You are on page 1of 8

HABARI

HABARIZA
ZA
NISHATI
NISHATI&MADINI
&MADINI

NewsBulletin
http://www.mem.go.tz

Toleo
ToleoNo.
No.5167

Limesambazwa
kwa Taasisi
na Idara
Limesambazwa
kwa Taasisi
nazote
IdaraMEM
zote MEM

Tarehe - 23-29
Januari
, 2015
Tarehe
- 15-21
Mei, 2015

Mkataba
nge
WabuUuzaji

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI AZINDUA RASMI BODI YA TANESCO -Uk2

Waimwagia sifa MEM,madini


TANESCO, REA

Somahabari Uk.2

ya Bati
wasainiwa

Kaimu Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika la
Madini la Taifa STAMICO
Mhandisi Edwin
Ngonyani

Waziri wa Nishati
na Madini, Profesa
Sospeter Muhongo

Naibu Waziri wa Nishati na


Madini, anayeshughulikia
Madini Stephen Masele

Naibu Waziri wa Nishati na


Madini anayeshughulikia
Nishati, Charles Kitwanga

Wachimbaji
wadogo Kyerwa
kunufaika
Wanunuzi
haramu
waonywa
Soma habari Uk. 2

Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO,


Mhandisi Felchesmi
Mramba

Mkurugenzi Mkuu wa
REA, Dk. Lutengano
Mwakahesya

Simbachawene: TANESCO sogezeni huduma vijijini... Uk 8


JWTZ wapongezwa kunusuru mtambo wa Msimbati-Uk4
Ofisi ya M awasiliano Serik alini inapokea habari za matukio mbalimbali
kwa ajili ya News Bullettin hii na Jarida la Wizar a ya Nishati na Madini
Ofisi ya Mawasiliano Serik alini inapokea habari za matukio mbalimbali
Wasiliana
nasi ya
Kitengo
cha
Mawasilianohii
kwa
simu
Namba
22 2110490
Fax 2110389
Mob: +255 732 999263
kwa ajili
News
Bullettin
na
Jarida
la+255
Wizar
a ya Nishati
na Madini
au Fika Ofisi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: badra77@yahoo.com
Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263
au Fika Ofisi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: badra77@yahoo.com

HABARI ZA NISHATI/MADINI

NewsBulletin
Bulle
http://www.mem.go.tz

Mkataba madini ya Bati


Na Issa Mtuwa STAMICO

meelezwa kuwa, kusainiwa


Mkataba wa ununuzi wa
madini ya Bati (Tin) baina
ya KYERWA TIN COMPANY LTD ambayo ni
kampuni tanzu ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) na DAR
GOLD DMCC LTD ya Dubai ni
moja ya mkataba wenye manufaa
na maslahi si tu kwa STAMICO
bali ni neema kwa wachimbaji wadogo wa madini hayo ya bati ya
wilaya ya Kyerwa, mkoani Kagera.
Akizungumza mara baada
ya kutiliana saini mkataba huo
ofisini kwake jijini Dar es Salaam
hivi karibuni, Kaimu Mkurugenzi
Mtendaji wa STAMICO Mhandisi Edwin Ngonyani, alisema
kuwa, wameingia mkataba huo
kwa kuzingatia maslahi ya Taifa
kwani Wachimbaji wadogo wa
madini ya Bati watanufaika kwa
kupata soko la uhakika na bei
nzuri.
Aidha, Ngonyani aliongeza
kuwa, bei ya kununulia kutoka
kwa wachimbaji wadogo itakuwa
inabadilika kwa kadri bei ya
kuuzia katika soko la metali la
Uingereza (LME) itakavyobadilika, ambapo muda wote STAMICO itabakiwa na faida isiyozidi
asilimia 5-10.
STAMICO haikusudii kupata
faida kubwa katika biashara hii
kwa sababu lengo mahsusi la
Shirika ni kuwasaidia wachimbaji
wadogo wainuke na sio kupata
faida, alieleza Ngonyani.
Mhandisi Ngonyani alisema
kuwa, katika mkataba huo masuala kadhaa yamezingatiwa hususan suala la bei. Kusainiwa kwa
mkataba huo kunaleta uhakika
wa soko la kuaminika la madini
ya bati jambo ambalo kwa muda
mrefu lilikuwa ni tatizo,alisema
Mhandisi Ngonyani.
Alisema moja ya makubaliano
waliyofikia ni kuwa, uuzwaji wa
madini hayo utakuwa unazingatia bei ya soko la dunia jambo
ambalo linaondoa mjadala wa
kujadili bei ya kuuzia.
Aliongeza kuwa, hivi sasa
uhakika wa kununua madini
hayo kutoka kwa wachimbaji
wadogo upo kwa kipindi chote
bila kusimama kwa kuwa uhakika
wa soko upo, tofauti na awali
ambapo tatizo la soko lilikuwa
ni kikwazo. Hivyo, amewaonya
wanunuzi haramu wanaotorosha madini hayo nje ya nchi
bila kulipa kodi stahiki wafunge
virago warudi walikotoka maana
kuanzia sasa hawatapata nafasi
ya kununua, na Serikali itakuwa

macho kulinda maslahi yake.


