You are on page 1of 48

TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA ILANI YA

UCHAGUZI YA CCM MWAKA 2015 – 2020


KATIKA JIMBO LA BUSANDA
2
YALIYOMO
1.UTANGULIZI ...................................................................................... 4
1.1 ENEO LA JIMBO LA BUSANDA NA IDADI YA ................. 5
1.2 HALI YA KISIASA .......................................................................... 6
1.3 UWAKILISHI ................................................................................... 6
2.MIRADI ILIYOTEKELEZWA .............................................................. 9
2.1 SEKTA YA AFYA ......................................................................... 10
2.1.1 UJENZI WA HOSPITALI ........................................................... 10
2.1.2 UPATIKANAJI WA GARI LA WAGONJWA........................ 12
2.1.3 UJENZI WA KITUO CHA AFYA NYARUGUSU .................... 13
2.1.4 UBORESHAJI WA KITUO CHA AFYA .................................. 15
2.1.5 UKARABATI WA VITUO VYA AFYA KWA ........................... 16
2.1.6 UKAMILISHAJI WA ZAHANATI ZA INYALA, ....................... 18
2.2 SEKTA YA ELIMU ........................................................................ 20
2.2.1 Mpango wa Elimu Bure ...................................................... 20
2.3. SEKTA YA MADINI .................................................................... 24
2.3.1 Ujenzi wa kituo cha wachimbaji cha ............................. 25
2.3.2 kushiriki na kupitisha marekebisho ya ............................. 25
2.3.3 Kutunga Sheria ya umiliki wa wananchi ....................... 26
2.4 SEKTA YA NISHATI...................................................................... 27
2.4.1 Mradi wa KV 220 Bulyanghulu – Geita ........................... 28
2.4.2 Mradi wa REA III .................................................................... 28
2.6 SEKTA YA MAJI .......................................................................... 37
2.6.1 Mradi wa Maji Chankorongo ............................................ 37
2.6.2 Mradi wa Maji Nyakagomba ............................................ 38
2.6.3 Miradi ya maji kupitia wadau wa .................................... 39
2.6.4 Mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria - ............................. 39
2.7 MICHEZO .................................................................................... 40
2.8 USHIRIKI KATIKA SHUGHULI ZA KIJAMII NA .......................... 40
2.8.1 FEDHA ZA MFUKO WA JIMBO ............................................ 43
3.SHUKRANI ....................................................................................... 44
MIRADI YA KIMKAKATI KATIKA JIMBO LA .................................. 47

3
TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA ILANI YA UCHAGUZI
YA CCM MWAKA 2015 – 2020 KATIKA JIMBO LA
BUSANDA

1.UTANGULIZI
Napenda kuchukua fursa hii kumshukuru
Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehema kwa
kunijalia afya njema na kuniwezesha kutekeleza
majukumu yangu ya kuwatumikia wananchi
katika Jimbo la Busanda.
Kwa heshima kubwa naomba kumpongeza Mhe
Rais wetu mpendwa Dkt John Pombe Joseph
Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama
Cha Mapinduzi (CCM) Taifa kwa uongozi wake
imara wenye weledi na umakini katika
kusimamia utekelezaji wa Ilani ya CCM ya
Mwaka 2015 ambao umeiwezesha Nchi yetu
kupiga hatua zaidi kimaendeleo.
Kipekee kabisa ninawapongeza ninyi viongozi
wote wa CCM kuanzia ngazi ya
Taifa,Mkoa,Wilaya, Kata, Matawi mpaka shina
na viongozi wote ndani ya Jimbo la Busanda
kwa hekima na busara mnazotumia kukiongoza
Chama Chetu ndani ya Jimbo hili. Maoni, ushauri
na ushirikiano mnaonipatia umeniwezesha
kutekeleza majukumu yangu kikamilifu.
4
Naomba kuchukua fursa hii kuwapongeza
Wananchi wote wa Jimbo la Busanda kwa
kufanya kazi kwa bidii na kuunga mkono Serikali
hasa wakati wa utekelezaji wa miradi mbalimbali
ya Maendeleo. Aidha ninawashukuru sana kwa
heshima kubwa mliyonipatia kuwa Mbunge
kwenye Jimbo la Busanda na ndiyo maana
nawakilisha taarifa hii.
Baada ya kusema hayo sasa ninaomba kutoa
maelezo ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha
Mapinduzi katika Jimbo la Busanda kwa kipindi
cha miaka mitano kuanzia 2015 hadi 2020 kama
ifuatavyo.

