You are on page 1of 6

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA UCHUKUZI
MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA
Simu ya mdomo: 255 22 2460 735/2460 706-8
Nukushi: 255 22 2460 735/700
Barua pepe: met@meteo.go.tz
Tovuti: www.meteo.go.tz

S.L.P. 3056
DAR ES SALAAM

Unapojibu tafadhali nakili:


Kumb. Na.: TMA/1622

4 Septemba, 2014

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


MWELEKEO WA MVUA KWA KIPINDI CHA OKTOBA - DISEMBA 2014 NCHINI
A:
UTANGULIZI
Taarifa hii inatoa tathmini ya mvua za masika
(Machi - Mei) 2014 na mwelekeo wa
mifumo ya hali ya hewa na mvua kwa kipindi
cha mwezi Oktoba hadi Disemba,
2014(Vuli).

Dondoo muhimu Mvua za Vuli OktobaDisemba, 2014


1. Mwelekeo wa mvua kwa kipindi cha Oktoba-Disemba,
2014 Vuli unaonyesha kuwa;

Hali ya mvua inatarajiwa kuwa ya kuridhisha


katika maeneo mengi ya nchi hata hivyo mvua za wastani
hadi chini ya wastani zinatarajiwa katika baadhi ya maeneo
ya kusini mwa nchi hususan mkoa wa Ruvuma.

Msimu huu mvua zinatarajiwa kuanza mapema mwezi


Septemba katika maeneo ya ziwa Viktoria, nyanda za
juu kaskazini mashariki na pwani ya kasikazini
2. Athari na Ushauri

Mvua za kutosha zinatarajiwa kwa shughuli za kilimo


katika maeneo mengi ya nchi.

Vina vya maji katika mito na mabwawa vinatarajiwa


kuongezeka katika maeneo mengi ya nchi.

Maji yatumike kwa uangalifu na kuzingatia taratibu za


uvunaji, uhifadhi na matumizi endelevu ya rasilimali
maji

Matukio ya migogoro inayosababishwa na mifugo,


wanyamapori na shughuli za binadamu na kilimo
hayatarajiwi kujitokeza kwa kiasi kikubwa.

Vipindi vya mvua kubwa vinaweza kuongeza matukio


ya mafuriko na uharibifu wa mali na miundombinu.

Milipuko ya magonjwa yanayosababishwa na kutuama


kwa maji na utiririshaji wa majitaka usiodhibitiwa

inaweza kujitokeza.

Hatua stahiki katika utunzaji wa mazingira, upatikanaji


wa maji safi na salama, na usambazaji wa madawa,
maji na chakula ikiwa ni hatua za kujiandaa na
kukabiliana na majanga yanayoweza kutokea

B:

