You are on page 1of 10

MAELEZO YA NDUGU JANUARY MAKAMBA (MB) WAZIRI WA

NCHI OFISI YA MAKAMU WA RAIS KATIKA MKUTANO NA


JUKWAA LA WAHARIRI KUHUSU ZIARA YA MAZINGIRA
KATIKA MIKOA KUMI 1 DISEMBA 2016
Kama mtakumbuka, nilifanya ziara ya siku 16 mfululizo katika
mikoa 10. Niliamua kufanya ziara hiyo ndefu ili kubainisha kwa
umma hali mbaya ya uharibifu wa mazingira nchini na
changamoto za hifadhi, utunzaji na usimamizi wa mazingira
nchini. Baadhi ya changamoto tulizishughulikia huko huko kwenye
ziara, na nyinginezo zilihitaji mashauriano baina ya Wizara na
taasisi na hatua za muda mrefu ndani ya Serikali.
Masuala ya mazingira ya umuhimu mkubwa sana kwa ustawi wa
nchi yetu. Hakuna sekta isiyotegemea mazingira iwe kilimo,
uvuvi, ufugaji, utalii, nishati, viwanda, usafirishaji, afya na
nyinginezo. Malengo ya maendeleo ya nchi yetu, hayawezi
kutumia bila kuweka masuala ya hifadhi ya mazingira sawa.
Tasnia ya habari ni muhimu katika kuamua ni suala gani nchi yetu
inalipa kipaumbele. Nimewaita leo kuwaomba tusaidieni na
kushirikiane kuifanya nchi yetu, jamii yetu na watu wetu wayape
kipaumbele masuala ya hifadhi ya mazingira.
Katika mazungumzo yangu ya siku ya leo, nitatumia ziara yangu
kuainisha changamoto za mazingira nchini, hatua tunazochukua
kukabiliana nazo, na mipango na mikakati ya Ofisi ya Makamu wa
Rais kuhusu suala hili kwa miaka mitano ijayo.
Madhumuni ya ziara hiyo yalikuwa ni kama ifuatavyo:1. Kuona hali ilivyo kwasasa ya mazingira, changamoto zake,
uharibifu uliotokea na unaoendelea kutokea katika maeneo
mbalimbali ya mikoa niliyoitembelea;
2. Kutambua na kusisitiza uundaji wa Kamati za Usimamizi wa
Mazingira katika ngazi na vitengo vyote vya Serikali, kama
Sheria ya Mazingira inavyoelekeza;
3. Kukagua hali ya vyanzo vya maji na vyanzo vya mito mikuu
nchini, kubaini changamoto zinazokabili rasilimali maji,
utekelezwaji wa sheria na kanuni za matumizi bora ya
rasilimali maji, utunzaji na jitihada za kukabiliana na
uharibifu wa mazingira katika vyanzo vya maji;
4. Kutambua harakati na juhudi zilizopo za uelimishaji,
uhamasishaji na umuhimu wa upandaji na utunzaji miti;
5. Kujua hatua zilizopo na jitihada zinazochukuliwa kukabiliana
na tatizo la ukataji miti bila vibali, uchomaji moto hovyo,
uvamizi wa maeneo ya hifadhi za vijiji kwa shughuli za
1

kilimo na ufugaji ambao ni holela usiozingatia taratibu,


sheria na kanuni za matumizi bora ya rasilimali ardhi;
6. Kubaini changamoto mbalimbali zinazohusiana na uharibifu
wa mazingira katika maeneo yaliyo na shughuli za uchimbaji
mdogomdogo wa madini;
7. Kusikiliza
na
kutatua
changamoto
za
mazingira
zinazowakabili wananchi na kuathiri jitihada zao za
kujiondelea umaskini, pamoja na kuwezesha jitihada
wanazozichukua katika harakati za utunzaji, uhifadhi na
usimamizi wa mazingira katika maeneo yao; na
8. Kutoa elimu, ushawishi, maelekezo na maamuzi katika
jitihada za kulinda mazingira.
Maeneo niliyotembelea ni haya yafuatayo:-

Na.

