You are on page 1of 20

Kopi zinaptikana MZALENDO.

NET

UMUHIMU WA KURA YA MAONI NA MUSTAKABALI WA

ZANZIBAR

IMETAYARISHWA NA DR. MOHAMED ADAM WA CHUO KIKUU CHA EAST

STROUDSBURG, PENNSYLVANNIA, MAREKANI

NA KUWAKILISHWA NA MWANADIPLOMASIA MSTAAFU, BW. MUHAMMAD

YUSSUF KATIKA KONGAMANO LA KURA YA MAONI NA SERIKALI YA

UMOJA WA KITAIFA LILILOTAYARISHWA MUWAZA IKISHIRIKIANA NA

ZANZIBAR LAW SOCIETY, ZANZIBAR LEGAL SERVICES CENTER NA JUMIKI

TAREHE 17-18 JULAI 2010

Maneno ya Msingi (Key words): Kura ya maoni, maamuzi, mustakabali wa

Zanzibar

1.0. UTANGULIZI

Makala hii lengo lake hasa ni kuzungumzia umuhimu wa kura ya maoni kwa mustakabali

wa nchi ya Zanzibar. Tukilinganisha nchi za Afrika na Marekani (USA) au Canada au

Ulaya kura ya maoni ni mara chache sana kutumika Afrika. Matumaini yangu utaratibu

huu wa kutoa maamuzi kwa kupiga kura ya maoni utaendelea kukua kwa kuwa ni

sehemu ya kutanuka kwa demokrasia iliyoanza kukua tokea mwanzo wa miaka ya tisiini

barani Afrika lakini pia hapa Zanzibar. Makala haina lengo la kushawishi mtu yeyote

1
Kopi zinaptikana MZALENDO.NET

kupiga kura ya ndio au hapana kwenye hoja ya kura ya maoni ya Serikali ya Umoja

itakayofanyika hapa Zanzibar tarehe 31 Julai, 2010, bali ni kuzungumzia tu umuhimu wa

kura ya maoni, na vipi inahusiana na mustakabali mzima wa nchi ya Zanzibar. Maelezo

yamegawiwa katika mtiririko wa kuchambuwa dhana moja moja kama vile kura ya

maoni, mifano mbali mbali ya dunia inayohusiana na kura ya maoni, kilicholetea kura ya

maoni wakati huu hapa nchini Zanzibar, usimamiaji wake, nini hasa umuhimu wa kura ya

maoni, na mambo yahusuyo mustakbali wa Zanzibar.

2.0. NINI KURA YA MAONI?

Kwa kuilezea kiutaalamu, Kura ya Maoni (Referendum) humaanisha upigaji kura katika

nchi nzima juu ya jambo maalumu (mara nyingi lenye mvutano baina ya pande mbili au

zaidi) ambalo kupitishwa kwake humaanisha au hupelekea kutatuwa tatizo hilo la kisiasa

ndani ya nchi. Katika ulimwengu wa leo, kura ya maoni ni moja ya njia zinazokubalika

katika kutatua masuala mbali mbali ya kisiasa. Wataalamu wa Sayansi ya Siasa

wanatueleza kuwa ziko aina mbili ya “Kura za maoni” ambazo kwa lugha ya Kiingereza

huzitafautisha kwa maneno tafauti. Kwanza ni ile inayoitwa kwa lugha ya Kiingereza

“initiative”ambayo tafsiri yake ya Kiswahili ni wazo au hoja binafsi au ya kundi la watu

katika kuanzisha hoja ya kura ya maoni. Hii hutafsirika kama ni kura ya maoni

inayoletwa baada ya msukumo wa wananchi wa kawaida wenyewe, kwa mfano, baada ya

wananchi kadhaa kusaini aridhilhali na kupeleka lalamiko lao kwenye Bunge au Baraza

la Wawakilishi, na baadae kudai upigwaji kura ya maoni. Aina ya pili ya Kura ya Maoni

kwa lugha ya Kiingereza inaitwa “Plebiscite”. Hii inamaanisha kuomba kura ya maoni

ifanyike kwa ajili ya kutatuwa suala maalumu la kisiasa linalotanza. Ukweli hasa badala

2
Kopi zinaptikana MZALENDO.NET

ya kuziita hizi kuwa ni aina mbili ya Kura za maoni, inawezekana kabisa kuziita

daraja/hatua mbili tu za kura ya maoni. Kwani “initiative” ni pale ambapo kura ya maoni

hupigwa hata kabla hapajatokea uvunjwaji wa Sheria au mzozo na hivyo ndio maana

ikaitwa hilo jina la “initiative” (kwa kuwa inanzisha tu wazo au hoja) na hii ya pili ya

“Prebiscite” huitishwa baada ya mzozo kwisha tokea (hasa wa kisiasa) na lengo lake ni

kuutatua huo mzozo uliopo. Na hii ya pili ndio inalingana na hii Kura ya Maoni

inayotayarishwa kupigwa hapa Zanzibar.

Ni vizuri kutafautisha upigaji kura katika uchaguzi mkuu na kura ya maoni.

Upigaji kura kwenye uchaguzi mkuu na kura ya maoni ni kuwa katika uchaguzi mkuu

mambo mengi ya sera za maendeleo, siasa, uchumi na jamii huchanganywa pamoja na

kujadiliwa wakati wa kampeni na mpigaji kura hutarajiwa kuwa na uwezo wa

kuyachambuwachambuwa mambo hayo mengi ya sera za uchumi, siasa, jamii, ufundi na

muungano na kuyafahamu, na si hayo tu, bali, pia pamoja kumfahamu mgombea kabla ya

mpiga kura huyo kufanya uamuzi wa kutia kura yake. Tafauti yao, ni kwamba Kura ya

maoni hutowa nafasi ya moja kwa moja kwa wananchi kulipigia kura jambo maalumu

linalojieleza kwa uwazi kabisa bila utata au mazonge yoyote ya kufahamika.

