You are on page 1of 34

TANZANIA YOUTH MINISTRIES-TAYOMI

“Change the Life of the Youths to Change the World”

National Prayer Rally 2023
“The lazy man does not, will not,
cannot pray, for prayer demands energy” (E.M. Bounds)

“Maombi ni shughuli inayostahili kufanyika

kabla ya shughuli nyingine yoyote”

UTANGULIZI
Bwana Yesu asifiwe.
Nawasalimu kwa jina la Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo. Pokeeni salamu za upendo na
neema tele kutoka ofisi za makao makuu.
Awali ya yote napenda kumshukuru Mungu kwa ajili yenu kwa jinsi mlivyojitoa kufanikisha
malengo ya huduma kwa mwaka 2022.
Mtakumbuka kwamba mwaka 2022 tumekuwa na mbio za maombi kwa muda wa miezi saba
(7month Prayer Rally) ambayo yamefanyika kwa mafanikio makubwa, maana kuna mambo
kadhaa tulioyaombea binafsi nimeona Mungu amejibu. Binafsi nakiri kwamba nimekuwa na
hatua moja zaidi kwa jinsi nilivyoshiriki katika maombi haya.
Mwaka huu wa 2023 ni mwaka ambao tunaanza mwaka wa 31 tangu kuanzishwa kwa maono
haya. Naweza kusema ni mwaka wa kwanza baada ya miongo mitatu (three decades) ya huduma
hii.
Napenda tena niwakaribishe wote katika maombi ambayo tutaendelea nayo kwa vipindi tofauti
tofauti katika mwaka huu wa 2023. Natambua kwamba baadhi ya madhehebu ya kipentekoste
huwa na ratiba za maombi mwanzoni mwa mwaka, hivyo tunawahimiza wanaCASFETA wote
pamoja na Waratibu kushiriki maombi katika makanisa wanayoabudu kwa uaminifu, huku kila
mmoja wetu akiombea mahitaji yetu ya huduma kama yanavyoelezwa katika waraka huu.

MUUNDO WA MAOMBI
Maombi haya yatakuwa yakifanyika sambamba na kufunga masaa 12 kwa siku. kuanzia
30/01/2023 mpaka 15/12/2023.
Kila mkoa utasimama katika maombi kulingana na ratiba. Aidha wajumbe wa kamati mbalimbali
za uongozi/Vikao vya Huduma; kwa mfano Kamati ya Rais wa CASFETA, Kamati ya EEMC Taifa,
Baraza la Waratibu la Taifa, Kamati ya Utendaji, n.k, wamepangiwa zamu katika ratiba, hata hivyo
bado watapaswa kushiriki katika zamu za mikoa yao.
Kwenye mikesha/mikutano ya maombi ya kimikoa, kiwilaya, tawi, n.k, mambo ya kuombea ya
wiki/siku husika yazingatiwe.
Page 1/29
Ratiba ya Maombi

Tarehe Wahusika Tarehe Wahusika

Januari 30-Februari 03 Baraza la Waratibu la Septemba 11-15 Baraza la Waratibu la Taifa.
Taifa.
Februari 06-10 Ofisi ya Rais wa CASFETA. Septemba 18-22 Kagera, Ruvuma, Dar es
salaam/Pwani.
Februari 13-17 EEMC Taifa. Septemba 25-29 Ofisi ya Rais wa CASFETA.
Februari 20-24 Kagera, Ruvuma, Dar es Oktoba 02-06 Mbeya, Morogoro, Geita,
salaam/Pwani. Manyara.
Februari 27-Machi 03 Mbeya, Morogoro, Geita, Oktoba 9-13 Mara, Rukwa, Kilimanjaro,
Manyara. Mwanza.
Machi 06-10 Mara, Rukwa Kilimanjaro, Oktoba 16-20 Mtwara & Lindi, Kigoma,
Mwanza. Tabora, Tanga, Iringa.
Machi 20-31 Wote. Oktoba 23-27 Arusha, Dodoma, Simiyu,
Shinyanga, Njombe.
Aprili 24-28 Mtwara & Lindi, Kigoma, Oktoba 30-Novemba 03 Wote.
Tabora, Tanga, Iringa.
Mei 15-19 Arusha, Dodoma, Simiyu, Novemba 06-10 Kigoma, Singida, Songwe,
Shinyanga, Njombe. Katavi, Zanzibar.
Juni (JNLC) Viongozi wote. Novemba 13-17 Viongozi wote.
Julai 31-Agosti 04 Kigoma, Singida, Songwe, Novemba 20-24 Sekretarieti.
Katavi, Zanzibar.
Agosti 07-11 Wote. Novemba 27-01 Desemba Baraza la Uongozi la Taifa.
Agosti 14-18 Baraza la Uongozi la Taifa. Desemba 04-08 Kamati Kuu TAYOMI
Agosti 21-25 Viongozi wote &BCF Desemba 11-15 Viongozi wote.
Septemba 04-08 Sekretarieti.

1. MAHITAJI YA KUOMBEA
30/01-03/02/2023 Baraza la Waratibu la Taifa
30/01/2023
Ombea Kazi ya Huduma za TAYOMI katika mikoa mipya
i. Ombea uamsho wa huduma katika mkoa wa Iringa, Mungu afungue milango ya huduma
kuenea zaidi mkoani humo.
ii. Ombea kazi ya Mungu kupitia TAYOMI izidi kuimarika Wilayani Makete Mkoani Njombe.
iii. Ombea huduma ipate kibali na mpenyo katika Wilaya nyingine za mkoa wa Njombe.
31/01/2023
Ombea Uamsho mpya kwa Kazi ya Huduma za TAYOMI katika mikoa ya kwanza kufikiwa na
huduma hii: Kilimanjaro, Dar es salaam, Mbeya, Tanga, Ruvuma na Morogoro
i. Omba Mungu alete uamsho mpya, akahuishe nguvu ya kiutendaji kwa watumishi wa
TAYOMI katika mikoa hii.
ii. Mungu akaiinue upya kazi na kuifanya ienee zaidi.
iii. Matawi yaliyokufa yakainuke tena, watendaji walioacha huduma wakarejee tena kwa
nguvu.

Page 2/29
iv. Mungu azidi kuachilia kibali cha ufunguzi wa matawi zaidi katika mikoa hii.
v. Ombea viongozi wa CASFETA na EEMC katika mikoa hii.
01/02/2023
Ombea vikao na makongamano ya Huduma
i. Vikao vya viongozi vifikie maamuzi yenye manufaa kwa ufalme wa Mungu.
ii. Ombea Makongamano ya JNLC na AGM: Mahudhurio, michango, Mafundisho, warsha
na semina.
iii. Ombea safari za wajumbe wa mikutano/vikao hivi.
iv. Mungu atuwezeshe kwa rasilimali, ujuzi na maarifa katika kutekeleza maamuzi ya vikao
vya huduma.
v. Kila mwenye hoja/jambo/maoni ya kufanikisha huduma ya mwili wa Kristo akawe tayari
kushirikisha wengine.
02/02/2023
Siku ya 20: 03/06/2022
Ombea huduma katika mikoa ya Songwe, Simiyu na Katavi
i. Mungu akaimarishe kazi katika mikoa hii.
ii. Mungu awape ujasiri watendaji wakafungue matawi kwa bidii.
iii. Mungu alete maelewano ya kimaongozi ili kazi ya huduma itendeke kwa ufanisi.
iv. Mungu awalinde wanaCASFETA dhidi ya mila na desturi zinazokwamisha safari zao
kielimu.

03/02/2022
Ombea mipango ya maendeleo ya Huduma
i. Ombea ununuzi/upatikanaji wa ardhi katika mikoa yote.
ii. Omba Kuhusu ada za uanachama, kila mwanachama akalipe kwa uaminifu.
iii. Ombea kuhusu michango ya huduma, kila mtumishi akajisikie kuhusika kuchangia
huduma.
iv. Ombea mpango wa kuchangia huduma kielektroniki na mfumo wa usajili wa wanachama.

06-10/02/2023 Ofisi ya Rais wa CASFETA

06/02/2023
Ombea mipango ya maendeleo ya Huduma
i. Ombea huduma ikatambulike duniani pote na Mungu aguse watu wa mataifa mbalimbali
kushiriki nasi na kuwekeza katika maono haya.
ii. Mungu awaguse watanzania kujitoa kwa nguvu kuchangia fedha huduma hii.
iii. Ombea wanataaluma wa CASFETA wajisikie kuhusika katika kuchangia fedha huduma hii.
iv. Ombea ujenzi wa Ofisi za Makao Makuu ya TAYOMI mkoani Morogoro.

Page 3/29
07/02/2023
Ombea watumishi wa Mungu wa Madhehebu ya Kipentekoste na Waratibu wa TAYOMI
i. Ombea Watoto wao wakue wakimjua Mungu wa kweli sawasawa na utumishi wa wazazi
wao.
ii. Kataa hali ya kukata tamaa kwa waratibu wote, omba Mungu akahuishe upya wito wao
ndani ya TAYOMI.
iii. Mungu awape neema ya maarifa ya kuweza kubalance huduma na kutunza familia zao.
08/02/2023
Ombea huduma za Injili kwa wanafunzi
i. Ombea Uhuru wa kuhubiri Injili shuleni/vyuoni uendelee.
ii. Ombea uhuru wa vyombo vya habari ukatumike kupeleka Injili ya Kristo.
iii. Ombea Wizara ya Elimu izidi kuwa na ushirikiano mzuri na taasisi zinazopeleka Injili kwa
wanafunzi.
09/02/2023
Ombea Mikutano ya Ibada za Wanafunzi chini ya TAYOMI
i. Mungu akaonekane katika ibada zote za CASFETA na BCF
ii. Wanafunzi waokolewe kupitia ibada hizi
iii. Joint-Fellowship zikawe na nguvu na udhihirisho wa Roho Mtakatifu
iv. Ombea miujiza Ishara na maajabu vikafanyike katika ibada hizi

10/02/2023
Ombea shule na taasisi za elimu ya juu Tanzania
i. Amani ikatawale katika shule.
ii. Kataa migomo na vurugu katika taasisi za Elimu.
iii. Walimu wawafundishe wanafunzi kwa upendo.
iv. Fahamu za wanafunzi zifunguke ili waelewe masomo yao.
v. Wanafunzi uwezo wakutendea kazi yale mambo wanayojifunza darasani.
vi. Uongozi wa shule/taasisi za elimu usiwe kikwazo kwa Injili.
13-17/02/2023 EEMC Taifa
13/02/2023
Ombea marafiki wa TAYOMI ndani na nje ya Tanzania
i. Ombea wadau wote wa TAYOMI ambao wamekuwa wakisaidia huduma hii kifedha
Mungu awakumbuke katika maisha yao na kuwazidishia zaidi pale walipotoa
ii. Mungu ainue watu zaidi ndani ya Tanzania watakowekeza katika ufalme wa Mungu
kupitia TAYOMI.
iii. Mungu aguse wanaCASFETA waliotawanyika duniani pote kusapoti huduma kwa mali
zao.
14/02/2023
Omba kwa ajili ya umoja, mshikamano na upendo katika huduma
i. Viongozi na wanachama walkawe na utii kwa Mungu.
Page 4/29
ii. Viongozi wa Kanda, Mikoa, Wilaya, Matawi wakatii maagizo kutoka taifani na
kuyatekeleza.
iii. Kataa kiburi na ubinafsi katika huduma.
15/02/2023

Omba kwa ajili ya maendelo ya kielimu kwa wanachama na wahudumu wote

i. Mungu atufanikishe katika elimu na taaluma.
ii. Mungu afungue kwa wale wenye milango ya kusoma zaidi.
iii. Walioko masomoni wakamalize kwa ushindi na mafanikio makubwa.
iv. Ombea wanaCASFETA wenye changamoto za ad ana matatizo ya kifamili; Mungu
awakumbuke katika shida zao.

