You are on page 1of 5

SEHEMU YA PILI

IJUE LEUKEMIA:

JE LEUKEMIA NI NINI?

Leukemia ni Saratani inayoshambulia chembechembe za damu, ni saratani inayoathili mfumo


( kiwanda) wa kutengeneza seli mbalimbali za damu unaofahamika kama ULOTO
unaopatikana ndani ya mifupa pamoja mfumo wa tezi za mwili, ambapo baada ya mabadiliko
hasi husababisha uzalishaji wa haraka uliopindukia wa seli za damu usio sahihi. Kwa kawaida
huathili seli nyeupe za damu zinazohusika na kinga ya mwili, ingawa pia huathili seli nyekundu
na zinazohusika na mgando wa damu.

Watu wanaokuwa kwenye mazingira yenye kiwango cha juu cha mionzi na kemikali yenye
sumu ya ki- Hydrokaboni ya Benzini wanao uwezekano mkubwa wa kupata aina tofauti za
Leukemia kama ilivyo kwa wavutaji sigara na aina za tumbaku, watu ambao wamewahi kupata
tiba ya kemikali katika kutibu maradhi mbalimbali na watu waliorithi magonjwa mbalimbali
ikiwemo yanayo athili mfumo wa damu.

❇️ AINA ZA LEUKEMIA

🔳Kuna aina mbalimbali za Leukemia. Madaktari huzitofautisha kilingana na sehemu


zinakoanzia na kuhusisha kama:-

▪️zinazoanzia na kuhusisha ULOTO (bone marrow) -huitwa 🖍️MYELOID au LYMPHOCYTIC


na

▪️Tokana na mfumo wa tezi- huitwa Lymphoma

▪️Au jinsi gani kwa haraka saratani inavyo inavyokua na kuleta athali ( acute leukemias)

▪️Au jinsi gani saratani hukua taratibu na athali zake kuonekana baada ya muda mrefu
kupita ( Chronic Leukemias). Hata hivyo dalili za saratani hizi hutofautiana kulingana na aina
ya saratani husika.

✏️ marekebisho kidogo nimeweka in bold hapo juu kwenye hiyo para

MATIBABU YA LEUKEMIA NA JINSI YA KUZUIA MADHARA YATOKANAYO NA


DAWA.

Matibabu anayopata mgonjwa wa Leukemia hutegemea na aina ya Leukemia aliyonayo mtu,


hali yako kiafya wakati ugonjwa unagundulika na umri wako.
Hakikisha unaufahamu vizuri ugonjwa wako, aina za matibabu na dawa zilizopo na jinsi gani
itakavyogusa na kuleta athali kwenye mwili wako na maisha yako. Ufahamu juu ya saratani
kwa ujumla, matibabu yake na maudhi madogo madogo yatokanayo na matibabu unayopata
yatakusaidia kushirikiana bega kwa bega na wataalamu wako wa afya ili kuboresha hali ya
afya yako wakati wa matibabu na baada ya matibabu. Kumbuka siku zote kuwa kila mgonjwa
huwa na njia zake tofauti za matokeo yatokanayo na matibabu anayopata na hivyo
kutofanana kwa kila mgonjwa.

🔳Mambo muhimu ya kukumbuka kila unapoonana na Daktari wako.

Mara baada ya kuufahamu vizuri aina ya ugonjwa wako, utatakiwa kushirikiana na watoa
huduma wako wote wanaokuhudumia, ili kufikia muafaka kuhusu stahiki ya huduma na
matibabu yako ili kufikia matokeo CHANYA.🖍️(rekebisha toka change to Chanya)

▪️kumbuka kuandika maswali au dukuduku lako ili umwulize Daktari wakati wa kliniki yako, na
aidha andika majibu kwa ufasaha kuepuka kusahau

▪️ongea na Daktari kuhusu jinsi gani unavyojisikia na kila dalili unayoona au kuhisi

▪️ongea na uliza kuhusu maudhi au madhara yatokanayo na matibabu na ni aina gani ambayo
utatakiwa kutoa taarifa kwa watoa huduma wako mara moja.

