You are on page 1of 52

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Sumbawanga Ngara 2012 OFISI YA WAZIRI MKUU TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

OFISI YA MKUU WA MKOA WA RUKWA

2012

Sumbawanga Ngara
Eng. Stella Martin Manyanya Mb Mkuu wa Mkoa wa Rukwa

Weka Manispaa yetu sa na Inayovutia ili kila mtu aseme Kwetu ni Sumbawanga

a
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa

Sumbawanga Ngara 2012

b
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa

Sumbawanga Ngara 2012

UDHIBITI WA MAZINGIRA

SUMBAWANGA NGARA

OFISI YA MKUU WA MKOA WA RUKWA


S.L.P. 128 Sumbawanga Simu: 025-2802137/ 2802318/ 2802131 Nukushi: 025-2802217/ 2802144 Barua pepe: rasrukwa@pmorallg.gp.tz / rasrukwa@yahoo.com Website: www.rukwa.go.tz Blog: rukwareview.blogspot.com

Novemba, 2012
i
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa

Sumbawanga Ngara 2012

YALIYOMO
MAONI YA BAADHI YA WADAU WA SUMBAWANGA NGARA ...............iv VIFUPISHO..ix DIBAJI .................................................................................................... x SHUKRANI ...........................................................................................xii MUHTASARI ....................................................................................... xiv 1. 1.1. 2. 2.1. 2.2. 2.3. 3. 3.1. 3.2. 3.3. 3.4. 4. 5. 5.1. 5.2. 5.3. 5.4. 5.5. 5.6. 5.7. 5.8. 5.9. UTANGULIZI .............................................................................. 1 Utekelezaji wa Pamoja kwa faida ya wote (SMART PARTNERSHIP) ....3 TAARIFA REJEA ......................................................................... 6 Maana ya taka ....................................................................................... 7 Madhara ya taka: .................................................................................. 7 Faida ya taka: ......................................................................................... 8 MALENGO YA MILENIA, DIRA NA SERA ZA TAIFA ............... 9 Malengo ya Milenia .............................................................................. 9 Dira ya Taifa ya Tanzania 2025 ........................................................10 Sera ya Mazingira................................................................................10 Sera ya Maendeleo ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati ya 2003 .....11 HALI HALISI YA HUDUMA YA TAKA SUMBAWANGA......... 12 WADAU WA TAKA .................................................................. 15 Wananchi ..............................................................................................15 Serikali ...................................................................................................15 Wafanyakazi .........................................................................................16 Wafanyabiashara.................................................................................16 Watu wa kujitolea ...............................................................................16 Vikundi na vilabu vya vijana vya Mazingira ..................................16 NGOs, CBOs, Vyama vya Kujitolea, na Jumuia za kijamii ...........16 Makampuni Binafsi ............................................................................ 17 Washirika wa Maendeleo .................................................................. 17

ii
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa

Sumbawanga Ngara 2012


6. 6.1. 6.2. 6.3. 7. 7.1. 7.2. 7.3. 7.4. 7.5. 8. UCHAMBUZI WA TATIZO ....................................................... 18 MKUKUTA .............................................................................................18 Sheria za Mazingira na Taka, Sera ...................................................18 Matokeo ................................................................................................22 NJIA NA MIKAKATI YA KUREKEBISHA HALI.......................23 Mikakati: ...............................................................................................23 Namna ya ushiriki wa wadau. ..........................................................26 Mduara wa Utekelezaji ......................................................................29 Ukusanyaji wa taka:............................................................................29 Upimaji wa Utekelezaji .......................................................................30 HITIMISHO..........................................................................................31

iii
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa

Sumbawanga Ngara 2012

MAONI YA BAADHI YA WADAU WA SUMBAWANGA NGARA


Mpango wa Sumbawanga Ngara ni mzuri na umesaidia sana usa wa Mji wa Sumbawanga. Siku ya kwanza tunaanza kusasha sikujua kama tungeendelea hivi. Lakini pia pale tulipoamua kuifanya siku ya Alhamisi kuanzia saa 2 hadi saa 3 ya kila wiki kuwa ni siku ya usa, hali ile wengi waliipokea kwa shingo upande, na hii ni kutokana na utamaduni wetu. Kumwambia mtu atoke osini tena baba mzima, au mama aliyejipara eti asashe kwa kiasi fulani ni ngumu kueleweka. Lakini sasa tumezoea, tunafurahi; kwanza imekuwa pia ni siku yetu ya kuwa pamoja na kuchanganyika watumishi wa ngazi zote bila kujali cheo. Inabidi tuendelee kwa nguvu zote kutafuta vitendea kazi kama magari ili kazi yetu iwe nzuri zaidi na zaidi. Na nimejifunza kwa wakati mwingine mambo haya yanahitaji kutumia nguvu kidogo. Alhaj Salum Mohammed Chima Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa. Sumbawanga Ngara inabebwa na pande kuu mbili, Wananchi na Serikali. Jambo la muhimu ni kuweka uelewa na kubadili tabia ya mazoea na badala yake kutambua kuwa jukumu la kuhifadhi mazingira ni la kila mmoja na ni jambo la siku zote. William Shimwela- Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga. Sumbawanga Ngara imeanza vizuri, nguvu ambayo imewekwa kutoka kwa Mkuu wa Mkoa, Watendaji na Wananchi. Watendaji na Serikali lazima waongeze juhudi katika kuelimisha na
iv
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa

Sumbawanga Ngara 2012


kuhamasisha ili hata msipokuwepo viongozi waanzilishi watu waendeleze hayo. Mhe. Dkt. Mzindakaya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mstaafu, Mbunge Mstaafu na Mwekezaji wa ndani wa Kiwanda cha Nyama (SAAFI) na Hoteli. Tangu Sumbawanga Ngara ilipoanzishwa na Mkuu wa Mkoa Eng. Stella M. Manyanya (Mb) Mji wa Sumbawanga umebadilika tofauti na siku za nyuma. Wito wangu ni kwamba kumbe kila kitu kinawezekana pale uhamasishaji unapofanyika. Wananchi wapo tayari kufanya vitu kwa maendeleo yao wenyewe iwapo watashirikishwa na kuhamasishwa ipasavyo. Hamza Temba Asa Habari na Mawasiliano Osi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Nimejifunza kuwa Eng. Stella M. Manyanya (MB) ni mpiganaji juu ya uharibifu wa mazingira hususan katika suala la taka. Mwanzo akiwa Dar es salaam aliposhughulika na taka nilikiri labda kwa ajili tu ya biashara. Sasa nimegundua kuwa kumbe hiyo ni ajenda yake ya kudumu. Na anajisikia furaha anapoona watu wake wanazingatia juu ya usa. Maria Komba Mwanafunzi chuo cha Mipango Dodoma Eng. Stella Manyanya (MB) ni mwana mazingira wa kweli. Nilishtushwa alipotembelea osini kwangu nikiwa Mratibu Elimu Kata wa Kihagara mahali anakozaliwa. Jambo la kwanza aliniuliza kwa nini mnaishi kama vile, kesho hamtakuwa hapa? Akauliza kwa nini mmeshindwa hata kusasha osi yenu? Na hapo aliniagiza kuwaita watoto wa shule, kisha akawapa elimu ya usa na kuwataka wajifunze kwa vitendo kwa kusasha eneo lile. Hali hiyo iliendelea kuleta hamasa maeneo mengi juu ya usa na uhifadhi wa mazingira ikiwemo kupanda miti na kutokata
v
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa

Sumbawanga Ngara 2012


miti kando ya ziwa Nyasa. Lakini pia kila anapoka kijijini kwake amekuwa akihamasisha vikundi vya vijana kusasha makaburi ya umma ya Tumbi na Mango, kukagua vyoo na usa wa wanafunzi. Mwl. Joseph Mhagama- Mwanafunzi Chuo cha Mipango Dodoma. Sumbawanga Ngara ni Kauli mbiu ya kuhamasisha na kuwaunganisha watu wa makundi mbalimbali ili kusaidiana kuufanya Mji wa Sumbawanga Upendeze. Lakini kauli mbiu hii haiwezi kuzaa matunda iwapo watu hawatatekeleza kwa vitendo yote wanayokubaliana. Mkisema leo ni siku ya usa basi kweli wote mtoke na mfanye usa. Mkikubaliana kuwa msichimbe mchanga barabarani basi wote kweli msichimbe. Mkishasema tupande miti basi wote kweli mpande miti. Na mtu yeyote asigeuze Sumbawanga Ngara kama shughuli ya kumfuraisha bosi wake au kuwafurahisha viongozi wake, pia viongozi wasione hiyo ni kama kazi ya kupata sifa ili mradi kwa kusema bila kuona matokeo. Ni vema wote kuhakikisha kuwa mabadiliko yanapatikana na yanalindwa kwa gharama yoyote. Lukaluka Innocent Mwanafunzi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Bsc EPE) Sumbawanga Ngara ni Mpango mzuri wa kuhakikisha mji wetu unakuwa sa. Uzuri wa Mpango huu unatekelezeka kirahisi na watu wa makundi yote na hauhitaji utaalam wa kipekee kwa sehemu kubwa ya wadau. Ni Mpango ambao unatoa ajira nyingi rasmi na zisizo rasmi. Kwa ajira zisizo rasmi hazihitaji mtaji mkubwa. Pia hutoa ajira endelevu kwa kuwa miji inaendelea kukua na watu wanaendelea kuzalisha taka. Shughuli za watu zinazoingiliana na uharibifu wa Mazingira pia zinaongezeka kutokana na watu kujitafutia kipato. Frank Jailos Mateni Katibu wa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa
vi
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa

Sumbawanga Ngara 2012


Usa wa Mji wa Sumbawanga na Halmashauri zote zilizopo Mkoani Rukwa lazima zizingatie usa, upandaji wa miti na Sheria za Miji lazime zizingatiwe. Halmashauri Kuu ya CCM ya Mkoa wa Rukwa 22 Septemba 2012 Sumbawanga Ngara ni suala jema na tunaliunga mkono, wananchi waendelee pia kuunga mkono, Suala hili linahitaji kusaidiwa. Serikali iwekeze vya kutosha haswa kwenye vitendea kazi vya kutosha kama magari. Sumbawanga Ngara imesaidia sana kwa sababu tangu tumeanza katika Manispaa ya Sumbawanga sasa tuna takribani mwaka mmoja hatujawahi tena kupata magonjwa ya mlipuko. Dkt Mussa Makore Mganga Mkuu Manispaa ya Sumbawanga Naifahamu Sumbawanga Ngara. Tunaomba tuongeze tu bidii ya usa maana Mkuu wa Mkoa angalau ametuonyesha mfano wa usa. Tunaomba utuhimize kwa nguvu tuzidi hapo. Mzee Barnabas Nchinga Mkazi wa Kata ya Katandala Tumeanza vizuri haswa katikati ya mji. Tuongeze nguvu kwenye Kata za pembezoni iwe ni agenda ya kila siku na tuzungumze. Mhe. Anthony Choma Diwani wa Malangali Nina mwaka mmoja Sumbawanga. Sijui kuhusu Sumbawanga Ngara. Nilikuwa nafanya kazi katika Hospitali ya Dkt Atman. Deonatha Sylvester Muuguzi Sumbawanga Ngara naijua na zoezi linaenda vizuri. Mimi ni dereva wa gari la Halmashauri ya Manispaa, tatizo kubwa ninaloliona ni vitendea kazi. Hakuna gari imara la taka. Mfano pale
vii
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa

Sumbawanga Ngara 2012


Sabato, Halmashauri wameweka vifaa vya kuhifadhi taka lakini taka hazitoki kwa wakati, hiyo inafanya zoezi hilo lisiwe zuri sana. Lakini pia sehemu ya kuhifadhi taka hapajajengwa kwa kiwango, inakuwa shida sana kupakia taka na hasa mvua ikinyesha gari linaingia kwa shida, ni vyema yakawekwa magogo na kupaezeka. Ikumbukwe kwamba Halmashauri ya Manispaa imetanuka na sasa ina wakazi wengi. Inahitaji kuongeza vitendea kazi gari zilizopo hazitoshi kutoa huduma lakini pia gari la kuhudumia wagonjwa halitoshi. Iddi Baruti Dereva wa Halmashauri ya Manispaa Sumbawanga.

viii
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa

Sumbawanga Ngara 2012

VIFUPISHO
APRM CBO CCM DKT EMA Eng. Mb MDG MSME NGO SME African Peer review Mechanism Community Based Organization Chama cha Mapinduzi Daktari Environmental Management Act Engineer Mbunge Millennium Development Goals Micro, Small and Medium Enterprises Non-Governmental Organization Small and Medium Enterprises

ix
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa

Sumbawanga Ngara 2012

DIBAJI
Udhibiti wa uharibifu wa Mazingira hususani udhibiti wa taka
ngumu na rejea, uzuiaji wa ukataji miti kiholela na uchomaji wa moto katika maeneo yaliyotengwa, uchomaji wa taka na uepukaji wa shughuli za kibinadamu zenye uchangiaji mkubwa katika uharibifu wa mazingira limepewa kipaumbele kuwa ni suala mtambuka. Uchafuzi unaoendana na kusambaa kwa taka ngumu na miminika umeleta athari kubwa kwa viumbe hai ikiwemo binadamu, wanyama wanyonyeshao na wasionyonyesha, wadudu ambao wengine ni muhimu katika maendeleo chanya ya ardhi, kuongezeka kwa mmomonyoko wa ardhi unaosababisha vina vya maji kupungua katika maziwa kama Rukwa na Tanganyika na kukauka kwa baadhi ya mito. Utiririshaji wa maji taka yenye viashiria vya sumu au sumu kamili vinavyotokana na mabaki ya bidhaa za viwandani zimekuwa na athari kwa viumbe hai waishio nchi kavu na majini na kusababisha kupungua kwa wanyama na baadhi ya aina za samaki, na wengine kubadilisha hata ladha yao ya asili. Kwa ujumla wake uharibifu huo umechangia kwa kiwango kikubwa mabadiliko ya tabia nchi hususan, hali ya hewa katika baadhi ya maeneo, na hivyo kubadili uzuri wa asili na kupoteza baadhi ya vivutio. Mfano ni kuhama kwa wanyama na ndege katika maeneo yao ya asili, kukauka kwa maporomoko ya maji na kadhalika. Uharibifu unaoendana na taka umesababisha miji yetu kuwa michafu na isiyovutia, milipuko ya magonjwa kama kuhara na kipindupindu, magonjwa ya ngozi kama upele, kudumaa kwa afya, kimsingi watu kuwa na afya hafu na vifo. Matumizi ya dawa

x
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa

Sumbawanga Ngara 2012


yamekuwa yakiongezeka, gharama kubwa kwa ajili ya kutoa huduma za afya, kushuka kwa kipato kutokana na kupoteza nguvu kazi, au kuwa na nguvu kazi hafu na kwa ujumla wake kuongezeka kwa umaskini uliokithiri hasa katika miji. Masuala haya yanayoendana na athari za uharbifu wa mazingira si mageni kwetu, wengi wanazo taarifa angalao za awali. Tatizo kubwa limekuwa katika kuchukua hatua za kurekebisha hali hiyo ambazo wengi wetu tumekuwa hatuzichukui kwa wakati au kutochukua kabisa. Mpango wa Sumbawanga Ngara unalenga katika kuungana na Serikali Kuu katika kukia Malengo ya Milenia, Sera ya ardhi, Sera ya Afya na Sera ya Mazingira hususan katika eneo la udhibiti wa Mazingira katika eneo la taka ngumu na uboreshaji wa makazi katika Manispaa ya Sumbawanga. Tunatambua changamoto zilizopo mbele yetu katika kufanikisha Mpango wa Sumbawanga Ngara, hasa juu ya upungufu wa rasilimali zetu. Lakini je, ni bora kusubiri mpaka siku rasilimali zitakapotosha? Na ni lini zitatosha?, basi ni vema tuanze sasa. Nina imani na moyo mkubwa kuwa kwa Umoja wetu na dhamira ya pamoja tutafanikiwa. Mama Theresa alisema Kama Kila mtu atasasha nyumba yake Dunia nzima itakuwa sa. Nasi tunasema endapo kila mtu atatekeleza chanya Mpango wetu wa Sumbawanga Ngara, kwa akili yake yote, bidii zake zote na uwezo wake wote, Sumbawanga itapendeza sana na hivyo kuwavutia wengi kuipenda Sumbawanga na Rukwa kwa Ujumla. Ukiona haliwezekani ujue hujachukua hatua !!!!!!.

Eng. Stella Martin Manyanya (Mb) Mkuu wa Mkoa - Rukwa

xi
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa

Sumbawanga Ngara 2012

SHUKRANI
Kwa heshima na unyenyekevu shukrani za pekee zimwendee Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Jakaya Mrisho Kikwete kwa upendo, hekima, kuniamini na kuwa na jicho la Jinsia. Namshukuru Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Mohammed Gharib Bilal kwa kukubali kutuzindulia Mpango wa Sumbawanga Ngara. Napenda pia kumshukuru Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda (Mb) kwa kukubali kutuzindulia kitabu hiki ambacho ni mwongozo wa kufanikisha Mpango wa Sumbawanga Ngara. Nawashukuru wananchi wa Mkoa wa Rukwa wakiwemo Baba Askofu Kyaruzi, Sheikh Akilimali, Wafanyabiashara, Viongozi wa Taasisi za Umma na Binafsi, Wazee, Wanawake, Vijana pamoja na wadau wengine wote wenye nia njema ya kuhakikisha kuwa mazingira yetu yanakuwa bora na salama na kuwezesha Mpango wa Sumbawanga Ngara kukubalika kuanzia hatua za awali za utekelezaji. Nitakuwa si mwingi wa fadhila endapo sitamshukuru kipekee Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa Alhaji Salum Mohammed Chima pamoja na watumishi wote wa Osi ya Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Mhe. Mathew Sedoyeka, Meya wa Manispaa ya Sumbawanga, Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga ndugu William Shimwela pamoja na Idara yake ya Usa na Mazingira, Osi ya Mganga Mkuu kwa kutaja mmoja Dkt. Temba pamoja na wana Kongano la Sumbawanga Ngara. Namshukuru Mhe, Jaji Pelagia Khaday kwa kutuunga mkono.

xii
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa

Sumbawanga Ngara 2012


Yote hayo yangeweza kuingia Dosari kama upepo wa kisiasa ungekuwa hasi nasi. Hivyo kipekee namshukuru Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa (CCM) Mhe. Hypolitas Matete, Wabunge na wanasiasa wengine. Kwa vile si rahisi kuwashukuru wote kwa kuwataja itoshe tu kusema asante kwa wadau wote wa Sumbawanga Ngara ikiwemo familia yangu. Eng. Stella Martin Manyanya (Mb) Mkuu wa Mkoa wa Rukwa

xiii
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa

Sumbawanga Ngara 2012

MUHTASARI
Mpango huu wa Sumbawanga Ngara ulianzishwa mnamo tarehe 12 Januari 2012, chini ya uasisi wa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Martin Manyanya (MB) ikiwa ni sehemu ya kusherehekea Sikukuu ya Mapinduzi ya Zanzibar. Siku hiyo Mkuu wa Mkoa, Katibu Tawala wa Mkoa, Watumishi wa Mkoa na Halmashauri ya Manispaa kwa pamoja na wadau wengine ikiwemo Mbunge wa Jimbo la Sumbawanga, Mwenyekiti wa Chama Tawala (CCM) na wananchi wa mitaa ya Hospitali ya Mkoa na Sokoni walihamasisha usa kwa kufagia barabara pamoja na kutoa mchanga katika mifereji iliyopo katika eneo hilo. Mpango huu ulizinduliwa rasmi tarehe 24 Februari na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Mohammed Gharib Bilal kwa kuweka jiwe la msingi kwenye mnara wa Sumbawanga Ngara uliopo kwenye makutano ya barabara ya Nyerere na Two way. Mnara huu umepewa heshima kwa akina mama, kwa ishara ya utamaduni wao (ngoma ya Kingwengwe}, ambayo huchezwa hasa na wanawake, ikizingatiwa kuwa kihistoria mdau mkuu wa usa ni mama.

xiv
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa

Sumbawanga Ngara 2012

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Billal akizindua rasmi mpango wa Sumbawanga Ngara Mkoani Rukwa tarehe 24 Februari, 2012.