3.0 MAPITIO YA KURA ZA MAONI KWA BAADHI YA SEHEMU MBALI

MBALI ULIMWENGUNI.

Kura ya maoni kwa uhakika si jambo geni na zimeshafanywa nyingi sana katika nchi

mbali mbali duniani. Kwahiyo hakuna ukosefu wa mifano duniani ya kuonyesha jinsi

kura za maoni zilivyotumika kutatuwa jambo maalumu la kisiasa. Ndani ya nchi ya

Marekani (USA) kuna jumla ya States 16 (yaani nchi kuminasita) zinazotumia Kura ya

3
Kopi zinaptikana MZALENDO.NET

maoni kuamua masuala mbali mbali makuu ya kisiasa katika nchi zao. Pia kwa Bara la

Ulaya, nchi zote ziliomo katika Jumuiya ya Ulaya (European Union) zimefanya kura ya

maoni katika kuamua aidha wakubali kutumia sarafu na noti ya aina Euro. Na zoezi hilo

kwa kweli limedhihirisha wazi wazi duniani nguvu za wananchi kufanya maamuzi

wenyewe wayatakayo pindipo Bunge na Serikali itawapa fursa hiyo ya kidemokrasia.

Katika baadhi ya nchi maamuzi ya wananchi yalikuwa kinyume na yale

waliyoyapendelea viongozi wa nchi. Inafaa kuangalia mifano zaidi ili kufahamu hoja

mbali mbali zinazopigiwa kura na matokeo yake. Kwa mfano:

• Nchi ya Spain mwaka 1976 walipiga kura ya maoni kubadilisha mfumo wao wa

kisiasa baada ya kifo cha Mtawala dikteta wa nchi hiyo Raisi Franco, na mwaka

1986 walipiga kura ya maoni kuhusu kujiunga na NATO (Jumuiya ya Mashirikiano

ya Kijeshi ya Ulaya na Marekani).

• Denmark pamoja na kuwa ni nchi iliyomo katika Jumuia ya Ulaya, lakini kwa kura ya

maoni kupitia wananchi wao waliamua kujitoa katika suala la kuwa na sarafu ya

pamoja ya Euro.

• Nchi ya Venezuela chini ya Serikali ya Hugo Chavez tokea mwaka 1999 imejiwekea

utaratibu kikatiba unaoruhusu wananchi kupigia kura ya maoni ya kuamuwa aidha

kiongozi aendelee na madaraka yake au aondolewe mradi tu kiongozi huyo ni

mtu aliyechaguliwa kwa kura katika uchaguzi mkuu. Na nafasi hiyo ya kikatiba

na kidemokrasia iliweza kutumiwa mwaka 2004 ambapo baadhi ya watu walidai na

haki ya kikatiba ikatumika kupiga kura ya maoni ya aidha Chavez aendelee na

madaraka au aondoshe na hatima ya matokeo ni kuwa Chavez alinusurika kubaki

madarakani.

4
Kopi zinaptikana MZALENDO.NET

• Nchi ya Puerto Rico ambayo sasa hivi bado ipo chini ya kukaliwa na Marekani,

iliwahi kufanya kura za maoni mara tatu (katika mwaka 1967,1993 na 1998) ili

WaPuerto Rico waamuwe wenyewe kama wanataka wawe nchi huru au wanataka

wabaki chini ya Marekani kama “Commonwealth” (kwa tafsiri ya makubaliano baina

ya nchi hizo mbili za Marekani Puerto Rico ni kuwa Puerto Rico ni nchi

inayojiendesha wenyewe ikiwa chini ya taifa la Marekani). Katika mara zote hizo tatu

matokeo ya kura wananchi waliamuwa hapana, kwa kumaanisha wananchi hao walio

wengi bado wanataka kuwa chini ya Marekani, na hivyo wanakataa kuwa nchi huru

inayojitegemea na uwakilishi katika umoja wa mataifa.

• Pia, katika jimbo la Quebec huko nchini Canada, kura ya maoni ilipigwa kwenye

mwaka wa 1995 kwenye hoja ya kuamua aidha jimbo la Quebec lijitenge na Canada

au kubaki bado kuwa sehemu ya Canada. Matokeo ya kura hiyo ni kuwa watu wengi

katika jimbo la Quebec walipiga ya kukataa kujitenga na shirikisho la Canada.

• Nchi kama za East Timor(iliyokiwa sehemu ya Indonesia) , Croatia (iliyokuwa

sehemu ya Yugoslavia) na Eritrea (iliyokuwa sehemu ya Ethiopia) kwa kutumia

utaratibu huu wa kura ya maoni, nchi hizo zilipiga kura kuamua aidha wabaki sehemu

ya nchi walizokuwemo wakiwa kama majimbo au wawe nchi kamili na huru.

Matokeo yake ni kuwa wananchi wan chi hizo zote wamepiga kura za kuwa huru na

zimekuwa huru.

• Mfano wa karibu yetu hapa Afrika Mashariki ni kura ya maoni iliyopigwa huko

Kenya mwaka 2005 kwa ajili ya kuamua ama kufanya mabadiliko ya Kikatiba au

5
Kopi zinaptikana MZALENDO.NET

kuiwacha katiba waliyonayo kuendelea. Matokeo yakawa ushindi ni kwa wale

waliotaka mabadiliko ya Katiba.

Mambo makubwa ya kisiasa ambayo yamewahi kupigiwa kura ya maoni duniani ni

mengi sana, na niliyotaja hapo juu ni sehemu tu ya mambo hayo. Wazanzibari na

viongozi wa Zanzibar wanafaa kuangalia kwa makini na bila woga vipi wanaweza

kutanuwa utumizi wa kura ya maoni ikiwa ni sehemu ya kukuza demokrasia ili kutatua

matatizo makuu ya kisiasa, jambo ambalo sio tu litasaidia kutatuwa matatizo ya kisiasa

bali pia litasaidia ufanisi na uwajibikaji katika sekta mbali mbali za kimaendeleo.

