You are on page 1of 9

THE INSTITUTE OF FINANCE MANAGEMENT STUDENTS’

ORGANISATION,

“ONE FOCUS ONE GOAL”

RIPOTI YA UTENDAJI KAZI YA NUSU MWAKA.


WIZARA YA KAMPASI NA MALAZI
2021/2022

IMEANDALIWA NA:
WAZIRI - FRED A. BUZIKA
CALL : 0623025002.
NAIBU WAZIRI - FAUZIA SULEIMAN
CALL : 0685822989.
SALAMU, NA NENO LA UFUNGUZI.
Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Naibu spika, Mheshimiwa katibu wa bunge,
Mheshimiwa Waziri Mkuu, Baraza la Mawaziri, Waheshimiwa Wabunge, Habari za
Wakati huu.

Awali ya yote Natanguliza shukrani zangu kwa Mola wetu mlezi aliyetuwezesha sisi
kukutana hapa siku ya leo katika bunge la pili la ISRC. Napenda kutumia nafasi hii
kumshukuru Mheshimiwa Rais wa serikali ya wanafunzi IFM, Mh. Al-Haidary
Khamis Ngomero kwa Imani aliyonayo juu yangu na kuniteua kuwa katika baraza
lake. Vilevile ninamshukuru Mh. Makamu wa Rais, Mh. Philemoni Mwakanyamale
na Mheshimiwa Waziri Mkuu, Mh.Shwaibu kwa iman zao na kunipokea katika
baraza hili wanaloliongoza. Aidha ninawashukuru kwa dhati kabisa viongozi
wenzangu katika baraza la mawaziri kwa ushirikiano wao wakipekee katika
majukumu yetu ya kila siku.

MUHTASARI.
Mheshimiwa Spika, Ripoti hii ninayokwenda kuisoma ni ripoti ya utendaji kazi wa
wizara ya kampasi na malazi katika muhula wa kwanza wa masomo wa mwaka
2021/2022. Ripoti hii imegawanyika katika sehemu tano, sehemu ya kwanza ni
utangulizi, shemu ya pili malengo wizara, sehemu ya tatu ni mafanikio ya wizara,
sehemu ya nne ni changamoto zinazoikumba wizara na sehemu ya tano mwisho wa
ripoti yaani hitimisho.
SEHEMU YA KWANZA
UTANGULIZI.
Mheshimiwa Spika, Wizara ya kampsi na malazi yaani “Ministry of campus and
accomodation” ni moja ya wizara tisa zilizounda serikali ya wanafunzi IFM mwaka
2021/2022. Wizara hii imetengwa na wizara ya Afya kwa kulinganisha na mwaka
jana ambapo ilikuwa ni wizara moja.
Wizara inaundwa na viongozi wawili ambao ni waziri na naibu waziri, Kwa sasa
waziri mwenye dhamana ni Fred Abely Buzika, na naibu waziri ni Fauzia suleimani
.

SEHEMU YA PILI
MALENGO YA WIZARA.
Mheshimiwa Spika, Wizara ya kampsi na malazi katika serikali ya wanafunzi IFM
mwaka 2021/2022 ina malengo kadhaa yakuyafikia kabla muda wake kuisha.
Malengo haya ni muhimu kwetu ili kuweza kuboresha mazingira na afya za
wanafunzi wa IFM pamoja na jamii nzima ya IFM kwa ujumla.
Mheshimiwa Spika, malengo katika wizara hii ni kama yalivyoainishwa hapa chini
na nitayasoma kama ifuatavyo.
i. Kuhakikisha unafanyika ukarabati wa Block C & D kwenye maeneo mbali
mbali
ii. Kuhakikisha ubadilishwaji wa madawati na viti vibovu vya Block A
Unafanyika kwa weredi na ukamilifu
iii. Kuhakikisha upatikanaji wa decoda ya Azam na Dstv vinapatikana na
kulipiwa kifurushi ili wanafunzi wasiteseke katka kuangalia kandanda safi la
mwamba wa Lusaka
iv. Kuhakikisha tunalinda na kuboresha mazingira ya chuo chetu cha IFM na
maeneo yanayozunguka chuo.
v. Kuhakikisha kunapatikana ufumbuzi au utatuzi wa changamoto yeyote ile ya
kimazingira ndani ya chuo chetu haraka iwezekanavyo kila pale changamoto
itakapojitokeza. Hapa tunakusudia zaidi zile changamoto zinazotokana na
uharibifu wa baadhi ya miundombinu au vitu
vi. Kuhakikisha tunalinda na kuboresha mazingira yote ya canteen na yanayo
izunguka canteen ili kulinda maslahi ya wanafunzi wetu.
vii. Kuhakikisha kunapatikana Vimbweta eneo la Maktaba ya Taifa ili wanafunzi
waweze kupata sehemu ya kujisomea
Kuhakikisha tunawapa wakazi wa hostel za kijichi huduma ambazo
zinapatikana apa main campus vifaa vya michezo na huduma zingine kama
television na mengine pia

SEHEMU YA TATU
MAFANIKIO YA WIZARA.

