You are on page 1of 19

AL-QALAM

AL-QALAM ni Makala inayotolewa


kwa lengo la kutoa elimu kwa jamii
ya Kiislam juu ya misingi tofauti
katika itikadi sahihi ya uislam. MAJUMUISHO YA ANUANI
Sifa zote njema zinamstahiki Allah
Ramadhan, 1443 – April, 2022 (Subhanahu Wataala), ambaye
ameumba mbingu na ardhi kwa haki.
Sala njema na salam ziende kwake
Anuani: “Mkusanyo huo KWETU ni mtukufu wa darja, kipenzi cha Allah na
Waislam wote Mtume Muhammad
Mwepesi”
(Alaihi Swalatu Wasalam).
Kwa maoni ama ushauri juu ya Nawasalimu kwa maamkizi matukufu ya
Makala hii usisite kuwasiliana na Amani ndugu zangu wasomaji, Assalam
waandishi: Alaikum Warahmatullah Wabarakatu.
1. Farid Bakar Hamad Ndugu zangu wapenzi wasomaji wa
2. Mohammad Abdallah Kifosha Makala za Al-Qalam kupitia Makala hii
tunakusudia kufanya majumuisho ya
Mawasiliano:
sehemu ya kwanza ya mtiririko wa
Simu: +255748202226 Makala zetu kuanzia Makala ya kwanza
Whatsapp: +255777002226 hadi Makala ya tano ambazo zilitoka
hapo awali katika vipindi tofauti.
Makala hii imerejelewa na
Aidha kupitia Makala hii tunakusudia
Akhy Mohamed Rajabu (Ibn Rajab
(kwa uwezo wa Allah) kufanya
Alhassany),
uchambuzi wa kina juu ya kauli ya Allah
Sudan,
(Subhanahu Wataala) ndani ya Qur’an
Khartoum/Jefer Gharbi
inayosema;
Ramadhan, 1443 – April 2022.
‫ض َع ْن ُه ْم ِس َراعا ً ٰذ ِﻟ َﻚ‬
ُ ‫شقﱠ ُق ٱﻷ َ ْر‬َ َ‫يَ ْو َم ت‬
﴾٤٤﴿‫ِير‬ٌ ‫علَ ْينَا يَس‬
َ ‫َﺣ ْش ٌر‬
“Siku itakapo wapasukia ardhi mbio
mbio! Mkusanyo huo kwetu ni
mwepesi.” (50:33)

1|Page
Katika mtiririko wa Makala zetu tuligusia kama mawaidha kwetu juu ya yote
anuani tofauti ambazo zote zikiwa na ambayo yatabainishwa ndani yake.
lengo la kuipa tanbih jamii ya kiislam juu
HAKIKA YA MTETEMEKO NA
ya athari na makatazo ya Allah
MPASUKO WA ARDHI
(Subhanahu Wataala) katika mambo
mbali mbali ikiwamo riba, shirki, Riya’a, Ndugu zangu wasomaji, kama utakuwa
Kibri na mengi mengineyo, ambapo unafatilia vyema Makala zetu, katika
katika kila kipengele tulibainisha kitabu chetu cha kwanza tulizungumziya
ghadhabu za Allah sambamba na mazito Matukio makubwa ambayo yatatokea
ambayo yameandaliwa kuwakabili wale siku ya kiyama ambayo miongoni mwa
ambao hawataacha kujiepusha na matukio hayo ni mpasuko na
madhambi hayo makubwa. Kupitia mtetemeko wa ardhi kama ambayo
Makala hii, tumesema ni mjumuisho wa Allah (Subhanahu Wataala) ameutolea
hayo yote kwa maana tunaenda kufanya ufafanuzi ndani ya Qur’an:
uchambuzi kupitia ushahidi ndani ya
Qur’an na Sunnah ya namna ambavyo ﴾١﴿‫ض ِز ْﻟزَ اﻟَ َها‬ ِ َ‫إِذَا ُز ْﻟ ِزﻟ‬
ُ ‫ت ٱﻷ َ ْر‬
wale ambao hawakuwaidhika, watavyo
“Itakapo tetemeshwa ardhi kwa
kusanywa na Allah (Azza Wa Jallah) siku
mtetemeko wake” (99:01)
ya Kiyama. Mkusanyo ambao kila mmoja
atakuwa na namna yake ya kufika Allah (Subhanahu Wataala)
kwenye viwanja vya mahshar (Kiyama) ataitetemesha ardhi kwa malengo
kama ambavyo Allah ameeleza kwamba maalumu, na moja katika malengo yake
tukio la mkusanyiko huo kwake ni ni ili ardhi itowe Mizigo ambayo
mwepesi sana. imehifadhi ndani ya matumbo yake,
pamoja na kutoa khabari zote ambazo
Hivyo kupitia makala hii tutaigawa Aya
zilifanywa juu ya mgongo wake.
hii katika sehemu kuu mbili;
Miongoni mwa mizigo iliyopo ndani ya
1. Ni ile kauli ya Allah (Subhanu tumbo la ardhi ni viumbe ambavyo
Wataala) “Siku itakapo wapasukia vilizikwa ndani yake.
ardhi mbio mbio!....”
Kwa mtetemeko huu kila kiumbe
2. Na ya pili ni; “….Mkusanyo huo
ambacho kilizikwa ndani ya tumbo la
kwetu ni mwepesi.”
ardhi kitatolewa tayari kwa ajili ya
Dhumuni kubwa la kuigawa aya hii kuitikia wito wa mwenye kunadi. Kwa
sehemu hizi mbili ni kuweza kuwafikishia kauli ya Allah:
faida za ndani ambazo tunazipata ndani
ya Qur’an, sambamba na kuangalia ﴾٤﴿‫ت‬ ُ ‫َو ِإذَا ْٱﻟقُب‬
ْ ‫ُور بُ ْعثِ َر‬
namna ambavyo Allah (Subhanahu
“Na Makaburi yatakapo fukuliwa”
Wataala) ameifanya Qur’an kuwa ni
(82:04)
uongofu juu ya kila jambo. Tusome
pamoja makala hii ili tufaidike na iwe ni

2|Page
Baada ya makaburi kupasuliwa na kutoka ndani ya kaburi lake atatahamaki
kufukuliwa viumbe wote wakuwa juu ya anakimbia kuifata sauti hiyo na kila
mgongo wa ardhi kwa ajili ya kuingia kiumbe siku hiyo itakuwa chini sauti
katika hatua nyengine ya maisha baada yake kwa khofu, uoga na uzito wa siku
ya maisha ya kaburini, Allah hiyo na hatakuwa na hiyari juu ya
(Subhanahu Wataala) ametumia neno kukimbilia huko ambako kila mtu
(mbio, mbio) katika aya ya anuani anapaswa kufika kwa kasi.
akimanisha kwamba kila kiumbe
Ndugu zangu wasomaji, chukuwa
kitatoka ndani ya mgongo wa ardhi
taswira hii, unaonaje wakati unasoma
akiwa anakimbia kwa kasi kubwa sana
makala hii, Mamlaka kuu ya dola ya
kuelekea kwenye viwanja vya hisabu.
sehemu uliyopo itoe taarifa ya kutaka
Imeelezwa na baadhi ya wanazuoni
watu wote wa eneo hilo kufika eneo
kwamba maana ya neno (Sira’a) ni kasi
maalumu lililowekwa bila kukosa kwa
ambayo inafananishwa na kasi ya
kipindi kidogo sana baada ya taarifa
mshale unapotoka kwenye mkuki. Hili
hiyo kutolewa!
limefafanuliwa waziwazi na kauli za
Allah (Subhanahu Wataala) ndani ya Unaweza kupata taswira ya hali itakavyo
Qur’an akisema; kuwa kwa wakati huo, kila mmoja
atakimbilia eneo hilo kwa namna yoyote
ِ ‫ور فَإِذَا هُم ِ ّمنَ ٱﻷ َ ْجدَا‬
‫ث ِإ َﻟ ٰى‬ ِ ‫ص‬‫َونُ ِف َخ ِفى ٱﻟ ﱡ‬ ile, unaonaje msongamano wa viumbe,
﴾٥١﴿ َ‫َر ِبّ ِه ْم َين ِسلُون‬ vipando utavyokuwa, chukuwa tena
taswira ya tabia ya viumbe haswa
“Na litapulizwa baragumu, mara binadamu kuhoji na kudadisi juu ya
watatoka makaburini wakikimbilia kwa taarifa hiyo, kwa tabia ya mwanadamu
Mola wao Mlezi” (36:51) wapo ambao watajaribu kukataa taarifa
Aidha Allah (subhanahu Watala) hiyo kwa kutaka kuona nini kitatokea
anasema pia; asipo itikia wito huo! Wapo ambao kama
asili ya binadamu watasubiri wengine
‫ث ِس َراعا ً َكأَنﱠ ُه ْم إِﻟَ ٰى‬
ِ ‫يَ ْو َم َي ْخ ُر ُجونَ ِمنَ ٱﻷ َ ْجدَا‬ wafike kwanza ili ajue nini haswa
﴾٤٣﴿ َ‫ب يُو ِفضُون‬ ٍ ‫ص‬ ُ ُ‫ن‬ kinaenda kutokea! Wapo ambao pia
watatumia fursa hiyo kupitisha tabia ya
”Siku watakapotoka makaburini kwa dhulma kwa wengine wasio jiweza ili
upesi kama kwamba wanakimbilia wajipatie kipato!
mfundo (Alama iliyowekwa
Hapa ndipo tunaweza kupata maana
kuifikia)” (70:43)
halisi ya anuani yetu juu ya mkusanyo
Ndugu zangu wasomaji, hii sio siku ya wa Allah (subhanahu Wataala) kila
mzaha na wala sio siku ya kuitilia shaka kiumbe hatakuwa na budi bali kuitikia
na kwa hakika kila mmoja wetu ajiandae na hakuna uwezekano wowote kwa mtu
nayo kwani pale ukelele wa baragumu yeyote kukata shauri ya aidha kuenda
utakapo pulizwa na kila kiumbe kuinuka au kutokuenda. Na hapa Qur’an

