You are on page 1of 19

zswage

The greatest WordPress.com site in all the


land!

UJIFUNZAJI/UFUNDISHAJI WA
KISWAHILI KWA WAGENI

MBINU ZA UFUNDISHAJI KISWAHILI KWA


WAGENI

1. Malengo ya ufundishaji lugha kwa wageni

Lengo kubwa ni kwamba ili mwanafunzi aweze kujua lugha hiyo kwa
stadi zote za lugha ile. Stadi za lugha ni 1. Kusikiliza 2.kuzungumza 3.
Kusoma 4.kuandika 5. Sarufi 6. Utamaduni wa lugha ile

Malengo ya jumla ya kufundisha ili ni pamoja


na:-

1) Kumwezesha mwanafunzi ili aweze kumudu lugha.

2) Kumwezesha mwanafunzi aweze kuwasiliana na wazawa wa lugha


husika
LUGHA YA KWANZA

Stern (1983) anasema kwamba lugha ya kwanza lugha ambayo mtoto


hupata kutoka kwa mama yake mzazi angali mchanga.

LUGHA YA PILI

Stern (1983) anasema kwamba lugha ya pili si lugha ambayo mtoto/mtu


aliipata alipoanza kukua na kupata lugha. Hii ni lugha ya kujifunza,kwa
maana ya kwamba mtu huyu huwa tayari ana lugha nyingine.mfano.
hapa Tanzania Kiswahili ni lugha ya pili kwa watu wengi

LUGHA YA KIGENI

Ni ile lugha ambayo unajifunza na kuitumia lakini wazungumzaji wake


wako nje ya nchi au mbali na jamii anapokaa mwanafunzi huyo. Mfn
lugha ya kiingereza ni lugha ya kigeni hapa Tanzania

MALENGO YA JUMLA YA UJIFUNZAJI NA


UFUNDISHAJI WA LUGHA YA KIGENI

Mara nyingi hii hutegemea taaasisi yenyewe lakini kuna malengo


ambayo ni ya jumla:

1) Kutaka kuwasiliana na wenyeji wa sehemu /nchi husika

2) Kujiandaa kusafiri kwenda nchi nyingine kwa shughuli mbalimbali

3) Kwa ajili ya kufanya biashara

4) Kukidhi vigezo vya masomo

5) Kufanya utafiti katika taaluma husika


6) Ili kupata ajira nchi za ngambo

KITU GANI KIANZE KUFUNDISHWA SASA?

Onyo: usijaribu kumfundisha mwanafunzi sarufi za lugha hiyo kwanza,


utamfundisha ikibidi lakini isiwe kipaumbele chako

W Anza na salamu za kawaida, salamu katika utamaduni wa mwafrika


ni kitu cha muhimu sana, hivyo fundisha salamu,maana lengo ni
kwamba huyo mtu aweze kuwasiliana.

MALENGO YA UJUMLA YA UFUNDISHAJI


LUGHA YA KISWAHILI KWA WAGENI

a) Ili mwanafunzi wa Kiswahili ajue mambo yafuatayo:

i. Aweze kumudu lugha ya Kiswahili

ii. Aweze kuwasiliana na watumiaji wa lugha ya Kiswahili

iii. Ili wanafunzi waweze kungamua mambo yafuatayo:- Namna ya


kusema jambo gani? Mfano anataka kwenda chooni Asemee wapi? Kwa
nini aseme? Kwa nani aseme? Mazingira gani aseme?

