Welcome to Scribd, the world's digital library. Read, publish, and share books and documents. See more
Download
Standard view
Full view
of .
Look up keyword
Like this
5Activity
0 of .
Results for:
No results containing your search query
P. 1
ANNUUR 1024

ANNUUR 1024

Ratings: (0)|Views: 3,549 |Likes:
Published by MZALENDO.NET

More info:

Published by: MZALENDO.NET on Jul 06, 2012
Copyright:Attribution Non-commercial

Availability:

Read on Scribd mobile: iPhone, iPad and Android.
download as PDF, TXT or read online from Scribd
See more
See less

07/19/2012

pdf

text

original

 
ISSN 0856 - 3861 Na. 1024 SHAABAN 1433, IJUMAA JULAI 6 - 12, 2012 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=
Sauti ya Waislamu
Mufti Bakwata amekosea
Wasema Wanazuoni Dar
Maamuzi ya kususia sensa yalikuwa ya ShuraKukiuka Shura ni kuvunja maelekezo ya Qur’an Angelirejesha Suala hilo katika Shura ya awali
 SHEIKH Nurdin Kishki.
Innalillahi wainna ilayhir rajiuun:Mzee wetu Alhaj Ali Hassan Mwinyi…
Reginald Mengi na Mtume
Muhammad wapi na wapi?
Mbona wapo kina Paulo, Petro na Luka?Ungemfananisha na ‘Mtume’ MwingiraWapo pia Mzee wa Upako, Mch. Rwakatare
Uk. 2
MAKAMU Mwenyekitiwa Chama cha MapinduziZanzibar Dk. Amani AbeidKarume amewatoa wasiwasiWazanzibari akisema kuwahakuna haja ya kuwahofiaUamsho.
Karume ampasha Borafia juu ya Masheikh Uamsho
 Afafanua msaada wao kwa wananchiWanawaamsha Wazanzibar waliolala
Na Mwandishi Wetu
Karume amesema, hata walewanaodhani hawawahitajiUamsho, watambue pia naoUamsho ina faida kwao lauwatatafakari kidogo.Mheshimiwa AmaniAbeid Karume akipiga
Inaendelea Uk. 2
Maandamano makubwa
kufanyika nchi nzima
Kupinga kudhalilishwa Sheikh Kishki, MuftiKamanda Ernest awaombe radhi Waislamu
 MASHEIKH wa Umoja wa Wanazuoni wa Kiislamu nchini wakitoa taarifa ya Waislamukutoshiriki katika zoezi la sensa katika Hotel ya Tansoma jijini Dar es Salaam Jumatanowiki hii .
 