16/02/2023
Ombea Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPCT)
i. Umoja wa mwili wa Kristo udumu
ii. Mungu atuepushe na migogoro makanisani
iii. Omba unyenyekevu kwa Maaskofu wote na viongozi wakuu wa Makanisa/huduma za
Kipentekoste
iv. Mungu awajalie viongozi wa Baraza Hekima, Maarifa na Ufahamu wa kimungu zaidi
katika uongozi wao.
17/02/2023
Ombea Bunge na Mahakama ya Tanzania
i. Mwombee Spika wa Bunge akaliongoze Bunge katika haki na kwa maslahi ya Watanzania.
ii. Watu wenye hofu ya Mungu wapate nafasi katika vyombi hivi.
iii. Ombea mawakili wa Tanzania wakaisaidie Mahakama kutenda haki.
iv. Haki ikatendeke katika maamuzi ya Mahakama.
20-24/02/2023 Kagera, Ruvuma, Dar es salaam/Pwani
20/02/2023
Omba kwa ajili ya viongozi wa kitaifa wa TAYOMI
i. Mungu awaongoze katika kusimamia maono haya
ii. Mungu azidi kuwatumia kwa karama za Roho Mtakatifu
iii. Mungu awalinde na kuwaepusha na kila hila za adui shetani
iv. Ombea familia zao
21/02/2023
Omba kwa ajili ya maendelo ya kielimu kwa wanachama na wahudumu wote
i. Mungu atufanikishe katika elimu na taaluma
ii. Mungu afungue kwa wale wenye milango ya kusoma zaidi
iii. Walioko masomoni wakamalize kwa ushindi na mafanikio makubwa

Page 5/29
iv. Ombea wanaCASFETA wenye changamoto za ad ana matatizo ya kifamili; Mungu
awakumbuke katika shida zao.
22/02/2023
Ombea usalama wa chakula katika nchi
i. Mungu atujalie mvua kwa majira yaliyokubalika
ii. Nchi ikazae mazao yenye afya
iii. Mungu atuepushe na baa la njaa
iv. Ombea wakulima wafanye kazi yao kwa bidii
v. Mapinduzi yatokee katika sekta ya kilimo
vi. Kemea na kataa magonjwa ya lishe kwa Watoto wa Tanzania
23/02/2023
Ombea ushirikiano wa TAYOMI na Serikali
i. Mshukuru Mungu kwa kutuwezesha kutii masharti ya usajili wetu serikalini.
ii. Mshukuru Mungu kwa ushirikiano tunaoupata kwa wakuu wa shule na vyuo nchini.
iii. Mungu azidi kutupa kibali kwa serikali na kuwa mfano wa kuigwa kwa kutii masharti ya
usajili.
iv. Viongozi na watendaji wa Wizara ya Elimu, Wizara ya Mambo ya Ndani, Wizara ya Katiba
na Sheria wazidi kudumisha uhuru na haki ya kushiriki masuala ya kiimani kwa wanafunzi.
24/02/2023
Omba kwa ajili ya Uinjilisti na kukua kwa huduma
i. Ufunguzi wa matawi ya CASFETA, kila shule ya Sekondari ikafikiwe na CASFETA-TAYOMI.
ii. Kampeni za Injili shuleni/vyuoni zikalete matokeo ya wengi kuokolewa.
iii. Mungu ainue wainjilisti wenye mzigo wa kuwafikia watu wenye dhambi.
iv. Ishara miujiza na maajabu vikaambatane nasi tunapopeleka Injili ya Kristo
v. Wiki ya mavuno mwezi Mei ikalete matunda mengi yatakayokaa
27/02-03/03/2023 Mbeya, Morogoro, Geita, Manyara
27/02/2023
Ombea wanataaluma wote ambao ni zao la CASFETA TAYOMI
i. Popote walipo wakawe nuru na chumvi ya ulimwengu.
ii. Ombea wajiepushe na rushwa na tamaa za kila namna katika nafasi walizonazo.
iii. Kwa wale ambao wapo kwenye nafasi za maamuzi watende haki na kuwahudumia watu
kwa moyo bila kutaka fedha ya aibu.
iv. Ombea wanataaluma wote wa CASFETA wakang’are katika utendaji wao, Mungu
akawaamini katika majukumu makubwa zaidi.
v. Omba Mungu akainue wataaluma waliookoka wenye uthubutu kama wa Esta na Daniel
watakaosimama kwa ajili ya ufalme wa Mungu pasipo hofu.
28/02/2023
Ombea maendeleo ya huduma ya muda wa kati na mrefu
i. Kila mkoa uwe na ardhi ndani ya miaka mitano (5) ijayo.
Page 6/29
ii. Ombea mchakato wa kuandaa master plan ya eneo la Melela Morogoro, Mungu atupe
fedha na watenda kazi hodari ma mahiri.
i. Ombea ujenzi wa Ofisi za Makao Makuu ya TAYOMI mkoani Morogoro.
iii. Ombea ujenzi wa kituo cha mikutano mkoani Morogoro.
iv. Ombea ujenzi wa kituo cha Mikutano/shule Mkoani Mbeya.
01/03/2023
Omba kwa ajili ya Serikali ya Tanzania
i. Rais wa nchi: Mungu amjalie Afya, maono, busara, hekima na maarifa, maamuzi sahihi.
ii. Rais na Baraza la Mawaziri waongoze taifa katika haki na kwa manufaa ya wananchi wote.
iii. Mipango na miradi mbalimbali ya maendeleo ya nchi.
02/03/2023
Ombea watu mbalimbali walioshiriki na kufanikisha kuanzisha na kuenea huduma ya TAYOMI:
Wataje kwa majina wale unaowafahamu/unaowakumbuka
i. Mungu awakumbuke kwa utumishi wao, akutane na mahitaji yao yote.
ii. Mungu awasaidie wasiiache imani ya kweli katika Kristo Yesu, wale ambao walipotea
dhambini wapate kurudi na kutubu.
iii. Mungu aendelee kuwapa moyo wa kusimamia ushuhuda wa maono haya na kuyasemea
vyema kwa watu wengine.
03/03/2023
Ombea uwezo wa kutumia akili kwa waaminio na simama kinyume na mafundisho ya uongo
i. Omba kwa ajili matumizi ya akili kwa watu wa Mungu, Mungu awape watu akili na maarifa
ya kupambanua mambo na kujiepusha na ujinga.
ii. Simama kinyume na mahubiri na wahubiri wa uongo; angusha na vunja mbinu za walimu
wa uongo.
iii. Ombea vijana wanaohudumiwa na TAYOMI, Mungu awaepushe wasivutwe na imani za
uongo na mafundisho ya uongo.

06-10/03/2023 Mara, Rukwa, Kilimanjaro, Mwanza

06/03/2023
Ombea Mikutano ya Ibada za Wanafunzi chini ya TAYOMI
i. Mungu akaonekane katika ibada zote za CASFETA na BCF
ii. Wanafunzi waokolewe kupitia ibada hizi
iii. Joint-Fellowship zikawe na nguvu na udhihirisho wa Roho Mtakatifu
iv. Ombea miujiza Ishara na maajabu vikafanyike katika ibada hizi
07/03/2023
Omba Mungu arejeshe program za kitaifa za wanachama zinazosuasua
i. Makongamano ya Elimu mwezi Februari kila Mwaka.
ii. ACTION Plan: Mungu akaliongeze kanisa lake kwa wanavyuo kuokolewa.
iii. Harvest Plan: Mungu akatutumie kwa uinjilisti ili tumletee Bwana mavuno.
Page 7/29
08/03/2023
Omba kwa ajili ya wafanyakazi sekta ya afya
i. Mungu awahifadhi dhidi ya hatari zinazoambatana na kazi zao.
ii. Wawe na moyo wa upendo kwa wagonjwa.
iii. Watoe huduma bora kwa wagonjwa zitakazowapa matumaini na kuboresha afya zao.
09/03/2023
Omba kwa ajili ya Elimu ya Tanzania
i. Mabadiliko ya mitaala ya Elimu nchini yakamwezeshe mhitimu wa Tanzania kuweza
kushindana katika soko la taaluma na weledi duniani.
ii. Mwombee Waziri wa Elimu aje na sera na mipango ya kuboresha elimu.
iii. Mungu ainue kizazi cha wanafunzi wanaopenda hesabu na sayansi.
10/03/2023
Ombea ushirikiano wa kihuduma kitaifa
i. Ombea huduma ikatambulike nchini pote na Mungu aguse watanzania mbalimbali
kushiriki nasi na kuwekeza katika maono haya.
ii. Mungu awaguse watanzania kujitoa kwa nguvu kuchangia fedha huduma hii.
iii. Ombea wanataaluma wa CASFETA wajisikie kuhusika katika kuchangia fedha huduma hii.
20-31/03/2023 Wote nchi nzima
20/03/2023
Ombea makambi ya Pasaka 2023
i. Ombea semina kwa walimu wa masomo ya Makambi ya Pasaka 2023
ii. Ombea maandalizi ya makambi mikoa yote yakamilike
iii. Omba kwa ajili ya walimu watakaofundisha makambi ya Pasaka 2023
iv. Makambi ambayo bado hawajapata venue Mungu awafungulie mlango
v. Omba kwa ajili ya mipango ya upatikanaji wa fedha za kuendesha makambi
21/03/2023
Ombea ushiriki wa wanaCLPD katika makambi ya Pasaka
i. Mungu awaguse wanataaluma kuchangia fedha makambi ya Pasaka katika mikoa yao
ii. Wawe na utayari wa kushiriki kufundisha katika makambi ya Pasaka
iii. Ombea kwa ajili ya mshikamano na ushirikiano wa CLPD na Waratibu katika kufaniskisha
makambi ya Pasaka.
22/03/2023
Ombea makambi ya Pasaka 2023
i. Omba nguvu za Mungu na mafuriko ya Roho Mtakatifu
ii. Omba usalama amani na utulivu wakati wa makamabi
iii. Omba ulinzi wa Mungu katika safari zote za makambi ya Pasaka
iv. Ombea wana CASFETA/BCF washiriki kikamilifu katika makambi ya Pasaka
v. Mafundisho yakalete mabadiliko kwa wanachama kama apendavyo Mungu

