You are on page 1of 14

Dhana ya fasihi ya watoto

-fasihi ya watoto ni ile ambayo imetengewa watoto kulingana na viwangi vyao kiumri. Kwa mujibu wa
Davis 1973 fasihi ya watoto humulika tajriba za watoto na mazingira Yao. Kupitia tanzu za fasihi ya
watoto, mtoto huweza kujigundukia mambo mengi yanayomhusu yy mwenyewe au watu wengine
wanaomzingira. Hivyo basi fasihi ya watoto humwezesha mtoto kupata tajriba mbalimbali. Baadhi ya
tajriba hizi ni pamoja na

1. Kujenga ushirikiano miongoni kwa watoto

2. Kumwezesha mtoto kuuelewa ulimwengu anamoishi

3. Kukuza lugha ya kujieleza kama mwanajamii halisi

4. Humwezesha kuuelewa utamaduni na desturi za jamii yake

5. Kumpa mtoto fursa ya kujiburudisha na kuepukana na mambo ashy yahitaji katika umri wake

wa kitoto

6. Hugundua dhamana za kijamii ambazi hujenga msingi Bora wa kimaadili katika ulimwengu wa kisasa.

7. Hujenga upendonkwa mazingira na nchi yake pamoja na uhuru wa kimawazo

8. Kupata fursa ya kuelewa na kukubali matatizo yanayowakumba wengine

9. Kujielewa yy mwenyewe na matatizo yake.

10. Kupata nafasi ya kushuhufia matukio na mawazo ya mtu mwingine.

1.2 MTOTO NI NANI.

Kwa mujibu wa UNICEF mtoto ni binadamu aliye na until wa miaka kumi na mitano kurudi chini.
TUCKERS1981 anasema kuwa watoto ni binadamu wa umri wa chekechea Hadi umri wa kubaleghe. Huu
ni kwa muktadha wa kifasihi. Kutokana na maono hayo tunagundua kwamba watoto wa umri mmoja
hubaleghe kwa wakati tofauti tofauti.

Fasihi yaweza kuwa ya kuchapishwa vitabuni au ile ya kusimuliwa kulingana na umri ya watoto.
Wataalam wengi wamchunguza na kupata kuwa mtoto ni yeyote yule aliye chini ya Miaka kumi na
minane na katika kozi hii tutaichukulia hiyo. Kwa hivyo fasihi ya watoto haihudu kazi za watoto tu mbali
kazi za kisanaa zinazoambatana na maono na kiwango Cha kiakili Cha mtoto. Kama fasihi ya watu
wazima, fasihi ya watoto ni zao LA jamii na watoto ni sehemu muhimu ya Jamii. Kwa hivyo fasihi ya
watoto inastahili kuwapa watoto nafasi nzuri ya kujifunza mambo mengi yanayomhusu maisha ya kila
siku ya mwanajamii.

Tunapozungumzia fasihi ya watoto mambo mawili hujitokeza.


1, kazi za kisanaa zilizoandaliwa watoto kama hadhira. Kazi hizi zaweza kuwa ziliandikwa na kutungwa na
watu wazima au kutungwa na kuanfikwa na watoto wenyewe. Ni muhimu kutilia maanani kuwa fasihi ya
watoto ni tofauti na watu wazima na kinachotofautisha ni:

1.hadhira lengwa na tajriba za hidhira hiyo

2.kiwango Cha hadhira yenyewe

Katika tajriba za watoto mandhari Yao ni shuleni, nyumbani, michezoni nk.Tajriba za watu wazima
huhusidga matanga, vita, siasa, sayansi na tecknolojia. Kwa ujumka tofauti ni kwamba za watoto
huzingatia kazi na uwezo wa watoto.

DHIMA YA FASIHI YA WATOTO

1. Hupitisha muda. Watoto wakiwa nyumbani au mahali popote pale baada ya kumaliza shughuli zao
huweza kupitisha muda kwa kujihusisha na mambo mbalimbali kama vile kuimba,,kuhadithiana, kusoma
vitabu vya hadithi n.k.

2. Huelimisha. Watoto huwezi kupata mafunzo mbalimbali kutokana na michezo wanayojihusisha nayo
kama vile chamama,,chababa,,miongoni mwa mingine. Hujifunza majukumu mbalimbali ya nyumbani
kupitia micheza kama hiyo.