Lengo la mpango huu ni kuhakikisha kuwa Manispaa ya


Sumbawanga inakuwa kinara katika udhibiti wa mazingira Tanzania kama vile uzoaji wa taka ngumu, uimarishaji wa mifumo ya taka miminika, upandaji wa miti, uzuiaji wa uchomaji moto ovyo na mambo mengine yenye athari kwa mazingira hususan ndani ya Manispaa na Mkoa wa Rukwa kwa ujumla. Mafanikio ya kazi hii ni heshima kubwa kwa wananchi wote wa Manispaa ya Sumbawanga na Mkoa wa Rukwa kwa ujumla hasa kwa wale wa kipato cha chini ambao juhudi zao za hali na mali ndizo nguzo kuu ya ushindi kwani msashaji ndiye msa. Kupitia kitabu hiki Osi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa imeandaa maelezo ya kina juu ya Mpango wa Sumbawanga Ngara ambayo yatatumika kama Mwongozo ama kioo cha tulikotoka, tulipo
xv
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa

Sumbawanga Ngara 2012


na tunakokwenda. Kutokana na Mwongozo huu itakuwa rahisi kwa Manispaa ya Sumbawanga, Halmashauri zote za Mkoa wa Rukwa pamoja na miji mingine ambayo bado haijafanikiwa katika udhibiti wa mazingira zikiwemo taka ngumu na miminika kuweza kujifunza na kuiga kutokana na matokeo yatakayopatikana kupitia mpango huu. Kwa kuwa sisi sote tuna kiu ya maendeleo ya kweli; hivyo basi tunao wajibu wa kuchangia kwa hali na mali ili kuwezesha kupata matokeo ya haraka yaliyokusudiwa na endelevu kwa manufaa ya wote. Sumbawanga Ngara imeonyesha mafanikio makubwa tangu kuanza kwake, hali ya uelewa wa wadau, usa na ushiriki katika shughuli za kuboresha Manispaa zimeongezeka.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Billal akigawa vifaa vya usa kwa wadau mara baada ya uzinduzi wa mpango huo tarehe 24 Februari, 2012.

xvi
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa

Sumbawanga Ngara 2012

1. UTANGULIZI
Mgaagaa na upwa hali wali mkavu, Mcheza kwao hutuzwa na Mwenye macho haambiwi tazama. Hii ni misemo au methali za wahenga wetu ambazo maana zake hazibadiliki kizazi hadi kizazi. Hivyo, methali hizi zimekuwa chachu iliyoamsha ari ya Osi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kuandika kitabu hiki kinachochochea nafasi ya wananchi katika kujiletea maendeleo. Mara nyingi tumejielekeza kusema kuwa tumeshindwa kufanikiwa katika kutafuta ufumbuzi wa matatizo katika jamii yetu kwa visingizio mbalimbali. Hayo yanajitokeza zaidi hasa katika siasa za sasa chini ya vyama vingi ambapo malalamiko yamekuwa makubwa kuliko kutafuta ufumbuzi wa matatizo yetu huku hali ya kujitoa katika kuchangia shughuli za maendeleo imeshuka. Mara nyingi majibu ya wananchi na vyombo vyote vya dola katika mapungufu ya kutekeleza majukumu na wajibu wao imekuwa ni kwa ajili ya ukosefu wa fedha, na Serikali imekuwa ndiyo ikitupiwa lawama zaidi kuwa haiwajibiki kwa wananchi, haikusanyi kodi kutoka kwa wafanyabiashara, haina mipango mizuri ya uhifadhi wa mazingira na kila linalowezekana kusemwa ili mradi tu mtu akipata nafasi atasema. Aghalabu si rahisi kusikia taasisi mbalimbali zikiwemo za kibunge kujadili misingi ya matatizo ya wananchi bila kuitupia lawama Serikali, Serikali hii haijali watu, watu wana umaskini wa kutupwa lakini Serikali haijali, watoto wameshindwa kwenda shule kwa sababu ya Serikali, watu wakiona taka ziko barabarani sababu ni Serikali na kadhalika. Katika taarifa ya mwaka 2012 African Peer Review Mechanism (APRM) yaani Mkataba ambao umekubaliwa na nchi wanachama wa Umoja wa Afrika kama mchakato wa kujifanyia tathmini inaeleza kuwa Watanzania wengi wanaamini kuwa Serikali ndiyo inastahili kufanya kila kitu kwa ajili yao. Kama ndivyo basi tuna tatizo kubwa, ni lazima liangaliwe kwa makini.
1
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa

Sumbawanga Ngara 2012


Maendeleo yoyote yanaanzia na mtu mwenyewe kwa kutumia fursa zinazomzunguka. Wajibu wa Serikali ni kutengeneza mazingira wezeshi na wananchi kushirikiana na Serikali yao katika kuleta maendeleo yao. Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alisema Usipokuwa na Mjomba, Jijombeze mwenyewe. Usitegemee kuletewa mafanikio na mtu mwingine, jitahidi mwenyewe. Baba wa Taifa Hayati Mwalimu alisisitiza juu ya umuhimu wa watu wote kufanya kazi kwa kusema kwamba, Ni lazima kila mtu atimize wajibu wake kwa kufanya kazi kwa bidii zake zote. Kwa hiyo suala la watu kuacha kufanya kazi na kutowajibika kwao wenyewe na familia zao ni kosa kubwa, kama inavyoelekezwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na marekebisho yake hadi 2012 Sehemu ya pili Ibara ya 8(a) (d). Ni kweli kuwa pesa zina nafasi kubwa katika kurekebisha tatizo. Lakini pesa pekeyake si jibu la matatizo yote. Wananchi wakijituma wanaweza kutatua sehemu kubwa ya matatizo yao. Mheshimiwa Benjamini William Mkapa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya tatu alisema kupitia hotuba zake Mtaji wa Maskini ni Nguvu zake Mwenyewe. Ili kuona kuwa jitihada za wananchi pamoja na Serikali yao zinajulikana na zinaweza kupimika, ni muhimu sana mipango na mikakati mbalimbali kutengenezewa miongozo itakayofuatwa na kuweka kumbukumbu kimaandishi. Miongozo hiyo pia itasaidia katika kupima matokeo ya jitihada zilizochukuliwa na kuthaminishwa. Tumeona mara nyingi katika maeneo ambayo wananchi wamejitolea, mchanganuo wa jasho lao haujitokezi moja kwa moja katika taarifa za kibajeti, na pengine hiyo inaweza kuwa sababu mojawapo ya kuwakatisha tamaa kwani michango yao haitoi maelezo ya kina na wakati mwingine haitolewi kimahesabu zaidi ya kusema, pamoja na michango ya wananchi.
2
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa

Sumbawanga Ngara 2012


Kitabu hiki kinaelezea Mpango wa Kwanza wa Mkakati wa Mabadiliko Rukwa unaohusu Uboreshaji wa Mazingira kwa Manispaa ya Sumbawanga yaani Sumbawanga Ngara. Mpango huu ni mpango chochezi kwa maendeleo ya Mkoa wa Rukwa. Mafanikio ya mpango huu yataweza kuleta ari na matumaini mapya kwa wana Manispaa ya Sumbawanga na kuigwa kwa Mkoa wote wa Rukwa na maeneo mengine nchini. Utekelezaji wa mpango huu una gharama kubwa ambazo kila mdau anayo nafasi yake ya kuchangia. 1.1. Utekelezaji wa Pamoja kwa faida ya wote (SMART PARTNERSHIP)

Baada ya kujifunza mbinu hii kupitia semina elekezi iliyotolewa na OWM TAMISEMI Chini ya Uongozi wa Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda (Mb) Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akisaidiwa na Mhe. Hawa Abdulraman Ghasia (Mb) Waziri OWM - TAMISEMI tarehe 15 mpaka 18 Novemba 2012 kwa Waheshimiwa Wakuu wa Mkoa, Ma RAS na Wakuu wa Wilaya wote, inajidhihirisha wazi kuwa ili kazi hii iwe nyepesi na yenye tija matumizi ya teknolojia kwa ajili ya Sumbawanga Ngara ni muhimu sana. 1. Katika msingi wa kwanza unaosisitiza juu ya matumizi ya teknolojia katika kuharakisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa manufaa ya wote, vitahitajika vifaa kama magari ya taka, vijiko, vihifadhi taka, uchakataji wa taka au taka rejea (recycling) ni muhimu sana. 2. Ubunifu yakinifu wa Ushindani: Katika eneo hili wananchi na taasisi za umma wataendelea kutengeneza utaratibu mzuri wa ushiriki pamoja na Serikali. Uratibu maalum utafanyika wa kuangalia namna shughuli za uhifadhi
3
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa

Sumbawanga Ngara 2012


wa mazingira zinavyoendeshwa katika Manispaa ya Sumbawanga. Mikakati mbalimbali ya ubunifu itafanyika katika kuifanya Sumbawanga Ngara kuwa endelevu. 3. Nguvu ya TEHAMA katika kuwezesha ukuaji shirikishi kijamii na kiuchumi: kuelimisha, Kuratibu shughuli za Sumbawanga Ngara na kuzitangaza kupitia mitandao kama www.rukwareview.blogspot.com, magazeti, vipaza sauti na television za kijamii na za kitaifa. 4. Ubora na viwango katika Nyanja mbalimbali za kiuchumi na kijamii: Shughuli za Sumbawnga Ngara zitatakiwa kuzingatia viwango vya kimataifa kwa kadiri inavyowezekana, mfano namna ya kuhifadhi taka, taratibu za usarishaji wa taka, upandaji wa miti raki kwa mazingira na kwa ujumla wake kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa. 5. Umuhimu wa Usalama na namna ya kuwezesha usalama katika Smart Partnership. Usalama ni muhimu katika shughuli zote za Sumbawanga Ngara. Hapa kutazingatiwa usalama wa aina mbili. Usalama wa mali na watu. Sheria za usalama mahali pa kazi kama inavyoshauriwa na OSHA na Shirika la Kazi Duniani (International Labour Organization ILO), juu ya usalama. Hali kadhalika baadhi ya taka hutoa gesi inayoweza kuwaka na kuunguza hivyo yote hayo inabidi kuyazingatia. Kuwa na vifaa vya zimamoto katika maeneo ambayo yatashauriwa na wataalam wa moto. Si suala la hiari kutumia vifaa vya kinga kama vile buti, viakisi mwanga na alama za tahadhari. Katika suala la Usalama wa raia ni vema wadau wa Sumbawanga Ngara kupewa elimu ya ulinzi shirikishi kwa ajili yao wenyewe na wananchi kwa ujumla. Taarifa mbalimbali zinaonyesha kuwa kumekuwa na ongezeko la matumizi ya dawa za kulevya katika
4
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa

Sumbawanga Ngara 2012


nchi yetu. Na wengi wa watumiaji hao wameonekana kutumia sehemu za vituo vya taka (dampo) pamoja na magofu ya nyumba kama macho, sehemu za biashara zao haramu na makazi yao. Wakati mwingine majambazi pia wamekuwa wakijichanganya na watu wanaojihusisha na kazi za taka pamoja na kutumia maeneo hayo kwa ajili ya kucha silaha. 6. Mbinu kongano zitatumika hasa katika kuwakutanisha wadau kutoka katika makundi mbalimbali ambao wote kwa pamoja shughuli zao zinaingiliana kiasi kwamba kutofanya vizuri katika shughuli mojawapo kutakwamisha mafanikio ya kundi jingine au wote. Katika sura inayofuata tutajifunza zaidi kuhusu taka, faida na hasara zake.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya na Katibu Tawala Mkoa huo Alhaj Salum Mohammed Chima wakishiriki kwa vitendo katika usa wa mazingira katika mitaa ya Mji wa Sumbawanga tarehe 12 Januari, 2012.

5
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa

Sumbawanga Ngara 2012

2. TAARIFA REJEA
Kabla ya kuendelea kuchambua katika maeneo mengine kuhusu udhibiti wa mazingira na huduma ya taka kwa ujumla ni vema tufahamu pia juu ya mpango wenyewe au mwongozo huu. Mpango wetu: SUMBAWANGA NGARA Kaulimbiu yetu: Mkakati wetu: Weka Manispaa yetu sa na inayovutia ili kila mtu aseme kwetu ni Sumbawanga Uwajibikaji wa pamoja kwa ajili ya mazingira yetu. Tuwe nyumbani, tuwe kazini, hospitali, kwenye nyumba, kwenye maeneo ya umma hata kwenye michezo na popote pale ambapo tupo, usa ni kipaumbele chetu. Tuifanye Sumbawanga ingare kuliko ilivyowahi ku Ngara tangu kuwepo kwake. Kila mtu anaweza akatimiza wajibu wake kwa kuweka mji wake pamoja na maeneo yake yanayomzunguka na pia ahakikishe maeneo ya wazi ni sa. Saidia Manispaa ya Sumbawanga, Makao Makuu ya Mkoa wetu yawe sa kulingana na hadhi yake. Saidia Manispaa hii iwe sa ili iwe mfano kwa wilaya nyingine za mkoa wa Rukwa, Tanzania kwa ujumla na popote Duniani. Sumbawanga Ngara itafanikiwa tu endapo tutakuwa tumefanikiwa kudhibiti taka
6
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa

Sumbawanga Ngara 2012


ngumu na miminika, kusasha maeneo yote yanayotuzunguka ikiwemo kufyeka majani, kulima magugu, kupanda miti na maua, kutengeneza mapambo ya mji pamoja na kuheshimu sheria ya Mipango Miji namba 8 ya mwaka 2007 na Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya mwaka 1997 na nyinginezo zinazohusiana. 2.1. Maana ya taka Kwa mujibu wa Sheria ya Afya (The Public Health Act, 2009) sehemu ya nne, kifungu cha 52 na 53 kinatoa maelekezo juu ya maana ya taka na kifungu 54 na 55 kinazungumzia hatua za kuchukuliwa dhidi ya wanaokiuka sheria hii. Kwa ujumla taka ni kitu chochote kinachoweza kuleta chukizo kwa wanaokiona kutokana na kutokuwa na mvuto au hali isiyo ya kawaida. Aidha, ni kitu kilichokaa pasipo mpangilio au kilichopo mahali pasipostahili, kinachotoa harufu mbaya, au kinachotia kinyaa na mazingira yote yasiyokubalika. Taka ziko katika hali kuu mbili, ngumu na miminika. Lakini pia unapozungumzia taka ni muhimu kuoanisha na uchafuzi wowote unaoleta chukizo au madhara kwa jamii. 2.2. Madhara ya taka: Taka zina madhara mengi, baadhi yake ni kama ifuatavyo:1. Taka zinahatarisha afya, usalama na ustawi wa jamii. 2. Taka zinawanya watu au jamii ionekane kuwa sio wastaarabu au hawana uwezo, na zinashusha hadhi 3. Taka zinaonyesha kuwa watu wake hawatii sheria za nchi yao na Mamlaka husika.

7
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa

Sumbawanga Ngara 2012


4. Taka zinafanya mji ushuke thamani yake na hadhi yake na hivyo kushusha hata bei ya bidhaa na kukosesha soko. 5. Taka zinafukuza wageni. 6. Taka zinagombanisha familia na zinaweza kusababisha kukimbiwa na mpenzi wako au maraki. 7. Taka zinakosesha amani, utulivu na ustarabu wa mtu au kitu. 2.3. Faida ya taka: Pamoja na madhara hayo kwa upande mwingine taka zina faida kwa kuwa kila siku miji inazalisha taka, na hivyo kutoa ajira ya kusasha taka. Hivyo basi ni muhimu watu binafsi au vikundi vya watu kushirikiana na Mamlaka husika kuhakikisha kuwa kila eneo linakuwa sa. Katika mpango huu wa Sumbawanga Ngara inategemewa kuzalisha jumla ya ajira zisizopungua elfu mbili (2000) kutokana na shughuli za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja. Mfano wa shughuli hizo ni pamoja na kusasha mifereji, kufyeka, kuokota taka, kupakia kwenye magari ya taka, kuendesha magari ya taka, kusimamia shughuli za taka, kuuza na, kuchakata taka rejea, kutengeneza mboji, kutengeneza mapambo, kupanda miti, kuboresha barabara, kutengeneza matofali, kusukuma mikokoteni, kutengeneza vinyago, kupaka rangi, kuhamasisha na kutoa elimu, machapisho, kujenga mabango na kuandaa matangazo, kuuza vifaa mbalimbali kama matoroli, uma, majembe, mapanga, mifagio, uandishi wa habari za taka, kuanzishwa kwa vikundi vya ujasiriamali wa taka, upandaji wa miti na bustani na kadhalika. Mpango huu ni matokeo ya utekelezaji na ufuatiliaji wa mipango mama pamoja na mikataba ya Kitaifa na Kimataifa, Sera na sheria mbalimbali za nchi zinazohusiana na uhifadhi wa mazingira kama baadhi yake inavyoonyeshwa katika sura inayofuata.
8
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa

Sumbawanga Ngara 2012

3. MALENGO YA MILENIA, DIRA NA SERA ZA TAIFA


3.1. Malengo ya Milenia Tanzania ni miongoni mwa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa ambazo zimesaini juu ya utekelezaji wa Malengo ya Milenia (Millenium Development Goals - MDGs). Malengo hayo ni kama ifuatavyo: 1. Kumaliza Umaskini na Njaa 2. Elimu kwa Wote 3. Usawa wa Kijinsia 4. Afya ya Mtoto 5. Afya ya Uzazi 6. Kupambana na Ukimwi 7. Mazingira Endelevu 8. Mahusiano ya Kimataifa Wajibu wetu hapa ni kujihusisha na kifungu cha saba kinachotutaka kuwa na mipango mahususi itakayofanya mazingira yetu kuwa endelevu. Katika kutilia mkazo inasisitizwa na Umoja wa Mataifa kuwa Usa kwa wote kukia 2015. Kampeni nyingi zimetangazwa mpaka siku za vyoo, lakini hadi leo bado kuna watu hawaheshimimu matumizi ya vyoo na maji salama.

9
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa

Sumbawanga Ngara 2012


3.2. Dira ya Taifa ya Tanzania 2025 Dira ya Maendeleo ya Taifa inatarajia kuona kuwa ikapo mwaka 2025, endapo Wananchi wake watakuwa wamewezeshwa na kujengewa mazingira mazuri ya kiuchumi kwa kutumia rasilimali walizonazo ikiwemo watu, ardhi, maji, madini, misitu na hali ya hewa na bila vitu hivyo kuharibiwa basi; a) Itakuwa na watu wa kiwango cha hali ya juu b) Amani, Utulivu na Umoja, c) Utawala Bora, d) Watu waliosoma na jamii iliyoelimika e) Uchumi wa kiushindani imara na kwa faida ya wote. Kwa hali hiyo ni muhimu kwa wadau wote wa kila eneo kuhakikisha kuwa malengo hayo yanakiwa. Kimsingi ustawi wowote ili kuwa endelevu lazima uzingatiwe na wananchi wenyewe. 3.3. Sera ya Mazingira Kwa kuzingatia umuhimu wa mazingira katika maisha ya binadamu, kwani ndiyo hutoa hifadhi ya viumbe vyote vyenye uhai, na ndio msingi wa rasilimali ya kuwezesha kuondoa unyonge wa maskini na kuongeza uwezo wa watu wa kipato cha chini, hivyo jukumu kuu la wadau wote ni kulinda Mazingira yetu kwa nguvu zote. Serikali ya Tanzania inatambua hatari hiyo ya kupoteza rasilimali hiyo na ndiyo maana ikatunga Sera ya Taifa ya Mazingira ya 1997 ikiwa na madhumuni yafuatayo; 1. Kuhakikisha udumishaji, usalama na matumizi sawa ya rasilimali kwa mahitaji ya msingi ya sasa na vizazi vijavyo bila kuharibu mazingira au kuhatarisha afya na usalama 2. Kuzuia na kudhibiti uharibifu wa ardhi, maji, mimea na hewa ambayo ndiyo husaidia uhai wetu.
10
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa

Sumbawanga Ngara 2012


3. Kuhifadhi na kuendeleza urithi wetu na ule unaotegemewa na binadamu ikiwa ni pamoja na maisha ya viumbe wa aina ya viumbe wa aina mbalimbali na pekee nchini Tanzania. 4. Kurekebisha hali na maeneo yaliyoharibiwa pamoja na makazi ya watu mijini na vijijini ili watanzania wote waweze kuishi katika hali ya usalama, kiafya, kuzalisha bidhaa pamoja na kuishi katika mazingira mazuri na yenye kuvutia. 5. Kungamua na kufahamu mahusiano kati ya mazingira na maendeleo na kuhimiza ushirikiano wa mtu binafsi na jamii katika kuhifadhi mazingira. 6. Kuendeleza kimataifa kuhusu ajenda ya Mazingira na kupanua ushiriki na mchango wetu kwa pande zote zinazohusika, ikiwa zinahusu nchi jirani na mashirika na mipango ya ulimwengu pamoja na utekelezaji wa mikataba. 3.4. Sera ya Maendeleo ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati ya 2003 (Small and Medium Entreprises SMEs Development Policy 2003) Sera hii inalenga kuwajengea wajasiriamali wadogo na wa kati mazingira mazuri ya kufanya shughuli zao na kukua. Kwa kutambua shughuli hizo za kiuchumi zinazoambatana na mambo mtambuka, Sera inasisitiza pamoja na suala la jinsia na UKIMWI, suala la mazingira pia linapewa kipaumbele. Aidha, Sera pia inasisitiza kutenga maeneo maalum ya kufanyia biashara na uendelezaji wa viwanda vya kati. Sera hii pia inasisisitiza juu ya umuhimu wa ubunifu katika kutengeneza shughuli za kujipatia kipato halali.
11
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa

Sumbawanga Ngara 2012

4. HALI HALISI YA HUDUMA YA TAKA SUMBAWANGA


Huduma ya taka ngumu katika Manispaa ya Sumbawanga kwa muda mrefu imekuwa ikitolewa na Manispaa yenyewe. Huduma hiyo imekuwa hasa ikizingatia kuondoa marundo ya taka ambayo yanazagaa hovyo, ambapo hupelekwa kwenye vizimba na hatimaye kupelekwa Dampo. Pamoja na msisitizo mkubwa katika ngazi ya taifa juu ya utunzaji wa mazingira na udhibiti wa taka ngumu na taka miminika, jukumu hilo kwa kiwango kikubwa bado limezoeleka kuwa kama ni la Manispaa au Halmashauri kama majukumu ya Serikali. Elimu mbalimbali kupitia makongamano, vipeperushi na matangazo zimekuwa zikitolewa. Lakini hali ya kukubalika juu ya utekelezaji wake umekuwa ni mdogo sana. Tatizo kubwa zaidi imekuwa hasa pale Manispaa au halmashauri zinapohitajika kugharimia huduma yote ya taka, yaani taka za majumbani (taka ngumu na miminika) pamoja na za viwandani ikiwemo maeneo yote ya taasisi za umma na binafsi. Jambo jingine linalojidhihirisha ni juu ya vipaumbele vya bajeti, mara nyingi pamoja na watu wengi kuonekana kuchukizwa na utupaji holela wa taka pamoja na uchafuzi wa maeneo ikiwemo makazi kwa ujumla, suala la udhibiti wa taka limekuwa halipangiwi bajeti ya kutosha. Hii ni kwa upande wa Serikali na hata watu binafsi. Agharabu ni mara chache kabisa au pengine hamna kukuta wadau wakiwa kwenye kikao cha mipango madhubuti kutoa kipaumbele kwa ajili ya udhibiti wa taka au uhifadhi wa mazingira kwa ujumla. Mara nyingi uhifadhi wa mazingira unachukuliwa uzito hasa tu katika kuridhisha kuwa ni
12
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa

Sumbawanga Ngara 2012


tatizo mtambuka kinadharia na kutenda kwa kiasi kidogo sana. Hasa kwa upande wa udhibiti wa taka, kama ilivyo jina lenyewe, mipango na shughuli za taka huhesabika pia kama taka. Manispaa imejikuta ikitoa huduma hafu sana kutokana na kuwa na bajeti nyu katika eneo hilo sambamba na mzigo wote wa kudhibiti taka kuachiwa yenyewe. Kwa muda mrefu mifereji imekuwa haizibuliwi, barabara hazifyekwi ipasavyo, wadau kutiririsha maji hovyo na kuacha makazi yao katika hali isiyoridhisha, Biashara kufanyika katika mazingira machafu na holela, na kwa ujumla wake kuwa na mji hatarishi, usiopendeza na uliozubaa. Matokeo yake kumekuwa na athari za kiuchumi kama vile magonjwa ya milipuko ya hapa na pale na hivyo kuongeza gharama za matibabu, kuwa na nguvu kazi isiyo na tija, mji usiovutia kwa wananchi wenyewe na wafanyabiashara ikiwemo wawekezaji na watalii. Hali kadhalika imechangia kuwa na mzunguko mdogo wa pesa, kupungua kwa ajira ya moja kwa moja kutokana na shughuli za taka pamoja na zile zisizo za moja kwa moja kupitia faida zinazopatikana kutokana na mafanikio ya kazi za taka. Katika mashindano mbalimbali ya Manispaa, Miji na Halmashauri, Sumbawanga imejikuta ikibwagwa kiusa hata na miji midogo kama vile Mji wa Mpanda ambao sasa ni Makao Makuu ya Mkoa wa Katavi wakati Mkoa wa Rukwa haujagawanywa. Mara nyingi ushindi wa Manispaa sa umekuwa ukichukuliwa na Moshi pamoja na Manispaa nyingine nje ya Rukwa. Baada ya kutafakari na kujifunza juu ya tatizo la taka katika Manispaa ya Sumbawanga, wadau wote kwa pamoja chini ya uasisi wa Mkuu wa Mkoa Rukwa Eng. Stella Martin Manyanya (Mb) wamedhamiria kuona kuwa Sumbawanga inaNgara
13
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa

Sumbawanga Ngara 2012


kuliko ilivyowahi kuNgara na kuwa Manispaa sa, salama na inayovutia kuliko zote Tanzania kiasi cha kila mtu kujivunia na kuita Sumbawanga ni kwao. Sambamba na dhamira hiyo Wadau wakuu wa shughuli hizi za uhifadhi wa mazingira ikiwemo taka wamechambuliwa kama inavyooneshwa katika sura inayofuata.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akiwa pamoja na wafanyakazi wa Osi yake ambao kwa pamoja hushiriki katika usa wa mazingira katika alhamisi ya kila wiki kuzunguka mazingira ya osi hiyo.

14
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa

Sumbawanga Ngara 2012

5. WADAU WA TAKA
Ili mpango huu wa Sumbawanga Ngara kuwa endelevu, ni lazima ushirikishe jamii ya watu wote waishio Sumbawanga pamoja na taasisi zake za kiserikali na binafsi kama ifuatavyo. Pia ni muhimu Suala la Sumbawanga Ngara lifahamike kwa wadau wengine wote wa maendeleo waishio Mkoani Rukwa na nje ya mkoa. Kwa kushirikisha makundi ya wadau wote, umiliki wa mradi huu utakuwa ni wa wote kuanzia chini (grassroot), ngazi ya uwezeshaji hadi Serikali yaani Serikali za Mitaa na Serikali Kuu. 5.1. Wananchi Hawa ni wananchi wa kawaida ambao pia ni wazalishaji wa taka za majumbani (domestic waste). Lakini pia wananchi ni nguvukazi katika kuondoa taka katika maeneo yao yanayowazunguka. Wananchi ndio wanufaika wakuu na wa moja kwa moja au kupitia fursa zinazoambatana na ajira za taka kama vile Usashaji, taka rejea, mbolea na mboji, pamoja na kuchangia huduma ya taka. Wananchi hao wanaweza kuwa ni mtu mmoja mmoja au vikundi vya kijamii, wanawake, wanaume, vijana, wazee, walemavu na kadhalika. 5.2. Serikali Kwa ajili ya kuhakikisha kuwa kunakuwa na Sera nzuri pamoja na sheria zinazosaidia kudhibiti taka. Kwa sasa baadhi ya wadau wakuu katika eneo hili ni Osi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM- TAMISEMI), Wizara ya Osi ya Makamu wa Rais -Mazingira, Ardhi, Afya, Nishati na Madini, Osi ya Mkuu wa Mkoa na Manispaa ya Sumbawanga. Wajibu wao ni pamoja na kuboresha miundombinu ya taka pamoja na vitendea kazi kama magari, vizimba sehemu ya kutupa taka n.k.

15
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa

Sumbawanga Ngara 2012


5.3. Wafanyakazi Waajiriwa wa Serikali pamoja na mashirika ya umma, Taasisi binafsi ambao watakuwa na wajibu wakuhakikisha kuwa familia zao zinatekeleza juu ya udhibiti wa taka, wakiwa kazini wanasimamia ipasavyo kuhakikisha kuwa maeneo yao ya kazi yanakuwa sa. Kwa watumishi waajiriwa wa Manispaa wao ni wadau wakuu katika kuchangia taarifa za kitaalam pamoja na kusimamia utekelezaji wa sheria zinazohusiana na taka. 5.4. Wafanyabiashara Kuhakikisha maeneo yao ya kazi ni sa, Kuuza vifaa vya usa ikiwemo mifagio, chepe, koleo, buti, visibao na kuhakikisha kuwa shughuli zao zinafanyika katika maeneo yanayostahili na yaliyoelekezwa na Manispaa. 5.5. Watu wa kujitolea Hawa ni watu waliohamasika na kuona kuwa mji wao unakuwa sa salama na mzuri. Wanaweza kuwa ni watu binafsi kama vile wakuu wa shule, madaktari, viongozi wa dini kama vile Maaskofu, Mashehe, mapadre, wachungaji na wengineo kutoka katika jamii zetu ambao watajihusisha kufanya usa wa moja kwa moja au kutoa hamasa ikiwa ni pamoja na michango ya kifedha. 5.6. Vikundi na vilabu vya vijana vya Mazingira Hivi vitajihusisha kupitia maeneo wanayokaa au vilabu vyao vya shule katika kuhamasisha pamoja na kutekeleza moja kwa moja. 5.7. NGOs, CBOs, Vyama vya Kujitolea, na Jumuia za kijamii Hizi ni asasi za kijamii na zisizo za kiserikali zinazoweza kuhusisha makundi mbalimbali ya kijamii kama vile wanawake, wajasiriamali, wajane, wastaafu na kadhalika.

