You are on page 1of 127

ZANZIBAR DOLA, TAIFA NA NCHI HURU

by

Dr. Yussuf S. Salim

Zanzibar Center of Human and Democratic Rights

(Kituo cha haki za Kibinaadam na Kidemokrasia Zanzibar)

Engvadvej 26

2650 Hvidovre

Denmark.

c Yussuf S. Salim
Table of Contents

Table of Contents i

1 ZANZIBAR NI NCHI NA TAIFA HURU 2

1.1 Utangulizi  2

1.1.1 Zanzibar ya kale  2

2 DOLA LA ZANZIBAR 4

2.1 Dola la Zanzibar  4

2.2 Muungano - kisheria na kisiasa  6

2.3 Misingi ya vyama vya kisiasa Zanzibar  7

2.4 Mzizi wa fitina  8

2.5 Utumwa  11

2.6 Utumwa na Uislaam  16

2.7 Ubepari  19

3 USULTANI NA UKOLONI 24

3.1 
Usultani wa jana na Utawala (Usultani) wa leo 24

3.2 Kumiliki Ardhi Zanzibar  25

3.3 Wahindi kudhibiti uchumi  29

3.4 Mngereza na mfumo wa matabaka  30

3.5 Vyama vya kisiasa kabla ya Mapinduzi  31

3.6 Muamko wa kudai uhuru  34

3.7 Upiganiaji Uhuru  36

i
3.8 Umma Party  44

3.9 Zanzibar kama tausi  47

3.10 Vugu vugu jipya la Upinzani  48

3.11 Serikali ya taifa  55

3.12 Malumpa wa Zanzibar  59

3.13 Mgomo wa 1948  61

4 MAPINDUZI 63

4.1 Siri ya Mapinduzi ya 1964 63

4.2 Haja ya Mfumo halali  72

4.3 Mapinduzi yalitekwa nyara  75

4.4 Afro-shirazi  77

4.5 Aboud Jumbe  78

4.6 Makosa ya Umma Party  80

5 MUUNGANO 84

5.1 Umma Party na Muungano  84

5.2 Makosa ya Mapinduzi  87

5.3 Vuguvugu la Venceremos  90

5.4 Awamu tafauti  96

5.5 Migogoro ya Nyerere na Karume  98

5.6 Tanganyika imepigwa kamba  102

5.7 CCM hazina ya baa na balaa  105

6 MFUMO MPYA 113

ii
6.1 CUF AU ZUF ?  113

6.2 Vyama vya Upinzani vya Tanganyika  117

6.3 Matarajio ya Mzanzibari  119

6.4 Demokrasia  122

1
Chapter 1

ZANZIBAR NI NCHI NA TAIFA HURU

ZANZIBAR DOLA,TAIFA NA NCHI HURU

1.1 Utangulizi

1.1.1 Zanzibar ya kale

Kiasi cha miaka millioni mia moja na khamsini (150 million) iliyopita Barahindi ilikuwa

ni sehemu ya Bara la Afrika na hatimae baada ya mgawanyiko wa pole pole wa ardhi,

Barahindi ikaelea elea hadi kujiegeza na ile milima leo ijulikanayo kama Milima ya Hi-

malaya. Ardhi na nafaka za Barahindi, miti na misitu yake, ufukwe wake wa pwani

uliyojaa minazi, viungo vyake (pili pili, mabizari, karafuu, mdalaasini, hiliki, achari to-

fauti n.k.), matunda yake (shoki shoki, madoriani, matufaa, embe), ndege wake, vinyama

vyake (komba, manyani, makima na tumbili), wanyama wake (tembo na chui) vyote hivi

vimefanana mno na hali ya Zanzibar, ingawa tembo na chui, kama vile nyangumi, kasa,

kobe na mamba, wametoweka Zanzibar kutokana na usasi wa kibiashara wa vipusa. Mi-

fano ya ardhi, wanyama na kadhalika kama hao wanaonekana sehemu mbali mbali za

mashariki ya karibu na za mashariki ya mbali kama Sri Lanka, Singapore, Malaysia,

Indonesia n.k.; wakati Malagasy, Ngazija na Mroni, Sheli-sheli (Seychalles), Sokotra

n.k. zikiwa mashariki ya kando, zina mlingano kama huo na Zanzibar. Kuna baadhi ya

wataalam wananakili kwamba visiwa viwili vya Unguja na Pemba vinatokana na asili

2
tofauti, wataalamu hao inaonyesha wamesahau kwamba asili ya Barahindi inaambatana

na ufukwe wa Mashariki ya Afrika, vile vile wataalam hao, na wale wanaowakariri,

kwa sababu zao za kisiasa, wakijaribu kuuhalalisha Muungano, wanasahau tofauti ya

ardhi ya kusini Unguja yaani Makunduchi/Mtende/ Kibuteni/Kizimkazi, zikiwa na udongo

mwekundu na mawe na majabali, ikifananishwa na ardhi za Unguja ya kati na ya kaskazini

zikiwa na rutuba tofauti. Kwa mujib wa historia ya kale ya enzi zetu, kuambatana na maan-

dishi ya "Perpulus of the Erythran Sea" na "Claudius Ptolemy", Edris, Chronicles of Kilwa

n.k. Zanzibar (Menouthias Island) ikijulikana kama nchi iliyokuwa na biashara na nchi

mbali mbali za Arabuni, Barahindi, Uchina na Japan tokea enzi za kale. Katika maandishi

hayo ambayo ni katiya ya zamani kabisa kuhusu Afrika ya Mashariki hakujatajwa nchi

au taifa lijulikanalo kama Tanganyika. Hadi April 28, katika mwaka wa 1885, sehemu

ya Mrima ikijuli kana kama ni Mamlaka ya Bara ya Sultani wa Zanzibar. Tarehe hiyo

yaani 28 April, mwaka 1885 ndiyo tarehe Serikali ya Kijarumani alipoamua kuzinyakuwa

maili 60,000 za eneo la Mrima. Baada ya hapo ndipo makubaliano baina ya Mngereza

na Mjarumani yakafikiwa, Muingereza ikachukuwa Hegoland, kama kiinuwa mgongo, na

Mjerumani kuchukuwa Mrima. Unyakuwaji wa Wazungu wa ardhi ya Bara la Afrika, uli-

tokea baada ya Mfalme wa Belgium kuitisha mkutano wa nchi zilokuwa zikiongoza Ulaya

katika mwaka 1876, huko Brussels, Ubelgiji. Muda mrefu sana kabla ya hapo Zanzibar

ilikwisha julikana kama ni nchi, taifa na dola kamili, kinyume na Tanganyika.

3
Chapter 2

DOLA LA ZANZIBAR

2.1 Dola la Zanzibar

Zanzibar ikiwa ni taifa kamili, lina haki kamili ya kuwa na vyama vyake huru vya kisiasa

bila ya kulazimishwa kuungana na chama chochote cha Taifa la Tanganyika, ambalo vile

vile ni taifa huru. Taifa, Dola au Nchi haziundwi kutokana na ndoto za mtu mmoja au

watu wachache. Ili taifa litambulike kama taifa, kunahitajika sifa maalum za lazima na

sio za kulazimishwa, kuzushwa au kubuniwa. Kwa mujib wa sifa za kimataifa Zanzibar

ni nchi na taifa kamili – bila ya kujali nani ana au wanabuni vyengine. Nchi ye nye

mipaka inayotambulika kimataifa, na kuwa na watu wenye sifa maalum za nchi hiyo, kwa

kusema lugha inayotambulika kuwa lugha ya au za nchi hiyo, yenye utamaduni na kabila

au makabila ya nchi hiyo, yenye jamii halisi na makhsusan, siasa inayoifuata na uchumi

wake wa kujitegemea wenyewe, inatambulika kama ni nchi, aidha ikiwa huru au ikiwa

imetawaliwa, yaani kama Zanzibar ilivyokuwa chini ya ukoloni wa Kiingereza (na hata

ukoloni wa sasa). Nchi kama hiyo ikiwa huru inatambulika na Umoja wa Mataifa kama ni

Nchi na Taifa huru.

Bila ya haja ya kukariri zaidi Zanzibar inazo sifa zote ambazo zina hitajika ili nchi itam-

bulike kama taifa huru, pamoja na kuwa na kiti chake katika Umoja wa Mataifa, ambacho

kipo wazi tokea kuundwa Muungano katika mwaka 1964. Kabla ya kuruhusiwa mfumo

wa vyama vingi vya kisiasa Tanzania, Zanzibar iliwekewa pingamizi na vikwazo vya

kutounda vyama vyake huru, na ilihitajika na kulazimika kwamba vile vyama vitakavy-

4
oundwa viwe na sifa za "Kitaifa" na visiwevya kijimbo, kidini n.k. kama alivyobuni Julius

K. Nyerere. Kwa vile nchi ilikuwa chini ya utawala wa chama kimoja chenye kawli na

amri ya mwisho, Wazanzibari na Watanganyika ikawabidi, shingo upande wafuate kauli

na amri ya watawala wao, wananchi wa nchi mbili hizo wakisubiri kwa hamu kubwa,

siku mambo yatakavyobadilika, na hatimae kuyabadilisha masharti hayo. Wengi zaidi

ya Wazanzibari na Watanganyika, ambao pia ni wenye sifa za kuwa nchi na taifa huru,

hawakuamini kwamba Tanzania ni nchi au ni taifa, kama isemekanavyo. Tanzania ni nchi

na taifa la kubuni, kama taifa la ndotoni na sio nchi au taifa halisi kwa mujib wa tafsiri za

kimataifa zinavyotambulika.

Tanzania si nchi wala si dola, bali ni Muungano wa nchi/taifa mbili huru zote mbili zi-

likuwa na uwakilishaji kamili katika Jumuiya ya Madola.Muungano wa Tanzania ni sawa

na Muungano wa Misri na Syria,"United Arab Republic" ambao umeshavunjika kwa hivi

sasa na kubaki jina tupu, na kila nchi kuwa na mamlaka yake wenyewe. Mfano mwengine

ni Muungano au shirikisho la Kisovieti-ambalo limeshamungunyika na mfano mwengine

ukiwa Muungano/shirikisho la iliyokuwa Yugoslavia;- tofauti na hali hiyo ni Vietnam am-

bayo ni nchi mmoja na imeshaungana, wakati Korea ikiwa na serikali mbili katika nchi

moja zilizotengwa na ukoloni kwa maslahi ya kikoloni. Muungano wa Tanzania ni sawa

na muungano wa Uingereza na Ireland ya kaskazini yaani baina ya mtawala na mtawaliwa,

ingawa Ireland inaweza kuunda vyama vyenye sifa ya Kiireland tofauti na Zanzibar. Mtu

au Chama tawala kinaweza kulazimisha watu wafuate na kuitii fikra au sheria fulani,

lakini hawawezi kulazimisha watu kuamini fikra hiyo ya kubuni, kama vile mtu anaweza

kula zimishwa kuamini kuwa nyoka ana miguu, lakini kutoweza kumfanya mtu huyo

aamini hivyo. Mzanzibari ni rahisi kulazimishwa kukariri kuwa Zanzibar si nchi wala

dola bali si rahisi kumfanya aamini hivyo. Kulazimisha uundaji wa vyama viitwavyo vya

5
kitaifa baina Tanganyika na Zanzibari ni kitendo kisichokuwa cha kihalali, kisichokuwa

na msingi na ni kitendo potofu. Hatua nyingi za kisiasa ni hatuwa za muda na za kupita,

sio hatua za kimaumbile; ni hatua zinazotungwa na kupitishwa na binaadam na kila kina-

choundwa na binaadam kinaweza kubadilishwa yaani si cha milele au cha kudra na lazima

kama roho. Mwenye Enzi Mungu ndie anayeumba binaadam na kuwapa roho na maisha,

kuwapa uume na uke, na kuwapa makabila na sura ili wajuane. Vile vile kuwapa viton-

goji, vijiji, mashamba na miji, nchi na mataifa ili waishi pamoja, wajiongoze, kujitawala

na kuheshimiana. Ikiwa mtu au watu watachukuwa wadhifa wa Mwenye Enzi Mungu,

ata au watakuwa wanakosea na yale watakayo ya jaribu kuyabadilisha yatawashinda na

hatimae kuwarudi. Nchi, kiini cha taifa, haiundwi kama ilivyokuwa watu hawaundwi

bali huumbwa. Majaribio ya kutaka kuliumba taifa la Tanzania yamezidi kuwa katika

sarakati ’lmawti (likikata roho) tokea Watanganyika walipozidi kuvinjari na kulidai taifa

lao wenyewe na Bunge lao wenyewe. Khatua hii imedhihirisha zaidi kukuwepo kwa

mataifa mawili huru, kinyume na madai ya hapo kabla kwamba Taifa lilikuwa ni moja tu.

Sasa wimbo wa kuwasingizia Wazanzibari kutaka kujitenga umeanza kupunguwa kasi na

ukweli wa mataifa mawili huru yaliyoungana, kuzidi kujichomoza. Zaidi ya yote hayo

mara nyingi watu husahau kwamba Tanzania si nchi bali ni: "Jamhuri ya Muungano wa

TanZania, "iliyoundwa kwa makubaliano ya watu wawili tu, Nyerere na Karume.

2.2 Muungano - kisheria na kisiasa

Mijadala mirefu na mingi ya kisheri imekaririwa kuhusu Muungano wa Tanzania, karibu

yote ya mijadala hiyo ikipinga uhalali wa kisheria wa uundaji wa Muungano huo. Wengine

badala yake kuuita uharamia wa kisheria na wa kisiasa.

6
Uchambuzi huo wa kisheria umesaidia kufafanua mambo mengi ya maana, ingawa bado

tunasubiri kauli sahih za baadhi ya wanasiasa waliyoshuhudia namna ya utekelezaji wa

tukio hilo. Kwa sababu ya pungufu za uhuru wa kutoa maoni na demokrasia kwa jumla,

mjadala wa suala hili muhimu wa kisiasa umekuwa pungufu na dufu. Kuna mambo mengi

mno ambayo hayajagusiwa kabisa kuhusu misingi ya uundaji ya Muungano huu. Itakuwa

ni jambo la maana sana ikiwa kutatupwa mchanga wa moto ili kuzidi kushajiisha mjadala

wa suala hili muhimu sana. Njia moja wapo, ambayo sio lazima ya pekee, itakayosaidia

kutupia nuru suala hili ni kujaribu kulidadisi suala hili kwa historia ya kisiasa ya chama cha

Afro shirazi Party, uundaji wake, siasa na maisha yake, kushiriki kwake kwenye mapinduzi

na katika Baraza la Mapinduzi na hatimae kuunganishwa na TANU.

2.3 Misingi ya vyama vya kisiasa Zanzibar

Ili kupata ufafanuzi kamili, madhubuti na wa kinaganaga kuhusu asili na misingi ya vyama

vya kisiasa Zanzibar, hapana budi kutafuta msaada kutokana na historia ya Zanzibar kwa

jumla na historia ya tawala zake makhsusan. Historia ya Zanzibar hasa ya kisiasa ina

upungufu mkubwa, na inahitaji uchunguzi na uchambuzi wa makini wa kisayansi na ulio

huru. Uchunguzi huu ni mgumu sana kwani mara nyingi utafiti wa historia unapambwa

kupendeza utawala uliyopo kama utakuwa unaandikwa wakati utawala wenyewe ukiwa

khatamuni, au kuambatana na aina ya siasa au idiologia ya muandishi au ya utawala unao-

husika. Kuna watu wengi wana nadharia ya kuweza kuandika au kushiriki katika uandikaji

wa historia ya punde ya Zanzibar, lakini ama wamekuwa wakiogopa kutokana na utawala

katili wa Zanzibar au utawala kandamizi wa Muungano, au kupungukwa na hamasa za

kisiasa waliyokuwa nazo watu hao kiasi cha miaka 30 na 40 iliyopita. Kuna wengine

7
wanachelea kuandika kwa sababu ya mazoefu mabaya ya usiri au kungojea mabadiliko

ya serikali, mambo ambayo ama yanapotosha historia kutokana na upungufu wa kuweza

kukumbuka au kutokana na vifo ama vya kawaida au vya kuuwawa kutokana na sababu

za kisiasa. Vile vile usiri huo unasaidia serikali za kikandamizaji kuzidi kubaki katika

utawala kwa vile wananchi wanakuwa hawaujuwi ukweli sahih uliyopitika nchini.

Ni matumaini ya kijitabu hichi kwamba, wale wenye ujuzi wa kihistoria muhimu wata-

jitokeza na kuchangia kumbukumbu muhimu kama hii na kwa hivyo kuwafichuwa wale

wanaoandika historia ya uwongo na ya kupendeza watawala. Ni jambo la maana kwa

hivyo kudokeza kidogo juu ya mgawanyiko wa jamii ya Kizanzibari wa tokea enzi za kale

ili kufahamu mfumo wa matabaka yaliyosababishwa na mgawanyiko wa jamii hizo. Hichi

ni kijitabu kidogo ambacho hakiwezi kuieleza au kuifafanua historia ya Zanzibar ambayo

ni nyingi na ya kupepea. Kijitabu hichi hakidai kutoelemea upande fulani wa kiidiologia,

ingawaje kinajaribu kwa kadri inavyowezekana kuchambua hali halisi na ya kinaganaga

ili kutoa mwangaza katika mambo fulani ambayo ingawa wengi wanayajuwa, lakini bado

hawajaamuwa kuyaeleza.

2.4 Mzizi wa fititna

Mzizi wa fitina wa siasa ya Zanzibar uko katika historia, na kabla mzizi huu haujakatwa

hapatokuwa na maendeleo ya maana ya kuwanufaisha Wazanzibari kwa jumla. Zanzibar ni

nchi yenye historia ndefu na nyingi, hasa kufananisha na eneo lake, ilitajirika kutokana na

maingiliano yake na kila aina ya watu wenye sifa mbali mbali bora na za kupigiwa mifano,

watu waliyotoka sehemu mbali mbali ulimwenguni. Kuingiliana kwa Wazanzibari na

8
staarabu mbali mbali tokea nyakati kabla kuzaliwa Nabii Issa I‘bn Mariam, kumeifanya

Zanzibar iwe sehemu mojawapo yenye sifa njema na ustaarab wa kuwekewa mfano. Katika

watu wa kale waliyotajika na waliyovuma kwa kiwango cha juu cha ustaarabu na elimu

ilikuwa ni Machina, Wahindi, Wamisri na Wagirigi. Zanzibar ilifaidika kupata matunda ya

staarabu hizo tokea enzi za kale. Zanzibar ilitembelewa na wataalamu na wafanya biashara

na wavuvi kutoka sehemu mbali mbali ulimwenguni, na baadhi yao walipendezwa na

majira hayo na utu wa majira hayo na kuamuwa kugeuza Zanzibar makwao na kutotaka

kurudi tena walikozaliwa, hapo wakaowa na kuzaliana na kuchanganya damu. Wengi wa

hao walitoka sehemu za Arabuni, Uajemi, Barahindi, Uchina n.k. Wengi wao walikuwa ni

wafanya biashara, wavuvi, mafundi, maagenti, wataalam na wana ahli l kitaab. Misafara

hiyo na uhamiaji huo ulitokea zaidi ya miaka elfu mbili iliyopita kabla ya utawala wa

Mashirazi, Wareno, Waomani au Wangereza; ingawa kuja kwa watawala hao baadae

nako kulichangia na kuhaibisha ustaarabu na utamaduni wa Zanzibar kwa kiwango fulani.

Wahamiaji kutoka Arabuni, Barahindi na Shiraz walihamia Zanzibar kwa sababu tofauti.

Wahamiaji wa Kishirazi wa mwanzo katika Afrika ya Mashariki wanasemekana waliwasili

Afrika ya Mashariki katika karne ya sita (The Arab Chronicles of Kilwa). Wahamiaji ha

wa walihama makwao ama kwa sababu za kisiasa, kidini au kibiashara. Katika karne ya

10 baada ya vita vya ukhalifa huko Uajemi, Sultan Hassan wa Shiraz pamoja na wanawe

sita wa kiume na majahazi yao saba kwa jumla yalitweka kutoka Shirazi, huko Uajemi, leo

kujilikanako kama Iran, yakaelekea Afrika ya Mashariki. Baada ya ku wasili pwani pwani

mwa Afrika ya Mashariki Washirazi hawa wakaendeleza utawala wao wa kifalme katika

Afrika ya Mashariki. Ishara na kumbukumbu zake bado ziko dhahiri pwani pwani mwa

Afrika ya Mashariki yote. Ukumbusho madhubuti katika visiwa vya Unguja na Pemba ni

ule wa Ufalme wa Mwinyi Mkuu, mfano mwema wa Mzanzibari aliyechanganya damu

9
akiwa na asili ya Kishirazi na Kizanzibari. Karne tano zilipita kabla Wazungu kuishitukia

Afrika ya Mashariki na Kati na mapambano makubwa ya mwanzo aliyoyapata Mwinyi

Mkuu yalikuwa alipopambana na mkoloni wa Kireno (Ruy Lourenco Ravasco 1503) katika

Unguja Ukuu, ambako kwa wakati huo ulikuwa ndio mji mkuu wa Zanzibar na baada ya

kushindwa na kusalim amri Wazanzibari hao na Mfalme wao walilazimishwa kulipa kodi

ya kila mwaka kwa mfalme wa Ureno. Katika mwaka 1509, mkoloni wa kireno, Duarte

deLemos, aliwasili Zanzibar kudai ushuru au kodi hiyo kuto ka kwa Wazanzibari, ambao

waligoma kulipa kodi hiyo, na hapo pakapigwa vita dhidi ya majeshi ya Kireno yaliyokuwa

na silaha bora zaidi za mabunduki na mizinga. Wazanzibari wakashindwa kwa mara ya

pili, kukimbilia misituni, huku nyuma Wareno wakaendelea na kwiba, kunyang’anya,

kuteketeza na kufisidi. Vita hivyo vilimfanya Mwinyi Mkuu akimbize watu wake na

ufalme wake kutoka katika ufukwe wa bahari na kujifichia maporini na hatimae kujenga

ngome yake huko Dunga

Kwa mara ya mwanzo, Wareno walipowasili Afrika ya Mashariki walistaajabishwa sana

na kiwango cha juu cha ustaarab. Kukuta mavazi ya haiba, ya lasi na haririr ya tunu na

tamashana, ujenzi wa sifa na ustadi wa kifani, uliyopendeza na kupambika. Wakakuta

ustaarabu uliyozalika kutokana na maingiliano ya karne na karne baina ya Afrika ya

Mashariki na madola ya mashariki ya kati hadi mashariki ya mbali, kutoka Yemen hadi

Uchina na Japan. Wareno, kabla kufika Afrika ya Mashariki, walipitia Afrika ya Magharibi,

na walitarajia kuikuta Afrika ya Mashariki katika kiwango cha ustaarabu sawa na ule

waliyoukuta Afrika ya Magharibi, lakini walistaajabishwa mno na kupigwa na mshangao

kukuta majenzi na mavazi ya haiba na kupendeza kabisa, na Wanaafrika wa Mashariki

walidharau kwa kejeli thamani ya zawadi walizoletewa na Wareno hao. Zanzibar kwa

wakati wote kabla ya hapo, yaani kabla hata ya kuzaliwa kwa Nabii Issa, lilikuwa ni

10
soko muhimu sana katika Afrika ya Mashariki na ya Kati, na kushughulika na biashara ya

vipusa, ngozi, nyangumi, miti, nafaka, mbao n.k.

2.5 Utumwa

Utumwa ni mojawapo katika njia za kuzalisha mali iliyotumika sehemu zote ulimwen-

guni. Wazungu mwanzo kuwafanya wazungu wenziwao watumwa, Machina kuwafanya

Machina wenzao, Wahindi kuwafanya wahindi wenzao watumwa na kadhalika. Chanzo

cha utumwa katika jamii zote ilikuwa ni kwa kawaida kushindwa vita, kudaiwa deni

na kutolipa, adhabu kufuatia uhalifu n.k. Wazungu baadae wakasahau kwamba wao

ndio waliyokuwa wahalifu wakubwa kabisa katika kuendeleza utumwa wa watu wao

wenyewe na hatimae wa Waafrika kwa niaba ya msalaba, baadae wakajaribu kuudan-

ganya ulimwengu kwamba wao ndio waliyoondosha utumwa, kutokana na wema wao.

Vile vile walisahau kusema kwamba walipopendekeza kuondoshwa kwa utumwa, ilikuwa

kwa sababu utumwa haukutia faida tena za kiuchumi na ulibidi ubadilishwe na uzalishaji

mali mpya wa "kibwanyenye" uliyoweza kukamuwa wanyonge faida kubwa zaidi bila ya

huruma. Jambo jengine wasilotuambia ni kwamba walikuja makwetu kwa madhumuni

ya kutukalia vichwani kwa kututawalia kisiasa, kiuchumi, kijamii na kitamaduni, kututia

chemere na kutunyonya, na sio kutufanyia wema au kututowa utumwani. Kwa njia ya ku-

dai kukandamiza utumwa manuwari za Kiingereza ziliteketeza na kuchoma moto madau

na majahazi ya wafanya biashara yakiwa yalikuwa na watumwa au bila ya watumwa. Wal-

idai kwamba vile vyombo vilivyokuwa havina watumwa vilichomwa moto kwa sababu

eti vyombo hivyo havikufaa kusafiriwa. Wakati ukweli wenyewe ni kwamba Maafisa hao

walipata mapesa mengi kutoka serikalini walipoteketeza vyombo hivyo, wakati huo huo

11
maafisa hao waliiba na kunyanganya mali za watu kinyume na sheria. Madhumuni hasa ya

khatua hizi ilikuwa ni kukata mshipa wakitovu wa biashara baina ya Afrika ya Mashariki

na nchi za Mashariki ya Bahari ya hindi. Kwa njia kama hizo Mngereza akaweza kuwa

na uhodhi wa uchumi wa Afrika ya Mashariki na Kati, na kuiuwa biashara ya makarne na

makarne baina ya Afrika ya Mashariki na nchi za Bahari ya Hindi. Biashara alizoziwacha

Mngereza kuendelea zilikuwa ni za papa, nguru na n‘gonda, majamvi na mikeka. Wan-

gereza wakati wakidai kupiga vita usafirishaji wa Watumwa kutoka Afrika ya Mashariki,

wakati huo huo waliruhusu uuzaji na uzalishaji mali wa Watumwa katika Bara la Afrika ya

Mashariki na kujinufaisha kisiasa na kiuchumikutokana na faida za utumwa. Ilidhihirika

mwishoni kwamba azma ya ukandamizajiwa utumwa ilikuwa ni kuitawalia Zanzibar, na

kwa vile Zanzibar ilikuwa kiini chautawala na biashara ya Afrika ya Mashariki na ya Kati,

alipiga ndege wawili kwajiwe moja, na kuweza kuuzitawalia nchi zote za sehemu hizo vile

vile.

Kama sehemu nyengine ulimwenguni, Afrika ya Mashariki na Kati ziliendeleza njia ya

kuzalisha mali na biashara ya Utumwa, na Zanzibar ikageuzwa bandari na sokomojawapo

muhimu la watumwa. Bandari, soko na vituo vyengine muhimu vya jiranivikiwa Bag-

amoyo, kwengineko ni Tabora, Kilwa n.k. Wengi wa watumwa hawa amawalibaki Mrima,

kusafirishiwa Arabuni, Uajemi, Barahindi na Visiwa jirani kamavile Seychelles, Re’union,

Ngazija, Mauritius, wengine hadi Marekani, Brazil n.k. Baadhi yao kufanya kazi katika

mashamba ya karafuu, wengine kufanywawachukuzi, mahamali, watumishi wa majum-

bani na kazi kama hizo ndogo ndogo.Ingawa Zanzibar ilikuwa bandari na soko muhimu

la watumwa, watumwa hawahawakutoka Zanzibar bali walitoka Mabara ama kutokana

na kusakwa na kuwindw ana wachuuzi wa watumwa wa Kiarabu na wa Kienyeji, au

kuwa mateka wa vita bainaya machifu, ufalme na makabila mbali mbali yaliyopigana vita,

12
kama vile Wahiyao,Wamakonde, Wamakua, Wandonde n.k., au kutokana na kushindwa

nguvu aukutegwa kwa ujanja wa wenzao. Inasemekana kwamba hakuna Mzanzibari asili-

aaliyeuzwa kama mtumwa, na ndio maana Wazanzibari asilia si watu wanaolimbikizachuki

za kitumwa, kirangi au za kikabila zenye misingi ya kitumwa. Katika mwaka wa kulipi-

tishwa sheria ya kukomesha biashara ya utumwa Zanzibar na watumwa wote kupewa au

kununua uhuru wao. Wengi wa watumwahawa hatimae walirudi mabara na wengi ya wale

waliyobaki walishiriki kikamilifu katika jamii ya Kizanzibari hata kabla ya kuondoshwa

utumwa na kuwa na hisiakamili za Kizanzibari. Ingawa Mngereza akidai kuukomesha

utumwa tokea wakatihuo lakini kwa kweli Wafaransa na Wareno waliendeleza biashara

ya watumwa baadaya hapo na Mngereza hakuinuwa hata ukucha kuwazuwiya wazungu

wenziwe katikabiashara hiyo ovu. Ingawa sheria ya kukomesha utumwa ilipitishwa katika

mwaka 1873, kuambatana na siasa ya ASYL, ya serikali ya Zanzibar na ya CCM, watali-

ihadi leo wanazugwa kwamba ati Zanzibar kulikuwa na utumwa hadi 1964.

Utumwa ni aina mojawapo ya njia za uzalishaji mali, ambayo ni ya kashfa, na kwamujib

wa sifa za utukuzaji wa ubinaadam, waliyokashifika zaidi wakiwa wale wauzajina hata ku-

liko watumwa wenyewe, kwani wao ndio waliokuwa wapungufu wa sifaza utut wa kibina

ada. Utumwa ulitumika ulimwenguni kote na kama historiainavyotukariria, nyenendo za

uzalishaji mali hubadilika wakati njia bora zaidi yauzalishaji mali inapozalika. Utumwa

haukuondoshwa na Uingereza au nchi za ulaya kwa jumla, kama nchi hizo zinavyodai

wanapojaribu kujipa sifa za utu bora. Nchiza Ulaya zilitumia njia za uzalishaji mali

za utumwa katika kunufaisha matabaka yajuu yaliyokuwa yaki tawala makwao. Mfano

dhahiri ni Waafrika waKimarekani wahuko Marekani, waliyoujenga uchumi wa Marekani

kwa damu na jasho lao, wakatitabaka lao likiselelea nyuma. Wazungu, hata baadhi ya jamii

zao wenyewewalizigeuza watumwa vile vile. Wakati utumwa ulivyokuwa haunufaishi

13
tena uchumiwa matabaka hayo, kwa vile kwanza mmilikaji watumwa ilibidi anunuwe wa-

tumwa n ahalafu awagharimie makaazi, chakula, nguo, matibabu na mapumziko wakiumwa

namahitaji yao mengineyo, njia yenye faida zaidi ya uchumi ilibidi ichukuwe pahalapa

uzalishaji mali wa utumwa. Maendeleo ya jamii kwa jumla hutokana na nyenendompya

za kupeleka njama mpya za kuendeleza maisha, njama mojawapo ikiwakuendeleza njia

bora za uzalishaji mali. Kwa hivyo tokea siku za "primitivecommunalism", (yaani maisha

ya kijamii ya enzi za kale na kale, kama vile uwindajiwa pamoja wa jamii), mabadiliko

ya jamii yalitokana na uendelezaji wa njia zakuzalisha mali. Ustadi wa kazi kama vile

wengine kuwa wavuvi, wengine wasasi,wengine kuwa mafundi na wengi-ne wahunzi ni

kati ya maendeleo ya kijamiiyanayoleta upigaji khatuwa mbele wa kijamii.

Wanawake, kutokana na upungufu wao wa nguvu za kimusuli, kwa wale waliyoishi karibu

na mito, maziwa na bahari walitega samaki, lakini wengine walishughulika zaidi na kazi

za uvunaji wa nafaka mwitu na uchumaji na ukusanyaji wa matundamwitu. Hizi ni kati ya

khatuwa za mwanzo za uendelezaji wa njia za kuzalisha maliza ukulima. Kujishughulisha

na ukulima wa kale kulitokana na ushupavu nauangalifu wa wanawake, ambao zaidi ya

kwamba wakilea watoto, na kukusanyavyakula mwitu, walitanabahi kwamba zile kokwa

za matunda nafaka na walizokulaambayo wakitupa tupa sehemu walizo piga kambi au

kuishi, hatimae zilitowa michena kutoa matunda na nafaka. Wanawake kwa ujasiri wao

ndio waliyokuwa watu wamwanzo, kutambua umuhimu wambegu na kuanzisha kilimo,

maana baada ya hapandio walipoanza kupanda mbegu na miche na hatimae kukuza uchumi

wa kilimo,kuanzisha kuhodhi, rasilmali na kuzidisha uwezekano wa ustadiwa kazi mbali

mbalizilowezekana kwa sababu ya maendeleo hayo. Zile sehemu zilizokuwa na wanyama

wengi wa kusaka na samaki wengi wa kuvua, ziliwafanya wasasi na wavuvi wa siku hizo

kuacha au kupunguza tabia ya kuranda randa kutafuta chakula. Baada yakwamba kupiga

14
kambi kulisaidia kilimo, kuliwezesha vile vile, kama tulivyoona hapo juu, ukuzaji wa aina

ya makazi mbali mbali kama vile mafundi wa kutengenezasilaha, kutengeneza mitumbwi,

mitego hatimae wahunzi na mafundi mbali mbaliwakazalika. Utengenezaji wa vifaa mbali

mbali uliendeleza ulimaji, usasi, uvuvi,ujenzi n.k.

Haya ndio aina ya mabadiliko katika jumuiya yanayoleta maendeleo katika jamii

nahatimae kuleta mabadiliko ya uzalishaji mali wa aina mpya. Haya ndio aina yam-

abadiliko ya uzalishaji mali ambayo hufanya mtindo wa uzalishaji mali fulani kamavile

wa utawala kubadilika. Njama mpya hizi huwa kwa desturi ni alama yamaendeleo iki-

fananishwa na nyenendo zilizo kwisha pita. Utumwa kwa vile ulikuwa uzalishaji mali

kongwe na zorota ulibidi ubadilike napahala pake kuchukuliwa na uzalishaji mali wa

"Kibwanyenye/Kimwinyi". Uzalishaji huu wa mali ulimfanya mtumwa kuwa huru kwa

kiwili wili, lakini si kiuchumi walakifikra, kwani uhuru aliyoupata ulikuwa uhuru wenye

vigezo na vikwazo fulani.Mtumwa hapo akawa mtumishi wa rasilmali na mfumo mpya wa

kisiasa, akiwa nakiwili wili chake tu huru wakati nguvu zake na akili yake zikiwa si mali

yake,yaani akiweza kuchagua tajiri/bwanyenye /bwana gani atamtumikia kwa malipoasiy-

ooweza kuyakatia uamuzi, na mara nyengine hata kutoweza kuchagua muajiriwake. Mtu

huyu baada ya kupata uhuru wake ilimbidi ijipatie makaazi, chakula,nguo, matibabu,

ulinzi n.k. yeye mwenyewe, wakati mambo hayo huko nyumayakihudumiwa na yule

aliye mmiliki. Kwa mara nyingi kiwanja chakujengea nyumba yenyewe au upangishaji

wake, ulitokana na muajiri wake, mara nyingiakiwa yule yule aliye mmiliki kabla na

maingiliano yao yakiwa hayana tofauti sana,kwa vile muajiri mpya alikuwa akimkamuwa

na kumnyonya kwa kumkodishakiwanja, nyumba, kumkopesha kwa matumizi ya chakula

na mengineyo nakumlipisha riba ya kiwango atakacho bwanyenye. Ingawaje sio waajiri

15
wotewaliyokuwa na mtindo huo , na inasemekana, hadhi ya watumwa Zanzibar ilikuwab-

ora zaidi kuliko kwingi kwengineko, kwa sababu ya imani ya kiislam. Ubwanyenye

ulikuwa njia ya uzalishaji mali bora zaidi ya uzalishaji mali wakiutumwa kwa vile ulipiga

khatua kubwa zaidi katika kuendeleza uchumi hasa wakilimo, kuruhusu na kushajiisha

kuweko kwa muuzaji wa bidhaa kama ni kiungobaina mali fulani na mali nyengine na

hatimae mchuuzi huyu kuweza kuhodhi nakutajirika kwa kutosha na kuweza kutanua njia

za usafiri na kuanzisha utumizi wa vifaa na mashine katika uzalishaji mali, kama vile meli

za stima. Hatimae kuletauwezekano wa maendeleo ya mafundi, wahunzi na wengineo.

