You are on page 1of 8

HABARI

HABARIZA
ZA
NISHATI
NISHATI&MADINI
&MADINI

NewsBulletin
http://www.mem.go.tz

ToleoNo.
No.5165
Toleo

Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM

Tarehe
1- 7 May
, 2015
Tarehe
- 23-29
Januari
, 2015

Wabunge

MWIJAGE
KUKAGUA
UMEME
KUSINI--Uk2
Uk 2
WAZIRI
WA NISHATI
NA MADINIMIRADI
AZINDUAYA
RASMI
BODI YA TANESCO

KERO YA UMEME
DAR SASA BASI

Waimwagia sifa MEM, TANESCO, REA

Ni baada ya kukamilika kwa vituo vikubwa vinne na vidogo 22 vya kupoza umeme
Kuwa jiji lenye miundombinu bora ya umeme Barani Afrika

ariarU
i Ukk..2
SomSoamhaahbab

Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kuanza kwa ziara yake kwenye vituo vya
umeme vilivyopo jijini Dar es salaam. Lengo la ziara yake lilikuwa ni kujionea maendeleo ya ujenzi wa vituo hivyo pamoja na kuzungumza na
Mkurugenzi MtendMkurugenzi Mkuu wa
Waziri
wa Nishati
watendaji.
Naibu Waziri wa Nishati na
Naibu Waziri wa Nishati na
aji wa TANESCO,
REA, Dk. Lutengano
na Madini, Profesa
Madini, anayeshughulikia
Madini anayeshughulikia
Mhandisi Felchesmi
Mwakahesya
Sospeter Muhongo
Madini Stephen Masele
Nishati, Charles Kitwanga
Mramba

Simbachawene aagiza Selcom kufungiwa- Uk 3

JWTZ wapongezwa kunusuru mtambo wa Msimbati-Uk4

Ofisi ya Mawasiliano Serik alini inapokea habari za matukio mbalimbali


kwa ajili ya News Bullettin hii na Jarida la Wizar a ya Nishati na Madini
Ofisi ya Mawasiliano Serik alini inapokea habari za matukio mbalimbali
Wasiliana
nasi ya
Kitengo
cha
Mawasilianohii
kwa
simu
Namba
22 2110490
Fax 2110389
Mob: +255 732 999263
kwa ajili
News
Bullettin
na
Jarida
la+255
Wizar
a ya Nishati
na Madini
au Fika Ofisi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: badra77@yahoo.com
Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263
au Fika Ofisi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: badra77@yahoo.com

HABARI ZA NISHATI/MADINI

NewsBulletin
http://www.mem.go.tz

KERO YA UMEME
DAR SASA BASI

Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (kushoto) akitoa maelekezo kwa watendaji wa kituo cha umeme cha
Mbagala mara baada ya kufanya ziara katika kituo hicho. Kulia ni Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) Mhandisi
Felchesmi Mramba.

Na Greyson Mwase

aziri wa Nishati na Madini,


George
Simbachawene
amesema kuwa ifikapo
mwezi Desemba mwaka
huu tatizo la kukatika kwa
umeme katika jiji la Dar es Salaam litakuwa
historia mara baada ya kukamilika kwa sehemu kubwa ya vituo vya kupoza umeme.
Simbachawene aliyasema hayo hivi karibuni
katika ziara yake aliyoifanya kwenye vituo
vya kupoza umeme vilivyopo jijini Dar es
salaam. Vituo hivyo ni pamoja na Kurasini,

MWIJAGE KUKAGUA
MIRADI YA UMEME
KUSINI
Na Teresia Mhagama

Naibu Waziri wa Nishati na Madini (Nishati),


Charles Mwijage anatarajia kuanza ziara ya
ukaguzi wa Miradi ya Umeme iliyo chini ya
Wakala wa Nishati Vijijini (REA), iliyoko
Kanda ya Kusini.
Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Ofisi
ya Naibu Waziri huyo, ziara hiyo ya siku
tatu, itaanza Aprili 1 na itahusisha Miradi ya
REA Awamu ya pili katika Mkoa wa Mbeya
na Ruvuma ambapo Naibu Waziri atajionea
utekelezaji wake pamoja na kuzungumza na
wananchi.
Aidha, katika ziara hiyo, Mwijage atazindua
Kituo cha Kufua Umeme kwa kutumia nguvu
ya maji kilichopo Mkoa wa Ruvuma.