3. Hupitisha ujumbe. Katika kazi za fasihi Kuna ujumbe fulani uliokusudiwa na mwandishi alipokuwa
akiandika kazi za fasihi simulizi. Kwa mfano katika nyimbo za watoto Kuna ujumbe ambao unanuiwa
kueleweka na mwimbaji wa fasihi hiyo.

4. Hupanua mawazo na uwezo wa kufikiria. Kwa mfano ili mchezo fulani uwezo kufanikishea na watoto
basi lazima watoto hao waweze kufikiria vema ili matukio ya mchezo huo yaweza kufuatana veme ili
mchezo huo uwe wenye kutiririka na kueleweka vema.

5. Hurilidhisha tamaduni na maadili ya kijamii. Kupitia fasihi ya watoto tamaduni mbalimbali za kijamii
hujidhirisha na kwa hivyo WATOTO hao huwa na uwezo wa kutambua kuwa ni mambo yepi ambayo
yanakubalika katika jamii na ni yepi ambayo hayakubaliki katika jamii.

6. Huburudisha. Kama ilivyo katika FASIHI byabwatu wazima , fasihi ya watoto have chukua jukumu la
kuburudidha hadhira husika wakati ambapo wanaendeleza utendaji wa fasihi ya watoto.

7. Huondoa msongo wa watoto. Ili watoto wasiwe na mawazo mengi wanapojipata kuwa wamechoka
sana basi hujishughulisha na michezo tofauti tofauti ili mawazo ambayo yanamsonga akilini mwake
yaweze kuondoka na kumwacha mtoto huyo akiwa vema.

8. Huchachawisha ubunifu. Ili mtoto aje na mchezo mwema are tendo zuri la kuburudidha hadhira yake
basi watoto hulazimika kuwa wabuniwa wa Hali ya juu kwa kuongeza mambo Yao kwa njia Moja au
nyingine.
9. Humuezesha mtoto kujieleza pamoja na wale wanaomzingira. Watoto hujielewa na huwaelewa
wengine katika mandhari Yao na kwa hivyo wanaouwezo wa kujieleza miongoni mwa wenzake

10. Huonya. Kupitia kwa fasihi ya watoto Kuna matukio mbalimbali ambayo hutumika kama vifaa vya
kuwaonya watoto dhidi ya kujihusisha na vitu visivyo vizuri

MAMBO YA KUZINGATIA KATIKA UTEUZI WA FASIHI YA WATOTO

Kazi za watoto

1. Ziwe za kusisimua na rahisi za kueleweka

2. Urefu na ufupi hutegemea kiwango Cha watoto

3. Sentensi ziwe fupifupi,,ploti sahili na wenye uradidi mwingi

4. Zihusu ualisia kuliko udhahania.

5. Vishighulikie maswala ya kimaadili katika maisha ya watoto

6. Ziwe na tajriba zinazoweza kuwasaidia kupata mahitaji yao

7. Ziwe na hadithi na nyimbo kwa wingi kwa sababu zunawatambulisha kuwa na utu wema.

8. Ziwe na wahusika wema wa kuigwa.

N/B. Kupitia vitabu vya fasihi ya watoto, watoto wanaweza kijihamasisha na utu wazima na kuandaliwa
kwa maisha ya baadae. Kazi hizi humwezesha mtoto kujitegemea badala ya kutegemea wengine. Kwa
mfano katika hadithi za kale, tunampata msichana mdogo anayetokroka nyumbani kwao kwa sababu ya
shida zitokanazo na mama wa kambo. Anarnda safari ya mbali na mwisho kujipata malkia katika nchi
nyingine.

Michezo ya watoto hutumiwa katika fasihi kulinganishwa na mambo ya kisasa katika ulimwengu wa
kitoto wa kisasa. Kupitia kwa Hadithi nyingi watoto huamini kuwa wakifanya jambo jema watatuzwa na
wakifanya kosa wataadhibiwa. Hivyi basi kazi za watoto ziwe na wahusika wanaoweza kuigwa.

NADHARIA ZA FASIHI YA WATOTO

NADHARIA YA KIMUUNDO:
Iliasisiwa na kuhusishwa na wanaisimi wa shule ya Praque.(SIP). Kuzuka kwa shule ya isimu ya Prague
kulihusiana kea kiasi kikubwa na urasimilu hasaa kikundi kimoja Cha wanaisimi wa Moscow.

