You are on page 1of 7

Barua pepe: secondary-school@duce.ac.

tz
Simu: +255 22 2850095
Tovuti: www.udsm.ac.tz
Nukushi: +255 22 2850095
www.duce.ac.tz

……/……/2021

NDUGU………………………………..…………..………………………….…………………

YAH: MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA SHULE YA SEKONDARI CHANG’OMBE


ILIOPO WILAYA YA TEMEKE MKOA WA DAR ES SALAAM MWAKA 2020
1.0 UTANGULIZI
Napenda kukutarifu kwamba umechaguliwa kujiunga na Kidato cha KWANZA katika shule hii mwaka
2021

1.1 Mahali ilipo shule


Shule ya Sekondari Chang’ombe ipo ndani ya eneo la Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE)
katika Manispaa ya Temeke, Dar es salaam. Shule ipo upande wa kaskazini mwa Uwanja mpya wa
Taifa
Muhula wa kwanza wa masomo utaanza tarehe ………………….ambapo unatakiwa kuripoti shuleni
kuanzia tarehe …………… saa 2:00 asubuhi ili upate kusajiliwa na kupatiwa maelekezo mengine
muhimu kuhusu shule, ukiwa pamoja na Mzazi/Mlezi wako.

2.0 MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA


2.1 Sare za shule
a) Wavulana : Suruali nyeusi mbili, mashati meupe mawili ya mikono mifupi na tai mbili,
viatu vyeusi vya kamba na vyenye kisigino kifupi, pamoja na soksi nyeusi. Suruali iwe na
malinda manne mbele ( mawili kulia na mawili kushoto).
Kumbuka : Suruali za kubana (model), fupi na mlegezo hazitakubaliwa shuleni

b) Wasichana : sketi za bluu bahari mbili mshono wa malinda box mbele na nyuma,mashati meupe
mawili mikono mifupi na tai mbili, Viatu vyeusi vya ngozi vyenye kamba na soksi nyeupe.
Kumbuka : Sketi fupi za kubana, fupi na mlegezo hazitakubaliwa shuleni
*Hijab kwa wanafunzi wa Kiiislamu: Ushungi mweupe usio na mapambo na uvaliwe na shati jeupe la
mikono mirefu(nusu kanzu) na sketi ya bluu bahari ndefu yenye malinda boksi mbele na nyuma
1
2.2 Sare ya michezo
Sare ya michezo ni kwa kila mwanafunzi ( Mvulana na Msichana) ni Fulana mbili ( Kijani na Nyekundu) na
bukta mbili ( nyeupe na njano) pamoja na raba ya michezo

2.3 Vifaa vingine muhimu kwa wote


o Dictionary
o Begi la kubebea vitabu
o Madaftari makubwa 13
o Mathematical set

N:B Matumizi na mahitaji ya mwanafunzi yanamtegemea zaidi Mzazi /Mlezi.Ni imani yetu kuwa
utampa mwanao msaada wa kila aina ili aweze kusoma kwa umakini na kwa ufanisi

2
SHERIA NA KANUNI MUHIMU ZA SHULE
Shule hii inaendeshwa kwa mujibu wa Sheria ya Elimu Na- 25 ya mwaka 1978, na kama ilivyorekebishwa kwa
sheria Na. 10 ya mwaka 1995. Aidha inazingatia miongozo yote inayotolewa na Wizara ya Elimu na Mafunzo
ya Ufundi yenye dhamana ya Elimu chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI yenye jukumu la Usimamizi
na Uendeshaji Elimu.

Unatakiwa kuzingatia mambo ya msingi yafuatayo


a) Heshima kwa viongozi, wazazi, wafanyakazi wote, wanafunzi wengine na jamii kwa ujumla ni
jambo la lazima.
b) Mahudhurio mazuri katika kila shughuli ndani na nje ya shule ni muhimu.
c) Kuwahi katika kila shughuli za shule na nyingine utakazopewa
d) Kufahamu mipaka ya shule na kuzingatia kikamilifu maelekezo juu ya kuwepo ndani na nje ya
mipaka hiyo wakati wote wa uanafunzi wako katika shule hii.
e) Kutunza usafi wa mwili na mazingira ya shule
f) Kuvaa sare ya shule wakati wote unapotakiwa
g) Kuzingatia ratiba ya shule wakati wote; na
h) Kutunza mali ya umma