1. USIMAMIZI WA MAREKEBISHO MBALIMBALI.


Mheshimiwa Spika, Kwa kushirikiano kutoka kwa wanafunzi, viongozi wenzetu,
mafundi wa chuo, ofisi ya majengo pamoja na uongozi wa chuo, wizara imefanikiwa
kuwezesha marekebisho ya maeneo mbalimbali baada ya uharibifu kutokea.
Miongoni mwa maeneo ambayo wizara imesimamia kwa ukaribu marekebisho yake
ni matengenezo madogo yaliyofanyika hostel (Block C & D)wanawake na
wanaume.

Mheshimiwa Spika, wizara inatambua changamoto zilizopo katika jengo hili la


hostel za wanaume na majengo mengine hapa chuoni. Hata hivyo, wizara ingependa
kulieleza bunge lako tukufu ya kwamba bado kuna matengenezo ya kati na
matengenezo makubwa yanahitajika na yatafanyika. Wizara ingependa kueleza wazi
kwa kuendelea na utatuzi wa changamoto hizi, marekebisho ya kati katika majengo
hayo yamefanyika hivi karibuni. Tukumbuke ya kwamba marekebisho haya ni yale
madogo na ya kati na bado marekebisho makubwa yanahitajika. Tukumbuke pia ya
kwamba marekebisho makubwa hayawezi kufanyika kukiwa na wakazi ndani, hivyo
ni lazima yafanyike wakati wa likizo ndefu.

Mheshimiwa Spika, Eneo jingine ni katika marekebisho ya viyoyozi madarasani na


kubadili baadhi ya vile vilivyoharibika zaid. Marekebisho haya yalifanyika mapema
mwezi wa kwanza na marekebisho mengine yanafanyika karibuni kabla ya kuanza
mitihani ili kuepusha adha ya joto madarasani.

Mheshimiwa Spika, Sisi kama wizara tulifanikiwa kusimamia suala zima la


farmigation katika maeneo yote ndani ya chuo na nje ya chuo kwa kipindi chote cha
likizo ya mwezi wa 7 ikiwemo maktaba ya taifa,kijichi na masaki nyumba za
walimu lengo nikupunguza au kuondoa wadudu watambaao na rukao wanao leta
madhra ya magonjwa ya mambukizi ambayo yanaweza kusababisha mlipuko kwa
wakazi waishio wamaeneo hayo.

Mheshimiwa Spika, wizara imefatilia suala zima la usafiri wa kijichi ambapo


mpaka sasa wanafunzi wetu wanaosoma hapa ifm na kurudi kijichi tuliweza kupata
gari inawafikisha hapo chuo cha mwalimu nyerere ni kwa sababu ya uchache wa
wanafunzi wanao toka kijichi kuja hapa ifm niwachache ,hivyo tulilazimika
kuchangia gari na wanafunzi wa mwalimu nyerere wanao ishi kijichi. Pia wizara
tulikaa nakuchagua DEOGRATIAS M.MASSAWE awe muwakilishi wa wakazi
wakijichi wakiwa na changamoto au matatizo mbalimbali yanayo wakumba wakazi
wa ishio eneo ilo ,tumefanya hivyo kwa sababu na yeye ni mmoja wa mkazi anaeishi
kijichi ,hivyo tunashirikiana kwa karibu na kufatilia mambo mbalimbali.
Mheshimiwa Spika,wizara ilifanikiwa kuwasaidia wanafunzi waliyo unguliwa na
hosteli kigamboni ,hivyo wanafunzi hao walipoteza mali zao zote,wakabakiwa kama
walivyo hawakufanikiwa kuokoa kitu chochote ,hivyo wizara tulifanikiwa kuwapa
msaada wa makazi ya kijichi kwa mda ili waweze kuendelea na masomo yao ambapo
mpaka sasa bado wapo katika makazi yakijichi.

2. KUFANIKISHA VIKAO VYA WAKAZI WA HOSTEL.


Mheshimiwa Spika, Wizara ikishirikiana kwa ukaribu na ofisi ya mshauri wa
wanafunzi imefanikiwa kuandaa vikao viwili vya wakazi wa hostel mpaka sasa.
Vikao hivi vilihusisha wakazi wote wa hostel, serikali ya wanafunzi na ofisi ya
mshauri wa wanafunzi. Kila kikao kilihusisha wakazi husika wa kila jengo, kikao
cha kwanza kilikuwa ni cha wanaume wakazi wa block C kilicho fanyika tarehe
01/02/2022 siku ya jumanne,kisha kikafata kikao cha kina dada wakazi wa block D
kilichofanyika siku ya jumatano tarehe 02/02/2022 na wale wachache wanaoishi
block C.mahudhurio ya wasichana yalikuwa jumla330 kati ya 628 na wavulana
walikua98 kati 345

Kila kikao kilihusisha kukumbusha sheria za chuo na sheria za ukazi wa hostel,


kushauri wanafunzi katika masuala mabalimbali ya kijamii na kimasomo lakini pia
kupokea changamoto mbalimbali zinazowakumba wanafunzi katika mazingira ya
chuo na kutolea ufafanuzi baadhi yake.hivyo tulifanikiwa kupita kila room block D
na C,nakuchagua viongozi wa kila chumba nakutengeneza group la viongoozi lengo
nikutatua changamoto za wakazi wa hostel kwa urahisi kupitia group hilo.

