You are on page 1of 3

Na Father Kidevu Blog

BARAZA la Ushauri la watumiaji wa Huduma za Usafiri wa nchi


Kavu na Majini (SUMATRA CCC), limezindua klabu ya wanafunzi
ijulikanayo kama Sumatra Club jijini Dar es Salaam.
Sumatra
Club
itakuwa
inatoa
mafunzo
na
mbinu
zitakazowawezesha wananfunzi kutambua haki zao katika huduma
ya usafiri nchini huku kauli mbiu yao ikiwa inasema, Mtetezi wa
haki, maslahi na wajibu wa abiria.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa klabu hiyo uliofanyika kwenye
viwanja vya sabasaba, Mwenyekiti wa Baraza hilo, Ayoob Omary
amesema kuanzishwa kwa vilabu vya Sumatra mashuleni
kutasaidia kutoa elimu kwa wanafunzi ili wajue haki zao katika
huduma ya usafiri.
Sumatra imeamua kuanzisha vilabu hivi mashuleni ikiwa na lengo
la kutoa elimu kwa wanafunzi watambue haki zao katika huduma
ya usafiri na wajue namna ya kutatua matatizo wanayokumbana
nayo katika vyombo vya usafiri, alisema Omar.

Sumatra Club vimesha zinduliwa katika mikoa ya tisa nchini,


miongoni mwayo ni pamoja na Mbeya, Mwanza, Mtwara na Dar es
Salaam na tayari wanafunzi wake wamenza kupatiwa mafunzo hayo
ya haki ya mtumiaji wa vyombo vya usafiri nchi kavu na majini.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Ushauri la watumiaji wa Huduma za


Usafiri wa nchi Kavu na Majini (SUMATRA CCC), Oscar Kikoyo
amesema mara nyingi watumiaji huduma za usafiri wamekuwa
wakinungunika
ilhali
wanapaswa
kulalamika
maana
manunguniko hayafiki popote.
Wanafunzi nimiongoni mwa wadau na watumiaji wakubwa wa
usafiri hasa wan chi kavu na wamekuwa wanungunikaji wakubwa
kwa muda mrefu lakini sasa tunataka wawe walalamikaji kwa
kufuata sheria na haki walizonazo katika huduma za
usafiri,Alisema Kikoyo.
Mnadhimu Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna
Msaidizi wa Polisi, Johansen Kahatano amesema jeshi la polisi kwa
kushirikiana na Sumatra pamoja na wanafunzi wenyewe wataweza
kumaliza changamoto ya usafiri kwa wanafunzi kama vilabu hivi
vitasimamiwa vizuri.
Tatizo la usafiri kwa wanafunzi litapungua na kuisha iwapo
tutasimamia vyema vilabu vyetu. Niwaombe wanafunzi wawe
waadilifu na watiifu wa sheria, msiwe chanzo cha vurugu kwenye
vyombo vya usafiri. Kuweni watatuzi wa matatizo, alisema
Kahatamo.
Uanzishwaji wa vilabu hivi imeelezwa kuwa ni moja ya mbinu
iliyobuniwa na baraza la hilo ili kukabiliana na changamoto ya
usafiri kwa wanafunzi. Kila mkoa utakuwa na vilabu vyake vya
Sumatra kwa utaratibu utakaowekwa na mikoa husika.
Mathias Kondrad mwanafunzi wa kidato cha tano kutoka shule ya
sekondari Kibasila amesema, Nimefurahi sana kuanzishwa kwa
vilabu hivi, tunaimani nasi sasa tutathaminiwa kama abiria
wengine. Tumekuwa tukichelewa shule kwa kukataliwa na hata

kupigwa na makondakta ili tusipande magari yao. Lakini sasa hivi


tutatumia sheria kudai haki yetu ya msingi kama abiria, alisema
Kondrad.

You might also like