Mbagala, Kinyerezi, Gongo la Mboto, Kipawa na City Centre ili kujionea maendeleo
ya ujenzi wa vituo hivyo pamoja na kuzungumza na wasimamizi wa vituo hivyo.
Akizungumzia mahitaji ya nishati ya
umeme katika jiji la Dar es Salaam, Simbachawene alisema kuwa, mahitaji yamekuwa makubwa kutokana na kasi ya ujenzi
wa maghorofa marefu yanayohitaji nishati
kubwa ya umeme hali iliyopelekea Serikali
kubuni miradi kwa ajili ya kuendeleza miundombinu ya umeme.
Kwa mfano Jengo la Mfuko wa Pensheni
kwa Watumishi wa Umma (PSPF)linatumia
umeme wenye kiwango cha megawati saba

kiwango ambacho ni zaidi ya baadhi ya


mikoa kwani ipo mikoa inayotumia megawati nne tu, alisema.
Alisema ili kuhakikisha kuwa jiji la Dar
es Salaam linapata nishati ya uhakika ya
umeme itakayoendana na kasi ya ukuaji
wake, Serikali kupitia Wizara ya Nishati na
Madini ilibuni miradi mbalimbali kwa ajili
ya ujenzi wa vituo vikubwa vinne na vingine
vidogo 22 kwa ajili ya kupoza umeme
ndani ya jiji la Dar es salaam.
Akielezea miradi hiyo Simbachawene alisema kuna mradi wa Electricity V unaosimamia vituo vya kupoza na kusambaza umeme
vya Ilala na Sokoine na kuongeza kuwa

mradi mwingine ni TEDAP kwa ajili


ya ujenzi wa vituo katika maeneo ya
Kurasini, Mbagala, Kipawa, Gongo la
Mboto na Oysterbay.
Aliendelea kusema kuwa kuna mradi
wa kusafirisha umeme kutoka Makumbusho hadi katika kituo cha City
Centre na kusambaza katika maeneo
ya Kariakoo na Jangwani
Alisisitiza kuwa kutakuwepo na kituo
cha kudhibiti usambazaji umeme
katika jiji la Dar es Salaam ambapo
kitahakikisha kuwa nishati ya umeme
inakuwa ya uhakika ndani ya jiji la
Dar es Salaam.
Mara baada ya kukamilika kwa miradi yote, hatutasikia Mbagala hakuna
umeme wakati huohuo Mikocheni
kuna umeme, itakuwa umeme ukikatika sehemu moja kifaa maalum kinaelekeza umeme mwingine sehemu
hiyo hiyo.
Simbachawene alisema kuwa mara
baada ya miundombinu ya umeme
kukamilika katika jiji la Dar es salaam,
jiji hilo litakuwa la kwanza barani
Afrika kwa kuwa na miundombinu
bora ya umeme.
Wakati huo huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Nchini
(TANESCO) Felchesmi Mramba
alisema kuwa uwekezaji katika miradi
ya umeme katika jiji la Dar es Salaam
ni mkubwa katika historia kwani haijawahi kutokea uwekezaji wa namna
hiyo kwa kipindi cha miaka 30.
Serikali imewekeza karibia shilingi
trilioni moja kwa miradi ya umeme
katika jiji la Dar es salaam, lengo
likiwa ni kuhakikisha kila mkazi wa
jiji hilo anapata nishati ya umeme na
umeme huo kuendana na mahitaji
yatakayoongezeka kwa sasa na hapo
baadaye. Alisema Mramba.
Mramba aliongeza kuwa umeme wa
uhakika utakaopatikana utaongeza
uwekezaji katika viwanda na
kuongeza fursa za ajira.

Mei Mosi Njema, Uzalendo


kwanza- Simbachawene
Awaasa kuwa wabunifu na kufanya kazi kwa bidii

Na Mohamed Saif

aziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene


ametoa salamu za Sikukuu
ya Wafanyakazi Duniani
(Mei Mosi) kwa kuwatakia
heri na fanaka wafanyakazi wote wa Wizara
na Taasisi zake katika kuadhimisha Sikukuu
hiyo.
Waziri Simbachawene amewaasa Wafanyakazi wote kufanya kazi kwa bidii na
uaminifu na kuhakikisha kila mmoja anatimiza wajibu wake ipasavyo kwa manufaa
ya Taifa.
Aidha, amewasihi wafanyakazi wote kuitumia Sikukuu hiyo kujitathmini kiutendaji
kwa lengo la kuboresha pale patakapokuwa
na mapungufu.
Tukumbuke kuwa suala la kuwatumikia
Watanzania ni jukumu letu sote. Hivyo
wakati tunasherehekea Sikukuu hii, ni
vyema pia tukajitathmini utendaji na uwa-

