Professional Documents
Culture Documents
MAFUNZO YA UALIMU
NA
UONGOZI WA SHULE YA AWALI NA MSINGI
2019/2020
Page | 1
NDUGU___________________________________
Wabillahit Tawfiiq.
………………………….
MKUU WA CHUO.
Page | 2
1. Utangulizi
Chuo cha Ualimu Kigogo ni kituo kinachotoa mafunzo ya ualimu na
uongozi wa shule ya Awali na Msingi.
Katika Chuo hiki maadili na elimu ni mambo yaliyopewa kipaumbele
kikubwa kabisa. Hii ni kutokana na ukweli kuwa Qur’an inatufahamisha
kuwa huwezi kusimamia jambo lolote kwa ufanisi sharti kwanza upate
elimu sahihi juu ya jambo hilo. Rejea Qur’an 2:31 na 96:1-5.
Kuhusu maadili, Qur’an inatufahamisha kuwa kwa mtu yeyote
anayetaraji malipo mema toka kwa Allah (sw) basi na aige mwenendo
wa Mtume Muhammad (s.a.w).
Misingi hii tuliyoainisha ndiyo kigezo kwa mwalimu anayeandaliwa
katika chuo hiki. Hii ni kwa sababu mwalimu ndiye wakala wa
mabadiliko yoyote ya maana katika jamii.
2. Lengo la Chuo
(i) Kuwaandaa walimu kwa kuwapatia elimu stahiki na kuwalea
kimaadili ili wakawe wasimamizi na walezi wa vijana katika suala la
elimu shuleni, vituo vya elimu na madrasa za aina zote katika eneo
lake la kazi. Huku wao wenyewe wakiwa wa kupigiwa mfano katika
jamii yetu hii ambayo maadili yamemomonyoka mno.
(ii) Kuwaandaa walimu watakao kuwa chachu ya mabadiliko katika
jamii ya waislamu na taifa kwa ujumla kwa kuwa na maadili na ari
ya kuitumikia dini na jamii kwa ujumla tukizingatia kuwa wengi wa
wanajamii hawakupata fursa ya kuyajua maadili ya dini yao.
(iii) Kuwaandaa walimu weledi watakaoweza kuanzisha,
kuendesha vituo vya elimu na kufundisha kwa ngazi ya awali na
msingi.
(iv) Kumwezesha mhitimu kuhifadhi juzuu moja kwa uchache.
(v) Malengo ya ujumla ni yale yapatikanayo kwa wahitimu wa
mafunzo ya ualimu ngazi ya cheti.
Page | 3
3. MASOMO YATOLEWAYO.
Masomo yanayofundishwa ni yale yote ya lazima yaliyoainishwa katika
mtaala wa serikali. Kulingana na malengo ya chuo mchanganuo wa
masomo yanayofundishwa ni
1. Ualimu
2. Vitendo vya awali
3. Masomo ya kufundishia shule za msingi
4. Uongozi
5. Daawa
6. Montessori
7. Ujasiriamali
8. Computer
9. Lugha
4. GHARAMA ZA MAFUNZO
Gharama za mafunzo ni nafuu. Mwanachuo wa kutwa atalipia ada shilingi
600,000 na mwanachuo wa bweni atalipia Tsh 1,200,000 na zitalipwa kwa
awamu nne,au awamu 12 kwa wale watakaokopeshwa na benki ya
kiislamu ya AMANA.Na gharama nyingine zimeainishwa kama jedwali
linavyoonesha hapo chini:-
MALIPO APRIL-JUNE JULY - AUG SEPT - OCT NOV-DEC
BWENI KUTWA BWENI KUTWA BWENI KUTWA BWENI KUTWA
ADA 300,000 150,000 300,000 150,000 300,000 150,000 300,000 150,000
B.T.P 50,000 50,000 050555 050555
BIMA YA AFYA 050,55 050,55
OASILUBMATIK 050555 050555
AAI I AI 050555 050555 050555 050555 050555 050555
OALITKLK
ABLMI ,050,55 6250,55 0050555 6550555 ,550555 6050555 0050555 6550555
N.B:
Malipo ya ada na mafunzo kwa vitendo (BTP) yanapaswa kufanyika
Benki kupitia Akaunti ya chuo na kuwasilisha Karatasi ya Malipo (Bank
Pay in Slip) kwa Mhasibu wa chuo.
Na malipo ya bima ya afya na kitambulisho yatafanyika chuoni
mwanachuo anapowasili. Kwa wanachuo ambao wana Bima ya
afya hawatowajibika kulipia bima ya afya(NHIF)
Page | 4
Kwa wanaosomeshwa na TESA watumie akaunti namba ya
(NMB) Jina la akaunti ni TESA mfuko wa elimu.