Kufuatia njia yauzalishaji mali wa Kibwanyenye, pakazaliwa daraja jingine la uzalishaji

malilijulikanavyo kama uzalishaji mali wa Kibepari, kama litavy okaririwa baadae, hiini

njia muhimu ya uzalishaji mali ya wakoloni.

2.6 Utumwa na Uislaam

Wakoloni wote pamoja na wa kiingereza walifanya/na wamo wakifanya njama za siri za

kujifanya wao wazuri na kuja kwao Bara la Afrika kulikuwa na madhumuni yakuleta

kheri na fanaka pasi na kuwa na lengo jengine lolote, la siri au la dhahiri.Njia yao moja

wapo muhimu waliyoitumia ilikuwa ni Makanisa na Mapadri. Kupigavita "ushenzi",

"utamaduni uliyoselelea wa Kiafrika" na kuleta ustaarabu waKizungu lilikuwa ni jambo

mojawapo waliyodai na kuliweka mbele. Tukifuata utamaduni wao tutakuwa kama wao

kuvaa nguo zao, kula kama wao, kutumia vituvyao na kuuwauzia vitu kwa bei zao na

kununua kutoka kwao, tukifanywa kuwana thamani kama zao. Wao, peke yao na wazungu

wenzao, walidai kuwa walistaarabika, wengineo wote ni wakiwa hawajastaarabika na

16
wakiwa washenzi,kwa mujib wa propaganda zao. Watu au tawala zozote zilizowaunga

mkono Wangereza katika njama zao za kuwatawalia watu wengine walipewa heshima,

ulwana ulinzi maalum.

Kwa Zanzibar, wakoloni wa Kiingereza, baada ya kuwanyanganya khatamu zenyewe, ndio

waliyoulinda na kuuhifadhi ufalme wa Kibunsaidi, lakini baadala yakuuita utawala huo

kwa jina lililostahiki, yaani wa Kibunsaidi, walitunga mbinu zakuupa jina ambalo lili kuwa

na azma ya kuwapa faida wao Wangereza zaidi. Kwahivyo wakaamuwa kuuita utawala huo

ni wa Waarabu, na hata sio wa Kiomani auWakimanga, maana kwa kweli, sio Waarabu wa

kila aina waliyotawala Zanzibar.Lengo la kuuita utawala huo ni wa Kiarabu, lilikusudia na

shabaha nyenginekabisa, nalo ni kwamba Waarabu ni Waislaam. Kuuita utawala wa Zanz-

ibar waKiarabu kulikuwa na shabaha mbili, moja wapo ni kuufanya Uislaama uonekanem-

baya na ukikandamiza Mwafrika na Uzungu na Ukiristo ukiwa ni mwema. Utumwa uli

kuwepo Afrika ya Mashariki hata kabla ya kuzaliwa Nabii Issa, kwa hivyo kabla ya ufuasi

wa Kiislaam wa Nabii Mohammad, salallah alayhi wasalaam. Lakini Mkolonikaufanya

Utumwa umeletwa na Mwaarabu, wakati huo huo, kwa kweli, akikusidiakuchochea chini

kwa chini na kusema ni Uislaaam ndio sababu ya Utumwa. Wakati ambapo utumwa

ulipigwa marufuku Zanzibar, wakati huo huo, Wareno na Wafaransa walishughulika na

biashara ya utumwa Afrika ya Mashariki, na kazihiyo waliifanya bila ya kuingiliwa kati

na manuwari za Kiingereza zilizowekwamaalum kulinda usafirishaji wa watumwa. Mn-

gereza, na vibaraka wake wakikiristo, hawasemi hayo wala hawasemi kwamba kulikuwa

na Wangereza hapo hapo Zanzibar wakifaidika kutokana na jasho la Watumwa, na ndio

maana mwanzoni kilekilichopigwa marufuku kilikuwa ni usafirishaji wa wa tumwa na sio

kumilikiwatumwa. Walisahau vile vile kusema kwamba huko kwao hapo zamani kulikuwa

nautumwa, ingawa huko makwao kulikuwa hakuna Uislaam. Wangereza walikuwahawat-

17
wambii juu ya maafa ya Waafrika wa Afrika ya Magharibi waliyopelekwa Marekani ya

kaskazini kusini na Caribbean ambako hakukuwa na Uislaam. Wazunguwalipo kwenda

Marekani walikwenda kwa niaba ya jina takatifu la Ukiristo, na kwa niaba ya jina la Msal-

aba, wakateteketeza wenyeji wa huko na kuwatawalia.

Njama za kuufanya Uislaam uonekane mbaya Afrika, ilikuwa kama kufanyakiini ma-

cho. Kuleta chuki za kugonganisha vichwa baina ya Wazanzibari kwa Wazanzibari,

Watanganyika na Watanganyika, ili kuweza kuwatawala kwa urahisi na kuweza kutam-

baza dini ya ukiristo, hilo ndilo lilokuwa lengo muhimu la kampenihiyo, ingawa wengi

wa wazungu hao walikuwa hata hawaamini Mungu, balikuutumilia ukiristo kuwatawalia

na kuwanyonya Waafrika. Mkoloni alisahau kwambakwa niaba ya ukiristo Christofer

Columbus aliwateketeza Wahindi Wekundu, nakazi hiyo ovu ikaja baadae ikaendelezwa

na wenye asili ya Kiingereza na kufikahadi kwamba leo Wahindi Wekundu baada ya

kuteketezwa wamekuwa wachache"minority" makwao wenyewe. Mkoloni hajatwambia

kwamba huko Australia na NewZealand aliwateketeza wenyeji wa huko,"ma aborigens"

kwa kutumia mbinu ovu mbali mbali, moja wapo ikiwa kuwagawiya watu wa huko

mablangeti yaliyokuwa na magonjwa mbali mabli, kama vile tetekuwanga, kifua kikuu,

ndui, magonjwa ambayo watu hao kwa wakati huo walikuwa hawana kinga viwili wil-

ini mwao kuwezakujikinga na magonjwa hayo. Kwa vile watu hao siku hizo walikuwa

hawakuchanjwawala kuwa na ulinzi wa kuzaliwa nao, walipukutika na kufiana kama

nzige nahatimae Wangereza wakaweza kumiliki makoloni na kufanya sehemu hizo ni

nchizao. Mitindo kama hiyo walikuwa wanataka kuifanya huko Afrika ya Kusini naZim-

babwe, lakini wakaula na chuwa. Na sisi Wazanzibari, baadala ya kuamka nakuzitambuwa

mbinu za Mkoloni za kutugonganisha vichwa, Waislaam kwa Waislaam,na Waafrika kwa

18
Waafrika, tukabaki tunauwana wenyewe kwa wenyewe, baadalaya kukaa kitako na ku-

jaribu kutatuwa tofauti zetu kwa njia za kisiasa na kidugu.Mkoloni alisahau kuwambia

wananchi kwamba katika biashara ya utumwa Zanzibar ,kuwa Waislaam hawakufanywa

watumwa na waliyosilim kutolewa utumwani.Lakusikitisha zaidi ni kuona hata wale waan-

dishi na wataalam wanaosifika kuwawameendelea, wametekwa nyara na tafsiri ya ukoloni

ya utumwa, na badala yakuukariri utawala huo kama ni wa kitabaka, mara nyingi na

wao wan ajiingiza katikamtego wa kibaguzi. Hadi hii leo Uislaam unapigwa vita sana

sehemu mbali mbaliulimwenguni, ingawa leo hazitumiwi sababu za utumwa bali sababu

nyenginezo,kama vile kuvunja Katiba ya Muungano wakati Zanzibar ilipojiunga na Umoja

wa Nchi za Kiislaam, na badala ya serikali ya Zanzibar kusimama kidete, kutetea utu, nchi

na imani zao, ikakubali kamsujudia Nyerere.

Kwa kutumia mbinu kama hizo, za kutumia Uislaam na Ukabila badala ya tafsiri yak-

itabaka, Mngereza alifanikiwa kuleta chuki na uhasama baina ya Wazanzibari,wakati yeye

akishirikiana na kuuhifadhi utawala huo huo aliyouita wa Kiaarabu.Kwa njia kama hiyo

Mngereza akafaulu kutufanya tukabane roho wenyewe kwawenyewe na kusahau kumpiga

vita yule adui wa kweli, yaani Mkoloni wa Kiingereza. Hivi sasa Mngereza kesha ondoka

hadharani, wamebaki vibaraka wakehasa huko Bara wanaoimba wimbo huo huo, ilhali

babu zao (machifu) ndiowaliyokuwa wakikamata watumwa hao na kuwauza.

2.7 Ubepari

Ubepari nao ukifananishwa na Ubwanyenye, na Utumwa n.k. ni njia iliyoendelea bora

zaidi katika kuleta maendeleo kwa jumla. Binaadam ni kiumbe anaeendelea kila usiku

19
ukicha na siku zote atataka kuona anaendelea zaidi, kwa hivyo njiafulani ya maendeleo

ikisha zorota inawekwa kando na kubadilishwa na njianyengine iliyo bora zaidi. Mn-

gereza anadai kwamba aliuondosha utumwa Afrika ya Mashariki, lakini alisahau kusema,

kama ilivyokaririwa hapo juu, kwamba kwao wenyewe waliendeleza uzalishaji mali wa

utumwa na jamaa zao wa Marekani walijenga na kuendeleza njiaza uzalishaji mali wao

kwa kupitia utumwa na hadi hii leo Waafrika wa Kimarekanibado wako katika daraja

la chini kabisa katika jamii zote za huko Marekani.Kukomeshwa kwa utumwa Ulaya na

Marekani kulipitishwa kwa sababu ya kwambaaina ya uzali shaji mali huo kwa wakati huo

ulikuwa umesha zorota na haukuletafaida za kiuchumi tena. Mbali ya Mngereza kusahau

kusema kwamba uchumi wasiku hizo ulikuwa haufaidiki tena kwa kutumia njia ya utumwa

kwa vile amilikaewatumwa ilimbidi awalipie gharama zote za kila siku, gharama ambazo

apata e uhuruwake ilimbidi ajihudumie mwenyewe. Vile vile amesau kusema kwamba

vita vyakedhidi ya utumwa viliambatana na uenezaji wa utawala wake wa kikoloni na

kusahaukusema kwamba uchumi wake ulifaidika kutokana na jasho la Watumwa.

Maendeleo ya uzalishaji mali ulimwenguni hayakwenda sambamba, kwa vile kuna

nchi mbali mbali katika uliwengu wa tatu ambamo maendeleo ya uzalishaji malihayakufu-

ata vidaraja kama vile vya nchi zilizoendelea, yaani kutoka utumwa, kwenda ubwanyenye

halafu kwendea ubepari. Kutokana na upungufu wamaendeleo ya kisayansi na kiteknolo-

gia karibu nchi zote za ulimwengu wa tatu hadihivi leo hazijafikia kiwango cha uzalishaji

mali wa kibepari. Mabepari wamehakikisha kwamba nchi hizi zinabaki nyuma na kuwa ni

masoko ya bidhaa zamabepari ambao walikuwa ni wakoloni wao, na ardhi yao kuigeuza

bustani za mauana mashamba ya chai, kahawa na viungo walivyovihitaji wao, wakati huo

huo kuwani bidhaa zisoweza kushibisha walimao au kutoweza kuwahatarishiya uchumi

20
wawakoloni. Ni hivi karibuni tu ambapo nchi chache za huko mashariki ya mbali ndizo

zilizoruhusiwa kutumia uzalishaji mali wa kibepari. Hali hiyo imemkinika kwasababu

ya gharama za uzalishaji mali huko Ulaya na Marekani zimekuw- a juu sanakutokana na

kupigania haki za wafanya kazi huko nchi zilioendelea. Hali hii ikawafanya Mabepari wa

nchi za magharibi kukimbilia zile nchi ambazo gharamahizo ziko chini na kujihakikishia

na kuweza kuhakikisha faida kubwa zaidi. Kinyume na ilivyo dai la baadhi ya wataalamu

fulani wa kisiasa na kihistoria, Zanzibar haikuwa na njia ya uzalishaji mali wa kibepari.

Katika nchi zilizoendelea hasa zile za kibepari, uzalishaji mali wa utumwa kwa desturi

hufuatiliwa na uzalishaji mali wa Kibwanyenye/Kimwinyi na hatimae ubepari kufuatia.

Baada yakuondoshwa utumwa Zanzibar hapajatokea maendeleo yoyote ya maana ya uzal-

ishajimali, bali msingi wa uchumi wa Zanzibar uliselelea pale pale na kuwa wa kale ukiwa

wa Kibwanyenye na ukitegemea vuno la karafuu, nazi na pilipili hoho, napakitumika njia

zile zile za kulimia za enzi za mababu na mababu. Ukulima wa vifaavya kisasa ulikuwa ni

jambo duni, na viwanda vya aina yoyote, zaidi ya viwanda vya lazima vya ukamuaji wa

mafuta ya karafuu na ya nazi, kiwanda cha sukari,kilicho-anzishwa na Barghash, vilikuwa

duni. Uendelezaji wa uzalishaji maliulikuwa ni dufu, Zanzibar ikiwa shamba la kuchumiya

ubepari wa kikoloni nakuselelea kuwa katika uzalishaji mali wa ki- bwanyenye na wakati

huo huo, kupitia tabaka la Wafanya biashara, kuwa soko la bidhaa za kibepari kutoka kwa

Wakoloni na kituo muhimu cha usambazaji wa bidhaa hizo katika sehemu nyengine za

Afrikaya Mashariki na ya kati.

Ubwanyenye au Umwinyi ndio uliyokuwa mwenendo wa kitawala na wa kuzalisha

mali Zanzibar na hadi leo hakuna mabadiliko makubwa katika fani hizi. Maingiliano .

ya "kimwinyi na kiskwatta (squatter)" ndio maingiliano yaliyojenga msingi wakisiasa wa

21
hivi sasa Zanzibar. Msingi huo ulionekana kama ni mfano wa kujengeamfumo wa uon-

gozi wa vyama vya kisiasa viwili muhimu vya Zanzibar yaani ASP naZNP. Umwinyi au

ubwanyenye vile vile ndio uliyokuwa msingi mmojawapo muhimuwa chuki za kikabila,

hasa kwa vile ya mamwinyi au mabwanyenye wa Kizanzibariwalikuwa waliyokuwa na

asili ama ya Kiarabu au ya Kishirazi na maskwatta wakiwawenye asili za Mrima/Bara.

Misingi miwili mingine muhimu iliyoleta chuki baina yajamii ya Kizanzibari ilikuwa ni

utawala wa Kisultan na utawala wa Kiingereza.Ingawaje, kabla ya kuja tawala mbili hizo

Zanzibar, tawala za wajukuu wa Hassan,Sultan wa Shiraz, hasa ya utawala wa Mwinyi

Mkuu, ilikuwa ni tawala iliyotumiautumwa kama ni njia ya uzalishaji mali - wa hapo

kale. Zanzibar ilipokuja chini ya mamlaka ya Seyyid Said bin Sultan (1832) palikuwa na

makubaliano baina ya Sultan huyo na Sultan Mwinyi Mkuu kwamba, kila mmoja atawale

na kuwa na mamlaka ya sehemu yake, hatimae pakatokea mfarakano mkubwa kwa vile

Seyyid Said alichukuwa utawala wote hata kutia ndani aukuhamisha nchi tawala za Kishi-

razi.

Inasemekana kwamba, kabla ya utawala wa Mabusaidi kutawala Zanzibar,Wazanzibari

walipeleka Ujumbe kwa Sultani wa Omani, wakiwaona kama Waislaam wenzao, waende

Zanzibar kuwasaidia kuondowa utawala wa makafiri wa Kireno. Usultani huo hatimae

ukaifanya Zanzibar mamlaka yake, pekee. Mabwanyenyewenye asili ya Kiomani wakawa

hatimae ndio wenye kumiliki ardhi kwa wingi zaidi na kunufaika zaidi kiuchumi na hali

hii ikawafanya kuwa tabaka la juu kabisa Zanzibar na wenyeji wao, Mabwanyenye wa

Kishirazi, wakashushwa hadhi na kuwatabaka dhaifu zaidi. Ingawaje, hili ni tabaka lililo-

jiwe za zaidi kuliko Waswahili wengine waliyokuwa hawana asili ya Kizanzibari halisi.

Karibu wote hawa wa kundila mwisho walikuwa katika tabaka la chini.

Utawala wa kisultani Zanzibar haukuwa wa Kiislaam, au wa Kiarabu kama Wangereza

22
walivyotufanya tuamini, kwani watawala hao hawakutawala kwa mujib sheria za kiislaam

na hawakutoka Arabuni kote bali walitoka Omani na hata huko Omani walikuwa ni watu

wa ukoo mmoja tu, nao ni Mabusaidi na sio aina zote zaMabusaidi. Na hata wale mab-

wabyenye wengine wa Kiomani waliyokuwa matajiri,kuwa na mashamba na nguvu nyingi

hawakuwa watu ambao wakiwakilisha maslahiya utawala wa Kibusaidi tu. Baadhi yao,

kama vile ilivyo desturi katika baadhi yawatawala au mabwanyenye tofauti, kulikuwa na

migongano, michuano na mivutanoya kujinufaisha binafsi. Katika Zanzibar, kwa mfano,

wengi wa Mabarwani hadi siku za mwisho za Usultani walisemekana kuwa wakipinga

Ufalme na msimamo huo walikuwa nao tokea siku za Juma Barwani alipochukuwa silaha

kupambana na Seyyid Said bin Sultan.

23
Chapter 3

USULTANI NA UKOLONI

3.1 Usultani wa jana na Utawala (Usultani) wa leo

Tabia ya kutawala au ya kunyanganyana utawala au mali, si sifa za Waarabu tu,Waomani

au Mabusaidi peke yao. Ulimwenguni kuna tawala tofauti, na tawala hizizinaweza ku-

gawika katika makundi mawili makubwa, moja likiwa na maslahi natabaka la utawala, na

kundi la pili likiwa na maslahi halali ya umma mzima nakuwapa watu haki sawa. Sifa

ya kuhifadhi maslahi ya takaba la utawala haitegemeiutawala huo una rangi gani, kwani

tumeona mifano ya utawala wa Sultan na utawalawa Karume. Utawala usio na maslahi ya

umma kwa desturi unakuwa ni wakutumiamabavu na kutowashirikisha wananchi katika

uamuzi wa mambo yao wenyewe.Utawala kama huo huchaguwa vibaraka wake kuwa-

tumilia katika kuendelezautawala au mtawala aliyehusika. Serikali nyingi za Kiafrika

zilisahau maagizo na ahadi walizozitowa wakati walipokuwa wakipigania uhuru, na kusa-

hau kwamba walichokipigania kilikuwa niserikali ya watu, iliyochaguliwa na watu kwa

maslahi ya watu. Karibu serikali zoteza Kiafrika baada ya kupata uhuru zilifuata mtindo

wa utawala wa Kidikteta nakusahau ahadi zote walizozitowa kabla ya hapo. Wengine

walitumia siasa dhidi yautumwa na kupinga Usultani kama ndio kampeni yao, lakini ha-

timae, walipopata khatamu za utawala wakaonyesha kuwa ni tawala akhasi za Usultani

na ukoloni.Baadhi yao walidai uhuru wa Mwafrika lakini walipopata khatamu za utawala

walizidi kumkandamiza Mwafrika, na waliendeleza siasa ya udikteta, utawala wamabavu

na kutaka kumtawalia huyo huyo Mwafrika kwa kujigeuza Mabwana/Wakoloni wepya,

24
kama Tanganyika na Zanzibar. Watawala wa Kiafrika wakipata khatamu za utawala wana

mtindo wa kutakakuselelea katika utawala milele na hata watakapo kwisha ondoka au

kulazimishwa kuondoka bado huwa wanataka kuingilia kati mambo ya utawala, kama vile

Nyerere, kupinga aumuzi wa Bunge la Tanganyika la kutaka Bunge na Serikali ya Tan-

ganyika na kuwalazimisha Wazanzibari bila ya khiari zao kubaki katika Muungano kwa

kulazimisha serikali moja. Tumemuona Karume, aliyedai siku zanyuma kumpimgania

Mwafrika na hatimae tukaona ukatili aliyomfanyia Mwafrika mwenziwe, mtu yule yule

ambaye aliyempa yeye nguvu hizo, ndiye hatimaealiyemgeuza adui na kumteketeza. Kwa

hivyo suala la kuliangalia kwa makini na kulidurusu kwa kituo ni aina yautawala uno-

husika, na kama utawala fulani una maslahi na wananchi au la , na siotu kwamba utawala

huo una jinsiya gani, ya kutoka Butiama au kwengineko. Kwanihata utawala usio wa

kikoloni unaweza kuwa mkatili hata kupitia ukoloni. Suala lakulizingatia ni kama utawala

huo ukiwa wa kienyeji unatekeleza maslahi ya umma au maslahi ya watawala na jamaa

zao, na hata ukiwa ni utawala wa kienyeji, mradi unakandamiza wananchi lazima up igwe

vita mpaka utokomee, na utawala halaliwenye misingi ya kidemokrasia uwekwe badala

yake.

3.2 Kumiliki Ardhi Zanzibar

Katika historia ya leo kuna madai mawili muhimu kuhusu umilikaji wa ardhi Zanzibar. Dai

moja ni la wale wanaodai wamenyangnywa ardhi baada ya Mapinduzi ya 1964, wakidai

warejeshewe ardhi zao walizo nyang’anywa, hizo zikiwa ni malizao za kihalali; wanadai .

Kwa upande wa pili kuna wale Wazanzibari wanaodaikwamba mababu zao walihamishwa

25
kwa nguvu kutoka zile sehemu zenye ardhi yarutba na kuhamishiwa kwenye sehemu za

ardhi duni (Kuna kikundi chengineambacho hakitajwi sana, nacho ni cha wale Wazanz-

ibari ambao ni vitukuu navirembwe wa watumwa waliyotoa jasho lao katika mashamba

hayo, bila ya kupatamalipo.) Suala muhimu, katika madai mawili haya, ni jinsi gani kupi-

tisha haki bainaya Wazanzibari bila upendelevu wowote, lakini kabla ya kuweza kufanya

hivyo itabidi ijulikane nani MNYANG’ANYA NA NANI MNYANG’NYWA. Hili sio su-

ala rahisi kwa sababu kwa uchache vitendo hivi vya uhodhi wa ardhi vilitokea kamamiaka

160 iliyopita yaani baada ya Seyyid Said kuhamia na kuhamishia mji mkuu wa utawala

wake kutoka Oman kuja Zanzibar. Seyyid Said mwenyewe alijigawiya ardhibora kabisa

yenye nafaka, na haifikiriki kwamba alimuomba Mhadimu, Mtumbatu,Mshirazi rukhsa ya

kuchukuwa ardhi hiyo au kujulikana kwamba ilikuwa ni ardhiisiyotumika kabla ya hapo.

Hatujui kwamba Mwiny i Mkuu nae alipochukuwa ardhialiomba au kununua ardhi kwa

nani au kwamba ardhi hiyo ilitumika kabla ya hapoau sivyo.

Baada ya "Harameli bin Ali" kuleta miche ya karafuu kutoka R’union katika mwakawa

1929 na Seyyid Said kutilia mkazo na kushajiisha upandishaji wa zao hilo muhimu, mfalme

huyo aligawa ardhi kwa zile koo za Kiomani zilizotukuzwa na ufalme huo, pamoja na

kuwa aila hizo zilikuwa na rasilmali ya kutosha ya kuwezakukuza zao hilo. Ingawaje huko

Pemba kati ya makabila muhimu yaliyotia mizizi kabla ya utawala wa Omani kudhibiti

Zanzibar, ilikuwa Mazrui na Mauli, namakabila haya yalikuwa yameshajizatit kuoleyan a,

kuchanganya damu na kumilikiardhi muda mrefu kabla ya vitendo hivyo kupitika Zanz-

ibar. Itakumbukwa kwambatokea kutolewa kwa Mreno kwa mara ya pili katika 1728

huko Mombasa, mara yakwanza ikiwa mwaka 1660, kabila la Mazrui lilikwisha tia mizizi

Momba sa na Pemba pia. Ingawaje hakuna ushahidi unaoonyesha kwamba watu hawa

ambao na wao piawaliyokuwa na asili za Kiomani walinunua ardhi hiyo kutoka kwa mtu

26
yeyote katikahizo siku za mwanzo au walizipata kwa sababu za kuingia ndoa. Lakini, vile

vile, hakuna ushahidi uliyotolewa unaoonyesha kwamba kulikuwa na watu waliyomiliki

ardhi hiyo hapo zamani, waliondoshwa mashambani ama kwa sababu wakiishi sehemu hizi

au kuzimiliki. Zanzibar ya kale haikuwa nchi ya ukulima na uchumi wake kutotegemea

uuzaji wa mazao ya ukulima na kwa hivyo si suala dhahirikwamba ardhi hiyo ilimilikiwa

kwa madhumuni ya ukulima wa biashara. Jambo wazini kwamba ardhi hiyo ilitumika

kwa madhumuni ya kujilisha wenyewe, jambo ambalohalikuhitaji sehemu kubwa ya ardhi

kutosheleza mahitaji hayo. Zaidi ya hayo idadiya Wazanzibari kwa wakati huo ilikuwa ni

ndogo sana hata kutoweza kutumia ardhiyote ama kwa makaazi au kwa ukulima au kwa

yote mawili, na ndio maana wakati wautumwa na wa baadae ilibidi kuleta watumwa na

vibarua kutoka Bara ku ja kutumikamashambani. Kabla kwa kuja kwa karafuu, uchumi wa

Zanzibar ulitegemea zaidibiashara baina ya nchi za Bahari ya Hindi na Afrika ya Mashariki

na ya Kati, naZanzibar ndio ikiwa kitovu au kiini cha biashara hiyo, yaani kuwa soko na

bandari muhimu, huu ndio uliokuwa msingi wa uchumi wa Zanzibar.

Suala muhimu ni, jee ni halali kwa mtu kutoka nchi nyengine na kuja kuikuta ardhi

haikaliwi, kuichukwa, kuilimiya na kudai ni yake. Ardhi ya nchi kwa ufupi nirasilmali ya

dola kwa jumla na atakayeitumia kwa maslahi ya maisha yake, ya ukoowake na ya nchi

kwa jumla atakuwa na haki ya kuitumia akijuwa wazi kwamba hiyoni mali ya umma. Kwa

desturi, vizazi vilivyozaliwa katika sehemu fulani kwa karne na karne, ndiwo wanaotam-

buliwa kuwa wamiliki wa sehemu fulani ya ardhi kwa vilewaliitolea jasho kwa kuifanyi

ya kazi sehemu hiyo. Ingawaje kuna wananchi wenginewa Zanzibar ambao hawakuishi

sehemu hizo za mashamba, bali waliishi mijini, nakwa desturi huwa hawamiliki ardhi

ingawa wana haki sawa ya kumiliki ardhi yanchi yao kwa jumla. Wale wanaosemekana

wamenunu wa ardhi, nao siku za mbelehuenda wakawa matatani, ikiwa kutakuwa na up-

27
ungufu wa ushahidi kutoka kwawale waliyowauzia ardhi hizo. Watumwa walifanyishwa

kazi katika mashamba tofautiZanzibar bila ya kulipwa, ingawa watumwa wengi walirudi

makwao mabara baadaya kupata uhuru wao, wale waliyobaki na kuigeuza Zanzibar nchi

yao kihalaliwanatakiwa kwa desturi wawe na haki ya kumiliki ardhi katika zile sehemu

walizolazimishwa kufanya kazi. Zanzibar ya leo ni Zanzibar yenye raiya (300/Km) kuwa

na wakaazi wengi hata ardhi kutotosha kwa wananchi wote kama itagawiwakihalali baina

ya wazalendo wote, ikitafsiriwa kwamba ardhi ni rasil mali ya umma. Wabara waliyowasil

Zanzibar kwa kazi za vibaruwa mashambani nao wanadai kuwana haki ya kumiliki ardhi

kupita wale wazalia wenye asili za Kiomani, wanadai hakihiyo si kwa sababu nyengine

zaidi, isipokuwa kuwa wao ni Waafrika na walikuwavibaruwa/maskwatta sehemu hizo.

Itaonekana kwamba watu hawa, tofauti nawatumwa, walilipwa kwa jasho lao waliloli-

towa baada ya kukubaliana kufanya kazi kwa mikataba. Mtumishi karakhanani hamiliki

karakhana, ingawa naye hunyonywa.Yupi mwenye haki zaidi ya ardhi ya Zanzibar, yule

mwenye uzalia wa Kizanzibaritokea 1660-1728 (kutolewa kwa Mreno) na 1832 au yule

jirani aliyekuja kwamkataba wa kibarua makhsusan katika karne ya ishirini. Vijukuu,

virembwe navitukuu vya Kizanzibari ambao mabibi na mababu zao walikuwa watumwa

waliyofanyishwa kazi katika ardhi fulani ni kati ya watu ambao madai yao ya ardhilazima

yatiliwe maanani, suala hili litakapojadiliwa siku za mbele.

Katika kujaribu kuleta usawa baina ya Wazanzibari, Serikali ya Mapinduzi ilitaifisha

ardhi na baadae kugawa "eka" tatu tatu kwa wananchi, ingawa nia yalengo hilo ilikuwa ni

nzuri lakini ugawaji wenyewe haukuwa wa kihalali. Kwanzasi Wazanzibari tu waliyo pewa

ardhi hiyo, pili ugawaji huo haukuwa wa usawa kwaniwale waliyojiweza walizidishiwa,

na kupewa (kuchukuwa) mashamba zaidi ya mojana yale yaliyokuwa na rutba zaidi, mfano

28
mzuri ni wa Memba wa Baraza laMapinduzi wenyewe ambao tayari walikuwa na misha-

hara miwili, wa Baraza laMapinduzi na Bunge la Tanzania. Uhalali wa kitendo hicho

umeingia dowa nakupotosha lengo na madhumuni ya ugawaji ardhi kihalali. Zaidi ya

hivyo, ardhihiyo iliyogawiwa umekuwa ikiuzwa ovyo ovyo, hivi karibuni hata serikali

ya Zanzibar imekuwa inagawa ardhi kwa madhumuni tofauti kwa njia za ama mapen-

deleo au kwa kilanguzi, kuzidi kuwapa walonacho na kuwanyima wasonacho. Serikali

vile vile inasemekana kuwagawiya au kuwakodisha kwa bei za bure wataliana na wageni

wengine ardhi ya Wazanzibari, wakati wageni hao wakifanya kejeli, ufudhuli wa kuwa-

fukuza wenyeji sehemu hizo na kuwazuwiya hata kuvua. Wataliana hao waliosabiliwa

ardhi hizo, inasemekana wanatumia sehemu hizo kwa uendelezaji wa biashara za madawa

ya kulevya. Chau chau gani wanoipata serikali hiyo haijulikani. Kuna watu wengine

wanasemekana wamerejeshewa ardhi zao, mali zao na majumba yao, bila ya kutolewa

kielezo chochote, wakati wengine bado hawajarejeshewa mali zao. Kutokana na hayo

machache kuhusu ardhi, Zanzibar itakapojipatia uhuru wake, kutoka Bara, pata kuwa na

haja ya kuunda Mahkama au Tume maalum ya kisheria kulijadili suala la ardhi ya Zanzibar

kihalali na kikamili.

3.3 Wahindi kudhibiti uchumi

Baada ya kuja kwa utawala wa Kiingereza Zanzibar, Seyyid Said akaonjeshwa shubiri

aliyowapa kina Mwinyi Mkuu. Kwanza kwa kukaliwa juu ya kichwa na Mngereza, pili

kwa Mngereza kuondosha njia ya uzalishaji mali ya Utumwa ambaoUfalme huo uki-

utegemea katika zao lake la karafuu na tatu kwa kutiliwa mkazo kwanjia nyengine ya

29
uzalishaji mali yaani ya kibwanyenye ambayo hatimae ilishajiishakukuwa kwa mfanya

biashara, ambae alikuwa Mhindi, wengi wao kuselelea kuwaraiya wa Kiingereza. Hati-

mae kugeuzwa karibu Mabwanyenye wote waliyokuwa naasili ya Kiomani kuwa kama ni

waangalizi tu wa mashamba ambayo kabla waliyamiliki, kwa vile karibu mashamba yote

yalikuwa yamewekwa rahhani, baadaya muflis uliyotokana na uuzaji wa watumwa, baada

ya hapo Wahindi wakapata satwa ya kuweza kuudhibiti uchumi wa Zanzibar. Kwa hivyo

khatamu za utawala na nguvu za uchumi hazijawa tena katika ukoo wa Kibunsaidi na Wale

Wazanzibari waliyokuwa na asili ya Kiomani, bali utawala ulikuwa chini ya Mngereza

na uchumiwa ndani ya nchi kuwa mikononi mwa Mhindi, wakipeana wadhifa, Mngereza-

kukamata serikali na uchumi wa nje na Mhindi kukamata uchumi wa ndani, akiwamjumbe

wa ubepari bila ya kuwa na njia za uzalishaji mali za kibepari.

3.4 Mngereza na mfumo wa matabaka

Kutawalia Zanzibar rasmi na Mngereza (1890), ambaye alikuwa na mgawanyiko wa

matabaka ya bayana zaidi kuliko yaliyokuweko Zanzibar wakati huo, kwa hivy oulizidi

kuyapanga matabaka Zanzibar kwa utulivu nabayana zaidi. Kwanza kwakuwapa Waarabu,

hasa wenye asili ya kiomani, na Wahindi ubora katika matabakaya jamii. Ingawaje

katika tabaka la wenye asili ya kiarabu na kihindi kulikuwa na mgawanyiko wa matabaka

mbali mbali, yakiwemo matabaka ya chini kabisa katikajamii. Baina ya tabaka la Mab-

wanyenye/Wafanya biashara wa juu, na matabaka yachini kabisa kulikuwa na tabaka la

kati na kati, ambalo lilikuwa na wafanyabiashara wadogo wadogo, maafisa wa serikalini,

mafundi waliyojimudu, wakulimana wavuvi waliyomiliki ardhi na vyombo vya kuvulia,

30
na wengine waliyojimudu kwanjia nyenginezo. Katika tabaka hili kulikuwa na makabila

ya mchanganyiko.Tabaka la chini likiwa ni vibarua, maskwata na maproletariati "walolala

hoi" wengiwa hawa walikuwa ni walalahoi waliyotoka nchi za jirani ambao walivutiwa na

hali bora ya kiuchumi ya Zanzibar au walikuwa wakikimbia ulipaji wa "kodi ya kichwa

" makwao. Wale waliyokuwa wakijiweza mabara walibaki huko. Mngereza alipojizatit

Zanzibar alihakikisha kwamba ugawaji wa matabaka ulizidi kutia mizizi na katika njama

zake za kawaida za "kugawa watu ili aweze kuwatawala" kwa urahisi zaidi,alihakikisha

matabaka haya yamejengeka kwa msingi wa elimu, kipato, rangi nakikabila .Tabaka la Mn-

gereza mwenyewe bila ya shaka kuwa ni bora kushindayote, na kuwa tabaka la juu kabisa

katika jamii hata kushinda la mfalme, na wakatihuo huo kuwatumilia wale waliyokuwa

katika matabaka ya juu kuendeleza utawalawa kikoloni. Sababu zinazotokana na mfumo

wa utumwa kwa jumla; sababu za kuondoshwa na kupunguzwa hadhi kwa utawala na

ubwanyenye wa kishirazi uliyofanywa na SeyyidSaid, na sababu za ujenzi wa matabaka

kwa msingi wa kikabila uliyonufaisha ukoloni ambao ulifumwa na Mngereza na kuza-

liwa kwa tabaka la walalahoi lilokuwana sehemu kubwa zaidi kutoka bara; zimeleta sio

mfumo maalum tu na chuki zakikabila visiwani, bali muhimu ya yote zimeleta Mapinduzi,

Muungano na CCM.

