You are on page 1of 72

HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA, MHESHIMIWA

SAADA MKUYA SALUM (MB) AKIWASILISHA


BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA
MATUMIZI YA WIZARA YA FEDHA KWA
MWAKA 2014/15
UTANGULIZI1. Mheshimiwa Spika, kufuatiataarif
ailiyowasilishwa hapa Bungeni na Mwenyekiti wa
Kamatiya Kudumu ya Bunge ya Uchumi, Viwanda
naBiashara, naomba kutoa hoja kwamba Bunge
lakoTukufu likubali kupokea, kujadili na
kupitishaMakadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya
Fedhakwa mwaka 2014/15.
2. Mheshimiwa Spika, awali ya yote napendakumshukuru
Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwakuniwezesha
kuwasilisha hotuba ya bajeti ya Wizara yamwaka 2014/15.
Aidha, natoa shukrani zangu za dhatikwa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete kwa kuniteua kuwa Waziriwa Fedha. Ninaahidi
kwamba nitatekeleza jukumu hilikwa weledi na uadilifu.
Vile vile, nawapongeza Mhe.Mwigulu Lameck Nchemba
(Mb) na Mhe. AdamKighoma Ali Malima (Mb) kwa
kuteuliwa kuwa NaibuMawaziri wa Wizara ya Fedha.
Kadhalika, namshukurupia aliyekuwa Naibu Waziri wa
Fedha Mhe. JanethZebedayo Mbene (Mb) kwa utendaji
kazi wake mahiri natunamuombea Mwenyezi Mungu
ampe nguvu na afyanjema katika kazi zake mpya Wizara
ya Viwanda naBiashara. Nichukue pia fursa hii
kumpongeza Bw.1Rished M. Bade kwa kuteuliwa kuwa
Kamishna Mkuuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania.
3. Mheshimiwa Spika, napenda kukupongeza
wewemwenyewe, Naibu Spika pamoja na Wenyeviti wa
Bungekwa kuongoza vyema majadiliano ya Bunge la
Bajeti.
4. Mheshimiwa Spika, naomba nitumie nafasi
hiikuishukuru kwa namna ya pekee Kamati ya Kudumuya
Uchumi, Viwanda na Biashara chini ya Mwenyekitiwake
Mhe. Luhaga Joelson Mpina (Mbunge wa Kisesa)na
Makamu wake Mhe. Dunstan Luka Kitandula(Mbunge wa
Mkinga) kwa maoni, ushauri namapendekezo waliyoyatoa
kwa Wizara wakati wakuchambua mapendekezo ya Bajeti
ya Wizara ya Fedha.Aidha, nachukua nafasi hii
kumshukuru Mwenyekitiwa Kamati ya Kudumu ya Bajeti
Mhe. Andrew JohnChenge (Mbunge wa Bariadi
Magharibi) pamoja naKamati nzima kwa ushauri wao.
Katika uandaaji wahotuba hii, Wizara imezingatia ushauri
na mapendekezoya Kamati hizo pamoja na ushauri na
maoni ya hojambalimbali zilizotolewa wakati wa mjadala
wa bajeti yaWizara kwa mwaka 2013/14.
5. Mheshimiwa Spika, kama unavyofahamu, Wizarailipata
pigo kwa kuondokewa na kiongozi wetu
mkuuMarehemuDkt.WilliamAugusta
oMgimwa.Tunawashukuru Viongozi wa Serikali,
WaheshimiwaWabunge, Washirika wa Maendeleo, Taasisi
mbalimbalipamoja na wananchi kwa ushirikiano
waliotupa kipindichote cha msiba. Tumeendelea kuenzi
misingi imaraaliyotujengea marehemu katika kutekeleza
majukumuya Wizara. Aidha, tunapenda kutoa pole kwa
ndugu na2jamaa kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa
ChalinzeMarehemu Saidi Ramadhani Bwanamdogo.
MwenyeziMungu azilaze roho za marehemu mahali pema
peponi.Amina.
6. Mheshimiwa Spika, napenda kuwapongeza, Mhe.Yusuf
Salim Hussein Mbunge wa Chambani, Mhe.Godfrey
William Mgimwa (Mbunge wa Kalenga) na Mhe.Ridhiwani
Jakaya Kikwete (Mbunge wa Chalinze) kwakuchaguliwa
kwao.
7. Mheshimiwa Spika, kwa namna ya kipekeenapenda
kutoa pongezi zangu za dhati kwa Mhe.Mizengo Peter
Pinda, Waziri Mkuu wa Jamhuri yaMuungano wa
Tanzania na Mbunge wa MpandaMashariki kwa hotuba
yake nzuri ambayo imetoamwelekeo wa shughuli za
Serikali kwa mwaka 2014/15.
8. Mheshimiwa Spika, katika hotuba yangu
nitaanzakuelezea mapitio ya utekelezaji wa mipango ya
Wizarakatika mwaka 2013/14. Nitaelezea pia
mikakatimbalimbali ambayo Wizara imeweka kwa
mwaka2014/15 ili kuendelea kuboresha utekelezaji
wamajukumu yake ya msingi yakiwemo: usimamizi
waBajeti ya Serikali; ukusanyaji mapato ya
Serikali;usimamizi wa misaada na mikopo; ulipaji wa Deni
laTaifa; usimamizi wa matumizi ya fedha za
umma;usimamizi na udhibiti wa ununuzi wa
umma;usimamizi wa utekelezaji wa MKUKUTA; na
usimamiziwa mashirika na taasisi za umma.
9. Mheshimiwa Spika, mwisho nitawasilisha bajetiya
mwaka 2014/15 kwa mafungu saba ya wizara yafedha
ambayo ni fungu 7, 10, 13, 21, 22, 23 na fungu50 pamoja
na fungu 45 la Mdhibiti na Mkaguzi Mkuuwa Hesabu za
Serikali.
MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA MPANGO NA
BAJETIYA WIZARA KWA MWAKA 2013/14 NA
MALENGO YAMWAKA 2014/15
10. Mheshimiwa Spika, uandaaji, utekelezaji nausimamizi
wa Mpango na Bajeti ya Wizara umezingatiamalengo ya
Mpango Mkakati wa Wizara wa mwaka2012/13 - 2016/17
ambao utaiwezesha Wizara kufikiamalengo ya Dira ya
Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2025;Mpango wa
Maendeleo wa miaka mitano 2011/12 -2015/16; Mkakati
wa Kukuza Uchumi na KupunguzaUmaskini Tanzania
(MKUKUTA II); Malengo yaMaendeleo ya Milenia 2015;
Mkakati wa Pamoja waMisaada Tanzania (MPAMITA)
pamoja na Programu yaMaboresho ya Usimamizi wa
Fedha za Umma PFMRP.Aidha, Mpango na Bajeti
ulizingatia Ilani ya Uchaguziya Chama cha Mapinduzi ya
Mwaka 2010 pamoja naMfumo wa Tekeleza Sasa kwa
Matokeo Makubwa (BigResults Now BRN).
11. Mheshimiwa Spika,katika mwaka 2013/14,Wizara
ilipanga kutekeleza yafuatayo: kuongeza mapatoya ndani
kufikia uwiano wa Pato la Taifa wa asilimia20.9 kwa
mwaka 2013/14 ikilinganishwa na asilimia17.7 kwa mwaka
2012/13; kukamilisha Ripoti za Utafitiwa Mfumo Bora wa
Kodi wa Serikali ya Jamhuri ya4Muungano wa Tanzania;
kuandaa na kusimamiautekelezaji wa bajeti ya Serikali;
kusimamia utekelezajiwa MKUKUTA-II; kufanya ukaguzi
wa miradi yamaendeleo na kutoa ushauri wa kitaalamu
kwawatekelezaji wa miradi hiyo; kukamilisha Sera ya
Maliya Umma; kufanya tathmini yausimamizi
nautekelezaji wa malipo ya mishahara ya watumishi
waumma; kusimamia utekelezaji wa mipango kazi
yaukaguzi na uzingatiwaji wa miongozo ya ukaguzi
katikaWizara, Idara zinazojitegemea, Wakala za Serikali,
naMamlaka ya Serikali za Mitaa; kuratibu na
kusimamiaupatikanaji wa misaada na mikopo nafuu
kutoka NchiWahisani, Mashirika na Asasi za Fedha za
Kimataifa;kuidhinisha miradi ya Ubia kati ya Sekta ya
Umma naBinafsi (PPP); na kukamilisha Sera ya Taifa ya
Ununuziwa Umma.
12. Mheshimiwa Spika, katika kipindi hicho, Wizarapia
ilipanga kukamilisha miradi ya MCA-T na
kukabidhimiradi iliyokamilika kwa taasisi husika;
kusimamiautekelezaji wa Mpango Mkakati wa Programu
yaMaboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma Awamu
yanne (PFMRP IV); kufanya uhakiki wa Wastaafu
waliopokatika Daftari la Pensheni la Hazina;
kuunganishaHazina Ndogo na Sekretarieti za Mikoa 24
katika mfumowa malipo kwa njia ya elektroniki kupitia
Benki Kuu yaTanzania (Tanzania Inter- Bank Settlement
System -TISS); kuimarisha utendaji kazi wa Ofisi ya
Msajili waHazina; na kuandaa na kuhuisha kanuni na
miongozoya utekelezaji wa Sheria ya Udhibiti wa Fedha
Haramuna Ufadhili wa Ugaidi.5Mfumo wa Tekeleza Sasa
kwa Matokeo Makubwa
13. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,kupitia
Tekeleza Sasa kwa Matokeo Makubwa, Wizaraya Fedha
katika maabara ya utafutaji wa rasilimalifedha iliwekewa
malengo yafuatayo: kuongeza mapatomapya ya kodi ya
shilingi trilioni 1.16; kuongezamapato mapya yasiyo ya
kodi ya shilingi bilioni 96.7;kudhibiti matumizi; na
kutafuta fedha za utekelezaji wamiradi ya Tekeleza Sasa
kwa Matokeo Makubwa katikasekta zinazotekeleza miradi
hiyo.
14. Mheshimiwa Spika, hadi mwezi Aprili 2014,ukusanyaji
wa mapato kutoka vyanzo vilivyoibuliwachini ya BRN
umefikia shilingi bilioni 338 sawa naasilimia 29.14 ya
lengo la kukusanya shilingi trilioni1.16. Matokeo
yasiyoridhisha yalisababishwa na baadhiya mapendekezo
ya BRN kutokutekelezwa katikamwaka 2013/14.
Mapendekezo hayo ni kubadilishamfumo wa ushuru wa
bidhaa zisizo za petroli kutokaspecific kwenda advalorem
(makisio shilingi bilioni 386)na kuanzisha kodi ya zuio ya
asilimia tano kwenyebidhaa zinazotoka nje ya nchi
(makisio shilingi bilioni225.6). Kwa vile ukusanyaji wa
mapato ndio msingi wakufanikiwa kwa BRN, Serikali
inachambua vyanzombadala vya kufidia mapato haya ili
kuhakikisha lengokuu la kuongeza mapato kwa shilingi
trilioni 3.48linafikiwa ifikapo mwaka 2015/16.6Mwenendo
wa Uchumi.
15. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,Wizara
kupitia Benki Kuu iliendelea na jukumu lakuandaa,
kusimamia na kutathmini utekelezaji wa seraya fedha
inayolenga kuwa na kiwango kidogo chamfumuko wa bei
kwa ajili ya kuhakikisha gharama zamaisha haziongezeki.
Kutokana na juhudi hizi,mfumuko wa bei umeshuka
kutoka wastani wa asilimia16 mwaka 2012 hadi kufikia
wastani wa asilimia 7.9mwaka 2013. Katika kipindi hiki
uchumi umeendeleakuimarika huku ukuaji halisi wa Pato
la Taifaukiongezeka kwa asilimia 7.0 katika kipindi cha
mwaka2013 ikilinganishwa na asilimia 6.9 katika
mwaka2012. Shughuli za kiuchumi zilizokua kwa
kiasikikubwa ni pamoja na mawasiliano asilimia
22.8,huduma za kifedha asilimia 12.2, ujenzi asilimia 8.6,
nauuzaji bidhaa wa jumla na rejareja asilimia 8.3.
Katikamwaka 2014/15, Wizara kupitia Benki Kuu
itaendeleakushirikiana na wadau wote katika
kuhakikishakwamba lengo la msingi la utulivu wa bei na
ukuaji wauchumi linadumishwa.Uandaaji na Usimamizi
wa Utekelezaji wa Bajeti yaSerikali


16. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,Wizara
imeratibu uandaaji wa Mwongozo wa Mpango naBajeti
kwa kipindi cha 2014/15 2016/17 kwa Wizara,Idara
zinazojitegemea, Mikoa na Mamlaka za Serikali zaMitaa
na kusambaza kwa wadau mwezi Desemba
kama7ilivyopangwa. Aidha, Wizara imeandaa na
kuchapishavitabu vya bajeti ya Serikali vya mwaka
2014/15(Volume I, II, III na IV) kama vilivyowasilishwa
Bungenikwa ajili ya mjadala wa Bunge la Bajeti la
mwaka2014/15 unaoendelea; kitabu cha tafsiri rahisi ya
bajetiya Serikali (Citizens Budget) kwa mwaka 2013/14;
naKitabu cha Budget Background and Medium
TermFramework 2013/14 2015/16.


17. Mheshimiwa Spika, Serikali inakusudia kuanzakutumia
mfumo wa Programu katika uandaaji,uidhinishaji na
utekelezaji wa Bajeti. Mfumo huuutasaidia Serikali kugawa
rasilimali kwa kuzingatiamatokeo na kuweka viashiria vya
kufikia malengo.Katika hatua za awali za maandalizi ya
utekelezaji wamfumo huu katika mwaka 2013/14, Wizara
ilitengafedha kwa ajili ya mafunzo kwa wataalam wa
Wizaranane za mfano. Maandalizi haya ya kimkakati
nakimfumo yataendelea katika mwaka 2014/15.
Wizarazilizotengwa kwa majaribio na ambazo
tayarizimefanyiwa mafunzo ni Wizara ya Maji, Wizara
yaUjenzi, Wizara ya Uchukuzi, Wizara ya Elimu
naMafunzo ya Ufundi, Wizara ya Afya na Ustawi wa
Jamii,Wizara ya Kilimo, Wizara ya Maendeleo ya Jamii,
Jinsiana Watoto na Wizara ya Fedha. Wizara hizi kwa
sasazinaendelea na zoezi la kuandaa programu na
viashiriavya kupima utekelezaji kabla ya mfumo
kuanzakutumika.


