kilipoelekea kuwepo chanzo cha moshi huo.
Ilinichukua muda mfupi tu kutoka mnazi mmoja hadi maktaba
kuu ya Taifa. Eneo hilo lilikuwa halina magari mengi hivyo niliendesha
kwa spidi ya kilometa 90 hivi kwa saa hadi nilipofika kona ya nyumba
ya sanaa. Hapo nikapunguza kidogo kukakata kushoto, kisha
nikaongeza mwendo tena hadi nilipofika Palm Beach Hotel. Nikiwa
maeneo hayo ndipo nilipoweza kuona vyema kuwa moshi ule ulikuwa
ukitoka katika moja ya majengo yaliyokuwa katika makutano ya

10
11 | SH U H U DA ZA J A SU SI – NDA NI YA IDA RA

barabara ya Ali Hassan Mwinyi, na Kinodoni. Hapo pia nikaanza


kusikia sauti za ving’ola vya magali na kengele za tahadhali za majengo
(Alarm) zikilia kwa sauti ya juu bila kukoma. Mchanganyiko wa kelele
hizo ulinifanya nihisi jambo lisilo la kawaida lilikuwa limetokea. Hata
hivyo sikuweza kuhisi ni jambo gani
Nilipofika taa za usalama barabarani zilizopo makutano ya
barabara ya Ocean Road (siku hizi Barack Obama) na Ali Hassan
Mwinyi sikuona sababu ya kupunguza mwendo. Taa zilikuwa
zimeniruhusu hivyo nilipita kwa spidi kali kana kwamba nakimbizwa.
Sikupunguza mwendo hadi makutano ya barabara za Kinondoni, Ali
Hassan Mwinyi, na Kenyata Drive. Hapo ndipo nilipoona moto
mkubwa ukiwaka katika jengo la ubalozi wa Marekani. Mara moja
nikatambua kuwa mlipuko ule ulikuwa umetokea katika ubalozi huo.
Bila kupunguza mwendo nikakata kulia kuelekea Kenyata Drive, halafu
mita chache mbele nikakata kushoto kuelekea mahali ilipokuwa ofisi ya
mkuu wa usalama wa Taifa wa mkoa (RSO) Dar es Salaam. Sekunde
kumi tu baadae nikawa nimefika ofisini hapo.
Ofisi ya RSO Dar es salaam ni mojawapo ya ofisi nilizokuwa
nimezizoea sana. Kila wiki nilikuwa nikienda ofisini hapo mara mbili
au tatu kwa sababu mbalimbali, kutegemea aina ya kazi niliyokuwa
nikifanya. Mzee Zuberi, aliyekuwa mkuu wa usalama wa Taifa mkoa
wa Dar es salaam (RSO) wakati huo, pamoja na maafisa wengine wa
ofisi hiyo walikuwa wakinijua vema. Nami nilikuwa nikizijua vizuri
sana taratibu zote za ofisi hiyo. Kwa ujumla sikuwa mgeni, na wala
sikuhitaji kujitambulisha kwa walinzi.
Pamoja na uzoefu wangu siku hiyo mambo yalikuwa tofauti sana.
Getini nilikuta lango limefungwa na sikuona dalili ya uwepo wa mtu
yeyote. Huku moyo wangu ukidunda kwa kasi nikabonyeza kengele ya
umeme iliyokuwa getini kuita mlinzi. Hakuna aliyejibu. Sekunde
kadhaa zilipita bila mtu yeyote kufungua geti au japo kunisemesha.
Nikiwa sina hakika na yanayoendelea ndani humo, nikapiga honi kwa
nguvu kuita mlinzi. Hazikupita sekunde kumi geti likafunguliwa na
maafisa wawili. Kila mmoja akiwa ameshikilia bunduki aina ya AK47
mikononi mwake, kidole kikiwa katika trigger tayari kufyatua risasi.
Nikashikwa na butwaa!
Maafisa hawa nilikuwa nikiwajua vema, na wao walikuwa
wakinifahamu vilivyo. Kila mmoja wao angeweza kuyataja majina
yangu matatu hata kama akiamshwa kutoka usingizini. Lakini siku hiyo

11
GO DW IN C H IL EWA | 12

waliniangalia kwa macho makali kana kwamba nilikuwa muhaini, au


nimemtukana rais wa nchi hadharani.
“Mimi Chilewa, jamani vipi mmenisahau?” Niliuliza kwa mshangao.
“Unatoka wapi?” mmoja wao aliniuliza kwa ukali.
Kabla sijajibu mwingine akadakia “Tunashambuliwa, ingiza pikipiki
yako ndani haraka” alisema huku akinifungulia geti.
Bila kuhoji nikatia gia pikipiki yangu na kuvuta Mafuta. haraka,
nikaingia ndani ya geti.
Siwezi kukueleza mshituko nilioupata baada ya kuingia ndani ya wigo
wa ofisi hiyo. Madirisha ya jengo la ofisi kuu yalikuwa yamevunjwa na
vioo kusambaa kila mahali. Ukuta wa upande wa kaskazini ulikuwa
umepasuka na kuonesha nyufa nyingi zilizofanya jengo zima
kuonekana kama pagale lililotelekezwa. Pembeni kwenye maegesho
kulikuwa na magari kadhaa yaliyokuwa yamevunjwa vioo na kubondwa
vibaya. Chini palizagaa vipande vya vyuma, makaratasi, matawi ya miti
na vikolokolo vingine vilivyojaa vumbi jeusi. Kwa ujumla eneo zima
lilionekana kama uwanja wa vita. Kitu kichonistaajabisha zaidi, ni
kwamba hapakuwa na dalili ya uwepo wa mtu mwingine yeyote zaidi
ya wale walinzi wawili walionifungulia lango.
“Tunashambuliwa kwa mabomu, kimbia haraka uka take cover”
(kujificha). Alinieleza yule mlinzi aliyeniruhusu kuingia huku
akinionesha kidole mahali pa maficho.
“Ubalozi wa marekani ndiyo ulioshambuliwa, nadhani vilivyokuja huku
ni vipande vya hilo bomu” nilimjibu huku nikiegesha pikipiki yangu
kwenye sehemu ya maegesho iliyokuwa karibu kabisa na lango kuu.
Nikavua kofia ya usalama (helmet) niliyokuwa nimeivaa kichwani na
kuipachika kwenye kioo (side mirror) ya upande wa kulia wa pikipiki.
“Maafisa wengine wako wapi? Niliuliza kwa mshangao huku
nikizungusha macho huku na kule.
“Wako mahali salama” mlinzi huyo alinijibu kwa sauti kavu na ya
mkato. Inaelekea walikuwa hawaniamini kabisa, kwani ujio wangu
ulikuwa haukutarajiwa.
Sikushangazwa na hali waliyokuwa nayo. Hawakujua mashambulizi
yametoka wapi, hivyo walikuwa wakijipanga kwa mapambano.
Tulipokuwa katika mafunzo ya ujasusi tulikuwa tukikumbushwa kila
wakati suala la kutomwamini mtu yeyote anayejitokeza ghafla baada ya
mashambulizi makubwa. Makamanda wetu walituonya tena na tena
kutomwamini mtu huyo hata kama ni baba yako mzazi. Sababu ilikuwa
wazi “Huwezi kujua adui atamtumia nani kuipenya ngome yenu”

12
13 | SH U H U DA ZA J A SU SI – NDA NI YA IDA RA

“Nakwenda ubalozi wa Marekani kuona kinachoendelea”


Niliwaambia walinzi hao huku nikianza kutembea kuelekea lango kuu.
“Chilewa, utakuwa salama? Mmoja wao aliniuliza kwa wasiwasi.
“Tuombeane” Nilijibu huku nikifungua geti na kuanza kutimua mbio
kuelekea eneo la tukio.

2
Ubalozi wa Marekani ulikuwa eneo la Kinondoni, nyumba namba
36 Laibon, iliyokuwa kwenye makutano ya barabara ya Ali Hassan
Mwinyi na mtaa wa Laibon. Ilinichukua dakika chache tu kutoka ofisi
ya RSO hadi kufika ubalozini hapo. Mbele ya jengo niliwakuta
wanajeshi wa Marekani (Marines) waliovaa mavazi ya kivita (combat gear)
huku bunduki za kivita aina ya M4 Carbine na Machine gun zikiwa
mikononi mwao, tayari kwa mapambano. Moto mkubwa ulikuwa
ukiwaka upande wa mashariki ya jengo, karibu kabisa na mahali
ilipokuwa ofisi ya mapokezi. Mbele kidogo, kiasi cha mita kumi na
tano hivi kutoka lango kuu kulikuwa na mioto mingine mikubwa
iliyokuwa ukiendelea kuteketeza magari yaliyokuwa yameegeshwa
katika eneo hilo. Upande wa kusini, kwenye ukuta wa wigo unaotazama
barabara ya Ali Hassan Mwinyi, kulikuwa na watu kadhaa waliokuwa
wakijitahidi kupanda ukuta huo ili waruke nje, kujinusulu na dhahama
iliyokuwa ikiendelea katika jengo hilo. Baadhi ya watu waliweza
kupanda na kusalimika lakini wengine hawakuweza kufanya hivyo
kutokana na majeraha waliyokuwa nayo, na au mshituko waliopata
kutokana na mlipuko mkubwa wa bomu. Wakati huo watumishi wa
balozi nyingine na wananchi wa maeneo ya jirani walikuwa wameanza
kumiminika katika eneo hilo kuangalia nini kilichokuwa kimetokea na
kutoa msaada kwa majeruhi.
Huku moyo ukinidunda nilitembea kwa kasi kumfuata kiongozi wa
wanajeshi (Marines) aliyekuwa upande niliotokea. Aliponiona
nikimfuata akashika vizuri bunduki yake na kunifuata huku akiwa
amenielekezea mtutu. Sikushituka, kwani nilikuwa nikitegemea kitu
kama hicho kutokea. Ukiwa umepitia mafunzo ya kijeshi, na au
kushiriki katika mapambano ya kivita unaweza kuhisi hatua anazoweza
kuchukua mpiganaji katika hali ya hatari kama iliyokuwapo wakati huo;
Kwa hiyo nilikuwa nimejiandaa ki mwili na kisaikolojia.
Nilipomkaribia, kiasi cha umbali wa mita kumi hivi nikanyoosha
mkono wangu wa kulia kumuonesha kitambulisho changu “Tanzania
government officer” nilimwambia kwa kujiamini huku nikimpa nafasi ya

13
GO DW IN C H IL EWA | 14

kutazama sehemu ya mbele ya kitambulisho hicho inayoonesha ngao


ya jamhuri ya muungano wa Tanzania, kisha nikakigeuza upande wa
pili kumuonesha picha yangu iliyopigwa muhuri wa ofisi ya rais.
“Thank you for coming sir, you are the first Tanzanian government officer here,
come with me” Aliniambia kwa uchangamfu ingawa sote tulikuwa katika
mazingira magumu. Bila kusita nikamfuata huku nikiwa sina hakika ya
mambo yatakayofuata. Pamoja na uzoefu wangu wa miaka kumi katika
idara, hii ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kushughulika na maafisa wa
jeshi la Marekani (Marines) baada ya kushambuliwa; ukizingatia kuwa
tukio hilo ndilo lilikuwa la kwanza katika historia ya Tanzania.
Kwa ujasili mkubwa nilifuatana na afisa huyo mpaka mahali
lilipotokea tukio (ground zero). Moto mkubwa ulikuwa ukiendelea
kuwaka kwa nguvu, ukiunguruma kwa utisho kadri ulivyoendelea
kuteketeza magari na vitu vingine vya thamani. Wafanyakazi wa kikosi
cha zimamoto wakiwa na gari moja kubwa la rangi ya njano walikuwa
wakijitahidi kwa nguvu zote kuukabili moto huo bila mafanikio.
Kengele za tahadhari (alarm) zilizokuwa katika jengo la ubalozi
ziliendelea kupiga kelele mfululizo, huku magari yaliyokuwa yakiteketea
kwa moto yakiendelea kuomboleza kwa miluzi na mipasuko ya matairi.
Ukichanganya na sauti za vilio vya majeruhi, na kelele za watu
waliokuwa wakihimizana kutoa msaada, vyote hivi vilifanya mahali
hapo kuonekana kama uwanja wa vita kule nchini Syria au Kosovo.
Lakini pamoja na vitisho hivyo wasamalia wema waliendelea
kumiminika kutoa msaada kwa majeruhi.
Wengi wa majeruhi waliotolewa walikuwa wameumia vibaya, na
wengine kupoteza fahamu kabisa. Nguo zao zilikuwa hazitamaniki
kutokana na damu, moshi, na uchafu mwingine uliotokana na vumbi
la kifusi. Hata hivyo macho yangu yalivutwa zaidi na mama mmoja
aliyetolewa akiwa hoi. Mama huyo alikuwa na tumbo kubwa hali
iliyoonesha kuwa alikuwa mjamzito wa miezi sita au saba. Nguo zake
zilikuwa zimelowa damu chapachapa. Alikuwa na fahamu, lakini hali
yake ki mwili na kisaikolojia ilikuwa mbaya mno. Binafsi nilihofia zaidi
usalama mimba aliyokuwanayo kwani ingeweza kutoka au angeweza
kujifungua wakati wowote ule. Yamkini sikuwa na hakika kama mtoto
aliyembeba tumboni mwake alikuwa salama. Kule kumwangalia tu,
kulinifanya mwili wote usisimke na nywele zangu kusimama wima. Bila
kupoteza muda tulitafuta gari ya kumkimbiza hospitali ya Agakhan
iliyoko eneo la Upanga.. Baadae niliambiwa mama huyo anaitwa Justina
Mdobilu, na ni mfanyakazi (translator) wa ubalozi huo.

14
15 | SH U H U DA ZA J A SU SI – NDA NI YA IDA RA

Tukiwa katika eneo hilo, afisa wa jeshi (Marines) aliyenipokea


alinieleza kuwa majira ya saa nne na nusu asubuhi, gari lililobeba bomu
liliingia ubalozini hapo na kulipua sehemu ya mbele ya ubalozi na
kusababisha madhara niliyokuwa nikiyaona. Mpaka wakati huo watu
wanne walikuwa wamethibitishwa kupoteza maisha yao, na wengine
walikuwa katika hali mbaya, hivyo idadi ya vifo ingeweza kuongezeka.
“Kwa sasa tumeelekeza nguvu zote katika kufanya uokoaji, lakini
hali itakapotulia kidogo nifuate nitakupeleka kwa maafisa watakaokupa
taarifa zote unazohitaji”
Alihitimisha maelezo yake aliyonipa kwa lugha ya kiingereza.
“Nashukuru sana, labda nikuulize swali moja tu la ziada”
Nilimwambia kwa kujiamini, nikijua kuwa hakuna muda wa
mazungumzo. “Kuna fununu yoyote kuhusu mtu, au kikundi kilicho
husika na tukio hili? Nilimuuliza nikiwa sina hakika kama analo jibu
sahihi kwani ilikuwa mapema mno.
“ It looks like Alqaida” Aliniambia akionesha kuwa na uhakika wa
asilimia mia moja na analoniambia.
“Tunajua ni wao kwa sababu yamefanyika matukio mawili kwa
wakati mmoja. Wamelipua hapa, na pia ubalozi wetu wa Nairobi nchini
Kenya, na pia kuna wasiwasi wanaweza kufanya hivyo katika ubalozi
wetu wa Kampala, Uganda. Nadhani Alqaida ndilo kundi pekee lenye
nguvu, na mtandao wa kuweza kufanya hivyo” Alinieleza.
“Vilevile kundi hili (Alqaida) limekuwa likiisumbua nchi yetu (USA)
kwa muda mrefu. Miaka michache iliyopita wafuasi wake walijaribu
kulipua jengo la biashara (World Trade Center) jijini New York na
sehemu nyinginezo. Kuna uwezekano mkubwa ni wao, ingawa bado
hatujathibitisha”. Alimalizia.
Wakati huo magari ya polisi kutoka kituo cha Oysterbay yakawa
yamefika. Aliyekuwa mkuu wa kituo hicho SSP Abdallah Msika,
akifuatana na mkaguzi wa Polisi (inspector) Goyayi na maafisa wengine
wakateremka na kuungana nasi kuokoa majeruhi na kuimarisha ulinzi.
Baada ya kuangalia hali ilivyokuwa, na kufanya tathmini ya haraka, SSP
Abdallah Msika aliamua kuagiza askari wa ziada kutoka kikosi cha
kutuliza ghasia (FFU) kuja kuimarisha ulinzi katika eneo la tukio.
Uamuzi huu ulikuwa wa maana sana, kwani ulisaidia kulinda usalama
wa ubalozi, mali zake, na watu waliokuwepo. Uamuzi huo pia ulisaidia
sana kulinda ushahidi katika eneo la tukio (contamination of the crime scene).
Dakika chache baadae aliyekuwa mkuu wa jeshi la polisi mkoa wa Dar

15
GO DW IN C H IL EWA | 16

es salaam kamanda Alfred Gewe akawasili, akifuatiwa na gari la kikosi


cha zima moto kutoka bandarini.
Kuwasili kwa askari hawa kulinipa ujasili mkubwa zaidi wa kufanya
kazi yangu bila wasiwasi. Katika hali ya kawaida eneo la ubalozi ni mali
ya nchi husika, na hulindwa na sheria za kimataifa. Kwa sababu hiyo ni
rahisi sana kwa mtumishi wa serikali au chombo cha dola kujikuta
umevuka mipaka, na au kuvunja sheria za kimataifa bila kujua. Hali
kama hiyo ikitokea unaweza kujikuta ukipoteza kazi yako, na au
kuchukuliwa hatua nyingine kubwa zaidi za kisheria. Tahadhali hii
nilikuwa nayo kichwani tangu nilipotia mguu wangu ubalozini hapo.
Kitu pekee kilichonipa wasiwasi, ni uwezekano wa kutokea kwa
shambulio la pili. Nilipokuwa katika mafunzo ya ujasusi nilifundishwa
kuwa magaidi hupenda kufanya hivyo kwa lengo la kusababisha
madhara makubwa, yenye kuwatia hofu kuu wananchi ili kufikisha
ujumbe wanaoutaka kwa jamii husika. Hivyo kila wanapofanya tukio
moja linalopelekea watu kukusanyika, kwao huwa ni fursa ya kufanya
shambulio lingine kubwa zaidi. Namshukuru Mungu kwamba mawazo
hayo hayakunitia hofu na kunifanya niondoke mahali hapo; badala yake
niiliendelea kushirikiana na maafisa wa polisi, pamoja na wananchi
wengine kuwasaidia majeruhi, huku nikiendelea kukusanya taarifa za
kiusalama kwa kadri nilivyoweza.
Idadi ya majeruhi ilikuwa kubwa kuliko tulivyodhani hivyo
ilitulazimu kufanya mambo kwa haraka na umakini mkubwa. Kila
majeruhi aliyetolewa katika jengo tulichukua jina lake kamili, tarehe
yake ya kuzaliwa, kabila, dini, anuani ya makazi yake, jina la kiongozi
wa serikali ya mtaa anaoishi, sehemu anakofanya kazi, au shule
anayosoma kama ni mwanafunzi, na taarifa nyingine muhimu
tulizoona zitasaidia kumpata muhusika kama akihitajika kusaidia
upelelezi, au kuwapata ndugu zake kama akipoteza maisha.
Ili kupata fununu ya tukio lilivyotokea SSP Msika aliwaagiza askari
wa upelelezi kuchukua maelezo ya wafanyakazi, na watu wengine
waliokuwepo katika eneo hilo wakati wa tukio. Hata hivyo, kwa sababu
ya mshituko majeruhi hawakuweza kueleza kwa ufasaha mambo
waliyoyaona, na wengine walieleza mambo yaliyo kinyume kabisa na
hali ilivyokuwa. Kwa ujumla maafisa wa polisi walijitahidi kufanya kazi
kwa weledi mno ingawa hali ilikuwa ya kutisha sana.
Kwangu huo ulikuwa ni wakati mzuri wa kukusanya taarifa za
kiitelejensia. Wakati polisi wakiendelea kuhoji watu waliodai
kushuhudia tukio, mimi niliendesha na zoezi la kuwatambua wale

16
17 | SH U H U DA ZA J A SU SI – NDA NI YA IDA RA

walioelekea kuwa na taarifa za maana, au wanaoweza kutumiwa na


idara kwa namna moja au nyingine kupata taarifa zaidi. Orodha ya watu
hao na maelezo ya namna ya kuwapata niliihifadhi pembeni kwa ajili ya
matumizi ya idara tu kulingana na taratibu zetu.
Dakika ishirini hivi zilikuwa zimeshapita tangu nilipofika ubalozini
hapo. Sikuwa nimefanya mambo makubwa, lakini moyo wangu
ulikuwa umeridhika sana kwa yale niliyokuwa nimeyafanya. Katika
muda huo nilikuwa nimeshiriki kikamilifu katika shughuli ya uokoaji
wa majeruhi, na nimekusanya taarifa za awali ambazo hakuna afisa
mwingine yeyote (wa TISS) alikuwa nazo. Ingawa taarifa zenyewe
zilikuwa chache kulingana na uzito wa tukio, nilijisikia vizuri mno
kwani nilizipata kutoka kwenye vyanzo vya uhakika. Zaidi ya yote
nilikuwa nimefunguliwa mlango wa kupata taarifa zaidi kutoka kwa
maafisa wa ubalozi na wanajeshi (marines) wa Marekani.
Wakati nikitafakari hatua ya pili ninayopaswa kuchukua, nikasikia
mtu akiniita kwa sauti nzito “Chilewa, hujambo?”
Nikageuka haraka ili nimuone mtu huyo aliyeweza kunitambua
katika mvurugano mkubwa namna ile. Nilipomuona sikuyaamini
macho yangu. Mwili ulinisisimka na moyo wangu uliongeza kasi ya
mapigo yake. Alikuwa mzee Evodius Walingozi, mkurugenzi wa
idara ya usalama wa Taifa anayeshughulika na operesheni za ndani
(Director of Internal Operations), wenyewe tulizoea kumuita DOI
“ Shikamoo mkuu” Nilimwamkia kwa heshima.
“Marahaba Chilewa, umefika muda gani?Aliniuliza kwa shauku.
Bila kusita nikamueleza kwa kifupi yaliyotokea tangu tuliposikia
mlipuko, jinsi nilivyofanikiwa kufika hapa, taarifa nilizokwisha
zikusanya, na malengo niliyokusudia kuyafanya muda mfupi ujao.
“Kazi nzuri sana Chilewa. Nimefika hapa kitambo, nikawa naangalia
hali ilivyo, lakini mpaka sasa sijamuona afisa mwingine ninayemjua. Hii
ina maana tuliopo ni mimi na wewe tu. Kwa hiyo endelea na kazi kwa
saa moja na robo zaidi. Baada ya hapo tukutane pale kwenye ile petrol
station iliyopo pale juu, ukiwa unaelekea mbuyuni (kanisa la mtakatifu
Peter). Hapo ndipo nilipoacha gari langu. Hakikisha saa sita na nusu
uko pale” Alisema kwa msisitizo huku akiwa amenikazia macho.
“Sawa mkuu, nitafanya hivyo” Nilijibu kwa heshima huku
nikijitahidi kuonesha ukakamavu.
Bila kuongeza neno mzee Walingozi akageuka na kutokomea
kwenye umati wa watu waliokuwepo. Nami haraka nikajichanganya
kuendelea na kazi kwa ari mpya, na nguvu mpya zaidi, nikijua uwepo

17
GO DW IN C H IL EWA | 18

wangu ubalozini hapo ulikuwa umepata kibali cha DOI, kiongozi wa


juu kabisa katika masuala yahusuyo operesheni za ndani katika TISS.
Kufikia wakati huo maafisa wa polisi waliokuwepo walikuwa
wameshajua mimi ni mwenzao, hivyo nilikuwa na nafasi nzuri ya
kuchukua maelezo ya watu waliokuwa wakiwahoji bila kubugudhiwa.
Pamoja na hayo SSP Msika aliwaagiza maaskari wake kunipatia nakala
za majina ya watu wote waliowahoji, majeruhi waliopelekwa hospitali,
na taarifa nyingine nilizozihitaji kutoka kwao. Kwa ujumla kamanda
huyu alinisaidia sana kupata taarifa muhimu bila kutumia nguvu ya
ziada, au kuulizwaulizwa maswali na askari. Kama SSP Msika angekuwa
afisa wa polisi asiye na weledi, bila shaka kazi yangu ingekuwa ngumu.
Jukumu la kuhoji watu walioshuhudia tukio lilikuwa muhimu sana;
lakini halikutufanya tuzembee katika shughuli ya uokoaji. Kila majeruhi
aliyetolewa jengoni alifanyiwa tathmini ya haraka kujua hali yake ya
kiafya, kisha tukamuuliza maswali machache ya kutusaidia mahali pa
kuanzia uchunguzi, baada ya hapo tukamuingiza katika gari
kumkimbiza hospitali. Utaratibu huu ulihusu majeruhi wote, hivyo hata
wale walioonekana kutokuwa na majeraha makubwa bado tulisisitiza
waende hospitali kufanyiwa uchunguzi wa kitaalam. Kwa vile
hatukuwa na magari rasmi ya wagonjwa (ambulance) kiasi cha
kutosheleza mahitaji, maafisa wa polisi walisimamisha magari binafsi
yaliyokuwa yakipita barabarani, na kuwaomba madereva kusaidia
kuwakimbiza majeruhi hospitali za Muhimbili na Agakhan. Ili
kurahisisha mapokezi ya majeruhi hao kwenye hospitali husika,
kamanda Msika alihakikisha kila msafara unaoondoka ubalozini hapo
unafuatana na askari polisi mmoja.
Baadae tulifahamu kuwa, wengi wa majeruhi walikuwa watu
waliokuwa wamekuja ubalozini hapo kuomba viza ya Marekani,
maafisa na watumishi wa ubalozi huo, wafanyakazi wa kampuni ya
ulinzi ya Ultimate Security iliyokuwa na dhamana ya kulinda ubalozi
huo, kina mama lishe waliokuwa wakiuza vyakula mbele ya jengo
lililolipuliwa, wakazi wa nyumba na maofisi ya jirani, na wapita njia
waliokuwa eneo hilo wakati mlipuko ulipotokea. Baadhi ya watu hawa
walikuwa wamejeruhiwa vibaya kiasi cha kutoweza kujitambua; lakini
wengine hawakuwa hata na mchubuko ingawa walikuwa hoi
kisaikolojia kutokana na mshituko mkubwa walioupata; aidha kwa
mshindo wa mlipuko, au ile hali ya kunusulika kifo. Ni wachache tu
kati yao waliokuwa na ujasili wa kutoa maelezo mara moja, na kwa

18
19 | SH U H U DA ZA J A SU SI – NDA NI YA IDA RA

usahihi. Hawa tuliwatengenezea utaratibu maalum wa kuwahoji wakati


huohuo ili kupata dondoo za kuanzia uchunguzi.
Kufikia saa sita kamili umati mkubwa ulikuwa umejaa katika
maeneo yote yanayozunguka ubalozi. Idadi kubwa ilikuwa ya watu wa
kawaida waliokuja kushuhudia mambo yaliyokuwa yakiendelea
ubalozini hapo. Hili lilikuwa tukio la kwanza la kigaidi kutokea nchini
Tanzania. Kabla ya tukio hili watanzania walikuwa wakisikia katika
radio na kuona katika luninga tu jinsi matukio ya kigaidi yanavyotisha.
Kwa ujumla tukio hili lilikuwa ndiyo kifumbua macho kwa kila
mtanzania kuwa ‘ubaya hauna kwao’ unaweza kutokea popote.
Pamoja na utisho wake bado wananchi wengi walielekea kuvutiwa
na mambo yaliyokuwa yakiendelea ubalozini hapo. Kwa wengine tukio
hili lilikuwa kama sinema vile. Wanajeshi wa kimarekani (Marines)
walikuwa wakizunguka huko na huko wakiwa wamebeba silaha zao za
kivita. Magari ya zimamoto yalikuwa yakiendelea kumwaga maji
mfululizo ili kuudhibiti moto uliokuwa ukiwaka. Polisi wa kikosi
maalum cha kutuliza ghasia (FFU) walikuwa wametanda eneo zima
wakikimbia huku na huku kuwadhibiti wananchi waliokuwa wakijaribu
kusogea karibu zaidi ili waweze kuona vizuri. Waandishi wa habari wa
vyombo vya ndani na wapiga picha binafsi nao walikuwa
wameshawasili na kuanza kupiga picha. Vituo maarufu vya luninga
(TV) ya Marekani CNN na BBC ya Uingereza vilikuwa zimeshafika, na
kuanza kurusha matangazo mubashara. Kufumba na kufumbua jina
maarufu la Tanzania ‘kisiwa cha amani’ lilikuwa limeingia doa.
Ilipotimia saa sita na dakika kumi hivi nikaanza kujiandaa kuondoka
eneo la tukio, kuelekea kwenye kituo cha Mafuta. Mahali tulipopanga
kukutana na DOI, mzee Walingozi. Ilinilazimu kuanza kujiandaa
mapema kutokana na ubovu wa mazingira niliyokuwepo. Sikujua nani
ni adui, na nani ni Rafiki wa kweli. Eneo zima lilikuwa kama uwanja wa
vita. Pamoja na hayo, maafisa wa idara huwa hatuanzi safari kwa
kukurupuka hata kama hali ni shwari. Afisa anayejitambua hupaswa
kujiandaa kabla ya kwenda popote, na hasa kama safari yenyewe ni ya
kukutana na mtu muhimu kama mkuu wa kazi, au mtoa habari (source).
Kusema kweli hakuna afisa makini asiyejua kwamba kutojiandaa ni
tiketi ya kumtia matatani yeye, na yule anayeenda kukutana naye.
Kabla sijaanza kuondoka nilitumia dakika kadhaa kuangalia umati
wa watu, nikijitahidi kumsoma (kama scanner) kila mtu aliyekuwepo
mahali hapo kujua kama yupo mtu aliyeonesha kuvutiwa na uwepo
wangu au kufuatilia nyendo zangu. Dakika tano tu ziliniwezesha

