You are on page 1of 65

THE ROAD TO SUCCESS.

ABSTRACT
Ni uchambuzi na uhariri katika lugha ya Kiswahili maana kusudiwa zilizo katika baadhi ya vitabu
muhimu vinavyofundisha biashara hii ya forex, ambapo katika nakala hii vimetolewa ufafanuzi
vitu vya msingi kutoka katika vitabu, tovuti na machapisho yenye vitu vya msingi kabisa
kuvifahamu kwa kina vihusuvyo forex. Nakala hii haikosoi wala kuongea tofauti na kile
kilichomaanishwa katika kitabu/chapisho/tovuti husika bali hujikita kuleta maana kusudiwa.

jonathanoscar@yahoo.com

UNDERSTAND FOREX
TABLE OF CONTENTS
1. YOUR MOST IMPORTANT INVESTMENT AS A FOREX TRADER…………………………………………………
2. FOREX TERMINOLOGIES…………………………………………………………………………………………………
3. FOREX CURRENCY PAIRS………………………………………………………………………………………………..
4. OTHER FINANCIAL MARKETS…………………………………………………………………………………………..
5. CLOSING AND OPENING OF FOREX MARKET………………………………………………………………………
6. FOREX TRADING SESSIONS……………………………………………………………………………………………..
♦ Best days to trade

♦ Best times to trade

♦ Worst times to trade

7. HOW FOREX TRADING OPERATES…………………………………………………………………………………………………


♦ Buying and selling simultaneously

♦ Currencies come in pairs ♦ The long and short of it.

♦ Base currencies and counter currencies

8. THE BID, ASK AND SPREADS…………………………………………………………………………………………………………..


9. HOW TO READ A FOREX QUOTE……………………………………………………………………………………………………..
10.HOW TO MAKE MONEY TRADING FOREX………………………………………………………………………………………..
11.KNOW WHEN TO BUY OR SELL A CURRENCY PAIR…………………………………………………………………………..
12. PIP, LOT AND LEVERAGE…………………………………………………………………………………………………………………

♦ How do pip, lots and leverage work together


13. TYPES OF FOREX ORDERS………………………………………………………………………………………………………………..

14. WHICH TYPE OF TRADER ARE YOU………………………………………………………………………………………………….

15. FUNDAMENTAL AND TECHNICAL ANALYSIS…………………………………………………………………………………….

16. BROKER…………………………………………………………………………………………………………………………………………..

17. RISK MANAGEMENT……………………………………………………………………………………………………………………….

1
1
UTANGULIZI....

{Nakala hii imeandaliwa na jopo la wahusika wafuatao, wachambuzi wa forex, wafanya


biashara wazoefu wa forex, bila kusahau wataalamu katika biashara ya forex (professional
traders)}.

LENGO KUU LA NAKALA HII.

(Ni kuwasaidia walioingia na wale wenye nia ya kutaka kuingia “na si kujaribu” katika
biashara hii kuweza kuijua, kuielewa na kutambua uhalisia na maana sahihi ya yale
yanayoihusu biashara hii yakiwa yameandikwa katika vitabu mbalimbali na kufundishwa
na watu mbalimbali katika kila pembe ya dunia hii, kisha huyu mtu anaetaka kuingia basi
aingie kwa ridhaa yake na si kwa ushawishi, huku huyu ambae tayari ameingia ajue kuwa
yupo mahali panapomuhitaji sana yeye kuliko yeye anavyopahitaji. Nakala hii inakupa na
kukukumbusha vitu vya msingi katika forex ambavyo hupaswi kuacha kuvijua na
kuvielewa).

KILICHOMO NDANI YA NAKALA HII

Ni uchambuzi na uhariri katika lugha ya Kiswahili, maana kusudiwa zilizo katika baadhi ya
vitabu muhimu vinavyofundisha biashara hii ya forex, ambapo katika nakala hii tutaenda
kuvitolea ufafanuzi vitu vya msingi kutoka katika vitabu na machapisho yenye vitu vya
msingi kabisa kuvifahamu kwa kina, baadhi ya vitabu vitakavyohusika katika nakala hii
kwa kuanzia tu ni NAKED FOREX, CURRENCY TRADING FOR DUMMIES, LETS GET TO KNOW
FOREX pamoja na kutoka katika tovuti mbalimbali ikiwemo babypips.com na nyinginezo.
Nakala hii haikosoi kile kilichomaanishwa katika kitabu/tovuti husika bali hujikita kuleta
maana kusudiwa “kwanini haikosoi” kwasababu asilimia kubwa kama si zote vitabu viko
sahihi bali mapungufu ya vitabu yanatokana na uakisi wa uelewa na ufahamu wa msomaji
juu ya yaliyoandikwa katika vitabu hivyo.

Sasa basi ni kivipi mtanzania ataweza kuwa huru kuamua kuifanya biashara hii ama
kutokuifanya na ilihali vitabu vilivyochambuliwa kwenye nakala hii vinakufundisha kwa
kusudi la wewe kuingia katika biashra hii?? Ni kweli ndio maana sasa waandaaji wa nakala
hii katika sura inayofwata ya nakala hii wamekuandikia maoni, ushauri, mapendekezo na
mtazamo wao kutokana na vile wanavyoijua na kuielewa forex kutokana na kuifanya
2
2
kwao. Hivyo hayo maoni, ushauri, mapendekezo na mtazamo wao ni ramani tosha kwako
kufanya maamuzi sahihi.

KITU MUHIMU CHA KUKIELEWA HAPA

(Walengwa wa nakala hii).

Inawahusu watu wa aina tatu (3), ya kwanza, wazoefu katika biashara hii, pili watu
walioianza hivi karibuni (miezi kadhaa), na tatu wale ambao hawajaianza kabisa biashara
hii. Maelezo katika makundi haya matatu;

Tukianza na kundi la kwanza “wazoefu” yawezekana ulivisoma na kuvielewa vizuri, ni


vizuri lakini nakala hii inaenda kukuongezea na kukuwekea msisitizo zaidi wa
ulichokielewa kwa utulivu kabisa hatua kwa hatua na kwa maana kusudiwa bila kuacha
chochote, ambapo kwako wewe sasa itakuwa ni “summary” na hivyo kukukumbusha hata
pale ulipokuwa umepasahau, pale ambapo haukupaelewa na pale ambapo ulipaelewa
tofauti.

Kundi la pili “walioianza hii biashara hivi karibuni” pamoja na kuwa hii nakala itakuwa
imekurahisishia lakini pia ni muhimu kuvisoma vitabu hivyo pamoja na machapisho hayo
kutoka kwenye hiyo tovuti na zingine zilizotumika kwa maana vinakupa msingi madhubuti
na endapo ukavielewa kwa maana kusudiwa basi itakurahisishia wewe kuweza kuvielewa
kwa uharaka zaidi vingine na kuepusha kurudiarudia ulichokwisha kujifunza na kukielewa,
hivyo inakuhitaji kuwa na utulivu mkubwa katika kuisoma nakala hii, lakini kama
umevisoma basi utaungana kwa yale niliyoyaeleza katika kundi la kwanza.

Kundi la tatu, hii nakala itakusaidia kuelewa kwa uharaka zaidi na kukupunguzia mzigo wa
kurudiarudia kuvisoma vitu ulivyokwisha kuvisoma utakapokumbana navyo katika vitabu
vingine, lakini pia kukupa msingi imara wa kuelewa maana halisi na kusudiwa. Nawe
hupaswi kuishia hapa tu bali utahitajika tena kuvisoma vitabu hivyo kwa lengo kama
lilivyoelezwa hapo juu.

N:B Haimaanishi haujui au hauelewi lugha ya kingereza hapana, uwe makini hapa, hii ni
kwa ajili ya kukupa msaada wa ziada ambao ni muhimu sana na wenye thamani kuliko

3
3
unavyofikiria. Na pia kuna kuielewa lugha kama nyenzo ya mawasiliano na pia kuielewa
pale inapotumika kama nyenzo ya biashara, nakala hii inakupa maana sahihi na kusudiwa
ya lugha ya kibiashara.

MAONI, USHAURI, MAPENDEKEZO NA MTAZAMO WA WAANDAAJI WA


CHAPISHO HILI KUHUSU BIASHARA YA FOREX MTANDAONI.
Biashara ya Forex kupitia mtandao ni biashara ambayo ipo muda mrefu sana miongo
kadhaa iliyopita pengine wengi wenu msomao chapisho hili mkiwa bado hamjazaliwa,
lakini imekuja kufahamika kwa kiwango kikubwa katika jamii yetu hii ya kitanzania siku za
hivi karibuni, japokuwa wapo walioifahamu muda mrefu kati yetu sisi watanzania.
Ufanyikaji wa hii biashara umekuwa ukiboreshwa kila kunapokucha, yote hiyo ni katika
kurahisisha kufanyika kwake ambapo sasa mtu yeyote anaweza kuifanya akiwa popote
katika dunia hii, pale tu atakapokuwa na uwezo wa kuwa na huduma ya internet na kifaa
kinachohusika.

Kichekesho ni kwamba kila kukicha biashara hii hurahisishwa uwepesi wa jinsi ya


kufanyika lakini siyo uwepesi wa jinsi ya kuifanya ufanikiwe kupata faida, kukurahisishia
wewe kuweza kufanya popote haihusiani na kurahisisha maarifa ya jinsi ya kuifanya
ikuletee faida. Hivyo uhitajikaji wa maarifa ya kuifanya hii biashara haujawahi
kurahisishwa kwamba sasa inahitaji maarifa kidogo la hasha! Bali ni kinyume chake, kadri
inavyokuwa rahisi kukufikia wewe ili uweze kuingia katika biashara hiyo, ndivyo ambavyo
inavyohitaji maarifa mengi zaidi ya wewe kuweza kuimudu na ikakuletea matokeo chanya.

Kitu kimoja ambacho hupaswi kukisahau hata sekunde moja ni kwamba binadamu ni
wabinafsi, hivyo ndivyo ilivyo na ndivyo inavyopaswa kuwa na ndio asili yetu
inavyotuhitaji tuwe na ni faida kuwa hivyo, kwasababu kuwa hivyo ndipo kunazaliwa
neno utofauti. Ili tuweze kuishi vyema katika ulimwengu huu yatupasa kuwa tofauti,
lazima awepo mwenye nacho na asiye nacho, ili hii dunia ifike mwisho basi binadamu
wote tufanane wote tuwe nacho au wote tusiwe nacho, wala dunia haitachelewa kufika
mwisho na ni kitu ambacho hakiwezekani sote kuwa sawa, haijawahi kutokea na wala
haitakuja kutokea tukawa sawa.
4
4
Kwahiyo mtu anapokuja kukufahamisha kitu ambacho ni cha mafanikio ujue ni kitu
ambacho hakipo tofauti sana na vingine ambavyo ukivifahamu pia vitakuletea mafanikio,
anapokuletea biashara ya forex usitegemee kuwa ni biashara pengine ya tofauti sana
kuliko zingine zote hapana, na kama ni tofauti sana kwamba inaleta mafanikio sana kuliko
zingine basi pengine usingesikia kila mtu akiipigia upatu kila kukicha kulingana na nature
yetu ya ubinafsi tuliyonayo hivyo basi kama kweli ina mafanikio makubwa kuliko zingine
basi ujue ugumu wake ni mkubwa pia na ni wa tofauti sana kulinganisha na zingine. kama
ingekuwa ni tofauti sana na ni rahisi tu basi asingekuja kukuambia na ingekuwa siri maana
hakuna binadamu asiyetaka anufaike sana pekee ili dunia impigie salute kutokana na
msingi ubinafsi tulioumbwa nao.

Na hata angekwambia bado asingetumia muda wake kukufundisha kisha umlipe kitu
kidogo bali angekuwa bize kuzivuna huko, hivyo anapokufundisha ni anakupa mlango wa
fursa kama fursa zingine kwamba endapo utaitumia vizuri kutegemea na uwepesi wa akili
yako basi itakuletea manufaa pengine hata zaidi yake mwenyewe. Nazidi kusisitiza hapa ili
uelewe usiende kama kipofu ambae huelewi unakokwenda, kwa hiyo si rahisi kama
inavyoweza kusikika.

Hivyo pale unapoona mtu anakushawishi sana akufundishe kitu cha wewe kutengeneza
hela nyingi sana huku yeye anahitaji hela yako ndogo, kuna kitu hakuweki sawa kuna
taarifa ya upande wa pili wa shilingi anakunyima kwa kuhofia wewe kukataa. Kwahiyo
anachokwepa hapo kukuweka sawa ni kwamba kuna changamoto za hicho
anachokuambia na ndio maana nayeye kwa kujua kuwa kuna changamoto zake ambazo
zinaweza kumzidi nguvu na yeye, ndio maana huja kwako ili angalau hicho kidogo
utakachompa kikatunishe mfuko na kujazia pale atakapozidiwa na changamoto akiwa
nayeye katika kuifanya.

Kwahiyo siyo kwamba anakwambia uongo kwamba unaweza ukatengeneza hela tena
nyingi hapana si uongo, lakini anakupa taarifa nusu na hata akikwambia taarifa kamili
bado itaegemea upande wa mafanikio na wakati uhalisia unaegemea upande mwingine
tofauti, hapo ndipo huonekana kuwa utapeli au uongo lakini si kweli kwamba ni utapeli au
uongo bali ni kukosekana kwa taarifa stahiki yenye uzito unaoegemea kwenye uhalisia na
si kuegemea kwenye upande unaoleta tabasamu tu. Kishike sana hiki mafanikio yako

5
5
katika forex yatategemea mtu wa kwanza atakae kuleta katika ulimwengu huu wa forex
kama utabahatika kupata mtu sahihi basi utafurahia lakini kinyume chake utajutia,
changamoto ni kumpata mtu sahihi wa kukuongoza.

Twende tukaangalie nini haswa ambacho unapaswa kukijua haijalishi upo katika kuifanya
au bado haujaingia nina imani kitakuwa msaada sana.

Biashara ya forex mtandaoni ni biashara ya kweli (a really business), ni biashara kama


biashara zingine unazozijua utofauti ni kwamba hii inaegemea katika nguvu kidogo akili
nyingi pengine kuzidi hata biashara zingine. Katika biashara hii kuna kufanikiwa na kufeli
pia, na ni asilimia kubwa ya wanaofeli kuliko wanaofanikiwa, zaidi ya asilimia 90 wanafeli,
Kwanini? jibu ni moja tu inahitaji akili nyingi na mtu nadhifu kiakili (a smart person).
Biashara hii inahitaji muda wa kutosha wa wewe kuijua kabla ya wewe kuanza kuifanya,
tena kuijua vyema na kuielewa biashara hii, kuijua kwake vizuri kunaegemea katika akili
na si hisia au mihemuko, tukisema muda wa kuijua tunamaanisha muda haswa wa kuweza
kuijua na kujua vikorombwezo vinavyoihusu si ajabu ukatumia muda wa miezi sita
kujifunza tena kwa jitihada kubwa hadi mwaka bila kuanza kuifanya au ukatumia zaidi ya
mwaka katika kutaka kuijua na kuielewa ni kitu cha kawaida.