1.1 ENEO LA JIMBO LA BUSANDA NA IDADI YA


WATU
Jimbo la Busanda lipo mkoani Geita katika
Halmashauri ya Wilaya ya Geita. Limepakana
na Wilaya za Chato, Mbogwe, Kahama na
Nyanghwale vilevile limepakana na ziwa
Victoria katika maeneo ya Bukondo,
Chankorongo Lulama, Nyakasenya,
Kasanghwa na Nungwe. Jimbo limeundwa na
Mamlaka ya Mji mdogo wa Katoro, tarafa 2
ambazo ni Busanda na Butundwe na jumla ya
kata 22 ambazo ni Butobela, Bukoli, Bujula,
Nyamalimbe, Kamena, Nyalwanzaja,
Nyarugusu, Nyaruyeye, Nyakamwaga,
5
Busanda Lwamgasa, Kaseme, Magenge,
Katoro, Ludete, Nyamigota, Nyakagomba,
Chigunga, Nyamwilolelwa, Butundwe,
Nyachiluluma na Bukondo.
Jimbo la Busanda lina jumla ya vijiji 83 na
vitongoji 367. Kutokana na sensa ya mwaka
2012 kuna Jumla ya watu laki sita. Shughuli za
kiuchumi zilizopo ni pamoja na kilimo, ufugaji,
ujasiriamali, uvuvi, ulinaji asali na uchimbaji wa
madini.

1.2 HALI YA KISIASA


Hali ya kisiasa katika Jimbo la Busanda ni
shwari. Chama cha Mapinduzi kinaendelea
kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya
Mwaka 2015 – 2020. Na hii ni kutokana na
uwepo wa Madiwani wote wa Kata 22 na
madiwani 7 wa Viti Maalum wote kutokana na
CCM.

1.3 UWAKILISHI
Kwa mujibu wa Ibara ya 61 ya Katiba ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jukumu la
Msingi la Mbunge ni Uwakilishi wa Wananchi,
kutunga sheria na kuisimamia Serikali ili iweze
kutekeleza majukumu yake kwa wananchi
kwa ufanisi.

6
Kwa madhumuni haya kwa miaka mitano
ziara mbalimbali zimefanyika ndani ya Jimbo
la Busanda katika kata zote 22 na jumla ya vijiji
83. Wananchi waliwasilisha kero zao katika
mikutano ya hadhara, vikundi vya kijamii
ikiwemo vikundi vya vijana, wajasiriamali,
vikundi vya wanawake, wafanyabiashara,
wachimbaji, madiwani, makongamano
mbalimbali yakiwemo ya kidini kwa lengo
kubwa kujua changamoto zinazowakabili
wananchi. Wananchi walipata fursa za kuuliza
maswali na kutoa hoja zao mbalimbali.
Kutokana na maswali hayo tulifanikiwa kubaini
kero na changamoto mbalimbali
zinazowakabili wananchi kwa ujumla.
Uwasilishaji wa kero mbalimbali za wananchi
kwenye ngazi mbalimbali za maamuzi
umefanyika. Katika ngazi ya Halmashauri kwa
kushirikiana na Waheshimiwa Madiwani kero
mbalimbali ziliwasilishwa.
Kwa ngazi ya Serikali kuu kupitia Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa
kipindi cha miaka mitano nimetekeleza wajibu
wangu kwa kuuliza maswali mbalimbali
yanayohusu umma hasa yanayogusa maslahi
ya wananchi katika Jimbo la Busanda, Wilaya,
Mkoa wa Geita na Tanzania kwa
ujumla.Michango katika hotuba mbalimbali
7
ilifanyika na maswali mbalimbali yakijumuisha
ya msingi na ya nyongeza yaliulizwa.
Michango hiyo imeiwezesha Serikali kujua
Changamoto zinazowakabili Wananchi pia
kuzitafutia ufumbuzi kero hizo. Serikali kuu kwa
kushirikiana na Halmashauri zimeendelea
kuzifanyia kazi changamoto zote hatua kwa
hatua jambo ambalo limesaidia miradi
mbalimbali kutekelezeka na huduma Serikalini
kuimarika. Kazi zingine ni pamoja na Kujadili
utekelezaji na bajeti za kila wizara wakati wa
mkutano wa Bunge wa kila mwaka wa bajeti
na kushiriki katika kutunga sheria.

Moja ya picha nikiwa bungeni wakati nachangia


hoja

8
Waziri mkuu alipotembelea jimboni Busanda

2.MIRADI ILIYOTEKELEZWA
Utekelezaji wa miradi ya Maendeleo ndani ya
Jimbo la Busanda ulizingatia Dira ya Taifa ya
Maendeleo ya Mwaka 2025 yenye malengo ya
kujenga uchumi wa viwanda na kufikia uchumi
wa Kati ifikapo 2025. Ilani ya Uchaguzi ya Mwaka
2015, Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa
Miaka mitano, Ahadi mbalimbali za Viongozi wa
Kitaifa, Ahadi Binafsi za Mbunge na mipango ya
kimkakati inayobuniwa na wananchi vijijini. Hivyo
utekelezaji wa mipango ya maendeleo umegusa
katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya Afya,
Maji, Nishati, Elimu, Madini, michezo na
utamaduni. Yafuatayo yametekelezeka kwa
kipindi cha 2015 – 2020.

9
2.1 SEKTA YA AFYA
Katika Sekta ya Afya – huduma bora za Afya ni
msingi wa kuondoa umaskini na kuharakisha
maendeleo ya wananchi. Katika Jimbo la
Busanda tumeendelea kutekeleza Ilani ya
Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015 inayoelekeza
kuwa na Hospitali kila Wilaya, Kituo cha Afya kila
Kata na Zahanati kila kijiji. Lengo ni kuongeza
upatikanaji wa huduma za Afya ya Msingi katika
ngazi zote ili kuboresha Maisha ya Wananchi na
kuchochea ukuaji wa uchumi. Hivyo kazi
zilizofanyika ni pamoja na;
Ufuatiliaji juu ya upatikanaji wa fedha za ujenzi
na ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za
Afya ndani ya Jimbo na haya hapa ni matokeo
yake.

