You are on page 1of 83

BLA 3226: THEORIES OF LITERARY CRITICISM

YALIYOMO
MHADHARIA WA KWANZA......................................................................................................1
NADHARIA ZA UHAKIKI WA FASIHI..................................................................................1
MHADHARA WA PILI................................................................................................................12
URASIMI MKONGWE WA KIMAGHARIBI........................................................................12
MHADHARA WA TATU............................................................................................................19
URASIMI MKONGWE WA WASWAHILI............................................................................19
MHADHARA WA NNE...............................................................................................................22
URASIMI MPYA WA KIMAGHARIBI..................................................................................22
MHADHARA WA TANO............................................................................................................30
URASIMI MPYA KATIKA FASIHI YA KISWAHILI...........................................................30
MHADHARA WA SITA..............................................................................................................37
UHALISIA.................................................................................................................................37
MHADHARA WA SABA............................................................................................................40
UHALISIA WA KIJAMAA – USULI......................................................................................40
MHADHARA WA NANE............................................................................................................47
UDHANAISHI/UTAMAUSHI.................................................................................................47
MHADHARA WA TISA..............................................................................................................55
UFEMINISTI.............................................................................................................................55
MHADHARA WA KUMI............................................................................................................60
NADHARIA ZINAZOHUSIANA NA MTINDO WA FASIHI...............................................60
MHADHARA WA KUMI NA MOJA..........................................................................................70
UJENGUZI, USEMEZANO NA UHALISIAJABU.................................................................70
MHADHARA WA KUMI NA MBILI.........................................................................................73
UJUMI-MWEUSI......................................................................................................................73
MHADHARIA WA KWANZA

NADHARIA ZA UHAKIKI WA FASIHI


Malengo

Baada ya mhadhara huu, mshiriki anafaa:

(a) Kubainisha vipengele vinavyotofautisha uhakiki na nadharia za uhakiki wa fasihi.

(b) Kuonyesha njia kuu za kuzalisha nadharia za uhakiki wa fasihi.

(c) Kuorodhesha vigezo vya kuainisha nadharia bora na kutoa mifano ya nadharia mwafaka.

Mwongozo huu umekusudia kumwongoza mshiriki kuzichanganua kazi za fasihi kwa njia ya

kitaalamu. Huu ni mwongozo tu. Mshiriki anatazamiwa kurejelea vitabu vingi na tahakiki nyingi

ili aweze kumudu uhakiki wenye manufaa. Natumaini kwamba mwongozo huu utakujulisha

japo kwa kiutangulizi namna ya kuhakiki kazi za fasihi.

Utangulizi

Katika maongozo huu, tunanuia kuzungumzia jinsi inavyofaa ya kusoma kazi ya fasihi.

Unapochukua riwaya, tamthilia au shairi na kuiweka mbele yako, huwa unafikiri nini kabla ya

kuanza kusoma? Je, usomaji wako huongozwa au huelekezwa na nini? Pengine umesikia hadithi

ya kaka sungura ikisimuliwa au ikitambwa. Au pending umeisoma katika kitabu fulani. Je, ni

mambo gani hukuongoza ili ukafahamu na kuyafurahia unayosoma? Usomaji wa kitaalamu wa

kazi ya fasihi unamuhitaji mwanafunzi au msomaji yeyote wa kazi ya fasihi kuelekezwa na

mwongozo fulani.

1
2.0 Nadharia

‘Nadharia’ ni istilahi ya kijumla inayomaanisha miongozo inayomwelekeza msomaji wa kazi ya

fasihi kuifahamu kazi ya fasihi katika vipengele vyake vyote. Nadharia ni maelezo ya jambo

kufungamana na vigezo vilivyowekwa au vinavyozalika kutokana na majaribio ya jambo hilo.

Hii ina maana gani? Ina maana kwamba nadharia inaweza kutokana na mawazo yaliyoundwa

kitambo na jopo la wataalamu au inaweza kutokana na usomaji makini wa kazi ya fasihi na mtu

binafsi. Katika hii hali ya pili pengine msomaji hana marejeleo maalumu yatakayomsaidia

kusoma kazi ya fasihi. Hivyo basi anapaswa kujitafutia vipimo vitakavyomwezesha kuisoma

kazi ya fasihi kwa utaratibu maalumu na kuainisha iwapo kazi hiyo imefaulu au haijafaulu. Kuna

nadharia nyingi kwa kuwa kila linalofanywa na mtu lina chembe za nadharia zinazoliongoza.

Nini maana ya nadharia?

3.0 Uhakiki

Uhakiki ni kazi au kitendo cha kutafakari, kuchambua na kufafanua kazi ya fasihi ili kuweka

bayana maadili na ujumbe uliomo katika kazi ya fasihi. Hivyo mhakiki sharti asome kazi ya

fasihi andishi au kusikiliza masimulizi ya fasihi simulizi kwa makini ili aweze kuyahakiki.

Eleza maana ya uhakiki

4.0 Shabaha za Uhakiki

Sababu za kuihakiki kazi ya fasihi ni nyingi. Moja kati ya sababu hizi ni kuifanya kazi

inayosomwa au inayosikilizwa kufahamika zaidi. Pili, uhakiki humzindua msomaji akapata

mshawasha wa kuisoma kazi ya fasihi upya. Katika uhakiki, mhakiki humfanya msomaji

2
mshiriki wake, akamkumbusha kutilia maanani baadhi ya mambo ambayo pengine hangetilia

maanani. Pamoja na haya uhakiki humsaidia mwandishi katika utunzi wa kazi zinazofuata zile

zilizohakikiwa. Huenda mwandishi arekebishe uandishi wake kufungamana na maelekezo ya

mhakiki. Au pengine kutokana na uhakiki, mwandishi atatilia mkazo zaidi mawazo fulani ya

kazi yake. Baada ya kuihakiki kazi fulani, mhakiki anaweza kuchambuliwa na mhakiki

mwingine. Jambo hili linaweza kusababisha maongezi baina ya wahakiki. Kutokana na

mazungumzo kati ya wahakiki tofauti tofauti, wasomaji wanaweza kufaidika zaidi. Shabaha

muhimu zaidi ya uhakiki ni kutoa uamuzi. Uamuzi hulenga kuonyesha iwapo kazi fulani

imefanikiwa au haijafanikiwa.

Kumbuka kwamba wasomaji wawili au zaidi wanaweza kusoma kitabu kimoja na wakatoa

uamuzi tofauti. Jambo hili litategemea udhibiti wao wa nadharia na tajriba zao kama wasomaji

wa kazi mbalimbali za fasihi.

5.0 Aina za Uhakiki

Kuna uhakiki wa aina mbalimbali:

(a) Uhakiki sadifa: Huu ni uhakiki unaotokea bila sababu maalumu. Kwa mfano unaweza

kusoma makala fulani na pasipo kutarajia ukatoa maoni yako.

(b) Marejeleo na bibliografia: Ni namna ya uhakiki wenye lengo la kuineza kazi fulani ya

fasihi. Kazi ambazo hazijulikani katika aina hii ya uhakiki hutangazwa na kujulikana.

(c) Uhariri: Ni uhakiki unaofanyiwa kitabu kabla ya kitabu hicho kuchapishwa. Katika

uhakiki wa aina hii, kitabu huweza kusahihishwa endapo kina makosa, mhariri hutoa

3
maoni yake, uzito na upungufu wa kazi inayoshughulikiwa. Baada ya kiwango hiki cha

uhakiki, muswada waweza kuchapishwa au kupigwa marufuku.

(d) Mapito: Haya hufanyiwa aghalabu kitabu kilichochapishwa hivi karibuni. Mapitio

hukijulisha kitabu kwenye umma mkubwa wa wasomaji.

(e) Ufundishaji: Unahusu ufafanuzi wa vitabu vya fasihi au masimulizi ya kifasihi. Uhakiki

unaweza kufanywa darasani, redioni, mihadharani au katika miongozo ya uhakiki

iliyotungwa na wahakiki. Katika ufundishaji wa fasihi, wanaofundisha wanatazamia

kwamba:

(i) Wanaofundishwa watakumbuka wanayofundishwa pengine kwa ajili ya kupita

mtihani.

(ii) Tajriba, hisia, mielekeo na mitazamo ya wafundishwao itabadilika kutegemea

mambo mapya wanayofundishwa.

(iii) Wafundishwao wataiga mitindo mipya ya uandishi na uhakiki na kuishilia kuwa

waandishi au wahakiki.

(f) Propaganda: Katika fasihi huu ni uhakiki unaosambaza malengo yasiyohusiana moja kwa

moja na fasihi. Uhakiki wa kipropaganda hufanywa kwa minajili ya kisiasa au kampeni

nyinginezo zisizojulikana.

(g) Upigaji marufuku: Ni uhakiki ambao hukusudia kupiga marufuku baadhi ya maandishi

kwa kuwa maandishi hayo hahaoani na maoni fulani katika jamii.

(h) Uhakiki wa kitaalamu:

Ni uhakiki ambao hufanywa na wataalamu, wasomi na wanachuo kwa kufuata kanuni

maalumu. Uhakiki wa aina hii huitathmini kazi ya fasihi kivyake na katika muktadha

wa kazi za fasihi nyinginezo.

4
Taja aina mbalimbali za uhakiki na uonyeshe jinsi zinavyoweza kumfaa msomaji wa
kazi ya fasihi

6.0 Nadharia za Uhakiki wa Fasihi

Nadharia za uhakiki wa fasihi ni miongozo inayomsaidia msomaji wa kazi ya fasihi kuifafanua

kazi ile kwa mujibu wa vigezo vilivyowekwa au vinavyozalika kutokana na uchunguzi wa aina

mbalimbali za fasihi. Pia, nadharia zinaweza kuchukulia kama jumla ya maelekezo

yanayomsaidia msomaji au mhakiki kuifahamu kazi ya fasihi kwa kufuata utaratibu maalumu.

Baadhi ya wataalamu wa fasihi wanapinga wazo la kusoma au kusikiza fasihi kutangamana na

mwongozo maalumu. Wapinzani hao wanadai kwamba badala ya kuitumia nadharia kuifafanua

kazi ya fasihi, msomaji anapaswa kukabiliana na kazi ya fasihi moja kwa moja kwa kuitumia

silika yake mwenyewe. Juu ya haya msomaji anayetumia silika yake atafaidika zaidi kwa kuwa

hataathirika na mawazo yasiyohusiana na imani zake za kimsingi.

Ukweli ni kwamba hakuna msomaji asiyekuwa na matarajio fulani kuhusu kazi anayosoma au

anayosimuliwa. Kutokana na malezi na tajriba tofautitofauti anazopitia mlimwengu huyo huwa

kitambo ana kusanyiko la mawzo yanayomwelekeza katika shughuli mbalimbali anazofanya.

Lugha ni chombo muhimu kinachosheheni utamaduni wa mtu. Nao utamaduni ni jumla ya kadia

zote anazofanya mtu katika maisha yake. Utamaduni unahisisha historia na matambiko

mbalimbali wanayofanya walimwengu katika harakati ya kuishi.

5
Utamaduni ni mila, asili, jadi na desturi za kundi la jamii fulani. Ni mila, asili na jadi za kundi

fulani au jamii fulani.

Kwa nini kitendo cha kusoma hakiepuki kitendo cha uhakiki? Eleza maana ya utamaduni.

Kwa sababu mtu hukulia katika muktadha wa kibinadamu, huwa kitambo amejikusanyia zana

mbalimbali za kuchujia hali mbalimbali za maisha yake zilizomzingira. Nadharia za uhakiki wa

fasihi humzindua mtu akajua kwamba usomaji mzuri hufanywa katika mipaka inayofahamika

wazi. Nadharia za uhakiki wa fasihi zinaweza kuchukuliwa kuwa moingozo au mikakati

maalumu inayomsaidia msomaji ili afaidike zaidi kutokana na kitendo cha kusoma. Nadharia za

uhakiki wa fasihi hulufanya tendo la uhakiki kuwa ni la makusudi kwa kuwa msomaji

analazimika kuwa na malengo maalumu wakati wa kuihakiki kazi ya fasihi.