iv. Ili kuwapa wanafunzi mbinu mbalimbali za kujifunza lugha ya


Kiswahili. Wanafunzi wafanye kwa vitendo ili waweze kujichukulia
misamiati ya kutosha

v. Wanafunzi wangamue umuhimu wa lugha wanayojifunza

b) ili wanafunzi waweze kutimiza malengo haya, mwalimu ni


lazima wape wanafunzi:

kuchunguzakugunduakutalii kuhusu lugha ya Kiswahili

c) wape uwezo wa kukuza lugha ya Kiswahili kila siku aweze kuongeza


msamiati kwa kusoma vitabu mbalimbali vya hadithi

d) wape nafasi kutumia mbinu mbalimbali lugha ili kukuza uelewa


wao
e) wape uwezo wa kukuza fikra zao na kudadisi

f) wasaidie kufanya utumbuizi wa vipengele vya mfumo na


utamaduni wa lugha ya Kiswahili

NADHARIA KUU ZA UJIFUNZAJI LUGHA

Kuna mambo mawili ambayo waalimu tarajili wanapaswa kujua

1) mbinu za kujifunza lugha ya pili ni nyingi kama ilivyo waalimu


wengi

2) manzingira halishi wakati wa ujifunzaji. Rogers (2001) anasema


kwamba wakati wa ufundishaji wa lugha ya kigeni hutumia mbinu
mbalimbali kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi wafikie malengo yao

kuna nadharia kuu nne (4)za ujifunzaji lugha:

1) NADHARIA YA UHULKA

Mwasisi wake ni Noamy Chomsky (1957)

Wazo kuu lake ni kwamba: binadamu huzaliwa akiwa na uwezo lugha.


Yaani kwenye ubongo wake ana mfumo ambao huzaliwa nao kwa ajili ya
kujifunza lugha. Ana kifaa kinachoitwa LAD (Kifaa cha upataji lugha)

Naye Brown (2000) aliunga mkono mawazo haya. Mwingine aliyeunga


mkono ni Ellis (1997) walikuwa na hoja kwamba kuna kipindi mtu
akifikia umri Fulani hawezi kupata lugha sawasawa na wazawa wa
lugha husika. Umri huo ni kuanzia 0-miezi 18. Kwa mujibu wa
wataalamu hawa mazingira hayana msaada wowote katika ujifunzaji
lugha.

2) NADHARIA YA UTABIA

Kwa mara ya kwanza ilidokezwa na E.Thonilke(1935). Kwa mujibu wa


wanatabia ujifunzaji wa lugha ni mwigo

Aliyetafiti zaidi katika nadharia ya ujifunzaji ni B.F SKINNER , Huyu


alikubali ni mwigo lakini akaongeza kuwa ni uimarikaji wa tabia, hivyo
mtoto mdogo hazaliwi na lugha bali huichota kutoka kwa wazazi
wake

Nadharia hii inayapa mazingira nafasi kubwa katika ujifunzaji lugha


Je mtu akitengwa na jamii anaweza kuwa na lugha? Jibu unalo wewe
mwenyewe!

3) NADHARIA YA UTAMBUZI
Nadharia hii iliasisiwa na Jean Hajet (1954)

Alidai kuwa binadamu anapozaliwa kuna kipindi maalum cha kupata


lugha

Alidai kuwa kujifunza lugha ni sehemu ya makuzi ya binadamu, kwa


kadiri unavyokua ndivyo unavyozidi kupata lugha

Alidai kuwa mtoto hupata lugha kabla ya kuzaliwa.

Arth(2003) anadai kuwa mtoto hupata lugha kabla ya


kuzaliwa,kuanzia 0-miezi 18

Nadharia hii haipingani na umuhimu wa mazingira katika ujifunzaji


lugha

4) NADHARIA YA UUMBAJI

Iliasisiwa na Jerome Brunner

Wazo kuu la nadharia hii inasisitiza nafasi ya mama katika upataji


lugha ya kwanza

Mtoto hutengeneza lugha kutegemeana na mawasiliano ambayo mama


yake anayatumia

Alidai, ili mtoto aweze kupata lugha ni lazima mambo yafuatayo


yatimizwe

Muktadha
Tajiriba (experience)
Upangilifu (organization)
Kujenga mazingira ya upekuzi (udadisi_

Hukaza zaidi kuhusu mazingira katika ujifunzaji lugha

NJIA ZA UJIFUNZAJI LUGHA YA KISWAHILI

Njia za ufundishaji Kiswahili ni nyingi kama na waalimu nao walivyo


wengi, lakini njia hizi itatengemea hali ya wanafunzi, hata hivyo njia
zifutazo zinapendekezwa zitumike.