19
GO DW IN C H IL EWA | 20

kuwatambua watu zaidi ya kumi na tano, waliokuwa wamejichanganya


katika umati uliosimama upande wa pili wa barabara ya Ali Hassan
Mwinyi, macho yao yakiwa yameelekezwa kwangu.
Mtu wa kwanza alikuwa mzee Chezi. Huyu alikuwa mkuu wa
usalama wa Taifa wilaya (DSO) Kinondoni wakati huo. Mzee Chezi
alikuwa akiangalia kwa makini kila jambo lilokuwa likifanyika ubalozini,
huku akinifuatilia kila hatua ninayopiga. Sikumshangaa, nilijua
hakutegemea kuniona nikiwa nimejichanganya na maafisa wa ubalozi,
Polisi na wanajeshi wa Marekani (Marines) namna ile.
Hatua chache kutoka mahali aliposimama DSO Chezi alikuwepo
afisa mwingine, mtu wa Mwanza. Wakati huo alikuwa kijana wa miaka
isiyozidi ishirini na saba hivi. Afisa huyu pamoja na umri wake mdogo
alikuwa mchapa kazi hodari kiasi cha kuaminiwa kuongoza ‘Kanda’
moja ya kiitelejensia.jinini Dar es Salaam. Kwa sababu za kiusalama
sitataja majina yake kamili, nitamwita MTW.
Upande wa magharibi wa barabara niliweza kuwaona na kuwatambua
maafisa wengine wawili kutoka ofisi ya DSO Kinondoni, na mmoja
kutoka kituo cha ufundi (technical). Hawa wote walikuwa makini
kufuatilia kila jambo linalofanyika ubalozini hapo. Uwepo wa maafisa
hawa ulinihakikishia kuwepo kwa maafisa wengine wengi. Nina hakika
sikuweza kuwaona kwa sababu walikuwa wamejichanganya, au
wamevaa mavazi ya kuzuia wasitambulike kwa urahisi. Kwa ujumla
tayari idara ilikuwa imeingia kazini.
Ukiacha maafisa wa idara ya usalama wa Taifa, na polisi, niliweza
pia kuwatambua watu kadhaa waliokuwa wakiniangalia kwa shauku.
Hawa walikuwa vijana wa Kinondoni, wasiojua lolote kuhusu kazi
niliyokuwa nikiifanya, hivyo hawakunipa wasiwasi mkubwa. Nilijua
shauku yao ilitokana na kunifahamu tu, kwani miaka hiyo nilikuwa
nikitembelea sana maeneo hayo.
Niliporidhika kuwa hali ni shwari kwa upande wangu, haraka
nikajipenyeza katikati ya umati uliokuwa karibu na jengo na kutembea
haraka kando ya barabara ya Ali Hassan Mwinyi kuelekea eneo la
Mbuyuni (Protea Apartments). Barabara ilikuwa imefurika mamia ya
watu waliokuwa wakitembea kasi, au kukimbia kuelekea ubalozi wa
Marekani kujionea kinachoendelea. Kwa kuwaangalia jinsi
wanavyokwenda tu, niliweza kutambua kuwa asilimia 98 ya watu hao
hawakuwa na ufahamu wowote wa mambo ya kiusalama. Walikuwa
wakijiendea bila kuchukua tahadhari ya aina yoyote.

20
21 | SH U H U DA ZA J A SU SI – NDA NI YA IDA RA

Nilipofika kwenye kituo cha mafuta nilimkuta mzee Walingozi


tayari ameshafika, amekaa ndani ya gari yake aina ya Mercedes Benzi
nyeupe yenye vioo vyeusi. Nilipokaribia gari yake akateremsha kioo cha
dirisha, upande niliokuwa nikitokea na kuniashiria nipande gari. Bila
kuuliza swali nikafungua mlango wa mbele na kukaa katika kiti cha
abiria. Gari ilikuwa imeshawashwa. Hivyo nilipoketi na kufunga
mkanda tu, akatia gia na kuirudisha nyuma, kisha akakata kona kuingia
barabarani. Mita chache mbele akakanyaga Mafuta zaidi kulifanya
Benzi likimbie vilivyo kuelekea makao makuu ya TISS
Tukiwa njiani DOI alinitaka nimueleze kwa mapana taarifa
niliyokuwa nimempa kwa ufupi pale ubalozini, na nyongeza ya yale
niliyokuwa nimeyapata baada ya kuonana naye. Kwa uangalifu mkubwa
nikamueleza habari yote, kuanzia shughuli yetu ya mnazi mmoja, jinsi
tulivyosikia mlipuko, uamuzi wa Morgan kunitaka nikafuatilie tukio
hilo makao makuu ya JWTZ, na jinsi nilivyotambua kuwa tukio hilo
limetokea ubalozini hapo. Nikaendelea kumueleza hali niliyoikuta
kwenye ofisi ya RSO Dar es salaam, uharibu uliofanyika na tahadhari
za kiusalama ambazo uongozi wa ofisi hiyo ulikuwa umechukua
endapo magaidi wangekwenda kushambulia ofisi hiyo. Baada ya
maelezo hayo ndipo nikamueleza jinsi nilivyofika ubalozi wa Marekani
na kujitambulisha kwa afisa wa Marines, mapokezi aliyonipa na jinsi
alivyokuwa tayari kunipatia taarifa husika.
Nilimueleza pia jinsi tukio lilivyotokea kwa mujibu wa taarifa
nilizokusanya, watu wanaotuhumiwa kuhusika na shambulio hilo,
sababu zinazofanya wamarekani waituhumu Alqaida, na hatua ambazo
ubalozi umechukua kuimarisha ulinzi. Kwa kumalizia nilimuonesha
karatasi nilizokuwa nimeandika majina ya wahanga wa tukio hilo,
nikianza na wale niliofahamishwa kuwa wamekufa, majeruhi, na
kumalizia na waliosalimika. Kwa wale waliopelekwa hospitali nikampa
majina ya madereva waliowachukua, aina na namba za magari
waliyokuwa wakiendesha, na hospitali walizoelekezwa na polisi
kuwapeleka. Vilevile nikampa majina ya wahanga waliokuwa na hali
nzuri kiafya kiasi cha kutohitaji matibabu, anuani ya makazi yao, na
mahali wanapoweza kupatikana endapo watakapohitajika.
Taarifa yangu ilimfurahisha sana DOI. Akaniambia “Chilewa nilijua
ungefanya kazi nzuri, na hukuniangusha, umeniwakilisha vema.
Nakushukuru sana” Maneno haya yalinitia moyo mno. Kwa
unyenyekevu mkubwa nikamshukuru kwa kuniamini kiasi hicho, na

21
GO DW IN C H IL EWA | 22

kumueleza kuwa nilifanya kile nilichoweza tu kwa kadri Mungu


alivyoniongoza.
Bila kuongeza neno akachukua simu yake ya mkononi na
kubonyeza namba kadhaa. Mtu wa upande wa pili alipopokea tu
akamuagiza utaratibu wa haraka ufanyike kudhibiti mipaka yote (entry
points) ili watu waliolipua ubalozi wasiweze kuvuka kwa urahisi. Pamoja
na hayo akaagiza kucheleweshwa kwa ndege za abiria katika viwanja
vya ndege vyote nchini ili kuwapa maafisa wa idara na polisi muda wa
kufanya upekuzi wa ziada kwa abiria wanaoondoka nchini.
Alipomaliza kuongea na simu hiyo, akapiga simu nyingine kwa mkuu
wa kitengo cha idara kinachoshughulika na mahoteli. Kwa maneno
machache akamwagiza muhusika kutumia nguvu ya ziada kupata
taarifa za wageni wote waliolala katika mahoteli na nyumba za wageni
katika kipindi cha miezi mitatu.
Wakati huo tukawa tumeshafika kwenye lango kuu la makao
makuu ya idara (TISS) eneo la Oysterbay jirani na kanisa katoliki la
mtakatifu Petro (st Peter). Maafisa wa kikosi cha ulinzi wa viongozi na
vituo muhimu waliokuwa langoni hapo walifungua geti mara tu
walipoona gari ya DOI ikikaribia lango hilo. Mzee Walingozi akaingiza
gari getini na kuisimamisha, kuwapa walinzi nafasi ya kufunga geti.
Mbio mbio maafisa wawili walioshika silaha wakasogea kwenye dirisha
la upande wa dreva, alikokuwa amekaa mzee Walingozi. Kwa
kuwaangalia tu nikatambua kuwa nao walikuwa katika hekaheka.
“Mpatie gate pass afisa huyu ninayeingia naye. Atatoka akimaliza kazi
iliyomleta” Aliwaambia maafisa hao kwa sauti kavu.
“Sawa mkuu” walijibu kwa pamoja huku wakinitazama usoni kwa
shauku ya kutaka kunijua.
“Samahani, unaitwa nani mkuu?”
Mmmoja wao aliniuliza kwa heshima.
“Chilewa…Godwin Chilewa” Nilimjibu kwa sauti kavu.
Bila kuuliza swali la ziada akageuka kuliendea dirisha lililokuwa umbali
wa mita mbili hivi kutoka gari ilipokuwa imesimama. Kwa sauti ya
chini akamnong’oneza jambo afisa aliyekuwa ndani ya chumba cha
walinzi akikodolea macho CCTV monitor iliyokuwa mbele yake.
Hazikupita sekunde therathini mlinzi huyo akarudi kwenye gari akiwa
ameshikilia kitambulisho chenye utepe wa kuvaa shingoni na kunipatia.
“Ahsante sana” nilimwambia wakati mkurugenzi akiondoa gari kwa
kasi kuelekea kwenye jengo kuu, mahali yalipokuwa maegesho maalum
kwa ajili ya gari lake.

22
23 | SH U H U DA ZA J A SU SI – NDA NI YA IDA RA

Sikuwa na mazoea ya kuja katika ofisi hii mara kwa mara kwani
hakikuwa kituo changu cha kazi. Ingawa miaka ya nyuma niliwahi
kufanya kazi kadhaa zilizonifanya nifike makao makuu mara kwa mara,
bado sikujenga mazoea yoyote na watu wa hapa. Tofauti na idara
nyingine za serikali, idara ya usalama wa Taifa ina utaratibu maalum
unaowazuia maafisa wake kwenda kwenye ofisi zisizo vituo vyao vya
kazi bila sababu ya msingi. Utaratibu huu huwahusu maafisa wote bila
kujali vyeo vyao, au idadi ya miaka waliyoitumikia idara.
Kwa ujumla hata kama ofisi ya kitengo kimoja iko kwenye jengo
moja na kitengo kingine, maafisa wa vitengo hivyo hawaruhusiwi
kutembeleana ofisini bila ruhusa au sababu za msingi. Endapo afisa
atalazimika kwenda katika ofisi nyingine, nje ya kituo chake cha kazi
kwa dharula au sababu nyingine yoyote hutakiwa kuomba kibali (gate
pass) ya kumruhusu kufanya hivyo. Vinginevyo anaweza kulazimika
kubaki kwenye ofisi ya mlinzi. Utaratibu huu uitwao compatimentation
huisaidia idara kutunza siri, kuendesha operesheni zinazojitegemea, na
kuwazuia maadui wa taifa kujipatia taarifa muhimu kwa urahisi (endapo
watapenyeza mtu wao ndani ya idara).
Idara imeweka kanuni na taratibu hizi ili kulinda nyaraka na siri za
idara, na pia kujenga nidhamu ya maafisa wake. Kwa ujumla kila afisa
anajua kwamba muda wowote katika ajira yake anaweza kuwa
anafuatiliwa nyendo zake kwa sababu mbalimbali. Aidha kwa lengo la
kuthibitishwa uwezo na umakini wake ili apandishwe cheo na kupewa
madaraka makubwa, au kwa kutiliwa mashaka. Kutokana na utaratibu
huu, hakuna afisa yeyote, wa mahali popote na au cheo chochote (hata
mkurugenzi mkuu wa idara –DGIS) anayeweza kujisifu kuwa anajua
kila kitu kinachotendeka ndani ya idara ya usalama wa Taifa.
Tulipofika sehemu ya maegesho, DOI akasimamisha gari na
kuzima injini. Sote wawili tukateremka na kutembea sambamba
kuelekea ndani ya jengo lililokuwa mita chache mbele yetu. Hali katika
ofisi hii ilikuwa nzuri kuliko ile niliyoikuta katika ofisi ya RSO Dar es
salaam. Baadhi ya vioo vya madirisha vilikuwa vimepasuka kutokana
na mshindo wa bomu lakini jengo lilionekana kuwa imara. Maafisa
wote walikuwa katika hali ya tahadhari kubwa ingawa walishaambiwa
mahali ulikotokea mlipuko. Walinzi wa kumbi (coridol) walionekana
kuwa na msongo zaidi. Kila kumbi tuliyopita walinzi walikuwa imara,
wameshikilia silaha kubwa za kivita tayari kwa mapambano. Tangazo
maalum lilikuwa limeshatolewa kuwajulisha maafisa hao kwamba
magaidi wamelipua ubalozi wa Marekani, na haijulikani kama

23
GO DW IN C H IL EWA | 24

wamekusudia kufanya shambulio linguine wapi na muda gani. Maafisa


wote walitakiwa kuwa katika hali ya tahadhari muda wote.
Tulipofika ofisini kwake, DOI aliniagiza niandike taarifa kuhusu
tukio husika ili aweze kwenda nayo kwenye kikao. Baada ya maagizo
hayo akamwita katibu wake (S1) na kumuagiza kuitisha kikao cha
wakurugenzi (wa idara ya usalama wa Taifa) kupanga mikakati ya
kukabiliana na janga lililotokea. Kikao hicho kilitakiwa kuanza katika
muda usiozidi dakika kumi na tano kuanzia muda wa agizo hilo, na
kufuatiwa na kikao cha wakuu wa idara ndogo na vitengo vyote vya
idara ya usalama wa Taifa. Hapo ndipo nilipofahamu kuwa mkurugenzi
mkuu (Director General of Intelligence and Security - DGIS) Colonel Abson
Mwang’onda alikuwa nje ya nchi kikazi. Mzee Walingozi (DOI) ndiye
aliyekuwa akikaimu nafasi hiyo kwa wakati huo.
Kikao cha wakurugenzi alichokiitisha kilipaswa kuhudhuliwa na
mkurugenzi wa operesheni za nje (Director of External Operations –
DEO), mkurugenzi wa uajiri utafiti na mafunzo (Director of Recruitment
Research and Training – DRRT), mkurugenzi wa utawala (Director of
Administration and Personnel – DAP wakati huo A1), na yeye mkurugenzi
wa operesheni za ndani (Director Of Internal operations - DOI) ambaye
kwa kukaimu nafasi ya mkurugenzi mkuu (ag DGIS) ndiye alikuwa
mwenyekiti wa kikao. Miaka hiyo nyadhifa za naibu mkurugenzi mkuu
(Deputy Director) na mkurugenzi wa habari na teknolojia hazikuwepo.
Dakika kumi na tano tu, zilinitosha kuandika taarifa yangu kama
nilivyokuwa nimeagizwa. Taarifa hiyo pamoja na viambatisho vyote
nikamkabidhi DOI mwenyewe, maana alikuwa akiisubiri kwenda nayo
kwenye kikao cha wakurugenzi.
“Excellent” Mzee Walingozi aliniambia baada ya kuisoma.
“Ahsante mkuu” Nilimjibu kwa unyenyekevu huku nikisimama tayari
kutoka ofisini humo, kwani kikao alichokuwa akienda kuhudhuria
kilikuwa hakinihusu. Pamoja na miaka kumi ya utumishi wangu ndani
ya idara ya usalama wa Taifa, cheo changu (cha kiidara) wakati huo
kilikuwa bado kidogo tu, naweza kusema sambamba na kile cha luteni
wa JWTZ tu si zaidi ya hapo; wakati mzee Walingozi alikuwa miongoni
mwa watu wachache wanaoiendesha idara hii nyeti.
Idara ya usalama wa Taifa kama zilivyo idara nyingi za kijasusi
duniani, ni Para military institute (yaani taasisi inayoendeshwa nusu
kijeshi nusu kiraia). Kwa sababu hii maafisa hulazimika kubadilika
kuendana na mazingira ya kazi. Mambo yanapokuwa shwari maafisa
hufanya kazi kama raia halisi, na pale mambo yanapo chachamaa ujeshi

24
25 | SH U H U DA ZA J A SU SI – NDA NI YA IDA RA

huchukua nafasi yake. Siku hiii ilikuwa mojawapo ya nyakati hizo,


maana hali ya usalama wa nchi ilikuwa tete kuliko ninavyoweza kueleza.
“Taarifa ni nzuri, ina details za kutosha na imetupa pa kuanzia. In
fact ukiacha other sources, hakuna afisa mwingine yeyote aliyefikia hatua
hii kwa sasa. Nakwenda kukutana na wakurugenzi wenzangu ili
tupange mikakati ya kulishughulikia hili, na kumjulisha rais. Kwa vile
mengi yatatoka kwenye taaifa yako, upo uwezekano mkubwa
wakurugenzi wakataka kukuuliza maswali, au kupata maelezo ya ziada.
Ili kuondoa usumbufu wa kukutafuta wakati tukiwa katikati ya kikao ni
bora usiondoke hapa. Subiri ofisini kwangu mpaka tutapomaliza kikao,
na kuthibitisha kuwa hatuhitaji maelezo ya ziada” DOI alimalizia
“Sawa mkuu” Nilimjibu
“Wakati tukiwa kwenye kikao unaweza kufuatilia mambo
yanayoendelea kwenye eneo la tukio kupitia television, maana CNN
wanaendelea kuonesha live” Aliniambia huku akiinyooshea kidole TV
kubwa iliyokuwa pembeni ya ofisi yake. Kabla sijasema lolote mlango
ukafunguliwa na katibu muhtasi wa DOI akaingia akiwa ameshikilia
mafaili mawili yenye rangi nyekundu. Akayaweka mezani, na
kumjulisha DOI kuwa wajumbe wote walikuwa wameshawasili kwenye
chumba cha mkutano.
“Ahsante kwa taarifa” Doi alimjibu kisha akaongeza
“Mpigie simu DSO wa Ilala, mama Murusuli. Mwambie afisa wake
Godwin Chilewa yuko ofisini kwangu kwa kazi maalum, hivyo
asihangaike kumtafuta.”
“Sawa mkuu” Dada huyo alijibu kwa unyenyekevu. Baada ya maagizo
hayo DOI akachukua faili lililokuwa na nyaraka za kikao na kutoka
ofisini humo. Kwa vile muda wa chakula cha mchana ulikuwa umefika,
na haikuwepo dalili yoyote ya kutoka ofisini hapo, dada huyo
alinyanyua simu na kumuagiza mmoja wa wahudumu aende kwenye
mgahawa wa idara kutuletea chakula na vinywaji.
Kikao cha wakurugenzi kilichukua muda mfupi kuliko
nilivyotarajia. Hazikuzidi dakika arobaini na tano tangu kuanza hadi
kumalizika. Kwa ujumla kikao chenyewe kilikuwa cha kupashana
habari na kupanga mikakati ya kuikabili kazi kubwa iliyokuwa
imejitokeza, na kuweka msimamo wa pamoja kabla ya kukutana na
wakuu wa idara kuwapa maagizo ya utekelezaji wa malengo mapya ya
idara yaliyoyokuwa yamejitokeza.

25
GO DW IN C H IL EWA | 26

DOI alirudi ofisini kwake mara tu baada ya kumaliza kikao cha


wakurugenzi. Bahati nzuri alinikuta nimeshamaliza kula chakula
nilichokuwa nimeletewa.
“Chilewa kikao kimeenda vizuri sana, na kama nilivyosema taarifa
yako ni nzuri kwa hiyo hakukuwa na maswali ya ziada” Anieleza mara
tu baada ya kuweka faili lake mezani na kukaa.
Akaendelea kunieleza kuwa kikao kiliazimia kuunda kikosi kazi
(task force) itakayofanya uchunguzi wa tukio zima ili kuwapata watu
waliofanya kitendo hicho. Task force hiyo iliazimiwa ishirikishe maafisa
wa idara ya usalama wa Taifa, makachero kutoka kikosi cha upelelezi
wa makosa ya jinai, na maafisa wa idara ya ujasusi ya jeshi la wananchi
wa Tanzania (Millitary Intelligence). Aliendelea kunieleza kuwa muda
mfupi ujao alikuwa akienda kuonana na makamu wa rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Dokta Omari Ali Juma
(Marehemu) kumpa taarifa kamili kuhusu tukio la kigaidi lililotokea na
hatua ambazo idara inacchukua kuimarisha ulinzi na usalama wa Taifa.
Kwa kawaida taarifa hii ilipaswa kupelekwa kwa rais, lakini siku hiyo
mheshimiwa Benjamin William Mkapa alikuwa nje ya nchi.
Baada ya maelezo hayo mzee Walingozi akaniruhusu kuondoka
ofisini hapo, kwenda kuendelea na shughuli zangu za kawaida (katika
kituo changu cha kazi). Kama ilivyo ada ya watanzania nikamuaga kwa
kumpa mkono, kisha nikageuka na kutembea taratibu kuelekea
chumba cha katibu muhtasi wake, mahali uliko mlango wa kutokea
ukumbini. Nikaingia katika chumba hicho na kuiendea meza ya dada
huyo ili niweze kumuaga kistaarabu. Lakini kabla
sijamfikia simu iliyokuwa mezani pake ikaita kwa sauti ya chini.
Akanyoosha mkono wake wa kushoto kuinyanyua huku akininyooshea
mkono wake wa kulia kuniashiria nisubiri kidogo.
“DOI amesema usubiri kidogo kuna mtu anakuja kukuona sasa
hivi.” Alinieleza baada ya kumaliza kuongea na simu hiyo.
“Sawa” Nilimjibu huku nikikiendea kiti kilichokuwa karibu na
mlango wa kuelekea ukumbini na kukaa. Sikuwa na fununu yoyote mtu
huyo alikuwa nani, na alitaka kuniuliza nini, au kunieleza jambo gani.
Taarifa zote nilizokuwa nazo nilikuwa nimeshazifikisha chunguni na
kubaki mikono mitupu. Hata hivyo sikuwa na la kufanya ila kusubiri.
Tulitumia muda huo kufahamiana zaidi na kuzungumza mambo
mbalimbali, ikiwa pamoja na kuelezana hali ilivyokuwa wakati mlipuko
wa bomu ulivyotokea. Yeye alinieleza hali ilivyokuwa ofisini hapo na
mimi nilimueleza kwa kifupi sana hali ilivyokuwa huko nje, huku kila

26
27 | SH U H U DA ZA J A SU SI – NDA NI YA IDA RA

mmoja akiwa muangalifu asivuke mipaka. Kadri tulivyokuwa


tukizungumza nikajikuta nikimfananisha dada huyo na kijana mmoja
niliyesoma naye shule ya upili jijini Dar es salaam. Kijana huyo
aliyekuwa akiitwa Riziki alikuwa madarasa mawili nyuma yangu. Baadae
alinifahamisha kwamba Riziki alikuwa mdogo wake wa tumbo moja.
Ghafla mlango ukafunguliwa. Afisa mmoja, mwanaume mwenye
umri usiozidi miaka therathini akaingia ndani. Baada ya kutusalimia
akajitambulisha jina lake, nami nikamfahamisha jina langu.
“Aaah, kumbe wewe ndiye afisa niliyekuwa nakufuata” Aliniambia
huku akinipa mkono kwa mara ya pili.
“DOI ameniagiza nikupe hii OP, na usafiri wa kukufikisha mahali
popote unapotaka kwenda” Aliendelea kunieleza huku akinikabidhi
bahasha nyeupe iliyoandikwa jina langu.
“Ahsante, nashukuru sana” Nilimjibu huku nikiipokea bahasha hiyo
na kuidumbukiza katika mfuko wa suruali yangu. Sikuwa na haja ya
kujiuliza kilichokuwemo maana aliyenipa alishaniambia kuwa ni OP
(operation fund) Neno la ki-idara lenye maana ya “fedha za kufanyia kazi”
Bila kupoteza muda nikamuaga katibu muhtasi wa DOI na kufuatana
na afisa aliyekuja kunichukua kuelekea nje ya jengo, mahali alipokuwa
dereva wa DOI akinisubiri.
Sikuwa na sababu ya kurudi ofisini kwa RSO Dar es salaam alasili
hiyo. Pikipiki yangu niliyoiacha huko nilikuwa na hakika itakuwa
salama muda wote itakaokaa hapo. Uzoefu wa kazi zetu ulinionya kuwa
endapo nitaenda ofisini hapo, basi sitaweza kuondoka mapema
kutokana na wingi wa maswali nitakayo kumbana nayo, au kazi
nitakazopewa. Kwa upande mwingine sikujisikia vema kurudi ubalozi
wa Marekani baada ya kazi niliyokwisha kuifanya. Niliona vema
kuwaachia wataalam wengine wafanyefanya kazi hiyo kwa mujibu wa
sheria na taratibu za kimataifa. Hivyo badala ya kumwambia dereva
anipeleke barabara ya Kenyata, nikamwambia anipeleke Kinondoni,
eneo la Mango Garden. Nilijua kutoka hapo ningeweza kupata usafiri wa
kunipeleka nyumbani, au mahali pengine popote nitakapotaka kwenda.

3
Siku ya jumatatu tarehe 10 August, 1998 nilifika ofisini, Ilala Boma,
mapema kuliko kawaida. Pamoja na kuwahi huko ofisini nilimkuta bosi
wangu, mama Murusuli na maafisa wengine wote wakiwa wameshafika,
wameketi kuzunguka meza ya mkutano, tayari kwa SITREP. Bila
kupoteza muda niliwajulia hali na kuketi katika kiti kilichokuwa wazi.