2.1.1 UJENZI WA HOSPITALI


Hatukuwa na Hospitali lakini sasa tunajenga
Hospitali Katoro kwa fedha kiasi cha shilingi Billion
moja na nusu (1,500,000,000) kutoka kwa Mhe
Rais DKt John Pombe Magufuli. Upatikanaji wa
eneo na michoro umekamilika na ujenzi
unaendelea kwa kutumia Force Account.
Mpango huu umelenga kupunguza gharama za
mradi. Ujenzi wa Hospitali hii utahusisha majengo
(7) ambayo yanajengwa kutumia shilingi Billion

10
1.5 zilizotolewa. Majengo hayo ni Utawala,
wagonjwa wa nje, maabara, Jengo la mionzi (X-
Ray), jengo la kufulia nguo na jengo la wazazi.
Aidha ujenzi huo utakamilika ifikapo June
2020.Vilevile ujenzi wa vituo vya kutolea huduma
kwenye vijiji vyote vya Jimbo la Busanda
unaendelea vizuri na ujenzi upo kwenye hatua
mbalimbali za utekelezaji.

11
Picha za majengo ya hosptali ya Wilaya inayojengwa
Katoro

2.1.2 UPATIKANAJI WA GARI LA WAGONJWA


Upatikanaji wa Gari Jipya la wagonjwa kwa ajili
ya kituo cha Afya Katoro ambalo limekuwa
msaada mkubwa sana katika utoaji wa huduma
hasa katika kuwasafirisha wagonjwa kuwapeleka
kwa matibabu zaidi kwenye Hospitali ya Rufaa.
Tulikuwa na gari moja mwaka 2015 na sasa tuna
magari mawili (2).

12
Picha ya Gari la Wagonjwa

2.1.3 UJENZI WA KITUO CHA AFYA NYARUGUSU


Kabla kata ya Nyarugusu haikuwa na kituo
cha Afya na sasa, kituo cha afya kinajengwa.
Tumepokea fedha kiasi cha shilingi Millioni mia
nne (400,000,000) kutoka Serikali kuu. Mpaka
sasa kazi zilizofanyika ni pamoja na ujenzi wa
maabara, wodi ya wazazi, Jengo la kliniki ya
mama, baba na mtoto. Ujenzi wa jengo la
upasuaji, ujenzi wa wodi ya watoto, jengo la
kuhifadhia maiti na ujenzi wa njia ya
kuunganisha majengo yote ya kutolea
huduma. Ujenzi upo katika hatua ya umaliziaji.
Aidha jengo la Mama, Baba na mtoto
limekamilika, chumba cha upasuaji, maabara
na wodi ya watoto zimekamilika. Kukamilika
kwa majengo haya kutasaidia kuboresha na
13
kusogeza huduma za Afya karibu na
Wananchi. Kwani Kituo hiki sasa kitatoa
huduma za upasuaji.

Picha za majengo katika hatua mbalimbali

14
2.1.4 UBORESHAJI WA KITUO CHA AFYA
KATORO
Pamoja na fedha zilizopokelewa Katoro kwa
ajili ya ujenzi wa Hospitali Vilevile Kata ya
Katoro imepokea jumla ya fedha million ishirini
(20,000,000) kutoka kwa Mhe Rais na million
mia moja kutokana na CSR za ujenzi wa
majengo mapya katika kituo cha Afya katoro.
Majengo hayo ni wodi ya kina mama na
watoto, wodi ya kina baba, jengo la upasuaji.
Ujenzi unaendelea vizuri na uko katika hatua
za kumalizia. Utakapokamilika utapunguza
msongamano uliokuwepo pia itapunguza
kusafirisha wagonjwa kwenda Hospitali ya
Rufaa ya Geita.

Picha za majengo na hatua ya utekelezaji

15
2.1.5 UKARABATI WA VITUO VYA AFYA KWA
UFADHILI WA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI
Katika kuendelea kuboresha huduma za Afya
tumefuatilia na tumepata ufadhili kutoka
AMREF kwa ajili ya ukarabati wa vituo vya
kutolea huduma ikiwemo kituo cha Afya
Chikobe, kituo cha Afya Kashishi, zahanati za
Lwamgasa na Nyamalimbe. Vikikamilika
vitasaidia kusogeza huduma karibu hasa za
upasuaji kwa kina mama wakati wa
kujifungua.