Biashara hii inaweza kukupa utajiri lakini siyo wa kulala masikini na kuamka tajiri, biashara
hii haitaki ukimbilie sana kuangalia shuhuda za waliofanikiwa kuijua jinsi
wanavyoshuhudia kununua Macerate au Range rover, vingine si vya kweli usiamini kila
kitu, inahitaji ukimbilie kwenye shuhuda ya nyenzo gani walizozitumia (Technics and
strategies). Biashara hii inawahitaji watu wenye utaratibu wa kujisomea vitabu na
kuvielewa siyo kusoma tu, unaweza kusoma vitabu hata zaidi ya 50 lakini ukatoka bila kile
kinachotakiwa hasa.

Biashara hii inahitaji nidhamu na utulivu wa moyo akili na mawazo pia haihitaji
kujisahaulisha vitu, biadhara hii inahitaji mtu ambae kwake kujifunza kitu kipya ni sehemu
ya maisha yake, mtu ambae kila siku akili yake inautayari wa kujifunza.

Biashara hii inahitaji mtu ambae anaweza kusimama mwenyewe katika kuifanya ambae
hasubiri “Call” ya mentor wake, inahitaji ambae anatafuta kuijua na kusimama yeye pekee

6
6
huku akipata msaada wa maandishi, hakuna ambacho hakipo katika maandishi, Inahitaji
mtu ambae anajitahidi kwa udi na uvumba kujaribu kuepusha makosa yasiyo ya lazima.

Unaihitaji kuijua bishara hii ili ikuletee mafanikio basi tafuta mwalimu (Mentor) hapa
itategemeana na uelewa wako si kila mtu anaweza kusoma na kuelewa vile
inavyotakikana, huyu mwalimu au mentor wako asiwe wa kukusimamia wewe jinsi ya
kubonyeza “Buy” na “Sell” bali awe zaidi ya mentor ambae atakufundisha kuijua biashara
hii kuanzia chini, watu hawajui kitu kimoja cha muhimu, kwenye semina hizi za siku tatu
au tano haendi mtu ambae hajui ambae ndo anaanza kujifunza bali anaenda mtu ambae
ameenda “tuition” kwanza, “tuition” ya forex ni sehemu unayojua kila kitu hizi semina ni
sehemu unayoenda kufanya mazoezi ya vitendo, ni kama tu elimu nyingine mwalimu wa
kemia hufundisha sana darasani mambo mengi mpaka daftari zinajaa siku ya kuingia
maabara kwa ajili ya mazoezi ya vitendo hawi na maelezo mengi, kwasababu anajua huyu
mwanafunzi alishayasoma darasani, ndivyo ilivyo, anzia “tuition” acha kuruka hatua.

Nenda kagharamie sana “tuition” pengine baadae utaona umuhimu wa hizo seminar si
mkubwa kama ulivyokuwa unafikiria, walimu wa kukufundisha “tuition” wapo japo siyo
wote waliosahihi, unang’ang’ania kukimbilia kucheza na demo account miezi ya kutosha
mwisho wa siku unaishia kukrem tu na wakati huo ni muda ambao ungeutumia tuition,
aliyesema “practice makes perfect” alisahau kukuambia endapo tu una practice kitu
ambacho ni sahihi, kwasababu unaweza uka practice mara elfu moja kitu ambacho si
sahihi na ukakizoea lakini haimaanishi kuwa utakibadili kiache usahihi kifwate mazoea
yako.

La mwisho, usishawishike kwa kuwa umejifunza wiki mbili zilizopita na juzi umefungua
biashara ukatengeneza dollars kadhaa ukaweka mikono mfukoni kisha miguu juu ya meza
ukijua umemaliza kazi, kubonyeza “Buy” na “Sell” kisha soko likaenda katika uelekeo
wako haimaanishi umeshaijua biashara zaidi itakuwa ni bahati imekuangukia na kwenda
kwa kutegemea bahati utakuwa unacheza kamari (gambling) na siyo kwamba utakuwa
unafanya biashara, kwasababu mwisho wa siku (in the long run) hasara itakuwa upande
wako pengine utakufa kabisa kibiashara na kuiacha, ukibonyeza “Buy” ujue kwanini na
ukibonyeza “Sell” ujue kwanini.

7
7
SURA YA KWANZA.
Twende tukaanze kuuweka ubongo wetu sawa kwa kuangalia kitu ambacho ni muhimu sana
kinachotuhitaji tukijue, ni nini tunachokiwekeza hasa kwenye biashara hii? pengine hata
kuisoma nakala hii ukawa ndio huo uwekezaji tunaouzungumzia, basi twende tukauangalie
ni upi huo, hapa tutasafiri mpaka katika tovuti ya babypips.com ambapo tutaenda kukutana
na kichwa kinachosema;

Your most Important Investment as a Forex Trader.


(Je ni uwekezaji upi muhimu sana kwako wewe kama mfanyabiashara ya forex?).

Kosa lilizoeleka sana kwa wafanyabiashara wengi wapya katika biashara hii ya forex ni
kwamba wanafikiri wanaweza kutengeneza pesa ... haraka! Pamoja na kwamba ni kweli
unaweza kutengeneza pesa kwa muda mfupi, haimaanishi utakuwa ukitengeneza faida ya
hivyo kila siku.

kwa kawaida wengi wao ni kwamba wafanyabiashara wapya husoma tu kidogo kuhusu
biashara ya forex, kisha hupata mifumo ya mitandaoni ambayo inadai kuwawezesha
kutengeneza pesa haraka, na kisha wanaruka ndani ya biashara kwa sababu wanahisi kama
tayari wameshapata uzoefu wa kutosha wa kutengeneza mamilioni ya dolla. “Dunia haiendi
hivyo wewe kichwa maji hamna pesa rahisi za hivyo”

Ghafla, baada ya kipindi cha "honeymoon" kuisha na baada ya msisimko na hulka na wenge
kutulia na mifumo ya mitandaoni kuonekana haitengenezi hela tena, mfanyabiashara huyo
mpya anafahamu kuwa biashara hiyo si rahisi kama alivyofikiria. Anaanza kuona mfumo
kutoonekana ukifanya kazi kama ilivyodaiwa kuwa ungemfanya atengeneze mamilioni ya
dolla, huku mfumo wenyewe ukibaki hata haujui kwa nini soko linafanya kile linachokifanya.

Hivyo ni nini haswa unachoweza kuwekeza hapa kwenye hii biashara ni hiki;

The most important thing you can invest in as a


forex trader is your TIME!
Kila siku moja unayofanya biashara ni siku ya kujifunza na kupata uzoefu, na ukiacha
kujifunza, basi hautakuja kuwa mfanyabiashara wa mafanikio hata siku moja. Kila siku

8
8
inahitaji muda wako wa kulichambua soko. Kwa sababu habari zinafanya soko kujongea
hivyo ni muhimu kuchunguza maendeleo ya kiuchumi yanayoendelea duniani kote na
kuifanya kuwa sehemu ya utaratibu wako wa kila siku.

Twende tukaangalie maana za Istilahi kadhaa muhimu katika forex japo kwa muhtasari
huku istilahi hizo zikichambuliwa zaidi katika sura zinazofuata na katika toleo la pili katika
mfululizo wa nakala hizi.

Haina maana kwamba umechelewa sana kujua mambo hapana, pengine unayajua
mengi ambayo mwingine hayajui, hivyo si vibaya tukaanza na neno kuu lenyewe ambalo ni
Forex ama wengine wanavyopenda kufupisha na kuita FX, nini maana yake.

Hii hapa, ina maana ya (Foreign-Exchange) mabadilishano ya fedha za kigeni kulingana na


uhitaji. Mfano kubadilisha hela ya kwetu hapa Tanzania (shilling) kuwa dolla (dollar) za
kimarekani na katika mabadilishano hayo kuna gharama zinatozwa ili kuweza kupata fedha
inayohotajika. Hivyo basi pale tunapokuja kuifanya kuwa biashara na kuiita biashara ya forex
tunazungumzia biashara inayohusika na kununua au kuuza fedha au bidhaa kufuatana na
kupanda au kushuka thamani ili kupata faida kupitia mtandao.

Twende tukaziangalie baadhi ya ISTILAHI (terminologies) za forex waweza ziita lugha za forex
kwa kurahisisha zaidi.

Tuanze na ya kwanza ambayo ni ASK PRICE (bei ya kununua), hii ni gharama ya


kununua fedha/bidhaa, sambamba na hiyo tuangalie na hii BID PRICE (bei ya kuuza), hii ni
gharama ya kuuza fedha/bidhaa, hizi istilahi mbili ni kama mapacha zinaenda pamoja na
kukamilisha kitendo cha biashara ambacho kinahusisha kuuza na kununua, kwa hiyo huenda
sambamba kwa maana ya kwamba pale utakapokuwa unanunua hiki basi utakuwa
unaruhusu uuzwaji wa kingine kwa muda huohuo.

Twendelee na Istilahi nyingine LEVERAGE (mfumo wa kukuinua kimtaji) huu ni


mfumo unaokuza mtaji wa mfanyabiashara wa Forex mara kiwango kinachowekwa na
wakala wake inaweza kuwa mara 50, mara 100, mara 200 au hata mara 1000 zaidi ya mtaji
wake. Ni uwiano wa mkopo wa kampuni katika kuthaminisha bidhaa zake, na mkopo huo
waweza kuuita mtaji unatolewa na wakala ili kuimarisha ujazo wa biashara. Kwa mfano
9
9
ikiwa unatumia leverage yenye uwiano huu 1:100 endapo utaweka kiasi cha dollar 100
katika akaunti yako basi itamaanisha kwamba kwa kila dolla moja uliyoingiza kwenye
akaunti yako, unaweza kuifanyia biashara katika PIP yenye ujazo wa $100.

Istilahi nyingine hii hapa SPREADS (Tozo), ni tofauti kati ya bei ya kuuza na
kununua. Haya ndio malipo kwa wakala katika huduma ya Forex. Ili kupata faida ni lazima
kumaliza tozo hiyo. Kanuni ya kupatikana kwa hiyo tozo=Bei ya kununua-Bei ya kuuza, hapa
ndipo panapomuhitaji huyu mfanyabiashara kuwa makini na wakala wake maana
wanatofautiana, wengine spreads ni kubwa huku wengine ni ndogo, spreads kubwa ni
hatari kwa afya yako ya kibiashara. Twende tuzidi kuziangalia istilahi zingine ambazo ni
muhimu kuzielewa vizuri maana ndo msingi wako wa wewe kuielewa vizuri biashara hii.

Istilahi nyingine hii hapa PIP (price interest point), hii ni tofauti ya kipimo katika
fedha zinazowiana, ni kipimo maalumu kinachoonyesha badiliko la thamani ya fedha, na
mara nyingi huwa ni badiliko linalotokea katika kiwango cha nne cha desimali (0.0001) au
katika kiwango cha pili cha desimali kutegemea na aina ya muunganiko wa fedha
zinazowiana (jozi ya sarafu). Tutapaangalia hapa vizuri tukiwa tunaangalia MAFUNGU YA
FEDHA ZA BIASHARA.

Tusonge na istilahi nyingine ambayo ni LOT hiki ni kipimo chenye usawa wa uniti
100,000 kwa thamani ya fedha. Kwa hiyo lot1=100,000. Na hiki ndicho kiwango cha kawaida
(standard lot), kwa maana rahisi ni kwamba kuna viwango vingine vilivyovikubwa juu ya
hicho na vilivyo vidogo chini ya hapo.

Istilahi nyingine ni hii VOLUME (ujazo wa biashara), hiki ni kiwango cha biashara
chenye kipimo cha (lot).

Tuangalie na nyingine hii EQUITY hii ni thamani halisi ya salio la akaunti wakati
biashara imefunguliwa. Kwa hiyo, EQUITY=Salio +- faida/hasara, hii ndio kanuni ya kuweza
kuipata kiasi cha equity katika akaunti yako.

Istilahi nyingine ni hii MARGIN hiki ni kiwango cha usalama wa akaunti kuhimili
biashara inayoendelea. Biashara inayoendelea (open trade) ni biashara iliyofunguliwa
haijalishi kwa kununua ama kuuza fedha kabla ya kufungwa.

10
10
Tuzidi kuziangalia hizi lugha za forex, MARGIN CALL hii ni taarifa ya wakala kwa
mfanyabiashara kuongeza usalama wa akaunti baada ya kiwango cha usalama wa akaunti
kupungua chini ya kiwango kinachohitajika. Mfano wake rahisi ni sawa pale unapoongea na
simu kisha unapata kengele huku ukiwa katikati ya mazungumzo ikikutaarifu kuwa salio lako
limepungua katika kiwango cha chini.

Istilahi nyingine ni MARGIN LEVEL hiki ni kiwango kinachowasilishwa katika


asilimia kinachohusiana na salio lililopo kwa salio lililotumika. Kwa hiyo, kanuni ya kuipata
hiyo margin level ni kama ifuatavyo Margin level = (equity/used margin) x 100.

Istilahi nyingine ni FREE MARGIN hili ni salio ambalo halijahusika na biashara


iliyofunguliwa na inaruhusu kufungua biashara zaidi. Kanuni ya kuipata free margini, Free
margin=balance- hasara ya muda huo (ikiwemo swap)-margin, Kadiri hasara
inavyoongezeka ndivyo kutolewa nje ya biashara (stop out) kunavyokaribiwa.

Istilahi nyingine ni STOP LEVEL hii ni hatua ambayo nafasi za biashara


zilizofunguliwa zinajifunga zenyewe baada ya asilimia ya usalama wa akaunti kupungua sana
hivyo kushindwa kuhimili muendelezo wa biashara. Kwa hiyo hizo ni istilahi au waweza
kuziita lugha za msingi za forex unazotakiwa kuzielewa wewe mfanyabiashara wa forex.

Toka kuanza kwa ISTILAHI tumekuwa tukiliimba neno fedha waweza kuliita pia sarafu,
tumeona katika maana ya forex tukisema ni mabadilishano ya fedha za kigeni, hivyo si
vibaya tukaangalia japo kwa muhtasari tu fedha hizo zikiwa katika mafungu neno zuri zaidi
tuseme zilizo katika jozi ambazo ndizo tunazozitumia katika biashara yetu hii ya forex,
baadae tutakuja kuziangalia tena kwa kina.

MAFUNGU YA FEDHA ZA BIASHARA/JOZI ZA SARAFU.

Tuanze na mafungu makuu

(haya ni yale yanayotumika sana kutokana na uimara wa fedha zinazounda mafungu hayo,
hivyo hupelekea kuwa na kiwango kikubwa cha kuuzika na kununulika katika soko (high
liquidity)).