27
GO DW IN C H IL EWA | 28

Kikao cha asubuhi hii kilikuwa muhimu sana, na cha aina yake.
Kwa maafisa wapya hiki kilikuwa kikao cha kwanza baada ya tukio
kubwa la kigaidi nchini hali iliyowafanya wawe na mchecheto wa aina
yake. Mimi pia nilikuwa katika hali isiyo ya kawaida. Matukio ya siku
mbili zilizopita yalinionesha wazi kazi, na hatari iliyokuwa mbele yetu.
Wakati huo ilikuwa imepita miaka tisa tu tangu nilipotoka kwenye
mapambano na magaidi wa RENAMO. Kwa mama Murusuli mambo
yalikuwa magumu zaidi. Yeye ndiye aliyekuwa katibu wa Kamati ya
Ulinzi na Usalama ya wilaya ya Ilala. Kamati iliyokuwa na jukumu la
kuhakikisha wilaya ya Ilala, (ambayo ndiyo kitovu cha Dar es Salaam)
inakuwa salama. Kutokana na wadhifa huo alipaswa kuwasiliana na
mkuu wa wilaya (ambaye ndiye mwenyekiti wa kamati) ili kuitisha kikao
cha dharula. Kikao kilitakiwa kufanyika mara tu baada ya SITREP ili
kuweka mikakati ya ulinzi na usalama wilayani.
Kama kawaida DSO ndiye aliyefungua kikao kwa kutoa maelezo
mafupi kuhusu hali ya usalama nchini. Tofauti na siku nyingine
ambapo masuala ya uchumi, siasa na huduma za kijamii yalitawala zaidi,
siku hiyo agenda kuu ilikuwa suala la ugaidi. Kwa dakika kumi hivi
DSO alitusomea taarifa maalum iliyotolewa na makao makuu kuhusu
shambulio lililotokea katika ubalozi wa Marekani. Taarifa hiyo ilieleza
kuwa watu 10 raia wa Tanzania, walikuwa wameshapoteza Maisha yao,
na wengine 72 walikuwa wamejeruhiwa. Wahanga hawa walikumbwa
na umauti wakiwa ndani ya ubalozi wa Marekani kwa shughuli za
kiofisi, au nje ya ofisi hizo kwa shughuli binafsi na biashara. Wengine
ni pamoja na wafanyakazi wa balozi za Nigeria na Ufaransa zilizokuwa
jirani na ubalozi wa Marekani, na wapita njia.
Kufuatia tukio hilo siku ya Jumapili, tarehe 9 August, rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mheshimiwa Benjamin Mkapa
alitembelea eneo la tukio kujionea hali halisi ilivyokuwa. Akizungumza
ubalozini hapo rais Mkapa alisema wahalifu waliolipua ubalozi huo
hawautakii mema uhusiano mzuri uliokuwepo kati ya Tanzania na
Marekani, na kusisitiza kuwa “Adui wa Marekani ni adui wa Tanzania” na
kuahidi kuwa serikali ya Tanzania itashirikiana na Marekani katika
kuwasaka wahalifu waliohusika. Pamoja na kutembelea ubalozi huo
rais Mkapa pia alitembelea hospitali ya Muhimbili ambako Watanzania
63 walikuwa wamelazwa kwa ajili ya kupatiwa matibabu. Majeruhi
wengine 18 walikuwa katika hospitali ya Agakhan.
Taarifa hiyo pia iligusia hali ilivyokuwa jijini Nairobi, nchini Kenya
kufuatia tukio la kigaidi lililofanyika sambamba na hili. Watu mia moja

28
29 | SH U H U DA ZA J A SU SI – NDA NI YA IDA RA

na saba (107) walikuwa wamepoteza Maisha yao, kati yao nane wakiwa
raia wa Marekani. Waokoaji walikuwa wakiendelea kuwatafuta
Wamarekani wengine watano waliokuwa bado wamefunikwa na
kwenye kifusi. Watu zaidi ya elfu mbili na mia mbili (2200) walikuwa
wamejeuhiwa, wengine wakiwa mahututi.
Taarifa hiyo pia iligusia uwepo wa cell ya kigaidi nchini. Uchunguzi
wa awali ulionesha magaidi waliohusika na shambulio la ubalozi wa
Marekani hawakuwa wababaishaji; bali watu wenye uzoefu wa hali ya
juu katika kupanga, na kutekeleza mashambulizi makubwa ya kigaidi.
Hii iliashiria uwepo kwa cell za kigaidi nchini, zinazofanya kazi kwa
ushirikiano au maelekezo ya kundi kubwa zaidi. Baadhi ya makundi
yaliyowekwa katika orodha ni Alqaida, linaloongozwa na Osama bin
Laden, Egyptian Islamic Jihad, Hizbollah, na Hamas. Idara ilipaswa
kuelekeza nguvu zake zote katika ukusanyaji wa taarifa za kiintelejensia
ili kuvitambua vikundi hivyo, washirika wake, wafadhili wake, na jinsi
vinavofanya kazi.
Baada ya maelezo hayo mama Murusuli alitoa nafasi kwa maafisa
kujadili taarifa hiyo kabla ya kuanza utekelezaji wake katika medani.
Morgan ndiye aliyekuwa wa kwanza kunyoosha mkono wake juu,
kuashiria kuwa anataka kuzungumza.
“DSO nakushukuru sana kwa taarifa uliyotupa” Morgan alianza
baada ya kupewa nafasi ya kuongea. “ Kusema kweli taarifa ya makao
makuu imegusia vitu vingi na vya msingi kwa ujumla wake. Lakini
mkuu, sisi tumebahatika kidogo. Mmoja wa maafisa waliofika katika
ubalozi wa Marekani mara tu baada ya tukio ni mwenzetu wa hapa
ofisini; na kwa bahati nzuri asubuhi hii tuko naye hapa. Nafahamu hilo
kwa sababu mimi ndiye niliyemuagiza kwenda kufuatilia mlipuko
tuliousikia. Kwa hiyo naomba kama inawezekana, umruhusu Chilewa
naye atueleze kwa kina mambo aliyoyashuhudia. Naamini maelezo
yake yatatupa picha nzuri zaidi, na tutakapoanza kudadavua tutakuwa
katika nafasi ya kufanya hivyo kwa mapana” Morgan alimalizia.
Hoja hiyo iliungwa mkono na maafisa wengine waliokuwa katika
SITREP. Maafisa hao walionesha shauku kubwa ya kutaka kujua
reaction ya wanajeshi wa Marekani (Marines) waliokuwa wakilinda
ubalozi, na hali halisi ilivyokuwa katika ofisi ya RSO Dar es Salaam
iliyokuwa umbali mfupi tu kutoka ubalozini.
“Nakubaliana nawe Morgan, Chilewa ana maelezo mazuri sana”
Alijibu mama Murusuli. “Hata hivyo taarifa yake haiwezi kuwa sehemu
ya SITREP hii, maana imeshawasilishwa makao makuu. Ila kwa faida

29
GO DW IN C H IL EWA | 30

ya maafisa mliopo hapa, namruhusi awaeleze kwa kifupi ili nanyi mjue
hali halisi ilivyokuwa” Mama Murusuli alimaliza maelezo yake huku
akiniashiria nianze kuzungumza.
Kwa kirefu nikawaeleza jinsi mambo yalivyokuwa tangu
nilipoachana na akina Morgan, hadi nilipoondoka ubalozini kurudi
nyumbani. Nilijitahidi sana kuwapa maelezo ya kina, ili kuwapa picha
halisi ya mfululizo wa matukio bila kugusia mawasiliano yangu na DOI
wala taarifa nilizokuwa nimeziwasilisha makao makuu. Mambo hayo
yalishaingia katika utaratibu wa usiri sambamba (compatimentation) hivyo
sikupaswa kuyaeleza kwa maafisa wengine.
Baada ya maelezo yangu tuliendelea na SITREP kwa dakika
zisizopungua arobaini na tano hivi, kujadili kila suala tuliloona ni
muhimu kufuatia hali tete iliyokuwepo nchini. Kubwa kuliko yote
lilikuwa suala la kuimarisha ulinzi na usalama katika maeneo
yaliyokuwa yakituhusu. Kwa bahati mbaya mpaka wakati huo tulikuwa
hatujapata fununu ya watu waliofanya tukio la kigaidi. Hatukujua
walikuwa wamekusudia kufanya matukio mangapi, maeneo gani, na
kwa wakati gani. Kwa sababu hiyo ulinzi wa hali ya juu ulihitajika katika
maeneo yote muhimu tuliyokuwa tukiyasimamia.
Maeneo tuliyoyapa kipaumbele zaidi ni pamoja na majengo ya
serikali, hospitali za Muhimbili, na Agakhan, masoko na sehemu
maarufu za biashara, mahoteli ya kitalii, stesheni na vituo vya mabasi,
shule maarufu hasa za mjini kati, kumbi za starehe, mitaa yenye
mikusanyiko ya watu wengi, na madaraja muhimu. Uimarishaji ulinzi
ulipaswa kufanyika kwa kushirikiana na jeshi la polisi, idara ya
Uhamiaji, na jeshi la wananchi wa Tanzania.
Jambo lingine tulilolitazama kwa kina, ni suala la wahamiaji
haramu waliokuwa wamejazana nchini. Suala hili lilikuwa nyeti kwa
sababu maafisa wengi walihisi magaidi waliolipua ubalozi wa Marekani
walikuwa raia wa kigeni, au watanzania waliofundishwa na kupewa
msaada na wageni walioingia nchini kutoka ughaibuni. Wakati huo
kulikuwa na idadi kubwa ya wakimbizi kutoka Rwanda, Burundi,
Somalia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), na Ethiopia.
Ongezeko la wageni hawa lilichangiwa kwa kiasi kikubwa na mauaji ya
kimbali yaliyotokea nchini Rwanda, na mapigano yasiyokwisha katika
nchi za Kongo, Burundi, na Somalia. Wengi wa wahamiaji hawa
walitokea katika makambi ya wakimbizi yaliyokuwa kaskazini mwa
Tanzania, au waliingia nchini kwa njia za panya.

30
31 | SH U H U DA ZA J A SU SI – NDA NI YA IDA RA

Sambamba na hilo, lilikuwepo pia ongezeko kubwa la wafanya


biashara, na wakazi haramu kutoka India, Pakistani, na nchi nyingine
za Asia. Wahamiaji hawa waliingia nchini kwa viza halali kama watalii,
au wageni wanaokuja kuwatembelea ndugu zao kwa muda mfupi. Hata
hivyo baada ya viza zao kuisha muda wake hawakuondoka nchini; bali
walijichanganya na watu wa kwao kufanya biashara, au kazi za kuajiliwa
bila ya kufuata taratibu husika. Ili kudhibiti hali hiyo tuliona vema
ifanyike operesheni maalum ya kuwatambua wageni wote walioingia
nchini ki halali na ki ujanjaujanja (wahamiaji haramu), ikiwa sehemu ya
uchunguzi wa kuwapata magaidi waliolipua ubalozi. Tuliazimia kazi
hiyo ifanyike kwa kushirikiana na maafisa uhamiji, jeshi la polisi, na
kitengo maalum cha idara kinachoshughulika na udhibiti wa wageni
katika mahoteli.
Tulimalizia SITREP kwa kuzungumzia mambo tuliyopaswa
kuishauri serikali, hususan hatua za kuchukua kulinda biashara ya utalii
na uwekezaji nchini. Kwa miaka mingi Tanzania ilikuwa ikijulikana
kama kisiwa cha amani, na hakuna mtu yeyote aliyefikiria kwamba
magaidi wangeweza kufanya shambulio katika ubalozi wowote,
majumba ya stalehe au majengo ya serikali. Hofu ilikuwepo miaka ya
mwishoni mwa 1980 kutokana na vita vya ukombozi vilivyokuwa
vikiendelea kusini mwa Afrika. Hofu hiyo iliyeyuka mara tu baada ya
kupatikana kwa uhuru wa Afrika ya Kusini, na Nelson Mandela
kuapishwa kuwa rais wa kwanza wa Afrika ya Kusini huru. Tangu
wakati huo Tanzania ilikuwa ikitamba kwa amani, hali iliyosaidia kwa
kiasi kikubwa kupata maelfu ya watalii katika mbuga za wanyama, na
vivutio vingine vilivyoko nchini. Tukio hili lilitia doa amani iliyokuwa
ikitangazwa na hivyo kuweza kushusha biashara ya utalii.
Wakati tukiendelea kudadavua suala moja baada ya jingine, simu
iliyokuwa mezani kwa DSO ikaita kwa kelele. Haraka mama Murusuli
akanyanyua kikonyo chake na kukipeleka sikioni.
“Halow” aliita kwa sauti kavu.
“DSO habari za asubuhi? ofisini kwa DOI hapa. Subiri
nikuunganishe na mkurugenzi” Upande wa pili ulijibu kwa sauti ya
msisitizo. Kusikia hivyo, mama Murusuli akatuashiria tutoke ofisini
kwake ili aweze kuzungumza na mkurugenzi. Mara moja sote
tukasimama na kutoka chumbani humo, huku Edward (EL) aliyekuwa
wa mwisho kutoka akifunga mlango ili kumpa faragha zaidi.
Wakati tukimsubiri mama Murusuli amalize mazungumzo na DOI,
tukaketi katika madawati yetu kuendelea na mazungumzo. Mimi ndiye

31
GO DW IN C H IL EWA | 32

niliyekuwa mzungumzaji mkuu, kwani maafisa wenzangu bado


walikuwa na kiu ya kujua hali ilivyokuwa katika ofisi ya RSO Dar es
Salaam, na ubalozi wa Marekani baada ya shambulio. Kila afisa kwa
wakati wake aliniuliza swali aliloona litanifanya nitoe maelezo ya kina
zaidi. Nami bila kuvunja miiko ya usiri sambamba (compatimentation)
niliwaeleza yote niliyoona wanastahili kuyajua. Kwa ujumla tukio zima
lilikuwa kama movie, au riwaya za Elvis Musiba.
Tukiwa katikati ya mazungumzo, katibu muhtasi wa DSO
akafungua mlango, na kuingia ofisini kwetu haraka haraka. Ingawa
ilikuwa kawaida ya dada huyu kuingia ofisini kwetu mara kwa mara,
ujio wake asubuhi huo ulionekana kana kwamba si kitu cha kawaida.
Sote tukageuka na kunyamaza kimya kumsikiliza.
“Chilewa unaitwa na DSO”
Dada huyo aitwae Bahati alisema kwa sauti kavu huku akitukazia
macho, halafu bila kuongeza neno akageuka kurudi alikotoka. Bila
kupoteza sekunde nikainuka, na kutembea kwa kasi kuelekea ofisini
kwa mama Murusuri. Nikafungua mlango na kuingia, kisha nikaufunga
taratibu.
Mama Murusuli alikuwa bado ameshikilia kikonyo cha simu,
akiendelea kuongea kwa sauti ya chini. Kwa heshima nikasimama
mbali, karibu na mlango ili kumpa nafasi ya kumaliza mazungumzo
yake. Alipoona hivyo akanyanyua mkono wake wa kulia kuniashiria
nisogee karibu, na kukaa katika moja ya viti viwili vilivyokuwa pembeni
ya meza yake. Bila kusema neno nikafanya kama alivyoniagiza.
“Mkurugenzi, Chilewa ameshafika, yupo tayari kwa maagizo yako”
Mama Murusuli alimwambia mtu aliyekuwa upande wa pili mara tu
alipoona nimeshakaa pembeni; halafu akanyoosha mkono wake
kunikabidhi kikonyo cha simu.“Ongea na DOI” aliniambia.
Kwa cheo na wadhifa niliokuwa nao katika TISS wakati huo,
sikuwa miongoni mwa watu wanaoweza kupigiwa simu na DOI kwa
sababu yoyote ile. Chain of command ilinitenga na wakubwa hata
nilipokuwa katika operesheni nyeti. Mara zote wakuu wa operesheni
hizo ndiyo waliokuwa na nafasi ya kuzungumza na wakurugenzi kwa
niaba yetu wakati sisi tukiwa katika mapambano. Mara zote sie watu
wa medani (field) kumbukumbu zetu zilibaki katika mafaili, na katika
vichwa vya wale tulioshirikiana nao katika vita. Kwa hiyo fursa ya
kuzungumza na DOI asubuhi hiyo ilinifanya nijisikie mtu muhimu
sana, japokuwa sikuwa na fununu ya jambo alilotaka kunieleza.

32
33 | SH U H U DA ZA J A SU SI – NDA NI YA IDA RA

“Shikamoo mkuu” Nilimsalimia kwa unyenyekevu mara tu baada ya


kuweka kikonyo cha simu katika sikio langu la kulia.
“Marahaba Chilewa, habari za tangu ijumaa?”
Aliniuliza kwa upole kama mzazi anayeongea na mwanawe wa kwanza,
mara tu baada ya kumuoza mke.
“Salama mkuu” Nilimjibu kwa unyenyekevu.
“Chilewa, sasa hivi nimemaliza kumpa DSO maelekezo, hata hivyo
nimeona si vibaya nikiongea nawe moja kwa moja ili uweze kuona
umuhimu wa jambo lenyewe” Akanyamaza kidogo kuruhusu mate
yapite kohoni mwake kisha akaendelea. “Kwanza nikupongeze tena
kwa kazi nzuri uliyofanya siku ya ijumaa. Kwa hakika umefanya kazi
nzuri na kuiwakilisha vema idara. Taarifa yako imetusaidia kupata
mahali pa kuanzia, na kwa niaba ya idara nakupongeza sana”
“Ahsante sana mkuu” Nilijibu kwa unyenyekevu, huku nywele
zikinisisimka kwa furaha.
“Kufuatia tukio lililotokea, na hali ilivyo nchini hivi sasa, idara
imeunda kikosi kazi (Task force) kitakachofanya uchunguzi wa kina
kuwapata magaidi waliohusika na tukio hili ili waweze kuchukuliwa
hatua za kisheria. Kikosi kazi hicho kitahusisha maafisa wa idara
(TISS), maafisa wa idara ya upelelezi wa makosa ya jinai (Criminal
Investigation Department) kutoka jeshi letu la polisi, na maafisa wa Federal
Bureau of Investigation (FBI) kutoka nchini Marekani. Operesheni hii ni
muhimu sana na ya aina yake. Kwa mara ya kwanza idara itafanya kazi
kwa ushirikiano na makachero wa FBI pamoja na mawakala wengine
kutoka mashirika mbalimbali ya kijasusi ya nchi hiyo. Kutokana na
unyeti wa kazi hii amri ya kazi imeshatengenezwa, na maafisa
watakaoshiriki kwenye task force hiyo wameshateuliwa”
Akanyamaza kidogo kana kwamba ananipa nafasi ya kutafakari
mambo aliyonieleza, kisha akaendelea “Uteuzi wa maafisa hao
umezingatia vigezo muhimu hususan uwezo wa kukusanya na
kuchambua taarifa, uwezo wa kujilinda na kupambana na adui, na
uzoefu wa kufanya kazi katika mazingira magumu na ya hatari.
Napenda kukufahamisha rasmi kuwa wewe ni mmoja wa watu
walioonekana kuwa na sifa hizo, hivyo idara imekuteua kuwa mmoja
wa maafisa watakaounda kikosi kazi nilichokieleza. Kwa hiyo
nimemjulisha DSO kwamba kuanzia sasa hutakuwa chini yake tena.
Utawajibika moja kwa moja kwa uongozi wa task force, na kupokea
maagizo kutoka makao makuu, kupitia channel husika. Mkuu wako wa
kazi kwa muda wote wa operesheni hii XYZ ambaye ndiye mkuu wa

33
GO DW IN C H IL EWA | 34

task force aliyeteuliwa na mkurugenzi mkuu. Maelezo ya namna ya


kuwasiliana, na mfumo wa utendaji utafahamishwa utakapokutana na
kiongozi wa kikosi kazi hicho. Mpaka hapo umenielewa?
“Nimekuelewa mkuu, na nashukuru sana kwa kuniamini” Nilimjibu
huku moyo wangu ukinidunda kwa kasi kutokana na mchanganyiko wa
furaha, na wasiwasi wa uzito wa mzigo niliokuwa nikijitwika.
“Nimempa maelekezo DSO kuwa baada ya mazungumzo haya
ukabidhi kazi zote ulizopewa ili aweze kuwapangia maafisa wengine.
Baada ya makabidhiano hayo utaondoka ofisini hapo kwenda
Oysterbay, mtaa wa Kimweri nyumba namba RST23 (Si namba halisi).
Hapo utakutana na kiongozi wa operesheni pamoja na maafisa
wengine utakaoshirikiana nao katika kikosi kazi. Mkiwa hapo kiongozi
wenu atawapa maelekezo ya awali, kisha mtaenda eneo la tukio
kukutana na maafisa wa FBI kwa ajili ya kufahamiana na kuanza kazi
rasmi. Masuala mengine ya kiutawala mtafahamishwa na kiongozi
wenu” Baada ya maelezo hayo mzee Walingozi akanitakia heri kwa
operesheni ninayokwenda kuifanya, kisha akaniomba nimpe simu
mama Murusuli ili aweze kumuaga.
Siwezi kuelezea kwa ufasaha jinsi nilivyojisikia baada ya kumaliza
mazungumzo na DOI. Tangu nikiwa kijana mdogo nilikuwa
nikitamani sana kuwa mpelelezi bora kama Willy Gamba aliyetajwa
katika riwaya za Elvis Musiba. Pamoja na ndoto hizo kamwe sikuwahi
kufikiria kama siku moja ningepata nafasi ya kushiriki katika uchunguzi
wa tukio lililotingisha dunia nzima kama hili. Kwa mara ya kwanza
tangu nijiunge na idara ya Usalama wa Taifa nilitamani mama yangu
mzazi aliyefariki miaka mingi iliyopita angekuwepo, kushuhudia
muujiza huu wa aina yake.

4
Ilinichukua dakika arobaini na tano tu, kukabidhi kazi zangu zote kwa
DSO. Mama Murusuli alinipongeza mno kwa kazi nzuri niliyoifanya
siku ya ijumaa kiasi cha kuuridhisha uongozi wa juu wa idara.
“Umefanya kazi nzuri iliyotujengea heshima sisi sote. Nilipoongea na
DOI amenipongeza sana. Amesema mama Murusuli unafanya kazi nzuri
mno. Vijana wako wana weledi wa hali ya juu. Hili si jambo dogo kwangu,
ni sifa kwangu binafsi na kwa maafisa wote walio chini yangu”
Aliniambia mama huyo aliyekuwa akinipenda na kunisaidia kama
mwanawe. Nami kama ilivyo ada nilimshukuru kwa kunipa majukumu

34
35 | SH U H U DA ZA J A SU SI – NDA NI YA IDA RA

yaliyonikomaza kikazi, kuniendeleza ki taaluma, na kunisaidia kwa kila


hali katika kipindi chote nilichofanya kazi chini yake.
Kufikia muda huo mama Murusuli alikuwa ameshawajulisha maafisa
wenzangu kuhusu kazi niliyoteuliwa kwenda kuifanya. Maafisa hao
walinipongeza kwa dhati kwa uteuzi huo, na kunishauri kuzingatia
miiko ya idara wakati wote wa operesheni. Baada ya kuagana na
kutakiana heri, nilitoka nje na kuingia katika gari ya DSO iliyokuwa
tayari kunipeleka Oysterbay.
Morgan ndiye aliyechukua jukumu la kuendesha gari hiyo aina ya
Mitsubishi Pajero. Lengo lilikuwa aniteremshe Oysterbay na kurudi
nayo ofisini ili iweze kutumika kwa kazi nyingine. Katika hali ya
kawaida ningeweza kutumia pikipiki yangu kwenda sehemu yoyote
ninayotaka; Lakini kwa sababu za kiusalama, niliamua kutoitumia
kabisa katika kipindi chote cha operesheni.
Tukiwa njiani tuliendelea kuzungumzia tukio la kulipuliwa kwa
ubalozi wa Marekani. Morgan alinieleza kuwa mmoja wa maaskari
waliofika katika ubalozi huo mara tu baada ya tukio ni mpwa wake,
anayefanya kazi kituo cha polisi Oysterbay. Askari huyo alishiriki kwa
kiasi kikubwa katika kazi ya uokoaji, na udhibiti wa usalama ubalozini
hapo. “Nakushauri umtafute, kuna uwezekano mkubwa akawa na
taarifa zitakazokusaidia” Aliniambia huku akinipa kipande cha karatasi
chenye jina na cheo cha askari huyo. Nilikipokea kikaratasi hicho na
kukiangalia kwa dakika kadhaa. Niliporidhika kuwa nimeshalishika jina
na cheo cha askari huyo nikamrudishia. Morgan akakipokea na
kukiweka kwenye mfuko wa shati alilokuwa amevaa. Baada ya hapo
tukaendelea na mazungumzo mengine, tukijaribu kupapasa huku na
kule jinsi tukio zima lilivyofanyika.
Kutoka Ilala boma tulichukua barabara ya Kawawa kuelekea
Kinondoni, kupitia Kigogo, Magomeni mapipa, Kinondoni mkwajuni,
hadi Moroco. Maeneo hayo yote hali ilikuwa shwari. Wananchi
waliendelea kufanya kazi zao, na kutembea mitaani kana kwamba
hakuna jambo lolote la ajabu lililotokea. Tofauti pekee tuliyoiona ni
ongezeko la askari polisi wenye silaha eneo la Magomeni, kwenye
makutano ya barabara za Morogoro na Kawawa. Hata hivyo askari hao
walikuwa katika hali ya utulivu hali iliyosaidia kutowatia hofu wananchi.
Tulipofika eneo la Moroco tukaiacha barabara ya Kawawa na
kuingia kulia, kufuata barabara ya Ali Hassan Mwinyi. Barabara hiyo
ilituongoza hadi karibu na eneo la tukio (ground zero). Hapo tulikata
kushoto kufuata barabara ndogo iliyotuingiza mtaa wa Bongoyo.

