You are on page 1of 2

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA WAZIRI MKUU

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


HATUA ZA HARAKA ZILIZOCHUKULIWA NA SERIKALI KATIKA
KUKABILI MAAFA YALIYOSABABISHWA NA MAFURIKO WILAYANI
KAHAMA, MKOA WA SHINYANGA

Kufuatia mvua kubwa zilizonyesha usiku wa tarehe 04 Machi,


2015 Wilayani Kahama mafuriko makubwa yalitokea na kuathiri
wakazi wa kata ya Mwakata katika vijiji vya Mwakata, Numbi na
Mwaguguma.
Kutokana na mafuriko yaliyotokea tathmini ya awali inaonesha
kuwa watu 42 wamepoteza maisha, watu 82 wamejeruhiwa na
watu wanaokadiriwa kufikia 574 wameathirika. Jumla ya nyumba
137 zimeathirika kwa viwango mbalimbali.
Hatua zilizochukuliwa
Serikali imechukua hatua za haraka kwa kushirikiana na wananchi
kuwafikia na kuwanusuru waathirika wa mafuriko hayo waliokuwa
wamezingirwa na mafuriko. Aidha vimeanzishwa vituo vya muda
kuwahifadhi wananchi hao kwenye Shule.
Serikali imepeleka misaada ya kibinadamu kama ifuatavyo;
i.
ii.

Chakula tani 20. Maharage tani 5, Mafuta ya kupikia lita


1,126 na Sukari tani 1.3
Vifaa vya matumizi ya ndani ambayo vinajumuisha
blanketi 650, ndoo 82 za lita 20, ndoo 82 za lita 10 ;
Vifaa vya kupikia seti 82 na madumu 82

Kwa kuwa bado Serikali inalo jukumu kubwa la kuwawezesha


waathirika kurejea katika maisha
yao ya kawaida; inapenda
kuwatangazia wale wote wanaoguswa na
maafa haya kuwa
Serikali inaendelea kupokea misaada mbalimbali ambayo
inahitajika kwa waathirika.
Mahitaji haya ni pamoja na sare za shule; daftari za wanafunzi;
mavazi ya kike na kiume; na chakula. Aidha kwa kuzingatia kuwa
waathirika hawa wamepoteza mali na fedha katika maafa haya;
misaada ya vifaa vya ujenzi (sementi, mabati, mbao, n.k.)
inahitajika sana.
Utaratibu wa kupokea misaada hiyo kwa walio Dar es Salaam
wanaweza kuiwasilisha misaada hiyo Idara ya Kuratibu Maafa,
Ofisi ya Waziri Mkuu au kuwasiliana na Mkuu wa Mkoa wa
Shinyanga_ Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Serikali itaendelea kuwasaidia Waathirika dhidi ya Changamoto
zinazoweza kujitokeza hususani za kiafya zinazosababishwa na
uchafuzi wa vyanzo vya maji na mazingira. Elimu juu ya ujenzi wa
nyumba bora na makazi maeneo salama itaendelea kutolewa.

IMETOLEWA NA
Dkt. Florens Turuka
KATIBU MKUU
OFISI YA WAZIRI MKUU
6 MACHI, 2015.

You might also like