3.5 Vyama vya kisiasa kabla ya Mapinduzi

Chanzo cha Mapinduzi kinatokana na misingi ya kisiasa na ya kijamii ya Zanzibar.Ili

kuweza kufahamu kwa urahisi zaidi matatanisho ya siku za nyuma kwa vijana waleo

wa Kizanzibari na baadhi ya Wabara; pana haja yakunakili uundaji, misingi,mifumo na

31
uendeshaji wa vyama vya kisiasa vya zamani hasa Afro Shirazi Party(ASP) na Zanzibar

Nationalist Party (ZNP) au Hizbu. Chama cha ASP kiliundwa katika mwaka 1957 kutokana

na muunganisho wa chama kile kilichojulikana kama African Association (AA) (ambacho

asili yake ilikuwa nikama tawi la TANU na kuwa na uongozi na wafuasi wa Bara) na Shirazi

Association(SA) chama chenye uasili wa Kizanzibari. Vyama hivi viwili vilikuwa na sura

zakikabila kutokana na misingi iliyowekwa na Mngereza kama ilivyokaririwa hapo juu.

Chini ya Uingereza watu waligawiwa kwa makundi ya kikabila na kwa kupitia njiakama

hizo ndipo makundi hayo yalipoweza kuwakilisha maslahi ya makundi yaoyaliyohusika.

Vikundi viwili hivi, yaani AA na SA, ni vikundi vilivyokuwa namaslahi tofauti yaliyokuwa

yakigongana. Shirazi Association ilikuwa ikiwakilishaWaafrika wenye asili ya Kishirazi,

waliyokuwa wazalia wa Kizanzibari kwa mababu na mababu. Wakati African Associ-

ation iliwakilisha Waafrika waliyozaliwa sehemembali mbali za Afrika ya Mashariki na

Kati, hasa bara la Nyika/Mrima, kati yaowalikuwemo waliyoishi Zanzibar kwa muda

mfupi ilhali wengine walikulia Zanzibarama bado wakiwa na uzi wao wa kitovu Bara

au wengine waliyokwisha kuukata uzihuo na kundi jengine likiwa wazalia wa Zanzibar

wenye asili ya Bara au kuwa naujamaa na Bara. Suala muhimu la pili liloyagawa makundi

hayo lilikuwa ni suala laki tabaka, Washirazi wengi walikuwa Mamwinyi wenye uwezo

bora wa kiuchumi, hatawafuasi wao wa chini ni waliyojiweza zaidi. African Associ-

ation iliwakilisha zaidi watu wa tabaka la chini zaidi, yaani wale waliyokuja Zanzibar

kwa kutafuta kaziza muda mfupi kama vile za vibarua, wachukuzi, makuli na wafanya

kazi wamashambani (maskwata). Uongozi wa SA vile vile ulikuwa umeelimika zaidi na

kwahivyo kuwa tabaka la juu zaidi. Kwa hivyo kulikuwa na mambo mawili muhimuam-

bayo yalivitenganisha vikundi viwili hivi. Vikundi hivi, mwanzoni vilipoundwa,havikuwa

na misingi ya kisiasa kama vyama vya kisiasa vya kawaida vinavyojulikana, bali kila

32
kimoja kikijaribu kutetetea uongozi wa kuwakilisha-0Bmaslahi ya jamii yake. Chanzo

cha uundaji wa AA, kwa kweli, haikuwa siasa au maslahi ya jamii yote kwa jumla, bali

kilianza kama ni chama cha riadha (mpira,ndondi) na hatimae kuanza kujishughulisha na

masuala ya kijamii, wakati baadaekikawa tawi la TANU. Ndani ya kila kikundi, kulikuwa

na mvutano, na baina yavikundi viwili hivyo kulikuwa na mchuano mkubwa wa kuweza

kuingia katika Majlis’ltashrih (LEGCO Legislative council). Muundo wa Legco siku hizo

ulikuwa nawawakilishi kwa misingi ya kikabila, kipato na kisomo. Hali hii ilipangwa na

Mngereza ili inufaisha mataba fulani na kunyima haki matabaka ya chini. Yalematabaka

yaliyonufaishwa kwa kuambatana na uteteaji wa maslahi yao walilindamaslahi yao kwa

kuzidi kumt-etea Mngereza na utawala wake. Siasa za kupigania uhuru zilipoanza, Ny-

erere alijaribu sana kuunganisha AA na SA, hasa kwa vile AA ilikuwa kama ni tawi la

Tanganyika African Association,historia hatimae imetushuhudushia lengo la Nyerere la

kusisitiza hivyo. Historiaimedhihirisha kwamba Nyerere kwa siku zote alikuwa na lengo

la kuimeza Zanzibar na hatimae kuigeuza jimbo. Baada ya jitihada kubwa ya Nyerere

AA na SA zikaungana- katika mwaka wa 1957 na kuwa Afro Shirazi Union, yaani umoja

wa Waafrika na Washirazi. Ingawaje sio SA yote iliyojiunga na kuwa Afro Shirazi kwani

viongozi wa SA wa Pemba waliamua kubaki huru na katika uchaguzi wa mwanzo wa Zanz-

ibar wa 1957, Washirazi wa Pemba, Mohammed Shamte na Ali Sharif Mussa,waligombea

uchaguzi huo kama watetezi huru na kushinda kwa kiwango kikubwasana na kuonyesha

kwamba tokea siku hizo chama mama cha ASP, ambacho kwawakati huo kikijulikana

kama Afro Shirazi Union (ASU), hakikuungwa mkono Pemba. Ndio maana leo serikali ya

CCM inawalipizia kisasi Wapemba kwa kuwanyimangazi zote za maendeleo na kuyafanya

maisha ya Pemba kuwa ya ufukara wa mwisho. Afro Shirazi Union ikashinda Unguja na

kupata viti vitatu kati ya vinnekimoja kuchukuliwa na mjumbe wa Muslim Association na

33
Shirazi Association kushinda viti vyote viwili vya Pemba, Hizbu kutopata hata kiti kimoja.

Kina Shamte hatimae wakajiunga na ASP iliyoongozwa na Abeid Amani Karume lakini

migongano mikali ilitokea kati ya uwongozi wa chama hicho.

3.6 Muamko wa kudai uhuru

Kumalizika kwa vita vya pili vya ulimwengu, kulileta muamko mpya katika makoloni

mbali mbali, kwanza kwa kushindwa kwa Mafashisti wa Kijerumani, Kijapani naKital-

iana, pili makoloni yaliyokuwa chini ya Wakoloni kama vile wa Kiingereza walianza kuwa

na muamko mpya. Nchi kama za India na Uchina kujinyakulia Uhuruwao katika miaka ya

1947 na 1949. Baadae hamasa za upiganiaji uhuru na zakimapinduzi za nchi za Arabuni

ambazo zilikuwa za kiislaam, pamoja na kwamba Mngereza (1949) aliwapa Majahudi nchi

ya Mapalastina ambao wengi wao walikuwani waislaam, zilifanya muamko wa Wazanz-

ibari dhidi ya Mngereza kuzidi kutia fora.Mapinduzi ya Jamal Abdil Nasser (1952) na vita

vya Mchirizi wa Suez vya Misri (1954) dhidi ya Mngereza, Mfaransa na Jahudi vilifanya

jazba na damu yaWazanzibari kuzidi kuchemka na kuleta muamko wa kupigania uhuru

na kujitegemea. Mapambano ya Nkurumah, ya Ben Bella, ya Mau Mau na wengineo

yalizidi kurekibisha gurudumu la mapambano ya Wazanzibari. Mchemko wavuguvugu la

Misri uliwafanya wale wanafunzi wa Kizanzibari waliyokuwa wakisomahuko na wataalam

wengine wa Kizanzibari kuchukuwa msimamo madhubuti dhidi yaUtawala wa Kiingereza.

Kati ya wale waliyokumbwa na muamko huo ilikuwa ni Arab Association ya Zanzibar

na kufika hadi katika mwaka wa 1954 kugomea kwendamajlisi ’l tasrih, mmoja kati ya

viongozi wake washupavu alikuwa Ali Muhsin. Jinsihamasa za uhuru na azma ya ku-

34
jitawala zilivyokuwa ziko hali ya juu na hamu yakutaka kumuondoa Mngereza ilivyokuwa

kubwa, mmoja wa wanachama wa ZA, Inspector Sultan Ahmed Mugheri, alipovunja

mgomo huo na kuhudhuria kikao cha Legco, alipigwa visu na kuuwawa. Mtu aliyejitolea

kumuuwa Sultan Ahmed alikuwasi mwengine, bali ni baba yake Lt. Humud Mohammed,

yaani Mohammed Humud. Katika mwaka 1951 Wangereza walitaka kuanzisha kuchan-

jwa n’gombe Zanzibar,lakini jinsi ya hamasa zilivyokuwa ziko juu dhidi ya Mngereza kati

ya wazalia wa Zanzibar, jambo lolote lile alilolitaka Mngereza kulifanya lilitiliwa shaka,

hasa kwavile tokea 1940 Mngereza alianza kuchukuwa ardhi ya wakulima wa Kiembe

Samakikujengea uwanja wa ndege. Hali hii ilizidi kutia fora baina 1949 na 1951 wakati-

Wangereza walipochukuwa ardhi iliyokuwa na Msikiti kwa madhumuni ya ujenzi.Kwa

hivyo watu walivyoambiwa n’gombe wao wachanjwe, waligoma na kuonakwamba Wan-

gereza walitaka kuwaulia n’gombe wao, kama ng’ombe wao walivyokufakufa Zanzibar

baada ya kukogeshwa katika madawa siku za kabla ya hapo, kwahivyo wakakataa. Badala

ya kutumia siasa, Mngereza akatumia kibri chake chakikoloni na kutumia nguvu na mabavu

kwa kuanza kutia viongozi wa wafugajin’gombe hao ndani na kuwapandisha Mahkamani.

Jambo hilo liliwakasirisha sanawazalia na kusababisha mgomo na mhadhara uliyoelekea

gerezani "kiinuwa miguu"na kuwatowa viongozi wao kwa nguvu. Mngereza kwa mara

nyengine tenaakaonyesha kibri chake cha kutumia nguvu na kupiga watu risasi, hapo

ndipovi kazuka "Vita vya N’gombe". Tukio hilo ni tukio muhimu sana katika sera za kisi-

asa za Zanzibar, kwani hapo ndipo gurudumu la kihistoria la kuleta mabadiliko na vuguvugu

la kuleta uhuru lilipozidi kupata nguvu. Vita hivyo vya N’gombeviliwaunganisha Wazanz-

ibari wa matabaka mbali mbali na kuondosha yale mabomaya Mngereza ya kubaguwa watu

kwa makabila. Chanzo cha mgomo wa kupingauchanjwaji wa n’gombe ulianza Kiembe

Samaki, na watu wa huko wakiungwa mkonona mashamba mbali mbali wakaunda chama

35
na kukiita Hizbu ’l Watan Raiyat Sultani,na baadhi ya viongozi wao walikuwa ni Vuai

kiteweo, Miraaj Shaalab, Maalim Zaid,Haji Hussein n.k. Mngereza kwa kutumia nguvu

za kisilaha, nguvu za gereza nanguvu za mahkama zao waliukandamiza mdhahara huo

na viongozi hao. Hatimae Mngereza alishinda kijeshi lakini hakutanabahi kwamba al-

ijichimbia kaburi lakisiasa na kupigwa pigo lisotibika. Kumbukumbu hilo likawafanya

viongozi waHizbu, ambao chanzo chao kilikuwa Kiembe Samaki, na waliyokuwa hawana

asili yakiarabu, kuchukuwa khatuwa muhimu katika historia ya Zanzibar. Kwa vilevion-

gozi hawa walikuwa hawana elimu ya kizungu waliuendea uongozi wa ArabAssociation

uwasaidie katika mapambano yao na Mngereza. Matekeo yake yakawavyama hivyo viwili

kuungana na kufanya chama kimoja kilichojulikana kama Hizbu’l Watan au kilojulikana

kwa jina la kiingereza Zanzibar Nationalist Party (ZNP).Wakati vuguvugu la kusonga

mbele na kudai uhuru katika bara la Afrika lilikuwakatika kiwango cha hali ya juu kabisa.

Majina na mifano ya viongozi kama kinaKwame Nkurumah, Patrice Lumumba, Sokou

Toure, Jamal Abdel Nasser, ModiboKeita, Ben Bella, Didan Kimathi, Jomo Kenyatta n.k.

yalikuwa ni majina yakusisimua, ya kimapinduzi na ya kujivunia kwa kila Mzanzibari

na kwa Bara zimala Afrika. Viongo zi hawa waliichemuwa Afrika nzima na kuwaamsha

Waafrika wotekupigania Uhuru wao.

3.7 Upiganiaji Uhuru

Kama ilivyotajwa hapo juu ZNP ilishindwa na ASU (ASP) katika uchaguzi wa 1957,

lakini baadae mabadiliko makubwa ya kisiasa yalitokea. Viongozi vijana waKizanzibari

waliyokuwa Uingereza walishauriwa na uongozi wa ZNP kurudi nyumbani kwa madhu-

36
muni ya kushiriki katika kuanzisha upangaji wa mikakati wakuongoza mapambano ya

kisiasa na vuguvugu la uhuru. Viongozi hawa walikuwana umoja wao huko Uingereza na

kati yao walikuwa A. M. Babu, Khamis AbdullaAmeir, Ali Sultan Issa n.k. Viongozi hawa

waliamuwa kumpeleka Babu Zanzibar kutoka Uingereza kwa madhumuni ya kuchunguza

hali ya mambo na alitakiwaaepuke kujiunga na kundi lolote baina ya ASP na ZNP. In-

gawaje, Babu alipofika Zanzibar hatimae akajiunga na ZNP. Wenzake walipomsaili kuhusu

kisa cha kuamuakujiunga na upande mmoja, akawajibu kwamba kwa wakati huo ZNP ndio

iliyokuwa ikifuata siasa ya kimaendeleo na kwamba ASP ilikuwa bado inapinga uhuru na

kudai kwamba Mngereza asiondoke mpaka Waafrika wa Zanzibar wasome ("It is quite true

that the African Association of Zanzibar and Pemba does not favourthe proposed Round Ta-

ble Conference. As we are the backward community in theseislands, we shall ever beg our

needs and claim our rights for the benefit of Africans in this Protectorate for it is the adopted

policy of AfricanAssociation to achieve advancement and endeavour to win rights for our

selvesso long as we are sons and dauhgters of the soil. So our immigrant friendsshould not

forget that our aim is African self government,....not Zanzibari self-government - May 5,

1955 - Rankie Constitutional proposals). Hicho ndichokilikuwa kiini cha msingi wa chama

hicho baadae. Sumu hiyo ya kutodai uhuru kwa ASP ilitiwa na vibaraka wakiingereza

waliyopenyeza katika uongozi wa ASP. Inagawa ASP ilidai kuchelewesha uhuru hadi

Waafrika wasome, baada ya Mapinduzi kati ya watu wa mwanzo kuuliwa na serikali ya

Mapinduzi walikuwa wale wale viongozi wa Kiafrika waliosoma na serikali kuendeshwa

na wale wasiosoma. Hatimae viongozi wengine wa Kizanzibari wakawasili Zanzibar ku-

toka Uingereza na shamra shamra na muamko wa kuendesha kampeni ukazidi kutia fora

na kabla ya miaka mitatu kupita vizuri, ZNP ikaweza kuchuwana na ASP katika uchaguzi

nakuweza kwenda karibu sare na ASP katika chaguzi za 1961. Kwa wakati huo ZNP

37
ndio iliyokuwa chem chem ya hamasa za upiganiaji uhuru wakati ASP ilitumia siasa ya

"Ugozi na Zuwiya", yaani Ugozi wa rangi nyeusi nazuwiya Uhuru mpaka gozi asome.

Kwa upande mmoja chama cha ASP kiliaibisha Zanzibar, hasa wakati kulipokuwa na

mikutano mikubwa ya nchi za Kiafrika, kama vile PAFMEC kwani msimamo wa ASP

katika mikutano hiyo ulikuwa ule ule waUgozi na Zuwiya uhuru hadi Waafrika wasome

na ndio maana walikataa kuwaungamkono Hizbu katika kudai Uhuru. Suala hili lilileta

aibu hata kufanya viongozikama kina Nkurumah na Kanyama Chiume kuingilia kati na

kuwalazimisha ASPkujiunga katika mapambano ya kudai uhuru, na hatimae kusababishwa

kuundwa "kamati ya uhuru" ya ASP na Hizbu katika mwaka 1958. Katika mikutanoilio-

fanyika PAFMECA, Mwanza 1958 na All African People’s Conference, 1959 Accra na

Zanzibar, ujumbe wa ASP, ulikuwa na wahka kwa sababu katika uongozi wake tokea hapo

nyuma kulikuwa na mgawanyiko baina ya Wa shirazi na Waafro, na katiya Wa Afro ku-

likuwa wale wazalia hasa wa mashamba na "malumpa" "walala hoi" na ambao wengi wao

walikuwa si wenye asili ya Kizanzibari, na kulikuwa na kikundicha wasomi. ASP mwan-

zoni walikataa kubadilisha siasa yao ya kuchelewesha uhuruna kukataa kutotumia ubaguzi

wa rangi kama ni msingi wa siasa yake, ingawajebaada ya kulazimishwa na PAFMECA

walikubali kufanya hivyo. ASP waliogopakusimama katika jukwaa la kudai uhuru pamoja

na ZNP kwa sababu waliogopakwamba suala hili lingeliondosha msingi wa siasa na kam-

peni yao ya kudai kwamba Hizbu ni chama cha Waraabu, ingawa Hizbu walikuwa wote ni

Wakizanzibari kwa auzalia. Nyerere kwa kisiri siri akazidi kupalilia moto kwa kutia sumu

ya kusema kwamba maingiliano ya Wazanzibari bado yalikuwa kama baina ya " Mab-

wana nawengine Watumwa". Ingawaje ASP ikadai katika PAFMECA kwamba, iko tayari

kuiunga mkono Hizbu katika kupigania uhuru na kuwacha ukabila mradi Hizbu nayo ingeli

ahidi kwamba pindi likitoka pande na kujigawa katoka ASP, hawataliunga mkono wala

38
kuungana nalo. Hizbu nao wakakubali masharti hayo kwamba hakuna upande wowote

ule utaounga mkono kundi lolote litalojitenga kutoka katika chama kimoja wapo. Kwa

kipindi fulani vyama vyote hivyo viwili vikawa vianapigania uhuru bega kwa bega kwa

hamasa za pamoja na kitaifa, hata kupanda majukwaa ya mikutano kwapamoja. Kutokana

na mvutano ambao kwa kimsingi ni wakitabaka na vile vile wenyemuelekeo wa uasilia

katika mwisho wa mwaka wa 1959, mvutano huo ulisababishakugawika kwa ASP na

kundi lenye mrengo wa kibwanyenye na kujitambua kamaWashirazi walitoka chama cha

ASP na kuunda chama cha Zanzibar and PembaPeople’s Party (ZPPP). Kwa upande wa

Hibzu nako kulikuwa na mirengo mitatu,mrengo wa kushoto ambao ulikuwa kina A. M.

Babu, Ahmed Badawi Qullatein, Ali Sultani, Abdulrazak Mussa Sima, Miraji Mpatani,

Abdulaziz Ali, Mzee wa Tarekh Muhsin Abeid, Amar Salim Kuku, Salim Ahnmed Salim

n.k.; mrengo wa kulia wa kina Juma Alley na wafadhila wa Wangereza waliyowacha kazi

za serikali dakika zamwisho na kuingia katika siasa, uhuru ulipokuwa unakaribia, kama

vile MohammedSalum Jinja, wengine wa mrengo wa kulia ambao ndio waliyopalilia siasa

ya chuki katika ZNP na kufuata mrengo wa kulia na kuzidi kuleta mifarakano ya kisiasa

baadala ya majadiliano na hatimae kutoka kwa Umma Party, ni Ahmed Lemky,Amani

Thani na Suleiman Malik. Kundi la kati na kati la ZNP lilikuwa ni akina Dk. Baalawi,

Maulidi Mshangama, Amour Zahor, Haji Hussein, Rashid Hamadi, Miraaj Shaalab, Vuai

Kiteweo, maalim Zaid na maalim Mandoa. Itaonekana kwamba hatakatika Kamati Kuu

ya Hizbu nako kulikuwa na mvutano mkubwa sana lakinimvutano huu ulikuwa zaidi baina

ya waliyoendelea wa mrengo wa kushoto na waselelea wa mrengo wa kulia. Kiongozi

wa Hizbu alikuwa Ali Muhsin na kwa sikuza mwanzo alikuwa ni kiongozi mshupavu wa

kujitolea kupigania uhuru wa Zanzibar. Vuai Kitoweo alikuwa Rais wa Hizbu na Katibu

Mkuu kuwa A. M. Babu. Kiongozi wa ASP alikuwa ni Abeid Amani Karume, ambae

39
alikulia Zanzibar, lak- ini Othman Sharif, msomi mmoja wapo katika ASP pamoja na

Abdulla Kassim Hanga, Hasnu Makame, Aboud Jumbe, Abdulaziz Twala walitarajiwa

hatimae kuchukwa uongozi kutoka kwa Karume, na Karume aliwaona hawa kama ni

wasaliti waliyojitayarisha kumpokonya n ofu lake la uongozi. Fungu lililomuunga mkono

Karume dhidi ya wasomi wa ASP walikuwa ni Afro Shirazi Youth League. ZPPP ili-

poundwa mrengo wa kulia wa Hizbu haukusita kunyakuwa nafasi yakuwaunga mkono na

kutarajia kupunguwa nguvu kwa ASP kinyume na ahadi walizozitowa katika PAFMECA,

Accra, ya kutoliunga mkono pande lolote litakalojigawa. Wakati huo, Hizbu ilipoun-

gana na ZPPP, Babu alikuwa safarini na aliporudi akakabiliwa na Karume na kusutwa

kwa maneno kama haya, "jee unaona tulisemaje sisi, unaona si wamewaunga mkono?"

Babu anadai kwamba alijaribu kusema na uongozi wa Hizbu, kwamba wamevunja ahadi

za Mkutano wa Accra bila ya kusikilizwa. Zaidi ya hayo kwa upande wa Hizbu wa

mrengo wa kulia walipata turufu mpya ya kuwapiga vita kina Babu kwa kupata msaada

wa mrengo wa kulia wa ZPPP. Kuundwa kwa ZPPP na kuongezwa katika uongozi wa

Hizbu kwa baadhiya vibaraka kama kina Amani Thani kwa bahati mbaya kulimbadilisha

msimamo na muelekeo wa Ali Muhsin na kumfanya kuelemea zaidi mrengo wa kulia

hata hatimae akishirikiana na Mngereza kumtia Katibu Mkuu wa ZNP A. M. Babu ndani,

akiwa kiongozi pekee chini ya ukoloni wakati wa serikali ya ndani, kuhukumiwa na ku-

fungwa kwa sababu za kisiasa. Njama za makusudi za kumfunga Babu zilipunguza kasi

ya mrengo wa kushoto na wakati katika uongozi wa Hizbu, namara tu alipofunguliwa

Babu mrengo wa kushoto ukadai watoke katika chamahicho. Babu akajaribu kuwazuia

wenzake kudai kwamba lazima wapambane navibaraka hao wakiwa ndani ya chama, na

hapo tu ndipo wangeliweza kuleta makubaliano ya kitaifa kwa maslahi ya Wazanzibari

wote bila ya kujali ufuasi wa chama. Upinzani ulikuwa mkubwa na katika mkutano wa

40
kupendekeza na kupanga watetezi wa uchaguzi wa 1963 kundi la mrengo wa kushoto la

ZNP likadai kwamba chama cha ZNP lazima kichukuwe msimamo wa kitaifa na kuwacha

mtindo zorota wakusimamisha watetezi wa uchaguzi kwa mujib wa rangi au kabila. Yaani

Babu alidai, Ali Muhsin si lazima asimamishwe jimbo la Malindi na Abdulrasul Alarakiya

jimbo la Shangani. Babu alipendekeza Abdulrazak Mussa Simai asimamishwe jimbola

Malindi (Forodhani) na Ali Muhsin asimamishwe jimbo jengine lolote la uhakika, ili

kuwathibitishia Wazanzibari kwamba msingi wa siasa ya Hizbu haukuwa wa kikabila. Na

kuweka wazi kwamba kile ilichotaka Hizbu ni kuleta usawa kwa Wazanzibari wote kwa

jumla. Wale waliyokuwa na kasumba za mrengo wa kulia wakapinga mapendekezo hayo

na hatimae mrengo wa kushoto ukaamuwa kutokubali kufuata siasa hiyo ya kibaguzi na

kujitowa katika Hizbu na Julai, mwaka 1963, kikaundwa chama cha Umma Party na Babu

akawa ni Rais wake. Kufuatilia uchaguzi wa 1957 palifanyika uchaguzi mara ya tatu,

katika mwaka 1961,mwezi wa Januari, matokeo yalikuwa ASP ilipata viti 10, ZNP viti 9

na ZPPP viti 3. Katika mwaka 1961, mwezi wa Juni ASP ilipata viti 10 na ZNP kupata viti

10 na ZPPP viti 3. Katika uchaguzi huu kulitokea ghasiya na maisha ya watu kupotezwa

bure na wengi katika hao waliyoshiriki katika ghasia hizi walikuwa ni watu waliyokuwa na

asili ya Bara. Katika uchaguzi huo mbinu mbali mbali za kuwezesha kushinda zilitumika

sehemu zote mbili. Njia mojawapo ZNP iliyotumia ilikuwa ni kutumia kura za ZPPP

pale ambapo wasingelishinda, kuhamisha wapigaji kura kutoka zile sehemu waliyokuwa

na uhakika watashinda na kupeleka zile sehemu waliyokuwa na wasi wasi wa kushinda.

Utafiti na uchunguzi wa makini na wautulivu ulifanywa na ZNP na kuweza kujua hesabu

ya kila mpigaji kura hadikuweza kujua tofauti ya kura moja. Katika uchaguzi wa mwaka

1963, mwezi wa Julai ASP ilipata viti 13, ZNP viti 12 na ZPPP viti 6 na kwa hivyo ZNP na

ZPPP wakaunda serikali. ASP nao walitumia mbinu zao katika kujitayarisha na uchaguzi

41
lakini mipango na njama zao zilikuwa koroma kwa vile wao walipigania wingi waidadi ya

kura na sio wingi wa ustadi wa upigaji kura.

Ahmed Hassan Diria (mmoja kati ya waliyowauza na kina Hanga na kuwanyanganya

mali Wapemba) na Ali Mwinyi Tambwe, huyu akiwa wa Tanganyika, walishughulika sana

katika siku za uchaguzi kuleta Watanganyika kutoka Bara na kuja kupiga kura Zanzibar.

Tatizo lao katika njama zao ilikuwa kwanza wametumia wageni na kwa vile hawa ilikuwa

ni wageni walipelekwa zile sehemu ambazo zikiunga mkono ASP na kwa hivyo watu

wa sehemu hizo hawakulalamika kwa vile hawa wageni walikuja kuwasaidia wao. Kwa

njia hiyo ASP ilizidisha idadi ya watu katika zile sehemu ambazo walikuwa tokea hapo

lazima washinde. Vile vile ghasia za Juni (ati leo tunaambiwa zilikuwa majaribio ya

mapinduzi, yaani kumpindua mgereza kwa magongo) zilikuwa na madhumuni yakuleta

vurugu ili watu wasishughulishwe na kuangalia wageni waliyokuja kupiga kura na vile

vile kutisha watu wasiende kupiga kura hasa zile sehemu ambazo ASP ilikuwa na wafuasi

wengi. Kitu kilicho wafaidisha ASP ni baada ya kuhisabiwa kura hizo kudai kwamba wao

ingawa walikuwa na kura nyingi zaidi na hata hivyo walishindwa. Dai hili halikuwa na

tija yoyote, kwani mbinu walizozitumia zilikuwa mbaya. Ushindi ulitegemea idadi ya viti

na sio idadi ya voti; pindi ASP ingelitumia maarifa mengine labda ingelifanikiwa zaidi, na

leo tungelikuwa tunasoma historia nyengine kabisa.

Umma Party haikushiriki katika uchaguzi wa 1963, na mara tu baada ya kujitoa katika

ZNP ilianzisha maingiliano ya kitaifa ya waandishi wa magazeti mbali mbali, vyama vya

wafanya kazi na kuungana na wale viongozi waliyoendelea wa ASP. Wakati huo Hizbu

ilishajiisha chuki kubwa sana dhidi ya Umma Party na hata kuwalazimisha viongozi hao

kuzihama zile sehemu walizoishi Mahizbu wengi, kwakuwafanyia kila kashfa na chuki

42
za kipuuzi viongozi hao wakalazimishwa kuhamia Miti Ulaya. Hii ilikuwa si siasa bali

ni upuuzi wa kisiasa. Kushirikiana kwa Umma Party na vikundi tofauti vya kipinzani

kuliwafanya viongozi washupavu, waliyoendelea na wa mrengo wa kushoto wa ASP kama

vile Hanga, Khamis Masoud, Twala, Saleh Sadalla n.k. kupata nguvu zaidi ndani ya ASP.

Kuundwa na kushiriki kwa ZPPP katika makubaliano ya mbinu za uchaguzi katika

uchaguzi wa 1963 kulirahisisha kushinda uchaguzi huo kwa urahisi zaidi, na hatimae ZNP

na ZPPP kuunda serikali. Serikali hiyo ambayo ilikuwa na Waziri Mkuu Mohammed

Shamte na Kiongozi wa serikali Ali Muhsin mara ilisahau wapi ilitoka nakuanza kutumia

mbinu mbaya za kisiasa za kutumia mabavu ambayo hata Mngereza hakuyatumia. Kitendo

chao cha mwanzo cha kidikteta kilikuwa ni kupitisha sheria ya kufungia chama cha Umma

Party, khatua iliyo kwenda kinyume na misingi ya demokrasia. Umma Party, kwa wakati

huo, kilikuwa kikijaribu kuunganisha Wazanzibari wote kwa jumla. Kwa bahati mbaya

Serikali ya Hizbu iliingiwa na wasiwasi mkubwa na vuguvugu la kitaifa lililokuwa likizidi

kupata nguvu, na serikali hiyo ikafikiria zaidi maslahi ya serikali yake kuliko ya nchi

nzima. Kama ilivyofichuliwa baadae serikali hiyo ilikwisha tayarisha nyaraka za kutiwa

ndani kwa viongozi mbali mbali wa Umma Party na ASP, lakini kwa bahati watu hao wali-

pata fununu na kukimbia nchi, Babu kukimbilia Dar es salaam. Serikali hiyo, ikapitisha

sheria nyengine kinyume na demokrasia, nayo ilikuwa kulifungia ruhu- sa yauchapishaji

gazeti mashuhuri la ZANEWS ambalo ndilo lililokuwa gazeti la maendeleo la kifani lisilo

kuwa na upuuzi wa chuki za kikabila na siasa ya kupendelea matabaka ya kikandamizaji.

Vitabu vingi vilikamatwa na kuchukuliwa na serikali, kuzuilia watu haki ya kidemokrasia

ya kuwa na uhuru wa kusoma. Mambo yote hayo yalikuwa yakiruhusiwa hata chini ya

utawala wa Ukoloni wa Kiingereza. ZNP ilikiogopa chama cha Umma Party kwa sababu,

chama hicho kilikuwa kikiungwa mkono zaidi na vijana wengi sana na wale waliyokuwa

43
na siasa ya kishupavu.

3.8 Umma Party

Chama cha Umma Party kama ilivyonakiliwa hapo juu kiliundwa kutokana na mchuano wa

kujaribu kuhifadhi misingi ya kijananchi ya usawa na umoja baina yaWazanzibari, kupi-

gania uhuru wa kweli na sio kivuli cha uhuru kilichomficha mwenye khatamu za kweli za

utawala, yaani uhuru wa bandia. Mwanzoni suala lakupigania uhuru wa kweli lilikuwa ni

lengo halisi la kuundwa kwa Hizbu, chama ambacho kilizalika na vuguvugu la kihamasa la

Ujananchi wa kugomea Majlis ‘ltashrih na "vita vya n’gombe" vilivyo ongozwa na akina

Vuai Kiteweo. Historia ya Hizbu inadhihirisha wazi kwamba chanzo cha mapambano

ya chama hicho kilikuwani ya kimaendeleo, kama "vita vya n’gombe" vilivyothibitisha,

msimamo wa chama hicho ukaendelea kuwa na nidhamu ya kupigiwa mfano wa kupinga

kutawaliwa,kudai uhuru bila masharti yoyote, kupigania utawala uliyowekwa na watu

wenyewe, kuendeshwa na watu wenyewe na kwa maslahi ya watu wenyewe, na kuunga

mkono upiganiaji uhuru na ukombozi wa nchi zote zilizokandamizwa nakuwa dhidi ya

ukoloni na ubeberu. Kutokana na siasa shupavu chama hicho kikaweza kwa muda mfupi

tu kugeuza kushindwa kabisa katika uchaguzi wa 1957na kuwa na nguvu za kupata viti

karibu sawa na chama cha ASP katika uchaguziwa Januari na Juni 1961. Siku hizo Hizbu

ililitukuzisha jina la Zanzibar katika vikao na mikutano mbali mbali ya kupigania haki

za waliyoonewa ulimwenguni kote. Kuunga mkono vuguvugu la kugombania uhuru wa

bara la Afrika na kupinga vikali udhalimu waliyofanyiwa Waafrika mbali mbali kama vile

kukamatwa, kuteswa nahatimae kuuwawa kwa mpiganiaji uhuru mashuhuri na mshupavu

44
Patrice Lumumba. Baadhi ya viongozi wa Hizbu walipoanza kuona uwezekano wa ku-

pata khatamu ukokaribu wakaanza kubadilika na wengine nyuso zao za kikweli zikaanza

kudhihiri.Wale viongozi washupavu waliyompinga Mngereza kinaga ubaga na kupinga

siasaya kibaguzi wakaanza kupikiwa majungu na kuwekewa vikwazo vya aina mbalim-

bali. Kutokana na mbinu kama hizo ndipo Katibu Mkuu wa ZNP, Babu, akabuniwa kesi

na kufungwa na serikali ya ndani ya chama ambacho alikuwa ni katibu wake. Hii ilikuwa

ni mbinu ya kumuondosha njiani ili kurahisisha kupitishwa kwa mamboambayo yeye an-

geliyapinga. Wakati huo ndipo vitimba kwiri waliyokuwa hawana ujuzi au uwezo wa

kisiasa navibaraka wa kiiengereza walipozidi kupenyezwa katika uongozi wa ZNP hasa

wale waliyokuwa wakifanya kazi serikalini chini ya Mngereza. Walipoingiya katikauon-

gozi vitimba kwiri na vibaraka hivyo vikapewa nyadhifa za juu na kutapakaza kasumba

zao na kutia sumu na ubaguzi katika chama ambacho sifa zake zilikuwa ni za kifani kabla

ya hapo.