18. Mheshimiwa Spika, Wizara iliratibu kikao kazicha
wataalamu wa wizara, mikoa na halmashaurikuhusu
mfumo wa ufuatiliaji, tathmini na utoaji wataarifa za
utekelezaji wa Bajeti. Katika kipindi hicho,8Wizara pia
ilifanya kikao kazi kilichohusisha washirikikutoka wizara,
idara za Serikali zinazojitegemea, mikoana Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa kwa lengo lakutathmini
uandaaji na uwasilishwaji wa Bajeti yaSerikali kwa mwaka
2012/13 na kufanya mkutano wamwaka wa wadau ambao
ulijumuisha Washirika waMaendeleo kwa lengo la
kutathmini utekelezaji waBajeti ya Serikali.


19. Mheshimiwa Spika, katika kusimamia nakudhibiti
utekelezaji wa bajeti ya Serikali ikiwemokufuatilia
matumizi ya fedha za umma, Wizara ilifanyaufuatiliaji na
ukaguzi wa matumizi ya fedha zilizotolewakwa ajili ya
maendeleo kwa miradi ya ASDP na DASIPikihusisha
wizara nne, mikoa sita na halmashauri 33.Aidha,
ufuatiliaji na ukaguzi ulifanyika kwa mapato namatumizi
ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Taifa yaChakula (NFRA)
na kwa fedha zilizotolewa kuhudumiavituo 16 vya Makazi
ya Wazee katika mikoa 14 nchini.


20. Mheshimiwa Spika, katika ukaguzi huo, Wizarailibaini
kuwapo kwa upungufu na changamoto katikamaeneo haya
ikiwa ni pamoja na: fedha kutowafikiawalengwa kwa
wakati kama ilivyopangwa; udhaifukwenye udhibiti wa
ndani wa matumizi na hivyokusababisha kuwapo kwa
huduma duni; na miradikutokamilika kwa wakati na
kuwepo kwa bakaa yafedha za maendeleo. Aidha,
zimekuwepo changamoto zakubadilika mara kwa mara bei
ya kununulia nafaka nagharama za usafirishaji, hivyo
kuathiri malengoyaliyopangwa ikiwemo kusababisha
madeni. Wizaraimewasiliana na wahusika na kutoa
nyaraka zamaelekezo ya kuhakikisha kwamba udhibiti wa
ndani9wa matumizi unaimarishwa katika ngazi zote
zausimamizi na inapobidi hatua za kisheria
zichukuliwekwa wahusika.


21. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15,Wizara
inatarajia kutekeleza yafuatayo: kupitia mfumowa
uwasilishaji wa bajeti za wizara, idara za Serikali,mikoa na
halmashauri na kuhakikisha kuwa sera namipango ya
kitaifa na ile ya kisekta vyote vimezingatiwaipasavyo
katika Bajeti ya Serikali na kutengewa fedha;kufanya
tathmini ya utekelezaji wa Bajeti ya Serikali,kuendelea
kuboresha mfumo wa mpangilio wa Bajeti
yaSerikalikwakuzingatiaprogram umbalimbali;kuimarisha
mifumo ya kompyuta ya uandaaji bajeti ilikukidhi mahitaji
ya taarifa mbalimbali zinazohitajika;kuendelea kujenga
uwezo wa wizara, idara za Serikali,mikoa na halmashauri
katika uandaaji wa Bajeti yaMuda wa Kati, usimamiaji
wake na utoaji taarifa zautekelezaji ikiwa ni pamoja na
ufuatiliaji na tathminikwa wakati; kutayarisha taarifa
mbalimbali zautekelezaji wa Bajeti ya Serikali ili
kuhakikisha uwazina uwajibikaji unazingatiwa; na
kufuatilia matumizi yafedha za umma zikiwemo fedha za
mishahara, matumizimengineyo na fedha za
miradi.Usimamizi wa Misaada na Mikopo


22. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,Wizara
ilifanikisha kusainiwa kwa mikataba 18 kwa ajiliya
misaada na mikopo nafuu yenye thamani ya jumlaya
shilingi bilioni 958.027 kutoka kwa Washirika
waMaendeleo. Aidha, Wizara imeendelea
kuratibuukamilishaji wa Mwongozo mpya wa Ushirikiano
wa10Maendeleo - Development Cooperation
Frameworkambao utachukua nafasi ya Mkakati wa
Pamoja waMisaada Tanzania (MPAMITA). Mwongozo huu
unalengo la kusimamia ushirikiano wa maendeleobaina ya
Serikali na Wadau wa Maendeleo nakuendeleza mafanikio
yaliyopatikana wakati wautekelezaji wa MPAMITA. Lengo
la ujumla nikupatikana ufanisi katika misaada kutoka
kwaWashirika wa maendeleo na kubainisha wajibu wakila
mdau wa maendeleo wakiwemo raia, wabunge,asasi zisizo
za kiserikali na sekta ya habari.


23. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15,Wizara
imepanga kufanya yafuatayo: kuzinduaMwongozo wa
Ushirikiano wa Maendeleo na kuandaampango kazi wake
pamoja na kuhamasisha matumiziyakekwa Washirika wa
Maendeleo, Wizara, IdaraZinazojitegemea, Serikali za
Mitaa, Taasisi Binafsi naWaheshimiwaWabunge;
kutathmini utekelezaji wamiradi na programu mbalimbali
inayotekelezwa kwafedha toka Washirika wa Maendeleo
kwa nia yakuhakikisha kwamba thamani ya fedha
inapatikanakatika miradi hiyo; kushiriki kwenye
majadiliano naJumuiya za kikanda na kimataifa; na
kuendeleakutafuta fedha za misaada na mikopo nafuu kwa
ajili yautekelezaji wa miradi ya maendeleo, na Misaada
yaKiufundi kutoka kwa Mashirika ya Kimataifa na
nchiwahisani.11Ulipaji wa Deni la Taifa


24. Mheshimiwa Spika, Deni la Taifa
limeendeleakusimamiwa na Sheria ya Madeni ya mwaka
1974 namarekebisho yake ya mwaka 2004. Wizara
imeendeleakutoa kipaumbele katika ulipaji wa madeni
kwa wakatiili kuepuka malimbikizo ya riba. Katika kipindi
chaJulai, 2013 hadi Aprili, 2014 malipo ya deni la
ndaniyalifikia shilingi bilioni 1,694.53 ambapo kati ya
malipohayo riba ni shilingi bilioni 581.20 na Mtaji
(principalrollover) ni shilingi bilioni 1,113.33. Aidha, deni
la njelimelipwa kwa kiasi cha shilingi bilioni 340.22, kati
yakiasi hicho malipo ya riba ni shilingi bilioni 201.52
nadeni halisi - principal ni shilingi bilioni 138.70.


25. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15,Wizara
itaendelea kulipa madeni ya ndani na nje kwawakati ikiwa
ni pamoja na kulipa kwa wakati
madenimbalimbaliambayoserikali
imeingiamikataba(Contractual Liabilities) na madai ya
dharura(Contingent Liabilities) pindi
yanapotokea.Usimamizi wa Matumizi ya Fedha za Umma


26. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kujengauwezo
wa usimamizi wa matumizi ya fedha za ummakwa
kudhamini mafunzo ya muda mrefu kwawatumishi 313 wa
kada ya uhasibu, ugavi na kompyutakutoka kwenye
wizara, idara za serikali, sekretariati zamikoa,manispaa,
halmashauri za miji na wilayawaliopo vyuoni na
watumishi 218 walipewa mafunzo yamuda mfupi kwa
lengo la kuongeza ufanisi katikausimamizi wa matumizi ya
fedha za umma. Aidha,12Wizara imeendelea kusambaza
Mfumo wa Malipo waKielektroniki -TISS mikoani ambapo
hadi sasa jumla yamikoa 20 imeunganishwa katika
mtandao huo. Mikoailiyounganishwa kwenye mtandao
huo ni Iringa,Morogoro, Pwani, Tanga, Kilimanjaro,
Mbeya, Rukwa,Ruvuma, Lindi, Simiyu, Mwanza, Kagera,
Geita, Mara,Mtwara, Kigoma, Shinyanga, Njombe, Dar es
Salaam naKatavi. Vile vile, mikoa mipya ya Geita, Simiyu,
Katavina Njombe imeunganishwa kwenye mtandao wa
malipowa Serikali (Intergrated Financial Management
System).


27. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea nampango wa
kutekeleza mfumo wa uandaaji wa taarifaza hesabu kwa
kuzingatia Viwango vya Kimataifa vyaUandaaji wa Taarifa
za Hesabu katika Sekta ya Umma -IPSAS Accrual Basis
ambapo hesabu za majumuisho zamwaka 2012/13
zimeandaliwa kwa kutumia mfumohuo kwa mara ya
kwanza na kuwasilishwa kwaMdhibiti na Mkaguzi Mkuu
wa Hesabu za Serikali kwawakati.


28. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15,pamoja na
mambo mengine, Wizara itaendeleakuboresha usimamizi
wa fedha za umma kwa kufanyayafuatayo: kuendelea
kutoa udhamini wa masomo yamuda mrefu na mfupi kwa
wahasibu, wakaguzi,maafisa ugavi na wataalamu wa
kompyuta kutokaSerikali Kuu na serikali za mitaa; kuweka
mitambokatika hazina ndogo zote ili kuwezesha
sekretariati zamikoa na hazina ndogo kufanya malipo kwa
kutumiamifumo ya malipo ya kielektroniki -
TISS/EFT;13kuendelea kutoa mafunzo ya TISS/EFT kwa
wahasibuna watumishi wa kada zingine ili kuimarisha
mfumo wamalipo; na kuanza ujenzi wa jengo la ofisi ya
HazinaNdogo Arusha.


29. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15 ilikuinua
kiwango cha fani ya uhasibu sambamba nakuimarisha
usimamizi wa fedha za umma Tanzaniaitakuwa mwenyeji
wa mkutano wa Wahasibu Wakuu waSerikali wa nchi za
Mashariki na Kusini mwa Afrika ESAAG.Programu ya
Maboresho ya Usimamizi wa Fedha zaUmma Public
Finance Management ReformProgramme (PFMRP)


30. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Programu
yaMaboresho ya Usimamizi wa Fedha za
Ummaimekamilisha utafiti wa mfumo wa kupeleka
fedhakwenye Serikali za Mitaa, mpango wa utekelezaji
wautafiti huo umeandaliwa na utekelezaji wake
utaanzamwaka wa fedha 2014/15. Aidha, utafiti juu ya
mifumoya fedha inayotumiwa na Serikali kwa lengo
lakuiunganisha mifumo hiyo ili kuboresha usimamiziwake
umekamilika. Vile vile, Wahasibu 522 kutokaWizara
mbalimbali, hazina ndogo na sekretarieti zamikoa walipata
mafunzo juu ya Viwango vya Kimataifavya Uandaaji wa
Taarifa za Hesabu katika Sekta yaUmma na watumishi
wengine 34 ambao wanasimamiaprogramu hii kutoka
katika wizara na taasisi walipatamafunzo ya kusimamia
Mabadiliko na Kuandaa14Mipango Mkakati -Change
Management and StrategicPlanning. Mafunzo haya
yalilenga kuwajengea uwezo wakuandaa mipango na bajeti
inayolenga katikakutekeleza maboresho ya usimamizi wa
fedha za umma.


31. Mheshimiwa Spika,katika mwaka 2014/15,Wizara
itaendelea kuboresha usimamizi wa fedha zaumma kwa
kuendelea na utekelezaji wa Awamu ya Nneya Programu
ya PFMRP kwa kufanya yafuatayo: kupitiana kuboresha
mifumo ya kifedha na kuangalia njia boraya kuiunganisha
baada ya utafiti kukamilika;nakuwajengea uwezo wakaguzi
wa ndani katika wizara,idara, wakala za Serikali na
halmashauri za Serikali zaMitaa juu ya ukaguzi wa mifumo
ya fedha, usimamizina ukaguzi wa vihatarishi, ukaguzi wa
bajeti namishahara, na ukaguzi wa miradi.Sera ya Ununuzi
wa Umma


32. Mheshimiwa Spika, katika kusimamia Sekta
yaUnunuzi wa Umma nchini, Wizara
imeendeleakutekeleza yafuatayo:kuandaa Sera ya Taifa
yaUnunuzi wa Umma; kuandaa mapendekezo ya
muundowa Vitengo vya Usimamizi wa Ununuzi na
UgaviSerikalini; na kufanya tathmini ya mahitaji ya
mafunzokwa maafisa ununuzi na ugavi walioko katika
Mamlakaza Serikali za Mitaa; na kuendelea kuhuisha
taarifa zamaafisa ununuzi na ugavi Serikalini, ambapo
taarifa zamaafisa 332 katika mikoa ya Shinyanga,
Kagera,Mwanza na Mara zimehakikiwa na kuingizwa
katikadaftari la maafisa ununuzi na ugavi.15


33. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15,Wizara
imepanga kufanya yafuatayo: kuandaa Mkakatiwa
Utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Ununuzi wa Ummana
kusimamia utekelezaji wa Sera hiyo; kuhuishamuundo wa
vitengo vya usimamizi wa ununuzi na ugaviserikalini;
kuipitia Sheria ya Ununuzi wa Umma Na.7ya mwaka 2011
na kanuni zake za mwaka 2013;kukamilisha tathmini ya
mahitaji ya mafunzo kwamaafisa ununuzi na ugavi
Serikalini; na kufanyatathmini juu ya ufanisi wa ununuzi
wa umma nchini.Udhibiti wa Ununuzi wa Umma


34. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,Wizara
kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi waUmma
imetoa mafunzo kuhusu sheria, kanuni nataratibu za
ununuzi kwa taasisi za umma 32 ambapowatumishi 747
walihudhuria mafunzo hayo. Aidha,Mamlaka ilitoa
mafunzo kuhusu mfumo wa upokeaji nausimamizi wa
taarifa za ununuzi nchini katika vituovinne vya Morogoro,
Arusha, Mwanza na Mbeya ambapojumla ya washiriki 330
kutoka taasisi 191 walishiriki.Vile vile, Mamlaka
imeendelea kusimamia mfumo waupokeaji na usimamizi
wa taarifa za ununuzi nchiniambapokatikakipindihicho
,taasisi191ziliunganishwa na kupatiwa mafunzo ya
kutumiamfumo huo na hivyo kufanya jumla ya
taasisizilizounganishwa na kupatiwa mafunzo kufikia
364,sawa na asilimia 80 ya taasisi zote.16


35. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Mamlaka
yaUdhibiti wa Ununuzi wa Umma imefanya
ukaguzikuhusu utoaji wa zabuni na utekelezaji wa
mikatabaitokanayo na ununuzi wa umma katika Taasisi
120zikiwemo wizara na idara zinazojitegemea 32,
mashirikaya umma 46 na serikali za mitaa 42. Ukaguzi
huuuilihusisha mikataba 5,867 yenye thamani ya
shilingibilioni 1,985.427 ikiwemo miradi 207 ya ujenzi
yenyethamani ya shilingi bilioni 777.2. Ripoti ya
ukaguziinaonesha wastani wa uzingatiwaji wa sheria
yaununuzi ulikuwa ni asilimia 64 ambayo ni chini yalengo
la asilimia 80. Maeneo yaliyobainika kuwa naudhaifu
mkubwa ni katika usimamizi wa mikataba nautunzaji wa
nyaraka za ununuzi.


36. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15,Wizara
imepanga kutekeleza yafuatayo: kuandaampango kazi wa
usimamizi wa utekelezaji wa Sheria yaUnunuzi wa Umma
ya Mwaka 2011; kuelimisha wadaumbalimbali kuhusu
Sheria mpya na kanuni zake;kuendelea na maandalizi ya
kuanzisha mfumo waununuzi kwa njia ya kielektronic (e-
procurementsystem); kufungua ofisi za kanda Dodoma,
Mbeya naMwanza; kushirikiana na TAMISEMI ili
kukabiliana nachangamoto zilizopo kwenye vitengo vya
ununuzi vyahalmashauri mbalimbali; kufanya kazi na
Asasi zaKiraia na Wanahabari ili kuongeza uelewa wa
masualaya Ununuzi wa Umma kwa wananchi; na
kuendeleakusimamia ununuzi katika sekta ya
Umma.17Huduma ya Ununuzi Serikalini


37. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,Wizara
kupitia Wakala wa Huduma ya UnunuziSerikalini
imetekeleza yafuatayo: kuongeza vifaa vyahuduma
mtambuka kutoka 86 vilivyokuwepo hadi 181;kuendelea
na ujenzi wa Ofisi na ghala katika mkoa waManyara;
kuendelea na ujenzi wa kituo cha mafutamkoa wa
Dodoma; na kununua magari mawilimakubwa yenye
uwezo wa kubeba lita 45,000 za mafutakila moja kwa ajili
ya kusafirisha mafuta toka kwawazabuni kwenda mikoani.
Aidha, Wakala wa Hudumaya Ununuzi Serikalini, imeanza
kufunga Mfumo waUdhibiti na Usimamizi wa Mafuta ya
Magari ambaoutaanza kwa majaribio Agosti, 2014 katika
mkoa waDar es Salaam ili kudhibiti matumizi ya mafuta
katikamagari ya Serikali.


38. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15,Wizara
kupitia Wakala wa Huduma ya UnunuziSerikalini
imepanga kutekeleza yafuatayo: kukamilishakazi ya
kufunga Mfumo wa Udhibiti na Usimamizi waMafuta ya
Magari katika mikoa ya Arusha, Mwanza,Dodoma, Iringa
na Mbeya; kuanza kazi za Ujenzi waOfisi katika mikoa ya
Njombe na Mara; kukamilishaujenzi wa visima vya mafuta
katika mikoa ya Geita,Katavi na Wilaya ya Ileje; na
kuongeza uwezo wakuhifadhi mafuta kufikia wastani wa
lita 50,000 katikavituo vya mikoa ya Arusha, Mwanza,
Kigoma, Mtwara,Lindi, Tabora, Pwani, Tanga na Ruvuma.
Aidha, Wakalawa Huduma ya Ununuzi Serikalini itahuisha
muundowake ili kuweza kutoa huduma ngazi ya wilaya
na18kuanza kutekeleza utaratibu wa ununuzi wa
magarikwa pamoja.Rufaa za Zabuni za Umma


39. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,Mamlaka
ya Rufaa za Zabuni za Umma imepokea jumlaya
mashauri35, kati ya hayo mashauri matatuyaliondolewa
na walalamikaji kabla ya kusikilizwa;mashauri 17
walalamikaji walishinda; mashauri 11walalamikaji
walishindwa; mashauri mawili yalifutwakufuatana na
sheria; shauri moja halikutolewa uamuzikutokana na
ukomo wa muda wa kulisikiliza; na shaurimoja lipo
kwenye hatua ya kusikilizwa. Aidha, katikamwaka
2014/15, Mamlaka itaendelea kusikiliza nakutolea
maamuzi malalamiko na rufaa katika Ununuziwa Umma
na kuelimisha umma na wadau juu yakuwasilisha
pingamizi za zabuni kwa mujibu wa Sheriaya Ununuzi wa
Umma ya mwaka 2011.Usimamizi wa Mali ya Serikali


40. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,Wizara
iliendelea kuandaa Sera ya Mali ya Umma.Lengo la sera
hii ni kusimamia na kutoa miongozo yaudhibiti wa mali ya
umma. Aidha, Wizara ilifanyauthamini wa mali ya Serikali
katika mikoa mitano nawizarambili,hivyokufanyawiza
ra,idarazinazojitegemea na wakala wa Serikali
zilizofanyiwauthamini kufikia 42. Katika kipindi hicho,
usimikaji wamfumo wa uhakiki wa mali ya umma
ulikamilika. Vilevile, Wizara iliendelea na zoezi la
kuondosha mali19chakavu katika wizara na idara za
Serikali ambapojumla ya shilingi bilioni 1.58 zilikusanywa
kutokana namauzo ya vifaa hivyo na shilingi milioni 12.83
kutokanana utoaji wa leseni za udalali.


41. Mheshimiwa Spika, Wizara ilifanya uhakiki wamali ya
Serikali katika wizara, idara zinazojitegemea nawakala za
Serikali kwa lengo la kudhibiti matumizi yamali katika
taasisi hizo. Aidha, Wizara imefanya uhakikimaalum
katika Bohari Kuu ya Madawa ambapo ushauriulitolewa
wa namna ya kupunguza hasara inayotokanana madawa,
vifaa tiba na vitendanishi kuisha mudawake wa matumizi
kabla ya kutumika.


42. Mheshimiwa Spika, katika mwaka, 2014/15,Wizara
imepanga kukamilisha Sera ya Mali ya Ummana
kuisambaza kwa wadau kwa ajili ya kupata maonikabla ya
kuanza utekelezaji wake. Aidha, Wizaraimepanga kufanya
uthamini wa mali katika mikoa sabana taarifa zake
kuingizwa kwenye Daftari la Mali yaSerikali. Vile vile,
Wizara itaendelea kuondosha malichakavu, mali
zilizokwisha muda wake na vifaa sinziakwa mujibu wa
Sheria na Kanuni za Fedha za Umma;kushughulikia taarifa
za ajali na potevu za mali
yaSerikali;nakuendeleakuchambu a,kufanyamajadiliano
na wadai na kulipa madai ya fidia na kifutamachozi
yanayotokana na amri ya Mahakama.Kadhalika, Wizara
itaendelea na uhakiki wa mali katikawizara, idara
zinazojitegememea na wakala za Serikali.Mpango wa
MilleniumTanzania (MCA-T)20ChallengeAccount


43. Mheshimiwa Spika, Programu ya MilleniumChallenge
Account Tanzania iliendelea na ukamilishajiwa miradi ya
ujenzi wa miundombinu ya usafirishaji,nishati ya umeme
na maji. Miradi yote ya barabaraimekamilika isipokuwa
sehemu ya Laela- Sumbawangakatika barabara ya
Tunduma- Sumbwanga ambayoinatarajiwa kukamilika
kabla ya mwisho wa mwaka2014. Miradi ya umeme na
maji imekamilika na ipokatika kipindi cha uangalizi.
Aidha, kutokana nautekelezaji wa kuridhisha, Tanzania
imekidhi vigezo nahivyo itanufaika na awamu ya pili ya
msaada waSerikali ya Marekani kupitia Shirika lake
laChangamoto za Milenia (MCC). Katika awamu ya
pili,miradi itakayofadhiliwa ni ya umeme na barabara
zavijijini Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar.Ukaguzi wa
Ndani


44. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,Wizara
imetekeleza yafuatayo: kutoa Mwongozo waKamati za
Ukaguzi katika Sekta ya Umma kwa lengo lakuhakikisha
utendaji wenye tija kwa Kamati zote zaUkaguzi; kutoa
mafunzo ya kuwajengea uwezowakaguzi wa ndani 458,
wajumbe wa Kamati zaUkaguzi na wadau wa ukaguzi wa
ndani wapatao 567;kufanya ukaguzi wa miradi ya
maendeleo 11; ukaguziwa orodha ya malipo ya mishahara;
na kuhakiki madaimbalimbali yaliyowasilishwa wizarani
kabla ya kulipwa.21


45. Mheshimiwa Spika, katika kuendeleza juhudi
zaSerikali za kudhibiti ubora wa utekelezaji wa
miradimbalimbali ya maendeleo, Wizara imenunua vifaa
vyakuhakiki ubora wa miundombinu. Vifaa
hivyovitatumika katika ukaguzi wa miradi inayotekelezwa
naWizara, Idara, Wakala za Serikali na Halmashauri
zaSerikali za Mitaa katika kuhakikisha kuwa miradi
namiundombinu inayotekelezwa inakuwa na
uboraunaokidhi viwango na hatimaye kupata thamani
yafedha. Hatua hii itaenda sambamba na
kuwajengeauwezo wakaguzi wa ndani Serikalini katika
kufanyaukaguzi wa kiufundi kwa miradi inayotekelezwa
katikataasisi zao.


46. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15,Wizara
itaendelea kusimamia kada ya ukaguzi wa ndanina kamati
za ukaguzi; kufanya ukaguzi wa Mfumo
waulipajiMishaharaSerikalini;k uhakikimadaimbalimbali
ya Serikali kabla ya kuyalipa; na kufuatiliautekelezaji wa
miongozo mbalimbali iliyotolewa. Aidha,Wizara inatarajia
kutoa miongozo ifuatayo: Mwongozowa Usimamizi wa
Viashiria Vya Udanganyifu; Mwongozowa Udhibiti wa
Ndani; Mwongozo wa Ufuatiliaji naTathmini ya Usimamizi
wa Vihatarishi; Mwongozo waUkaguzi wa Ununuzi; na
Mwongozo wa Ukaguzi waMikataba. Vile vile, wizara kwa
kushirikiana na Taasisiza Serikali itaendelea kuimarisha
ofisi za MkaguziMkuu wa ndani kwa lengo la kusimamia
matumizi yafedha.Ukaguzi wa Hesabu za Serikali22


47. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14, Ofisiya
Taifa ya Ukaguzi imetekeleza kazi zake kwa mujibuwa
sheria. Ofisi imeendelea kuwa mshirika katika Bodiya
Ukaguzi ya Umoja wa Mataifa katika kukagua taasisiza
Umoja wa Mataifa. Aidha, Ofisi imeendesha mafunzokwa
Kamati za Kudumu za Bunge za Hesabu za Serikalina
Kamati ya Bajeti kwa lengo la kuzijengea uwezo
wakuimarisha uwajibikaji na utawala bora. Vile
vile,ukaguzi wa mapato na matumizi ya vyama vya
siasavyenye usajili wa kudumu unaendelea.


48. Mheshimiwa Spika, katika juhudi za kuondoawakaguzi
katika majengo ya wakaguliwa, Ofisi ya Taifaya Ukaguzi
imekodi majengo ya ofisi katika mikoa yaMwanza, Tabora,
Tanga, Iringa, Kagera na Geita. Aidha,ujenzi wa ofisi
katika mkoa wa Dodoma unaendeleaukiwa katika hatua za
mwisho. Vile vile, Ofisiimeendelea na uunganishaji wa
ofisi zake zilizokomikoani na makao makuu kwa njiaya
mtandaompana. Kwa mwaka huu ofisi 4 zimeunganishwa
nahivyo kufanya ofisi zilizounganishwa kufikia 14.


49. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2014/15,
Ofisiinatarajia kufanya yafuatayo: kukagua mafungu yote
49ya Wizara na Idara za serikali, hesabu za Mikoa yote
25ya Tanzania Bara, Hesabu za Halmashauri zote 161
zaWilaya, Miji, Manispaa na Majiji, Mashirika ya
Umma177, Balozi zote 32 zilizoko nje ya nchi na Wakala 33
zaSerikali pamoja na kufanya ukaguzi wa thamani yafedha
katika maeneo sita; kuendelea na ukaguzi wamapato na
matumizi ya vyama vyote vya siasa; kuanzaukaguzi katika
sekta ya gesi na mafuta pamoja na23ukaguzi wa miradi
mikubwa inayoendeshwa kwa ubiawa sekta ya Umma na
Sekta binafsi; kuendeleakushiriki kikamilifu katika
jukumu la kukagua taasisiza Umoja wa Mataifa sanjari na
wanachama wenginewanaounda Bodi ya Ukaguzi ya
Umoja wa Mataifa.