Utumiaji wa nadharia za uhakiki wa fasihi unalenga nini?

7.0 Aina za Nadharia

Aina za nadharia zinatokana na jinsi nadharia hizo zilivyoundwa.

(a) Nadharia asilia: Hii ni nadharia isiyotokana na nadharia nyingine yoyote. Nadharia asilia

inajitosheleza na haina uhusiano wa moja kwa moja na nadharia nyingine.

Tunapozingumzia nadharia ya uhalisia, tuna maana ya jinsi ya kuzitunga na kuzihakiki kazi

maalumu za fasihi.

(b) Nadharia nyambuaji – ni nadharia iliyokuwepohapo awali. Kwa hivyo nadharia ya aina hii

ni kimelea cha nadhaaria iliyoitangulia. Kwa mfano, vigezo vinavyoubanisha urasimi wa

6
kimagharibi ni uigo na ufuasi wa sheria. Urasimi-mpya ni kimelea cha urasimi mkongwe.

Umejengeka kwenye kufuata sheria.

(c) Nadharia changamano – ni nadharia ambayo imeundwa kutokana na nadharia mbili au zaidi.

Kuna nadharia inayoitwa uhalisia. Pia, kuna mfumo wa kuzalisha mali ambao unaitwa

ujamaa. Uhalisia ni nadharia ya kutunga na kuhakiki kazi za fasihi inayonuia kuionyesha

jamii katika uyakinifu wake. Nao ujamaa ni mfumo unaolenga kuwasawazisha walimwengu

wote kwa vile ambavyo wanapaswa kuwa na mahusiano sawa na njia za kuzalisha mali.

Yaani wanadamu wote wanapaswa katika mfumo huu kuwa katika tabaka moja kiuchumi.

Sasa uhalisia wa kijamaa.

Kumbuka: Nadharia ni nyingi lakini ni za aina tatu pekee!


Kwa kifupi, nadharia asilia haina uhusiano na nadharia nyingine yoyote, iwe inayoitangulia au

inayoifuata. Urasimi, uhalisia na ulimbwende ni nadharia asilia. Nadharia nyambuaji ni kimelea

cha nadharia nyambuaji. Hatimaye nadharia changamano inajumuisha zaidi ya nadharia moja

ambayo historia yake hailingani. Mfano mzuri wa nadharia changamano ni uhalisia wa kijamaa

na ufeministi wa kidhanaishi.

Eleza tofauti kati ya nadharia asilia, nadharia nyambuaji na nadharia mchangamano

8.0 Nadharia Mwafaka

Pamoja na kwamba kuna aina tatu za kuzalisha nadharia, si lazima kila nadharia inayoundwa iwe

bora. Ubora wa nadharia unatokana na utendakazi wake. Baadhi ya vigezo viinavyoianisha

nadharia mwafaka ni:

7
(a) Nadharia bora inapaswa kutokana na majaribio mengi na uchunguzi mwingi. Nadharia

inayotegemewa inatazamiwa kutokana na usomaji wa vitabu vingi au usikilizaji wa

ngano nyingi, ikiwa shughuli la utafiti linahusiana na utanzu huo wa fasihi simulizi.

(b) Nadharia nzuri pia ina sifa ya umfumo. Mfumo ni mpangilio ambao una vipengele

vinavyojengana na kukamilishana. Nadhaira nzuri inaf`anya kazi kama mfumo. Inajaribu

kufafanua mambo yote yanayopatikana katika kazi fulani ya fasihi.

(c) Ubora wa nadharia unatokana na jinsi ianvyoelezwa. Ikiwa nadharia haiwezi kuelezwa

kwa ufasaha, basi hiyo si nadharia mwafaka. Nadharia inayoelezwa kwa ufasaha

itatumiwa kueleza kadhia nyingine za kifasihi kwa ufasaha.

(d) Swali jingine ambalo huulizwa katika kuiteua nadharia bora ni: Je, hii nadharia ina

manufaa kwa muundaji wake? Nadharia nzuri ni ile ambayo muundaji wake una imani

kwamba ina thamani kwa watumiaji wake. Pia nadharia nzuri inapaswa kuwa na manufaa

kwa yeyote anayetaka kuitumia.

(e) Hatimaye nadharia nzuri hubadilika endapo sababu zitatokea zitakazolazimisha

kubadilika huko.

Nadharia mwafaka ni nadharia ya aina gani?

9.0 Sura za Nadharia

Nadharia ni nyingi na zinasawirika katika sura mbalimbali ziwe asilia, nyambuaji au

changamano.

(a) Nadharia inaweza kuchukuliwa kama mwongozo unaomsaidia msomaji kuifahamu kazi ya

fasihi vizuri zaidi. Mwongozo mzuri ni ule unaomfafanulia msomaji maeneo mbalimbali ya

kazi ya sanaa yanayotazamiwa kushughulikiwa. Kitabu cha Al-Amin Mazrui Uchambuzi

8
wa Riwaya na Mwongozo wa Mui Huwa Mwema kinaorodhesha baadhi ya vipengele

vinavyotarajiwa kuzingatiwa katika uhakiki wa riwaya.

(b) Nadharia inaweza kujibainisha kama sheria za kutunga na kuhakiki kazi za fasihi. Ars

Poetica cha Horace ni mfano mzuri wa italiki nadharia zinazojidhihirisha kama sheria. Lau

sheria hizo hazifuatwi, waitifaki wake watachukulia kwamba kazi ya sanaa haijafanikiwa.

(c) Dhima nyingine ya nadharia huonekana pale ambapo nadharia huwa mkakati wa kusoma.

Dhima hii ya nadharia inasisitiza mitazamo maalumu inayosisitizwa katika nadharia fulani

na ambayo inaweza kuajiriwa kusoma na kutathmini kazi za sanaa. Katika miaka ya sabini

na themanini tasnifu nyingi zilizoandikwa na wanafunzi wa vyuo vikuu nchini Kenya

zilitumia mkakati wa kijamaa – kuzithathmini.

(d) Baadhi ya nadharia husisitiza ujarabati katika kuisoma kazi ya sanaa. Ujarabati ni ufafanuzi

wa ujuzi unaozingatia mambo halisi yanayoonekana, yanayoshikika na yanayohisika kwa

fikra na mishipa ya fahamu. Nadharia kama umaumbo itanuia kuonyesha sifa za kazi za

utanzu wa fasihi kwa kutilia maanani sifa za utanzu ule.

(e) Tulipokuwa tukizungumzia nadharia mwafaka, tulitaja kwamba nadharia bora ile

inayoshughulikiwa fasihi kimfumo. Vivyo hivyo, nadharia inaweza kutazamwa kama

usomaji wa kimfumo. Nadharia ni kama njia ya kusoma inayozingatia kazi ya fasihi katika

vipengele vyake vyote. Miongozo mingi ya fasihi imeandikwa kwa kufuata nadharia hii.

Katika miongozo mizuri riwaya au tamthilia zinashughulikuwa katika vipengele vyake

vyote – kuanzia maudhui, mtindo na hata muktadha uliomzaa mwandishi.

(f) Hatimaye, nadharia wakati mwingine huchukuliwa kuwa usemaji unaolenga kuwawezesha

baadhi ya wanajamii kuwamiliki wengine.

9
Wananadharia wengi wa wakati wetu wakiwemo Edward Said na Michel Foucault wanafikiria

kwamba njia teule za usemaji zimeumbwa ile zitumiwe kuutawala ulimwengu. Kama ambavyo

watawala wa kisiasa hujiteua katika matabaka maalumu, njia za kuuzungumzia ulimwengu pia

zimegawanywa katika matabaka maalumu. Nadharia za uhakiki wa fasihi ni vivyo hivyo.

Zinaweza kutumiwa kuainsiha matamshi mateule kutokana na matamshi duni – au ambayo

hayathaminiwi sana na wanajamii.

10.0 Nadharia na Historia

Nadharia kama ambavyo zilivyo amali nyingine za kijamii ni zao la utamaduni na historia ya

jamii inayohusika. Nadharia huzuka na hutumiwa kufungamana na maswala ya kihistoria

yaliyoizalisha. Hata hivyo baadhi ya maswala yanayozungumzia katika baadhi ya nadharia za

uhakiki yanapiku muktadha maalumu wa kihistoria. Ingawa nadharia nyingi ni zao la muktadha,

baadhi ya nadharia zinaweza kutumiwa katika miktadha tofautitofauti na kudhihirisha kwamba

wakati mwingine maswala ya kinadharia yanapita maswala ya miktadha maalumu. Kufanana

kwa baadhi ya nadharia kunthibitisha kuwa endapo maswala yanayoshabihiana yatazuka katika

maeneo mbalimbali basi yatasuluhishwa kwa njia zinazofanana.

Nadharia zitakazozungumziwa katika kazi hii zimeangaliwa kwa kuzingatia maswala ya

kihistoria ili kuzipa mtazamo wa kueleweka katika mpito wa wakati.

Onyesha tofauti zilizopo kati ya Uhakiki na Nadharia ya Uhakiki

Marejeleo

Craig, David. Marxist on Literature. Harmondsworth: Penguin, 1975

10
Keesey, Donald. Contexts for Criticism. London: Toronto, 2003

Mazrui, Al. Amin. Uchambuzi wa Riwaya. Mwongozo wa Mui Huwa Mwema. Nairobi.

Longman, 1981.

Wamitila, W. K. Kamusi ya Fasihi. Istilahi na Nadharia. Nairobi: Focus Books 2003.

Wafula, R. M. na Kimani, Njogu: Nadharia za Uhakiki wa Fasihi. Nairobi. Jomo Kenyatta,

2007.

MHADHARA WA PILI

URASIMI MKONGWE WA KIMAGHARIBI


2.1 Malengo

(a) Kufafanua maana na sifa za urasimi kwa ujumla na kutambua kwamba kila jamii ina

urasimi wake.

(b) Kuainisha warasimi wakongwe wa kimagharibi, kueleza mawazo yao kuhusu fasihi, na

kuorodhesha mihimili ya mikondo yao ya kirasimi.

(c) Kulinganisha na kulingana maoni ya Plato na Aristostle juu ya fasihi.

Urasimi ni wakati maalumu ambapo misingi ya kazi za sanaa huwekwa na kukubalika kuwa

vipimo bora kwa kazi nyingine. Hii ina maana kwamba kila jamii ina urasimi wake. Urasimi

katika fasihi ya Kiswahili ulikuwepo kati ya karne ya nne (K.K) na takribani karne ya nne (B.K).

11
Ni jambo la kusikitisha kwamba mara nyingi wasomi wanapozungumzia urasimi, huwa na

maana ya misingi iliyowekwa na Wagiriki na Waroma wa kale. Yaelekea kwamba ukosefu wa

uthibati za kutosha kutoka katika jamii nyinginezo umetufanya kurejelea urasimi wa kimagharibi

kama chanzo cha kila kitu.

2.2 Sifa za Urasimi kwa Ujumla

(i) Kazi ya kirasimi huwasilishwa katika lugha inayoeleweka kwa urahisi. Hii ina maana

kwamba wazo linaelezwa moja kwa moja. Mitindo ya kinjozi haitumiwi. Uhalisia

unasisitizwa.

(ii) Kwa kuwa kazi ya kirasimi ni mfano bora, haichoshi kusoma. Husomwa mara nyingi na

kila inaposomwa jambo jipya hupatikana mle. Umberto Eco katika kitabu chake What is

a Classic? ameasema kiutani kwamba kazi ya kirasimi huwa imesomwa na wote. Na hata

yule ambaye hajaisoma atajitia kaisoma, kwamba amesome. Huu unafiki watokana na

umuhimu wa kazi ya karasimi.