▪️Uliza ni jinsi gani utaweza kutuliza au kuondoa maudhi na madhara yatokanayo na matibabu

▪️Uliza kuhusu taarifa mpya zilizopo zinazohusu majaribio mbalimbali ya tiba ya Leukemia

▪️Uliza maswali kwa weredi na kuhakiki umeelewa vizuri ulichoelekezwa na watoa huduma
wako

▪️Pata taarifa sahihi kwa kutumia lugha nyepesi kwako ya mawasiliano na ikiwezekana pata
hata michoro kama ni muhimu na lazima katika kurahisisha uelewa wako

▪️Wakati mwingine ambatana na ndugu wa karibu atakaye kuwa msaada na njia ya


kumbukumbu na usikivu kwako

▪️Kama kuna gharama zitokanazo na matibabu omba ushauri toka kwa watoa huduma yako
jinsi ya kupunguza gharama hizo

▪️Ni muhimu sana kutumia dawa zako kama maelekezo yalivyo, lakini ni muhimu kuwaeleza
watoa huduma wako kama imetokea kuwa uliruka au hukutumia dawa kama ilivyopangwa, pia
wafahamishe kama kuna aina yoyote ya maudhi madogo madogo ya dawa yaliyosababisha
ukashindwa kutumia dawa zako kwa mpango
▪️Angalia kama watoa huduma wako hawashirikiani nawe katika kutatua changamoto
mbalimbali za matibu unazopitia, fikiria kuomba mbadala wa watoa huduma wengine watakao
kusaidia.

ASANTE SANA

MICHUBUKO

 Michubuko isiyoelezeka ambayo hutokea sehemu zisizo


tegemewa kama vile, mikononi, mgongoni na miguuni
 Michubuko mbalimbali inayojitokeza bila sababu yeyote
 Inachukua muda mrefu kiasi kupona

FEVER OR NIGHT SWEATS = HOMA AU KUTOKWA JASHO USIKU.


 Kutokwa na jasho wakati wa usiku mara kwa mara ambalo
hukusababisha kuamka nyakati za usiku
 Homa, kukoho au kuharisha sambamba na kutokwa jasho
 Kupungua uzito kusikokuwa na sababu ikiambatana na
kutokwa jasho usiku
 Kutoelewa kwa nini unatokwa na jasho usiku wakati
umelala sehemu ya ubaridi

MAAMBUKIZI YANAYOJIRUDIA RUDIA


 Maambukizi yanayojirudia kila wakati, inawezekana ikawa
ni dalili ya ugonjwa kabla haujagundulika
 Mwili kutozalisha chembe nyeupe za kutosha kwahiyo
zinashindwa kuharibu virusi , bakteria na fangasi hatarishi
 Maambukizi yanaweza kujitokeza mahali popote mwilini na
kusababisha homa, kutokwa vidonda koonii, kukohoa,
uvimbe mwekundu, maumivu kuzunguka kidonda

UCHOVU
 Uchovu ni dalili ya kawaida anayoiona mtu kabla ya
kigundulika ugonjwa
 Udhaifu au uchovu ambao unachukua muda mrefu zaidi ya
majuma 2 na/au kupungua uzito
 Kuchoka kupita kiasimfululizo, kupumua kwa shida wakati
au baada ya kufanya kazi hata wakati mwingine ukiwa
umelala usiku
 Kupungua uwezo wa kufikiri na kuchanganyikiwa kwa
urahisi

KUTOKWA NA DAMU
 Kutokwa damu kusiko kawaida kwenye sehemu zisizo
tegemewa
 Kutokwa na damu nyingi
 Vipele vidogo vidogo , alama nyekundu kwenye ngozi
zijulikanazo kama PETECHIAE

You might also like