Professional Documents
Culture Documents
Hivyo nadharia ni sayansi au sanaa inayohusika na kanuni za kijumla ambazo zinatumiwa katika
uchunguzi wa jambo au kitu Fulani.
Athari za makundi rika yasiyofaa, katika kitabu cha kilio chetu mwandishi amejaribu kuonesha
namna makundi rika yanavyosababisha matatizo mbali mbali na kuwafanya vijana kujiingiza
katika masuala ya ngono na uvutaji bangi badala ya kusoma kwa bidii ili kufikia malengo
yao.Mfano mwandishi ameonesha wahusika kama vile Joti na marafiki zake akina
Jumbe,Mwarami na Choggo kama kundi lisilofaa kwa sababu badala ya kusoma wanajiingiza
katika kuangalia picha za X vilevile wanashauriana kujiingiza katika mapenzi wakiwa bado
wadogo.Mfano katika uk20, Jumbe anasema leo si ndio siku ya picha ya x?
umesahau?.Mwishoni Joti anapata UKIMWI na Suzi kupata ujauzito.Kutokana na nadharia ya
uhalisia suala kama hili lipo katika jamii kwani wapo vijana ambao ni wanafunzi na
wanajihusisha katika masuala ya ngono na matumizi ya bangi kitu ambacho kinapelekea
matatizo katika masomo yao na jamii kwa ujumla kuathirika.
Umuhimu wa elimu ya jinsia, katika kitabu cha kilio chetu,mwandishi ameeleza juu ya
umuhimu wa kutoa elimu ya jinsia,hasa pale mwandishi alipo watumia wahusika kama Baba
Anna na Mjomba kama mfano wa kuigwa katika jamii ambapo wanaona kumpatia mtoto elimu
ya jinsia akiwa bado mdogo inamsaidia kuepukana na matatizo katika ukuaji wake.Kwa mfano
katika (uk15), Baba Anna anasema mimi bwana nitaendelea kusisitiza juu ya elimu hii watoto
wajazwe elimu.Pia wahusika kama Mama Suzi,Baba Joti wanawakilisha wahusika wanaofikiri
kuwa kumpatia mtoto elimu ya jinsia akiwa bado mdogo ni kumpotosha au kumharibu
1
mtoto.Mfano katika (uk11), Mama Suzi anasema huko si ndiko kunifundishia mwanangu
umalaya?.Hivyo basi kutokana na nadharia ya uhalisia tunaona kuwa kuna wazazi ambao bado
wanaona kuwa ,kuwapatia watoto elimu ya jinsia ni kupoteza muda na ni kuwafundisha umalaya
na tabia mbaya kama alivyosema Mama Suzi ,hali hii ndiyo hupelekea watoto au vijana wengi
kujiingiza katika mambo yasiyofaa na kuharibikiwa kabisa ,kutokana na wazazi kutokuwa na
muda wa kukaa na wanawe na kuwaasa juu ya mambo yanayoendelea katika jamii.
Suala la imani potofu, imani potofu ni uhalisia unaojitokeza katika tamthiliya hii ya kilio chetu
pale mwandishi anapomtumia mhusika Jirani alipokuwa anashauri kuwa Joti apelekwe kwa
mganga wa jadi ambaye ni Chongo kwa ajili ya kupata matibabu pindi anapoumwa.Mfano Jirani
anaposema Hivyo mie naonelea kungefanyika jitihada niwapelekeni kwa fundi mmoja
anaitwa Chongo... Mambo haya katika nadharia ya uhalisia ,yanadhihirisha uhalisia wa mambo
yanayo fanyika katika jamii na uhalisia wake,kwani katika jamii zetu suala la imani potofu
linaonekana waziwazi pale watu wanapougua hukimbilia kwa waganga wa jadi badala ya
kwenda hospitalini kwa ajili ya kupata matibabu.
Suala la umasikini, suala hili ni uhalisia unaojitokeza katika tamthiliya ya kilio chetu ambapo
mwandishi anamtumia mhusika Mama Suzi kuonesha uhalisia wa umasikini,hasa pale ambapo
analalamika kuwa anaungua mikono wakati wa kupika vitumbua ili aweze kupata pesa za
kumsomesha mwanae Suzi ambaye anaonekana kushawishika na kujiingiza katika suala la
mapenzi katika umri mdogo,ambapo matokeo yake anaambulia kupata ujauzito.Hivyo kutokana
na nadharia ya uhalisia tunaona katika jamii zetu wazazi hutafuta pesa kwa shida ili waweze
kuwasomesha watoto wao,lakini watoto hao hao hujiingiza katika suala la mapenzi kutokana na
vishawishi hata bila kujali hali ngumu wanayopitia wazazi wao katika kuhakikisha wasome na
kufikia malengo yao ya baadae.
2
Suala la usaliti, ni uhalisia mwingine unaojitokeza katika tamthiliya hii,kwa mfano mwandishi
anaonesha suala la usaliti kwa kumtumia Baba Joti ambaye anamsaliti mke wake na kujihusisha
kimapenzi na mwanamke mwingine,pia Joti anamsaliti Suzi kwa kuwa na wasichana wengine
kama vile;Gelda,Sikujua na Yoranda, mwandishi analithibitisha suala hili akimtumia Suzi pale
anaposema ndio maana mie nilikua nakataa Joti,nishambiwa kuwa una wasichana wengi
shuleni na mtaani kwetu(uk.21),hivyo katika jamii zetu uhalisia wa usaliti upo kwani tunaona
usaliti unapotokea baina ya wanandoa,wapenzi,marafiki na hata baina ya majirani.
Hivyo basi kutokana na matatizo mbali mbali yanayojitokeza katika jamii kama
tulivyoona,jamii haina budi kutoa elimu ya jinsia kwa watoto kuzingatia malezi bora kwa watoto
na kuachana na mila potofu kama vile kuamini waganga wa jadi zaidi kuliko mdaktari.Mbali na
hili,wazazi wanatakiwa kuwa nafasi ya kwanza katika kurekebisha tabia za watoto,kwani mzazi
ndiye mwalimu wa kwanza katika jamii.
3
MAREJELEO
4
KITIVO : ELIMU.
IDARA : LUGHA NA ISIMU.
JINA LA KOZI : NADHARIA YA UHAKIKI NA MAENDELEO YA FASIHI YA
KISWAHII.
MSIMBO : SW125.
JINA LA MHADHILI : MUKAMA SHUKURU.
MWAKA WA MASOMO: MWAKA WA KWANZA, 2016/2017.
AINA YA KAZI : KAZI YA KIKUNDI.
MKONDO : BAED 1 A.
KUNDI : NAMBA 04.
NAMBA MAJINA NAMBA ZA USAJILI SAHIHI