Zanzibar ya leo na siku za usoni, ili iweze kuwa imara na mustakabali mzuri basi ni

lazima iendelee kukuza demokrasia na kusaka maendeleo kwa nguvu, hasa tukizingatia

katika dunia ya leo iliyojaa ushindani wa kibiashara, mafanikio hutegemea

mazingira mazuri ya kisiasa, yenye uwazi ya kidemokrasia, utulivu na umoja ndani

ya nchi. Labda nifunge maelezo yangu ya kifungu hichi kwa kusisitiza kuwa, pamoja na

mifano mbali mbali ya kura za maoni niliyoitaja hapo juu, kura ya maoni inayotakikana

kufanyika Zanzibar ni mfano wa aina yake. Kura hii ya maoni imeletwa kwa ajili

umuhimu na ulazima ambao Baraza la Wawakilishi waliuona wa kuunda serikali ya

umoja wa kitaifa baina ya Chama kitachoshinda uchaguzi na kuvishirikisha vyama

vingine vyote vitakavyoshiriki na kushinda asilimia kubwa ya viti katika uchaguzi. Bila

shaka yeyote ile, kwa anayefuatilia siasa za Zanzibar ni rahisi kufahamu, ikiwa

hayakutokezea mabadiliko makubwa sana ya kuteteresha moja ya vyama viwili vikubwa

vyenye ushindani nchini Zanzibar, basi washiriki wakuu wa serikali hii ya Umoja pindipo

itakubalika kwa kura basi watakuwa ni CCM na CUF.

6
Kopi zinaptikana MZALENDO.NET

4.0. KUTOFAHAMIANA NA MAFAHAMIANO YALIOLETEA HALI YA KUJA

KWA KURA YA MAONI:

Kuanzia mwanzo wa miaka ya tisiini katika karne iliyopita (Karne ya ishirini), karibu

nchi zote za Afrika zililazimika kuanzisha demokrasia ya vyama vingi kutokana na

sababu mbali mbali za kisiasa, uchumi na jamii za ndani ya nchi zao na pia msukumo

wan chi za nje na jumuiya na mashirika ya kimataifa. Zanzibar pia ilikuwa katika

mkumbo wan chi hizo na kuanzisha demokrasia ambapo ukuwaji wake tunaona kwa vile

leo tunajadili kuhusu kura ya kuulizwa wananchi (kura ya maoni). Ni jambo

lisiloepukika na linaloeleweka kwa yeyote mwenye kuifahamu demokrasia kuwa

“Demokrasia ya kweli kawaida huruhusu mabadiliko”. Sio tu kubadilisha vyama

vinavyotawala, bali huwa ni changa moto wa mijadala inayoweza kuleta mabadiliko juu

ya masuala mbali mbali makuu ya kisiasa, ama miundo ya Serikali, au mifumo ya

utawala, au mabadiliko makubwa ya kikatiba, na kadhalika na kadhalika. Na pia ni rahisi

kuona kwa uwazi kabisa bila hata ya uchunguzi wa kina kwa yeyote yule anayefuatilia

siasa za Zanzibar, kuwa, Wazanzibar wa marika yote ni wana demokrasia halisi wenye

kudai mabadiliko ndani ya vyama vyao na nje ya vyama vyao, katika utendaji wa serikali

za Zanzibar na Muungano.

Zanzibar imepitia vipindi vigumu vya kisiasa kabla ya uhuru na baada ya uhuru, na pia

kabla ya demokrasia ya vyama vingi iliyoanza 1992. Kila uchaguzi kuanzia ule wa 1995

ulikuwa na migogoro na vurugu. Pia chaguzi za Zanzibar za mwaka 2000 na 2005

7
Kopi zinaptikana MZALENDO.NET

zimeifanya Zanzibar ionekane na dunia mfano wa nchi inayoshindwa kabisa kuendesha

uchaguzi kwa kistaarabu na ustahamilivu bila ya kuwepo na umwagaji wa damu, jambo

ambalo halikubaliki duniani kimataifa na halipendezi hata katika macho ya wananchi

wenyewe nchini.

Ni dhahiri, miafaka kadhaa baina ya vyama vya CCM na CUF na jitihada mbali mbali za

wapatanishi kutoka nje ya nchi na ndani na hata mwisho wake Raisi wa Jamhuri ya

Muungano wa Tanzania, Mhe Jakaya Mrisho Kikwete, wote wameshindwa. kuleta

makubaliano yaliyokamilika kiutekelezaji na mustakabali mwema nchini. Jamii ya

KiZanzibari imeendelea kugawika katikati hasa katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni

kwa msingi wa vyama vya CUF na CCM, na hii ni alau kwa kuutaja mmoja tu ya

mgawiko wa WaZanzibari ambao ni wa kisiasa. Chuki zikaendelea kumea baina ya

wananchi hata katika masuala ya jamii, kibinaadamu na mlahaka. Kuna taarifa kuwa

kuna sehemu, watu wameshindwa hata kuzikana, au watu kunyimana huduma za

kibiashara, au watu kushindwa kusaidiana baina ya ndugu na majirani waliokuwa na

mlahaka mzuri hapo awali. Haya yote na mengine zaidi yote yamechangia kuzoroteka

kwa maendeleo kutokana na wananchi na viongozi wa nchi kukosa umoja na ushirikiano.

Professa Issa Shivji katika barua yake ya wazi kwa Mheshimiwa Rais Dk. Amani A.