Page 8/29
23/03/2023
Ombea maandalizi ya mtu mmoja mmoja kwa kuelekea makambi ya Pasaka 2023
i. Jiombee binafsi utayari wa kupokea kutoka kwa Bwana
ii. Omba usikivu na uelewa wa kile ambacho Mungu ameandaa kwa ajili yetu kupitia makambi
ya Pasaka
iii. Ombea vinywa vya wahudumu wote wa makambi vikanene maarifa ya kimungu
iv. Ombea ushiriki wa kutosha wa wachungaji katika makambi ya Pasaka
24/03/2023
Omba Mungu akaibue na kudhihirisha vipawa na karama za WanaCASFETA/BCF wakati wa
Makambi ya Pasaka
i. Roho Mtakatifu afungue mlango wa watu kutambua karama vipawa.
ii. Omba karama za Roho Mtakatifu zikatende kazi kuujenga mwili wa Kristo wakati wa
Makambi ya Pasaka.
iii. Omba udhihirisho wa Roho Mtakatifu kupitia uponyaji miujiza,ishara na maajabu wakati
wa Makambi ya Pasaka.
iv. Mungu awajalie viongozi ubora katika kuendesha makongamano ya Pasaka.
v. Ishara miujiza na maajabu vikaambatane nasi tunaponena kweli ya Injili wakati wa
Makongamano ya Pasaka.
25/03/2023
Ombea ushiriki wa makanisa/madhehebu marafiki katika Makambi ya Pasaka
i. Makambi haya yakawe sehemu ya kuimarisha zaidi uhusiano wa TAYOMI na madhehebu
mbalimbali ya kipentekoste
ii. Ombea wachungaji watakaoalikwa kufundisha katika makambi
iii. Madhehebu yakaielewe zaidi TAYOMI wakati huu wa makambi ya Pasaka
iv. Simama kinyume na changamoto za kimadhehebu wakati wa makambi ya Pasaka
26/03/2023
Omba ulinzi wa Mungu wakati wa Makambi ya Pasaka
i. Safari za wahudumu wote
ii. Safari za wanachama kwenda kwenye makambi ya Pasaka
iii. Amani na utulivu katika vituo vyote
iv. Afya njema wakati wote wa makambi kwa watu wote
27/03/2023
Ombea Makambi ya Pasaka kulingana na uhitaji wa Mkoa/Wilaya yako
28/03/2023
Ombea maandalizi ya mtu mmoja mmoja kwa kuelekea makambi ya Pasaka 2023
i. Jiombee binafsi utayari wa kupokea kutoka kwa Bwana.
Page 9/29
ii. Omba usikivu na uelewa wa kile ambacho Mungu ameandaa kwa ajili yetu kupitia makambi
ya Pasaka.
iii. Ombea vinywa vya wahudumu wote wa makambi vikanene maarifa ya kimungu.
iv. Ombea ushiriki wa kutosha wa wachungaji katika makambi ya Pasaka.
29/03/2023
Omba ulinzi wa Mungu wakati wa Makambi ya Pasaka
i. Safari za wahudumu wote
ii. Safari za wanachama kwenda kwenye makambi ya Pasaka
iii. Amani na utulivu katika vituo vyote
iv. Afya njema wakati wote wa makambi kwa watu wote
v. Ondoa vizuizi vyote dhidi ya mafanikio ya makambi ya Pasaka 2023
30/03/2023
Ombea makongamano ya Pasaka 2023
i. Omba nguvu za Mungu na mafuriko ya Roho Mtakatifu
ii. Omba usalama amani na utulivu wakati wa makamabi
iii. Omba ulinzi wa Mungu katika safari zote za makambi ya Pasaka
iv. Ombea wana CASFETA/BCF washiriki kikamilifu katika makambi ya Pasaka
v. Mafundisho yakalete mabadiliko kwa wanachama kama apendavyo Mungu
31/03/2023
Omba Mungu akaibue na kudhihirisha vipawa na karama za WanaCASFETA/BCF wakati wa
Makambi ya Pasaka
i. Roho Mtakatifu afungue mlango wa watu kutambua karama vipawa.
ii. Omba karama za Roho Mtakatifu zikatende kazi kuujenga mwili wa Kristo wakati wa
Makambi ya Pasaka.
iii. Omba udhihirisho wa Roho Mtakatifu kupitia uponyaji miujiza,ishara na maajabu wakati
wa Makambi ya Pasaka.
iv. Mungu awajalie viongozi ubora katika kuendesha makongamano ya Pasaka.
v. Ishara miujiza na maajabu vikaambatane nasi tunaponena kweli ya Injili wakati wa
Makongamano ya Pasaka.

24-28/04/2023 Mtwara/Lindi, Kigoma, Tabora, Tanga, Iringa

24/04/2023
Mshukuru Mungu kwa ajili ya kufanikisha makambi ya Pasaka
i. Mshukuru kwa kila jambo tuliloliombea wakati wa maandalizi ya Makongano ya Pasaka.
ii. Mshukuru Mungu kwa kutujalia maongozi ya Roho Mtakatifu katika uendeshaji wa
Makambi ya Pasaka.
iii. Mshukuru Mungu kwa jinsi alivyosema nawe wakati wa makambi ya Pasaka

Page 10/29
25/04/2023
Omba Mungu akalete badiliko bora katika maisha ya wote waliohudhuria/shiriki katika
makambi ya Pasaka 2023
i. Mwombe Mungu akujalie kutendea kazi yale uliyojifunza katika makambi ya Pasaka
ii. Omba kwa ajili ya badiliko chanya kwa kila aliyehudhuria makambi ya Pasaka
iii. Omba Mungu azidi kuwabariki wote walioshiriki kufanikisha makambi ya Pasaka
26/04/2023
Omba kwa ajili ya Uinjilisti na kukua kwa huduma
i. Ufunguzi wa matawi ya CASFETA, kila shule ya Sekondari ikafikiwe na CASFETA-TAYOMI.
ii. Kampeni za Injili shuleni/vyuoni zikalete matokeo ya wengi kuokolewa.
iii. Mungu ainue wainjilisti wenye mzigo wa kuwafikia watu wenye dhambi.
iv. Ishara miujiza na maajabu vikaambatane nasi tunapopeleka Injili ya Kristo
v. Omba kwa ajili ya wiki ya uinjilisti mwezi Mei
27/04/2023
Ombea wahudumu wa TAYOMI ngazi zote
i. Ujasiri na nguvu ya kuwatumikia vijana na watoto kwa moyo wote.
ii. Wawe na ubunifu na ugunduzi katika kuhudumia kizazi cha sayansi na teknolojia.
iii. Roho ya hekima, maarifa na ufahamu katika kumjua Mungu.
iv. Uvumilivu, imani na moyo wa upendo kwa vijana.
28/04/2023
Omba kwa ajili ya wanafunzi wa Shule za msingi na sekondari
i. Mungu akawape neema ya kuiamini Injili
ii. Kemea/kataa matendo maovu yanayowaandama wanafunzi
iii. Omba kwa ajili ya mitihani mbalimbali shule za sekondari na msingi, Mungu awasaidie
wanafunzi wafaulu vizuri mitihani yao.
iv. Mungu awape ufahamu na uajsiri wa kukataa na kujiepusha na matendo maovu na
yasiyo ya kimaadili.

15-19/05/2023 Arusha, Dodoma, Simiyu, Shinyanga, Njombe

15/05/2023
Omba kwa ajili ya viongozi wote nchi nzima katika ngazi mbalimbali za huduma
i. Uaminifu katika kusimamia maono
ii. Utii kwa Mungu na kwa viongozi wa juu yao
iii. Umoja na mshikamano baina ya viongozi
iv. Mafanikio ya kielimu kwa viongozi

16/05/2023
Omba Uamsho wa Roho Mtakatifu katika CASFETA TAYOMI
i. Tunda la Roho ikawe tabia ya wanachama
ii. Karama za Roho Mtakatifu
Page 11/29
iii. Shauku ya kuomba na kujifunza Neno la Mungu kwa bidii ikazaliwe upya ndani yao
iv. Omba maongozi ya Roho Mtakatifu katika maamuzi.
17/05/2023
Ombea BCF na huduma ya Watoto makanisani
i. Mungu atupe kibali kuwafikia Watoto wengi zaidi kupitia BCF.
ii. Ombea walimu wa Sunday School za Watoto katika makanisa.
iii. Mungu ainue watu wenye mzigo kwa ajili ya kuwahudumia Watoto kwa Injili.
iv. Mungu awaepushe na kuwalinda Watoto dhidi ya vitendo vya unyanyasaji
18/05/2023
Ombea Huduma ya TAYOMI ikue na kuimarika katika ukanda wa pwani
i. Ufunguzi wa matawi zaidi maeneo ya Kisarawe, Handeni, Kilindi, Mkuranga, Mafia, Kibiti,
Rufiji, Lindi, Bagamoyo, Chalinze, Kibaha, Mtwara, Bumbuli, n.k
ii. Mungu atupe walezi na Waratibu wa kulea matawi yatakayofunguliwa.
iii. Ombea wana CASFETA TAYOMI katika maeneo haya; wakue katika imani nakuwa nuru na
chumvi, wawe bora katika elimu, mwenendo na tabia.
19/05/2023
Ombea Huduma ya TAYOMI katika mikoa mipya
i. Mungu akainue watu ambao wapo tayari kujitoa kuhakikisha kazi ya Mungu inaanza na
kuimarika katika maeneo ambayo hayajafikiwa mkoani Njombe.
ii. Ombea Mkoa wa Simiyu, Kazi izidi kukua na kuimarika.
iii. Ombea mafanikio ya kielimu kwa wanaCASFETA wa mikoa ya Njombe na Simiyu.
17-20/06/2023: Viongozi wote (JNLC). Itategemea ratiba za kufunga shule zitakavyokuwa

Jumamosi 17/06/2023: Ombea maendeleo ya huduma ya muda wa kati na mrefu

i. Kila mkoa uwe na ardhi ndani ya miaka mitano (5) ijayo.
ii. Ombea mchakato wa kuandaa master plan ya eneo la Melela Morogoro, Mungu atupe
fedha na watenda kazi hodari na mahiri.
iii. Ombea ujenzi wa Ofisi za Makao Makuu ya TAYOMI mkoani Morogoro.
iv. Ombea ujenzi wa kituo cha mikutano mkoani Morogoro.
v. Ombea ujenzi wa kituo cha Mikutano/shule Mkoani Mbeya.