Kwa upande wake mratibu
wa mradi huo Raymond Rwe-

Alisema moja ya
makubaliano waliyofikia
ni kuwa, uuzwaji wa madini hayo utakuwa unazingatia bei ya soko la dunia
jambo ambalo linaondoa
mjadala wa kujadili bei ya
kuuzia.

humbiza alisema kuwa, mkataba


ulioingiwa una maslahi na Shirika
halitapata hasara kutokana na
jinsi mradi huo utakavyoendeshwa, kutokana na kwamba, awali

tatizo la soko lilikuwa ni kikwazo


kikubwa cha mradi.
Rwehumbiza alieleza kuwa,
kuanzia kwa Shirika litaanza
kumuuzia mteja wao huyo mpya
jumla ya tani 40 za madini ya Bati
zilizopo Kayanga wilayani kyerwa
kwa kuzingatia makubaliano ya
mfumo wa bei ya dunia siku ya
kuuza.
Kuhusu bei ya kununulia
kutoka kwa wachimbaji wadogo
Rwehumbiza alisema wachimbaji
wadogo watanufaika kwanza na
uhakika wa kununuliwa madini
yao muda wote watakapoyapata
lakini pili ni ununuzi utakaozingatia hali ya bei ya soko la dunia
kwa kipindi husika. Kwa kuwa
STAMICO lengo letu ni kuboresha na kuinua hali na vipato vya
wachimbaji wadogo ni dhamira
ya Shirika kununua kwa bei
nzuri, aliongeza Rwehumbiza.

Vijiji, Halmashauri

washauriwa
kuomba leseni
madini
ya ujenzi

Na Greyson Mwase,
Dodoma

aziri wa Nishati na Madini George


Simbachawene
amesema kuwa
kwa leseni za uchimbaji wa madini
ya ujenzi ipaumbele kiwe kwa vijiji
na Halmashauri badala ya kumilikiwa na watu binafsi ili kuongeza
kipato kwa wananchi wa eneo
husika
Simbachawene aliyasema hayo
wilayani Kibakwe mkoani Dodoma
wakati wa ziara yake ya kukagua
miradi ya umeme vijijini inayosimamiwa na Wakala wa Nishati
Vijijini (REA) Awamu ya Pili kwa
kushirikiana na Shirika la Umeme
Nchini (TANESCO) pamoja na
kuzungumza na wananchi.
Alisema kuwa leseni za uchimbaji wa mchanga na mawe zinapomilikiwa na watu binafsi wenye
kuhodhi maeneo makubwa, kijiji
hukosa mapato yake stahiki.
Ndugu zangu napenda ifikie
mahali leseni za uchimbaji wa
mchanga na mawe zimilikiwe
na kijiji ili kuongeza pato la kijiji
badala ya kuwapa watu binafsi
ambao hunufaika zaidi, alisema
Simbachawene.
Akielezea mikakati ya kuwawezesha wachimbaji wadogo,
Simbachawene alisema kuwa
Serikali kupitia Wizara ya Nishati
na Madini imekuwa ikitoa ruzuku
kwa wachimbaji wadogo wenye
vigezo na kuwataka kuchangamkia
fursa hiyo kwa kuunda vikundi
vidogo vidogo na kuomba ruzuku.
Alitaja vigezo vinavyotumika
wakati wa kutoa ruzuku kuwa
ni pamoja na kuwa na leseni ya
uchimbaji madini na kuwa na eneo
lililofanyiwa utafiti.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Mhandisi


Edwin Ngonyani (kulia) akisaini moja ya mikataba ambayo STAMICO imewahi
kuingia na wadau mbalimbali. Kushoto ni Mwanasheria wa STAMICO,
Mudrikat Kiobya. (Picha na Maktaba)