A: Mahudhurio
Kila mwanafunzi ni lazima afike shuleni asubuhi saa 12:30 na kufanya usafi wa mazingira na kuhudhuria
gwaride la ukaguzi wa usafi na kuchangamsha mwili.
1. Mwanafunzi yeyote haruhusiwi kuondoka (Kutoroka) katika eneo la shule bila kupata kibali/ruhusa
kutoka kwa mwalimu wa darasa au wa zamu. Aliyepata kibali ni sharti akionyeshe kwa mlinzi
getini.
2. Siyo ruhusa kwa mwanafunzi kukosa kufika shuleni bila kupata kibali.
Ruhusa itatolewa kwa sababu maalum tu na hata hivyo mzazi/mlezi
analazimika kufika kuomba ruhusa na kujieleza kimaandishi. Mwanafunzi akikosa zaidi ya siku
tatu mfululizo atalazimika kufika mbele ya kikao pamoja na mzazi/mlezi ajieleze. Ieleweke
kwamba ni mzazi/mlezi halisi na siyo wa bandia
3. Kila mwanafunzi ni lazima ahudhurie vipindi vyote vya darasani na shughuli za michezo na
uzalishaji mali atakavyotakiwa na ratiba bila kuchelewa.
4. Mwanafunzi ni lazima afanye mitihani na majaribio ya masomo yote anayosoma.

B: Tabia na Mwenendo
Kila mwanafunzi lazima awe na nidhamu ya hali ya juu kuwaheshimu wafanyakazi wote na wanajumuiya kwa
jumla. Mwanafunzi asiye na nidhamu atapoteza nafasi yake.

1. Mwanafunzi haruhusiwi kufanya yafuatayo:


a) Kuvaa Pete
b) Kunyoa nyusi
c) Kuvaa Hereni
d) Kupaka Hina na Rangi za Kucha
e) Kuwa na Kucha ndefu
f) Kusuka nywele
g) Kuweka dawa nywele.
h) Kunyoa kipara au mitindo
i) Kuvaa mlegezo wa Sketi au Suruali
j) Kuwa na ndevu
k) Kuvaa rozari au tasbihi
2. Makosa yafuatayo yatapelekea mwanafunzi kuadhibiwa na kuonywa;
a) Uchelewaji wa sehemu yoyote anapohitajika
b) Kutofanya kazi za usafi wa mazingira
3
c) Kutojali masomo na uzalishaji mali
Aidha, Mwanafunzi anazo nafasi mbili tu za kuonywa na baada ya hapo kikao kinachohusika
kitamchukulia hatua kali zaidi.
C: Makosa yanayoweza kumfukuzisha/kumsimamisha mwanafunzi bila ya kuonywa
a) Wizi
b) Uasherati na ushoga
c) Ubakaji
d) Ulevi na matumizi ya madawa ya kulevya kama vile Bangi, cocaine, mirungi, kubeli n.k
e) Kupigana au kupiga
f) Kuharibu kwa makusudi mali ya umma
g) Kudharau bendera ya Taifa
h) Kuwa mjamzito/kupata mimba
i) Kuoa au kuolewa
j) Kutoa mimba
k) Kugoma, kuchochea na kuongoza au kuvuruga amani na usalama wa shule au watu
l) Dharau,ukaidi,ubishi,utoro,uvivu,upigaji kelele,kukaa maeneo yasiyoruhusiwa
m) Kukataa adhabu kwa makusudi.
n) Kuwa na simu ya mkononi shuleni
D:Mambo mengine muhimu yanayopaswa kukamilishwa na kuwasilishwa shuleni wakati wa usajili.
a) Fomu ya Mzazi/Mlezi kukiri kukubaliana na sheria, kanuni na taratibu za shule pamoja na
maelekezo mengine yatakayotolewa shuleni. ( Fomu A)
b) Medical Examination form ambayo itajazwa na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Serikali, aidha fomu
hii itakabidhiwa kwa mkuu wa shule mara utakaporipoti shuleni kabla ya kuanza muhula wa
masomo.(Fomu B)
c) Fomu ya maelekezo binafsi kuhusu historia ya mwanafunzi na mkataba wa kutoshiriki katika
migomo, fujo na makosa mengine ya jinai.(Fomu C )
d) Nakala ya Cheti cha kuzaliwa,Cheti cha kumaliza Elimu ya Msingi na Passport Size 4 za rangi
na apige akiwa katika vazi la shule kama mwanafunzi.
N.B : Tafadhali soma kwa makini maelezo/maagizo hayo na kuyatekeleza kikamilifu.
Kauli mbiu yetu ni “ELIMU NI MAENDELEO”

Karibu Sana!
__________________
A.MANANIKA
MKUU WA SHULE

4
FOMU A

SHULE YA SEKONDARI YA MAZOEZI CHANG’OMBE

FOMU YA KUANDIKISHWA SHULENI

A. TAARIFA ZA MWANAFUNZI (ijazwe na mwanafunzi)

1. Jina kamili la mwanafunzi …………………………………………………... PICHA YA

2. Tarehe ya kuzaliwa …………………………………………………………. MWANAFUNZI

3. Mahali alipozaliwa ………………………………………….( wilaya/Mkoa)


4. Taifa ………………………………………………………………………….
5. Uraia ………………………………………………………………………….
6. Dini ……………………………………………………………………………
7. Shule alizosoma/aliyosoma kabla ya kuja shule ya Sekondari Chang’ombe