Karume na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad aliweka wazi maoni yake

kama aonavyo kwamba sababu kuu ya jitihada zilizokuwa zikifanywa kuleta upatanishi

kutokuzaa matunda ni kuwa wanasiasa wa Zanzibar waliweka maslahi yao ya muda

mfupi mbele ya maslahi ya taifa/jamii (Mzalendo.net, jan 2010). Ni wazi kabisa, katika

8
Kopi zinaptikana MZALENDO.NET

hii n’ngwe ya mwisho ya Uraisi wake, Mheshimiwa Amani Karume, uamuzi waliofikia

yeye Raisi Amani Karume (ambaye pia ni kiongozi wa CCM) na, Maalim Seif Sharif

Hamad (Katibu Mkuu wa CUF) kwamba wazungumze na wazizike tafauti zao za kisiasa

kwa maslahi ya taifa la Zanzibar kwa kiasi kikubwa kumechangia kuleta hisia mpya

nchini ya umoja na ushirikiano miongoni mwa Wazanzibar. Tukikubaliana na uchambuzi

wa Professa Shivji basi tendo la Mheshimiwa Amani Karume na Maalim Seif Sharif

kuzika tafauti zao, limeashiria kukubalika na wananchi kuwa viongozi hawa

wametanabahi kuwa maslahi ya taifa wameyapa nafasi yake ya juu yanayostahiki kuliko

yale ya binafsi ya vyeo vya uraisi au uchama.

Makubaliano hayo ndio yaliyokuwa chachu iliyopelekea hata kufika hatua ya kupitisha

Sheria itayoruhusu kuwepo kura ya maoni na kuleta muundo wa Serikali ya Umoja

nchini. Hapa ndipo Wanasiasa wa Zanzibar walipoanza kuonesha upevu wa kuelekea

kwenye safari refu ya demokrasia ya kweli, safari ambayo itaweza kulinda mustakabali

wa nchi ya Zanzibar. Katika nchi kadhaa zenye demokrasia duniani, baadhi ya

masuala makubwa ya kisiasa yanapotokezea, si ajabu kabisa kwa viongozi kutoa

nafasi kwa wananchi wenyewe kuamua kwa kura ya maoni. Hiyo ni njia moja ya

utanuwaji wa uga/uwanja wa demokrasia ambao humpa nafasi kila mwananchi kutoa

maamuzi katika suala hilo. Utafiti na maoni mbali mbali yameonyesha kuwa hadi sasa

kuna waliotuliza vichwa vyao na kutoendekeza ushabiki, woga au uchama wao, na

wanasema hii ni nafasi adimu isiyofaa kuachwa ikapotea. Hao, ndio katika wanaotaka

mabadiliko haya yaje na yalete Serikali ya Umoja. Na kura nyingi za ndio katika Baraza

la Wawakilishi ilikuwa ni sehemu ya uwakilisho wa mawazo yao. Lakini lazima

ikubalike, katika kuleta mabadiliko yoyote makubwa ya kisiasa ni wazi kuna wale

9
Kopi zinaptikana MZALENDO.NET

ambao hawatokubaliana na njia hiyo ya kuleta mabadiliko, aidha wakiwa na njia

mbadala au hata ikiwa hawana au wanapenda tu hali iliyopo iendelee. Pindipo hoja

inakubalika na wengi haina maana wale walioikataa/walioipinga au moyo wao

ulikuwa na mashaka na hoja hiyo kuwa sio wazalendo au wana walakini, ni lazima

kabisa katika demokrasia inayopevuka au iliopevuka ijenge mihimili ya

ustahamilivu. Wana demokrasia katika kura ya maoni ni lazima kuheshimu matokeo

pale hoja inapokubaliwa au kukataliwa. Pia lazima kuwaheshimu wale walioikataa hoja,

ijapokuwa kukataa kwao hakutokuwa kumeweza kuletea kuzuia mabadiliko. Kizazi kipya

ni busara kuandaliwa na kibadilika ili kuachana na siasa za chuki na uhasama ambazo

zinarudisha nyuma maendeleo na badala yake kuimarisha umoja wa kitaifa. Ili kufikia

hatua hiyo, ni lazima taifa na vyama kutowa kipaumbele kwenye suala la mafunzo juu ya

uvumilivu wa kisiasa na ushindani wa vyama vya siasa. Pindipo hilo litachukuliwa uzito

kama ambavyo umoja wa kitaifa unavyotakiwa upewe uzito, hiyo itakuwa ni dawa ya

kuondosha misukosuko, chuki na uadui uliotawala ndani ya siasa za Zanzibar.

5.0. WAZO LA KURA YA MAONI NA UFUATILIAJI WAKE.

Wazo la kupiga kura ya maoni lilitolewa Januari mwaka huu wa elfu mbili na kumi na

Kiongozi wa Upinzani katika Baraza la Wawakilishi, Abubakari Khamis Bakari. Mhe.

Bakari aliwasilishwa Barazani mswada uliopendekeza yafanyike mabadiliko katika

Katiba ya Zanzibar iweze ruhusu kuwepo kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa. Mswada

huo ulijadiliwa katika Baraza la Wawakilishi na kupigiwa kuwa na Wawakilishi wote, na

ukapitishwa na wawakilishi hao wote kwa asilimia mia. Ulipitishwa kwa sharti ya

10
Kopi zinaptikana MZALENDO.NET

kwamba wapewe nafasi Wazanzibari kwa kutumia kura ya maoni ili waweze kuamua

kama wanataka serikali ya umoja au la.

Wakati akiwasilisha mswada huo, Mhe. Abubakar Khamis Bakari aliilezewa kwa uwazi

na ufasaha kabisa sababu ya kuleta hoja hii ya Serikali ya Umoja ni kwamba hii anaiona

ni njia pekee itakayopelekea kuleta ufumbuzi wa kudumu wa tatizo sugu la ugomvi wa

kisiasa utokeao kila baada ya uchaguzi na pia itawaunganisha wananchi wa Zanzibar

(Daily News, March 30,2010). Lakini, tukiangalia dunia nzima, suala la Serikali ya

Umoja nalo sio geni na limeshatumika nchi kadhaa duniani katika nia hiyohiyo ya

kutatuwa mizozo. Serikali za Mseto au Umoja wa Kitaifa mara nyingi huanzishwa pale

inapojitokeza nchi inakuwa na mvutano mkubwa wa kisiasa baina ya vyama

vinavyoshindana au vurumai limetokezea na mara nyengine hata damu kumwagika. Kwa

mfano, Kenya au Zimbabwe ni mfano mzuri wa nchi zilizo Barani Afrika kama ilivyo

Zanzibar ambazo damu zilimwagika ndipo Serikali ya Umoja wa kitaifa ikaundwa.