Hata hivyo wanaisimi hao walohusisha umuundo na Fredinaed De sossoure na Edmund Husserl.
Walichunguza muundo wa ndani wa kazi za kifasihi na hasa za kishairi. Karen ika hatua za mwanzo,
wahakiki kwa mfano Roman Jacobson na wengine walivutiwa na kiwango Cha sauti katika ushairi. Wao
walichunguza suala LA shina katika ushairi wa Ki-Zeshi.

Baadae wahakiki hao walichunguza Sanaa wakilinganisha na Hali za kijamii. Baina ya Miaka ya 1938 na
1948 harakati za SIP ziliathiriwa na uvamizi wa ujerumani kwa nchi ya Zeshislovakia.

Uvamizi huu uliwalazimu baadhi ya wahakiki kama vile Roman Jacobson na Wellek kutoka Marekani.
Ferdinand alitofautisha kati ya matamashibya kiusemi na mfumo wa Mpana wa lugha . Wahakiki hao
wanaamini kuwa lugha ya just fasihi ni tofauti na lugha ya kawaida. Mkabala wa KImuundo unashikilia
kuwa maana huundwa katika lugha na kwa hivyo inafumbatwa na kuahidiwa na msemaji.

Ferdinand De sessure alieleza lugha kama mfumo wa ishara amvazi huunganika pamoja na kuunda
mjufu wa ishara. Kila ishara huwa na sehemu mbili kuu. Sehemu ya kwanza ni kiashiria na sehemu ya pili
ni kiashiriwa.

Kikombe√√☕kiashiriwa

Kiashiria

NADHARIA YA UFEMINISTI:.

Tangu jadi mkabala wa kiumeni umetawala jamii nyingi. Jambo hili limesababisha kupuuzwa kwa Haki
za wanawake kama viumbe kamili. Kauli za kidini na kitamaduni zimetumiwa kishadidia uwezo wa kiume
dhidi ya ule wa like. Hii ni NADHARIA inayokinzana na mkabala wa kiumeni. Ni kinyuma Cha ubabedume.
Kuna mielekeo mikali hasaa kutoka Merekani kwamba mwanamume ni adui ya mwanamke na kamwe
hawezi kishiriki katika ukombozi wa mwanamke. Mielekeo hii inaunga mkono ndoa za jinsia Moja.

Hata hivyo wanaume walio na itikadi za kimaendeleo wanaweza kuchangia katika ukombozi wa
wanawake. Pia wanawake walio na mtazamo wa kijadi wanaweza kushiriki katika kiwakandamiza
wanawake wenzao. UFEMINISTI ulishika kazi katika miaka ya themanini. NADHARIA hii inuia yafuatayo:

1. Kutumia FASIHI kueleza kwa utakinifu Hali inayomkumba mwanamke

2. Kupigania jamii mpya yenye msingi katika amali za kibinadamu bila kujali maumbile

3. Kuhamasisha watungaji wa kazi za Sanaa ili wawe na wahusika wa kike ambao ni vielelezo wenye
uwezo, nguvu na WA kuigwa.

4. Hujuza na kuendeleza hisia za unoja kwa wanawake kama kundi linalodhulumiwa.


5. Kuzindua mwamko miongoni mwa wana wa kike ili wawe watendaji Zaid ya washitiki katika harakati
za ukombozi wao.

6. Kuvumbua na kuweka waziwazi kazi za snaa zilizotung a na wanawake.

N/B. Licha ya kuwa wnafasihi wengi wamewachora wanawake kama viumbe duni, Kuna wanafadihi
kadha wa kadha wa kiafrika ambao wamempa mwanamke nafasi ya kipekee. Miongoni mwaoni Kidhaka
Mberia, Al Amin Mazrui, Said Ahmed Muhamed, Mulokozi na Penina Mulama.

NADHARIA YA KIMAPINDUZI:

NADHARIA ya KIMAPINDUZI Iliasisiwa na John Dewey. NADHARIA hii inafungamana na Imani kwamba
ijapokuwa mwanadamu hazakowi akiwa mjuzi wa mambo, uwezo wa kujua yaliyomo katika mazingira
yake huwa nao kuanzia tumboni mwa make. Hivyo basi mtu azaliwapo tu ubongo wake unaanza kufanya
kazi ya kuyachambua na kuyachanganua yote anayoyaona na kuyasikia. Huyapanga hayo yote akilini
mwake katika mpangilio ulio na maana.