Wakati bahari ilipokuwa chafu na mawimbi kuwa makali, waungwana hao walificha

kucha zao na kungoja ufukweni, lakini kazi ngumu ilipomalizika na bahari kuwashuwari

wakaanza kujipenyeza katika uongozi, wengine kupewa nyadhifa wasizozimudu na kum-

tumikia Mkoloni ama kwa kujua au kwa kutotambua. Hali hii iliaibisha sana kwa kuitia

ZNP doa na baka pale ambapo nuru ikin’gara. Nguvu za mrengo wa kushoto na wa kati wa

ZNP zikazidi kupunguwa na kufifia na vitimbakwiri na vibaraka wakazidi kukaza kamba

huku wakiiangamiza Zanzibar. Wakati A. M. Babu alipomaliza kifungo chake na kutoka

gerezani dosari lilikuwa ni kubwa mno bila ya kuweza kutengezeka. Ingawa walijaribu

kuirejesha ZNP katika mkondo wake wa kijananchi, wa kimaendeleo na wakimapinduzi,

haikuwezekana tena kwa vile athari iliyofanywa na kina Amani Thani ilikwisha tendeka

na kupitia mpaka.Waliyotoka serikalini kwa Mngereza walitoka pamoja na kasumba zao

45
bila ya kuweza kujirekibisha na kuwa na fikra zile zile za kitabaka na kibaguzi kama

walivyotiwasumu, vipi wafikiri. Ingawa hawa walikuwa ni Wazanzibari wa kizalia, lakini

kwa vile walikuwa karne za nyuma na asili ya kiarabu na kuwa wasomi, wakatafsiriwa na

wale waliyokuwa na upungufu na upeo wa kisiasa, wakafanywa kama ni kisingizio cha

kuwadanganya makabwela kuwa ni watu waliyotaka kuleta utawala wa kiarabu na wa wa-

somi. Wanasiasa waliyokuwa wenye fikra za kikasumba walikuwa ndani ya vyama vyote,

hata na wale waliyojiita Waafrika. Ubovu wao ulitokana na fikra zao na sio namna ya sura,

rangi au makabila yao au kwamba walikuwa wasomi au pangu pakavu. Kwa wakati huo

Bara la Afrika zima pamoja naZanzibar lilikuwa na wataalam wa hali ya juu bila ya kuwa

na asili ya Uarabu, naingawa Waafrika wa asili na jadi walikuwa na elimu ya juu kabisa

haikuwafanya wote kuwa na fikra za kisiasa madhubuti na za kimaendeleo, kwani kati yao

kulikuwa na waliyokuwa na kasumba ya hali ya juu kabisa. Ujuzi wa kisiasa una miko yake

nasio kila mtu anaweza kuwanayo. ZNP kuegemea viongozi waliyokuwa na upungufuwa

sifa za kisiasa na kuwa na sifa nyengine tofauti za kibwanyenye ilikuwa nimakosa ambayo

yaliirejesha Zanzibar nyuma sana. Wale waliyotumia siasa yaukabila walifanya hivyo

kwa sababu ya ukosefu wa mfumo wa siasa maalum yaku tatua matatizo ya nchi kisiasa.

Wakati wa kabla ya uhuru kupatikana, ulikuwa ni wakati muhimu sana katika historia ya

Zanzibar, kwani ilikuwa ni wakati huo ambapo hali ya juu kabisa yakisiasa ilikuwa itumike

kwa manufaa ya watu wote. Huo ulikuwa sio wakati ambapovyama vya kisiasa vili kuwa

vipapatikie ullwa na khatam za serikali. Huo ulikuwani wakati wa vyama tofauti vya

kisiasa kuungana na kuyalinda na kuyachungamaslahi ya Zanzibar na sio vuta n’kuvute.

Wale wenye akili za mchwa za kuila nyumba wakayo walitumilia hali hiyo ya ubina fsi

na kuzidi kutia chuki baina yaWazanzibari, chuki ambazo kwa desturi ni fikra za wale

watu ambao hawana kinaau upeo wa ufahamivu wa kisiasa, watu wa aina hii walikuwako

46
katika vyama vyoteviwili vikubwa vya kisiasa . Mwenye ujuzi wa kisiasa hutumia ho ja

za kisiasa na sioza kikabila, kwani siku zote kiini bora cha kisiasa huwa kinaambatana na

sababuza kimsingi nazo ni kukomesha sababu ambazo hujengeka kwa ubaguzi wakitabaka.

3.9 Zanzibar kama tausi

Kabla kuundwa kwa Umma Party, wale viongozi wa ZNP waliyokuwa na mrengo wa

kimaendeleo walijaribu kuunganisha Wazanzibari wa vyama mbali mbali, kuondosha

ubaguzi wa aina mbali mbali katika ZNP. Mapambano ndani ya ZNP yalikuwa nimagumu

na kama ilivyoelezwa huko nyuma wengi wa mrengo wa kushoto walitakakujitoa katika

chama hicho lakini A.M.Babu alisisitiza wapambane wakiwa ndani yachama na kwa njia

kama hiyo ndio wangeliweza kuubadilisha mfumo wa chama hichokuwa bora zaidi. In-

gawaje hatimae hata yeye nae, yaani Babu, alipungukiwa nasubra wakati Kamati Kuu

ya ZNP alipokuwa akiteuwa wagombeaji uchaguzi wamwaka 1963. Katika kikao hicho

Babu alisisitiza kwamba ili ZNP ionekane kwambani chama cha Kizanzibari kisichokuwa

na ubaguzi wa aina yoyote ile na kwa vile ZNP ilikuwa ni chama chenye mchanganyiko

wa watu wenye asili mbali mbali basi,ilibidi uwekwe mfano dhahiri kwa kila mtu kuona

kwa macho yake mwenyewe. Kwahivyo katika mkutano huo Babu, kama ilivyotajwa

hapo juu, akapendekezaAbdulrazak Mussa Simai, msemaji mashuhuri katika mikutano ya

hadhara ya Hizbuambae alikuwa hana asili ya kiarabu, awe mtetezi wa jimbo la uchaguzi

la Malindi.Hili lingekuwa pigo kubwa kwa siasa ya Mngereza ya kutaka kugawa watu

kwamafungu ya kikabila na ingelikuwa ushindi mkubwa kwa siasa ya ZNP ya kukome-

sha ukabila na kuweka Wazanzibari w-ote sawa. Mrengo wa kulia waHalmashauri Kuu

47
ya ZNP ikapinga pendekezo hilo na hapo ndipo maji yalipomwagika na kina Babu, Ab-

dulrazak Mussa Simai, Muhsin Abeid, AbdulazizAli, Miraji Mpatani, Ali Sultani, Amar

Salim Kuku, Ahmed Badawi Qulllatein, Salim Ahmed Salim, Dr. Ahmed Rashid, Tahir

Adnan na wengineo kutoka chama nakuunda Umma Party iliyokuwa na siasa ya Wazanz-

ibari wote kuwa sawa. Dr. Idarus Baalawi na Maulid Mshangama walikuwa ni viongozi

wawili wa ZNP waliyokuwawakitia na kutoa kujiunga na Umma Party na kwa kweli mku-

tano wa mwanzo wawaandishi wa magazeti wa Umma Party ulifanywa katika nyumba ya

MaulidiMshangama, huko Mbuyuni. ZNP ilisahau kusisitiza uendelezaji wa sura ya Zanz-

ibar yakuwa nchi iliyokuwa na mchanganyiko wa damu, makabila, mila, jamiina utamaduni

tofauti, nchi yenye rangi kama za tausi, tofauti ya rangi zake zikiwandio sifa na pambo lake.

3.10 Vugu vugu jipya la Upinzani

Chama cha Umma Party kilikuwa hakina kasumba za ugozi au ukabila, lengo lake lilikuwa

kuwakombowa Wazanzibari kisiasa, kiuchumi, kijamii na kitamaduni. Lengola Umma

Party halikuwa kuimba wimbo wa kupigania uhuru tu bali ilileta mfumo mpya wa kisiasa

ambao uliwavutia Wazanzibari tofauti kutoka matabaka tofauti.Umma Party ilipendeza

kwa Wazanzibari kwa sababu haikuwa tu inadai uhuru bali ilikuwa imeshatayarisha pro-

gram/sera iliyohitajika ya kufanya maisha ya Mzanzibari bora. Ilikwisha tayarisha jinsi ya

haki za mfanyakazi zilindwe, kuhakikisha kwamba mtuanapata kipato kwa mujib wa mahi-

taji yake, yaani yule mwenye ukoo mkubwaalikuwa apatiwe kipato cha kutosheleza ukoo

wake wote. Kuwahakikishia wafanyakazi kazi bora, sheria za kuwalinda na kuwaepusha

na ukosaji kazi.Kuwahakikishia wafanya kazi mapumziko ya likizo marefu na malipo yake

48
yakutosha. Kuwahakikishia malipo ya kujitizama wakikosa kazi. Kuwajengea makaaz-

ibora na ya siha njema ili wawe watu wenye siha nzuri za kuweza kuitumikia jamii yao

vyema. Wakulima walikuwa wahakikishiwe uuzaji wa bidhaa zao kwa bei muwafaka na ku-

patiwa misaada wanayohitaji katika jukumu lao la uzalishaji mali bora. Walikuwa wapewe

vifaa vya lazima vilivyoendelea, kupewa mikopo ya kuendeleza kilimo bora,kusaidiwa

kwa ujuzi wa kisasa na kujengwa kwa sehemu za mashamba ili kuwezakujitegemea na

kuwekewa Benki ya maendelo ya ukulima na uvuvi. Mashambakuweza kuwa na huduma

zote zilizopatikana mjini bila ya haja ya kusafiri safiri.Kuwahaki kishia watu wa mashamba

umeme, maji safi ya mfereji, makaro, usafi namaskuli ya madarasa ya juu yaliyokuwa na

sifa sawa na mijini. Kuwajengea watuwa mashamba vituo vya siha vilivyoweza kuhudumia

magonjwa yote ya kawaida namagonjwa makubwa sana tu kupelekwa Spitali Kuu. Ujenzi

wa mashamba ulikuwauwe na vituo mbali mbali ambavyo vitu vyote vilikuwa viweze ku-

patikana katika"centa" maalumm bila ya kulazimika kwenda mijini. Kulipangwa ujenzi wa

viwandambali mbali katika sehemu hizo za mashamba. Wavuvi walipangiwa uvuvi bora

wakutumia vifaa, mitambo na vyombo bora. Kuhakikishiwa usalama wao wakiwabaharini

kwa kuweza kuwasiliana na vyombo vya dola kama wangelipata matatizo.Walikuwa wa-

hakikishiwe vyumba vya barafu vya samaki wao na kuhakikishiwaviwanda vidogo vidogo

vya kutia samaki katika vibati. Wavuvi kwa vile wengi waoni watu wa mashamba wangeli-

pata huduma kama zile wakulima waliyozipata kwa vilewote wakiishi katika mazingara

ya aina moja.

Maisha ya Wanawake yalikuwa yaendelezwe kwa kila fani, sehemu za wazazi maspital-

ini zilikuwa ziendelezwe ili kumtukuza mzazi na kumfanya ajivunie kuzaana kutambuwa

kwamba kuzaa kwake kulikuwa ni kutekeleza wajib mtukufu katikajamii. Wazazi wa-

likuwa wapewe mapumziko maalum baada ya uzazi, wale waliyofanyakazi kuhakikishiwa

49
mishahara yao kamili kwa muda wa kutosha na wale waliyokuwawakifanya kazi za kutunza

ukoo kuhakikishiwa kipato sawa na mahitaji yao. Siha za watoto wao zilikuwa zitunzwe,

kuangaliwa na kufuatilizwa tokea wakiwa wachanga. Kuhakikishiwa kupata chakula bora,

kuchanjwa, kupimwa kwa majira kuhakikishiwa malezi bora ikiwa kwa kusaidiwa mabibi

zao waliyowaleya au kuwajengea sehemu maalum za kutunzwa wakati wazazi wao wakiwa

wameshughulikana kazi. Ilipangwa kuwahakikishia mabibi kazi na majira bora ya kazi

na kuwahakikishia kipato bora na haki sawa katika jamii. Elimu ya mabibi ilikuwaitiliwe

mkazo mkubwa zaidi.

Wazee wote waliyokuwa na jamaa au bila ya jamaa walikuwa wahakikishiwe maisha

bora bila ya kupata taabu zozote. Walikuwa watizamwe katika vituo maalum vyawazee,

pale ambapo pangelihitajika. Wagonjwa, wasiyojiweza na vilema walikuwa wapewe

haki saha na wananchi wengine na walikuwa watizamwe na kutunzwa bila ya ubaguzi

au dharau yoyote.Ilipangwa wapewe huduma zote za lazima bila malipo au mapendeleo

yoyote,kuhakikishiwa elimu na siha bora wakiwa chini ya uangalizi wa watu waliyoji-

funzakazi hizo. Vijana walikuwa wahakikishiwe maisha bora majumbani mwao ambako

wazee wao walikuwa wahakikishiwe maisha bora na jamii kwa jumla ilikuwa iwahakik-

ishie kipato cha kutosha na kwa hivyo jamii kuweza kuwatizama vijana na kuwahakikisha

maisha bora. Kama vijana wangelihakikishiwa maisha bora majumbani mwao wangeli-

weza kushiriki kikamilifu katika masomo tofauti ya kujiendeleza. Masomo ya aina mbali

mbali ya kutosheleza matakwa ya kijana wa Kizanzibari yalikwishapangwa ambayo yal-

isisitiza umuhimu wa masomo mbali mbali kuambatanana mazingara yetu. Skuli za

kawaida zilikuwa ziende sambamba na maskuli mbalimbali ya ufundi kwa madhumuni

ya kutajirisha siasa+ na uchumi wa Zanzibar.Maskulini elimu ya kilimo ilikuwa itiliwe

mkazo kuambatana na mazao tuliyokuwanayo na yale ambayo yangewezekana kupan-

50
dishwa baada ya uchunguzi nautaratibu makini na maaluum. Mfano mwengine maskuli

hayo yangelifundisha zaidikuhusu bahari ya Zanzibar na hazina yake na kujuwa jinsi ya

kuitumia, kuitunza na kuihifadhi bahari hiyo. Masomo kama haya na mengi mengineyo

kama ya siha,uchumi, n.k. yalikuwa yaendelezwe tokea skuli za msingi na hatimae vi-

jana kuwana uzoefu bora wa kuchaguwa na kujua walichotaka kufanya baadae katika

maishayao yakiambatana na majingara ya nchi. Vijana walikuwa walindwe na uhuni

nakuzurura ovyo na baadala yake walikuwa wapewe nafasi tofauti za kuwawezesha ku-

tumikia jamii na kujifurahisha wenyewe kama vile katika riadha na michezo mbalimbali.

Vijana ndio walitizamiwa hatimae kulijenga taifa la Kizanzibari na kwa hivyo mipaka ya

kujiendeleza walikuwa wawe nayo wenyewe. Wazanzibari wote walipangiwa wawe na

haki sawa sawa na haki hizo kulindwa nakuhifadhiwa na Mahkama huru, zenye msingi wa

Katiba na Sheria halali.

Wafanyakazi serikalini walikuwa na haki ya kufuata siasa yoyote waliyoitaka,lakini walipokuwa

makazini mwao walikuwa wawe na wajib wa kuutumikia umma wa Kizanzibari bila

ya kujali imani na vyama vyao. Na serikali yoyote ambayoingelitawala isingelitakiwa

iwabadilishe wale wafanyakazi wa serikali ambao imanizao zisingeliambatana na siasa ya

serikali. Wafanya kazi hao walikuwa wahakikishiwe ulinzi wa haki zao zote za kifanya

kazi, kupewa haki zote zilizostahiki. Wale ambao wangelikosa kazi wangelifanyi wa mi-

pango ya kulipwa hadi kupata kazi upya. Wazanzibari walikuwa wahakikishiwe kushiriki

kikamilifu katika ujenzi wa dolalao na kupewa uhuru wa kuchaguwa viongozi ambao

wangeli wawakilisha katika Bunge halali na kuhifadhiwa haki zao zote za Kidemokrasia,

kama vile uhuru wakusema, wa kusoma na kuandika, wa kujikusanya na wa kufanya

mikutano,kugoma na kuuandamana, haki za kibinaadam kwa jumla n.k. Mipango ili-

wekwa kuhakikisha kwamba hakutakuwa na tofauti yoyote baina ya Pemba na Unguja.

51
Umma Party ilikataa kujishughulisha na siasa za kipuuzi za Ugozi na Ukabila kwa sababu

ilikuwa na program maalum ya kuihifadhi na kuinusuru Zanzibar. Umma Party ilikuwa

na mpango maalum wa Uchumi wa kuinusuru Zanzibar. Mpango wa uchumi huo ulikuwa

ni usambazaji wa vituo tafauti katika sehemu maalum mbalimbali za Unguja na Pemba.

Vituo hivyo vilikuwa viwe kama chem chem, kiini chahuduma tafauti, zenye michirizi ya

kiuchumi, michirizi hiyo ilikuwa iizunguka chemchem hizo kutoka kila pembe. Michirizi

hiyo ilikuwa iwe kama mishipa ya damu,ikiwa na sifa zote za kijamii zikinufaisha maisha

ya mwananchi, kwa mfano mchirizi mmoja ungelikuwa unawakilisha tu seme ukulima au

uvuvi. Kwanza mchirizi huu ungelijengwa kwa mujib ya uwezo na mazingara maalum

ya sehemu inayohusika naungelipangiwa mipango ya hali ya juu kabisa kuambatana na

uchunguzi wakisayansi ili kuwezesha kuzalisha mazao bora kabisa. Mchirizi huo ungeli-

hakikishiwa usafiri bora kabisa na sio mabarabara mabovu yenye mashimo matupu, bara

bara zilikuwa ziwe za kuweza kusafirishia bidhaa kwa haraka na kwa usalama. Bara bara

hizo wakati huo huo zingelifaidisha maendeleo ya jumla yasehemu inayohusika na nchi

nzima kwa jumla na kuwezesha uuzaji na usambazajiwa vifaa na bidhaa tofauti. Michirizi

mingine ungelihusika na vitu kama vile ujenzi wa viwanda vidogo vidogo mbali mbali,

ujenzi wa majumba bora, ujenzi wa maspitalina maskuli, usambazaji wa umeme, soko na

vituo vya biashara, siha bora: vituobora vya siha, maji safi , makaro n.k. Upangaji makini

wa mambo hayo ungelizaamakazi mbali mbali katika sehemu hizo na kukuza hali bora

ya maisha ya wananchi sehemu zote. Vituo kama hivyo vingelisambazwa sehemu tafauti,

kila kimojakujishughulisha na mambo maalum yaliyohitajika nchini na yaliyoambatana

namazingara yao na vingeliingiliana kwa madhumuni ya kusaidiana na kushirikiana.Fedha

za ujenzi huo zingelitokana na uchumi wa nchi kwa jumla, uchumi ambao hatimae un-

gelinufaika kutokana na maendeleo hayo. Kwa wakati huo uchumi wa Zanzibar ulikuwa

52
umenona. Wananchi wa sehemu hizo mbali mbali wenyewe walitarajiwa kupatiwa ujuzi

uliyohusika na hatimae wenyewe kuendesha miradi hiyotofauti ikipewa muongozo na

marekibisho tu na Serikali Kuu.

Siasa ya miaka ya mwanzo ya 1960 na kuendelea ilikuwa ni siasa iliyonuka mizoga ya

kikabila na ugozi, tofauti kabisa na siasa ya leo, wakati ambapo Wazanzibari karibu wote

wanapigania Uzanzibari na kukataa kumezwa na Bara. Ingawa leo wanaotumia siasa ya

ukabila ni wachache na wasiyokuwa na maana, juu ya hivyo bado pana haja kubwa sana ya

kukariri ubaguzi wa kikabila ili kufaham historia nasababu za kutumia njama hizo. Suala

hili litakaririwa zaidi wakati tukio la Mapinduzi na siasa ya CCM zitakapochambuliwa.

Umma Party ilibahatika kuwa na viongozi na wafuasi wengi waliyosoma, kushir- ikikatika

kuijenga ZNP na kwa kupitia njia hiyo kuweza kukielewa chama h- icho vizurizaidi jambo

lililokuwa na umuhimu mkubwa mno baadae. Baadae U- mma Party kwakupitia "United

Front" iliweza kusaidia kurekibisha mfumo wa wale viongozi waASP waliyokuwa mrengo

wa kushoto. Siasa ya Umma Party ilikuwa kuwapiganiawanyonge na ilibahatika kuwa na

mizizi katika tabaka la wafanyakazi na wakulima vile vile, hali hii ilizidi kupata nguvu

kwa kuungwa mkono na Umoja wa Wafanyakazi wa FPTU (Federation of Progressive

Trade Unions) ambao ulikuaUmoja wenye msimamo madhubuti, imara na wa kimaen-

deleo. Kuungwa mkono kwaUmma Party na FPTU kulikuwa na umuhimu mkubwa sana

kwa vile Umoja huuulikuwa umeshatia mizizi katika umma wa wafanyakazi na wakulima

na Umoja ambao ulikuwa unaaminika na kuwa na maingiliano mazuri na ZPFL (Zanz-

ibar and Pemba Federation of Labour) Umoja wa Wafanyakazi uliyofanyakazi pamoja na

ASP. Maingiliano haya hatimae yakazalisha Zanzibar Revolutionary Trade Unions. Kwa

muda mfupi wa maisha ya Umma Party, kabla ya chama hicho kupigwa marufuku nana

serikali ya ZNP, kiliweza kuunganisha wanasiasa na vijana wote wa mrengo wakati na wa

53
kushoto. Wakati wa kuundwa Chama cha Umma nyoyo za watu wengizilifurahika na kuwa

na tamaa kubwa ya chama hicho kuleta mabadiliko yakimaendeleo Zanzibar. Pindi inge-

likuwa chama hicho hakikufungiwa na Hizbu miezisita tu baada ya kuundwa, basi Zanzibar

leo ingelikuwa inajitawala wenyewe, ikiwana wataalam wake wote na utajiri wake wote

mikononi mwake wenyewe kwa manufaaya kila Mzanzibari. Na maingiliano ye- tu na

Tanganyika yangelikuwa ya kidugubaina ya nchi mbili huru zinazohishimiana, kutukuzana

na kusaidiana kimaendeleo,na sio kutawaliana. Siasa ya chama cha Umma ilipendeza kwa

haraka sana hasa katika jamii ya vijana na baina ya watu wa matabaka ya chini wa vyama

vyote viwili vikubwa. Lengomojawapo muhimu ilikuwa ni kujaribu kuleta masikilizano

mema hasa na mrengo wakushoto wa ASP na haikuchukuwa muda mrefu vyama vyote

hivi viwili vikubwavikaanza kuingiwa na wasi wasi walipoona vijana na wafanya kazi wa

sehemu zotembili wakikaribiana katika mfumo mpya wa uhuru na umoja. Kushirikiana

huku na ASP, vyama vya wafanya kazi na vyama vya waandishi magazeti na wengineo

vilileta imani na muamko mpya visiwani. Hapo pakaundwa United Front "muunganisho

wa vyama na fikra tofauti " na muelekeo wa mapambano ukaanza kutia sura mpya. Huu

ni wakati mmoja wapo muhimu sana katika historia yaZanzibar kwa ni kipindi hichi cha

muda wa miezi sita, kutoka Juni, 1963 hadiJanuari 64, nchi nzima ulipambwa na jazba

za kinajananchi zilizofanya damu zawana nchi kuchemka na kuwa na matumainio ya hali

ya juu kabisa. Jambo muhimu lililofanya hamasa za kijananchi wa Kizanzibari ilikuwa

ni uundaji wa Umma Party,kwani baada ya kuundwa chama hicho, mfumo wa upinzani

ulichukuwa sura mpyakabisa. Hali hii ya kujitolea ilitokana na program ya Umma Party

katika kuipangiaZanzibar mikakati ya kimapambano ya siku za usoni. Kuunganisha kwa

vikosi mbalimbali vya utayarishaji mabadiliko yakuleta neema nchini uliwafanya vion-

gozi mbalimbali wa vyama vilivyounga mkono ASP, kungana kwa dhati na Umma Party

54
katikakuijenga Zanzibar mpya. ASP kwa wakati huo ilikwisha shindwa katika uchaguziwa

1963 na viongozi wake waliparaganyika na kutokuwa na msimao madhubuti, nakutokuwa

na siasa na sera mkakati ya kupambana na serikali ya Hizbu. Kwa hivyokuchomoza kwa

chama cha Umma Party na kuchukuwa dhamana ya kujengaupinzani mpya kwa kuunga

nisha waandishi wa upinzani, vyama vya wafanyakazina wakulima, vijana na wanawake

na viongozi "militant" wa ASP na Umma Party,ulifanya muamko wa Zanzibar kupata

hamasa mpya. Wadhifa wa mwanzo wa umojahuu mpya ulikuwa kukuza elimu ya kisiasa

na kupanga mbinu za kupambana,kuweka misingi mipya ya kufanya kazi za kichama na

aina mpya ya mfumo wamapambano. Hali hii iliwezekana kutokana na ukakamavu na

uzoefu wa mipango yakisiasa wa uongozi na wafuasi wa Umma Party. Upinzani mpya

ukazalika na tamaaya kujikombowa ikazidi kutia nuru.

3.11 Serikali ya taifa

Muda ulikuwa mfupi kwa chama cha Umma kuweza kushiriki katika kampeni za kujian-

daa kichama, kwa hivyo chama hicho hakikupata wakati wa kukuwa nakujisambaza zaidi.

Nguvu za wana Umma hao zilikwishatumika kujenga siasa ya msingi ya kupigania uhuru.

Umma kwa sababu hizo iliamuwa kutoshiriki katika uchaguzi wa 1963 na badala yake iliji-

palilia kutowa elimu ya siasa ya kimsingi katika jukumu la kujaribu kuwaleta Wazanzibari

wote pamoja. Kwa mara ya mwanzo tokea kuanza kwa siasa za kupigania uhuru palikuwa

na tamaa ya Wazanzibari wote kuungana, hasa katika mambo fulani ya kimsingi.

Wakati huo muungano wa ZNP na ZPPP ndio uliyokuwa ukiendesha serikali ya ndani

na kufuatia uchaguzi wa 1963 vyama viwili hivyo vikaishinda ASP na kuendelea kuende-

55
sha serikali peke yao, hadi kupatikana kwa uhuru Disemba 10, ingawa ASP ilipendekeza

kuundwa kwa serikali ya kitaifa yaani ASP nayo kuwemo serikalini. ASP ilivunjika moyo

sana kwa kutoshirikishwa katika uongozi wa nchi hasa kwa vile uhuru ulipiganiwa na

vyama vyote, na mada ya uongozi wa nchi ni wadhifa wawananchi wote kwa jumla, bila

kujali ufuasi wa chama fulani. Pindi pangelikuwa na serikali ya Kitaifa basi Zanzibar

leo ingelikuwa nyengine na kuweza kupiga khatuwa kubwa sana, kwani kusingelikuwa

na Muungano na nchi ingelitononeka. Katika serikali hiyo ya 1963, ni ZNP kwa kweli

ndiyo hasa iliyokuwa ikiendesha serikali na Mohammed Shamte alikuwa kawekwa kama

kilemba tu.

Serikali ya ZNP, badala ya kujishughulisha na uongozi wa taifa kwa njia ya kiusawa na

kihalali, kwa kweli ilishughulishwa zaidi na kuipiga vita Umma Party hata kuvisahau

vyama vya ASP na ZPPP. Ilifanya hivyo kwa sababu ilihisi kwamba Umma Party ilikuwa

na uwezo na ujuzi wa kuweza kupambana na ZNP na hatimae kuweza hata kuwachukuwa

wafuasi wa ZNP, hasa kwa vile ni makada wa Umma ndio waliyoijenga ZNP na wakiz-

ijuwa mbinu na mipango yote. Kwa vile ZNP ilitambua ukweli huo. Chini kwa chini,

kwa siri kabisa, ikaanza kupika majungu ya siri kwa kugawa silaha baina ya wafuasi

wake chini ya uongozi wa wale vijana waliyofunzwa mambo ya kijeshi huko Misri, kati

ya vijana hao walikuwemo baadhiya wana ZNP wa mwanzo waliyofariki katika mapin-

duzi ya 1964. Silaha hizo hazikutolewa kwa maksudi ya kupigia paredi. Moja kati ya

njama zilizopangwa naserikali ya Hizbu ilikuwa ni kumkamata Babu, pamoja na viongozi

fulani wa ASP, lakini Babu alizipata fununu hizo na kutoroka Unguja na kwenda Dar

es salaam. Ilidhihirishwa baadae kwamba kulikuwa na listi ya watu 120 serikali hiyo

ya ZNP alitaka kuwatia mbaroni, listi hiyo ilikamatwa baada ya Mapinduzi. Baada ya

uhuru serikali hiyo ikapitisha sheria za kikandamizaji ambazo hata mkoloni Mngereza

56
hakuzipitisha wakati wa ukoloni, nazo sheria hizo zilikuwa kinyume na dhidi ya haki za

kibinaadam na demokrasia kwa jumla. Hapo ndipo haki na uhuru wa kutoa maoni kuanza

kukandamizwa, uhuru wa kukutana na kuchapisha ukanyimwa, uhuru wa mtu kujiunga na

chama atakacho ukaingiliwa kati, uhuru wa kusafiri ukapunguzwa na uhuru wa mahkama

huru ukaingiliwa katikwa kuwa na kupalilia sheria ya kumweka watu vizuizini. Hatua

zote hizi za kuvunja haki za kibinaadam zilikuwa zimepangiwa Umma Party, chama am-

bacho kilipigwa marufuku, kama ilivyotajwa hapo juu. Gazeti lake la Sauti ya Umma

na ZANEWS kufungiwa na kupanga mipango ya kuwakamata viongozi wote wa Umma

pamoja na viongozi wengine wa Upinzani, yaani wa ASP, FPTU na ZPFL. Mipango hii

ndio kwa upande mmoja iliyosababisha na kuharakisha kufanyika kwa Mapinduzi(Hizbu

wasimlaumu mtu kuhusu Mapinduzi kwani wame yapaliliya wenyewe). Hatuwa hizi za

kikandamizaji zilizidi kuwaleta pamoja viongozi wa Umma na wamrengo wa kushoto

wa ASP pamoja na vyama vyao vya wafanyakazi na waandishiwa magazeti pamoja na

vijana. Kwa upande mwengine kuungana kwa Umma na mrengo wa kushoto wa ASP

ambao ulikuwa na karibu wataalam wote wa ASP na wakati huo huo wakiwa ni Wazanz-

ibari asilia, ulileta mgogoro katika uongozi wa ASP. Uongozi wa ASP nao ulikuwa na

migogoro yake wenyewe hata kabla ya kuundwa kwa Umma Party. Itakumbukwa huko

nyuma, kwamba tokea kuundwa kwa ASP katika mwaka 1957 kulikuwa na matatizo baina

ya Washirazi na wale waliyokuwa na asili ya Bara na hapo ikabidi Nyerere aingie kati

na kufudikiza fudikiza. Matatizo hayo hayakutatuka nahatimae kina Shamte wakaunda

chama chao baada yakiongozi mmoja mashuhuri wa Shirazi Association, Sh. Ameir Tajo,

kuadhiriwa katika mkutano wa hadhara wa ASP na kufukuzwa chama. Ingawaje mgogoro

huu baina ya wenye asili ya kibara na ya Kizanzibari haukumalizika hapo kama tutavy-

oona huko mbele. Mvutano mwengine ulitokana na waliyosoma na wasiyosoma, mfano

57
huu ulikuwa zaidi baina ya Karume, Othman Sharif na Abdulla Kassim Hanga. Waasis

wa ASP waliyotoka tokea African Association walijiona kuwa na haki zaidi ya uongozi

wa ASP. ASP ilikuwa na Umoja wa vijana wa aina mbili mmoja ukiwa wa YASU, yaani

Young African Social Union, Umoja ambao ulijitambulisha kama chama cha "kijamii na

kitamaduni" lakini kwa kweli kilikuwa chama cha vijana wa Kiafrika wenye muelekeo

wao wenyewe nyeti wa kisiasa. Wanachama wake wote walikuwa ni waliyosoma na waza-

lia wa Kizanzibari. Kiongozwao alikuwa Othman Sharif, lakini Aboud Jumbe, Hasnu

Makame na Mdungi Usi nikati ya waliyoshiriki katika Uongozi wa vijana hao. Chama

hichi hakikujitambulisha wazi kuwa ni chama cha vijana wa ASP ingawa wote wao ama

walikuwa ni wafuasi au waunga mkono wa Chama hicho. Sh. Ameir Tajo ndiye aliyowa-

patia msaada wakujenga jumba lao la YASU, huko Miembeni, baada ya Mapinduzi chama

hicho kilipigwa marufuku, ingawa chama hicho kilikuwa kikitowa huduma kwa watoto

wakiswahili ambao wengi leo wana elimu ya juu kabisa. Chama hasa cha vijana wa ASP

kilijulikana kama Afro shirazi Youth League, ASYL. Viongozi wa chama hichi walikuwa

ni wale waliyokosa elimu na wengi wao wakiwa na asili ya bara, ingawaje wafuasi wa

chama hichi hawakuwa vijana wa kweli kama vile vijana wa YASU bali walikuwa ni watu

wazima karibu wote wakiwa watabaka la chini kabisa, malumpa, walala hoi wakiwa wengi

wao wasiyokuwa wazalia wa Zanzibar. Hawa walimuunga mkono Karume kwa sababu

yeye mwenyewe hakuwa msomi kama wao, akiwa mtu wa tabaka la chini, asiyekuwa

mzalia wa Zanzibar bali alikuja Zanzibar akiwa ni mtoto. Na Karume nae kwa upande

wake akiwaamini ASYL kwa sababu hizo hizo, na siasa yao ilikuwa ni kutumia ugozi bila

ya kuwa na mfumo, muelekeo au sera zozote maalum za kisiasa za kuinusuru Zainzibar.

Zaidi ya mgawanyo huo, kulikuwa na chama cha wafanya kazi cha ZPFL ambacho ingawa

kilikuwa na baadhi ya wazalia wa Bara katika uongozi wake, kilikuwa na mfumo afad-

58
hali wa kimaendeleo ukifananisha na mfumo wa ubaraka , ingawa viongozi wachache wa

chama hichi ndio waliowauza kina Twala na Hanga. Kwa hivyo ndani ya uongozi wa ASP

kulikuwa na migawanyo ya migongano ambayo imeathiri sana hali bora ya Visiwa vyetu.

3.12 Malumpa wa Zanzibar

Malumpa, "walalahoi" au watu walio tabaka la chini kabisa la jamii ni kwa desturi ni watu

wenye malalamiko mengi zaidi katika jamii za kila aina. Tabaka hili, siku zote liko tayari

kushiriki katika kuleta mabadiliko ya kijamii kwa sababu kama inavyosemekana ni tabaka

ambalo katika mapambano ya ana kwa ana, halijali, kutoogopa wala kuwa na wasi wasi,

kwa sababu huwa hawaogopi kupoteza maslahi yoyote , kwani wakipotezacho si zaidi bali

ni minyororo yao ya kisiasa na kiuchumi . Hili kwa desturi ni tabaka linyonywalo zaidi,

linalokandamizwa kuliko tabaka lolote na linaloteseka kikomo cha juu kabisa ukifananisha

na matabaka mengine ya jamii. Tabaka hili likipata uongozi mzuri ndilo tabaka linaloleta

mabadiliko ya kuendeleza maisha bora ya kila mwananchi. Ingawaje tabaka hili likikosa

viongozia u uongozi bora linaweza kuleta athari kubwa mno katika jamii. Zanzibar karne

za karibuni imekuwa ni nchi iliyofaidika na kunufaika kiuchumi.Watu wake walikuwa na

kipato cha kutosha na kuwafanya kutokubali kutumwa. Kwa kawaida ijapokua Mzanz-

ibari asilia alikuwa hali ya chini, aliweza kuwa na kipato cha kutosha cha kujiepusha

kuingia katika tabaka la "ulumpa". Siku za uvunaji karafuu ilieleweka kwamba idadi ya

Wazanzibari wote kwa jumla ilikuwa ndogo zaidi kushinda ile iliyohitajika katika vuno la

karafuu, kwa hivyo Zanzibar ilibidi kuagiza wafanyakazi wa majira kutoka Bara la Afrika

ya Mashariki na Kati, wengi wao kutoka Mrima/Tanganyika. Jambo lililowavutia majirani

59
hawakuja kufanya kazi Zanzibar ilikuwa ni utajiri Zanzibar uliyokuwa nao kwa wakati

huo, na kuweza kulipa mishahara mikubwa zaidi kuliko nchi jirani na wakati huo huo

watu hao walikua hawatozwi kodi ya kichwa Zanzibar tofauti na kule walikotoka. Kwa

mfano mishahara ya vibarua wa Zanzibar katika miaka 1930 nakuendelea ilikuwa ni sh.