3|Page
inatufafanulia zaidi kwamba siku hiyo ni akhera. Ama kwa makusudio ya
hakutakuwa na sauti yoyote nyengine Makala hii, tutagusia hii mikusanyiko
kutoka kwa viumbe, hakuna wa kuuliza miwili ya Akhera na kwa uwezo wa Allah
wala kujibu, hakuna wakulalamika wala tukipata nafasi nyengine tunatachambua
kushauri, kwa kauli ya Allah; hiyo mikusanyiko ya duniani.

ِ َ‫ى ﻻَ ِع َو َج ﻟَهُ َو َخ َشع‬


‫ت‬ َ ‫يَ ْو َمئِ ٍذ َيت ﱠ ِبعُونَ ٱﻟدﱠا ِع‬ Kama anuani ya makala yetu
‫لر ْﺣ َم ٰـ ِن فَﻼَ تَ ْس َم ُع ِإﻻﱠ‬
‫ص َواتُ ِﻟ ﱠ‬ ْ َ ‫ٱﻷ‬ inavyoeleza juu ya mkusanyo mbele ya
Allah (Subhanau Wataala) kabla ya
﴾١٠٨﴿ً ‫ه َْمسا‬ mkusanyo huo Qur’an imeeleza kwamba
kwanza viumbe wote watatolewa kutoka
“Siku hiyo watamfuata muitaji asiye na
katika makaburi yao tayari kwa ajili ya
upotofu. Na sauti zote zitamnyenyekea
kukusanywa mbele ya Allah kwenye
Arrahmani Mwingi wa Rehema. Basi
uwanja wa hisabu, hapa kuna jambo la
husikii ila mchakato na mnong’ono”
kuzingatia ndugu yangu msomaji, nukta
(20:108)
hii ni muhimu kutambuwa kwamba
Katika Tafsir ya Ibn Kathir (Radhi za wakati viumbe wakikimbilia kuelekea
Allah ziwe juu yake) amemnukuu Ibn kwa muitaji, sio kila kiumbe kitafufuliwa
Abbas akisema maana neno “Hamsa” akiwa na hali sawa na mwengine kila
kwamba ni ukimya uliopitiliza, aidha mmoja ama kundi watatofautiana kwa
Sa’d bin Jubayr amesema kwamba ni mujibu wa Amali ambazo walizifanya
ukimwa isipikuwa sauti ya mchakato wa wakati wa uhai wake.
hatua zinavyokanyaga ardhi.
Tunapaswa kutambuwa pia kwamba
MKUSANYO (‫ر‬ ٌ ‫ ) َﺣ ْش‬MBELE YA Allah Subhanahu Wataala atawakusanya
viumbe huko akhera katika mikusanyo
ALLAH (SUBHANAHU WATAALA)
miwili, moja ni mkusanyo wa kutokea
Ndugu zangu wasomaji, sehemu yetu ya makaburini kuelekea kwenye viwanja
pili ya uchambuzi ni kugusia mkusanyo vya hukumu na pili ni mkusanyo
ambao Allah (Subhanahu Wataala) kutokea viwanja vya hukumu kuelekea
ameuelezea kwamba kwake ni aidha Jannat (Allah atujaaliwe tuwe
mkusanyo mwepesi, ingawaje kwa jicho miongoni mwao) au mkusanyo
la kibinadamu likiwa haswa limekosa kuelekeya kwenye moto wa Jahannam
taqwa ya kweli huweza kupata (Allah atukinge na kutuepusha na
mashaka. mkusanyo huu).
Baadhi ya wafasir wa Qur’an wanasema Na katika kila mkusanyo Allah
kwamba ndani ya Qur’an tukufu, Allah atawaweka viumbe kwenye makundi
(Azza wa Jallah) amezungumzia yanayofanana, kwa maana ya kwamba
mikusanyo ya aina nne (04) ambapo mathalan, kama mja alikuwa ni
wanaeleza ya kwamba mikusanyiko mshirikina, wakati mkusanyo wa kwanza
ٌ ‫ ) َﺣ ْش‬miliwi ni hapa duniani na miwili
(‫ر‬ kuelekea kwenye viwanja vya hukumu

4|Page
atakusanywa na wanaofanana naye na ila kwa upande wa waumini wakifika
kama ni Muumin basi atakusanywa zilipo pepo hizo watakuta milango
kwenye kundi moja na waumini imeshafunguliwa hii ni fanisi ya Qur’an
wengine. Hii inathibishwa kwa kauli za ambayo tunahitaji kuipambanuwa ili kila
Allah; mmoja wetu aweze kupata mazingatio.

‫َوسِيقَ ٱﻟﱠذِينَ َكـفَ ُر ۤواْ ِإﻟَ ٰى َج َهنﱠ َم ُز َمرا ً َﺣت ﱠ ٰى ِإذَا‬ Baada ya kuthibisha kwamba mikusanyo
‫ت أَب َْوابُ َها َوقَا َل ﻟَ ُه ْم خَزَ نَت ُ َهآ أَﻟَ ْم يَأْتِ ُك ْم‬
ْ ‫َجآ ُءوهَا فُتِ َح‬ yote miwili ya akhera, Allah
‫ت َربِّ ُك ْم َويُنذ ُِرونَ ُك ْم ِﻟقَـآ َء‬ ِ ‫س ٌل ِ ّمن ُك ْم يَتْلُونَ َعلَ ْي ُك ْم آيَا‬
ُ ‫ُر‬ atawakusanya viumbe katika mkusanyo
ْ wa kwanza (Kutoka Makaburini
‫ب َعلَى‬ ِ ‫ت َك ِل َمةُ ٱﻟ َعذَا‬ ْ ‫َي ْو ِم ُك ْم َه ٰـذَا قَاﻟُواْ َبلَ ٰى َوﻟَ ٰـ ِك ْن َﺣقﱠ‬
kuelekea viwanja vya Hukumu)
﴾٧١﴿ َ‫ْٱﻟ َكافِ ِرين‬
wakiwa katika makundi ambayo
“Na walio kufuru wataongozwa kuelekea wanafanana na matendo yao, ndipo
Jannamu kwa makundi. Mpaka sasa watasimamishwa mbele ya Allah
watakapo ifikia itafunguliwa milango wakiwa kwenye ardhi mpya aliyoiumba
yake, na walinzi wake watawaambia; Allah kwa lengo hilo, ardhi ambayo
kwani hawakukujilieni Mitume miongoni itakuwa safi yenye kunyooka na isiyo na
mwenu wakikusomeeni Aya za Mola hata chembe ya uchafu wowote wala
wenu Mlezi na kukuonyeni mkutano wa haina alama yoyote kutoka kwenye
siku yenu hii? Watasema: kwani! Lakini athari za viumbe. Hili linathibishwa
limekwisha thibiti neno la adhabu juu ya ndani ya Qur’an kwa kauli za Allah
makafiri.” (39:71) (Subhanahu Wataala) akisema;

Na kwa upande mwengine Allah ﴾٣﴿‫ﱠت‬ ُ ‫َو ِإذَا ٱﻷ َ ْر‬


ْ ‫ض ُمد‬
anasema;
“Na Ardhi itakapo tanuliwa” (84:03)
‫َوسِيقَ ٱﻟﱠذِينَ ٱتﱠقَ ْواْ َربﱠ ُه ْم إِﻟَى ٱﻟّ َجنﱠ ِة ُز َمرا ً َﺣت ﱠ ٰى إِذَا‬
Ibn Kathir katika tafsir yake
‫ت أَب َْوابُ َها َوقَا َل ﻟَ ُه ْم خَزَ نَت ُ َها َسﻼَ ٌم‬
ْ ‫َجآ ُءوهَا َوفُتِ َح‬
amesherehesha kwa kusema maana ya
﴾٧٣﴿ َ‫ع َل ْي ُكـ ْم ِط ْبت ُ ْم َفٱ ْد ُخلُو َها خَا ِﻟدِين‬
َ aya hii ni kusema kwamba ardhi siku
“Na walio mcha Mola wao Mlezi hiyo itaongezwa upana wake, na
wataongozwa kuendea Peponi kwa kutawanywa kuwa kama uwanda
makundi, mpaka watakapo fikilia, nayo mmoja.
milango yake imekwisha funguliwa. Baadhi ya makafiri waliposomewa aya
Walinzi wake watawaambia: Salaam hii wakauliza kuhusu majabali na milima
Alaikum, Amani iwe juu yenu! itakuwaje kama ardhi itakuwa
Mmet’ahirika. Basi ingieni humu make imetawanywa. Allah (Subhanahu
milele” (39:73) Wataala) akawajibu kupitia Surah Ta-Ha
Unaweza kuona utofauti wa makundi ‫ع ِن ْٱﻟ ِجبَا ِل فَقُ ْل َين ِسفُ َها َر ِبّى‬
َ ‫َويَسْأَﻟُون ََﻚ‬
haya hata namna ya mapokezi yao
wanayopokelewa, wale wa Jahannamu ﴾١٠٥﴿ً ‫نَسْفا‬
wanapofika ndipo milango hufunguliwa