(iii) Maudhui na mtindo katika kazi ya kirasimi ni mambo yaliyofinyangwa kwa kutumia

mbinu kamilifu na teule. Daima kuna ufungamano uliokamilika kati ya kinachoelezwa na

jinsi kinavyoelezwa mawazo ya mtunzi binafsi.

(iv) Mwanasanaa anayetunga kazi ya kirasimi humezwa na mkondo wa fikra uliomzalisha.

Haiwezekani kuyaanisha.

Urasimi Mkongwe wa Kimagharibi

12
Ni kupotosha ukweli kufikiria kwamba urasimi ulianzia Ugiriki au Uroma. Kila jamii ina

urasimi wake. Hata hivyo, kwa sababu ya ukosefu wa rekodi za kutosha kutoka jamii

nyinginezo, wataalamu wengi hurejelea urasimi wa Ugiriki na Kiroma kufahamu sifa za urasimi

wa jamii nyinginezo.

Nini maana ya Urasimi? Urasimi mkongwe ni nini?

Ijapokuwa kuna warasimi wakongwe, tutazungumzia watatu kuwakilisha wengine.

Tutazungumzia Plato, Aristotle na Horace.

Plato alikuwa mwanafilosofia wa Kigiriki. Aliishi kati ya mwaka 428 na mwaka 348 kabla ya

Yesu Kristo kuzaliwa. Plato alikuwa na hoja mbili kuu kuhusu chanzo cha fasihi na sifa za fasihi.

Chanzo cha fasihi, Plato anasema ni jadhba inayotokana na miungu wa sanaa. Jadhba au jazba ni

aina ya pepo linalomwingia nabii kabla hajaanza kubashiri au kuagua yale yatakayotokea

baadaye. Vivyo hivyo Plato anashikilia kwamba mwanasanaa hupangdwa na jaziba kabla ya

kutunga kazi ya sanaa.

Kuhusu sifa kuu ya fasihi, Plato, anasema kwamba fasihi ni uigaji wa mazingira na hali

nyinginezo anamopatikana binadamu. imani ya Plato inatokana na nadharia yake kuhusu jinsi

ujuzi na mawazo huzaliwa. Kwake Plato vitu vyote vilivyomo humu duniani ni taswira hafifu ya

vitu hivyo kama vianvyobainika katika ulimwengu dhahania, ambao ndio ulimwengu halisi wa

kiplato. Ulimwengu huu ndio yakini kwa mujibu wa maelezo ya Plato. Kutokana na maelezo ya

Plato, vitu vilivyomo ulimwenguni haviwasilishi ukweli. Kinyume na haya, huwasilishwa

taswira ambazo zimekengeuka mara tatu kutokana na ukweli wa kiuplato.

13
Pamoja na kusema kwamba uigaji si yakini, Plato anasisistiza kwamba huo uigaji hupotosha

maadili. Wahusika katika sanaa ya uigaji hubadilishana nyadhifa pasina kujali viwango vya

uadilifu vya viumbe vinavyoigizwa. Kutokana na imani hii, Plato anaipigia marufuku fasihi.

Hata hivyo baadaye anasema kwamba iwapo kutaundwa kamati ya majaji wazee watakaoichuja

fasihi kuainisha ile inayofaa kusomwa au kusikilizwa na wanajamii wa Jamhuri yake dhahania,

basi fasihi hiyo itakubalika katika Jamhuri yake.

Maelezo ya Plato yanamfundisha mwanafunzi wa fasihi mihimili kadha ya nadharia yake:

(i) Fasihi inatokana na uigaji wa mazingira ya mtu

(ii) Fasihi inapaswa kuhakikiwa

(iii) Lengo kuu la fasihi ni kuadili na isippfanya kazi hii ya kuadili, inaweza kupigwa

marufuku.

Eleza misingi ya ujuzi wa Plato. Je, msingi huu inaathiriaje ufafanuzi wake wa fasihi?

Marejeleo

Plato, ‘Kitabu cha Kumi’, The Republic, New York: Barnes & Noble, Inc. 1999.

Rajan, B & A. G. George (Wahariri): Makers of Literary Criticism Vol. 1 London: Asia

Publishing House, 1965.

ARISTOTLE

Alikuwa mwanafunzi wa Plato. Ingawa hakuna ushahidi kwamba Atistotle alinuia kumpinga au

kumjibu Plato moja kwa moja, mawazo na mapendekezo yake yanadhihirisha kwamba

14
alifahamikiwa na fikra za mwalimu wake. Aristotle anayarejelea maswala yayo hayo

aliyoyazungumzia Plato. Anakubaliana na Plato kwamba fasihi ni sanaa inayoiga mazingira

yaliyomzunguka mtu. Hata hivyo, hali hii ya kuiga ndio huifanya fasihi kutukuka. Aristotle

anasisitiza kwamba fasihi haigi kikasuku: kinyume na haya fasihi huiga kiubunifu kwa

kuzingatia mambo yanayoathiri maisha ya binadamu. fasihi humtukuza mwanadamu, sifa zake

za kuweza kuumba zikamleta karibu na mwenyezi Mungu.

Aristotle alitumia ujuzi wa mwanasayansi asili kufikia maamuzi yake. Mwanasayansi asili

hutumia mishipa yake ya fahamu kufanya majaribio na kufikia uamuzi kuhusu kadhia

mbalimbali anazochunguza. Aristotle anaanza ziara yake kwa kutambua orodha ya tanzu za

fasihi zinazopatikana katika ujirani wake. Baadhi ya tanzu za fasihi anazotambua ni nyimbo

ambazo hughaniwa pamoja na ala za muziki kama zeze au kinibi, futuhi na tanzia. Tanzu za

fasihi zinagawanywa katika makundi tofauti tofauti kulingana na:

(i) Usawiri wa wahusika:

- Wahusika wanaweza kuchorwa katika upotovu wao (futuhi) au katika utukufu wao

(tanzia)

- Wahusika wanaweza kusawiriwa kiunyakinifu bila kupigiwa chuku au kudunishwa

kupita kiasi.

(ii) Kuchanganya masimulizi na maongezi: Mtunzi anaweza kuchanganya masimulizi na

maongezi kama anavyofanya Homer katika tenzi zake.

15
Kilele cha juu ya kuzungumzia tanzu mbalimbali za fasihi kinafika wakati ambapo Aristotle

anazungumzia tanzia. Katika kufanya hivi Aristotle anazungumzia asili na dhima ya fasihi na

wakati huo huo kutupilia mbali mawazo ya Plato.

Kwa mujibu wa maelezo ya Aristotle, tanzia ni maigizo ya matukio yenye ujume mzito

yanayowasilishwa kwa lugha inayonawiri, yazindue hofu na huruma ili hatimaye maigizo hayo

haripue hisia za ndani kutoka katika nafsi za hadhira.

Tanzia ina sehemu tatu muhimu: Mwanzo, katikati na mwisho. Hatimaye kutokana na uchunguzi

wa Aristotle, tanzia nyinge za kigiriki zilikusudia kuthibitisha kwamba ‘jitihada haiondoi

kudura’. Juu ya sifa hii, katika tanzia ya kigiriki kuna mabadiliko katika mkondo wa matendo

yanayofanyika hivi kwamba mhusika mkuu hujikuta katika hali zilizo kinyume na matarajio

yake. Taharuki, vinyume vya mambo na kejeli huyakumba maisha ya mhusika mkuu. Pia,

mhusika tanzia ana fahari inayomsukuma hadi mwisho wa maisha yake. Fahari hiyo wakati

mwingine huwa ni ‘kiburi’ ambacho humshurutisha mhusika kuishilia katika hali ya

kuhuzunisha. Hatimaye, maadili hukusanywa na kutolewa na ‘wazee’ kuhusiana na tajriba

alizopitia mhusika mkuu. Tamthilia alizotumia kama data kufikia sifa za tanzia ni zile za mtunzi

mashuhuri wa kigiriki, Sofokile. Miongoni mwa tamthilia hizi ni Mfalme Edipode na Antigone.

Antigone ilitafsiriwa katika lugha ya Kiswahili mnamo mwaka wa 2009 na R. M. Wafula.

Soma tamthilia ya Sofokile ya Mfalme Edipode au Antigoni.


Ainisha na ufafanue sifa za tanzia alizoziona Aristotle.

16
Aristotle na Mihimili ya Fasihi kwa Ujumla

(i) Anasema kwamba fasihi si uigo wa kikasuku. Ni ubunifu unaomwezesha binadamu

kumkaribia Mungu.

(ii) Ploti au msuku ni muhimu katika ubunifu wa sanaa. Jambo hili linaonyeshwa pale

ambapo Aristotle anazungumzia tanzia na utendi.

(iii) Aristotle anatuonyesha kwamba fasihi itaeleweka vizuri zaidi ikiwa itagawanywa

katika tanzu tofauti tofauti.

Soma tamthilia ya Kinjeketile iliyotungwa na Ebrahim Hussein. Ainisha baadhi ya sifa


zake za kitanzia.
Je, maoni ya Aristotle yanakusaidia aje kutambua sifa hizo.

Marejeleo

Daiches, Davice. Critical Approaches to Literature. London: Longman, 1986.

Dorsch, S. T. (Mhariri): Classical Literary Criticism. London: Penguin, 1965.

Wafula, R. M. (Tafsiri): Antigoni. Nairobi. Longman, 2009

HORACE

Alikuwa Mroma. Horace aliyachukua mawazo ya Aristotle na kuyageuza kuwa sheria

zilizopaswa kufuatwa na watunzi chipukuzi. Katika makala yake, The Art of Poetry ambayo

yamenukuliwa na S. T. Dorsch katika kitabu cha Classical Literary Criticism, Horace

anaorodhesha baadhi ya haya maelekezo:

(i) Fasihi lazima ilenge kuadili na kusisimua.

(ii) Tamthlia lazima iwe na maonyesho matano.

(iii) Utungaji mzuri unatokana na uigaji wa kazi watunzi mashuhuri walioishi zamani za kale.

17
Soma tamthilia ya Kithaka wa Mberia, Kifo Kisimani. Kuna masharti yoyote ya Horace humo?

MHADHARA WA TATU

URASIMI MKONGWE WA WASWAHILI


Malengo

(a) Kubainisha sifa za nadharia madhubuti.

(b) Kuorodhesha baadhi ya kazi za kisanaa za urasimi mkongwe wa Kiswahili.

(c) Kuhitamidi kutokana na kazi hizo mihimili ya urasimi mkongwe wa Kiswahili.

Urasimi mkongwe wa Waswahili ni nadharia asili; lakini vile vile ni nadharia madhubuti.

Nadharia madhubuti ni nadharia inayotokana na deta zilizokusanywa au kuandikwa na

18
kuchanganuliwa. Kutokana na uchanganuzi huo mihimili ya nadharia inaweza kuhitamidiwa.

Yaani, kutokana na sifa mahsusi za kazi zilizoandikwa katika kipindi urasimi mkongwe,

zinaweza kuchujwa na mihimili yake kupatikana.

Kazi za kirasimi katika fasihi ya Kiswahili zipo. Hata hivyo uhakiki wa kirasimi kuhusu kazi

hizo ni nadra kupatikana. Msomaji wa kazi za kirasimi katika fasihi ya Kiswahili anapaswa

kuhitamidi uhakiki wake kutokana na utunzi wenyewe. Urasimi wa fasihi ya Kiswahili ulifikia

kilele chake katika karne ya 18 na 19 katika enzi yetu. Urasimi mkongwe wa Kiswahili ni

nadharia ya kimkondo na kiwakati.

Huenda Utenzi wa Tambuka au Chuo cha Herekali ulioandikwa na Mwengo bin Athumani

(1728) ndio wa kwanza kuandikwa katika lugha ya Kiswahili. Katika mwaka wa 1749, Said

Aidarus alitoa tafsiri ya utenzi kutoka Misri uliotwa Umma-Ul-Quarra au Kasidatul Hamziya.

