You are on page 1of 2

RISALA YA WAHITIMU KIDATO CHA NNE KWA MGENI

RASMI NOVEMBA - 2015


Ndugu Mgeni Rasmi, wageni waalikwa, wazazi, walimu, wanafunzi wanaobaki shule
nyote mliohudhuria hafla hii, kwanza kabisa tunamshukuru Allah (s.w) kutujaalia afya
njema na kuifikia siku ya leo. Pia tunatoa shukrani za dhati kwa kuacha shughuli zenu
na kuja kujumuika nasi katika hafla hii ya kuhitimu kidato cha nne.
Ndugu Mgeni Rasmi
Walioko mbele yako ni wahitimu wa kidato cha nne ambao tulianza masomo mwaka
2012 tukiwa jumla ya wanafunzi 180 ambao kati ya hao wavulana walikuwa 75 na
wasichana walikuwa 105. Leo tunahitimu tukiwa wanafunzi 47 ambao wavulana ni 26
na wasichana ni 21, baadhi yao walishindwa kufika hapa tulipo kwa sababu mbali mbali
kama vile ukosefu wa ada, kuhama shule, kushindwa kufikia wastani wa shule na utovu
wa nidhamu.
Ndugu mgeni rasmi
Katika kipindi tulichoishi tulipokuwa hapa shuleni yafuatayo ni mafanikio tuliyoyapa;
1. Ufaulu mzuri kwa mitihani ya ndani na nje ya shule, hili linadhihirishwa kwa
kutazama takwimu ya mtihani wa mock kidato cha pili ambapo shule ilishika
nafasi ya nne kati ya shule zilizo shiriki ,na katika mtihani wa kidato cha pili
tulifanya mtihani jumla ya wanafunzi 86 na wote tulifaulu kuingia kidato cha
tatu.
2. Kusoma masomo ya sayansi kwa njia ya vitendo (Practical) na pia tumekua
wanafunzi wa kwanza kufanya mitihani yote ya sayansi kwa vitendo hapa
shuleni, hii ni kutokana na shule kujenga maabara na kununua vifaa mbali mbali
kama kemikali za kufanyia majaribio na viumbe vya kufanyia majaribio.
3. Kupatikana makazi (hostels) ya furaha kwa wanafunzi baada ya kuanzishwa kwa
bweni la wavulana na kuongezwa chumba cha bweni la wasichana ,hii
imetusaidia kujipatia muda wa kutosha wa kujisomea, kufanya majadiliano ya
sisi kwa sisi na kuwa karibu na waalimu kwa msaada zaidi.
4. Kujipatia elimu ya kujitegemea kwa kushiriki kikamilifu katika ufyatuaji wa
tofari katika eneo la Mtumba na tofari hizo kutumika katika maendeleo ya dini
yetu kwa kujengea misikiti na vituo vya elimu ikiwemo shule yetu.
1

Ndugu mgeni rasmi


Palipo na mafanikio hapakosi changamoto. Zifuatazo ni changamoto zilizo tukumba
katika maisha ya uanafunzi hapa shuleni;1. Upungufu wa vifaa na madawa ya kufanyia majaribio kwa vitendo,hali
iliyosababisha kutofanya mazoezi ya kutosha kwa ajili ya maandalizi ya mtihani
wa kidato cha nne.
2. Ukosefu wa wataalamu wa maabara (Laboratory technician) wa kusimamia
masomo ya sayansi kwa vitendo hali iliyosababisha kutumia wataalamu kutoka
nje ya shule.
3. Kutokamilika kwa jengo la maabara na kupelekea masomo yote ya sayansi kwa
vitendo kufanyikia katika chumba kimoja tu.
4. Ukosefu wa bwalo la kulia chakula kwa wanafunzi wa bweni hali
inayosababisha wanafunzi kulia chakula sehemu ya wazi. Hali hiyo husababisha
usumbufu wakati wa chakula hususani wakati wa mvua.
5. Kutokamilika kwa jengo la msikiti hali inayosababisha ugumu wa kutekeleza
ibada ya swala hasa wakati wa mvua na jua kali kwani swala hufanyikia eneo la
wazi.
6. Upungufu wa vitabu vya kiada na ziada kwa wanafunzi kujipatia maarifa
mbalimbali hali hii inapelekea kitabu kimoja kutumiwa na mwanafunzi zaidi ya
mmoja hivyo kusababisha wanafunzi kutegemea maarifa kutoka kwa walimu
badala ya kujisomea vitabu wenyewe.
Ndugu mgeni rasmi.
Ni matumaini yetu kuwa wewe na wote mliohudhuria hafla hii mtakua chachu ya
kuzitatua changamoto hizo ili kuchochea ufanisi zaidi. Tunawaombea kwa Allah [s.w]
kheri na baraka mrudipo nyumbani mfike salama.
Risala hii imeandaliwa na wahitimu wa kidato cha nne na kuwasilishwa na;
1. Hussein Hamisi Noboka.
2. Hassan Saidi Jumanne.

Wabillah tawfiq.
2

You might also like