You are on page 1of 1

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI

UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA


MKOANI NJOMBE
Tume ya Taifa ya Uchaguzi inawatangazia wananchi wote wa Mkoa wa Njombe, kuwa itaanza zoezi la Uboreshaji
wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa kutumia teknolojia ya Biometric Voters Registration kuanzia tarehe
16/03/2015 hadi tarehe 12/04/2015. Aidha katika kata ya Utengule ya Mji mdogo wa Makambako Uboreshaji
utafanyika kuanzia tarehe 9-15/03/2015. Uandikishaji huo utahusisha Halmashauri zifuatazo:Mkoa

Wilaya

Kata

NJOMBE

NJOMBE TC

ZOTE

WANGINGOMBE DC

ZOTE

NJOMBE DC

ZOTE

LUDEWA DC

ZOTE

MAKETE

ZOTE

MAKAMBAKO

UTENGULE

Idadi

ya Tarehe Ya Uandikishaji

Vituo
16/03 12/04/2015

12

11-17/03/2015

Vituo vya Uandikishaji vitakuwa kwenye Vijiji, Vitongoji na Mitaa


Watakaohusika katika zoezi hili ni wananchi wote:

Waliotimiza umri wa Miaka 18 na kuendelea na wale wote watakaotimiza miaka 18 ifikapo mwezi
Oktoba, 2015.

Waliojiandikisha awali kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura la zamani ili kuhuisha taarifa zao na
kupata kadi mpya za kupigia kura.

Wale wote ambao wanazo sifa za kujiandikisha lakini hawajawahi kujiandikisha kwenye Daftari.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi inasisitiza wananchi wote wa Mkoa wa Njombe kujitokeza kwa wingi kuanzia tarehe
16/03/2015 mpaka tarehe 12/04/2015 kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ili kuwawezesha
kupiga Kura ya Maoni na kuchagua Viongozi wao katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu 2015.
Vituo vya kujiandikisha vitafunguliwa kuanzia saa 2:00 Asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni
Kumbuka:- Hutaweza kupiga Kura ya Maoni au Kupiga Kura wakati wa Uchaguzi Mkuu kama utakuwa
hujajiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. Nenda kajiandikishe sasa.
Tangazo hili limetolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi, S.L.P. 10923, Dar es Salaam

You might also like