George Simbachawene

NewsBulletin
Bulle

HABARI ZA NISHATI/MADINI

http://www.mem.go.tz

MEM

Tahariri
Na Badra Masoud

Kupatikana kwa
soko la madini ya
Bati, fursa muhimu
kwa wachimbaji
wadogo

abari kubwa katika jarida la leo ni kusainiwa kwa Mkataba


wa ununuzi wa madini ya Bati (Tin) baina ya kampuni ya
KYERWA TIN LTD ambayo ni kampuni tanzu ya Shirika
la Madini la Taifa (STAMICO) na DAR GOLD DMCC
LTD ya nchini Dubai.
Tumeelezwa kuwa huu ni moja ya mkataba wenye manufaa na
maslahi makubwa sio tu kwa STAMICO bali ni neema kwa wachimbaji wadogo wa madini ya bati nchini hasa katika wilaya ya Kyerwa,
mkoani Kagera ambapo madini hayo yanapatikana kwa wingi.
Akizungumza mara baada ya kutiliana saini mkataba huo ofisini
kwake jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Mhandisi Edwin Ngonyani, alisema kuwa, STAMICO imeingia mkataba huo kwa kuzingatia maslahi ya Taifa kwani
Wachimbaji wadogo wa madini ya Bati watanufaika kwa kupata soko
la uhakika na bei nzuri.
Ngonyani alisema kuwa STAMICO haikusudii kupata faida kubwa katika biashara hii kwa sababu lengo mahsusi la Shirika hilo ni
kuwasaidia wachimbaji wadogo wainuke na sio kupata faida.
Kusainiwa kwa mkataba kunathibitisha uhakika wa kuwepo kwa
soko la kuaminika la madini ya bati jambo ambalo kwa muda mrefu
lilikuwa ni changamoto kwa wachimbaji wa madini husika.
Jambo la kutia moyo ni kuwa pande hizo mbili zimekubaliana
kuwa uuzwaji wa madini hayo utakuwa unazingatia bei ya soko la dunia jambo ambalo linaondoa mijadala mirefu ya kujadili bei ya kuuzia.
Hii ni kusema kuwa suala la kuwadhulumu wachimbaji wa madini
haya sasa limefikia tamati.
Vilevile wachimbaji wetu sasa wana uhakika wa kuuza madini
hayo kwa kipindi chote bila kusimama kwa kuwa uhakika wa soko
upo, tofauti na awali ambapo tatizo la soko lilikuwa ni kikwazo.
Baada ya kusaini mkataba huo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa
STAMICO Mhandisi Edwin Ngonyani alitoa onyo kwa wanunuzi
haramu wanaotorosha madini hayo nje ya nchi bila kulipa kodi stahiki
wafunge virago warudi walikotoka maana kuanzia sasa hawatapata
nafasi ya kununua, na Serikali itakuwa macho kulinda maslahi yake.
Hili linawezekana kwa kuwa sasa wachimbaji wadogo wanajua wapi
pa kupeleka madini yao na si kuwauzia wafanyabashara haramu.
Ili kuonyesha kuwa suala hili si bla bla, Kwa kuanzia STAMICO
itaanza kumuuzia mteja wao huyo mpya jumla ya tani 40 za madini ya
Bati zilizopo katika eneo la Kayanga wilayani Kyerwa kwa kuzingatia
makubaliano ya mfumo wa bei ya dunia siku ya kuuza.
Heko STAMICO chini ya Kaimu Mkurugenzi, kwa kuwa
mnaonesha kwa vitendo jinsi mnavyoendelea kuwasimamia vyema
wachimbaji wetu wadogo nchini katika masuala mbalimbali ikiwemo
utoaji wa elimu kuhusu Sekta ya Madini na kuwatafutia masoko ya
madini yao.
Tunawatakia kila la heri STAMICO kwa kufungua njia kwa
wachimbaji wadogo ikiwemo hao wa Kyerwa na wengine ambao wanahitaji kuwezeshwa.

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage (wa sita kutoka kushoto, mstari wa mbele)
akiwa katika picha ya pamoja na Mameneja Tanesco wa mikoa na wilaya katika Nyanda za Juu
Kusini Magharibi pamoja na wakandarasi wanaotekeleza miradi ya REA ya usambazaji umeme
vijijini, Awamu ya pili katika kanda hiyo, mara baada ya kumaliza kikao kilicholenga kujadili
utekelezaji wa miradi husika. Kulia kwa Naibu Waziri ni Meneja Mwandamizi wa Tanesco Kanda
ya Nyanda za Juu Kusini Magharibi, Salome Nkondola na kushoto kwa Naibu Waziri ni Kaimu
Meneja wa Tanesco katika mkoa wa Mbeya, Magwila Mbalamwezi.

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage (wa pili kushoto) akiangalia nguzo
zinazotumika kusambaza umeme vijijini katika wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya kabla ya
kuzindua mradi wa umeme ambao umewezesha vijiji sita katika kata hiyo kuunganishwa na
huduma ya umeme. Vijiji hivyo ni Kapyo, Ilongo, Ilaji, Igalako, Mchongole na Igalako. Wengine
katika picha ni Kaimu Meneja wa Tanesco katika mkoa wa Mbeya, Magwila Mbalamwezi (kulia
kwa Naibu Waziri) na Afisa Miradi kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Emmanuel Yesaya
(kushoto kwa Naibu Waziri).
KWA HABARI PIGA SIMU
KITENGO CHA MAWASILIANO