16
17
Picha za majengo yanayokarabatiwa na miradi ya
maji safi chini ya ufadhili wa shirika la WEDECO

2.1.6 UKAMILISHAJI WA ZAHANATI ZA INYALA,


BUZIBA NA MAGENGE
Tumekamilisha ujenzi wa Zahanati za Msasa,
Isima,Inyala, Buziba na Magenge katika
kuendelea kutekeleza ahadi tulizozitoa wakati
wa uchaguzi juu ya kuwa na Zahanati kwa kila
Kijiji. Kukamilika kwa Zahanati hizi
kumesababisha ongezeko la idadi kufikia
Zahanati 21 ndani ya Jimbo la Busanda.
Jambo lililobaki ni kuendelea kukamilisha ujenzi
wa zahanati katika kila kijiji ambazo ujenzi uko
katika hatua mbalimbali. Vilevile tutaendelea
kufuatilia upatikanaji wa watumishi wa Afya ili
huduma zianze kutolewa katika vituo hivi
kurahisisha huduma bora za Afya kuwa karibu
na wananchi.
18
Hivyo kwa upande wa vituo vya kutolea
huduma za Afya hatukuwa na Hospitali na
sasa tunajenga. Tulikuwa na Vituo vya Afya 4
na Zahanati 15 na sasa tuna Vituo vya Afya 5
na zahanati 21. Vielelezo kwa baadhi ya
majengo vimeonyeshwa katika picha hapa
chini.

19
2.2 SEKTA YA ELIMU
2.2.1 Mpango wa Elimu Bure
Ilani ya CCM 2015 – 2020 katika Sekta ya Elimu
iliahidi Elimu bure kuanzia darasa la kwanza hadi
kidato cha nne. Kabla ya hapo elimu kuanzia
shule za msingi hadi kidato cha nne ililipiwa lakini
sasa watoto wanasoma Elimu bure bila malipo
na imesababisha watoto wengi kuandikishwa
shule hivyo kusababisha ongezeko kubwa la
watoto wanaokwenda shule.Vile vile tumefuatilia
fedha kwa ajili ya kuboresha miundombinu
mbalimbali ikiwemo madarasa madawati na
vyoo. Tulifanikiwa kupata fedha kupitia nguvu za
Wananchi, michango kutoka kwa wadau wa
Elimu, miradi maalum ya Serikali kuu kwa PFR
pamoja na CSR

Mhe. Mbunge akiwa Shule ya Msingi Mbegete


Zilizojengwa Na Mradi wa PFR.

20
i. Ujenzi wa Miundombinu ya Elimu kwa Mradi
wa(PFR)
a. Uanzishwaji wa kidato cha tano na sita katika
shule ya sekondari Kamena
Tayari tumepokea fedha shilingi milioni
miamoja tisini (Tshs 190,000,000) kwa ajili ya
ujenzi wa madarasa mawili na hosteli mbili
katika shule ya sekondari Kamena. Ujenzi
ukikamilika lengo ni kuanzisha kidato cha tano
na sita.
b. Ujenzi wa shule maalum kwa ajili ya
wasichana
Tumepokea milioni tisini (Tshs 90,000,000) kwa
ajili ya kuanza ujenzi wa Sekondari
Nyalwanzaja na ujenzi unaendelea.
c. Ujenzi wa sekondari Busanzu
Vilevile tumepata shilingi milioni miamoja na
kumi (Tsh 110,000,000) kwa ajili ya ujenzi wa
shule mpya ya sekondari Busanzu.
d. Ujenzi wa shule ya msingi Simbachawene
Tulipokea shilingi millioni miamoja themanini
(Tshs 180,000,000) kwa ajili ya ujenzi wa shule
ya Msingi Simbachawene na shule
imefunguliwa.
e. Ujenzi wa shule ya msingi Ludete
Tulifuatilia na kupata shilingi million miamoja
themanini (Tshs 180,000,000) kwa ajili ya ujenzi

21
wa shule ya msingi Ludete na shule
imekamilika.
f. Ujenzi wa miundombinu kupitia CSR na nguvu
za Wananchi
Kupitia CSR, wadau wa Maendeleo na nguvu
za Wananchi madarasa 117 yamejengwa na
kukamilika.

Hapa chini ni vielelezo vya baadhi ya kazi


zilizofanyika

Majengo ya Hostel katika shule ya Sekondari


Kamena

22
Majengo katika shule ya msingi Lishe Nyalwanzaja

Majengo katika shule ya sekondari Nyalwanzaja

23
Majengo katika shule ya Sekondari Busanzu

2.3. SEKTA YA MADINI


Jimbo la Busanda ni miongoni mwa maeneo
ndani ya Mkoa wa Geita Nchini Tanzania
yenye wingi wa madini ya dhahabu hivyo
uchumi wake kutegemea shughuli za
uchimbaji wa madini ya dhahabu na
kusababisha uchimbaji wa madini kuwa
miongoni mwa chanzo kikubwa cha kiuchumi.
maeneo maarufu kabisa kama Nyarugusu
Nyakagwe, Lwamgasa, Tembomine Backleef,
Nyaruyeye ndizo sehemu zijulikanazo kwa
uwepo wa wachimbaji wadogo wengi.
Tumefuatilia leseni za maeneo mengi
yaliyokuwa hayaruhusiwi kuchimba na sasa
wananchi hususani wachimbaji wadogo
wanachimba bila bugudha yeyote kwenye

24
maeneo ya Stamico – Nyarugusu, Bingwa leaf
– Lwamgasa, na Nyaruyeye.

