You are on page 1of 9

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI)
HALMASHAURI YA WILAYA YA MISUNGWI

Simu:2555-732980745
(W), Fax: 255-732980745
Teknolojia,Habari,

Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji


Kitengo cha

Baruapepe: dedmisungwi@gmail.com

Mawasiliano na Uhusiano
S.L.P 20
MISUNGWI.

TAARIFA YA UFAFANUZI KWA UMMA KUHUSU TAARIFA ILIYOSAMBAZWA


KATIKA MITANDAO YA KIJAMII YA KUDHALILISHWA KWA MWALIMU WA
SEKONDARI YA SHILALO TAREHE 17 OKTOBA,2016.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, Eliurd Mwaiteleke


anapenda kuwataarifu Wananchi wote na Umma kwa ujumla kuhusu taarifa
iliyosambazwa kwenye Mitandao ya Kijamii tarehe 17 0ktoba,2016 kuhusiana na
kitendo cha Udhalilishaji wa Mwalimu mmoja katika Shule ya Sekondari Shilalo iliyopo
katika Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi.
Hivyo,kutokana na taarifa hiyo ilizosambazwa kwenye mitandao ya Kijamii yenye
kichwa cha habari,MKURUGENZI MISUNGWI AMWAMURU MWALIMU APIGE
DEKI

MBELE

YA

WANAFUNZIambayo

ilieleza

kuwa

Mkurugenzi

huyo

alimuamrisha Mwalimu kudeki darasa huku wanafunzi wake wakimshuhudia ambapo


1

wanafunzi hao wa kidato cha nne walikuwa wakijisomea kwa ajili ya maandalizi ya
Mitihani,kwa mujibu wa taarifa rasmi kuhusiana na hali Halisi katika tukio hilo taarifa
iliyotolewa ya kwamba alimuamrisha kudeki darasa si ya kweli kutokana na sababu na
mambo yafuatayo:i/.Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi alianza Ziara
ya kikazi tarehe 4 oktoba,2016 katika Kata ya Mondo kwa lengo la kutoa
Mwelekeo wa shughuli za Serikali ya awamu ya tano kwa Watendaji wa Kata na
Vijiji na Wataalam wote wa Ngazi ya kata na vijiji pamoja na mambo mengine
ikiwa ni kukagua utekelezaji wa shughuli na miradi ya maendeleo vijijini
iliyotekelezwa kuanzia mwaka 2013/2014- mwaka 2015/2016 pia aliambatanana
na baadhi ya Wataalamu

wa Idara na Vitengo

mbalimbali vya

Halmashauri,ambapo alifanya kikao cha ndani pamoja na Uongozi wa Kata na


kutembelea katika taasisi za Elimu,Maji, barabara, Kilimo,Mapato na Afya
ambazo ni Shule za Msingi na Sekondari pamoja na Zahanati na Vituo vya Afya.
Kwa Mantiki hiyo, katika ziara hiyo alibaini baadhi ya Mafanikio makubwa
yaliyoko kwenye miradi mbalimbali iliyopo vijijini na kupongeza juhudi
zilizofanyika pamoja na hayo aliona Changamoto na kasoro katika baadhi ya
Miradi na maeneo ya Kiutendaji kwa baadhi ya Watumishi wa umma ambao
hawawajibiki ipasavyo na kutozingatia maadili ya Utumishi wa umma
Mfano:Usafi wa Mazingira ya ndani na nje ya eneo la Taasisi, Madarasa, Vyoo
na Mazingira,Kufanya kazi kwa bidii na Weledi,Kuzingatia Sheria, Taratibu na
Kanuni na Miongozo ya kazi.
Alitoa maelekezo ya jumla kwa Viongozi wa ngazi ya
watendaji