11
11
• EURUSD

• GBPUSD

• USDCHF

• AUDUSD

• USDCAD
Yafuatayo ni mafungu ya wastani
(yanatumika katika kiwango cha kati)

• NZDUSD

• EURGBP

• GBPJPY

• GBPCHF

Huku yakibaki mafungu ya fedha zingine ambazo zinaitwa EXOTIC PAIRS) na huwa na chini
ya asilimia 10 ya kufanyiwa biashara.

Hizo ni baadhi ya istilahi na maana zake pamoja na mafungu ya fedha za biashara, hivyo ni
vitu muhimu unavyopaswa kuvijua na kuvielewa wewe kama mfanyabiashara hata
ukikurupushwa kutoka usingizini basi unamwelezea mtu bila kumung’unya maneno. Twende
tuzidi kuzama katika vitabu vilivyotajwa kwenye utangulizi pamoja na tovuti.

Baada ya kuziangalia hizo istilahi na maana zake pamoja na mafungu ya fedha za


biashara, hivyo ni vitu muhimu unavyopaswa kuvijua na kuvielewa wewe kama
mfanyabiashara hata ukikurupushwa kutoka usingizini basi unamwelezea mtu bila

12
12
kumung’unya maneno. Twende sasa tukazame katika vitabu vilivyotajwa kwenye utangulizi
pamoja na tovuti.
Umekwisha kuona toka tulipoanza tumekuwa tukiiongelea currencies (Sarafu)
pekee, lakini si vibaya ukajua masoko mengine yanayofanana na hii na wakati ambapo
yanakuwa na uhusiano wa moja kwa moja kwamba kupungua au kuongezeka kwa hiki basi
kuna athiri moja kwa moja sarafu Fulani ambayo tunaitumia katika forex, hivyo ni muhimu
pia kuyajua, na kwa yule ambae alikwisha kujihusisha nayo maarifa ya jinsi ya ufanyikaji
wake yanaweza kuwa ni msaada mkubwa wa kukurahisishia kuweza kuielewa forex kwa
uharaka.

Masoko hayo mengine (other financial markets) yanahusisha vitu hivi vifuatavyo
Oil, stocks, bonds pamoja na Gold, Tunaenda kuliangalia hili katika kitabu cha Currency
Trading for dummies kuanzia page ya 8 ambapo kimeandikwa kichwa hiki Currencies and
other financial markets. Ni kitu gani cha muhimu ambacho hupaswi kuacha kukizingatia
katika sehemu hii kilichozungumziwa ni hiki hapa.

Yawezekana kwamba unaweza ukawa umekwisha kuyasikia haya masoko


mengine tuliyoyataja kwamba ni Gold, Oil, Stocks na Bonds. Kitu muhimu ulichosisitiziwa
hapa ni kwamba “Daima ikukae akilini mwako kukumbuka kwamba masoko mbalimbali ya
fedha ni masoko yanayosimama kama yenyewe na hufanya kazi kwa mujibu wa mienendo
yao ya ndani kulingana na data, habari, nafasi, na hisia” kwa maana hiyo wewe
mfanyabiashara pale utakapoamua kufanya biashara ya sarafu (currencies) basi fanya ya
sarafu, ukiamua kuangalia haya masoko mengine basi jikite huko pia kwasababu kila kitu
kinasimama katika nafasi yake na kwa upana wake, siyo leo Forex kesho stocks keshokutwa
bonds utaishia kutangatanga usifanikiwe huku wala kule.

Twende tukayaangalie hayo masoko mengine.


GOLD.

Kitu cha kuondoka nacho hapa kwako wewe mfanyabiashara ni hiki hapa “Dhahabu
huonekana kwa kawaida kama ukingo dhidi ya mfumuko wa bei, mbadala wa dolla ya U.S.,
na huwa duka la thamani wakati kunapokuwa na mdororo wa mambo ya kiuchumi au ya
kisiasa. Kwa mujibu wa tathmini ya kipindi kirefu, uhusiano wake na dola huwa ni kinyume

13
13
chake, pale ambapo dolla inapokuwa dhaifu zaidi ndipo ambapo huongozana na bei ya juu
ya Gold, na pale ambapo dola inakuwa ina nguvu basi huongozana na bei ya chini ya Gold.

Ijapokuwa sasa ukichukilia katika kipindi kifupi kila soko linakuwa na mienendo yake
lenyewe, ambayo inafanya mahusiano ya kibiashara ya muda mfupi yawe mepesi au
kutokuonesha utofauti mkubwa. Kwa hiyo kitu cha kukusisitizia zaidi hapo ni kwamba pale
kunapokuwa na harakati kali ama kuchanganya katika bei za Gold huwavutia
wafanyabiashara wengi wa sarafu kuweka umakini wao huko kwasababu hali hiyo
itashawishi dolla kwa namna yoyote ile kwenda katika hali iliyo kinyume ambayo ni dolla ya
marekani kuwa dhaifu, kwa hiyo wewe kama mfanyabiashara makini wa forex unatakiwa
kufwatilia kujua taarifa zinazohusu Gold.

OIL.

Kitu cha kuondoka nacho hapa kwenye mafuta kwa wewe mfanyabiashara ni hiki hapa
“Kumekuwa na taarifa nyingi sana mitandaoni zinazokanganya kuhusu uhusiano uliopo kati
ya Oil na dolla au sarafu nyingine yoyote kama vile JAPAN YEN (JPY). Hapa suala ni kwamba,
kwa sababu baadhi ya nchi ni wazalishaji wa mafuta, sarafu zao huwa na nguvu au
kuporomoka zikiathiriwa na ongezeko au kupungua kwa bei ya mafuta. Ikiwa nchi ni
muingizaji wa mafuta, basi itakuwa hivi, sarafu yake itayumba au kuimarika kutokana na bei
ya juu au ya chini ya mafuta.

Kitu cha kukiweka akili hapa ni kwamba endapo utaamua kufanya biashara yako katika soko
hili la Oil basi itakulazimu ufwatilie kwa makini sana juu ya taarifa za bei za mafuta
ulimwenguni kote ili kujua bei ikoje na kwa nani, lakini pia katika kuangalia uhusiano wake
na dolla au fedha zingine ni hivi, masomo ya utafiti wa uwiano hayaoneshi mahusiano ya
moja kwa moja kama huathiriwa na hali ya soko la Oil, hususani katika muda mfupi, ambapo
ndipo biashara nyingi za sarafu zinapoegemea. Lakini tukija kuangalia katika uhusiano wa
muda mrefu, ni dhahiri kabisa kwamba huenda kinyume (kama Gold) na ni kinyume zaidi ya
kinyume hiyo ya (Gold) na huenda kinyume pia dhidi ya sarafu nyingine yoyote. Wewe kama
mfanyabiashara makini wa forex inakulazimu ufwatilie taarifa kama hizi katika nchi
mbalimbali hususani nchi zile ambazo sarafu zake tunazitumia katika forex yetu.

14
14
STOCKS

Hapa kwenye stocks ni vizuri sana kama utaelewa uhusiano wake (kufanana kwake na
utofauti mkubwa uliopo baina ya vitu hivi viwili) wa moja kwa moja na forex, iko hivi stocks
ni dhamana ndogo za kiuchumi, huongezeka au kushuka kwa kukabiliana na matokeo ya
kampuni binafsi na matarajio, wakati forex ni dhamana ya kiuchumi ya uchumi kwa ujumla,
ambayo ni matokeo ya kukabiliana na maendeleo makubwa ya kiuchumi na kisiasa.

Kwa hivyo, kuna sababu ndogo sana ya kwamba masoko ya hisa yanahusiana na sarafu.
Matokeo ya utafiti ya masomo ya uwiano unaotokea baada ya kipindi kirefu yanaonesha
kuwa hakuna uhusiano wowote kati ya mafungu ya fedha yanayohusisha dolla na masoko ya
hisa (stocks) kwa zaidi ya miaka mitano iliyopita. Hivyo ukitaka kufanya biashara ya stocks
jua umeingia katika uwanja mwingine kabisa.

BONDS.

Kati ya masoko yote tuliyoyaangalia hapo juu, soko hili lina uhusiano wa moja kwa moja na
soko la sarafu, ni nini kinachofanya uhusiano utokee hapa ndicho ambacho yakupasa
ukizingatie ni hivi soko hili la bonds lina uhusiano mzuri zaidi na soko la forex kwa sababu
yote yanaathiriwa sana na matarajio ya kiwango cha riba.

Kwa hiyo pointi ya msingi hapa kwa wewe mfanyabiashara ni ipi, ni hii hapa, kwa hakika
unahitajika kuweka jicho kwenye matokeo ya vifungo (bonds) vya serikali vya nchi zenye
fedha imara ili kufuatilia vizuri matarajio ya soko la kiwango cha riba. Mabadiliko katika
viwango vya riba (interest change) hufanya ushawishi mkubwa kwenye masoko ya forex.

Hivyo ndivyo masoko mengine yalivyo kwa ufupi na uhusiano wake wa moja kwa moja na
soko la sarafu ambayo unaweza ukaamua kujikita huko pia siyo dhambi.

Twende sasa tukaangalie kitu muhimu kabisa kingine tena ambacho ni muhimu
kukizingatia, Japo kuna biashara ambazo zinafanyika 24/7 bila hata ya kupumzika, hii forex
yetu inatutakia mema katika afya zetu kwa kututaka tuweze kupumzika na kujitathmini
kuwa tumefanya nini katika siku kadhaa zilizopita za biashara yetu, hivyo soko letu la forex
lina kitu kinachoitwa;

15
15
KUFUNGWA NA KUFUNGULIWA KWA SOKO LA FOREX.

Soko letu la forex hufungwa kuanzia siku ya ijumaa jioni hadi mwanzoni mwa siku ya jumapili
kwa mbali linaanza kujiachia mapema alasiri ya jumapili katika Amerika ya kaskazini,
ambapo inakuwa ni mishale ya jioni kule London.

Soko letu la forex linapofungwa haimaanishi ni lazima kila kitu kisimame kupisha kufungwa
huko la hasha bali unaweza ukaiacha biashara yako uliyoifungua ikaendelea kuwepo wazi na
kisiharibike kitu chochote na pindi soko litakapofunguliwa utaendelea kuiangalia biashara
yako inavyozidi kusonga mbele, hii yote ni kwasababu tunatofautiana mwingine anaweza
akawa amefungua biashara ya masafa marefu inayochukua muda hadi wa miezi kadhaa
mpaka mwaka.

Kwa wewe mfanyabiashara yakupasa uelewe siku gani soko la eneo fulani
linakuwa linashughulika (active) ili kukusaidia kujua ni fungu gani la fedha eneo lake liko
active kwa muda huo na siyo unakisia fungu la fedha la kuliangalia. Turudi tena katika kitabu
chetu cha Currency trading for dummies katika page ya 5 ambapo kuna kichwa
kinachosema;

THE OPENING OF THE TRADING WEEK.

Pointi ya msingi hapa kwa wewe mfanyabiashara ni hii hapa;

Kufunguliwa jumapili inawakilisha pointi ya kuanzia (Resuming) ambapo masoko ya sarafu


yanaianza biashara kutoka pale ilipoishia siku ya Ijumaa wakati soko linafungwa katika
Amerika ya Kaskazini (saa11 jioni majira ya Mashariki). Hii ndio huwa nafasi ya kwanza ya
soko la forex kuitikia habari na matukio ambayo yaliweza kujitokeza mwishoni mwa wiki. Bei
inaweza kuwa ilifungwa katika kiwango fulani katika biashara soko lilipokuwa katika uwanda
wa New York, lakini kulingana na matukio, biashara inaweza kuanzia katika viwango tofauti
wakati wa kufunguliwa Jumapili.

Ni nini cha kukichukua hapa, ni kwamba soko linapofungwa halimaanishi uende ukaweke
miguu juu ukisubiri lifunguliwe usiku a manane wa jumapili kwa majira yetu ya kitanzania.
Bali linakupa kazi ya kwenda kuangalia nini kimetokea au nini kinaenda kutokea kwasababu
vina athari kubwa katika soko hili la forex.
16
16
Twende tukaangalie soko linapokuwa linashughulika (active) katika vipindi na maeneo
tofauti tofauti.

TRADING IN THE ASIA-PACIFIC SESSION.

Point ya msingi hapa kwako wewe mfanyabiashara ni kama ifuatavyo, miji mikuu ya biashara
za kifedha soko linapokuwa katika session hii ni Wellington New Zealand; Sydney Australia;
Tokyo Ujapani; Hong Kong; na Singapore. Iweke akilini vizuri miji hiyo, katika suala la
mafungu ya fedha za biashara ambayo yanafanyiwa biashara kwa wingi ni kwamba taarifa
(report) za habari na data kutoka New Zealand, Australia, na Japan zitaligonga soko katika
session hii.

Lakini kubwa kuliko yote ambalo wewe mfanyabiashara unatakiwa kulifahamu katika
session hii ni kwamba Kwa sababu ya ukubwa wa soko la Kijapani na umuhimu wa takwimu
za Kijapani kwenye soko, vitendo vingi katika kipindi hiki cha Asia-Pasifiki vitajikita moja kwa
moja katika mafungu ya fedha yanayohusisha fedha ya kijapani (japan yen).

TRADING IN THE EUROPEAN/ LONDON SESSION.

Point ya msingi hapa kwako wewe mfanyabiashara ni kama ifuatavyo, Karibia na katikati ya
siku ya biashara ya Asia, vituo vya kifedha vya Ulaya vinaanza kufunguliwa na soko linaanza
kukaa katika mkondo wake kamili. Session hii ya ulaya inaanza kujitokeza katikati ya siku ya
biashara ya Asia na wakati huohuo ikiwa inapandana na session ya Amerika Kaskazini, kitu
ambacho hupaswi kukisahau hapa ni kwamba katika kipindi hiki kiwango cha uuzaji na
ununuaji pamoja na riba (liquidity na interest) ndipo hapa vinapokuwa katika kilele chake.

Point ya pili ya msingi ambayo unapaswa kuizingatia ni hii hapa, Habari na data za matukio
kutoka katika ukanda wa ulaya (eurozone) (na nchi binafsi kama Ujerumani na Ufaransa,
Uswisi na Uingereza) hutolewa mara nyingi katika masaa ya mapema ya asubuhi katika
session hii ya Ulaya. Matokeo yake, kunakuwa na mjongeo (moves) kubwa ya kibiashara na
uangavu (activeness) wa biashara hutokea katika sarafu za Ulaya (EUR, GBP, na CHF) pamoja
na mafungu ya euro cross currencies (EUR / CHF na EUR / GBP).