TEL-2110490
FAX-2110389
MOB-0732999263
BODI YA UHARIRI
MHARIRI MKUU: Badra Masoud
MSANIFU: Essy Ogunde
WAANDISHI: Veronica Simba, Asteria Muhozya, Greyson
Mwase Teresia Mhagama, Mohamed Saif, Rhoda James
na Nuru Mwasampeta

FIVE
PILLARS OF
REFORMS
INCREASE EFFICIENCY
QUALITY DELIVERY
OF GOODS/SERVICE
SATISFACTION OF
THE CLIENT
SATISFACTION OF
BUSINESS PARTNERS
SATISFACTION OF
SHAREHOLDERS

HABARI ZA NISHATI/MADINI

NewsBulletin
Bulle
http://www.mem.go.tz

Tanzania
Kushirikiana na Japan Sekta ya Nishati
Na Veronica Simba, Dar es Salaam

izara ya Nishati
na Madini inapanga kushirikiana na Kampuni
ya Mitsubishi
Hitachi Power System ya Japan
katika kuendeleza Sekta ya Nishati
nchini.
Kamishna Msaidizi wa Umeme
wa Wizara, Mhandisi Innocent
Luoga aliyasema hayo hivi karibuni baada ya kukutana na uongozi
wa juu wa kampuni hiyo, Makao

Makuu ya Wizara jijini Dar es Salaam.


Mhandisi Luoga alisema katika
kikao hicho, Ujumbe wa kampuni
ya Mitsubishi Hitachi Power Systems Ltd uliwasilisha mapendekezo ya matumizi ya teknolojia ya
kisasa ya kufua umeme kutokana
na vyanzo mbalimbali ikiwemo
makaa ya mawe, Jotoardhi na Gesi.
Sisi kama Serikali, kupitia
taasisi zetu tumeona ni vema tushirikiane na Kampuni hii ambayo
inajishughulisha na kutengeneza
mitambo ya kufua umeme wa
Gesi, Makaa ya Mawe na Jotoardhi
kwa kutumia teknojia ya kisasa.
Hii ni kutokana na vyanzo vipya

vya umeme tulivyonavyo hususan


makaa ya mawe na jotoardhi, ambavyo hatujaanza rasmi kuvitumia
kuzalisha umeme, alisema Kamishna Luoga.
Aliongeza kuwa, lengo la Serikali ni kuhakikisha umeme wa kutosha, wa uhakika na wa bei nafuu
unazalishwa na kusambazwa nchini ili kuwaletea wananchi maendeleo na hivyo kuinua pato la Taifa
kwa ujumla.
Alisema kuwa, Kampuni hiyo
ilishafanya majadiliano kuhusu
ushirikiano katika Sekta ya Nishati
na taasisi zilizo chini ya Wizara ambazo ni Shirika la Umeme Tanzania
(Tanesco), Shirika la Maendeleo ya

Petroli Tanzania (TPDC), Kampuni


ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania
(TGDC) pamoja na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO).
Akizungumzia kuhusu faida
za matumizi ya teknolojia hiyo ya
kisasa inayotumika kufua umeme,
Kamishna Luoga alizitaja kuwa ni
pamoja na kuwa rafiki wa mazingira, kuwezesha uhakika wa kufua
umeme kwa bei nafuu pamoja na
kufua umeme kwa ufanisi mkubwa.
Awali, katika kikao hicho baina
ya Wizara na Kampuni hiyo, Rais
wa Kampuni, Takato Nishizawa
alisema kampuni yake iko tayari
kutoa mafunzo ya namna ya ku-

tumia mitambo yao inayotumia


teknolojia hiyo ya kisasa kwa Wahandisi wa kitanzania.
Aidha, Nishizawa alitoa mwaliko kwa wataalamu hao kutoka
Tanzania, kutembelea mitambo
hiyo nchini Japan kwa lengo la kujifunza zaidi.
Katika hatua nyingine, ilielezwa kuwa Kampuni ya Mitsubishi
Hitachi Power System Ltd, tayari
imeingia mkataba na Kampuni
ya Sumitomo ambayo inatekeleza
Mradi wa Kufua Umeme wa gesi
wa Kinyerezi II unaofikia kiasi cha
Megawati 240, kwa kazi ya kufunga
mitambo ya kufua umeme (gas
turbines) aina ya Hitachi.