35
GO DW IN C H IL EWA | 36

Taratibu Morgan aliendesha gari kufuata mtaa huo hadi tulipoiona


nyumba namba RST23 (Mtaa/nyumba halisi imehifadhiwa)
Ilikuwa nyumba kubwa, na nzuri kama zilivyo nyumba zote za
Oysterbay. Wakati huo nyumba za maeneo hayo zilikuwa zikimilikwa
na serikali, na wengi wa wakazi wake walikuwa watumishi wa ngazi za
juu serikalini, wakurugenzi wa mashirika ya umma, au viongozi
wastaafu. Jambo ambalo wananchi wengi hawakujua, ni kwamba idara
ya Usalama wa Taifa ilikuwa ikimiliki nyumba kadhaa maeneo hayo.
Idara ilizitumia nyumba hizo kama ofisi, makazi ya maafisa wake, au
nyumba salama za kificho (safe house) kwa ajili ya kazi maalum. Kwa
kuwa ilikuwa mara yangu ya kwanza kufika hapo, sikuwa na hakika
kama nyumba hiyo ilikuwa ofisi, au safe house.
Katika hali ya kawaida nilitarajia kukuta hali ya utulivu katika eneo
lote linalozunguka nyumba hiyo; lakini haikuwa hivyo. Kuanzia umbali
wa mita mia moja hivi kutoka mahali ilipo nyumba yaliegeshwa magari
yasiyopungua kumi na tano. Magari mawili aina ya Landrover 110 ya
jeshi la polisi yaliegeshwa kwenye majani, nje kabisa ya barabara. Ndani
ya magari hayo walikuwemo askari kumi na wawili waliovaa sare na
wanne waliovaa kiraia. Yalikuwepo pia magari mengine ya aina
mbalimbali ikiwa pamoja na Landcruiser, Nissan Patrol, Toyota Hiace
na mengineyo. Magari haya yaliegeshwa kando ya barabara, huku
madereva wake wakiwa kwenye usukani wakisubiri maelekezo.
Baadaye nilifahamishwa kuwa magari hayo (rental car) yalikodiwa na
ubalozi wa Marekani kwa ajili ya kutumiwa na maafisa wa FBI na
wageni wengine wa ubalozi huo. Lango kuu la kuingilia kwenye jengo
lilikuwa wazi kuruhusu watu waliokuwa wakiingia na kutoka. Pembeni
ya lango hilo alisimama mwanajeshi wa Marekani (Marines) mweusi,
mwenye mwili uliojengeka vema. Alivalia nguo za vita (fatigue combat
uniform), na radio ndogo ya mawasiliano kifuani kwake. Mkononi
alishikilia bunduki ya kivita aina ya M4 Carbine tayari kwa
mapambano. Kwenye paja la mguu wake wa kulia alining’iniza mfuko
maalum (hoster) uliohifadhi bastola kubwa aina ya Kimber 1911.
Mita kumi hivi kutoka mahali aliposimama mwanajeshi huyo
kulikuwa na lundo la magunia yaliyojazwa mchanga, na kupangwa
vizuri kutengeneza nusu duara yenye urefu wa mita tano kwenda juu,
na kipenyo cha mita sita hivi. Nilitambua maramoja kuwa hiyo ni
ngome ya kuzuia mashambulizi ya risasi. Hatua chache nyuma ya
ngome hiyo walisimama marines wawili, mmoja akiwa nyuma ya
bunduki kubwa aina ya machine gun iliyowekwa juu ya magunia ya

36
37 | SH U H U DA ZA J A SU SI – NDA NI YA IDA RA

mchanga. Mwanajeshi wa tatu alisimama pembeni akiwa ameshikilia


kiona mbali (darubini) huku bunduki ya kivita aina ya M4 Carbine
ikining’inia kifuani kwake, mdomo wa mtutu ukitazama chini.
Mbele zaidi, karibu na jengo kulikuwa na wanajeshi wengine
wapatao kumi na tano hivi wakizunguka zunguka. Wanajeshi sita kati
yao walikuwa wameshikilia bunduki kubwa za kivita. Waliobaki
walibeba bastola kwenye mifuko (hoster) zilizofungwa mapajani mwao,
au kifuani upande wa kwapa la kushoto. Pamoja nao walikuwepo watu
wengine zaidi ya hamsini, wengi wao wakiwa wazungu, na wachache
wakiwa na asili ya Afrika. Hawa walivaa suruali za khaki zenye mifuko
mingi (cargo pants) au jeans na fulana za rangi mbalimbali. Watu hawa
walikuwa wakiingia na kutoka katika jengo, kutoa masanduku ya vifaa
na kuvipanga uwanjani hapo.
Kwa sekunde kadhaa nilijiuliza kama nimepotea au vipi. Sura
zilizokuwa mbele yangu zilinifanya nijione kama niko nje ya Tanzania.
Lakini nilipogeuza shingo kidogo kutazama kushoto, nikaona kundi la
watu wapatao kumi na nne hivi, wakiwa wamejikusanya chini ya mti
wakizungumza. Mara moja niliwatambua watu watano kati yao kuwa
ni maafisa wa idara ninaowajua vema.
“Inaelekea maafisa wa FBI waliokuja nchini wako hapa” Morgan
aliniambia huku akiegesha gari katika sehemu wazi iliyokuwa kando ya
barabara.
“ Nadhani, maana panaonekana kama kambi ya jeshi” Nilimjibu.
“Wamarekani ndivyo walivyo. Huwa hawafanyi utani kwenye masuala
ya usalama. Kila wakienda sehemu yoyote ya hatari, hujiandaa vilivyo
kwa mapambano” Morgan aliongezea.
“Ni kweli” Nilimjibu huku akili yangu ikiwa mbali kidogo.
“Nenda karipoti. Mimi nitaegesha gari hapa kwa dakika kumi hivi.
Kama si hapa, au utahitaji kwenda pahala pengine, njoo nikukimbize
haraka. Lakini kama dakika kumi zkipita bila kukuona, nitajua umefika.
Nitapiga gari moto kurudi ofisini” Morgan aliniambia huku akinipa
mkono kunitakia heri kwa mara nyingine. Nikamshukuru na kuteremka
kwenye gari. Haraka haraka nikatembea kuliendea lango kuu.
Kama nilivyotarajia mwanajeshi aliyekuwa langoni alinizuia,
akataka nijitambulishe kabla ya kuingia. Nikamueleza kwa kifupi mimi
ni nani, na kwa nini nilikuwa pale. Baada ya maelezo hayo
nikamuonesha kitambulisho changu. Bila kusema neno mwanajeshi
huyo akakiangalia kitambulisho hicho kwa makini. Halafu kama
kwamba hakuridhika na alichokiona, akatoa simu ya mkononi

37
GO DW IN C H IL EWA | 38

iliyokuwa mfukoni mwake na kupiga namba fulani. Upande wa pili


ulipopokea tu, akataja jina langu na kuuliza kama naruhusiwa kuingia.
Baada ya kupokea maelezo mafupi, akakata simu na kunielekeza mahali
walipokuwa maafisa wenzangu.
Niliwakuta maafisa wa idara (TISS) wapatao kumi na nne, wakiwa
wamesimama kimya, wakimsikiliza kwa makini mzee Zuberi. Yeye
ndiye aliyekuwa mkuu wa usalama wa Taifa mkoa (RSO) Dar es salaam
wakati huo. Kwa wadhifa aliokuwanao kulinganisha na maafisa
wengine waliokuwepo, nikahisi bila shaka ndiye aliyepewa jukumu la
kuongoza kikosi kazi (task force)
“Shikamoo mkuu” Nilimwamkia mara tu nilipoona ameacha kutoa
maelezo na kunitazama usoni.
“Marahaba Chilewa, hujambo?
Alinijibu kwa sauti kavu.
“sijambo mkuu”
“Nani amekwambia uje hapa?
Aliniuliza kwa sauti kali huku akinikazia macho.
Sikuwa nimelitarajia swali hili hivyo nilijisikia unyonge kidogo. Kwa
heshima nikamjibu “DSO, mama Murusuli ndiye aliyenituma” .
“Mimi ndiye RSO sasa mama Murusuli anawezaje kukwambia uje
huku bila idhini yangu? Isitoshe hii ni operesheni ya makao makuu,
ambayo haihusiani na Wilaya ya Ilala, sasa mama Murusuli anawezaje
kukupangia kuja kufanya kazi na wageni bila kibali?
Mzee Zuberi aliendelea kunihoji kwa ukali bila kujali kundi la
maafisa wengine waliokuwepo. Kwa dakika kadhaa nilijisikia kama
niliyevuliwa nguo. Pembeni yangu alikuwepo DSO wa Kinondoni,
mzee Chezi, afisa Mfaume kutoka Kanda, maafisa Galus, MTW, na
wengineo walionijua vema. Wote walinitazama kwa mshangao huku
wakijiuliza imekuwaje nimejipeleka katika kazi hiyo bila kuambiwa.
“Samahani mkuu” nilisema kwa unyenyekevu.
“Mama Murusuli alipigiwa simu na DOI, mzee Walingozi kumtaka
anijulishe nije kuripoti kwenye kikosi kazi.” Nilijitetea.
“Haiwezekani” Mzee Zuberi alinikatiza.
“Hivi wewe Chilewa ni mgeni katika idara? Aliniuliza kwa ukali.
“Hapana mkuu” Nilimjibu.
“Hebu mwambieni huyu” Alisema akiwaangalia maafisa wengine.
“Idara ina chain of command. Haiwezekani hata siku moja DOI ampigie
simu DSO (Mama Murusuli) eti kumpa maagizo, bila kuniambia mimi

38
39 | SH U H U DA ZA J A SU SI – NDA NI YA IDA RA

(RSO) jambo hilo halipo. Pili mimi nina majina ya maafisa wote
wanaotakiwa kuwepo hapa. Jina lako Chilewa halipo.”
Nikabaki kimya, maana sikuwa na jibu lolote.
“Kwa hiyo Chilewa sasa hivi ondoka. Rudi kwenye kituo chako cha
kazi. Na ukifika tu, andika maelezo kwa nini umekuja kwenye kazi
inayohusisha wageni (FBI) bila kibali. Halafu maelezo yako mpe DSO,
mama Murusuli aniletee ofisini kwangu kesho asubuhi. Umenielewa?
Alimaliza huku akinitazama kwa ukali.
“Nimekuelewa mkuu” Nilijibu huku nikihisi jasho jembamba
likitiririka usoni kwangu. Kwa aibu nikageuka na kuondoka taratibu
kuelekea lango kuu. Vishindo vya hatua zangu vilisindikizwa na
vicheko, miguno, na minong’ono ya maafisa wenzangu, waliokuwa
wakinishangaa kwa kitendo nilichofanya.
Morgan alikuwa akijiandaa kuondoa gari kurudi ofisini.
Aliponiona nikitembea haraka haraka kumfuata, akanisubiri ili
anipeleke ninapotaka kwenda.
“Vipi Chilewa, kulikoni? Mbona sura imekubadilika?”
Aliniuliza mara tu nilipofungua mlango wa Pajero na kujirusha katika
kiti cha abiria.
“Turudi ofisini” nilimwambia huku sauti yangu ikiwa na mitetemo.
“Kazi hamuanzi leo? Au mnakutana baadae?
“Hapana, RSO mzee Zuberi amenifukuza” Nilimwambia huku
nikijaribu kutabasamu kuzuia hasira iliyokuwa imeanza kunipanda.
“Amekufukuza? Una maana gani? Aliniuliza kwa mshangao.
Bila kuficha nikamueleza mambo yote tangu mwanzo hadi mwisho.
“Unasema ulimwambia kuwa DOI amepiga simu yeye mwenyewe
kumpa maagizo DSO ? Morgan aliniuliza kwa mshangao
“Nimemwambia kila kitu”
“Na bado akasisitiza uondoke?
“Ndiyo”
“Siamini” Morgan alijibu kwa mshangao.
“Wakati tunazungumza maafisa wote walikuwepo, kwa hiyo siwezi
kupunguza wala kuongeza neno” Nilimwambia kwa kusisitiza baada ya
kuona haniamini.
“Siyo sikuamini, nashangaa kwamba RSO amekataa maagizo ya
DOI mbele ya maafisa wote hao. Anajipalia makaa ya moto”
“Labda kuna mabadiliko. Inawezekana DOI alibadili uamuzi wake
baada ya kuongea na mama Murusuli. Au pengine kuna jambo
tusilolijua”

39
GO DW IN C H IL EWA | 40

“Kama DOI angebadili uamuzi wake lazima angempigia simu


DSO kumwambia urudi ofisini; na bila shaka mama Murusuli angetuita
kwenye radio kutujulisha turudi ofisini. Nadhani kuna jingine” Morgan
alimalizia huku akiondoa gari taratibu.

5
Ofisini tuliwakuta maafisa wenzetu wakiwa wamesharudi kwenye
madawati yao. Maafisa hao walishangaa mno kuniona, kwani walikuwa
na hakika kazi niliyokuwa nikienda kuifanya ingechukua muda mrefu
kuikamilisha. Hata hivyo hatukuwa na sababu ya kuwaeleza
kilichotokea. Sote wawili tukaenda moja kwa moja ofisini kwa DSO.
Tulimkuta Mama Murusuli akiwa bado ameketi mahali palepale,
akisoma mojawapo ya mafaili yaliyokuwa mezani kwake. Alipotuona
tukiingia, akafunga faili hilo na kutugeukia
“Vipi?” aliuliza kwa mshangao
“RSO amenirudisha” Nilimjibu huku nikivuta kiti na kukaa.
Morgan naye akazunguka na kukaa katika kiti kilichokuwa upande wa
pili wa meza.
“Una maana RSO Zuberi? Aliuliza kwa mshangao.
“Ndiyo”
“Yeye kakurudisha kama nani?
“Nadhani yeye ndiye anayeongoza task force. Sina uhakika, maana
sikupewa utambulisho wowote”
“Ulimwambia kwamba DOI ndiye ameagiza uende?
“Nimwambi” Nikamueleza kila kitu kilichotokea tangu nilipofika hadi
mahali hapo hadi tulivyoondoka. Sikuishia hapo tu, nikamueleza pia
jinsi nilivyojisikia kwa kudhalilishwa mbele ya maafisa wenzangu.
“Usijisikie vibaya Chilewa. Mzee Zuberi ndivyo alivyo, ana
misimamo ya ajabu. Sisi tumeshamzoea. Wewe ulikuwa hujaingia
kwenye aanga zake ndiyo maana umeshituka hivyo” Mama Murusuli
alijaribu kunipooza huku akicheka.
“Ngoja nimpigie simu nimfahamishe kuwa DOI ndiye aliyeagiza
uwepo kwenye hiyo task force” alimalizia.
“Samahani mkuu” Morgan alidakia “Kwa mujibu wa maelezo ya
Chilewa, inaonekana RSO hakufurahishwa na kitendo cha DOI
kupigia simu moja kwa moja kwako, badala ya kumpigia yeye. Kwa
hiyo ukimpigia, mnaweza msielewane vema. Maana hata kule
kumwambia Chilewa aandike maelezo, halafu akupe wewe uyapeleke

40
41 | SH U H U DA ZA J A SU SI – NDA NI YA IDA RA

ofisini kwake ni mtego tu. Anachojaribu kufanya ni kuku- victimize


uonekane umekiuka taratibu za idara. Hatujui kwa lengo gani”
“Unalosema ni kweli Morgan, RSO hakufurahia DOI kunipigia
simu moja kwa moja. Lakini hatujui kwa nini aliamua kufanya hivyo.
Hatujui kama alijaribu kumtafuta, hakumpata, au kama taarifa
ilipelekwa ofisini kwake kupitia ufundi ikachelewa kumfikia. Lakini pia
hatuwezi ku rule out kwamba DOI aliamua makusudi, kutomwambia
kwa sababu zake binafsi. DOI ni mtu mkubwa mno. Anaweza kufanya
lolote analoona ni sahihi. Ndiyo maana nilitaka nimtahadhalishe
Zuberi asije akajichanganya” Mama Murusuli alisisitiza.
“Vyovyote unavyoona sahihi mkuu. Lakini kama ulivyosema, RSO
ana misimamo yake ya tofauti. Mimi nakushauri umpigie DOI,
umweleze kuwa Chilewa amekwenda kuripoti katika task force kama
alivyoagiza, lakini RSO amemrudisha. Sasa DOI ndiye aamue la
kufanya. Kama ni kumpigia Zuberi au la”
“Ushauri mzuri Morgan, ngoja nimpigie DOI”
Mama Murusuli alisema huku akinyanyua kikonyo cha simu ya mezani
na kuzungusha namba za ofisini kwa DOI.
Haikuchukua sekunde therathini operator wa makao makuu akajibu
na kumuunganisha na DOI. Taratibu mama Murusuli akamueleza
mzee Walingozi mambo yote yaliyotokea tangu mwanzo hadi mwisho.
“Zuberi anathubutuje kumrudisha mtu niliyemteua mimi kuwemo
katika task force? DOI alisema kwa ukali baada ya mama Murusuli
kumaliza maelezo yake.
“Hajui kuwa Chilewa ndiye alikuwa afisa wa kwanza kufika katika eneo
la tukio, na taarifa yake ndiyo iliyoweka msingi wa taarifa
tuliyomwandikia rais? Ana sababu gani za kumrudisha? Aliuliza kwa
mshangao
“Sijui mkuu, hata mimi bado najiuliza” DSO alijibu
“Kwa hiyo Chilewa amerudi ofisini, yuko hapo?
“Yupo mkuu, amerudi hapa amenyong’onyea kabisa”
“Nipe nizungumze naye”
“sawa mkuu” Mama Murusuli alijibu kwa heshima, kisha akanipa
kikonyo cha simu.
“Chilewa hapa mkuu” Nilisema baada ya kuweka kikonyo cha simu
kwenye sikio langu la kulia.
“DSO amenieleza yaliyotokea, pole sana”
“Ahsante mkuu”
“Nini hasa kilichotokea? Hebu nieleze vizuri”

41
GO DW IN C H IL EWA | 42

Kwa uangalifu mkubwa nikamueleza mambo yote yalivyokuwa, tangu


nilipotia mguu wangu kituoni hapo, hadi nilipoondoka.
“Kwa hiyo maafisa wote walisikia mlichozungumza”
DOI aliuliza mara tu nilipomaliza maelezo yangu.
“Ndiyo mkuu”
“Una hakika ulimwambia kuwa mimi ndiye niliyetoa maagizo
uende kwenye task force”
“Ndiyo mkuu”
“Na bado akasisitiza uondoke”
“Ndiyo mkuu, alisema yeye anayo majina ya watu wote
walioteuliwa kushiriki kwenye task force, lakini jina langu halimo”
Nilieleza taratibu huku moyo wangu ukiongeza mapigo kwa kujua
uzito wa maneno niliyokuwa nikiyasema. Nilijua idara huwa haina
mzaa, mambo yakibadilika huwa balaa!
“Ahsante kwa maelezo yako Chilewa. Mwambie mama Murusuli
nampigia RSO, nikimaliza kuzungumza naye nitampigia tena” DOI
alimaliza na kukata simu.
Kwa dakika tano hivi mimi, Mama Murusuli na Morgan tukabaki
ofisini hapo tukizungumza, wakati tukisubiri simu ya DOI. Mama
Murusuli ndiye aliyekuwa msemaji mkuu, akituonya na kutuelimisha
umuhimu wa nidhamu kazini, na hatari ya kujiamini kupita kiasi.
“RSO angeweza kuzuia malumbano haya kwa kupiga simu ofisini
kwa DOI kuthibitisha uteuzi wa Chilewa. Lakini kujiamini kwake,
kumefanya mambo yawe makubwa” Alieleza mama Murusuli.
Wakati tukiendelea kutafakari hayo, simu ikaita tena. Mama
Murusuli akainyanyua na kuita “Halow”
“DSO ni DOI tena hapa”
“Ndiyo mkuu”
“Nimeongea na Zuberi. Ameniambia eti Chilewa alimwambia
ametumwa na DSO kwenda pale, ila hakufafanua kuwa mimi ndiye
niliyeagiza awemo katika task force. Hiyo ndiyo sababu pekee iliyofanya
amrudishe. Kwa hiyo, mwambie Chilewa, aondoke hapo sasa hivi,
arudi kwenye task force, na atakuwa huko mpaka atakapopewa maagizo
mengine toka kwangu, au toka kwa DGIS. Nimemwagiza Zuberi
anipigie simu mara tu Chilewa atakapofika”
“Timamu mkuu” Mama Murusuli alijibu.
Baada ya mazungumzo mengine yasiyonihusu, DOI akakata simu.

__________

42
43 | SH U H U DA ZA J A SU SI – NDA NI YA IDA RA

SURA YA PILI

IDARA (TISS)

T
ukio la kulipuliwa kwa ubalozi wa Marekani jijini Dar es
salaam, lilikuwa kama kengele ya tahadhari kwa vyombo vya
ulinzi na usalama vya Tanzania. Kwa miaka mingi nchi hii
ilikuwa ikisifika kama kisiwa cha amani katika Afrika, hali
iliyoifanya kuwa kimbilio la wakimbizi. Wakati Kongo DRC, Rwanda,
Burundi, Uganda, na nchi nyingine jirani zikikumbwa na migogoro ya
kisiasa, au vita vya wenyewe kwa wenyewe, watanzania waliendelea
kuwa wamoja, watulivu, na wavumilivu hata pale walipokosa sukari, au
mchele wa kuwalisha watoto wao. Utulivu huo ulichangiwa kwa kiasi
kikubwa na misingi ya siasa ya ujamaa na kujitegemea, iliyoasisiwa
mwaka 1967 na baba wa taifa, mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Misingi hiyo iliyojulikana kwa jina la Azimio la Arusha, pamoja na
lugha ya Kiswahili vilijenga umoja wa kitaifa na kuimarisha heshima ya
ki utu isiyojali kabila, lugha, wala udini.
Pamoja na utulivu huo, idara ya usalama wa Taifa (TISS) chini ya
mkurugenzi mkuu Emilio Mzena ilikabiliwa na changamoto za kila
namna. Baadhi ya changamoto hizo zilitokana na uchanga wa Taifa
kisiasa na ki-uchumi. Tanzania ilipata uhuru wake mwaka 1961 kutoka

43
GO DW IN C H IL EWA | 44

kwa Waingereza ambao walilipokea taifa hili toka Umoja wa Mataifa.


Hii ilikuwa baada ya Ujerumani kunyang’anywa makoloni yake kufuatia
kushindwa katika vita kuu ya pili ya dunia. Ki msingi Uingeleza
ilikabidhiwa taifa hili si kwa lengo la kulitawala bali kulilea mpaka
litakapokuwa tayari kujitawala. Hata hivyo, chini ya uangalizi wa
waingeleza, Tanzania (wakati huo Tanganyika Territory) ilishuhudia
unyonyaji, ukandamizaji na ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu
sawasawa na ule uliokuwepo wakati wa utawala Mjerumani. Kwa
sababu hiyo, ilipopata uhuru wake Tanganyika ililazimika kujipanga
upya kwa kujenga misingi imara ya siasa, uchumi na utamaduni wake.
Changamoto nyingine ilikuwa vita baridi iliyokuwa ikiendelea kati
ya mataifa ya maghalibi na mashariki. Katika kipindi hicho mataifa ya
Ulaya mashariki (Urusi, China, Korea, Poland, Ujerumani mashariki
n.k) yalikuwa yakifuata siasa na uchumi wa kikomunisti/kisoshalisti
unaotia msukumo kwa serikali (umma) kumiliki njia kuu za uchumi na
kuzitumia kwa manufaa ya wote. Siasa hizo zilipingwa vikali na mataifa
ya magharibi (Marekani, Uingereza, Ujerumani maghalibi n.k)
yaliyokuwa yakifuata siasa za kibepari (Capitalism / Market economy)
zinazotia msukumo kwa mtu mmoja mmoja (Individualism/private sector)
kumiliki njia kuu za uchumi. Ili kupanua dola zao kiuchumi na kiulinzi,
kutafuta kuungwa mkono, na kusambaza siasa zake ulimwenguni,
mataifa ya mashariki yalijenga urafiki na kuzisaidia nchi changa
(zilizopata uhuru wake karibuni), vyama vikubwa vya siasa vyenye
muelekeo wa kuchukua dola, na vikundi vya wapigania uhuru katika
nchi zaAfrika, Asia, na Mashariki ya kati. Mkakati huo ulisaidia siasa za
kisoshalisti kusambaa duniani kwa kasi kama moto wa gesi.
Kukabiliana na hali hiyo, mataifa ya magharibi chini ya usimamizi
wa Marekani yalianzisha mpango maalum wa kuzuia kuenea kwa
ukomunisti duniani. Mpango huo uliojulikana kama Sera ya Udhibiti
(Policy of Containment) ulilenga kuudumaza ukomunisti kwa kuhakikisha
hauvuki mipaka au kusambaa katika nchi mpya; bali unabaki ndani ya
nchi ambazo tayari zimeshaupokea. Katika kufanikisha sera hiyo,
Marekani ilitumia idara yake ya kijasusi (CIA) kuhujumi uchumi wa
nchi changa zilizoukaribisha ukomunisti, kuwaondoa madarakani
viongozi wenye msimamo wa kikomunisti, na kuweka vibaraka wao.
CIA pia ilitumia vibaraka wake na kusambaza uzandiki (propaganda)
kwa wananchi kuchochea wachukie na kupinga sera za kikomunisti.
Tanzania ilijikuta ikiwa muhanga wa vita hivi mara tu baada ya
kutangaza kufuata mfumo wa siasa ya ujamaa na kujitegemea, chini ya

44
45 | SH U H U DA ZA J A SU SI – NDA NI YA IDA RA

mwongozo wa Azimio la Arusha. Mataifa makubwa ya kimagharibi


hususan Marekani, Uingereza na Ujermani yalianzisha mikakati
mbalimbali ya siri, iliyokuwa na lengo la kuiyumbisha Tanzania kisiasa,
kiuchumi na kiutamaduni, ili iweze kusalimu amri na kutupilia mbali
siasa ya ujamaa na kujitegemea.
Kufuatia hali hiyo malengo ya idara ya usalama wa Taifa chini ya
uongozi wa Dr. Lawrence Gama, aliyeteuliwa mwaka 1975 yalijikita
zaidi katika kupiga vita mfumo wa siasa na uchumi wa kibepari
(unyonyaji), kuzuia hujuma na uzandiki uliochochewa na vita baridi, na
kuweka mikakati ya kufuta ujinga ili kuimarisha umoja. Pamoja na hayo
idara ilishiriki vema katika kusaidia vita vya ukombozi wa kusini mwa
Afrika. Kwa kutumia maafisa na sources wake idara ilihusika moja kwa
moja katika kupanga mikakati ya vita, kukusanya habari za kiusalama
dhidi ya adui (ujasusi) na kutoa mafunzo ya kijeshi kwa wapiganaji wa
Msumbiji, Afrika ya Kusini, Namibia, na Zimbabwe.
Mwaka 1978 hali ilikuwa tete zaidi baada ya majeshi ya rais Iddi
Amin Dada wa Uganda kuvamia upande wa kaskazini wa mto Kagera
na kuikalia kimabavu. Uvamizi huo ulipelekea Tanzania kuingia katika
vita kali ya kuyaondoa majeshi hayo katika ardhi ya Tanzania, na
kuwakomboa waganda kutoka utawala wa Iddi Amin Dada, aliyekuwa
amejipa urais wa maisha. Ingawa vita hiyo ilidumu kwa muda wa
mwaka mmoja tu, madhara yake kisiasa na kiuchumi yaliendelea
kuonekana kwa zaidi ya miaka therathini. Uchumi wa Tanzania
uliyumba na kufanya hali ya Maisha ya wananchi kuwa ngumu. Katika
kipindi hicho Idara ya usalama wa Taifa chini ya uongozi wa Dr. Hansy
Kitine (1978) licha ya kuendelea na mapambano ya kisiasa na kiuchumi,
pia ililazimika kuendelea na mikakati yake ya kusaidia wapigania uhuru
wa Zimbabwe, Namibia na Afrika ya kusini kwa kutoa mafunzo, na
kushiriki katika operesheni mbalimbali.
Kati ya mwaka 1980 hadi 1983 idara chini ya uongozi wa Dr.
Augustine Mahiga ilijikuta ikilazimika kuelekeza nguvu kubwa zaidi
katika kulinda uchumi, kwa kupambana na uhujumu uchumi. Hali hiyo
ilisababishwa na uhaba mkubwa wa bidhaa muhimu uliojitokeza baada
ya vita ya kuikomboa Uganda. Licha ya kutumia mabilioni ya fedha za
kigeni katika vita hivyo, Tanzania ilijikuta ikiwa na wajibu wa
kuwasaidia wananchi wa Uganda waliokuwa wameathiriwa vibaya na
utawala mbovu wa rais Iddi Amini. Baada ya kumalizika kwa vita
waganda walijikuta wakiwa na upungufu mkubwa wa chakula, mafuta,
madawa ya hospitali, sukari, sabuni, vifaa vya shule, na bidhaa nyingine

45
GO DW IN C H IL EWA | 46

muhimu kwa matumizi ya kila siku. Kwa sababu za ki-utu, serikali ya


rais Julius Kambarage Nyerere iliamua kuokoa maisha ya wananchi hao
kwa kuwapelekea bidhaa walizokuwa wakihitaji. Uamuzi huo uliokoa
Maisha ya waganda na kutengeneza jina zuri la Tanzania katika jumuia
ya kimataifa; lakini, uliigharimu serikali ya Tanzania fedha nyingi na
kusababisha uhaba mkubwa wa bidhaa nchini.
Uhaba ulipoanza kujitokeza, wafanya biashara wakubwa, na baadhi
ya watu wenye mamlaka, walianzisha utaratibu haramu wa kununua
bidhaa kwa wingi, na kuzificha katika maghala ili kusababisha
mfumuko wa mahitaji.. Baada ya kusababisha taharuki, ndipo
walipozitoa na kuziuza kwa siri, na kwa bei ya juu kuliko kawaida. Hali
hii ilisababisha usumbufu mkubwa kwa wananchi, na kuzidi
kuyumbisha uchumi wa taifa uliokuwa ukichechemea.
Katika kipindi hicho idara ya usalama wa Taifa ilifanya kazi kubwa
ya kudhibiti vuguvugu la mapinduzi ya kijeshi yaliyokuwa yameshamiri
katika nchi nyingi za kiafrika, na kujipenyeza katika Tanzania.
Vuguvugu hilo kwa kiasi kikubwa lilichochewa na hali ngumu ya
maisha iliyofanya wengi wasiyaone matunda ya uhuru. Mwaka 1982/83
idara ilifanikiwa kuzima jaribio la Mapinduzi ya kijeshi lililopangwa na
maafisa wachache wa jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ)
wakiongozwa na Thomas Lugangila (Uncle Tom), Kepteni Zacharia
Hanspope, Kepteni Kadego, Kepteni Hatibu Ghandi (Hatty McGee),
Kepteni Eugene Maganga, Luteni Vitalis Mapunda, Luteni Pius
Lugangila, na Luteni Kajaji Badru. Maafisa hao walikamatwa na
kufunguliwa kesi ya uhaini iliyosikilizwa mwaka 1985. Afisa mwingine
Kepteni Tamimu aliuawa kwa kupigwa risasi na afisa usalama wa Taifa
Radi Simba, wakati wa jaribio la kumkamata lililofanyika maeneo ya
Kinondoni mkwajuni, jijini Dar es Salaam.
Tarehe 12 April mwaka 1984, Idara ya Usalama wa Taifa ilipata
pigo kubwa baada ya aliyekuwa waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Edward Moringe Sokoine kufariki katika ajari ya gari
iliyotokea eneo la Wami - Dakawa, nje kidogo ya mji wa Morogoro.
Msafara wa waziri mkuu ukilindwa na maafisa wa TISS ulipata ajali
hiyo ukitokea Dodoma alikokuwa amekwenda kuhudhuria kikao cha
Bunge. Gari aina ya Land Cruiser iliyomgonga ilikuwa ikiendeshwa na
Dumisan Dube, mkimbizi wa Afrika ya kusini, aliyekuwa akiishi
kwenye kambi ya wakimbizi, Mazimbu. Edward Sokoine ndiye
kiongozi aliyekuwa akitarajiwa kurithi kiti cha rais Julius Kambarage
Nyerere, aliyekuwa ametangaza kupumzika uongozi mwaka 1985.