Ni lazima sote
kwa pamoja tuwe
wazalendo ili tuliwezeshe Taifa letu
kuondokana na
umaskini,

jibikaji wetu kwa Watanzania, anasema Waziri


Simbachawene.
Waziri Simbachawene amewahimiza wafanyakazi wote kuwa wazalendo kwa kutimiza
ipasavyo wajibu wao wa kuwatumikia Watanzania. Ni lazima sote kwa pamoja tuwe wazalendo ili tuliwezeshe Taifa letu kuondokana na
umaskini, amesema Simbachawene.
Amesema wafanyakazi ni rasilimali muhimu
katika maendeleo ya uchumi wa Taifa. Kwa kutambua umuhimu huo, Simbachawene amesema
Serikali inaendeleza juhudi zake za kuboresha
mazingira ya kazi kwa wafanyakazi ili kuwa na
uchumi imara.
Simbachawene ameendelea kusisitiza kwamba
ni wajibu wa kila mfanyakazi wa Wizara na
Taasisi zake kutekeleza kwa mafanikio na
malengo Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025.
Amewaasa wafanyakazi wote kuongeza nguvu
na weledi katika kutimiza majukumu yao ili
kukuza mchango wa Wizara ya Nishati na
Madini kwa Pato la Taifa.

NewsBulletin

HABARI ZA NISHATI/MADINI

http://www.mem.go.tz

Simbachawene aagiza
Selcom kufungiwa

MEM

Tahariri

Na Badra Masoud

Hongera kwa
kupatikana kwa
mwarobaini wa
kukatika umeme
Dar es Salaam

Na Greyson Mwase

aziri wa Nishati na Madini, George


Simbachawene ameliagiza Shirika la

Umeme Nchini (TANESCO) kuifungia mara moja kampuni ya kuuza umeme wa LUKU ya Selcom ikiwa ni pamoja na kuichukulia hatua kali za kisheria
kutokana na kutoa huduma zisizokidhi viwango.
Simbachawene aliyasema hayo katika ziara
yake aliyoifanya kwenye vituo vya kupoza umeme
vilivyopo jijini Dar es salaam kwa lengo la kujionea
maendeleo ya vituo hivyo pamoja na kuzungumza
na wasimamizi wake.
Alisema kuwa awali baada ya kufanyika kwa

taratibu za manunuzi kampuni mbili yaani Selcom


na Maxcom zilishinda tenda ya kuuza umeme kwa
njia ya LUKU na kuanza kazi mara moja.
Alisema kuwa, kumekuwepo malalamiko mengi kutoka kwa wananchi juu ya hitilafu zinazojitokeza wakati wa manunuzi ya umeme wa LUKU
kupitia kampuni ya Selcom hali iliyopelekea Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) na Serikali kutupiwa lawama.
Sisi kama Serikali kazi yetu ni kuhakikisha
kuwa wananchi wanapata huduma ya umeme bila
vikwazo vyovyote, sasa kama kampuni inashindwa
kutoa huduma bora ni bora ikafungiwa na kutafuta kampuni nyingine inayofaa, alisisitiza Simbachawene.