Jumapili 18/06/2023: Ombea mataifa mbalimbali ambayo yalishiriki kuleta Injili Afrika
(Sweden, Norway, Marekani, Canada, Denmark, Finland n.k)
i. Mungu awajalie uamsho mpya wa nguvu za Roho Mtakatifu.
ii. Mungu akawapiganie dhidi ya uhuru unaokiuka maagizo ya Mungu.
iii. Mungu ainue kizazi kipya cha wamisionari kwa ajili ya kuyafikia mataifa kwa Injili.
iv. Mungu awasaidie kuhusu mmomonyoko wa maadili.
v. Ombea vijana wa mataifa haya Mungu awatoe katika utumwa wa madawa kulevya, ulevi
na uvutaji sigara.
Page 12/29
Jumatatu 19/06/2023: Omba kwa ajili ya afya ya mwili na akili katika taifa
i. Simama kinyume na magonjwa: Kisukari, kansa, presha za kupanda na kushuka, malaria,
vidonda vya tumbo, n.k
ii. Ombea moyo wa kiasi katika utendaji wa shughuli kwa watu ili kuepukana na changamoto
hizo hapo (i) juu.
iii. Kemea vifo vya Watoto wachanga katika taifa.
iv. Omba Mungu atuondolee roho za hofu na mashaka na atuvike roho ya ujasiri na nguvu
v. Simama kinyume na ujinga, umasikini, maradhi, kujipendekeza, upendeleo, rushwa na kila
aina ya uonevu katika taifa.
Jumanne 20/06/2023
Ombea wafanyakazi wa Tanzania
i. Uadilifu ukatawale katika utendaji wao
ii. Ombea madaktari wa Tanzania wakafanye kazi zao kwa moyo wa kujituma
iii. Mungu awalinde dhidi ya hatari zinazoambatana na kazi zao
iv. Ombea ubunifu na ugunduzi katika sekta za mawasiliano, usafirishaji

Julai 31-Agosti 04 Kigoma, Singida, Songwe, Katavi, Zanzibar.

31/07/2023
Mwombe Bwana wa mavuno alete watenda kazi katika shamba lake
i. Mungu ainue watu na watumishi mbalimbali na kuwaleta kushiriki nasi kuhudumia vijana na
watoto.
ii. Ombea ongezeko la walimu wa Neno la Mungu kwa Watoto shuleni na makanisani.
iii. Mungu ainue kizazi kipya cha wachungaji wanaoelewa maono ya TAYOMI.
iv. Mungu ainue kizazi kipya kitakachoendeleza maono ya TAYOMI.

01/08/2023
Omba kwa ajili ya Uinjilisti na kukua kwa huduma
i. Ufunguzi wa matawi ya CASFETA, kila shule ya Sekondari ikafikiwe na CASFETA-TAYOMI.
ii. Kampeni za Injili shuleni/vyuoni zikalete matokeo ya wengi kuokolewa.
iii. Mungu ainue wainjilisti wenye mzigo wa kuwafikia watu wenye dhambi.
iv. Ishara miujiza na maajabu vikaambatane nasi tunapopeleka Injili ya Kristo

02/08/2023
Omba kwa ajili ya watoto
i. Ombea Watoto wanaoishi mazingira magumu.
ii. Ombea uwajibikaji katika familia ili watoto wasitangetange mitaani.
iii. Ombea yatima; Mungu awakumbuke na kuwafungulia milango ya maisha bora.
iv. Mungu awalinde dhidi ya matendo ya unyanyasaji kimwili, kihisia na kiroho.

Page 13/29
03/08/2023
Ombea uwezo wa kutumia akili kwa waaminio na simama kinyume na mafundisho ya uongo
i. Omba kwa ajili matumizi ya akili kwa watu wa Mungu, Mungu awape watu akili na maarifa
ya kupambanua mambo na kujiepusha na ujinga.
ii. Simama kinyume na mahubiri na wahubiri wa uongo; angusha na vunja mbinu za walimu wa
uongo.
iii. Ombea vijana wanaohudumiwa na TAYOMI, Mungu awaepushe wasivutwe na imani za
uongo na mafundisho ya uongo.

04/08/2023
Ombea wahitimu wa vyuo
i. Mungu awafungulie fursa za ajira.
ii. Kwa wanaopenda kujiajiri Mungu akawape kuona fursa mbalimbali za uwekezaji.
iii. Kataa hali za upendeleo na kujuana katika soko la ajira.
iv. Taaluma zao likalifae taifa na kanisa

Agosti 07-11 Wote

07/08/2023
Ombea Shule ya Dr. Mezger Sekondari
i. Mungu akaifanye kuwa shule bora kabisa katika taifa hili.
ii. Mungu akatupe maono, na ubunifu wa kiuendeshaji ili kuifikisha katika viwango vya juu.
iii. Ombea wanafunzi wote wanaojiunga na shule hii wakawe na bidii ya kusoma ili wafaulu.
iv. Ombea walimu na uongozi wa shule, Mungu akawape moyo wa uwajibikaji; kataa uzembe na
uvivu kwa jina la Yesu Kristo.

08/08/2023
Ombea Huduma ya TAYOMI ikue na kuimarika katika ukanda wa pwani
i. Ufunguzi wa matawi zaidi maeneo ya Kisarawe, Handeni, Kilindi, Mkuranga, Mafia, Kibiti,
Rufiji, Lindi, Bagamoyo, Chalinze, Kibaha, Mtwara, Bumbuli, n.k
ii. Mungu atupe walezi na Waratibu wa kulea matawi yatakayofunguliwa.
iii. Ombea wana CASFETA TAYOMI katika maeneo haya; wakue katika imani nakuwa nuru na
chumvi, wawe bora katika elimu, mwenendo na tabia.

09/08/2023
Ombea BCF na huduma ya Watoto makanisani
i. Mungu atupe kibali kuwafikia Watoto wengi zaidi kupitia BCF.
ii. Ombea walimu wa Sunday School za Watoto katika makanisa.
iii. Mungu ainue watu wenye mzigo kwa ajili ya kuwahudumia Watoto kwa Injili.

Page 14/29
10/08/2023
Ombea Huduma ya TAYOMI katika mikoa mipya
i. Mungu akainue watu ambao wapo tayari kujitoa kuhakikisha kazi ya Mungu inaanza na
kuimarika katika maeneo ambayo hayajafikiwa mkoani Njombe.
ii. Ombea Mkoa wa Simiyu na Songwe, Kazi izidi kukua na kuimarika.
iii. Ombea mafanikio ya kielimu kwa wanaCASFETA wa mikoa ya Njombe, Sogwe, Iringa na
Simiyu.
iv. Mungu aimarishe ushirikiano wa Madhehebu ya kipentekoste na TAYOMI.

11/08/2023
Omba kwa ajili ya usalama nchini
i. Usalama katika anga, ardhi na baharini, kemea ajali na uzembe wa waongozaji wa vyombo
vya moto.
ii. Mungu atulinde na majanga ya matetemeko, vimbunga na magonjwa ya mlipuko.
iii. Mungu atuepushe na matishio ya watu wabaya.
iv. Mungu aweke ulinzi katika mipaka yetu.

Agosti 14-18 Baraza la Uongozi la Taifa

14/08/2023
Ombea wahudumu wa TAYOMI ngazi zote
i. Ujasiri na nguvu ya kuwatumikia vijana na watoto kwa moyo wote.
ii. Wawe na ubunifu na ugunduzi katika kuhudumia kizazi cha sayansi na teknolojia.
iii. Roho ya hekima, maarifa na ufahamu katika kumjua Mungu.
iv. Uvumilivu, imani na moyo wa upendo kwa vijana.

15/08/2023
Ombea uhusiano wa Tanzania na mataifa mengine
i. Mungu atupe kuishi kwa amani na mataifa jirani.
ii. Mungu alinde mipaka yetu.
iii. Ushirikiano imara wa kidiplomasia na kibiashara kwa maendeleo ya Tanzania.
iv. Mungu atufungulie masoko kwa ajili ya mazao ya mashambani na bidhaa za viwandani.

16/08/2023
Ombea ushirikiano wa TAYOMI na Serikali
i. Mshukuru Mungu kwa kutuwezesha kutii masharti ya usajili wetu serikalini.
ii. Mshukuru Mungu kwa ushirikiano tunaoupata kwa wakuu wa shule na vyuo nchini.
iii. Mungu azidi kutupa kibali kwa serikali na kuwa mfano wa kuigwa kwa kutii masharti ya usajili.
iv. Ombea viongozi na watendaji wa Wizara ya Elimu, Wizara ya Mambo ya Ndani, Wizara ya
Katiba na Sheria wazidi kudumisha uhuru na haki ya kushiriki masuala ya kiimani kwa
wanafunzi.
Page 15/29
17/08/2023
Ombea ushirikiano wa Huduma kimataifa
i. Omba kwa ajili ya kila taifa ambalo TAYOMI inajulikana, (kwa mfano Norway, USA, Ujerumani,
Uswisi, Afrika ya Kusini, Malawi, Botswana, Zimbabwe, Nigeria n.k) Mungu akafungue milango
zaidi kwa watu wengi kuifahamu huduma na kutoa mkono wa shirika.
ii. Mungu akawaguse watu wa mataifa mbalimbali kuchangia maendeleo ya huduma.
iii. Mungu akaseme na watu ambao hawajawahi kuisikia TAYOMI na awalete kwa ajili ya utumishi
katika TAYOMI.
iv. Mungu atuunganishe na huduma mbalimbali za kipentekoste duniani.

18/07/2023
Omba kwa ajili ya huduma (wahudumu) za (wa) Injili Mataifa mbalimbali: Mungu awatumie na
kuimarisha huduma zao, Mungu akawape ushindi katika changamoto wanazopitia, maono yao
yakathibitike kwa uweza na nguvu za Roho Mtakatifu.
i. Ombea huduma ya Youth with a Mission dunia nzima.
ii. Pastor Gair Johannesen wa Salem Church Norway.
iii. Pastor Siegfried Haussler na Kanisa la Church of God Ujerumani.
iv. Kanisa la Philadelphia Norway.
v. Prayer House Kristiansand Norway.
vi. Ev. Daniel Kolenda na Christ for All Nation.
vii. World Missionary Press

Agosti 21-25 Viongozi wote & BCF

21/08/2023
Ombea Mikutano ya Ibada za Wanafunzi chini ya TAYOMI
i. Mungu akaonekane katika ibada zote za CASFETA na BCF
ii. Wanafunzi waokolewe kupitia ibada hizi
iii. Joint-Fellowship zikawe na nguvu na udhihirisho wa Roho Mtakatifu
iv. Ombea miujiza Ishara na maajabu vikafanyike katika ibada hizi

22/08/2023
Omba kwa ajili ya wazazi na ndugu zako
i. Mungu awabariki katika kazi zao
ii. Mungu awape neema ya kukulea katika njia ifaayo
iii. Mungu awalinde dhidi ya hila za shetani
iv. Omba afya njema kwa familia
23/08/2023
Omba kwa ajili ya Watoto wa Tanzania
i. Mungu awalinde dhidi ya vitendo viovu
Page 16/29
ii. Wawe watii kwa wazazi
iii. Wapende kujifunza neno la Mungu
iv. Wapende masomo shuleni
v. Mungu awasaidie Watoto yatima na kuwalinda
24/08/2023
Ombea BCF na huduma ya Watoto makanisani
i. Mungu atupe kibali kuwafikia Watoto wengi zaidi kupitia BCF.
ii. Ombea walimu wa Sunday School za Watoto katika makanisa.
iii. Mungu ainue watu wenye mzigo kwa ajili ya kuwahudumia Watoto kwa Injili.