Jina la Shule ya Msingi Tarehe na mwaka alioanza Tarehe na mwaka aliomaliza


i
ii
iii
iv

Saini ya mwanafunzi …………….…… Tarehe ………….….…

B: TAARIFA YA MZAZI/MLEZI (Ijazwe na Mzazi/Mlezi)

1. Jina kamili la Mzazi/Mlezi ……………….…………………………..……………………………


2. Utaifa ……………………………..………………………………………
3. Uraia ……………………………………..……………………………….
4. Anuani ya DSM ………………………….…………………………….…. PICHA YA
………… ………………………………………………………………… MZAZI/MLEZI
5. Sehemu unayoishi ………………………….………………………..…….
6. Mtaa ………………………………………….…………………….……..
7. Namba ya nyumba ………………………..………….…………….……..
8. Simu: Nyumbani………….…..…………….……………………
Ofisini ………………..…..………….……………….…
Mkononi …………………………………….……(Ikibadilika toa taarifa)
Eleza kama mtoto ana matatizo yoyote ya kiafya ……………………………………..
……………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………..………………………………..

C: MAELEZO YA KIKAZI (Mzazi/Mlezi)


i. Jina la Mwajiri ………………………………………………………………………..
ii. Anuwani ………………………………………………………………………………..
iii. Kazi ya mzazi/Mlezi …………………………………………………………….……
iv. (Mfano,Karani,Mwalimu n.k)

Saini ya Mzazi/Mlezi ………………………… Tarehe…………………….

5
FOMU B

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA


CHANG’OMBE DEMONSTRATION SECONDARY SCHOOL

REQUEST FOR MEDICAL EXAMINATION


To be filled by Government Medical Officer and return to the HEAD OF SCHOOL CHANG’OMBE SECONDARY SCHOOL, P.
O. BOX. 2329, DAR ES SALAAM

To the Medical Officer


…………………………….
……………………………..
……………………………...

A: RE: …………………………………………………………………………………………………………
Please examine the above mentioned student. Comment on his/her fitness by responding to the problems below. Say Yes or No
to each problem and if yes then state:

………………….
Head of School

Date………………….

Please insert (v) in the boxes provided


i Hearing yes [ ] No [ ]

ii Speech yes [ ] No [ ]

iii Sight yes [ ] No [ ]

iv T.B. yes [ ] No [ ]

v B.P yes [ ] No [ ]

vi Diabetes yes [ ] No [ ]

vii Mental case yes [ ] No [ ]

viii Physical disability yes [ ] No [ ]

ix Any other
………………………………………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………

B: Recommend if the student is fit for studentship (i) Yes (ii) No


………………………………………………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………
C: Any other advice
………………………………………………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………

…………………………………
Name, Designation and Signature Date ………………… Stamp……………………..

6
FOMU C

FOMU YA KUKUBALI KUJIUNGA NA AHADI

MKUU WA SHULE,
SHULE YA SEKONDARI CHANG’OMBE,
S.L.P 2329,
DAR ES SALAAM.

TAMKO LA MWANAFUNZI

Mimi (Mwanafunzi) ……………………………………………………………………….. (Jina kamili)

Ninakubali nafasi niliyopewa kuingia kidato cha ……………......... Mwaka…………………………… katika


Shule ya Sekondari Chang’ombe.

Ninaahidi kwamba:

1. Nitatii sheria zote za shule kama nilivyozisoma


2. Nitaweka bidii katika masomo, kazi na shughuli zote za kishule.
3. Nitashiriki kikamilifu katika shughuli za uzalishaji mali, kuzalisha mali iliyo bora bila kushurutishwa.
4. Sitaitia hasara shule kwa kuharibu au kupoteza malighafi (raw materials)
5. Nitakuwa mwanafunzi mwenye nidhamu ya hali ya juu, mkakamavu na mwenye mwenendo safi wakati
wote hata nikiwa nje ya shule kwa madhumuni ya kuipa na kutunza sifa ya shule ya sekondari
Chang’ombe.

Saini ya Mwanafunzi …………………..……………. Tarehe …………………………

TAMKO LA MZAZI/MLEZI

Mimi ( Jina kamili la Mzazi/Mlezi) …………………………………………………………….

Mzazi/Mlezi wa Mwanafunzi …………………………………………………………………..

Naahidi kwamba

1. Nitampatia mtoto wangu mahitaji yote muhimu ya shule kama yalivyoelezwa katika maelekezo ya
kujiunga na shule
2. Nitakua tayari kutoa msaada wowote utakaohitajika (maoni,adhabu n.k) katika kumlea mtoto wangu
3. Nitamhimiza mtoto wangu kusoma kwa bidii, kufanya mazoezi ya masomo yake (Home work) na
kufuatilia maendeleo na tabia yake shuleni.
4. Mtoto wangu akiwa nyumbani nitamlea katika maadili mema anayostahili ili awe mfano mzuri shuleni
na katika jamii kwa ujumla.

Saini ya Mlezi/Mzazi …………………..………… Tarehe ………………………………

You might also like