ivi karibuni, Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene alifanya


ziara kwenye vituo vya kupoza umeme
vilivyopo jijini Dar es salaam. Vituo
hivyo ni pamoja na Kurasini, Mbagala,
Kinyerezi, Gongo la Mboto, Kipawa na City Centre ili
kujionea maendeleo ya ujenzi wa vituo hivyo pamoja
na kuzungumza na wasimamizi wa vituo hivyo.
Akiwa katika ziara yake Simbachawene alisema
kuwa ili kuhakikisha serikali inakabiliana na miundombinu chakavu ya umeme, na mahitaji makubwa
ya umeme kwenye majengo marefu yanayojengwa
kwa kasi ndani ya jiji la Dar es Salaam, Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini imebuni miradi
mbalimbali inayohusisha ujenzi wa vituo vikubwa
vinne na vingine vidogo 22 vya kupoza na kusambaza umeme.
Alisema kuwa miradi hii ni pamoja na mradi wa
Electricity V unaosimamia vituo vya kupoza na kusambaza umeme vya Ilala na Sokoine na kuongeza kuwa
mradi mwingine ni TEDAP kwa ajili ya ujenzi wa
vituo katika maeneo ya Kurasini, Mbagala, Kipawa,
Gongo la Mboto na Oysterbay.
Mradi mwingine ni ule wa kusafirisha umeme kutoka Makumbusho hadi katika kituo cha City Centre na
kusambaza katika maeneo ya Kariakoo na Jangwani.
Alisema pia kutakuwepo na kituo cha kudhibiti usambazaji umeme katika jiji la Dar es Salaam ambapo
kitahakikisha kuwa Nishati ya Umeme inakuwa ya
uhakika ndani ya jiji la Dar es Salaam na kuongeza
kuwa inapotokea hitilafu ya umeme sehemu moja,
katika kituo hicho kutakuwa na kifaa maalum kitakachoelekeza umeme kwenda kwenye eneo husika.
Simbachawene alisema kuwa mara baada ya miundombinu ya umeme kukamilika katika jiji la Dar es
salaam, jiji hilo litakuwa la kwanza barani Afrika kwa
kuwa na miundombinu bora ya umeme.
Nishati ya umeme ni muhimu sana hususan katika
jiji linalokua kwa kasi kama Dar es salaam. Tunaamini
mara baada ya kukamilika kwa miradi yote kukatika
kwa umeme kutakuwa ni historia na kufungua fursa
za ajira kutokana na uwekezaji kuongezeka.
Kupatikana kwa umeme wa uhakika ndani ya jiji la
Dar es salaam kutachochea ukuaji wa uchumi kwani
asilimia zaidi ya 60 ya umeme nchini unatumika jijini
Dar es Salaam.
Tunapongeza juhudi zinazofanywa na Serikali
kupitia Wizara ya Nishati na Madini na tunashauri
wadau wote kuiunga mkono Serikali katika juhudi
zake za kuhakikisha nishati ya umeme inakuwa ni ya
uhakika.

Waziri wa
Nishati na
Madini, George
Simbachawene
akizungumza na
waandishi wa
habari (hawapo
pichani)

KWA HABARI PIGA SIMU


KITENGO CHA MAWASILIANO

TEL-2110490
FAX-2110389
MOB-0732999263
BODI YA UHARIRI
MHARIRI MKUU: Badra Masoud
MSANIFU: Essy Ogunde
WAANDISHI: Veronica Simba, Asteria Muhozya,
Greyson Mwase, Teresia Mhagama, Mohamed Saif,
Rhoda James, Zuena Msuya na Nuru Mwasampeta

FIVE
PILLARS OF
REFORMS
INCREASE EFFICIENCY
QUALITY DELIVERY
OF GOODS/SERVICE
SATISFACTION OF
THE CLIENT
SATISFACTION OF
BUSINESS PARTNERS
SATISFACTION OF
SHAREHOLDERS

HABARI ZA NISHATI/MADINI

NewsBulletin
http://www.mem.go.tz

MAKAA YA MAWE RUKWA KUZALISHA MEGAWAT 300 ZA UMEME


Zuena Msuya

ampuni ya uchimbaji madini ya makaa ya mawe


ya Kibo Mining inatarajia kuzalisha umeme wa
megawat 300 na kuliuzia
Shirika la Umeme Nchini (TANESCO)
,umeme ambao utakaotokana na makaa
ya mawe mkoani RUKWA.
Hayo yameelezwa hivi karibuni na
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Kibo
Mining, Louis Coetzee alipokutana na
Waziri wa Nishati na Madini, George
Simbachawene , jijini Dar Es Salaam.
Coetzee alisema wanatarajia kuanza
uzalishaji mwishini mwa mwezi Desemba mwaka 2018 pindi shughuli za
upembuzi yakinifu pamoja na taratibu
zingine muhimu zitakapokamilika.
Sasa tuko katika hatua nzuri ya
upembuzi yakinifu na kufuata taratibu
nyingine na mara baada ya kukamilisha
tutazalisha megawati 300 za awali na
kuziuzia TANESCO alisema Coetzee
Aidha amesema katika mgodi huo
wanatarajia kuajiri watanzania zaidi
500 hadi 100 katika hatua za awali za
uzalishaji.
Kwa upande wake Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene
amewataka wawekezaji hao wa kamapuni ya Kibo Mining kuharakisha kukamilisha upembuzi yakinifu pamoja
na taratibu za leseni ili kuanza kufanya
kazi ya uzalishaji.
AidhaSimbachawene
amewataka
wawekezaji hao kuwekeza pia katika
nishati itokananyo na maji, upepo,jua
pamoja na gesi.