1. Njia ya majadiliano-njia hii haifai kwa mwanafunzi ambaye ndio kwa


mara ya kwanza anasikia Kiswahili. Lakini ni njia nzuri kwa
mwanafunzi ambaye amewahi kusikia habari za Kiswahili
2. Njia ya mahojiano. Mfano mwalimu aandae maswali, awaambie
wanafunzi wajipe vyeo mfano mmoja anakuwa daktari mwingine
anakuwa mgonjwa n.k
3. Mchezo wa maswali. Kwa mfano. Kama wewe ungekuwa rais wa
marekani ungefanyaje kuhakikisha unakomesha ugaidi duniani?
Watajibu na kujipatia msamiati kibao
4. Njia ya uigizaji-mwli awape wanafunzi mwongozo wa maigizo
5. Njia ya maswali ya papo kwa papo (ana kwa ana) mfano: mimi ni Seni,
wewe ni nani?
6. Njia ya uwandani. Mfno ukitaka kuwafundisha misamiati ya sokoi
wapeleke sokoni.
7. Njia ya kutumia mazingira mbalimbali. Mfano kama mwalimu
anataka kuwafundisha michezo wapeleke uwanja wa mpira
8. Njia ya usomaji. Mfano kusoma pande nne za dunia,kuwapa matini
mbalimbali wanafunzi
9. Njia ya majadiliano funge. Yaani wanafunzi wanajadili vitu ambavyo
vimewekewa mipaka

Angalizo:uteuzi wa njia ipi itumike itategemea aina ya wanafunzi na kazi


zao!

HULKA/TABIA YA UANAFUNZI KUJIFUNZA


LUGHA

Wanafunzi hutofautiana kulingana na hulka zao, mwalimu anahitaji


kuangalia mielekeo ya wanafunzi wake. Baadhi ya tabia zao ni kama vile:
ucheshi, hasira, aibu, hasira za kutojua, hapendi kusahihishwa, mkimya
nk

ATHARI ZA KIJAMII KUHUSU


LUGHA/WANALUGHA

Kila jamii ina mtazamo wake kuhusu ujifunzaji lugha, mtazamo hasi ndio
ambao huathiri ujifunzaji lugha na kupelekea kutopata motisha wa
kujifunza lugha. Baadhi ya mambo yanayoathiri ni kama vile

i. Nia au lengo la kujifunza lugha hiyo

ii. Jinsia

iii. Umri
iv. Mazingira

v. Umilisi wa lugha kama akiwa na umilisi mdogo

Malengo ya mwalimu ni kuhakikisha anafanya mambo yafuatayo:

i. Kuwatia motisha wa kujifunza lugha

ii. Kumsaidia kuondokana na hasira

iii. Kuondoa dhana potofu ya ujifunzaji lugha. Mf. Kuna


wanaoamini kwamba Kiswahili ni lugha ya kiislamu

iv. Kuondoa utata katika vipengele vya kisarufi

v. Kuwaelezea aina mbalimbail za lugha na mahali zinapotumika

Kuhusu matumizi ya lugha ya ishara ni muhimu sana kujua ishara


zinazotumika katika jamii. Hivyo mwalimu anapaswa awaeleze mambo
yafuatayo

i. Baadhi ya utamaduni huangalia usoni, tabasamu na kujiamini

ii. Matumizi ya mkono wa kushoto au wa kulia

iii. Kuonyesha vidole-jamii zingine haziruhusu kabisa

iv. Namna ya kusimama na kuelezea jambo

Ili kutimiza hayo yote mwaimu lazima awe na sifa zifuatazo:

i. Awe muwasilishaji mzuri

ii. Awe na mpangilio mzuri

iii. Awe mstahimilivu

iv. Awe na ujuzi wa kufundisha

v. Awe na uhusiano mzuri na wanafunzi

vi. Awe na maarifa ya somo

SIFA ZA MJIFUNZAJI LUGHA

a) Awe na utayari wa kujifunza lugha ya Kiswahili bila kulazimishwa

b) Afanye mazoezi ya kuitumia lugha hiyo


c) Atumie akili kupambanua dhana mbalimbali ili kugundua mambo
ambayo jamii Fulani inayafanya

d) Awe na uhuru wa kuzungumza lugha hiyo

e) Awe na ratiba ya kujifuza

f) Aweze kulinganua na kulinganisha lugha anayojifunza

g) Awe na ukarimu ili aweze kuwa na uhusiano na jamii husika

h) Awe mtendaji

i) Azingatie ubora ili aweze kujifunza zaidi

MOTISHA

Ni tabia au msukumo katika kutimiza malengo Fulani. TUKI (2004)


wanadai kuwa motisha ni kitu kama fedha inayotolewa ili kumtia mtu
hamasa kujifunza jambo.

Hata hivyo, si lazima umpe kitu bali unamtia moyo mwanafunzi na


kumsaidia. Mwalimu anapaswa kutumia motisha chanya sio hasi. Mfn
hutakiwi kuchapa fimbo

Brown (1994) anasema kuwa motisha:

a) Ni kiwango cha uchaguzi ambacho unafanya kuhusu lengo


unalotaka kufikia

b) Jitihada atumiazo mtu kufikia malengo hayo

SKINNER &WATTSON-hawa wanaangalia zawadi na uhimizaji kwa


wanafunzi pamoja na adhabu ili kufifisha na kujenga hali Fulani

AINA ZA MOTISHA

1. Mwamko wa mjifunzaji mwanyewe


2. Mazingira mazuri ya kufundishia Kiswahili mfano, darasa, nje n.k
3. Jamii inayomzunguka ni motisha pia
4. Mwalimu anaweza kuwa motisha kwa mwanafunzi
5. Zana/vifaa vya kujifunzia pia ni motisha
6. Motisha wa ndani-

MOTISHA IPO KATIKA MAKUNDI MIWILI

Haitegemei vitu vya nje ya yenyewe

Hiki ni kile kinachoonekana kwa mjifunzaji lugha mwenyewe

Hii haibadiliki kulingana na muktadha wowote ule

2. Motisha wa nje

Ni aina ya motisha ambayo mwanafunzi hutegema kupewa, kupata,


kusikia au kuona

Hivi vitamsaidia katika kujifunza lugha

Mwalimu wasaidie wanafunzi kutumia lugha kulingana namuktadha.


Hapa kuna mambo ya kuzingatia:-

a) Akili ya mwanafunzi: lazima utambue tofauti zao katika akili zao ili
kujifunza lugha

b) Kipaji chao-kuna wengine wana vipaji vya kujifunza lugha

c) Umri-watu wazima huchelewa kujifunza lugha

d) Jinsia-inasemekana wanawake wanaweza kupata lugha haraka


kuliko wanaume

UFUNDISHAJI LUGHA KIMAWASILIANO

Ni muhimu kuhakikisha kwamba katika kujifunza lugha ufundishaji


uwe wa mawasiliano

Ni mbinu ya kufundisha lugha ngeni na lugha ya pili

Husisitiza mwingiliano maathiriano kama mbinu ya kujifunza lugha


KAZI ZA LUGHA

Van (1975) anasema kuwa kazi ya lugha ni:

a) Kutoa habari

Kusimulia
Kuuliza
Kutoa taarifa

b) Kutafuta taarifa za kitaaluma

c) Kuelezea mihemuko na misisimko. Mfno mapenzi, misisimko

d) Kuelezea masuala ya uadilifu.mfn kuomba msamaha, ibada etc

e) Kwenye mambo ya ushirikiano. Mfn kuamkia watu, kujitambulisha


nk

Angalizo: hata kama mwanafunzi ana malengo mengine ya kujifunza


lugha hiyo ni lazima umfundishe umuhimu wa lugha hiyo kulingana na
muktadha

MASHARTI YA KUZINGATIA

a) Azingatie majukumu ya kijamii mfn ataanzaje kuzungumza na mtu


asiyemjua? Watu wengine ni wenye mamlaka Fulani, hivyo kuna namna
ya kuzungumza nao

b) Majukumu ya kisaikolojia-mfano asipendelee upande wowote mfn


CHADEMA CUF na CCM

c) Mazingira ya lugha ilipo. Je ni lugha ya taifa? Watu


wanaokuzunguka wanatumiaje?

