You are on page 1of 3

FATNA MNUNKA

S. L. P 5000
DAR-ES-SALAAM
21. 01. 2022
MKUU WA SHULE
SHULE YA SEKONDARI MINAZI MIREFU
S. L. P 18195
DAR-ES-SALAAM
Ndugu,
YAH: OMBI LA NAFASI YA MWALIMU WA SOMO LA KISWAHILI
Husika na kichwa cha habari hapo juu.

Nachukua nafasi hii kuwasilisha barua yangu mezani kwako baada ya kuvutiwa na tangazo la
shule yako kuhitaji mwalimu Kiswahili katika gazeti la Mwananchi lililotoka tarehe
10/01/2022 lenye kumbukumbu namba MW202295749.

Mimi ni mhitimu wa shahada ya kwanza ya elimu ya watu wazima na nimejikita zaidi katika
somo la Kiswahili. Nina ujuzi, maarifa na umahiri wa hali ya juu katika kufundisha somo hilo.
Nimefundisha katika shule kadha wa kadha na kuwajenga wanafunzi kifikra, kimtazamo na
kimatamanio juu ya somo la Kiswahili kitu kilichochochea ufaulu mkubwa katika shule zote
zilizofanikiwa kupita.

Iwapo nikipata nafasi ya kuwa mwalimu wa Kiswahili katika taasisi hii, nitahakikisha
wanafunzi wanakuwa na ari ya kufanya vizuri katika somo hilo, situ kiwilaya, bali kitaifa.
Nitatumia maarifa na uzoefu nilionao kuandaa, kufundisha, kuhamasisha na kuunganisha
wanafunzi wa somo la Kiswahili na kuhakikisha wanashirikiana vya kutosha katika
kubadilishana maarifa na ujuzi walionao na kuinua vipawa vyao katika Kiswahili.

Wasifu wangu wa kimasomo na uzoefu kazini nimeuambatanisha katika barua hii. Natumaini
ombi langu litapewa kipaombele na litakubaliwa.

Wako Mwaminifu katika Kazi


F. S. M
Fatna Mnunka
Mwombaji

1
WASIFU WA FATNA S. MNUNKA

FATNA S. MNUNKA
Anuani: S. L. P 5000
Dar es salaam, Tanzania.
Namba ya simu: 0657451751/0764741044
E-mail: fatnamnunka@yahoo.com

TAARIFA BINAFSI
Tarehe ya kuzaliwa: 12 Disemba, 1989
Mahali alipozaliwa: Kagera, Tanzania
Utaifa: Mtanzania
Jinsi: Kike
Ndoa: Ameolewa
Dini: Muislamu
Lugha: Kiswahili na Kiingereza

ELIMU
MWAKA CHETI TAASISI

2021-2022 Shahada ya Elimu ya Watu Wazima Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima


2019-2020 Stashahada ya Elimu ya Watu Wazima Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima

2007-2008 Astashahada ya Elimu Chuo cha Ualimu Vikindu

2003-2006 Cheti cha Elimu ya Sekondari Bariadi Sekondari

1996-2002 Cheti cha Elimu ya Msingi Shule ya Msingi Mlimani

UZOEFU KAZINI
2009-2012: Mwalimu wa Kiswahili na Maarifa ya Jamii katika shule ya msingi Mwakipesile.
Kazi na Majukumu;
✓ Kuchambua muhtasari wa somo na kuandika azimio la kazi.
✓ Kuandika andalio la masomo, zana za kufundishia pamoja na nukuu zote za masomo
✓ Kuingia darasani kufundisha na kuongoza wanafunzi ipasavyo katika masomo hayo
✓ Kusimamia majukumu mengine yasiyo ya kitaaluma kama vile usafi wa mazingira, kuandika
takwimu, kuongoza vipindi vya dini na michezo.
✓ Kuhudhuria warsha na semina mbalimbali za walimu.

2
2013-2015: Mwalimu katika shule ya Msingi Kalulu kwa masomo ya Kiswahili, Uraia na Historia.
Kazi na Majukumu;
✓ Kuchakata muhtasari, kuandika azimio la kazi pamoja na andalio la somo.
✓ Kuandaa zama za kufundishia na kuandika nukuu za masomo yote.
✓ Kufundisha na kuongoza wanafunzi kujifunza masomo hayo kwa weledi wa hali ya juu.
✓ Kuwaongoza na kuwashauri wanafunzi juu ya mambo kadha wa kadha ya kijamii.
✓ Kuratibu, kusimamia na kuhakikisha shughuli zote zisizo za kitaaluma zinafanyika ipasavyo.
✓ Kukutana na wazazi wa wanafunzi na kuzungumza nao juu ya maendeleo ya watoto wao
kitaaluma.
2016-2018: Mwalimu katika shule ya msingi Azimio kwa somo la Kiswahili pekee.
Kazi na Majukumu;
✓ Kuchakata muhtasari wa somo na kuandika azimio la kazi kwa mwaka mzima.
✓ Kuandaa zana za kufundishia, kuandika nukuu za somo na kuandika andalio la somo kwa kila
kipindi.
✓ Kuongoza wanafunzi kujifunza somo la Kiswahili kwa kufuata mada pamoja na andalio la
somo linavyoelekeza.
✓ Kusimamia nidhamu za wanafunzi kama mwalimu wa nidhamu wa shule.
✓ Kukaa vikao na wazazi na kujadiliana namna bora ya kuhakikisha tabia za watoto wao ni
nzuri na zinazofaa kuigwa na jamii.
✓ Kushirikia katika usimamiaji na usahihishaji wa mitihani ya kitaifa hususani somo la
Kiswahili.
MAPENZI
Ninapenda kuangalia tamthiliya, kusikiliza na kucheza muziki, kusoma vitabu vya fasihi na kuandika
kazi mbalimbali za fasihi.
UZOEFU, MAARIFA NA UJUZI MWINGINE
❖ Matumizi ya kawaida ya kompyuta
❖ Ujuzi katika kuratibu na kusimamia klabu ya wanafunzi ya upigaji vita rushwa
❖ Uongozi katika nyanza mbalimbali hususani ni kusimamia nidhamu ya wanafunzi
❖ Utunzi na uandishi wa kazi mbalimbali za fasihi.

WADHAMINI
FRANK NSARO LILIAN MALIMA
Mkuu wa Shule ya Msingi Kalulu Mratibu Elimu Idara ya Elimu TAKUKURU
Kazi: Mwalimu Kazi: Mratibu Elimu
Namba ya Simu: 0710000000 Namba ya Simu: 0710000001

UTHIBITISHO
Mimi Fatna Mnunka nathibitisha kwamba, maelezo yote niliyotoa katika wasifu huu ni sahihi kabisa
na endapo kuna udanganyifu wa aina yoyote basi sheria ichukue mkono wake ipasavyo.

You might also like