3: KUFANIKISHA UPATIKANAJI WA SEHEMU YA MALAZI KWA VIONGOZI


HUSIKA.

Mheshimiwa Spika, Wizara imefanikiwa upatikanaji wa sehemu za malazi katika


hostel za ndani ya chuo kwa baadhi ya viongozi. Viongozi hao husika ni kama
walivyoainishwa katika bajeti ya serikali ya wanafunzi ambao ni Rais, makamu wa
rais, waziri mkuu, spika wa bunge, pamoja na viongozi wa wizara ya kampasi na
afya.

3. KUSAIDIA WANAFUNZI KATIKA ZOEZI LA KUPATA MALAZI HOSTEL ZA


KIJICHI
Mheshimiwa Spika, Wizara imefanikiwa kusaidia wanafunzi kupata malazi katika
hostel mpya zilizopo eneo la kijichi. Pia wizara imefanya matembezi katika hostel
hizo ili kusaidia wale waliokuwa na nia ya kuhamia kule kufika, kuziona na kuzuru
hostel hizo pamoja na eneo linalozunguka. Vilevile wizara imefanya na inaendelea
kufanya juhudi kubwa ya kuzitangaza hostel hizo ili wanafunzi waweze kupata
malazi katika sehemu nzuri, salama na kwa bei nafuu. Wizara haikuishia hapo tu,
bali imefanikiwa na inaendelea kutatua changamoto mbalimbali zinazojitokeza kwa
upande wa wakazi wa hostel za kijichi.

Wizara inapenda kuwashukuru viongozi wote na hasa viongozi wa juu wa serikali


ya wanafunzi pamoja na ofisi ya mshauri wa wanafunzi kwa ushirikiano mkubwa
tuliokuwa nalo katika kufanikisha jambo hili

SEHEMU YA NNE.
CHANGAMOTO ZINAZOIKUMBA WIZARA.
Mheshimiwa Spika, Kama ilivyosehemu nyingine sehemu yeyote yenye mafanikio
haikosi changamoto, hivyo wizara ya kampasi na malazi inakumbana na
changamoto kadhaa katika utendaji wake. Miongoni mwa changamoto hizo ni
pamoja na;

i. Mlolongo mrefu wa utekelezaji katika uongozi wa chuo, hivyo kupelekea baadhi


ya vitu hasa matengenezo kutofanyika ndani ya wakati.
ii. Wanafunzi kutozingatia matangazo pindi wizara inapoyatoa.
iii. Wanafunzi kupuuza sharia, kanuni na taratibu za hostel.
iv. Ushirikiano hafifu kutoka kwa wanafunzi wenzetu.

SEHEMU YA TANO.
MWISHO.
Mheshimiwa Spika, Wizara inapenda kutoa shukrani za dhati kwa wale wote
wanaliohusika na wanaoendelea kutoa ushirikiano katika utendaji kazi wa wizara.
Kwa kipekee wizara ingependa kutambua mchango wa viongozi wenzetu kutoka
wizara mbalimbali ndani ya serikali ya wanafunzi pamoja na wawikilishi wa
madarasa (CRs) kwa ushirikiano wenu.

Kipekee kabisa wizara inathamini mchango kutoka katika uongozi wa juu wa


serikali ya wanafunzi. Wizara inawashukuru Mheshimiwa Rais, Mheshimiwa
Makamu wa Rais pamoja na Mheshimiwa Waziri mkuu kwa uongozi wao thabiti
na mzuri katika utendaji kazi wetu.

Shukrani zaidi tunazielekeza kwenye uongozi wa chuo kwa ushirikiano wao


wanaoendelea kutupatia,ofisi ya mshauri wa wanafunzi, ofisi ya majengo, ofisi ya
ulinzi na usalama pamoja na mwenyekiti wetu wa kamati ya kampasi na malazi
Mh.jackline mtei ,ofisi nyingine zote za chuo na wafanyakazi wake.

Mungu ibariki wizara ya kampasi na malazi, Mungu ibariki IFMSO,


Mungu ibariki IFM,Mungu ibariki TANZANIA.
ONE FOCUS ONE GOAL

Email: ministryofcampusifmso@gmail.com

Imeandaliwa na wizara

Waziri:Fred A.Buzika

Naibu waziri: Fauzia Maulidi

You might also like