5|Page
“Na wanakuiliza khabari za milima. mema ya ibada, kuomba msamaha kwa
Waambie: Mola wangu Mlezi ataivuruga makosa tuliyoteleza na kuhakikisha
vuruga” (20:105) tunajiweka mbali na kila jambo ambalo
linamkasirisha Allah kwani ghadhabu za
Hii yote ni kuthibithisha kwamba kwa
Allah ni kali na hakuna kati yetu
hakika siku hiyo ardhi itapitia katika
mwenye kuweza kuzihimili. Kumbuka
marekebisho makubwa kwa ajili ya
uzito na mateso ambayo yapo ndani ya
kuwapokea viumbe kwa ajili ya
mkusanyo huu wa kwanza tu ni mazito
mkusanyo wa kwanza katika kisimamo
kwa yoyote ambaye alifanyia mzaha
cha siku ya hukumu. Siku hii imeitwa
maneno ya Arrahman. Mkusanyo huu
siku ya kiyama kwamaana ya siku ya
wa kwanza unafunganishwa na
kisimamo ikiwa na ubainifu kwamba
kisimamo kirefu sana ambacho Allah
viumbe wote watasimama na hakuna
amekieleza ndani ya Qur’an kwamba
ambaye atakaa mbele ya Allah (Azza wa
siku hiyo kadiri yake ni sawa na miaka
Jallah) kama inavyothibitishwa ndani ya
khamsini elfu! (Surah Al-Ma’arij 70:4).
Qur’an Surah Al-Mutaffifin;
Hiki ni kisimamo kirefu sana ambacho
﴾٦﴿ َ‫اس ِﻟ َربّ ِ ْٱﻟ َعاﻟَ ِمين‬
ُ ‫َي ْو َم َيقُو ُم ٱﻟنﱠ‬ kwa makafiri na wale walio jisahau hapa
duniani itakuwa ni mkusanyo mzito sana
“Siku watapo msimamia watu Mola Mlezi
mbali na adhabu mbali mbali ambazo
wa walimwengu wote” (83:06)
zitakuwa zimeambatana na mkusanyo
Ibn Kathir katika kuifafanuwa aya hii, huu kuufikia uwanja wa hisabu ambazo
amenukuu hadith ya Imam Malik kuwa tutaziangalia hapo mbeleni, tuna kila
amepokea kutoka kwa Nafi’ ambaye sababu ya kujiandaa vyema haswa kwa
amepokea kutoka kwa Umar kwamba kutumia vipindi muhimu vya ibada
Mtume (Swallahu Alaihi Wassalam) (Kama Ramadhan) ambavyo ni vipindi
amesema; Hiyo ndio itakuwa siku vya mavuno ambavyo amali ya kawaida
ambayo viumbe watapo msimamia Mola hulipwa ujira maradufu.
wao Mlezi wa walimwengi wote, hadi
Kwa maana miongoni mwa faida za
mmoja azame ndani ya jasho lake
kumcha Allah unaweza kuziona kuanzia
kufikia katika usawa wa masikio yake.
katika mkusanyo huu wa kwanza ambao
Na ndio maana imepokelewa katika
unakadiriwa kisimamo chake kuwa sawa
kitabu cha Sunan Abu Dawud kwamba
na miaka Khamsini elfu, kwani Mtume
Mtume wa Allah akiomba na kujikinga
wa Allah ametoa bishara njema kwamba
kwa Allah kutokamana na uzito wa siku
urefu wa kisimamo hichi utasahilishwa
hii ya hukumu.
kwa waumini na kusahilishwa zaidi hadi
Ewe ndugu yangu msomaji hakika kuwa ni kisimamo chepesi zaidi ya
hakuna mzaha, na wala hakuna kisimamo cha Sala ya faradhi kama
chochote kinachoweza kutupa wepesi ilivyonukuliwa katika hadith sahihi ya Abi
katika siku ya mkusanyo huu zaidi ya Said Al Hidhrii kwamba; Mtume wa Allah
kujikurubisha kwa Allah kwa matendo aliisoma aya ya Surah Ma’arij alipofika

6|Page
kuelezea kwamba kisimamo cha siku MKUSANYO KUTOKA KUFUFULIWA
hiyo kitakuwa sawa na miaka khamsini MAKABURINI KUELEKEA VIWANJA
elfu, maswahaba wakamuliza; Ewe VYA MAHSHAR (Viwanja vya
Mjumbe wa Allah hiyo itakuwa ni siku Hisabu)

‫ض َع ْن ُه ْم ِس َراعا ً ٰذ ِﻟ َﻚ‬
ndefu sana! Mtume wa Allah akawajibu
kwamba Naapa kwa Mola Mlezi ambaye ُ ‫شقﱠ ُق ٱﻷ َ ْر‬َ َ‫َي ْو َم ت‬
nafsi yangu ipo mikononi mwake hakika ﴾٤٤﴿‫ِير‬ٌ ‫علَ ْينَا يَس‬
َ ‫َﺣ ْش ٌر‬
siku hiyo itakuwa sahali kwa muumini
zaidi ya kisimamo cha sala yake ya “Siku itakapo wapasukia ardhi mbio
faradhi. mbio! Mkusanyo huo kwetu ni
mwepesi.” (50:33)
Na katika kuliwekea ufafanuzi zaidi hili
Allah (Subhanahu Wataala) anasema Kwa kina, tumeshafanya ufafanuzi juu
katika Surah Muddaththir; ya sehemu ya kwanza ya aya hii juu ya

‫ير‬ َ ‫فَ ٰذ ِﻟ َﻚ يَ ْو َم ِئ ٍذ يَ ْو ٌم‬


ٌ ‫ع ِس‬
mpasuko wa ardhi na namna ambavyo
﴾٩﴿ viumbe watasimamishwa mbele ya

َ ‫َعلَى ْٱﻟ َكا ِف ِر‬


‫ين َغي ُْر‬
Allah. Sehemu hii sasa tunataka
kufafanuwa namna ambavyo Allah

﴾١٠﴿‫ير‬ ٍ ‫يَ ِس‬


atawakusanywa viumbe katika makundi
na hali watakayokuwa nayo kila kundi
kwa mujibu wa amali na matendo yao
“Siku hiyo, basi, itakuwa ngumu. Kwa duniani. Na huu ndio mkusanyo wa
makafiri haitakuwa nyepesi. (74:09-10) kwanza mbele ya Allah kama tulivyo
bainisha hapo awali.
Wafasiri wa Qur’an wanaeleza kwamba
ufahamu wa aya hizi ni kwamba Allah Viumbe wote watafufuliwa kutoka
anabainisha uzito wa siku hiyo kwa kwenye makaburi yao wakiwa na sifa
makafiri na kwamba kwao hautakuwa tatu kama alivyofafanuwa Ibn Kathir
mwepesi, na kueleza kwamba mbali na kwamba wote watafufuliwa wakiwa
ugumu wake ila kutakuwa na wepesi peku (hawana viatu), hawana nguo
kwa wasiokuwa makafiri. Hivyo hii iwe (kama walivyo zaliwa) na
ni kama ibrah kwetu ili tujiangalie ni hawajatahiriwa. Hapo sasa kila mmoja
nafasi gani tunataka kuwepo, aidha atakusanywa na wale anaofanana nao,
katika wale ambao kwao itakuwa ngumu kama washirikina watakuwa na kundi
ila Allah ataifanya iwe sahali ama katika lao, waliokula riba na kundi lao, wazinifu
upande wa wale ambao kwao na kundi lao na waumini pia watakuwa
hakutakuwa na wepesi. na kundi lao. Na hapa ndipo Allah
aliposema kwamba juu ya yote hayo
Allah atujalie tuwe ni miongoni mwa “Mkusanyo huo kwake ni mwepesi”.
waja wa Allah ambao watasahilishiwa
kisimamo.