30/ kwa mwezi, wakati mishahara ya kibarua au skwatawa Kenya haukufikia hata sh. 15/

seuze ile ya Tanganyika ambayo ilikuwa chini zaidi. Mishahara ikaendelea kupanda hadi

1948 wakati kibarua akipata sh. 3/30 kwa siku. Kutokana na kuagiza vibarua kutoka

nchi za jirani idadi ya wakaaazi wa Zanzibar ilikuwa kama ifuatavyo: Kutokea mwaka

1923 hadi 1931 wafanyakazi wote waliyoingia Zanzibar walikuwa 21,852 na waliyoon-

doka katika muda huo huo 14,055, katika miaka ya 1927 na 1928 jeduweli za wahamiaji

hazikuchapishwa. Baada ya hapo inakisiwa kwamba kiasi chawatu 2000 waliingia Zanz-

ibar kwa mwaka, wengine wengi waliingia kwa magendo bila ya kujulikana na kuhisabiwa.

Sensa zifuatazo zinaonyesha idadi ya wabara waliyokuwa Zanzibar. Katika mwaka 1924

kulikuwa na Wabara 64,828 Wazanzibari wenyewe wakiwa 119,360 (yaani Wabara kuwa

z aidi ya thuluthi moja ya wakaazi wa Zanzibar ) sensa ya mwaka 1931 ilionyesha idadi

ya kiasi cha Wabara 74,492 wakati sensa ya mwaka 1948 ilionyesha Wabara waliyoishi

Unguja na Pemba kuwa watu 51,227 wakati Wazanzibari wenyewe wakiwa 148,480 yaani

zaidi ya robo ya wakaazi wote kwa jumla na zaidi ya thuluthi moja ya Wazanzibari wote.

Baada ya mgomo wa Wafanya kazi wa 1948 wahamiaji kutoka Bara hawakuwa wakija

kwa wingi hasa kwa vile hata mishahara ilikuwa imepunguwa.

60
3.13 Mgomo wa 1948

Mgomo huo uliyotajwa hapo juu wa agosti-septemba 1948 ulikuwa ni wa wafanya kazi wa

chini kabisa hasa wale wa bandarini, makuli, wachukuzi, vibarua, wafanyakazi wa P.W.D,

hospitali na kadhalika. Kwa vile Zanzibar ikiagiza vibarua kutoka mabara, mgomo huu

ulikuwa umefanywa zaidi na Wabara kwani wao ndio waliyokuwa sehemu kubwa kabisa

ya tabaka hilo. Mgomo huo ulishajiishwa zaidi na mgomo wa Mombasa wa 1939 na

wa Dar es salaam wa 1947. Kutokana na mgomo huo ukakamavu na msimamo imara

wa wafanyakazi ukajichomoza na hatimae wengi wao walipokosa au kuachishwa kazi,

wakaingizwa katika tabaka jipya, na kupata sura mpya ya kilumpa, maprolitari wasokuwa

na kazi. Wagomaji hao, ingawaje walipokuwa wakigoma, waliungwa mkono na jamii

nzima ya Kizanzibari katika madai yao halali na kupata misaada tofauti na hata mashamba,

waliwaletea vyakula, na watu wengine wa jamii kama vile Watumbatu kukataa kuvunja

mgomo huo kwa kufanya kazi baadala ya wagomaji hao, na akina mama wa Kizanzibari

kuwapikia vyakula wagomaji hao.

Malumpa hawa wakiwa wengi wao ni Wabara, kutokana na mgomo huu wakaanzisha

kikundi kilichokuwa na upungufu wa mfumo, upungufu wa siasa, sera au mipango maalum,

lakini watu hawa walikuwa ni watu wenye maslahi ya aina moja na waliyokuwa hawana

uongozi madhubuti. Lengo lao kubwa lilikuwa si la kitaifa bali la kuongezewa msha-

hara tu, bila ya kuwa na mfumo wa kisiasa ya kitaifa. Baadae vyama vya wafanyakazi

vilipoanzishwa watu hawa wakawa katika mstari wa mbele na washabiki wakubwa. Ku-

tokana na hali ya tabaka lao la hali ya kuonewa kwa kunyonywa na kudhulumiwa, walipata

maarifa na elimu fulani ya kisiasa kutoka katika mgomo huo. Na kama desturi, malumpa

ni watu waliyokuwa tayari kuchukuwa khatuwa za kimapinduzi wakati wowote, ingawaje

61
wakipata uongozi mbaya matokeo yake huwani balaa kubwa mno.

62
Chapter 4

MAPINDUZI

4.1 Siri ya Mapinduzi ya 1964

Kama ilivyokaririwa hapo juu njama za serikali ya ZNP ya kuwakamata viongozi waupin-

zani iliharakisha na kusisimua haja ya kufanya mapinduzi kwa haraka, hata kabla mata-

yarisho ya mapinduzi hayo kuwiva vizuri. Vile vile ile hali ya kwamba ASP ilipata

idadi ya voti nyingi zaidi kupita ZNP na ZPPP kwa jumla, iliwafanya ASP kuingiwa na

uchungu mkubwa na kwa hivyo wakaamuwa kulipiza kisasi kwa kufanya ghasia kama zile

za mwezi wa juni 1961. Lakini mwaka huo, wa 1964, walikusudia kuchoma moto sehemu

zote za mjini, yaani stone town, pamoja na vituo vya kuuzia mafuta ya petroli. Wapangaji

halisi wa mpango huo hawakuwa Afro-shirazi yenyewe bali ilikuwa Afro Shirazi Youth

League, wale waliyokuwa wanachama wa Chama cha Haki za Binaadam na askari polisi

wa bara waliyofukuzwa kazi na serkali ya Hizbu pamoja na baadhi ya wafuasi wa Bahai.

Mipango yao waliiweka siri sana hata karibu wote viongozi wa juu kabisa wa ASP wal-

ifichwa nakutokujulishwa kiini cha mipango yenyewe mpaka dakika za mwisho. Kwani

wakati huo uongozi wa ASP ulikuwa umeparaganyika na mchuano mkubwa wa kudai

nakupigania uongozi ulifukuta chini kwa chini. Baadhi ya viongozi wa ASP walijihisi

wao wakiwa ni Wazanzibari halisi walikuwa na haki zaidi ya uongozi kuliko wale wenye

asili ya Kibara ambao vile vile walikuwa hawana elimu. Migongano mikali ilitokana

baina ya Wazanzibari kutaka uongozi. Othman Sharif, Hasnu Makame, Saleh Sadalla

na Idris Abdul Wakil iliwabidi wajiuzulu tarehe 2 januari, 1964 na kutoka katika ASP.

63
Katika mvutano huo kwenye dakika za mwisho kabla ya Mapinduzi, tarehe 10, 11 januari,

Othman Sharif kwa siri kabisa alimuendea Waziri Mkuu Mohammed Shamte na kumpen-

dekezea waunde serikali ya pamoja ya ASP na ZPPP. Wakati huo Othman Sharif alikuwa

amekwishapata fununu za Mapinduzi ambayo alikuwa hayataki kwa sababu yalikuwa si

ya ASP wala ya Wazanzibari khalisi. Shamte akawakatalia viongozi hao na kuwambia

kama walitaka kushiriki serikalini basi iliwabidi watoke katika ASP na waunganishe viti

vyao vya Bunge kwenye ZPPP, kina Othman Sharif wakashindwa na masharti hayo. Mi-

gogoro hii jinsi ilivyokuwa ya hali ya juu, hata jina la Abdulla Kassim Hanga hatimae

lilionekana kukuwemo katika ile listi ya John Okello ya wale Viongozi waliyotakiwa na

ASYL kuuwawa mara baada ya Mapinduzi. Kwa hivyo kuuliwa kwa kina Hanga na ASYL

baadae sijambo la kustaajabisha. Ushahidi wa kupindukia ulionyesha kwamba Mapinduzi

ya 1964 hayakupangwa, kutayarishwa, kuandaliwa au kuongozwa na ASP. Na inaonyesha

wazi kwamba viongozi waliyotajwa hapo juu, waliyopendekeza kuu ngana kwa ASP na

ZPPP, yaani kina Othman Sharif, walifanya hivyo kutokana na upinzani wao wa kukataa

kuendeshwa na Wabara na hiyo ndio sababu wakawa wamekwisha hukumiwa kuuwawa

hata kabla ya ghasia hizo kufanyika. Wale waliyoanza suala la kutaka kuleta ghasia, ku-

choma moto, kuuwa na kuleta fujo kwa jumla walikuwa ni Afro shirazi Youth league na

kiini kilikuwa ni Kamati yawatu 14 yaani:

Committee of "14"

John Okello*

Abdulla Mfarinyaki*

Seif Bakari*

Abdulla Said Natepe*

Yusuf Himid

64
Ramadhan Haji

Hafidh Suleiman

Khamis Darwesh*

Pili Khamis

Said Bavuai

Said wa Shoto*

Mohammed Abdulla*

Hamid Ameir

Khamis Hemedi

Wageni wengine ambao walishiriki mstari wa mbele wa viongozi katika Mapinduzi

walikuwa ni Absolom Amoi Ingen, Matias Simba, Mzee Kenyatta n.k.

Nusu ya wanakamati ya "Committee of 14" hao wakiwa wasio na uzalia wa Kizanz-

ibari yaani hao wenye alama ya *. Itaonekana kwamba viongozi wanne wa- juu kabisa

hawakuwa ni Wazanzibari na hata Karume alikuwa hayumo katika Kamati hiyo ya watu

14. Karume alitiwa katika kamati hiyo baada ya Mapinduzi na baada ya kuondoshwa kwa

Okello na kushika pahala pa Okello. Katika mipango yao ASYL waliandaa Fete usiku

wa tarehe 11 kuamkia tarehe 12 januari 1964. Kama ilivyotajwa hapo juu ASYL haiku-

panga kufanya Mapinduzi bali ilikuwa imepanga kufanya ghasia, fujo na kuchoma moto

mjini, Stone Town. Kutokana na hali ya kisiasa ya wakati huo, vyama vyote vya upinzani

vilikuwa vimeungana katika United Front. Kutokana na hali hiyo kiongozi mmoja wa

Umoja wa Wafanyakazi wa FPTU ambaye vile vile alikuwa ni kiongozi wa Umma Party

akadokezewa kwamba kulitaka kufanywa hizo fujo, ghasia na uchomaji moto sehemu za

mjini na wale makomred wenye jamaa zao huko sehemu za mjini wawaondoshe. Kiongozi

65
huyo, Ahmed Badawi Qulatein, kutokana na muamko wake wa kinadharia na msimamo

wa kimaendeleo akawaonya na kuwashauri viongozi hao wa ASYL kutofanya kitendo

hicho, kwani kufanya hivyo kungelikuwa ni sawa na kuwauwa watu wasio na hatia yoy-

ote, ambao karibu wote wakiwa ni wafuasi tu. Kati ya wale ambao wangeliuwawa bure

wangelikuwemo watoto, wanawake na wazee, kwa ufupi kungelikuwa kuuwa wananchi

ambao hawana hatia yoyote. Zaidi ya hivyo kitendo kama hicho kingeliwafanya wananchi

wakauwana ovyo na hatimae wale ambao wangelizianza ghasia hizo wangelikamatwa

kufugwa na kuuwawa pamoja na uongozi wote wa upinzani bila ya kuweza kuleta mabadi-

liko yoyote ya kimaendeelo. Ndipo Qullatein akawaasa kwamba kama wanataka kufanya

jambo la maana basi bora wangelifanya "MAPINDUZI" na hatimae wachukuwe serikali

na ndipo watapoweza kuleta mabadiliko katika jamii. Kwa njia hiyo kuuwawa kwa watu

bure bure kutaepukika na wakati huo huo serikali itapopatikana mfumo wa jamii ulio bora

ungeliweza kuzalishwa. Sababu hizo zikawatwanga viongozi hao wa ASYL hasa kwa

vile kulikuwa na uwezekano wa wao wenyewe kuuwawa katika ghasia hizo. Ingawaje,

wakati huo fununu za ghasia zilikuwa zimeshaifikia idara ya usalama wa serikali ya Hizbu,

Karume mwenyewe akiwa mtoaji siri mmoja wapo, kwani alimuendea Ofisa mmoja wa

Polisi wa Kiingereza, na kumwambia kwamba amesikia fununu kwamba kulitaka ku-

fanywa ghasia, baina ya tarehe 11 12 Januari, lakini yeye alijikosha kutoka na ghasia

hizo kwani alisema kwamba alikuwa hayumo katika mipango hi yo. Kamishna wa polisi

akazidharau khabari hizo. Hasa kwa vile serikali ya Hizbu na Polisi wakishughulishwa

na kuwaandama Wana Umma, kuwadharau ASYL, na kutoona harakati zozote za Wana

Umma, habari hizo wakazidi kuzidharau. Ingawaje mchana kutwa wa tarehe 11 januari

1964, hadi masaa ya usiku kuliwekwa vizinga njia na askari wa PMF kuranda kutwa.

Tarehe 11 hiyo magariya PMF (Police Mobile Force) yakiwa yamejaa maaskari yalikuwa

66
yakiranda mchana kutwa sehemu zote za mjini silaha zao walizopewa zikiwa marungu

matupu. Usiku ulipoingia askari wa vikosi hivyo vilipoona Umma Party wameingia kulala

bila yaishara ya harakati zozote na hao askari wa polisi na wa PMF wakadharau habari hizo

na kwenda kulala Mtoni, ambako mara mbili pamema usiku huo kulipigwa matarumbeta

ya hadhari. Wale polisi wa Ziwani nao wakajiendea kulala, wakuu wao wa polisi na wa

PMF kuchukuwa nyum bani funguo za ghala za silaha. Kosa mojawapo kubwa serikali

ya Hizbu ililolifanya ilikuwa kuwafukuza na kuwapa notice ya kuwaachisha kazi polisi

waliyokuwa wana asili ya Kibara, baadala yakuwapa watu hao uraiya na kutukuza ujuzi

na uwezo wao. Baada ya- kuwawachisha kazi watu hao, serikali hiyo haikuwapa wote

wao nauli na kuwa-tayarishiya safariza kurudi makwao, kati yao hatimae, walisaidia katika

Mapinduzi kwa ujuzi waliyokuwa nao.

Saa sita za usiku wa tarehe 11 Januari, malumpa wa Youth League wakazishambulia kambi

ya polisi ya Ziwani na ya Mtoni wakiwa na mapanga, mishare, magongo, mawe, visu na

kadhalika. Baada ya kuiteka Mtoni, chini ya uongozi wa Ramadhan Haji, walinyakuwa

bunduki za aina ya rifle 200 , sub machineguns 25, Brengun nyepesi 2, bastola nyingi, ma-

grenedi, mabomu ya moshi na risasi. Wakati huo simu baina ya vituo vya polisi zilikatwa,

na mfano kituo cha polisi cha Malindi kilipojaribu kuwasiliana na kambi ya Ziwani na

Mtoni kilishindwa na hatimae kupeleka gari la polisi la 999 huko Mtoni kwenda kuchun-

guza. Gari hilo lilipofika huko likakuta Mtoni imekwisha tekwa na askari hao ikabidi

wasalimishe roho zao kwa kukimbia na wengine kuogelea baharini kutoka Mtoni hadi

mjini.

Baada ya ushindi wa ghafla kikosi kutoka Ziwani chini ya Okello, wengi wakiwa na

mabunduki bila hata kujuwa namna ya kuyatumia wakaelekea Raha Leo ambako ndiko

kulikokuwa Makao Makuu. Baada ya hapo ndipo jina la John Okello likaanz kusikika

67
na vitisho vikaanza kuzagaa visiwani. Kwa kutumia Sauti ya Unguja,Okello aliwatia

terra sio wananchi tu kwa jumla, bali hata viongozi wote wa ASP hasa kwa vile wa-

likuwa hawamjui Okello ni nani. Okello alifanikiwa na kuwadanganya walalahoi wenzake

kwamba ati alishiriki katika vita vya Mau Mau, na hao kwa upungufu wa maarifa na

ujuzi wao kuhusu mapinduzi wakaamini nakumfuata kama vipofu. Sababu ya kutoroka

Okello kutoka sehemu mbali mbali za Uganda, Kenya na Pemba na Unguja, inasemekana

kwamba alikuwa jambazi, na ndio maana akawa na mwenendo wake wa kikatili. Wana

ASYL wakiwa wenyewe wakiongoza na kutekeleza maazimio yao bila ya kushirikisha

uongozi wa ASP waliteka Ziwani na Mtoni kwa usiku huo. Baadae huko Makao Makuu

Raha Leo ukakuweko uongozi uliyokuwa si wa ASYL. Bahati ni kwamba Aboud Jumbe,

Badawi Qullatein, Abdulaziz Twala, na Khamis Abdulla Ameir wakafika hapo na muon-

gozo wa kisiasa ukawa unatolewa, ingawa Jumbe kwa uwoga wake akajiweka chini ya

Okello. Ingawaje Jumbe alisaidia katika kupunguza upotovu fulani. Makomred wengine

wakashiriki katika ulinzi wa Makao Makuu, Raha Leo, wakiwemo Abdulla Juma, Salim

Saleh, Haji Othmani n.k. Hata kabla ya Mapinduzi kuanza Karume alikwisha penya na

kukimbilia Dar es salaam, kunusurisha roho yake, katika safari hiyo alimuomba Hanga

amshindikize. Babu kwa wakati huo alikuwa akiishi Dar es salaam tokea kukimbia

kukamatwa, kama ilivyotajwa huko nyuma. Wakiwa Dar es salaam, Nyerere hatimae

akawaita viongozi wote hao watatu, yaani Babu, Hanga na Karume na kuwashauri warudi

Zanzibar kwenda kuzuwia watu kuto uwana ovyo . Hapo ndipo Babu, Hanga na Karume

wakachukuwa boti la wayahudi Feinsilber na Abramovich tarehe 14 Januari 1964, kuelekea

Zanzibar na kushukia Fumba kwa madhumuni ya kuzuiya umwagaji wadamu. Ingawa se-

hemu mbili muhimu za kiusalama zilikwisha tiwa mikononi, usiku wa baina ya tarehe

11 na 12 ya 1964, bado kulibaki sehemu fulani muhimu za kiusalama ambazo zilishinda

68
kuziteka. Kati ya sehemu hizo ilikuwa ni kituo cha polisi cha Malindi, ambacho Seif

Bakari alipewa wadhifa wa kukiteka lakini akashindwa na Gereza la Kiinua Miguu am-

balo lilikataa kusalim amri na sehemu hizo kupigana vikali na kusabababisha kuuwawa

kwa watu wengi sana waliyoshiriki katika kupindua . Hapo ndipo walipohitajika wenye

ujuzi na uwezo wa kupambana katika vita vya kimapinduzi mchana kumekucha kweupe,

kwani ASYL walipokwenda Ziwani na Mtoni walikuta askari wamelala na hawana silaha.

Lakini baada ya mchana kuingia vituo vyengine havikusalim amri bali vilikamata bunduki

na kupigana. Kituo cha polisi cha malindi kilikuwa na askari 70 waliokuwa na silaha

kamili na risasi zakutosha, chini ya uongozi wa Inspekta Salim Hakim Khasibi. Askari

hawa wakilindwa na makuta ya jumba hilo na kwa kutumilia urefu wa ghorofa, na ki-

tuo hicho kuwa njia panda, waliweza kuteketeza watu wengi sana waliyojaribu kukaribia

na kutaka kukiteka kituo hicho. Wengi wa wale waliyokwenda kushambulia mwanzoni

walikuwa wamakonde ambao walikuwa mara ya kwanza kushika bunduki na walipewa

mafunzo ya kutumia silaha na makomred, wengine kati yao walijitwangana risasi wenyewe

kwa wenyewe walipo jaribu kumlenga adui. Wengine kama kina Seif Bakari walikamatwa

hapo na kuachiliwa na kugeuz wamjumbe wa kupeleka salamu kwa wakubwa zake, kuto-

tambuwa kwamba Seif alikuwa mmoja kati ya viongozi wa juu wa mapinduzi yenyewe.

Washambuliaji wengi sana walifariki hapo Malindi na wengine huko gereza la Kiinuwa

Miguu. Malumpa- walipoona mambo yanawazidi wakawaomba Makombred wa Umma

Party kwenda kuwasaidia kuviteka vituo vilivyobaki. Hapo ndipo kwa mara ya mwanzo

kwa Makomred walishiriki katika Mapinduzi kisilaha. Baada ya mashambulizi makali

yaliongozwa na komred Amour Doughesh, askari wa kituo cha Malindi wakakimbiana

gereza la Kiinuwa Miguu liliposikia makomred, wakiongozwa na Hemed Hilal walikuwa

wakijiandaa kuchukuwa dhamana ya utekaji wa ngome hiyo, gereza hilo likasalim amri.

69
Na baada ya hapo makada wa kikomred wakaendelea kuchukuwana kulinda vituo mbali

mbali kama kituo cha simu ya upepo. Kituo hicho kilichukuliwa chini ya uongozi wa

Hashil Seif na Kadiria Mnyeji. Aboud Jumbe akiwa ndiye aliyetowa amri ya kukiteka

kituo hicho. Ali Muhsin na Mawaziri wake, hatimae, walikwenda kwenye kituo hicho cha

simu ya upepo na kusalim amri kwa makomred, Kadiria Mnyeji na Hashil Seif, waliwapa-

tia usafiri na ulinzi wakupelekwa Raha Leo, kwa usalama na amani. Uwanja wa ndege na

kituo cha simu vilichukuliwa baaadae na makomred. Hizbu kabla ya mapinduzi, itakum-

bukwa huko nyuma, kwamba ilikuwa imeshaanza kujitayarisha kutaka kukamata viongozi

wa upinzani na kujuwa kwamba vitendo hivyo vingekasirisha wafuasi wa viongozi hao.

Kwa hivyo Hizbu inasemekana ilikwisha jitayarisha na mapambano hayo kwa kugawa

silaha kwa wafuasi wake.Zaidi ya kugawa silaha waliwatayarisha baadhi ya wafuasi wao

washupavu katika mbinu mbali mbali za mapigano. Hizbu ilikuwa na wataalam fulani

waliyojifunza mbinu za kijeshi za kigorilla, wakiwa huko Misri na Dhofar. Kati ya askari

hao wasiri wa Hizbu walishiriki katika kujaribu kuikowa serikali ya hizbu isiangushwe siku

za Mapinduzi na walikuwa wakifanya mazinga ombo yao sehemu za Bubu, Bumbwini na

Kianga. Kati ya askari hao kuna waliyowahi kukamatwa mara tatu wakifanya operation

hizo siku zile za mapinduzi. Sehemu hizo zilizotajwa hapo juuzi liteketeza washambulizi

wengi mno hasa kwa vile Hizbu wa sehemu hizo walikuwa wametayarishwa vizuri na kuwa

na silaha madhubuti, kinyume na washambulizi waliokuwa na mapanga, magongo n.k. Ili-

bidi vikosi kutoka mjini kwenda mashambani huko na kuwateka, baada ya kusalim amri

kwao. Serikali ya Hizbu iliwatomeza wafuasi wake waliyokuwa mashamba kutoa roho zao

kuhami serikali ya Hizbu, lakini wao viongozi wenyewe walisalim amri na kusalimisha

roho zao, kutoroka nchi na kusaliti, wakati wananchi wakiuwana wenyewe kwa wenyewe.

Katika mapinduzi watu wengi waliuwawa, na kutoka sehemu zote mbili, wengine wal-

70
iuwawa bure na wengine waliuwawa katika mapigano au kwa sababu walishiriki katika

mapigano. Kati ya wale waliyouliwa bure ni wa huko Bambi ambako makatili waliyokuwa

na msimamo wa kigozi waliwakamata wanawake, watoto kwa wazee, wakawatumbukiza

katika visima, kuwatilia makozi, makarare, na madufu, kuwaminia mafuta ya taa na

kuwatia moto, watu hao wakiunguwa hali watu wakiwa wazima wazima. Unyamana

ukatili huo hauitwi mapinduzi bali ni, ukafiri wa kikatili na wa kinyama kabisa,unaotokana

na chuki za kijinga walizotiwa na mwishowe kusahau kama hao waliowauwa ama wa-

likuwa ni ndugu zao, majirani zao au mara nyingine wema waona kuwa waislaam wenzao.

Baadala ya kuulani unyama waliyofanyiwa watu wa Bambi, Karume akawatunukia watu

hao kwa kuwajengea kati ya nyumba nzuri na bora kabisa baada ya mapinduzi. Mapin-

duzi yasiyotayarishwa na wanamapinduzi washupavu wenye intidham na muamko wa

kisiasa uliyokomaa na wa hali ya juu lazima utakuwa na matokeo ya uovu wa kuvunja

sheria, kufanya mambo maovu na machafu. Kwa vile mapinduzi ya 1964 hayakupangwa

vilivyo, wahuni wengi na malumpa kadhaa walichukulia nafasi hiyo na kufanya mambo

maovu kama vile kuuwa ovyo, kuwaingilia wanawake na wanawari kwa nguvu, kuiba na

kuchukuwa ngawira, kuvunja na kupiga watuovyo. Jambo la kusikitisha zaidi ni kuona

kwamba katika watu waliyoiba walikuwemo viongozi ambao hatimae wakawa mawaziri

na mabalozi, wengine sasa kuwa mawaziri wa serikali ya Muungano na kuna ushahidi

kwamba walishiriki kuiba dhahabu na mali nyingi za watu wa Pemba na zaidi ya hayo

kushirikiana na Okello kupiga viboko watu wazima wenye heshima zao. Wengi wa hawa

watu waliyoonewa walikuwa ni raiya wa kawaida wasiyokuwa na uongozi au uhasama

wowote. Bahati nzuri kulikuwa na Makomred ambao vile vile walisaidia kupunguza

uuwaji na ukashifishaji wa wanawake, wizi na maovu mengi mengineyo kwa sababu ya

elimu bora waliyopewa ya kisiasa. Kushiriki mwishoni katika Mapinduzi kwa makomred

71
kulipunguza balaa jingi kwa sehemu zote mbili za ASP na ZNP.

4.2 Haja ya Mfumo halali

Mfumo wa kijamii wa Zanzibar kwa wakati huo ulikuwa unahitaji mabadiliko makubwa,

kwani ulikuwa si mfumo wa kihalali wa kuwapa wananchi wote haki sawa. Ulikuwa ni

mfumo ambao uliwaweka wengi kwenye unyonge na umasikini wa kusononesha, ilhali

wakati huo huo wengine walikuwa wakiogelea katika utajiri. Kutokana na utajiri, ulwa na

ubwanyenye, wale watu wa matabaka ya juu walikuwa na kibri kikubwa na kuwadharau

wananchi wenzao, kuzidi kuwanyonya na kutumia utawala kulinda maslahi yao dhidi ya

haki ya waliyokuwa chini, na wakati huo huo kujidai kuwa ni waislaam wema. Kwa

hivyo Zanzibar kwa wakati huo palihitajika mabadiliko ya mfumo wa jamii na mabadiliko

yenyewe yaliyohitajika ni kuubadilisha mfumo uliyokuwepo wakati huo, kwa kutumia njia

ya kimapinduzi, kwa vile kulikuwa hakuna njia nyengine ya kuleta mabadiliko. Mapin-

duzi yaliyo hitajika yalikuwa yale yaliyopangwa kwa makini na kuwa na wanamapinduzi

wenye siasa ya kimapinduzi makini, waliyopevuka kisiasa, wakiwa na sera za kuleta maen-

deleo na waliyokuwa wakijuwa nini wakifanya. ASYL walikuwa ni watu wasiosoma na

kutowaamini wote waliyokuwa na elimu, kwa hivyo ndio maana hawakutaka kuwashirik-

isha viongozi wa ASP waliyokuwa na elimu katika mipango ya Mapinduzi yao. Karume

mwenyewe alikuwa hakusoma, aliwaamini waliyokuwa hawana asili za Kizanzibari, na

kuwaogopa wana ASP waliyosoma, kwa hivyo alielemea zaidi kwa ASYL na ASYL

wakamuamini Karume kwa maslahi kwa sababu kama hizo. Youth League katika uongozi

wa ASP ikamuarifu Karume pekeyake baadhi ya siri kuhusu mipango yao, ingawa hata

naye hawaku mwambia siri zote. Hiyo ndiyo sababu mojawapo, wakati ghasia zilipokuwa

72
zikipangwa wiki mbili kabla ya Mapinduzi, viongozi fulani wa ASP wakajiuzulu kutoka

kwenye ASP tarehe 2 Januari, 1964, na hiyo ndio- sababu moja wapo mnamo tarehe 10, 11

Januari1964, viongozi fulani wa ASP, katika dakika za mwisho, wakamuendea Mohammed

Shamte kwa madhumuni ya kuunda serikali pamoja ili kuepuka Mapinduzi. Aboud Jumbe

alifanya kazi kubwa ya kuwaunganisha viongozi wa ASP na kuwahakikishia kwamba wao

ndio watakaondesha hiyo serikali baada ya mapinduzi kwani ASYL walikuwa hawana

uwezo huo. Kina Othman Sharif wakakubali hatimae kushiriki katika serikali hiyo, bila

ya kujuwa hatari gani iliyowangoja huko mbele. Kuambatana na orodha ya Gazeti Kuu

la Serikali la tarehe 24 januari, 1964 orodha ya Baraza la Memba wa Mapinduzi ni kama

ifuatavyo:

1. Rais Abeid Karume

2. Makamo wa Rais Abdulla Kasim Hanga **

3. Mhe. Abdulrahman Mohammed Babu*

4. Mhe. Hasnu Makame*

5. Mhe. Aboud Jumbe

6. Mhe. Saleh Sadalla**

7. Mhe. Idris Abdul Wakil*

8. Mhe. Othman Shariff**

9. Mhe. Abdul Aziz Twala**

10. Mhe. Hassan Nassor Moyo

11. Kamishna wa Polisi - Edington Kisassi

12. Field Marshal John Okello

13. Mhe. Yusuf Himid

14. Mhe. Seif Bakari

73
15. Mhe. Ramadhan Haji

16. Mhe. A.S. Natepe

17. Mhe. Pili Khamis

18. Mhe. Khamis Hemedi

19. Mhe. Hamid Ameir Ali

20. Mhe. Said Iddi Bavuai

21. Mhe. Siad wa Shoto

22. Mhe. Mohammed Abdulla

23. Mhe. Abdulla Mfarinyaki

24. Mhe. Hafidh Suleiman

25. Mhe. Khamis Darwesh

26. Mhe. Khamis Abdulla Ameir

27. Mhe. Muhammed Mfaume Omar

28. Mhe. Muhsin bin Ali

29. Mhe. Muhammed Juma

30. Mhe. Daud Mahmoud

Viongozi halisi wa ASP wenye alama za ** wameuliwa na wengine wenye alama za

* kuhamishwa nchi kama itavyokaririwa wakati suala la Muungano litapojadiliwa katika

kurasa za mbele. Kwa siku za mwanzo mara tu baada ya Mapinduzi, Karume pamoja na

Viongozi wengi wa ASYL, kutokana na hamasa za Mapinduzi, walionyesha kuwa ni watu

wenye fikra za kimaendeleo, baadae kwa sababu za njama za kuunda Muungano viongozi

hao wakatiwa fitina na chuki, na kutekwa akili na Nyerere. Katika majadiliano ya siri ya

Muungano ilionekana kwamba ikiwa Umma Party pamoja na viongozi waloendelea katika

74
ASP watashiriki katika serikali ya Mapinduzi kikamilifu, basi Muungano wa Nyerere wa

aina hii ya leo wa kututawalia usingewezekana. Na kwa kuwaondosha Umma Party na

viongozi hao wa juu kabisa wa ASP njiani Muungano ukawezekana kundwa haraka haraka,

kama- itakavyakaririwa huko mbele.

4.3 Mapinduzi yalitekwa nyara

Madhumuni ya mapinduzi ilikuwa ni kuleta usawa baina ya Wazanzibari, kuondosha

dhulma, mapendeleo, ubaguzi, umasini, kuoneyana, kuleta usawa, haki, elimu bora, siha

bora, uchumi bora, sheria halali, heshma ya kila Mzanzibari n.k. Mara tu baada ya mapi

duzi kulichomoza ishara mbaya dhidi ya matumaini hayo. Kati ya ishara hizo ilikuwa ni

uvunjaji sheria kwa baadhi ya viongozi na kuchukuwa sheria mikononi mwao. Sababu

moja wapo ya kufanya mapinduzi na kuondosha serikali ya Hizbu ilikuwa, Hizbu ilipi-

tisha sheria zilizo kuwa dhidi ya demokrasia, za kunyima haki huru ya mtu, ya kuunda

na kujiunga na chama atakacho mwenyewe, kama vile kufungia chama cha siasa, kama

vile kupiga marufuku chama cha Umma Party. Kwa hivyo kunyima haki ya chama cha

upinzani, kunyima haki za kuchapisha khabari/fikra huru au mtu kusoma na kuandika fikra

huru na azitakazo, kama vile kufungia ZANEWS na Sauti ya Umma, kuzuiliya haki za

kusafiri huru kwa watu wenye fikra tafauti na mengineyo, haikuwa mwendo halali na wa

kidemokrasia. Hatua hizo za serikali ya Hizbu zilikuwa ni ishara za mwanzo za udikteta,

udikteta ambao leo tunaupiga vita.

Kwa mshangao mkubwa, mara tu baada ya Mapinduzi, ikaonekana kwamba na ile serikali

ya Mapinduzi nayo ilikuwa na njama za kuto heshimu misingi ya demokrasia. Serikali hiyo

75
baada tu ya kushika khatamu, ilianza kwa ishara mbaya, kama vile kuwahukumu vifo vion-

gozi wa serikali iliyopita, adhabu ambayo haifanani na makosa yao na wala wakuwa peleka

mahakamani. Kama isingeli kuwa kutetewa kwa vikali sana na A. M. Babu katika Baraza

la Mapinduzi basi viongozi hao wa Hizbu leo wangelikuwa marehemu, kwani walikwisha

hukumiwa hukumu za vifo. Walipoponea hukumu za kifo ikaamuliwa viongozi hao watiwe

vizuizini, na wakawekwa ndani bila ya kupandishwa Mahkamani, hadi miaka 10, baada ya

vyama vyao kufungiwa. Ingelikuwa jambo la busara kama serikali ya mapinduzi ingeli-

wapeleka watu hao Mahkamani, na kupata adhabu kuambatana na makosa yao wakipewa

fursa ya utetezi. Kufutwa kwa vile vyama vilivyokuwa vya serikali iliyopita pamoja na

kufutwa tena kwa chama cha Umma Party chini ya serikali ya Mapinduzi kilikuwa si

kitendo cha kimaendeleo; lingekuwa jambo la maana zaidi pindi serikali ya Mapinduzi

ingeliruhusu vyama vya upinzani. Na inakisiwa kwamba kama vyama hivyo vingelien-

delea kuweko, kwanza ingelikuwa mfano mwema wakuheshimu haki za kibinaadam na

za kidemokrasia na hapana shaka sheria halali zingeheshimiwa, na vifo vya akina Hanga,

Othman Sharif, Salum Jinja, Mohammed Humud, Saghir, Ali Othman, Mdungi Ussi,

Khamis Masoud, Abdulaziz Twala, Mikidad, Humud, Ahmada, Chwaya, Shindano, Said

Nassor na wengi wengineo, vingeepukika pindi watu hao wangelipandishwa Mahkamani

na Wazanzibari leo wangeliujuwa ukweli wa dhahiri. Hali hiyo ingeliendeleza uzoefu

wa kidemokrasia wa watu kushambuliana majukwaani na katika vikao maaluum na kuwa

ndugu wanao sikilizana na kushirikiana kujenga taifa kwa pamoja katika maisha ya desturi,

bilaya kujali nani ana fikra gani.

76
4.4 Afro-shirazi

Kama ilivyokaririwa huko nyuma, vyama vyote vya zamani vya Zanzibar vilikuwana

migongano ndani ya vyama vyao, Hizbu ilikuwa na kundi la Babu na la Ali Muhsin, ZPPP

kuwa na kundi la Mohammed Shamte na Ali Sharif, Umma Party kuwana kundi la Haki na

la Wasaliti wakati ASP kulikuwa na kundi la wale waliyoendelea ambalo limeteketezwa,

kundi la waliyopigania ukubwa, kundi la waliyokuwa na asiliya Kizanzibari na kundi la

waliyokuwa na asili ya Bara. Kundi hili la mwisholilikuwa limetia mizizi katika ASYL

chama ambacho ndicho hasa kilichopanga nakuyatekeleza Mapinduzi na ndio maana ma-

tokeo ya Mapinduzi yakenda kamayalivyo kwenda. ASP kwa hivyo ikameguka meguka

na hatimae kusababisha uuwaji wa kikatili wa viongozi wa ASP uliyopitishwa na ASYL.

