You are on page 1of 4

MAPENDEKEZO KWA DK.

JAKAYA KIKWETE, RAIS


WA JAMHURI YA MAUUNGANO WA TANZANIA
KATIKA KIKAO CHAKE NA WAWAKILISHI WA
CHAMA CHA ALBINO TANZANIA, IKULU, TAREHE
5/3/2015
JUU YA NAMNA YA KUSAIDIA
KUKOMESHA MAUAJI, UKATAJI VIUNGO, UTEKAJI
NA UKATILI DHIDI YA WATU WENYE UALBINO NA
FAMILIA ZAO
Mh. Rais,
Kutokana na kuendelea kushamiri kwa mauaji, ukataji
viungo, utekwaji na ukatili dhidi ya watu wenye
ualbino na familia zao, Chama Cha Albino Tanzania
kina mapendekezo yafuatayo kwako:
1. Ushughulikiwaji wa kesi zinazohusiana na mauaji,
ukataji viungo, utekwaji na ukatili wa aina hiyo
kwa watu wenye ualbino upewe kipaumbele,
kupitia mkakati maalum, kwamba:
a. Mashauri yote ambayo hayajapelekwa
mahakamani
uchunguzi
na
upelelezi
ukamilishwe
mapema
na
yapelekwe
mahakamani;
b. Kesi
zilizoko
mahakamani
zisikilizwe
mapema, kupitia mahakama au utaratibu
maalum na kwa watakaokutwa na makosa
hukumu itekelezwe mara moja;
c. Kuwepo mpango maalum wa kufuatilia kesi
hizi, hasa kupitia Tume ya Haki za Binadamu
na Utawala Bora, ili kutoa msaada wa
kisheria
ikiwemo
kwa
wale
ambao
hawajaridhishwa na maamuzi ya mahakama
waweze kukata rufaa.
2. Ulinzi shirikishi katika jamii uimarishwe katika
ngazi zote, kuanzia ngazi ya vijiji au mitaa
zijengewe uwezo ili ziwe na mipango maalum ya
kutoa ulinzi kwa watu wenye ualbino kwa
kushirikiana na jamii kwani pia wao ndio

wanaowatambua wageni na kupitia wao ni rahisi


hata kupata ushahidi katika kesi mbalimbali. Ni
rahisi pia kupitia kamati hizi kuzitambua kaya
zilizoko katika mazingira ambayo sio salama na
kufanya uraghbishi, ikiwemo kuzihamishia katika
makazi salama.
3. Serikali iwe na mkakati maalum, endelevu na
shirikishi wa kuelimisha jamii juu ya ualbino na
haki za binadamu na mpango huu wa elimu kwa
jamii uwe na bajeti maalum ambayo itakuwa
vyema kwa kuanzia ijadiliwe katika bunge lijalo la
bajeti;
4. Wahanga wa matukio haya wakiwemo watoto
wasaidiwe ili kuboresha maisha yao na
kuwajengea misingi mizuri ya maisha ya baadae:
a. Watoto walio katika kambi wasaidiwe kupata
mahitaji yao ya msingi kama vile chakula,
afya, malazi na mavazi kupitia serikali;
b. Kambi hizi ziangaliwe kwa namna pana,
ikiwa ni pamoja na kuwapa mafunzo kupitia
vyuo mbalimbali vijana walioishi kwa muda
mrefu kambini ili waweze kujitegemea na pia
kupunguza athari nyingine zinazoweza
kutokea,ikiwemo mimba na udhalilishwaji wa
kingono kama ambavyo imekuwa ikiripotiwa
katika taarifa mbalimbali;
c. Watu wazima wanaoishi katika kambi hizi
wasaidiwe kuishi maisha ya staha, ikiwemo
kupata ajira japo ndani ya kambi hizo hizo ili
waweze kujikimu na kutoa mchango wao
kwa kuwatunza watoto wakati huu ambao
hawawezi kurudi nyumbani;
d. Wale waliopata ulemavu au kujeruhiwa
serikali iwasaidie waweze kujimudu. Kuna
ambao maisha yao yamekuwa ya magumu
sana kwa mambo mengi hivyo kuwa mzigo

mzito kwa familia zao ambazo nazo nyingi ni


masikini;
e. Kambi hizi zisichukuliwe kama za kudumu,ila
zijengewe
mazingira
ya
kutoa
elimu
jumuishi, kuanzia elimu ya awali;
f. Wahanga na familia zao wapewe ushauri
(counseling) kwani wengi huwa wanaathirika
sana kisaikolojia na hapajawa na mkakati wa
kuwafuatilia.
5. Kwa kuwa mauaji yanayoendelea yanatokana na
imani za kishirikina, na katika matukio waganga
wa kienyeji wanahusika, Sheria ya Tiba Asili na
Tiba Mbadala pamoja na Sheria ya Uchawi
zipitiwe upya, zifanyiwe maboresho ili kuweza
kutofautisha vizuri juu ya aina hizi za tiba au
huduma, na jamii ishirikishwe katika uratibu wa
shughuli za waganga wa tiba mbadala au tiba
asili.
6. Kiundwe Kikosi Kazi maalum kufanya uchunguzi
wa kina kubaini wanaotuma na wanaoununua
viungo
vya
watu
wenye
ualbino
ili
washughulikiwe na kuondoa kabisa jambo hili
ambalo limekuwa na kadhia kubwa kwa watu
wenye ualbino, familia zao na jamii na Taifa kwa
ujumla.
7. Itengenezwe kanzidata (database) kwa watu
wenye ualbino kote nchini ambayo itakuwa na
taarifa mbalimbali (demographic information),
zikiwemo idadi na mahali (makazi); jinsi na umri;
elimu na ajira na; hali ya saratani ya ngozi, ili
kuisaidia serikali na wadau wengine waweze
kupanga na kutekeleza mikakati mbalimbali ya
ulinzi na jinsi ya kuboresha maisha ya watu
wenye ualbino kwa ustawi wa jamii na
maendeleo ya Taifa letu.

8. Tunapendekeza kukawepo na Kamati Maalum ya


Kitaifa, ambayo ni jumuishi, iwe inakutana kwa
vipindi maalum (mara kwa mara) kila mwaka
kujadili, kutoa mrejesho na kuishauri serikali na
wadau wengine. Kamati hii iwe chini ya Ofisi ya
Rais au Makamu wa Rais au Waziri Mkuu ili iwe
rahisi kuratibu mambo yake kwa kushirikiana na
Baraza la Taifa la Watu Wenye Ulemavu. Kwa
kuanzia, kamati hiyo pia ifuatilie utekelezaji wa
mapendekezo haya kama ambavyo utaona
yafaa, Mh. Rais.
Mh. Rais tunakushukuru sana kwa kutusikiliza.
Mapendekezo haya na mengine yatakayochangiwa na
wadau yatasaidia kukomesha mauaji na kuwafanya
watu wenye ualbino na familia zao kuishi kwa amani
kama watu wengine. Utayari wetu wa kushirikiana
nawe na serikali yetu kama ambavyo tumekuwa
tukifanya wakati wote hauhitaji msisitizo.
_________________
Ernest N. Kimaya
Mwenyekiti wa Chama Cha Albino Tanzania

You might also like