2.3.1 Ujenzi wa kituo cha wachimbaji cha


mfano Lwamgasa
Hatukuwa na kituo maalum kwa ajili ya
kusaidia wachimbaji wadogo kwa sasa kituo
cha kisasa cha mfano kwa ajili uchenjuaji wa
dhahabu kimejengwa Lwamgasa na kiko
katika hatua ya ukamilishaji na kimegharimu
Jumla ya Tshs 1,345,040,000. Ni kituo
kimojawapo kati ya vituo vinne tu Tanzania
nzima.

Picha ya kituo cha mfano cha uchimbaji na


uchenjuaji madini Lwamgasa

Mambo mengine yaliyofanyika ni pamoja na;


2.3.2 kushiriki na kupitisha marekebisho ya
sheria ya madini ya mwaka 2010 SURA 123.
25
2.3.3 Kutunga Sheria ya umiliki wa wananchi
wa maliasili ya Taifa
Kushiriki na kupitisha marekebisho ya sheria ya
kodi SURA 332 na Kodi ya Ongezeko la
thamani SURA 148 kwa kuondoa kodi ya zuio
asilimia 5 na kuondolewa kwa kodi ya
Ongezeko la thamani asilimia 18 kwa biashara
ya madini inayofanywa na wachimbaji
wadogo kwenye masoko yetu ya ndani ya
Nchi.
Kuanzishwa kwa masoko 4 ya dhahabu katika
eneo la Katoro, Lwamgasa, Nyarugusu na
Nyakagwe.

Jengo la soko la dhahabu Lwamgasa

26
Picha ya soko la dhahabu la Nyakagwe

2.4 SEKTA YA NISHATI


Katika Sekta ya Nishati Kutokana na ilani ya
CCM ya 2015 – 2020 pia Mpango wa Taifa wa
Maendeleo wa Miaka mitano kuanzia 2015/16
hadi 2020/21 ambao umelenga kupeleka
umeme kwenye vijiji vyote vya Tanzania.
Katika Jimbo la Busanda tumefuatilia na vijiji
vyote 76 vimeingia kwenye Mpango wa
Serikali wa Miaka 5 wa kupatiwa umeme wa
REA na kwa sasa vijiji vyote vipo kwenye
mpango na utekelezaji unaendelea.
Tumebahatika pia kupata mradi wa 220KV
kutoka Bulyanghulu hadi Geita na mradi wa
Geita – Nyakanazi ambapo miradi hii mitatu
itahusika kusambaza umeme katika Jimbo la
Busanda.

27
2.4.1 Mradi wa KV 220 Bulyanghulu – Geita
Mradi huu umehusisha ujenzi wa kituo cha
kupoza umeme cha Geita KV 220. Kupitia
mradi huu jumla ya shilingi billioni 4.10
zimetumika kutekeleza mradi wa usambazaji
wa umeme katika vijiji 10. Kati ya vijiji 10
vilivyopo kwenye mradi huu vijiji 7 viko katika
Jimbo la Busanda kwenye kata za Kamena ni
vijiji vya Imalampaka, Ndelema na Kamena,
kata ya Nyalwanzaja ni vijiji vya Lishe na
Nyalwanzaja na kata ya Nyakamwaga ni vijiji
vya Buyagu na Bugalahinga.

2.4.2 Mradi wa REA III


Pamoja na mradi wa 220 KV vilevile mradi wa
REA III unaendelea na utekelezaji. Tayari vijiji 15
vimesambaziwa umeme kupitia mradi wa REA
III katika kata za Butobela vijiji vya Butobela,
Shahende na Mhande, kata ya Nyamalimbe
kijiji cha Nyamigogo, kata ya Bujula vijiji vya
Nyamiboga, Ihemelo na Bujula, kata ya
Nyamwilolelwa vijiji vya Nungwe, Saragulwa
na Nyamwilolelwa, kata ya Nyakagomba kijiji
cha Luhuha na kata ya Bukoli vijiji vya Ntono,
Ihega na makao makuu ya kata ya
Nyaruyeye . Kupitia miradi hii miwili tayari Kata
17 kati ya 22 zimefikiwa na mradi huu ambapo
jumla ya vijiji 22 vinaendelea kufungiwa na
28
kuwashiwa umeme. Mradi huu ukikamilika
utaongeza idadi ya vijiji vyenye umeme kutoka
10 hadi kufikia vijiji 32.
Utekelezaji wa mradi wa Geita – Nyakanazi
bado haujaanza. Matarajio ni kwamba
ukianza kutekelezwa mwezi July 2020 vijiji 32
vitasambaziwa umeme na kati ya vijiji hivyo 27
vipo katika Jimbo la Busanda. Ni imani yetu
kuwa kwenye bajeti ya mwaka 2020/2021 vijiji
vyote vilivyobaki vitapatiwa huduma ya
umeme kutokana kwamba vijiji vyote vimo
ndani ya mpango wa serikali kwa ajili ya
kupatiwa umeme wa REA III.
Vilevile mradi wa umeme wa Ujazilizi
unaendelea kutekelezwa kwenye Mamlaka ya
Mji mdogo wa Katoro ili kuwezesha wananchi
wengi kupata huduma ya umeme majumbani
na kwenye biashara hasa za uchenjuaji wa
madini na viwanda vya uongezaji thamani
mazao ya kilimo.