Kata kuwasimamia

na Watumishi wote walioko chini yao ili kuleta tija na matokeo

yanayonekana kwa muda mfupi,wa kati na mrefu na utoaji wa taarifa kwa


wakati na kushauri mapema Miradi ambayo haitekelezwi kwa kiwango na
ubora kulingana na thamani ya fedha,Mfano:Baadhi ya Majengo ya Nyumba

katika Zahanati ya kijiji na shule ya Msingi Ntulya yameanza kubomoka na


kuhatarisha maisha ya watu.
ii/.Katika Kata ya Shilalo alifanya Ziara tarehe 5 oktoba,2016 na kutembelea na
kukagua miradi na shughuli za Maendeleo katika maeneo ya Shule za Msingi 6,
Sekondari ya Shilalo, Ujenzi wa Ofisi ya kata,Ujenzi wa Zahanati 3,Ujenzi wa
Masjala ya Ardhi 2,Lambo la kunyweshea Mifugo na Uhamasishaji wa Michango
ya CHF kwa jamii.Hata hivyo,Mkurugenzi Mtendaji huyo aliwapongeza
Viongozi na Wataalamu wa kata na vijiji kwa mafanikio hayo na kuwasihi
waendelee na kasi hiyo ya maendeleo kwa kuzingatia kanuni, sheria na taratibu
pamoja na kuongeza bidii katika ukusanyaji wa Mapato kwa kutumia njia ya
mashine za Kielektroniki.
iii/.Baadhi ya mambo yaliyobainika na kutolewa taarifa na watendaji na
wataalamu wa kata hiyo katika kuboresha na kuimarisha utendaji kazi ni pamoja
na Serikali kuongeza idadi ya wataalamu katka sekta ya Elimu na Afya na
Vitendea kazi ikiwemo Usafiri, na kutoa fedha za kukamilisha miradi iliyoko
katika hatua mbalimbali za ujenzi.

iv/.Mkurugenzi Mtendaji Wilaya pamoja na Wataalamu kutoka wilayani na


Wataalamu wa ngazi ya kata na vijiji walibaini na kushuhudia baadhi ya
Changamoto mbalimbali zikiwemo,Uchafu wa Mazingira ya nje na ndani ya
Madarasa 5 na Vyoo vya Walimu na wanafunzi katika Shule ya Sekondari
Shilalo,hali ambayo haikuwafurahisha timu yote ilifika Shuleni hapo,ambapo
Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya alitoa Maelekezo kwa Walimu wote
waliokuwepo kutimiza wajibu wao wa kuwasimamia kikamilifu wanafunzi
kufanya Usafi na kutunza Mazingira ikiwemo usafi wa madarasa,vyoo na ofisi
zao na kusisitiza Mwalimu wa darasa na wa Zamu kuwajibika katika majukumu
yao kwa kuwasimamia wanafunzi kufanya usafi kwa ujumla kila siku pamoja na
kudeki Madarasa yao angalau mara 2 kwa wiki na kupanda miti kupanda katika
mazingira ya shule.
3

v/.Vile vile timu katika ukaguzi wake, ilibaini shule ya Msingi Mwamboku
ikiwa na mazingira yenye uchafu uliokithiri hususan upande wa vyoo vya
wanafunzi,hali ambayo wajumbe wote wa ziara waliona na kufedheheshwa na
hali ya mazingira hayo hatarishi ya wanafunzi kujisaidia juu ya sakafu na nje
ya jengo la choo,ambapo Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya aligundua kuwa
baadhi ya watendaji wanafanya kazi kwa mazoea na uzembe wa hali ya
juu,kitendo ambacho kinaweza kusababisha mlipuko wa magonjwa kama
kichocho na kipindupindu.Aidha,Mkurugenzi huyo alichukua hatua ya kumvua
Madaraka ya Ualimu mkuu aliyekuwa Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo,na
kuagiza abaki na nafasi ya Ualimu wa kawaida shuleni hapo.
vi/.Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya katika Majumuisho ya ziara aliwapa
maelekezo ya jumla,na kuwataka wataalamu wote kuwa Waadilifu,kuwajibika
na kufanya kazi kwa uzalendo.Pia alisisitiza Maafisa watendaji wote Kata na
vijiji kuhakikisha wanafanya usafi wa mazingira ya maeneo ya Taasisi zao na
kusimamia wananchi katika kutekeleza Agizo la Mheshimiwa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania,Dkt,John Pombe Magufuli la kufanya usafi kwenye
maeneo yote,pamoja na Mkakati wa Mkoa na Wilaya uliowekwa wa kufanya
usafi wa mazingira kwa kila Jumamos ya kila mwisho wa Mwezi.
vii/.Hivyo pamoja na maelekezo ya Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya kwa
wataalamu ngazi ya kata na vijiji kusisitiza uwajibikaji,vile vile Wakuu wa Shule
za Sekondari na Walimu wakuu wameagizwa kutekeleza vyema majukumu yao
ya kila siku na kuzingatia mpango kazi,kwa barua yenye

kumb

Na.MZA/MDC.F.10/63/13 ya tarehe 12/10/2016,iliyosainiwa na Afisa Elimu


Sekondari Wilaya ya Misungwi.