Baadhi ya wataalamu wanafikiria kwamba Utenzi wa Umma-Ul-Quarra ulitafsiriwa mnamo

mwaka wa 1690. Kazi nyingine zilizoandikwa wakati huu zilikuwa Al-Inkishafi (1810 – 1820),

Utenzi wa Mwanakupona ambao tarehe za kutungwa kwake hazijulikani kwa uhakika. Ukweli ni

kwamba tarehe za kutungwa kwa tenzi hizi ni za kukisia. Hata hivyo imekubalika kwamba

nyingi ziliandikwa kati ya Karne ya 18 na nusu ya kwanza ya Karne ya kumi na tisa.

Ni nini maana ya Nadharia Madhubuti?

Kutokana na maoni ya E. Kezilahabi (1983), Kimani Njogu na Rocha Chimerah (1999) na

R.M.Wafula & Kimani Njogu(2007):

(i) Al-Inkishafi ndio utenzi wenye uzito wa falsafa na usanii.

19
(ii) Hamziya nao unatumia lugha ya kale zaidi kupita tenzi zote. Mtunzi wake anatumia

lahaja ya kingozi.

(iii) Utenzi wa Mwanakupona ndio utenzi mashuhuri zaidi uliondikwa na mwanamke.

(iv) Kwa upande wa mashairi ya unne (tarbia), watunzi waliosifika zaidi walikuwa Muyaka

wa Muhaji, Mohammed Mataka na Ali Koti.

Sifa za Fasihi ya Kiswahili katika Misingi ya Kirasimi

(i) Huu ndio wakati ambapo misingi ya ushairi andishi wa Kiswahili ilipowekwa.

(ii) Mengi ya mashairi ya kirasimi yalipokezwa kwa mdomo na uhakiki pia ulifanywa kwa

njia ya kimasimulizi. Katika majibizano mbalimbali, katika ‘kufungiana na kufunguliana

nyamba’, watunzi na wahakiki waliweza kuchamguliana kazi zao.

(iii) Ingawa Waswahili hawakuwa na wahakiki wanajulikana wazi, inathibitika kutokana na

tungo zao kwamba utungaji wa fasihi yao ulitokana na mazingira ambamo anapatikana

mwanadamu.

(iv) Mashairi yalitumia lugha teule.

Some utenzi wa Al-Inkishafi na baadhi ya mashairi ya Muyaka kuthibitisha madai


haya.

Kama walivyo watunzi wa kirasimi wa mahali popote na wakati wowote, warasimi wa

Kiswahili walitumia lugha rahisi iliyoeleweka na ujirani wao bila shida yoyote.

(v) Pia, washairi wa kirasimi wanazingatia arudhi katika utunzi wao, jambo linalomwezesha

mhakiki wa zama zetu kuuainisha ushairi wao katika tanzu mbalimbali.

20
(vi) Masimulizi marefu kama utnezi yana mwanzo, katikati, na hatima yake. Inapaswa

kukumbukwa kwamba:

Soma utendi wa Al-Inkishafi. Jaribu kuugawa katika sehemu mbalimbali, yaani


mwanzo, katikati na mwisho.

Tendi zinaanza kwa njia ile ile

Nini tofauti kuu kati ya urasimi wa kimagharibi na urasimi wa fasihi ya Kiswahili?

Marejeleo

Abdulaziz, Mohamed Hassan. Muyaka: 19th Century Popular Swahili Poetry. Nairobi: Kenya

Literature, 1979.

Chiraghdin, Shihabdin. Malenga wa Karne Moja. Nairobi. Longman, 1987.

Kezilahabi, Euphrase. ‘Uchunguzi katika Ushairi wa Kiswahili’. Makala za Semina ya Kimataifa

ya Waandishi wa Kiswahili III: Fasihi. Dar es Salaam: Taasisi ya Uchunguzi wa

Kiswahili, 1983.

Njogu Kimani & Rocha Chimerah. Ufundishaji wa Fasihi: Nadharia na Mbinu. Nairobi. Jomo

Kenyatta Foundation, 1999.

Wafula, R.M. & Kimani Njogu. Nadharia Za Uhakiki wa Fasihi. Nairobi: Jomo Kenyatta

Foundation, 2007.

Wa Mlamali, Muhammad. Inkishafi. Nairobi. Longman, 1980.

21
MHADHARA WA NNE

URASIMI MPYA WA KIMAGHARIBI


Malengo

(a) Kufika mwisho wa mhadhara huu mshiriki anapaswa kutoa hali zilizosababisha kuzuka

kwa urasimi mpya wa kimagharibi.

(b) Mshiriki anatazamiwa kutaja majina ya waasisi wa urasimi wa kimagharibi na

kuorodhesha sifa za fasihi za wakati wao.

(c) Mshiriki anatarajiwa kuorodhesha mihimili ya urasimi mpya wa kimagharibi.

(a) Urasimi Mpya wa Kimagharibi

Nadharia hii ya fasihi inaitwa urasimi mpya kwa sababu kanuni zake nyingi zilitokana na

urasimi-asilia uliotokana na Wagiriki na Waroma wa kale. Kipindi cha urasimi mpya

kilishuhudia ufufuo wa kanuni na kaida zilizoheshimika na warasimi katika kuitathmini fasihi.

Hata hivyo, mtazamo huu wa fasihi haukufuatana moja kwa moja na urasimi mkongwe.

Takribani miaka 1700 ilipita baada ya urasimi mkongwe kabla urasimi mpya kuanza.

Miaka iliyotangulia urasimi mpya haikudhihirisha ubunifu unoastahili kurejelewa katika

mawanda ya fasihi. Baada ya kuanguka kwa utawala wa Kiroma na tamalaki zilizofuatia,

ambazo ziliibuka katika ujanibu wa mji wa Constantinople, ulimwengu wa Kimagharibi

ulitawaliwa na enzi ya giza. Ilikuwa kana kwamba saa ya historia ya Ulaya ilikuwa imesimama

kwa kuwa hakuna ithibati ya uvumbuzi muhimu uliokuwepo kabla ya kipindi cha urasimi mpya

kutokea.

22
Karne ya 17 na 18 katika mapisi ya kimagharibi zimehusishwa na ufanisi wa kisiasa, kijamii na

kisayansi. Pamoja na utengemano wa kisiasa kuwepo, watu wa karne hizi walikuwa na

matumaini ya kuiona kesho nzuri. Njia za kisayansi za kudadisi ulimwengu zilikuwa zimetia

fora. Huu ulikuwa wakati wa Galileo mnajimu, Kepler mwanahesabu, Newton mwanasayansi

asilia na Descartes, mwanafalsafa. Watu wengu walithamini ujuzi uliotokana na ujarabati.

Ujarabati ni ufafanuzi wa ujuzi unaozingatia tu mambo halisi yanayoshikika na yanayohisika

kwa fikra na mishipa ya fahamu.

Kuna uhusiano gani kati ya urasimi mkongwe Kimagharibi na urasimi mpya wa


Kimagharibi?

Hata imani kwamba Mungu yupo ilipaswa kuthibitishwa. Kuwa kuwa wakazi wa karne hizi

waliyajua mazingira yao kwa udhahiri, walikuwa na tumaini la kuudhibiti ulimwengu wao

vilivyo. Hatimaye, watu hawa walifikiria na kusadiki kwamba maendeleo na ufanifu wa

binadamu ulikuwa karibu kufikia kilele. Enzi hii ilikumbusha kipindi alichotawala kaizari

Agosto. Enzi ya kaizari Agosto ilikuwa na amani na utengemano hata ikadiriki kuitwa ‘Pax

romana’. Yaani amani ya Roma. Wanajamii wa kipindi cha urasimi mpya walikiita kipindi hicho

‘enzi ya Agosto’. Ilikuwa kama kwamba ustaarabu wa Ugiriki na Uroma wa kale ulikuwa

umezaliwa upya.

(b) Fasihi na Urasimi Mpya wa Kimagharibi

Fasihi nayo ilijidhihirisha vipi katika mazingira haya ya matumaini ya Kisayansi? Wasanii weng

waliamini kwamba fasihi nzuri ilitokana na Ugiriki na Uroma wa kale. Wanasanaa

walizichimbua kazi zilizotungwa zamani na kuzichambua kwa uangalifu. Kisha wakaianisha na

kuirodhesha miundo na mitindo iliyofuatwa na wakongwe katika utungaji wa uhakiki wa kazi

23
zao. Walizichambua tahakiki za wataalamu wa kale kama Plato, Aristotle, Horace na Ovid na

kutunga zao kwa kuzingatia miongozo ya watangulizi wao.

Kama ilivyogusiwa hapo awali, katika urasimi mpya wa Kimagharibi, wanajamii waliabudu

misingi ya kisayansi katika utekelezaji wa miradi yao ya kitaalamu. Wanafasihi hawakuachwa

nyuma katika shughuli hizi. Mitindo ya kisayansi ilibainika katika utunzi na uhakiki wa kazi zao.

Kwanza, waliepukana na tungo za kinjozi na kidhahania. Tungo za aina hii zilishukiwa kuwa

uzushi. Lugha halisia ilihimizwa. Wahakiki waliunda na kukusanya msamiati uliotumiwa

kuainishia tanzu mbalimbali za fasihi. Kwa kufanya hivi, walikuwa wakiwaiga wanasayansi hasa

wataalamu wa elimu-uhai waliozua msamiati wa kubainisha pande tofauti tofauti za ujuzi wao.

Ikiwa wanabaolojia waligawa maumbile katika vikundi mbalimbali, wanfasihi nao waligawa

fasihi katika tanzu mbalimbali. Kwa kifupi, fasihi iliathiriwa na sayansi. Hata na waandishi

waliotumia kejeli kushambulia maovu ya kijamii walipata motisha wa kufanya hivyo kutoka kwa

wanasayansi. Kipengele cha kejeli kilikuzwa kuwatusia wataalamu bandia.

Wahakiki muhimu wa kipindi hiki walikuwa Samuel Johnson, Alexander Pope na Johna Dryen.

Nao watunzi walikuwa Jonathan Swift, John Milton na Edumund Spenser miongoni mwa

wengine. Moja kati ya makala muhimu yaliyoorodhesha kanuni za fasihi kama zilivyoelekeweka

na warasimi wapya yaliitwa Essay on Criticism (Pope).

Fasihi ilifaidika vipi kutokana na sayansi katika nadharia ya urasimi mpya wa Kimagharibi?

24
(c) Mihimili ya Urasimi Mpya wa Kimagharibi

(i) Wahakiki wengi wanaopatikana katika muhula huu wanakubaliana kwamba kaida za

mazoea maalum yanapaswa kufuatwa katika utungaji wa kazi za fasihi. Katika Essay on

Criticism, Pope anasema kwamba kama ambavyoo kuna kawaida zinazokubalika na watu wengi

katika mavazi, maandalizi ya maakuli na maposo, kuna taratibu zinazopaswa kufuatwa katika

uandishi wa fasihi.

Pope anarejelea mifano mbalimbali kudhihirisha ukweli na ustahiki wa madai yake. Mtu huvaa

mavazi kufungamana na sherehe au dharura anayotazamia kuhudhuria. Hapana haja ya kuvaa

sare safi na viatu vinavyonawiri ikiwa lengo na kwenda bustanini na kulima. Kufanya hivyo ni

kujidunisha kwa vile kunakiuka matendo yaliyozoeleka. Stiari ya nguo na sherehe imetumiwa na

Pope kuonyesha kwamba uzuaji wa maudhui na mitindo ya fasihi ni mambo yanayopaswa

kuoanishwa na mazoea ya wafinyanzi wa fasihi hiyo.

Kulingana na mazoea ya wahakiki wa karne ya 18, utenzi ulizungumzia maudhui mateule.