29
Utekelezaji unajieleza zaidi katika picha za
matukio mbalimbali hapa chini

Miundombinu ya TANESCO na REA katika kata ya


Nyamalimbe

Mhe. Waziri akizindua umeme kijiji cha


Nyamwilolelwa kata ya Nyamwilolelwa.
2.5 SEKTA YA BARABARA
Sekta ya Barabara ni muhimu sana kwa
maendeleo ya kiuchumi katika eneo lolote. Ili
kuhakikisha tunaunganisha maeneo ndani ya
Jimbo la Busanda na maeneo jirani kwa ajili ya
kurahisisha mawasiliano. Tumefuatilia na tayari
matengenezo ya barabara yako katika hatua
mbalimbali kama ifuatavyo;
Mhe. Waziri akizindua umeme Kijiji cha
Nyamwilolelwa Kata ya Nyamwilolelwa

30
2.5.1 BARABARA ZILIZO KATIKA UTEKELEZAJI WA
MARA KWA MARA
i. Barabara za Mkoa (Tanroads)
Lengo ni kusimamia na kuhakikisha Barabara
za mkoa zinapitika wakati wote ikiwemo;
Barabara ya Geita – Bukoli – Kahama ni
barabara inaunganisha mkoa wa Shinyanga
na utekelezaji umefanyika na inapitika wakati
wote.
Barabara ya Geita – Nyalwanzaja – Bukoli –
Kahama ; utekelezaji umefanyika na inapitika
wakati wote
Barabara ya Katoro – Ushirombo hii barabara
ni barabara ya Mkoa (Tanroad)
imetengenezwa na inapitika wakati wote
Barabara ya Chibingo – Bukondo - Barabara
hii iko katika utekelezaji wa mara kwa mara
na inapitika wakati wote.
ii. Barabara zilizopandishwa hadhi kuwa
Tanroads
Barabara ya Mbogwe boader – Wigo -Bukoli –
Bujula – Nyamigogo – Nyanghwale. Hii
barabara imepandishwa hadhi kuwa
barabara ya Tanroad kutokana na umuhimu
wake na utekelezaji wake utaanza hivi
karibuni. Lengo kubwa ni kurahisisha namna ya
usafiri na usafirishaji ndani ya Jimbo la Busanda

31
na maeneo jirani ya Wilaya ya Mbogwe na
Nyanghwale.
iii. Barabara zilizofunguliwa
Barabara ya Buyagu – Bufunda – Lwamgasa –
Mbogwe – Barabara hii imefunguliwa ili
kurahisisha mawasiliano na Wilaya ya Mbogwe
na tayari utekelezaji wake umekamilika na
tayari imeanza kutumika.
iv. Barabara zilizo katika Matengenezo ya Muda
a. Barabara za TARURA
Barabara nyingi za Tarura zipo kwenye
utaratibu wa matengenezo ya muda maalum.
Hivyo tumefanikiwa Barabara ya Kamena –
Bushishi – Bunegezi (4.2km) kuifanyia
matengenezo na yamekamilika ambayo
yalihusisha matengenezo ya sehemu korofi
pamoja na ujenzi wa makaravati.

Picha ya barabara ya Bushishi – Kamena

32
Barabara ya Katoro – Nyabulolo – Nyamigogo
ilihusisha matengenezo ya km 19.
Matengenezo yamekamilika kutoka Katoro –
Nyabulolo – Kamena na kamena –
Nyamigogo bado utekelezaji
unaendelea.Barabara zingine
zilizotengenezwa ni pamoja na Barabara ya
Mnekezi – Lubanda, Nyamalimbe – Ngula –
Nyakagwe, Nyaruyeye – Wigo – Mbogwe,
Barabara ya Ntono – Buzigula – Ivumwa,
Barabara ya Chemamba – Nyachiluluma,
barabara ya Chigunga – Nyakafuru –
Nyachiluluma, Barabara ya Magenge –
Nyamalulu, barabara ya Kaseme – Nyamalulu
– Mbogwe.

Picha ya barabara ya Magenge – Nyamalulu

33
Matengenezo mengine ni Barabara za ndani
ya Mamlaka ya Mji mdogo wa katoro
ambapo matengenezo yalihusisha barabara
ya Mbagala 1 na 2 kwenda Mbagala Int,
Barabara ya CCM – Ofisi ya kata ya Ludete na
Barabara ya CCM – Kaduda – Ipalamasa.
v. Barabara ambazo ziko kwenye utekelezaji
kwa sasa
Barabara ambazo zipo kwenye utekelezaji hivi
sasa kulingana na bajeti ya mwaka 2019/2020
ni kama ifuatavyo;
a. Barabara ya Katoro – Inyala – Nyakagomba,
b. Barabara ya Katoro – Lwamgasa – Buziba –
Nyarugusu na
c. Barabara ya Nyarugusu – Nyabulolo – Buyagu
Pamoja na mafanikio katika utekelezaji wa
ujenzi wa barabara uliofanyika kutokana na
baraka za mvua mwaka huu kumekuwa na
uharibifu katika baadhi ya barabara hizi na
kuhitaji uboreshaji wa haraka.
Hivyo Bajeti ya mwaka 2020/2021 inakusudia
kuangalia na kuzifanyia kazi changamoto hizi
zilizojitokeza. Vilevile kuanza utekelezaji wa
ahadi za Mhe Rais juu ya Ujenzi wa km 10 za
lami Katoro/Buseresere na ujenzi wa barabara
ya Geita – Bukoli – Kahama kwa kiwango cha
lami.