16
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa

Sumbawanga Ngara 2012


5.8. Makampuni Binafsi Makampuni yatanufaika kutokana na kupata kazi za ukarabati wa miundombinu kama barabara pamoja na mifereji, kuwa wateja wa taka rejea kama vile vyupa vya plastiki, mipira, vyuma chakavu, karatasi, mapambo, kupata machine za taka rejea (waste recycling machines) na taka hai zinazoozeshwa na magari ya taka. Pia kuingia katika ushirika wa usashaji pamoja na Serikali. Makampuni binafsi pia yanao uwezo wa kufadhili miradi midogo ya watu binafsi na vikundi vya wajasiriamali wa taka, na wapandaji wa miti, watengenezaji wa sanamu za mapambo. Makampuni haya yataweza kufaidika kutokana na kujulikana kwao kupitia matangazo ya midomo ya watu kwa kuwasifu baada ya kuona matokeo na hivyo kuwa maraki wa bidhaa zao. Kutumia fursa ya kuboresha mwanga wa mitaa wanaweza kufunga mabango yao katika taa za barabarani ambazo watakuwa wamedhamini. Kwa ujumla wake makampuni yataweza kunufaika na ukuaji wa soko lao kutokana na kufahamika kwa wateja wengi zaidi, kwani watachukuliwa kama maraki katika kuondoa kero zao. 5.9. Washirika wa Maendeleo Hao ni taasisi pamoja na Mashirika ya Kimataifa ambao kwa namna moja au nyingine wameguswa na mpango huu wa Sumbawanga Ngara. Hawa wanaweza kusaidia katika kutafuta vifaa vya kazi kama magari, Kuchangia fedha zitakazowezesha kurekebisha na kuboresha miundombinu ya taka kama vile mifereji, barabara za mji, maeneo ya soko, kutengeneza vipeperushi na vijitabu, kuchangia vifaa moja kwa moja kama matoroli, ufundi, kutafuta wafadhili na kadhalika. Baada ya kuwafahamu Wadau wa taka ufuatao ni uchambuzi wa kina wa tatizo lenyewe.

17
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa

Sumbawanga Ngara 2012

6. UCHAMBUZI WA TATIZO
6.1. MKUKUTA Kwa muda mrefu sasa Tanzania imekuwa ikitekeleza Mpango wa kupunguza Umaskini na Kukuza Uchumi (MKUKUTA) ambao juhudi mbalimbali zimetumika katika kutoa elimu pamoja na kuwawezesha wananchi. Katika eneo hili la kuboresha miji, hususan katika eneo la taka ngumu na taka miminika Serikali pamoja na wadau wa maendeleo kama vile Shirika la Kazi Duniani (International Labour Organization ILO) imejaribu kutengeneza mikakati mbali mbali ili kuona kuwa miji inakuwa sa. Lakini nguvu kubwa imekuwa ikielekezwa hasa katika miji mikubwa kama Dar es Salaam, Mwanza na Arusha.

6.2. Sheria za Mazingira na Taka, Sera Sheria ya Uhifadhi wa Mazingira Tanzania ya mwaka 2004 au kama ilivyoandikwa kwa lugha ya Kiingereza (The Environmental Management Act-EMA 2004) Sehemu ya sita (6) ya sheria inaelekeza wajibu wa mtu yeyote aishiye Tanzania kulinda na kuhifadhi Mazingira. Katika tafsiri neno Mazingira linajumuisha mambo yote yenye mahusiano yanayomzunguka Binadamu zikiwamo hewa, ardhi, maji, hali ya hewa, mwanga, harufu, vionjo, vijidudu au vimelea, shughuli za kilimo, ufugaji, mimea, rasilimali za kiutamaduni na masuala yoye yanayohusiana na shughuli za kiuchumi ikiwemo ujenzi. Waraka wa Waziri wa Nchi Osi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mheshimiwa George Huruma Mkuchika (wakati huo) unaoelekeza juu ya kufuatilia usa wa Mazingira wa mwaka 2012. Pia Waziri wa Osi ya Makamu wa Rais Mazingira
18
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa

Sumbawanga Ngara 2012


Dkt Terezya Huvisa amekuwa akitoa maelekezo ya mara kwa mara kupitia vyombo vya habari kuhusu umuhimu wa jamii kushiriki katika usa. Kufuatana na taarifa zilizotolewa na vyombo vya habari kama vile This Day ya Machi 2010 ilyoandikwa na Simbarashe Msasanuri na tati mbalimbali zinaonyesha kuwa hakujawa na viwango maalum kwa ajili ya usimamizi na upimaji wa shughuli za taka nchini. Tatizo la taka limeonekana kuwa ni suala sugu, na hivyo Serikali kulaumiwa kwa kushindwa kudhibiti suala la taka katika miji mikubwa na midogo. Katika taarifa za mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa Serikali za 2010 zinaonyesha kuwa uwezo wa Serikali katika kuondoa taka ngumu katika halmashauri ni chini ya asilimia hamsini (50%) ya taka zinazozalishwa. Inakadiriwa kuwa uwezo wa kaya kuzalisha taka ni sawa na kilo 1.8 taka za Manispaa ya Sumbawanga. Ukuaji wa uzalishaji wa taka za Manispaa ya Sumbawanga umekuwa ukiongezeka siku hadi siku. Kwa taarifa za Manispaa uzalishaji wa taka unakadiriwa kuwa ni tani 25,200 kwa mwaka na sasa ukuaji wa uzalishaji huo unakadiriwa kuwa ni asilimia tatu (3%) kwa mwaka. Hali kadhalika kumekuwa na ongezeko la idadi ya watu ambayo inakadiriwa kuwa ni sawa na asilimia tatu (3%) kwa mwaka. Hali hiyo inaonyesha kuwa ongezeko la uzalishaji wa taka litazidi kukua. Katika mkoa wa Rukwa kumekuwa na hatua mbali mbali zinazolenga kukuza uchumi wa watu wake. Hatua hizo zimepata kasi mpya zaidi hasa kutokana na jitihada za Serikali za kujenga barabara kwa kiwango cha lami kutoka Tunduma hadi Sumbawanga, Sumbawanga hadi Matai, na Sumbawanga hadi Mpanda ambayo ni Makao Makuu ya mkoa wa Katavi; Kutangaza fursa mbalimbali za kiuchumi na kuwawezesha wananchi katika shughuli za ujasiriamali, kilimo na kadhalika.

19
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa

Sumbawanga Ngara 2012


Aidha kwa malengo ya kiuchumi, kumekuwa na ongezeko la wahamiaji kutoka maeneo mbalimbali ya nchi, nchi jirani kama Zambia, Malawi, Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, Burundi, Rwanda na Kenya. Lakini pia kumekuwa na ongezeko la wageni kutoka nchi za mbali duniani kama Afrika ya kusini, nchi za Mabara ya Ulaya, Asia na Marekani. Kumekuwepo pia na ongezeko la matumizi ya Bidhaa za viwandani ambavyo mara nyingi huhitaji vifungashio maalum na visivyooza kirahisi kama vile plastiki na vyuma. Ufugaji holela katika miji na matumizi ya ardhi yasiyozingatia sheria katika kuendesha shughuli za kiuchumi na kujamii, Kukosa uelewa wa kutosha juu ya suala zima la udhibiti wa taka na usa wa miji kwa ujumla. Baadhi ya wafanya biashara ndogo ndogo (MSMEs) wamekuwa nao wakichangia suala la uchafuzi kutokana na kutozingatia taratibu za usa, mfano anaweza akauza miwa, ndizi au mahindi wateja wake wakala hapo na maganda yake kutupwa ovyo. Suala la uchomaji ovyo wa taka, uchomaji moto wa maeneo tengefu na utupaji ovyo wa taka za mkononi limechukuliwa kama ni jambo la kawaida. Baadhi ya Wajasiriamali wadogo wadogo kama Mama Lishe, gereji, mafundi seremala, mafundi wa Ushonaji, Saluni, Maduka ya nyama, wenye maduka na shughuli nyingine wamekuwa wakiacha maeneo yanayowazunguka au sehemu wanazofanyia kazi kuwa chafu, na wengine wakiamini sehemu hizo zikiwa chafu watachukuliwa kama biashara zao ni hafu hivyo hawatalazimika kulipa kodi. Pia wengine wanaamini kuwa watachukuliwa kuwa bidhaa zao ni za kimaskini, hivyo ni kwa ajili ya watu wasio na uwezo kwani watadhani ni za bei nafuu. Kwa upande wa watu wasioheshimu sheria wanaamini kuwa sehemu hizo hawawezi kwenda watu wa kada fulani, mfano viongozi hivyo kuwa ni sehemu salama kwao.