46
47 | SH U H U DA ZA J A SU SI – NDA NI YA IDA RA

Kifo hicho kilizua mtafaruku mkubwa miongoni mwa wananchi,


na hasa wanasiasa. Wako walioituhumu idara kwa kutumiwa na baadhi
ya wanasiasa kupanga mauaji hayo, kwa lengo la kuteka nafasi ya urais.
Wengine waliwatuhumu viongozi wa juu, hususan mawaziri wakuu
wastaafu Rashid Mfaume Kawawa, Cleopa Msuya, na Salim Ahmed
salim kwa kutumia nguvu za giza (uchawi) kumuua kiongozi huyo.
Wako pia waliovumisha kuwa mauaji hayo yalipangwa na rais Nyerere
mwenyewe baada ya kuona Sokoine ataipeleka nchi pabaya. Kadri
muda ulivyokwenda tuhuma hizo zilipuuzwa na kuthibitika kuwa ni
uzushi usiokuwa na ushahidi. Hata hivyo idara ya Usalama wa Taifa
ilifanya kazi kubwa ya kujisafisha na kuzuia kifo hicho kisisababishe
machafuko nchini.
Katika miaka ya 1983 hadi 1955, idara chini ya uongozi wa Meja
Jenerali Imran Kombe ilipata mafanikio makubwa kutokana na
ushirikiano kutoka kwa wananchi. Idara iliwatumia vema vijana
waliopitia mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa mujibu wa
sheria, na wazee waliopitia mafunzo ya mgambo katika kukusanya na
kutoa taarifa kwa hiari, na mara nyingine bila kujua. Kimsingi mawazo,
misingi na itikadi za ujamaa na kujitegemea ziliwasukuma watanzania
wengi kujivunia utaifa wao, na kuonesha uzalendo kwa kujitolea
kulitumikia taifa kwa hali na mali.
Hali ilianza kubadilika mwaka 1985 baada ya mheshimiwa Ali
Hassan Mwinyi kuapishwa kuwa rais wa pili wa Jamhuri ya muungano
wa Tanzania. Rais huyu alifanya kazi kubwa ya kubadilisha mfumo wa
siasa na uchumi kutoka ujamaa asilia, kwenda kwenye mfumo wa
biashara huria. Badala ya kujifungia kibiashara (kwa kulazimisha
matumizi ya bidhaa zinazozalishwa nchini) kwa mara ya kwanza
Tanzania ikafungua mipaka yake. Wafanyabiashara wakaruhusiwa
kuingiza bidhaa za nje nchini, na kuuza bidhaa za Tanzania katika
masoko ya kimataifa chini ya usimamizi wa Board of External Trade
(BET). Uamuzi huu ulisaidia sana kupunguza ugumu wa maisha ya
watanzania, uliotokana na kukosekana kwa bidhaa muhimu.
Mwaka 1989 idara ilikumbwa na jinamizi lingine baada ya magaidi
wa The Mozambican National Resistance (MNR) wa Msumbiji
kuvamia maeneo ya kusini mwa Tanzania. Magaidi hao ambao pia
hujulikana kwa jina la RENAMO (Resistência Nacional Moçambicana) au
BANDITO walianza kuipinga FRELIMO miaka ya 1970 kabla hata
nchi hiyo haijapata uhuru. Magaidi hao walipata nguvu zaidi mwaka
1975 baada ya kuungwa mkono na idara ya ujasusi ya makaburu wa

47
GO DW IN C H IL EWA | 48

Rhodesia (Zimbabwe) Rhodecian Central Intelligence Organization


(CIO) iliyokuwa na lengo la kutokomeza ukomunisti Afrika.
Rhodecian Central Intelligence Organization ilifanya kazi zake kwa
maelekezo, na kwa kushirikiana na shirika la ujasusi la Marekani Central
Intelligence Agence (CIA) lililokuwa likitekeleza sera za kudhibiti
kuenea kwa ukomunisti (Policy of containment)
Uvamizi wa RENAMO ndani ya Tanzania hakikuwa kitu
kilichotarajiwa. Kwa muda mrefu magaidi hawa walikuwa wakipigana
na majeshi ya FRELIMO ndani ya msumbiji, bila kusababisha madhara
kwa watanzania. Mambo yaligeuka baada ya magaidi hao kupokea
kipigo kikubwa kutoka kwa majeshi ya serikali, na kukosa sehemu ya
kukimbilia ndani ya nchi yao. Ndipo walipovuka mpaka kuingia
Tanzania, wakiwa na uhakika kuwa majeshi ya msumbiji hayawezi
kufanya vita ndani ya nchi nyingine.
Wakiwa ndani ya ardhi ya Tanzania, magaidi wa RENAMO
walijikuta wakiishiwa chakula, madawa, sigara, na vitu vingine muhimu
walivyokuwa wakihitaji kuweza kuishi. Ndipo walipoamua kuvamia
vijiji vya mipakani kupora chakula, madawa ya hospitali, mavazi ya
kiraia, na kisha kubaka wanawake kabla ya kurudi msituni kujificha.
Hali hii ilisababisha taharuki kwa wananchi wa maeneo hayo. Wengi
wao waliamua kukimbia makazi yao, na au kukubali kuishi na baadhi
ya magaidi waliovaa kifuniko cha ufanya biashara au uvuvi.
Kudhibiti hali hiyo idara ya Usalama wa Taifa ilifanya kazi kubwa
na kwa ushirikiano wa karibu na jeshi la wananchi wa Tanzania
(JWTZ). Operesheni hiyo iliyofanywa sambamba na nyingine ya
kifuniko (Operesheni uhai) ilihusisha makomando wa TISS na
makomando wa jeshi la wananchi wa Tanzania toka kikosi namba tisini
na mbili (92KJ) Ngerengere. Baada ya kazi ngumu iliyodumu kwa zaidi
ya miezi tisa makomando hao walifanikiwa kuwatokomeza kabisa
magaidi wa RENAMO na kurejesha amani katika mikoa ya kusini.
Mwaka 1988 idara ilijikuta ikiwa katika ‘sintofahamu’ baada ya
kufumuka kwa mageuzi makubwa ya kisiasa na kiuchumi duniani.
Mageuzi haya yaliyochochewa na ‘perestroika’ yalipelekea kuvunjwa
kwa ukuta wa Berlin (mwaka 1989), kusambaratika kwa dola ya Urusi
(United Soviet Socialist Republic) mwaka 1991, na kumalizika kwa vita
baridi (Cold war) kati ya Ulaya magharibi na Ulaya mashariki. Pamoja
na kutotajwa sana katika historia ya Tanzania, mageuzi haya ki-halisia
ndiyo yaliyochangia kwa kiasi kikubwa mabadiliko ya jumla ya mfumo
wa siasa na uchumi wa Tanzania, ikiwa pamoja na mfumo, muundo na

48
49 | SH U H U DA ZA J A SU SI – NDA NI YA IDA RA

utendaji wa idara ya usalama wa Taifa.


Miaka mingi kabla ya mageuzi, TISS ilikuwa ikifanya kazi katika
mlengo wa kijamaa, kwa kufuata mfumo wa siasa wa chama kimoja,
chini ya mwamvuli wa ofisi ya rais. Baada ya mageuzi idara ilijikuta
ikilazimika kubadilisha mfumo na malengo yake ili kwenda sambamba
na mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi, na kutengeneza muundo wa
kuiwezesha kufanya kazi zake kwa kujitegemea. Miezi michache baada
ya kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi nchini, idara ilipeleka
mapendekezo ya marekebisho ya mfumo na muundo wa idara kwa rais
Ali Hassan Mwinyi. Mapendekezo hayo yalikataliwa.
Mwaka 1995 rais Benjamin Mkapa alimteua Cornel Apson
Mwang’onda kuwa mkurugenzi mkuu wa idara ya Usalama wa Taifa
badala ya Meja Jenerali Imran Kombe aliyekuwa akistaafu. Cornel
Apson alitumia nafasi ya ukaribu wake na rais Mkapa kupendekeza kwa
mara ya pili mabadiliko ya mfumo na muundo wa idara. Rais Mkapa
aliridhia mapendekezo hayo na kuagiza uandaliwe muswaada ili uweze
kupelekwa bungeni. Miezi michache baadae, muswaada wa sheria ya
usalama wa Taifa (Tanzania Intelligence and Security Service Act No. 15 of
1996) ulipitishwa na bunge, na kusainiwa na rais Benjamin Mkapa
tarehe 20 Januari 1997. Kupitishwa kwa sheria hiyo kunatajwa kuwa
mojawapo ya mafanikio makubwa ya Cornel Apson Mwang’onda,
ambaye wakati wa uongozi wake idara ilikumbwa na misukosuko
mingi, ikiwa pamoja na kulipuliwa kwa ubalozi wa Marekani.

2
Mashambulizi ya mabomu katika ofisi za ubalozi wa Marekani
jijini Dar es Salaam na Nairobi Kenya yalifanyika wakati asilimia kubwa
ya raia wa Marekani wakiwa usingizini. Ingawa jijini Dar es salaam
muda huo ilikuwa ni saa nne na nusu asubuhi, jijini Washington DC
ilikuwa ndiyo kwanza imetimia saa tisa na nusu alfajiri. Muda muafaka
wa kuchapa usingizi. Hata hivyo mamilioni ya wamarekani wanaofanya
kazi za usiku (night shift) viwandani, katika majumba ya starehe,
mahospitalini, na idara nyingine nyeti walikuwa macho kushuhudia
kituo cha televition cha CNN international kikirusha matangazo yake
mubashara kuelezea janga lililotokea.
Kati ya watu waliopata taarifa mapema zaidi, walikuwa Louis
Free, mkurugenzi mkuu wa idara ya ukachelo ya Marekani Federal
Bureau of Investigation (FBI) yenye makao yake makuu jijini Washington
DC na Richard Alan Clarke aliyekuwa mratibu wa usalama wa Taifa,

49
GO DW IN C H IL EWA | 50

ulinzi wa miundo mbinu, na udhibiti wa magaidi (National Coordinator


for security, infrastructure Protection, and Counter terrorism). Mara tu baada ya
kupata taarifa hiyo, Richard Alan Clarke aliitisha kikao cha dharula cha
kikundi maalum cha usalama, kinachoshughulikia kupambana na
ugaidi kijulikanacho kwa jina la Counteterrorism Security Group (kwa kifupi
CSG). Kwa vile baadhi ya wajumbe wa kikundi hiki walikuwa nje ya
Washington DC, Louis Free aliazimiwa kikao kifanyike kwa njia ya
mtandao (Video Conference).
Kikao kilianza saa kumi na moja alfajiri kwa kufunguliwa na Alan
Clarke mwenyewe ambaye kwa wadhifa wake aliyekuwa ndiye
mwenyekiti wa kikao hicho. Waliohudhuria walikuwa ni pamoja na
msaidizi wa rais anayeshughulikia masuala ya Afrika Bibi Gayle Smith,
msaidizi wa waziri wa mambo ya nchi za nje (Assistant Secretary of State
for African Affairs) anayeshughulikia masuala ya Afrika Bibi Susan Rice,
mjumbe wa NSC kutoka wizara ya nishati (Department of Energy) Bibi
Lisa Gordon Hagerty, na wajumbe wengine kutoka idara za ulinzi na
usalama wa nchi hiyo.
Ajenda kuu katika kikao hiki ilikuwa kupanga namna ya
kukabiliana na shambulio lililojitokeza. Mashambulizi ya mabomu jijini
Nairobi, Kenya na Dar es Salaam yalikuwa yamesababisha madhara
makubwa kupita kiasi. Ukiacha idadi kubwa ya watu waliopoteza
Maisha yao, wengine wengi walikuwa bado wamefunikwa kwa vifusi.
Kutokana na kutokuwepo kwa vikosi maalum vya uokoaji, na uhaba
wa vifaa vya kisasa, idadi ya vifo ilitarajiwa kuongezeka kwa kasi.
Msaada wa haraka ulihitajika ili kunusuru maisha ya wahanga hao.
Baada ya majadiliano ya muda mfupi, wajumbe wa CSG
walikubaliana kutumia mawakala wa idara ya uokoaji ya nchi hiyo
Federal Emmergence Management Agency (FEMA) kusaidia katika
mchakato wa uokoaji nchini Kenya na Tanzania. FEMA ina uzoefu
mkubwa katika kukabiliana na majanga, na ina wataalam nguli
waliofuzu kufanya uokoaji katika mazingira ya aina yoyote ile. Louis
Free alipendekeza wataalam hawa waondoke Marekani haraka
iwezekanavyo kwenda Afrika mashariki kusaidia kuoaji wa
waliofunikwa na vifusi, na kupata miili ya waliokufa kabla haijaharibika.
Wajumbe hao pia walikubaliana kutuma ndege ya jeshi inayotoa
huduma za matibabu (Airforce Medical Nightingale Flights) nchini Kenya
na Tanzania, kuwachukua raia wa Marekani waliojeruhiwa na
kuwakimbiza Ulaya kwa ajili ya matibabu ya dharula, kabla ya
kuwapeleka nyumbani (Marekani) kwa huduma zaidi. Pamoja na

50
51 | SH U H U DA ZA J A SU SI – NDA NI YA IDA RA

kuwachukua majeruhi hao, kikao kilikubaliana pia kutoa msaada wa


matibabu kwa wenyeji wote walioathiriwa na mabomu.
Ili kuhakikisha usalama wa wamarekani waliokuwa Kenya na
Tanzania, mratibu wa usalama Bwana Richard Clarke aliiomba wizara
ya Ulinzi (Department of Defense) kutumia makomando wake wa jeshi la
majini (Navy) wanaounda vikosi vya msaada katika mapambano ya
ugaidi Fleet Anti-terrorism Support Teams (FAST) kuimarisha ulinzi katika
vituo muhimu, majengo, na mali (assets) zote za Marekani. Kufuatia
ombi hilo, Department of Defense iliagiza wanajeshi wake (Marines)
kuondoka nchini humo mara moja kuelekea Afrika mashariki.
Jambo la tatu lilihusu kuwatafuta magaidi waliohusika na uhalifu
huo na kuwafikisha katika vyombo vya sheria. Akiwa mkuu wa idara
inayohusika na upelelezi wa tukio hili, Richard Clarke alitambua
umuhimu wa kufanya uchunguzi wa eneo la tukio kabla halijavurugwa,
na kupata maelezo ya mashahidi kabla hawajatoweka. Haya yote
yalitakiwa kufanyika kwa makini ili kuweka msingi wa mashitaka, na
kuwezesha upatikanaji wa wahalifu. Ili kurahisisha utekelezaji wake,
ulihitaji ushirikiano wa dhati kati ya idara yake na vyombo vya usalama
vya nchi husika. Hata hivyo, suala hilo haikuwa sababu ya kuchelewa
kumjulisha John O’neill na mawakala wenzake wa FBI ofisi ya New
York kuondoka mara moja kuelekea Nairobi na Dar es Salaam.
Suala lingine la msingi, ilikuwa namna ya kuzuia matukio mengine
ya kigaidi kutokea katika balozi na vituo vingine vya Marekani duniani.
Wajumbe wa SCG walitambua, na kukubaliana kuwa mashambulizi
katika balozi za Tanzania na Nairobi ni mwanzo tu. Ulikuwepo
uwezekano mkubwa wa matukio mengine mengi kufuatia. Kwa sababu
hiyo ilionekana vema kuwapa mamlaka mabalozi wa Marekani katika
nchi zote kutathimini hali ya usalama, na kufanya maamuzi ya kufunga
au kutofunga balozi zao bila kuwasiliana na Washington DC.
Kabla ya kikao kumalizika, wajumbe walipewa taarifa ya CIA
iliyoeleza kuwa shirika hilo la kijasusi lilikuwa na ushahidi kuwa kundi
la kigaidi liitwalo Alqaida linaloongozwa na Osama Bin Laden ndilo
lililohusika na mashambulizi ya mabomu katika balozi za Dar es Salaam
na Tanzania. Taarifa hiyo ilieleza kuwa CIA walipokea taarifa mapema
kuwa Alqaida ilikuwa imefanikiwa kuunda kikundi (cell) nchini Kenya,
na ilikuwa ikipanga kufanya mashambulizi. Hata hivyo baada ya
kufanya uchunguzi kwa kushirikiana na maafisa wa usalama, na polisi
wa nchi hiyo CIA iliamini cell hiyo imesambaratishwa. Taarifa hiyo
iliendelea kueleza kuwa, kundi la Alqaida lilikuwa likiendelea kufanya

51
GO DW IN C H IL EWA | 52

mipango ya mashambulizi mengine katika nchi za Albania, Uganda, na


Rwanda.
Kufuatia taarifa hiyo, wizara ya nchi za nje ya Marekani (Department
of State) iliamuru kufungwa kwa ubalozi wake nchini Albania; na
kuwarudisha nyumbani maafisa wote walioonekana kuwa hatarini.
Sambamba na hilo, wizara ya ulinzi (Department of Defense) ilichukua
hatua za haraka kutuma wanajeshi wake (Marines) kuimarisha ulinzi wa
balozi na mali zake nchini Rwanda na Uganda.

3
Masaa machache baadae, maafisa wa juu wa serikali ya Marekani
walifanya kikao cha dharula na viongozi wa serikali ya Jamhuri ya
muungano wa Tanzania. Mazungumzo hayo yalilenga kuweka mikakati
ya pamoja katika kusaidia wahanga wa bomu, kuimarisha uhusiano wa
kirafiki, na kushirikiana katika mapambano dhidi ya ugaidi. Kwa miaka
mingi ushirikiano kati ya Tanzania na Marekani ulikuwa kubabaisha tu
kutokana na tofauti za kisiasa zilizokuwepo kwa zaidi ya robo karne.
Kulegalega kwa uhusiano kati ya Tanzania na Marekani
kulichangiwa kwa kiasi kikubwa na msimamo wa Tanzania katika
kupigania ukombozi wa kusini mwa Afrika. Wakati Tanzania ikiwa
mwenyekiti wa nchi tano zilizo mstali wa mbele katika ukombozi wa
kusini mwa Afrika, Marekani na Uingereza walikuwa ndiyo washirika
wakubwa wa serikali ya makaburu wa Afrika ya kusini, iliyokuwa
ikongozwa na P.W Botha na washirika wake.
Ili kukwamisha harakati za ukombozi wa Afrika ya kusini, shirika
la ujasusi la Marekani (CIA) lilifanya hujuma nyingi, na propaganda za
kila namna zilizolenga kuiyumbisha Tanzania kiuchumi. Baadhi ya
hujuma hizo zilifanikiwa, nyingine zilibainika na kuzimwa kimya kimya,
na nyingine zilitumiwa kama propaganda ya kupinga ubeberu wa
Marekani na washirika wake. Kwa mfano, katika miaka ya mwishoni
mwa 1970 Tanzania iliituhumu Marekani kwa kuzalisha, na kusambaza
wadudu wa mazao waitwao viwavi jeshi. Wadudu hao, kama lilivyo
jina lao, walikuwa wakitokea kwa makundi makubwa (kama ya nzige)
kushambulia mazao ya chakula hususan mahindi yaliyokkuwa
mashambani. Tofauti na nzige ambao walipotokea (miaka ya nyuma0
wananchi walikuwa wakiwakamata na kuwala, viwavi jeshi walikuwa
hawaliki, wala hawatamaniki. Sambamba na viwavi jeshi, pia waliibuka
wadudu wanaoshambulia mahindi yaliyokaushwa, na kuhifadhiwa
ghalani. Wadudu hawa waliojulikana kama dumuzi waliharibu kwa kiasi

52
53 | SH U H U DA ZA J A SU SI – NDA NI YA IDA RA

kikubwa akiba ya mahindi iliyokuwa katika maghala ya hifadhi ya


chakula ya taifa, hali iliyosababisha njaa kubwa nchini.
Mashambulizi ya wadudu hayakuishia hapo tu! Wakati Tanzania
ikihangaika kupambana na wadudu wa mazao ya chakula, wakajitokeza
wadudu wengine walioshambulia mazao ya biashara. Wadudu hao
walishambulia tumbaku, pamba, kahawa na korosho kiasi cha
kuyumbisha kabisa uzalishaji, na ubora wa mazao hayo. Ili kujipatia
fedha, na kujikimu kimaisha wananchi wengi walilazimika kupunguza
uzalishaji wa mazao ya biashara, na kugeukia kulima mazao ya chakula.
Hali hii ilipunguzia taifa fedha za kigeni, na kuifanya ishindwe kumudu
kutekeleza baadhi ya miradi muhimu kwa maendeleo ya Taifa.
Ingawa miaka mingi ilikuwa imepita tangu kuanguka kwa
ukomunisti duniani, kuenea kwa mfumo wa siasa na uchumi wa soko
huria, na Tanzania kufuata mfumo wa siasa wa kidemokrasia wa vyama
vingi (unaoungwa mkono na Marekani) makovu ya uadui yalikuwa
bado hayajapona. Viongozi wengi wa serikali, walioshuhudia unyama
wa Marekani barani Afrika walijikuta wakiwa katika mtihani mgumu
wa kuiamini au kutoiamini nchi hiyo na washirika wake. Pamoja na
hayo yote, katika janga la ugaidi ushirikiano ulikuwa haukwepeki.
Zipo sababu nyingi zilizofanya ushirikiano katika uchunguzi wa
mlipuko wa bomu kuwa kitu cha kisichokwepeka. Sababu ya kwanza
ni aina ya shambulio na mahali lilipofanyika. Shambulio lilifanyika
katika ubalozi wa Marekani ulioko katika ardhi ya Tanzania. Hali hii
ilifanya nchi zote mbili (Marekani na Tanzania) kuwa na haki ya
kufanya uchunguzi, kuwakamata washitakiwa, kuwafikisha katika
vyombo vya dola na kuchukua hatua za kulinda raia na mali zake.
Ingawa Tanzania ilikuwa na haki zote kisheria, za kuchukua hatua
inazoona zinafaa ki ulinzi, sheria za kimataifa, chini ya mikataba ya
Geneva ilikuwa ikiipa Marekani haki hiyo hiyo kwa kuzingatia kuwa
eneo la ubalozi ni milki ya nchi inayomiliki ubalozi huo.
Sababu ya pili ni haja ya Tanzania kuonesha kutofurahishwa na
kitendo cha kigaidi kilichotokea, na pia kuihakikishia serikali ya
Marekani na watu wake kuwa Tanzania haihusiki kwa namna yoyote
katika kutoa mafunzo, fedha, vifaa, au msaada wowote kwa wahalifu
hao. Kutokufanya hivyo kungeweza kuiweka Tanzania miongoni mwa
maadui wa Marekani. Kutokana na umuhimu wa hatua hii, siku mbili
tu baada ya tukio hilo, rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania,
mheshimiwa Benjamin Mkapa alitembelea eneo la ubalozi uliolipuliwa
kujionea hali halisi, na kuwapa pole maafisa wa ubalozi huo. Akiwa

53
GO DW IN C H IL EWA | 54

ubalozini hapo rais Mkapa alilaani vikali shambulio hilo, na kuahidi


kutoa ushirikiano wa hali ya juu kwa serikali ya Marekani katika
kuwatafuta waliohusika na kuwafikisha katika mkono wa sheria.
Sababu ya tatu ni kuwa waathirika wakuu katika tukio hili walikuwa
raia wa Tanzania. Ingawa magaidi walilenga kuwaangamiza raia wa
Marekani, matokeo ya mlipuko yalikuwa tofauti sana. Kati ya watu
kumi na moja waliopoteza maisha yao walikuwa watanzania, na hakuna
mmarekani yeyote aliyeuawa katika tukio hilo. Wamarekani kadhaa
walikuwa wamejeruhiwa vibaya, na kukimbizwa katika hospitali ya
Agahkan walikopatiwa matibabu ya hali ya juu.
Sababu ya nne na ya muhimu zaidi, ni kuwa nchi zote mbili ziliona
umuhimu wa kushirikiana katika kufanikisha upelelezi. Mawakala wa
mashirika ya ujasusi na upelelezi ya Marekani yalikuwa na nyenzo zote
zinazohitajika katika kufanya uchunguzi. Walikuwa na maafisa
waliofuzu vema mafunzo, na uzoefu kufanya uchunguzi wa milipuko,
kufanya upelelezi, na kukusanya taarifa za kijasusi kwa kutumia watu
na vyombo. Hata hivyo maafisa hawa walikuwa katika eneo (territory)
wasilolijua kabisa. Hawakuwa na uzoefu wowote wa kuzungumza
lugha ya kiswahili inayotumiwa na watanzania wengi, wala ujanja wa
kuzunguka mitaa na vichochoro vya Dar es salaam. Si hivyo tu, maafisa
hao hawakuwa na uzoefu wowote wa mila, tabia na desturi za makabila
tofauti ya Tanzania; jambo muhimu katika kufanya mahojiano, na
kutambua viashiria vya uadui au nia ya kutenda kosa. Kinyume chake,
maafisa wa Tanzania walikuwa na sifa zote walizopungukiwa maafisa
wa Marekani, lakini hawakuwa na nyenzo zinazohitajika, wala uzoefu
wa kuchunguza matukio ya mashambulizi ya bomu.
Sababu hizi pamoja na nyingine nyingi ziliweka msukumo
mkubwa kwa nchi zote mbili kutaka kushirikiana kwa kila hali, katika
kuwasaka magaidi waliohusika, kuwakamata, kuwafikisha katika
vyombo vya sheria, na kutengeneza mtandao mkubwa wa kupambana
na matukio ya kigaidi katika Afrika mashariki.