Mfano mzuri ni Afrika ya Kusini ambayo ni nchi iliyotokana na mifarakano mikubwa

katika historia yake kabla ya uchaguzi huru na haki ulioshirikisha raia wao wote wa

mwaka 1994. Ili kuepusha nchi yao kuendelea kukumbwa na mifarakano mikubwa nchini

mwao, Chama cha African National Congress (ANC) kilichoshinda uchaguzi na kutwaa

madaraka ya Serikali chini ya Uongozi wa Mandela (mmarufu huko kwa kwa jina la

Madiba) walihakikisha wanaimarisha maslahi ya taifa lao kwanza kuliko ya binafsi na

uchama na waliamua kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa. Hili lilimpa nyongeza

nyengine kubwa sana ya sifa Raisi Mandela lakini uongozi mzima wa chama chao na

nchi yao kuheshimiwa na nchi nyengine duniani. Mfano wa Afrika ya Kusini ni mzuri

11
Kopi zinaptikana MZALENDO.NET

zaidi kuigwa kuliko hata ule wa Zimbabwe au Kenya ambao Serikali zao za Umoja

zimeletwa baada ya damu nyingi kumwagika na mali nyingi kupotea na hata heshima ya

taifa lao. Afrika ya Kusini walichukua tahadhari kabla ya athari haijawa kubwa. Inaingia

akilini kabisa, ikiwa njia hii ni tabibu kwa mizozo ya kisiasa, na Zanzibar inao mzozo wa

kisiasa kila uchaguzi, basi ni busara kabisa kukubali kutumia dawa hii iwe tabibu wa

gonjwa la kisiasa hapa Zanzibar. Tukiachilia mbali Serikali ya Umoja wa kitaifa, hata

mbinu ya uundwaji Serikali za Mseto hutumika sana nchi za ulaya ili kuondoa mivutano

na kufanya nchi ziendelee kutawalika, kuwa na utulivu na wananchi wake wafaidike na

sera za maendeleo zinazotekelezwa na serikali iliyopo madarakani ya mseto. Mfano huu

upo kwa nchi nyingi kama vile Israel, Ujarumani, Italy na hata Australia ambazo zote hizi

huwa na serikali za mseto.

Kwa kuendelea kukaa juu ya mstari katika mada hii inayohusu ufuatiliaji wa upigaji kura

ya maoni. Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) inabidi ijadiliwe. Kutokana na maelezo

ya Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi Bw. Khatib Mwinyichande ( July 13, 2010) ni

kwamba Tume ya Uchaguzi Zanzibar imewezeshwa kuendesha shughuli za Upigaji kura

ya Maoni baada ya kuitishwa Sheria ya namba 6 ya mwaka 2010 chini ya maelezo

yaliyomo katika kifungu 3, kijifungu 1. Kwa mujibu wa maelezo ya Bw. Mwinyichande

ni kuwa kifungu hiki ni muhimu sana kwa demokrasia inayoambatana na upigaji kura ya

maoni kwani imeweka “precedence” (kigezo cha msingi kisheria) ambacho kinaweza

kufuatwa kwa suala lolote jengine la kisiasa ikihitajika upigaji kura wa maoni.

imepitishwa kuweza kuiruhusu iweze kusimamia upigaji kura huo”. ikiwa ni pamoja na

kupanga tarehe na kuelimisha wananchi juu ya umuhimu wa kushiriki.

12
Kopi zinaptikana MZALENDO.NET

Kwa mujibu wa muswada huo, ni Wanzibari waliojiandikisha kwenye Daftari la Kudumu

la Wapiga kura tu, ndio watakaopiga kura ya kuulizwa ama kujibu ndio au hapana na

gharama za shughuli hiyo zitabebwa na Wizara ya Fedha. Tume ya Uchaguzi itatumia

majimbo yale yale yaliyopangwa kwa ajili ya uchaguzi mkuu na vituo vile vile katika

kuendesha kura hiyo. Na Tume ya Uchaguzi (ZEC) ndio watakaotangaza matokeo na

kama kutatokea shaka katika matokeo hayo, haitatiliwa maanani. Pia, kama ikitokea

matokeo hayo yakafungana (yaani yamekuwa sare), Tume itatangaza tarehe nyingine

katika kipindi cha mwezi mmoja baada ya matokeo hayo, kwa ajili ya upigaji kura

mwingine. Itakuwa ni kosa kwa mtu au taasisi kutangaza matokeo ya kura hizo kabla ya

ZEC na unapendekeza faini ya kati ya Sh milioni moja hadi 10 au kifungo cha miaka

mitatu jela au adhabu zote kwa pamoja. Kwa maelezo ya Mwenyekiti Khatib

Mwinyichande pindipo patatokea jambo lililokuwa katika uendeshaji wa kura hiyo ya

maoni halikuelezwa katika sheria ya kura ya maoni au ipo khitilafu katika vifungu vyake,

basi sheria ya Uchaguzi ya mwaka 1984 (ambayo imefanyiwa marekebisho mara kadhaa

kila uchaguzi) ndiyo itakayofuatwa.

Kura ya maoni inatarajiwa tarehe 31 Julai 2010, na hivi sasa ZEC kupitia msaada ya

Shirika la Umoja wa mataifa la Misaada ya Maendeleo (UNDP) imeweza kufanya

maendeleo ya elimu ya wapiga kura kupitia vikundi na jumuia mbali mbali za katika

mitaa na vijiji. Hizi jumuia ndio zinasaidia hata kusambaza taarifa na karatasi matangazo

au maandishi (posters and leaflets). Ni ZEC yenyewe iliyoandaa na kuendesha kura ya

maoni Julai 31 kwa kutumia wafanyakazi ambao wamewaajiri na wanawapa mafunzo

kwa sasa hivi.