Angalizo: lugha sio sarufi tu au fonolojia bali ni chombo cha


mawasiliano, hivyo inahitaji kufundishwa kimawasiliano zaidi
MUKTADHA WA UFUNDISHAJI LUGHA

Haya ni mazingira halisi ambapo tukio la ufundishaji lugha hufanyika


kwa kuzingatia wadau wakuu watatu

a) Mwanafunzi

b) Mwalimu

c) Jamii

Pamoja na motisha ufundishaji uzingatie sana mambo yafuatayo:

Utoaji wa kazi na mazoezi mengi


Tumia lugha katika mazingira halisi na yanayostahili ukilenga kwenye
stadi nne za lugha
Matumizi ya lugha kwa kuzingatia muktadha
Utumizi wa mazingira halisi ya darasa.mfn picha, katuni. Nk
Himiza ushirikiano miongoni mwa wanafunzi baina yao na baina
yako mwalimu
Tumia mbinu zaidi ya moja. Mfn vikundi, majibizano nk (rejea mbinu)
Fafanua kwa uangalifu masuala ya kisarufi
Ajue maono ya mwanafunzi. Mfn huzuni, ucheshi nk
Kuunda mazingira ya utani darasani

UFUNDISHAJI WA DARASA MSETO

TUKI (2013) Mseto ni hali ya kuwa na mchanganyiko wa makabila


mbalimbali kutengeneza kitu fulani

Hapa ni mchanganyiko wa darasa lenye wanafunzi wanaotoka sehemu


mbalimbali na wenye umri tofauti, malengo tofauti nk

Hivyo mwalimu inakubidi utofautishe sana katika ufundishaji wako na


uwe makini ili usije ukawakwaza wanafunzi wengine
NAMNA YA UFUNDISHAJI DARASA MSETO

a) Lazima mwalimu uwe na maarifa ya wanajamii mfn utamaduni


wao. Kama ni wazungu, wachina nk jua utamaduni wao

b) Uwe na usisitizaji wa lugha lengwa. Kama ni Kiswahili basi pendelea


kutumia Kiswahili ili usiwakwaze sana. Hata hivyo lazima wawe na
lugha ambayo wewe unaijua

c) Tumia vitendo halisi, ishara nk

d) Arika wageni mbalimbali waje waeleze kuhusu lugha na mazingira

e) Puuza(ignore) malengo ya wanafunzi

f) Ufundishaji wa masuala ya utamaduni lazima ufungamane na


muktadha husika

SIFA ZA MPATAJI LUGHA

Mpataji lugha ni lazima awe na sifa kuu mbili tu:

1. Umilisi wa kiisimu

Ni uwezo alio nao mjifunzaji lugha ambao unamwezesha kutofautisha


viambo, miundo tofauti ya lugha na msamiati wa lugha

pia kuweza kutamka lugha ile.

2. Umilisi wa kiisimujamii

Ni umilisi ambao mtumiaji wa lugha hupata lugha inayomwezesha


kujifunza lugha na kuzingatia muktadha

NADHARIA /MBINU /MIKABALA ZA


KUJIFUNZA LUGHA YA KIGENI
Nadharia ni mkondo wa mawazo unaotumika kuelezea jambo

Mtesigwa(2009) anasema nadharia ni kiunzi cha mitazamo, mawazo


au vitendo vinavyohusisha uchunguzi, mpangilio na uchanganuzi wa
matukio katika kukabili suala fulani kisayansi

kuna mambo mawili ambayo lazima tujikumbushe:

a) Njia za ufundishaji lugha ya kigeni ni nyingi kama waalimu walivyo


wengi

b) Kumbuka hali ya darasa. Tumia njia mbinu zaidi ya moja darasani,


usitumie njia moja tu.