TATHMINI YA MVUA KIPINDI CHA MACHI MEI, 2014

Katika msimu uliopita wa mvua za Masika Machi hadi Mei, 2014. Maeneo mengi ya nchi yalipata
mvua za wastani hadi juu ya wastani isipokuwa maeneo machache ya mikoa ya Mwanza, Singida
na Dodoma ambayo yalipata mvua za chini ya wastani. Matukio ya vimbunga hususan Kimbunga
Hellen kilichotokea katika Rasi ya Msumbiji kusini magharibi mwa bahar ya Hindi kilisababisha
ongezeko la mvua katika eneo la Pwani ya kaskazini.
Maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka:
Kanda ya Ziwa Victoria: Viwango vya mvua vilivyopimwa katika vituo vya Bukoba na Musoma
vilikuwa juu ya wastani. Kituo cha Shinyanga kilipima mvua kiwango cha wastani wakati katika
kituo cha Mwanza kiwango cha mvua kilikuwa chini ya wastani.
Nyanda za juu kaskazini mashariki: Vituo vya Arusha, Lyamungo na Kilimanjaro vilipima mvua
juu ya wastani ilihali vituo vya Moshi na Same kiwango cha mvua kilikuwa cha wastani.
Pwani ya kaskazini na visiwa vya Unguja na Pemba: Vituo vya Dar es Salaam, Morogoro na
Pemba vilipima mvua za juu ya wastani na vituo vya Zanzibar, Amani, Kizimbani pamoja na Tanga
mvua zilikuwa wastani.
Maeneo yanayopata msimu mmoja wa mvua kwa mwaka:
Nyanda za juu kusini magharibi: Vituo vya Mbeya, Tukuyu, na Mahenge vilipima mvua juu ya
wastani na kituo cha Sumbawanga kiwango cha mvua kilikuwa cha wastani.
Kanda ya magharibi: Mvua juu ya wastani ilipimwa katika kituo cha Kigoma ilihali vituo vya
Kibondo na Tabora mvua zilikuwa ni za wastani.
Pwani ya kusini: Kituo cha Kilwa kilipima mvua juu ya wastani na vituo vya Mtwara pamoja na
Naliendele mvua zilikuwa za wastani.
Kanda ya kati: Vituo vya Singida na Dodoma vilipima mvua chini ya wastani na kituo cha
Hombolo mvua za wastani.
Kanda ya kusini: Kituo cha Songea kiwango cha mvua kilichopimwa kilikuwa juu ya wastani.
C: MIFUMO YA HALI YA HEWA
Katika kipindi cha miezi ya Oktoba hadi Disemba, 2014 hali ya joto la bahari katika maeneo ya
magharibi na kusini -magharibi mwa bahari ya Hindi inatarajiwa kuwa juu ya wastani, upande wa
mashariki mwa bahari ya Hindi hali ya joto la wastani inatarajiwa. Hali hii inatarajiwa kusababisha
upepo wenye unyevunyevu kutoka bahari ya Hindi kuelekea katika eneo la Pwani ya Africa
Mashariki. Aidha, hali ya joto la chini ya wastani katika eneo la mashariki mwa bahari ya Atlantiki
(Pwani ya Angola) inatarajiwa kusababisha ongezeko la hewa yenye unyevunyevu kutoka katika
misitu ya Kongo kuelekea katika maeneo ya magharibi na kusini Magharibi mwa nchi.
Hali ya joto la juu ya wastani katika eneo la Tropikali ya bahari ya Pasifiki linatarajiwa kuendelea
kwa kipindi cha miezi ya Oktoba hadi Disemba, 2014. Hali hiyo inatarajiwa kuchangia ongezeko
la mvua katika baadhi ya maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua. Hali ya joto la juu ya
wastani katika eneo la kusini magharibi mwa Bahari ya Hindi linaashiria kuwepo kwa matukio ya
vimbunga katika msimu wa mvua za Vuli kuanzia mwezi Novemba, 2014.
D:
MWELEKEO WA MVUA OKTOBA - DISEMBA 2014:
Kutokana na mwelekeo wa mifumo ya hali ya hewa inayotarajiwa, mvua za kipindi cha Oktoba
2

hadi Disemba, 2014 zinatarajiwa kuwa kama ifuatavyo:


(i) Mvua za Vuli (kwa maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua)
Msimu wa mvua wa Oktoba hadi Disemba (Vuli) ni mahususi katika maeneo ya nyanda za juu
kaskazini mashariki, pwani ya kaskazini, kanda ya Ziwa Viktoria na kaskazini mwa mkoa wa
Kigoma.
Katika msimu huu mvua zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani katika maeneo ya
pwani ya kaskazini (mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Tanga, kaskazini mwa mkoa wa Morogoro,
pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba), nyanda za juu kaskazini mashariki (mikoa ya
Kilimanjaro, Arusha na Manyara) pamoja na mikoa ya Mwanza, Geita, Simiyu, Shinyanga na
kaskazini mwa mkoa wa Kigoma.
Msimu wa mvua za Vuli unatarajiwa kuanza mwezi Septemba, 2014 katika ukanda wa Ziwa
Viktoria na kusambaa katika maeneo mengine. Hata hivyo, mvua hizo zinatarajiwa kuanza
mapema katika maeneo ya ukanda wa pwani (Mkoa wa Tanga na kisiwa cha Pemba) na katika
baadhi ya maeneo ya nyanda za juu kaskazini Mashariki.
Kanda ya Ziwa Victoria: (Mikoa ya Kagera, Mara, Mwanza, Geita, Simiyu na Shinyanga):
Mvua zinatarajiwa kuanza katika wiki ya kwanza na ya pili ya mwezi Septemba, 2014 katika
mkoa wa Kagera na kaskazini mwa mkoa wa Kigoma na kuendelea kusambaa katika mikoa ya
Mwanza, Geita, Shinyanga, Simiyu na Mara. Mvua hizo zinatarajiwa kuwa za juu ya wastani
katika maeneo ya mikoa ya Kagera, Geita, Mara, Mwanza pamoja na kaskazini mwa mkoa wa
Kigoma. Maeneo mengi ya mkoa wa Shinyanga yanatarajiwa kuwa na mvua za wastani hadi juu
ya wastani.
Ukanda wa Pwani ya Kaskazini: (Mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Pwani, Morogorokaskazini pamoja na Visiwa vya Unguja na Pemba):
Mvua zinatarajiwa kuanza wiki ya kwanza ya mwezi Septemba, 2014 katika maeneo ya mikoa ya
Tanga, Dar es Salaam pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba na kusambaa maeneo ya mkoa wa
Morogoro. Mvua hizi zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani katika maeneo mengi.
Nyanda za juu Kaskazini Mashariki: (Mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara):
Mvua katika maeneo haya zinatarajiwa kuanza wiki ya pili na ya tatu ya mwezi Septemba, 2014
na zinatarajiwa kuwa juu ya wastani katika maeneo mengi ya mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na
kaskazini mwa mkoa wa Manyara. Hata hivyo, kusini mwa mkoa wa Manyara, mvua zinatarajiwa
kuwa za wastani hadi juu ya wastani.
(ii)
Mvua za Msimu (Novemba Aprili) kwa maeneo yanayopata msimu mmoja wa
mvua.
Msimu wa mvua za Novemba hadi Aprili ni mahususi kwa maeneo ya Magharibi mwa nchi,
kanda ya kati, nyanda za juu kusini-magharibi, kusini mwa nchi na pwani ya kusini. Katika kipindi
cha Oktoba hadi Disemba, 2014 maeneo mengi yanatarajiwa kupata mvua za wastani hadi juu ya
wastani.
Kanda ya Magharibi (Mikoa ya Kigoma, Tabora, Katavi na Rukwa):
Mvua zinatarajiwa kuanza wiki ya pili ya mwezi Novemba, 2014. Mvua hizi zinatarajiwa kuwa za
juu ya wastani katika maeneo ya mikoa ya Rukwa, Katavi pamoja na kusini mwa mkoa wa
Kigoma. Hata hivyo, maeneo mengi ya mkoa wa Tabora yanatarajiwa kuwa na mvua za wastani
3