50. Mheshimiwa Spika,mambomengineyatakayoteke lezwa
katika mwaka 2014/15, ni pamojana: kuendelea na zoezi la
kuwaondoa wakaguzi katikamaeneo ya wakaguliwa katika
wizara zote na katikamikoa 6 iliyobaki; kuendelea
kuzijengea uwezo kwa njiaya mafunzo Kamati za Kudumu
za Bunge za Hesabu zaSerikali na Kamati ya Bajeti katika
maeneo ya kuelewakwaundanitaarifazaukagu
ziwahesabuzinazoandaliwa na wakaguliwa; kukamilisha
ujenzi waofisi katika mkoa wa Rukwa pamoja na kuanza
ujenziwa ofisi katika mikoa ya Mara na Iringa; na
kutoamafunzo kwa watumishi ili kuimarisha uwezo
waokatika kutumia mfumo wa TeamMate ili kuendana
namabadiliko ya teknolojia katika ukaguzi wa
kisasa.Uratibu wa Utekelezaji wa MKUKUTA


51. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea
kuratibuutekelezaji wa MKUKUTA II kwa kufanya
ufuatiliaji,tafiti, na tathmini na kuandaa taarifa ya
utekelezaji nahali ya Umaskini nchini ili kuwezesha
maamuzi yakisera, kibajeti na kiutekelezaji. Kazi ya
uandaaji waTaarifa ya Mwaka ya Utekelezaji wa
MKUKUTA IIimekamilika na kuwekwa katika tovuti ya
Wizara.Aidha, Wizara inaendelea kukamilisha Taarifa
ya24Maendeleo ya Malengo ya Milenia. Taarifa ya
awaliinaonesha kuwa umaskini wa mahitaji ya msingi
kwaTanzania Bara ni asilimia 28.2 ambapo kwa Dar
esSalaam ni asilimia 4.2, maeneo mengine ya mjini
niasilimia 21.7 na maeneo ya vijijini ni asilimia
33.3.Umaskini wa chakula ni asilimia 9.7 ambapo kwa
Dares Salaam ni asilimia 1.0, maeneo mengine ya mjini
niasilimia 8.7 na maeneo ya vijijini ni asilimia 11.3.


52. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15,Wizara
imepanga kutekeleza yafuatayo: kukusanya nakuchambua
taarifa mbalimbali kutoka katika Wizara,Idara na Wakala
za Serikali ili kuandaa Taarifa yamwaka ya Utekelezaji wa
MKUKUTA II; kuandaa taarifaya mwisho ya kutathimini
utekelezaji wa Malengo yaMaendeleo ya Milenia; kufanya
mapitio ya MKUKUTA II;kukamilisha Mpango wa
Utekelezaji wa Kinga ya Jamiipamoja na kuainisha
viashiria vya upimaji juhudi zakinga ya jamii; na kuratibu
mkutano wa kitaifa wakujadili sera za kupambana na
Umaskini nchini. PiaWizara kwa kushirikiana na wadau
mbalimbaliinaandaa mapendekezo ya hatua zitakazofuata
baadaMKUKUTA II kufikia kikomo mwezi Juni, 2015.


53. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Mradi waSELF II
imeendelea kutoa mikopo kwa wajasiriamaliambapo hadi
kufikia Aprili 2014, mikopo yenye thamaniya shilingi
bilioni 8.6 ilikopeshwa kwa wajasiriamali4,943 kupitia
Asasi ndogo 103. Kati ya waliokopeshwa,wanawake ni
2,040 sawa na asilimia 41 na wanaume ni2,903 sawa na
asilimia 59. Kwa wastani, urejeshwaji waMikopo ya Mradi
wa SELF umeendelea kuwa wa ufanisi25mzuri katika
kiwango cha asilimia 90 hivyo kuwezeshafedha za mkopo
kuzunguka na kuwafikia wananchiwengi zaidi.


54. Mheshimiwa Spika, SELF II imetoa mafunzo
kwawatendaji280waAsasi115zinaz okopeshawajasiriamali
wadogo. Aidha, mafunzo yametolewa kwawajasiriamali
wadogo 1,670 katika taaluma yauendeshaji miradi ya
biashara. Vile vile, MaofisaUshirika 81 kutoka mikoa ya
kanda za Kaskazini naZiwa walipatiwa mafunzo ya utoaji
mikopo. Kadhalika,Mradi umeendelea kuelimisha umma
kupitia vituo vyatelevisheni vya TBC, ZBC na redio za
jamii. Katikamwaka 2014/15, Mradi wa SELF utaendelea
namajukumu yake ya kutoa huduma za mikopo
kwawajasiriamali wadogo na kuimarisha huduma
zakifedha kwa njia ya kujenga uwezo wa
Asasizinazokopesha wajasiriamali wadogo.Sheria na
Miswada ya Fedha


55. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,Wizara kwa
kushirikiana na Ofisi ya MwanasheriaMkuu wa Serikali
ilifanya marekebisho ya Sheriambalimbali za Fedha
kupitia Sheria ya Fedha ya mwaka2013 -The Finance Act,
2013. Lengo la marekebishohayo ni kuweka usimamizi
mzuri wa kodi na fedha zaumma. Aidha, Sheria
mbalimbali zilizopitishwa naBunge ni pamoja na Sheria ya
Mfuko wa Akiba waGEPF wa Mafao ya Wastaafu ya
mwaka 2013 -The GEPFRetirement Benefit Fund Act,
2013 na marekebisho yaSheria ya Ushuru wa Bidhaa ya
mwaka 2013 (The26Excise (Management and Tariff)
(Amendment) Act, 2013)yaliyopitishwa na Bunge katika
Mkutano wa 13 mweziDesemba, 2013 yaliyolenga kuondoa
kodi ya ushuru wabidhaa kwenye Sim Card.


56. Mheshimiwa Spika, Wizara pia iliandaa
Kanunimbalimbali ili kuwezesha usimamizi na utekelezaji
waSheria za fedha. Kanuni hizo ni pamoja na Kanuni
zaKodi ya Mapato kuhusu Gharama za Kuhamisha -
Transfer Pricing Regulations, 2013, Kanuni za Sheria
yaUnunuzi wa Umma, 2013 - Public
ProcurementRegulations, 2013, Kanuni za Uanzishwaji wa
Baraza laUsuluhishi wa Bima, 2013 -The Insurance
OmbudsmanRegulation, 2013, Kanuni za Uanzishwaji wa
chombocha kushughulikia Rufaa za masuala ya Bima,
2013 -The Insurance Appeals Tribunal Regulations, 2013
naKanuni za Bima Ndogo The Micro-
InsuranceRegulations, 2013.


57. Mheshimiwa Spika, katika mkutano wa Bunge laBajeti
unaoendelea Wizara inatarajia kuwasilishaMuswada wa
kutunga Sheria mpya ya Kodi yaOngezeko la Thamani -
Value Added Tax -VAT na Sheriaya Usimamizi wa Kodi -
Tax Administration Act.


58. Mheshimiwa Spika, katika mwaka
2014/15,Wizaraitakamilishamaandaliz
iyakufanyiamarekebisho Sheria ya Msajili wa Hazina -
TreasuryRegistrar Act, Sheria ya Takwimu (Statistics Act)
naSheria ya Fedha za Umma -Public Finance Act.
Aidha,Wizara ipo katika maandalizi ya kuwezesha
kutungwakwa Sheria ya Kodi ya Hoteli -Hotels Tax Act na
kufanya27marekebisho ya Sheria ya Mikopo, Misaada
naDhamana za Serikali - Government Loans, Grants
andGuarantees Act.Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta
Binafsi PPP


59. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kupokeana
kuchambua maandiko ya miradi
inayokusudiwakutekelezwa kwa utaratibu wa ubia kati ya
Sekta yaUmma na Sekta Binafsi. Katika mwaka
2013/14,Wizara imepokea na kuchambua miradi minne ya
PPP.Katika uchambuzi wa miradi imebainika kwamba
kunaupungufu katika upembuzi yakinifu pamoja na
ukosefuwa Wataalam wa kufanya upembuzi huo. Aidha,
Wizaraimeshiriki kutoa mapendekezo ya kurekebisha
Sheriaya Ubia Na. 18 ya mwaka 2010 pamoja na kanuni
zakekwa lengo la kuweka usimamizi mzuri wa ubia.


60. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15Wizara
imetenga fedha za kuanzisha Mfuko waKuwezesha
Utekelezaji wa Miradi ya Ubia -PPPFacilitation
Fund.Udhibiti wa Fedha Haramu na Ufadhili wa Ugaidi


61. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,Wizara
kupitia Kitengo cha Udhibiti wa Fedha Haramuimepokea
na kuchambua taarifa 46 za miamala shukuinayohusu
fedha haramu na ufadhili wa ugaidi
nataarifa14zakiintelijensia28z imewasilishwa kwenye
vyombovinavyosimamiautekelezaj i wa sheria. Aidha,
mafunzo ya kudhibitifedha haramu na ufadhili wa ugaidi
yametolewa kwawatoa taarifa 135 na washiriki 86 kutoka
katikavyombo vinavyosimamia utekelezaji wa Sheria
yaUdhibiti wa Fedha Haramu na Mali Athirika. Vile
vile,mafunzo hayo yametolewa kwa washiriki 49
kutokaMamlaka za Udhibiti.


62. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15,Wizara
kupitia Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramuitatekeleza
yafuatayo: kupokea na kuchambua taarifaza miamala
shuku inayohusu utakasishaji wa fedhaharamu na ufadhili
wa ugaidi; kutoa mafunzo kwavyombo vinavyosimamia
utekelezaji wa sheria na kwawatoa taarifa; kutoa miongozo
ya kudhibiti fedhaharamu na ufadhili wa ugaidi kwa watoa
taarifa;kuratibu zoezi la kutathmini mianya na viashiria
vyafedha haramu na ufadhili wa ugaidi katika
sektambalimbali nchini; na kuendelea na hatua za
kujiungana Umoja wa Kupambana na Biashara ya
FedhaHaramu na Ufadhili wa Ugaidi Duniani -
EGMONTGroup of Financial Intelligence Units.Tume ya
Pamoja ya Fedha


63. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,Wizara
kupitia Tume ya Pamoja ya Fedha imekamilishaStadi ya
Kubainisha Mfumo Bora wa Kodi wa Jamhuriya
Muungano wa Tanzania, pamoja na kuendelea
na29Uchambuzi wa Uhusiano wa Mwenendo wa Uchumi
naMapato ya Muungano.


64. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15,Wizara
kupitia Tume ya Pamoja ya Fedha inatarajiakukamilisha
Stadi ya Kubainisha Mwenendo waUchumi na Mapato ya
Muungano wa Tanzania, nakufanya Stadi ya Uwekezaji
katika Mambo yaMuungano. Aidha, Tume inatarajia
kuhuisha Takwimumbalimbali za Stadi zilizofanywa na
Tume.Habari, Elimu na Mawasiliano kwa Umma


65. Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha kwambaWadau
mbalimbali wanapata taarifa zinazohusu kazina
majukumu ya Wizara, Wizara imetoa elimu kwaumma
kupitia vyombo mbalimbali vya habari. Aidha,Wizara
imeandaa machapisho na vipeperushi kwa ajiliya kuelezea
mafanikio, changamoto na njia zilizotumikakatika
kukabiliana na changamoto hizo.


66. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15,Wizara
itaendelea kuandaa taarifa kuhusu utekelezajiwa
majukumu yake na kuelimisha umma kupitiavyombo vya
habari, maonesho, machapisho navipeperushi. Aidha,
Wizara itakamilisha Mkakati waMawasiliano.Masuala ya
Watumishi




67. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea
kuchukuahatua mbalimbali za kujenga uwezo wake ili
iwezekutekeleza majukumu yake kwa ufanisi. Hatua hizo
ni30pamoja na: kupeleka watumishi katika mafunzo
yamuda mfupi na mrefu, kuajiri watumishi 10,kuthibitisha
watumishi 21 kazini, kupandisha vyeowatumishi 131,
kuboresha mazingira ya kazi kwakukarabati baadhi ya ofisi
na kununua vifaa vya ofisi.Aidha, Wizara imeendelea
kutoa huduma stahiki kwaWatumishi wa Wizara
wanaoishi na virusi vya UKIMWIna kutoa elimu ya afya
kwa wafanyakazi.


68. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15,Wizara
inatarajia kuajiri watumishi 257 wa kadambalimbali;
kupandisha vyeo watumishi 490; nakuthibitisha kazini
watumishi 10. Aidha, Wizarainatarajiakuwapatiawatum
ishi642mafunzombalimbali ya kuwajengea uwezo katika
kutekelezamajukumu yao, kutoa elimu kuhusu magonjwa
sugu nakutoa huduma stahiki kwa watumishi wa
wizarawanaoishi na virusi vya UKIMWI.Usimamizi wa
Mashirika na Taasisi za Umma


69. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,Wizara
kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina imechambuana
kutangaza katika Gazeti la Serikali mashirika 10ambayo
yanatakiwa kuchangia asilimia 10 ya mapatoghafi katika
Mfuko Mkuu wa Serikali. Hadi
kufikiaAprili2014,kiasichashil
ingibilioni25.0kimekusanywa ikiwa ni asilimia 69.4 ya
makadirio yakukusanya shilingi bilioni 36 kwa mwaka
2013/14.31Aidha, katika kutekeleza zoezi la kuingia
mikataba yautendaji na Bodi za mashirika ya umma,
Wizarainakamilisha majadiliano na Bodi za mashirika
yaumma. Vile vile, zoezi la kumpata Msajili wa
Hazinalimefikia hatua za mwisho. Matarajio ni kwamba
uteuziutafanyika kabla ya mwisho wa mwaka huu wa
fedha.


70. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15,Wizara
inatarajia kutekeleza yafuatayo: kusimamiautendaji wa
Bodi za Wakurugenzi wa mashirika nataasisi za umma na
kuingia mikataba ya utendaji naBodi za mashirika ya
umma; kusimamia mikakati yakurekebisha mashirika ya
umma na kufanya tathminina ufuatiliaji wa Mashirika ya
Umma yaliyobinafsishwa;na kuimarisha usimamizi wa
mashirika na taasisi zaumma ili kuongeza mapato ya
Serikali.


71. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,Wizara
kupitia Shirika Hodhi la Mali za Umma (CHC)imeendelea
na zoezi la ubinafsishaji na urekebishaji wamashirika ya
Umma. Wizara inaendelea na zoezi
latathminiyautendajiwamashirik
amengineyaliyobinafsishwa kwa lengo la kufahamu
kamamakubaliano ya mikataba ya mauzo yanazingatiwa
nakuchukua hatua stahiki.Mafao ya Wastaafu na Mirathi


72. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea
kuboreshakumbukumbu za Wastaafu, kulipa mafao na
michango32ya kisheria kwa wakati. Hadi Aprili 2014,
kumbukumbuza wastaafu 142,014 zimehifadhiwa kwenye
mfumo wakompyuta - SAPERION na shilingi bilioni
220.79 sawana asilimia 87 ya makadirio kimelipwa kama
mafao yawastaafu wanaolipwa Pensheni na Hazina.
Aidha,Wizara imefanya uhakiki wa wastaafu walio
kwenyeDaftari la Pensheni la Hazina katika mikoa tisa.
Vilevile, shilingi bilioni 522.86 sawa na asilimia 76
yamakadirio ya mwaka kimelipwa kama michango
yamwajiri kwa watumishi wa Serikali Kuu na Serikali
zaMitaa wanaochangia kwenye Mifuko ya Hifadhi ya
Jamiipamoja na michango ya Bima ya Afya.


73. Mheshimiwa Spika,Wizaraimeendeleakusimami a na
kuratibu shughuli za Mfuko wa Penshenikwa Watumishi
wa Umma - PSPF, Mfuko wa Pensheniwa PPF na Mfuko
wa Mafao ya Kustaafu - GEPF.Utekelezaji wa Mifuko hiyo
kwa mwaka 2013/14ulikuwa kama ifuatavyo:Mfuko wa
Pensheni kwa Watumishi wa Umma - PSPF


74. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Aprili 2014,Mfuko wa
Pensheni kwa Watumishi wa Ummaulikusanya shilingi
bilioni 492.29 ambapo kati ya hizomichango ya
wanachama ni shilingi bilioni 402.24 namapato
yatokanayo na vitega uchumi ni shilingi bilioni90.05.
Aidha, shilingi bilioni 490.95 zilitumika kulipamafao ikiwa
ni pamoja na mafao ya kiinua mgongo napensheni za kila
mwezi. Katika mwaka 2014/15, Mfukounatarajia
kukusanya jumla ya shilingi bilioni 798.12kutoka vyanzo
mbalimbali.33Mfuko wa Mafao ya Kustaafu - GEPF


75. Mheshimiwa Spika, Mfuko wa Mafao ya Kustaafuwa
GEPF ambao awali ulikuwa ukijulikana kama Mfukowa
Akiba ya Wafanyakazi Serikalini, umebadili mfumowa
malipo ya mafao kutoka akiba na kwenda kwenyemfumo
wa pensheni. Mabadiliko haya yamefanywa kwamujibu wa
Sheria Na. 8 ya mwaka 2013 iliyopitishwa naBunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. HadiAprili 2014,
Mfuko umeweza kusajili jumla yawanachama 10,289
ambapo wanachama 8,138 nikutoka sekta isiyo rasmi.
Aidha, michango yawanachama ilifikia kiasi cha shilingi
bilioni 31.68 sawana asilimia 79.95 ya lengo la kukusanya
jumla yashilingi bilioni 39.62 ifikapo Juni 2014. Vile
vile,mapato yatokanayo na vitega uchumi yamefikia
shilingibilioni 17.86 ambayo ni sawa na asilimia 84 ya
lengo lakukusanya shilingi bilioni 21.26 kufikia Juni
2014.Thamani ya Mfuko hadi mwezi Aprili 2014 imekua
nakufikia shilingi bilioni 239.56.


76. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15,Mfuko
utaendelea na jitihada zake za kupanua wigo
wawanachama na hivyo kusajili wanachama zaidi
katikasekta zote kwa maana ya sekta rasmi na sekta
isiyorasmi. Mfuko unatarajia kusajili jumla ya
wanachama23,190 na kukusanya michango yenye thamani
yashilingi bilioni 47.54. Aidha, mapato yanayotokana
navitega uchumi yanatarajiwa kuongezeka hadi
kufikiashilingi bilioni 23.99. Thamani ya Mfuko
inategemeakukua hadi kufikia shilingi bilioni 310 ifikapo
Juni,2015.34Mfuko wa Pensheni wa PPF


77. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013, Mfukowa
Pensheni wa PPF ulikusanya shilingi bilioni 278.57ikiwa ni
michango ya wanachama ambayo ni ongezekola asilimia
18 ikilinganishwa na shilingi bilioni 235.89zilizokusanywa
mwaka 2012. Aidha, idadi yawanachama wanaochangia
katika Mfuko imeongezekakufikia wanachama 247,418
kutoka wanachama203,981 mwaka 2012. Vile vile, mapato
yatokanayo nauwekezaji yaliongezeka kufikia shilingi
bilioni 305.2kutoka shilingi bilioni 111.15 mwaka 2012
ikiwa niongezeko la asilimia 174.5. Kadhalika, thamani
yamfuko imeongezeka kufikia shilingi trilioni 1.49 ikiwa
niongezeko la asilimia 36.5 ikilinganishwa na thamani
yamfuko ya shilingi trilioni 1.092 ilivyokuwa mwaka
2012.78. MheshimiwaSpika,ThamaniyaMfuko inategemea
kukua hadi kufikia shilingi trilioni 1.729ifikapo mwishoni
mwa mwaka 2014. Aidha, mapato yauwekezaji
yanatarajiwa kufikia shilingi bilioni 180.64.Vile vile,
Mfuko unategemea kuandikisha jumla yawanachama
80,000 kutoka katika sekta ya Umma nabinafsi.Mamlaka
ya Mapato Tanzania TRA


79. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Aprili 2014,mapato
halisi ya kodi yalifikia shilingi bilioni 7,771.5sawa na
asilimia 75 ya lengo la mwaka la kukusanyashilingi bilioni
10,395.4. Kodi zilizochangia zaidi ni35pamoja na Kodi ya
Ongezeko la Thamani, Kodi yaKampuni na Kodi ya
Mapato ya Ajira ambazo kwapamoja zilichangia zaidi ya
asilimia 80 ya mapato hayo.




80. Mheshimiwa Spika, licha ya hatua mbali mbaliambazo
zimechukuliwa katika kipindi cha mwaka2013/14,
kumekuwa na changamoto katika kufikialengo la
makusanyo ya mapato. Sababu zilizochangiakutofikia
malengo ni pamoja na: mapato pungufu yaKodi ya
Kampuni kuliko ilivyotarajiwa kutoka kwenyebaadhi ya
kampuni za madini; kushuka kwamakusanyo hususan
Kodi ya Zuio kutokana nakupungua kwa makusanyo
kwenye shughuli za utafitiwa gesi na mafuta. Sababu
nyingine ni pamoja nakufutwa kwa Tozo ya Kadi za Simu
SIMcard levy; namakusanyo hafifu kutoka kwenye Ushuru
wa Bidhaawa Huduma za Uhawilisho wa Fedha (Money
Transfers).Kwa upande wa Forodha sababu
zilizochangiakutofikiwa kwa lengo la makusanyo ni ukuaji
mdogo wauingizwaji wa bidhaa kutoka nje, na ongezeko
lakuingiza bidhaa kupitia njia zisizo rasmi (panya roads)na
bandari bubu.


81. Mheshimiwa Spika, katika jitihada za
kudhibitiukwepaji kodi, wizara kupitia TRA inachukua
hatuakadhaa za kudhibiti upotevu wa mapato kupitia
bandaribubu na panya roads, kwa kufanya upelelezi
ilikuzigundua njia hizo na kuzidhibiti kwa kutumia
KikosiKazi cha Kuzuia Magendo (Flexible Anti-
SmugglingTeam). Aidha, elimu kwa wafanyabiashara na
wananchiwanaozunguka eneo la Pwani imeendelea
kutolewa,ushirikiano na vyombo vingine vya udhibiti
yaani Polisi36Uhamiaji na Usalama wa Taifa
umeanzishwa; nakufanya doria katika maeneo hayo.


82. Mheshimiwa Spika, katika juhudi za
kuimarishamakusanyo ya kodi, Mamlaka inaendelea
kuimarishamatumizi ya Mashine za Kieletroniki za kutoa
Risiti(Electronic Fiscal Devices-EFDs) ambapo kwa
sasainakamilisha zoezi la kuwaingiza wafanyabiashara
wotewanaostahili kuanza kutumia mashine hizo,
kuanzishaMfumo wa Uthamini wa Mizigo ya Forodha
TanzaniaCustoms Integrated System-TANCIS ambao
umeanzakutumika mwezi Aprili 2014 pamojamatumizi
yamfumo wa kuthamini magari chakavu; na,
kuanzishaKitengo cha Kodi ya Kampuni za Kimataifa
InternationalTax Unit kwa lengo la kubaini na kudhibiti
mianya yakupotea kwa kodi inayolipwa na kampuni za
kimataifazilizowekeza nchini.


83. Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Mamlaka
yaMapato Tanzania imeanza kutekeleza makubaliano
yaJumuiya ya Afrika Mashariki ya kuweka mazingira
yakuanzishwa kwa Mfumo wa Himaya Moja ya
Forodha(Single Customs Territory - SCT) kuanzia Januari,
2014.Ili kuhakikisha kwamba mizigo ya nchi jirani
haiuzwinchini kinyume na utaratibu wa forodha, mfumo
wa ki-eletroniki wa ufuatiliaji wa mizigo
inayosafirishwautatumika. Kupitia mfumo huu, mizigo na
ama vyombovya usafirishaji hufungwa lakili ya ki-
eletroniki(electronic seal) na kifaa cha mawasilaino
ambavyohuunganishwa na mfumo mkuu ili
kuonesha37mwenendo mzima wa usafiri hadi mzigo
husikautakapovuka mpaka wa nchi. Aidha, mbinu
nyingine zaudhibiti saidizi kama doria, usuluhishi wa
taarifa(reconciliation) na ukaguzi zitatumika ili
kuongezaudhibiti.Rufaa za Kodi


84. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14, Bodiya
Rufaa za Kodi, imepokea jumla ya rufaa 129 namaombi 37,
na imesikiliza na kutolea maamuzi rufaa116 na maombi
28. Aidha, Bodi ipo katika hatua yakuchapisha Ripoti ya
Maamuzi yaRufaa za Kodizilizoamuliwa kuanzia mwaka
2009 - 2010. Kwa upandewa Baraza la Rufaa za Kodi,
jumla ya rufaa 34 namaombi 4 yamepokelewa ambapo
rufaa 41 na maombi9 yamesikilizwa na kutolewa maamuzi.
Idadi hiiinajumuisha rufaa na maombi ambayo
hayakusikilizwamwaka 2012/13.


85. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15,Wizara
kupitia Bodi ya Rufaa na Baraza la Rufaa zaKodi
itaendelea kupokea, kusikiliza na kutoleamaamuzi rufaa za
kodi; kutoa elimu kwa walipa kodijuu ya taratibu za kukata
rufaa za kodi; na kutoamafunzo kwa wajumbe wa Bodi na
Baraza juu yataratibu za kutatua migogoro ya kodi
itokanayo nasheria za Kodi zinazosimamiwa na Mamlaka
ya MapatoTanzania. Aidha, Bodi ya Rufaa na Baraza la
Rufaa zaKodi linatarajia kuchapisha Ripoti ya Maamuzi ya
Rufaa38za Kodi zinazojumuisha maamuzi yaliyotolewa
mwaka2011 hadi 2012 kwa ajili ya rejea kwa wadau
wake.Huduma za KibenkiBenki Kuu ya Tanzania


86. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Benki
Kuuimeendelea kusimamia Sekta ya Kibenki ambapo
katiya kipindi cha Machi 2013 na Machi 2014, idadi
yabenki na taasisi za fedha imeongezeka kutoka 51
namatawi 585 hadi 53 na matawi 625 kote nchini. Jumlaya
mali ya sekta ya kibenki imekua kutoka shilingitrilioni 17.9
hadi shilingi trilioni 21.1. Kiwango chamitaji kilifikia
wastani wa asilimia 18.5 ikilinganishwana kiwango cha
asilimia 10 kinachotakiwa kwa mujibuwa sheria. Aidha,
Mfumo wa Taarifa za Wakopaji CreditReference Bureau
unaendelea vyema, ambapo hadi sasakampuni mbili
zimepewa leseni ambazo ni: kampuni yaCreditinfo
Tanzania Limited iliyoanza kazi Juni 2013,na kampuni ya
Dun & Bradstreet Credit Bureau (T)Limited iliyoanza kazi
Septemba 2013. Kampuninyingine kwa jina la Transunion,
nayo hivi karibuniimepewa leseni ya muda na inajiandaa
kuanza kufanyakazi.


87. Mheshimiwa Spika, Kampuni hizi kwa
sasazinaandaataarifazawatejaku tokakwenyekumbukumbu
ambazo zinahifadhiwa Benki Kuu.Taarifa hizi bado
zinafanyiwa uhakiki kabla ya kuanzakutumika rasmi.Mara
baada ya data bank hiyo39kukamilika, makampuni haya
ya Credit Referenceyataanza kufanya kazi hiyo kikamilifu
na kwa usahihi.Benki Kuu inaendelea kuyahimiza mabenki
ambayobado hayajawasilisha taarifa kufanya hivyo.