2
 AN-NUUR
SHAABAN 1433, IJUMAA JULAI 6-12, 2012
AN-NUUR
S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786
Cel: 0784 370 208, 0652 849227, 0755 260 087, DSM.
www.ipctz.org E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk
Ofisi zetu zipo: Manzese Tip TopUsangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam
MAONI YETU
TahaririMakala
Reginald Mengi na Mtume
Muhammad wapi na wapi?
YUPO Sheikh mmojaaliwahi kusema mbele yaNyerere kuwa ni faradhina amri ya Qur’an kwaWaislamu kutii viongozi waserikali. Mwalimu Nyerereakamuuliza, “hata akiwaKaburu ?”
Kwa mujibu wa taarifa zavyombo vya habari mwishonimwa wiki iliyopita, RaisMstaafu Alhaji Ally HassanMwinyi amemfananisha Dr.Reginald Mengi na MtumeMuhammad (s.a.w).“Rais mstaafu waawamu ya pili, Alhaj AliHassan Mwinyi, amesemaMwenyekiti Mtendaji wamakampuni ya IPP Limited,Dkt. Reginald Mengi, anasifa za kuitumikia jamiikama alivyokuwa MtumeMuhammad (s.a.w)”,limeripoti gazeti la Nipashela Jumapili iliyopita.“Alhaj Mwinyi: Mengiana sifa kama za Mtume(Muhammad s.a.w)”,liliandika gazeti hilo katikakichwa cha habari hiyo nakisha kufafanua kuwa AlhajMwinyi amesema kuwaWaislamu wanavutiwa sanana tabia za Mengi kwanizinafanana na alizokuwanazo Mtume Muhammad(s.a.w).“Sifa hizo (za Mengi)ndizo alikuwa nazo MtumeMuhammad S.A.W. ambayeumma wa Waislamuunamheshimu”, alifafanuaMwinyi kama alivyonukuliwana Nipashe.Mzee Mwinyi aliyasemahayo katika hafla yakumtunuku Mengi TuzoIliyotukuka ya Hudumakwa jamii iliyotolewa nailiyotajwa kuwa Kamati yaAmani ya Viongozi Mkoawa Dar es Salaam.Mwenyekiti wa Kamatihiyo ni Sheikh Alhad MussaSalum ambaye alisema kuwawanamsomea Dua maalumDr. Mengi kwa kutambuamchango wake katika jamii. Katika hafla hiyo Dr.Reginald Mengi alivaa kofiasafi ya Waislamu wa Pwanina Zanzibar ile ya kushonwakwa mkono.Ukitaja jina MtumeMuhammad (s.a.w) mbeleya Mkristo yeyote, kwakehuyo ni nabii wa uwongo.Kwa Mkristo yeyote, jinaMuhammad linaleta picha yamtu aliyefanya kazi kubwa yakuvunja misingi ya Ukristokwa kutangaza na kuwaonyawale wanaosema kuwa Yesuni Mungu. Ni Mtume (s.a.w) kupitiaWahay aliopewa na Allah(S.W.T), aliyesema kuwaYesu si Mungu wala si mmojakatika wale waungu watatuwanaoitakidiwa na Wakristo. Ni Mtume Muhammad(s.a.w) aliyefundisha kuwaYesu hakufa Msalabaniwala hatabeba dhambi zaWakristo kama wenyewewanavyoamini kwamba Yesualiteswa kwa ajili ya dhambizao. Katika kusisitiza somohilo, Mtume (s.a.w) akasemakuwa kwa hakika ni makafiriwale waliosema kuwa Yesumwana wa Mariam ni Mungu. Na kafiri mahali pake niJahannam, siku ya Kiama.Atafurahi muda mfupi dunianikwa mali zake, watoto nacheo kwa sababu Allah niAr-Rahmaan. Lakini kwamujibu wa yale aliyofundishaMtume Muhammad (s.a.w),kafiri hana chake siku yakiama. Kwake itakuwa Fiinari Jahannam; khaalidinafiiha abada.Kwa msemo uliozoeleka waMaaskofu, ambao ni viongoziwa kiroho wa ReginaldMengi, Mtume Muhammad(s.a.w) anakashifu Ukristo.Masheikh na Wahadhiri waKiislamu wanaodarasisha nakusimama kwenye majukwaana kuvunja “Utatu” (Trinity),ambayo ni imani ya msingikatika Dini ya Mengi, basimwalimu wao ni MtumeMuhammad (s.a.w).Wahadhiri hao wa Kiislamuwanawatanabahisha piaWakristo kwamba Yesu SiMungu na kwamba “Hakuwayeye Yesu ila ni Mtume tu, ni binadamu ambaye yeye namama yake wakila chakulana kwenda haja kubwa.Wahadhiri wanaoyasemahaya kama yalivyokuja katikaQur’an 5:75), Mwalimuwao ni Mtume Muhammad(s.a.w).Sasa kama Maaskofuna Wakristo kwa ujumlawanasema kuwa Wahadhirihawa wanakashifu Ukristo,ina maana kuwa MtumeMuhammad (s.a.w) ndiyeMwalimu Mkuu wawanaokashifu Ukirsto. Hiimaana yake ni kuwa kamaMtume Muhammad (s.a.w)angekuwa hai leo, ilikuwaawe wa kwanza kukamatwakatika ile kadhia ya mauwajiya Mwembechai ambapovyombo vya habari vya BwanaReginald Mengi vilifanyakazi kubwa sana katikakuwabamiza Waislamu. Ni kwa mantiki hii, sisihatudhani kuwa Mzee AlhajiAlly Hassan Mwinyi atakuwaamemtendea haki Mwenyekitiwa Makampuni ya IPP, Dr.Reginald Mengi kumfananishana ‘Mtume wa uwongo’kwa mujibu wa imani yake.Hatuamini pia kuwa Dr. Mengialifurahi kufananishwa na mtuambaye kwa imani yake nakwa msimamo wa Maaskofuwake ni ‘Mwalimu Mkuu’wa Wahadhiri wanaokashifuUkristo.Japo lengo la Mzee Mwinyililikuwa