Rogers&Richards (2001)wanasema kuwa tunapojiandaa kwenda


kufundisha tunahitaji kujiuliza maswali yafuatayo:-

a) Malengo ya ufundishaji lugha lengwa(LL) ni yapi? Mfano labda


lengo lao linaweza kuwa wanataka kuzungumza tu.

b) Upi ni msingi asili wa lugha lengwa na unaathiri vipi njia za


kufundisha. Mfn kaida za lugha ya Kiswahili ni zipi?

c) Ni misingi ipi inatumika kuchagua mambo katika ufundishaji lugha?

d) Ni misingi ipi ya upangiliaji wa mada. Mfano kwa kuzingatia suala la


utamaduni, mfano salamu nk

e) Je lugha mama ya mwanafunzi ina jukumu gani katika kujifunza


lugha? Mfano miundo ya lugha mama inafanana na lugha lengwa?

f) Je wanafunzi binafsi watumie mbinu zipi katika kujifunza lugha


hiyo?

g) Je ni mbinu na vitendo vipi hufanikisha vizuri ujifunzaji lugha ya


pili (kigeni)?

NADHARIA ZA KUJIFUNZA

1. Mbinu ya tafsiri sauti


2. Mbinu ya moja kwa moja(direct method
3. Mbinu ya usomaji(reading approach method)
4. Kusikia na kusimulia (audiolingual method)
5. Kushirikisha jamii (community langaage learning method)
6. Mbinu ya ukimya (silence method)
7. Mbinu ya mawasiliano (communicative language approach)
8. Mbinu ya mwitiko jumuishi(total physical response)
9. Mbinu ya utambuzi (communitive code method)
10. Mbinu ya upendekezi (suggestopidia method)
1. Mbinu ya tafsiri sarufi

wakati mwingine hujulikana kama mbinu ya kimapokeo. Huu ni


mkabala ambao ufundishaji wa lugha ya kigeni umejiegemeza katika
sarufi ya lugha ya Kiratini. Iliasisiwa/anzishwa na Meidinger (1783) na
Ploetz (1849) wakati ule iliaminika kwamba lugha ya kiratini ndiyo lugha
pekee.

Nafasi ya lugha mama ilipuuzwa kwa kiasi kikubwa na ilijikita katika


sarufi ya Kiratini, na hivyo mwalimu alipaswa kujikita katika kufundisha
sarufi ya Kiratini na vipengele vingine vilipuuzwa

Huu ulikuwa ni mkabala elekezi-yaani unawaelekeza watu namna ya


kutumia lugha na sivyo wanajamii wanavyotumia lugha hiyo

2. Mbinu ya moja kwa moja(direct method)

Iliasisiwa na Gouin(1880)

Nadharia hii inazingatia uzungumzaji wa lugha husika

Mbinu zilizopaswa kufundishia ni zile zilizohamasisha wanafunzi


kuzungumza. Mfn mbinu ya majadiliano,uigizaji,maswali katika vikundi

Masomo yalianza kwa hadithi fupi halafu wanafunzi wanauliza


maswali kuhusu hadithi waliyosimuliwa na mwalimu aliwaambia watoe
maoni yao kuhusu hadithi hiyo.

Matumizi ya vielelezo vilitumika zaidi. Mfano picha, ramani, katuni n.k

Kipengele vya sarufi kilifungushwa kwa kufuata muktadha halisi


ambamo lugha inatumika

Kipengele cha utamaduni kilifundishwa kwa uchache sana

3. Mbinu ya usomaji (reading approach method)

Mbinu hii inatumika kufundishia kwa wanafunzi wanaojifunza lugha


ya kigeni ambao hawatarajiwi kutoka nje ya nchi ambapo lugha hiyo
inatumika

Malengo yake huwa kuendeleza uwezo wao wa kusoma ile lugha

Vipengele vinavyofundishwa ni vile vinavyohusu usomaji, hivyo


vipengele vingine havihusiki. Mkazo wake ni kwamba anayejifunza lugha
aweze kusoma vitu vingi kwa wakati mmoja.

