You are on page 1of 4

HUDAIBYA EXAMINATION COMMITTEE (HEC)

CHAMAZI ISLAMIC SEMINARY


KIDATO CHA I – MTIHANI WA MUHULA WA PILI ,2023
015 – ELIMU YA DINI YA KIISLAM

TIME:2:30 HOURS
Maelekezo

1. Mtihani huu unasehemu A, B, C.

2. Jibu maswali yote kutoka sehemu A na B na maswali mawili tuu kutoka


sehemu C

3. Zingatia maelekezo ya kila swali

4. Udanganyifu wa aina yoyote ni haramu

5. Andika jina lako kamili katika kila ukurasa wa kujibia.

SEHEMU A: (alama 15)

Jibu maswali yote

1. Chagua jibu sahihi katika kipengele (i) - (ii) kisha andika herufi yake katika
karatasi yako ya kujibia.
A). Mtume amesema mwenye kutubia kabla jua halijachomoza upande
wa magharibi mwenyezi Mungu (S.W) atamkubalia toba yake". Hadithi
hii inatufundisha kiwa:-
a. Kuleta toba ni jambo la hiari kwa waumini
b. Allah (S.W) hakubali Toba wakati wa mchana.
c. Allah (S.W) waja wake wakati wa kuchomoza jua.
d. Ni muhimu kuomba msamaha kwa Allah(S.W) kabla ya swala ya
magharibi.
e. Ni wajibu kuleta toba pale tuu mja anapokosea
B). ..........................ni miongoni mwa watu waliofanikiwa kuruka handaki
katika vita vya handaki na kuingia upande wa waislamu.
a. Abuu sufiani
b. Umati bin Abdul Aziz
c. Amr bin Abduud
d. Zaid bin harith
e. Utbah bin Rabia

Page 1 of 4
C). Hamisa alikuwa na rafiki zake alikuwa anamsifia Zawadi kuwa ni
muumini wa kweli. Hamisa alikuwa maanisha kuwa:-
a. Zawadi anasimamisha swala
b. Zawadi naamini nguzo zote za imani
c. Zawadi anasimamisha nguzo tano za uislamu
d. Zawadi anaambatanisha maneno yake na matendo
e. Zawadi amheshimu kila mtu
D). Profesa Harith ni mtaalamu aliyebobea katika fani ya uchumi ikiwemo
mfumo wa uchumi katika uislamu. Je profesa Harith atakuwa
amesomea fani gani?
a. Fiqhi muamalat
b. Fiqhi ibadat
c. Fiqhi ya zaka na sadaka
d. Fiqhi Mushariqat
e. Fiqhi ya mudharabat
E). Miongoni mwa masharti ya swala ya maiti i
a. Maiti awe ameoshwa na amevikwa sanda.
b. Maiti awe muislamu na aswaliwe na waislamu
c. Maiti asiwe mnafiki wala shabiki.
d. Sehemu ya kuswalia iwe tohara na maiti awekwe mbele ya
wanaomswalia.
e. Zote ni sahihi.
F). Kwanini mwaka aliozaliwa mtume liitwa mwaka wa tembo?
a. Mwaka huu ulitokea uharibifu mkubwa wa mazao uliofanywa na
tembo
b. Mwaka huu kulitokea vitaambapo majeshi walitumia tembo.
c. Mwaka huu tembo walizaliwa kwa wingi uarabuni.
d. Mwaka huu ndio abraha alitumia tembo ataka kubomoa Al-
Qaaba
G). Uandishi wa hadithi katika kipindi cha wafuasi wa maswahaba
ulianza kipindi gani?
a. 11 AH - 101 A.H
b. 11 A.H - 100 A.H
c. 101 A.H - 200 A.H
d. 101 A.H - 201 A.H
e. Wakati wa Malik bin Ana's
H). Sehemu ya masimulizi ya hadithi tokea kwa mtume (S.A.W) au
swahaba hadi kuandikwa kwake hujulikana kama?
a. Rawi
b. Matini
c. Riwaya
d. Isnadi
e. Muttafaq Alaihi
I). Historia ya kuhifadhi hadithi katika maandishi imegawanyika katika
atua ngapi?
B. Mbili

Page 2 of 4
C. Tatu
D. Nne
E. Tano
F. Saba
J). Moja kati ya zifuatazo miongoni mwa nguzo za khutba ya Ijumaa.
a. Kumshukuru mwenyezi Mungu (S.W)
b. Kumswalia mtume (S.A.W)
c. Kuwahusia waislamu kumcha Allah (S.W)
d. Kusoma Qur-an
e. Kuwaombea dua Mashekh wetu wakubwa.