Kwa vile viongozi wakuu karibu wote wa ASP waliuwawa na wale waliyobakishwa zaidi

ya Karume na Thabit Kombo, walikuwa ni viongozi wazee au wa chini kama kina Sh.

Daud Mahmoud, Ibrahim Sadalla, Ali Shariff ambao walikuwa ni kama watu waliyotekwa

nyara, kwa vile ndugu zao walikuwa wameshauwawa na kwa hivyo wao kuogopea roho zao

pindi wangeliteleza. Saa zote walikaa na wasiwasi kama mtu aliyewekewa kisu cha roho.

ASP/ASYL iliwadanganya wafuasi wao, kwamba ukabila na utumwa ndizo sababu ya

maafa yao yote, lakini viongozi hao hao walivyopata khatamu za utawala baadaya Mapin-

duzi, walisahau madai hayo na kuwatia wananchi wote kwa jumla, pamoja na wanachama

wa ASP, katika maafa makubwa ya kimaisha. Pindi viongozi hao wa ASYL(ASP) wan-

gelichukuwa msimamo wa kijananchi wa kufanya mazungumzo yamasikilizano baina ya

wananchi mapema, badala ya kuendeleza siasa ya kikatili, ya chuki na ya kipinga maen-

deleo, uhasama ugelikuwa ndoto. Kwa njia kama hiyo maovu mengi tungeliyaepuka

kutokana na makosa hayo na wapenda maendeleo wasingeliuwawa bure na nchi yetu leo

77
ingelikuwa imeendelea kiwango bora zaidi.

4.5 Aboud Jumbe

Ndani ya chama cha ASP na hatimae ASYL, kulitokea maafa mengi, kama vile kuteketeza

viongozi wa chama hicho na chama chenyewe tu, bali hata kuwapatisha taabu wafuasi

wa kawaida wa chama hicho bila ya kiasi. Wafuasi wa ASP wengi walivunjika moyo

sana kuona chama chao wenyewe kikiwatesa. Wafuasi hao vile vile walishangazwa sana

kwa kutoshirikishwa katika ujenzi wa nchi yao, katika uongozi wa chama na serikali yao,

kutojulishwa au kushauriwa katika jambo lolote lilohusu chama au serikali yao. Wana-

ASP na Wazanzibari wote kwa jumla wana haki yakujuwa nini kilichotendeka katika

nchi yao. Wazanzibari wanastahili ukweli kutoka kwa kiongozi mkweli kuhusu mambo

mengi ambayo yaliwakuta Wazanzibari. Jumbe kwa vile alikuwa msomi na asiyekuwa

kati ya viongozi wa ASYL iliwashangaza wengi kuweza kuepuka haku uwawa kinyume

na viongozi wengine wa ASP, kuna fikra tatu kuhusu jambo hilo; moja ni kwamba Jumbe

alikuwa myenyekevu sana kwa Karume ambae akitumia manufaa ya kisomo cha Jumbe.

Vile vile wakati Hassan Nassor Moyo na Diria walivyowauza kina Hanga kwa Karume

walimtaja Jumbe kwamba alihudhiria mikutano hiyo. Karume alipomuuliza Jumbe kwa

nini haku ripoti, Jumbe akasema aliliona jambo hilo ni la upuuzi ndio maana haku liripoti

kwa Karume. Tafsiri ya tatu inasemekana kwamba Jumbe hakuuwawa kwa sababu yeye

kinyume na viongozi wa juu waliyouwawa alikuwa kazaliwa Bara. Pana haja muhimu

sana kwa mtu kama Jumbe kujitokeza na kuandika historia ya ukweli ya ASP na serkali ya

mapinduzi kama anavyoikumbuka yeye, kabla wauwaji hawajamteketeza. Jumbe alishiriki

katika mitihani mbali mbali, kuiona na kuwezakupitia mitihani tofauti, kuishuhudia mi-

78
gogoro ya ndani ya ASP. Jumbe akiwa ni msomi, lakini wakati huo huo aliyezaliwa Bara,

kuwa na marafiki na wahisani wasio maafro kama kina marehemu Maalim Zubeir, ni mtu

aliyeziona nyuso zote mbili zasarafu. Jumbe anasemekana alipinga msingi wa ghasia za

uchaguzi mwaka 1961. Kabla ya uhuru alikuwa na sifa za uongozi wa kitaifa, kushiriki

katika mijadala hadhara ya kisiasa na kijamii akichuana na watu waliyokuwa na siasa

tofauti na zake. Kama vile majadiliano ya hadhara na A.M.Babu. Jumbe tokea mapema

januri 12, 1964 alikuwa pamoja na Umma Party na kuweza kujuwa mchango wao katika

mapinduzi. Anajuwa kuhusu vifo vya kina Hanga .Alikuwa kalamu na tupa ya Karume.

Baada ya kuuwawa Karume, Jumbe ndiye aliyechukuwa jukumu la kutangaza kifo cha

Karume katika radio na kujuwa vilivyo hali ya Viongozi wenzake wakati huo. Baada ya

kifo hicho alipambana na kuwa na migogoro mingi na Seif Bakari katika kuwaniya kanda

za khatamu za utawala. Jumbe ndiye aliyejaribu kuifufuwa ASP kwa kuitisha Kongres ya

mwanzo baada yamapinduzi huko Pemba, lakini jaribio hilo kutofaulu, kwani khatamu za

chama zikashikwa na wale wale ASYL. Hatimae Jumbe alifanikiwa kwa kiwango fulani

kuwapunguzia Wazanzibari maafa kwa kupunguza nguvu za Baraza la Mapinduzi kwa

kuwa sambaza sambaza na kuwaleta vijana wepya serikalini, vijana ambao wengine wao

walikuwa wana YASU na wengine kutokuwa wanasiasa hapo kabla, hatimae vijana hao

walikuwa ndio shina la utawala wa Jumbe. Jumbe alifanikiwa kwa kiwango fulani kuware-

jeshea watu haki zao za kuweza kutoa maoni. Kosa kubwa mojawapo alilolifanya Jumbe

lilikuwa ni kufuta Chama cha kisiasa Zanzibar na kuifanya Zanzibar izidi kumezwa, al-

ifanya hivyo kwa kutarajia kupewa Urais wa Tanzania, hatimae. Kutokana na kuzidi

kujitambulisha na dini ya kiislaam na kutambuwa mbinu za Nyerere za kutaka kuifanya

Zanzibar jimbo, Jumbe, alitanabahi na kuzindukana, na kuchukuwa khatuwa za kuitoa

Zanzibar katika Muungano na kwa hivyo akaporopolewa na Nyerere. Haya ni baadhi tu

79
ya mambo ulimwengu unayoyangoja kutoka katika kauli ya kweli ya Jumbe. Historia ya

Zanzibar haitokamilika bila ya Jumbe kuichangia kwa ukweli anaoujuwa.

4.6 Makosa ya Umma Party

Chama chochote cha kisiasa hakina budi na kufanya makosa ya kisiasa, mara nyengine

makosa hayo huwa madogo na mara nyingine huwa makubwa mno. Makosa kama hayo

yalifanywa na vyama vyote pamoja na Umma Party na hatimae kusababisha athara kubwa

visiwani Unguja na Pemba. Moja katika makosa ya Umma ilikuwa kujiweka nyuma na

kuonyesha kwamba wao ni watu wenye roho safi na wasiopapatikia khatamu za utawala,

kusahau kwamba wao wakiwa hawatakuwa na uroho wa utawala, kutakuwa na wengine

wengi ambao hawatopapatikia utawala tu bali watautumilia dhidi ya maslahi ya umma.

Kuogopa kwa Umma Party kushika khatamu za utawala kulitokana na uwoga wa kuhutu-

miwa kwamba walikuwa na njaa ya utawala, na kwamba badala ya kupigania wanyonge,

lile walilolitaka lilikuwa ni ulwa wa kuwatawalia wengine. Mawasiliano mazuri ya Umma

Party na baadhi ya viongozi wa ASP pamoja na vyama vilivyoshirikiana na ASP ili-

wafanya Umma Party kuwa na imani kwamba ASP badaya kupata khatamu za utawala

itatawala kihalali na kupitisha haki. Umma Party ilisahau kwamba si viongozi wote wa

ASP waliyokuwa na ujuzi au nia safi, na kwamba wengine walishughulishwa zaidi na

maslahi yao binafsi. Umma Party haikutarajia kwamba viongozi wa ASP Youth League

watawageukia wengi wa viongozi wa ASP, viongozi ambao walikuwa na fikra za maen-

deleo. Umma Party vile vile, katika jazba na hamasa za kimapinduzi ilisahau kwamba,

viongozi wa ASYL ingawa walijitolea kufanya mapinduzi, walikuwa kwanza ni watu

80
wasiyoelewa mambo ya kiserikali na kwa hivyo ilikuwa ni rahisi kubabaika na kulevywa

na khatamu za utawala. Umma ilisahau kwamba hawa watu walikuwa wanaupungufu wa

ujuzi wa kuendesha serikali. Badala ya kwamba Umma ilikuwa iwahakikishie viongozi

hawa wa ASYL kipato na satwa ya kudumu kwa mchango wao katika mapinduzi, wali-

wawachia kuendesha serikali kama rikwama, wakitarajia kwamba yale mapendekezo ya

kimaendeleo waliyoyatowa Umma Party yatatumika katika kuendeleza nchi. Viongozi wa

chache wa Umma Party, waliyokuwa na sifa za ubinafsi, walisaliti na kujichukulia jukumu

la kuzidi kuwapeleka mbele baadhi ya viongozi wa ASYL, wakijuwa wazi kwamba watu

hawa walikuwa hawawezi kuziendesha nyadhifa hizo kama ilivyotakiwa. Badala yake

viongozi hao wa ASYL kutokana na upungufu wa ujuzi wao wakawa wana wahka na kuona

adui katika kila pembe, na badala ya kuinuwa maslahi ya wanyonge wakazidi kuwakan-

damiza wanyonge hao hao ambao walidai kuwatetea. Pindi Umma Party ingelihakikisha

udhibiti mshupavu wa khatamu za utawala katika mikono halali na madhubuti, basi nchi

ingeliendelea kwa haraka na kwa amani. Um- ma wa Kizanzibari usingeliteseka, mauwaji

yangeliepukwa, vifungo na kutiwa watu vizuizini kwa miaka hadi kumi kungeliepukika.

Utawala wa mashirikiano ya Umma na viongozi wa ASYL na viongozi waliyoendelea wa

ASP ungeweza kuondosha uhasama na chuki za kisiasa na hatimae kuleta masikilizano hata

na ZNP na ZPPP, pindi ASYL wangeliwahiwa kupewa elimu ya siasa ya mapema na ya

kutosha. Wazanzibari wangeliweza kuwa kitu kimoja na pasingekuwa na haja ya Karume

kuwa na wasi wasi na kujiingiza katika Muungano bila ya kupenda. Khatuwa za kurek-

ibisha dira ya muelekeo wa nchi zingelifaa kutendeka mapema, yaani muda tu baada ya

mapinduzi au hata kabla ya ufanyaji wa mapinduzi yenyewe na hatimae kungeliepusha nchi

leo kutawaliwa na kuselelea nyuma. Ingawaje, wakati tu baada ya Mapinduzi palikuwa na

migogoro na mifarakano fulani hasa kwa vile baadhi ya watu, kwa jina la Mapinduzi, wal-

81
ifanya kila aina ya uovu. Haya mambo hayakuwafurahisha wana Umma, na ikafika hadi

baadhi ya wana Umma fulani waka mkabil John Okello na kumwambia awache kuadhibu

raiya wasiyokuwana makosa. Wakamueleza Okello kwamba akishindwa na kuzuwiya

vitisho nakufanya ukatili huo basi ingelimbidi akabiliane na wana Umma kisilaha ana kwa

ana. Okello wakati huo alikuwa akitakabar sana na nchi ilikuwa kama ikiendeshwa na

Marais wawili, upande mmoja Karume na wa pili Okello. Wakati huo viongozi wengi,

akiwemo na Karume, wakimuogopa sana Okello. Okello inasemekana mara kwa mara

akisafiri kwenda Kenya na Uganda kupeleka mali ya ngawira. Safari moja, mwanzoni

mwa march 1964, Okello aliporudi kutoka Dar es salaam, akalikuta Baraza la Mapinduzi

likimsubiri uwanja wa ndege kwa madhumuni ya kumfukuza nchi. Okello, wakati huo,

alikuwa akiogopwa sana kwa hivyo ilibidi waagizwe Makada wa Umma Party wakiwa na

silaha kamili. Baada ya Okello kusomewa madhambi yake na Karume, mbele ya memba

wa Baraza la Mapinduzi, huko uwanjawa ndege. Makada wa Umma Party waliyokakamaa

na silaha mkononi wakamshindikiza Okello hadi ndani ya ndege iliyokuwa ikimsubiri na

kumsafirisha kwendea Dar es Salaam na hatimae kurejeshwa kwao Uganda.

Absolom Ingen,aliyekuwa makamu wa Field Marshal Okello na kuwa kati ya waliy-

oogopwa sana na waliyofanya fujo nyingi, utesaji mkubwa na kashfa nyingi baada ya

Mapinduzi nae alipotaka kuoondoshwa alitiwa mbaroni na makada wa Umma silaha

mkononi na baadae akarejeshwa kwao Kenya. Kama makada wa Umma tokea mwan-

zoni wangelipewa nyadhifa kama hizo basi wale watesaji na wauwaji wasingelipata nafasi

hizo na nchi isingelikwenda mramba. Watu wawili hao, yaani Okello na Ingen, ni kwa

wakati huo viongozi wa juu kabisa katika mapinduzi, na ambao wakiogopwa Zanzibar

nzima, lakini ilipohitajika makada wa Umma Party waliwatia mbaroni kama mchezo wa

mdako. Hayo ni makosa ya Umma Party ambayo yanafaa kujadiliwa ili yaepukwe siku za

82
mbele.

83
Chapter 5

MUUNGANO

5.1 Umma Party na Muungano

Muda fulani baada ya Mapinduzi, fununu zilianza kuhusu kuundwa kwa Muungano , kwa

wakati huo Memba wengi wa Baraza la Mapinduzi hawakujua hatari ya Muungano, hata

Karume alo uunda Muungano pamoja na Nyerere, hakuelewa uzito wa khatuwa kama

hiyo. Umma Party mara tu kusikia fununu hizo za Muungano ikaanza kuupinga, na

ilikuwa kwa sababu ilitanabahi kwamba Zanzibar ingelipoteza uhuru wake pindi khatua

hiyo ingelitekelezwa. Umma Party ilitambua umuhimu wakuwa na umoja baina ya nchi

za Kiafrika, lakini umoja huo haukuwa lazima uwe wa Muungano wa nchi mbili huru.

Wakati huo kiongozi wa Umma Party, Babu, alikuwa safarini Indonesia, kungojewa amek-

wisha ondoka na kutoshauriwa kwa makusudi, kuhusu uundaji wa Muungano huo. Huku

nyuma makada walivyo kuwa wakipinga Muungano, tarehe 23, mwezi wa marchi 1964,

wakaitwa Ikulu, Zanzibar na huko Karume akawaambiya kwamba kama hawakuwacha

upinzani wao wa Muungano, basi wangeliletewa Wamakonde kufyeka fyeka na kuwapiga

mishare na Wamakonde hao. Karume alisahau Okello na Ingen walivyofirigiswa na

makada hao. Makada hao hawakushitushwa na vitisho hivyo vitupu, kwani waliujuwa

uwezo wa Wamakonde katika medani ya mapambano, wakitumia mishare kupambana

na vyombo vya automatic (Karume hatimae akawafukuza nchi wamakonde hao hao ).

Zanzibar wakati huo kukawa na vikundi viwili vikubwa, vya Umma, kimoja kikitaka

kuchukuwa " khatuwa za kuhitajika" za kuzuwiya Muungano na wengine wakapendekeza

84
asubiriwe Babu arudi kutoka safarini, na kufanya mazungumzo namashauriano. Wakati

akiwa njiani, akirudi nyumbani kutoka Indonesia, Babu, huko Pakistan, akapambanishwa

na khabari za waandishi wa magazeti na kuulizwa kama alijuwa kuhusu matayarisho ya

kuunda Muungano huo na kutakiwa kutoa msimao wake,kwamba aliunga mkono khatuwa

hiyo au la; jawabu lake likawa," ndio, alijuwa nakusema kwamba aliliunga mkono suala

hilo". Ukweli ulikuwa ni tafauti kabisa nausemi huo na kwamba Babu alikuwa hajajulishwa

kuhusu Muungano, na kwa desturi mtu hawezi kuunga mkono au kupinga kitu asichoki

juwa. Huku nyuma,Tanganyika, kumbe kulikuwa kumekwisha tayarishwa cello maaluum

katika gerezala Simbawanga la kumtilia Babu ndani pindi angelipinga Muungano. Ha-

timae ikaonekana kwamba majungu ya Muungano huo yalipikwa na shirika la kijasusi

la Kimarekani la CIA; kumtia chuki, hofu na wasi wasi Karume, kumghilibu na kum-

lazimisha mtu huyo kuunda Muungano. Aliyeshirikiana namajasusi hao katika mipango

hiyo ya Muungano, alikuwa ni Nyerere. Wakati huo kulikuwa askari wa Tanganyika wa-

likuja Zanzibar kusaidia kulinda usalama.Nyerere kwa hivyo alitishia kuondosha askari

polisi wake Zanzibar, pindi Karume angelikataa kujiunga na Muungano. Habari hizo

zinakaririwa kwa urefu katika kitabu cha Amrit Wilson (US Foreing policy and Revo-

lution - The Creation ofTanzania) kuhusu vipi Zanzibar ililazimishwa kushiriki katika

Muungano huo. Ingelikuwa Umma Party haikusisita, kuchelea na kujiweka nyuma basi

labda Muungano wa Marekani na Nyerere usingeliwezekana. Umma Party kama chama

chengine chochote lazima kujiendeleze kwa mujib wa wakati na hali ya kinchi na kil-

imwengu kwa jumla. Kati ya njia moja wapo ya kujiendeleza ni kujikosoa na kukosowana,

na chama chochote cha kisiasa kinachojiheshimu na kutizama, kulinda na kuweka maslahi

ya nchi mbele, kinawajib wa kutumia mtindo wa kujikosoa na kukosowana. Ingawaje,

kuna umuhimuwa kuhadhari na kuweza kujuwa mpaka baina ya siasa ya kinadharia na

85
yautendaji. Umma Party imetumia muda mwingi sana kwa sera hiyo, yaani kutumia wakati

kujadili siasa ya kinadharia. Hatimae, mijadala hiyo haikuchukuwa muda mwingi tu, bali

imechelewesha utekelezaji wa yale yaliyojadiliwa na hatimae hata kuleta migongano ile

isio yakihasama na ile yakihasama. Babu kiongozi wa Umma Party alikuwa mmoja wapo

wa wale ambao wakitumia siasa nyingi sana, pale ambapo wakati mwengine palihitaji

vitendo. Hasa kwa vile huko Bara baadae kulizuka mkondo wa vijana wenye fikra za

kimaendeleo ambao walikuwa na hamu ya kusaidia urekibishaji wa hali ya mambo Visi-

wani (Wengine hata kutaka kuundwa upya kwa Umma Party). Hali hii baadae ikaipa

Umma Party sifa ya kuwa wanasiasa wakinadharia tu, ambao wanakaa wenyewe kwa

wenyewe hata kutokaribisha vijana wengine waliokuwa na hamu ya kujiunga nao, katika

mijadala ya kisiasa. Hali kama hiyo iliwafaidisha wale tu waliyoweza kushiriki katika

baraza hizo na kuwapa nafasi ya kupata elimu bora ya kisiasa. Hali hii ilisababisha hata

kukuweko kwa pengo la kisiasa baina ya mwananchi wa kawaida na Uongozi wa Umma

Party. Ingawaje, Umma Party ilitanabahi baadhi ya makosa yake, kujikosoa baadhi ya

makosa yake na kuweza kusababisha mengi ya mafanikio ya Zanzibar yanayodhihirika

hivi leo, na viongozi na wanachama wake kujiunga na mkondo wa maendeleo wa leo.

Siasa ya Umma Party, kwa ujumla haikuwa yenye kupinga Umoja au Muungano wa nchi

za kiafrika yaliyoamuliwa na kukubaliwa na wananchi wote kwa kupitia kuraya maoni,

mradi Umoja au Muungano wenyewe una maslahi ya umma na kuwafikiwa na umma.

Mfumo wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wa miaka thelathini iliyopita, si mfumo

wa halali, bali ni wenye sura za kikoloni wa mkubwa kumtawalia mdogo na wa kuigubika

Zanzibar isahaulike na isijulikane, na hatimae kuigeuza jimbo. Wazanzibari wengi zaidi

hawaupenedelei Muunagano wa aina huo, kwa hivyo Muungano huo unafaa uvunjwe na

kama pana haja ya kuunda Muungano wowote basi kufanywe kura ya maoni ya Muungano

86
au Shirikisho, ikiwa kama Muungano au Shirikisho la Afrika ya Mashariki yote au la

Zanzibar na Tanganyika, mradi kila nchi iwe na utawala wake kamili, kuwa na Rais wake

ikiwa Seif Sharif Hamad au Salmin Amour, pamoja na Baraza la Mawaziri na Bunge huru.

Na serikali ya Muungano huo au Shirikisho hilo liwe na mawaziri na wakuu wa maidara

wa Shirikisho au wa Muungano wakishughulikiya mambo ya Muungano/Shirikisho hilo

tu na sio kuingilia kati katika serikali huru za Tanganyika na Zanzibar, ambazo ziwe na

Mabunge yao huru. Nyota ya Muungano imekuwa ikizidi na kuzidi kufifiana kufika hadi

CCM kuuogopa Uzanzibari hasa katika uchaguzi ujao na kutaka kuuondowa Uzanzibari.

Nyerere yumo katika kulazimisha serikali moja, lakini ajuwe kwamba hili ndilo suala

litakalo iuwa CCM moja kwa moja visiwani Zanzibar, na vyovyote Nyerere atakavyo

lazimisha, ikiwa seriakli moja au mbili, hata kufa kabla Zanzibar kuwa huru na kuwa na

serikali yake wenyewe.

5.2 Makosa ya Mapinduzi

Kutekwa nyara kwa mapinduzi kumeathiri kazi muhimu iliyofanywa na Wazanzibari katika

kupigania haki zao halali. Udhalimu katika jamii kwa kawaida ndio sababu inayoleta

Mapinduzi, ingawaje mara nyingi jina la Mapinduzi linatumika vibaya, au maana yake

kutumika ovyo, kutumika pale ipasapo na isipopasa, kama vile Kuudi-ACtaa, Puuch, Kuu

ya Ikulu, Kuu ya Kijeshi, mabadiliko yote hayo hali huitwa Mapinduzi, ingawa sifa zake ni

nyengine kabisa na zisizo za Kimapinduzi, mfano mzuri wa Kuu ya Ikulu ni ule wa Jumbe

kuondoshwa madarakani. Mara nyingi watu hudhani kupindua serikali kwa mabavu ndio

Mapinduzi, ilhali ukweli wenyeweni kinyume kabisa. Kwanza hakuna Mapinduzi bila ya

kuwa Mapinduzi ya"kimapinduzi", kuangusha serikali bila ya misingi ya kimapinduzi si

87
Mapinduzi.Ujana mapinduzi au siasa ya kimapinduzi haina lazima kuambata na kupin-

dua serikali. Fikra za kimapinduzi ni yale mawazo yanayokusudia kubadilisha maisha ya

wanyonge, yaliyoselelezwa nyuma na ya kudhulumiwa kwa madhumuni ya kuleta maisha

bora, ya haki na usawa, yaani kubadilisha hali iliyoselelea nyuma na kuleta iliyoendelea.

Fikra hizi zinaweza kukuwepo kabla ya mapinduzi ya serikali; bila ya mapinduzi ya serikali

au baada ya mapinduzi ya serikali. Hakuna lazima kuwa baada ya kupinduwa serikali siasa

itakayofuatiya lazima itakuwa ya kimapinduzi.Siasa ya kimapinduzi ni ile inayopigania

mabadiliko ya mfumo wa jamii bora nakuondosha maovu. Hali hii inawezekana kukuwepo

ama kwa kupindua serikali au hata bila ya kutumia mabavu ya kupindua serikali. Serikali

ya Hizbu imepinduliwa kwa kutumia njia za kimapinduzi, lakini kitendo cha mapinduzi

yenyewe mwanzoni hayakuongozwa na wanamapinduzi au na f- ikra za kimapinduzi.

Ni baadae ndipo uongozi na fikra za kimapinduzi zilish- irikishwa.Ingawaje, baada ya

kuonekana hatari ya kuleta mapinduzi ya kimapinduzi katika Afrika Mashariki ilibidi watu

fulani wayasaliti Mapinduzi hayo. Katika muda mfupiwa Mapinduzi ya kimapinduzi ya

Zanzibar, program ya kimapinduzi iliweza kupendekezwa na kutekelezwa kama vile, Mat-

ibabu na siha bora bure; kupendekezwa -Elimu bure kuanzishwa, Mpango wa Uchumi wa

kihalali kupangwa, Ardhi kugawiwa sawa kwa wote, Haki za kimsingi kuhakikishwa, uhuru

wamaandishi na wa fikra kupendekezwa, haki za wafanyakazi kuhakikishwa,kupangwa

uondoshaji wa vibanda na kuhakikisha makaazi bora kwa masikini naupangaji wa mengi

mengineyo ambayo yalitokana na program ya chama cha Umma Party. Hiyo ilikuwa

program ya kimapinduzi iliyokuwa na azma ya kubadilishamfumo wa kijamii kongwe na

kuleta mfumo wa halali. Siku za mwanzo za Mapinduzi, program hiyo ilitekelezwa kwa

kiwango fulani, lakini hatimae, baada ya viongozi walivyo endelea wengi kuhamishwa

kupelekwa Bara na kwengineko, kama itavyokaririwa baadae, program hiyo ilisalitiwa .

88
Matibabu bora yakawekewa Memba wa Baraza la Mapinduzi, kwa kufunguliwa Mapin-

duzi Wing, Madaktari, Manasi na Wafanyakazi waliyo kuwa na ujuzi tofauti hospitalini

na sehemu mbali mbali serikalini na katika jamii wakapigwa vita na kukimbiya nchi na

siha, elimu na huduma zote za jamii kurejeshwa khatuwa nying nyuma. Kukiondowa kituo

cha siha cha Umoja wa Mataifa (WHO) na kusababisha utapakaaji upya wa magonjwa na

kurejea kwa malaria, ugonjwa uliyokuwa umeshatoweka Zanzibar ni kati ya usaliti wa hisia

za kimapinduzi. Thamani ya elimu ikashuka kwa kufukuza walimu na wale waliyokuwa

na ujuzi, kuwafanya wakimbie nchi na badala yao kuwaweka watoto wa skuli kusomesha

maskulini. Kuwapa wataalamu waliyorudi masomoni ng’ambo mishahara ya chini kabisa

ya shillingi mia nne (400/ ) wakiwa na shahada za elimu ya juu na ambao wazazi wao

wakiwahitajia wawatizame wakishamaliza kusoma, kuliwafanya wakimbie nchi.Kuleta

ubaguzi baina ya wanafunzi, kuzuwiya wanafunzi kupata elimu ya juu na kutoa elimu kwa

ubaguzi. Kipato kutoka karafuu (shina la uchumi wa nchi)kuhodhiwa na Karume na shirika

la biashara la ZSTC, kutoagizia chakula na watu wakawekwa na njaa. Kutotekelezwa kwa

mpango wa uchumi wa miaka mitatu, na badala yake kubuni uchumi usioku- wa na mbele

wala nyuma. Kuchukuwa kwa eka tatu tatu za ardhi zenye rutba, na zaidi ya moja, na

Memba wa Baraz- a la Mapinduzi. Viongozi wa Baraza la Mapinduzi kujenga majumba

mazuri kwa kuiba mali ya serikali, kama vile vitu vya maonyesho vya Makumbusho na

kuwaibia watu binafsi milango na madirisha yao na kutia katika majumba yao. Pamoja

na kuiba nakunyanganya mali tofauti pamoja na kuozwa kwa watu kwa nguvu na mengi

mengineyo yakina Ali Mzee Mbalia na wengineo, hayakuwa mambo ya kimapinduzi,bali

ya upinduzi. Haki za kimsingi karibu zote kupigwa marufuku, kama vile kutolewa kauli

ya kutofanywa uchaguzi kwa miaka 50, kutoruhusu uandishi na usomaji huru, kuondosha

Mahkama za kisheria na haki ya utetezi huru, kuendeleza sheria yakuweka watu kizuizini

89
na kuuwawa kwa watu kwa sababu ya fikra zao za kisiasa. Kufunga Umoja wa vyama vya

Wafanyakazi na Wanafunzi (The Federation of Revolutionary Trade Unions na Zanzibar

Revolutionary Students Union). Kufuja mipango ya kuwapatia Wazanzibari wote nyumba

nzuri zilizoambatana na mazingara ya Zanzibar, kama zile nyumba za Bambi, ilivurugwa

vur ugwa na hatimaepakajengwa nyumba za mabogi ya gari la moshi pasipo na ujuzi

wowote. Kwenda kinyume huku na program ya kuwatowa Wazanzibari katika mfumo

zorota ulitokana na upungufu wa ufahamivu wa fikra za kimapinduzi ndio ulosababisha

leo kuifanya Zanzibar iko nyuma, masikini na kuwezesha kutawaliwa na Muungano.

5.3 Vuguvugu la Venceremos

Kwa nini kulikuwa na haja ya kuunda Muungano na nani hasa aliyetaka Muungano

huo. Ingawa fununu kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar yalikuwa yameshawafikia Wakoloni

pamoja na Mashirika ya Kijasusi, kama ilivyokwisha kaririwa huko nyuma. Watu hao

walishindwa kuamini habari hizo, hasa kwa vile nyendo za Umma Party zilikuwa hazi

kuonyesha harakati zozote zilizokuwa si za kawaida, kwa hivyo habari hizo zikadha-

rauliwa. Walipokuja kutahamaki, serikali ya Hizbu imekwisha pinduliwa na baada ya

hapo hali ya hewa na mazinga ra ya Zanzibar yalibadilika kwa ghafla na kujaaa hamasa

za kimapinduzi na muamko wa kimaendeleo, kukataa sera kongwe za kijamii na kuleta

mfumo mpya wa kujikombowa. Bila ya muda mrefu kupita upepowa kimapinduzi ukaanza

kupepea Afrika ya Mashariki nzima na kutikisa mizizi ya tawala za kitimba kwiri za nchi

hizo. Wamarekani na Wangereza walipoanza kusikia "Venceremos Patriomuerte "(tu-

takubali kufa lakini si kushindwa) wakashituka na kudhani Cuba ya pili imekwisha zaliwa

na wakaona maslahi yao yako hatarini hasa kama wangeliruhusu upepo wa kimapinduzi

90
uliyojaa jazba za kijananchi na nia ya kujitolea uliyokuwa ukipepea Zanzibar na ku-

tambaa Afrika ya Mashariki na ya Kati. Viongozi wa Afrika ya Mashariki nao, akina

Nyerere, Obote na Kenyatta wakaingiwa na wasi wasi wakupinduliwa na kwa pamoja

na kwa msaada wa Marekani na Mngereza wakawa wanajitayarisha kuivamia Zanzibar

kijeshi. Kenyatta na Obote hatimae wakajitoa katika mipango hiyo na mwishowe akabaki

Nyerere peke yake (soma kitabu cha Amrit Wilson kinachokariri jinsi Nyerere na Uja-

susi wa Kimarekani walivyo shirikiana kuulazimisha Muungano wa Tanzania). Nyerere

akamshawishi naku- mtia uoga Karume na kila mmoja kati yao akiwa na sababu zake,

wakashirikiana kuunda Muungano huo bila ya kuwashauri watu wao. Sababu mojawapo

iliyomfanya Nyerere ashituke na kuogopa mapinduzi ilitokana na hatuwa ya jeshi lake ku-

taka kumpinduwa na sababu yake ya pili ilimbidi awatumikie wafadhili na mabwana zake

Marekani na Mngereza (ambaye alimuokoa kijeshi siku za ghasia za Colito Barrackswiki

tu baada ya Mapinduzi ya Zanzibar). Wamarekani na Wangereza walitishwa na mfumo

mpya uliokuwa na program ya ki mapinduzi na kuhatarisha maslahi yao ya kiuchumi na

kisiasa. Karume, kwa upande wake, alikuwa na matatizo yake mbalimbali na yale ya

mstari wa mbele yalikuwa kwa uroho, kujaribu kuhifadhi uongozi wake usichukuliwe na

Othman Sharif na Abdalla Kassim Hanga, watu hawa wakishirikiana na viongozi wengine

waliyosoma na waloendelea katika ASP. Kwa upande wa pili Karume alihisi kwamba siasa

yake ya zamani haikuweza kuwaletea wana Afro tija yoyote, wakati siasa mpya iliyokuwa

na program ya kimapinduzi, ghafla iliibadilisha sura ya Zanzibar na kungwa mkono na

Wazanzibari wengi. Kwa hivyo Nyerere hakuwa na haja ya kutumia ustadi mwingi wa

kumfanya Karume kukubali pendekezo la Muungano, wote wawili walitaka kuhifadhi

khatamu zao za utawala na maslahi yao wenyewe. Kwa kisiri siri na haraka haraka, na kwa

msaada wa wataalam wa sheria wa kikoloni, ikaundwa Katiba ya muda ya Muungano bila

91
yakushirikishwa Wanasheria wa Zanzibar au maoni ya wananchi kuulizwa. Katiba hiyo

ilifuata mfano wa katiba ya Uingereza na Ireland ya Kaskazini, yaani baina ya mtawala na

mtawaliwa, Tanganyika ya Nyerere ikiwa mtawala. Maandishi mengi yakisheria yame-

jadili upungufu wa Uhalali wa Katiba hiyo na Muungano wenyewe kwa jumla. Serikali

ya Tanzania bado haija jibu hoja hizo, isipokuwa kila usiku uchao kuleta mapendekezo

mepya ya kuidhibiti Zanzibar. Utangazaji wa makubaliano hayo baina ya Nyerere na

Karume yalifanywa makusudiwakati A. M. Babu kiongozi wa Umma Party alipokuwa

hayupo nchini. Baada yahapo, karibu viongozi wote waliyokuwa na fikra za kimaendeleo

au waliyokuwa na haki ya kuongoza ASP wa kaondoshwa nchini, ama kupelekwa Bara au

katika Mabalozi mbali mbali. Kati ya waliyoondoshwa nchini kwa sababu ya Muungano

na upingaji wa udikteta na ukoloni mambo leo walikuwa A. M. Babu, A. K. Hanga,Othman

Sharif, Salim Ahmed Salim, Salim Rashid, Mohammed Ali Foum, Hasnu Makame, Idris

Abdulwakil, Ali Mwinyi Gogo, Adam Mwakanjuki, Ali Khamis nawengi wengineo. Wale

viongozi wa ASP waliyobaki Zanzibar na kupinga udikteta na Muungano na kuwa na fikra

za kimaendeleo, karibu wote waliuwawa; hawa ni akina Sa leh Sadalla, Abdulaziz Twala,

Mdungi Usi, Khamis Masoud, Jimmy Ringo,Idrisa Majuya, Jaha Ubwa, Ngwali Usi n.k.