Iwapo mambo yatabadilika, basi ataubafilisha mpangilio wake wa awali na kuunda mpya. Hali hii ya
kupanga upya utaendelea Hadi Pale ambapo kinachopangwa kitapata ruwaza yenye kueleweka yaani
kuingia akilini. Katika mfumo huu, hakuna elimu iliyokamilika. Mtu hujifunza tangu anapozaliwa Hadi
pale atakapoaga dunia.uhimi zaidi no nmtu huweza kibashiri yanoyoweza kutokea siku za usoni
kutokana na ujuzi wake wa matendo ya binadamu wa Rika lake na waliomtangukia ulimwenguni. Hii
hutokana na uwezo wake wa kulingalisha vitushi katika mazingira yake finyu na Yale mapana ya
ulimwengu mzima. Msingi wa NADHARIA hii ni kwamba mtu hujifunza kupitia ugunduzi au uvumbuzi.

UCHAMBUZI WA KAZI ZA WATOTO:

MTINDO WA UANDISHI:

Kuhusu namna lugha inavyotuniea katika muktadha fulani na mtu fulani na mwenye Nia fulani. Suala LA
MTINDO ni muhimu sana katika fasihi ya watoto. MTINDO uoane na Hadith pamoja na maudhui. Ili
kuwezesha mawasiliano na maelewano kwa urahisi, mtindo uwe sahihi. Watoto hupendelea mtindo
wenye asilimia kubwa ya maneno ya kuwasiliana Moja kwa Moja na yenye msamiati mwepesi.

PLOTI:

Ni mtiririrko wa mawazo au vitushi katika fasihi ya watoto. PLOTI huipa hadithi maana na lengo.
Husisitiza mambo muhimi ambayo mwandishi angependa msomaji apate. PLOTI huwasilisha
maandishiniwa msomaji. PLOTI nzuri humwezesha mwandishi kupitisha maudhui yake kwa urahisi.
Kupitia kwa ploti, watoto hupata maadili kupitia wahusika na vitendo vyao.
Ploti ni tofauti na hadithi kwa sababu hadithi huuliza swali ni nini kilichofuata na ploti huhitaki kujua ni
kwa nini kilifuata.

WAHUSIKA:

Wahusika ni wale ambao hutenda mambo kimantiki kuanzia mwanzo Hadi mwisho wa Hadithi.
Uzuri wa wahusika uhalisia na utepetevu wao hutegemea uwezo wa mwandishi. Jambo hili ni muhimu
kwani huonyesha watoto Hali ya kihalisia. Watoto wapewe wahusiy wanaoweza kuigwa ili kukuza
maadili mema. Wahusika waonyeshe Hali ya kila siku kwani yawe mambo ya kila siku ambayo
wanayafahamu kulingana na mazingira Yao ili waweze kulingalisha Hali hizo mbili. Mhusika mkuu apewe
tatizoi Kisha kitendo kianzie hapo.

Wahusika wawe mashujaa wenye kukumbana na visiki maishani na mwisho kuchorea washindi. Pale
ambapo shujaa anapewa tatizo kubwa zaidi, wahusika wengine wawe watu wazima ili uhalisia uonekane
kupitia wao kumwezesha mhusika mkuu kuutatua tatizo. Muonoulimwengu wa watoto utiliwe maanani.
Huyu shujaa anapopewa majukumu kama mtoto, huamini kuwa matendo mema huzawadiea na mabaya
huadhibiwa.

TAMATI ZA KAZI ZA WATOTO

Mwisho wa kazi a watoto unastahiki kuwa wazi Ila usiwe wa taharuki. Kila mhusika ashughulikiwe
mwishoni mwa hadithi ili asiachwe akielea. Kila mhusika apewe haki mwishoni mwa hadithi

USEMEZANO KATIKA KAZI ZA WATOTO

Ni Hali ya kutumia mazungumzo katika kazi za watoto. Mara nyingi mbinu hii hutumika Katika kazi za
kidrama. USEMEZANO unaweza kutumiwa pamoja na maelezo ili kuwawezesha watoto kuwafichua
wahusika maudhui au mandhari ya hadithi. Usemezano utumie sentensi fupifupi zenue wazo Moja
kulingana na hadhira lengwa. Ni muhimu kutumia lugha sanifu ili iigwe. Usemezano hujenga hadithi na
kumsisimua msomaji.

PICHA NA MICHORO (VIELELEZO):

Vielelezo ni matumizi ya picha kuelezea zaidi. Vielelezo viandamane na bihusiane na matini Moja
kwa Moja.