Mkoa

1. Morogoro

Wilaya

Eneo

Morogoro

a. Manispaa ya
Morogoro
b. Mto Morogoro
(Mambogo)
c. Bwawa la
Mindu
d. Mto Mzinga

Kilosa

Kilombero

2. Iringa

Kilolo

a. Mto Mkondoa
b. Kijiji cha
Mbwade
c. Kijiji cha
Twatwatwa
a. Kijiji cha
Katurukila
b. Mto Lumemo
c. Bonde la
Lower Kihansi
a. Kijiji cha
Mwatasi na
Lukosi
b. Vyanzo vya
Maji Mwatasi
c. Shamba la
Miti Lukosi
a. Kituo cha
Maji

Iringa
2

Manispaa
b. Shule ya
Msingi
Mlandege
c. Mto Ruaha
Mkuu
3. Mbeya

Mbarali

a. Kijiji cha
Madibira
b. Mashamba ya
Mpunga
Mbarali
a. Jiji la Mbeya
b. Safu za
Milima ya
Mbeya
c. Kituo cha
Kusambaza
Maji Mbeya
Mjini

Mbeya

4. Njombe

Wangingombe
Makete

Njombe
5. Songwe

Ileje

6. Rukwa

Sumbawanga
Manispaa
Sumbawanga
Vijijini
Kalambo

Nkasi
3

a. Kijiji cha Ijima


b. Kijiji cha
Mdandu
a. Kijiji cha
Ikuwo
b. Makete Mjini
c. Hifadhi ya
Kitulo
a. Njombe Mjini
b. Bwawa la
Maji Njombe
c. Ileje Mjini
d. Kijiji cha
Lubanda
a. Manispaa
Sumbawang
b. Bonde Oevu
la Lwiche
a. Ziwa Rukwa
a. Kijiji cha
Samazi
b. Kijiji cha
Ilimba
a. Namanyere
(Msitu wa

Mfili)
b. Mradi wa Maji
wa
Namanyere
7. Katavi

Mpanda
Tanganyika

8. Kigoma

Kigoma

Uvinza
Kasulu

9. Tabora

Kaliua

a. Manispaa ya
Mpanda
a. Kijiji cha
Kabage
b. Kijiji cha
Bugwe
c. Kijiji cha
Mwese
a. Bonde la Mto
Katuma
b. Hifadhi ya
Taifa ya
Katavi
a. Hifadhi ya
Taifa ya
Gombe
b. Vijiji vya
Mwambao wa
Ziwa
Tanganyika
(Mtanga)
c. Taasisi ya
Jane Goodal
a. Shamba la
Chumvi la
Uvinza
a. Kambi ya
Wakimbizi
Nyarugusu
b. Msitu wa
Makere Kusini
c. Kijiji cha
Kagerankand
a
a. ISAWIMA
katika kijiji
cha Igagala
No.5 eneo la
Ufulaga
b. Matanuru ya
Tumbaku
Ufugala

Urambo
Tabora

Nzega

Igunga

a. Urambo Mjini
a. Manispaa ya
Tabora
(Kiwanda cha
Mkaa cha
Kuja na
Kushoka)
a. Kiwanda cha
Dhahabu
Ipilili
b. Bwawa la
Maji Uchama
c. Bwawa la
Maji Kilimi
d. Eneo la
Wachimbaji
Wadogo No. 7
a. Kijiji cha
Mazingira
(eco-village)
Mbutu