Mbinu hii haimpi mjifunzaji lugha uwezo wa kuzungumza lugha


husika bali ni kuisoma tu.

4. Kusikia na kusimulia (audiolingual method)

Nadharia hii ilitokana na haja ya ukarimani nchini marekani miaka


1940.

Iliasisiwa na Bloomfield (1942) na Fries (1945)

Msingi mkubwa wa nadharia hii ni kile kinachosemwa

Maandishi hayakupewa fursa kubwa bali kile kilichosemwa ndicho


kilikuwa cha muhimu sana. Bloomfield alisema kuwa lugha si katika
maandishi bali ni kile ambacho kinasemwa.

Inahusisha kusimulia mada mbalimbali na kupima uwezo wa kusikia

Walipenda sana kutumia miziki, nyimbo, usimulizi na ughanaji

Walisisitiza stadi ya kusikiliza, kuzungumza, kusoma na kuandika

Waliongeza kitu kingine cha kuona

5. Kushirikisha jamii (community langaage learning method)

Iliasisiwa na curran (1976)

Dai la nadharia hii ni lugha ni watu, kwa maana ya kwamba huwezi


kutenga jamii na lugha

Walidai kwamba ili uweze kumfundisha mwanafunzi mgeni basi


nenda kwenye jamii husika

Walidai pia kwamba kama utaamua kufundishia darasani bali darasa


lako lifanye angalau lifanane fanane na jamii ya lugha husika

Ili uweze kufundisha watu ni lazima ushirikishe watu wanaotumia


lugha hiyo.

Mwanafunzi atapata vichocheo vya aina nyingi katika jamii na kubaini


ni mambo gani yanafaa na mambo gani hayafai

Nadharia hii inaipa kipaumbele jamii kama chombo muhimu katika


kujifunza lugha
6. Mbinu ya ukimya (silence method)

Nadharia hii inaamini kwamba kila lugha ina mfumo wake tofauti na
lugha nyingine, hivyo ufundishaji wa lugha ya pili ulenge kumfanya
mjifunzaji wa lugha kuwa mmilisi au kukaribia kuwa mmilisi wa lugha
anayojifunza

Nadharia hii inadai kwamba ujifunzaji wa aina yoyote ile unahusisha


vitu viwili.

Kichocheo Mwitikio mgeuko

(Mwalimu) (mwanafunzi)-(anabadilika)

Ili kuweza kutimiza hili, mwalimu anahitaji kujenga mazingira ya


utani katika darasa jambo ambalo litaleta matokeo mazuri ya umilisi wa
lugha husika

Nadharia hii inamhitaji mwalimu kufanya tathimini kwa wanafunzi


wake ili kubaini kama kuna badiliko

7. MBINU YA UTAMBUZI (COMMUNITIVE CODE METHOD)

Nadharia hii inatokana na ukosoaji/udhaifu wa nadharia ya mbinu ya


sarufi na ile ya moja kwa moja

Ilianzishwa mwaka 1970

Wanadai kwamba mwanafunzi apewe vipengele vyote vya lugha kwa


ujumla mwanafunzi kumpa maarifa mapana kuhusu lugha,
kumpakanuni za msingi kuhusu lugha, halafu yeye mwenyewe
kulingana na utambuzi wake aweze kuielewa lugha.

Uwafundishe kanunu za msingi. Kwa mfano katika lugha ya Kiswahili


ni lazima ujue ngeli za majina-hii itakusaidia kutumia nomino katika
mazingira tofauti tofauti, vitenzi-waeleze namna ambavyo vinaweza
kukaa peke yake kama sentensi

8. Mbinu ya mwitiko jumuishi(total physical response)

Nadharia hii pia hujulikana kama mkabala asilia.

Iliasisiwa na James na Asher

Inatilia mkazo mfumo na muundo wa lugha.