_______

54
55 | SH U H U DA ZA J A SU SI – NDA NI YA IDA RA

SURA YA TATU

KIKOSI KAZI
(TANBOMB)

Kikosi kazi (task force) kilichoundwa kilijulikana kama TANBOMB na


kilihusisha maafisa wa Tanzania na Marekani. Jina TANBOMB
lilichaguliwa na maafisa wa FBI ili kutofautisha kikosi kazi kingine
kilichoundwa nchini Kenya kwa lengo kama hili, ambacho kiliitwa
KENBOMB. Katika kikosi chetu Tanzania iliwakilishwa na wataalam
wa ujasusi kutoka idara ya Usalama wa Taifa, na maafisa upelelezi
kutoka idara ya upelelezi wa makosa ya jinai. Maafisa usalama wa Taifa
waligawanyika katika makundi makuu mawili: Kundi la kwanza
lilihusisha maafisa waliopewa jukumu la kufanya kazi bega kwa bega na
mawakala wa idara za ujasusi na ukachero za Marekani. Maafisa hawa
walipewa kibali (kwa lugha nyingine walikuwa wametolewa sadaka) na
idara kutambuliwa na majasusi wa nchi nyingine (lugha ya ki-idara
kuumbuka) kwa faida na usalama wa Taifa.
Katika hali ya kawaida, maafisa wa idara ya Usalama wa Taifa
hawapaswi kufahamika kwa mawakala wa mashirika ya kijasusi ya nchi
nyingine kwa hofu ya kushawishiwa kutoa siri, kutumika kama double
agents, kupoteza uwezo wao (access) wa kufanya kazi, na kulinda usalama
wao na familia zao. Inapotokea kazi inayolazimu kufanywa kwa
ushirikiano na majasusi wa nje kama hivi, idara huchukua hatua
madhubuti kulinda usalama wa maafisa wake. Hatua hizo ni pamoja na
kuwapa vitendea kazi, kuwapa ushauri wa kitaalam, na kufuatilia
nyendo zao kila inapobidi.
Kundi la pili lilihusisha maafisa wa kitengo cha ufundi (Technical).
Maafisa hawa walikuwa na mafunzo maalum ya kutumia vyombo vya

55
GO DW IN C H IL EWA | 56

kisasa vinavyotamba katika sanaa ya ujasusi. Kazi kubwa ya maafisa


hawa ilikuwa kutoa msaada (support) kwa maafisa walioko katika
medani (field) katika kuunganisha nukta zinazopungua kwenye taarifa
wanazofuatilia. Kwa kifupi maafisa hawa (ufundi) ndiyo wanaofanya
kazi ya kunasa radio za mawasiliano ya adui, kusikiliza mazungumzo ya
simu (Telephone bugging) na kuchungulia barua pepe ( email interception) za
watuhumiwa, ndugu na washirika wao. Maafisa hawa pia hutumika
kufanya ufuatiliaji (surveillance) wa watuhumiwa, na washirika wao,
kufungua milango ya nyumba zinazolindwa kwa mitambo maalum ya
kuzuia wahalifu bila kuacha ushahidi wowote, na kufanya upekuzi wa
siri (secret searches) katika nyumba zinazoshukiwa kuhifadhi watu au vitu
vinavyotafutwa.
Maafisa wa idara ya upelelezi wa makosa ya jinai (CID)
waligawanyika katika makundi matatu. Kundi la kwanza lilihusisha
maafisa wapelelezi waliokuwa na jukumu la kushirikiana na maafisa wa
TISS, pamoja na mawakala wa FBI kufanya uchunguzi, kukamata na
kuhoji watuhumiwa, kukusanya ushahidi na vidhibiti vitakavyotumika
mahakamani. Kundi la pili lilikuwa na wataalam wa uchunguzi wa eneo
la tukio (Forensic experts). Makachelo hawa walipaswa kushirikiana na
wataalam wa FBI katika kukusanya na kuchunguza alama za vidole,
nyayo, na vinasaba ili kuthibitisha uwepo wa mtuhumiwa katika eneo
husika, na kuchunguza maganda ya risasi, nyaraka, na vielelezo vingine
vinavyoweza kutumika kama ushahidi mahakamani. Kundi la tatu
liliundwa na maafisa wa kitengo cha intelijensia cha idara ya upelelezi
wa makosa ya jinai. Maafisa hawa walikuwa na jukumu la kukusanya
taarifa za kiusalama katika maeneo waliyopangiwa, na kuziwasilisha
kwenye task force ili ziweze kufanyiwa kazi.
Serikali ya Marekani iliwakilishwa na mawakala (special agents)
kutoka idara ya upelelezi - Federal Bureau of Investigation (FBI), Polisi wa
kitengo cha upelelezi wa makosa ya jinai (Criminal Investigation
department) wa jiji la New York (New York Police Department - NYPD),
idara ya kupambana na matumizi mabaya ya pombe, tumbaku, na silaha
(Alcohol Tobaco and Firearms – ATF) , kikosi cha siri cha ulinzi (Secret
Service), mawakala wa wizara ya mambo ya nchi za nje (Department of
State), na shirika la ujasusi la Marekani (Central Intelligence Agency).
Maafisa wa FBI waligawanyika katika makundi matatu. Kundi la
kwanza lilijumuisha wataalam wa milipuko (Bomb Squad). Mawakala
hawa walikuwa na jukumu la kufanya uchunguzi wa eneo la tukio ili
kutambua aina ya bomu lililotumika, vifaa na aina ya vilipuzi

56
57 | SH U H U DA ZA J A SU SI – NDA NI YA IDA RA

vilivyotumika kutengeneza bomu, nguvu na uzito wa mlipuko husika,


na madhara yaliyosababishwa na bomu. Makachelo hawa pia walipaswa
kushirikiana na wataalam wa uchunguzi wa eneo la tukio (Forensic
experts) kutambua chombo kilichotumika kubeba bomu (kama ni gari,
pikipiki nk) na kukusanya ushahidi unaoweza kutumika kumpata
mmiliki, au dereva wa chombo kilichobeba bomu. Pamoja na
majukumu hayo, kundi hili pia lilikuwa na wajibu wa kufanya
uchunguzi wa viungo vya watu waliouawa katika shambulio, na
kupambanua akina nani ni wahanga, na nani wana viashiria vya kuwa
wabebaji au wasafirishaji wa bomu.
Kundi la pili lilihusisha mawakala wapelelezi (Investigators). Hawa
walikuwa na jukumu la kufanya kazi bega kwa bega na maafisa wa TISS,
pamoja na makachelo wa idara ya upelelezi wa makosa ya jinai katika
kupeleleza, kukamata na kuhoji watuhumiwa, kufanya upekuzi, na
kukusanya ushahidi utakaotumika mahakamani kwa mujibu wa sheria
za Tanzania na Marekani. Wakati huo ilikuwa bado haijaamuliwa kama
mashitaka yafunguliwe katika mahakama ya Tanzania au Marekani.
Kundi la tatu lilikuwa la mawakala wa FBI kutoka kikosi maalum
cha ukamataji na udhibiti wa wa wahalifu sugu kinachojulika kama
SWAT (Special Weapons and Tactics). Mawakala hawa walikuwa na
mafunzo maalum ya kutumia silaha na mbinu za hali ya juu za
kukamata wahalifu. Mawakala hawa waliletwa maalum kwa ajili ya
kusaidia kuwakamata magaidi husika mara tu itakapojulikana ni akina
nani na wako wapi.
Kundi la nne lilijumuisha mawakala wa kitengo cha udhibiti
Tumbaku Vileo na Silaha za moto ( Alcohol Tobaco and Firearms - ATF),
Secret Service (SS), makachelo wa kitengo cha upelelezi wa makosa ya
jinai cha jiji la New York (NYPD -Criminal Investigation Department) na
majasusi wa CIA. Hawa walijichanganya na mawakala wa FBI na au
kutumia kifuniko cha wizara ya mambo ya nje ya Marekani (Department
of State) kufanya kazi zao. Utaratibu huo uliwasaidia kulinda
utambulisho wao (identity) na kuepuka maswali toka kwa waandishi wa
habari na watu wengine wasiohusika.

2
Saa sita mchana ilinikuta nikiwa na maafisa wengine kumi na nne
walioteuliwa kushiriki katika kikosi kazi. Maafisa hawa walikuja kutoka
kwenye ofisi na vitengo mbalimbali vya idara. Nusu ya maafisa hao
nilikuwa nikifahamiana nao vema kwa sababu mbalimbali; Aidha

57
GO DW IN C H IL EWA | 58

niliwahi kufanya nao kazi, au tulikutana katika kona nyinginezo. Robo


yao nilikuwa nikiwafahamu kwa sura na majina tu, lakini hatukuwa
karibu kwa namna yoyote ile. Waliobakia sikuwa nikiwafahamu kabisa,
ilikuwa ndiyo mara yangu ya kwanza kukutana nao. Hata hivyo dakika
chache tulizokuwa pamoja zilitufanya tujione kama tumefahamiana
kwa miaka mingi.
Mpaka wakati huo sikuwa na fununu yoyote kuhusu vigezo
vilivyotumika kuwaingiza maafisa wengine katika kikosi kazi. Maafisa
wawili, DSO Chezi wa Kinondoni, na afisa MTW kutoka Kanda
sikuhitaji kuelezwa habari zao. Hawa niliwaona pale ubalozini muda
mfupi baada ya tukio, hivyo nilijua wana mengi vichwani mwao. RSO
Dar es Salaam mzee Zuberi naye sikuhitaji kuambiwa habari zake.
Wadhifa wake, na mahali lilipotokea tukio ilikuwa sababu tosha ya yeye
kuwemo katika kikosi kazi hiki. Afisa mwingine ambaye sikushangazwa
na uwepo wake ni Daudi (N) maarufu kama Kijiko, kutoka Kanda.
Huyu alikuwa akifahamika sana kwa umahili wake kwenye operesheni
za ndani hususan zilizowashirikisha polisi. Aina ya utendaji kazi wake,
na majukumu aliyokuwa akiyasimamia vilimpa nafasi ya kuajiri (recruit)
watoa habari wengi katika maeneo mbalimbali jijini.
Kikao kilifanyikia faragha, mahali tulipoona tungeweza
kuzungumza kwa uhuru bila kubughudhiwa au kusikilizwa na majasusi
wengine. Kama kawaida kikao kilianza kwa utambulisho wa maafisa.
Kila afisa alipewa muda mfupi wa kujitambulisha na kuzungumza
machache aliyoona yanafaa kwa hali na wakati tuliokuwanao. Baada ya
maafisa wote kujitambulisha ndipo RSO Zuberi aliyekuwa akiongoza
kikao hicho akamtambulisha afisa Romeo (Jina bandia) kutoka makao
makuu ya TISS. Afisa huyu ndiye alikuwa ameteuliwa na mkurugenzi
mkuu (DGIS) kuwa kiongozi wa maafisa wa idara katika kikosi kazi.
Romeo alikuwa afisa nguli, mwenye elimu na uzoefu wa hali ya juu
katika kazi za kijasusi. Licha ya kushiriki katika operesheni lukuki ndani
ya nchi pia alishafanya kazi katika nchi kadhaa za Ulaya, na kukamilisha
malengo ya idara kwa ufanisi mkubwa. Wakati operesheni hii
ikifanyika, Romeo alikuwa na zaidi ya miaka therathini katika idara.
Muda huo ulimuwezesha kujenga rekodi ya utendaji bora kulinganisha
na umri wa kati aliokuwa nao.
Baada ya kujitambulisha na kueleza historia yake kwa kifupi,
Romeo alitueleza kwa kirefu kirefu kazi tuliyokuwa tunapaswa
kuifanya, na namna tunavyotakiwa kuifanya. Mengi ya maelezo yake
yalirejea Amri ya Kazi (Operation Order) tuliyokuwa tumepewa. Kutia

58
59 | SH U H U DA ZA J A SU SI – NDA NI YA IDA RA

uzito maelezo yake, Romeo alianza kwa kusisitiza kwamba kila afisa
aliyeteuliwa kushiriki katika task force alikuwa amewekwa kwenye
mizani, na kuonekana anafaa kwa kila hali. Kwa sababu hiyo
mkurugenzi mkuu ana uhakika wa kuona kazi ikitendeka kwa weledi
na kwa kufuata misingi na kanuni za idara.
“Wengi wenu itakuwa mara yenu ya kwanza kufanya kazi na
mawakala wa nje (FBI) na pia kufanya uchunguzi wa mlipuko wa
bomu; hata hivyo, idara imewaamini kuwabebesha jukumu hilo. Ni
wajibu wenu kujifunza na ku adapt mbinu na mazingira ya kazi
mnayokwenda kuifanya haraka iwezekanavyo ili msiwe mzigo kwa
wageni. Kumbukeni, mawakala wa FBI na wengine wote watakuwa
wakifuatilia utendaji wenu kwa ukaribu zaidi kuliko wenzenu wa idara
ya upelelezi wa makosa ya jinai. Hii ni kwa sababu idara ya usalama wa
Taifa ndiyo kipimo cha ukamilifu wa uwezo na ufanisi wa vyombo vya
ulinzi na usalama nchini” Alieleza kwa hamasa.
“Jambo la pili mnalotakiwa kufanya kwa weledi wa hali ya juu ni
kuangalia nyendo za wageni wote mtakaofanya nao kazi. Kama
mjuavyo serikali ya Marekani imeleta mawakala kutoka idara, vitengo,
na mashirika yake yote ya ukachelo na ujasusi. Mawakala hawa
wamekuja kwa lengo moja lililo wazi, kuchunguza tukio la mlipuko wa
bomu. Lakini kama ilivyo kawaida ya mashirika yote ya kijasusi, kila
unapopatikana mwanya wa kuingia katika nchi nyingine, huwa ndiyo
nafasi ya kufanya kila linalowezekana. Kwa hiyo ingawa tunashukuru
kwamba wageni hawa watatusaidia kuwatafuta magaidi waliohusika na
unyama huu, na kuvunja mtandao wao, ni lazima pia tuangalie mambo
gani mengine watakayo onesha interest. Ni jukumu letu kufanya hivyo,
na kwa umakini wa hali ya juu ili tusichezwe shere nyumbani kwetu.
Kwa hiyo kila afisa atawajibika kuangalia kwa makini nyendo za
mawakala atakaokuwa nao. Jua wanafanya nini, wapi na kwanini. Kama
wanakutana na mtu sikiliza wanauliza maswali gani, Je, maswali hayo
yanahusiana moja kwa moja na tukio la bomu, au yanalenga kukusanya
taarifa tofauti kwa malengo mengine? Kama wana interest ya kujua vitu
tofauti fuatilia kujua ni vitu au habari za aina gani, kutoka kwa watu wa
aina na kariba gani, na nini muitikio wa watu hao” Alisisitiza
Jambo lingine tunalotakiwa kufuatilia kwa makini, ni uwezekano
wa mawakala hawa ku recruite watoa habari katika idara, jeshi la polisi
na idara nyingine za serikali. Kumbukeni CIA ni mabingwa wa kuajiri
watoa habari duniani, na kwa bahati mbaya katika timu ya wapelelezi
waliokuja hatuna hakika wakala yupi ni FBI hasa, na yupi ni wakala wa

59
GO DW IN C H IL EWA | 60

CIA anayetumia kifuniko cha FBI. Lakini hata kama tungekuwa na


uhakika, bado hatatuwezi kuwaogopa CIA na kuwapuuza mawakala wa
FBI. Itakuwa ni sawa na anayeogopa simba na kumpuuza chui, wakati
Wanyama hao wote ni jamii ya paka hatari. Vilevile mawakala hawa
wote tunapaswa kuwaona ni majasusi wa Marekani wanaofanya kazi
kwa interest ya nchi yao, na wanaweza ku recruit mtanzania yeyote.
Kwa ujumla kitu tulichofanya ni sawa na mtu kuruhusu mgeni
kulala chumbani kwake. Lolote litakalofanywa na mgeni huyo
litategemea maandalizi atakayoyakuta chumbani humo. Kama akikuta
dawa ya meno (mswaki) mezani, bila shaka akiamka asubuhi ataitumia
kusafisha meno yake; Lakini kama asipoikuta atalazimika kutumia dawa
aliyokuja nayo, au kumuomba mwenyeji wake ampatie dawa hiyo.
Halikadharika sisi tumewakaribisha majasusi hawa ndani kwetu. Ni
wajibu wetu kudhibiti kila kitu wanachofanya ili kuhakikisha
hawatuzunguki. Ili kufanikisha zoezi hilo, kila afisa atalazimika
kuangalia tabia na mwenendo wa maafisa na askari wa idara ya upelelezi
wa makosa ya jinai atakaofanya kazi nao. Pia mtafuatilia mwenendo wa
askari polisi, maafisa uhamiaji, na watumishi wengine wa ofisi za
serikali mtakao wakutanisha na FBI wakati wa uchunguzi, na mtu
yeyote atakayeonesha dalili ya kutumiwa, kujipendekeza, au kujenga
mahusiano ya karibu na wakala yeyote nje ya kazi anayofanya. Taarifa
za kila mtu anayetiliwa mashaka, pamoja na nyingine zote zifikishwe
kwangu, au katika ofisi ya task force makao makuu kwa utaratibu
maalum ulioelezwa kwenye operation order.”
Maneno ya Romeo yalituingia vema na kututia hamasa ipasavyo.
Kila afisa aliahidi kufanya kazi kwa juhudi na maarifa ili kuijengea nchi
yetu heshima. Kwa ujumla hakuna aliyeonesha wasiwasi wa kubeba
mzigo tuliobebeshwa. Sote tulikuwa tumepitia mafunzo ya kijeshi
yanayojumuisha matumizi ya silaha za moto, mbinu za kujilinda kwa
mikono mitupu (unarmed combat), ujasili, ukusanyaji wa taarifa za
kiitelejensia katika mazingira magumu, kuajiri watoa habari (recruitment
of sources), kufanya upelelezi wa kipolisi (criminal investigation), uchunguzi
wa maeneo ya tukio (crime scene investigation), na sheria ya ushahidi (Law
of evidence). Kwa kifupi tulikuwa tumekamilika.
Miaka ya nyuma, idara ya usalama wa Taifa ilikuwa haina utaratibu
wa kufundisha maafisa wake sheria ya ushahidi na mafunzo mengine
yanayohusisha kazi maalum za kipolisi. Idara ilikuwa haifanyi hivyo
kwa kuamini kuwa kazi zake ni za kificho (SIRI). Maafisa wake
hawakamati kama kipolisi, na wala hawahitajiki kutoa ushahidi

60
61 | SH U H U DA ZA J A SU SI – NDA NI YA IDA RA

mahakamani. Mambo yalibadilika mwaka 1985 wakati mahakama kuu


ilipokuwa ikisikiliza kesi ya uhaini iliyokuwa ikiwakabili maafisa wa
jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) Kepteni Thomas Lugangila
(Uncle Tom), Kepteni Hatibu Gandhi (Hatty McGhee), Kepteni
Zacharia Hans Pope na wenzao waliokuwa wakituhumiwa kutaka
kumpindua rais Julius Kambarage Nyerere.
Akisikiliza kesi hiyo jaji wa mahakama kuu mheshimiwa Nassoro
Mzavas alilazimika kuwapandisha kizimbani Maafisa kadhaa wa idara
ya usalama wa Taifa kutoa ushahidi dhidi ya watuhumuwa. Jaji Mzava
alifikia hatua hiyo baada ya upande wa utetezi ukiongozwa na wakili
Multaza Lakha kuiomba mahakama kufanya hivyo ili waweze kuhojiwa
(cross examination). Hatua hiyo iliitia matatani idara kwani maafisa wake
waliotambulishwa kwa majina bandia (shahidi X, shahidi Y na
wengineo) walipata taabu sana kujibu maswali ya mawakili wa utetezi
kwa sababu, hawakuwa na utaalam wowote wa sheria, wala uzoefu wa
kutoa ushahidi mahakamani. Jambo lililoidharilisha idara.
Kufuatia kizungumkuti hicho, idara ilianzisha utaratibu maalum wa
kuwafundisha maafisa wake mafunzo ya kipolisi ikiwa pamoja na
Criminal investigation (kwa jicho la kipolisi), uchunguzi wa eneo la tukio
(Crime scene investigation), na uandishi wa taarifa za kipolisi. Idara pia
ilianza kuwatumia wanasheria wake Kiriba na Madafa kutoa mafunzo
ya sheria, hususan mwenendo wa mashitaka (Criminal proceidure) na
sheria ya ushahidi (Law of evidence) kwa maafisa wapya ili kuwawezesha
kujua taratibu za kimahakama, na kumudu vitimbi vya mawakili
endapo watahitajika kutoa Ushahidi mahakamani.
Katika kipindi hicho, idara pia ilianzisha mkakati maalum wa
kuwasomemesha wengi wa maafisa wake elimu ya juu (ikiwa pamoja
na shahada ya sheria, udaktari, na uhandisi) ili kujihakikishia uwepo wa
wataalam wa kutosha katika sekta za kisiasa, kiuchumi, kisheria na
kijamii.

3
Kazi ya uchunguzi ilianza rasmi baada ya kikao cha pamoja kati
ya maafisa wa Tanzania na mawakala wa FBI na washirika wake. Kikao
hicho ndicho kilichoweka msingi wa jinsi kazi itakavyofanyika. Maafisa
wote wa idara walioteuliwa kushiriki katika operesheni hii walihudhuria
kikao hiki. Maafisa wa idara ya upelelezi wa makosa ya jinai pia
walikuwepo wakiongozwa na msaidizi wa mkurugenzi wa makosa ya
jinai (DCI) kamisha mwandamizi msaidizi wa polisi (Senior Assistant

61
GO DW IN C H IL EWA | 62

Commissioner) Robert Manumba aliyemuwakilisha mkurugenzi wa


makosa ya jinai (DCI) kamishna mwandamizi wa Polisi (CP) Rajabu
Adadi. Maafisa wengine waliokuwepo ni Senior Assistant Commissioner
Kasala, kutoka makao makuu, SSP Abdallah Msika kutoka kituo cha
Oysterbay, Inspector Valentino Mlowola kutoka makao makuu ya Polisi,
Inspector Goyayi kutoka kituo cha Oysterbay, Inspector Omari, na Inspector
Robert kutoka makao makuu ya polisi, Ditective SSgt Nyasi kutoka
makao makuu, Ditective Sgt Nicholaus, Ditective Coplo David, Ditective
Constable Cosmas Mahenge kutoka Oystebay na wengineo.
Awali ya yote kikao kilipokea taarifa fupi iliyoeleza jinsi shambulio
la bomu lilivyofanyika. Hii ilikuwa hatua muhimu katika kutuweka
sawa baada ya kuvurugwa na taarifa za vyombo vya habari. Siku mbili
baada ya kutokea milipuko, msemaji wa jeshi la Polisi Tanzania, Senior
Assistant Cammissioner of Police (SACP) Mwamunyange alivieleza
vyombo vya habari kuwa bomu lililolipua ubalozi wa Marekani jijini
Dar es Salaam, liliingizwa hapo na gari la kubeba maji (boza) la ubalozi
huo, lililokuwa likiendeshwa na dereva Mtanzania. Habari hizo
zilitokana na taarifa za awali zilizokusanywa na polisi kutoka kwa
wafanyakazi wa kampuni ya ulinzi ya Ultimate Security walionusulika
kifo, na watu wengine walioshuhudia tukio hilo. Hata hivyo, taarifa
zilizopatikana baadae zilionesha kukinzana na taarifa zilizotangazwa na
SACP Mwamunyange, ambazo pia zilitolewa bila kuwashirikisha FBI.
Taarifa sahihi zilieleza kuwa, gari lingine lililokuwa halijatambuliwa
ndilo lililotumika kubeba bomu, na si boza (tanker) la ubalozi kama
ilivyotangazwa. Gari hilo lilifika ubalozini hapo muda mfupi tu baada
ya boza lililobeba maji ya ubalozi kuingia. Kuhitimisha usahihi wa
taarifa yao, FBI walisisitiza kuwa mkanganyiko ulioonekana katika
maelezo ya walinzi, ulisababishwa na ukaribu wa magari hayo mawili
wakati yalipokuwa yakiingia ubalozini, na ukubwa wa mlipuko ambao
bila shaka uliwaondolea ufahamu kwa muda.
Kwa vile kikosi kazi chetu (TANBOMB) kilikuwa kikifanya kazi
sambamba na (KENBOMB) kilichokuwa jijini Nairobi, Kenya,
tulielezwa kwa kifupi hali ilivyokuwa nchini humo. Kwa ujumla hali
ilikuwa mbaya sana kulinganisha na nchini kwetu. Mpaka wakati huo
watu zaidi ya 200 kati yao 14 wakiwa raia wa Marekani walikuwa
wamepoteza Maisha na wengine 4000 kujeruhiwa vibaya. Makao
makuu ya majeshi ya ulinzi wa Marekani (Pentagon) iliwataja maafisa
wa jeshi hilo waliouawa ni Air Force Senior Master Sgt Sherry Lynn Olds
mwenye umri wa miaka 40 kutoka Panama City, Florida, Marine Sgt.

62
63 | SH U H U DA ZA J A SU SI – NDA NI YA IDA RA

Jesse N. Aliganga, mwenye umri wa miaka 21 kutoka Tallahassee,


Florida, Army Sgt. Kenneth R. Hobson II mwenye umri wa miaka 27
kutoka Nevada. Wakati huohuo Department of State nayo ilikuwa
imetoa taarifa yake iliyowataja raia wengine wa Marekani waliouawa.
Raia hao ni pamoja na Jay Bartley, mtoto wa afisa wa ubalozi (Consul
General), Julian Bartley, Jean Dalizu toka ofisi ya mwambata wa kijeshi
(Defense attache), Molly Hardy toka kitengo cha utawala (Administrative
office), Prabhi Kavaler toka ofisi ya huduma (General services office) Arlene
Kirk, toka kitengo cha misaada ya kijeshi (military assistance office),
Michelle O’connor toka ofisi ya huduma (General services office) na Tom
Shah wa kitengo cha siasa (Political section).
Ukubwa wa mlipuko uliharibu vibaya jengo la ubalozi wa
Marekani, na kuporomosha sehemu kubwa ya jengo la Ufundi lilokuwa
makazi ya wanafunzi wa chuo cha uhazili. Majengo mengine zaidi ya
hamsini pia yaliharibiwa katika eneo la kilometa moja za mraba. Wakati
huo kikosi cha wanajeshi 170 wa kikosi cha uokoaji kutoka nchini Israel
kilikuwa kimeshafika katika eneo la tukio kushirikiana na waokoaji
wengine kutoka Ufaransa, Marekani na Kenya. Kikosi hicho kilisaidia
mno kuokoa Maisha ya watu waliofukiwa na kifusi katika jengo la
Ufundi. Kikosi hicho chini ya uongozi wa Kanali Isaac Ashkenazi
kilitumia uzoefu wake katika matukio ya aina hii, teknolojia ya hali ya
juu, na mbwa wa uokoaji kutambua mahali walipofukiwa wahanga,
kuondoa kifusi, na kuwatoa majeruhi bila kusababisha madhara.
Mpaka kufikia asubuhi ya siku hiyo hakuna mtu yeyote aliyekuwa
amefikishwa mahakamani kwa kuhusika na tukio hilo. Maafisa wa FBI
walikuwa wakiendelea kufuatilia taarifa za mtu mmoja aliyeonesha dalili
za kutia mashaka. Mtu huyo aliyetambuliwa kwa jina la Khalid Salim
Saleh Bin Rashid alifika katika hospitali ya Nairobi akiwa na majeraha
mgongoni, na sehemu nyingine za nyuma ya mwili wake. Hali hiyo
iliwapa mashaka madaktari waliomtibu kwamba huenda alijeruhiwa
wakati akikimbia kutoka katika eneo la tukio. Madaktari hao
waliwapigia simu polisi wa Kenya ambao walimfuatilia na kumuweka
chini ya ulinzi. Taratibu za kumfanyia mahojiano zilikuwa zikiendelea.
Tulielezwa pia kuhusu mtuhumiwa mwingine aliyekamatwa katika
uwanja wa ndege wa Karachi, nchini Pakistani wakati akijaribu kuingia
nchini humo kutokea Kenya. Mtuhumiwa huyo alikamatwa baada ya
maafisa wa uhamiaji kugundua alisafiri kwa kutumia passport bandia
yenye jina la Abdulbasit Awadh. Baada ya kupekuliwa mtuhumiwa
alikutwa akiwa na tiketi ya ndege iliyotumika, begi la nguo, saa ya

63
GO DW IN C H IL EWA | 64

mkononi, vitabu, na fedha mchanganyiko (Shilingi za Kenya na dola


za kimarekani) zinazofikia kiasi cha $560. Maafisa wa usalama wa
Pakistan walikuwa wakiendelea kumuhoji mtu huyo, wakati mipango
ya kumrudisha nchini Kenya ikiendelea.
Taarifa nyingine ilihusu aina ya adui tuliyekuwa tukimuwinda, na
tahadhari za kuchukua wakati wa operesheni nzima. Ilielezwa kuwa,
masaa machache baada ya mashambulizi katika balozi za Marekani jijini
Nairobi na Dar es Salaam, mtu mmoja aliyejitambulisha kuwa msemaji
wa kikundi kiitwacho Army for the Liberation of Islamic Shrine
alipiga simu katika ofisi ya gazeti la kiarabu la Al-Hayat jijini Cairo
Misri, akidai kundi lake ndilo lililohusika na mashambulizi hayo. Mtu
huyo aliyekuwa akizungumza lugha ya kiarabu, hakueleza sababu za
shambulio hilo, hakutaja uraia wake, na wala hakueleza kwa kina
shabaha ya kundi analoliwakilisha.
Maelezo ya msemaji huyo yalishabihiana kwa kiasi kikubwa na
taarifa za kiintelejensia zilizopatikana kutoka vyanzo (sources)
mbalimbali vya CIA katika ukanda huo. Vyanzo hivyo vilionesha
uwepo wa vikundi vidogo dogo vya kigaidi vinavyofanya kazi chini ya
kundi la Egyptian Islamic Jihad lililokuwa likiongozwa na Aymenn al-
Zawahiri. Vikundi hivyo pamoja kundi la Hamas lilokuwa likiongozwa
na Khaled Meshaal, na Hizbullah lililokuwa likiongozwa na Hassan
Nasrallah vinatofautiana ki itikadi na mikakati; lakini vyote vinaunga
mkono vita dhidi ya Israel na ukombozi wa nchi takatifu.
Kundi la Egyptian Islamic Jihad (ambalo pia huitwa Islamic Jihad)
lilianzishwa miaka ya 1970 kwa lengo la kuiondoa madarakani serikali
ya Misri. Baada ya miaka mingi ya mikakati isiyofanikiwa, kundi hili
liligawanyika katika makundi madogodogo yanayojitegemea. Mwaka
1981 baadhi ya wanachama wake walishiriki katika mauaji ya rais
Anwar sadat, aliyekuwa kiongozi wa Misri wakati huo. Baadae kundi
lilibadilisha malengo yake kutoka siasa za ndani ya Misri, kuelekea
ugaidi wa kimataifa baada ya kuvutiwa na sera za kundi la Al-Qaeda
chini ya uongozi wa Osama Bin Laden. Jambo kubwa lililofanya kundi
hili kuwa kivutio kwa CIA, ni fatwa iliyotolewa na kiongozi wake,
kuhamasisha kuangamizwa kwa raia wa Marekani ili kulipiza kisasi kwa
wanachama wa kundi hilo waliokamatwa nchini Albania.
Kundi la HAMAS (Ḥarakat al-Muqāwamah al-Islāmiyyah) ambalo
kwa kiingereza huitwa Islamic Resistance Movement lilianzishwa
mwaka 1987 na Ahmed Yassin pamoja na wapiganaji wengine wa
Muslim Brotherhood kwa ushirikiano na wapinzani wa Yasir Arafat,