Waziri wa Nishati
na Madini, George
Simbachawene akiwa
na mkurugenzi wa
kibo mining Louis
Coetzee na ujumbe
wake pamoja na
watendaji wengine wa
wizara ya nishati na
madini wakiwa katika
mazungumzo kuhusu
shughuli zinazofanywa
na kibo mining.

Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene akiwa na mkurugenzi wa kibo


mining Louis Coetzee pamoja na watendaji wengine wa wizara ya nishati na madini
wakiangalia ramani inayoonesha maeneo ya uchimbaji.

Mwanafunzi katika Kampuni ya Madini ya TanzaniteOne, Darwesh


Iddy Lacha, akingarisha tanzanite katika banda la kampuni hiyo
kwenye Maonyesho ya Vito ya Arusha yaliofanyika hivi karibuni
katika Hoteli ya Mount Meru jijini humo.

Meneja Miradi Mikubwa ya Umeme kutoka Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) Mhandisi Emmanuel
Manirabona (kushoto) akimweleza jambo Afisa wa Ubalozi wa Finland Nchini anayeshughulikia
masuala ya ukuaji wa uchumi Oscar Kass (kulia) katika kituo cha umeme cha Mbagala.

NewsBulletin
http://www.mem.go.tz

HABARI ZA NISHATI/MADINI

Balozi wa Sudan nchini, Dr. Yassir Mohamed Ali (kushoto)


akimweleza jambo Waziri wa Nishati na Madini, George
Simbachawene wakati alipomtembelea na kujitambulisha na
kueleza nia ya nchi yake kuja kuwekeza katika masuala ya
gesi.

Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene akimwonesha Mkurugenzi wa Kibo Mining, Louis
Coetzee pamoja na watendaji wengine wa Wizara ya Nishati na Madini wakiangalia ramani inayoonesha
maeneo ya uchimbaji.

Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Nchini (TANESCO)


Felchesmi Mramba (katikati) akimweleza jambo Waziri wa
Nishati na Madini, George Simbachawene (kushoto) alipofanya
ziara katika kituo cha kupoza umeme cha Kurasini.

Meneja Miradi Mikubwa ya Umeme kutoka Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) Mhandisi Emmanuel
Manirabona (kushoto) akimwonesha Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene ( wa pili kutoka
kushoto) mpango wa ujenzi wa kituo cha umeme cha Mbagala mara Waziri alipofanya ziara katika kituo
hicho. Katikati ni Kamishna Msaidizi wa Umeme Mhandisi Innocent Luoga. Kulia ni Mkurugenzi wa Shirika
la Umeme Nchini (TANESCO) Mhandisi Felchesmi Mramba.

HABARI ZA NISHATI/MADINI

NewsBulletin
http://www.mem.go.tz

Kitwanga aendeleza ziara kukagua shughuli za madini nchini

Na Mohamed Saif

aibu Waziri wa Nishati na Madini


(Madini), Charles
Kitwanga anatarajia kuendelea na ziara yake ya
ukaguzi wa shughuli za uchimbaji madini maeneo ya Kanda

ya Ziwa.
Kwa mujibu wa taarifa
iliyotolewa na Ofisi ya Naibu
Waziri Kitwanga, kiongozi
huyo atatembelea Mgodi wa
Dhahabu wa North Mara na
kukagua shughuli za uchimbaji wa dhahabu zinazofanywa
na mgodi huo ikiwa ni pamoja
na kuzungumza na Uongozi

wa Mgodi.
Aidha, pamoja na kutembelea mgodi huo, taarifa imeeleza kwamba Kitwanga
atatembelea maeneo mbalimbali yenye uchimbaji mdogo
ili kujionea shughuli za uchimbaji madini zinazofanywa na
wachimbaji wadogo wa mae-

Wanafunzi na
watumishi wa
Kituo cha Jimolojia
Tanzania (TGC)
wakiwa katika hafla
ya uzinduzi wa Kituo
hicho ulioambatana
na mahafali ya
wanafunzi 15 katika
fani ya uongezaji
thamani madini.

Sehemu ya
umati wa watu
waliohudhuria
uzinduzi wa Kituo
cha Jimolojia
Tanzania (TGC).
Kituo hicho
kilizinduliwa na
Waziri wa Nishati
na Madini, George
Simbachawene.