17
17
TRADING IN THE NORTH AMERICA SESSION

Point kubwa hapa ya kuizingatia kwako wewe mfanyabiashara katika hii session ni hii hapa,
ujazo wa biashara unakuwa juu sana katika session hii, Baadhi ya harakati kubwa na zenye
maana zaidi zinazoiongoza bei ya soko hufanyika wakati wa kipindi hiki. Kitu cha muhimu
sana kukijua ni kwamba katika amerika ya kaskazini asubuhi na mapema taarifa za kiuchumi
za kimarekani zinaachiwa ambazo zinafanya maamuzi muhimu kabisa wa thamani ya dola.
Jambo la muhimu zaidi hapa ni kwamba twende tukaangalie muda ambao taarifa hizi
hutolewa, kwa kiasi kikubwa taarifa kutoka Amerika huwa zinatolewa saa mbili na nusu
asubuhi kwa majira ya mashariki (8:30 a.m ET), huku zingine zikija kutolewa mida ya saa tatu
na saa nne (9 and 10 a.m ET). Wakati huohuo taarifa za Canada huachiwa nazo muda
unaoendana na huo kati ya saa moja hadi saa tatu asubuhi (betwee 7 and 9 a.m ET). Lakini
taarifa zingine za kiuchumi za amerika (U.S) huachiwa mchana muda wa saa nane kamili
mchana (2:00 a.m ET)

Kitu kingine cha kukiweka akilini hapa ni kwamba kuanzia muda huo wa mchana kwa masaa
ya mashariki soko la London na vituo vingine vya masoko ya biashara kwa ukanda wa ulaya
huanza kufifia na kisha kufungwa.

18
18
Picha hapo juu inaonesha muda wa kufunguliwa masoko katika vituo mbalimbali, lakini
jedwali letu lina majira ya masaa ya Singapore, ili kupata masaa ya ET ni kinyume chake
hivyo huku Singapore ikiwa ni a.m basi ET itakuwa p.m, ndio maana ya wino mweusi
(maandishi yaliyoandikwa kwa makapeni katika jedwali hilo (EST).

Baada ya kuangalia masoko katika sessions mbalimbali tukamalizie kwa


kuangalia siku nzuri katika wiki za kufanya biashara ya forex pamoja na hilo tutaangalia na
muda unaofaa na muda ambao haufai kuingia sokoni, japo hakuna mtu atakaekuzuia
kufungua biashara muda wowote utakaotaka. Hili tutaenda kuliangalia katika tovuti ya
babypips.com. Ambapo kuna kichwa kinachosema;

BEST DAYS OF THE WEEK TO TRADE FOREX.

Katika sessions zote ni session ya London/European ndio ambayo iko busy (inashughulika)
zaidi, lakini pia kuna siku fulani katika juma ambapo masoko yote huonesha harakati za
mjongeo (movements) zaidi. Twende tukaangalia hii chati hapa chini inayoonesha wastani
wa PIP kwa mafungu ya fedha makuu kwa kila siku ya wiki:

19
19
20
20
Kama unavyoweza kuona kutoka kwenye chati hapo juu, inafaa sana kufanya biashara
wakati wa katikati ya juma, kwa kuwa hapo ndipo shughuli nyingi (most actions) hutokea.
Point nyingine ya msingi kwako wewe mfanyabiashara ni kwamba kwasababu biashara ya
forex ni 24hrs haimaanishi kuwa ufanye kila muda kwa wewe mfanyabiashara unaetaka
kunufaika na hii biashara, hivyo kama tulivyoweza kuona kutoka hapo kwenye chati yetu
kwamba katikati ya juma ndio siku nzuri za kufanya biashara lakini sasa twende tukaangalie
muda mzuri na muda mbaya kufanya biashara katika juma kwa ujumla.

21
21
Best Times to Trade:
Pale ambapo sessions mbili zinapopandana(overlapping).
Point ya msingi hapa ni kwamba hizi ni moja ya nyakati ambapo matukio makuu ya habari
hutokea ambazo hupelekea mabadiliko ya haraka na ya bila kutegemewa katika soko
(volatility) pamoja na kusababisha mjongeo unaotoa uelekeo wa soko. Nini cha muhimu
unachopaswa kuwa nacho hapa ni hiki, kuhakikisha unakuwa na sheet inayoonesha masaa
ya soko (market hours) ili kukukumbusha na kukuonesha muda wa masoko mbalimbali
kufunguliwa na kufungwa.

Muda mwingine mzuri kwako kufanya biashara ni huu;

Pale unapokuwa muda wa session ya ulaya.


Hii ndo session ambayo inakuwa busy kuliko zingine zote hivyo kunakuwa na mabadiliko
mengi katika soko na mijongeo yenye nguvu inayoliongoza soko katika uelekeo fulani.
Muda mwingine mzuri ni huu;

katikati ya juma.

Hii ni kama tulivyoweza kuangalia hapo juu kutokana na chati yetu, ambapo kunakuwa na
mjongeo mkubwa wa biashara katika siku hizo unaopelekea kutokea kwa wastani mkubwa
wa PIPS zinazokuwa zinatembea kwa wastani katika siku hizo kulinganisha na siku zingine
rejea kwenye chati yetu pale juu.

Baada ya kuangalia muda mzuri hebu sasa tugeukie muda MBAYA ambao kwa
wewe mfanyabiashara makini inatakiwa uwe makini zaidi hata kama utahitaji kufungua
biashara.

22
22
Worst Times to Trade:
Jumapili.

Hatakama Amerika ya kaskazini soko linaanza kurudi tena ulingoni baada ya kufungwa na
kusimama (pause), si siku nzuri sababu ni kwamba watu wengi “wafanyabiashara wengine”
kote ulimwenguni wanakuwa wamepumzika wakiifurahia weekend yao.

Muda mwingine ambao si mzuri kuanza kushughulika ni huu;

ijumaa
hii ndo siku ambayo soko linaanza kufifia kwa kuelekea kufungwa katika session ya Amerika
ya kaskazini, kwa kukazia hapa ni hivi soko siku ya ijumaa linakuwa busy mpaka kufikia saa
sita kamili mchana (12:00 p.m EST) baada ya hapo soko linaanza kuporomoka kwa kasi
mpaka kufikia saa kumi na moja jioni (5:00 p.m EST) ambapo linafungwa katika session hiyo,
kwa hiyo kwa siku ya ijumaa tunaiita nusu siku ya biashara. Muda mwingine mbaya katika
kufanya biashara ni;

kipindi cha likizo

Hapa ni kwamba kila mtu anakuwa amepumzika.

muda mwingine mbaya ni kipindi cha;

Tamthilia ya GAME OF THRONES, pamoja na kipindi cha fainali za NBA,


unaweza ukaona ni sababu zinazochekesha, kitu unachopaswa kuelewa hapa ni kwamba
kuanzia kipindi ambacho watu wanakuwa likizo, weekend, au wako busy kuangalia
tamthilia, au wako busy na fainali za NBA, vipindi vyote hivyo vinasimamia katika sababu ya
msingi sana moja kuu ambayo inakuwa ni kutokuwepo uhusika wa wafanyabiashara wengi
katika soko katika kipindi fulani, kumbe pale kila mmoja anapokuwa kwenye soko hupelekea
soko kuwa busy ambapo tumesema soko linapokuwa busy ndio muda mzuri wa wewe
kushughulika na biashara na tukasema kabisa soko linakuwa busy sana katika session ya
ukanda wa ulaya.

Muda mwingine wa kuuangalia kwa makini sana na kwa jicho la tatu ni katika kipindi
ambacho kunakuwa na matukio ya habari au taarifa kubwa sana (Major news Events
23
23
[M.N.E]), hapa kunakuwa na utata wakati kila mmoja anakuwa anajihakikishia kuwa soko
litakimbilia kwenye mjongeo huu ndipo ambapo mambo hugeuka na kuja tofauti na vile kila
mmoja alivyokuwa ametegemea, pointi ya msingi hapa ni kwamba utaweza kwenda napo
sawa ikiwa ni mtu uliyekomaa katika biashara hii na una mbinu madhubuti katika ufanyaji
wako biashara (good strategies).

SURA YA PILI
JINSI BIASHARA YA FOREX INAVYOFANYIKA.

Tuangalie ufanyikaji wa biasharaa hii ya forex. Kwanza tuanzie hapa, umeweza kuona
maneno haya kutoka kwenye sura ya kwanza ambayo ni ununuaji na uuzaji twende
tukaangalie uhusiano wake. Hapa tutakuwa tunarudi tena katika kitabu chetu cha Currency
Trading for Dummies, katika page 11 ambapo utakutana na kichwa hiki;

BUYING AND SELLING SIMULTANEOUSLY.

Moja ya sehemu inayowagonga sana vichwa wageni katika biashara hii ya forex na wale
waliozoea aina nyingine za biashara zinazoendana na hii kama vile stocks ni kwamba hii
biashara ya sarafu inahusisha vitu viwili vinavyoenda kwa pamoja ambavyo ni UNUNUZI na
UUZAJI (Purchase and Sale).

Tuchukulie mfano katika biashara ya stocks leo mtu akinunua share 100 za google, atakuwa
tayari anamiliki share hizo huku akitegemea kuwa bei itaongezeka. Siku atakayokuja kutoka
katika nafasi hiyo ya kushikilia share hizo (kutoka kwenye kuzishikilia au kuzimiliki share hizo
ni kwamba tayari bei imepanda kisha anaziuza share zake ili apate kile kilichoongezeka pale
juu kama faida) kwa maana nyepesi ni kwamba utakuwa unakiuza ulichonunua mwanzoni.
Sawasawa na kusema kwamba ulinunua na kisha umeuza hivyo umehusisha vitu hivi viwili
lakini kila kimoja kwa nafasi yake na kwa muda wake bila kuambatana na mwenzie vipi
upande wa biashara ya forex?

24
24
Katika upande wa biashara ya forex ni kwamba ununuzi wa sarafu moja inahusisha uuzaji wa
sarafu nyingine kwa wakati mmoja, na ndio maana ya neno mabadilishano (exchange)
linalopatikana katika maana ya forex (foreign exchange), kwa mfano leo ukisema natazamia
dolla ya kimarekani kupanda swali ni je kupanda dhidi ya nani?? Jibu ni kwamba dhidi ya
sarafu nyingine. Hivyo ukisema dola imepanda dhidi ya sarafu nyingine maana halisi ni
kwamba hiyo sarafu nyingine imeshuka kulinganisha na dolla, Na ndio maana sasa katika
sura ya kwanza uliweza kuona mafungu ya fedha na mafungu hayo yanakuwa katika jozi ya
sarafu mbili tofauti, twende tukaangalie kichwa kinachosema;

CURRENCIES COME IN PAIRS

Masoko ya forex huhusika na ufanyaji wa biashara kwa kuhusisha sarafu mbili zilizo katika
jozi, na majina ya jozi hizo huwa ni matokeo ya mchanganyiko wa sarafu hizo mbili tofauti
zitakazohusika katika mlolongo wa kufanyiwa biashara au "mbadilishano," baina ya sarafu
moja dhidi ya nyingine katika jozi husika.

Na majina ya jozi hizo hupendelewa kuandikwa kama vifupisho vya majina ya sarafu
zilizounda jozi hiyo, tuliweza kuangalia japo kwa muhtasari katika mafungu ya fedha sasa
basi twende tukaangalie majina hayo kwa urefu pamoja na majina yake ya utani
(nicknames).

25
25
MAJOR CURRENCY PAIRS

Tunazitambuaje hizo jozi kuu (major currency pairs)? Ni hivi, Jozi kuu zote za sarafu
zinahusisha dolla ya marekani kwa upande mmoja wa jozi hiyo. Kitu tu cha kukumbuka hapa
ni kwamba uratibiwaji wa hizo sarafu zinazoungana kuunda jozi na huku tukizitambua kuwa
ni jozi kuu haukuwekwa tu ilimradi bali uliwekwa kwa kufuata au kutumia kanuni za
Kimataifa za Shirikisho la viwango (ISO [International Standardization Organization]) kwa
kila sarafu.

Tuliweza pia kuziangalia cross pairs tulipoyaainisha mafungu ya fedha, tweñde


tukaangalie Majina kamili ya sarafu zinazounda jozi hizo pamoja na majina yake ya utani.

26
26
CROSS-CURRENCY PAIRS

Je hizi Cross-currencies zikoje? Ni jozi yoyoote ya fedha ambayo haijumuishi dolla ya


kimarekani. Je zinakusaidiaje wewe mfanyabiashara kama faida kwa upande wako? Jozi hizi
hukuwezesha wewe mfanyabiashara kuzilenga moja kwa moja sarafu zenyewe binafsi na
kuchukulia kama faida kutokana na habari au matukio yanayozilenga moja kwa moja sarafu
hizo nje ya dola.

Pointi ya msingi kwako wewe mfanyabiashara ni kwamba mara nyingi tunahusika na aina
tatu ya hizi crosses ambazo ni EUR, JPY, and GBP na zinajulikana kama euro crosses, yen

crosses, and sterling crosses.


Twende tukayachambue zaidi mafungu ya fedha au waweza kuita jozi za sarafu
tutaenda kukutana na kichwa katika page ya 14 kinachosema;

BASE CURRENCIES AND COUNTER CURRENCIES.

Vitu ambavyo hupaswi kuacha kuvielewa hapa ni kama ifuatavyo, pale unapokuwa
unayaangalia mafungu ya fedha au jozi hizi za sarafu utagundua kwamba sarafu hizo katika
jozi fulani zimeungana katika utaratibu wa ajabu, kwa mfano, sterling-yen (GBP/JPY) kwanini
muda mwingine isiandikwe yen-sterling (JPY/GBP)?, sababu ni kwamba utaratibu huu wa
kuziweka jozi hizi ulitokea miaka mingi ilikuwa ni kuakisi fedha zenye nguvu toka kipindi
hicho dhidi ya fedha dhaifu kijadi, na sarafu yenye nguvu ndio iliyokuwa inakuja mbele
kwanza ndipo ifuatiwe na hiyo dhaifu katika mlinganyo wa hizo mbili.
27
27
Sarafu ya kwanza katika fungu/jozi ndio inayoitwa Base currency, kitu cha kukiweka akilini
hapa kwako wewe mfanyabiashara ni kwamba unapofanya kitendo kimojawapo kiwe cha
kuuza au kununua katika jozi fulani ukiwa unafanya biashara hii ya forex, hii base currency
ndio ambayo itakuwa inahusika na uuzwaji au ununuaji huo.

Kwa mfano, ukiamua kununua 100,000 EUR/JPY maana yake ni kwamba umenunua euro
100,000 na kuuza kiasi hicho hicho katika yen ya Kijapani. Mfano wa pili ukiamua kuuza
100,000 GBP/CHF maana yake ni kwamba umeuza pounds 100,000 za Uingereza na
kununua kiasi hicho hicho kwa fedha za Uswisi.

Sarafu ya pili katika jozi yenyewe inaitwa counter or quote currency, au pia secondary

currency. Wafanyabiashara wengi wanaipa uzito mdogo hii kwa sababu ya udhaifu wake
kulinganisha na base currency, lakini kitu ambacho unatakiwa kukizingatia wewe
mfanyabiashara makini ni kwamba hii sarafu ya pili ndio inayohusika na kupanda au kushuka
na hata faida au hasara unayokuwa unaipata, kwa mfano, Ikiwa umenunua GBP / JPY, na
ikaenda juu, na ukachukua faida, faida yako haipo katika paundi, bali katika yen.