2. Oanisha sentensi zilizopo kifungu A na maneno yaliyopo katika ifungu B


Kisha andika herufi ya jawabu kwenye kitabu chako ulichopewa.
KIFUNGU: A KIFUNGU: B
1. Ni swala inayosawaliwa muda A. Istiqaa
wowote kwaajili ya kuomba B. Kupatwa kwa jua
msaada kutoka kwa Allah (S.W) C. Istikhara
2. Ni swala yenye rakaa mbili na D. Tahajjud
tukufu mbili kwa kila rakaa moja E. Dhuha
3. Ni swala ya sunna kwa ajili ya
kuomba mvua.
4. Ni swala inayoswaliwa baada ya
jua kupanda kiasi
5. Ni swala inayoswaliwa rakaa
nane usiku na kumalizia kwa witri
rakaa tatu.

SEHEMU B
Jibu maswali yote kwa ufupi.
3. a. Qur-an ni nini?
B). Bainisha misingi mitatu ya usomaji wa Qur-an.
C). Ni ipi tofauti iliyopo kati ya sura za Makka na madina? Hoja tatu.
4. Mzee Ally amekuwa akimsisitiza sana mtoto wake kuwa ajitahidi
kusoma sana elimu ya dunia na elimu ya Akhera kwa mtazamo wako
wewe unadhani mzee Ally yupo sahihi?. Hoja sita.
5. a. Dini ni nini kwa mtazamo wa uislamu?
b. Ni ipi tofauti iliyo juu ya dhana ya dini kati ya mtazamo wa uislamu
na ule usiokuwa wa uislamu. Hoja tatu.
c. Unadhani kwanini mwanadamu hawezi kuishi bila ya dini? Hoja
tatu.
6. a. Nimambo yapi ya msingi aliyoyafanya Mtume (S.A.W) mara tuu
alipofika Madina hoja nne (4)
b. Mkataba wa madina ulikuwa na sehemu kuu mbili ni zipi hizo?
c. Fafanua kwa ufupi vitimbi vya wanafiki katika kuizuia nuru ya Allah
(S.W) (uislamu) madina. Hoja tatu.
7. a. Hadithi ni nini kisheria?

Page 3 of 4
I. Onesha tanzu nne za hadithi za mtume (S.A.W) kwa kigezo cha
sahihi.
II. Tumia hoja tatu kuonesha udhaifu wa madai ya wapinzani wa
hadithi za mtume (S.A.W) kuonesha kuwa hauwezi kutekeleza Qur-
an bila ya hadithi za mtume (S.A.W)
8. Ukiwa kama mwanafunzi wa kidato cha tatu mfahamishe rafiki yako
asiyejua uwepo wa malaika kwa kuonesha malaika ni nani kisha tumia
ushahidi dhahiri kumuonesha kazi 6 za viumbe hao.

SEHEMU C: ALAMA 30
Jibu maswali mawili tuu.
9. Bila ya shaka tumekwisha kupa kushinda kuliko dhahiri" (48:01). Kwa
kurejea aya hiyo tumia hoja sita kuonesha namna mkataba wa
hudaibiyah uliotolewa shindi kwa waisilamu.
10. Bibi jaria amepatwa na faradhi ya kuondokewa (kufiwa) na mtoto
wake wake wa kike wa miaka 8, lakini ameshindwa kujua namna gani
anatakiwa amkafini. Ukiwa kama mtaalamu wa fiqhi hebu
mfahamishe namna atakavyoweza kumkafini. Mfahamishe hatua kwa
hatua.
11. "Tuongoze katika njia iliyonyooka ....." (01:06) unadhani kwanini
mwanadamu anahitaji muongozo utoka kwa Mwenyezi Mungu. Hoja
5.

Wabillah Tawfiq

Page 4 of 4

You might also like