You are on page 1of 1

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA UCHUKUZI MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA

Simu: 255 22 2460735/2460706 FAKSI: 255 22 2460735/2460700 Barua pepe: met@meteo.go.tz Tovuti: www.meteo.go.tz Unapojibu tafadhali nakili: Kumb. Na.: TMA/1622

S.L.P. 3056 DAR ES SALAAM

10 Aprili, 2014

Taarifa kwa Umma: Vipindi vya mvua kubwa, upepo mkali na mawimbi makubwa baharini vinatarajiwa.
Taarifa Na. Muda wa Kutolewa Saa za Afrika Mashariki Daraja la Taarifa: Kuanzia: Tarehe Mpaka: Tarehe Aina ya Tukio Linalotarajiwa Kiwango cha uhakika: Maeneo yanayotarajiwa kuathirika 201404-01 Saa 9:30 Alasiri Tahadhari 11 Aprili, 2014 14 Aprili, 2014

Vipindi vya mvua kubwa inayozidi milimita 50 ndani ya saa 24, upepo mkali unaozidi kilometa 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayofikia mita 2 katika ukanda wa pwani, vinatarajiwa.
Wastani (70%) Visiwa vya Unguja na Pemba, mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Tanga, na uwezekano wa kusambaa katika mikoa ya Lindi, Mtwara na Morogoro. Hali hii inatokana na kuimarika zaidi kwa ukanda wa mvua Intertropical convergence zone (ITCZ) ambao umeambatana na ongezeko la unyevunyevu katika eneo la bahari ya Hindi. Wakazi wa maeneo hatarishi, watumiaji wa Bahari pamoja na mamlaka zinazohusika na maafa, wanashauriwa kuchukua tahadhari stahiki. Mamlaka ya Hali ya Hewa inaendelea kufuatilia hali hii na itatoa mrejeo kila itakapobidi.

Maelezo:

Angalizo: Maelezo ya Ziada

Imetolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania.

You might also like