88. Mheshimiwa Spika, Tarehe 30 Novemba 2013,Marais
wa Afrika Mashariki walitia sahihi Itifaki yaUmoja wa
Fedha ya Afrika Mashariki. Tukio hili, ndilolimeanzisha
safari yetu ya kwenda kwenye hatua yakuwa na sarafu
moja ifikapo mwaka 2024. Chini yaItifaki hii,
tumekubaliana vigezo ambavyo tutatakiwatufikie kabla ya
kuingia kwenye umoja huo na roadmap ya miaka 10
ambayo itaanza kutekelezwa mara tubaada ya nchi zote
kuridhia utekelezaji wake. Katikampango huo, mambo
muhimu ni; kukamilishautekelezaji wa Umoja wa forodha
na Itifaki ya soko lapamoja; kuoanisha mifumo ya kifedh,
sera zaubadilishaji wa fedha za kigeni, sera za bajeti,
namifumo ya malipo; uhuisha mifumo ya takwimu
na;kuhuisha sheria zote zinazohusiana na uanzishwaji
waumoja wa kifedhaBenki ya Maendeleo TIB - TIB
Development Bank


89. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,
TIBDevelopment Bank (zamani Benki ya
Rasilimali)iliendelea na marekebisho ya ndani ambapo
shughuli za40Benki zimegawanywa katika kampuni mbili
ambazo niTIB Development Bank Limited inayohusika na
shughuliza maendeleo na TIB Corporate Finance
Limitedinayohusika na shughuli za biashara.


90. Mheshimiwa Spika, katika mwaka ulioishiaDesemba
2013, Benki ya Maendeleo TIB ilipata faida(kabla ya kodi)
ya shilingi bilioni 11.9 ikiwa ni ongezekola asilimia 78 toka
shilingi bilioni 6.7 zilizopatikanamwaka ulioishia Desemba
2012. Aidha, waraka mizaniawa benki ulifikia shilingi
bilioni 408.7 ikilinganishwa nashilingi bilioni 338.4
Desemba 2012;Mikopoiliongezeka kufikia shilingi bilioni
307.0 toka shilingibilioni 242.9 Desemba 2012.


91. Mheshimiwa Spika, Dirisha la Kilimo katika Benkiya
Maendeleo TIB liliendelea kutoa mikopo kwawakopaji
mbalimbali kwa riba nafuu. Tangu kuanzakwa Dirisha
mwaka 2010 hadi kufikia Aprili 2014,maombi yenye
thamani ya shilingi bilioni 58.8yaliidhinishwa. Kati ya
hizo, shilingi bilioni 33.6zilikopeshwa kwa kampuni za
wakulima wadogo na wakati, shilingi bilioni 8.7 zilienda
kwa taasisi ndogo zafedha zinazokopesha wakulima
wadogo na wa kati; nashilingi bilioni 16.5 zilikopeshwa
kwa vikundi vyakuweka na kukopa (SACCOS).Benki ya
Maendeleo ya Kilimo - TADB


92. Mheshimiwa Spika, kufuatia uamuzi wa
Serikalikuanzisha Benki ya Kilimo, Wizara
imetekelezayafuatayo: kuzindua Bodi ya Wakurugenzi wa
Benki;41kukamilisha zoezi la upatikanaji wa Mtendaji
Mkuu naWakuu wa Idara; kuandaa Muundo wa Benki
naMuundo wa Utumishi; kuandaa majukumu
yawafanyakazi; kuandaa rasimu ya Mpango wa
Biashara;na kupatikana kwa ofisi za Benki. Mwaka
2014/15,Benki ya Maendeleo ya Kilimo inatarajia kupata
leseniya biashara, kuajiri wafanyakazi na kuanza
kutoahuduma.Twiga Bancorp


93. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,Twiga
Bancorp imeendelea kutoa huduma kwa kutumiamatawi
makubwa matano na madogo matano. Hadikufikia Aprili
2014, mikopo ya shilingi bilioni 41.9ilitolewa kwa wateja
mbalimbali. Uwekezaji kwenyeDhamana za Serikali na
Amana katika Benki zingineulikuwa shilingi bilioni 3.6 na
mapato yaliyokusanywana Taasisi yalifikia ya shilingi
bilioni 3.86.


94. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15Wizara
itaendelea kuboresha utendaji wa Taasisi kwakuimarisha
uongozi. Aidha, Taasisi itaongeza wigo wahuduma kwa
kuanzisha huduma mbalimbali kama vileMax Malipo, Tigo
Pesa, M-Pesa na Airtel Money nabiashara kwa uwakala.
Vile vile, Taasisi inatarajiakufungua tawi jipya
Kigamboni.Benki ya Posta TPB


95. Mheshimiwa Spika, katika kupanua wigo wabiashara
na kupeleka huduma za kibenki vijijini, Benkiya Posta
kupitia ofisi za Shirika la Posta Tanzania42imeziunganisha
ofisi nane za Tunduma, Makambako,Peramiho, Masasi,
Njombe, Nachingwea, Kilwa naKahama katika mtandao
wa TEHAMA na hivyokuongeza idadi ya ofisi za Shirika la
Posta ambazozinatoa huduma za kibenki kufikia 17. Aidha,
hudumakwa wateja zilitolewa kwa kutumia mashine 185
zaATM.


96. Mheshimiwa Spika, amana za wateja
ziliongezekakutoka shilingi bilioni 138.86 mwaka 2012
hadi kufikiashilingi bilioni 170.03 mwaka 2013 sawa na
ongezeko laasilimia 22.4. Aidha, uwekezaji katika
dhamana zaSerikali uliongezeka kutoka shilingi bilioni
39.67 hadikufikia shilingi bilioni 45.73 katika kipindi
hicho sawana ongezeko la asilimia 19.8. Aidha, thamani ya
mikopoinayotolewa kwa wateja iliongezeka kutoka
shilingibilioni 100.89 hadi kufikia shilingi bilioni 119.73
ikiwani ukuaji wa asilimia 18.7. Vile vile, faida kabla ya
kodiimeongezeka kutoka shilingi bilioni 5.67 hadi
kufikiashilingi bilioni 6.99 sawa na ongezeko la asilimia
23.4.


97. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014, TPBinatarajia
kufikia malengo yafuatayo: kukuza rasilimaliza benki hadi
kufikia shilingi bilioni 237.10; kuongezaidadi ya wateja
wapya 300,000; kuongeza amana zawateja kufikia shilingi
bilioni 200.10; kuongeza mikopoya wateja kufikia shilingi
bilioni 47.16; kupata faidakabla ya kodi ya shilingi bilioni
8; na kuendelea nataratibu za kurekebisha sheria
iliyoianzisha Benki ilikuisajili chini ya Sheria ya
Kampuni.43Sera ya Taifa ya Huduma Ndogo za Kifedha


98. Mheshimiwa Spika, Wizara imeanza kufanyamapitio
ya Sera ya Taifa ya Huduma Ndogo za Kifedha -National
Microfinance Policy, 2000 ili kuondoamapungufu ya
kisheria yaliyojitokeza katika utekelezajiwake kwa lengo la
kuzingatia mabadiliko ya kiuchumina kijamii pamoja na
kuweka mazingira mazuri katikaukuaji wa sekta hiyo.
Aidha, katika mwaka 2014/15,Wizara itakamilisha
maandalizi ya Sera ya Taifa yaTaasisi Ndogo za Huduma
za fedha pamoja na kutungaSheria ya Taasisi ndogo za
huduma za kifedha -Microfinance Act.Huduma za
BimaMamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima TIRA


99. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,Wizara
kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli zaBima
imekamilisha na kutoa Mkakati wa KuendelezaBima ya
Watu wa Kipato cha Chini - National MicroInsurance
Strategy 2014-2017. Aidha, hadi kufikia Aprili2014,
kampuni 30, madalali 100 na mawakala 500 wabima
walisajiliwa. Vile vile, mauzo ya bima yaliongezekakutoka
shilingi bilioni 406.7 mwaka 2012/13 hadikufikia shilingi
bilioni 481.7 sawa na ongezeko laasilimia 18.5.


100. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15,TIRA
inatarajia kutekeleza yafuatayo: kuendelea namaandalizi
ya kufungua ofisi nyingine za kanda;44kuendelea na
utaratibu wa uoanishaji sheria na kanuniza soko la bima
katika eneo la Afrika Mashariki na lilela nchi za SADC;
kuendelea na tafiti za bima ya kilimo,mifugo, pamoja na
bima za watu wa kipato cha chini;na kukamilisha taratibu
za kuanzisha bima ya Takaful.Shirika la Bima la Taifa
NIC


101. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,Wizara
ilikamilisha urekebishaji wa Shirika la Bima laTaifa na
usimikaji wa mfumo wa TEHAMA kwa lengo lakuongeza
ufanisi. Utendaji wa Shirika kibiasharauliendelea
kuimarika ambapo mapato ya bimayaliongezeka kutoka
shilingi bilioni 27.38 mwaka 2012,hadi kufikia shilingi
bilioni 31.53 mwaka 2013,ongezeko hilo ni sawa na
asilimia 15. Mapato hayayalitokana na makusanyo ya bima
za mtawanyo, vitegauchumi na mapato mengine.


102. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Desemba 2013,NIC
ililipa madai ya wateja ya shilingi bilioni 8.31.Malipo hayo
yalilipwa kwa wateja wa bima za maishakiasi cha shilingi
bilioni 5.71 na wateja wa bima zakawaida kiasi cha shilingi
bilioni 2.60.


103. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2014/15,Wizara
itaendelea na mkakati wa kuligawa Shirikakatika kampuni
mbili, ambayo ni Kampuni ya Bima zaMaisha na Kampuni
ya Bima za Kawaida. Aidha,Shirika litaendelea na mkakati
wa kujitangaza zaidi na45kuongeza biashara kwa kubuni
bima mpya zinazokidhimahitaji ya wananchi.Masoko ya
Mitaji na DhamanaMamlaka ya Masoko ya Mitaji na
Dhamana


104. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,Wizara
kupitia Mamlaka ya Masoko ya Mitaji naDhamana
imeendelea kusimamia Soko la Hisa la Dar esSalaam,
kampuni za udalali na ushauri wa uwekezaji,mipango ya
uwekezaji wa pamoja na kampunizilizoorodheshwa
kwenye Soko la Hisa . Aidha, Mamlakaimetekeleza
yafuatayo: kuzindua Soko la KukuzaKampuni na
Ujasiriamali ambapo Benki ya Maendeleoiliorodhesha hisa
zake; na kuendelea na maandalizi yauanzishwaji wa soko
la Hatifungani za Manispaa.


105. Mheshimiwa Spika, katika kutimiza azma yaSerikali
ya kuhakikisha kampuni za Mawasiliano, Gesina Madini
zinaorodhesha hisa zake kwenye soko la Hisala Dar es
Salaam, Wizara kupitia Mamlaka ya Masokoya Mitaji na
Dhamana kwa kushirikiana na wadauiliandaa taratibu
zinazotakiwa kuzingatiwa. Aidha,Mamlaka iliendelea
kuelimisha umma kuhusu masokoya mitaji na uwekezaji
kwa kupitia warsha, matangazokatika vyombo vya habari,
vipeperushi na machapisho.


106. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15,Wizara
kupitia Mamlaka ya Masoko ya Mitaji naDhamana
imepanga kutekeleza yafuatayo: kukamilishamaandalizi
kwa ajili ya uzinduzi wa Soko la Bidhaa;kuzindua mfumo
wa uwekezaji kwa kutumia mitandao46ya simu za
mikononi (M-akiba) kwa wawekezaji wadogo;kutayarisha
taratibu za kisheria na usimamizi wabidhaa na huduma
mpya zinazotarajiwa kuingizwasokonizikiwemohatifun
ganizahalmashauri;kukamilisha uandaaji wa Mpango
Mkuu wa Kitaifa waMaendeleo ya Masoko ya Mitaji na;
kuanzisha misingiya kusimamia masoko kwa kuzingatia
uzito wa athari.Aidha, Mamlaka itaendelea kuboresha
programu yaelimu kwa umma ili kuboresha na kupanua
ushiriki wawananchi katika masoko ya mitaji.


107. Mheshimiwa Spika, Serikali iko katika hatua
zamwisho za kupata taasisi mbili zitakazoendesha zoezi
latathmini ya kupima uwezo wa nchi wa kukopa nakulipa
madeni yake. Mwezi Februari 2014, Wizarailiziandikia
kampuni za Fitch, Moodys InvestmentServices na
Standard and poors kuwasilisha fomu zaoza mikataba kwa
hatua za uchambuzi. Tayari kampuniya Fitch na Moodys
zimewasilisha fomu za mikatabakupitia kwa mshauri
mwelekezi Citi Group. Aidha,kuchelewa kwa zoezi hili
kulitokana na kampuni hizi zaupimaji (Rating Agencies)
kutokukubaliana na aina yafomu za mikataba
zinazoandaliwa na serikali pamoja nakuleta nyongeza ya
gharama nje ya makubalianoyaliyosainiwa awali.Soko la
Hisa Dar es Salaam


108. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,Soko la
Hisa Dar es Salaam liliorodhesha Hatifunganiza Serikali
zenye thamani ya shilingi bilioni 690 ambazoni asilimia 83
ya makadirio ya mwaka. Kwa upande wahisa za kampuni,
Soko liliorodhesha hisa za Benki ya47Maendeleo zenye
thamani ya shilingi bilioni 4.5 na hisaza ziada na
upendeleo za kampuni ya TOL Gases Ltdzenye thamani ya
shilingi bilioni 4.5. Aidha, Kampuniya Swala Oil and Gas
(T) Ltd (Australia), MwanzaCommunity Bank ya mkoani
Mwanza na UchumiSupermarket(Kenya)ziliwa
silishamaombiyakuorodheshwa. Maombi haya yako katika
hatuambalimbali za kuidhinishwa.109.
MheshimiwaSpika,Thamaniyasokoi meongezeka kutoka
shilingi trilioni 14.10 Julai 2013hadi shilingi trilioni 18.06
Aprili 2014, ambayo ni sawana asilimia 28. Mafanikio
haya yametokana naongezeko la bei ya hisa za kampuni
zilizoorodheshwapamoja na kuorodheshwa kwa kampuni
mpya sokoni.Aidha, idadi ya wawekezaji iliongezeka
kutoka 180,458mwezi Julai 2013 hadi 192,419 mwezi
Aprili 2014.


110. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai2013 hadi
Aprili 2014 hisa zenye thamani ya shilingibilioni 245
ziliuzwa na kununuliwa. Aidha, hatifunganiza Serikali
zenye thamani yashilingi bilioni 286ziliuzwa. Kwa ujumla
mwenendo wa shughuli za Sokokatika kipindi kilichoishia
Aprili 2014 ulikuwa wakuridhisha na viashiria vya
mwenendo wa sokovinaonesha mwelekeo chanya.111.
MheshimiwaSpika,shughulinyingi nezilizotekelezwa na
Soko la Hisa Dar es Salaam nipamoja na: uboreshaji wa
Mfumo wa Mnada kwakuweka Mfumo Mpana Wide
Area Network48unaowawezesha madalali kuuza na
kununua hisawakiwa mahali popote nchini. Aidha, Soko la
Hisa Dares Salaam limekamilisha ukarabati wa jengo la
OfisiMbadala Wakati wa Majanga Disaster Recovery Site
najengo hilo limeanza kutumika.


112. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15,Soko la
Hisa Dar es Salaam linatarajia kutekelezayafuatayo:
kuendelea kuhamasisha na
kuelimishakampuniumuhimuwakuji
orodheshaSokoni;kurahisisha shughuli za minada kwa
kutumia simu naintaneti; kuboresha mfumo wa kuuza na
kununua hisasokoni; na kuendelea na juhudi mbalimbali
zinazolengakuongeza ufahamu wa masuala ya masoko ya
mitajikwa umma.Dhamana ya Uwekezaji Tanzania UTT


113. Mheshimiwa Spika, Dhamana ya UwekezajiTanzania
imebadilisha muundo wake na kuanzishataasisi ndogo
tatu ambazo ni: Taasisi ya Miradi naMaendeleo ya
Miundombinu (UTT Project andInfrastructure
Development Plc), Taasisi ya UtoajiMikopo (UTT
Microfinance Institution UTT MFI), naTaasisi ya
Usimamizi wa Rasilimali za Uwekezaji naHuduma Kwa
Wawekezaji (UTT Asset Management andInvestor Services
- UTT AMIS). Hadi kufikia Aprili, 2014mikopo ya jumla ya
shilingi bilioni 4.3 imetolewa naUTT MFI kwa wananchi
5,785, wanawake wakiwa 4,744na wanaume 1,041.49


114. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15,UTT MFI
inatarajia kuanzisha aina mpya ya mikopo ilikukidhi
mahitaji mbalimbali ya wananchi. Mikopo hiyoni: mikopo
kwa ajili ya wafanyabiashara nawakandarasi; mikopo kwa
ajili ya huduma za afya;mikopo kwa ajili ya kilimo na
viwanda vidogo vidogo;mikopo kwa wakala wa huduma za
fedha; na mikopo yamatengenezo ya nyumba.


115. Mheshimiwa Spika, UTT AMIS inasimamiamifuko
mitano ya uwekezaji wa pamoja ambayo niMfuko wa
Umoja, Mfuko wa Wekeza Maisha, Mfuko waWatoto,
Mfuko wa Jikimu na Mfuko wa Ukwasi. Katikakipindi cha
Julai 2013 hadi Aprili, 2014, thamani yamifuko hiyo
iliongezeka kutoka shilingi bilioni 119.03hadi shilingi
bilioni 167.37 sawa na ongezeko la asilimia40.62.
Ongezeko hili lilitokana na mauzo ya vipandepamoja na
ongezeko la thamani za rasilimali zaDhamana ya
Uwekezaji. Katika mwaka 2014/15, UTTAMIS imepanga
kuanzisha mfuko wa uwekezaji wapamoja katika majumba
(Real Estate Investment Trust REIT).Taasisi za Kitaalam
na Huduma NyinginezoOfisi ya Taifa ya Takwimu


116. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,Ofisi ya
Taifa ya Takwimu imetekeleza yafuatayo:kutayarisha
takwimu za mfumuko wa bei kila mwezi;kutayarisha na
kusambaza Takwimu za Pato la Taifakwa Robo ya Kwanza
na ya pili ya mwaka 2013;50kutayarisha Takwimu za Pato
la Taifa kwa mwaka 2013kwa bei za mwaka 2001; na
kukamilisha matokeo yaawali ya Utafiti wa Mapato na
Matumizi ya Kaya BinafsiNchini wa Mwaka 2012. Aidha,
Ofisi ya Taifa yaTakwimu imefanya uchambuzi wa taarifa
mbalimbali zaSensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 na
kutoaChapisho la Kwanza la Mgawanyo wa Watu kwa
Umrina Jinsia katika Ngazi ya Taifa, Mkoa, Wilaya, Kata
naShehia; Chapisho la Pili lenye Taarifa za Msingi
zaMgawanyo wa Watu Kiumri na Kijinsia. Vile
vile,Chapisho la Tatu lenye Taarifa za Msingi
zaKidemografia, Kijamii na Kiuchumi kwa Jamhuri
yaMuungano wa Tanzania, Tanzania Bara na
TanzaniaZanzibar limekamilika.


117. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15,Ofisi ya
Taifa ya Takwimu itaendelea kuboreshatakwimu rasmi za
kiuchumi na kijamii na kutoamachapisho mbalimbali
kuhusu Sensa ya Watu naMakazi ya mwaka 2012.Aidha,
Ofisi itaendeleakuboresha takwimu za Pato la Taifa kwa
kurekebishamwaka wa kizio wa bei za 2001 kwenda 2007
ikiwa nimoja ya hatua za kuboresha takwimu za kiuchumi
nakijamii ili zilingane na hali halisi ya maendeleo
yauchumi. Vile vile, Ofisi ya Taifa ya Takwimu
itaendeleakufanya Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa
Kufanya Kaziwa mwaka 2014; Utafiti wa Ajira na Bei wa
Mwaka2014; Sensa ya Viwanda ya Mwaka 2014; Utafiti
waKilimo wa mwaka 2014/15; na kuendelea namaandalizi
ya Sheria mpya ya Takwimu.Bodi ya Taifa ya Wahasibu na
Wakaguzi wa Hesabu51


118. Mheshimiwa Spika, hadi Aprili, 2014, Bodi yaTaifa ya
Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu imeendeshamafunzo
ya kitaaluma na kuhudhuriwa na jumla yawashiriki 2,242.
Aidha, Bodi imekamilisha silabi mpyaya mitihani ambapo
mitihani ya kwanza inatarajiwakufanyika Novemba, 2014.
Vile vile, wahitimu 228wamesajiliwakamawatunzavita
bu;Wahasibuwahitimu wanaopatiwa uzoefu wa kazi 2,631;
WahasibuwaliosajiliwangaziyaCP
A1,270;Wahasibuwaliosajiliwa kama Wakaguzi wa Hesabu
katika ngaziya CPA-PP 492; Kampuni za Ukaguzi wa
Hesabuzilizosajiliwa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na
Wakaguziwa Hesabu 170; na Kampuni za Uhasibu
zilizosajiliwana Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi
wa Hesabu19. Vile vile, Bodi imeendelea na awamu ya pili
yaujenzi wa Kituo cha Taaluma ya Uhasibu eneo la Bunju-
Dar es Salaam unaotarajiwa kukamilika
mwaka2014/15.Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi


119. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,Bodi ya
Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi imesajiliwataalamu
2,404 katika ngazi mbalimbali kwa mujibuwa sheria.
Aidha, Bodi imeendesha mafunzo yakitaaluma yaliyolenga
kuboresha uwezo wa utendajiunaozingatia maadili. Vile
vile, Bodi imetahini jumla yawanafunzi 2,455 ambapo
wanafunzi 1,115 walifauluhivyo kufanya idadi ya wahitimu
kufikia 24,660. Bodi52pia imeendelea kutoa mafunzo ya
vitendo kwa wahitimukutoka vyuo vya elimu ya juu. Katika
mwaka 2014/15,Bodi inatarajia kuboresha mazingira ya
kujifunzia kwakuboresha mitaala yake ili iendane na soko
la ajira laUtandawazi.Bodi ya Michezo ya Kubahatisha


120. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,Bodi ya
Michezo ya Kubahatisha imeendelea kutekelezamajukumu
yake ya kusimamia michezo ya kubahatishaambapo hadi
kufikia Aprili 2014, jumla ya kodiiliyokusanywa na Bodi
ilifikia shilingi bilioni 10.78 sawana ongezeko la asilimia
14.4. Aidha, Bodi ilichangiashilingi milioni 532.48 katika
mfuko mkuu wa Serikalisawa na ongezeko la asilimia
0.85.Taasisi za MafunzoTaasisi ya Uhasibu Arusha


121. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,Taasisi ya
Uhasibu Arusha imeendelea kutoa mafunzo53katika fani
za uhasibu, ugavi, benki, Usimamizi waFedha, Usimamizi
wa Rasilimali, Utawala wa Biashara,Teknolojia ya Habari
na Sayansi ya Kompyuta naMasomo ya Kimkakati. Aidha,
jumla ya wanafunzi3,341 wamedahiliwa, ambapo kati yao
wanaume ni1,847 sawa na asilimia 55 na wanawake 1,494,
sawa naasilimia 45.


122. Mheshimiwa Spika, Taasisi kwa kushirikiana naChuo
Kikuu cha Galgotias cha India imeanzishamafunzo ya
shahada za uzamili katika sayansi yakompyuta ambazo ni
Master in Software Engineering,Master in Information
Security na Master in ComputerApplication. Aidha, Taasisi
inaendesha E-learningLibrary ambayo imeonesha
mafanikio makubwa na piaipo katika hatua za awali za
kuanzisha E-learningCenter.


123. Mheshimiwa Spika, Katika mwaka 2014/15,Taasisi
inakusudia kuanzisha mafunzo katika: Shahadaya Uzamili
ya Ununuzi na Ugavi, Shahada ya MafunzoMkakati -
Bachelor in Strategic Studies, Shahada yaSayansi ya
Kijeshi - Bachelor in Military Science naStashahada ya
uzamili katika mafunzo ya bima -Postgraduate Diploma in
Insurance.Chuo cha Usimamizi wa Fedha54


124. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,Chuo cha
Usimamizi wa Fedha kilidahili jumla yawanafunzi 9,998
katika fani mbalimbali. Kati ya haowanawake 3,532 sawa
na asilimia 35 na wanaume6,466 sawa na asilimia 65.
Aidha, Chuo kimeanzishaShahada za Uzamili katika fani
za Uhasibu na Fedha,Fedha na Uwekezaji na Rasilimali
Watu. Vile vile, Chuokimeanzisha tawi katika Jiji la
Mwanza ambapomasomo kwa wanafunzi wa ngazi ya Cheti
naStashahada katika fani ya Uhasibu na Benki
yalianzakutolewa mwaka 2013.Taasisi ya Uhasibu
Tanzania


125. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,Taasisi ya
Uhasibu Tanzania ilidahili jumla yawanafunzi 9,769 kati
ya hao wanawake 4,776 sawa naasilimia 49 na wanaume
4,993 sawa na asilimia 51Aidha, Taasisi ilianzisha kozi
mbili mpya ambazo niUhasibu katika Sekta ya Umma -
Public SectorAccounting na Masoko na Uhusiano wa
Umma -Markerting and Public Relations katika ngazi za
Cheti,Stashahada na Shahada. Vile vile, Taasisi
imeanzaujenzi wa jengo la mihadhara katika Kampasi
yaMtwara lenye uwezo wa kuchukua wanachuo 500.


126. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15,Taasisi
inatarajia kudahili wanafunzi 9,729, kufunguatawi jipya
katika mji wa Kigoma na kuendelea na ujenziwa jengo
katika Kampasi ya Mtwara.55Chuo cha Mipango na
Maendeleo Vijijini


127. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,Chuo
kimedahili jumla ya wanafunzi 5,052 kati yaowanawake
2,360 sawa na asilimia 47 na wanaume2,692 sawa na
asilimia 53. Aidha, wanafunzi 1,846walihitimu masomo
katika kozi mbalimbali ambapo katiya hao wanaume ni
1,037 sawa na asilimia 56 nawanawake walikuwa 809 sawa
na asilimia 44. Vile vile,Chuo kimekamilisha ujenzi wa
jengo la pili la taaluma.Kadhalika Chuo kimetayarisha
taarifa za Hali yaUchumi na Kijamii za Wilaya (District
Socio-EconomicProfiles) za Halmashauri za Bunda,
Ulanga, Kahama,Geita na Manispaa ya Dodoma.


128. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15,Chuo
kitatoa mafunzo ya muda mfupi ya kujenga uwezokwa
watendaji namna ya kupanga, kutekeleza nakusimamia
mipango ya maendeleo kwenye sehemu zaoza kazi.Chuo
cha Takwimu Mashariki mwa Afrika


129. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,Chuo
kilidahili wanafunzi 269 kati ya hao wanawake108 sawa na
asilimia 40 na wanaume 161 sawa naasilimia 60. Aidha,
Chuo kimeanzisha Shahada yaUzamili katika Takwimu
Rasmi na tayari chuo56kimedahili wanafunzi 32 kutoka
nchi za Ethiopia,Ghana, Nigeria, Swaziland na
Tanzania.CHANGAMOTO


130. Mheshimiwa Spika,katikakutekelezamajukumu yake,
Wizara ilikabiliwa na changamotozifuatazo:i. Kuongeza
mapato ya ndani ya Serikali ili kukidhimahitaji
yamatumizi ya maendeleo na yakawaida;ii. Mabadiliko ya
hali ya uchumi na uongozi katikanchi za washirika wa
maendeleo ambapozimepelekea kushindwa kutimizwa
kwa baadhi yamiadi;iii. Uwezo wa kusimamia mikataba
katika kutekelezabaadhi ya miradi na programu za
maendeleo; naiv. Upatikanaji wa mikopo ya kibiashara
kwa wakatikunakotokana na kubadilika kwa
mashartikutoka kwa wakopeshaji.


