You are on page 1of 2

TGNP MTANDAO

P.O. Box 8921, Dar es Salaam, TANZANIA; Gender Resource Centre, Mabibo Road
Tel. 255 22 2443450/ 2443205/ 2443286: Mobile 255 0754 704050/0785 784050/0715784050:
Fax 255 22 2443244; Email: info@tgnp.org web www.tgnp.org

TAMKO KWA VYOMBO VYA HABARI


UTEUZI WA BARAZA LA MAWAZIRI UZINGATIE USAWA WA KIJINSIA
TGNP Mtandao, Action Aid Tanzania, FemAct

pamoja na wanaharakati ngazi ya jamii tumekuwa

tukifuatilia kwa ukaribu mchakato mzima wa uchaguzi kuanzia hatua za awali, upigaji kura na baada ya
matokeo kutangazwa. Nia yetu ni kufuatilia na kudai ushiriki kamilifu wa wanawake kwenye mchakato
mzima kama wagombea na wapiga kura.
Tunawapongeza Wanawake wote walioshiriki kwa kujitokeza kujindikisha kwenye daftari la kudumu la
wapiga kura, waliojitokeza kupiga kura na zaidi kabisa Wanawake wote waliogombea nafasi mbalimbali za
uongozi bila kuvisahau vyama vya siasa na jamii zotezilizowawaunga mkono na kufanikisha ushindi.
Tunawapongeza wanawake wote waliothubutu kujitokeza katika kinyanganyiro za uchaguzi kuanzia ngazi ya
uteuzi ndani ya vyama na hatimaye baadhi yao kuingia kama wagombea. Kipekee tunampongeza Makamu
wa Rais Mama Samia Suluhu kwa kudhubutu na kufanikiwa kuwa makamu wa kwanza wa Rais Mwanamke
tangu taifa letu kupata uhuru. Pamoja na hayo tunampongeza aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya chama
cha ACT wazalendo Anna Mghwira kwa kuwa mgombea pekee mwanamke wa nafasi ya Urais kwa
udhubutu na ujasiri aliouonesha. Tunatambua na kuthamini jitihada zake sio kugombea kwake tu, bali hata
jinsi alivyobeba ajenda za msingi za wanawake na wananchi wa kawaida wakati wa kampeni.
Ndugu waandishi wa habari, takwimu zinaonesha kuwa, idadi ya wanawake mawaziri iliongezeka kutoka
14.8% (2003/05) kufikia 31.25% (2013/15) wakati idadi ya manaibu waziri wanawake ikipungua kutoka
30% (2003/05) hadi 24% (2013/15). Aidha, idadi ya makatibu wakuu wa wizara wanawake ilipungua kutoka
28% (2003/05) hadi 18.2% (2013/15) wakati idadi ya manaibu katibu wakuu wa wizara wanawake
ikiongezeka kutoka 12.5%(2003/05) hadi 40.7% (2013/15).
Tanzania ni moja kati ya Mataifa yaliyosaini mikataba mbalimbali ya Kimataifa na kikanda inayoweka
misingi ya usawa kwa binadamu ikiwemo haki na usawa katika ushiriki kwenye uongozi wa ngazi zote.
Moja kati ya Mikataba hiyo ni Tamko la Umoja wa Matifa la Haki za Binadamu(UDHR:1948), Mkataba wa
Kimataifa wa Kutokomeza aina zote za Ubaguzi dhidi ya Wanawake (CEDAW: 1979, Articles 7: a, b na c),
Mpango Kazi wa Beijing (1995), Mkataba wa Ziada wa Maputo, na Mkataba wa Nyongeza wa jinsia na
Maendeleo kusini mwa Africa (SADC Gender Protocol,) ambayo inaelekeza serikali husika kuhakikisha
wanawake wanapewa nafasi sawa na wanaume katika ngazi mbalimbali za uongozi.
Idadi ya wabunge wa kuteuliwa iliongezeka kutoka 20% (2003/05) hadi 40% (2013/15); Idadi ya wakurugenzi na manaibu wakurugenzi wa wizara
iliendelea kuongezeka kutoka 26% na 25% (2003/05) hadi kufikia 30.9% na 37% (2013/15). Idadi ya wanawake makamishna na manaibu kamishna
kufikia agusti 2015 ilikuwa ni 26.3% na 40%; Wakati makatibu tawala wa mikoa na wilaya wanawake waliongezeka kufikia 40% (2013/15) kutoka
19% na 21.1% (2003/05). Wanawake wakuu wa mikoa waliongezeka kutoka 10% (2003/05) hadi kufikia 24% (2013/15). Mabalozi wanawake
wameongezeka kutoka 5.6% (2003/05) hadi 25%(2013/15) kadhalika majaji wanawake 34% (2003/05) hadi 35.8% (2013/15). Licha ya hayo, ni
dhahiri kuwa, nchi yetu bado haijafikia lengo la ushiriki wa Wanawake 50/50 kwenye nafasi zote za uongozi.