Maudhui mateule humsawiri mtu katika utukufu wake. Lugha inayotumika kutunga utendi

inapaswa kuafiki uteule wa dhamira zake. Nao ushairi unapaswa kuzingatia lugha inayojirejelea,

inayojibodoa na inayojitambulisha yenyewe. Ni lugha inayozindua hisi za msomaji. Mashairi

yaliyotungwa mashambani hayakutilia maanani umakinifu wa uwasilishaji. Yakisomwa hata

sasa, inakisiwa kula lugha yake inanukia ushamba.

(ii) Wataalamu wa fasihi waliamini kwamba kila utanzu wa fasihi una sheria zake – sheria

zinazoelekeza utungaji wake. Warasimi wapya walisisitiza kwamba usanii bora hufanyiwa katika

25
mipaka inayokubalika na kushabihiana na mtazamo wa wengi. Sheria zilizochotwa na kutumiwa

na warasimi wapya ziliazimwa kutoka kwa wahakiki wa Ugiriki na Uroma wa Kale. Maoni ya

warasimi wapya yalikuwa kwamba kukataa kufuata kanuni ni kiburi. Kulingana na maoni ya

waasisi na waitifaki wa urasimi mpya, mshairi hangeweza kugundua chochote kuhusu hali ya

kibinadamu kwa kuwa ukweli wote kuihusu hali hiyo ilikuwa imegunduliwa yeyote aliyethubutu

kutunga miundo mipya ya kisanaa alishukiwa kuwa mwenye uchoyo na kujipendekeza. Katika

makala ya Essay on Criticism, Pope anatetea ufuasi wa sheria kwa kudi kwamba ukamilifu

hauwezi kutokana na mambo mapya. Aliyekuwa na nia ya kuzungumzia mambo mageni alikuwa

hajafunukiwa na mikakati yote ya kuzungumzia jambo hili. Hivyo basi, alipaswa kutumia njia

zilizodhihirika kitambo kuwa yakini.

(iii) Tumesema kwamba waitifaki wa urasimi – mpya walichelea kuwatukuza watunzi

waliozua mitindo mipya. Sababu yao ilikuwa wazi-uwezo wa mtu binafsi haukutegemewa wala

kuaminika kuwa mwongozo madhubuti wa utunzi. Si ajabu kwamba watunzi walishauriwa kuiga

mitindo ya utunzi na uhakiki kutokana na wataalamu walioishi zamani za akina Aristotle na

Horace. Warasimi – wapya wengi walifikiria kwamba Wagiriki na Waroma waligundua yote

yaliyotarajiwa kugunduliwa katika mawanda ya fasihi na ilikuwa sharti waigwe. Katika kipindi

hiki, urejeleaji wa matamshi yaliyosakini ukale lilikuwa jambo la kuheshimika. Msanii

aliheshimika kwa kuwatunika heshima magwiji wa zamani. Kwa kuwadondoa wahenga wale,

mtunzi alionyesha utaalamu wake, alionyesha kwamba yeye ni msomi. Haikukuwa muhali

warasimi wapya wakizungumza juu ya ‘Dulce et utile’ na ‘Des Trois Unitez’.

26
Ili kutafuta heshima, watetezi wa urasimi mpya walitafsiri tungo za kale zilizoandikwa katika

Kigiriki na Kiroma. Baada ya kuzitafsiri tungo hizo, waliiga mitindo ya watangulizi wao na

kisha kujitungia tungo zao wenyewe. Yaani baada ya tungo kama vile za Homer na Virgil

kutafsiriwa, akina John Milton na Edmund Spenser waliandika tenzi zao kutangamana na imani

zao. Dryden, mmojawapo wa wahakiki walioishi katika kipindi hiki alinukuliwa akisema

kwamba drama ni uigizaji wa tajriba anazopitia mwanadamu. Ili uigo mzuri kufanywa, unapaswa

kufuata mwongozo maalumu. Dryden anamalizia kwa kusema kuwa mwongozo huu unapaswa

kutokana na fasihi ya Kigiriki na Kiroma. Maoni ya kijumla ya Warasimi wapya yalikuwa

kwamba uigaji a miongozi ya kutunga pamoja na ustaarabu uliandamana na miongozo hiyo

ulikuwa upeo wa juu wa mafanikio.

(iv) Jambo moja lililojadiliwa na Aristotle na ambalo liliwatatanisha sana Warasimi wapya

lilihusu ufungamano wa fani tatu katika utunzi wa tamthilia (Des Trois Unitez). Alipokuwa

akizungumza juu ya muundo wa Tanzia, Aristotle alidiriki kusema.

 Tanzia ilipasa kuwa na ploti moja pasipo kuingiliwa na ploti nyingine ndogo ndogo au

mirando isiyofungamana na ploti hiyo kuu.

 Pili, Tanzia ilipaswa kuigizwa au kuigizika mahali pamoja.

 Mwisho, maigizo yalitarajiwa kufanywa kwa siku moja.

Aristotle hakusema kwamba shuti kanuni hizi za kimuundo zizingatiwe katika uandishi wa

tamthilia yoyote ile. Alikuwa akielezea yale aliyoyaona kuwa mikondo ya jumla ya Tanzia ya

Kigiriki. Kwa bahati mbaya, warasimi wapya waliyameza maelezo ya Aristotle bila fasiri nzuri.

27
Ikiwa sasa wanafuata kanuni hii kuitumwa. Kutokana na utumwa huu, warasimi wapya

walizitupilia mbali tamthilia nzuri nyingi.

Kwa mfano, mwanasanaa Shakespeare (1564 – 1616) alikemewa vikali kwa kutofuata ‘Des

Trois Unitez’, yaani ufungamano wa vitushi, wakati na mahali. Ni ajabu kwamba hapo baadaye,

Shakespeare alisifika sana. Hivi sasa tamthilia zake zinasomwa zaidi kuliko tungo nyingine

zozote za fasihi.

(v) Fani muhimu iliyotumiwa na Warasimi wapya na pengine ambayo inasawiri upekee wa

kipindi hiki ni ufyozi. Wanajamii wa karne ya 17 na 18 hawakusita kuyasuta madai yoyote

yaliyokosa mantiki. Njia iliyochipushwa ya kufanikisha muradi huu ilikuwa ufyozi. Mwanasanaa

aliyetumia vizuri njia hii alikuwa Swift. Katika riwaya yaa Safari za Gulliver, Gulliver anapofika

Laputa anachekelea ujuzi wa Walaputa ambao wanaamini kwamba nchi yao ni kisiwa

kinachoelea angani. Swift anatumia kisiwa hiki kama kielelezo cha utaalamu wa uwongo

uanoelea angani bila mashiko yoyote.

Ufyozi ni aina ya kejeli inayotumiwa kushambulia maovu kwa dhamira ya kuyasahihisha maovu

hayo. Kejeli kwa kawaida inaweza kushambulia, kuchekesha na kuadili. Kejeli inayoshambulia

bila kuchekesha ni masimango. Katika karne ya 17 na 18, kejeli ilisheheni sehemu ambazo

zimegusiwa kitambo. Zilikuwa (i) shambulio, (ii) kicheko na (iii) onyo.

Kushambulia kutupu haukuhimizwa. Aidha, vichekesho ambavyo haivukubeba mafunzo

vilichukuliwa kuta mzaha tu. Nayo maonyo ambayo hayakunyunyuziwa chembe za vicheko ni

28
mahubiri kavu. Iliaminika kwamba mwenye kukejeli hakukuwa na uchoyo bali alikuwa na imani

na walimwengu. Alikuwa na imani kwamba ulimwengu aliokuwa akilundikia masuto

ungetegemea na kuwa mahali bora pa kuishi.

(vi) Warasimi wapya walizingatia ubunifu na umakinifu katika kuwaza na kuwasilisha fikra

zao. Anapozungumzia ubunifu, Pope ana maana kwamba:

 Mtunzi ana uwezo wa kukumbuka matamshi mateule, madondoo yanayotokana na

wataalamu wa kale. Pia, mtunzi anatarajiwa kuzungumzia hikima inayotokana na tajriba

zake.

 Mwanasanaa ana uwezo wa kuwaza na kufikia kilele cha ukamilifu ili tungo nzuri ziweze

kutungwa.

 Kitambo imesemwa kwamba waitifaki wa urasimi mpya walitilia mkazo ufuasi wa sheria

na kaida za utungaji. Lakini mipaka ya sheria na kaida ilikuwa mipana ya kutosha

kumwezesha mwana sanaa kuzua na kukuza na mitindo mipya katika mipaka

iliyokubalika. Huu ulikuwa ubunifu na umakinifu katika utunzi wa kazi za sanaa.

Eleza sifa kuu za urasimi mpya wa Kimagharibi? ‘Historia hujirudia ijapokuwa katika sura
tofautitofauti’. Jambo hili linadhihirishwa vipi katika uhusiano wa urasimi mkongwe na urasimi
mpya wa kimagharibi?

MUHIMU: Hakikisha unatambua aina zote za urasimi uliojadiliwa katika mwongozo huu.

Marejeleo:

Pope, Alexander. ‘Essay on Criticism’, Makers of Criticism, B. Rajan & A.G. George

(Wahariri). London: Asia Publishing House, 1965.

29
MHADHARA WA TANO

URASIMI MPYA KATIKA FASIHI YA KISWAHILI


Malengo

(a) Mshiriki anapaswa kutambua tofauti zilizopo kati ya urasimi mpya wa kimagharibi na

urasimi mpya ya Kiswahili.

(b) Mshiriki anatarajiwa kueleza hali ya kihistoria na kifasihi zilizosababisha kuzuka kwa

urasimi mpya wa Kiswahili.

(c) Mshiriki anatazamiwa kutambua kwamba urasimi mpya una wahakiki wanaotambulikwa

kwa majina.

(d) Mshiriki anapaswa kuainisha mihimili ya nadharia ya urasimi wa Kiswahili.

(e) Mshiriki anatarajiwa kuonyesha jinsi mihimili hiyo inavyoweza kutumiwa kuzichanganua

kazi za fasihi.

Baada ya kuzungumzia urasimi mpya wa kimagharibi, sasa na tuzame kwenye urasimi mpya wa

Kiswahili. Kipindi hiki kinatanguliwa na enzi ya kiza katika fasihi ya Kiswahili. Enzi ya kiza

ilikuwepo kati ya mwaka wa 1885 na 1945. Ijapokuwa Mulokozi na Sengo wanafanya utafiti

unaoelekea kuonyesha kwamba washairi walikuwepo katika kipindi cha giza, ukweli uliopo na

wa kutegemewa ni kwamba kuna ithibati chache kuonyesha uyakini wa madai haya. Maandishi

machache yaliandikwa yakiwemo Utenzi wa Vita vya Majimaji.

Kihistoria tumeambiwa na E. Kezilahabi kwamba huu ndio wakati ambapo mataifa ya ulaya

yalikuwa yakiling’ang’ania na kuliparamia bara la Afrika. Pili, kulikuwepo na vita vya dunia

30
mara mbili. Hali hizi mbili zilisimamisha uandishi. Lakini wakati ambapo vita vya dunia vya pili

vilipiganswa, wakazi wengi wa Afrika Mashariki walipitia katika tajriba mpya, wakamulikwa

kwa nuru mpya kuhusu uhuru na usawa wa wanadamu wote. Utenzi wa Vita vya Uhuru na

Maisha Yangu na Baada ya Miaka Hamsini (1966) vinaelezea tajriba hizi. Katika kipindi cha

urasimi mpya, mwandishi wa Kiswahili anatafuta mizizi yake kwa hamasa kubwa. Anajaribu

kuibainisha nafasi yake katika ulimwengu unaotawaliwa na Mzungu. Ili kufaulisha jaribio lake,

mtunzi wa Kiswahili anachimbua miundo na maumbo ya mashairi ya akina Muyaka na Ali Koti,

na kuyatumia kuyatunga yake mwenyewe.