7|Page
[Allah atukusanye tukiwa katika kundi la na bashaha mbele ya Allah (Subhanahu
Waumin] Wataala).
Ndugu yangu msomaji sasa tuangalie Ibn Abi Hatim amepokea kutoka kwa
baadhi ya makundi pamoja na hali Amr bin Qays Al-Mula’i ambaye nae
ambayo watakuwa nayo wakati amepokea kutoka kwa Ibn Marzuq
wanakusanywa katika mkusanyo wa amesema kwamba siku ambayo
kwanza na Allah (Subhanahu Wataala) waumini watakapo kusanywa kutoka
i. Mkusanyo wa Waumini na kwenye makaburi yao wataonana na
wacha Mungu vijana wazuri sana ambao hajawahi
kuwaona na wakiwa wananukia vizuri
Hakika Qur’an imebainisha bishara sana. Na watauliza, Ni nani wewe?
njema sana kwa waumini ambao Atajibu: “Je haunifahamu mimi?
wamekuwa wakiyafanyia kazi Waumini watasema: “Hapana
maamrisho yote ya Allah na kujiweka
hatuwafahamu ila kwa hakika Allah
mbali zaidi na makatazo yake. Kwa
wamewaumba wazuri mkiwa na
hakika Allah Subhanahu Wataala
manukato mazuri” wale wavulana
ameandaa mapokezi yaliyotukuka kwa
watasema: “Sisi ni matendo yenu
wacha mungu siku ya mkusanyo wa
mema, na hivi ndivyo
kundi la wacha mungu. Kundi hili
mlivyotupendezesha na kutuweka
litakusanywa na Allah kutoka katika
manukato mazuri katika maisha ya
makaburi yao wakiwa na heshima
kubwa mbele ya Allah, kama Qur’an dunia.
inavyoelezea ndani ya Surah Maryam; Kwa hakika hizi ni fadhila zisizo na kifani
kwa waumini, na kila mmoja wetu
‫ش ُر ْٱﻟ ُمتﱠقِينَ إِﻟَى ﱠ‬
﴾٨٥﴿ً ‫ٱﻟر ْﺣ َم ٰـ ِن َو ْفدا‬ ُ ‫يَ ْو َم ن َْح‬ anapaswa kujitathmini nafasi yake kwa
“Siku tutayo wakusanya wachamungu Allah, na bado milango ya Allah ipo wazi
kuwapeleka kwa Arrahman Mwingi wa kwa yeyote ambaye aliteleza kwenye
Rehema kuwa ni wageni wake” (19:85) maisha yake ilhali bado amerudhukiwa
pumzi, tusikate tama na rehema za
Ibn Kathir (Radhi za Allah ziwe juu Allah hakika ni kunjufu kwa waja wake.
yake) anafafanuwa mafhum ya aya hii Na huo ndio utakuwa mkusanyo wa
kwamba Allah anafahamisha namna waja wa Allah ambao zimetulia nafsi zao
bora ambayo atawakusanya waja wake katika kumcha yeye na basi mwisho wao
wema kutoka kwenye makaburi yao ni kupata radhi za Allah katika siku
wakiwa ni wageni waheshimiwa ambao nzito.
wameandaliwa mapokezi ya ugeni
maalumu wa Allah. Anaendelea
kufafanuwa kwamba watafika wakiwa
wamepanda vipando vya heshima vya
Akhera na watapokelewa kwa heshima

8|Page
ii. Mkusanyo wa viumbe ameiharamisha riba. Basi aliye fikiwa na
wanaokula na kupokea mawaidha kutoka kwa Mola wake Mlezi,
riba Kisha akajizuia, basi yake ni yaliyo
kwisha pita, na mambo yake yako kwa
Kwa wafuatiliaji wa makala zetu,
Allah. Na wenye kurudia basi hao ndio
tulizungumza kwa upana uharamu wa
watu wa motoni, humo watadumu”
riba na athari zake katika jamii ya
(02:275)
kiislam na hatma ya viumbe ambao
wanajihusisha na miamala ya Riba. Ibn Kathir amesema juu ya Kauli ya
Kupitia makala ya Riba tulibainisha aina Allah “Wale walao riba hawasimami
za riba, makatazo yake ndani ya Qur’an ila kama anavyo simama aliye
pamoja na athari ambazo miamala ya zugwa na Shet’an kwa kumgusa”
Riba inaleta katika jamii ambapo ni Maana yake ni kwamba, siku ya Kiyama,
pamoja na kuongeza dhiki ya maisha na wale viumbe waliokuwa wakila riba
umasikini. watafufuliwa kutoka katika makaburi
yao wakiwa kama wamepandwa na
Athari za Riba hazikomi kwenye maisha
kichaa ama wamekumbwa na shetani
ya hapa duniani, bali viumbe ambao
mbaya. Ibn Abbas, naye amefafanua
wanatoa na kupokea Riba watajikuta na
kauli hii na kusema kwamba “Siku ya
hali ngumu sana siku ya mkusanyo wa
Kiyama watu hao watafufuliwa kana
kufufuliwa kutoka ndani ya makaburi
kwamba wamepandwa na kichaa na
yao kuelekea katika viwanja vya hisabu
wanatetemeka”
kwani Allah (Subhanahu Wataala)
anasema ndani ya Qur’an tukufu kupitia Ndugu zangu wasomaji, sote tunajuwa
Surah Al-Baqarah kwamba: madhila anayokumbana nayo kiumbe
ambaye yupo kwenye hali ya ukichaa
‫ٱﻟربَا ﻻَ يَقُو ُمونَ ِإﻻﱠ َك َما يَقُو ُم‬ ّ ِ َ‫ٱﻟﱠذِينَ يَأ ْ ُكلُون‬ ama amekumbwa na shetani, basi hiyo
‫س ٰذ ِﻟ َﻚ ِبأَنﱠ ُه ْم‬ ّ ِ ‫ان ِمنَ ْٱﻟ َم‬ ُ ‫ط‬ َ ‫ش ْي‬
‫طهُ ٱﻟ ﱠ‬ ُ ‫ٱﻟﱠذِى يَت َ َخبﱠ‬ ndio itakuwa hali yao mara tu
‫ٱﻟربَا َوأ َ َﺣ ﱠل ٱ ﱠ ُ ْٱﻟبَ ْي َع‬ ّ ِ ‫قَاﻟُ ۤواْ ِإنﱠ َما ْٱﻟبَ ْي ُع ِمثْ ُل‬ watakapofufuliwa kutoka kwenye
‫ظةٌ ِ ّم ْن ﱠر ِبّ ِه‬ َ ‫ٱﻟربَا فَ َمن َجآ َءهُ َم ْو ِع‬ ّ ِ ‫َو َﺣ ﱠر َم‬ makaburi yao. Baadhi ya wanazuoni
wanasema kwamba watu hawa
َ ‫ع اد‬ َ ‫ف َوأ َ ْم ُره ُ ِإﻟَى ٱ ﱠ ِ َو َم ْن‬ َ َ‫سل‬ َ ‫فَٱ ْنت َ َه ٰى فَلَهُ َما‬ watakusanywa wakiwa
‫ار ُه ْم فِي َها‬ ِ ‫اب ٱﻟنﱠ‬ُ ‫ص َح‬ ْ َ ‫فَأ ُ ْوﻟَ ٰـئِ َﻚ أ‬ wamechanganyiwa, hawajitambui
﴾٢٧٥﴿ َ‫خَا ِﻟد ُون‬ wanagaragara kisha wanainuka, na
wataendelea na hali hiyo hadi wafike
“Wale walao riba hawasimami ila kama kwenye viwanja vya hukumu.
anavyo simama aliye zugwa na Shet’an
kwa kumgusa. Hayo ni kwa kuwa Hakika hii tosha ni adhabu juu ya
wamesema: Biashara ni kama riba. adhabu, huku wakisubiri hukumu
Lakini Allah ameihalalisha biashara na kwenye kisimamo kirefu ambacho
wafasiri wa Qur’an wanakieleza kwamba