64
65 | SH U H U DA ZA J A SU SI – NDA NI YA IDA RA

kiongozi wa Palestine Libaration Organization (PLO), kundi mama


lililokuwa likipigania ukombozi wa wapalestina. Mpango wa kuundwa
HAMAS ulianza rasmi baada ya maandamano makubwa ya kuipinga
serikali ya Israel kufuatia mauaji ya wapalestina sita katika ajali ya gari
iliyokuwa ikiendeshwa na dereva muisraeli. Kwa ujumla Yassin na
wenzake hawakuwa wakipendezwa na mazungumzo ya amani, pamoja
na mikakati mingine iliyokuwa ikiendelea kati ya Yasir Arafat na
viongozi wa Israel. Kwa mtazamo wao, mikakati hiyo ilikuwa ikitoa
mwanya kwa Israeli kupora haki za wapalestina waishio katika ukanda
wa Gaza, na ukingo wa magharibi wa mto Jordan.
Ili kuilazimisha Israel kubadili msimamo wake dhidi ya wapalestina,
HAMAS ilianzisha intifadah, vita takatifu dhidi ya Israel ambapo
wapiganaji wake walishambulia makazi na vituo muhimu vya Israeli.
Vita hivyo viliisaidia sana HAMAS kupata umaarufu, na kuungwa
mkono na mataifa ya kiarabu yanayopinga uwepo wa taifa la Israeli
katika mashariki ya kati. Mwaka 1989 maafisa wa shirika la ujasusi la
Israel MOSSAD walifanikiwa kumkamata Ahmed Yassin na baadhi ya
wafuasi wake. Tukio hilo liliisukuma HAMAS kubadilisha muundo wa
utendaji wake, na kumchagua Khaled Meshaal a.k.a Khaled Mashal
kuwa kiongozi mpya wa kundi. Jambo kuu lililoisukuma CIA
kulifuatilia kwa karibu kundi hili, ni msimamo wake wa kuhimiza
kuondolewa kwa makafir (wasio waislam) katika nchi takatifu ya
waislam. Msimamo uliolenga kuangamizwa kwa taifa la Israel na
washirika wake katika mashariki ya kati.
Kundi la Hizbullah ambalo pia hujulikana kama Hezbollah au ‘Hizb
Allah’ (chama cha Mungu) lilianzishwa nchini Lebanon kufuatia
uvamizi wa Israel nchini humo (1975 – 1990). Lengo kuu la awali la
kundi hilo ilikuwa kuwaondoa wavamizi (Israel na washirika wake)
nchini Lebanon na kuunda jamhuri ya kiislam inayofuata madhehebu
ya Shia (Shiite). Kutokana na misimamo yake kundi hili liweza
kuungwa mkono haraka na jamhuri ya kiislam ya Iran. Mwaka 1985
uongozi wa Hizbullah ulitoa manifesto iliyotaka kuangamizwa kwa
makafir (wasio waislam) waliovamia nchi takatifu. Zipo sababu nyingi
zilizofanya CIA na vyombo vingine vya usalama kuliangalia kundi hili
kwa macho mawili. Sababu ya kwanza ni itikadi ya kundi, na msimamo
wa viongozi wake unaohimiza kuangamizwa kwa mataifa ya Israel,
Marekani, na washirika wao. Sababu ya pili ni uwezo mkubwa wa kundi
hilo katika kupanga na kutekeleza mashambulizi ya mawindo (target)
magumu. Mwezi April 1983 kundi la Hizbullah lilifanikiwa kulipua

65
GO DW IN C H IL EWA | 66

ubalozi wa Marekani jijini Beirut, Lebanon ambapo watu 63 waliuawa.


Miezi sita baadae, Oktoba 1983 kundi hili lilifanya shambulio jingine
katika eneo la makazi ya askari (barracks) wa Marekani na Ufaransa jijini
Beirut ambapo watu 305 waliuawa. Tukio hili lilifuatiwa na jingine
lililofanyika 1984 katika ubalozi mdogo (Embassy Annex) jijini Beirut,
Lebanon ambapo makumi ya watu waliuawa. Mwaka 1992 Hizbullah
walishambulia ubalozi wa Israel jijini Buenos Aires, Argentina, na
mwaka 1994 walifanikiwa kualipua ubalozi wa Israel jijini London
Uingereza. Kufuatia matukio haya, mwaka 1997 serikali ya rais Bill
Clinton wa Marekani ilitangaza rasmi kuliweka kundi la Hizbullah
katika orodha ya makundi ya kigaidi, na kuchukua hatua Madhubuti ya
kuwadhibiti viongozi, wanachama na wafadhili wake.
Pamoja na makundi haya matatu kuwekwa katika orodha ya
watuhumiwa, uongozi wa FBI ulisisitiza kuelekeza nguvu zetu katika
kulifuatilia kundi la Al-Qaeda lililoonekana kuwa tishio zaidi. Kundi
hili lilikuwa miongoni mwa makundi hatari ya kigaidi yaliyotangaza
fatwa dhidi ya raia wa Marekani. Mwaka 1993 kundi la Al-Qaeda
lilihusika katika jaribio la kulipua majengo ya World Trade Center
(twin towers) jijini New York ambapo watu 6 waliuawa na wengine
1,000 kujeruhiwa. Aidha, wiki moja kabla ya kushambuliwa kwa balozi
za Marekani Afrika ya mashariki, kiongozi wa kundi hilo shekhe
Osama Bin Laden alitoa onyo kuwa kundi lake litalipiza kisasi dhidi ya
Marekani kwa sababu inaisaidia Israel kuikalia kwa mabavu nchi
takatifu ya waislam.
Katika fatwa aliyoitoa mwezi Februari 1998 wakati akihojiwa na
mtangazaji wa kituo cha luninga cha ABC News, na baadae kurushwa
na kituo cha Al-Jazeera, Osama Bin Laden alisema fatwa hii itawahusu
wanajeshi wa Marekani ambao pamoja na kuonywa, bado
wameendelea kung’ang’ania kuinajisi nchi ya waislam, Pamoja na wote
wanaowasaidia Israel kuikalia nchi takatifu. Bib Laden aliongeza
kusema kuwa, Marekani imekuwa mstari wa mbele katika
kuwaangamiza waislam, na inaonesha kufurahia kuwepo kwa majeshi
yake nchini Saudi Arabia ambako imepata kibali cha watawala. Kwa
sababu hiyo si rahisi kwa wamarekani kuondoka kwa hiari. Kwa sababu
hiyo, inabidi walazimishwe kubeba masanduku ya mbao, na majeneza
yaliyosheheni maiti za wanajeshi na raia wao mpaka watakaposalimu
amri, na kuondoka. Bin Laden aliendelea kuilani Marekani kwa kusaidia
kukamatwa kwa wanachama wa kundi la Islamic Jihad nchini Albania,
na akasisitiza kuwa atalipa kisasi kwa ajili yao.

66
67 | SH U H U DA ZA J A SU SI – NDA NI YA IDA RA

Fatwa hiyo ilipokelewa kwa tahadhari kubwa na vyombo vya


usalama vya Marekani. Mara moja CIA kwa kushirikiana na vyombo
vingine vya ujasusi duniani vilianza kazi ya kutambua windo (target)
ambalo Al-Qaeda ilikusudia kushambulia. Mashaka yaliongezeka zaidi
baada ya kuthibitisha uwepo wa uhusiano wa karibu kati ya Osama Bin
Laden na kiongozi wa Islamic Jihad, Aymenn al-Zawahiri.
Baada ya taarifa hizo tulianza utaratibu wa kugawana malengo ya
kushughulikia. Ili kurahisisha mizunguko ya mjini na ufuatiliaji wa leads
nyingi kwa wakati mmoja, tulikubaliana kugawanyika katika makundi
madogo madogo ya utendaji. Kila kundi lilikuwa na mawakala wa FBI
kati ya watatu hadi kumi na tano, afisa wa idara ya usalama wa Taifa
(TISS), afisa wa idara ya upelelezi wa makosa ya jinai mwenye cheo
cha mkaguzi (inspector) na askari wengine wa cheo cha chini
(Noncommissioned officers). Msisitizo uliwekwa kuwa idadi ya maafisa wa
TISS na CID iliongezeke au kupungua kwa kadri uongozi utakavyoona
inafaa katika kipindi chote cha operesheni.. Baadae kila kundi lilipewa
magari mawili au matatu, pamoja na dereva wa kutuendesha. Magari
hayo yalikodiwa na ubalozi wa Marekani kutoka mawakala mbalimbali
jijini Dar es salaam hivyo yalikuwa na namba za kiraia.
Kwa vile mawakala wa FBI hawakuwa wakilijua vema jiji la Dar es
Salaam, tulikubaliana maafisa wenyeji tubebe jukumu la kuongoza
misafara katika sehemu zote tunazokwenda, na kusaidia kutafsili pale
itakapoonekana mtu anayehojiwa hawezi kuzungumza lugha ya
kiingereza kwa ufasaha. Pamoja na hilo, tulitakiwa kuhakikisha usalama
wa mawakala wa FBI muda wote tutakaokuwanao kazini. Katika
kutekeleza hilo askari wa kikosi cha upelelezi wa makosa ya jinai
waliagizwa kumkamata mtu yeyote atakayejaribu kutoa vitisho, kupora
mali, au kuhatarisha usalama wa mawakala hao kwa namna yoyote ile.
Kwa sababu hiyo tuliwataka maafisa wa FBI wasiende mahali popote
(kikazi), bila kufuatana na afisa mmoja wa TISS, pamoja na askari wa
idara ya upelelezi wa makosa ya jinai.
Baada ya mgawanyo wa vikundi kukamilika, tuligawana majukumu
kulingana na mkakati wa utendaji. Kundi la kwanza lilipewa jukumu la
kufanya kazi ya uchunguzi wa eneo la tukio. Kundi hili lilihusisha idadi
kubwa ya mawakala wa FBI wataalam wa milipuko (Bomb Squad –
Evidence Response Team), wataalam wa uchunguzi wa eneo la tukio
(Forensic experts), wapelelezi (investigators), maafisa wa idara (TISS) sita
(mimi nikiwa mmojawapo) na askari zaidi ya kumi na tano wa idara ya
upelelezi wa makosa ya jinai.

67
GO DW IN C H IL EWA | 68

Kundi la pili lilihusisha mawakala (FBI) wapelelezi (investigators)


maafisa wa idara (TISS) wanne, na askari kadhaa wa CID. Hawa
walikuwa na jukumu la kufuatilia majeruhi waliolazwa katika hospitali
ya Muhimbili na Agakhan kwa ajili ya matibabu. Kundi hili lilikuwa na
wajibu wa kuwahoji, kuchukua maelezo yao kwa kufuata taratibu za
kisheria, na kuwatambua wale waliokuwa na taarifa muhimu
zinazoweza kusaidia katika upelelezi. Kwa vile wengi wa majeruhi hao
walikuwa wameshatambuliwa, na taarifa zao kuchukuliwa muda mfupi
baada ya mlipuko (siku ya Ijumaa) kazi ya kuwapata ilikuwa rahisi.
Kundi la tatu lilikuwa na mawakala wa FBI (Investigators) wanne,
maafisa wa idara (TISS) wawili, afisa mmoja wa CID mwenye cheo cha
mkaguzi (inspector) na askari wawili wa vyeo vya chini. Hawa walikuwa
na jukumu la kufuatilia mawasiliano ya simu yaliyofanywa na
watuhumiwa kupitia simu za mkononi. Kwa jinsi tukio lilivyofanyika,
tulikuwa na kila sababu ya kuamini kwamba wahusika walikuwa na
mtandao mkubwa, uliohusisha washiriki na wafadhili walioko nje ya
nchi, na walikuwa na mawasiliano ya simu. Kundi hili lilikuwa na
wajibu wa kufuatilia kwa makini kumbukumbu zote za simu
zilizopigwa nje ya nchi katika kipindi cha miezi sita. Wakati huo nchini
Tanzania kulikuwa na makampuni matatu tu yanayotoa huduma za
simu. Makampuni hayo ni pamoja na Shirika la Posta na Simu Tanzania
(TTCL) lililokuwa likitoa huduma ya simu za ndani tu (Landline) na
makampuni binafsi mawili, MOBITEL na TRITEL yaliyokuwa yakitoa
huduma ya simu za mkononi (cellphones).
Kundi letu ndilo lililokuwa na jukumu la kufanya uchunguzi wa
eneo la tukio. Mawakala wa FBI tuliokuwanao walikuwa wataalam wa
uchunguzi wa milipuko (Bomb Squad – Evidence Response Team) na
wachunguzi wa eneo la tukio (Forensic experts) wenye uzoefu mkubwa
katika medani hiyo. Wengi wao walishiriki kikamilifu katika uchunguzi
wa mlipuko wa bomu uliotokea mwaka 1996 katika majengo ya
Khobar Towers jijini Khobar, Saudi Arabia. Wachache miongoni mwa
hao walishiriki katika uchunguzi wa shambulio jingine lililotokea
mwaka 1983 katika ubalozi wa Marekani jijini Beirut, Lebanon.
Kwa upande wetu (maafisa wa Tanzania) hakuna yeyote aliyekuwa
na uzoefu wa taaluma ya uchunguzi wa mabomu (Bomb expert). Tukiwa
mafunzoni, maafisa wa TISS tulifundishwa namna ya kutengeneza, na
kutumia mabomu madogo kwa kutumia vitu vinavyopatikana
nyumbani, na jinsi ya kutumia mabomu makubwa ya TNT. Katika
somo la ulinzi wa viongozi tulijifunza kukagua na kutambua mabomu

68
69 | SH U H U DA ZA J A SU SI – NDA NI YA IDA RA

ya kutegwa katika vyombo vya usafiri na majengo, na njia rahisi ya


kuyategua. Lakini kwenye uchunguzi wa milipuko mikubwa
hatukujifunza lolote la maana, zaidi ya nadharia (theory) ya juu juu bila
mazoezi yoyote ya vitendo. Wenzetu wa CID nao hawakuwa na
utaalam wowote wala vifaa vya uchunguzi wa aina hii. Hali hii
ilichangiwa kwa kiasi kikubwa na amani iliyokuwepo nchini, pamoja na
muelekeo wa nchi kiuchumi, kisiasa na kijamii uliotufanya tujiamini na
kujisahau katika mambo mengi. Tukio hili lilitudharilisha kwa wageni;
lakini pia lilitufumbua macho kwa kiasi kikubwa.
Kwa kuwa kazi yenyewe ilihitaji umakini wa hali ya juu, mawakala
wa FBI walilazimika kutupa maelekezo thabiti ya mambo tunayotakiwa
kufanya katika kila hatua. Aliyetuelekeza alikuwa wakala wa FBI
aliyebobea katika fani hiyo. Wakala huyo alianza kwa kutueleza jinsi ya
kutengeneza bomu kubwa lenye mlipuko wa nguvu ya paundi elfu
moja (1000 pounds) kwa kutumia vifaa vinayopatikana kwa urahisi.
Lengo la maelezo hayo ilikuwa kutupa picha ya aina ya vifaa
tunavyotakiwa kuvisaka katika eneo la tukio vikiwa vizima, vipande, au
mabaki ya vifaa vilivyoteketezwa kwa moto. Vipande hivyo ni muhimu
sana katika kutambua aina ya bomu, n ahata kikundi au mtu
aliyelitengeneza. Ingawa kila kikundi cha kigaidi kina namna yake ya
kutengeneza mabomu, vifaa vya msingi huwa ni vilevile (TNT,
detonator, simu au radio, saa n.k). Hata hivyo, kila kikundi huwa kina
namna yake ya kuunganisha (setting) na kulipua mabomu. Vikundi
vingi hupendelea kutumia vitu vya ziada kama goroli, misumari,
vipande vya nondo na kadharika kwa lengo la kuacha alama (signature)
katika eneo la tukio. Baada ya utangulizi huo aliendelea kutuelekeza
utaratibu unaotumika katika kukagua eneo ulipotokea mlipuko wa
bomu, vifaa vinavyohitajika, na namna ya kushughulika na kila kipande
cha ushahidi (exhibit) kinachopatikana ili kiweze kusaidia uchunguzi na
kukubalika mahakamani.
Eneo tulilopaswa kulifanyia uchunguzi lilikuwa na nusu kipenyo
cha maili moja (mita 1609.345) kutoka kwenye kitovu (center) cha
mlipuko. Hii ina maana tulilazimika kukagua eneo la duara lenye
mzunguko wa mita za mraba 5,053.343 sawa na maili 3.14 za mraba.
Ukitaka kujua kwa usahihi ukubwa wa eneo hilo (kwa lugha ya mtu wa
kawaida) fikiria (imagine) kama ukichukua kipande cha mti na
kukichomeka katikati ya mahali ulipotokea mlipuko, halafu ukachukua
kamba yenye urefu wa maili mbili na kufunga ncha moja kwenye
kipande cha mti, na ncha ya pili ukamfunga mbuzi. Eneo ambalo

69
GO DW IN C H IL EWA | 70

mbuzi ataweza kuzunguka kula majani akiwa ameinyoosha kamba


ndilo tulilopaswa kulikagua. Ukubwa wa eneo hilo ulikadiliwa
kutokana na uzito wa mlipuko uliosababisha kurushwa mbali kwa
vipande vya bomu hususan nyaya, vifaa vya radio au simu, mabaki ya
gari yenye vumbi la mlipuko, viungo vya binadamu, na vitu vingine
vilivyohitajika kusaidia uchunguzi.
Tuliligawa eneo la tukio katika sehemu kuu mbili: sehemu ya
kwanza ilianzia mahali kilipokuwa kitovu (center) cha mlipuko hadi
umbali wa mita ishirini na tano mzunguko. Eneo hili walikabidhiwa
wataalam nguli wa milipuko kushughulika nalo. Kwenye kitovu cha
eneo hilo kulikuwa na shimo kubwa (crater) lenye kipenyo cha mita
mbili hivi. Wataalam hao walilichukulia shimo hilo kama eneo
palipogundulika zana za kale, au machimbo ya dhahabu. Kwa kutumia
mafagio, brashi na miswaki taratibu walisogeza vumbi la udongo
mweusi lililokuwa limeziba eneo ili waweze kuona kuona vitu
vilivyofukiwa. Kazi hiyo ilifanyika kwa tahadhari ya hali ya juu
kuepusha uharibifu wa ushahidi. Kila kipande cha kidhibiti
kilichoonekana kilipigwa picha na kuorodheshwa katika daftari.
Baada ya vumbi la juu na mchanga kupekuliwa, na kusogezwa
pembeni, wataalam hao walitumia majembe, sululu na makoleo
kutanua upana wa shimo, na kuongeza kina chake. Katika kila hatua
waliyochimba walikusanya udongo, vyuma, mabati na vitu vingine
vilivyopatikana humo na kuvipeleka sehemu maalum iliyotengwa kwa
ajili ya uchunguzi zaidi. Hapo udongo ulichujwa kwa machekeche
makubwa yaliyotengenezwa kwa mbao na nyavu. Udongo laini
ulitupwa pembeni; lakini kila kipande cha chuma, waya, kifaa cha radio
au simu, bati, plastiki au chochote kilichoonesha dalili ya kuweza
kusaidia uchunguzi kilichukuliwa. Baadae ukaguzi wa pili ulifanyika
ambapo vipande vilivyoonesha umuhimu zaidi vilipewa namba,
vikapigwa picha, na kuorodheshwa katika daftari maalum la vidhibiti
(exhibit) kabla ya kukabidhiwa kwa forensic experts kwa ajili ya uchunguzi
zaidi.
Sehemu ya pili ya eneo ilianzia mita ishirini na tano hivi kutoka
kwenye kitovu (crater) cha mlipuko kuendelea mbele, umbali wa maili
moja mzunguko kila upande. Eneo hili tulikabidhiwa sisi kushughulika
nalo. Kazi kubwa ilikuwa ni kupekua kila inchi ya eneo hilo kwa lengo
la kupata ushahidi uliorushwa mbali. Tofauti na wenzetu waliokuwa
katika kitovu cha mlipuko, sisi hatukupaswa kuchimba mahali popote.
Tulichotakiwa ni kutembea taratibu, kuangalia kwa makini, na

70
71 | SH U H U DA ZA J A SU SI – NDA NI YA IDA RA

kutambua kila kipande cha ushahidi kilichoonekana. Kwa hiyo


hatukuwa na haja ya kubeba majembe na makoleo kama wenzetu;
badala yake tulivaa mifuko ya mikono (gloves) na kubeba ndoo za
plastiki, mifuko ya karatasi na plastiki, fimbo za kusogezea majani, na
wachache kamera za kupigia picha.
Ukifikiria haraka haraka, unaweza kudhani kundi letu lilipendelewa
kwa kupewa kazi rahisi zaidi. Nakuhakikishia sivyo kabisa! Kazi hii
ilikuwa ngumu, inayohitaji umakini wa hali ya juu, na yenye kuumiza
mno viungo vya mwili, hasa mgongo, shingo na macho. Zingatia
kwamba tulitakiwa kukagua eneo lote pasipo kuacha hata sehemu moja
inayopitika. Tatizo ni kuwa eneo lenyewe lilikuwa na vikwazo vingi,
kwani ubalozi wa Marekani ulikuwa eneo la makazi, na maofisi ya watu.
Kwa kifupi, mtua maafisa walioanzia ubalozini, kwenda upande
wa maghalibi walilazimika kuvuka barabara ya Ali Hassan Mwinyi na
kuendelea mbele maili moja hadi lilipokuwa eneo la wazi. Walioelekea
upande wa kusini walilazimika kufanya upekuzi hadi mbele ya daraja la
Salender, na mzunguko wa baharini. Upande wa mashariki ulikuwa na
vikwazo zaidi maana ni eneo la makazi ya watu na maofisi. Eneo hilo
pia ndiko ilikokuwa ofisi ya mkuu wa Usalama wa Taifa mkoa wa Dar
es Salaam (RSO). Upande wa kaskazini maghalibi ulikuwa umezibwa
kidogo kwani mlipuko ulitokea upande wa mashariki ya jengo. Hata
hivyo kila inchi ya maeneo hayo ilipaswa kukaguliwa kwa kadri
ilivyowezekana.
Kuhakikisha umakini wa upekuzi wa eneo lote, tulitumia njia kuu
mbili. Njia ya kwanza ilihusisha upekuzi mzunguko (spiral search).
Upekuzi huu hufanyika kwa kujipanga mstari, na kulikagua eneo la
tukio kwa kulizunguka taratibu kuanzia kwenye kitovu (crater) cha
mlipuko, kuelekea nje kama buibui anavyotengeneza utando wake. Njia
hii ni nzuri lakini haikutufaa kutokana na vikwazo, hususan majengo
yaliyozunguka eneo hilo. Hata hivyo tulitumia njia hii katika maeneo
ya wazi, yasiyokuwa na vikwazo vingi.
Njia ya pili ni upekuzi mraba (square search). Upekuzi huu
hufanywa kwa kuligawa eneo linalopekuliwa katika vyumba vidogo,
vya futi moja moja. Vyumba hivyo huhesabiwa, na jumla yake
hugawanywa kwa idadi ya wapelelezi waliopo. Hata hivyo, mpelelezi
mmoja huweza kupewa vyumba vichache au vingi zaidi kutegemea
mazingira na vikwazo vilivyopo katika eneo lenyewe. Njia hii
ilitupunguzia usumbufu, na kutuwezesha kuwa makini zaidi katika
upekuzi. Kupunguza mkorogano, kila wakala mpelelezi alitakiwa

71
GO DW IN C H IL EWA | 72

kuweka alama kwenye ramani ya vyumba (squres) alivyovikagua ili


wapelelezi wengine wasipoteze muda kuvirudia.
Tulipoanza upekuzi hatukujua tutapata ushahidi wa thamani kiasi
gani; na au kama tutafanikiwa kupata kitu chochote kitakacho tuelekeza
kuwajua wahalifu. Eneo lenyewe lilikuwa kubwa, na kwa kiasi fulani
lilikuwa limevurugwa na watu waliokuwa wakiishi au kupita wakiwa
matembezini. Kwa hiyo kila kipande cha chuma, waya, plastiki, au
kiungo cha mtu kilipoonekana kilipigwa picha kikiwa chini, kabla ya
kuokotwa, na kuingizwa kwenye ndoo ya plastiki au mfuko wa
kubebea. Hatua hiyo ilikuwa muhimu sana katika kuthibitisha mahali
kilipookotwa, umbali kiliorushwa kutoka eneo la tukio, na uhusika
wake katika tukio zima.
*******
Upekuzi wa eneo la tukio uliendelea kwa masiku kadhaa. Kazi
ilianza saa mbili asubuhi na kuendelea hadi saa kumi na moja jioni. Kila
eneo la wazi lilikaguliwa, kila kichaka kilichokonolewa, na kila paa
liliangaliwa kwa makini kuhakikisha hakuna kipande cha ushahidi
kilichoachwa. Upekuzi ulikuwa rahisi zaidi katika maeneo ya wazi
yenye sakafu, mchanga, au nyasi fupi zilizoruhusu kuona, na kuokota
vidhibiti bila usumbufu. Changamoto kubwa ilikuwa katika maeneo
yenye miti mingi, na nyumba zenye mapaa mafupi yaliyodaka vipande
vilivyorushwa juu. Pamoja na changamoto hizo tulihakikisha kila
kipande kilichoonekana kinatunguliwa na kuorodheshwa katika daftari
la exhibit.
Kwa vile nyumba za Oysterbay zina maeneo makubwa,
yaliyozungushiwa wigo, ilitulazimu kuomba ruhusa kwa wenye nyumba
kabla ya kuingia kwenye maeneo yao. Utaratibu huo ulitupa nafasi
nzuri ya kuwahoji wahusika, pamoja na familia zao kwa lengo la kupata
dondoo yoyote ya kutusaidia katika uchunguzi. Ili kuokoa muda na
kuwaengua watu wasiokuwa na taarifa muhimu, kila afisa alitakiwa
kumuliza mtu anayemuhoji maswali matatu ya msingi:
1. Ulikuwa wapi siku ya ijumaa tarehe 8 August 1998?
2. Ulisikia au kuona nini?
3. Kuna jambo lolote la kutia mashaka uliloliona kabla au baada
ya tukio?
Majibu ya maswali haya ndiyo yaliyotuwezesha kuamua kama tuendelee
na maswali mengine kupata taarifa zaidi au la! Kwa mfano, mtu
aliyeulizwa swali la kwanza akijibu siku ya tukio alikuwa nje ya nchi, au