{kutoka kwenye picha yetu hapo juu utaweza kuona GBP (Great Britain Pound) kushoto
kwako na ya kwanza katika jozi/fungu hilo na hii ndio tunayoiita Base currency, huku ile
ikiwa kulia kwako ikifwatia kuandikwa katika jozi hiyo ambayo ni USD hii ndio ambayo
tunaiita Counter currency/quote currency/secondary currency. Huku tukiwa na tarakimu
ambazo ni 1.51258 hizi tunaziita kiwango cha ubadilishaji (“exchange rate”) tutaenda
kuiangalia mbele kidogo ya sura hii}.
28
28
Tukaangalie kitu kingine kinachoshabihiana na hapa ni kwamba katika soko la
forex huku pia tunatumia misemo sawasawa na ile inayotumika katika masoko mengine ya
kifedha (other financial markets) katika page hiyo hiyo ya 14 twende tukakiangalie kichwa
kinachosema;

THE LONG AND SHORT OF IT.

Tuanze na cha kwanza GOING LONG.

Utakapokuwa umeenda long katika biashara yetu hii ya forex ni kwamba umenunua jozi ya
sarafu. Ukiwa umefanya hivyo utakuwa unatazamia bei kupanda juu, ili uweze kuuza kwa bei
ya juu zaidi kuliko ile uliyonunulia.

Cha pili GETTING SHORT.

Hapa kwa maana rahisi ni kwamba umeiuza jozi ya sarafu. Kwa kukazia zaidi ili ikae akilini
mwako wewe mfanyabiashara ni kwamba umeuza base currency na umenunua counter
currency. Ukiwa umefanya hivyo unachokuwa unategemea hapo ni kwamba bei iende chini
ili uje uuze katika faida. Ijapokuwa wafanya biashara wengi hawapendelei sana hii short
lakini kwa mfanyabiashara makini ni kitu ambacho unapaswa kukiwekea akili na kukitazama
kwa jicho pevu.

Cha tatu na cha mwisho ni SQUARING UP.

Hapa ni pale unapokuwa haujaamua kushikilia nafasi yoyote katika soko, unapoamua
kutokufungua biashara hapa ndipo unapokuwa uko square au unaweza kuita uko flat. Kwa
kushindilia hapa ni kwamba Wakati pekee ambapo unakuwa haupo sokoni na haujajiweka
katika hatari yoyote ya kifedha ndio huo wakati tunaosema uko flat.

Kabla hatujaenda kuangalia ni jinsi gani tunatengeneza hela katika forex twende
tukaangalie kwa kina ISTILAHI zifuatazo Pamoja na kwamba tuliziangalia kwa muhtasari tu
katika sura ya kwanza, twende tukaziweke vizuri kichwani, hapa tunaenda kukutana na
kichwa kinachosema;

29
29
The Bid, Ask and Spread.

“Quotes” (utazielewa vizuri hizi quotes katika kipengele kitakachofuata baada ya hiki) zote
za forex ni lazima ziwe “quoted” katika bei mbili ambazo tunaziita BID na ASK. Bei hii
tunayoiita bid kwa sehemu nyingi inakuwa chini kuliko ile ya ask, utaweza kuona hata
kwenye picha hii hapo juu.

Japo tuliweza kuangalia katika sura ya kwanza si vibaya tukisisitizia hapa kwamba BID PRICE
ni bei nzuri iliyopo ambayo wewe (mfanyabiashara) utaweza kuiuza kwenye soko. Tukazie na
hapa kwenye ASK PRICE, sasa hii kwa jina lingine unaweza kuiita OFFER PRICE ni bei nzuri
iliyopo ambayo wewe mfanyabiashara unaweza kununua kwenye soko.

Tuangalie na SPREAD ambayo tunasema ni tofauti kati ya bid price na offer/ask price, kwa

mahesabu marahisi ni kwamba offer/ask price kutoa bid price tunapata hiyo spread.
Ukiangalia katika picha yetu hapo juu ni kwamba kwenye hiyo quote hapo juu ya

EUR/USD, bid price ni 1.34568 na ask price ni 1.34588. Tukaiangalie picha hapa
chini inayotuonesha vitu vyote kwa pamoja.

30
30
Katika mfano wetu hapo juu kwenye picha utaweza kuona kuna 2 pips ambazo ndio namba ya
spread. Ni kipengele muhimu sana hiki cha spread kwa wewe mfanyabiashara kuweza
kukielewa vizuri kwani mawakala (brokers) wengi hutumia hapo kujinufaisha

wakitumia uelewa mdogo wa wafanyabiashara wanaoingia katika biashara hii, hili


tutaliangalia vizuri tukifika katika kipengele cha mawakala (brokers).

Twende tukaliangalie neno hili la msingi kabisa ambalo ni forex quote, nini
maana ya quote katika forex ni hii hapa, ni thamani ya hivi karibuni ya soko ambayo asasi ya
msingi (underlying asset) ilikuwa ikifanyiwa biashara katika thamani hiyo, kwa maana ya
kwamba mnunuzi na muuzaji walikubaliana kutumika kwa bei hiyo. Twende tukaangalie
kichwa hiki katika tovuti yetu hii hii ya babypips.com kinachosema;

How to Read a Forex Quote


Kwa kawaida sarafu zinakuwa “quoted” katika jozi kwa mfano GBP/USD au USD/JPY usiache
kukumbuka kwamba huwa katika jozi ili kukamilisha kitendo chetu cha biashara ambacho ni
kununua na kuuza ambapo tumesema katika biashara yetu hii ya forex vitendo hivyo
vinaenda kwa sambamba (simultaneously).
31
31
Tuangalie jinsi ya kuisoma hiyo forex quote, hapa tutahusianisha uhusika wa kiwango cha
ubadilishaji (exchange rate), twende tukaanze na wakati wa kununua, wakati wa kununua
kiwango cha ubadilishaji kinakuambia ni kiasi gani cha “units” unapaswa kulipa za quote
currency ili kununua unit moja ya base currency.

Katika mfano tuliouona kwenye picha yetu ni kwamba unapaswa kulipa dolla 1.51258 U.S. ili
kununua pound 1 ya Uingereza. Kulisindikiza vizuri hili kwenye ubongo ni kwamba kiwango
cha ubadilishaji kinakuhitaji units ambazo unapaswa kulipa ambazo ni 1.51258 za USD
ambayo ndio quote currency ili kuweza kununua unit moja ya base currency ambayo ni
GBP.

Tuangalie kuuza, kiwango cha ubadilishaji kinakuambia ni “units” ngapi za sarafu ya


upendeleo (quote currency) unapata kwa kuuza “unit” moja ya sarafu ya msingi (base
currency), tukirudi katika mfano wetu itakuwa sawasawa na kusema kwamba utapokea
dolla za U.S. 1.51258 pindi utakapoiuza pound 1 ya Uingereza.

Twende tukaangalie sasa ni jinsi gani tunaweza kutengeneza hela kwenye biashara ya
forex, tutaenda kwenye tovuti ya babypips.com tukikutana na kichwa kinachosema;

How to Make Money Trading Forex


Kama tunavyojua katika soko la forex kazi zetu sisi wafanyabiashara ni mbili kuuza au
kununua sarafu. Jinsi ya ufanyikaji wa biashara katika soko hili si tofauti sana na masoko
mengine kama stock market, hivyo kama umewahi kuhusika na masoko mengine ya kifedha
kama hayo basi hapa itakuwa ni rahisi kwenda napo sawa kwa haraka na wepesi.
Dhamira yetu kuu katika biashara hii ya forex ni kuibadilisha sarafu moja dhidi ya nyingine
huku tukiwa na matumaini kwamba bei itabadilika.

Cha kukiweka akilini hapa ni kwamba ile sarafu utakayoinunua utakuwa unategemea
kuimarika thamani yake kulinganisha na ile uliyoiuza. Twende tukaangalie mfano;

Unanunua 10,000 euros katika jozi ya EUR/USD huku Kiwango cha ubadilishaji kikiwa ni
1.1800 nini maana yake hapa ni kwamba sawasawa na +10000EUR huku upande wa sarafu
ya pili ikiwa -11800 USD, baada ya wiki mbili baadae unaamua kuibadilisha 10,000 euros
irudi katika dola katika kiwango cha ubadilishaji cha sasa ambacho ni 1.2500 (kwa lugha
rahisi unaiuza tena euro yako uliyoinunua katika kiwango cha 1.1800 sasa unaiuza katika
32
32
kiwango kipya cha 1.2500). Itakuwa sawasawa na -10,000EUR huku dola ikiwa +12500 USD,
mpaka hapo utakuwa umetengeneza kiasi cha +$700.

Kwa kurahisisha kwa kifupi ni hivi

*EUR 10,000 x 1.18 = US $11,800


** EUR 10,000 x 1.25 = US $12,500.
Nini maana ya kiwango cha ubadilishaji (exchange rate) hapa ni uwiano wa sarafu moja

yenye thamani dhidi ya sarafu nyingine. Tukazie hapa zaidi Mfano USD/CHF kiwango cha

ubadilishaji huonesha franc ngapi fedha za Uswisi unazohitaji kununua dolla moja ya U.S.

Tuangalie kitu kingine, tumekwisha ona katika sura zilizotangulia kwamba pale utakapoamua
kununua “Buy” basi utakuwa na matumaini ya kwamba bei itaongezeka kutoka ilipo sasa, na
pale utakapoamua kuuza “Sell” basi utakuwa na matumaini ya bei kushuka chini au
kuporomoka kutoka pale ilipo sasa. Sasa ni muda gani huo utakaokuwa unaamua kufanya
hivyo? Au utaenda kwa kukisia tu kuwa sasa bei inaenda kupanda au sasa bei inaenda
kushuka, twende tukakiangalie kichwa kinachosema;

Know When to Buy or Sell a Currency Pair


Kwa hiyo hatufanyi maamuzi kwa kukisia, iko hivi, tuanzie hapa kama tulivyosema katika jozi
ya sarafu yoyote unayoijua, pale tutakapokuwa tunaamua kununua au kuuza basi
inayohusika hapo ni base currency, kwa hiyo huyo base currency ndio pekee anaetuambia
kuwa tununue au tuuze? Vipi uhusika wa quote currency kukuambia nunua au uza sasa?
twende tukaaangalie hapa.

Tutaenda kwa mifano, tuchukulie mfano tuna jozi yetu hii EUR/USD, katika jozi yetu hii ni
kwamba euro ndio sarafu ya msingi “base currency” kwa kununua/kuuza. Kama unaamini
kwamba uchumi wa marekani utaendelea kudhohofika, kitu ambacho ni kibaya kwa dolla ya
marekani basi utafanya uamuzi wa kununua “BUY” EUR / USD. Kwa kufanya hivyo utakuwa
umenunua euro kwa matarajio ya kwamba itaendelea kuwa imara kithamani kulinganisha
na dolla ya kimarekani.

33
33
Kumbe ni nani hapo aliyekuambia kuwa sasa nunua ni huyo quote currency ambae ni USD
katika mfano wetu huo, twende tukaangalie muda ambao tutaamua kuweka “Sell”. kama
unaamini kwamba uchumi wa Marekani uko imara hivyo kwa namna yoyote ile Euro
itadhoofu dhidi ya dolla ya kimarekani basi utakuwa ni muda wa wewe kufanya maamuzi ya
kuuza “SELL” EUR / USD. Kwa kufanya hivyo utakuwa umeuza Euro kwa kutegemea kwamba
itaporomoka kulinganisha na dolla ya marekani.

Kwa hiyo kwa asilimia kubwa quote currency ndio inayotuambia sasa nunua au uza, hivyo
hatuendi kwa kukisia ni baada ya kuona quote currency je itaendelea kudhoofu au itaenda
kuimarika lakini kujua yote hayo kwamba itaenda kudhoofu au kuimarika ni baada ya wewe
mfanyabiashara kufwatilia taarifa mbalimbali za kiuchumi za nchi mbalimbali hususani nchi
ambazo sarafu zake tunazitumia katika biashara hii ya forex, biashara hii inakuhitaji uwe
unaenda na muda na matukio pia (updated).

Twende tukaangalie kitu kingine hapa, tuliweza kuangalia maana ya istilahi hizi
PIP, LOTS AND LEVERAGE katika sura ya kwanza, kama tulivyosema kuwa tutazirudia kwa
kuziangalia tena kwa kina ikiwa ni pamoja na kuangalia uhusiano wake, twende tukaanze na
maana zake kwanza, bado tutabakia katika tovuti yetu ya babypips.com

Tuanze na PIP.

Tunakazia zaidi hapa ili uweze kuelewa na si kukremu ni vitu vidogo ambavyo vina umuhimu
mkubwa kwa wewe mfanyabiashara kujua na usije ukafikiria kuanza kufanya biashara hii ya
forex mpaka pale tu utakapokuwa na uelewa mpana na wa kutosha juu ya hiki kinachoitwa
Pip ambapo kwa hicho utaweza kujua kukokotoa faida na hasara.

Tuliangalia maana yake katika sura ya kwanza labda tu kwa kukazia vizuri akilini tuweke
mfano huu kama jozi hii ya sarafu EUR/USD itajongea kutoka 1.1050 kwenda 1.1051,
itakuwa ni sawasawa na .0001 USD, Ongezeko la thamani ambalo ni ONE PIP.

34
34
(Kama ambavyo utakuwa unajionea katika picha hiyo juu.)

Kama tujuavyo kwamba Pip ndio kiwango cha mwisho cha desimali tunachokizingatia zaidi
katika “quotation” ambapo tulisema kwa jozi nyingi za sarafu ni katika kiwango cha mwisho
cha desimali ambacho ni cha nne, isipokuwa kwa zile jozi zinazohusisha sarafu ya kijapani
(Japan yen “JPY”), lakini cha nyongeza hapa ni kwamba baadhi ya mawakala wana quote
mpaka katika kiwango cha tano kwa jozi zisizo husisha sarafu ya Kijapani na kiwango cha
tatu cha desimali kwa jozi zinazohusisha sarafu ya Kijapani.

Kiwango hicho tunakiita PIPETTE kwa wale wana kemia wasije wakafikiri ni kile kifaa cha
maabara hapana, lakini pia unaweza kuita FRACTIONAL PIP. Tuangalie mfano, kama
GBP/USD itajongea kutoka 1.30542 kwenda 1.30543, ambayo itakuwa sawasawa na .00001
USD thamani iliyoongezeka itakuwa ni ONE PIPETTE.

35
35
(Kama ambavyo unaweza kuona hapo juu kwenye picha.)

Twende tukaiangalie LOT, tuliweza kuangalia maana yake katika sura ya kwanza
tulipokuwa tukiangalia istilahi mbalimbali za forex na tukasema standard Lot ni 100,000
units za sarafu, lakini pia tuliongezea kwa kusema hiyo ni Lot ambayo ni standard hivyo
kutakuwepo na Lot nyingine zaidi ya hapo na chini ya hapo. Muhimu sana ni zilizo chini ya
standard twende tukaziangalie.