kumsifu Mengi, lakinihatudhani Dr. Reginald Mengiamefikia mahali pa kupendasana sifa kiasi cha kutokujalini sifa gani anapewa auanafananishwa na nani. Ni kwa sababu hiyo,hatudhani kuwa Mengi atakuwaamefurahi kufananishwa namtu anayekanusha uungu wamwokozi wake Yesu Kristu.Sisi tunamjua Dr. Mengikwamba ni mtu wa dini. Nimtu wa Kanisa na ni mtuanayelipenda sana Kanisalake. Mengi atakuelewaukimtajia Petro, Marko naMatayo. Lakini sio AbuHuraira, Imam Shafii auhata Barnabas aliyekuwamwanafunzi wa Yesu.Tunavyojua sisi Wakristohawana upungufu katikawatakatifu wala manabii.Wapo mpaka akina Kambarageambao Kanisa hivi sasa lipokatika mchakato wa kumpautakatifu.Hapana shaka Dr. ReginaldAbraham Mengi angefurahisana kama angesifiwa nakufananishwa na watu ambaoanawakubali kwamba niwatakatifu kama ‘MtumePaulo’ au hata hawa Manabiiwa kileo kama kina Mwingira,Mzee wa Upako na MchungajiGetrude Rwakatare.
Karume ampasha Borafia juu ya Masheikh Uamsho
Inatoka Uk. 1
mfano mwepesi kabisakumfanya Borafia kufahamu,aliwafananisha Uamsho sawana waamsha daku.Akasema, kuna Waislamukatika mwezi wa Ramadhanihawahitaji kuamshwa kuladaku, wanaamka wenyewe.Lakini wapo wengine, bilakupita kigoma cha kula dakuwanaweza wasile daku sikuhiyo.Katika hali hiyo akasemakuwa, yule ambaye hanausingizi wa kuhitajiakuamshwa, anaweza kuwaona“kula daku” kama kero.Lakini akitokeakukurupushwa na kigomacha kula daku, japo anawezakukasirika, lakini akitizamasaa akiona muda umefika,atafurahi na kula daku yake.Akizungumza katikamkutano uliofanyika Jimbola Rahaleo Mkoa wa MjiniMagharibi Unguja, Dk.Karume alisema kwamba CCMhaijalala hivyo wanachamawa CCM hawana sababu yakuwa na hofu na Uamshokwani wao hawakulala nawenye kuamshwa ni walewaliolala.“Kwani nyie mmelalampaka muamshwe, nyie mkomacho eti…hao ni kama walewanaoamsha daku utakasirika,lakini ukiamka unasema ahaakumbe muda wa kula daku;tena hofu ya nini?” AlisemaDk. Karume na kuwachekeshawaliohudhuria mkutano huo.Makamu huyo Mwenyekitialilazimika kutoa maelezohayo baada ya Mwenyekitiwa CCM Wilaya ya MjiniUnguja, Borafia SilimaJuma kueleza wasiwasi wawanachama wa CCM kuhusuvurugu zilizotokea mwezi Meimwaka huu na kuhusishwa nakundi la Uamsho.Dk. Karume akijibu hilo,alisema juhudi za kuiwekaZanzibar katika hali yamaelewano ilifanywa naJumuiya za Kimataifa naMataifa kutoka nje, lakinihawakuweza kusuluhishamigororo ya kisiasa iliyodumukwa takriban miongo mitatu,lakini baada ya Wazanzibariwenyewe kuamua kuachatofauti zao maridhianoyalifikiwa mwaka 2009.Akitoa historia feru namiafaka na maridhiano, Dk.Karume alisema wakati wautawala wake walihakikishakabla ya kumaliza kipindicha utawala wake anaiwachaZanzibar ikiwa salama, yenyeumoja na mshikamano naisiyokuwa ya vipande vipandeambapo hali hiyo ilifanikishwa baada ya kufikiwa kwamaridhiano ya kisiasa bainaya Chama ch Wananchi (CUF)na Chama cha Mapinduzi(CCM).“Mimi na Katibu Mkuuwa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad tulikutana Ikulu nakukazungumza kwa ninitusimalize tofauti zetu maanasisi sote ni wamoja na leomafanikio yake ndio haya yaZanzibar imetulia kwa hivyonatoa wito wa kuendelezaumoja huu”. Alisema Dk.Karume.Akizungumzia suala lamaoni kuhusu Muungano,Makamu huyo Mwenyekitiwa CCM alisema watu wotewanaotoa maoni kimsingiwanatumia haki ya kikatibana kidemokrasia hivyo wanaCCM wanachotakiwa nikuendelea kusimamia azmaya ujenzi wa chama chaohuku wakiendelea kuheshimumisimamo yao bila yakuyumbishwa.“Msipatwe na homa,ondoeni hofu na wasiwasi, waacheni Masheikhwajibishane na Masheikhwenzao na sisi wanasiasatutafute majibu mujarabyatakayofaa ikiwa ni pamojana kuwaelimisha vijana wetukutambua mahali tulikotoka,tulipo sasa na kule tuendako”,alisema.Mkutano huo uliofanyikakatika Tawi la Gulioni ambakoalizungumza na wanachamawa matawi mawili la Gulioni naMwembeladu ni wanachamawachache waliohudhuriatofauti na matarajio ya watuwengi ambapo kuliwekwamabomba nje ya tawi hilolakini wasikilizaji walikuwakidogo mno.Viongozi walioambatanana Dk. Karume ni pamojana Mwenyekiti wa CCMMkoa wa Mjini, Yussuf Mohammed, Mwenyekiti waCCM wilaya ya Mjini BorafyaSilima, Mbunge wa Rahaleo,Abdallah Juma Abdallah(Maabodi), na Mwakilishiwake Salim Nassor (Aljazira),
 
