You are on page 1of 1

GEITA ISLAMIC SECONDARY SCHOOL

S.L.P 334, GEITA-TANZANIA


TEL. No, 0786955221/0757342492/0718192138/0743619659.
Email: geitaislamicsecondary@gmail.com

Ndugu, Mzazi/Mlezi wa………………………………………………………


Uongozi wa shule ya sekondari ya Geita Islamic kwa kushirikiana na taasisi ya
ufadhili ya Tanzania Education Supporting Agency(TESA), unayofuraha kubwa
sana kukupongeza kuwa mwanao aliyemaliza Darasa la saba mwaka 2023 na
kupata ufaulu wa wastani/Daraja……….…, amechaguliwa kujiunga na shule yetu
ili aweze kuendelea na masomo yake ya elimu ya sekondari na kutimiza ndoto
zake na mzazi mwenye kiu ya kusomesha katika shule zenye ufaulu bora pamoja
na usimamizi wa taaluma na malezi mema baada ya kujiridhisha kuwa ana sifa za
kuendelea na masomo hayo. Hii itamwezesha mwanao kupata muda mwingi zaidi
wa kujisomea na kusimamiwa zaidi ili kupelekea kupata ufaulu mzuri zaidi kwani
shule yetu haina msongamano wa wanafunzi wengi hivyo ni rahisi kumfuatilia
mwanafunzi kulingana na uwezo wake.

Hivyo, mwanao ataendelea na masomo yake ya sekondari akiwa anafadiliwaa na


mfuko wa TESA ambao utamlipia ADA nzima kila mwaka na mzazi utachangia
gharama ndogo kwa ajili ya chakula na mchango wa shule.

Pia kuna wanafunzi watakaochaguliwa kwenda katika shule zetu nyingine kama
vile:- Ibanda Islamic iliyopo Mwanza mjini, Ali Hassan Mwinyi sekondari iliyopo
Tabora mjini,Hijra na Jamuhuri sekondari zilizopo Dodoma mjini, Ilala Islamic
sekondari iliyopo Dar es salaam, Arusha Girls iliyopo Arusha na nyingine nyingi
ili wapate elimu bora na malezi bora .

Kwa maelezo zaidi kuhusu utaratibu wa kujiunga na shule sambamba na kujaza


fomu za ufadhili na shule, fika shuleni Geita Islamic au Ofisi yoyote ya TESA
iliyopo mkoani kwako au wasiliana nasi kupitia simu nambari
0757342492 /0786955221/0718192138

KUMBUKA:Shule ipo Geita Mjini barabara ya Bugomora mtaa wa


MWATULOLE karibia na kanisa la RC. Shule ya Bweni na Kutwa, inachukua
wanafunzi jinsia zote(wavulana na wasichana) na DINI zote.

Nakutakia maandalizi mema na mungu akutanguile


Wako katika malezi
……………………………….
Mkuu wa shule.

You might also like