Kama ilivyo nadharia ya usikizi nadharia hii pia inasisitiza umuhimu


wa kumudu mazungumzo kama sehemu ya umilisi wa lugha

Ufundishaji uhusishe mazoezi ya kurudia rudia ambayo angalau


unamfanya mwanafunzi kumudu anachojifunza
Nadharia hii inasisitiza matumizi ya vitendo na ishara mbalimbali
kama nyenzo mojawapo katika kujifunza lugha.

9. Mbinu ya upendekezi (suggestopidia method)

Ilianzishwa na Lonzano georgi (1979)

Nadharia hii inayapa mazingira bora ya ujifunzaji lugha kama nyenzo


muhimu mojawapo katika kujifunza lugha. Hii inamaanisha kwamba
mazingira yanayotumika kujifunzia lugha ni lazima yamkumbushe
mwanafunzi kile alichojifunza jana yake

Wanaelezea namna ya mkao wakati wa kufundisha wanafunzi wageni.


Mkao katika darasa uwe ni wa kutazamana, maana yake vikae kwa
duara.

Wanasisitiza matumizi ya mziki laini na mziki nyororo

1. MBINU YA MAWASILIANO (COMMUNICATIVE LANGUAGE


APPROACH)

Inasisitiza maingiliano na maathiriano katika ya mwalimu,


mwanafunzi na jamii

Wanakaza kwamba kujifunza lugha ni kujifunza kuwasiliana.

Kujua lugha kwa hakika sio kujua kanuni za lugha ile bali ni kujua
namna ya kuwasiliana na watu wa jamii ile kwa kuzingatia mikitadha
mbalimbali ambamo lugha hiyo inatumika

Ni nadharia ambayo imeshaididiwa na wataalam wengi akiwamo


Noamy Chomsky

Hii ndiyo nadharia ambayo inafaa kutumia kwa ajili ya kujifunza


lugha

VIWANGO VYA WANAFUNZI

Hapa inamaanisha uwezo alio nao mtu wa kutumia lugha Fulani.


Viwango hivi viliwekwa na shirika/taasisi moja isiyokuwa ya
kibiashara wala kiserikali liitwalo Interagence Language Round Table
(ILRT)
Kulingana na shirika hili wajifunzaji lugha wako katika viwango
vitatu

a) Wanafunzi wa daraja la msingi (Kisw.DAMSA) Beginners Level

b) Wanafunzi wa daraja la kati (DAKATI)Intermediate Level

c) Wanafunzi wa daraja la juu (DAJUU) Advanced Level


a) Wanafunzi wa daraja la msingi (Kisw.DAMSA) Beginners
Level

Daraja limegawanyika katika viwango hivi

Kiwango cha 0-mwanafunzi hawezi kabisa kuzungumza lugha


Kiwango cha +0-mwanafunzi amekaririshwa tu mahitaji muhimu
akibadilishiwa tu basi Amepotea
Kiwango cha 1-mwanafunzi anaweza kusitahimili mazungumzo ya
ana kwa ana ila hawezi kuanzisha mazungumzo
Kiwango cha +1-huyu anaweza kuanzisha mazungumzo yeye
mwenyewe, hata hivyo ni kwa ajili ya kukidhi matarajio yake

INTERMIDIATE

Daraja la 2-lugha si kamilifu lakini anaeleweka kwa urahisi


Kiwango cha 3-anaweza kuzungumza lugha kwa muundo sahihi, ana
msamiati wa mazingira fulani fulani tu ili kukidhi mahitaji ya
kitaaluma
Anaweza kukithi mahitaji ya kitaaluma

b) Wanafunzi wa daraja la kati (DAKATI)Intermediate Level

c) Wanafunzi wa daraja la juu (DAJUU) Advanced Level

CONTACT ME 4 MORE +255 763 059 054/+255 788 059 054


Share Your Passion
Create a professional website
and start blogging today

Get started

APRIL 22, 2014


LEAVE A COMMENT

You might also like