25/08/2023

Agosti 28- Septemba 01 Sekretarieti
28/08/2023
Ombea wanaCASFETA mabinti na mabinti wa makanisani:
i. Mungu awape moyo wa utulivu na ufahamu wa kumjua Mungu.
ii. Mungu awaepushe na kuwalinda dhidi ya tamaa na dhidi ya watu wenye tamaa.
iii. Mungu awape kiasi na uvumilivu katika kuungoja wakati wa Bwana uliokubalika.
iv. Mungu ainue wamama wenye ufahamu wa kimungu ili wawati akili vijana wa kike.

29/08/2023
Ombea ushirikiano wa kihuduma kitaifa
i. Ombea huduma ikatambulike nchini pote na Mungu aguse watanzania mbalimbali kushiriki
nasi na kuwekeza katika maono haya.
ii. Mungu awaguse watanzania kujitoa kwa nguvu kuchangia fedha huduma hii.
iii. Ombea wanataaluma wa CASFETA wajisikie kuhusika katika kuchangia fedha huduma hii.

30/08/2023
Omba kwa ajili ya Elimu ya Tanzania
i. Mabadiliko ya mitaala ya Elimu nchini yakamwezeshe mhitimu wa Tanzania kuweza
kushindana katika soko la taaluma na weledi duniani.
ii. Mwombee Waziri wa Elimu aje na sera na mipango ya kuboresha elimu.
iii. Mungu ainue kizazi cha wanafunzi wanaopenda hesabu na sayansi.
iv. Uadilifu katika sekta ya Elimu

Page 17/29
31/08/2023
Ombea kazi ya Huduma ya TAYOMI na Kanisa la Mungu katika Mkoa/Wilaya yako
i. Mungu aimarishe huduma hii iwafikie vijana na kukidhi mahitaji yao sawasawa na mzingira
yao.
ii. Taja changamoto zinazokabili kazi ya Mungu katika eneo lako, omba Mungu ashughulike na
changamoto hizo.
iii. Omba kwa ajili ya viongozi wa Kanisa katika eneo lako.

01/09/2023
Ombea watu mbalimbali walioshiriki na kufanikisha kuanzisha na kuenea huduma ya TAYOMI:
Wataje kwa majina wale unaowafahamu/unaowakumbuka
i. Mungu awakumbuke kwa utumishi wao, akutane na mahitaji yao yote.
ii. Mungu awasaidie wasiiache imani ya kweli katika Kristo Yesu, wale ambao walipotea
dhambini wapate kurudi na kutubu.
iii. Mungu aendelee kuwapa moyo wa kusimamia ushuhuda wa maono haya na kuyasemea
vyema kwa watu wengine.

Septemba 04-08 Sekretarieti

04/09/2023
Ombea uchumi wa nchi
i. Watu wenye akili kama Yusufu wakapate nafasi katika maamuzi ya kiuchumi katika taifa.
ii. Watendaji wa Benki kuu wawajibike kusimamia uimara wa uchumi wa nchi na kudhibiti
mfumuko wa bei.
iii. Sera za kikodi zitekelezwe kwa haki bila kukandamiza wala kuwaonea walipa kodi.
iv. Funga milango ya biashara za magendo mipakani na ndani ya mipaka.

05/09/2023
Ombea maendeleo ya huduma ya muda wa kati na mrefu
i. Kila mkoa uwe na ardhi ndani ya miaka mitano (5) ijayo.
ii. Ombea mchakato wa kuandaa master plan ya eneo la Melela Morogoro, Mungu atupe
fedha na watenda kazi hodari ma mahiri.
iii. Ombea ujenzi wa Ofisi za Makao Makuu ya TAYOMI mkoani Morogoro.
iv. Ombea ujenzi wa kituo cha mikutano mkoani Morogoro.
v. Ombea ujenzi wa kituo cha Mikutano/shule Mkoani Mbeya.

06/09/2023
Ombea wanataaluma wote ambao ni zao la CASFETA TAYOMI
i. Popote walipo wakawe nuru na chumvi ya ulimwengu.
ii. Ombea wajiepushe na rushwa na tamaa za kila namna katika nafasi walizonazo.

Page 18/29
iii. Kwa wale ambao wapo kwenye nafasi za maamuzi watende haki na kuwahudumia watu
kwa moyo bila kutaka fedha ya aibu.
iv. Ombea wanataaluma wote wa CASFETA wakang’are katika utendaji wao, Mungu
akawaamini katika majukumu makubwa zaidi.
v. Omba Mungu akainue wataaluma waliookoka wenye uthubutu kama wa Esta na Daniel
watakaosimama kwa ajili ya ufalme wa Mungu pasipo hofu.

07/09/2023
Omba kwa ajili ya AGM 2023 makambi ya Pasaka 2024
i. Ombea mahudhurio, michango na masomo.
ii. Ombea viongozi wabadilike na kukua kiroho na kiuongozi.
iii. Masomo yenye nguvu za Mungu na yanayoleta mabadiliko kwa vijana na watoto.
iv. Mungu akaongeze idadi ya watu wanaojitolea kuhudumu katika makambi haya.
v. Mungu afungue milango ya fedha kwa ajili ya maandalizi ya makambi yenye ubora.
vi. Mungu afungue milango ya kupata venue nzuri na kwa urahisi.

08/09/2023
Omba kwa ajili ya Mkoa wa Rukwa na Katavi
i. Injili iwafikie vijana waokolewe.
ii. Wanafunzi wajue wajibu wao na wajitambue ili waepukane na mimba za utotoni.
iii. Mungu atufanikishe kuifikia mikoa hii kwa programu za EEMC ili kuleta hamasa kubwa ya
Elimu kwa wanafunzi.
iv. Watendaji wa TAYOMI wakawe msaada kutatua changamoto za kielimu zinazowakabili
wanafunzi katika mikoa hiyo.

Septemba 11-15 Baraza la Waratibu la Taifa

11/09/2023
Mwombe Bwana wa mavuno alete watenda kazi katika shamba lake
i. Mungu ainue watu na watumishi mbalimbali na kuwaleta kushiriki nasi kuhudumia
vijana na watoto.
ii. Ombea ongezeko la walimu wa Neno la Mungu kwa Watoto shuleni na makanisani.
iii. Mungu ainue kizazi kipya cha wachungaji wanaoelewa maono ya TAYOMI.
iv. Watenda kazi wanaotii na kuishi maagizo ya Mungu kama yasemavyo maandiko
matakatifu.
v. Watenda kazi wasiotafuta fedha ya aibu.
12/09/2023
Ombea uwezo wa kutumia akili kwa waaminio na simama kinyume na mafundisho ya uongo
i. Omba kwa ajili matumizi ya akili kwa watu wa Mungu, Mungu awape watu akili na maarifa
ya kupambanua mambo na kujiepusha na ujinga.
Page 19/29
ii. Simama kinyume na mahubiri na wahubiri wa uongo; angusha na vunja mbinu za walimu
wa uongo.
iii. Ombea vijana wanaohudumiwa na TAYOMI, Mungu awaepushe wasivutwe na imani za
uongo na mafundisho ya uongo.
13/09/2023
Omba kwa ajili ya maendelo ya kielimu kwa wanachama na wahudumu wote
i. Mungu atufanikishe katika elimu na taaluma.
ii. Mungu afungue kwa wale wenye milango ya kusoma zaidi.
iii. Walioko masomoni wakamalize kwa ushindi na mafanikio makubwa.
iv. Ombea wanaCASFETA wenye changamoto za ada na matatizo ya kifamili; Mungu
awakumbuke katika shida zao.
14/09/2023
Ombea shule na taasisi za elimu ya juu Tanzania
i. Amani ikatawale katika shule.
ii. Kataa migomo na vurugu katika taasisi za Elimu.
iii. Walimu wawafundishe wanafunzi kwa upendo.
iv. Fahamu za wanafunzi zifunguke ili waelewe masomo yao.
v. Wanafunzi uwezo wakutendea kazi yale mambo wanayojifunza darasani.
vi. Uongozi wa shule/taasisi za elimu usiwe kikwazo kwa Injili.
15/09/2023
Ombea Matawi ya vyuo vikuu
i. Mungu akainue wasomi wenye wito wa kuujenga ufalme wa Mungu.
ii. Ombea wana CASFETA uwezo wa kutumia kwa vitendo maarifa wanayopata vyuoni
iii. Umoja na mshikamno wa mwili wa Kristo katika vyuo vikuu.
iv. Ombea outreach mission za kila chuo.
Septemba 18-22 Kagera, Ruvuma, Dar es salaam/Pwani
18/09/2023
Ombea wanafunzi wenye mahitaji maalum
i. Wapate haki yao ya kujifunza kama wanafunzi wengine.
ii. Ombea jamii kuelewa haki za watu wenye ulemavu.
iii. Ombea walimu wa elimu maalum, waongezeke na watekeleze wajibu wao ipasavyo.
19/09/2023
Ombea uhusiano wa Tanzania na mataifa mengine
i. Mungu atupe kuishi kwa amani na mataifa jirani.
ii. Mungu alinde mipaka yetu.
iii. Ushirikiano imara wa kidiplomasia na kibiashara kwa maendeleo ya Tanzania.
Page 20/29
iv. Mungu atufungulie masoko kwa ajili ya mazao ya mashambani na bidhaa za viwandani.

20/09/2023
Ombea vijana wa kiume wa CASFETA na wa Makanisani
i. Wawe na kiasi na moyo wa kujituma na kukubali majukumu yao.
ii. Waache uvivu na uzembe.
iii. Wawe na bidii katika kuimarisha uhusiano wao na Mungu.
iv. Mungu awape neema ya kujiandaa kwa usahihi kuwa viongozi wa familia.