131. Mheshimiwa Spika, katika kukabiliana nachangamoto
hizo, Wizara imeendelea kuchukua hatuambalimbali ikiwa
ni pamoja na:i. Kubuni vyanzo vipya vya mapato na
kudhibitimatumizi pamoja na kupunguza upotevu
wamapato;ii. Kuboreshaushirikianonawashirik
awamaendeleo yenye lengo la kuwa na uelewa sawakuhusu
masuala mbali mbali katika ushirikianowetu;iii. Kuendelea
kuzijengea uwezo Wizara, Taasisi naMamlaka za Serikali
za Mitaa katika kusimamia57iv.v.na kutekeleza mikataba
ya miradi na programu zamaendeleo;Kuendelea
kutekeleza Programu ya Maboresho yaUsimamizi wa
Fedha za Umma - Public FinancialManagement Reform
Programme (PFMRP); naKushauri Wizara, Mikoa na
Mamlaka za Serikaliza Mitaa kuzingatia vipaumbele
wakati wakupanga na utekelezaji kulingana na
bajetiiliyotengwa.Kuanza mazungumzo mapema na
wakopeshaji wamikopo ya kibiashara.Mapitio ya Mapato
na Matumizi ya Mafungu yaWizara kwa Mwaka 2013/14


132. Mheshimiwa Spika, katika mwaka
2013/14,majukumu ya Wizara yalitekelezwa katika
mafungusaba ya kibajeti. Mafungu hayo ni Fungu 50 -
Wizara yaFedha; Fungu 23 - Idara ya Mhasibu Mkuu wa
Serikali;Fungu 22 - Deni la Taifa; Fungu 21 HAZINA;
Fungu13 - Kitengo cha Udhibiti wa Fedha Haramu; Fungu
10 Tume ya Pamoja ya Fedha; na Fungu 7 Ofisi
yaMsajili wa Hazina. Aidha, Fungu 45 - Ofisi ya Taifa
yaUkaguzi ambayo inajitegemea linaombewa
fedhaBungeni na Waziri wa Fedha kwa mujibu wa
Sheria.Fungu 50 Wizara ya Fedha


133. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Fungu 50ilitarajia
kupata shilingi bilioni 126.48 kutoka vyanzombalimbali
vya mapato yasiyo ya kodi ambavyo nimauzo ya mali,
uuzaji wa nyaraka za zabuni na mapato58kutoka katika
Mashirika ya Umma na Taasisi zaSerikali (Gawio,
Michango na Marejesho ya mikopo).Hadi kufikia mwezi
Aprili, 2014, makusanyo yalifikiashilingi bilioni 66.79
sawa na asilimia 52.81 ya lengo.Kiwango hicho
kinatarajiwa kuongezeka katika robo yanne ya mwaka wa
fedha baada ya Mashirika mengikuandaa hesabu za
mwaka na ukaguzi wa hesabu hizokukamilishwa.


134. Mheshimiwa Spika, makadirio ya matumizi yaFungu
50 kwa mwaka 2013/14 yalikuwashilingibilioni 54.71 kwa
ajili ya matumizi ya kawaida nashilingi bilioni 233.67 kwa
ajili ya matumizi yamaendeleo. Hadi kufikia mwezi Aprili,
2014, matumiziya kawaida yalifikia shilingi bilioni 36.60
sawa naasilimia 66.89 ya makadirio na matumizi ya
maendeleoyalifikia shilingi bilioni 219.97 sawa na asilimia
94.14ya makadirio.Fungu 23 Idara ya Mhasibu Mkuu wa
Serikali


135. Mheshimiwa Spika, makadirio ya matumizi yaFungu
23 kwa mwaka 2013/14 yalikuwashilingibilioni 80.83 kwa
ajili ya matumizi ya kawaida nashilingi bilioni 4.76 kwa
ajili ya matumizi ya maendeleo.Hadi kufikia mwezi Aprili,
2013, matumizi ya kawaidayalifikia shilingi bilioni 45.63
sawa na asilimia 56.45 yamakadirio na matumizi ya
maendeleo yalifikia shilingibilioni 1.22.59Fungu 22 - Deni
la TaifaMheshimiwa Spika, makadirio ya matumizi ya
Fungu22 kwa mwaka 2013/14 yalikuwa shilingi
bilioni3,319.01. Hadi kufikia mwezi Aprili, 2014 matumizi
yafungu hili yalifikia shilingi bilioni 2,795. 43 sawa
naasilimia 84.22 ya makadirio.Fungu 21- HAZINA


136. Mheshimiwa Spika, makadirio ya matumizi
yakawaida ya Fungu 21 kwa mwaka 2013/14
yalikuwashilingi bilioni 1,367.29 na matumizi ya
maendeleoshilingi bilioni 38.15 . Hadi kufikia mwezi
Aprili, 2014,matumizi ya kawaida yalifikia shilingi bilioni
420.28sawa na asilimia 30.74 ya makadirio, na matumizi
yamaendeleo yalifikia shilingi bilioni 19.78 sawa
naasilimia 51.85 ya makadirio.Fungu 13
KitengoHaramuchaUdhibiti waFed ha


137. Mheshimiwa Spika, makadirio ya matumizi yaFungu
13 kwa mwaka 2013/14 yalikuwashilingibilioni 1.94 kwa
ajili ya matumizi ya kawaida na shilingibilioni 0.39 kwa
ajili ya matumizi ya maendeleo. Hadikufikia mwezi Aprili,
2014, matumizi ya kawaidayalifikia shilingi bilioni 0.91
sawa na asilimia 46.90 yamakadirio, na matumizi ya
maendeleo yalifikia shilingibilioni 0.07 sawa na asilimia
17.95 ya makadirio.60Fungu 10 Tume ya Pamoja ya
Fedha


138. Mheshimiwa Spika, makadirio ya matumizi
yakawaida kwa Fungu hili yalikuwa shillingi bilioni
2.06,hadi kufikia Aprili, 2014 matumizi yalifikia
shilingibilioni 1.04 sawa na asilimia 49.76 ya
makadirio.Fungu 7 Ofisi ya Msajili wa Hazina


139. Mheshimiwa Spika, makadirio ya matumizi yaFungu
7 kwa mwaka 2013/14 yalikuwa shilingi bilioni38.08 kwa
ajili ya matumizi ya kawaida na shilingibilioni 1.66 kwa
ajili ya matumizi ya maendeleo. Hadikufikia mwezi Aprili,
2014, matumizi ya kawaidayalifikia shilingi bilioni 33.06
sawa na asilimia 86.8 yamakadirio, na matumizi ya
maendeleo yalifikia shilingibilioni 0.62 sawa na asilimia
37.35 ya makadirio.Fungu 45 - Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi


140. Mheshimiwa Spika, makadirio ya matumizi yaFungu
45 kwa mwaka 2013/14 yalikuwashilingibilioni 57.4 kwa
ajili ya matumizi ya kawaida na shilingibilioni 21.45 kwa
ajili ya matumizi ya maendeleo. Hadikufikia mwezi Aprili,
2014, matumizi ya kawaidayalifikia shilingi bilioni 43.11
sawa na asilimia 75.1 yamakadirio, na matumizi ya
maendeleo yalifikia shilingibilioni 2.97 sawa na asilimia
13.84 ya makadirio.61MAKADIRIO YA MAPATO NA
MATUMIZI KWAMWAKA WA FEDHA
2014/15MapatoMheshimiwa Spika, katika mwaka
2014/15, Wizaraya Fedha Fungu 50 inakadiria kukusanya
mapatoyasiyo ya kodi yapatayo
shilingi126,188,104,000(bilion i 126.19Maombi ya
FedhaFungu 50 Wizara ya Fedha.


141. Mheshimiwa Spika, katika fungu hili
kwamwakawafedha2014/15,Wizarainaombakuidhinishiwa
kiasi cha fedha kama ifuatavyoa)(b)Matumizi ya kawaida
Shilingi 66,239,790,000(bilioni 66.23). Kati ya hizo
mishahara ni shilingishilingi5,620,668,000(
bilioni5.62)namatumizi mengineyo shilingi
60,619,122,000(bilioni 60.61).Miradi ya Maendeleo
Shilingi 29,803,232,000(bilioni 29.71).Kati ya hizoi)
Fedha za Ndani - Shilingi 19,350,000,000(bilioni
19.35).(ii) Fedha za Nje - Shilingi 10,453,232,000(bilioni
10.45).Fungu 23 Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali:62


142. Mheshimiwa Spika, katika fungu hili
kwamwakawafedha2014/15,Wizarainaombakuidhinishiwa
kiasi cha fedha kama ifuatavyoa)Matumizi ya kawaida -
Shilingi 82,170,024,000(bilioni 82.17). Kati ya hizo
mishahara shilingi5,012,762,000(bilioni 5.01) na
matumizimengineyo shilingi 77,157,262,000
(bilioni77.16).(b)Miradi ya Maendeleo Shilingi
7,950,000,000(bilioni 7.95) Kati ya hizoi) Fedha za Ndani
-Shilingi 4,800,000,000(bilioni 4.80).(ii) Fedha za Nje-
Shilingi 3,150,000,000(bilioni 3.15).Fungu 22- Deni la
Taifa


143. Mheshimiwa Spika, katika fungu hili
kwamwakawafedha2014/15,Wizarainaombakuidhinishiwa
kiasi cha Shilingi 4,354,865,076,000(bilioni 4,354.86).
Kati ya hizo mishahara ni shilingi10,341,136,000 (bilioni
10.34), Deni la Taifa shilingi3,650,612,000,000 (bilioni
3,650.61) na matumizimengineyo ni shilingi
693,911,940,000 (bilioni693.91).Fungu 21 - HAZINA


144. Mheshimiwa Spika, katika fungu hili
kwamwakawafedha2014/15,Wizarainaombakuidhinishiwa
kiasi cha fedha kama ifuatavyo:63(a)(b)Matumizi ya
kawaida Shilingi 790,325,216,000(bilioni 790.32). Kati ya
hizo mishahara nishilingi4,015,511,000(bilion
i4.01)namatumizi mengineyo shilingi
786,309,705,000(bilioni 786.31) ambazo ni kwa ajili ya
matumiziya Idara na Taasisi zilizo chini ya Fungu
hili,nyongeza ya mishahara ya Watumishi wa Serikalina
matumizi maalum.Miradi ya maendeleo ni shilingi
57,417,015,000(bilioni 57.42). Kati ya hizo;(i)Fedha za
Ndani- Shilingi 17,000,000,000(bilioni 17.0)(ii)Fedha za
Nje- Shilingi 40,417,015,000(bilioni 40.42)Fungu 13
KitengoHaramu:chaUdhibit iwaFe dha


145. Mheshimiwa Spika, katika fungu hili
kwamwakawafedha2014/15,Wizarainaombakuidhinishiwa
kiasi cha fedha kama ifuatavyoa) Matumizi ya kawaida -
Shilingi 2,000,000,000(bilioni 2.0).(b) Miradi ya
Maendeleo, fedha za nje Shilingi195,000,000 (bilioni
0.19).Fungu 10 Tume ya Pamoja ya Fedha:


146. Mheshimiwa Spika, katika fungu hili
kwamwakawafedha2014/15,Wizarainaombakuidhinishiwa
kiasi cha Shilingi 2,318,661,000 (bilioni642.32) kwa
matumizi ya kawaida. Kati ya fedha hizo,shilingi
318,661,000 (bilioni 0.32) ni kwa ajili yamishahara na
shilingi 2,000,000,000 (bilioni2.0) nimatumizi
mengineyo.Fungu 7 Ofisi ya Msajili wa Hazina:


147. Mheshimiwa Spika, katika fungu hili
kwamwakawafedha2014/15,Wizarainaombakuidhinishiwa
kiasi cha fedha kama ifuatavyoa)Matumizi ya kawaida -
Shilingi 88,455,278,000(bilioni88.45).K
atiyahizoshilingi670,328,000 (bilioni 0.67) ni kwa ajili
yamishahara na shilingi 87,784,950,000 (bilioni87.78) ni
matumizi mengineyo.(b)Miradi ya Maendeleo Shilingi
1,943,000,000(bilioni 1.94)Kati ya hizoi)Fedha za Ndani
Shilingi 650,000,000(bilioni 0.65).(ii)Fedha za Nje-
Shilingi 1,293,000,000(bilioni 1.29).Fungu 45 - Ofisi ya
Taifa ya Ukaguzi


148. Mheshimiwa Spika, katika fungu hili
kwamwakawafedha2013/14,Wizarainaombakuidhinishiwa
kiasi cha fedha kama ifuatavyoa) Matumizi ya kawaida
shilingi 69,843,825,000(bilioni 69.84). Kati ya hizo
mishahara ni shilingi6510,408,402,000 (bilioni 10.41) na
matumizimengineyoshilingi59,43
5,423,000(bilioni59.43).(b) Miradi ya maendeleo shilingi
13,011,432,000(bilioni 13.01), kati ya hizoi)Fedha za ndani
shilingi 8,000,000,000(bilioni 8.0).(ii) Fedha za nje
shilingi 5,011,432,000 (bilioni5.01).HITIMISHO


149. Mheshimiwa Spika, napenda kutoa shukrani zadhati
kwa Wakuu wa Idara na Vitengo, Wafanyakazi waWizara
ya Fedha wakiongozwa na Katibu Mkuu Dkt.Servacius B.
Likwelile na Naibu Makatibu WakuuNdugu Elizabeth J.
Nyambibo, Prof. Adolf F. Mkenda naNdugu Doroth S.
Mwanyika kwa kazi kubwawanayoifanya katika kutekeleza
majukumu ya Wizara.Vile vile, napenda kuwashukuru
Wakuu wa Taasisi naWakala wa Serikali chini ya Wizara
kwa michango yaokatika utekelezaji wa majukumu ya
Wizara.
150. Mheshimiwa Spika, napenda
kuwashukuruWaheshimiwa Wabunge wote kwa
kunisikiliza.
Hotubahii pia inapatikana katika tovuti ya
Wizara(www.mof.go.tz)
151. Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja.
WAZIRI WA FEDHA, MHESHIMIWA SAADA
MKUYA SALUM (MB)

You might also like