01
03
1
2

02

Makamu Rais wa Kampuni ya Mitsubishi Hitachi Power System Ltd,


Satoshi Uchida (Kulia), akifafanua jambo kwa Wataalamu wa Wizara
ya Nishati na Madini, wakati wa kikao baina yao kilichojadili ushirikiano katika sekta ya nishati. Kikao kilifanyika Mei 12, 2015 Makao
Makuu ya Wizara jijini Dar es Salaam.
Makamu Rais wa Kampuni ya Mitsubishi Hitachi Power System Ltd,
Satoshi Uchida (Kulia), akifafanua jambo kwa Wataalamu wa Wizara
ya Nishati na Madini, wakati wa kikao baina yao kilichojadili ushirikiano katika sekta ya nishati. Kikao kilifanyika Mei 12, 2015 Makao
Makuu ya Wizara jijini Dar es Salaam.
Rais wa Kampuni ya Mitsubishi Hitachi Power System Ltd, Takato Nishizawa (Kushoto) na Kamishna Msaidizi wa Umeme wa Wizara ya
Nishati na Madini, Mhandisi Innocent Luoga (Kulia) (Walioshikana
mikono), wakiwa katika picha ya pamoja na Maofisa kutoka Kampuni
hiyo na Wataalamu wa Wizara, mara baada ya kikao baina yao kilichojadili ushirikiano katika sekta ya nishati nchini. Kikao kilifanyika Mei
12, 2015 Makao Makuu ya Wizara, jijini Dar es Salaam.

NewsBulletin
Bulle
http://www.mem.go.tz

HABARI ZA NISHATI/MADINI

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI GEORGE SIMBACHAWENE KATIKA


ZIARA YA UKAGUZI WA MIRADI YA UMEME YA REA MKOA WA DODOMA

Baadhi ya watendaji kutoka Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) na Kamishna Msaidizi


wa Madini Kanda ya Kati, Sosthenes Masolla (wa nne kutoka kulia) wakifuatilia hotuba
iliyokuwa inatolewa na Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (hayupo
pichani) katika kijiji cha Chinyanghuku wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma.

Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (kulia) akisalimiana na Diwani wa


Kata ya Mulunduzi Hitler Chambilu (kushoto) mara baada ya kuwasili katika kata hiyo
iliyopo katika wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma.

Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (kulia chini) akiangalia mafundi


kutoka Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) waliokuwa wakiendelea na kazi ya ujenzi
wa miundombinu ya umeme katika Kata ya Mulunduzi wilayani Mpwapwa mkoani
Dodoma.

Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (kushoto) akikabidhi mfano wa


zawadi ya jezi kwa mmoja wa wasanii wa kikundi cha sanaa kijulikanacho kama Neema
Group, Ackley Mwaluka katika kijiji cha Chaludewa kilichopo wilayani Mpwapwa mkoani
Dodoma.

Sehemu ya wakazi wa Kata ya Mulunduzi wakifuatilia kwa makini hotuba iliyokuwa


inatolewa na Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (hayupo pichani)

Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (kushoto) akikabidhi zawadi ya


jezi na mpira wa miguu kwa mmoja wa wanamichezo wa timu ya mpira wa miguu ya
Chaludewa wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma.

HABARI ZA NISHATI/MADINI

Tanesco yaagizwa
kutoa vibali kwa
mafundi umeme

Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (kushoto) akitoa maelekezo kwa Afisa Uhusiano - Huduma kwa
Wateja wa Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) mkoa wa Dodoma, Innocent Lupenza (kulia) mara baada ya kuwasili
katika wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma kwa ajili ya kukagua miradi ya umeme vijijini. Waziri Simbachawene
aliyekuwa mkoani Dodoma kwa ajili ya kukagua miradi ya umeme inayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA)
Awamu ya Pili na Tanesco pamoja na kuzungumza na wananchi. Katikati ni Katibu wa Waziri Simbachawene Mhandisi
Joseph Kumburu.

Na Greyson Mwase, Dodoma

aziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene ameliagiza Shirika la Umeme


Nchini (Tanesco) kutoa mafunzo pamoja
na vibali kwa mafundi umeme nchini kote
watakaofanya kazi ya kuweka mifumo ya umeme kwenye
nyumba kabla ya kuunganishwa kwenye miundombinu
ya umeme inayojengwa na Wakala wa Nishati Vijijini
(REA) kwa kushirikiana na Tanesco.
Simbachawene alitoa agizo hilo katika ziara yake aliyoifanya katika wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma ya
kukagua miradi ya umeme vijijini ili kujionea maendeleo
yake, pamoja na kuzungumza na wananchi. Miradi hiyo
iliyopo chini ya Awamu ya Pili ya REA inatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Juni mwaka huu.
Alisema katika kujiandaa na huduma ya umeme, wananchi wanatakiwa kuwekewa mifumo ya umeme (wiring) katika nyumba zao na wataalamu waliothibitishwa na
Tanesco na kupewa leseni pamoja na mafunzo ili kuondokana na majanga ya moto yanayosababishwa na ufungaji
holela wa mifumo ya umeme.
Alieleza kuwa katika utekelezaji wa miradi ya REA
kumekuwepo na mafundi wasiotambulika na Tanesco
wanaojulikana kama vishoka ambao wamekuwa wakijitokeza kwenye makazi ya watu na kudai kuwa ni mafundi kutoka Tanesco na kuwawekea mifumo mibovu ya
umeme hali inayopelekea hasara kubwa ya kuunguliwa na
nyumba baadaye.
Alisisitiza kuwa ili kukabiliana na mafundi ambao
ni vishoka Tanesco inatakiwa kuchagua makampuni na
mafundi binafsi ambao ni wataalamu wenye leseni na kutambuliwa na shirika hilo na kuwapa mafunzo kabla ya
kuanza zoezi la kuweka mifumo ya umeme kwenye nyumba za wananchi wanaotarajiwa kufungiwa umeme chini
ya mradi wa REA awamu ya pili.
Aliongeza kuwa mara baada ya mafundi hao kupatiwa
mafunzo na Tanesco, watapewa barua maalum za utambulisho au hati maalum zitakazotumika wakati wa uendeshaji wa zoezi hilo
Simbachawene alisema kuwa hatua hiyo inatokana
na mikakati ya serikali katika kuwapunguzia wananchi
gharama na muda wa kufuatilia huduma za kufungiwa
mifumo ya umeme katika nyumba zao mijini.