Sehemu ya
umati wa watu
waliohudhuria
uzinduzi wa Kituo
cha Jimolojia
Tanzania (TGC).
Kituo hicho
kilizinduliwa na
Waziri wa Nishati
na Madini, George
Simbachawene.

neo hayo na vilevile kuzungumza nao kuhusu masuala


mbalimbali yanayohusu shughuli za uchimbaji wa madini.
Waziri Kitwanga pia atakutana na watendaji waliopo
katika ofisi za madini katika
Kanda hiyo ili kupatiwa taarifa
mbalimbali za mafanikio na
changamoto katika usimamizi

wa shughuli za madini kwenye


maeneo wanayosimamia.
Ziara hiyo ni muendelezo
wa Ziara ambazo Naibu Waziri Kitwanga amejipangia kwa
lengo la kuboresha sekta ya
madini nchini ili kuhakikisha
mchango wa sekta hiyo kwenye pato la Taifa unaongezeka.

Wahitimu TGC
waomba kuongezwa
muda wa masomo

Na Veronica Simba
Aliyekuwa Arusha

ahitimu wa kwanza
wa Kozi ya Uongezaji
thamani madini katika
Kituo cha Jimolojia
Tanzania (TGC), wameiomba Serikali kuongeza muda wa masomo
hayo kutoka miezi sita hadi kufikia
mwaka mmoja.
Akisoma risala kwa niaba ya wahitimu wenzake, katika mahafali yaliyofanyika katika viwanja vya Kituo
hicho kilichopo jijini Arusha, hivi karibuni Beatrice Mpeta alisema kuwa
miezi sita ya mafunzo iliyopangwa
ni michache kulingana na mafunzo
husika.
Tunapendekeza
kuongezwa
kwa muda wa kujifunza angalau kufika mwaka mmoja. Tunayo matumaini kwamba maombi yetu umeyasikia na utayafanyia kazi ukiwa ni
Waziri wa Wizara ya Nishati na Madini ambayo inasimamia Kituo hiki,
alisema.
Pamoja na ushauri huo, Wahitimu waliishukuru Serikali kupitia
Wizara ya Nishati na Madini kwa
kuanzisha Kituo hicho na kuwapatia mafunzo ambayo walisema
wanaamini yatawasaidia kuendesha
maisha yao.

Walisema wamejifunza mambo


mbalimbali ikiwemo utambuzi wa
madini. Tumeweza kutambua aina
mbalimbali za madini, utofauti wake
na thamani yake. Tumejifunza kukata na kungarisha madini ya vito
ili kuyaongezea thamani. Kupitia
mafunzo haya, tutaweza kuajiriwa
na kujiajiri wenyewe kupitia vikundi
na mtu mmoja mmoja, alisema.
Akijibu risala hiyo, wakati wa
hotuba yake kwa wahitimu, Waziri
wa Nishati na Madini, George Simbachawene, ambaye alikuwa Mgeni
Rasmi katika mahafali hayo, yaliyokwenda sambamba na Ufunguzi
rasmi wa Kituo hicho cha Jimolojia,
alisema amepokea ushauri wa wahitimu na kuagiza uongozi wa TGC
kuufanyia kazi.
Simbachawene alisema anaamini
Kituo cha TGC kitasaidia kupunguza tatizo la upungufu wa rasilimali
watu katika fani za ukataji, jimolojia,
utengenezaji wa bidhaa za mapambo
na uchongaji wa vinyago vya mawe.
Kituo cha Jimolojia Tanzania
kilifunguliwa rasmi Aprili 23, 2015
na Waziri wa Nishati na Madini,
George Simbachawene ambapo pia
kulifanyika mahafali ya kwanza ya
wanafunzi 15 katika fani ya uongezaji thamani madini ya vito. Wahitimu
hao wote ni wanawake.

NewsBulletin

HABARI ZA NISHATI/MADINI

http://www.mem.go.tz

http://www.mem.go.tz

Uholanzi kuwanoa Watanzania sekta ya petroli


Rhoda James na Zuena
Msuya

erikali ya Uholanzi imesema


itaendelea kuwajengea uwezo Watanzania katika masuala ya petroli ikiwa ni pamoja
na kushirikiana katika sekta
ya nishati.
Haya yalisemwa na Balozi wa
Uholanzi nchini, Jaap Frederiks katika
kikao na Waziri wa Nishati na Madini,
George Simbachawene hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
Serikali ya Uholanzi itaendelea
kuwajengea Watanzania uwezo kwa
masuala ya Petroli na tutafuatilia kwa
umakini kuhakikisha kwamba kozi
zilizotolewa na nchi nyingine za EU

hazirudiwi, alisema Frederiks.


