You are on page 1of 5

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

MAKUMBUSHO YA TAIFA LA TANZANIA

MAKUMBUSHO YA MAJI MAJI NA MAKUMBUSHO YA DKT. RASHID M. KAWAWA

TAARIFA YA OUTREACH PROGRAM WILAYA YA NAMTUMBO MKOANI RUVUMA


MACHI 2023 MWAKA WA FEDHA 2023/2023

Machi, 2023
1
1.0. UTANGULIZI
Makumbusho ya Taifa ilianzishwa kwa Sheria ya Makumbusho ya Taifa Na. 7 ya
Mwaka 1980 kwa malengo ya kutafiti, kukusanya, kuhifadhi, kuelimisha jamii Urithi wa
Utamaduni na Asili. Ofisi ya Makumbusho ya taifa kupituia kituo cha Makumbusho ya
Maji Maji na Dkt. Rashid M. Kawawa iliendesha program ijulikanayo kama outreach
program ikiwa na lengo la kutangaza utalii pamoja na historia adhimu inayohusu vita
vya majimaji vilivyopiganwa mwaka 1905 mpaka 1907 vikihusisha makabila
yanayopatikana Kusini mwa Tanzania. hivyo, kupitia program ya outreach tulitembelea
jumla ya shule Ishirini (20) za msingi na sekondari, kwani wanafunzi ni wadau muhimu
sana wa Makumbusho zetu katika kuendeleza urithi wa utamaduni pamoja na
kutangaza utalii wetu. Program hiyo ilifanyika kuanzia tarehe 20/03/2023 hadi
24/03/2023 Wilayani Namtumbo Mkoani Ruvuma katika shule za msingi na sekondari
zipatikanazo wilayani humo.

2. DIRA,DHIMA NA MALENGO YA TAASISI

Dira ya Makumbusho ya Tanzania ni kuwa na jamii inayothamini, inayohifadhi na


kutumia urithi wake kwa maendeleo endelevu. Aidha, Makumbusho ya Taifa ina dhima
ya kukuza urithi wa kitaifa kupitia uhifadhi wa makusanyo, utafiti na usambazaji wa
maarifa kwa faida ya ubinadamu. Ili kutimiza dira na malengo yake kupitia mpango
mkakati wa taasisi wa mwaka 2021/2026, makumusho ya Taifa ina malengo yafuatayo:
i. Kuzuia na kupambana na HIV/AIDS na maradhi yanayoambukiza mahali kazi.
ii. Kuzuia na kupambana ya rushwa
iii. Kuimarisha uhifadhi wa rasilimali za urithi wa asili na kitamaduni
iv. Kuendeleza na kukuza bidhaa za asili na utamaduni
v. Kuimarisha uwezo wa taasisi kuboresha huduma zake
vi. Kuimarisha vyanzo vya mapato ikiwemo kufikisha idadi ya watalii 2,000,000
ifikapo Juni 2026.

3. MALENGO YA OUTREACH PROGRAM

Moja ya njia ya kutimiza dira, dhima na malengo ya Makumbusho ni utoaji wa elimu ya


urithi kwa jamii kwa njia ya outreach program. Katika kipindi cha mwaka wa fedha
2022/2023, Makumbusho ya Taifa kupitia Makumbusho ya Dkt. Radhid M. Kawawa na
Makumbusho ya Maji Maji ilipanga kutekeleza oureach program Ishirini (20) katika
Halmashauri Namtumbo. Program hii ililenga kutangaza vivutio vya utalii vya
Makumbusho vilivyopo mkoa wa Ruvuma, kuhamasisha utalii wa ndani kwa jamii, na
pia kutoa elimu ya urithi wa asili na utamaduni ili kuongeza idadi ya watalii na mapato
ya makumbusho ya Majimaji na Dkt. Rashid M. Kawawa.

2
4.0 NJIA ZA UWASILISHAJI WA OUTREACH PROGRAM NA VITENDEA KAZI
Makumbusho ya Taifa kupitia Makumbusho ya Dkt. Rashid M. Kawawa na
Makumbusho ya Maji Maji ilitumia njia zifuatazo katika utoaji na uwasilishaji wa elimu
ya urithi wa asili na utamaduni: Mhadhara, Ushirikishaji, Maswali na majibu na
“Demosntration”. Vitendea kazi vitavyotumika: Kibali cha Mkurugenzi wa Halmashauri
ya Wilaya ya Namtumbo, “Tarrif Menu” mpya ya Makumbusho ya Taifa, vipeperushi,
kibali cha kuanzisha Klabu za Historia na Uzalendo, Mada za Kazi Mradi.