Watunzi na wahakiki muhimu wa wakati huo walikuwa Shaaban Robert, AMRI Abedi, Khamis

Amani, Mathias Mnyampala na Ahmad Nassir miongoni mwa wengine. Swali kuu lililowakabili

wahakiki lilihusu maana na muundo wa shairi la Kiswahili. Wengi miongoni mwa wahakiki

hawa walikuwa watunzi waliokomaa. Matamshi na maandishi yanayopatikana katika tangulizi za

tungo zao mbalimbali yanaonyesha ya kuwa walitaka sana kuufahamu ushairi wa Kiswahili

kinadharia. Shaaban Robert katika Swahili Poetry (1962) kilichohaririwa na Lyndon Harries

anaeleza maana ya ushairi hivi:

Ushairi ni sanaa ya vina inayopambanuliwa kama


nyimbo, mashairi na tenzi. Zaidi ya kuwa sanaa ya
vina, ushairi una ufasaha wa maneno machache au
muhtasari. Mwauliza wimbo, shairi na tenzi ni nini?

Wimbo ni shairi ndogo. Shairi ni wimbo mkubwa.


Utenzi ni upeo wa ushairi. Mwauliza tena, kina ni
nini? Kina ni mlingano wa sauti za herufi. Kwa
maneno mengine huitwa mizani au sauti, na ufasaha
ni uzuri wa lugha (Uk. 282)

Kwa upande wa maudhui yanayowasilishwa katika mashairi, Shaaban Robert anasema kwamba

mashairi yanapaswa kufundisha jamii nyenendo zinazofaa.


31
Naye Mathias Mnyampala, katika utangulizi wa diwani yake (1965) anatuambia ‘Ushairi ni

msingi wa maneno ya hekima tangu kale. Ndicho kitu kilicho bora sana katika maongozi

ya dunia kwa kutumia maneno ya mkato na lugha nzito yenye kunata yaliyopangwa kwa

urari wa mizani na vina malumu’. Upeo ni juu wa kipindi cha urasimi-mpya wa fasihi ya

Kiswahili ulitokea kilipochapishwa kitabu cha Sheria za Kutunga Mashairi na Diwani ya Amri

(1954). Kulingana na maoni ya Kezilahabi (9183), kitabu hiki kilikuwa kiungo cha wakati

uliopita na urasimi-mpya.

Wahakiki wa hivi karibuni kama Ibrahim S. Noor (1988) wanamkosoa Amri Abedi kwa

kutozungumzia yote aliyopasa kushughulikia. Hata hivyo, aliyoyafanya Amri kwa wakati huo

yanastahili pongezi. Alizungumzia ushairi wa wakati wake kinadharia. tukizingatia mkondo wa

fikra wa ushairi kama wa Shaaban Robert, Chiraghdin Shihabbudin, Abdilatif Abdalla na Sheikh

Ahmad Nabhany, mihimili kadhaa kuhusu utungaji ushairi inachipuka.

(i) Kwanza kabisa, tunajulisha kwamba nguzo ya ushairi wa Kiswahili ni muundo. Ignawa

bahari za ushairi wa Kiswahili zinaweza kuanishwa kwa kutumia vigezo vya kimaudhui

(kama wajiwaji, kasida, madhuma na ushairi burushi), kwa ujumla, bahari za mashairi ya

Kiswahili hubainishwa kimuundo. Mifano ifuatayo inathibitisha jambo hili.

a. Tathnitha – shairi la mistari miwili kwa kila ubeti.

b. Tathlitha – shairi la mistari mitatu kwa kila ubeti:

Mi nawe mbali tungawa, nakukumbuka

Lau ngekuwa na mbawa, ningaliruka

32
Ni muhali hili kuwa, nasikitika.

Mi nawe mbali tungawa, muhibu wangu

Kamwe hayatapunguwa, mapenzi yangu

Hii kaa kijuwa, wewe u wangu.

(Abdalla, 1972:11)

c. Tarbia – shairi la mistari minne kwa kila ubeti. Mashairi ya tarbia ni mengi zaidi

kuliko aina zingine za mashairi.

Mwanadamu hasifiki, ushupavu na kiburi,

Kiburi huzaa chuki, majitapo si mazuri,

Ulimwengu hautaki, jambo lenye taksiri,

Hujafa hujaumbika, jilinde na majitapo

(Snow White, 1982:11)

d. Takhmisa – shairi lenye mistari mitano kwa kila ubeti.

Mbuyu mkizikaanga, watu wa chini ya gae,

Hadaa huzua janga, pakajiri na kiwewe

Msitufanye wajinga, ujinga nani mwenyewe?

Mambo mkiyabananga, lawama msitutie

Kwani mbele tutasonga, ili haki tukapewe.

(Shaaban Robert, 5, 1967:72)

e. Kuna aina zingine za mashairi kama:

(i) Tashlita – shairi la mistari sita kwa kila ubeti.

(ii) Shairi la mistari kumi kwa kila ubeti

33
(iii) Masivina – shairi lenye mlingano wa mizani lakini sio wa vina.

(iv)Ukawafi – shairi la vipande vitatu kwa kila ubeti:

Mkono inuka, inuka hima twaa kalamu

Upate ya’ndika, kwkhati njema, hino nudhumu

Ipate someka, wenye kusoma, waifahamu

Wapate yashika, na kuyapima, yaliyo humu.

(Abdalla, 1972:34).

(v) Msuko – shairi lenye kibwagizo kilichofupishwa

(vi)Sakarini – shairi ambalo linatumia aina nyingi za ushairi.

(vii) Kikwamba – katika shairi la aina hii, neno moja hurudiwarudiwa na ndilo

linalokuwa la mwanzo wakati wote kwa kila mstari.

Wastara hazimbuki, wahenga waliyasema,

Wastara haumbuki, ni mtu mwenye hekima,

Wastara na hachoki, daima hutenda mema, (Mnyampala, 1965:9)

Ni vigumu kuorodhesha aina zote za mashairi. Haya yanatosha kudhihirisha madai ya awali

kwamba mashairi mengi ya Kiswahili hubainishwa kimuundo.

(ii) Katika ushairi uliotungwa katika kipindi cha urasimi mpya, watunzi walizingatia

mikatale, mapokeo na makatazo ya kijamii. Shaaban Robert anawanaisihi watunzi au

wanaonuia kuwa washairi hivi. ‘Ni mwiko tukano katika ushairi, mwiko fitina katika

ushairi, mwiko fitina katika ushairi, mwiko nuksani katika ushairi; msengenyo,

mwao, fitina na nuksani ni tabia mbaya. Mashairi yenye vipopo vya fikra, vita vya

34
adili na utukufu wa matendo ambayo watu wa karne zote hawataridhia kuyatupa na

kuyasahau ndiyo mashairi yatakiwayo’ (Mhina, 1970).

Miongoni mwa maonyo ya mwisho kwa mtunzi chipukizi, Abedi anataja: ‘Usitunge

mambo ya kihuni bali mambo yanye maarifa yanayoweza kuwafaa watu’ (1954:40-

42).

(iii) Watunzi waliopatikana katika kipindi hiki hawakupuuza arudhi asilani. Kama

tulivyoonyesha hapo awali, miundo mbalimbali ya ushairi ilikuwepo na ingeweza

kufafanuliwa kinadhaira. Ilikuwa juu ya mshairi mahiri kuipa miundo hiyo minofu ya

mawazo na ya lugha.

(iv) Mwisho, katika kipindi hiki, inaweza kukisiwa kwamba palizuka istilahi za

kuelezea dhana mbalimbali za kuelezea aina za ushairi. Mifano ya istilahi hizi ni:

 Mshororo - mstari wa shairi

 Mwanzo - mstari wa kwanza

 Mloto - mstari wa pili

 Mleo - mstari wa tatu

 Kipokeo - mstari unaorudiwarudiwa

 Ukwapi - kipande cha kwanza katika mstari wa shairi

 Utao - kipande cha pili

 Mwandamizi - kipande cha tatu

 Tabdila - kunga katika ushairi ya kufupisha sauti bila

kubadilisha maana

 Inkishafi - kunga ya kufupishwa maneno kitaalamu


35
 Mazida - kunga ya kurefusha neno kitaalamu bila kupotosha

maana asili.

 Takriri - silabi zinazolingana

Marejeleo

Njogu, Kimani na Rocha, Chimerah. ‘Nadharia katika Uhakiki wa Fasihi (3 – 19)’ Ufundishaji

wa Fasihi: Nadharia na Mbinu. Nairobi: Jomo Kenyatta Foundation, 1999.

Abedi, Amri. Sheria za Kutunga Mashairi na Diwani za Amri. Nairobi: Kenya Literature

Bureau, 1979.

Mulokozi, Mugyabuso, na Kahigi Kulikoyela. Kunga za Ushairi na Diwani Yetu. Dar es Salaam:

Tanzania Publishing House, 1979.

Senkoro, F. E. M. K. Ushairi: Nadharia na Tahakiki. Dar es Salaam: Dar es Salaam University

Press, 1988.

Wafula, R. M na Kimani Njogu. Nadharia za Uhakiki. Nairobi. Jomo Kenyatta Foundation,

2007.

36
MHADHARA WA SITA

UHALISIA
Malengo

Katika sura hii tutazungumzia uhalisia katika muktadha wa fasihi ya kimagharibi na fasihi ya

Kiswahili.

(a) Fasihi ya Kimagharibi

Uhalisia ndio nadharia muhimu zaidi kutokea katika karne ya kuni na tisa na ishirini. Katikati ya

karne ya kumi na tisa huko Ulaya, nguvu za mapinduzi ya kisiasa zilikuwa zimeanza kulegea.

Mapinduzi ya kiviwanda nayo yalikuwa yamefikia kilele chake. Ulaya ilikuwa imeendelea sana

kwa upande wa teknolojia. Wanajamii walianza kukabiliana na matatizo yanayohusiana na miji

inayopanuka harakaharaka. Tabaka la makabwela lilizuka. Uyanikinifu wa hali ya binadamu

ulithaminiwa sana. Huu ndio wakati ambapo Karl Marx alianza kuzungumzia jamii kisayansi

huku akiagua ya kwamba mapinduzi ya makabwela yangetokea baadaye.

Katika mawanda ya fasih, uhalisia wa matatizo yaliyokuwa yakiwakabili watu uliwafanya

wanasanaa kuutuhumu ulimbwende. 1


Matamanio ya kilimbwende yalikuwa ya kinjozi zaidi

yakilinganishwa na taabu zilizokuwa zikiwakabili watu. Walimbwende walikuwa wakijitungia

mambo yasiyoweza kutimia. Waliishi ndotoni.

1
Taz. Wafula, R.M. na Kimani Njogu. Nadharia za Uhakiki wa Fasihi. Nairobi. Jomo Kenyatta Foundation, 2007.
37
Kutokea mwaka wa 1800 na kuendelea mbele wahakiki na watunzi walianza kuwadhihaki

walimbwende. Gustav Flaubert mmojawapo wa waanzilishi wa uhalisia alishikilia kwamba,

‘Mtu hufikiria kwa kichwa chake, hafikiri kwa moyo wake’. Kwa kifupi, Flaubert alikuwa

akilaani na kukejeli dhana iliyowaongoza walimbwende katika utungaji wao.

Mihimili ya Uhalisia

(a) Unaozingatia njia ya kisayansi ya kutekeleza jambo.

(b) Unaosisitiza upinzani dhidi ya mtazamo wa kinjozi juu ya maisha.

(c) Unaopingana na ulimbwende.

(d) Una mashiko katika hali halisi ya maisha ya watu. Unakaribia wasifu na tawasifu za watu

binafsi

(e) Unaonyesha hali ya kisaikilojia ya wahusika ambao msomaji anakumbana nao.