MAJUKUMU YA VIELELEZO

1. hufafania matini
2.hufanya kazi ivutie

3.huangazia mambo muhimi katika kazi ya watoto

4. Humsisimua msomaji

5. Humsadia mtoto kujumbuka hadithi

ANWANI /JALADA ZA VITABU VYA WATOTO

Ingawa ANWANI ni muhimu, vielelezo ni muhimu zaidi kwa sababu huweza kutoa maelezo zaidi
Kuhusu ANWANI. Hata hivyo ni muhimu kwa waanfishi kuteua ANWANI zinazovutia.

TANZU ZA FASIHI YA WATOTO

Kama fasihi ya watu wazima, fasihi ya watoto Ina tanzu nyingi. Tanzu hizi ndizi zinazojenga kazi zote za
fasihi ya watoto. Zinajumuisha

1. Drama na michezo

2. Ushairi na nyimbo

3. Hadithi

4. Fasihi simulizi.

DRAMA BA MICHEZO

Michezo huchezwa tu bila kuanfikwa. Tamthikia huandikwa vitabuni na wahusika wote wanapaswa
kuyaiga matendo na maneno yote yaliyomo kwenye tamthili. Kwa kawaida watoto hupenda kuigiza na
hii ni muhimu kwao kwa ajili ya kujiburudisha. Drama hubs resha ukuaji wa mtoto kiakili na pia kijamii.
Ni Nia Bora kwani huwawezesha watoto kutemda ma kupata tajriba za Moja kwa Moja.

Njia za kidrama za kitamaduni kama vile michezo ya watoto, na hadithi hupitisha Mambo muhimu na
maarifa kama vile maadili na ushirikiano ambao humaliza tabia za kibinafsi kama vile uchoyo. Kupitia
michezo ya kugiza, watoto huweza kijiangazia wenyewe ukweli wa maisha na kuwawezesha
kujitambulisha.

Michezo iliyoandikwa huwa Bora kwa watoto iwapo inazingayltia umri wa watoto wanaolengwa.
Wahusika katika michezo ya watoto ni muhimu kwa sababu wao ndio hufanya michezo kuwa na uhalisia
mwingi. Ni muhimu kwa wahusika wa michezo kupewa majina ya kipekee kuliko majina ya makundi.
Mhusika mkuu ajitokeze Moja kwa Moja . Mwandishi atumie mbinu ya ulinganishi kuwalinganisha
wahusika hao.

Wahusika wapewe sifa tofauti tofauti na zijitokeze katika wahusika kibinafsi. Lugha iwe ya utendaji
yenye sentensi fupifupi. Mhusika kuu ajitokeze kuwa mshindi kupitia juhudi zake mwenyewe na awe na
umri unaowazidi wasomaji.

USHAIRI NA NYIMBO

Mashairi huweza kuganwa au kuimbwa. Mashairi na nyimbo hupendelea sana na watoto kuliko watu
wazima. Ni vyema kuzingatia yafuatayo katika ushairi na nyimbo za watoto.

~. Kiwango na umri wa wahusika

~ Uhusiano kimaudhui kati ya shairi na hadhira

~. Yasiwe na mafumbo Bali yawe wazi na uradidi wa vina na maneno yanayoimbika

~. Yawe na kipokea/kiitikio

~ Urefu utegemee hadhira na Yale mwandishi anataka kupitisha

© BEMBEZI KAMA FASIHI YA WATOTO* ✓✓Pia huitwa bembea au beblmbelezi. Ni NYIMBO


zinazotumiwa na wazazi au watoto kuwabembeleza watoto waache kulia au walale.

✓SIFA ZA BEMBEZI

✓huimbwa na wazazi au walezi

✓huimbwa kwa kurudiarudia maneno au kibwagizo au kwa wakati mwingine wimbo wote hurudiwa.
Kurrudia rudia huku kinanasa makinia ya watoto na kufanya maneno ya ate katika akili ya mtoto

✓huwa fupi kwa uamilifu wa kutomchosha mtoto

✓hutumia lugha shawishi ma yenye ahadi nyingi kwa mtoto

✓hutifautisha kutoka jamii Moja Hadi nyingine hutegemea mahitaji ya Jamii husika katika malezi ya
watoto.