NewsBulletin
Bulle
Wananchi epukeni
matapeli wa madini
http://www.mem.go.tz

Aliendelea kusema kuwa mbali na kuwapunguzia wananchi gharama na muda wa ufuatiliaji wa kufungiwa mifumo ya umeme katika nyumba zao, mpango huo utaleta
ushindani wa gharama kati ya makampuni na mafundi
binafsi wenye leseni zinazotambuliwa na Tanesco.
Akielezea hali ya uunganishaji wa umeme nchini
Simbachawene alisema mwaka 2005 wakati Serikali ya
Awamu ya Nne inaingia madarakani, ni asilimia 10 tu ya
wananchi walikuwa na umeme lakini hadi kufikia mwaka
2015, asilimia 36 ya wananchi wana umeme na kusisitiza
kuwa mara baada ya miaka mitano asilimia ya wananchi
wenye umeme itakuwa ni 45 na kuifanya Tanzania kuwa
nchi inayoongoza Kusini mwa Jangwa la Sahara kwa kuwaunganishia umeme wananchi waishio vijijini.
Hii ni hatua kubwa ambayo tumepiga kama Serikali
na bado tutaendelea kuhakikisha kuwa wananchi wote
hasa waishio vijijini wanapata umeme wa uhakika ingawa tutafanya kwa awamu tofauti tofauti, alisema Simbachawene.
Simbachawene alifafanua kuwa ingawa sio rahisi kuweka umeme katika vijiji vyote kwa pamoja nchi nzima,
miradi ya REA itatekelezwa kwa awamu tofauti tofauti.
Simbachawene aliwataka wananchi kushirikiana na
Tanesco pamoja na REA katika utekelezaji wa miradi ya
ujenzi wa miundombinu ya umeme kwa kutoa sehemu
ndogo ya mashamba yao ili ziweze kuwekwa nguzo za
umeme ili waanze kunufaika na umeme huo mara moja.
Wakati huo huo Afisa Uhusiano - Huduma kwa Wateja wa Tanesco mkoa wa Dodoma Innocent Lupenza alisema kuwa kwa wananchi wenye nyumba zenye vyumba
viwili hawatahitaji kufungiwa mifumo ya umeme, badala
yake watawekewa kifaa maalumu kujulikanacho kwa jina
la UMETA yaani Umeme Tayari.
Akielezea kifaa hicho, Lupenza alisema kuwa kifaa hicho kitamwezesha mtumiaji kuwasha taa mbili pamoja na
matumizi mengine madogo kama pasi na kuongeza kuwa
kifaa hicho kitauzwa kwa shilingi 42, 480
Akielezea taratibu za kufungiwa umeme kwenye nyumba Lupenza alisema wananchi waliopo umbali wa
mita 30 toka ilipo miundombinu ya umeme watalipia
shilingi 27,000.
Alisema katika hatua za awali wananchi watatakiwa
kulipia fomu kwa shilingi 5900 na baada ya hapo mkandarasi atafanya ukaguzi wa mifumo ya umeme iliyowekwa katika nyumba husika kabla ya kuiunganisha nyumba hiyo
na miundombinu ya umeme.