3
 AN-NUUR
SHAABAN 1433, IJUMAA JULAI 6 - 7, 2012
Habari
ZIPO taarifa kuwaWaislamu nchini wanapangakufanya maandamanonchini kupinga kitendo chakudhalilishwa Sheikh waoNurdeen Kishki pamoja naMasheikh wengine aliokuwanao.
Habari zinasema kuwalengo jingine ni pamoja nakumtaka Kamanda wa PolisiMkoa wa Pwani kuombaradhi kwa udhalilishaji huona serikali kutoa tamko lakukemea kitendo hicho.Kwa mujibu wa taarifazilizopatikana tukiendamitaani, kuna vikao vyaushauri vinaendelea katikaMisikiti, Taasisi na Jumuiyambalimbali za Kiislamuambapo baadae itafanyikaShura ya pamoja kuamua ninila kufanya juu ya kadhia hii.Shura na vikao hivovinakuja kufuatia taarifa yakukamatwa na kudhalilishwaSheikh Nurdin Kishki.Tukio hilo limeelezwakuwa ni katika kuendelezamwitikio wa kile kinachoitwamapambano dhidi ya ugaidi.Katika tukio hilo,Sheikh Nurdin Kishki naMasheikh wenzake wakiwawameambatana na ujumbewa Masheikh kutoka Yemenakiwemo Mufti wa Yemen, juzi Jumatano walifanyiwaudhalili mkubwa na polisi baada ya kukamatwa nakudaiwa kuwa ni majambazi.Wakiwa njiani kutokeaTanga kuja jijini Dar esSalaam, Sheikh Kishki nawenzake walivamiwa na polisi Bagamoyo mkoaniPwani na kuamriwa kulalachini huku wakisukwasukwa wakishukiwa kuwa nimajambazi.Umati wa watu wakiwemowatoto wadogo walijazanakatika eneo la tukio kushuhudiaMasheikh hao baada yataarifa kuzagaa kwambawatu wanaodhaniwa kuwani majambazi wamekamatwana polisi.Hata hivyo wengiwalishangaa na kupigwa na butwaa baada ya kukuta kuwawatu waliokuwa wakishukiwakuwa ni majambazi, walikuwani Masheikh akiwemo Muftiwa Yemen, ambao walikuwawamelazwa chini huku polisiwakiwazingira chini ya ulinzimkali.Hata baada yaMasheikh hao kujieleza nakujitambulisha kwamba waosio majambazi kama taarifaza polisi zinavyosema bali niMasheikh waliokuwa safarinikuja Dar es Salaam, utetezihuo haukutosha kuwafanya polisi kuacha kuwadhalilishakwani waliendelea kupigwa
Na Shaaban Rajab
na kugaragazwa sakafunikama majambazi.Hata hivyo taarifa zinaelezakuwa taarifa zilipelekwa kwaMkuu wa Mkoa wa PwaniBi. Mwantum Mahiza ilikuja kuingilia kati tukio hilokufuatia askari waliowakamatamashekh hao kuendeleakushikilia msimamo wao wakuwadhalilisha.Shuhuda mmoja wa tukiohilo alieleza kuwa kufuatiaMkuu wa Mkoa kupewataarifa hiyo, alijibu kuwatayari amemwagiza OCDwa Wilaya ya Bagamoyokuchushughulikia mkasa huohivyo Waislamu wavute subraOCD huyo hadi atakapofikamkuu huyo katika kituo cha polisi Bagamoyo ambakondiko Sheikh Kishki nawenzake wanashikiliwa.Wakati Mkuu huyo waPolisi Wilaya akisubiriwa,Waislamu walishamiminikakituoni hapo kujua hatma yaMasheikh hao.Kufuatia umati kuwamkubwa, polisi waliamuruWaislamu kuondoka maramoja kituoni hapo lakiniwaligoma na kusisitizakwamba hawawezi kuondokahadi wafahamu sababu yakukamatwa Masheikh hao nakujua hatma yao.Hata hivyo baada ya polisihutakiwa kueleza ni kwa niniwamefikia kuwadhalilishaMasheikh hao bila kuwa naudhibitisho wa makosa, polisiwalidai kuwa wao