hadi juu ya wastani.


Kanda ya kati (Mikoa ya Singida na Dodoma):
Mvua zinatarajiwa kuanza wiki ya tatu ya mwezi Novemba, 2014 na zinatarajiwa kuwa za wastani
hadi juu ya wastani.
Nyanda za juu Kusini Magharibi: (Mikoa ya Mbeya, Iringa, Njombe na kusini mwa
Morogoro):
Mvua zinatarajiwa kuanza wiki ya kwanza na ya pili ya mwezi Novemba, 2014 na zinatarajiwa
kuwa za wastani hadi juu ya wastani katika maeneo mengi. Maeneo ya magharibi mwa mkoa wa
Mbeya, mvua zinatarajiwa kuwa juu ya wastani.
Maeneo ya kusini na pwani ya kusini (mikoa ya Ruvuma, Lindi na Mtwara)
Mvua zinatarajiwa kuanza wiki ya kwanza na ya pili ya mwezi Novemba, 2014 na zinatarajiwa
kuwa za wastani hadi juu ya wastani isipokuwa maeneo mengi ya mkoa wa Ruvuma, yanatarajiwa
kuwa na mvua za wastani hadi chini ya wastani katika baadhi ya maeneo.

Kielelezo: 1 Ramani ikionesha Mvua kushoto:


Wastani wa mvua Mwezi Oktoba hadi
Disemba; Kulia: Mwelekeo wa Mvua katika msimu huu wa Oktoba hadi Disemba 2104.
Izingatiwe kuwa pamoja na kuwapo kwa uwezekano wa matukio mengi ya mvua kubwa
katika maeneo yanayotarajiwa kupata mvua juu ya wastani, hali hiyo pia inaweza kujitokeza
katika maeneo yanayotarajiwa kupata mvua za wastani hadi chini ya wastani.
Matukio ya Vimbunga katika eneo la kusini magharibi mwa Bahari ya Hindi yanatarajiwa
kuchangia katika mwenendo wa mvua nchini. Maeneo ambayo hali ya mvua inaweza kuathiriwa
zaidi na vimbunga ni pamoja na kanda ya kati, Nyanda za juu Kusini Magharibi, Magharibi
mwa nchi na maeneo ya ukanda wa Pwani.
E: ATHARI NA USHAURI
Maeneo mengi ya nchi yanatarajiwa kupata mvua za wastani hadi juu ya wastani isipokua baadhi
ya maeneo ya kusini mwa nchi yanayotarajiwa kupata mvua za wastani hadi chini ya wastani.
Matarajio ya mvua hizo pamoja na ushauri kwa baadhi ya sekta za kiuchumi na kijamii
zimeainishwa kama ifuatavyo;
Kilimo na Usalama wa Chakula
Katika maeneo mengi ya nchi hali ya unyevunyevu wa udongo inatarajiwa kuwa ya kutosheleza
4