Na Greyson Mwase, Dodoma

ananchi wametakiwa kuepuka matapeli


katika biashara ya madini kwa kuwasilisha mawe wanayohisi kuwa yana madini
kwenye ofisi za madini ili kuweza kubaini
thamani yake.
Wito huo ulitolewa na Kamishna Msaidizi wa Madini
Kanda ya Kati, Sosttenes Masolla wakati wa ziara ya Waziri
wa Nishati na Madini George Simbachawene aliyoifanya katika mkoa wa Dodoma kwa ajili ya kukagua miradi ya umeme
inayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) pamoja
na kuzungumza na wananchi.
Akitoa ufafanuzi katika moja ya mikutano hiyo, Masolla
alisema kuwa imekuwa ni kawaida ya wananchi, kupeleka
mawe wanayohisi kuwa yana madini kwa watu wasio wataalam wa madini ambao ni matapeli na hivyo kupata hasara
kubwa.
Akieleza hatua za kufuata baada ya kupata mawe wanayohisi kuwa yana madini, Masolla alisema kuwa mwananchi
anapoona jiwe hilo anatakiwa kufika nalo katika ofisi za
madini na kukabidhi kwa wataalam wa madini ambalo watakagua jiwe hilo ili kubaini aina na kiwango cha madini kilichopo.
Alisema mara baada ya kubainika kwa kiwango cha madini katika jiwe, wataalam wa madini watampatia mwananchi
fomu ya maombi ya leseni ya uchimbaji madini baada ya
kubaini eneo kama liko wazi.
Baada ya kufanikiwa kupata leseni, mwananchi atakuwa
huru kufanya shughuli za uchimbaji wa madini na kulipa kodi
kama mchimbaji mwingine yeyote, alisema Masolla.
Masolla aliongeza kuwa ofisi pia inaweza kusaidia kumuunganisha mchimbaji wa madini na wanunuzi wa madini
wenye leseni kupitia Wizara ya Nishati na Madini.
Masolla alisema kuwa mara nyingi wananchi wanapowapatia matapeli mawe wanayohisi kuwa yana madini, matapeli hao huchukua mawe yao na kuwazunguka kwa kuomba
leseni na kumilikishwa maeneo bila ya wao kuwa na taarifa
hali inayopelekea kuwepo kwa migogoro.

Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kati, Sosthenes Masolla akitoa


ufafanuzi wa jinsi ya kupata leseni za madini mbele ya wananchi wa
kijiji cha Ikuyu huko Kibakwe mkoani Dodoma.

NewsBulletin
Bulle

HABARI ZA NISHATI/MADINI

http://www.mem.go.tz

http://www.mem.go.tz

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI, CHARLES MWIJAGE KANDA YA KUSINI

ZIARA YA MWIJAGE

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage (mwenye shati


la mistari) akiangalia jinsi wateja wanavyohudumiwa katika ofisi za
Tanesco, Makambako, mkoani Njombe. Naibu Waziri alitembelea
ofisi hizo akiwa katika ziara ya kukagua miradi ya umeme
inayotekelezwa katika Kanda ya Kusini pamoja na kuzindua kituo
cha kufua umeme mkoani Ruvuma.

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage (kushoto)


akizungumza na wananchi katika katika kijiji cha Lilondo, wilaya ya
Songea Vijijini, mkoani Ruvuma, mara baada ya kuzindua mradi wa
umeme wa kiasi cha kilowati 40 uliobuniwa na wananchi hao ambao
umeshanufaisha nyumba 100.

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage (mwenye suti ya kaki)


akilakiwa na wananchi katika kijiji cha Kanga wilayani Chunya wakati alipofika
kijijini hapo ili kukagua utekelezaji wa miradi ya usambazaji umeme vijijini
Awamu ya Pili inayotekelezwa na TANESCO kwa kushirikiana na REA.

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage (wa tatu kutoka kushoto)
akiangalia nyaya zinazotumika kusambaza umeme mkubwa wa 33/11KV na
umeme mdogo wa 400/230V katika wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya kabla ya
kuzindua mradi wa umeme ambao umewezesha vijiji sita vya Kapyo, Ilongo, Ilaji,
Igalako, Mchongole na Igalako kuunganishwa na huduma ya umeme.

. Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro (wa pili kushoto) akimwonyesha


Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage (wa kwanza kushoto, ramani ya
mkoa wa Mbeya ambayo pia inaonyesha kilipo chanzo cha jotoardhi mkoani humo
ambacho kikiendelezwa kitazalisha nishati ya umeme. Naibu Waziri alifika katika
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kabla kufanya kikao na Mameneja Tanesco wa
mikoa na wilaya katika Nyanda za Juu Kusini Magharibi pamoja na wakandarasi
wanaotekeleza miradi ya REA ya usambazaji umeme vijijini, Awamu ya pili katika
kanda hiyo

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage (wa tatu


kulia) pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu
na Bunge, Jenista Mhagama (katikati) ambaye pia ni Mbunge wa
jimbo la Peramiho, wakifunua kitambaa kuashiria uzinduzi wa
mradi wa umeme wa kiasi cha kilowati 40 uliobuniwa na wananchi
katika kijiji cha Lilondo, wilaya ya Songea Vijijini, mkoani Ruvuma.