wamepatataarifa (information) kutokaTanga kwamba kunamajambazi wanakuja. Hatahivyo hawakufafanua zaidi.Akizungumzia katikatukio hilo, Sheikh NurdinKishki alisema kuwa tukiohilo limewadhalilisha sanaMashekh hao na viongoziwa Waislamu na Waislamukwa ujumla hivyo amemtakaInspekta Janerali wa Jeshi laPolisi nchini, Said Mwemakufanya uchunguzi mapemana maofisa waliowadhalilishawachukuliwe hatua maramoja. Alisema udhalilishwajihuo kamwe hautakaliwakimya.Alisema hata kama maofisahao wa polisi walikuwawanawashuku, hawakustahilikuwaburuza na kuwalalishachini kama wahuni.“Kama wametushukuna walikuwa wamekusudiakufanya uchunguzi dhidiyetu, wangetuhoji kistaarabuhapo kituoni kwao nakama hawakuridhika, basiwangetuhifadhi kistaarabu kwakuwa tayari tulikuwa kituoni,naamini kama wangekuwani Mapadri udhalilishwajihuu usingefanyika hata kamawangeshukiwa ujambazi.Lakini kwa kuwa Kishkiamevaa kanzu ana kofia nakilemba, basi hao ndio, wakulazwa chini, kupigwa,kufanyiwa kejeli, tena tukiwana wageni wetu kutoka nje yanchi, hili latosha kuwafanyaWaislamu watambue kuwahivi ndivyo wao na viongoziwao wanavyohudumiwakwa sababu ya itikadi yao”.Alibainisha Kishki Naye Sheikh WaziMaduga alisema kuwa tukiola kudhalilisha Masheikhakiwemo Mufti wa Yemen, niagenda ya kuwatoa Waislamukatika mada zao ya msingihivi sasa ya kutoshiriki zoezila sensa na kutaka Baraza laMitihani nchini livunjwe.Alisema msimamo namaamuzi ya Waislamuyataendela kubakia pale palehata zikiletwa agenda zakutengenezwa ili kuwahamishaWaislamu katika msimamowao.Alisema, Masheikhwanaojipendekeza serikalihuku serikali hiyo hiyoikija kuwadhuru Waislamu,wao waendelee na njia yaohiyo kwani Waislamu tayariwamejiweka katika njia yaonyingine ya haki katika kudaihaki zao na watabaki katikakutetea haki zao hizo.Hata hivyo Waislamuwengi wanaamini kuwasababu kubwa ya kukamatwaSheikh Kishki na wenzakeni zilezile zilizozoeleka zakuhusishwa na ugaidi, japosafari hii polisi wamejaribukupamba sababu hizo kwaujambazi.
HAPANA shaka hivi sasaWaislamu watakuwawanatokota kwa hasira.Wanajiuliza, vipi ingekuwamsafara wa MchungajiZakaria Kakobe, Polisiwangemkamata nakumburura chini?
Vipi ingekuwa ni msafarawa mapadiri na Kanzu zaoza Kipadiri na misalaba yaoshingoni, Kamanda Ernestiangewatuhumu kuwa nimajambazi na kuwalaza chinikifudifudi na kuwagaragarazakatika vumbi?Waislamu wanajiulizamaswali haya baada yakupata habari kuwa Sheikh Nurdeen Kishki na msafara waMasheikh wengine aliokuwanao, walikamatwa na polisi juzi na kudhalilishwa. Ni kutokana na taarifahizo, Waislamu wanajiuliza,hivi ungekuwa msafarawa mchungaji SylvestaGamanywa na watumishi waMungu wenzake, Kamandawa Polisi Mkoa wa Pwani,Afande Ernesti angewafanyiauhuni na udhalilishaji huualiowafanyia Masheikhwetu?Japo zimetajwa tuhumaza ujambazi, lakinikinachojidhihirisha ni kuwa
Maandamano makubwakufanyika nchi nzima
Muoneeni huruma Kamanda Ernesti
Hakudhalilishwa Kishki pekeeHata Mkapa alishadhalilishwa