9|Page
ni kisimamo ambacho jua litasogezwa tutamfufua hali ya kuwa kipofu”
karibu na utosi wa viumbe. Huku (20:124)
wakisubiri mkusanyo wa pili kuelekea
Ibn Kathir (Radhi za Allah ziwe juu
Jahannam na huko adhabu hazita
yake) amemnukuu Ikrima kwamba kauli
simama wala kupunguzwa. Na namna
ya Allah kwamba atafufuliwa akiwa
hiyo ndivyo kundi hili litakavyo
kipofu maana yake ni kwamba hataona
kusanywa na Allah na huo si mzaha.
chochote isipokuwa moto mkali wa
iii. Mkusanyo wa Makafiri na Jahannam atakapo buruzwa huko.
waliopuuza makatazo ya
Katika kutilia nguvu mkusanyo wa
Allah (Subhanahu
idhilali wa kundi hili Allah anasema pia
Wataala)
ndani ya Qur’an;
Kundi hili ni wale ambao walifikiwa na
mawaidha kupitia Mitume na ُ ‫ش ُر ُه ْم يَ ْو َم ْٱﻟ ِقيَا َم ِة َعلَ ٰى ُو ُجو ِه ِه ْم‬
ً ‫ع ْميا‬ ُ ‫َون َْح‬
wakapuuzia kwa makusudi huku ‫ص ّما ً ﱠمأ ْ َوا ُه ْم َج َهنﱠ ُم‬
ُ ‫َوبُ ْكما ً َو‬
wakiamini itikadi zao na kuipa mgongo
“…Na tutawakusanywa Siku ya Kiyama
Qur’an. Watu hawa watakuwa na idhilali
hali wakikokotwa juu ya nyuso zao, nao
ya hali ya juu kuanzia hapa duniani na
ni vipofu na mabubu na viziwi. Na
hata ukimuona ni mwenye mafanikio ya
Makazi yao ni Jahannamu…” (17:97)
namna gani hapa duniani, anakula
anachotaka, anavaa anachotaka na Abuu Katada baada ya kusikia aya hii
kuishi katika maisha mazuri. alimuuliza Mtume wa Allah kwamba ni
vipi watu hao watatembea juu ya nyuso
Basi ujuwe kuna siri usiyo ijua juu ya
zao? Mtume wa Allah akamwambia
idhilali wanayokumbana nayo na moyo
kama ambavyo Allah aliwafanya
wake hautakuwa na amani wala utulivu
watembee duniani kwa miguu yao basi
kutokana na kukosa misingi sahihi ya
ni hivyo hivyo atawafanya watembee
kuifata, na kisha siku ya kukusanywa
juu ya nyuso zao.
kwao Allah ataendelea kuwaadhibu kwa
kuacha kwao kuyafata yale Ama kwa hakika mkusanyo huo
waliyoteremshiwa kupitia Mitume na kwa Allah ni mwepesi
vitabu vitukufu. Haya yanathibitishwa na
Kutokana na adhabu hizo na mateso
Qur’an ndani ya Surah Ta-Ha kwani
hayo hawatoacha viumbe hawa
Allah anasema;
kulalamika kwa Allah (Subhanahu
ً‫ض َعن ِذ ْك ِرى فَإ ِ ﱠن ﻟَه ُ َم ِعيشَة‬ َ ‫َو َم ْن أَع َْر‬ wataala) na kusema;
﴾١٢٤﴿‫ش ُرهُ َي ْو َم ٱ ْﻟ ِقيا َم ِة أ َ ْع َم ٰى‬ُ ‫ضنكا ً َون َْح‬
َ “Ewe Mola wangu Mlezi! Mbona
umenifufua kipofu, nam nilikuwa
“Na atakaye jiepusha na mawaidha nikiona?” (20:125)
yangu, basi kwa yakini atapata maisha
yenye dhiki, na siku ya kiyama
10 | P a g e
Allah (Azza wa Jalla) atawajibu kama ardhi wala kufikia urefu wa milima. Haya
ilivyokuja katika Qur’an kwamba; yote ubaya wake ni wenye kuchukiza
kwa Mola wako Mlezi.” (17:37-38)
‫قَا َل َك ٰذ ِﻟ َﻚ أَتَتْ َﻚ آ َياتُنَا فَنَسِيت َ َها َو َك ٰذ ِﻟ َﻚ ْٱﻟ َي ْو َم‬
Allah anasema pia katika Surah Al-
﴾١٢٦﴿‫س ٰى‬ َ ‫ت ُ ْن‬ Luqman;
“(Mwenyezi Mungu) atasema: Ndivyo
vivyo hivyo. Zilikufikia ishara zetu, nawe
‫اس َوﻻَ ت َ ْم ِش ِفى‬ َ ُ ‫َوﻻَ ت‬
ِ ‫ص ِ ّع ْر َخدﱠ َك ِﻟلنﱠ‬
ukazisahau; na kadhalika leo ‫ض َم َرﺣا ً ِإ ﱠن ٱ ﱠ َ ﻻَ ي ُِحبﱡ ُك ﱠل ُم ْختَا ٍل‬ ِ ‫ٱﻷ َ ْر‬
unasahauliwa” (20:126) ﴾١٨﴿‫ور‬ ٍ ‫فَ ُخ‬
Ibn Kathir (Radhi za Allah ziwe juu “Wala usiwatame (watu) kwa upande
yake) amesherehesha maana ya aya hii mmoja wa uso, wala usiende katika
na kusema kwamba; hawa ni wale walio ardhi kwa maringo, hakika Allah
zipa mgongo ishara za Allah na hampendi kila ajivunae ajifaharishe”
wakazifanya kama vile wamezisahau hali (31:18)
ya kuwa walisha elimishwa na
kufunuliwa maana zake. Walizidharau Tumeanza na kueleza maneno ya Allah
na kuziacha hivyo “kana kwamba Subhanahu wa Taala juu ya kibri, na
wamesahauliwa juu ya rehema za Allah. hakika makatazo ya kibri ndani ya
Qur’an yamekuwa yakibainishwa
iv. Mkusanyo wa viumbe waziwazi ili muumini asizame kwenye
waliokuwa na Kiburi, makosa haya. Kibri, majivuno, na
majivuno na dharau majigambo ni katika tabia mbaya
Duniani iliyokemewa vikali ndani ya Qur’an.
Ndugu yangu msomaji, kabla ya kujikita Kwamaana mtu mwenye kibri hujiona
kwenye namna ambavyo Allah kuwa ni bora, wa juu na wa maana zaidi
Subhanahu wa Taala atawakusanya, kuliko mwengine, kibri huweza
kwanza napenda tupite kwenye baadhi kusababishwa na neema za Allah kama
ya aya juu ya tabia ya Kiburi ambazo mali, watoto, elimu, madaraka,
zitatupa msingi wa hiki ambacho umaarufu na mengine, kibri humpelekea
tunaenda kukitolea ufafanuzi. mtu kudharau mwengine na hadi kufika
Allah amesema; hatua mbaya zaidi ya kudharau hata
makatazo na maamrisho ya Allah
َ‫ض َم َرﺣا ً ِإنﱠ َﻚ ﻟَن ت َ ْخ ِرق‬ ِ ‫َوﻻَ ت َ ْم ِش فِى ٱﻷ َ ْر‬ Subhanahu wa Taala ambaye ndiye
﴾٣٧﴿ً‫طوﻻ‬ ُ ‫ض َوﻟَن تَ ْبلُ َغ ْٱﻟ ِجبَا َل‬
َ ‫ٱﻷ َ ْر‬ aliye mruzuku neema hizo.

Kibri na majivuno huzaa maovu ya


َ َ‫ُك ﱡل ٰذ ِﻟ َﻚ َكان‬
﴾٣٨﴿ً ‫س ِيّئُهُ ِع ْندَ َر ِبّ َﻚ َم ْك ُروها‬ dharau, ukatili, uonevu, udhalimu na
“Wala usitembee katika ardhi kwa kutoshaurika hata kupitia misingi ya
maringo. Hakika wewe huwezi kuipasua dini. Na hii ndio sababu kubwa Allah

11 | P a g e
Subhanahu wa Taala alikataza kiumbe moto wa Jahannam juu yao watakuwa
kujivisha tabia hii na hapa tunaona wamefunikwa na moto na watakuwa
kupitia Hadith Al-Quds; Abuu Hurairah wananyweshwa usaha wa watu wa
(Radhi za Allah ziwe juu yake) motoni.”
amesimulia kuwa Mtume wa Allah Alaihi
Namuomba Allah atukinge sisi na
Salatu Wa Salam amesema: Allah
nyinyi na adhabu na aina hii.
amesema: “Utukufu ni nguo yangu na
kibri ni kilemba changu. Yeyote Kwa mujibu wa Hadith hii watu wenye
atayeshindania kimoja wapo katika hivi kiburi Allah Subhanahu wa Taala
ataangamia. (Muslim). atawakusanya wakiwa dhalili na wakiwa
mithili ya punje ndogo wakiwa katika
Katika Riwaya nyengine, Abu Hurairah
umbile la binadamu. Tujenge picha
(Radhi za Allah ziwe juu yake) amesema
namna ambavyo tumefafanuwa viumbe
kuwa Mtume wa Allah amesema: “Yule
watavyofufuliwa kutoka katika makaburi
ambaye moyoni mwake mna chembe
wakielekea kwenye kisimamo huku
(punje) ya kibri hataingia peponi”
wakipiga mbio kisha tengeneza taswira
Sahaba mmoja akauliza: “Je, kama mtu
ya hali itavyokuwa kwa viumbe ambao
anapenda nguo nzuri na viatu?” Mtume
watakuwa na hali hiyo ya udogo wa
wa Allah akasema: “Allah Subhanahu wa
mithili ya punje ndogo, ni idhilali ya kiasi
Taala ni mzuri na anapenda vizuri, kibri
gani!
ni kukataa ukweli na kupuuza watu.”
(Muslim) Baadhi ya Riwaya zinaeleza kwamba
kutokana wa udogo wao basi watakuwa
Hivyo kutokana na makatazo haya
wanaburuzwa na kusukumwa hadi
sambamba na ubaya ulioelezwa juu ya
kufikia katika gereza lililopo ndani ya
kibri Allah Subhanahu wa Taala
moto wa Jahannam ambalo Mtume wa
atawakusanya viumbe wenye kujivesha
Allah amelitaja kwa jina la “Bulas.” Na
tabia hii wakiwa katika hali mbaya sana
hali hii ni kutokana namna
ya udhalili na kudharaulika, ambayo ni
walivyojikweza na kuwadharau wengine,
mithili ya namna mtu huyo alivyo
wakiwadhulumu na neema walizopewa
jipandisha na kujikweza hapa duniani.
na Allah, basi nao watakusanywa
Namna ambavyo Allah awatawakusanya wakiwa wameshushwa chini kuliko walio
ameelezea Mtume wa Allah; Amepokea chini.
Abdullah Ibn Amr (Radhi za Allah ziwe
v. Mkusanyo wa Washirikina
juu yake) amesema: Mtume wa Allah
Alaihi salatu wa salam amesema: Kwa wafuatiliaji wa Makala zetu,
“Watafufuliwa wale wenye kiburi siku ya tulieleza kwa undani juu ya madhara na
kiyama wakiwa mfano wa punje (ndogo) makatazo ya Shirki ndani ya Qur’an na
wakiwa wamefunikwa na udhalili na tukafafanua namna ambayo dhambi ya
watapelekwa katika gereza ndani ya shirki inavyoweza kumfanya mtendaji