13
Kopi zinaptikana MZALENDO.NET

Katika jumla ya haki za mpiga kura hiyo ya maoni ni kwamba, Mzanzibari aliyepiga kura

anaruhusiwa kukata rufaa katika Mahakama Kuu ya Zanzibar. Uamuzi wa mahakama

hiyo ndio utakuwa wa mwisho na hakuna rufani itakayokubaliwa katika Mahakama ya

Rufani, Lakini kabla ya mtu kukata rufaa dhidi ya matokeo ya upigaji kura huo, atatakiwa

kwanza kuwa na wapiga kura 10 kutoka kila mkoa visiwani hapa, wanaomuunga mkono

na kulipa Sh milioni tano kwa ajili ya kufungulia kesi siku 30 baada ya matokeo

kutangazwa. Shindikizo langu katika mada hii ni kuwa kuwaelimisha wananchi sio tu

namna ya kupiga kura yenyewe bali pia kuwaeleza ina umuhimu wa Kura hiyo ya maoni

kwa maslahi ya taifa zima la Zanzibar kwa kipindi cha muda mfupi na baadae. Katika

demokrasia yoyote ni wajibu sio tu kuwafanya wapige kura bali wajadili kwa kina na

kuelewa ili wajue faida na hasara za kuwa na muundo huo mpya na faida na hasara za

muundo uliopo. Hili ni muhimu kwani maamuzi ya hao wananchi ikiwa ni kura ya Ndio,

uamuzi huo utawafanya waishi na huo muundo mpya kwa miaka ifuatayo, na

wakaiamuwa kutia kura ya Hapana ama kwa kutokuelewa au kughilibiwa wataendelea

kuishi na mfumo uliopo. Kura ya maoni kwenye nchi mbali mbali huelimisha na

huchangamsha jamii kwa ngoma, nyimbo, mashairi, vifijo, alama na vichekesho kila mtu

anapojitahidi kueleza au kuunga mkono au kukataa hoja. Kwahiyo kuachiwe uhuru wa

kutia kampeni.

6.0. KURA HII YA MAONI INA UMUHIMU GANI NA ITASAIDIA NINI

KATIKA MUSTAKABALI WA ZANZIBAR .

a) Kutoa nafasi zaidi ya kutanuka kwa demokrasia: Umuhimu wa kura ya maoni ya

mwaka huu pindipo wananchi watasema ndio au hapana, basi la kwanza kabisa

14
Kopi zinaptikana MZALENDO.NET

lililopatikana ni kuwa Zanzibar imeshajijengea utaratibu wa kisheria utaoruhusu kupiga

kura ya maoni kwenye masuala muhimu ya kisiasa, uchumi, kero za muungano au hata

uongozi.

b) Kuwafanya wananchi wafahamu kuwa wanayo sauti katika masuala muhimu ya

kisiasa katika nchi: Pindipo masuala mengi makubwa ya kinchi ambayo hatima yake

yanawaathiri wananchi kila siku yanafanywa bila ya kuwashirikisha wananchi , basi si

ajabu kuwa na wananchi wanaolalamika na kutoridhika sana na Serikali na viongozi wao.

Na hakuna njia bora ya kuwashirikisha wananchi katika maamuzi inayoizidi hii ya Kura

ya maoni.

c) Kisiasa: Kuondosha siasa za utengano, chuki, ubaguzi, uhasama, ugomvi na visasi

miongoni mwa wananchi na kuleta siasa za umoja, maelewano na mashirikiano (Seif

Sharif hamad, 2010)

d) Kiusalama: Kuondoa khofu na wasiwasi kwa kufuta viashiria vinavyoweza kuwa

chanzo cha fujo na ghasia na ambavyo vingeweza kutumiwa hata na maadui wa Tanzania

kuhatarisha usalama wa nchi na badala yake kuleta hali ya amani na usalama ambayo

inavifanya hata vyombo vya ulinzi na usalama kufanya kazi zao katika hali ya utulivu na

ushirikiano na wananchi wote (Seif Sharif hamad, 2010)

c) Kiuchumi: Kuondoa hali iliyokuwepo ya sehemu ya wananchi kujiona

hawashirikishwi au hawapaswi kushiriki katika harakati za ujenzi wa nchi na kuwaleta

pamoja wananchi wote ili kwa pamoja tushiriki katika ujenzi wa Zanzibar mpya(Seif

Sharif hamad, 2010)

15
Kopi zinaptikana MZALENDO.NET

d.)Kijamii: Kuondoa hali ya utengano na kutoaminiana miongoni mwa wafuasi wa

vyama tofauti vya siasa na kuwafanya wapendane na washirikiane katika shughuli zote za

kijamii wakijua kuwa wote ni wananchi wa nchi moja (Seif Sharif hamad, 2010). Katika

dunia ya leo, Serikali pekee hazikidhi mahitaji yote ya jamii kwenye huduma za elimu,

afya, maji safi , umeme na kadhalika. Jamii iliyoshikamana hujikusanya na kusaidiana

kupitia jumuiya zisizo za kiserikali. Ushirikishwaji wa wananchi wa Zanzibari walio

ndani na nje ya nchi katika ujenzi wa taifa utaweza kusaidia hasa maeneo ya huduma za

jamii kuitia jumuia zisizo za Kiserikali.

e) Haja ya kuwa katika Muungano usiodhoofisha mamlaka ya Zanzibar kwa

mujibu wa katiba zote mbili za Muungano na Zanzibar: Zanzibar ilioyo na

viongozi walioshikamana kwa maslahi ya taifa ni Zanzibar imara ndani ya muungano.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari wakati akigombea nafasi ya uraisi kwa

tiketi ya Chama cha mapinduzi, Bw. Muhammad Yussuf Mshamba alieleza kuwa

kuimarisha Muungano haina maana hata kidogo ya kuingiza kila kitu katika orodha

ya mambo ya Muungano. Na kusisitiza kuwa ukweli usiofichika kuwa Muungano

utaimarika zaidi ikiwa hatua za makusudi zitachukuliwa kuyaondoa yale mambo yote

yaliyomo katika orodha ya Muungano ambayo upande mmoja wa Muungano

unaamini kuwa kuendelea kubakia kwake hakuleti faida wala maslahi mazuri kwake

na hivyo kuna muelekeo wa kuuathiri vibaya upande wake. Hili halina mjadala ikiwa

dhana ya kuanzishwa kwa Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar imejengeka

kikweli kweli katika misingi ya usawa, uhuru na upendo tokea hapo awali.