shughuli za kilimo. Hata hivyo, kwa maeneo machache ya kusini mwa nchi (hususan Mkoa wa
Ruvuma) vipindi vya upungufu wa mvua vinatarajiwa mwanzoni mwa msimu na hivyo kuathiri
kiwango cha unyevunyevu wa udongo. Hali ya unyevunyevu wa udongo kupita kiasi
inayoambatana na vipindi vya mvua kubwa inaweza kusababisha ongezeko la magugu, matumizi
makubwa ya pembejeo, hivyo kuongeza gharama za uzalishaji. Wakulima wanashauriwa kuandaa
mashamba na pembejeo mapema pamoja na kuzingatia ushauri wa wataalam wa kilimo kwa
matumizi sahihi ya ardhi na mbegu.
Malisho na maji kwa ajili ya mifugo na wanyama pori
Hali ya malisho na upatikanaji wa maji kwa ajili ya mifugo na wanyama pori inatarajiwa kuwa
nzuri katika maeneo mengi nchini. Hata hivyo, wafugaji wanashauriwa kuzalisha malisho na
kuyahifadhi kwa matumizi wakati wa kiangazi. Aidha, wafugaji wanashauriwa kufuata maelekezo
ya wataalam wa ugani katika maeneo yao hususan matumizi ya maji na malisho na kukabiliana na
magonjwa ya mlipuko yanayoweza kujitokeza. Kutokana na hali ya mvua inayotarajiwa, matukio
ya migogoro inayosababishwa na mifugo, wanyamapori na shughuli za binadamu na kilimo
hayatarajiwi kujitokeza kwa kiasi kikubwa.
Maliasili na Utalii
Mamlaka za usimamizi wa shughuli za utalii na hifadhi za wanyamapori zina shauriwa kuchukua
hatua stahiki katika kuzuia uharibifu wa miundombinu kama barabara na madaraja ndani ya
hifadhi dhidi ya adhari za mvua kubwa na za juu ya wastani katika maeneo husika. Aidha,
wawindaji, wapiga picha za kitalii na makampuni ya kitalii yanashauriwa kuchukua tahadhari ya
uwepo wa mafuriko kutokana na mvua zinazotarajiwa.
Maji na Nishati
Mtiririko wa maji katika mito na vina vya maji katika mabwawa vinatarajiwa kuongezeka katika
maeneo mengi ya nchi kutokana na mvua za msimu wa Vuli. Pamoja na matarajio ya kuwepo kwa
mvua za juu ya wastani inashauriwa kuwa maji yatumike kwa uangalifu na kuzingatia taratibu za
uvunaji, uhifadhi na matumizi endelevu ya rasilimali maji.
Mamlaka za Miji
Inashauriwa kuchukua hatua za kuhakikisha kuwa mifumo na njia za kupitisha maji
zinafanyakazi katika kiwango cha kutosha kuhimili mvua zinazotarajiwa ili kuepusha maji
kutuama na kusababisha mafuriko na uharibifu wa miundombinu, upotevu wa maisha na mali
katika maeneo husika.
Sekta ya Afya
Ushauri unatolewa kwa jamii na sekta husika kuchukua hatua stahiki katika kuzuia milipuko ya
magonjwa yanayosababishwa na kutuama kwa maji na utiririshaji wa maji taka usiodhibitiwa
katika maeneo yao.
Menejimenti ya Maafa
Mamlaka za maafa na wadau wengine wanashauriwa kuchukua hatua stahiki katika utunzaji wa
mazingira, upatikanaji wa maji safi na salama, na usambazaji wa madawa, maji na chakula ikiwa ni
hatua za kujiandaa na kukabiliana na majanga yanayoweza kutokea kutokana na vipindi vya mvua
kubwa na mvua za juu ya wastani zinazotarajiwa.
Vyombo vya habari
Vyombo vya habari vinashauriwa kufuatilia, kupata na kusambaza taarifa sahihi za mienendo ya
hali ya hewa kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na kutumia wataalam wa sekta
husika katika kuandaa na kufikisha taarifa za masuala mtambuka ya hali ya hewa kwa jamii. Aidha,
5

jamii nayo inashauriwa kufuatilia na kuzingatia taarifa sahihi za hali ya hewa na mirejeo yake
kupitia vyombo vya habari.
Angalizo: Mwelekeo wa mvua uliotolewa hapa umezingatia zaidi kipindi cha msimu (miezi
mitatu) na hali ya mvua katika maeneo makubwa. Hivyo, viashiria vinavyochangia mwenendo
wa mifumo ya mvua na mabadiliko ya muda mfupi katika maeneo madogo utazingatiwa katika
uchambuzi wa utabiri wa muda wa kati na mfupi. Watumiaji wa taarifa za utabiri huu
wanashauriwa pia kufuatilia tabiri za saa 24, siku 10 pamoja na wa mwezi kama zinavyotolewa
na Mamlaka ya hali ya Hewa Tanzania.
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania Itaendelea kufuatilia mwenendo wa mifumo ya hali ya
hewa na kutoa taarifa za mwelekeo wa mvua nchini.

Dkt. Agnes L. Kijazi


MKURUGENZI MKUU

You might also like