Kutokana na sababu na maelezo hayo,yenye mantiki Mkurugenzi Mtendaji wa


Wilaya ya Misungwi katika ziara hiyo ya kikazi ameweza kutimiza wajibu wake
kwa mujibu wa sheria na miongozo ya Serikali inayosisitiza viongozi katika
Maeneo yao kutembelea na kukagua shughuli zote za Mendeleo
4

ikiwemo

miradi mbalimbali na kutoa maelekezo na maagizo.Pamoja na hayo ziara yake


inaendelea ambapo amepanga kutembelea kata 2 kila wiki na kukamilisha kata
zote 27 za Wilaya ya Misungwi ifikapo mwezi Disemba,2016.
Katika mwendelezo wa ziara hiyo tarehe 18 oktoba,2016 amefanya ziara katika
kata ya Gulumungu na kutembelea Taasisi zote ndani ya kata na kubaini
mabadiliko makubwa katika baadhi ya maelekezo na maagizo aliyoyatoa kwa
kata alizotembelea awali ikiwemo na suala la usafi wa mazingira hususan katika
usafi wa vyumba vya madarasa,vyoo na mazingira kwa ujumla pamoja na
watumishi kuanza kubadilika kwa kuonyesha matokeo ya muda mfupi na
hakusita kutoa pongezi kwa watendaji waliofanya vizuri na kwa ubunifu, na
kuagiza Mwalimu mmoja wa shule ya Msingi Lukanga mwenye ubunifu katika
sanaa ya uchongaji na uchoraji kuhamishiwa katika shule maalum ya Mitindo.
Kwa matukio zaidi ya picha Bofya chini.

Picha inayoonyesha jengo la choo katika shule ya msingi Lukanga,Kata ya Gulumungu.Ikionyesha hali
halisi ya usafi wa vyoo ulivyo kwa sasa baada ya kupokea maelekezo ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Misungwi.

Jengo la choo cha shule ya msingi ,Mwamboku likionyesha hali isiyoridhisha katika usafi wa mazingira na
rafiki kwa matumizi ya wanafunzi ndani na nje .Hali hiyo ilibainika baada ya ziara ya Mkurugenzi
Mtendaji wa Wilaya ya Misungwi na kutoa maelekezo kwa shule zote kuzingatia usafi wa
mazingira.Aidha alimwagiza Mganga Mkuu wa Wilaya kuhakikisha anawapima wanafunzi endapo
wameambukizwa Magonjwa ya kuambukiza kama kichocho na Mengineyo na kutoa taarifa za kitabibu.

Picha ya jengo la nyumba ya Mganga Mfawidhi katika zahanati ya kijiji cha Ntulya ikionyesha nyufa
zilizokwisha jitokeza ikiwa ni miaka 2 tangu ifunguliwe na Mheshimiwa Rais wa awamu ya
nne.Dkt,Jakaya Kikwete mwaka 2013.Hali inayoonyesha namna ya baadhi ya watendaji wasioweza
kusimamia utekelezaji wa miradi na kutokuwa wazalendo kwa Taifa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Misungwi ,Eliurd Mwaiteleke akitoa maelekezo ya kiutendaji kwa
wataalamu wa Kata ya Shilalo katika kikao cha ndani kabla ya ukaguzi wa shughuli na Miradi ya
Maendeleo kwenye taasisi za Kata hiyo.Walioketi kutoka kushoto ni Afisa mtendaji wa Kata,Mheshimiwa
Diwani wa Kata ya hiyo Mayila Maguha,Kulia Mchumi Sylvia Rwehabura, akifuatiwa na Mwakilishi wa
Mganga Mkuu Wilaya.Picha zote na Thomas Lutego Misungwi.

Imetolewa na:
Thomas Lutego
Kaimu Afisa Habari na Mawasiliano (W)
MISUNGWI
18 Oktoba,2016

You might also like