16
Kopi zinaptikana MZALENDO.NET

Mustakabali wa Zanzibar utapatikana ikiwa katika kuimarisha misingi ya usawa,

uhuru na upendo utaimarishwa Zanzibar basi ni wazi misingi hiyo ionekane katika

muungano. Kwani hayo ndio yatakuwa maadili ya Wazanzibari. . Kwa mfano tu,

Suala la Mambo ya Nje kweli ni la Muungano, lakini ni wazi masuala ya

Mashirikiano ya Kimataifa kwa Maendeleo (International Development) haya

yalikuja baadae. Ni masuala mashirikianao ya kimataifa kwa misaada ya maendeleo

ndio mara nyingi tunakuwa na mivutano. Zanzibar inahitaji kuwa na uhuru wa

kutosha kushirikiana na nchi mbali mbali na jumuiya mbali kwa missada ya

maendeleo bila kuingiliwa na SMT. Hii ni sehemu ya mustakabali wa Zanzibar.

f) Haja ya kusimamia imara rasilmali za nchi : Mwananchi mpenda nchi ni yule aliye

imara kulinda mali za nchi. Mwananchi mpenda nchi huwa si mla rushwa na mwenye

kutetea na kuona uchungu pindipo mali ya taifa anaiona inaporwa. Mwananchi

mpenda nchi ni yule anayetaka haki, na mali binafsi za raia mwenzake zilindwe

kama atakavyo zake zilindwe. Nchi yenye raia wasio na hisia na nchi yao huwa

hawajali mali za taifa lao na si walinzi wa raia mwenziwao/wenziwao. Mustakabali

wa Zanzibar utapatikana kuziimarisha hisia hizi. Serikali ya umoja inayo nafasi

kubwa kuzijenga hisia hizi. Masuala kadhaa nyeti yamejitokeza kwa jina la kero za

muungano yanahusu rasilmali za Zanzibar. Zanzibar haina muda wa kupoteza

kwenye mambo ya kutofahamiana wenyewe kwa wenyewe na kushindwa kutumia

wakati wake vizuri kujiimarisha kwenye madai na mijadala inayohusu umilikaji wa

mafuta au uchangiaji gharama za muungano na mgawanyo wa mapato yapatikanayo.

7.0. HITIMISHO:

17
Kopi zinaptikana MZALENDO.NET

Mwisho, waraka huu unahitimisha kwa maoni ya kwamba kura ya maoni ni muhimu kwa

vile inaruhusu msimamo wa walio wengi kukubalika kama ndio ridhaa ya wananchi na

ndio uamuzi wa mwisho kinyume na hali ambayo uamuzi ungefanywa na wachache

katika vyombo vya dola. Kwa maana hii basi kura ya maoni inawakilisha matakwa ya

kweli, inaonyesha matarajio na matamanio ya kweli kabisa ya wananchi wenyewe katika

jamii au nchi. Kura ya maoni inastahiki na ina faida sana pale ambapo kuna masuala

nyeti ya kitaifa kwa ajili ya taifa. Kuna misemo mitatu ya wasia iliyousiwa na Mpigania

Haki za binaadamu maarufu huko Marekani (Martin Luther King) na Maraisi wawili

(Abraham Lincoln na John F. Kennedy) wote ni katika wanaohishimika nchini huko na

duniani ambayo ni mizuri kufungia makala hii. Wa kwanza ni wa Martin Luther King

ambao ukiusia wanaadamu kuondokana na chuki, usemao “Like an unchecked cancer,

hate corrodes the personality and eats away its vital unity. Hate destroys a man's sense of

values and his objectivity. It causes him to describe the beautiful as ugly and the ugly as

beautiful, and to confuse the true with the false and the false with the true” Kwa tafsiri ni

kuwa, Chui ni kama maradhi ya Saratani yasiyotibiwa, humuharibia mtu utu wake na

huharibu umoja. Chuki humfanya mwanadamu akaliita baya ni zuri na zuri ni baya, na

humfanya akashindwa kuchanganuwa baina ya ukweli na uwongo na baina ya uwongo na

ukweli. Hili inabidi tulizingatie ili kuondokana na siasa za chuki. Wasia wa pili, ni wa

Raisi Abraham Lincoln usemao ‘A house divided against itself cannot stand’ yaani

‘Nyumba iliyogawanyika haiwezi kusimama’. Lengo lake kuhimiza umoja na kuepukana

na migawiko ndani ya nchi. Wa tatu ni ule maarufu sana wa Rais Kennedy usemao “ Ask

not what your country can do for you--ask what you can do for your country” yaani

18
Kopi zinaptikana MZALENDO.NET

“Usiulize nchi ukifanyie nini, uliza nini kinahitajika uifanyie uifanyie nchi yako”.

Ikiwezekana timiza wajibu wako.

Marejeo (References)

1. Mark N. Franklin, Cees van der Eijk and Michael Marsh, (1995) Referendum

outcomes and trust in government: Public support for Europe in the wake of

Maastricht, West European Politics, Vol 18, 1995

2. Muhammad Yussuf, (2010), Hotuba iliyotolewa kwa waandishi wa Habari na

Bwana Muhammad Yussuf kuelezea azma yake ya kutaka kugombea nafasi ya

Urais wa Zanzibar kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi katika ukumbi wa

EACTROTANAL siku ya Alkhamisi tarehe 24 Juni 2010, Zanzibar.