21/09/2023
Ombea Shule ya Dr. Mezger Sekondari
i. Mungu akaifanye kuwa shule bora kabisa katika taifa hili.
ii. Mungu akatupe maono, na ubunifu wa kiuendeshaji ili kuifikisha katika viwango vya juu.
iii. Ombea wanafunzi wote wanaojiunga na shule hii wakawe na bidii ya kusoma ili wafaulu.
iv. Ombea walimu na uongozi wa shule, Mungu akawape moyo wa uwajibikaji; kataa uzembe
na uvivu kwa jina la Yesu Kristo.
22/09/2023
Omba kwa ajili ya wanamichezo
i. Neema ya Mungu iwafikie hukohuko katika viwanja vya michezo.
ii. Wanamichezo waliookoka wakawe nuru na chumvi kwa wenzao.
iii. Ombea huduma za kupeleka Injili kwa njia ya michezo.
Septemba 25-29 Ofisi ya Rais wa CASFETA
25/09/2023
Ombea ushirikiano wa Huduma kimataifa
i. Omba kwa ajili ya kila taifa ambalo TAYOMI inajulikana, (kwa mfano Norway, USA,
Ujerumani, Uswisi, Afrika ya Kusini, Malawi, Botswana, Zimbabwe, Nigeria n.k) Mungu
akafungue milango zaidi kwa watu wengi kuifahamu huduma na kutoa mkono wa shirika.
ii. Mungu akawaguse watu wa mataifa mbalimbali kuchangia maendeleo ya huduma.
iii. Mungu akaseme na watu ambao hawajawahi kuisikia TAYOMI na awalete kwa ajili ya
utumishi katika TAYOMI.
iv. Mungu atuunganishe na huduma mbalimbali za kipentekoste duniani.
26/09/2023
Omba kwa ajili watu wote waliowahi kuwa viongozi wa CASFETA katika ngazi zote, Taifa,
Mikoa, Wilaya na Matawi.
i. Mungu awaimarishe katika imani, walioacha imani wakarudi tena.
ii. Ombea moto wa kuipenda huduma hii ukawake kwa upya ndani yao.

Page 21/29
iii. Omba Mungu awape mzigo wa kurejea na kutoa kile walichofaidika nacho kuwasaidia
wanaCASFETA wa leo.
27/09/2023
Ombea wanafunzi wa kidato cha nne na cha pili
i. Mungu awasaidie katika masomo yao.
ii. Awape afya njema wanapoelekea mitihani yao.
iii. Mungu awajalie kumbukumbu na akili njema ili wafaulu mitihani yao.
iv. Mungu awape fursa ya kuendelea na masomo kwa ngazi zinazofuata mbele yao.
28/09/2023
Ombea ushirikiano wa kihuduma kitaifa
i. Ombea huduma ikatambulike duniani pote na Mungu aguse watu wa mataifa mbalimbali
kushiriki nasi na kuwekeza katika maono haya.
ii. Mungu awaguse watanzania kujitoa kwa nguvu kuchangia fedha huduma hii.
iii. Ombea wanataaluma wa CASFETA wajisikie kuhusika katika kuchangia fedha huduma hii.

29/09/2023
Ombea wanataaluma wote ambao ni zao la CASFETA TAYOMI
i. Popote walipo wakawe nuru na chumvi ya ulimwengu.
ii. Ombea wajiepushe na rushwa na tamaa za kila namna katika nafasi walizonazo.
iii. Kwa wale ambao wapo kwenye nafasi za maamuzi watende haki na kuwahudumia watu
kwa moyo bila kutaka fedha ya aibu.
iv. Ombea wanataaluma wote wa CASFETA wakang’are katika utendaji wao, Mungu
akawaamini katika majukumu makubwa zaidi.
v. Omba Mungu akainue wataaluma waliookoka wenye uthubutu kama wa Esta na Daniel
watakaosimama kwa ajili ya ufalme wa Mungu pasipo hofu.

Oktoba 02-06 Mbeya, Morogoro, Geita, Manyara

02/10/2023
Ombea shule na taasisi za elimu ya juu Tanzania
i. Amani ikatawale katika shule.
ii. Kataa migomo na vurugu katika taasisi za Elimu.
iii. Walimu wawafundishe wanafunzi kwa upendo.
iv. Fahamu za wanafunzi zifunguke ili waelewe masomo yao.
v. Wanafunzi uwezo wakutendea kazi yale mambo wanayojifunza darasani.
vi. Uongozi wa shule/taasisi za elimu usiwe kikwazo kwa Injili.

03/10/2023
Omba kwa ajili ya umoja, mshikamano na upendo katika huduma
i. Viongozi na wanachama walkawe na utii kwa Mungu.
Page 22/29
ii. Viongozi wa Kanda, Mikoa, Wilaya, Matawi wakatii maagizo kutoka taifani na kuyatekeleza.
iii. Kataa kiburi na ubinafsi katika huduma.
iv. Kemea roho za masengenyo na manung’uniko
v. Simama kinyume na roho ya kukata tamaa katika huduma

04/10/2023
Ombea Huduma ya TAYOMI ikue na kuimarika katika ukanda wa pwani
i. Ufunguzi wa matawi zaidi maeneo ya Kisarawe, Handeni, Kilindi, Mkuranga, Mafia, Kibiti,
Rufiji, Lindi, Bagamoyo, Chalinze, Kibaha, Mtwara, Bumbuli, n.k
ii. Mungu atupe walezi na Waratibu wa kulea matawi yatakayofunguliwa.
iii. Ombea wana CASFETA TAYOMI katika maeneo haya; wakue katika imani nakuwa nuru na
chumvi, wawe bora katika elimu, mwenendo na tabia.
05/10/2023
Ombea Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPCT)
i. Umoja wa mwili wa Kristo udumu
ii. Mungu atuepushe na migogoro makanisani.
iii. Omba unyenyekevu kwa Maaskofu wote na viongozi wakuu wa Makanisa/huduma za
Kipentekoste.
iv. Mungu awajalie viongozi wa Baraza Hekima, Maarifa na Ufahamu wa kimungu zaidi katika
uongozi wao.

06/10/2023
Ombea usalama wa chakula katika nchi
i. Mungu atujalie mvua kwa majira yaliyokubalika.
ii. Nchi ikazae mazao yenye afya.
iii. Mungu atuepushe na baa la njaa.
iv. Ombea wakulima wafanye kazi yao kwa bidi.
v. Mapinduzi yatokee katika sekta ya kilimo.
vi. Kemea na kataa magonjwa ya lishe kwa Watoto wa Tanzania

Oktoba 9-13 Mara, Rukwa, Kilimanjaro, Mwanza

09/10/2023
Ombea huduma ya Muziki na Uimbaji
i. Mungu alete uamsho mkubwa katika uimbaji na muziki kwa utukufu wake.
ii. Uamsho kwa waimbaji na wapiga muziki, wakatumike kwa nguvu za Roho Mtakatifu kwa
viwango vya ajabu.
iii. Ombea mahitaji ya kimaisha ya wanamuziki wa Injili.

Page 23/29
10/10/2023
Omba kwa ajili ya watendaji/wafanyakazi wa kada ya Elimu
i. Ombea walimu wa Shule za awali, msingi na Sekondari, wakufunzi wa vyuo na wahadhiri
wa vyuo vya elimu ya juu.
ii. Ombea watunga sera na wasimamizi wa sera wakajali na kuzingatia ushauri wa
wanataaluma.
iii. Taifa likawekeze katika utafiti na maendeleo.
11/10/2023
Ombea wanaCASFETA mabinti na mabinti wa makanisani:
i Mungu awape moyo wa utulivu na ufahamu wa kumjua Mungu.
ii Mungu awaepushe na kuwalinda dhidi ya tamaa na dhidi ya watu wenye tamaa.
iii Mungu awape kiasi na uvumilivu katika kuungoja wakati wa Bwana uliokubalika.
iv Mungu ainue wamama wenye ufahamu wa kimungu ili wawati akili vijana wa kike.

12/10/2023
Ombea huduma ya Muziki na Uimbaji
i. Mungu alete uamsho mkubwa katika uimbaji na muziki kwa utukufu wake.
ii. Uamsho kwa waimbaji na wapiga muziki, wakatumike kwa nguvu za Roho Mtakatifu kwa
viwango vya ajabu.
iii. Ombea mahitaji ya kimaisha ya wanamuziki wa Injili.

13/10/2023
Ombea wahitimu wa vyuo
i. Mungu awafungulie fursa za ajira.
ii. Kwa wanaopenda kujiajiri Mungu akawape kuona fursa mbalimbali za uwekezaji.
iii. Kataa hali za upendeleo na kujuana katika soko la ajira.

Oktoba 16-20 Mtwara & Lindi, Kigoma, Tabora, Tanga, Iringa.

16/10/2023
Ombea Mikutano ya Ibada za Wanafunzi chini ya TAYOMI
i. Mungu akaonekane katika ibada zote za CASFETA na BCF.
ii. Wanafunzi waokolewe kupitia ibada hizi.
iii. Joint-Fellowship zikawe na nguvu na udhihirisho wa Roho Mtakatifu.
iv. Ombea miujiza Ishara na maajabu vikafanyike katika ibada hizi.
17/10/2023
Omba kwa ajili ya watendaji/wafanyakazi wa kada ya Elimu
i. Ombea walimu wa Shule za awali, msingi na Sekondari, wakufunzi wa vyuo na wahadhiri wa
vyuo vya elimu ya juu.
ii. Ombea watunga sera na wasimamizi wa sera wakajali na kuzingatia ushauri wa
wanataaluma.
iii. Taifa likawekeze katika utafiti na maendeleo.
Page 24/29
18/10/2023
Ombea wanaCASFETA mabinti na mabinti wa makanisani
i. Mungu awape moyo wa utulivu na ufahamu wa kumjua Mungu.
ii. Mungu awaepushe na kuwalinda dhidi ya tamaa na dhidi ya watu wenye tamaa.
iii. Mungu awape kiasi na uvumilivu katika kuungoja wakati wa Bwana uliokubalika.
iv. Mungu ainue wamama wenye ufahamu wa kiMungu ili wawatie akili vijana wa kike.

19/10/2023
Ombea shule na taasisi za elimu ya juu Tanzania
i. Amani ikatawale katika shule.
ii. Kataa migomo na vurugu katika taasisi za Elimu.
iii. Walimu wawafundishe wanafunzi kwa upendo.
iv. Fahamu za wanafunzi zifunguke ili waelewe masomo yao.
v. Wanafunzi uwezo wakutendea kazi yale mambo wanayojifunza darasani.
vi. Uongozi wa shule/taasisi za elimu usiwe kikwazo kwa Injili.

20/10/2023
Ombea watumishi wa Mungu wa Madhehebu ya Kipentekoste na Waratibu wa TAYOMI
i. Ombea Watoto wao wakue wakimjua Mungu wa kweli sawasawa na utumishi wa wazazi
wao.
ii. Kataa hali ya kukata tamaa kwa waratibu wote, omba Mungu akahuishe upya wito wao
ndani ya TAYOMI.
iii. Mungu awape neema ya maarifa ya kuweza kubalance huduma na kutunza familia zao.