Katika maeneo hayo, niliona na kubaini mambo mengi, lakini


masuala makubwa na kwa muhtasari ni kama yafuatayo:1. Kuna uharibifu wa kutisha wa vyanzo vya maji katika
maeneo mengi tuliyopitia. Kwa sehemu kubwa, shughuli za
kibinadamu ikiwemo kilimo, ufugaji, ufyatuaji matofali, na
nyinginezo zinafanyika ndani vya vyanzo vya maji kinyume
na mahitaji ya Sheria ya Mazingira na Sheria ya Usimamizi
wa Rasilimali Maji. Matokeo yake, tumebaini sehemu nyingi,
hata ambapo uwekezaji mkubwa wa miundombinu ya
usambazaji maji umefanyika, bado kuna shida ya maji
kwasababu vyanzo vimeharibiwa;
2. Kuna uharibifu mkubwa vya vyanzo vya mito. Tumebaini
kwamba baadhi ya mito iliyokuwa inategemewa kutiririsha
maji kwenye maeneo mengi kwa sehemu kubwa ya mwaka
kwa ajili ya kilimo na shughuli nyinginezo sasa mito hiyo
aidha imekufa kabisa au imekuwa mito ya misimu;
3. Kuna uchepushaji mkubwa wa mito. Tumeona mito mingi
inachepushwa na watu wabinafsi kwa ajili ya matumizi yao
binafsi (ikiwemo umwagiliaji, utengenezaji matofali) na
5

kupoteza mtiririko wake wa asili na hivyo watu wengine


wengi kukosa maji na wakati mwingine kusababisha
mafuriko wakati mvua zikinyesha. Katika Mto Katuma,
ambao ndio mhimili wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi, tulihesabu
michepusho 40, ambayo imepelekea maji yasifike mbugani
na hivyo kusababisha viboko na wanyama wengine
kutaabika na hata wakati mwingine kufa. Suala hili pia
tumeliona kwenye Mto Ruaha Mkuu;
4. Kuna uteketezaji mkubwa na wa kasi wa misitu. Tumeona
hali ya misitu ilivyo mbayana kasi ya misitu hiyo kutoweka.
Misitu hiyo ni ya iana zote ya hifadhi na isiyo ya hifadhi
inapukutika kwa kasi. Sababu kubwa ya kuteketea kwa
misitu hiyo ni kilimo cha kuhamahama, uchomaji wa mkaa,
uvamizi kwa ajili ya ufugaji, uchomaji moto, na uvunaji
haramu wa mbao na magogo;
5. Kuna uchimbaji wa madini katika sehemu nyingi vijijini usio
na vibali stahiki lakini unaotumia sumu zilizokatazwa
ambazo huingia kwenye mito ambapo shughuli hizo
hufanyika;
6. Kuna udhaifu mkubwa katika utendaji wa Mamlaka za
Mabonde mbalimbali. Mamlaka hizo ndizo zilizopewa nguvu
za kisheria za usimamizi wa rasilimali maji ikiwemo kutoa
vibali vya matumizi ya maji, hata hivyo mamilioni ya watu
wanatumia maji bila vibali na kwa njia isiyo endelevu;
7. Kuna uhaba mkubwa wa ardhi kwa ajili ya wafugaji, na kuna
mifugo mingi kuliko maeneo ya kulishia, hivyo kulazimisha
wafugaji kulisha kwenye maeneo ya hifadhi, na hata
maeneo yanayomilikuwa na wakulima;
8. Kuna mikoa imefanya vizuri katika zoezi la upandaji na
utunzaji miti lakini kuna mikoa pia bado iko nyuma sana na
utamaduni wa kupanda na kutunza miti haupo kabisa;
9. Sehemu kubwa ya nchi ilikuwa na ukame, unaotokana na
kuchelewa kunyesha mvua, lakini pia unaotokana na athari
za mabadiliko ya tabianchi;
6