Viongozi wachache wa Wafanyakazi walibaki Zanzibar na hata hao baada ya muda kupita

na wao wakaombolea gerezani na kuteswa. Karibu makada wote wa Umma waliyo somea

mapambano ya kigorilla huko Cuba pamoja na makada wengine wakasafirishwa kwenda

ama Urusi au Indonesia. Wengi kabisa wa Wazanzibari waliyosoma walilamika kuhama

au kuhamishwa nchi, wengi wao kuifaidisha Bara kwa elimu na ujuzi wao na kuwacha

pengo kubwa la ujuzi Zanzibar. Baada ya vikosi vyote hivyo vya kijananchi kuondoshwa

Zanzibar, Muungano ukazidi kutia mizizi, hatimae kuletewa wataalam wa mabibo kuja

kutibu mikarafuu. Ingawaje Wazanzibari hawaku kubali kukaa kimya bali mapambano

92
na vuguvugu la chini kwa chini yaliendelea. Katika mwaka 1972,mwezi wa Aprili tarehe

saba Karume akapigwa risasi na kuuwawa, na mandhara mpaya ya kisiasa ikachipuka.

Kufuatia tukio hilo maelfu ya watu wakatiwa ndani,kati yao wakiwa wengi wa Viongozi

wa Umma Party pamoja na baadhi ya makada. Baadae pakafanywa kesi, na kesi hiyo

ikaendeshwa katika Mahkama iliyokuwa siya kisheria kwa vile Mahakimu hao walikuwa

hawana ujuzi wa kisheria, waliyokuwa ni watu wenye sura za kimapendeleo kwa vile

walikuwa wafuasi wa chama tawala tuna washtakiwa kutoruhusiwa mawakili wa kisheria

wa kuwatetea. Mkuu wamashtaka hayo ndie wakati huo huo akiwashtaki na wakati huo

huo kupewa wadhifa wa kuwatetea washtakiwa hao hao. Baadhi yao walishtakiwa wakiwa

hawapo, yaani wakiwa Bara na mmoja Salim Ahmed Salim akiwa nchi za nje kama Balozi

waTanzania, mashtaka yake hatimae yakafifirishwa. Wafuatao ndio waliyoshtakiwa:

1. A. M. Babu

2. Khamis A. Ameir

3. A. B. Qullatein

4. Amar Salim Saad

5. Nurbhai Issa

6. Ali Sultan Issa

7. Abdulrazak M. Simai

8. Mussa Shaaban

9. Moh’d A. Baramia

10. Kadiria Mnyeji

11. Miraji Mpatani

12. Ali Mshangama

13. Haroub M. Salim

93
14. Hussein Mbaruk

15. Moh’d S. Mtendeni

16. Cpt.Abdulla Khamis

17. Said Moh’d Said

18. Ali Seif Karkoboi

19. Cpt. Abdull Moh’d

20. R. Moh’d Rashid

21. Lt. M. A. Chululu

22. Lt. Salim A.Rashid

23. Sgt. Humud Ali

24. Yusuf Ramadhan

25. Col. Ali Mahfoudh

26. Cpt. Hassan Makame

27. Moh’d Ali Seif

28. Said Salim Said

29. Naaman Marshed

30. Ali Hemed Humud

31. Ishaq Juma Harakati

32. Rashid M. Ahmed

33. Juma Mussa Juma

34. Ibrahim M. Hussein

35. Khamis Masoud

36. Moh’d A. Ladha

37. Moh’d A. Sahir

94
38. Moh’d Khalef Moh’d 39. Salim Abdalla Saleh

40. Saleh Ali Saleh

41. Moh’d Said Moh’d

42. Khamis Abeid Omar

43. Ibrahim Omar Soud

44. Abdulla Mussa Moh’d

45. Alawi Tahir Moh’d

46. Moh’d Khalfan Salim

47. Ahmada Shafi

48. Hassan Said

49. Tahir Adnan

50. Ali Mzee Mbalia

51. R. M. Rashid

52. Lt.Salum A. Rashid

53. Seif Said Hamadi

54. Lt.Mikidadi Abdulla

55. Lt. Ali Othman

56. Abas Mohammed

57. Lt. Abdulla Juma

58. Lt. Ahmed M. Habib

59. Cpt. Suleiman Moh’d

60. Lt.Hashil S. Hashil

61. Cpt. Hemed Hilal

62. Lt. Shaaban Salim

95
63. Lt. Amour Dg’hesh

64. Maj. Salim S. Salim

65. Lt. Haji Othman

66. Tahir Ali

67. Badru Said Badru

68. Abdulaziz Abdkadir

69. Ali Salim Hafidh

70. Ali M. Ali Nabwa

71. Moh’d A. Ameir

72. Ali Y. Baalawy

73. Saleh Abdulla

Waliyoshtakiwa wote walikuwa 81, wengine waliwachiliwa mapema.

5.4 Awamu tafauti

Baada ya kuuwawa Karume hali ya mambo ikaanza kubadilika Zanzibar. Kwanza kulikuwa

na mchuano mkubwa wa kugombania khatamu za utawala baina ya Aboud Jumbe na Seif

Bakari, ambaye ndie aliyekuwa chini ya Karume. Nyerere akaamua kumuunga mkono

Aboud Jumbe. Jumbe alileta mabadiliko tofauti visiwani, kama vile kuruhusu watu kutoa

maoni yao, kukosoa bila ya kuogopa kutiwa ndani. Aliruhusu waliyoshutumia katika kesi

ya uhaini kupandishwa Mahkamani, ingawa Mahkama yenyewe ilikuwa haijatoa ruhusa

ya utetezi huru au kuwa na Mahakimu waliyosomea sheria. Katika utawala wake Jumbe

aliweza kuondosha khofu, kuheshimu wasomi, kupunguza nguvu za Memba wa Baraza la

96
Mapinduzi, na kuleta nafuu kwa kadri fulani. Alianzisha Baraza la Wawakilishi. Ingawaje

kwa sababu yamigongano yake na Baraza la Mapinduzi likiongozwa na Seif Bakari akazidi

kuitia Zanzibar katika kabari ya Muungano. Baadae Jumbe nae akaanza kuwa muamuzi

wapekee. Baada ya muda fulani kupita Jumbe nae kama Karume, akaanza kutan- abahi

uovu wa Muungano na akaanzisha mbinu za kuitoa Zanzibar katika Muungano. Lakini

kwa bahati mbaya makosa aliyokwisha yafanya ya kuizamisha Zanzibar katika matope

ya Muungano yalikuwa ni mengi na kumzamisha mwenyewe kila alipojaribu kujitowa.

Kosa kubwa kabisa alilolifanya Jumbe dhidi ya maslahi ya Zanzibar ilikuwa ni kukifufua

chama cha ASP (viongozi wake halisi kwisha kuteketezwa) na baadae kukiunganisha

na TANU na hatimae ku- zaliwa CCM, MAMA WA BALAA LOTE. Baadae chama

hicho hicho cha CCM alichokuwa mmoja wawakunga wake kikamfukuza kwenye uongozi

kama kitakataka. Baada ya kuondoshwa na kuuzuliwa Jumbe kwa muadhara mkubwa,

akawekwa Ali Mwinyi, ambaye siku za mwanzo alipendeza sana Zanzibar lakini baadae

akababaishwa na Urais wa Muungano na kuusahau Uzanzibari wake. Idris Abdul-wakil

(mmoja kati ya wale viongozi waliyojitowa ASP 1964) baada yakuchukuwa pahala pa Ali

Mwinyi akagonganishwa na Wazanzibari wenzake.Kufuatia tukio hilo kundi la watu Saba

likiongozwa na Seif Sharif Hamadi likafukuzwa Chama na kutolewa madarakani. Idris

Abdulwakil nae nyota yake mwishowe ikafifia katika CCM ya Nyerere, na wakati CCM

inapanga kumuuzulu, Idris akawawahi na kujiuzulu mwenyewe na kujikosha na balaa la

Muungano. Salmin Amour akashika ukanda lakini kabla hajawahi kukaa vizuri katika

Kiti chake Salmin akajiona kwamba alikuwa "Chui wa Karatasi" asiyekuwa na meno

walamakucha. Hali hiyo ilidhihirika wakati alipoiunganisha Zanzibar na Jumuiya wa

Nchi za Kiislaam. Bila ya mapenzi yake akaambiwa aitowe Zanzibar katika Jumuiya hiyo.

Hapo akatanabahi kwamba Urais wake wa Zanzibar ulikuwa ni wa jina tupu, usiyokuwa na

97
nguvu sawa hata za Waziri mdogo wa Bara. Wakati huo alitakiwa Rais Amour aonyeshe

"Ushupavu" wake kama Kiongozi mwenye uzito na ama kuitoa ASP katika CCM au

kuitoa Zanzibar katika Muungano. Wapiiii, kipindi cha kihistoria kimempita Rais Amour

na Wazanzibari itabidi wangojee ushupavu wa Rais mpya atakayekuwa na ukakamavu na

ushupavu wa kutosha unostahiki Rais wa nchi. Amour nyota yake nae imekwishafifia katika

CCM na Nyerere yumo kumtayarisha Dr. Omar au mwengine kama huyo kuchukuwa

madaraka.

5.5 Migogoro ya Nyerere na Karume

Nyerere kwa mara nyingi katika historia ya Zanzibar amekuwa akijaribu kuwaamulia

Wazanzibari nini la kufanya kama vile wao wenyewe hawajajiweza. Kwa ujanja na ulaghai

wake aliweza kufanikiwa kutia fitina baina ya Wazanzibari wenyewe kwa wenyewe kama

vile Mngereza alivyofanya siku za nyuma. Wakati wa mwanzoni watu wengi hawakuelewa

nini azma ya Nyerere, na kumdhani kama ni mtu mwema, lakini hatimae ilidhihirika

kwamba alikuwa akitaka kuitawala Zanzibar. Kwa upande mmoja, kati ya baadhi ya njama

zake, baada ya kuundwa Muungano, alisaidia na kuhakikisha kwamba wale Wazanzibari

waliyokuwa wamesoma walihamishwa Zanzibar. Kwa njia kama hiyo sehemu kubwa ya

uongozi uliyobaki Zanzibar ulikuwa ni wa wale wasiosoma, ambao aliweza kuwaendesha

na kuwadanganya kama alivyotaka. Kwa upande wa pili, ingawa suala la usalama lilikuwa

chini ya Muungano na Nyerere ndiye aliyekuwa mkuu wa Muungano, ili kuhifadhi maisha

ya Muungano huo alikataa kuhami maisha ya viongozi wa Kizanzibari waliyouwawa kwa

sababu ya kuwa na fikra tofauti za kisiasa. Kwaupande wa tatu Nyerere aliwatumilia

wale waliyoitwa Wabunge wa Zanzibar, Bungeni Dar es salaam, kuwazuwia Wabunge

98
wa Tanganyika kumshambulia Nyerere na serikali yake. Wabunge hao wa Zanzibar wali-

ogopa kuwasaidia Wabunge wa Tanganyika kwa vile waliporudi Zanzibar walim’haha

Karume ambaye asingelisita kuwapeleka chuoni kwa Mandera, kwenda kudurusu. Kwa

njia hii Nyerere aliweza kudhibiti utawala wa Tanganyika na wa Zanzibar kwa wakati

mmoja. Ingawaje, kulifika wakati fulani ambapo, maingiliano baina ya Karume na Ny-

erere hayakuwa mazuri na Karume alifanya njama na mbinu za kum adhiri Nyerere kila

alipopata nafasi. Katika mwaka wa 1971 Karume alifanya mbinu i li ahakikishe kwamba,

ikiwa kwa sababu yoyote Nyerere atasita kuwa Rais, basi yeye Karume ndiye ahakikishiwe

Urais wa Tanzania. Mipango hiyo aliwahi kuipendekeza hatambele ya mkutano wa Baraza

la Mawaziri. Nyerere akamshitukiya Karume, na akamsail Karume mbele ya mawaziri,

na kumuuliza kama Karume alitarajia kuchukuwa Urais akifa Nyerere. Kama kawaida

ya mgogoro kama huo, Jumbe aliingilia kati na kumhakikishia Nyerere kwamba" Karume

hakuwa na azma mbaya na yeye, bali Karume alieleweka vibaya". Nyerere bi- la ya ku-

fikiri na kutanabahi sana, kwa haraka haraka, kama desturi yake akatunga sheria mpya ya

Tanzania Bara, na kuipa serikali uwezo wa kuwa na Waziri Mkuu, ili kama yeye Nyerere

kwa sababu hii au ile angelikutwa na ajali ya kifo cha ghafla, basi Waziri Mkuu huyo

ndiye aliyekuwa achukuwe ukanda wa Urais wa Muungano na sio Makamu wa Kwanza

wa Rais, yaani Karume .Uamuzi huu ulimkasirisha sana Karume kwa vile aliona kwamba

uwezekano wake wa kuwa Rais, pindi Nyerere akifa ulififirishwa na kuondoshwa, na

kwamba Waziri Mkuu huyo atakuwa wa Zanzibar vile vile. Ingawaje, Karume hakukubali

kushindwa, kwani alidai kwamba kitendo hicho cha Nyerere cha kujiamuliya hivyo ilikuwa

ni, kuiruka na kuikuuka Katiba ya Muungano na kujiamulia kuteuwa na kuanzisha Wad-

hifa wa Waziri Mkuu kulikuwani kinyume na Katiba ya Tanzania. Kwa hivyo Karume

akaamuwa kumpeleka Nyerere Mahkamani kwa kuikiuka Katiba. (Tutakumbuka baadae

99
hata Jumbe nae alitaka kumpeleka Nyerere katika Mahkama kwa kukiuka makubaliano

ya maandhishi ya Muungano.) Karume tokea mwaka 1970 alikuwa ameanza kampeni

kali sana ya kwenda sehemu mbali mbali kama vile Kariakoo na kwenda kuwahutubia

makabwela na kutia fitna dhidi ya Nyerere na kuwaahidi makabwera kazi na nyumba

bure Zanzibar kama Nyerere angelishindwa kuwapatia vitu hivyo Bara. Karume vile vile

alikuwa akitowa mapesa kuwapa vilabu vya mipira vya Bara ili kuwavutia na siasa yake,

wakati huo huo Wazanzibari wakikaa na njaa. Karume alijaribu kuwashawishi wanajeshi

wa Kizanzibari waliyokuwa Bara, kumpelekea khabari za kijasusi dhidi ya utawala wa Ny-

erere. Isitoshe katika sherehe za miaka kumi ya uhuru wa Tanganyika, Karume alipeleka

Dar es salaam majeshi ya Zanzibar na silaha kubwa kubwa, ikiwemo mizinga tofauti.

Majeshi hayo yanasemekana yalikuwa yajiandae sehemu mbili tofauti za Uwanja wa Taifa

ambako sherehe hizo zilikuwa zifanyike. Uwanja huo uliwekwa katikati na makombora

na mafashi fashi yalikuwa yakutanie katika ya anga ya Uwanja huo. Makombora hayo

yalikuwa yatupwe kutoka hizo sehemu mbili tofauti, moja sehemu ya Mgulani na nyengine

sehemu za Mjini. Hapo watu wangelikuwa wakishughulika na kutizama mafashi fashi an-

gani, na wale askari wa jeshi la Zanzibar waliyoshiriki katika paredi hiyo wangelimtwanga

risasi Nyerere na Karume angelishika ukanda kufuatia kifo cha Nyerere. Kiongozi mmoja

wa jeshi la Zanzibar aliyekuwa aongoze majambo hayo, bahati mbaya amekwishakufa,

nae alikuwa Col. Mussa Maisara, lakini wakuu wengine wengi wa kitendo hicho bado

wahai. Kwa bahati wanajeshi wa Bara walishituka, kutokana na hemkahemka na kwa

sababu ya idadi ya askari wa kushiriki katika sherehe hizo kutoka Zanzibar iliwashitua

Jeshi la Bara na vile vile kushitushwa na wingi wa silaha hasa zikiwa silaha kubwa kubwa.

Vile vile kile kitendo cha wanajeshi wa Zanzibar waliyo omba kutumia nafasi ya zile

sehemu zilizokuwa na ulinzi mkali ili kutekelezea matayarisho ya tafrija zao, zilitia wasi

100
wasi. Baada ya kuchekechwa kwa makini Wanajeshi wa Bara wakanusia harufu ya hatari

na kwa hivyo hizo sherehe zikaaghirishwa na Nyerere kujificha. Baada ya tukio hilo

Col. Ali Mahfoudh akarejeshwa Zanzibar. Karume hakumuwahi Nyerere bali akawahiwa

yeye. Baada ya kuuwawa kwa Karume, Nyerere akaanza kutamba. Katika maziko ya

Karume, Nyerere akatokwa na machozi ya mamba, huku akichekelea ndani kwa ndani na

kuukaribisha wakati mpya. Ingawa wakati Karume alipokuwa hai Nyerere alidai kwamba

Wazanzibari walivyokuwa wakiteswa na kuuliwa yeye hakuwa na uwezo wa kuingilia

kati mambo ya ndani ya serikali ya Zanzibar, lakini mara tu baada ya kuuwawa Karume,

Nyerere mwenyewe hakusita kuchukuwa fursa ya kuwatiya ndani maelfu ya Wazanzibari

waliyokuwa Tanganyika. Wengi ya Wazanzibari hao hawakuwa hata wanasiasa, wangine

walikamatwa kwa kusingiziwa ati wamesherehekea kifo cha Karume kwa kupika pilau ya

kuku, huko Bara; au mtu mmoja, Mzee Salim, alitiwa ndani kutoka kijiji cha Ujamaa, ati

kwa sababu aliweka dhamiri kwamba, ikiwa Karume atak- ufa basi atakula ugari chini,

mchanga ukiwa sahani yake, na mtu huyo akatiwa ndani atikwa sababu alionekana akila

huo ugari chini. Ingawaje kutiwa ndani kwa watu wengine baada ya kufa Karume kulikuwa

na madhumuni maalum ya kuunufaisha utawala wa Nyerere. Shabaha moja muhimu ya

kwa nini mfano Babu alitiwa ndani, ilikuwa na madhumuni maalum kama yale ya 1964

ya kumuondosha Babu, Hanga n.k. wasije kuchafuwa mambo ya Muungano, kwani kwa

mujib wa ngazi za utawala wa Zanzibar Kinara alikuwa Karume, chini yake akawa Hanga

na baada ya Hanga alikuwa Babu. Kwa hivyo maadhali Hanga, kwa wakati huo alikuwa

amekwisha uwawa, kwa hivyo kufuatilia kifo cha Karume aliyekuwa ashike ukanda wa

madaraka ya Utawala wa Zanzibar alikuwa awe Babu (tazama orodha ya Baraza la - Mapin-

duzi, 1964) na sio Jumbe ambae alikuwa kiongozi wa tano katika orodha hiyo. Muungano

uliundwa kuizuwiya Zanzibar isifuate mwenendo wa kimaendeleo ambao hatimae ungeli-

101
wafanya Watanganyika kudai maendeleo kama hayo na hatimae kumuondosha Nyerere.

Babu na Umma Party, pamoja na mamilitanti wa ASP walionekana kama ni watu waliy-

oitakia Zanzibar msimamo madhubuti, uliyokuwa huru na wakimaendeleo, na kuwa dhidi

ya azma na njama za Muungano wa Nyerere.Kwa hivyo kuuwawa kwa viongozi tofauti

Zanzibar na kutiwa ndani kwa Babu kufuatia kifo cha Karume kulikuwa na madhumuni

yale yale kama ya kuunda Muungano, yaani kuimarisha Muungano usiyoamuliwa na watu.

Babu na Umma Party kwa jumla waliwekwa ndani kwa miaka sita, bila ya kufunguliwa

kesi yoyote huko Tanganyika ya wale aliyokuwa wametiwa ndani Tanganyika, na wale

waliyokuwa gerezani Zanzibar kuteswa kikatili, wengine kuuwawa na halafu kufanyiwa

kesi isiyokuwa na Mahakimu wa Kitaalam, wasiopendelea upande wowote, wala kuwa na

uwezo wa kupata mawakili wakuwatetea ambao waliwachaguwa na kuwataka wenyewe.

Kama Nyerere angelikuwa ametaka kesi halali ifanyike, asingelishindwa kufanya hivyo,

kwani kwa wakati huo ule aliyekuwa akimuogopa alikuwa hayuko tena na alikuwa na

nguvu za kutoshaza kuweza kufanya atakacho Zanzibar, kama tulivyoona baadae, alivyo

wasambaza kina Seif Bakari. Nyerere aliogopa kesi kufanyika Tanganyika kwa sababu

aliogopa ufichuliwaji wa mizoga aliyoificha katika makasha na makabati yake na kuogopa,

kama Babu angelimuacha nje Wazanzibari wangelimtaka awaongoze.

5.6 Tanganyika imepiga kamba

Tanganyika kwa kuunganishwa na Zanzibar imeathirika kama Zanzibar ilivyoathirika, na

kugeuzwa kama watu wawili waliyopeyana migongo, kufungwa kamba pamoja na kuam-

biwa washindane mbio kila mmoja akielekea kwake, halafu atafutwe mshindi. Sababu

mojawapo ya kuunganishwa kwa nchi mbili hizi ilikuwa nikupunguza kasi za maendeleo

102
ya Zanzibar na kwa njia hiyo kuepusha hamasa kama hizo zisije zikatambaa Tanganyika

na kuwafanya wananchi wa huko kuanza kuzidi kudai haki zao zilizotokana na majasho

yao. Hali hii hatimae ingelileta mgogoro kwa Wakoloni mambo leo, mabeberu na wany-

onyaji kwa jumla. Kuambatana na vuguvugu hilo wananchi wa Tanganyika wangelidai

maendeleo zaidi ambayo hatimae yangeliwafanya kuweza kujitegemea zaidi na kuwa huru

zaidi. Wapata hasara wangelikuwa ni watawala wa Kibeberu waliyomiliki njia na fun-

guo zote za uzalishaji mali na ambao wanaamua thamani ya jasho la mfanya kazi na

bei za bidhaa ulimwenguni, bidhaa ambazo kwa daima zikimdhalilisha, kunmyonya na

kumkandamiza mnyonge ambae ni Mtanganyika na Mzanzibari wa chini. Wakati huo

huo kumlazimisha alime chai, kahawa na pili pili hoho na asilime chakula chake chaku-

jishibisha yeye na ukoo wake na kuhakikisha kwamba uchumi umedhibitiwa na wale wale

watawala wetu wa zamani. Kutokana na utawala wa kikatili wa kijerumani Watanganyika

hata alipokwisha ondoka Mjerumani huko Tnaganyika, walibaki kuwa wananchi watiifu

sana, waliyopenda usalama na waliyokuwa hawapendi vurugu. Suala jengine muhimu- lilo

wasononesha Watanganyika ni lile la mwaka 1964 wakati walipojaribu kuchukuwa silaha

dhidi ya Nyerere, hatimae walimuona Mngereza kaleta majeshi yake kumtetea Nyerere na

kuwakandamiza Watanganyika, kwa hivyo Watanganyika walihisi kwamba kama wange-

limu ondosha Nyerere basi Mngereza angeli rudisha tena kwa kutumia mabavu na ndio

maana baadae walisita sita kumuondowa Nyerere, hasakwa vile wale waliyokuwa na fikra

kama hizo waliambulia kuwekwa vizuizini hadi kuota ukungu. Hii ni sababu mojawapo

ambayo ilimuwezesha Nyerere kuweza kuwatala Watanganyika bila vuguvugu au mapam-

bano makali. Kwa vile Tanganyika kulikuwa na makabila mbali mbali, Watanganyika vile

vile walishindwa kuunganana kuweza kumpa Nyerere upinzani wa kutosha ambao hati-

mae ungeli waletea maendeleo. Waliyoathirika na kuteseka zaidi katika Muungano huu,

103
walikuwa bila ya shaka yoyote, ni Wazanzibari, kwani wao walitawaliwa mara mbili, yaani

walitawaliwa na Muungano na wakati huo huo kutawaliwa na utawala wa kikatili, wautesaji

na wa kiuwaji. Watanganyika walitawaliwa na Muungano (ambao kwa kweli ukiendeshwa

na serikali ya Tanganyika) wa Nyerere tu, in- gawa baadhi ya Watanganyika walipowekwa

vizuizini walivushwa kwenda Unguja kushuhudia nakuonja mateso ya gerezani kwa Man-

dera. Chini ya jina la Muungano, Watanganyika walinyimwa me ngi, hata mambo yale ya

kawaida ya nchi huru, kama vile kuwa na Bunge lao wenyewe, ambamo wangeliweza kukaa

kwa siri au kwa dhahiri na kuamuwa mambo ya maslahi yao wenyewe. Kunyimwa kwa

Watangayika kwa kikao huru kama hiki hakijawanyima Watanganyika tu ku jitambua kama

Taifa na Nchi huru, bali papo kulileta athara kubwa mno kwa- Wazanzibari. Watanganyika

walikuwa wakijuwa wazi mateso ya kikatili yaliyokuwa yakiwapata Wazanzibari wakati

wa Karume; kinyimwa chakula, kunyimwa masomo, kuozwa kwa nguvu,kufukuzwa nchi

walizozaliwa, kutokuwa na usalama, kunyanganywa wake zao kwa nguvu, kutishwa saa

zote, kupewa mishahara ya chini, kutokuwa na haki za kifanyakazi na kikulima, wanawake

kutoheshimiwa na kutowakilishwa, vijana kulazimishwa kufanya kazi makambi ya kazi

bila manufaa yoyote, kuzuiliwa kusafirikwa wanafunzi, kupigwa risasi watu msikitini,

kutiwa vizuizini kwa mashekhe, kukimbizwa kwa wataalam na kufukuzwa kwa shirika

la siha la Umoja wa Mataifa(WHO), kuhamisha Wazanzibari waliyosoma na waliyokuwa

na fikra za kimaendeleo,kunyang’anywa ovyo kwa mali za watu, kutiwa nd ani kwa ovyo

kwa watu wenye fikra tofauti vizuizini, kuteswa kwa vipigo vya kinyama mbali mbali

kwa waliyotiwa vizuizini, kuuwawa kwa Viongozi wa Kisiasa waliyokuwa na fikra to-

fauti na Karume na mengi mengine maovu; ingawa yote haya wakiyajuwa, Watanganyika

waliyanyamazia kimya, maonevu yote haya ya kikatili, kutotetea haki za kibinaadam za

Wazanzibari na badala yake walinong’ona pembeni pembeni tu.Pindi Watanganyika wan-

104
gelikuwa na Bunge lao huru wakati huo, basi Wazanzibari wanaamini kwamba mateso hayo

ya Wazanzibari wasingeliyanyamaziya na waasingeliruhusu jeshi la Tanz- ania kumhami

Karume. Kwa hivyo Watanganyika hawana haki tu ya kuwa na Bunge lao huru kama Taifa

na Nchi yeyote huru ulimwenguni, bali wana lazima na wajib wa kupiganiwa haki hiyo.

Kuwepo kwa Bunge huru la Tanganyika kunatarajiwa kuleta haki za kidemokrasia halali

zitazopigania hata haki za Wazanzibari. Na Mzanzibari yeyote yule ambaye atapinga haki

za Watanganyika kuwa na Bunge huru basi si mpinga mandeleo ya Tanganyika peke yake,

bali wakati huo huo mtaka kuwaona Wazanzibari wanateseka milele.

5.7 CCM hazina ya baa na balaa

Kama ilivyokwisha kaririwa huko nyuma Mapinduzi ya 1964 hayakupangwa wala kutekelezwa

na ASP, bali na sehemu ya ASYL na hatimae Umoja huo wa Vijana ukahakikisha kutoweka

kwa karibu viongozi wote wa juu wa ASP, wakiwemo kina Hanga, Othman Sharif, Saleh

Sadalla, Mdungi Usi, Ngwali Usi, Khamis Masoud, Abdulaziz Twala n.k. Chama hasa

kilichokuwa kiki tawala Zanzibar baada ya Mapinduzi, kwa hivyo hakikuwa ASP bali

ilikuwa ASYL ambayo ilishirikiana na Karume kuuwa, kutawala kwa mabavu, na nguvu

za mwisho zikiwa katika Kamati ya Watu 14 wa Baraza la Mapinduzi ambao wote wa-

likuwa ni ASYL, Karume aliingizwa baada ya Okello kufukuzwa nchi. Aboud Jumbe,

hakuwa- mwana ASYL, wala kuwa mwana kamati wa Kamati ya watu 14, kwa hivyo

Jumbe alipopata khatamu za utawala akiungwa mkono na Nyerere ikambidi ajenge Boma

lake mwenyewe. Kwahivyo akajaribu kuifufua ASP, lakini hichi hakikuwa kile chama

cha ASP kilichotambulika kabla, kwani viongozi wake wote halisia walikwisha toweshwa,

kwa hivyo viongozi wa juu wa chama hicho kipya hatimae wakabaki wale wale wana

105
ASYL. Itakumbukwa, mara tu baada ya kuuwawa Karume jinsi Aboud Jumbe alivyokuwa

akitatanishwa na Seif Bakari, ambae alijihisi kuwa na haki ya Urais wa Zanzibar, baada

ya kufa Karume. Wakati Seif Bakari alipotishia kutumia nguvu za kijeshi, kwa vile jeshi

la Zanzibar lilikuwa chini yake, Nyerere akaingilia kati na kumkanya Seif Bakari awache

njama za kutaka kumpinduwa Jumbe na kama angelijaribu kufanya hivyo basi angelikiona

cha mtema kuni Nyerere; Seif Bakari akaufyata. Kufuatia shida na matatizo ya kila aina

ya Zanzibar wanachama wa zamani wa ASP ndio waliyoteseka zaidi kuliko hata wafuasi

wa vyama vyengine, kwa hivyo wanachama hao wakaamuwa kutokiunga mkono chama

hicho kipya, kwani walijuwa kwamba balaa litakuwa ndilo lile au akhasi ya hivyo. Kwa

vile nguvu za utawala wachama hicho bado zilikuwa chini ya ASYL, Jumbe akaharakiza

kuungana na TANU ili kuvunja nguvu za ASYL. Kile alichokifanya Jumbe ilikuwa sio

kuunganisha TANU na ASP, chama ambacho kilikuwa hakipo tena. Kwa hivyo, bila ya

kutanabahi, kile Jumbe alichokiunganisha ilikuwa ni ASYL na TANU, kwani mwishowe

viongozi hao hao, yaani wa ASYL, ndio waliyowakilisha Zanzibar katika Kamati Kuu ya

CCM, kiini na kinara cha Utawala wa Tanzania. ASYL wakiwa nusuya viongozi katika

Kamati hiyo. Wakiwa pamoja na Nyerere na baadhi ya vibaraka wa Bara, ASYL waliweza

kuhakikisha kwamba siku zote walikuwa wengi katika kuunga mkono baa na balaa la CCM.

Kwa njia hiyo hata waliweza kuibadilisha siasa ya TANU na ya Tanganyika kwa jumla na

kuzidi kuzirejesha nyuma Zanzibar na Tanganyika kwa pamoja. Kabla ya hapo, TANU

haikuonyesha ishara yoyote ya dhahiri ya kuwa na msingi wa siasa ya kikabila, tofauti

na ile siasa iliyofatwa na ASYL. ASLY kwa vile walikuwa hawana sera au siasa yoyote

maalum ya kufuata iliwabidi waung’an’ganiye ukabila. Baada ya hapo uongozi wa juu,

katika Kamati Kuu ya CCM, ukawa unawakilishwa na siasa mbovu ya ukabila ya ASYL

na hatimae CCM ikafilisika na kuanza kutumia siasa dufu ya kudai kwamba Mzanzibari

106
yoyote aliyedai haki za Kizanzibari, haki za kibinaadam na za kidemokrasia alibuniwa

kwamba anataka kurejesha utawala wa Sultani na kutaka utawala wa Waarabu urudi. Siasa

hii ilionyesha wazi jinsi CCM ilivyokwisha filisika kisiasa na kutaka kung’an’gania katika

utawala kwa kutumia kila mbinu, nzuri au ovu. ASYL iliimba wimbo h uo kwa sababu

ilikuwa haina mfumo wa kisiasa maalum wa kutatua matatizo ya kisiasa, kiuchumi, ki-

jamii na kitamaduni ya Zanzibar. Kwa hivyo siasa za chuki zilikuwa na madhumuni

ya kuwanusisha Wazanzibari kasumba ili walale milele nawasishughulike na ukweli wa

mambo ya leo, na kuacha kutafuta sababu zakuwajulisha kwa nini maisha yao yako chini

na vipi watayabadilisha. CCM ikaingia katika shangwe la kuitikia wimbo huo na kusahau,

kwa makusudi, mambo muhimu sana kuhusu historia ya TANU na historia ya Tanganyika,

makhsusan. CCM ilisahau kwamba katika mapambano ya Watanganyika, palipiganiwa

haki sawa katika midani tofauti baina ya Watanganyika wa kawaida, ukifananisha na yale

matabaka yaliyopendelewa na utawala wa Kiingereza, huko Tanganyika. CCM, mtoto wa

TANU, vile vile inasahau kwamba wakati Zanzibar kulikuwa na tabaka la juu la Ukoo wa

Kisultan, (watu hawa wakiwa wazalia na raia wa Zanzibar), Tanganyika nako kulikuwa

na Koo zilizotukuzwa na kupata manufaa zaidi kupita raia wengine, Koo hizi zilikuwa za

Kifalme wa Bara, yaani za Kichifu. Kila mtu anaweza mwenyewe kukisia kwa nini Koo

za Kichifu hizo hazijatajwa kama ni Koo za tabakali lomuunga mkono, kumtukuza, kum-

tumikia na kupendelewa na Mngereza. CCM imesahau vile vile ule ubaguzi uliyofanyika

dhidi ya Waislaam wa Kitanganyika katika kila fani na hata kulazimishwa waislaam

kubadilisha utu wao "identity" yao, na kubadilisha majina yao ili kuweza kupata elimu ya

kwenda maskuli. CCM haijashughulishwa na kubaguliwa kwa Wazanzibari Tanganyika

wala kushughulishwa na ubaguzi wa Baraza la Mapinduzi wa wale Wazanzibari ambao

ama wanafikra tofauti au asili tofauti, wakati wengi wa hao hao Baraza la Mapinduzi

107
wakiwa na asili za kutoka nje ya Zanzibar. CCM imesahau kwamba kwa mujib wa tafsiri

ya kilimwengu ya haki za bidaadam, hata wale walio wengi kuwabaguwa walio wachache

ni haramu. CCM inapoleta ubaguzi wa asili visiwani Zanzibar kwa kutarajia kuungwa

mkono na wananchi, inafaa ikumbuke kwamba wengi wa wake wa viongozi wa Zanzibar,

ni wenye asili za Kiarabu hiyo kuwafanya hata watotowao kuwa wenye asili ya kubag-

uliwa. Viongozi hao wa ASYL/ASP walipopata vyeo hawakwenda kumuowa Mwanakheri

wa Ng’ambo, Chwaka, Mkokotoni au Kizimkazi. Kwa kasumba zao za kubabaishwa na

singa na rangi, waliwaona ndugu zao kinyaa na kutafuta masinga, halafu wakitubabaisha

sisi kuhusu Waarabu. Viongozi hao wa leo wanaishi kwa anasa, utukufu na kuwa na nguvu

zaidi ya huo Usultani wa Kibunsaid wanaotubabaishia.

Mwanzoni Wazanzibari wengi walivyosikiya kwamba ASP (yaani ASYL Zanzibar)

itaondoshwa na kuunganishwa na TANU, walipata tamaa na kudhania kwamba hali ya

kisiasa Zanzibar itabadilika na kuona bora chama hicho kikorofi cha ASYL kikiondoshwa.

Haukupita muda mrefu Wazanzibari wakavunjika moyo kuona kwamba CCM badala ya

kufuata siasa njema ya kidemokrasia na iliyoheshimu haki za kibinaadam, ilianza kuon-

gozwa kwa vitisho na utawala wa mabavu ule ule uliyotumika na ASYL, na wengi wa

viongozi wake wa Kamati Kuu walikuwa ni walewale waliyoiangamiza Zanzibar.