5.0 MATARAJIO YA MATOKEO YA KAZI


i. Kuzitangaza Makumbusho zetu.
ii. Jamii kupata elimu ya uhifadhi wa urithi wa utamaduni na waasili.
iii. Kuimarika kwa mawasiliano ya kihuduma kati ya makumbusho na jamii(Shule).
iv. Kuongezeka kwa idadi ya wagaeni/watalii (Shule za Msingi na Sekondari)
kutoka Wilaya ya Namtumbo .
v. Kukua kwa pato la mwananchi, taasisi (Makumbusho ya Maji Maji na
Makumbusho ya Dkt. Rashid M. Kawawa.
vi. Jamii kushiriki kamilifu katika uhifadhi wa urithi wa asili na utamaduni
vii. Kuanzishwa kwa klabu ya historia na uzalendo shule za msingi na sekondari.

6.0 TAASISI ZILIZOTEMBELEWA

Kwa kipindi cha Mwaka wa Fedha 2022/2023, Makumbusho ya Maji Maji na


Makumbusho ya Dkt. Rashid M.Kawawa zilitembelea jumla ya shule Ishirini (20)
Wilayani Namtumbo. Kati ya hizo Shule za Msingi zilikuwa Kumi (10) na Shule za
Sekondari zilikuwa Kumi (10) kama ilivyo katika jedwali hapa chini.

Na. SHULE YA MSINGI SHULE YA SEKONDARI


1 Namtumbo 1 Nasuli
2 Lucenti 2 Narwi
3 Minazini 3 Nandungutu
4 Lwinga 4 Umoja
5 Selous 5 Luna
6 Mkapa 6 Nanungu
7 Namabengo 7 Namabengo
8 Mtwara Pachani 8 Luwegu
9 Luwegu 9 Uhuru
10 Litora 10 St. Benedict

Jedwali Na. 1 Idadi ya shule za msingi na sekondari zilizotembelewa wakati wa


outreach program wilayani Namtumbo Mkoani Ruvuma mwezi Machi, 2023.

3
Kielelezo Na.1Picha ikionesha baadhi ya wanafunzi wa shule ya Msingi Lumecha
Wilayani Namtumbo siku ya Program ya outreach tarehe 21.03.2023.

7.0 RASILIMALI WATU

Utekelezaji wa Outreach Program ulifanywa na jumla watumishi Saba(7) wa


Makumbusho za Dkt. Rashid M. Kawawa na Makumbusho ya MajiMaji. Watumishi
walioshiriki katika Program ni: Balthazar Nyamusya, Rose C. Kangu, Erick Soko,
Veronica Muro Danford Majogo, Emil Laurent na Bakari Issa.

8.0 RASILIMALI MUDA

Utekelezaji wa Outreach Program ulitumi siku Tano kuanzia tarehe 20/03/2023 hadi
24/03/2023.

4
9.0 RASILIMALI FEDHA/ BAJETI

Outreach program iligharimu jumla ya kiasi cha Tshs. 2,125,000.00 .katika mchanganuo
ufuatao:

NA. JINA MAHITAJI Kiasi(Half-Per Jumla Kuu


Diem)
1 Rose C. Kangu Posho 65,000x 5 (Siku) 325,000.00
2 Balthazar Nyamusya Posho 65,000x 5 (Siku) 325,000.00
3 Erick Soko Posho 65,000x 5 (Siku) 325,000.00
4 Veronica Muro Posho 65,000x 5 (Siku) 325,000.00
5 Danford Majogo Posho 65,000x 5 (Siku) 325,000.00
6 Emil Laurent Posho 50,000x 5 (Siku) 250,000.00
7 Bakari Issa Posho 50,000x 5 (Siku) 250,000.00
Jumla Kuu 2,125,000.00

Naomba kuwasilisha.

Rose C. Kangu

AFISA ELIMU

You might also like