12 | P a g e
akakumbana na ghadhabu za Allah siku Ndugu yangu msomaji, katika maisha ya
ya kukutana naye. Kwa hakika shirki ni dunia tunaelewa uzito wa mtu ambaye
miongoni mwa dhambi kubwa na iwe ni alikuwa na mali nyingi, kulala na
shirki ndogo ama kubwa zote malipo kuamka amepata khasara ya mali zote si
yake ni adhabu yenye kudhalilisha. jambo jepesi basi hiyo ndiyo hali
ambayo watakuwa nayo washirikina siku
Kupitia makala yetu ya shirki tulieleza na
ambayo watakusaywa kutoka kwenye
kubainisha njia mbali mbali ambazo
makaburi yao, na kwa hali hii ni dhahiri
wanazitumia washirikina kuwahadaa
kwamba hawatakuwa na tama ya
viumbe ili waingie kwenye shirki. Kupitia
kupata rehema wala huruma za Allah.
makala hii tutabainisha namna ambavyo
Allah anafafanuwa hali hiyo kupitia aya
Allah atawakusanya washirikina kutoka
nyengine ndani surah Az-Zumar;
kwenye makaburi yao kuelekea kwenye
viwanja vya hisabu. Ndani ya Qur’an َ ْ‫َو َي ْو َم ْٱﻟ ِقيَا َم ِة ت َ َرى ٱﻟﱠذِينَ َكذَبُوا‬
ِ ‫علَى ٱ ﱠ‬
Allah Subhanahu wa Taala amemueleza
﴾﴿ ٌ ‫ُو ُجو ُه ُهم ﱡمس َْودﱠة‬
Mtume wake na kumpa tahadhari juu ya
shirki sambamba na matokeo yake siku “Na siku ya kiyama utawaona walio
ya kukutana naye, Allah amesema ndani msingizia uwongo Mwenyezi Mungu
ya Surah Az-Zumar; nyuso zao zimesawijika. (39:60)

‫ى إِﻟَي َْﻚ َوإِﻟَى ٱﻟﱠذِينَ ِمن قَ ْب ِل َﻚ َﻟ ِئ ْن‬ ُ


َ ‫َوﻟَقَ ْد أ ْو ِﺣ‬ Ibn Kathir katika tafsir yake ameeleza
َ‫ط ﱠن َع َملُ َﻚ َوﻟَتَ ُكون ﱠَن ِمن‬ َ ‫أَ ْش َر ْك‬
َ َ‫ت َﻟيَ ْحب‬ mafhum ya aya hii kwamba siku ya
kiyama kuna viumbe sura zao zitang’aa
﴾٦٥﴿ َ‫ْٱﻟخَا ِس ِرين‬
kwa nuru na hawa ni waumini, bali kuna
“Na kwa yakini yamefuniliwa kwako na wengine sura zao zitasawijika kwa weusi
kwa walio kuwa kabla yako: Bila shaka wa kiza na hawa ni wale ambao
ukimshirikisha Mwenyezi Mungu a’mali walimshirikisha Mwenyezi Mungu na
zako zitaanguka, na lazima utakuwa kumfanyia washirika.
miongoni mwa wenye kukhasirika” vi. Mkusanyo wa
(39:65) Wafanyabiashara
Kuanguka maana yake ni kufutika kwa Allah Subhanahu wa Taala amehalalisha
matendo yote mema ambayo kiumbe juu ya viumbe wake kutafuta riziki na
aliyafanya wakati wa uhai wake na neema zake kwa njia mbali mbali za
atafufuliwa akiwa mtupu katika mizani halali ikiwamo ndani ya hizo biashara
ya kheri zake. Hivyo kwa ujumla ni (halali). Kwa hakika biashara ni jambo
kwamba wale waliomshirikisha Mola ambalo limeruhusiwa kuwa ni sababu ya
Mlezi watafufuliwa wakiwa watupu kipato kwa viumbe pale tu itakapofata
kwenye upande wa matendo yao masharti na kuchunga mipaka ya Allah,
ambayo yangeweza kuwaokoa na kwani Allah Subhanahu wa Taala
adhabu ya moto na hii ndio kukhasirika. ameweka mipaka yake juu ya kila tendo
13 | P a g e
kwa viumbe wake ili kuchunga na ambazo ni matokeo ya biashara yake
kujikinga na haramu ambazo ambayo akiifanya hapa duniani.
zimekatazwa.
 Mfanyabiashara usitegemee
Wafanyabiashara kama viumbe wengine rehema za Allah kama hautaacha
ndani ya dunia wanaweza kuwa wema hadaa na viapo vya uongo kwa
ama waovu wa matendo yao, ila kwa wateja wako. (mfano: Unakuta
Allah kuliweka kundi hili la mtu anaapa kwamba bidhaa hii ni
wafanyabiashara katika mikusanyo yake bora ili tu ununue kumbe haina
ni kwa lengo la kuhakikisha chochote kinacholingana na
wafanyabiashara wanafata maamrisho ubora aliwokula kiapo kuuhusu)
na wanaacha yale yote yaliyo katazwa  Mfanyabiashara usitegemee
ndani ya Qur’an. Allah Subhanahu wa rehema na msamaha wa Allah
Taala, ameelezea masharti ya msingi ya kama haukuacha kuwa na mkono
biashara ili kumnusuru mfanyabiashara wa birika kwa wahitaji – masikini,
na ghazabu za zake ikiwamo; mayatima, wafungwa na
wasiojiweza miongoni mwa
a. Kujiepusha na viapo na ahadi
wazee.
za uongo.
 Mfanyabiashara usitegemee
b. Kutenda haki kwenye mizani
reheme za Allah kama hautaacha
ya vipimo.
kuthamini biashara yako juu ya
c. Kujikumbusha malengo yake
ibada kwa wakati wake –
ya kuwepo duniani na kupewa
Unapuuza muito wa sala ya
neema hiyo.
faradhi ili usiache shilingi ambazo
d. Kuacha tabia ya ubaghili juu
wateja wamekuzunguka.
ya ahadi yake kwa Allah
 Mfanyabiasha usitegemee
(Subhanahu wa Taala)
rehema za Allah kama hautaacha
e. Kujikumbusha kwamba
kupunja na kutokutenda haki
maisha ya Akhera ni bora
kwenye mizani za vipimo.
zaidi kuliko mali anazochuma
na kusahau kushukuru neema [Zaidi ya hapa Allah (Subahanahu
za Allah. wa Taala) ndio mjuzi zaidi, kwani
yeye ni mwingi wa kusamehe na
Ukisoma ndani ya Qur’an unaweza
mwenye hekima]
kuona nukta zote hizi ambazo
tumezibainisha hapo juu zimetolewa Hivyo basi kama biashara yako itakuwa
ushahidi na kuwekwa kama masharti imezungukwa na haya ambayo
kwa kundi hili. Na hichi ndicho kipimo tumeyabainisha hapa juu elewa
cha kumjuwa ni yupi kati yao watakusanywa wakiwa ni waovu
atakusanywa na Allah akiwa wakubwa na watafufuliwa kutoka ndani
amesalimika na azabu za siku hizo ya makaburi yao wakiwa uovu wao

14 | P a g e
unaonekana kupitia sura zao na Allah vii. Mkusanyo wa Wanyama
atawafanyia wepesi zaidi kuufikia moto
Wanyama ni miongoni mwa viumbe wa
wa Jahannam ili wawahi kuunguzwa
Allah (Subhanahu wa Taala) na kama
humo, kwa kauli ya Allah ndani ya Surah
ambavyo Allah amebainisha ndani ya
Al-Layl:
Qur’an kwamba kila kiumbe kitarudi
﴾٨﴿‫َوأ َ ﱠما َمن َب ِخ َل َوٱ ْستَ ْغن َٰى‬ kwake hivyo siku ya kiyama wanyama
watakusanywa kwa ajili ya kudhihirisha
﴾٩﴿‫ب بِ ْٱﻟ ُح ْسن َٰى‬
َ ‫َو َكذﱠ‬ kwamba siku hiyo ni siku ya haki na
hakuna kiumbe yeyote ambaye
﴾١٠﴿‫س ُِرهُ ِﻟ ْلعُس َْر ٰى‬
ّ َ‫فَ َسنُي‬ atadhulumiwa.