Kama unavyòweza kuona katika picha hapo juu ni kwamba siyo tu tuna standard Lot pekee
bali pia tuna MINI, MICRO na NANO, ambazo umeweza kuona na namba za units zake kwa
kila moja. Kama ambavyo unajua kuwa, mabadiliko ya thamani ya sarafu kuhusiana na
sarafu nyingine yanapimwa katika "pips," ambayo ni asilimia ndogo sana ya uniti ya thamani
ya sarafu.

Sasa ili uweze kuona faida angalau inakubidi utumie kiasi kikubwa cha fedha kwa mfano ili
angalau uione thamani ya badiliko la kutoka 0.0001 kwenda 0.0002 basi inatakiwa angalau
uwe na $100,000 ambapo badiliko hilo litakuwa na thamani ya 10 na ndio maana ikawepo

36
36
hiyo Lot na tunapata kiburi cha kuitumia hiyo lot kwa sababu ya uwepo wa Leverage
kwamba pamoja na kwamba akaunti ya mfanyabiashara kuwa ina $100 lakini kwasababu
broker wake anatoa hadi Leverage ya 1:1000 ina maana kwa hiyo $100 kwenye akaunti yake
ana uwezo wa kushikilia position yenye thamani ya $100,000, kwa maneno marahisi
anaweza kufanya biashara yenye ujazo wa $100,000.

Leverage nayoTutaenda kuiangalia vizuri tuendele kidogo na Lot, Hebu tuchukulie kwamba
tutaenda kutumia Lot size ya 100,000 (ambayo tunaifahamu kuwa ndio standard lot, Sasa
hebu tukakokotoe mifano kadhaa ili kuona jinsi hiyo Lot inavyoathiri thamani ya pip.

1. USD/JPY katika kiwango cha ubadilishaji (exchange rate) cha 119.80:

(.01 / 119.80) x 100,000 =

$8.34 per pip.

Mfano wa pili.

2. USD/CHF katika kiwango cha ubadilishaji (exchange rate) cha

1.4555:

(.0001 / 1.4555) x 100,000 =

$6.87 per pip.

Twende tukaangalie mfano ambao unahusisha jozi ya sarafu ambayo USD siyo base
currency.

1. EUR/USD katika kiwango cha ubadilishaji (exchange rate) cha 1.1930:

37
37
(.0001 / 1.1930) X 100,000 = 8.38 x 1.1930 = $9.99734 rounded up will be

$10 per pip

Mfano wa pili

2 GBP/USD katika kiwango cha ubadilishaji (exchange rate) cha 1.8040:

(.0001 / 1.8040) x 100,000 = 5.54 x 1.8040 = 9.99416

rounded up will be

$10 per pip.

Tukamalizie na Leverage, tuliweza kuangalia kwa muhtasari tu katika sura ya


kwanza, twende tukakazie maarifa hapa.

Tuliweza kuangalia maana yake, tuendelee kwa kusema kwamba kiasi cha Leverage
utakachotumia kitategemeana na wakala wako, mawakala hutofautiana viwango vya
mwisho vya Leverage wanavyotoa, hivyo wewe utakuwa huru kuchagua kiwango kipi
utakachojisikia nacho vizuri kwa mfano kama ni 1:50 au 1:100 au 1:1000.

Kitu cha kuzingatia ni kwamba huyu broker siyo kwamba tu atakuazima hiyo hela bila hata
kuweka chochote kwenye account yako hapana, pale utakapokuwa umeweka amana

ya biashara (trade deposit) ambayo hujulikana pia kama account margin au initial margin.
Hivyo mara baada tu baada ya kuweka (deposit) hela kwenye akaunti yako tayari utakuwa
na uwezo wa kuanza kufanya biashara.

Twende sasa tukaangalie uhusiano uliopo kati ya PIP, LOT na LEVERAGE.

kwasasa tutaenda kuangalia katika kitabu cha LET’S GET TO KNOW FOREX ambapo
tutaenda kukutana na kichwa kinachoitwa;

SO HOW DO PIPS, LOTS AND LEVERAGE WORK TOGETHER?

Hebu tuchukulie kwamba umenunua 10,000 EUR/USD katika leverage ya 50:1, mpaka hapo
nafikiri utakuwa umeelewa kuwa kiwango cha $200 kwenye akaunti yako kitahusika ili

38
38
kuweza kufanya biashara yenye ujazo wa 10,000 kwa leverage ya 50:1. Twendelee, sasa
tuchukulie ununuzi ulifanyika bei ikiwa 1.3000 kisha ukaja kufunga biashara yako kwa kuuza
katika bei ya 1.3020. Hii inamaanisha utakuwa umepata pips 20.

Mahesabu yatakuwa hivi;

0.0001 X US$10,000 = US$1 thamani ya pip moja

Hivyo kwa hizo pips zako 20 ulizozipata kwenye biashara hiyo, utakuwa umejipatia kiasi cha
US$20.

Pointi ya msingi kwako wewe mfanyabiashara ni kwamba Sio pips zote utakazopata zitakuwa
na thamani ya $ 1. Thamani ya pip inategemea mambo haya matatu, la kwanza kiwango cha
lot unachotumia katika biashara yako (Lot size), la pili jozi ya sarafu unayoifanyia biashara
(currency pair) na la tatu na mwisho ni aina ya sarafu iliyo katika akaunti yako kama ni dola
au euro ama japan yen.

Kwa kumalizia kwenye mfano wetu hapo juu ni kwamba tumetumia lot size ya 10,000
ambayo ni MINI Lot. Na kingine kukurahisishia ni kwamba usije ukashtuka pale utakapoona
unaandikiwa Lot 1 au 0.1 ni kwamba kwa standard Lot ambayo ni 100,000 ni sawasawa na
Lot 1 hivyo MINI Lot itakuwa 0.1 huku MICRO Lot ikiwa ni 0.001 na NANO Lot ikiwa ni
0.0001.

Ikiwa ni pamoja na kuwa na uwezo wa kukokotoa mwenyewe kupata thamani ya pip, kizuri
zaidi ni kwamba umerahisishiwa sana kwa kuwa unaweza kutumia kikokotozi cha pip (Pip
calculator), lakini pia kwa kurahisisha zaidi baadhi ya majukwaa ya biashara “platform”
wanakokotoa “automatic” na kuipeleka kwenye aina ya sarafu unayoifanyia biashara.

Twende sasa tukaangalie mfano mwingine ambao tutaenda kutumia 1 Lot ambayo ndio
standard Lot huku tukitumia leverage yetu ile ile ya 50:1. Tizama picha hii chini;

39
39
‘’Kama tunavyoona kwenye picha hapo juu ni kwamba Pip moja itakuwa na thamani ya $10’’

Jambo la kukumbuka hapo ni kwamba tumeangalia katika uelekeo mmoja hiyo mifano
kwamba umenunua na kweli bei imeenda upande wako na kisha ukapata faida, usijisahaulishe
kwamba kama bei itaenda tofauti kwa hizo Pips hapo juu basi ungekuwa umepata hasara hiyo.
Hivyo ndivyo tunavyopata faida au hasara katika biashara yetu ya forex.

Turudi kwenye tovuti yetu ya babypips.com twende tukaangalie aina za ORDER


hatumaanishi order ya chakula hapana ni orders ambazo tunaweza tukaziagiza katika soko la
40
40
forex, ambazo zitahusu jinsi gani utaweza kuingia au kutoka nje ya biashara hapa tutaenda
kukutana na kichwa kinachosema;

TYPES OF FOREX ORDERS

Kitu cha kwanza cha kuzingatia hapa ni kwamba hakikisha kuwa unajua aina gani za orders
ambazo broker wako anazikubali. Kama unavyojua Brokers wako tofauti na pia hutofautiana
pia kuzikubali/kuzipokea aina za orders za forex. Lakini kuna zile aina-msingi ambazo karibia
kila broker anazipokea twende tukaziangalie hizo na tutatumia mifano zaidi ili kurahisisha
uelewa.

Market Order
Waweza kuiita market Execution, hii ni order inayokuwezesha kununua au kuuza kwa bei
iliyopo.

Kwa mfano, bid price kwa jozi ya EUR/USD kwasasa iko katika 1.2140 na ask price ikiwa
katika 1.2142. Ikiwa unataka kununua EUR / USD kwenye soko, basi ingeweza kuuzwa kwako
katika ask price ya 1.2142. Ni kwamba kubofya kwako kununua basi jukwaa lako la biashara
(trading platform) linaenda kutekeleza papo hapo order ya kununua kwa bei hiyo.

Order ya pili Limit entry order.


Hii ni order iliyowekwa kwamba unaweza kununua chini ya bei ya soko iliyopo au kuuza juu
ya soko iliyopo kwa bei fulani. Kama tunavyoweza kuona order hii inahusisha pande mbili
ambazo ni kuuza na kununua, lakini hizi ni pande mbili ambazo kila moja inajitegea ambapo
zinaitwa Buy Limit na Sell limit hebu tuangalie maelezo ya picha haya hapa chini;

41
41
Ngoja tupate maelezo ya moja kwa moja, Buy Limit, tukiangalia hapo kwenye picha yetu juu
ni kwamba hiyo doti kubwa ya rangi ya blue ndiyo alama ya bei ya soko kwa sasa hivyo
nikitaka kuweka Buy limit order nitaweka chini ya bei hiyo ya sasa ambapo kwenye picha
yetu hapo utaweza kuona mstari wenye alama ya kijani chini ya hiyo doti ya blue ambayo
ndo bei ya sasa.

Tupate maelezo ya Sell Limit, kama unavyoweza kuona katika picha yetu juu ni kwamba hiyo
doti ya blue ndio bei ya soko ya sasa nikitaka kuweka Sell Limit order nitaweka juu ya bei
hiyo ya sasa ambapo kwenye picha yetu hapo utaweza kuona mstari wenye alama
nyekundu. Tuangalie mfano kwa tarakimu.

EUR/USD bei ya sasa iko katika 1.2050. Unataka kuja kuuza bei ikifikia 1.2070. Hapo ndipo
utakapoenda kuseti Sell Limit order kisha ukaendelea na misele yako mingine pindi tu bei
itakapofikia 1.2070, jukwaa la biashara yako litafanya moja kwa moja utaratibu wa kuuza
katika bei hiyo ya 1.2070.

Order ya tatu Stop Entry Order.


Hii ni order iliyowekwa kwamba unaweza kununua kwa bei ambayo iko juu ya bei ya soko ya
sasa au kuuza chini ya bei ya soko ya sasa kwa bei fulani. Kama unavyoweza kuona hapo

42
42
kuna pande mbili hapo ambazo ni kununua na kuuza, twende tukapate msaada wa maelezo
ya picha kidogo.

Tuanze na moja moja hapa pia, tuangalie Buy Stop kama kawaida kirungu cha blue
kinaonesha bei ya soko ya sasa, ambapo ukiweka Buy Stop ni kwamba bei ya soko
itakapopanda mpaka kufikia bei fulani ambapo kwenye picha yetu hapo juu umechorewa
mstari wa kijani bei ikifika hapo jukwaa la biashara litafanya utaratibu wa kununua katika
bei niliyokuwa umeiweka.

Tuje Sell Stop kama kawaida kirungu/kidoti cha blue kinaonesha bei ya soko ya sasa kwamba
sasa bei itakaposhuka kufikia kiwango fulani kama kwenye picha yetu hapo juu
inavyoonesha mstari wa rangi nyekundu basi jukwaa la biashara litakuwa moja kwa moja
linafanya utaratibu wa kuuza katika bei niliyokuwa nimeiweka.

Twende tukaangalie order ya mwisho na muhimu san kwako mfanyabiashara kuijua na


kuizingatia hii hapa;

43
43
Stop Loss order.
Hii ni aina ya order inayohusishwa na biashara kwa madhumuni ya kuzuia hasara ya ziada au
hasara iliyopitiliza ikiwa bei itakwenda kinyume na matarajio yako. Order ya Stop Loss
inabaki ikifanya kazi mpaka pale utakapoamua kufunga biashara yako au mpaka pale
utakapoamua kuiondoa Stop Loss yenyewe. Kitu cha kukiweka akilini hapa ni kwamba Stop
loss ni ya muhimu sana kuiweka kwa kila biashara utakayokuwa unaifungua.

SURA YA TATU

Kwa mfanyabiashra makini hupaswi kufanya hii biashara bila kujijua kwamba wewe
ni aina gani ya mfanyabiashara, usiingie tu katika biashara ilimradi, turudi kwenye tovuti yetu
ya babypips.com tukaangalie aina za wafanyabiashara wa forex kisha ujichagulie aina
itakayoendana nawewe, tutakutana na kichwa kinachosema;

Which Type of Trader Are You?


Kutofautiana kwa haiba zetu kunapelekea pia kutofautiana katika namna ya
ufanyaji wa biashara, hatuwezi kufanana, kuna wengine hupendelea kuchukua vijifaida
vidogo vidogo muda wote wakati wengine hawajali kupoteza kidogo ili kuja kupata faida
kubwa pale watakapokuwa wameshinda. Kujaribu kulazimisha aina fulani ya ufanyaji
biashara ambayo hauendani na haiba yako itapelekea tu kuchanganyikiwa na kujikuta
hukipati kile ulichokitarajia, ikiwa ni kushindwa kutengeneza faida za kudumu (consistent

profits).
Twende tukaangalie hizo aina tukaanze na ya kwanza ambayo ni:

Scalping.

Ni aina ya ufanyaji biashara inayohusisha sekunde kadhaa hadi dakika kadhaa kwa
mfanyabiashara kuweza kufungua na kufunga biashara yake. Lengo kuu la hawa Scalpers ni
kunyakua kiasi kidogo cha pips kadri wawezavyo katika muda wote ambapo soko linakuwa
busy katika hiyo siku. Kwa wastani hulenga 5 to 10 pips kwa kila biashara wanayoifungua. Cha

44
44
kukuongezea hapa kwa faida yako binafsi ni kwamba chati zinazotumika hapa ni ya 1M na 5M
time frame katika jukwaa lako la biashara (platform) yako.

Hapa panamuhitaji mtu anae “focus” kwa kina na umakini na pia yuko chapu kufikiria
“anafikiria kwa haraka” katika kulisoma soko, aina hii si kwa wale wanaofikiria kutengeneza
kiasi kikubwa sana katika trade moja hapana bali wale ambao mwisho wa siku zile faida
ndogo ndogo walizokuwa wanazichukua jumla yake ndo ije iwe ni faida kubwa.

Sifa za kuwa Scalper.

 Siyo mtu wa subira ni mtu usieweza kusubiri biashara zinazochukua muda mrefu.

 Ni mtu ambae una uwezo wa kufikiri haraka na kuweza kubadili maamuzi na uelekeo
haraka

 Hupendi kutumia muda mrefu wa masaa katika kuzisoma chati, muda huo huna au
unakereka kufanya hivyo.