34
35
Picha za matukio Mhe. Mbunge akizindua ujenzi
wa Kilomita tano za lami ambazo mi ahadi ya Mhe.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

36
2.6 SEKTA YA MAJI
Sekta ya maji ni muhimu sana kwenye
maendeleo ya jamii. Kutokana na Ilani ya CCM
ya 2015-2020 ilikusudia kuhakikisha upatikanaji
wa maji safi na salama kwa asilimia 95 mijini na
asilimia 80 vijijini. Kwa kipindi cha miaka mitano
miradi mbalimbali imeendelea kutekelezwa
baadhi imekamilika na mingine bado ipo
kwenye utekelezaji. Miradi hii ni pamoja na mradi
wa maji Chankorongo, mradi wa maji
Nyakagomba na miradi mingine iliyopata
ufadhili wa wadau mbalimbali wa maendeleo.

2.6.1 Mradi wa Maji Chankorongo


Nikianza na mradi wa maji Chankorongo mradi
huu umehusisha kuvuta maji kutoka Ziwa Victoria
ambayo yamesambazwa kwenye vijiji 5 ikiwemo
Chikobe, Chankorongo, Chigunga, Kabugozo na
Chemamba. Kulingana na ukubwa wa pump
iliyofungwa matarajio yetu ni kuongeza
usambazaji wa maji kwenye vijiji vilivyo karibu na
chanzo.

37
Mradi wa maji Chankolongo

2.6.2 Mradi wa Maji Nyakagomba


Mradi huu umekamilika na kuwezesha vijiji vya
Luhuha na Nyakagomba kupata maji. Mradi
ambao ulizinduliwa na Mhe Waziri wa
Tamisemi.

Mradi wa maji kijiji cha Luhaha Kata ya


Nyakagomba

38
2.6.3 Miradi ya maji kupitia wadau wa
Maendeleo
Miradi ya maji kwa ufadhili wa Water Aid
imefanikiwa kusambaza maji katika kata za
Lwamgasa, Nyamalimbe, Nyarugusu,
Nyakamwaga na Nyachiluluma. Miradi hii
imeelekezwa zaidi katika vituo vya kutolea
huduma za Afya, shule na jamii inayozunguka.

Utekelezaji wa mradi wa kisima cha maji


Nyakagwe kisima ambacho kina maji mengi
sana kimewanufaisha wananchi wa kijiji cha
NYakagwe. Mpango uliopo ni kuyambaza maji
hayo kwenye vijiji vinavyozunguka kata ya
Butobela.

2.6.4 Mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria -


Katoro/Buseresere
Mradi huu upo kwenye mpango na upembuzi
yakinifu tayari. Lengo la mradi ni kuvuta maji
kutoka ziwa Victoria na kusambaza kwenye
Mamlaka ya Mji mdogo wa Katoro na Buseresere
pamoja na kata zinazozunguka mamlaka.
Nimshukuru Mhe Rais DKT John Pombe Magufuli
akiwa kwenye mkutano Katoro alisema
tumwachie suala la maji kwani analitafutia
ufumbuzi.

39
2.7 MICHEZO
Tumefuatilia na serikali imetekeleza kwa kuratibu
UMITASHUMTA na UMISSETA jambo ambalo
limesababisha watoto wengi kushiriki michezo
mbalimbali
Tumeshiriki kwa vitendo Kuhamasisha masuala ya
michezo kwenye jamii pamoja na kudhamini na
kusaidia vifaa vya michezo pale inapohitajika.
Kwa sasa jamii imehamasika na timu mbalimbali
vijijini zimeundwa na zinashiriki michezo.

Mhe. Mbunge akitoa Vifaa vya michezo Kata ya


Magenge timu ya Wanawake.

2.8 USHIRIKI KATIKA SHUGHULI ZA KIJAMII NA


KIUCHUMI
Maendeleo ya Jimbo ni pamoja na Kushiriki
katika shughuli za kijamii kwa kuhamasisha na
kuchangia ujenzi wa nyumba za ibada na

40
shughuli za kiroho. Yote haya yamefanyika
mathalani Kuchangia ujenzi wa shule, vikundi vya
kiuchumi, vikundi vya kijamii,nyumba za
watumishi n.k kwa vyote hivi vimefanyika kwa
kushirikiana na wananchi.

41
Mhe. Mbunge akiwa katika Mkutano wa Umoja wa
Wafanyabiashara Katoro kama Ilivyo katika picha
za matukio bbalimbali hapo juu.