Oktoba 23-27 Arusha, Dodoma, Simiyu, Shinyanga, Njombe

23/10/2023
Ombea maadili katika taifa
i. Mungu atoe kibali sauti ya Mkakati wa EEMC isikike kila kona ya nchi hii.
ii. Ombea kupitia EEMC wengi wavutwe na wamjue Mungu na kubadili mwenendo.
iii. Kataa na simama kinyume dhidi ya matendo yote ambayo ni kinyume na maadili ya katika
taifa: wizi, ulevi, ubakaji, ibada ya sanamu, uzinzi, uongo, ulafi, uongozi mbovu, uzembe,
uvivu, upuuzi, mizaha, ulawiti, rushwa, n.k,
24/10/2023
Omba kwa ajili watu wote waliowahi kuwa viongozi wa CASFETA katika ngazi zote, Taifa,
Mikoa, Wilaya na Matawi
i. Mungu awaimarishe katika imani, walioacha imani wakarudi tena,
ii. Ombea moto wa kuipenda huduma hii ukawake kwa upya ndani yao,
iii. Omba Mungu awape mzigo wa kurejea na kutoa kile walichofaidika nacho kuwasaidia
wanaCASFETA wa leo.

Page 25/29
25/10/2023
Ombea mataifa mbalimbali ambayo yalishiriki kuleta Injili Afrika
(Sweden, Norway, Marekani, Canada, Denmark, Finland n.k)
i. Mungu awajalie uamsho mpya wa nguvu za Roho Mtakatifu.
ii. Mungu akawapiganie dhidi ya uhuru unaokiuka maagizo ya Mungu.
iii. Mungu ainue kizazi kipya cha wamisionari kwa ajili ya kuyafikia mataifa kwa Injili.
iv. Mungu awasaidie kuhusu mmomonyoko wa maadili.
v. Ombea vijana wa mataifa haya Mungu awatoe katika utumwa wa madawa kulevya, ulevi
na uvutaji sigara.
26/10/2023 Ombea wanataaluma wote ambao ni zao la CASFETA TAYOMI
i. Popote walipo wakawe nuru na chumvi ya ulimwengu.
ii. Ombea wajiepushe na rushwa na tamaa za kila namna katika nafasi walizonazo.
iii. Kwa wale ambao wapo kwenye nafasi za maamuzi watende haki na kuwahudumia watu kwa
moyo bila kutaka fedha ya aibu.
iv. Ombea wanataaluma wote wa CASFETA wakang’are katika utendaji wao, Mungu
akawaamini katika majukumu makubwa zaidi.
v. Omba Mungu akainue wataaluma waliookoka wenye uthubutu kama wa Esta na Daniel
watakaosimama kwa ajili ya ufalme wa Mungu pasipo hofu.

27/10/2023
Ombea Mikutano ya Ibada za Wanafunzi chini ya TAYOMI
i. Mungu akaonekane katika ibada zote za CASFETA na BCF
ii. Wanafunzi waokolewe kupitia ibada hizi.
iii. Joint-Fellowship zikawe na nguvu na udhihirisho wa Roho Mtakatifu.
iv. Ombea miujiza Ishara na maajabu vikafanyike katika ibada hizi

Oktoba 30-Novemba 03 Wote

30/10/2023
Ombea wafanyakazi Waliookoka katika maeneo mbalimbali ya kazi
i. Wakatende kwa uaminifu, bidii na weledi.
ii. Mungu awalinde dhidi ya uonevu katika maeneo yao ya kazi.
iii. Mungu awakumbuke ambao wanastahili kupandishwa vyeo lakini hawajapata haki yao kwa
muda mrefu.
iv. Waliofukuzwa kazi kwa uonevu wakarudishwe kazini.
31/10/2023
Ombea wanafunzi wa kidato cha nne na cha pili
i. Mungu awasaidie katika masomo yao.
ii. Awape afya njema wanapoelekea mitihani yao.
iii. Mungu awajalie kumbukumbu na akili njema ili wafaulu mitihani yao.
iv. Mungu awape fursa ya kuendelea na masomo kwa ngazi zinazofuata mbele yao.

Page 26/29
01/10/2023
Omba Uhuru wa kujieleza na uhuru wa vyombo vya habari ukatumike kwa utukufu wa Mungu
i. Ombea Uhuru wa kuhubiri Injili shuleni/vyuoni uendelee.
ii. Ombea uhuru wa vyombo vya habari ukatumike kupeleka Injili ya Kristo.
iii. Ombea Wizara ya Elimu izidi kuwa na ushirikiano mzuri na taasisi zinazopeleka Injili kwa
wanafunzi.

02/10/2023
Ombea Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPCT)
i. Amani umoja na mshikamano vikatawale baina ya Madhehebu/huduma wanachama.
ii. Mipango ya ujenzi wa ofisi za makao makuu ya CPCT ukafanikiwe.
iii. Kila mwanachama akawajibike kuchangia ujenzi wa ofisi kama ilivyopangwa na Baraza
iv. Viongozi wa Baraza wakawe na kibali kwa Mungu na Wanadamu.

03/10/2023
Ombea maadili katika taifa
i. Mungu atoe kibali sauti ya Mkakati wa EEMC isikike kila kona ya nchi hii.
ii. Ombea kupitia EEMC wengi wavutwe na wamjue Mungu na kubadili mwenendo.
iii. Kataa na simama kinyume dhidi ya matendo yote ambayo ni kinyume na maadili ya katika
taifa: wizi, ulevi, ubakaji, ibada ya sanamu, uzinzi, uongo, ulafi, uongozi mbovu, uzembe,
uvivu, upuuzi, mizaha, ulawiti, rushwa, n.k,

Novemba 06-10 Kigoma, Singida, Songwe, Katavi, Zanzibar

06/11/2023
Omba kwa ajili vyombo vya dola
i. Majeshi ya ulinzi, Mungu akawape moyo wa uzalendo na uaminifu katika kulinda mipaka ya
nchi yetu.
ii. Ombea jeshi la polisi; Mungu awalinde na kuwapa ushindi wanapopambana na uhalifu.
iii. Nidhamu na uwajibikaji vitawale.
iv. Kemea rushwa na roho ya kupenda fedha.

07/11/2023
Ombea wafanyakazi wa Tanzania
i. Uadilifu ukatawale katika utendaji wao.
ii. Ombea madaktari wa Tanzania wakafanye kazi zao kwa moyo wa kujituma
iii. Mungu awalinde dhidi ya hatari zinazoambatana na kazi zao.
iv. Ombea ubunifu na ugunduzi katika sekta za mawasiliano, usafirishaji

Page 27/29
08/11/2023
Ombea kazi ya Huduma ya TAYOMI na Kanisa la Mungu katika Mkoa/Wilaya yako
i. Mungu aimarishe huduma hii iwafikie vijana na kukidhi mahitaji yao sawasawa na mzingira
yao.
ii. Taja changamoto zinazokabili kazi ya Mungu katika eneo lako, omba Mungu ashughulike na
changamoto hizo.
iii. Omba kwa ajili ya viongozi wa Kanisa katika eneo lako.

09/11/2023
Omba kwa ajili ya Elimu ya Tanzania
i. Mabadiliko ya mitaala ya Elimu nchini yakamwezeshe mhitimu wa Tanzania kuweza
kushindana katika soko la taaluma na weledi duniani.
ii. Mwombee Waziri wa Elimu aje na sera na mipango ya kuboresha elimu
iii. Mungu ainue kizazi cha wanafunzi wanaopenda hesabu na sayansi.

10/11/2023
Omba kwa ajili ya maendelo ya kielimu kwa wanachama na wahudumu wote
i. Mungu atufanikishe katika elimu na taaluma.
ii. Mungu afungue kwa wale wenye milango ya kusoma zaidi.
iii. Walioko masomoni wakamalize kwa ushindi na mafanikio makubwa.
iv. Ombea wanaCASFETA wenye changamoto za ada na matatizo ya kifamili; Mungu
awakumbuke katika shida zao.

Novemba 13-17 Viongozi wote

13/11/2023
Ombea Mahitaji yako binafsi
i. Ombea familia yako, kanisa lako, Mchungaji wako.
ii. Ombea huduma, vipawa/karama ulizopewa na Mungu zitumike kwa utukufu wake.
iii. Ombea mahitaji mengine sawasawa na unavyohitaji kutoka kwa Bwana.
14/11/2023
Ombea Waratibu wote na familia zao
i. Mungu awalinde, awazidishe na kuwaongeza kiroho,
ii. Mungu azidi kuwapa wito wa kumtumikia kwa furaha katika huduma hii
iii. Ombea uchumi wao, Mungu akakutane na mahitaji yao yote,
iv. Mungu awafungulie milango ya baraka ili wafanikiwe katika kazi zao, katika biashara, zao,
katika kila walifanyalo.
v. Omba Mungu awape macho ya kuona fursa mbalimbali za uwekezaji ili wainue pato lao na
familia zao kiuchumi.

Page 28/29
15/11/2023
Ombea vikao na makongamano ya Huduma
i. Vikao vya viongozi vifikie maamuzi yenye manufaa kwa ufalme wa Mungu.
ii. Ombea Makongamano ya JNLC na AGM: Mahudhurio, michango, Mafundisho, warsha na
semina.
iii. Ombea safari za wajumbe wa mikutano/vikao hivi.
iv. Mungu atuwezeshe kwa rasilimali, ujuzi na maarifa katika kutekeleza maamuzi ya vikao vya
huduma.
v. Kila mwenye hoja/jambo/maoni ya kufanikisha huduma ya mwili wa Kristo akawe tayari
kushirikisha wengine.

16/11/2023
Ombea vijana wa kiume wa CASFETA na wa Makanisani
i. Wawe na kiasi na moyo wa kujituma na kukubali majukumu yao.
ii. Waache uvivu na uzembe.
iii. Wawe na bidii katika kuimarisha uhusiano wao na Mungu.
iv. Mungu awape neema ya kujiandaa kwa usahihi kuwa viongozi wa familia.

17/11/2023
Ombea mahitaji binafsi
i. Omba ulinzi wa Mungu juu yako na familia yako: Mungu akulinde dhidi ya watu wabaya,
akulinde dhidi ya magonjwa, akulinde dhidi ya ajali za kila namna, akuepushe na watu
wabaya.
ii. Omba ulinzi dhidi ya mishale yote ya yule mwovu, Bwana akatupe ngao ya imani tuweze
kuizima mishale yote ya adui.
iii. Ombea ndugu zako, familia yako, marafiki, n.k
iv. Ombea mahitaji mbalimbali ya watumishi wengine wa TAYOMI.

Novemba 20-24 Sekretarieti

20/11/2023
Omba kwa ajili vyombo vya dola
i. Majeshi ya ulinzi, Mungu akawape moyo wa uzalendo na uaminifu katika kulinda mipaka ya
nchi yetu.
ii. Ombea jeshi la polisi; Mungu awalinde na kuwapa ushindi wanapopambana na uhalifu.
iii. Wasiwashitaki watu kwa uongo.
iv. Wasishiriki katika uhalifu.
v. Kemea rushwa na roho ya kupenda fedha kwenye vyomba vya dola.