DHIMA YA BEMBEZI KAMA FASIHI YA WATOTO

1. Hutumbuiza na kuwaongoa watoto yaani kuwapimbaza na kuwafanya watoto walale


2. Hutumiwa kumpa sifa mtoto mtulivu

3. Husawiri mfumo wa kiuchumi wa jamii husika kwa mfano kama mama ni mfanyibiashara ataimbiwa
hivi

Mama atararudi lala

Kutoka sokoni lala

Alete machungwa lala

4. Humuelimisha mtoto licha ya umri wake mdogo umuhimu wa majukumu ya wanajamii-si malezi tu

5. Husawiri falsafa na mtazamo wa jamii Kuhusu jinsia na matarajio ya Jamii kwa jinsia fulani.

HADITHI.

Kuna aina nyingi za hadithi katika fasihi ya watoto. HADITHI nyingi huhusu miktadha tofauti tofauti kama
vile shuleni, mwiruni ,michezoni na hizi tunaziita hadithi ka kihalisia. Kuna hadithi za matukio za kiajabu
na visa vya kutisha na wakati mwingine visa hivyo hisisimua . Hizo ni hadithi za mazimwi. Pia Kuna
Hadith za kindoto ammbzo mara nyingine hisisimua. Kuna hadithi za kitamaduni ambazo katika upejee
wake huwasilisha kaida za jamii husika.

Kuna hekaya ambazo wahusika wake ni wanyama. Ni fupi , wahusika wachacje na mwishoni Kuna funzo
la kimaadili. Huwa na masimilizi za kubuni ambazo ni za kisayanzi. Aina nyingine no Hadithi za ajira
ambazo huelezea jinsi watu huajiriwa. Aidha Kuna Hadith za kidini ambazo huzungumzia mambo ya
muumba aliye na uwezo wa kuwazidi wanadamu. Mwisho Kuna taasifu na tawasifu ambazo huangazia
maisha ya watu fulani katika jamii .

FASIHI SIMULIZI

√mchongoano

√vitendawili

√vitanza ndimi

MASUALA YA KIJINSIA KATIKA FASIHI YA WATOTO


Kupitia kwa kazi za watoto twaweza kupata mtazamo wa jamii. Chochote kinachosemwa humjenga
msomaji na huwasilisha hoja ya kuwa mvulana/msichana au mwanamume/mwanamke kama vile dada,
mama, kaka,mjomba, shangazi n.k.

Mbali na kujenga stadi na kiwango Cha lugha, kazi za watoto hupitisha tamaduni za jamii na vile vile kile
kinachoshikikiwa na jamii husika. Usawiri wa kijinsia Katika kazi za watoto huchangia pakubwa ile taswira
wanayopata watoto akilini mwao kuwahusu wao wenyewe na jinsia Yao katika jamii. Ubaguzi wa kijinzia
unaweza kujitokeza kwa njia mbalimbali Katika kazi za watoto.

Hii ni kwa sababu kazi za watoto zimetawaliwa na wahusika wa kiume. Ernst 1995 alifanya utafiti kubusi
ANWANI ya vitabu za watoto na lipata kuwa majina ya wavulana yalijitokeza mara nyingi kuliko ya
wasichana. Utafiti huu vile vile ulipata kuwa hata vitabu vilivyokuea na majina ya wasichana mara nyingi
huzungukia mhusika wa kiume kama mhusika mkuu.

Vitabu vingi vilivyo na wahusika wa kike huwasawiri katika majukumu ya kike yaani ya kinyumbani na
vile vile hupendelea jinsia ya kiume. Fox 1993 anasema kuwa vitabu vingi vya watoto husawiri wasichana
kama wahusika bubu. Anaendelea kusema kuwa wasichana husawiriea kama wanaopendelela wasio na
hila , wenye kufuata kanuni na wasioweza kujitegemea. Wavulana nao wamesawiriea kama wënÿë
nguvu wanaojitegemea, jasiri na wanaojiweza. Wamepewa majukumu kama wapiganaji, waokoaji na
wenye ujasiri.

Wasichana wamepewa majukumu ya ulezi na wanaohitaji kuokolewa. Temple 1993 anaeleza kuwa mara
nyingi wahusika ambao ni wasichana.wajeonyeshwa kuwa kufauli katika Hadithi kwa sababu
wamesaidiwa na wengine. Kwa upande mwingine wavulana wamechorwa kufaulu kwa sababu ya
uvumilivu na ukakamavu wao. Pale ambapo wasichana wanasawiriwa kama wakakamavu mwanzoni
mwa Hadithi hujitokeza kama wahusika bubu mwishoni. Ni wasichana wachache tu wanaobaki kuwa
wakakamavu Hadi mwishoni mwa hadithi.

