You are on page 1of 1

UKOMO WA MUDA KATIKA KUANZISHA SHAURI LA MIRATHI KATIKA

MAHAKAMA ZA MWANZO TANZANIA

Sheria ya Mahakimu sura 11 Marejeo ya mwaka 2018, kifungu Na. 18, 19, 20,
21 vya sheria hii vinaelezea wazi namna gani Shauri la MIRATHI liko chini ya
mamlaka ya Mahakama hii kulingana na Thamani ya Mali husika ya urithi
(within the court's pecuniary jurisdiction).

Na pia Mashauri haya yanafunguliwa chini ya vifungu 2 (a) au 2 (b) vya


nyongeza ya 5 ya Sheria ya Mahakimu, muda wa ukomo unaangukia katika
sehemu ya 3 ya nyongeza ya Sheria ya Ukomo ambayo inatamka kuwa maombi
yeyote yanayofanywa chini ya Sheria ya Mahakimu ukomo wake ni siku 60
tangu tarehe ya chanzo cha maombi, endapo muda wa ukomo haujatajwa.
Hivyo kwa kuzingatia Sheria ya Ukomo, maombi ya uteuzi wa usimamizi wa
mirathi au kutekeleza wosia yanapaswa kufikishwa Mahakamani ndani ya siku
60 baada ya kifo kutokea.

Hata hivyo Ukomo wa muda katika Shauri la MIRATHI ni muhimu kuzingatiwa


sababu uchelewaji unaweza kupelekea Mali za marehemu kutumika vibaya, na
pia kuna haki ambazo zinaweza kupotea. Mfano Mashauri ya madai
yanafungwa na sheria ya ukomo, hivyo kama marehemu alikuwa na madai
yake kwa mtu mwingine na Msimamizi wa mirathi yake akichelewa kuteuliwa
sheria ya ukomo (miaka 6 tangu dai la marehemu kuanza) itamzuia kudai haki
hiyo ya marehemu. Hali pia ipo hivyo katika madai ya umiliki wa ardhi.
Kama Msimamizi hakuteuliwa kwa wakati na ukapita muda wa miaka
12 basi Msimamizi hataweza kudai haki ya ardhi ya marehemu kwa
kuwa atafungwa na sheria ya ukomo wa muda.

hivyo basi baada ya kifo cha Marehemu Inabidi taratibu za msingi zifuatwe ili
kupelekea maombi ya uteuzi wa Msimamizi wa MIRATHI ya marehemu
ufanyikie Mahakamani ili kulinda Mali na haki za marehemu sababu muda
katika Mashauri ya madai Sheria ya Ukomo wa Muda (Law of Limitations)
inahusika sana hapa.

Hata hivyo Mahakama Kuu (Mhe. Mruma, J.) katika kesi ya Majuto Juma
Nshahuzi vs Issa Juma Nshahuzi PC Civil Appeal No. 9 of 2014 HC at
Tabora 28 ilitoa mtazamo mpana zaidi juu ya ukomo wa kufungua Mashauri ya
mirathi ambapo Mahakama ilitamka kwa kimombo:-

“… there is no specific time limit for petition for letters of


administration and in my view, it would not be in the
interest of justice to have such a provision …”

Pamoja na hayo Mahakama ya Rufani katika Shauri la Mwaka Musa vs Simon


Obedi Simchimba Civil Appeal No. 45 of 1994 CAT at Dar es Salaam
(unreported) katika ukurasa wa 8 wa Hukumu, imesisitiza kuwa endapo
Shauri la mirathi litapelekwa Mahakamani miaka 3 baada ya kifo cha
marehemu, maombi yanapashwa kuambatana na maelezo ya sababu za
uchelewaji huo. Hivyo basi ni muhimu kuzingatiwa kwa taratibu maalumu ili
kuepuka usumbufu, japo hakuna gharama kubwa katika kufungua Mashauri
ya namna hii kwa mujibu wa Court Fees Rules.

You might also like