Hupaswi kuwa Scalper endapo kama una sifa zifuatazo;

 Unapendelea kutumia muda wa kutosha katika kulichambua soko kwa ujumla ili
kupata taswira ya soko.

 Unapendelea kuchukua biashara chache ambazo zinalenga kupata faida kubwa


kidogo

 Unachanganyikiwa pale biashara inapokuwa na mazingira ya mijongeo ya haraka


hivyo hukufanya ushindwe kutoa maamuzi sahihi na kujikuta unapata msongo tu.

Baadhi ya vitu vya muhimu vya kuzingatia unapotaka kuwa Scalper.


Cha kwanza, zifanyie biashara zile jozi zenye ujazo mkubwa, kichwa
kinachozungumzia hapa kinasema (Trade only the most liquid pairs). Jozi zenyewe ni kama
vile EUR/USD, GBP/USD, USD/CHF, and USD/JPY ni nini kinachotokea kwenye Jozi hizi ni
kwamba zinakuwa na ujazo wa kibiashara mkubwa sana hupelekea kuwa na spreads zisizoachana

45
45
sana (tighter spreads). Hivyo utahitaji tighter spreads kwasababu utakuwa ukifungua biashara
kila mara.
Cha pili, fungua biashara zako pale tu soko linapokuwa “busy” katika siku husika,
tulishaangalia hapa kwamba soko linapokuwa busy tunamaanisha nini na ni katika session
gani hasa soko ndo huwa busy zaidi. Labda cha kukukumbusha ili kikukae vizuri kichwani ni
hiki kwamba mara nyingi soko linakuwa busy pale sessions zinapopandana (sessions
overlapping) tulilielezea hili kwa hiyo inakupasa ukumbuke na majira kabisa kuwa inakuwa
saa ngapi ambapo ni kutoka saa 8:00 alfajiri hadi 10:00 alfajiri na kutoka saa 2:00 asubuhi
hadi saa 6:00 mchana majira ya Mashariki (EST).
Cha tatu, Jaribu kuizingatia jozi moja kwanza, Scalping inahitaji umakini sana hivyo
kama utaamua kuwekeza nguvu yako katika jozi moja, utakuwa na nafasi nzuri ya
kufanikiwa. Kujaribu kukukuruka na jozi nyingi nyingi kwa wakati mmoja utakuwa unajiua.

Cha nne, Hakikisha unakuwa na usimamizi mzuri wa fedha zako na unaufwata, hili
linazihusu aina zote za biashara, hapa tunasisitiza zaidi kwa kuwa unafanya biashara nyingi
sana ndani ya siku moja hivyo ni muhimu sana kuwa unajikita kwenye usimamizi mzuri wa
fedha zako ili kuepusha hatari.

Aina ya pili ya ufanyaji biashara ni Day Trading, twende tukaiangalie;

Day Trading ni mtindo mwingine wa biashara mfupi, lakini tofauti na scalping, ni kwamba
hapa wewe unachukua biashara moja inayoweza kushikiliwa kwa siku nzima kwa maana ya
kwamba unakuja kuifunga hiyo biashara wakati siku imekwisha. Wafanyabiashara wa hapa
hufanya maamuzi yao pale siku inapoanza, kulingana na matakwa au mategemeo yao, na
kisha huimalizia siku kwa kufunga mahesabu ambayo yanaweza kuwa ni faida au hasara.

Day Trading inafaa kwa wafanyabiashara wa forex ambao wana muda wa kutosha katika
siku ilikuweza kuichambua, kuitekeleza na kufuatilia mwenendo wa biashara.

Sifa za kuwa Day trader.

• Unapendelea kuanza na kumaliza biashara yako ndani ya siku, ukifanya chini ya siku
unaona kama utafanya maamuzi ya kukurupuka huku pia unaona ukifanya zaidi ya
siku unaona utaanza vizuri lakini baadae unaweza kuharibu.

46
46
• Unao muda wa kutosha wa wewe kuweza kuchambua masoko pale siku inapoanza
na ukawa unaifwatilia na kuangalia mwenendo wa biashara yako kwa siku nzima.
• Unapenda kujua matokeo ya biashara yako ikiwa unashinda au kupoteza mwishoni
mwa siku, matokeo yanayokuonesha kuwa kutwa nzima ya leo umevuna nini je ni
faida au hasara.

Hupaswi kuwa Day trader endapo una sifa zifuatazo.

• Unapenda biashara ya muda mfup sana au mrefu sana, yaani unapendelea kupata
matokeo ya papo kwa papo hauna uvumilivu wa kusubiri, au unapendelea biashara
ya masafa marefu siku moja unaona haitoshi unaona angalau siku tatu au nne.
• Huna muda wa kuchambua masoko na kuangalia mwenendo wa biashara kwa siku
nzima kwa siku husika.

• Una kazi nyingine ya kutwa, muhimu hapa unaweza ukawa ni mwajiriwa hivyo kutwa
nzima uko kazini hivyo aina hii haitakufaa.

Baadhi ya vitu vya muhimu vya kuzingatia unapotaka kuwa Day Trader.
Cha kwanza Uwe na habari au taarifa juu ya matukio ya hivi karibuni ya kukusaidia
kuchagua mwelekeo wa biashara kwa siku hiyo. Utahitajika kujiweka mjuvi (updated)
kwenye habari za hivi karibuni za kiuchumi ili uweze kufanya maamuzi yako ya biashara pale
siku inapoanza.

Cha pili, do you have time to monitor your trade? Ikiwa una kazi unayoifanya kutwa
nzima, fikiria ni jinsi gani utaweza kusimamia muda wako kati ya kazi yako na biashara.
Kimsingi ... usije ukafukuzwa kazi yako kwa sababu tu muda wote unatazama chati zako!

Day Trading ina aina zake twende tukaziangalie.


Ya kwanza;

Trend Trading;
Ikoje hii ni pale unapotazama chati ya muda mrefu (angalau chati ya 4hrs) ili
kutambua mwenendo wa jumla wa biashara. Mara tu utakapoutambua mwenendo wa
jumla wa biashara yako, hamia kwenye chati ya muda mfupi na kuangalia fursa za biashara

47
47
kwa kufuata uelekeo wa mwenendo huo. Kwa Kutumia viashiria (indicators) katika chati ya
muda mfupi, vitakusaidia kukupa pointi ya sehemu gani nzuri ya wewe kufungua biashara au
kuingia katika soko.

Tuangalie Chati ya masaa manne hii hapa chini.

(kama unavyoweza kuona kwenye picha yetu ni kwamba mwenendo wa biashara kiujumla ni
wa kwenda chini, hivyo twende tuhamie kwenye chati ya muda mfupi (angalau dk 15) ili
tuweze kupata pointi nzuri ya sisi kuingilia katika soko, au pointi nzuri ya kuweza kufungua
biashara. Twende tukaiangalie chati ya dk 15 ikituonesha pointi ya kuingilia.)

48
48
(Utaweza kuona hapo kwamba huo mfano kwenye chati yetu mshale unaonesha
kuwa ulipaswa kufungua biashara kwa kuuza (getting short)).

Aina ya pili counter trend trading


Ikoje hii ni hivi ni sawa na trend trading isipokuwa unapotambua mwenendo wa jumla wa
biashara, unaanza kuiangalia biashara katika mwelekeo tofauti na huo unaouona kwa muda
huo. Pointi hapa ni kung’amua mwisho wa mwenendo huo uliokuta na kuingia mapema
katika uelekeo tofauti ambapo unatarajia kuwa punde tu mwenendo huo ulioukuta
utageuka. Hii ni hatari kidogo lakini inaweza kuwa na faida nzuri na kubwa.

Tuangalie chati hii hapa chini

49
49
(Katika mfano huu, tunaona kwamba tulikuwa na mwenendo wa kuelekea chini (downtrend)
ya muda mrefu na yenye uchovu kwenye chati ya masaa manne 4hrs. Hii inatupa dalili ya
kwamba soko linaweza kuwa tayari kwa kubadili uelekeo au mwenendo wake.)

Kwa kuwa mawazo yetu ni countertrend "mwenendo mbadala", tutaangalia biashara katika
uelekeo kinyume na mwenendo uliopo wa jumla kwa kutumia
chati ya dakika 15. Tuiangalie hapa chini;

50
50
(Kumbuka kwamba kwenda kinyume na mwenendo ni hatari sana, lakini ikiwa
umepatia kwa usahihi, inaweza kuwa na faida kubwa).

Tuangalie Aina ya tatu na ya mwisho ya Day Trading ambayo inaitwa;


Breakout Day Trading.

Hii ikoje ni hivi, ni pale unaitazama mifikio ambayo jozi fulani ya sarafu imeifanya kwa muda
wa masaa kadhaa yaliyopita, kisha unaamua kuweka biashara yako upande wowote, ukiwa
na matumaini ya kunyakua biashara itakayovuka mifikio hiyo katika uelekeo wowote.

Tuelezee kidogo hiyo mifikio ni kwamba mwenendo wa biashara unakuwa unacheza katika
eneo fulani hauzidi sana hapo wala haushuki sana hapo, hivyo breakout ni pale ambapo
unategemea mwenendo huo utaweza kupitiliza kutoka na kuuvunja huo mfikio ambao
ulikuwa kama ukinzani, na hapa ndipo ukuta wa juu tunauiita Resistance level na ule wa
chini unaitwa support level na hilo eneo huwa linajitengeneza kwa muda fulani kabla ya
kuvunjwa kisha kuzaliwa pengine tena.

Hii inakuwa na ufanisi sana pale mifikio ya jozi husika inapokuwa karibu karibu yani
mwenendo wa biashara kwenda juu unakuwa siyo mrefu sana wala kwenda chini haushuki
51
51
sana, ukisha kuona eneo ambapo biashara hufikia katika uelekeo wa juu na chini ujue ni
dalili nzuri ya breakout kwenda kutokea baada ya muda Fulani.

Hapa mfanyabiashara ni kwamba unatakiwa tu kuwa na utayari pale tu mvunjiko


utakapotokea (breakout) uwe tayari kufungua/kuingia katika biashara hiyo na ili kuliweka
hilo sawia unaweza ukaseti order zako chini na juu mbali zaidi na eneo la mifikio ili pale
itakapokuja kwenda katika upande wowote biashara yako inafunguka na utaweza kutega
hivyo kwa kuweka order za kusubiri ambazo tuliweza kuziangalia kwa kukumbusha tu ni hizi
(BUY/SELL STOP/LIMIT).

Aina ya tatu ya ufanyaji biashara inaitwa


Swing Trading;

Ni aina ya ufanyaji biashara inayochukua kipindi kirefu kidogo, na inahitaji uvumilivu


kushikilia biashara yako uliyoifungua kwa siku kadhaa bila kuifunga. Hii ni nzuri kwa wale
ambao hawawezi kufuatilia chati zao kutwa nzima lakini wanaweza kujitolea masaa kadhaa
kuchunguza soko muda wa usiku.

52
52
Huenda hii ikawafaa zaidi wale ambao wana kazi za kutwa nzima wote au wanasoma shule
lakini wana muda wa kutosha wa kuwa wajuvi na kwamba hawaachwi nyuma kwa yale
yanayotokea katika uchumi wa kimataifa.
Aina hii ya ufanyaji biashara hujaribu kuzitambua "swings" ndani ya mwenendo wa muda
fulani wa kati (siyo mrefu sana wala mfupi sana) uliopita na kisha kuamua kuingia au
kufungua biashara pale tu kunapoonekana kuwa na uwezekano mkubwa wa nafasi ya
kushinda.
Hivyo kuingia katika soko au kufungua kwako biashara kutajikita katika hizo swings kwamba
sasa nunua au uza, twende tukaziangalie hizo swings ni zipi.

Kama unavyoona katika chati yetu hapo utaweza kuziona hizo Swings ambapo kuna Swing High
na Swing Lows. Kwenye Swing high ina maana utauza “SELL” na kwenye Swing lows utanunua
“BUY”.

53
53
Twende sasa tukaangalia sifa za kuwa Swing trader.
 Pamoja na sifa nyingi hapa lakini kubwa kabisa unafaa sana hapa ikiwa wewe ni mtu
wa subira, mvumilivu na mstahimilivu.
 Una uwezo wa kubaki na utulivu wakati biashara inaenda kinyume nawewe. katika
kipindi chote hiki cha kuishikilia biashara kwa siku hizo kadhaa hivyo kuna
uwezekano mkubwa wa kuona biashara inaenda kinyume nawewe katika vipindi
vifupi vidogo vidogo ukiwa bado unausubiria muda wako ule ulioulenga ufike.
 Nini unapaswa kufanya hapo na ni muhimu kuweza kuwa na utulivu katika kipindi
hicho na pia uwe na imani katika uchambuzi wako uliokupelekea kufungua biashara
hiyo.

Ukiwa na sifa hizi basi Swing Trading haitakufaa;

 Ni mtu usiye na subira huwa unafurukutwa kutaka kujua kama uko sahihi au Laah!
 Jasho linakuporomoka pale unapouona mwenendo wa biashara unaenda kinyume
nawewe, na unakuwa mtu wa wasiwasi kupita maelezo basi aina hii haikufai kabisa.
 Hauwezi kutumia muda wa kutosha katika kulichambua soko, ni mtu uliyekosa
utulivu na ufwatiliaji hata pale unapokuwa umepata muda.
Twende tukaangalie aina ya nne ya ufanyaji biashara inayoitwa

Position Trading.
Ni biashara inayochukua kipindi kirefu zaidi na inaweza kuwa ni biashara ambayo ikadumu
kwa miezi kadhaa hadi miaka kadhaa. Aina hii ya biashara ya forex ni mahususi kwa
wafanyabiashara wenye uvumilivu uliopitiliza, na inahitaji ufahamu mzuri wa misingi ya
visababishi (fundamentals).

Kwa sababu biashara ya aina hii inafanyika kwa muda mrefu, kuegemea katika
fundamentals itakuwa ndio kitu cha msingi kuzingatia wakati wa kuchambua masoko. Na
kuifanya aina hii lazima uhakikishe kuwa una mtaji mzuri la sivyo kuna uwezekano mkubwa
wa kupata margin call.

54
54
Katika kipindi chote cha kuishikilia biashara yako Unaweza kupata swings kubwa kubwa na
lazima uwe na utayari na uwe na utulivu mzuri kwa wakati huo huku ukiamini katika
uchambuzi wako.
Twende tukaangalie sifa za kuwa
Position Trader.

Uweze kujitegemea kimawazo. Uweze kupuuza maoni ya watu wengi na kusimamia


maamuzi yako mwenyewe kuhusu mahali ambako soko litaenda.

Hakikisha una ufahamu mkubwa juu ya fundamentals, na una jicho zuri katika kuona jinsi
gani hizo fundamentals zitakavyoathiri jozi yako ya fedha kwa muda mrefu.