USAWIRI WA KIJINSIA KATIKA VITABU VYA WATOTO

Watafiri wengi wamesema kuwa wasomaji hujitambulisha na jinsia Yao Katika vitabu. Hivyo basi ukosefu
wa wahusika wa kiume au kike hupunguza nafasi zao za kujitambulisha na jinsia Yao na kuhalalisha
nafasi zao Katika jamii. Namana ambavyi jinsia husawiriea katika jamii huathirir mielekeo ya watoto
kuhusiana na masuala ya kijinsia. Usawiri hasi wa jinsia Katika kazi za watoto, husababidha wavulana na
wasichana kukubali jinsi walivyo na kukosa kujikomboa kutokana na mitazamo ya kijadi.

Uimarishaji wa taswira za kijinsia huwafanya watoto kukubali Uhusiano mzuri Katika jamii. Usawiri
mbayabwa kijinsia Katika kazi za watoto huathirir jinsia zote. Wasichana wanaposawiriwa kama wasio
wakakamavu, na kupewa majukumu yasiyo muhimu hujidunisha katika jamii. Wavulana nao
wakionyeshwa kama wasio na mihemko ya huzuni na uwoga na kupewa majukumu ambayo hawapiganii
uhodari , wataathirika vibaya.

Hali hii huwafanya wavulana na wasichana wasipiganie haki ya kujieleza bali kukubali tu namna jamii
inaeleza. Wao wataiga mambo jinsi vitabu vinavyohitaji na sito kutokana na hutaki g ya nafsi zao
MAMBO YA KUZINGATIA KATIKATI UTEUZI WA VITABU VYA WATOTO

√ Viwe na wahusika wa jinsia zote mbili.

√Wasichana na wanawake wapewe majukumu ya kisasa ili wasiwe wahusika bubu.

√ Wapewe majukumu sawa na ya wavulana/wanaume

√ Mavazi yafafanuliwe kimatumizi Wala sio kwa istilahi za kijinsia

√ Kila mhusika awe anaweza kukabikiana na Hali mbalimbali

√ Lugha inayotumika isidhalikishe jinsia yoyote

√ Kuwe na ujumbe unaofaa jinsia zote.

N/B Ikumbukwe kuwa kubadili maono ya watu Kuhusu usawa wa kijinsia siyo jambo linaloweza
kukamilika kwa siku Moja tu, Bali huhitaji muda mrefu.

UBADILISHAJI (adaptation) KATIKA FASIHI YA WATOTO

Ubadilishaji ni kule kuiweka (kubadilisha) kazi ya fasihi kutoka Hali asilia Hadi nyingine. Kwa mfano

1. Riwaya au tamthilia kubadilishwa na kuwa filamu.

2. Hadithi kuwa wimbo au shairi kuwa hadithi.

Kazi hizi hubadikishwa ili kufaa matumizi yake mapya (hadhira lengwa). Ubadilishaji huu hufanywa katika
viwangi mbalimbali

√vitabu vigumu hubadilishwa ili vieleweke kwa urahisi na kutumika ka hadhira lengwa

√. Riwaya inaweza kubadilishwa iwe hadithi kwa minajili ya kiwasilishea kwenye jukwaa kwa kusema.

√ kazi za kifasihi Katika lugah tofauti tofauti zinaweza kubadilishwa ili zifae kikundi kilicho na utamaduni
tofauti.

√ubadilishaki haumanishi kufulidha kaxlzi ili iwe na maneno machache lakini mambo mengi
hushughulikiwa katika mchakto huu wa ubadilishaji. Kwa mfano msamiati, aina za sentensi , matumizi ya
lugha,, vielelezo na mtindo wa UANDISHI. Hii hufanywa ili kazi ilenge hadhira husika (WATOTO).