Na Omar Msangi
walidhaniwa kuwa ‘magaidi.’Sheikh Kishki anafahamika.Polisi hasa katika ngaziya makamanda wa mikoawanamjua sana kutokana namihadhara yake na kanda zakezilizosambaa nchi nzima.Kishki alikuwa akitokeaArusha na Tanga na kotehuko Polisi walikuwepo nawalimwona akitoa mawaidha,akiongea na Waislamu. Kwahiyo suala la Kamanda waPwani kupewa taarifa nayule wa Tanga kwamba kunamajambazi yanakuja kamaAfande Ernest anavyodaihalipo. Ni uwongo.Lakini Kishki alikuwa naMasheikh kutoka Yemen na‘Yemen ni nchi ya magaidi’kama ilivyo ‘Pakistan’ na‘Afghanistan’. Na hii sikwa mujibu wa taarifa zakiusalama za akina Ernestna wanausalama wetu waTanzania kwa ujumla.Lakini kwa mujibu wamaelezo tunayopewa kutokaWashington na kwa mujibuwa “False Flag Terror Attacks”zinazoendelea kutekelezwakatika nchi hizo. Nina wasiwasi, na nina hakiya kuwa na wasiwasi, kuwaudhalilishaji waliofanyiwaMasheikh wetu paleBagamoyo, hayakutokana nataarifa za kikachero za Polisiwetu. Japo waliotekeleza niwao, na hawawezi kuepukalawama, lakini inavyoonekanawalikuwa wakitekelezamaelekezo kama yalewaliyopewa wakawakamataWatanzania wenzetu wasio nahatia wakati akija Bush.Inavyoonekana Polisiwetu waliomgaragazaSheikh Kishki, walishindwakukataa kutekeleza maelekezowaliyopewa kama ambavyowalishindwa kuzuiya mbwawa Marekani kumdhalilishaMheshimiwa BenjaminWilliam Mkapa na kamawalivyoshindwa kuwazuiyamakachero wa Marekanikupanda darini Ikulu nchinimwetu.Kwa hiyo, pamoja nahasira ambazo watakuwanazo Waislamu hivi sasa,lakini binafsi naona badala yakukasirika, pengine ingekuwavema zaidi kuwaonea hurumahawa akina Ernest maanawakati mwingine wanakuwahawajui walifanyalo.Kama tutatanguliza hasira,tutakosa huruma kwa wenzetuhawa halafu tutashindwakuwasaidia na hasara itakuwa pia juu yetu na kwa nchi yetukwa ujumla.Wakati tukitafakari kadhiahii ya kudhalilishwa Sheikhwetu Kishki, ndio nikasematukumbuke pia kile kisa chakudhalilishwa aliyekuwa Raiswetu Mheshimiwa BenjaminWilliam Mkapa pale Arushaambapo mbwa wa polisiwa Marekani walinusa garilake ili kuhakikisha kuwahapakuwa na gaidi ndani au bomu la kigaidi ambalo laulingelipuka, lingemdhuruBwana Mkubwa kutokaMarekani, Bill Clinton!Katika tukio lile, akinaErnesti wetu walikuwepo nahata vyombo vya usalama vyanchi yetu, lakini hawakuwezakumsaidia Rais wetuasidhalilishwe.Ukitaka kujua uzito wa jambo hili, hebu jaaliya rafiki
Inaendelea Uk. 10

Activity (5)

You've already reviewed this. Edit your review.
1 hundred reads
1 thousand reads
Mushrif Chorah added this note
mufti tanzania,kwanini usikae chini na masheikh ili kupata maamuzi sahihi,wewe sio kilakitu kwa waislam ndugu yangu,kumbuka kidole kimoja hakivunji chawa mzee,,arusha upingwe na mikoa mingine hata morogoro pia?mzee fungua macho na kuhitaji ushayri babaaa

You're Reading a Free Preview

Download
scribd
/*********** DO NOT ALTER ANYTHING BELOW THIS LINE ! ************/ var s_code=s.t();if(s_code)document.write(s_code)//-->