HABARI ZA NISHATI/MADINI

NewsBulletin
Bulle
http://www.mem.go.tz

TANESCO
Sogezeni huduma vijijini Simbachawene
Na Greyson Mwase, Dodoma

aziri wa Nishati na
Madini, George Simbachawene amelitaka
Shirika la Umeme
Nchini (TANESCO) kusogeza
huduma ya kuwaunganishia
umeme wananchi vijijini badala
ya wananchi kufunga safari mjini kwa ajili ya kufuata huduma ya
kuunganishiwa umeme kwenye
nyumba zao.
Simbachawene alitoa agizo
hilo akiwa Kibakwe mkoani Dodoma alipokuwa katika ziara ya
ukaguzi wa miradi ya umeme vijijini inayotekelezwa na Wakala
wa Nishati Vijijini (REA) Awamu
ya Pili kwa kushirikiana na Shirika la Umeme Nchini (TANESCO)
pamoja na kuzungumza na wa-

nanchi ili kutatua kero zao.


Alisema ili kuwarahisishia
wananchi maombi ya kuunganishiwa umeme, ni vyema Tanesco
ikapanga siku maalum na kwenda
katika kijiji husika na kuwasaidia
wananchi kujaza fomu, pamoja
na kulipia badala ya wananchi
kufunga safari hadi mjini kufuata
fomu, kujaza na kuzirejesha.
Mfano fomu ya maombi ya
kuunganishiwa umeme ni shilingi
5,900 sasa mwananchi anapotumia zaidi ya shilingi 20,000 kama
gharama ya nauli kwenda kufuata
fomu halafu ajaze na kurudisha
inakuwa ni kazi nzito yenye gharama kubwa na kupoteza muda wa
mwombaji, hii inapelekea zoezi
kusuasua, hivyo basi wanachi
wasogezewe huduma karibu, alisisitiza Simbachawene.

Alisema kwa kutambua


umuhimu wa umeme katika ukuaji wa uchumi wa nchi, serikali
imekuwa ikiweka mikakati mbalimbali ya kusambaza umeme hususan maeneo ya vijijini pamoja
na kuwakaribisha wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi.
Vilevile alitoa angalizo kuwa,
wananchi
wanatakiwa
kuchangamkia fursa zinazowekwa
na serikali kwa kujipatia kipato na
hivyo kuwa na maisha bora badala ya kulalamika. Aliendelea kusema kuwa ile kauli ya Maisha bora
kwa kila mtanzania haikumaanisha serikali kumfanyia mwananchi kila kitu bali mkakati wa
serikali ni kuwawezesha wananchi
kwa kuwapa fursa za kiuchumi
ikiwa ni pamoja na umeme.

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA NISHATI NA MADINI


TANZANIA GEMOLOGICAL CENTRE
MAOMBI YA UDAHILI NGAZI YA CHETI KWA MWAKA WA MASOMO 2015/2016
Kituo cha Tanzania Gemological Centre(TGC) kinakaribisha maombi ya kujiunga ngazi ya
cheti kwa kozi zifuatazo, zitakazoanza 15 Juni 2015
1.Ukataji na usanifu wa madini ya vito (Lapidary)
2.Uchongaji wa Vinyago vya Mawe (Stone Carving)
Muda wa kozi ni miezi sita (6)
SIFA ZA MUOMBAJI
Muombaji anatakiwa awe amehitimu kidato cha nne na kufaulu kwa kiwango cha daraja D
katika masomo ya Kiingereza na Hisabati na masomo mawili kati ya masomo yafuatayo;
Kemia, Fizikia, Jiografia, Biashara, Bookkeeping, na Accounts au Uchumi
JINSI YA KUOMBA
Fomu za maombi zinapatikana kituoni (TGC), ofisi za madini kanda na ofisi za maafisa madini wakazi nchi nzima. Ada ya maombi kiasi cha shilingi 10,000/= ilipwe kupitia
benki: National Microfinance Bank (NMB), Jina la Akaunti: Tanzania Gemological Centre, Namba ya Akaunti: 40801000074. Fomu ya kuweka fedha benki iwasilishwe kituoni
kama ushahidi wa malipo. Kituo hakipokei fedha taslimu. Mwisho wa kupokea maombi ni
22/05/2015
Maombi yatapokelewa na kufanyiwa kazi yakiwa na fomu ya kuweka fedha benki, maelezo
binafsi ya muombaji yaliojitosheleza na historia ya elimu yake pamoja na vivuli vya vyeti
vya elimu ya kidato cha nne na cheti /ushahidi unaodhibitisha sifa za muombaji pamoja
na cheti cha kuzaliwa.
Maombi yaambatanishwe na vivuli vya vyeti vya elimu yatumwe kwa;
Mratibu,
Tanzania Gemological Centre,
P. O. Box 119, ARUSHA.

Kwa wadau wa sekta za Nishati na Madini, tembelea kurasa mpya za Wizara kwenye Mitandao
ya Kijamii ya Twitter na Facebook kwa anuani ya Nishati na Madini Karibu tuhabarishane na
tujadili kuhusu sekta za Nishati na Madini kwa maendeleo ya Watanzania wote.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

You might also like