3. Natelson, Robert G. (1999), Are Initiatives And Referenda Contrary To The

Constitution's "Republican Form Of Government"?

4. Norman, A. S1 and Kwadwo, Sarfo Kantanka, (1999), The role of referendum: A

case of Ghana, African Journal of History and Culture (AJHC) Vol. 1 (1), pp.

001-005, May, 2009 -Available online at http://www.academicjournals.org/AJHC

5. UNDP, (2010), Election Support project, Newsletter No. 6, May 2010

6. Gay, Oonagh and Wood Edward, (2000) House of Commons, 2000, The Political

Parties, Elections and Referendums Bill – Referendums and Broadcasting Bill 34

1999-2000

7. Zanzibar: Democracy on Shaky Foundations, Article 191, April 2000

19
Kopi zinaptikana MZALENDO.NET

Marejeo kutoka Mtandaoni

8. Shivji, Issa, 2010, Barua ya wazi kwa Mheshimiwa Rais Karume na Maalim Seif

- http://hakinaumma.wordpress.com/2010/01/

9. Issa Seif Sharif Hamad , 2010, Maridhiano na Mustakbali wa Zanzibar, Januari,

23,2010-http://hakinaumma.wordpress.com/2010/01/23/maridhiano-na-

mustakbali-wa-zanzibar/)

10. http://www.thefreedictionary.com/referendum

11. http:// www.Mzalendo.net

12. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Rasimu ya Mswada wa Sheria ya Mabadiliko

ya nane katika Katiba ya Zanzibar ya 1984.

Mahojiano kwa Simu

13. Bw. Khatib Mwinyichande, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, tarehe 13 Julai

2010.

14. Bw. Ramadhan Omar, wa Mwembetanga, 13 Julai 2010

15. Bw. . Zahor Mzee Salum, Miembeni, 6 Julai,2010.

16. Bw. Juma Janja, Kiembesamaki 12 Julai, 2010

20

You might also like

  • Annuur 1092
    Annuur 1092
    Document16 pages
    Annuur 1092
    annurtanzania
    No ratings yet
  • Annuur 1087
    Annuur 1087
    Document7 pages
    Annuur 1087
    annurtanzania
    No ratings yet
  • Annuur 1082
    Annuur 1082
    Document16 pages
    Annuur 1082
    MZALENDO.NET
    100% (1)
  • Annuur 1091
    Annuur 1091
    Document16 pages
    Annuur 1091
    MZALENDO.NET
    No ratings yet
  • Rasimu Ya Katiba (Toleo La Pili)
    Rasimu Ya Katiba (Toleo La Pili)
    Document0 pages
    Rasimu Ya Katiba (Toleo La Pili)
    Muhidin Issa Michuzi
    0% (1)
  • Annuur 1078
    Annuur 1078
    Document12 pages
    Annuur 1078
    MZALENDO.NET
    No ratings yet
  • Annuur 1076
    Annuur 1076
    Document12 pages
    Annuur 1076
    MZALENDO.NET
    No ratings yet
  • Annuur 1063
    Annuur 1063
    Document16 pages
    Annuur 1063
    Hassan Mussa Khamis
    No ratings yet
  • Annuur 1065
    Annuur 1065
    Document12 pages
    Annuur 1065
    MZALENDO.NET
    No ratings yet
  • An-Nuur 1071
    An-Nuur 1071
    Document12 pages
    An-Nuur 1071
    MZALENDO.NET
    No ratings yet
  • Annuur 1030
    Annuur 1030
    Document16 pages
    Annuur 1030
    MZALENDO.NET
    No ratings yet
  • Annuur 1077
    Annuur 1077
    Document12 pages
    Annuur 1077
    MZALENDO.NET
    No ratings yet
  • Annuur 1072
    Annuur 1072
    Document12 pages
    Annuur 1072
    MZALENDO.NET
    No ratings yet
  • Annuur 1062
    Annuur 1062
    Document16 pages
    Annuur 1062
    MZALENDO.NET
    No ratings yet
  • Annuur 1067
    Annuur 1067
    Document12 pages
    Annuur 1067
    annurtanzania
    No ratings yet
  • Annuur 1046
    Annuur 1046
    Document12 pages
    Annuur 1046
    MZALENDO.NET
    No ratings yet
  • Annuur 1057
    Annuur 1057
    Document16 pages
    Annuur 1057
    MZALENDO.NET
    No ratings yet
  • Annuur 1060
    Annuur 1060
    Document16 pages
    Annuur 1060
    MZALENDO.NET
    No ratings yet
  • Annuur 1061.
    Annuur 1061.
    Document16 pages
    Annuur 1061.
    MZALENDO.NET
    No ratings yet
  • Annuur 1049
    Annuur 1049
    Document12 pages
    Annuur 1049
    MZALENDO.NET
    No ratings yet
  • Annuur 1031
    Annuur 1031
    Document16 pages
    Annuur 1031
    MZALENDO.NET
    No ratings yet
  • Annuur 1059
    Annuur 1059
    Document16 pages
    Annuur 1059
    MZALENDO.NET
    No ratings yet
  • Annuur 1022
    Annuur 1022
    Document12 pages
    Annuur 1022
    MZALENDO.NET
    No ratings yet
  • Nadharia Ya Meli
    Nadharia Ya Meli
    Document6 pages
    Nadharia Ya Meli
    MZALENDO.NET
    No ratings yet
  • Annuur 1029
    Annuur 1029
    Document20 pages
    Annuur 1029
    annurtanzania
    100% (1)
  • Annuur 1028
    Annuur 1028
    Document16 pages
    Annuur 1028
    MZALENDO.NET
    No ratings yet
  • Annuur 117
    Annuur 117
    Document16 pages
    Annuur 117
    annurtanzania
    No ratings yet
  • Zaka 3
    Zaka 3
    Document61 pages
    Zaka 3
    MZALENDO.NET
    No ratings yet
  • Annuur 1027
    Annuur 1027
    Document16 pages
    Annuur 1027
    MZALENDO.NET
    No ratings yet