72
73 | SH U H U DA ZA J A SU SI – NDA NI YA IDA RA

mkoa mwingine, alikuwa tayari amepunguza kwa kiasi kikubwa idadi


ya maswali ambayo tungemuuliza kama angejibu alikuwa jijini Dar es
Salaam. Hata hivyo bado tulimuuliza swali la pili kumpa nafasi ya kutoa
taarifa nyingine kama anazo. Kama majibu yake yakiwa negative, yaani
hakuona wala hakusikia chchote, bado tulimuuliza swali la tatu
linalotoa wigo mpana zaidi wa kujieleza.
Mamia ya watu tuliozungumza nao walikuwepo nyumbani, au
maeneo mengine ya Oystebay wakati mlipuko uliotokea. Watu hao
walieleza walisikia mshindo mkubwa wa mlipuko uliosababisha
kuvunjika kwa madirisha ya vioo, na uharibifu mwingine. Hata hivyo
ni wachache tu waliohisi kwamba mlipuko huo ulisababishwa na
bomu. Wengi wao walidhani mlipuko huo ulisababishwa na kupasuka
kwa transforma, au matanki ya Mafuta katika kituo cha Mafuta
kilichokuwa umbali wa maili moja hivi kutoka ubalozini. Watu hao,
waliongezea kuwa waliona moshi mweupe uliopaa angani na
kutengeneza wingu kubwa.
Tulipowauliza swali la tatu, asilimia 99 walijibu hakuna jambo
lolote la kutia mashaka waliloshuhudia kabla au baada ya tukio. Mtu
mmoja tu ndiye alieleza kuwa aliwaona watu fulani wakishangilia
kitendo cha kulipuliwa kwa ubalozi huo. Watu hao walisema Marekani
inastahili kuadhibiwa kwa sababu inajifanya ni polisi wa dunia.
Tulipomuuliza anafikiri ni nani aliyefanya kitendo hicho, mtu huyo bila
kusita alijibu “Sadam Hussein.” Majibu hayo yalitufanya tumuulize
maswali mengine mengi ambayo hata hivyo hayakutusaidia lolote.
*******
Wakati kundi letu likiendelea na uchunguzi wa eneo la tukio,
wenzetu waliopewa kazi ya kuhoji wahanga katika hospitali za
Muhimbili, Agakhan, na ofisi ndogo (ya muda) ya ubalozi wa Marekani
walikuwa wakiendelea. Wengi wa watu hao hawakuwa na maelezo
mengi kwani walishitukizwa na mlipuko kiasi kwamba hawakujua ni
kitu gani hasa kichotokea. Hata hivyo baadhi yao waliweza kueleza kwa
ufasaha hali ilivyokuwa.
Mmojawapo wa watu waliokuwa na kumbukumbu nzuri ya tukio
hilo alikuwa John Lange, balozi mdogo wa Marekani nchini Tanzania.
Balozi huyo alieleza kuwa wakati wa tukio, yeye pamoja na maafisa
wengine sita wa ubalozi huo walikuwa katika kikao cha kazi
kilichokuwa kikifanyika ghorofa ya tatu. Lengo la kikao hicho lilikuwa
kuandaa mapokezi ya balozi mpya aliyeteuliwa kuiwakilisha serikali ya

73
GO DW IN C H IL EWA | 74

Marekani nchini Tanzania. Ghafla ulitokea muungurumo mkubwa


uliopasua vioo vya madirisha na kusambaza vitu vyote vya ofisini.
Alipogeuka kuangalia nini kilichotokea, alishituka kuona damu
ikimiminika kutoka kwa kila mtu aliyekuwemo ofisini humo. Kila mtu
alikuwa amejeruhiwa vibaya. Kwa sekunde kadhaa aliendelea kusikia
mfululizo wa miungurumo mingine midogo dogo inayofanana na milio
ya bunduki. Baadae alitambua kuwa milipuko hiyo ilisababishwa na
kupasuka kwa matairi ya magari yaliyokuwa yakiungua kwenye
maegesho iliyokuwa nje, mbele ya ubalozi. Kwa vile majeraha aliyopata
hayakuwa mbaya sana, Lange aliweza kuinuka, na kuwasaidia wengine
kutoka nje ya jengo. Akiwa hapo, balozi wa Ufaransa nchini Tanzania
alimfuata, akamchukua kumpeleka ubalozini kwake. Balozi huyo
alikuwa mmoja wa mamia ya wasamalia wema waliokimbilia eneo la
tukio kutoa msaada.
Afisa mwingine Elizabeth Slater, (Information officer) wa US
Department of State, alikieleza kikosi kazi kuwa, kupona kwake ni
muujiza mkubwa.kwani mlipuko wa bomu ulimfanya apoteze fahamu
kabisa. Alipozinduka alijikuta akiwa amefunikwa na kifusi, huku mwili
wake ukiwa umelowa kitu kinachofanana na Mafuta. Sekunde chache
baadae alipata fahamu vizuri na kutambua kuwa maji yale hayakuwa
mafuta, bali damu iliyokuwa ikibubujika, na kuchanganyika na vumbi.
Wakati akihangaika kujiinua, watoa msaada walifika na kuondoa kifusi
kilichokuwa kimemfunika yeye na mwenzake, hali iliyowawezesha
kutoka katika chumba hicho. Akiwa njiani kuelekea nje, Elizabeth
aliona vipande vya nyama na viungo vya watu vilivyosambaa kila
mahali, hali iliyomfanya mwenzake asite kukanyaga eneo hilo bila
viatu. Alipofika nje, kwenye kibanda cha walinzi mahali kilipokuwa
kitovu cha mlipuko, alimuona mlinzi mmoja wa kampuni ya Ultimate
security akiwa ameungua mwili mzima. “He didn’t have any skin left…I
just wished he would hurry up and die” alisema akiwa na maana “Hakuwa
na ngozi yoyote iliyobaki (mwilini mwake)…nilitamani afe haraka
iwezekanavyo.”
Kikosi kazi pia kilimuhoji Justina Mdobilu, mtafsili (translator) wa
ubalozi wa Marekani. Dada huyo aliyekuwa na ujauzito wa miezi nane,
alikuwa mmoja wa watu waliohudhuria kikao kilichoitishwa na balozi
mdogo John Lange ofisini kwake. Katika maelezo yake Justina
aliwaeleza maafisa wa kikosi kazi TANBOMB kwamba, wakati kikao
kikiendelea, ghafla aliona mwanga mkali (flash) kama radi. Mwanga huo
ulifuatiwa na muungurumo mkubwa ulioambatana na vumbi, vipande

74
75 | SH U H U DA ZA J A SU SI – NDA NI YA IDA RA

vya vioo na vitu vinginevyo vilivyorushwa kwa nguvu. Vitu hivyo


vilimpiga, na kumchana mikono aliyokuwa ameitumia kujiziba uso
wake. Kwa sekunde kadhaa aliduwaa asijue la kufanya. Alipopata
fahamu alijiona akiwa chini, damu imetapakaa kila mahali. Alipoangalia
vizuri alimuona kila mtu aliyekuwa ofisini humo akivuja damu. “I
thought I was dreaming” alimalizia, akiwa na maana “Nilidhani naota.”
Maelezo hayo yaliendana kabisa na maelezo aliyonipa siku ya Ijumaa,
tarehe 7 August 1998, muda mfupi baada ya tukio.
Kikosi kazi pia kilimuhoji Edward Rutahesherwa aliyekuwa
mlinzi wa kampuni ya Ultimate Security. Mlinzi huyo alieleza kuwa siku
ya Ijumaa ya tatrehe 8 August 1998 alikuwa na wajibu wa kulinda
sehemu ya mbele, kwenye geti la kuingilia ubalozini. Hata hivyo, dakika
kumi hivi kabla ya mlipuko, mlinzi mwenzie aliyekuwa akilinda upande
wa nyuma alimfuata kumtaka wabadilishane maeneo ya ulinzi ili aweze
kunywa chai. Edward alikubali kufanya hivyo na baada ya
makabidhiano alienda kwa mama lishe waliokuwa wakiuza chakula
mbele ya ubalozi huo. Mara tu baada ya kununua vitafunio hivyo,
Edward alienda nyuma ya ubalozi, mahali alipotakiwa kukaa wakati
akinywa chai. Lakini kabla hajaketi, akasikia mlipuko mkubwa
uliotingisha kila mahali. Kwa sekunde kadhaa alijikuta amebutwaa
asijue kilichotokea; lakini ghafla akaona moto mkubwa ukiwaka mbele
ya ubalozi. Haraka akakimbia kwenda upande huo kuangalia
kilichotokea. Alipofika alishitushwa kuona damu nyingi, na viungo vya
binadamu vikiwa vimesambaa kila mahali. Mlinzi aliyemfuata
kubadilishana lindo alikuwa mmoja kati ya waliouawa.
Kikosi kazi hiki pia kiliwahoji mamia ya watu wengine
waliokuwepo katika eneo la tukio. Watu walioonekana kuwa na taarifa
za maana waliorodheshwa na kupangiwa siku ya mahojiano. Kwa vile
wengi wa watu hao bado walikuwa katika hali mbaya ki afya ya mwili
na saikolojia, iliamuliwa mahojiano ya pili yakafanyikie majumbani
kwao, ubalozini, au mahali pengine watakapojisikia huru kuzungumza
kwa uhuru, bila hofu.
*******
Wakati kundi la pili likiendelea kuhoji watu mbalimbali, kundi la tatu
lilikuwa katika ofisi za makampuni ya simu kufuatilia kumbukumbu za
simu zilizopigwa nje ya nchi. Kwa jinsi maandalizi na utekelezaji mzima
wa shambulio hili ulivyofanyika tulikuwa na hakika ya asilimia mia moja
kuwa magaidi husika walikuwa na mawasiliano mazuri

75
GO DW IN C H IL EWA | 76

yaliyowawezesha kufanya uratibu wa kila hatua. Kwa vile wakati huo


matumizi ya barua pepe yalikuwa hayajasambaa sana kutokana na
uchache wa computer, na migahawa ya mtandao; njia pekee ya
mawasiliano ya haraka, na salama ilikuwa simu za mezani na mkononi.
Tofauti na leo ambapo makampuni yanayotoa huduma za simu za
mkononi ni mengi, wakati huo makampuni mawili tu ndiyo yalikuwa
yakitoa huduma hiyo: MOBITEL na TRITEL.
Kampuni ya MOBITEL ndiyo iliyokuwa ya kwanza kuanzisha
huduma ya simu za mkononi nchini mnamo mwaka 1993/94. Mmiliki
wa kampuni hiyo alikuwa Millicom International Cellular ya
Luxembourg, pamoja na wana hisa wake Ultimate Communications
Ltd, na Tanzania Telecomunications Corporation Limited (TTCL) ya
Tanzania. Huduma zilianza wakati mtandao wa analogue ukitumika, kitu
kilichofanya wateja kutozwa bei ya juu mno. Kabla ya kuunganishiwa
huduma, mteja alilazimika kutanguliza (deposit) ya shilingi 600,000 na
kulipa ghalama nyinginezo ili aweze kupewa namba. Kwa hiyo ni
wafanya biashara matajiri, viongozi wa juu serikalini, na wajanja
wachache tu walioweza kumudu huduma hiyo. Mwaka 1998 kampuni
ya MOBITEL ilianzisha huduma ya ‘Simu Poa’ iliyowawezesha wateja
kulipia huduma kwa kutumia ‘kadi poa’ (prepaid cards). Utaratibu huo
uliiwezesha kampuni kupata wateja wengi zaidi na kujitanua mikoani.
Kampuni ya TRITEL (Tri-Telecomunication (T) Ltd ilikuwa ya pili
kuanzisha huduma hiyo nchini. Kampuni hii ilianzishwa mwaka
1994/95 ikiwa ni muungano wa kampuni ya VIP Engineering and
Marketing ya Tanzania, na Technology Resources Industries Berhad
(TRI) ya Malaysia. Ingawa kampuni hii ilichelewa kuingia nchini,
ilikuwa ya kwanza kutumia mfumo wa GSM (digital) uliokuwa bora
zaidi kulinganisha na ule uliokuwa ukitumiwa na washindani wake.
Kwa sababu hiyo, matajiri na watu wengine wenye uwezo waliihama
MOBITEL kujiunga na TRITEL, au walinunua simu ya ziada.
Uchunguzi ulianzia katika kampuni ya MOBITEL iliyoonekana
kutumiwa na watu wengi zaidi. Siku hiyo, majira ya saa sita mchana,
kundi la mawakala wanne wa FBI wakifuatana na afisa usalama wa
Taifa GK (jina bandia), afisa wa CID mwenye cheo cha mkaguzi wa
polisi (Inspector) Valentino Mlowola, na askari wengine wawili walifika
katika ofisi ya MOBITEL iliyokuwa mtaa wa Lugoda, eneo la Gerezani
na kuegesha gari katika maegesho yaliyokuwa mbele ya ofisi hiyo.
Walipoingia ndani walipokelewa na dada mmoja, aliyewasalimu kwa
uchangamfu akidhani ni wateja wapya. Uchangamfu huo uliyeyuka

76
77 | SH U H U DA ZA J A SU SI – NDA NI YA IDA RA

kama siagi katika kikaango baada ya inspector Valentino kujitambulisha,


na kuwatambulisha mawakala wa FBI aliofuatana nao.
“Unaitwa nani? Inspector Valentino alimuuliza.
“Naitwa Joyce” (jina bandia)
Baada ya kuulizana maswali mengine ya kuwawezesha kufahamiana
zaidi Valentino akaingia moja kwa moja kwenye suala la msingi.
“Tunafanya uchunguzi wa tukio la mlipuko wa bomu uliotokea
katika ubalozi wa Marekani siku ya ijumaa asubuhi. Tumekuja hapa
kwa sababu tunaamini ofisi yenu inaweza kutusaidia. Sijui uko tayari
kwa hilo? Inspector Valentino alimueleza taratibu kwa lugha ya
kiingereza ili mawakala wa FBI waweze kuelewa kinachozungumzwa.
“Itategemea aina ya msaada mnaouhitaji, kama uko chini ya uwezo
wangu sawa, kama sitaweza kuwasaidia natumaini hamtanilaumu..”
alijibu kwa maringo huku akiwaonesha mahali pa kukaa.
“Kama nilivyosema, tunafanya uchunguzi wa tukio la bomu katika
ubalozi wa Marekani. Kutokana na utaalam tulionao, na jinsi tukio
lilivyofanyika, tunaamini waliohusika walikuwa na mawasiliano ya
simu, yaliyowawezesha kuratibu mipango yao. Kwa hiyo tunahitaji
utupatie record za simu zote zilizopigwa nje ya nchi katika kipindi cha
miezi mitatu; yaani kuanzia mwezi March mpaka sasa, ili tuangalie simu
hizo zilipigwa na kwa nani, kwenda nchi gani, na kwa nani.”
Inspector Valentino alieleza kwa umakini mkubwa.
“Sheria za kampuni hazituruhusu kutoa taarifa za wateja kwa mtu
yeyote. Taarifa hizo ni siri ya mteja na sisi kama kampuni hatuwezi
kumpa mtu yeyote bila idhaa ya mwenyewe. Kwa kifupi kufanya hivyo
ni kosa linaloweza kunifukuzisha kazi” Alijibu kwa kujiamini.
“Naelewa kuna sheria za kazi, lakini hili ni swala nyeti linalohitaji
kushughulikiwa haraka. Isitoshe taarifa hizo huzitoi kwa mtu binafsi,
unazitoa kwa serikali. Ndiyo maana kabla ya kukueleza hitaji letu
nilijitambulisha kuwa mimi ni afisa upelelezi kutoka idara ya upelelezi
wa makosa ya jinai, na hawa ni mawakala wa FBI sasa tatizo liko wapi?”
Valentino alijaribu kumuelewesha.
“Najua ni suala nyeti, lakini sheria hainiruhusu kufanya hivyo.
Labda niwapeleke mkazungumze na bosi wangu pengine yeye anaweza
kuwasaidia”
“Sawa tupeleke kwa bosi wako”
Mara moja msichana huyo aliinuka na kuwaongoza katika ofisi
nyingine iliyokuwa pembeni kabisa.
“Bosi kuna wageni hawa wanahitaji msaada wako” Alimwambia

77
GO DW IN C H IL EWA | 78

kijana mmoja mtanashati aliyekuwa amekaa kwenye kiti kilichokuwa


nyuma ya meza kubwa iliyopangwa vizuri.
“Wewe umeshindwa kuwasaidia?” Aliuliza kwa mshangao.
“Wasikilize tu bosi” alijibu huku akicheka.
“Karibuni sana, naitwa Calvin” alijitambulisha
Kwa mara nyingine inspekta Valentino alijitambulisha, na
kuwatambulisha mawakala wa FBI aliofuatana nao. Mawakala hao kila
mmoja akatoa kitambulisho chake na kumuonesha kijana huyo.
“Tunajua una kazi nyingi sana, hivyo tusingependa kukupotezea
muda mwingi, tutajitahidi kujieleza kwa kifupi sana” Wakala wa FBI
aitwae Stephene alimueliza kijana huyo baada ya inspector Valentino
kumuashiria aendelee na mazungumzo.
“Hakuna tatizo, tunaweza kuzungumza”
“Unaitwa nani?
“Naitwa Calvin, (jina bandia) ni meneja wa huduma za wateja”
“Mr Calvin, Bila shaka umepata habari za mlipuko wa bomu
uliotokea wiki iliyopita”
“Ndiyo, nimesikia katika vyombo vya habari, poleni sana”
“Ahsante sana. Kama ulivyosikia shambulio hilo mpaka sasa
limesababisha vifo vya watu zaidi ya 220. Kati ya hao 10 ni raia wa
Tanzania, 14 ni raia wa Marekani, na waliobaki ni raia wa Kenya na
nchi nyinginezo. Idadi ya vifo hivyo inaweza kuongezeka muda
wowote ule kwa sababu baadhi ya majeruhi wana hali mbaya sana.
Ukiacha watu waliokufa, ambao kwa vyovyote hatuwezi kuwarudisha,
watu wengine zaidi ya 5000 wamejeruhiwa katika milipuko hiyo. Wako
waliopoteza macho yao, na hawataweza kuona tena. Wako
waliopoteza miguu yao, hawataweza kutembea tena, na wengine
wamevunjika mgongo, na viungo vinginde hivyo Maisha yao
hayatakuwa kama zamani; yameharibika kabisa.” Alitulia kidogo
kumpa nafasi ya kutafakari kisha akaendelea.
“Kitu kinachokera, ni kwamba waliopanga tukio hili, na
kughalimia utekelezaji wake sasa hivi wapo mahali fulani wanacheka na
kufurahia Maisha, pengine wamelala usingizi, au wanakunywa pombe,
who knows! Sisi tunaomboleza, wao wanaendelea na maisha kama
kawaida. What a shame? Ndiyo maana mimi na mawakala wenzangu wa
FBI tumesafiri maelfu ya maili kuja hapa kuhakikisha watu hao
wanapatikana. Ndiyo maana Inspector Valentino, kamishna
Manumba, na DCI Adadi hawalali usingizi kuhakikisha watu hao
wanapatikana. Nina hakika hata wewe unatamani sana watu hao

78
79 | SH U H U DA ZA J A SU SI – NDA NI YA IDA RA

wapatikane, sivyo Calvin? Alimuuliza huku akimkazia macho.


“Ndiyo, ndiyo” Calvin alijibu
“Ndiyo maana tuko hapa, tunaamini unaweza kutusaidia. Inspector
Valentino atakueleza msaada tunaoutaka kutoka kwako” Stephen
alimalizia huku akimgeukia Valentino kumuashiria aendelee.
“Bwana calvin, natumaini umeyasikiliza kwa makini maelezo ya
Stephen, kwa sababu hiyo sina sababu ya kuyarudia. Msaada tunaohitaji
kutoka kwako ni record ya simu zote zilizopigwa nje ya nchi kuanzia
mwezi Machi hadi sasa. Hatuna uhakika ni nyingi kiasi gani, lakini
tungependa kuzipata zote ili tuweze kuzifanyia uchunguzi” Inspector
Valentino alisisitiza.
“Afande mnaniweka katika wakati mgumu sana. Kwa sababu
mimi, kama Calvin sina kipingamizi na hilo, lakini sheria za kampuni
haziniruhusu. Kimsingi, mteja anaweza kuifikisha kampuni
mahakamani endapo atagundua taarifa zake zimetolewa bila ridhaa
yake. Kwa hiyo mimi kwa nafasi yangu, siwezi kutoa taarifa hizo. Lakini
naamini kwa suala hili, mkizungumza na bosi anaweza kuwaruhusu.”
“Bosi wako yupo tuongee nae? Stephen alimuuliza.
“Hapana, lakini atakuwepo hapa kesho asubuhi”
“Lakini bwana Calvin, huoni kama kufanya hivyo ni
kutuchelewesha kazi tunayotakiwa kuifanya ?
“Hapana afande, sina nia ya kuwachelewesha” alijibu huku akianza
kupoteza uchangamfu aliokuwa nao. Baada ya majadiliano ya muda
mfupi, Inspekta Valentino akashauri suala hilo liashirishwe mpaka siku
inayofuata ili taratibu za kiofisi zifanyike kuruhusu upatikanaji wa
taarifa zinazohitajika..

_____________

.
.

79
SURA YA NNE

FUNUNU

W
iki zilipita kwa kasi kama kufumba na kufumbua. Wingi
wa majukumu na kashikashi zake ulitufanya tulazimike
kusahau maisha ya uhuru na starehe tuliyokuwa
tumeyazoea. Kila siku ilikuwa na mambo mapya,
muhimu, na ya kuumiza kichwa kuliko siku iliyotangulia. Kila saa mbili
asubuhi tulikutana kwenye eneo la tukio, au ofisini kwa msaidizi wa
mkurugenzi wa makosa ya jinai Senior Assistant Commissioner of Police
(SACP) Robert Manumba kupeana taarifa (briefing) ya maendeleo ya
uchunguzi. Taarifa hiyo ilikuwa muhimu sana katika kupanga namna
ya kufuatilia leads zilizopatikana toka vyanzo mbalimbali. Kwa ujumla
kazi yetu ilikuwa imeanza kuzaa matunda, na muelekeo wa upelelezi
ulikuwa umeanza kujipambanua.
Katika kipindi hicho pia tulipata fursa ya kutembelewa na
aliyekuwa mkurugenzi mkuu wa shirika la ukachero la Marekani (FBI).
Bwana Louis Free. Mkurugenzi huyo aliwasili nchini tarehe 20 August
1998 kujionea madhara yaliyosababishwa na shambulio la bomu na pia
kututia moyo maafisa wa kikosi kazi (Task Force) tuliokuwa tukifanya
kazi ya kuwasaka magaidi husika ili waweze kuchukuliwa hatua za
kisheria. Akiwa jijini Dar es Salaam mkurugenzi Louis Free alipokea
taarifa ya uchunguzi kutoka kwa viongozi wetu, na akashiriki katika
kupanga mikakati ya kuimarisha ulinzi, na kutanua wigo wa upelelezi
Yapo mambo mengi ya kutia moyo yaliyokuwa yameshafanyika
kufikia wakati huo. Jambo la kwanza lilikuwa mafanikio ya uchunguzi
wa eneo la tukio. Baada ya kazi ngumu ya siku kadhaa, wataalam wa
uchunguzi wa milipuko (Bomb Squad) wakishirikiana na timu ya
uchunguzi wa eneo la tukio (Forensic experts) walifanikiwa kupata

80
81 | SH U H U DA ZA J A SU SI – NDA NI YA IDA RA

vipande vya ushahidi vilivyoleta nuru ya matumaini katika uchunguzi


wa tukio zima. Vipande hivyo vilikabidhiwa kwa mtaalam wa
uchunguzi vyuma (metallurgy analyst) wakala wa FBI (Special Agent)
Kathleen Lundee aliyekuwa akichunguza kwa makini kila kipande cha
chuma kilichopatikana. Ili kupata majibu sahihi, Kathleen alitumia ICP
process kutambua muundo wa kikemikali na viasilia vilivyogandana
katika vyuma. Matokeo ya uchunguzi huo yalibainisha kuwa baadhi ya
vyuma vilikuwa vipande vya mitungi ya gesi iliyotumika kutengeneza
bomu. Taarifa ya Kathleen iliungwa mkono na ya wataalam wengine
wa milipuko (Bomb Squad) waliochambua muundo wa viasilia na
kemikali zilizotumika kutengeneza bomu (chemical profiling of explosives).
Katika taarifa yao wataalam hao pia walithibitisha kutumika kwa
mitungi ya gesi za oksijen, acetylene na hydrogen. Kipande kingine
kilikuwa na namba maalum zilizochongwa ubavuni, na viasilia vyake
vilikuwa tofauti na vile vya mitungi ya gesi. Uchunguzi ulibainisha
chuma hicho kilikuwa sehemu ya chassis ya gari lililobeba bomu, na
namba iliyochongwa ubavuni mwake ilikuwa Chassis number.
Matokeo haya yalituweka katika nafasi nzuri ya kumpata mmiliki
wa gari lililobeba bomu. Kwa kifupi namba inayochapwa katika chassis,
ambayo pia huchapwa sehemu ya mbele kwenye makutano ya kioo cha
mbele na kiwiliwili (body) cha gari, ndiyo namba halisi ya utambulisho
wa gari. Kwa kawaida watu wengi huipa umuhimu mkubwa namba ya
leseni (lisence plate number) kwa sababu ndiyo inayoonekana haraka. Hata
hivyo namba hiyo si ya kudumu, na hubadilishwa kila gari inapopata
usajili mpya. Chassis number ambayo pia huitwa Vehicle Identification
Number (VIN) ndiyo namba ya kudumu inayobeba taarifa za kipekee
zinazoitambulisha gari. Taarifa hizo ni pamoja na muundo wa gari hiyo,
kampuni iliyotengeneza, mahali ilipotengenezwa, ukubwa wa injini,
mahali ilipounganishwa (assembled) na alama ya siri ya mtengenezaji
(security code) inayothibitisha uhalali wa VIN number yenyewe. Ili
kurahisisha mtiririko wa taarifa, namba hii huunganishwa na taarifa
binafsi za mmiliki wa gari hususan kitambulisho au leseni yake ya
udereva, hati ya bima, anuani ya makazi, na taarifa nyingine
zinazoweza kusaidia kumtambulisha muhusika kama ikitokea ajali au
tukio la uhalifu. Kimsingi namba hii tunaweza kuifananisha na alama
za vidole vya mwanadamu.
Mara tu baada ya kukamilika kwa uchunguzi wa vipande hivyo,
wataalam wa milipuko walituma taarifa yao kwenye data base ya FBI
kuona kama kuna taarifa zozote zinazoihusu gari hiyo. Muda mfupi tu

81
GO DW IN C H IL EWA | 82

baadae yalipatikana majibu kuwa chasses hiyo ilikuwa ya roli dogo (truck)
aina ya Nissan Atlas lililotengenezwa nchini Japan. Ili kupata taarifa
zaidi kikosi kazi kilituma namba hiyo kwenye ofisi za Interpol na
mawakala wengine ili waweze kufuatilia kiwanda kilichotengeneza gari
hiyo kujua iliuzwa wapi na kwa nani. Haikuchukua muda mrefu
tukaletewa ujumbe kuwa gari hiyo iliingizwa nchini Tanzania na
kampuni iitwayo JABA Tanzania Limited. Kampuni hii ilikuwa
ikifanya biashara ya kuagiza magari toka sehemu mbalimbali duniani
na kuyauza kwa wateja wao kwa fedha taslimu. Mengi ya magari hayo
yalikuwa yaliyotumika (used cars) hivyo yaliuzwa kwa bei nafuu iliyovutia
watu wa kipato cha kawaida.
Bila kupoteza muda siku hiyohiyo waliteuliwa maafisa watano
kutoka miongoni mwetu kuifuatilia kampuni ya JABA. Lengo la
ufuatiliaji huo lilikuwa kujua kama kampuni hiyo bado ilikuwa mmiliki
halali wa gari hiyo iliyotuhumiwa kubeba bomu. Kama JABA ilikuwa
mmiliki halali basi ilipaswa kueleza gari hiyo iilikuwa wapi wakati huo,
na kama liliuzwa lilinunuliwa nani, na kwa utaratibu gani. Pamoja na
hayo maafisa hao walipaswa kuwatambua wamiliki wa kampuni hiyo,
kujua taratibu za uendeshaji wa kampuni hiyo, na kama ina uhusiano
wowote na vikundi vya kigaidi na au washirika wake.
Jambo la tatu kwa umuhimu likuwa matokeo ya uchunguzi wa
mawasiliano ya simu za watuhumiwa. Baada ya safari nyingi kwenye
ofisi zote za makampuni ya simu nchini, hatimaye tulifanikiwa kupata
namba za simu kadhaa zilizoonesha dalili ya kutumiwa na watuhumiwa
wa ugaidi. Namba ya kwanza ilikuwa 6880488
. Lorem ipsum dolor sit abet, constitutor despising alit. Prion sod
mi id ligula truism moles tie. Pelletize critique frangible augur, id
laborites’ pursue. Crams dui mi, macules egret rises id, sagittal pharetra
nigh. Present varies molls nulled. Present consequent magna a pharetra
ornate. Sid magna ulna, cangue vitae torpid a, blander dipygus eras.
Varmus gravida semper null, varies molies risks susceptive evet. Fusc
tempos risks ague, majestic a junto dictum non. Duisk vet puros
convallis, modesties eques utricles, Bibendum veldt. Nam quam nisi,
gravida vet subscript sod, plenitude sit abet sem. Pharsalus au dictum
orca. Pelletize in pharetra libero. Sid a ornate nisi, diapaus effector

82

You might also like