21/11/2023
Ombea wanataaluma wote ambao ni zao la CASFETA TAYOMI
i. Popote walipo wakawe nuru na chumvi ya ulimwengu.
Page 29/29
ii. Ombea wajiepushe na rushwa na tamaa za kila namna katika nafasi walizonazo.
iii. Kwa wale ambao wapo kwenye nafasi za maamuzi watende haki na kuwahudumia watu kwa
moyo bila kutaka fedha ya aibu.
iv. Ombea wanataaluma wote wa CASFETA wakang’are katika utendaji wao, Mungu
akawaamini katika majukumu makubwa zaidi.
v. Omba Mungu akainue wataaluma waliookoka wenye uthubut

22/11/2023
Ombea Injili iwafikie watu wote katika taifa letu:
i. Ombea Mikutano yote ya Outreach za wanaCASFETA nchini
ii. Omba Mungu watu wengi wakaokolewe kupitia huduma hizi.
iii. Mungu akajenge umoja na mshikamano kati ya TAYOMI na Madhehebu katika kupeleka
Injili.
iv. Mungu akainue miongoni mwa wanaCASFETA wahubiri wakubwa wenye mzigo wa
kuwafikia wenye dhambi kwa Injili.

23/11/2023
Ombea Shule ya Dr. Mezger Sekondari
i. Ombea uaminifu kwa wafanyakazi, usalama wa shule na mali za shule.
ii. Omba Mungu alete wanafunzi wengi zaidi katika shule hii kwa mwaka 2024.
iii. Omba Mungu aguse watu na mashirika mbalimbali kuwekeza katika shule hii.
iv. Ombea nidhamu ya wanafunzi na wafanyakazi.
v. Ombea ufadhili wa masomo unaotolewa na TAYOMI ukawe endelevu na kuwafaidisha
watoto wakitanzania wengi zaidi.

24/11/2023
Omba kwa ajili ya maendelo ya kielimu kwa wanachama na wahudumu wote
i. Mungu atufanikishe katika elimu na taaluma.
ii. Mungu afungue kwa wale wenye uhitaji milango ya kusoma zaidi.
iii. Walioko masomoni wakamalize kwa ushindi na mafanikio makubwa.
iv. Ombea wanaCASFETA wenye changamoto za ada na matatizo ya kifamilia; Mungu
awakumbuke katika shida zao.
v. Waliofeli na kukata tamaa warudi tena katika masomo na wafanye vizuri

Novemba 27-01Desemba Baraza la Uongozi la Taifa.

27/11/2023
Ombea wafanyakazi Waliokoka katika maeneo mbalimbali ya kazi
i. Wakatende kwa uaminifu, bidii na weledi.
ii. Mungu awalinde dhidi ya uonevu makazini.
iii. Mungu awakumbuke ambao wanastahili kupandishwa vyeo lakini hawajapata haki yao kwa
muda mrefu.

Page 30/29
iv. Waliofukuzwa kazi kwa uonevu wakarudishwe kazini.

28/11/2023
Ombea shule na taasisi za elimu ya juu Tanzania
i. Amani ikatawale katika shule.
ii. Kataa migomo na vurugu katika taasisi za Elimu.
iii. Walimu wawafundishe wanafunzi kwa upendo.
iv. Fahamu za wanafunzi zifunguke ili waelewe masomo yao.
v. Wanafunzi uwezo wakutendea kazi yale mambo wanayojifunza darasani.
vi. Uongozi wa shule/taasisi za elimu usiwe kikwazo kwa Injili.

29/11/2023
Ombea ndoa za waaminio
i. Amani ikatawale.
ii. Akili na maarifa vikaongoze ndoa.
iii. Watoto wakalelewe katika maisha bora yenye mafanikio kiroho, kielimu, kihisia na
kiufahamu.

30/11/2023
Omba kwa ajili ya viongozi wa kitaifa wa TAYOMI
i. Mungu awaongoze katika kusimamia maono haya
ii. Mungu azidi kuwatumia kwa karama za Roho Mtakatifu
iii. Mungu awalinde na kuwaepusha na kila hila za adui shetani
iv. Mungu awalinde dhidi ya kiburi na awape unyenyekevu
v. Ombea familia zao

01/12/2023
Ombea marafiki wa TAYOMI ndani na nje ya Tanzania
i. Ombea wadau wote wa TAYOMI ambao wamekuwa wakisaidia huduma hii kifedha Mungu
awakumbuke katika maisha yao na kuwazidishia zaidi pale walipotoa.
ii. Mungu ainue watu zaidi ndani ya Tanzania watakowekeza katika ufalme wa Mungu kupitia
TAYOMI.
iii. Mungu aguse wanaCASFETA waliotawanyika duniani pote kusapoti huduma kwa mali zao.

Desemba 04-08 Kamati Kuu TAYOMI

04/12/2023
Ombea vijana wa kiume wa CASFETA na wa Makanisani
i. Wawe na kiasi na moyo wa kujituma na kukubali majukumu yao.
ii. Waache uvivu na uzembe.

Page 31/29
iii. Wawe na bidii katika kuimarisha uhusiano wao na Mungu.
iv. Mungu awape neema ya kujiandaa kwa usahihi kuwa viongozi wa familia
05/12/2023
Ombea Huduma katika mkoa wa Manyara, Singida, Shinyanga
i. Mungu akalete walezi katika ngazi za matawi.
ii. Mungu atupatie timu imara za Waratibu.
iii. Mungu afuafue kazi katika mkoa wa Shinyanga.

06/12/2023
Omba kwa ajili ya maendelo ya kielimu kwa wanachama na wahudumu wote
vi. Mungu atufanikishe katika elimu na taaluma.
vii. Mungu afungue kwa wale wenye uhitaji milango ya kusoma zaidi.
viii. Walioko masomoni wakamalize kwa ushindi na mafanikio makubwa.
ix. Ombea wanaCASFETA wenye changamoto za ada na matatizo ya kifamilia; Mungu
awakumbuke katika shida zao.

07/12/2023
Ombea ushirikiano wa kihuduma kimataifa
i. Ombea huduma ikatambulike duniani pote na Mungu aguse watu wa mataifa mbalimbali
kushiriki nasi na kuwekeza katika maono haya.
ii. Mungu awaguse watu/huduma/madhehebu mbalimbali ya nje ya Tanzania kushiriki nasi
kihuduma na kuchangia huduma fedha.
iii. Mungu atufungulie mlango na huduma/asasi mbalimbali za kipentekoste duniani.

08/12/2023
Omba kwa ajili ya watoto
i. Ombea Watoto wanaoishi mazingira magumu.
ii. Ombea uwajibikaji katika familia ili watoto wasitangetange mitaani.
iii. Ombea yatima; Mungu awakumbuke na kuwafungulia milango ya maisha bora.
iv. Mungu awalinde dhidi ya matendo ya unyanyasaji kimwili, kihisia na kiroho.

Desemba 11-15 Viongozi wote

11/12/2023
Mshukuru Mungu kwa utendaji wa mwaka 2023
i. Mshukuru Mungu kwa kutufanikisha katika matukio yote ya kitaifa: Easter Conference,
JNLC, AGM, Faith Building, ACTION Plan, Harvest Plan, Education Motivation, Gospel
missions n.k,
ii. Mshukuru Mungu kwa mafanikio ya wana CASFETA, kielimu, kiroho, kiuchumi, n.k,

Page 32/29
iii. Mshukuru Mungu kwa kadiri alivyokutendea katika mwaka 2023
12/12/2023
Omba kwa ajili ya Uinjilisti na kukua kwa huduma
i. Ufunguzi wa matawi ya CASFETA, kila shule ya Sekondari ikafikiwe na CASFETA-TAYOMI.
ii. Kampeni za Injili shuleni/vyuoni zikalete matokeo ya wengi kuokolewa.
iii. Mungu ainue wainjilisti wenye mzigo wa kuwafikia watu wenye dhambi.
iv. Ishara miujiza na maajabu vikaambatane nasi tunapopeleka Injili ya Kristo.

13/12/2023
Omba uamsho katika kanisa la Kristo
i. Kataa na simama kinyume na hali ya kupoa kwa kanisa
ii. Omba Mungu akaliongeze kanisa kiidadi na kiroho pia
iii. Mungu amimine Roho wake zaidi juu ya waaminio
iv. Omba mongozi ya Roho Mtakatifu kwa waaminio
v. Waaminio wakawe watii kwa maongozi ya Roho Mtakatifu
14/12/2023
Omba kwa ajili ya makambi ya Pasaka 2024
i. Mungu azidi kutupa ufunuo na ujumbe mahususi kwa mwaka 2024.
ii. Ongezeko la wanachama wanaohudhuria makambi (mafuriko).
iii. Omba nguvu za roho mtakatifu na ishara na maajabu katika makambi ya Pasaka 2024.
iv. Omba kwa ajili ya walimu watakaofundisha, Mungu awatumie kwa utukufu wake.
v. Mungu afanikishe mipango yote ya maandalizi.

15/12/2023
A. Omba kwa ajili ya utendaji wa huduma mwaka 2024
i. Kila kongozi akasimame katika zamu yake
ii. Mungu atupe neema ya kuweka bidii katika utendaji
iii. Mungu atungoze kupitia Roho wake Mtakatifu tukatende mapenzi yake katika mwaka
2024
iv. Mwombe Mungu azidi kufungua milango ya fedha kwa ajili ya utendaji wa kazi ya huduma

B. Mshukuru Mungu kwa kumaliza mbio za maombi haya

i. Mshukuru Mungu kwa mahitaji yote tulioyaombea
ii. Toa sadaka yako ya shukurani kwa kufuata utaratibu ufuatao;
a) Kila mmoja (Waratibu, walezi, viongozi wote na wanachama wote katika mikakati
yote ya TAYOMI) anaweza kutoa sadaka yake yeye mwenyewe moja kwa moja
kwenye Lipa namba za huduma zifuatazo:

Page 33/29
MPESA: 003003 Jina TANZANIA YOUTH MINISTRIES
TIGOPESA: 332332 Jina CASFETA TAYOMI
AIRTEL MONEY: 946555 Jina TAYOMI

b) Au Kiongozi wa tawi/wilaya atakusanya sadaka za wanachama wa CASFETA wa

tawi na kuzituma kwa simu kwa Lipa namba kama zinavyoonekana hapo (a) juu.
c) Namba ya kumbukumbu ya malipo (reference number) andika neno SHUKURANI
ikifuatiwa na jina lako au namba yako ya uanachama (kama umeshapata namba).
d) Kama Sadaka za tawi zitatumwa kwa pamoja andika namba ya kumbukumbu
SHUKURANI ikifuatiwa na Jina la tawi.
******************************************************************************
Wenu katika Kristo Yesu,
Isaya Raphael Mwanyamba
Mkurugenzi Mtendaji
Tanzania Youth Ministries
January 2023
#Christocentric IQ

Page 34/29

You might also like