20
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa

Sumbawanga Ngara 2012


Wakati mwingine watu wamekuwa hawajali hata kufyeka maeneo yanayozunguka viwanja na makazi yao. Magofu na majengo yasiyoisha yamekuwa ndio sehemu za kutupa taka na hivyo kuwa mazalio ya wadudu hatarishi kama vile mbu, nyoka nge na kadhalika. Baadhi ya watoto wamekuwa wakicheza katika maeneo hayo, na kuwa macho yao ya kufanya vitendo viovu kama vile uvutaji bangi na madawa ya kulevya, hasa kwa watoro wa shule jambo ambalo ni hatari na linarudisha nyuma maendeleo yetu. Maeneo hayo pia huweza kutumika kwa macho ya Majambazi. Baadhi ya watu katika Jamii kutozingatia matumizi ya vyoo bora, Kujisaidia mahali pasipohusika kama vile vichakani, kukojoa pembezoni mwa barabara, kutiririsha maji machafu ovyo na wakati mwingine kuunganisha taka miminika kutoka mifumo ya vyoo vyao katika mifereji ya maji ya mvua, kumwaga maji machafu barabarani au katika maeneo ya wazi. Baadhi ya Mamlaka na Taasisi kutozingatia wajibu wao, kwa mfano Mamlaka za Maji kutorekebisha kwa wakati mifumo ya maji sa na taka hasa mabomba yanapokuwa yamepasuka. Suala la upandaji miti na bustani za maua limechukuliwa kama ni suala la anasa na la hiari, na wakati mwingine kuchukuliwa kuwa ni suala la kiuwezo. Mtu maarufu, kiongozi mkubwa, Taasisi kubwa, na pengine Mzungu ndiye anatakiwa kuwa na bustani nzuri ya maua. Kuna tabia ambazo zimekuwa kama ndio utamaduni wa kupenda kukatiza katika maeneo ya bustani bila kujali uharibifu wa maua, miti na mapambo yaliyowekwa. Sumbawanga Ngara ni pamoja na kuzingatia usa wa mtu binafsi. Unaweza kukuta mtu anafanya biashara yake, nguo zake ni chafu, nywele chafu, vyombo anavyofanyia kazi vichafu, lakini
21
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa

Sumbawanga Ngara 2012


kwa kweli ukifuatilia sababu za kuwa hivyo pengine ni kwa ajili ya uvivu tu. Gharama kubwa zinazojitokeza katika kuendesha shughuli za taka, uchakavu wa vitendea kazi na jukumu hilo kuachiwa Serikali kwa kiwango kikubwa. Hadi sasa Wananchi wa Manispaa ya Sumbawanga hawachangii moja kwa moja huduma ya taka pamoja na kuweka uzuri wa Manispaa (Solid waste management and Municipal Beautication). 6.3. Matokeo Katika siku za nyuma hali hiyo ilipelekea kuona taka za aina mbalimbali zikizagaa katika maeneo ya Manispaa ya Sumbawanga pamoja na kata zake hasa katika maeneo ya wazi, barabara, mifereji, kwenye makazi, kuzunguka maeneo ya Taasisi na kadhalika. Lakini pia kuwa na Mji usiopendeza au kuvutia. Kwa wageni wanaotoka maeneo mengine hususan wanaotoka nje ya Tanzania, wamekuwa wakiona tofauti kubwa ukilinganisha na maeneo wanayotoka. Hali hiyo hupunguza ari ya kuwekeza na kupunguza utalii katika Mkoa wetu. Pamoja na kuwepo kwa sheria ndogo za udhibiti wa taka na uharibifu wa mazingira, kwa kiwango kikubwa sheria hizo zimekuwa hazizingatiwi na wadau. Lakini mbali na uwepo wa sheria hizo, bado hazitoshelezi kwani hazielekezi rasmi namna ya kukusanya, kutenganisha, kuhifadhi, kusarisha, kuchakata na kutupa hasa kwa upande wa Manispaa, japo pamoja na mapungufu yaliyoainishwa hiyo haitoi unafuu kwa mkazi yoyote katika Manispaa ya Sumbawanga kutokutekeleza matakwa ya sheria ndogo hizo.

22
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa

Sumbawanga Ngara 2012

7. NJIA NA MIKAKATI YA KUREKEBISHA HALI


7.1. Mikakati: Katika jitihada za kurekebisha kasoro zilizopo, majadiliano ya Wadau wa Manispaa ya Sumbawanga kwa kutumia Mbinu Kongano ni muhimu sana. Katika kutekeleza haya mtazamo wa waliochangia mwongozo huu ni kama ifuatavyo: 1. Mpango wa Sumbawanga Ngara kuwa ni kipaumbele cha mkoa na uzungumzwe katika vikao, mikutano na mipango yake yote. 2. Kuwa ni shughuli mojawapo kila mgeni Mkuu wa Kiserikali anapofanya ziara Mkoani Rukwa. 3. Kuunda Kongano la Usa na Udhibiti wa Mazingira (Environmental Cluster initiatives) litakaloshirikisha wadau mbalimbali watakaofanya kazi kwa pamoja na kwa ushindani katika kuhifadhi mazingira kwa ajili ya mafanikio ya wote. 4. Kuendelea kupata ushauri kutoka kwa wadau wa Mpango huu juu ya namna bora ya kushughulikia masuala yanayohusiana. 5. Kuhamasisha wadau kwa kutoa elimu ili kukuza uelewa juu ya umuhimu wa kuwa na mji unaovutia na udhibiti wa taka. Elimu hiyo itatolewa kwa njia ya matangazo ya vipaza sauti, redioni, kanisani, misikitini na kadhalika. 6. Kushirikisha makundi maalum katika kuhifadhi mazingira kwa ujumla hususan kutoa fursa kwa vikundi kwa mfano, vikundi vya wanawake, walemavu vijana kutegemeana na majukumu yao, Makampuni na Taasisi za Umma na
23
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa

Sumbawanga Ngara 2012


makundi ya kujitolea katika kusasha na kuchangia. 7. Serikali Kupitia Uongozi wa Mkoa, Wilaya na Manispaa kuhakikisha kuwa miongozo ya mara kwa mara, ufuatiliaji na usimamizi wa taka na usa wa Mji kwa ujumla unakuwa endelevu. 8. Kuifanya siku ya jumamosi ya kila wiki kuwa ni siku ya usa, kwa hiyo wadau wote watatakiwa kushiriki katika zoezi hilo hususan katika maeneo yao wanayoishi. Pia Kila Osi na Taasii Kutenga saa moja katika katika wiki kwa ajili ya usa wa maeneo yao ya osi. 9. Kushindanisha mitaa ya Manispaa, Taasisi za Umma, Osi za Serikali, Jumuia za kidini na watu binafsi kiusa ili kuwahamasisha wanajamii kushiriki kikamilifu katika kuweka mji wao sa na kuwavutia wengine kuishi katika Mkoa wa Rukwa. 10. Kupitia wanafunzi kuhamasisha juu ya usa, Upandaji miti na Bustani. 11. Kuhamasisha vikundi mbalimbali katika kubuni mikakati ya usa. 12. Kutumia vyombo vya Habari katika kutoa elimu ikiwemo kutangaza kwa vipaza sauti, Televisheni, radio, blog na magazeti 13. Kuboresha sheria zilizopo 14. Kuishirikisha vyombo vyote vya dola, Serikali, Bunge na Mahakama katika kusimamia sheria ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua zinazostahili wale wote wanaokiuka sheria na taratibu zilizowekwa. 15. Kushindanisha vyuo vya elimu, chuo kikuu huria na vyuo vya uganga katika kubuni mikakati namna ya kuwasaidia
24
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa

Sumbawanga Ngara 2012


wajasiriamali na shughuli za usa katika Manispaa ya Sumbawanga 16. Kufanya matembezi ya mshikamano kwa ajili ya kuchangisha fedha, na makongamano ya kuhamasisha wadau juu ya Mpango huu.

17. Kutenga maeneo ya shughuli za kiuchumi na kuwapanga wadau kadiri inavyofaa. 18. Kutafuta wafadhili ikiwa ni pamoja na kutafuta maraki wa Manispaa ya Sumbawanga Kiusa. 19. Kuendelea kutoa elimu kupitia sanaa na michezo. 20. Kuhamasisha wadau kuchangia gharama pamoja na kufadhili vikundi vinavyojihusisha na kazi za taka. 21. Kutengeneza maeneo maalum ya bustani na sehemu za kuchezea watoto. 22. Kuweka alama za barabarani. 23. Kuzuia ujenzi holela. 24. Kupata takwimu za miti iliyopo. 25. Kutenga na kuhifadhi maeneo ya vyanzo vya maji. 26. Elimu kwa wanafunzi Sumbawanga Ngara. na kuanzisha vitabu vya

27. Kuzuia kilimo kisichozingatia kanuni bora za kilimo na taratibu za mipango miji. 28. Kuzuia shughuli za uchimbaji wa madini zisizo na kiwango kufuatana na Sheria za Mji na Mazingira. 29. Kuondoa mizoga yote barabarani. 30. Kutumia mbinu zisizo na uharibifu au uchafuzi katika uvunaji wa Kumbikumbi. 31. Kuweka utaratibu wa kupuliza dawa za kuua mazalio ya mbu.
25
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa

Sumbawanga Ngara 2012


32. Kupata taarifa ya macho ya watoto wa mitaani na wanaojihusisha na madawa ya kulevya na vitendo vingine visivyofaa. 33. Kuweka vibao vya namba za nyumba na majina ya mitaa na vijiji. 34. Kuingiza namba za nyumba na wamiliki wote katika kumbukumbu za ngamizi (Computer Database). 35. Kuzitambua shughuli zote za wajasiriamali wadogo wadogo waliopo mtaani. 36. Kuzingatia kutenga maeneo maalum kwa ajili ya shughuli za biashara, taasisi za umma, makazi, viwanda n.k. 37. Kupanda miti inayoonyesha mwisho wa barabara kuu na za mitaa ili kuzuia uvamizi. 38. Kutengeneza barabara za mtaa kwa kutumia vikundi kazi, 7.2. Namna ya ushiriki wa wadau. 1. Kila Mwananchi na Mkazi wa Manispaa ya Sumbawanga ndiye Mdau Mkuu katika kufanikisha usa wake mwenyewe na mazingira yanayomzunguka. 2. Mkuu wa mkoa atakuwa na wajibu wa kutoa maelekezo ya mara kwa mara kuhusiana na hali ya Usa na mazingira kwa ujumla ya Manispaa ya Sumbawanga na Mkoa kwa ujumla ili kusaidia maboresho yanayohitajika. 3. Mkurugenzi wa Manispaa ndiye mmiliki mkuu wa mpango huu katika kufuatilia kazi za kila siku pamoja na gharama zinazohusika, pamoja na kuratibu maendeleo ya Mpango huu kwa kushirikisha wadau wengine pale inapobidi. 4. Halmashauri ya Manispaa itakuwa na wajibu wa kutenga maeneo kwa ajili ya matumizi ya biashara na shughuli za Mpango huu ikiwa ni pamoja na kulipima eneo la muda
26
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa

Sumbawanga Ngara 2012


(Temporary waste stations) na la kudumu (Dump site) kwa ajili ya kuhifadhi taka. 5. Halmashauri ya Manispaa itatakiwa kuhakikisha kuwa kila wakati kunakuwa na sheria ndogo zinazokidhi uwezeshaji wa Mpango huu. 6. Wadau wa Mpango kwa kushirikiana na Manispaa watasaidia katika kuchangia mawazo, rasilimali watu na fedha ikiwemo shughuli za kitaalam kama vile kuandaa maandiko mbalimbali yanayolenga kutafuta fedha, vifaa na kadhalika. 7. Kila Diwani atatakiwa kusimamia kiukamilifu utekelezaji wa Sumbawanga Ngara katika eneo lake. 8. Kila Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa au kijiji atatakiwa kuja na mkakati wa eneo lake ukitafasiri mpango huu katika mazingira halisi ya eneo lake. Mfano kutambua kaya, maeneo ya kuhifadhi taka, namna ya kuchangia gharama ikiwemo kusasha, kupanda miti, nyasi, bustani, kuondoa vifusi, kufukia mashimo barabarani, kuzibua mifereji, kuondoa mizoga na kadhalika. 9. Kila familia/kaya, au Taasisi yoyote ile itawajibika kutekeleza matakwa ya mpango huu. 10. Watu binafsi au Vikundi mbalimbali vyenye nia ya kufanya kazi za kibiashara kuhusiana na mpango huu vitatakiwa kusaidiwa kwa kuwakewa utaratibu maalum usio na usumbufu na kuwatafutia kituo maalum (informal) ambacho kitasaidia kutoa anuani yao. 11. Asasi zisizo za Kiserikali (NGO) na Asasi za Kijamii (CBO) kuhakikisha kuwa mpango huu unajulikana kwa wengi na hivyo kusaidia kufanya kampeni, makongamano na utetezi wa uharibifu wa mazingira.
27
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa

Sumbawanga Ngara 2012


12. Wanasiasa na viongozi wa dini watatakiwa kuunga mkono mpango huu na kuhamasisha wafuasi wao kupitia mikutano yao mbalimbali. 13. Wanafunzi watatakiwa kupewa elimu juu ya Mpango huu na wao kuwa vinara kupitia vilabu vyao vya mazingira. 14. Vyuo na taasisi za elimu vitatakiwa kufanya tati na kubuni mikakati itakayosaidia kuongeza kasi ya udhibiti wa mazingira na kuongeza ajira bora kupitia mpango huu. 15. Kila kituo cha kazi (kijiwe) cha biashara kuweza kupewa elimu ya usa mahali walipo kwenye shughuli zao. 16. Mifugo hairuhusiwi kuzurura ovyo katika Manispaa badala yake ifugwe kwenye Mazizi (Zero Grazing) na iwe michache. 17. Huduma zote za kijamii zinazohusiana na taka zizingatie sheria zilizopo, kwa mfano Machinjio na Minada ya bidhaa mbalimbali. 18. Kila makazi na maeneo ya huduma lazima kuwa na vyoo madhubuti. 19. Miti yote ya Manispaa lazima ihesabiwe na isikatwe bila kupewa idhini ya Manispaa. 20. Kwa Ujumla kila Mkazi atatakiwa kuzingatia sheria na taratibu za miji.

28
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa

Sumbawanga Ngara 2012

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akishiriki kwa vitendo usa wa mazingira kwa kusasha mitaro katika mji wa Sumbawanga tarehe 12 Januari, 2012.

7.3.

Mduara wa Utekelezaji

7.4. Ukusanyaji wa taka: Katika hatua ya kwanza mtu binafsi, kaya au Taasisi za Umma watakuwa na wajibu wa kuhakikisha kuwa taka kuzunguka maeneo yao au sehemu zisizohitajika zinakusanywa na kuhifadhiwa vizuri kutegemeana na aina ya taka, mfano karatasi, plastiki, chupa za vioo na kadhalika. Katika hatua ya pili taka za hatua ya kwanza zitapelekwa kwenye vituo vya muda kwa kutumia watu binafsi, mikokoteni ya vikundi au magari binafsi na ya makampuni au Taasisi. Katika hatua ya tatu Magari ya manispaa au mawakala wao ndio watahusika katika kuondoa taka hizo na kuzipeleka katika kituo cha kudumu yaani Dampo. Gharama za kazi hiyo zitapangwa kadiri ya taratibu zitakazowekwa na Manispaa.
29
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa

Sumbawanga Ngara 2012


7.5. Upimaji wa Utekelezaji Upimaji wa utekelezaji wa mpango huu utafanyika kwa kuangalia mambo yafuatayo: Ushahidi wa macho utakaoonyesha ushiriki wa wadau na kupungua kwa taka Kupitia ukaguzi utakaofanyia kila wiki, itaweza kubainishwa hali inavyoendelea kwa kuona, kuuliza, kwa taarifa za kazi za ukusanyaji wa taka. Taarifa za magonjwa ya hospitali zitaonyesha kupungua kwa magonjwa yanayoambatana na uchafu Ushuhuda kutoka kwa wadau kuwa Manispaa inapendeza na maeneo mengine ya Mkoa wa Rukwa yatakayokuwa yameiga. Ustaarabu utaongezeka mfano vitendo vya wizi vitapungua kwa sababu baadhi yao watajihusisha na shughuli za uhifadhi wa mazingira. Pia kutokana na kuelimika watu watapunguza kutupa taka ovyo, vituo vya kazi vitapendeza na kuheshimika zaidi. Nyaraka mbalimbali zinazosaidia utekelezaji kama vile karatasi za Ilani, matangazo na kadhalika. Taarifa au takwimu rasmi zitakazoonyesha uratibu wa shughuli za taka mfano idadi ya miti, waliochukuliwa hatua kama vile kupelekwa mahakamani,kulipa faini na kadhalika.Pia taarifa zinazoonyesha ratiba za usa Taarifa za ongezeko la Biashara na Uwekezaji Kupungua kwa kero za taka na uharibifu wa mazingira kwa ujumla. Machapisho mbalimbali juu ya Udhibiti wa taka kupitia blogs na magazeti na vyombo vingine vya habari. Kupitia tati kujua hali ilivyo.
30
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa

Sumbawanga Ngara 2012

8. HITIMISHO
Tumeamua kuanza mpango huu kwa manufaa ya Sumbawanga, Mkoa wetu wa Rukwa na Tanzania nzima kwa ujumla. Naomba sote tudhamirie na tujitoe kuufanikisha mpango huu kwa ustawi wa leo na kesho wa Sumbawanga yetu, Rukwa yetu na Taifa letu. Kama alivyosema yule Mwandishi wa Marekani Hellen Keller kwamba, Peke yetu tunafanya machache, pamoja tunafanya mengi. Tukijitoa sote kufanya kazi kwa bidii, ufahamu na maarifa hata yale yanayoonekana hayawezekani yatawezekana na hata yale yanayoonekana magumu yatakuwa mepesi. Na tuanze sasa safari hii yenye heri na mafanikio tukimuomba Mungu atusaidie. Maandishi haya yatuongezee nguvu ya kuanza safari yetu ya kuhakikisha kuwa Sumbawanga ina Ngara na Halmashauri nyingine za Rukwa zifuate. Tutaendelea kuboresha maandishi haya siku hadi siku, huku tukivuna uzoefu na kuweza kuyaboresha kadiri tunavyojifunza na kupata ushauri mbalimbali hasa ule wa kitaalam. Inawezekana, kila mtu atimize wajibu wake.

Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Rukwa.

31
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa

Sumbawanga Ngara 2012

OFISI YA MKUU WA MKOA WA RUKWA


S.L.P. 128 Sumbawanga Simu: 025-2802137/ 2802318/ 2802131 Nukushi: 025-2802217/ 2802144 Barua pepe: rasrukwa@pmorallg.gp.tz / rasrukwa@yahoo.com Website: www.rukwa.go.tz Blog: rukwareview.blogspot.com

Novemba, 2012

32
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa

Sumbawanga Ngara 2012

33
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa

Dhamira ya dhati inazaa matunda bora!! Kukosea ni kujifunza, Kurekebisha ni ukamilifu..!


Eng. Stella Martin Manyanya (Mb) alizaliwa katika kijiji cha Mango mnamo mwaka 1962. Alimaliza Mafunzo ya Ufundi Mchundo wa Umeme mwaka 1983 DIT, na Stashada ya juu ya uhandisi umeme (ADE) mwaka 1993 DIT, Stashahada ya Uzamili ya Uhandisi umeme katika chuo kikuu cha Sayansi na Technolojia NTNU Norway 1996. Pia alimaliza Stashada ya Uzamili (PGDEED) mwaka 2007 na Shahada ya Uzamili (MEED) 2009 katika fani ya Ujasiriamali na Uendelezaji wa Biashara- Chuo kikuu cha Dar Es Salaam (UDSM - UDBS). Aliajiriwa na STAMICO kama fundi umeme na kisha kuajiriwa na TANESCO kama Mhandisi wa Umeme mpaka mwaka 2005. Eng. Stella M. Manyanya (MB) ana Uzoefu Mkubwa katika masuala ya umeme, Ujasiriamali na Siasa. Pia ameshiriki katika kazi za udhibiti wa mazingira toka mwaka 2000 akiwa Dar es Salaam. Eng. Stella M. Manyanya (Mb) ni mpenzi wa kujisomea na kujiendeleza kupitia vitabu, midahala, makongamano, machapisho na mitandao mbalimbali. Ni mtu anayependa kujumuika na watu wa makundi yote.Ni mama wa Familia. Kwa sasa Eng. Stella M. Manyanya (Mb) analitumikia Taifa la Tanzania katika nafasi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa na Ubunge Viti Maalum CCM Mkoa wa Ruvuma.

Sumbawanga Ngara 2012

Sumbawanga Ngara
Umoja wetu ni Ushindi!
34
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa

You might also like