42
2.8.1 FEDHA ZA MFUKO WA JIMBO
Jimbo la Busanda lilipokea fedha za kuchochea
maendeleo mwaka hadi mwaka na Kamati
Maalum ya Mfuko wa Jimbo ilipitisha kulingana
na mahitaji mbalimbali. Kwa mwaka 2016/2017
kiasi cha Tsh. 115,898,267.16 kilipokelewa kati ya
fedha hizo Tshs. 51,659,267.16 ilikuwa bakaa ya
mwaka 2015/2016 na Tshs. 64,239,000.00 fedha
ya mwaka 2016/2017. Kulingana na uhitaji katika
Jimbo kuwa ni tatizo la barabara hali iliyokuwa
inachangia kukwama kwa shughuli mbalimbali
za maendeleo katika Jimbo. Jumla ya Tshs.
51,659,267.16 zilielekezwa katika matengenezo
ya barabara hasa za vijijini zenye jumla ya Km.
33.5. Awamu ya pili ya matengenezo ya
barabara iligharimu kiasi cha Tshs. 45,000,000
ambapo jumla ya Km. 47.5 zilitengenezwa.
Pamoja na matengenezo ya barabara sehemu
ya fedha zilizobaki zilifanya shughuli nyingine za
maendeleo ambapo jumla ya Tshs. 19,239,000/-
zilitumika.
Katika mwaka wa fedha 2017/2018 fedha
zilizopokelewa zote zilipelekwa kutekeleza miradi
ya ujenzi wa Zahanati na vituo vya Afya ambapo
fedha zote zilitumika kununua mifuko 2100 ya
simenti ambapo mifuko 94 iligawanywa kwa kila
kata kwenyeJimbo la Busanda. Mwaka
2018/2019 zilipokelewa kiasi cha shilingi
43
76,192,400/= fedha ambazo zilielekezwa katika
utekelezaji wa miradi mbalimbali iliyoibuliwa na
wananchi.

3.SHUKRANI
Kabla ya kuhitimisha taarifa hii nipende kutoa
shukrani zangu za dhati kwa Wananchi wote wa
Jimbo la Busanda kwa kuniamini na kunipa
ridhaa ya kuwatumikia pia kwa ushirikiano
mkubwa walionipa kwa kipindi chote cha
utumishi wangu katika Jimbo la Busanda.
Napenda kutambua mchango wa Viongozi
wenzangu katika kufanikisha utekelezaji wa
majukumu. Kipekee kabisa shukrani ziwaendee
Waheshimiwa Madiwani wote wa Jimbo la
Busanda kwa ushirikiano na usimamizi wa
shughuli za maendeleo katika Jimbo la Busanda.
Aidha nitambue ushirikiano na mchango wa
Mwenyekiti wa Halmashauri pamoja na
madiwani wote katika Halmashauri ya Wilaya ya
Geita.
Napenda kutambua mchango mkubwa wa
viongozi wenzangu katika Ofisi ya Mbunge Jimbo
la Busanda katika utekelezaji wa majukumu.
Kipekee kabisa namshukuru Mh Masudi Bahari
Kimondo diwani mstaafu kata ya Kaseme Katibu
Jimbo la Busanda na Mh Amina Kanijo - Diwani
kata ya Bujula ambaye ni Makamu Mwenyekiti
44
kamati ya Mfuko wa Jimbo kwa ushauri na
usimamizi mzuri ulioleta ufanikishaji wa shughuli
mbalimbali za maendeleo katika Jimbo.
Nitakuwa mchoyo wa fadhila nisipowashukuru
Viongozi wote katika ngazi mbalimbali
wakiwemo Mawaziri, Manaibu Waziri, Mkuu wa
Mkoa wa Geita na ofisi yake, Mkuu wa Wilaya ya
Geita na ofisi yake, Mkurugenzi wa Halmashauri
ya Wilaya ya Geita na ofisi yake na watendaji
wote kwa ushirikiano na utendaji mzuri wa kazi
katika kutekeleza ilani ya CCM ndiyo maana
tumeweza kufikia malengo yetu.
Nichukue fursa hii pia kipekee kabisa
kuwashukuru wadau wa maendeleo na
mashirika mbalimbali ya Maendeleo ambayo
yameendelea kushirikiana na serikali yetu katika
kutekeleza mipango ya maendeleo na katika
uboreshaji wa huduma kwa wananchi. Wadau
hao wa maendeleo mniruhusu nitaje angalau
wachache ni pamoja na GGM, NMB, AMREF,
Water Aid, Plan International, makampuni yote
yanayojishughulisha na uchimbaji madini ndani
ya Jimbo letu.
Aidha niwashukuru wananchi kwa mchango
mkubwa katika utekelezaji wa miradi mbalimbali
kwenye jamii. Mafanikio ya utekelezaji wa
majukumu Jimbo la Busanda yametokana na
ushirikiano mzuri baina ya serikali, wadau wa
45
maendeleo Wananchi na Viongozi katika ngazi
mbalimbali.

“KWA PAMOJA TUTASHINDA”

46
MIRADI YA KIMKAKATI KATIKA JIMBO LA
BUSANDA
Ipo Miradi mbalimbali ya kimkakati ambayo
ipo katika hatua za ujenzi. Miradi hiyo ni
pamoja na ujenzi wa soko la kisasa la Katoro,
ujenzi wa mnada Katoro, ujenzi wa hospitali ya
Wilaya na ujenzi wa shule maalumu ya
wasichana ya Nyarwanzaja.

47
48

You might also like