Kuzalishwa kwa CCM katika mwaka 1977 hakumaanishi kwamba TANU imeungana

na chama cha kisiasa Zanzibar, wala kumaanisha kwamba hiyo TANU iliunganishwa na lile

tawi lake la Zanzibar la African Association. Kwa hivyo CCM haitokani na muunganisho

wa chama cha kisiasa cha Tanganyika na chama cha kisiasa cha Zanzibar, maana Zanzibar

kulikuwa hakuna chama cha kisiasa tena. Chama cha ASYL kilikuwa ni chama cha vijana

108
na sio chama cha kisiasa kilichotambulika kuwana sifa na ufuasi wa chama cha kisiasa

kilichobainika Zanzibar, kwani hata kabla ya uhuru chama hicho cha vijana kilikuwa na

wafuasi wachache sana. Ingawaje kila Mzanzibari anakumbuka namna Makao yao Makuu

ya Darajani yalivyokuwayakitisha. Kwa hivyo TANU kwa kweli imejibadilisha jina tu na

kujiita CCM bilaya kuwa na sehemu ya chama cha kisiasa kilichowawakilisha Wazanzib-

ari. Kwa hali hii CCM haina uhalali wowote wa kuwakilisha siasa ya Zanzibar. CCM

kwa hivyo ni chama cha Bara ambacho hakija tekeleza masharti waliyoyaweka wenyewe,

yakwamba "chama lazima kuwakilishwa kote Tanganyika na Zanzibar", na kwa mujibwa

mantiki za uchaguzi, chama hicho hakina haki ya kuweka mtetezi yoyote wauchaguzi

Zanzibar, na wale wanaojitamba kuwa wana CCM Zanzibar itawabidi amawaende wakasi-

mamie uchaguzi Tanganyika, au waunde chama chao kipya kabisa, kisicho ASP, kwani

viongozi wa chama hicho wote ni mahtuti, labda ingelikuwa jambo la maana kama wan-

geliunda chama kimpya cha ASYL ZANZIBAR. Kutokana na wimbi jipya ulimwenguni

la kutokomeza udikteta na kuleta hishma kwa binaadam na kuthamini maisha ya kawaida

ya binaadam kwa kuondosha uvunjaji wahaki za kibinaadam na kuanzisha demokrasia;

serikali nyingi ulimwenguni zililazimishwa na wafadhila wao kuanzisha siasa ya vyama

vingi. Mojawapo katikahizo ilikuwa Tanzania, ambayo ilikuwa na utawala wa chama

kimoja. Chama hicho hatimae kilikuwa baadala ya kutizama maslahi ya wananchi, kuy-

atukuza maisha yabinaadam na kupigania haki sawa za wananchi , kikazidi na kuzidi

kufuata siasa yaufidhuli na utumiaji mabavu. Chama hicho kilisahau msingi wake na

kusahaukwamba kuna tofauti baina ya "Serikali na Chama", na kwamba chama kwa

kawaida kinashughulikia siasa maalum ya chama hicho na jinsi inavyotumia siasa yake

kuifaidisha nchi nzima na sio viongozi wake tu, bali wananchi wote hata wale ambao si

wanachama wake. Baadala ya kwamba chama hicho kilikuwa kiipe serikali muongozo wa

109
kisiasa, kikaanza kuingilia kati katika kila medani, na chama kujifanya serikali yenyewe,

na mara nyingi viongozi wa chama kuingilia mambo wasiyoyaelewa. Hali hiyo ikawafanya

na wale watumishi wa serikali wajifanye/ au wafanywe wanasiasa, bila hata ya kuwa na

ujuzi au sifa za kisiasa. Kwa njia kama hiyo, ndani ya nchi iliyo filisiwa bila ya kiasi,

ama walipata maslahi bora yaki binafsi katika makazi yao, kupata vyeo pasi na kustahiki

au kuwafanya wale waliyokuwa na vyeo na madaraka serikalini hatimae kugeuzwa kuwa

viongozi wa Chama. Hali hii ilivu- ruga mambo na kuufanya mkono wa kushoto kuto-

juwa nini mkono wa kulia unafanya na kinyume cha hivyo. Hapo maamuzi ya kiajabu

ajabu kupitishwa, na mtu kutojuwa nini siasa ya Chama na nini wadhifa wa serikali na

wamtumishi serikalini. Ili mtu aweze kupata- ulwa, hata bila ya kustahiki ilitosha kwa

mfano kujipendekeza na kumtukuza Mwenyekiti wa Chama. Yule aliyepiga makelele

mengi zaidi, ya kumsifu na kumuenzi Mwenyekiti, ndiye aliyezidi kupewa cheo kikubwa

zaidi. Mwenyekiti akalevywa na kutukuzwa huko, na hata kutojali nakutotia maanani

uwezo na ujuzi wa mtu akipewa wadhifa fulani, mradi akimtukuza Mwenyekiti. Kwa

hali hiyo ikawa Mwenyekiti anazungukwa na watu wa "hewallabwana" bila- ya kuthubutu

kumkosoa au kumrekibisha Mwenyekiti. Siasa ya chama chote ikafuata msingi huo huo wa

kutoruhusu wala kustahamili urekibishaji wamawazo au utoaji fikra au makosa. Kasum-

ba hiyo ikatambaa serikalini hasa kwa vile wakuu wa maidara/jeshi/polisi wote walikuwa

wameshageuzwa wanasiasa. Wakuu hao walijuwa kwamba mradi Chama kilikuwa nyuma

yao, wangeliweza kufanya jambo lolote lililowapendeza bila ya kutarajia kurudiwa au

kuadhibiwa. Hali ya ulanguzi, wizi na unyang’anyi ikawa inapaliliwa serikalini, na kila

kitu kikawa kinahitaji chau chau. Wale waliyoiba na kufanya ulanguzi wakipewa uhamisho

au kupewa vyeo vikubwa zaidi sehemu nyengine. Yule aliyekuwa nacho kuzidi kupewa

na masikini ya Mungu kuzidi kunyang’anywa. Wanachama wa CCM walikadiriwa kama

110
millioni mbili, wengi wa hawa kutojiunga na chama hicho kwa hiari zao, bali kwa kutizama

maslahi yao ya kibinafsi , au kwa kulazimishwa, na hakuna mtu anayeweza kuwalaumu,

kwa vile nchi ilikuwa na njaa. Hali kama hii iliwalazimu wanajeshi, polisi na jeshi la

usalama wa siri, pamojana wafanya kazi wengi wa serikali na wale wote waliyotegemea

ama huduma zachama au za serikali. CCM ilikuwa na maofisi na maafisa mbali mbali

bila ya kiasi, wakiwa na vyeo tofauti bila kujulikana hasa kazi na wadhifa wao ni nini.

Hali hii pamoja na utumizi wa vifaa na matumizi tofauti kama vile kusafiri ng’ambo kwa

sababu za "maji kup- wa na maji kujaa" kumekifanya Chama hicho cha CCM, kiwe na

matumizi makubwa mno. Kwa vile CCM ilikuwa haina fedha zake wenyewe, ilibidi fedha

hizo izichote kwenye hazina serikalini, fedha ambazo ni za wananchi wote,yaani hata za

wale millioni ishirini na tano waliyokuwa si wananchama wa CCM. CCM haikuweza wala

kutaka kutafautisha madaraka ya Chama na ya Serikali, kwa hivyo walikuwa wakijitumilia

huduma zote za serikali jinsi walivyotaka wenyewe na kwa vile kulikuwa hakuna chama

cha upinzani, hakuna aliyeweza kulisaili suala hilo. Yule aliyethubutu kuulizia au kuyake-

mea mambo kama hayo, ambayo ni hakina halali yake, alijikuta amepumzishwa pahala

maalum, kwa usalama wakemwenyewe. CCM hadi leo, kukiwa na mfumo wa vyama

vingi, imezoweya mtindo huowa kufanya na kujidhani kuwa wao ni Serikali na Dola, na

kufikiri kwamba nchi ni mali ya CCM na hata leo kutoruhusu vyama vya upinzani kutumia

huduma za nchisawa na CCM, mfano kufanya mikutano na matayarisho mengine katika

heka heka za kampeni na kujitayarisha katika uchaguzi ujao. Kuzuwiya uundaji wa NGO

mbalimbali zenye madhumuni ya kukuza maisha ya wananchi wote kwa jumla.

Hali hii ni bayana zaidi Zanzibar hasa kwa vile serikali imeshatambua kwamba haina

uwezo wa kushinda katika uchaguzi ujao, Zanzibar. CCM Zanzibar, bado ina uzoefu wa

kudhani kwamba CCM ndio serikali na ndio yenye uamuzi wa mwisho. Kutoweza kujirek-

111
ibisha na kutambua kwamba sasa kuna mfumo wa vyama vingi, na maana yake ni kwamba

serikali si mali ya chama fulani bali ya vyama vyote na ya nchi nzima. Kwa desturi kile

chama chenye khatamu za utawala kwa muda fulani ni chama chenye dhamana tu ya kuen-

desha serikali kwa muda na sio kumiliki serikali kwa milele. Hali ya kuvizuiliya vyama

vya upinzani ruhusa ya kufanya mikutano au kuwachelewechea haki hizo, kuwanyima

kutumia huduma za nchi kama TV na Redio, magazeti huru, ufunguwaji wa matawi n.k.

sio khatuwa zitakazowavunja moyo wananchi bali kuzidi kulipamba moto vugu vugu la

upinzani. Kwani kama vile kila usiku ukizidi giza, asubuhi hupambazuka, ni sawa na kila

ukandamizaji ukizidi, ukombozi kukaribia. Hali ya kukandamiza upinzani hatimae, kwa

desturi, inaleta mapambano makali na kuwapa wananchi muamko wa hali ya juu kabisa.

Viongozi wa CCM wa Zanzibar inafaa waamke na kutambuwa kwamba hakuna njia yoy-

ote watakayoitumia itakayowafanya washinde katika uchaguzi ujao. Kwa hivyo itakuwa

ni jambo la maana kama wakitafuta njia ya kuungana na Wazanzibari wenzao. Vitisho,

sabotaji, kuvunja haki za kibinaadam, kupinga wimbila demokrasia, kutumia mabavu, ku-

ufumbi a macho ukweli na kudhani kama haupo, hautawasaidia kitu, bali kuharibu maslahi

ya nchi kwa jumla.

Wakati umefika kwa Wazanzibari kwa jumla kukaa pamoja na kutafuta maslahi ya nchi

na sio ya kibinafsi au ya ubinafsi. Zanzibar ina haja kubwa ya kupiga khatuwa mbele na

kuendeleza maisha ya wananchi wake, na haina haja ya NONGWA NA UBINAFSI. Wakati

umefika wa Wazanzibari kuunda Baraza jipya la kutunga Sheria mpya na Katiba mpya ya

Zanzibar kwa maslahi ya Wazanzibari wote. Mirengo yote ya kisiasa inafaa iwakilishwe

katika Baraza hilo la muda litakalokuwa namadhumuni ya kuheshimu haki za kibinaadam

na kuje nga misingi mipya yaKidemokrasia.

112
Chapter 6

MFUMO MPYA

6.1 CUF AU ZUF ?

CUF, chama cha wananchi, sehemu ya Zanzibar, ndicho chama kinachotaraji kushinda

kwa kiwango kikubwa Zanzibar katika uchaguzi ujao wa vyama vingi Tanzania. In-

gawaje, CUF si jina halisi la Kizanzibari linalopendeza sana baina ya Wazanzibari wote.

Kukubali kwa CUF na vyama vyengine vya upinzani Zanzibar, kujiunganisha na vyama

vya Tanganyika bila ya kuwa na maslahi ya aina moja na misingi ya kisiasa ipatanayo

na inayoambatana, kumefanya uamuzi huo uonekane kama kuuza heshima ya Uzanzibari.

Kama vyama vya upinzani vya Zanzibar pamoja na wale wanaojiita CCM Zanzibar wan-

gelishikilia uzi ule ule wa kudai Zanzibar ni nchi huru, taifa huru na dola huru linalostahiki

kuheshimiwa kama taifa, basi bila ya shaka yoyote wangelishinda kuirejeshea Zanzibar

heshima yake . CCM na Nyerere wasingelithubutu kuilazimisha serikali ya Zanzibar ku-

jitoa katika Jumuiya ya Waislaam na wanasiasa wa Tanganyika wasingeli thubutu kupita

na kutumia lugha ya matusi dhidi ya Wazanzibari na viongozi wake. Sababu muhimu mo-

jawapo ya kufanya Zanzibar kuzidi kutothaminiwa, ni kwa sababu Viongozi wa Serikali

na Viongozi wa Upinzani wa Zanzibar walishindwa kusimama madhubuti na kidete ku-

sisitiza kwamba walidai vyama vya Kizanzibari, na kama madai yao yasingekubaliwa,

basi wangelidai kwamba vyama vyote vingelikataa kujiandikisha katika uchaguji huo.

Wakosa zaidi, katika suala hili ni CUF, kwani ilikuwa CUF ndiyo iliyotarajiwa kuilaz-

imisha Serikali ya Zanzibar kuchukuwa khatuwa kama hiyo. Ingawa CUF na Serikali ya

113
Zanzibar zina siasa na malengo tofauti, sehemu zote mbili, bila ya kificho zinataka uhuru

zaidi kutoka Tanganyika. Pindi makundi haya mawili, pamoja na makundi mengine ya

upinzani ya Zanzibar yangelishikilia madai hayo na kutojiandikisha, basi serikali ya CCM

ingelilazimika kuyakubali madai hayo, au kujitayarisha na kulaaniwa ulimwenguni kote.

Kama serikali ya CCM ingeliendelea na kushikilia na njozi za vyama ati vya "kitaifa"

basi ingelikosa misaada ya kiuchumi kutoka kwa wafadhila wao, misaada ambayo Tan-

zania Bara isingeliweza kuikosa, wakati Zanzibar kwa miaka na miaka ilikuwa haiitaraji

misaada hiyo iliyokuwa ikiishiya na kumalizikia Tanganyika. CUF, ikiwa Zanzibar na

wafuasi wasiyopunguwa asili mia themanini, iliwajibika nakusisitiza ibaki ZUF, na hata

kama wasingelisajiliwa katika uchaguzi basi nguvuzao hatimae zingezidi kuwa kubwa na

kuifyeka CCM moja kwa moja. Chini ya mwavuli wa ZUF, fikra tofauti za Kizanzibari

zilikuwa zikiwakilishwa, kutetewa, kujadiliwa na kupelekwa mbele. Wazanzibari wengi

hata wale wa CCM waliitambuwana kuiheshimu ZUF kwa sababu walijuwa kwamba, ZUF

ikiwakilisha na kutetea Uzanzibari na utaifa wake, wakati huo huo ZUF ikitambulika kama

ni mchanganyikowa fikra za kimapambano karibu za Wazanzibari wote, wakiwemo na wale

wanaojiita CCM. Wengi wa Wazanzibari hao wanaojiita CCM, wanafanya hivyo kwa vile

hawanabudi na pindi wangeli kuwa na satwa ya kuchukuwa khatwa zao wenyewe bila

yakuomba ruhusa Dodoma, basi angalau wangelijiita CMZ, yaa- ni Chama Cha Mapin-

duzi cha Zanzibar, baadala ya CCM. ZUF kukubali kujiita CUF ilikuwa nimakosa, kwani

sasa CUF inatambulika kama chama cha siasa cha Tanzania wakati,ZUF haikutambulika

kama ni chama kimoja tu bali vyama tofauti vya Kizanzibari vilivyokuwa vikipigania

maslahi ya Zanzibar. Pindi ZUF ingeliendelea kuwa kamaZUF, basi bado ungelikuweko

uwezekano wa vyama vyote na fikra zote za Kizanzibari kuwa chini ya mwavuli mmoja.

Hali hii ingeliiwezesha Zanzibar hatakuweza kuwa na serikali moja ya Taifa ikiwakilisha

114
vyama, fikra na misingi tofautikwa maslahi ya Zanzibar yote kwa jumla na kuepusha

mgogoro wa leo wa kupiganiana kung’ang’ania Kiti cha Urais, kwani katika serikali hiyo

wangelikuwemo Afro-shirazi na CCM Zanzibar vile vile. Viongozi wa ZUF walidhani

kwamba njia pekee na ya urahisi ya kuipatia Zanzibar utaifa wake ni kukamata khatamu za

serikali na kutarajia kwamba mambo yatakaa sawa wenyewe baadae. Kwa bahati mbaya,

hali hii haionekani kuwa inamkinika. ZUF ilikuwa sio chama kimoja tu cha kisiasa, bali

ni muungano wa mikondo ya fikra mbali mbali; fikra ambazo zilitiliwa mkazo na dai la

"Kura ya maoni" . Leo kura ya maoni hatuisikii tena. Mbele kuna khatari fulani inakuja

na hatuna tena ZUF yakutulinda na khatari hiyo; na kama hatujatahadhari mapema, itapita

miaka thelathini mengine bila ya kupata uhuru wetu.

Lengo la baadhi ya Viongozi wa CUF leo ni kukamata khatamu za serikali, na- kwamba

wao pekee ndio wenye haki ya kuiongoza Zanzibar. Baadhi ya viongozi hao wanasahau

vipi wao wameweza kupata nafasi ya kuwa viongozi, wamesahau kwamba roho mbichi

za watu zime toka, wamesahau kwamba watu wameteseka na kuteswa kadri kiasi hata

leo tukafika tulipo fika. Kuna baadhi ya viongozi wa CUF wanahitaji wajisomeshe kisi-

asa kabla hawajaanza kutaka kuwafundisha wengine siasa, hasa wanachohitaji ni kukariri

historia ya kisiasa ya Zanzibar ya tokea 1964.Kati ya Viongozi hao wachache katika uon-

gozi wa CUF wasiote kwamba, CUF ikishashika serikali, wao watakuwa mabwana au

kwamba CUF pekee au viongozi wa CUF pekee ndio watakaokuwa na haki ya uamuzi

wa mwisho wa mambo ya visiwa vyetu. CUF lazima iwaelimishe baadhi ya viongozi

wake tokea hivi sasa kwamba,Wazanzibari hawataki siasa ya chama kimoja kwa sababu

wanapinga CCM tu. Hata sivyo hivyo, kile wanachokipinga Wazanzibari ni mfumo wa

ki- dikteta na wa chama kimoja, na kupinga huko ni kwa kimsingi, yaani hata itapokuwa

CUF ina khatamuza serikali Zanzibar, patatakiwa lazima pawepo vyama vya upinzani

115
na kidemokrasia- kwa jumla. Wadhifa wa kuijenga Zanzibar mpya umo katika viganja

vya mikono vya Wazanzibari wote kwa jumla. Uongozi wa nchi vile vile ni wadhifawa

Wazanzibari wote wenye uwezo na waliyokuwa tayari kuitumikia nchi kwamaslahi ya

nchi na sio maslahi ya ubinafsi. CUF inawajib wa kuhakikisha kwamba wale viongozi

wenye sifa za kudhani ni wao tu wenye haki ya kuongoza Zanzibar,wanachujwa tokea

leo na wasipewe nafasi za hatimae kuleta tena rushwa, ulanguzi,wizi, unyanganyi ubinafsi

na udikteta. CUF inatarajiwa isome kutoka na makosa ya Hizbu ya kusahau kwamba

ASP na- Umma Party vilikuwa ni vyama vya upinzani ambavyo ililazim vitambuliwe na-

vihishimiwe. Vile vile iepuke makosa ya Hizbu ya kukana kujitayarisha ku- unda serikali

ya Kitaifa na kutokubali kujiandaa kwa siku za mbele pindi chama hicho kingelishindwa

katika uchaguzi na hatimae kuwa chama cha upinzani. CUF vile vile inawajibika kuepuka

makosa ya ASP ya kuufyeka upinzani wa ndani na wa nje ya chama, na kuwauwa wanasiasa

wapinzani, wakisahau kwamba na wao wakati fulani walikuwa wapinzani. CUF lazima

iepuke makosa ya UMMA PARTI yakulinyamazia Baraza la Mapinduzi na kutochukuwa

hatuwa mpaka maji yalipomwagika na kujikusanya wao wenyewe tu. CUF lazima ilaani

uuwaji wa Wazanzibari wote na sio Wazanzibari fulani tu. CUF inatakiwa iepuke siasa

ya Baraza la Mapinduzi la kuwafukuza wazalia wa nchi kwa sababu wa likuwa na fikra

tofauti za kisiasa, kuwageuza Wazanzibari hao wakimbizi ilhali nchi yao ikiwahitaji,na

wakati huo huo kuwafukuza kazi na kuwanyanganya mali zao. Hivi ni vitendo vilivyo

dhidi ya haki za kibinaadam na ambavyo lazima vipigwe vita, kwani kila mwananchi ana

haki ya kuwa na fikra huru na kufuata mkondo atakao. CUF ikipata khatamu za serikali

inafaa ipendekeze uanzishaji wa kuruhusu Uraiya wa nchi mbili kwa wale Wazanzibari

waliyolazimika kuchukuwa uraiya wa nchi nyengine. Vile vile CUF inalazimika iepuke

siasa ya CCM ya kukaa Dodoma na kuugubika Umma wa Kizanzibari na Wakitanganyika

116
utawala wao bila ya kuwashauri au kuwashirikisha katika kutawala nchi zao na kuwanyima

kila haki ya kushiriki katika ujenzi wa nchi zao. CUF lazima tokea mapema iwaelimishe

wazi wale viongozi dhaifu kwamba madai ya demokrasia na ya kuheshimu haki za kibi-

naadam hayatasita baada ya serikali yachama kimoja cha CUF kupatikana, bali kwamba

CUF itahakikisha kutekelezwa kwamfumo wa vyama vingi, kutekelezwa kwa malengo ya

demokrasia na kuheshimiwakwa haki za kibinaadam, na sio kwamba CUF ikipata serikali

basi haya mambo yatasahaulika. Ikiwa CUF itashindwa kuyatekeleza malengo hayo basi

kuna haja muhimu na ya haraka ya kuifufuwa na kuiimarisha ZUF.

6.2 Vyama vya Upinzani vya Tanganyika

Vile vyama vya upinzani vya huko Tanganyika vinatakiwa vipewe haki za kidemokrasia

za kikamilifu bila ya kuwekewa vikwazo vyovyote, vya siri au vya kidhahiri. Kwa vile

misingi ya kisiasa, ya kitamaduni, ya kiuchumi na ya kijamii ya Tanganyika na ya Zanzibar

inatafautiana, lazima mazingara ya vyama vya nchi mbili hizo vitafautiane. Ni kinyume

na muelekeo wowote wa kisiasa kuwatarajia Watanganyika waweze kuanzisha chama cha

kisiasa Zanzibar, kuweza kujuwa shida za Wazanzibari na kuweza kuzitetea shida hizo

vilivyo. Kwa minttaraf ya mantiki za kisiasa ya kinadharia na ya kitendaji, ni kinyume

kabisa na uzoefu wa kisiasa wa kidemokrasia ambayo ina msingi wa kihalali, kulazimisha

vyama vyenye misingi yao huko Tanganyika kutafuta wafuasi Zanzibar katika dakika za

mwisho za kampeni ya uchaguzi. Ikiwa CCM (pamoja na vyama mama vilivyoizaa)

kwa muda wa miaka thelathini imeshindwa kupata zaidi ya asilimia kumi na tano ya

wapigaji kura wa Zanzibar wa leo, na asilimia kumi ya wa Bara, vipi itatarajia chama

117
kipya cha Tanganyika kuwa na uwezo huo kwa muda mfupi sana. Vyama vya Tanganyika

vinatakiwa vidai kwamba, kama CCM itashikilia msimamo huo, basi Zanzibar iwe na

majimbo na wagombaniaji uchaguzi sawa na wale wa Tanganyika, yaani kama Tanganyika

kuna watetezi 100 na Zanzibar kuwe na watetezi 100, katika Bunge lawajumbe 200 na

chama chochote ambacho kitashinda kwa asili mia kubwa zaidi katika nchi moja wapo ama

pekee au kikiungana na vyama nyengine, kiwe na hakiya kuendesha serikali ya Tanzania

nzima, yaani kama CUF itapata asili mia 80 au zaidi Zanzibar na CCM asili mia 60

Tanganyika, basi CUF ndio itakiwe kuendesha serikali ya Tanzania nzima. Kwa vile CUF

inatarajiwa kushinda Zanzibar zaidi ya asilimia themanini, kwa urahisi inaweza kuongoza

serikali hasa ikiunganisha viti vyake na vile vyama vingine vya Tanganyika. Kwa njia

kama hiyo Bunge na serikali itayofuatia inaweza kubadilisha sheria na kuweza kuanzisha

usajili mpya wa vyama wa kihalali na uondoshaji wa sheria na kanuni potofu za hivi sasa

ambazo zimebuniwa na Nyerere peke yake.

Vyama vya kitaifa vya Kitanganyika na vya kitaifa la Kizanzibari vinatakiwa kuwa na

uwezo wa kujiamualiya wenyewe na kuwa na uhuru wa kusimamisha watetezi wauchaguzi

sehemu zile wazitakazo. Kama vyama vya Tanganyika vitaamua kusimamisha watetezi

wa uchaguzi sehemu ya Tanganyika pekee waweze kufanya hivyo, na kama watapendelea

kusimamisha mjumbe au wajumbe Zanzibar, iwe wenyewe ndio watakao amuwa na sio

kulazimishwa. Vyama vya Zanzibar navyo viwe na haki kama hiyo. Katika nchi za

kidemokrasia vyama vya kisiasa vina haki yakusimamisha au kutosimamisha watetezi

katika jimbo lolote bila ya kulazimishwa na mtu yeyote. Watanganyika kama walivyo

Wazanzibari wana haki kamili za kujiamulimambo yao wenyewe.

118
6.3 Matarajio ya Mzanzibari

Matarajio ya Mzanzibari ni kupata ulinzi kamili wa uhuru wake kamili, kupata kuheshimiwa

kwa haki za kibinaadam kama zilivyodaiwa katika Tangazo la Haki za Kibinaadam la

Umoja wa Mataifa la 1949, ambalo linatetea:

uhuru, heshima na haki sawa

kupinga ubaguzi wa kikabila, rangi, uume au uke, lugha, dini, wa fikra tofauti, asili,

kitaifa, kijamii, mali, wa jinsi ya mtu au msimamo mwengine wa kijamii.

linatetea haki ya maisha, uhuru na usalama wa nafsi ya mtu kupinga utumwa wa aina

yoyote

kupinga kuadhibiwa au kufanyiwa mtu ukatili

inatetea kutambuliwa mtu kisheria ulimwenguni kote

watu wote kuwa sawa mbele ya sheria

kutetewa kwa mtu na sheria kwa mujib wa katiba/sheria

mtu asikamatwe bure, kuwekwa kizuizini au kufukuzwa kazi au nchi

kila mtu ana haki kwa kupitia mahkama huru kushughulikiwa kihalali na hadharani

kuhusu shtaka lolote dhidi yake - mshtakiwa hana makosa mpaka kosa lake lithibitishwe

na mahkama halali na ya hadhara akiwa amepewa haki za utetezi kamili mtu hana kosa

kisheria ikiwa kitendo hicho alikifanya kabla ya sheria hiyo kutungwa

mtu alindiwe haki zake za kibinafsi pamoja na maandishi ya barua zake , heshma, staha

na haki zake zilindwe kisheria

mtu ni huru kwenda na kuishi atakako

mtu ana haki ya kuhama na kurejea nchi yoyote

mtu ana haki ya kuomba ukumbizi

119
haki hiyo asiweze kunyang’anywa kwa makosa ambayo si ya kisiasa

watu wote wana haki ya kuwa na uraiya

mtu asinyang’anywe uraiya kwa maonevu au kukataliwa haki ya kubadilisha uraiya

watu wenye umri wa kujitegemea wana haki za ndoa na ya kuanzisha ukoo na kuwa

na haki ya kuingia harusi

jamii inawajibika kulinda ukoo

kila mtu ana haki ya kumiliki rasilmali

mtu asinyang’anywe mali bila ya sababu

mtu ana haki ya kuwa na fikra huru, muamko, dini au imani huru

kila mtu ana haki ya kuwa na uhuru wa fikra na wa kujieleza, kuwa na uhuru wa

haki hizo bila ya kuingiliwa kati, kadhalika kuwa na haki ya kutafuta, kupokea na kutoa

habari/fikra kupitia chombo chochote cha habari bila ya kujali mipaka ya nchi

kila mtu kwa usalama ana haki huru ya kufanya mikutano na kuunda chama

mtu yeyote asilazimishwe kujiunga na chama fulani

mtu ana haki ya kuweza kushiriki katika Serikali ya nchi yake au kwa kupitia njia ya

mtetezi wake aliyechaguliwa katika uchaguzi halali

kila mtu ana haki sawa katika huduma za kiserikali za nchi yake

Matakwa ya umma ndio yawe msingi wa uongozi wa serikali, kwa kupitia uchaguzi wa

halali wa majira, wenye kanuni za kidesturi, pakiwa na haki sawa za kupiga kura; uchaguzi

wenyewe uwe wa siri na huru.

kila mtu ana haki ya kiuchumi, kijamii na kitamaduni

kila mtu ana haki ya kufanya kazi, kuchagua kazi, kuwa na haki halali za kufanya kazi

na kulindwa na ukosefu wa kazi

kila mtu ana haki ya kupata mshahara sawa kwa kazi sawa

120
mfanya kazi ana haki ya kupata mshahara halali na wakutosha, kuhakiki sha maisha

yake na ya ukoo wake, kwa mujib wa thamani na heshima ya kibinaadam, kupandishiwa

mshahara inapomkinika

kila mtu ana haki ya kuunda na kujiunga na umoja wa wafanya kazi kuhifadhi maslahi

ya kazi yake

kila mtu ana haki ya mapumziko, kujistarehesha, kuwa na kiwango maalum cha saa za

kazi na kupata malipo katika likizo

kila mtu ana haki za lazima kama vile chakula, mavazi, nyumba, matibabu na huduma

nyengine za jamii, kama vile akiwa mgonjwa, kizuka, mzee au kutoweza kujitazama nafsi

yake

Mzazi na mtoto mchanga wachungwe na watizamwe

kila mtu ana haki ya elimu huru tofauti

elimu irekibishwe kuendeleza utu

kila mtu ana haki huru ya kushiriki katika utamaduni wa jamii, kunufaika na sanaa na

sayansi

kila mtu ana haki ya himaya kutokana na maandishi yake yote yakiwemo ya kisayansi

au kisanifu

kila mtu ana haki ya kufaidika na Tangazo hili

kila mtu anawajibika kwa jamii ambayo hatimae itamhakikishiya utu wake

kila mtu ana wajib wa kutekeleza sheria halali yenye msingi wa kidemokrasia uhuru

na haki hizi uepukwe kutumiwa dhidi ya maazimio na msingi wa Umoja wa Mataifa

ni kharamu kwa nchi, kikundi au mtu yoyote kutumilia kifungu chochote katika

Tangazo hili kuvunja haki au uhuru kama ilivyotajwa

121
Katika mkutano wa haki za Kibinaadam wa Umoja wa Mataifa huko Viena, Austria,katika

mwaka 1993 mambo yafuatayo yalisititizwa:

Usawa, heshima na kustahamiliana

kulaani ukabila, ubaguzi wa kikabila, chuki ya wageni na tabia nyengine ya kutosta-

hamiliana

Kuheshimu haki za watu wa mataifa madogo, wenyeji asilia (indegenous - people)

makabila madogo madogo, dini au lugha tofauti

kulinda haki za wafanya kazi wa kigeni

haki za sawa sawa na haki sawa za kibinaadam kwa wanawake

kuhifadhiwa kwa haki za watoto (kutumiliwa kisiasa na kuharibiwa mais- ha yao kwa

sababu ya matumizi ya madawa (unga) ya kulevya)

kuepusha mateso ya utesaji na kuwashitaki wale wanaoshiriki katika uo- vu huo

kukomesha sheria ya kuweka watu vizuizini

kukomesha kupotezwa/kutoweshwa kwa watu (wanasiasa/wapinzani)

Upungufu wa utekelezaji misingi hiyo uchunguzwe na kujulishwa Center ya Haki za

Binaadam, New York, Umoja wa Mataifa.

Ulinzi wa haki za kibinaadam ni jambo la lazima na inatarajiwa wakati CUF itapopata

khatamu za utawala itaanzisha usomeshaji wa haki za kibinaadam hizi maskulini na sehemu

zote zinazotowa huduma ya jamii pamoja na katika Redio na Televisheni.

6.4 Demokrasia

Kukubaliwa kwa uanzishaji wa vyama vingi nchini ni moja tu katika misingi yakutekeleza

demokrasia. Kwa mujib wa hali ilivyo Tanzania, hasa Zanzibar , hata suala hili hali-

122
jatekelezwa kikamilifu, kwani vyama vya upinzani ha- vipewi haki sawana Chama cha

CCM, na CCM bado ina uzoefu wa kujifanya kama ni serikali badalaya kuwa ni chama.

Kwa hivyo vyama vya upinzani si vyama vyenye uhuru wakuendesha kazi zao huru, wala

kuwa na uhuru wa kuamua jina la chama chao auchama hicho kiwakilishe taifa gani.

Mfumo wa vyama vingi wa Tanzania hauheshimu misingi ya Haki za kibinaadam na

Kidemokrasia. Zanzibar panahitajika utekelezaji wa misingi wa vyama huru vya kisiasa

vyen- yemisingi halali ya kidemikrasia.

Upinzani unatakiwa upewe haki zote za kidemokrasia za kuweza kufanya kazi hurbila

ya kuingiliwa kati na wafuasi wake kutopatishwa taabu na kufukuzwa kazi kwa sababu ya

fikra zao. Zanzibar kunatakiwa kuwe na uwezekano wa kufanya mikutano huru nchini kote

, kaskazini, kusini, mashariki na magharibi. Utoaji waruhusa hizo uwe chini ya mikono

ya idara isiyo pendelea na sio vyama hivyo kucheleweshwa cheleweshwa wanapodai haki

zao. Upinzani uwe na uandishi na utangazaji wa habari huru kwa kutumia vyombo vyao

wenyewe pamoja na vyombo vya dola. Upinzani uhakikishiwe kuweko kwa uchaguzi huru

utakaoangaliwa na wachunguzi kutoka Umoja wa Mataifa na upinzani ushirikishwe katika

tume ya kupanga nakutekeleza uchaguzi. Upinzani lazima kushirikishwa katika Baraza la

utungaji wa katiba na utungaji washeria mpya za Zanzibar. Upinzani upewe haki katika

huduma mbali mbali za kitaifa . Upinzani ushirikishwe katika madaraka tofauti serikalini.

Upinzani ushirikishwe katika kuanzisha mipango ya Mahkama huru. Upinzani uwe na

uhuru wa kuunda vyama vyenye utaifa au jina walitakalo. Upinzani ishirikishwe katika

mazungumzo ya kuirejeshea Zanzibar kiti chake katika Umoja wa Mataifa. Upinzani

uruhusiwe kufanya maandamano na kugoma . Upinzani uruhusiwe kuunda vyama vya

wafanyakazi. Upinzani uwe na haki ya kuunda vyama vya wanawake. Upinzani uwe na

haki ya kuunda vyama vya vijana. Upinzani na wananchi wa kawaida wawe na haki ya

123
kuunda NGO tofauti.

Ili kuhakikisha maisha bora ya Mzanzibari, kuishi kwa usalama na amani,kuheshimu

maisha na haki za binaadam za kila Mzanzibari, kumhakikishia kila Mzanzibari haki zote

za kihalali za kidemokrasia, pana wajib mkubwa sana kwa wanasiasa wote wa Kizanzibari

kutizama na kulinda maslahi ya Wazanzibari wote kwa jumla bila ya kujali chama wakifu-

atacho. Kwa hivyo viongozi wote wa kisiasa lazima wasahau tofauti zao na kuungana na

kutizama maslahi ya nchi nzima. ASP,CCM(ZNZ), Um- ma Parti, ZNP na ZPPP lazima

watambuwe kwamba wanawajib mkubwa sana kwa nchi yao na vizazi vyao, na bila ya

kuungana watu wataendeleakuangamizana na nchi kuselelea nyuma milele. CUF ni chama

pekee kinachowakilisha mirengo yote hiyo tofauti Zanzibar. Kwa hivyo itakuwa jambo

lamaana ikiwa viongozi wa ASP, CCM (ZNZ), Umma Party, ZNP na ZPPP wote wataingia

katika CUF kuendeleza maslahi ya Zanzibar na CUF wenyewe kabla hawajaungwa mkono

na vyama hivyo lazima wakubali kujibadilisha jina na kujiita ZUF na wakati huo huo

kuwahakikishia uongozi wa juu wakuu wa vyama vyote hivyo vitakavyojiunga nao.

124

You might also like