Kamati za Bodi 10. Bodi inaweza, kwa madhumuni ya kutekeleza
majukumu yake kwa ufanisi, kuunda na kuteua kutoka miongoni mwa wajumbe wake, kamati zozote kadri itakavyoona inafaa.
Uteuzi wa 11.-(1) Kutakuwa na Mkurugenzi Mkuu wa Tume
Mkurugenzi Mkuu ambaye atateuliwa na Rais. (2) Mtu atateuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu ikiwa ana sifa zifuatazo: (a) amehitimu katika chuo kikuu kinachotambulika na ana angalau shahada ya kwanza katika nyanja za TEHAMA, uhandisi, sheria, uchumi, fedha au utawala; (b) ana uzoefu wa utumishi usiopungua miaka kumi katika angalau moja ya nyanja zilizotajwa katika aya (a); na (c) ana ujuzi au utaalamu katika nyanja ya ulinzi wa taarifa.
Muda wa 12. Mkurugenzi Mkuu atashika madaraka kwa kipindi
kuhudumu wa Mkurugenzi cha miaka mitano na baada ya kipindi hicho kumalizika, Mkuu anaweza kuteuliwa tena kwa kipindi kingine kimoja.
Watumishi wa 13.-(1) Tume, kwa kuzingatia sheria za utumishi wa
Tume umma, itaajiri watumishi kwa idadi itakayohitajika kwa madhumuni ya utekelezaji bora wa majukumu ya Tume. (2) Tume inaweza kuteua washauri na wataalam katika taaluma mbalimbali kwa kuzingatia vigezo na masharti yatakayowekwa na Tume.
SEHEMU YA TATU USAJILI WA WAKUSANYAJI NA WACHAKATAJI WA TAARIFA BINAFSI
Usajili wa 14.-(1) Mtu hatakusanya au kuchakata taarifa binafsi
wakusanyaji na wachakataji bila kusajiliwa kama mkusanyaji au mchakataji chini ya Sheria hii. (2) Mtu anayekusudia kukusanya au kuchakata taarifa atawasilisha maombi ya usajili kwa Tume. (3) Tume inaweza, katika muda utakaoainishwa katika kanuni, kukubali au kukataa maombi yaliyowasilishwa kwa mujibu wa kifungu kidogo cha (2).