You are on page 1of 1

TUNAKUJA NA VIPAJI

  Alfred Ossonga
1.Tunakuja na vipaji vyetu, mbele zako ee Bwana
Tunatoa shukurani zetu, kwako Baba Muumba

Tunaleta mavuno, Bwana Mungu pokea


Tunaleta na fedha, Bwana Mungu
pokea
Mkate na divai, Twakuomba upokee

2.Ni matunda ya mashamba yetu, uliyotujalia


Ndilo jasho letu sisi Bwana, twakuomba pokea

3.Watumishi wako tunakuja, na zawadi kidogo


Twakusihi sana Mungu Baba, pokea mikononi

4.Nafsi zetu zote mali yako, utupokee sisi


Ee Bwana utujalie afya, uzima na baraka

You might also like