UMUHIMU WA UBADILISHAJI WA NGANI ZA USI KUWA HADITHI ZA WATOTO

1. Vina vivutio vingi kwa watoto kama vile fantasia na mambo ya ajabu
2. Vina maadili kulingana na jamii

3. Hupitisha utamaduni wa jamii

4. Huwapa watoto changamoto tele ili kyona umuhimu wa mpangilio wa maisha. Mfano Mzee Kobe na
sungura wanoofanyiana ujanja katika mbio na wote wanankubaliana kushirikiana. Mtoto anajua kuwa
ushindi hupatikanankwa kujaribu tena na kushirikiana na wenzake

5. Ngano za kale hisisimua kwa sababu matumizi ya wanyama Kam wahusika huwasisismua watoto.

6. Matumizi ya fantasia katika mfano hujenga akili ya mtoto

7. Humwezesha mtoto kuelewa mambo ya kimiujiza na yasiyo ya kawaida

8. Humwezesha mtoto kuelewa Hali halisi ya ulimwengu.

9. Hujenga ubunifu wa mwandishi kwa kutalii utamaduni wa jamii na kubalishanhaki ili ifanane na ya
kisasa

10. Zinaweza kubadilishwa kuwa drama za watoto

11. Huisha kwa furaha.

UDHAIFU WA UBADILISHAJI WA NGANI ZA USULI

√ huwenda zikawa na wahusika na mandari yasiyofaa jamii ya Sasa na ambao watoto hawatapenda
kujitambulisha nao

√ Ngano zinafaa kutambwa na zinapotendwa kipengeke Cha kimtindo hupotea

√ baadhi ya waandishi hawafafanui USULI wa ngano zenyewe na Katika uhusika hawaeliesi watoto Hali
ilivyokuwa wakati huo

√ ubadilishaji wa ngano huhitaji ubunifu wa Hali ya juu

FASIHI YA WATOTO NA TEKNOLOGIA MPYA

Kwa ujumla fasihi imeadhirika na kuzuka kwa tecknolojia mpya. Kuadhirika huko ni kwa njia chanya na
Hasi. Twasema hivyo kwa sababu tecknolojia imerahisisha kazi ya fasihi andishi na kuchangia kudidimia
kwa fasihi simulizi.

UMUHIMU WA TECKNOLOJIA MPYA KWA FASIHI YA WATOTOi


* Imerahisisha usambazaji wa fasihi ya watoto kupitia kwa njia mbalimbali

* Imetumika katika uhifadhi wa kazi za fasihi simulizi

* Watoto wameweza kupevushana kimawazo kupitia kwa kuzuka kwa tecknolojia mpya katika nyanja
mbalimbali za fasihi ya watoto

* Tecknolojia mpya imewezesha uridhishaki wa mambo za kitamaduni kupitia kwa fasihi simulizi

* Tecknolojia mpya huleta burudani miongoni mwa watoto wanapotazama fasihi ya watoto kupitia kwa
vipindi mbalimbali

* Tecknolojia mpya huleta Ari ya kutaka kuona tena kazi za fasihi ya watoto wakiwa na tarajio la kuona
jambo fulani katika kipindi fulani katika televisheni.

* Tecknolojia mpya imeweza kudumisha ubunifu miongoni mwa watoto kwani wanapotazama vitu kama
vile vibonzo wanakuwa na uwezo wa kuchukua nafasi ya kibonzo alichokitazama na Kisha baadaye
akaiga tabia ya kibonzo kile ili kufanikishea uwasilishaje wake

* Watoto huweza kujifahamisha na mambo mbalimbali mbali ya kijamii kama vile ulezi, uwajibikaji n.

* Imechangia uwezo wa kubashirir mambo ya baadae kupitia kwa anayotazama kwa watoto

UDHAIFU WA TECKNOLOJIA MPYA KWA FASIHI YA WATOTO

* Hupoteza mahadhi katika uwasilishaje wa kazi za fasihi ya watoto

* Imeweza kuadhiri afya ya watoto kwani hutazama telesheni kwa muda mrefu sana

* Imeweza kuzua uzembe miongoni mwa watoto kwa anamaliza muda mrefu katika utazamaji wa
televisheni

Kudhiofika kwa nidhamu pia kumeshuhudiwa.

* Matumizi ya tecknolojia mpya inahitaji vifaa kama vile televisheni, umeme na hivyo basi inakuwa
vigumu kwani si wote watakaomudi mahitaji hayo

* Watoto huiga tabia za watu wabaya kwani mara nyingi wahusika hawa hutumiwa njia Hadi ili kijipaliza
ushindi na kwa hivyo mtoto anapata kumpenda kutokana na ushindi wake licha ya kuwa mhusika huyo
ni Hadi.

*Vitabu*

Binti kisirani
Mashairi kwa vitendawili

You might also like