(f) Unasisitiza muundo na muwala katika kazi ya fasihi.

(g) Unaiona kazi ya sanaa kama zao linalojitosheleza. Yaani ulimwengu ni yakinifu.

(h) Wahusika ni vielelezo vya wanadamu halisi wanaoishi katika ulimwengu unaofahamika.

Wahusika na wahakiki wengi waliotumia nadharia ya uhalisia waliamini ya kwamba dhima ya

mwandishi ni kuonyesha ukweli kama ulivyo. Mhakiki naye alimtathmini mwandishi kwa nama

huyo mwandishi alivyojibidiisha kuonyesha ukweli. Haja kubwa ya kuigiza ilikuwa kuonyesha

picha ya mazingira ambamo jamii inapatikana mathalan kioo kinavyotumika kutoa picha za

mwanadamu. Kulingana na wataalamu hao, mwandishi anapaswa kuitoa picha ya jamii bila

kuidunisha wala kuipigia chuku. Dhana ya fasihi kuwa ‘ni kioo cha jamii’ ilitokana na uhalisia.

38
Ukweli ni kwamba ijapokuwa fasihi huzungumzia ukweli, mwandishi huchagua mambo

anayotaka kuzungumzia. Mwandishi huchagua, akachanganua na kutenganisha anayozungumzia.

Baadhi ya waandishi huonyesha misimamo yao juu ya ile wanalozungumzia. Hapo ndio

tunapouona uhalisia hakiki, ambapo pamoja na msanii kujizatiti kuchora hali halisi ya maisha

kama yalivyo, hutetea watu fulani na kuwashambulia wengine kutegemea na msimamo wake.

Katika kufanya hivyo, si lazima mwandishi awe na itikadi maalumu na bayana kuhusu maisha.

Itikadi hudhihirika zaidi katika uhalisia wa kijamaa.

Mhakiki anaposema fasihi ni kioo cha jamii huwa anamaanisha nini? Soma riwaya ya Kiu
kisha ainisha baadhi ya sifa za kihalisia zinazopatikana mle.

39
MHADHARA WA SABA

UHALISIA WA KIJAMAA – USULI


Malengo

(a) Mshiriki anatazamiwa kufahamu usuli wa uhalisia wa kijamaa, kwa kutambua dhima ya G.

F. Hegel, Karl Marx na Fuerbach katika ujenzi wake.

(b) Mshiriki anapaswa kutambua jukumu la Maxim Gurki na chamaa ya waandishi cha Soviet

katika uundaji wa nadharia hii.

(c) Mshiriki anatarajiwa kuainisha mihimili ya uhalisia wa kijamaa na kuonyesha jinsi

inavyoweza kutumiwa kuhakikia kazi mbalimbali za fasihi.

Ili kuufahamu uhalisia wa kijamaa misingi yake inapaswa kujulikana. Misingi hii inatokana na

mawazo ya Karl Marx. Lakini Karl Marx hakuyaunda mawazo yake kutoka angani. Fikra zake

zilikuwa kilele cha mabadiliko na maendeleo ya kizazi cha mtu yaliyoanza tangu kuchipuka kwa

mtu huyo katika sayari hii. Mwanafalsafa aliyemtangulia Marx na kuiathiri falsafa yake kwa

kiasi kikubwa alikuwa G. F. Hegel.

Kama ilivyokuwa na Mgiriki Plato, Hegel aliamini kwamba vitu vyote vinavyopatikana humu

ulimwenguni ni picha hafifu ya vitu hivyo kama vinavyodhihirika katika dunia ya kinjozi. Plato

alikuwa dhahiri zaidi kumliko Hegel aliposema kwamba vitu vyote vilivyomo humu duniani

vimechujuka mara mbili kutokana na halisi wa kidhahania. Kutokana na haya, aliendelea Plato

sanaa umithilitshi zimekenguka zaidi, maana zimekengeuka ngazi tatu kutokana na ukweli. Kile

ambacho Plato hazungumzi bayana ni namna picha hafifu za viumbe zinavyofikia ukamilifu na

udhahania wa kimbingu.

40
Hegel kwa upande wake anajaribu kutupatia jawabu. Kwake, ijapokuwa vitu vinavyopatikana

humu duniani ni picha dhaifu ya vile vinavyopatikana katika sura za kinjozi, lakini vitu hivyo

huendelea kukua na kubadilika, hata vikiwa humu duniani kuuelekea ukamilifu wa kinjozi. Hali

hii hutokea hivi. Taz. Katika (Encyclopedia Britannica. ‘Dialectical Idealism’).

Jambo au kitu cha kwanza kisichokuwa kikamilifu huitwa tasnifu. Tasnifu ni hali asili ya kitu au

jambo. Kwa kuwa tasnifu haijakamilika wala kujitosheleza, hujizalishia mikinzano ya kindani.

Sehemu ya mkinzano wa tasnifu huitwa tabaini. Tabaini ikigongana na tasnifu huzalisha

kusanisi. Lakini kusanisi huku huwa kumetokea mapema zaidi katika maendeleo ya kitu

kinachozungumziwa kwa hivyo, si kukamilifu. Hivyo kusanisi huku hujenga tasnifu mpya tena.

Tasnifu hii vile vile haijajitosheleza na hujiibukia mgogora mwingine wa kindani, yaani aina

mpya ya tabaini. Tena, mwingiliano wa tansifu wa tabaini huzalisha kusanisi kwingine.

Kwa mujibu wa maelezo ya Hegel, mgongano wa tasnfiu na tabaini huendelea mpaka hali

kamilifu na ya kidhahania ya kitu inapofikiwa. Hali hiyo ya kidhahania ndiyo kamilifu na

tamilifu kuliko zote. Kuna wiano kati ya fikra ya Hegel kuhusu ukamilifu wa kitu na ile ya

Darwin kuhusu maendeleo ya mwanadamu. Baada ya kufanya majaribio na uchunguzi juu ya

wanyama, Darwin alihitimisha kwamba binadamu amefikia kiwango alichoko cha ukamilifu kwa

kuvipitia viwango vya awali vingine visivyokuwa vikamilivu. Hegel alipoitafsili nadharia yake

kihistoria, aliamini kwamba kuna roho ambayo husababisha tasnifu, tabaini na kusanisi, au

katika maneno mengine, kisio, kinyume cha kiso hilo na suluhisho linaloatokana na mwingiliano

wa kisio na kinyume chake. Roho ndio huleta mabadiliko na maendeleo. Hegel aliamini kwamba

roho hiyo husonga, ikitoka mashariki ikielekea magharibi. Ndipo Hegel alipokatikiwa kwamba

41
chanzo cha historia ni Ugiriki na sehemu zinazopakana nao na mwisho wake ni Ujerumani. Hili

ni dai ambalo limetupiliwa mbali na wanahistoria, hasa wanahistoria wa Kiafrika ambao

wanafikiria kwamba Hegel alikuwa akionyesha taasubi ya Kijerumani tu. Mwanafalsafa

mwingine aliingia kati ya Hegel na Marx. Naye alikuwa Fuerbach. Kwake Fuerbach, vitu vyote

vinatokana na kushia mumu humu duniani. Marx aligeuza imani ya Hegel kichwa mgomba na

kuikoleza na maoni ya Fuerbach kuhusu ulimwengu na kisha kufikiria kuhusu ulimwengu upya.

Marx

Alikuwa Myahudi wa Kijerumani. Aliyachukua dhana za Hegel, akaazima dhana ya Fuerbach,

na kuibadilisha falsafa yote ya Hegel kichamgomba. Badala ya kuzungumzia ukamilifu wa

kidhahania unaotokana na kusonga kwa roho, Marx alizungumzia mambo yaliyohusu

maendeleo ya jamii thabiti.

Aliazima fikra ya Hegel. Lakini kwake Karl Marx, maendelo ya jamii huthibitika katika vipindi

vya maisha ambavyo kizazi cha binadamu kimepitia. Kulingana na Karl Marx, tabaka la jamii

hutoweka na lingine kichipuka kwa sababu ya mgongano unaotokea kati ya tabaka tawala na

tabaka tawaliwa. Marx anasema kwamba kunu kinachoendesha histori ni mgongano wa kitabaka.

Mgongano huu hutokea kwa sababau kila mara kuna tabaka la wanyonyaji na wanaonyonya.

Hivyo inabidi kuwa na mapinduzi dhidi ya mifumo ya kuzalisha mali inayohimili unyonyaji.

Mapinduzi yanayotokea baadaye yanaongeza tumaini la ujenzi na uimarishaji wa jamii

inayozingatia usawa. (Taz. Katika: Encyclopedia Britannica ‘Dialectical Materialism’).

42
Marx unamwona binadamu kuwa kiini cha historia yote na matendo yote yanayotendeka humu

duniani, Umarx unawabudu binadamu. Ndiye mwenye urazini wa kuifanya dunia itengenee na

kuwa mahali bora pa kuishi. Marx anampa binadamu tumaini la kuing’oa mizizi yote ya

unyonyaji na unyanyasaji na kujenga ulimwengu wa kinjozi usiokuwa na madhila. Vidato

ambavyo jamii ilipasa kupitia kabla ya kufika ukamilifu kwa kinjozi ni vifuatavyo:

(i) ujima (iii) umwinyi (v) ujamaa

(ii) utumwa (iv) ubepari (vi) ukomiunisti

Kulingana na maoni ya Marx, ukomiunisti ndicho kidato kikamilifu zaidi katika maendelo ya

kibinadamu.

Maoni ya Karl Marx yaliathiri pakubwa nadharia ya uhalisia wa kijamaa.

Eleza uhusiano uliopo baina ya mawazo ya Hegel, Karl Marx na Fuerbach

Uhalisia wa Kijamaa – Maelezo Zaidi

Ni mbinu ya utunzi na uhakiki inayomzingatia binadamu kama uti wa mgongo wa kuwepo kwa

ulimwengu na maana ya ulimwengu ule. Waundaji wa nadharia hii wameathiriwa na mtazamo

wa kimarx kuhusu ulimwengu na historia. Maxim Gorki, mmojawapo wa waasisi wa uhalisia

wa kijamaa anasema:

Chochote tunachopata chenye uzuri wa kutamanika kimeumbwa au kuelezwa na mtu. Ni


jambo la kuhuzunisha kwamba mtu amezalisha na kuendeleza dhuluma dhidi ya mtu.
Hata hivyo, ijapokuwa nipo wakati mwingien katikati ya dhuluma hilo, huwa nini shauku
ya kupinga na kutupilia mbali idhilali za aina yoyote. (Uk. 64 On Literature)

Akizungumzia maana ya uhalisia wa kijamaa, Gorki anaendelea kusema:

Maisha ni matendo: Maisha ni uumbaji. Lengo la kuishi ni kukuza na kusambaza vipawa


vitakavyomwezesha mtu kupigana na kushinda pingamizi dhidi yake. Madhumuni ya
43
maisha pia ni kudumisha afya ya mtu, kumwezesha kuishi kwa furaha, afurahie uwezo
wake wa kuidhibiti na kuitawala dunia (uk. 64. On Literature)

Katika tungo zinazoongozwa na uhalisia wa kijamaa, mwandishi/mhakiki huongozwa na

mihimili ifuatayo:

(i) Wahusika wa kimaendeleo: Wahusika wa kimaendeleo ni wahusika wanaounuia

kuipindua na kuibadilisha hali yao ya maisha.

(ii) Pamoja na kusawiri matukio kihistoria, wahusika hutekeleza matendo yao kitabaka.

(iii) Uhalisia wa kijamaa huzingatia maslahi ya makabwela. Hawa ni mafukara wa ulimwengu

wenye nia ya kuimarisha udikteta wa makabwela.

(iv) Binadamu huonyeshwa kiuyakinifu. Wahusika wanaotumiwa kama vipazasauti vya

watunzi hupuliziwa uhai mathala wanadamu wa kawaida wanaoishi katika ulimwengu

tunaofahamikiwa nao.