Hivyo basi tunategemea kulingana na ahadi za viongozi wetu wakati wanaomba kura kuwa watasimamia
utekelezaji wa mikataba mbalimbali ya kikanda na kimataifa, ni matarajio yetu kuwa serikali mpya chini ya
Mhe. Rais John Magufuli itatekeleza kwa vitendo ahadi hizo hususan katika kuwateua Wanawake zaidi
katika nafasi za juu za uongozi katika mihimili mikuu mikuu mitatu ya serikali (Mahakama, baraza la
mawaziri na bunge).
Pia ikumbukwe kuwa, Mhe. Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akiwa katika Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa
viongozi wa nchi wanachama uliofanyika mwaka huu 2015 nchini Marekani aliahidi kuwa Tanzania
itasimamia utekelezaji wa kanuni ya 50/50 na kuweka mifumo mizuri ya ufuatiliaji na uwajibikaji wa
utekelezaji wa masuala yote ya usawa wa kijinsia na matamko ya kimataifa na kikanda katika ngazi ya taifa
na jamii.
Kwa kuzingatia hayo, tunasisitiza kuwa Baraza la Mawaziri lijalo pamoja na nafasi zote za uteuzi serikalini
zibebe sura ya usawa wa Kijinsia. Nafasi nyinginezo ni pamoja na uteuzi wa wakuu wa mikoa, wakuu wa
wilaya, makatibu wakuu na naibu makatibu wakuu wa wizara mbalimbali, wakurugenzi na wakuu wa taasisi
na mashirika ya umma kadhalika uteuzi wa bodi mbalimbali katika mashirika na taasisi hizo bila kusahau
uteuzi katika mihimili ya mahakama na bunge. Ni matarajio yetu kuwa, mamlaka za kiuteuzi ikiwa ni
pamoja na Rais, Waziri Mkuu na Mawaziri wa wizara mbalimbali watazingatia kikamilifu usawa wa kijinsia
katika uteuzi wowote watakaofanya. TGNP Mtandao na Action Aid tutahakikisha kuwa tunafuatilia kwa
karibu teuzi zitakazofanyika.
Mwisho tunawataka Wanawake wote waliochaguliwa kwenye nafasi za uongozi Ubunge na udiwani
kuwajibika kikamilifu kwa kuitumikia Jamii iliyowapa ridhaa, waoneshe mfano wa kuigwa kwa kujenga
hoja za msingi zenye maslahi mapana kwa Jamii hasa Wanawake wanapokuwa kwenye Bunge au vikao vya
Halmashauri ili kuleta tija na mabadiliko chanya kwa Jamii. Tunarajia kama ilivyokuwa katika awamu
zilizopita sisi asasi za kiraia tutaendelea kushirikiana na serikali iliyoingia madarakani katika kuleta
maendeleo ya Taifa.
Imesainiwa na:

Grace Kisetu
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji
TGNP Mtandao

Idadi ya wabunge wa kuteuliwa iliongezeka kutoka 20% (2003/05) hadi 40% (2013/15); Idadi ya wakurugenzi na manaibu wakurugenzi wa wizara
iliendelea kuongezeka kutoka 26% na 25% (2003/05) hadi kufikia 30.9% na 37% (2013/15). Idadi ya wanawake makamishna na manaibu kamishna
kufikia agusti 2015 ilikuwa ni 26.3% na 40%; Wakati makatibu tawala wa mikoa na wilaya wanawake waliongezeka kufikia 40% (2013/15) kutoka
19% na 21.1% (2003/05). Wanawake wakuu wa mikoa waliongezeka kutoka 10% (2003/05) hadi kufikia 24% (2013/15). Mabalozi wanawake
wameongezeka kutoka 5.6% (2003/05) hadi 25%(2013/15) kadhalika majaji wanawake 34% (2003/05) hadi 35.8% (2013/15). Licha ya hayo, ni
dhahiri kuwa, nchi yetu bado haijafikia lengo la ushiriki wa Wanawake 50/50 kwenye nafasi zote za uongozi.

You might also like