10.
Kujaa tope (siltation) kwenye mito na maziwa, hasa
Ziwa Rukwa ambalo lipo hatarini kupotea, kutokana na
shughuli za kibinadamu kufanyika kingoni kwa mito na
maziwa;
11.
Tumeona hatari kubwa ya mafuriko kwenye baadhi ya
miji, ikiwemo Kilosa na Kilombero, kutokana na mito
kutengeneza mikondo mingine kwasababu ya uharibifu wa
mazingira.
Hatua tulizochukua
Katika ziara hiyo, kuna baadhi ya hatua tulizochukua mara
moja na kwa haraka katika kukabili changamoto tulizozikuta.
Baadhi ya hatua hizo, ni kama zifuatazo:1. Kwa kutumia mamlaka niliyopewa katika Sheria ya
Mazingira, nimeanza taratibu za kutangaza baadhi ya
maeneo
kuwa
maeneo
ya
mazingira
nyeti
(environmentally-sensitive areas) ambapo yatapata ulinzi
wa ziada kwa kutangazwa kwenye Gazeti la Serikali.
Maeneo hayo ni pamoja na eneo linalozunguka Ziwa
Rukwa na maeneo ya Safu za Milima ya Mbeya;
2. Nilielekeza mamlaka za Serikali za Mikoa, Wilaya,
Halmashauri na Vijiji kuweka alama (beacons) katika mita
60 kutoka kwenyevyanzo vya maji na kingo za mito, na
kuweka mabango ya kuzuia watu kutofanya shughuli za
kibinadamu katika maeneo hayo;
3. Nilielekeza kwamba watu waliovamia vyanzo vya maji
waondolewe haraka sana;
4. Nilielekeza kwamba watu wote waliochepusha mito
washtakiwe na michepusho iliyojengwa ibomolewe
haraka ili mito itiririke katika mitiririko ya asili;
5. Nilielekeza kwamba wachimbaji wote wanaochimba
madini kwa kutumia sumu bila vibali wala kuzingatia
kanuni za mazingira wasimamishwe shughuli zao na
wapewe jukumu la kurekebisha hali ya mazingira kwenye
maeneo wanayofanyia kazi.
7

6. Nilielekeza kuandikwa kwa Sheria Ndogo kali za


Mazingira kwa ngazi za vijiji na Halmashauri. Niliahidi
kwamba Ofisi yetu itasaidia Halmashauri na vijiji kuwapa
mwongozo (template) ya sheria ndogo bora za mazingira;
7. Niliagiza kufanyika kwa Tathmini ya Athari kwa Mazingira
kwa shughuli za umwagiliaji maji kwenye Bonde la
Usangu
ili
tuweze
kutoa
masharti
mapya
yatakayowezesha shughuli hizo kufanyika kwa kuzingatia
kanuni za mazingira na kuwezesha maji kuendelea
kupatikana kwa watumiaji wengine;
8. Niliagiza ushirikiano wa karibu kati ya Mamlaka za
Mabonde, NEMC na Serikali za Mikoa na Wilaya ili
kuongeza ufanisi katika shughuli za hifadhi na usimamizi
wa mazingira;
9. Nilielekeza kwamba, watumiaji wakubwa wa magogo na
kuni, ikiwemo wachoma chokaa, waanze utaratibu wa
kutafuta nishati mbadala au waanzishe mashamba yao
wenyewe ya kuni;
10. Nilielekeza kuitishwa kwa kikao kikubwa cha kitaifa
cha wadau wa mkaa nchini ili kujadili namna ya kudhibiti
biashara hii ili isiendelee kuwa chanzo kikubwa cha
uharibifu wa mazingira;
11.
Nilielekeza kila kijiji kiunde Kamati ya Mazingira, na
pale ambapo pana migogoro kutokana na matumizi ya
rasilimali asili, ikiwemo maji na ardhi, paundwe Kamati za
Amani;
12. Nilielekeza Sensa ya Mifugo ifanyike, kwa mujibu wa
Sheria, na haswa mara baada ya wafugaji kuelemishwa,
ili pale Serikali tutakapoamua kwa pamoja nini kifanyike
kuhusu wafugaji waishio na kuchunga kwenye Hifadhi
nyingi za misitu, basi walau idadi halisi ya mifugo iwe
inafahamika;
8