Hakikisha una mtaji wa kutosha kuhimili pips mia kadhaa ikiwa soko litakwenda kinyume na
wewe. Na pia uwe ni mtulivu na mvumilivu usiyeingia na kimuhemuhe cha kutaka kuisitisha
biashara yako pale utakapoona umevuna 50 pips ukaona zinakutosha na wakati halikuwa
lengo lako ukiona uko hivyo basi jua aina hii siyo ya kwako rudi kwenye swing au aina
zingine za muda mfupi.

Tuangalie sifa ambazo ukiwa nazo ujue aina hii haikufai.

Siyo mtulivu wala mvumilivu, hauna mtaji wa kutosha kuhimili mikikimikiki ya biashara,
unayumbishwa sana na maoni ya watu kila unalolisikia unaliona liko sahihi na kujiona hauko
sahihi, hauna ufahamu mzuri kuhusu fundamentals. Hizo ni sifa kadhaa ambazo ukiwa nazo
basi aina hii ya ufanyaji biashara haikufai.

Katika baadhi ya sehemu katika chapisho hili umeweza kukutana na neno


fundamentals, sasa ni nini maana yake na vipi kama kuna lingine linaloendana na hili katika
forex yetu na linaitwaje? Twende sasa katika kitabu chetu cha LET’S GET TO KNOW FOREX.
Tunaenda kukutana na maneno makuu mawili tuanze na la kwanza ambalo ni kichwa cha
habari kinachosema;

55
55
WHAT IS TECHNICAL ANALYSIS?

Maana yake ni hii, ni utafiti juu ya mijongeo na mitindo inayojirudia katika soko.
Wafanyabiashara wengi wanaitumia hii njia ya Technical Analysis kufuatilia mijongeo ya
sasa na iliyopita ya jozi za sarafu, kusaidia kutambua mwenendo wa soko na kuwaongoza
katika pointi zipi nzuri za kuingia na kutoka katika biashara zao.

Kama tunavyojua wafanyabiashara hatufanani hivyo kuna mamia ya zana na mbinu za


uchambuzi ambapo unaweza kujichagulia unazozitaka kutoka humo. Kati ya hizo kuna hizi
kadhaa ambazo walio wengi hupendelea kuzitumia.

SUPPORT AND RESISTANCE LEVELS.


Hizi ni pointi za bei ambazo soko hugonga mara kwa mara kisha hugeuza mwelekeo wake.
Support level ni pointi ambayo bei hudondokea hapo na haivunji kitako hicho kwa kipindi
fulani ikapitiliza, bali ikigonga hapo hugeuza mwelekeo kuelekea juu tena na kudumu kwa
muda Fulani unaoweza kuwa mrefu au mfupi. Resistance level ni pointi ambayo bei ikiwa
katika kuongezeka kuelekea juu hugonga na kubadili mwelekeo pasipo kukivunja kizuizi
hicho kwa kipindi Fulani.

56
56
(Katika mchoro wetu hapo juu unaweza kuona maeneo hayo ambapo sasa pale bei
itakaposhuka mpaka kwenye usawa wa support level hapo ndipo wafanyabiashara wengi
hununua “BUY” wakitegemea bei kubadili uelekeo na kuanza kurudi juu. Vivyo hivyo bei
ikifika kwenye usawa wa Resistance level wengi wa wafanyabiashara huuza “SELL”
wakatarajia bei itageuza mwelekeo na kurudi chini.)

Cha nyongeza hapa kwako wewe mfanyabiashara ni kwamba siyo lazima bei igonge iishie
hapo kisha ibadili mwelekeo inaweza ikavunja kitako hicho au kizuizi hicho na kuendelea na
safari huku wewe ukishindwa kuamini macho yako na ndio maana tumesema kitako ama
kizuizi hicho hudumu kwa muda fulani.

Tuangalie zana ya pili


INDICATORS.

Hizi huonesha mistari ya mwenendo wa soko, inaweza ikawa ni juu ya mijongeo ya soko ya
sasa kwenye chati au ikajitenga katika eneo lake la chini ambalo ni nje na eneo la hizo chati.
Bollinger Bands, Average Directional Index (ADX) and Moving Averages hiyo yote ni
mifano ya Indicators. Hizi Indicators zinaweza zikawa ni Lagging kwa maana ya kwamba
zinachambua mijongeo ya bei iliyopita ya soko, au zikawa ni Leading zikitutabiria uelekeo wa
mjongeo wa bei unaokuja.

57
57
Twende tukaangalie mfano katika picha hapa chini;

Twende tukaiangalie
WHAT IS FUNDAMENTAL ANALYSIS?
Ni utafiti juu ya mijongeo ya biashara inayokuja kama matokeo ya taarifa na habari
mbalimbali. Taarifa au habari au waweza kuita nguvu (forces) huwa ni za kisiasa, kiuchumi
na kijamii maeneo hayo ndiko ambako wafanyabiashara hutega masikio yao huko. Hizo
nguvu huwasaidia katika kutabiri uimara au udhaifu wa sarafu fulani utakaoenda kutokea.

Kama utakuwa na kumbukumbu nzuri toka sura ya kwanza tulipokuwa tukiongelea masoko
mengine ya kifedha kama Oil na Gold, tulisisitiza kupata taarifa zinazohusu masoko hayo na
kwa kuwa tulisema yanauhusiano wa moja kwa moja na dolla basi ni muhimu kupata hizo
taarifa zake na habari zake. Pia tuliangalia kufunguliwa kwa masoko na kwa kwamba
ufwatilie taarifa mbalimbali zitakazokuwa zinalihusu soko husika linaloenda kufunguliowa,
Sasa basi yote tuliyokuwa tunaiongelea hapa ni hiyo fundamental analysis, kwamba pale
58
58
taarifa hizo zitakapokusaidia kubaini uelekeo wa soko na ukafanya hivyo basi utakuwa
umefanya maamuzi yako kutokana na uchambuzi wako ambao upo katika upande wa
fundamentals.

Cha kukuongezea hapo ni kwamba ni taarifa au habari kama zipi? ni kama hizi, mabadiliko ya
kiwango cha riba (interest rate changes) na maamuzi ya serikali (Government decisions)
lakini kumbuka hapa zaidi ni kwa nchi zile ambazo sarafu zake tunazitumia katika biashara
yetu hii hivyo usije ukaanza kukimbizana na maamuzi ya serikali ya Tanzania au malawi
ukadai uko unafanya fundamental analysis.

Wafanyabiashara wageni katika forex wanakuza ujuzi wao juu ya fundamental analysis kwa
kufuata matukio ya habari na matangazo ya kiuchumi yaliyopangwa.

Jambo la msingi sana la kukumbuka hapa ni kutakuwa na wakati ambapo mijongeo ya bei ya
jozi ya sarafu haitaenda kama vile ulivyoamini na ikaenda kinyume na uchambuzi wako wa
fundamental analysis, hapo ndipo tunaposema kuna umuhimu mkubwa wa kuchanganya
Technical Analysis pamoja na Fundamental analysis katika ufanyaji wako biashara ya forex.

59
59
Picha hii hapa chini itakusaidia sana.

WAKALA (BROKER).
Soko la fedha za kigeni linahusisha zaidi ya dolla trillion 4 kwa wastani thamani ya biashara
inayofanyika kila siku, thamani hiyo inalifanya kuwa soko kubwa zaidi la fedha duniani. Kwa
kuwa hakuna kituo maalumu kilichojengwa kwamba hapo ndipo soko la forex lilipo pekee na
kwamba wafanyabiashara wote inabidi wakutane hapo kuifanya, hivyo wafanyabiashara
wanapaswa kuchagua broker wa forex kuwasaidia kufanya shughuli zao za biashara, kwa
kuwa sehemu inakofanyikia hii biashara ni mtandaoni hivyo unaweza kuifanya popote pale
duniani.

Kila kunapokucha Kuna idadi kubwa na inayoongezeka ya mawakala wa forex ulimwenguni


kote, na kumchagua mmoja ambae ni mkweli na wa uhakika inahitaji kuchagua kwa

60
60
uangalifu kwa kufanya uperuzi na utafiti kupitia idadi kubwa ya vyombo vya habari na
mitandao ya kijamii pamoja na kuuliza kutoka kwa wafanyabiashara wengine kwasababu kila
broker mtandaoni hujinadi kuwa yeye ndiye bora kuliko mwingine yeyote, hivyo ni ngumu
kumjua vizuri kwa kumsikiliza broker mwenyewe.

Ni eneo muhimu sana hili kwa mfanyabiashara kulielewa ili kufanya uchaguzi sahihi, kukosea
kuchagua huyu anaeitwa Broker ni sawa na kukosea kuoa mke, ni sawasawa na
kujiangamiza kibiashara, katika toleo hili tutaenda kugusia kitu kimoja kati ya vingi
vinavyomuhusu broker ambacho hupaswi kusahau kwa kila dk inayopita ukiwa kama
mfanyabiashara, mengine mengi yamuhusuyo broker tutaanza nayo katika toleo la pili.

Kwasasa tutaenda kuangalia katika tovuti inayoitwa www.investopedia.com

katika kipengele kinachosema 5 THINGS FOR SELECTING FOREX BROKER, tutaenda


kuiangalia pointi inayosema Commissions and Spreads, pointi hii inazungumzia jinsi gani
huyu wa kuitwa broker anavyotengeneza hela kupitia wewe mteja wake ambae ni
mfanyabiashara hii ya forex.

Broker hutengeneza hela kupitia Commissions na Spreads. Broker anaetumia


Commissions humtoza mfanyabiashara kupitia asilimia fulani za Spread, Ambayo ni tofauti
kati ya Bid Price na Ask price ya jozi fulani ya sarafu. Hata hivyo kuna brokers hujinadi
kuwa hawatozi Commissions (hatari sana hawa) hawa badala yake hutengeneza hela kwa
kupitia ukubwa wa Spreads. Na hapa ndipo pointi ya msingi ilipo, twende tukaangalie
mfano kabisa ili tupaelewe vizuri hapa.

Tuchukulie mfano Spread ni fixed ambazo ni 3 Pips mfano hapa katika jozi ya EUR/USD
katika quote ya 1.3943 - 1.3946 ambapo hapa tunapata 3 Pips. Tuliza akili, hapa pana
maana kwamba pindi huyu mfanyabiashara atakapoamua kufungua biashara yake kwa
kununua “BUY” katika bei hiyo ya 1.3946, “position” yake hiyo itakuwa tayari imekwisha
poteza 3 Pips, hapo ni pale ulipoifungua lakini anachukua tena 3Pips pale utakapoifunga
position yako hivyo kwa hiyo position moja kuifungua na kuifunga atakuwa kachukua pips
zake 6, hivyo kujua wewe umepoteza kiasi gani itategemeana na thamani ya Pip moja uliipa
kiasi gani. Umeona jinsi inavyokuwa? hivyo kama broker wako anatoa Spreads kubwa ni

61
61
hatari kwa afya yako ya biashara. Hivyo huyu broker wako huchukua cha kwake mapema bila
kusubiri kupata kwako au kukosa kwako baadae katika biashara yako hiyo uliyoifungua.

Tuangalie kitu kingine muhimu kabisa kinachoitwa


RISK MANAGEMENT.
Hapa tutarudi katika kitabu cha LET’S GET TO KNOW FOREX ambapo utakutana na
kichwa kinachoitwa: HOW DO I HANDLE RISK? Kuna mambo manne ya kuyaangalia hapa
twende tukaanze na la kwanza.

PROTECT YOUR POSITION WITH STOPS, LIMITS AND OTHER ORDER TYPES.

Kuna order nyingi katika biashara ya forex na tulikwisha kuziangalia lakini kubwa kuliko zote
ya kutusaidia hapa ni Stop orders hii inatusaidia kutambua mapema kiasi gani
tutakachoenda kupoteza endapo mambo yakituendea kombo, hivyo hupaswi kuacha
kuizingatia, katika biashara hii kuna mambo mawili, wageni katika forex wanapofungua
biashara zao hukimbilia kuwaza ni kiasi gani wataenda kukitengeneza huku professional
traders wenyewe huwaza ni kiasi gani kinaweza kupotea/watapoteza endapo soko litaenda
uelekeo tofauti na uliokusudiwa.

SET PROPER LEVELS.

Hapa tuongelee mfano kuwa ndio unataka kuseti hiyo stop loss yako lakini hauna uelewa
mzuri wa wapi uiseti kukurahisishia hapa ni kwamba hakikisha hauiweki karibu sana na
pointi uliyoingilia katika biashara hiyo au pointi uliyofungulia biashara yako, kuiweka kwako
karibu kwa kutaka kupoteza kidogo sana kutapelekea wewe kufungua biashara mara kwa
mara ambako mwisho wa siku utakuja kujikuta umepoteza kiwango kikubwa zaidi. Hivyo
iweke mbali zaidi ikupe uwanja mpana wa kuiacha biashara yako ipumue.

CHECK YOUR EMOTIONS.

Hapa ndipo panapogusa saikolojia ya forex na ndipo eneo lenye asilimia nyingi za wewe
kufanikiwa katika forex, achilia mbali kujua mbinu na kuwa na zana za kila aina lakini
saikolojia ya biashara ndio kila kitu hapa. Angalia picha hii chini mlinganyo wa hizi asilimia;

62
62
Hapo utaweza kujionea ni jinsi gani saikolojia ilivyo na nafasi kubwa katika kufanikiwa
kwako, inatakiwa akili yako iwe na utulivu wa hali ya juu pale unapopoteza usikimbilie
kufungua biashara nyingi nyingi kwa lengo la kulipiza kisasi, huyo utakaekuwa unagombana
nae siyo mtu kwamba ataziogopa hasira zako bali hilo ni soko ambalo halimjui mtu yeyote.

CREATE A TRADING PLAN AND STICK TO IT.

Mikakati na mipango yako juu ya biashara hii inatakiwa iwe thabiti kwani ukiwa na plan
nzuri basi ndio mafanikio yako katika biashara yako hii. Siyo tu itakusaidia kufikia malengo
yako kadhaa bali itakuonyesha ufanyaji wako wa biashara itakuongoza kukijua kiwango gani
ambacho ukikipoteza hakitakuletea mawaa na itakuongoza jinsi ya kujilinda ili usipoteze
zaidi.

63
63
‘’shukrani za pekee ziende kwa wale wote waliohusika kuandaa toleo hili la kwanza, Chini
ya Chief Directors HIZZA ATHUMAN na JONATHAN HIZZA, shukrani za dhati ziende kwa
Logic translator ADAM KHOO kutoka Singapore. Usikose kufwatilia matoleo mengine.

Tutoe Rai kwako wewe unae yasoma haya, popote utakapopata ugumu wowote jisikie
huru kuuliza, kupitia mawasiliano yatakayoongezwa, lingine ni kwa wewe unaehitaji
kufundishwa course ya forex, njoo ufundishwe”

‘’Simama kwa miguu yako mwenyewe katika forex’’

Barua pepe jonathanoscar@yahoo.com


hydrazineazine@gmail.com

Tell:
+255752259931.

+255625934471.

64
64

You might also like