”Na ama mwenye kufanya ubakhili, na Riwaya zinasema kwamba siku hiyo
asiwe na haja na wenzake, na wanyama nao watakusanywa kwenye
akakanusha lilio jema, tutamsahilishia viwanja vya hisabu kisha ataletwa
yawe mazito” (92:8-10) mnyama ambaye alipigwa pembe hali ya
kuwa yeye hakuwa na pembe kisha
Ibn Kathir (Radhi za Allah ziwe juu ataletwa yule mnyama aliyempiga na
yake) amefafanuwa kauli ya Ikrima zitahamishwa pembe zake kupewa yule
kuwa amemnukuu Ibn Abbas akisema aliyepigwa na ataamrishwa kumrudishia
kwamba maana ya kauli ya Allah [Na pigo la pembe ambalo alimpiga hapa
asiwe na haja na wenzake] inaamanisha duniani ili kisasi kipite na kila mmoja
mtu huyo alikuwa hayupo tayari awe amelipwa ujira wake.
kushirikiana na wengine kwa hali zote
juu ya mali zake na akajiona hana haja Hii inadhihirisha uadilifu wa Allah
hata na Mola Mlezi. (Subhanahu wa Taala) na kwa hakika
hakuna yeyote miongoni mwa viumbe
Hivyo kutokana na kujiona hivyo basi ambaye atazulumiwa siku hiyo, kwa
naye siku ya kiyama atakusanywa akiwa kauli ya Allah (Subhanahu wa Taala)
hakuna mwenye shida naye wala ndani ya Surat Al-Anbiya’;
kushirikishwa na yeyote ndipo
itarahisishwa njia yake kuelekea kwenye ْ ُ ‫ط ِﻟ َي ْو ِم ْٱﻟ ِق َيا َم ِة فَﻼَ ت‬
‫ظلَ ُم‬ َ ‫ض ُع ْٱﻟ َم َو ِازينَ ْٱﻟ ِق ْس‬
َ َ‫َون‬
mateso ya Jahannam. ‫س َشيْئا ً َو ِإن َكانَ ِمثْقَا َل َﺣبﱠ ٍة ِ ّم ْن خ َْردَ ٍل‬ ٌ ‫نَ ْف‬
Abu Bakr As-Siddiq (Radhi za Allah ziwe ﴾٤٧﴿ َ‫أَتَ ْينَا بِ َها َو َك َف ٰى بِنَا َﺣا ِسبِين‬
juu yake) amenukuliwa katika tafsir ya
“Nasi tutaweka mizani za uadilifu kwa
Ibn Kathir kwamba Mtume wa Allah
Siku ya Kiyama. Basi nafsi
amesema: “Kila Mwanadamu
haitadhulumiwa kitu chochote. Hata
atasahilishiwa kufanya yale matendo
ikiwa ni uzito wa chembe ya khardali
ambayo watakupelekea kwenye sababu
tutaileta. Nasi tunatosha kuwa washika
ya kuumbwa kwake.”
hisabu.” (21:47)

15 | P a g e
Ndugu yangu msomaji kwa hakika hayo kiongozi wa kundi la Waumini. Na hili
ndio baadhi ya makundi ya viumbe linathibitishwa na Hadith ya Mtume
ambao Allah atawakusanya na namna Alaihi Salatu wa Salam ambayo ametaja
ambavyo watakusanywa kutoka katika kwamba yeye ana majina matano katika
makaburi yao kuelekea viwanja vya hayo majina matano moja wapo Al-
hisabu na huu ndio utakuwa kwa Hashri ikiwa na maana ya kuwa wa
mkusanyo wa kwanza kwa upande wa kwanza katika kukusanywa.
akhera. Tumuombe Allah atukusanye Kwa hakika siku hiyo wale walio mcha
pamoja na waumini wenye heshima Mwenyezi Mungu hawatakuwa na khofu
mbele ya Allah (Subhanahu wa Taala). wa majuto kwani watakuta rehema za

ٌ ‫ٰذ ِﻟ َﻚ َﺣ ْش ٌر َعلَ ْينَا يَس‬


Mola wao Mlezi zinawasubiri. Allah
‫ِير‬ anaeleza namna ambavyo waumini
“…Mkusanyo huo kwetu ni mwepesi.” watakavyo kusanywa kuelekea kwenye
(50:33) pepo za Allah ndani ya Surah Az-Zumar:

MKUSANYO KUTOKA KWENYE ‫َو ِسيقَ ٱﻟﱠذِينَ ٱت ﱠ َق ْواْ َربﱠ ُه ْم ِإ َﻟى ٱﻟّ َجنﱠ ِة ُز َمرا ً َﺣت ﱠ ٰى‬
VIWANJA VYA HISABU KUELEKEA َ َ‫ت أَب َْوابُ َها َوق‬
‫ال ﻟَ ُه ْم خَزَ َنت ُ َها‬ ْ ‫إِذَا َجآ ُءوهَا َوفُتِ َح‬
AIDHA KWENYE PEPO AU MOTO
﴾٧٣﴿ َ‫سﻼَ ٌم َعلَ ْيكُـ ْم ِط ْبت ُ ْم فَٱ ْد ُخلُوهَا خَا ِﻟدِين‬ َ
Ama baada ya kila kiumbe kukusanywa
katika mkusanyo wa kwanza, na kila “Na walio mcha Mola wao Mlaezi
kundi kusomewa hisabu yake kwa wataongozwa kuendea Peponi kwa
mujibu wa matendo yake, wakiwa makundi, mpaka watakapo fikilia, nayo
katika hali hizo hizo walizokusanywa milango yake itakuwa imekwisha
katika mkusanyo wa kwanza, Allah funguliwa. Walinzi wake watawaambia:
(Subhanahu wa Taala) atawakusanya Salam Alaikum, Amani iwe juu yenu!
tena mkusanyo wa pili kwa mujibu wa Mmet’ahirika. Basi ingieni humu make
matokea ya mizani za matendo milele.” (39:73)
waliyoyatanguliza. Ibn Kathir (Radhi za Allah ziwe juu
Mkusanyo huu wa pili utakuwa ni yake) amefafanuwa juu ya kauli hii ya
kuwaondoa viumbe kutoka kwenye Allah na kusema kwamba Allah
viwanja vya Mahshar na kila kundi anatueleza kwamba watakusanywa
kuelekea katika makazi yao ya milele. wacha mungu na kuongozwa kuelekea
kwenye pepo kundi moja baada ya
Waumini ambao hapa sasa watakuwa ni lengine, likianza kundi la walio bora
waheshimiwa kama tulivyo bainisha zaidi, kisha kufata walio bora na
awali, watasindikizwa kuzikaribia pepo mengine kufatia, kila kundi litajumuisha
tukufu za Allah huku wakiongozwa na watu wanaofanana kimatendo na
Mtume wa Allah Muhammad Alaihi Mtume wa Allah Alaihi Salat wa Salam
Salatu wa Salam kwani yeye atakuwa ni ndio atakuwa kiongozi wao na makundi
wa kwanza kufufuliwa na ndio atakuwa yote yatakuwa na watu waliolingana