13. Katika baadhi ya maeneo ambapo wananchi walidai


hawana pa kulima wala kufuga kwasababu eneo la
hifadhi ni kubwa na mahitaji ya shughuli zao
yameongezeka, nilishauri kwamba mchakato wa kisheria
wa kuomba maeneo hayo ufuatwe ili Serikali ifikie
maamuzi sahihi kwa manufaa ya watu wake;
14. Niliagiza kwamba, licha ya changamoto za rasilimali,
NEMC iwepo kila pahala kuweza kutoa ushauri na
mwongozo kwa mamlaka nyinginezo na kwa wananchi
kuhusu masuala ya hifadhi kwa mazingira;
15. Nilielekeza uongozi wa Wilaya za Kilosa na Kilombero
wapeleke haraka kwenye Ofisi ya Maafa ya Taifa maelezo
ya hatari ya miji ya Kilosa na Ifakara kukubwa na
mafuriko ili Ofisi hiyo ichukue hatua stahiki;
16. Nilielekeza Shirika la Kimataifa la Kuhudumia
Wakimbizi kwamba ndani ya mwaka mmoja, liwezeshe
wakimbizi katika kambi zote nchini kuacha kukata miti
kwa ajili ya kuni. Vilevile, nilielekeza kwamba, Tathmini
ya Athari kwa Mazingira, ifanyike kwa kambi zote za
wakimbizi hapa nchini ili kuniwezesha kutoa masharti ya
kisheria ya ukaaji kambini ambao utazingatia hifadhi ya
mazingira;
17. Tulitumia Sheria ya Mazingira kifungu 196 kutoa
katazo kwa matumizi ya mabani (majiko) ya kukausha
tumbaku ya kienyeji ambayo yanatumia magogo
makubwa na yenye thamani kubwa kuliko hata tumbaku
yenyewe na kuelekeza yatumike mabani ya tofali za
kuchoma ambayo yanatumia kuni za kawaida na matawi
ya miti; na
18. Nilielekeza wataalam wa Ofisi yetu kutengeneza
andiko la maalum kwa ajili ya kupata fedha kwa maeneo
yenye ukame mkali (arid areas) kutoka katika Mfuko wa
Kimataifa wa Kukabiliana na Athari za Mabadiliko ya
Tabianchi (Adaptation Fund).
9

Baada ya hatua hizi zimeanza kuchukuliwa. Haya ni


muhtasari na kwa uchache. Tuliyoona ni mengi na
maelekezo tuliyoyatoa ni mengi. Tunayo ripoti kubwa
ambayo tumeiwasilisha Serikalini kwa wenzetu kwa hatua za
pamoja za ndani ya Serikali. Pamoja na ripoti hiyo,
tumetengeneza Mpango-Kazi (Action-Plan) ya utekelezaji wa
maagizo na maelekezo tuliyoyatoa kwenye ziara hiyo.
Yapo mambo makubwa kadhaa ambayo
kipaumbele na kuyafanyia kazi kama Ofisi.

tunayapa

1. Ujenzi wa Uwezo wa NEMC na Ofisi ya Makamu wa


Rais pamoja na Halmashauri zetu katika kusimamia
masuala ya mazingira na mabadiliko ya tabia nchi.
2. Upunguzaji wa matumizi ya mkaa na kuwezesha
nishati endelevu ya kupikia kutumika;
3. Kuimarisha uwezo wa kitaasisi wa usimamizi wa
sheria ya mazingira.
4. Kuendelea kutafuta rasilimali na miradi mikubwa ya
kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi,
ikiwemo
miradi
ya
maji
kwenye
maeneo
yaliyokumbwa na ukame mkubwa.
5. Kuweka msukumo mpya kwenye upandaji wa mti

nchini na hifadhi ya vyanzo vya maji;


6. Kuondoa matumizi ya mifuko ya plastiki, kukabiliana

na utupaji wa taka hatarishi, na kudhibiti uvuvi


haramu wa kulipua mabomu na kutumia sumu.

January Y. Makamba (Mb.),


WAZIRI WA NCHI,
OFISI YA MAKAMU WA RAIS (MUUNGANO NA
MAZINGIRA)
1 Disemba 2016

10

You might also like