You are on page 1of 1

Uganda yafuta sheria dhidi ya ushoga

Mahakama ya kikatiba nchini Uganda imefutilia mbali sheria dhidi ya wapenzi wa jinsia moja
ambayo ilisababisha mataifa ya magharibi kuinyima msaada.

Kadhalika sheria hiyo ilizua gumzo sana sio tu Uganda bali kote duniani ambapo mataifa ya
Magharibi yalilazimika kuingilia kati.

Mahakama ilisema kuwa mswada huo kabla ya kuidhinishwa kuwa sheria ulipitishwa na
wabunge ambao idadi yao haikutosha kupitisha mswada na kwa hivyo ni kinyume na sheria.


Baadhi ya waandamanaji waliounga mkono serikali kwa kuharamisha mapenzi ya jinsia moja
Vitendo vya mapenzi ya jinsia moja, tayari vilikuwa vimeharamishwa Uganda , lakini sheria
hiyo mpya pia iliharamisha hatua zozote za kueneza mapenzi ya jinsia moja na wakati huu hata
kuwajumuisha wanawake wasagaji kama sehemu ya wapenzi wa jinsia moja.

Mataifa kadhaa ya Magharibi yamesitisha msaada kwa Uganda hasa baada ya sheria hiyo mpya
kupitishwa.


Chanzo.
BBC SWAHILI

You might also like