16 | P a g e
katika amali na wale walio ambatana ‫َو ِسيقَ ٱﻟﱠذِينَ َكـفَ ُر ۤواْ إِﻟَ ٰى َج َهنﱠ َم ُز َمرا ً َﺣت ﱠ ٰى ِإذَا‬
nao katika kuzitenda.
‫ت أَب َْوابُ َها َوقَا َل ﻟَ ُه ْم خَزَ َنت ُ َهآ أَﻟَ ْم‬ْ ‫َجآ ُءوهَا فُ ِت َح‬
Ibn kathir pia amemnukuu Abu ‫ت َر ِبّكُ ْم‬ِ ‫يَأ ْ ِت ُك ْم ُرسُ ٌل ِ ّمن ُك ْم َيتْلُونَ َعلَ ْي ُك ْم آيَا‬
Khurayrah (Radhi za Allah ziwe juu
‫َويُنذ ُِرو َنكُ ْم ِﻟقَـآ َء يَ ْو ِم ُك ْم َه ٰـذَا قَاﻟُواْ بَلَ ٰى َوﻟَ ٰـ ِك ْن‬
yake) kwamba amesema: Amesema
Mtume wa Allah (Alaihi Salat wa Salam) ﴾٧١﴿ َ‫علَى ْٱﻟ َكافِ ِرين‬ َ ‫ب‬ ِ ‫ت َك ِل َمةُ ْٱﻟعَذَا‬ ْ ‫َﺣقﱠ‬
“Kundi la Umma wangu, makundi sabini
“Na walio kufuru wataongozwa kuendea
elfu yataingia Peponi huku sura zao
Jahannam kwa makundi, Mpaka
ziking’aa kama mwezi mpevu kwenye
watakapo ifikia itafunguliwa milango
usiku wenye kiza” (Imesahihishwa na
yake, na walinzi wake watawaambia:
Maimamu Wawili)
Kwani hawakukujilieni Mitume miongoni
Baada ya hayo yote kufanyika na mwenu wakikusomeeni Aya za Mola
waumini kupokelewa ndani ya Pepo wenu Mlezi na kukuonyeni mkutano wa
zenye rehema. Allah (Subhanahu wa siku yenu hii? Watasema: Kwani! Lakini
Taala) akasema tena baada ya hapo: limekwisha thibiti neno la adhabu juu ya
makafiri.” (39:71)
َ ‫َوقَـاﻟُواْ ْٱﻟ َح ْـمدُ ﱠ ِ ٱﻟﱠذِى‬
‫صدَ َقنَا َو ْعدَهُ َوأَ ْو َرثَنَا‬
ُ ‫ض نَتَبَ ﱠوأ ُ ِمنَ ْٱﻟ َجنﱠ ِة َﺣي‬
‫ْث نَشَآ ُء فَ ِن ْع َم أ َ ْج ُر‬ َ ‫ٱﻷ َ ْر‬
Ibn Kathir (Radhi za Allah ziwe juu
yake) amefafanuwa juu ya kauli hii ya
﴾٧٤﴿ َ‫املِين‬ ِ ‫ْٱﻟ َع‬ Allah na kusema kwamba siku hiyo
makafiri watasukumwa kwenye
“Nao watasema: Alhamdulillah, sifa
Jahannam kwa nguvu zenye vitisho
njema zote ni za Mwenyezi Mungu aliye
vikali. Kama ambavyo Allah amesema
tutimizia ahadi yake, na akaturithisha
kwenye Surah At-Tur;
ardhi, tunakaa katika Bustani popote
tupendapo. Basi ni malipo mazuri ﴾١٣﴿‫َار َج َهنﱠ َم دَعا‬
ِ ‫يَ ْو َم يُدَعﱡونَ ِإﻟَ ٰى ن‬
yaliyoje ya watendao!” (39:74)
“Siku watapo sukumwa kwenye Moto
[Tunamuomba Allah Subhanahu wa
kwa msukumo wa nguvu” (52:13)
Taala atukusanye pamoja wa waja
wema ili tuwe miongoni mwa Wanazuoni wa Tafsir amefafanuwa pia
watao rithishwa ardhi na kufaidi kwamba walinzi wa Moto
neema za Pepo yake] waliozungumzwa kwenye Aya hii ni
wengi na wenye nguvu na
Kwa upande wa pili [Allah atuepushe na
watawasemesha kwa kauli za ukali na
upande huu] Makafiri, washirikina, Wala
zenye kutisha na mara tu watakapo
riba, Wenye kiburi nao pia
waona wanaukaribiria Moto wataifungua
watakusanywa katika mkusanyo wa pili
milango yake haraka haraka ili
katika makundi yao na kuburuzwa
kuiwahisha adhabu yao.
kuelekea Jahannam kwa kauli ya Allah
Azza wa Jallah; Na Allah (Subhanahu wa Taala)
anaeleza namna ambavyo

17 | P a g e
atawakusanywa na kuwachunga chunga “…Mkusanyo huo kwetu ni mwepesi.”
watu hawa kuelekea kwenye Moto, na (50:33)
kwamba katika kila kundi miongoni mwa
Ndugu yangu msomaji wa Makala hii,
makundi ambayo tumeyafafanuwa awali
bado tuna nafasi ya kurudi kwa Allah
litakuwa na kiongozi ambaye ataongoza
juu kila ambapo tuliteleza ili kusudi
kundi lake kama ambavyo waumini
tusije kutumbukia katika janga ambalo
walivyoongozwa na Mtume wa Allah, na
atakuwa ni yule ambaye alikuwa ni halitakuwa na msaidizi wala muombezi.
kinara katika dhambi ya aina ya kundi Tupo katika mwezi mtukufu wa
hilo, hili limethibiti kwa kauli ya Allah Ramadhan ambao ndani yake Allah
ndani Surah Maryam aliposema: anatangaza msamaha wa wazi kwa waja
wake, kwanini tusitumie fursa hii ili
َ َ ‫ع ﱠن ِمن ُك ِّل ِشي َع ٍة أَيﱡ ُه ْم أ‬
‫شدﱡ َعلَى‬ َ ‫َنز‬ ِ ‫ث ُ ﱠم ﻟَن‬ kutujiepusha na haya. Kisha tumlilie
﴾٦٩﴿ً ‫ٱﻟر ْﺣ َم ٰـ ِن ِع ِتيّا‬
‫ﱠ‬ Allah atuhifadhi na kutudumisha kwenye
Taqwa na kwa hakika ndio pekee
ِ ‫ث ُ ﱠم َﻟن َْح ُن أ َ ْعلَ ُم بِٱﻟﱠذِينَ هُ ْم أَ ْوﻟَ ٰى بِ َها‬
﴾٧٠﴿ً ‫ص ِليّا‬ kinachoweza kutuokoa na mkusanyo wa
aina hii.
“Kisha kwa yakini tutawatowa katika kila
kundi wale miongoni mwao walio zidi Kwanini tuendelee kuwa na kibri kwa
kumuasi Arrahman, Mwingi wa Rehema. neema ambazo Allah (Azza wa Jallah)
Tena hakika sisi tunawajuwa vyema ameturuzuku, kwanini tuendelee
zaidi wanao stahiki kuunguzwa humo.” kuwadhulumu wengine kwa nafasi
(19:69-70) tulizonazo ambazo ni dhamana na ni
mtihani kwetu, kwanini tuendelee
Kwa hakika huu utakuwa ni mkusanyo kujifunganisha na miamala ya riba ilhali
mzito kwa viumbe vya Allah ambao inatupa khasara hapa duniani na itatupa
walipuuza makatazo yake na wakaipa msiba wa kudumu siku ya kukusanywa
mgongo Qur’an kwa ulevi wa dunia na mbele ya Allah, kwanini tuendelee
mapambo yake. Baada ya hapo katika kukiuka mipaka ya Allah kwenye
kukamilisha mkusanyo huu Allah biashara zetu kwa hadaa na dhulma.
anasema;
Hakika kila mmoja wetu ni mchunga
َ ‫ِقي َل ٱ ْد ُخلُ ۤواْ أَب َْو‬
َ ْ‫اب َج َهنﱠ َم خَا ِﻟدِينَ فِي َها َف ِبئ‬
‫س‬ kwa mwenzake, tumewakusanyia
﴾٧٢﴿ َ‫َمثْ َوى ْٱﻟ ُمتَ َكـبِّ ِرين‬ maudhui haya ili iwe ni ibrah kwenu
ndugu zetu na iwe ni sababu ya kila
“Itasemwa: Ingieni milango ya mmoja wetu kujitathimini nafasi yake
Jahannam mdumu humo. Basi nayo ni katika makundi haya. Hakika watakao
ubaya ulioje wa makazi ya wanao faulu ni wale ambao watamjuwa Allah
takabar!” (39:72) kwa kweli na kujuwa mipaka yake na

ٌ ‫ٰذ ِﻟ َﻚ َﺣ ْش ٌر َعلَ ْينَا َيس‬


kuichunga. Na wale walio khasirika ni
‫ِير‬

18 | P a g e
wale watakao puuza baada ya
kuwabainikia haki isiyo na shaka.

HITIMISHO

َ‫علَ ٰى أَنفُ ِس ِه ْم ﻻ‬
َ ْ‫ِى ٱﻟﱠذِينَ أَس َْرفُوا‬ َ ‫قُ ْل ٰي ِع َباد‬
َ ُ‫طواْ ِمن ﱠر ْﺣ َم ِة ٱ ﱠ ِ ِإ ﱠن ٱ ﱠ َ َي ْغ ِف ُر ٱﻟذﱡن‬
‫وب‬ ُ ‫ت َ ْق َن‬
﴾٥٣﴿‫ٱﻟر ِﺣي ُم‬‫ور ﱠ‬ ُ ُ‫َج ِميعا ً ِإنﱠهُ ُه َو ْٱﻟغَف‬
‫َوأَنِـيب ُۤواْ ِإﻟَ ٰى َر ِبّ ُك ْم َوأ َ ْس ِل ُمواْ ﻟَهُ ِمن َق ْب ِل أَن‬
﴾٥٤﴿ َ‫ص ُرون‬ َ ‫اب ث ُ ﱠم ﻻَ تُن‬ ُ َ‫يَأ ْ ِت َي ُك ُم ْٱﻟعَذ‬
“Sema: Enyi waja wangu walio
jidhulumu nafsi zao! Msikate tama na
rehma ya Mwenyezi Mungu. Hakika
Mwenyezi Mungu husamehe dhambi
zote. Hakika yeye ni Mwenye kusamehe,
Mwenye Kurehemu. Na rejeeni kwa
Mola wenu Mlezi, na silimuni kwake,
kabla ya kuwajieni adhabu. Kisha hapo
hamtanusurika.” (39:53-54)

Wabillah Tawfiq.

19 | P a g e

You might also like