Akizungumza katika
kikao hicho, Mratibu wa
Nishati katika Ukanda wa
Tanzania na Msumbiji,
Marijn Noordam alisema
kuwa Uholanzi tayari imeshaanza kutoa mafunzo
kuhusu masuala ya Petroli
katika Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam ambapo wanafunzi 13 wanaendelea na
mafunzo hayo.
Aidha, alisema Uholanzi ilitoa mafunzo ya muda
mfupi kwa watumishi
wa taasisi mbali mbali za
Serikali nchini zikiwemo
TPDC, TRA na Wizara ya

Nishati na Madini.
Kwa upande wake Waziri wa Nishati na Madini,
George
Simbachawene
alisema amefurahishwa na
mpango huo na kuwaomba kuendelea kutoa mafunzo hayo ikiwezekana kuendeleza mpango huo kwa
mafunzo ya muda mrefu
kufikia ngazi ya uzamivu.
Aidha, Simbachawene
alisema Tanzania inatarajia kujiunga na masuala
ya Energy Charter ambapo
mkutano unao husu masuala hayo utafanyika tarehe
21 Mei mwaka huu nchini
Uholanzi.

Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (Katikati) na Maafisa wa Wizara ya Nishati na Madini
(kulia), katika kikao na Balozi wa Uholanzi nchini, Jaap Frederiks (wapili kushoto). Balozi huyo aliambatana
na Mratibu wa Nishati Ukanda wa Tanzania na Msumbiji, Marijn Noordam (kushoto).

Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene


(kulia) akisalimiana na Balozi wa Uholanzi nchini, Jaap
Frederiks.

WAFANYABIASHARA
MADINI VITO
WAPONGEZWA
Wachanga zaidi ya milioni 100
kusomesha wanawake

Sehemu ya umati wa watu waliohudhuria ufunguzi wa Maonesho ya Vito Arusha, wakimsikiliza


Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (hayupo pichani).

Na Veronica Simba
Aliyekuwa Arusha

afanyabiashara
na
Wachimbaji wa Madini
ya Vito nchini
wamepongezwa kwa kuanzisha Mfuko wa kuchangia
mafunzo ya Uongezaji thama-

ni madini kwa wanawake.


Pongezi hizo zilitolewa
hivi karibuni jijini Arusha na
Waziri wa Nishati na Madini,
George Simbachawene wakati
wa ufunguzi wa Kituo cha Jimolojia Tanzania (TGC), ul-

iokwenda sambamba na Mahafali ya kwanza ya wanafunzi


15 katika fani ya uongezaji
thamani madini.
Ninawashukuru
sana
kwa kuchangia fedha kwa ajili
ya kugharamia mafunzo ya
ukataji madini kwa ajili ya watoto wa kike. Endeleeni hivyo
hivyo, iwe ni ajenda ya kudumu, alisema Waziri.
Pongezi hizo zimetokana
na wadau wa sekta ya madini vito kuchangia jumla ya
shilingi 100,900,000 kwa ajili
ya mafunzo husika wakati wa
hafla ya chakula cha usiku
ikiwa ni sehemu ya programu

ya Maonesho ya Kimataifa ya
Vito ya Arusha (AGF) yaliyofanyika Aprili 21 hadi 23, 2015
jijini humo.
Hii ni mara ya nne kwa
wafanyabiashara hao wa madini vito kuchangia Mfuko wa
kusomesha watoto wa kike katika uongezaji thamani madini.
Utaratibu huo wa kuchangia
hufanyika kila mwaka wakati
wa Maonyesho ya Kimataifa
ya Vito ya Arusha.
Mpaka sasa, wanawake
15 wanaofadhiliwa na Mfuko
huo wamehitimu mafunzo ya
uongezaji thamani madini katika Kituo cha TGC, Arusha.