AKAUNTI YA MALIPO
BENKI JINA LA AKAUNTI NAMBA YA AKAUNTI
AMANA BANK CHUO CHA UALIMU KIGOGO 004120564370001
NMB BANK TESA MFUKO WA ELIMU 20310006554
5. MAHITAJI YA MWANACHUO
i. Vifaa
Wanafunzi wa Wanafunzi wa
KIKE KIUME
SN AINA YA KIFAA
BWENI KUTWA BWENI KUTWA
1 Seti ya vitabu vya maarifa ya uislamu darasa la watu wazima(7) √ √ √ √
2 Rimu 1 A4 √ √ √ √
3 Seti ya vitabu vya daawa (11) √ √ √ √
4 Nguo za kushindia zizingatie vigezo vya vazi la kiislam. √ X √ X
5 Nguo za kulalia √ X √ X
6 Mas’haf moja ya tafsiri (AL - FARSIY) √ √ √ √
7 Madaftari (Counter Book 2 quires) 20 √ √ √ √
8 Kalamu na penseli za kutosha √ √ √ √
9 Mkebe wa vifaa vya hisabati (Mathematical set) √ √ √ √
10 Saa ya mkononi √ √ √ √
11 Shuka na foronya TATU za rangi ya BLUE, PINKI NA NYEUPE √ X X X
12 Shuka na foronya TATU za rangi ya BLUE, PINKI NA KIJANI x X √ X
13 Godoro (fut 21/2 x 6) na mto √ X √ X
14 Ndoo ya kufulia √ X √ X
15 Sahani ya chuma yenye vyumba vya mboga, kijiko, kikombe √ X √ X
16 Sanduku la bati(Tranka) √ X √ X
17 Mkoba wa madaftari √ √ √ √
Page | 5
ii. MAVAZI YA WANACHUO
Kwa sasa hakutakuwa na sare rasmi za chuo. Mwanachuo atatakiwa
kuvaa vazi linalozingatia miiko na maadili ya kiislam na fani ya
ualimu.
Wanachuo wa kiume wanaruhusiwa kuvaa shati, T-SHIRT yenye kola
na suruali za vitambaa sio jinsi. Na Mwanachuo wa kike atatakiwa
kuvaa baibui na juba au mtandio mrefu unaovuka kiwiko cha mkono.
Mavazi yote yazingatie sifa zifuatazo;
a) Vazi lisibane,lisiwe la mpira, lisishikane na mwili.
b) Lisiwe na mapambo, Maandishi wala Picha
c) Lisioneshe (transparent)
d) Liwe ni vazi la watu wema kwa asli
e) Lisitiri mwili wote.
f) Mwili (kucha, uso, miguu n.k) usiwe na mapambo
Page | 7
(viii) Ni marufuku kwa Mwanachuo wa Jinsia yoyote kuvaa mapambo
wakati akiwa chuoni na akiwa nje ya chuo.
(ix) Ni marufuku wanachuo kufuga kucha, kupaka rangi za kucha,
rangi za mikono, rangi za midomo, kupaka hina, kunyoa nyusi,
kuvaa viatu vya kuchuchumia au vinavyotoa sauti, kuweka
nywele dawa au kutia rangi au kusuka rasta n.k
(x) Ni marufuku Mwanachuo kuchochea,kushawishi,kuhamasisha au
kushiriki mgomo kwa namna yoyote.
(xi) Mwanachuo asionekane katika vilabu vya pombe, nyumba za
kupangisha wageni (guest house), kumbi za dansi na sinema.
(xii) Kila Mwanachuo ni mlinzi wa mali za chuo, mali zake binafsi na
mali za wenzake. Mwanachuo atakayeharibu au kusababisha
uharibifu au upotevu au wizi wa mali ya chuo atachukuliwa hatua
kali ikiwa ni pamoja na kulipa
(xiii) Kuiba ni kosa kubwa, Mwanachuo atakayethibitika kuiba mali ya
chuo au ya mwenzake atachukuliwa hatua za kinidhamu ikiwa ni
pamoja na kulipa.Hivyo Mwanachuo atakapogundua wizi wa mali
chuo, au mali ya mwenzake atoe taarifa kwa uongozi husika mara
moja.
(xiv) Kila Mwanachuo awe msafi na ahakikishe anashiriki vyema Usafi
wa Mazingira ya chuo.
(xv) Kelele za aina zozote hazitaruhusiwa iwe darasani, koridoni,
ndani ya bweni au popote katika eneo la chuo iwe kwa
Mwanachuo mmoja au wengi (kundi).Rejea Qur’an 31:19
(xvi) Mwanachuo hatoruhusiwa kutoka nje ya eneo la chuo bila kibali
maalum cha maandishi.
(xvii) Kila Mwanachuo analazimika kushirikiana na wanachuo wenzake,
wakufunzi na wafanyakazi wengine katika wema na uchamungu
ili kufikia lengo la chuo. Rejea Qur’an 05:02
(xviii) Hairuhusiwi kwa Mwanachuo kuja chuoni na vifaa vya ‘electronic’
kama vile TV,Redio, Simu ya mkononi, line za simu, n.k
(xix) Kila Mwanachuo atalazimika Kuswali swala ya Tahajjud
(Qiyaamul-layl) kila usiku wa ijumaa kuamkia Jumamosi na usiku
wa Jumamosi kuamkia jumapili.
(xx) Kusema uongo,kuficha uovu wa aina yoyote au kuzusha ni kosa
kubwa kwa mwanachuo na hatua za kinidhamu zitachukuliwa
ikibainika mwanachuo amefanya hayo .
Page | 8
(xxi) Ni marufuku kwa wanachuo wa Jinsia tofauti kukaa faragha
wakiwa wawili hata kama ni ndugu wa damu. Pia si ruhusa
kufanya shughuli yoyote ikiwemo kazi za makundi au group
discussion kwa wanachuo wawili wa Jinsia tofauti.
Wabillah Tawfiiq.
MKUUWA CHUO.
Page | 9