HABARI ZA NISHATI/MADINI

NewsBulletin
http://www.mem.go.tz

Serikali yajizatiti kusimamia


Mpango wa Power Africa Initiative
Na. Greyson Mwase, Dar es Salaam

aimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na


Madini Mhandisi Ngosi Mwihava amesema
kuwa Serikali imejizatiti katika utekelezaji wa
mpango wa Serikali ya Marekani wa kusaidia
maendeleo ya sekta ya umeme barani Afrika, unaoitwa
Power Africa Initiative.
Mpango huo uliozinduliwa na Rais Barack Obama
wa Marekani wakati alipotembelea Tanzania, mwezi Julai 2013, unainufaisha Tanzania pamoja na nchi nyingine
kama Ethiopia, Ghana, Nigeria, Liberia na Kenya.
Mhandisi Mwihava aliyasema hayo kwenye warsha
ya kujadili uendelezaji wa miundombinu ya usafirishaji
wa umeme nchini iliyofanyika mapema wiki hii ambapo
ilikutanisha wadau mbalimbali kutoka taasisi za ndani
ya nchi ikiwa ni pamoja na Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) Wizara ya
Fedha, Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na
Maji (EWURA), Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na
Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB).
Wawakilishi wengine walitoka katika makampuni ya
umeme kutoka nchi za Ufaransa, Hispania, Afrika ya
Kusini, Zambia na Marekani.
Akielezea juhudi zilizofanywa na Serikali, Mhandisi
Mwihava alisema kuwa ni kufanya mabadiliko ya sekta
ndogo ya umeme na utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN)
Alisema kuwa lengo la Mpango wa Power Africa
Initiative ni kwa ajili ya uendelezaji wa miundombinu
ya usafirishaji umeme Tanzania ili kukidhi mahitaji ya
umeme yatakayoongezeka kuanzia sasa hadi mwaka
2025.

Sehemu ya washiriki wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zikiwasilishwa kwenye


warsha ya kujadili uendelezaji wa miundombinu ya usafirishaji wa umeme nchini iliyofanyika mapema wiki hii jijini Dar es salaam. Warsha ilikutanisha taasisi mbalimbali
kutoka nchini na wataalam wa makampuni ya umeme kutoka katika nchi za Ufaransa,
Hispania, Afrika ya Kusini, Zambia na Marekani.

Megawati 10,000
kuzalishwa ifikapo
mwaka 2025
Na Greyson Mwase,
Dar es Salaam.

erikali imesema kuwa ina


mpango wa kuongeza uzalishaji wa umeme hadi kufikia
megawati 10,000 ifikapo mwaka 2025
Hayo yalisemwa na Kamishna
Msaidizi wa Umeme Mhandisi Innocent Luoga katika mahojiano maalum
na MEM Bulletin kwenye warsha ya
kujadili uendelezaji wa miundombinu
ya usafirishaji wa umeme nchini iliyofanyika mapema wiki hii jijini Dar es
Salaam ambapo ilikutanisha wadau
mbalimbali kutoka taasisi za ndani
na wataalamu kutoka makampuni ya
umeme nje ya nchi.
Mhandisi Luoga alisema kuwa
mahitaji ya umeme kwa sasa ni
makubwa, hivyo serikali inabuni miradi mbalimbali pamoja na kuwakaribisha wawekezaji kuwekeza kwenye
sekta ya umeme ili kuhakikisha kuwa
lengo la kuongeza upatikanaji wa
umeme kwa wananchi kutoka asilimia 36 ya sasa hadi kufikia asilimia 75
ifikapo mwaka 2025 linatimia.
Akielezea mikakati ya Serikali
katika kuhakikisha nishati ya umeme
inakuwa ya uhakika, Mhandisi Luoga
alisema kuwa serikali imebuni vyanzo mbalimbali vya nishati mbadala
ikiwa ni pamoja na gesi na jotoardhi.
Alisema kugundulika kwa gesi
nchini kutawezesha upatikanaji wa
nishati ya umeme ya uhakika na nyingine kuuzwa nje ya nchi.

WIZARA YA NISHATI NA MADINI

SIKUKUU YA WAFANYAKAZI- MEI MOSI 2015


Menejimenti na Wafanyakazi wa Wizara ya
Nishati na Madini pamoja na Taasisi zake
wanaungana na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt Jakaya Mrisho
Kikwete na
Wafanyakazi wote nchini katika kuadhimisha
Sikukuu ya Wafanyakazi (Mei Mosi).

Waziri wa Nishati na Madini,


George Simbachawene

Rai yetu kwa Wafanyakazi wote nchini ni


kuongeza bidii na weledi kazini ili kuliletea
Taifa letu maendeleo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt


Jakaya Mrisho Kikwete

Kwa wadau wa sekta za Nishati na Madini, tembelea kurasa mpya za Wizara kwenye Mitandao
ya Kijamii ya Twitter na Facebook kwa anuani ya Nishati na Madini Karibu tuhabarishane na
tujadili kuhusu sekta za Nishati na Madini kwa maendeleo ya Watanzania wote.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

You might also like