(v) Huonyesha matumaini juu ya kizazi cha binadamu. hii inamaanisha kwamba mtu

atakuwa mshindi au ni mshindi dhidi ya uunyonyaji na unyanyasaji wa aina yoyote.

(vi) Lugha inayotumiwa katika uhalisia wa kijamaa inaendeleza malengo na mapendekezo ya

walio wengi katika jamii.

Ni lugha rahisi inayoeleweka na maskini. Upungufu unaoweza kutokana na nadharia hii ya

kutunga ni kwabma imekolea na itikadi sana hivi kwamba masuala ya kisanaa yanaweza

kupuuzwa. Lugha inayotumiwa inaweza kuwa kavu, ikakosa matumizi ya kugna za kifasihi

kama sadifa, taharuki na tamathali nyingine za usemi. Baadhi ya tamthilia, diwani za ushairi za

riwaya zinaweza kuhakikiwa kwa misingi ya uhalisia.

44
Mfano wa Tamthilia ya Kilio cha Haki (A. M. Mazrui)

Tamthilia ya Kilio cha Haki inahusu kilio cha wafanyikazi juu ya ukandamizwaji wao. Kili cha

Haki hakionyeshi kukata tamaa bali tumaini. Tamthilia inazungumzia ukoloni na ukoloni mambo

leo na madhara yake juu ya mtawaliwa.

Uhalisia wa kijamaa unabanika pale ambapo tunakabiliana na wahusika wa kimaendeleo, wa

kimapinduzi na wa kimabadiliko kama Lanina, Dewe na Musa. Juu ya haya maisha ya wahusika

yameelezwa kihistoria. Hali za sasa za wanaonyanyaswa zinatokana na mapisi yao. Katika

sehemu ya kwanza ya tamthilia, Mazrui anatumia mbinu-rejeshi, kuthibitisha namna matendo

yaliyopita yanavyoathiri matendo na maamuzi ya hivi sasa ya Musa na Dewe.

Kuna matabaka mawili muhimu. Kwa upande mmoja, kuna tabaka linalowakilishwa na Delamon

ambaye anasimamia ubepari wa kimataifa. Kwa upande mwingine, kuna tabaka la akina Lanina,

tabaka la mafukara ambao wanalenga kuboresha hali yao ya maisha. Tabaka la wanyonyaji

linajaribu kwa vyoyote vile kuendeleza sera zake hali tabaka la wanayonyanyaswa linajizatiti

kuinua hali ya maisha ya wanachama wake.

Mgongano unatokana na malengo yanayohitilafiana kati ya wanaonyonywa na wanaonyonya.

Mbali na kukamatwa na kushikwa kwa Lanina, wahusika wengine kama Musa na Dewe

wanaazimia kuendeleza harakati zilizoanzishwa na Lanina. Hii ni ishara ya matumaini

yasiyokwisha katika vita vya mafukara dhidi ya madhulumu wao.

Orodhesha mihimili ya nadharia ya uhalisia wa kijamaa.


Ihakiki riwaya ya Kiza katika Nuru (S.A. Mohamed) kwa kutumia nadharia ya uhalisia wa
kijamaa.
45
Marejeleo

Lucas, Georg. The Meaning of Contemporary Realism. London: Merlin Press, 1963.

Craig, David (Mhariri): Marxists on Literature. Harmondsworth: Penguin, 1975.

Gorki, Maxim. On Literature. Moscow: Progressive Publishers (Mwaka wa kuchapishwa kwake

haujulikani).

Wafula, R. M. ‘Harakati za Ukombozi katika Kilio cha Haki’, Uhakiki wa Tamthilia: Historia

na Maendeleo yake. Nairobi: Jomo Kenyatta Foundation, 1999.

46
MHADHARA WA NANE

UDHANAISHI/UTAMAUSHI
Malengo

(a) Mshiriki anatarajiwa kufahamu na kueleza historia ya nadharia ya kifalsafa inayoitwa

udhanaishi/utamaushi.

(b) Mshiriki anatazamiwa kuainisha na kufafanua mikondo mitatu ya nadharia ya udhanaishi.

(c) Mshiriki anapaswa kuorodhesha mihimili ya udhanaishi na kuonyesha jinsi inavyoweza

kutumiwa kuhakiki kazi za fasihi.

Katika sura hii tutashughulika na nadharia ya utamaushi au udhanaishi. Udhanaishi ni falsafa

kuhusu ‘dhana ya maisha’. Kwa upande mwingine, istilahi ya ‘utamaishi’ inatokana na neno

‘kutamauka’. Kutamauka ni kutokuwa na furaha (pengine kwa kushika tama) kwa kujua kuhisi

kwamba hakuna tumaini katika maisha haya kama yalivyo.

Utamaushi ni falsafa inayoshughulikia maswala kuhusu ‘maisha’. Ni mtazamo unaokagua kwa

upembuzi hali ya nafasi ya mtu katika ulimwengu anaoishi. Pia, ni falsafa inayozungumzia

uhusiano uliopo kati ya mtu wa Mungu, na iwapo mtu anapaswa kuamini kuwepo kwa Mungu.

Baadhi ya wahakiki wanasema kwamba mtazamo huu juu ya maisha ni ushuhuda madhubuti wa

kuporomoka kwa ustaarabu wa kimagharibi. Misingi inayozowewa ya maisha kama dini na

sayansi ili asiwa. Dai hii linaeleweka ikitiliwa maanani kwamba falsafa ya utamaushi ilitia fora

zaidi katika miongo iliyokumbwa na vita vya dunia mara mbili. Wahakiki na wanafalsafa wa

kimarx wanauita utamaushi juhudi za mwisho za mabepari katika harakati za kutaka kuendelea

kushinda licha ya kulemewa kwao na kupitwa na wakati. Katika kuhudi hizo za mwisho,

47
mahitaji ya kibepari (ubinafsi, uchoyo, upweke) yalisisitizwa zaidi kuliko maslahi ya jamii kwa

ujumla.

Kwa upande mwingine, kuna wale wanaoamini kwamba utamaushi ni upinzani yakini dhidi

mielekeo na mitazamo iliyokuwa ikichipuka ambayo ilitilia maanani umuhimu wa jamii kuliko

mtu binafsi. Hivyo, basi mtu alihitaji kupingana na jamii kwa kutetea ubinafsi wake, ubinafsi

ambao ilitilia maanani umuhimu wa jamii kuliko mtu binafsi. Hivyo, basi mtu alihitaji kupingana

na jamii kwa kutetea ubinafsi wake, ubinafsi ambao daima ulikuwa ukinyimwa uhuru na

masharti na mikatale ya kijamii.

Licha ya madai haya, utamaushi haukuanza katika karne ya ishirini. Wataalamu wengi

wanaamini kwamba falsafa ya utamaushi inatokana na mawazo ya Soren Kierkgaard (19813 –

1855) kutoka Denmark. Katika vitabu vyake vya Fear and Trembling, the Concept of Dread na

Sickness unto Death, Kierkgaard anashikilia kwamba mtu ni kikaragosi cha nguvu

zilizomuumba. Na ni katika kuzicha nguvu hizi ambapo mtu huyu anaweza kupata utulivu wa

kiroho.

Wanafalsafa wengine ambao wamezungumza juu ya utamaushi ni Martin Keidegger na Karl

Jaspers. Pamoja na kuuelezea mtazamo huu ka mapana, wanaigiza ndani yake dhana ya

kutomwamini Mungu.

Kwa ujumla watamaaushi wengi wanafikiria kwamba mtu kwanza huzaliwa, akawepo, kisha

mambo mengine yakafikiriwa naye baadaye. Wanashikilia kuwa binadamu ndiye kiini cha

48
kuwepo kwa ulimwengu. Kama mtu hangekuwepo, basi na ulimwengu wote pia haungekuwepo.

Ukweli ni kwamba ulimwengu haungepewa jina kwa vile yote yanayoelezwa kuhusu ulimwengu

yanafafanuliwa katika muktadha wa maish ya binadamu.

Ujuzi wa mtu, tajriba anazopitia, hisia na dhana zake zote zinatokana na kule kuwepo kwake.

Chambilecho Jean Paul Sarte, mtu kwanza huhisi kwamba anaishi, kisha mambo mengine

yakamfungukia katika hali yake ya kuishi.

Kwa mujibu wa maelezo ya Sartre, mtu huzaliwa au hujipata katumbukia kwenye ombwe la aian

fulani. Ana uhuru wa kukaa katika ombwe hilo na kuishi maisha ya utulivu na kukabiliana

vilivyo na ulimwengu uliomzunguka. Kwa kuwa hana uwezo juu ya masuala kama maumivu na

mateso, anaweza kukata tamaa. Hata hivyo, kabla ya kukumbwa na mauti mtu huyo atafanya

matendo yanayotoa maana juu ya maana ya maisha yake.

Waandishi wengi ambao wanajadili kuhusu utamaushi wanatilia mkazo matatizo halisi

yaliyomsibu mwanadamu. Wanakwepa imani ya kinjozi na kifikra juu ya maana ya kuishi.

Kwao, kwamba Mungu yupo au aliuumba ulimwengu ni suala ambao hawalishughulikii kwa

sababu halioani na mantiki ya fikra zao.

Baadhi ya maudhui yanayotajwa na kuelezwa na watamaushi ni kama: uhuru wa mtu binafsi,

uwezo wa mtu wa kujifikiria na kujiamulia na wajibu wa binadamu katika ulimwengu. Kwa vile

mwanadamu angekuwa chochote, ubinafsi ni muhimu kwa sababu jukumu la kujitekelezea na

kujiridhisha ni la kibinafsi. Maudhui mengine yaliyotagaa katika utamaushi ni; ukengeushi, hali

49
ya kutokuwa na uhakiki (chochote chaweza kutokea), kukataa tamaa na mauti. Hata hivyo kuna

watamaushi wanaosawiri tumaini fulani.

Ugwe unaowaunganisha watamaushi wote, wenye kukata tamaa kwa wenye kutumaini ni

kwamba wanahisi na huzungumzia kwa hamasa tanzia iliyokurubiana na maisha ya binadamu.

wanaonyesha kwamba juhudi za mtu za kujitafutia maana ya maisha mara nyingi huishia katika

mvunjo au uvunjikaji wa juhudi hizo-hasa katika mauti. Mwisho wa mwanadamu ni kifo.

Mchango wa utamaushi unahusiana na uwezo wake wa kutalii maisha ya binadamu kihisia na

kinafsia. Pamoja na haya, utamaushi unajadili hali kama fadhaa, mashaka, na uchovu na jinsi

zinavyoathiri maisha ya binadamu. waandishi wa fasihi ya Kiswahili wanaoweza kuhakikiwa

kwa kutumia udhanaishi ni E. W. Mkufya (Zirani na Zirail), S. A. Mohamed, (Amezidi, Tata za

Asumani na Jangal la Werevu) na E. Kezilahabi (Rosa Mistika, Kichwamaji, Dunia Uwanja wa

Fujo, Kichomi, Karibu Ndani na Dhifa

Mfano wa Kazi za Euphrase Kezilahabi

E. Kezilahabi ni mwandishi wa riwaya, mashairi na insha zinazohakiki fasihi. Fununu

zinazopatikana katika maandishi yake zinaonyesha kwamba pengine ama yu miongoni mwa

watamaushi wasiokuwa na uhakikia kwamba Mungu yupo au miongoni mwa wale wasiokuwa

waumini kabisa. Ushahidi wa maoni haya unapatikana katika riwaya ya Kichwamaji (1975)

ambapo kipaza-sauti cha mwandishi (mhusika Kazimoto) anasema:

Mambo yaliharibika nilipoanza kuwaambia kwamba huenda hakuna Mungu. Wazee wote

walikataa kabisa. Mzee mmoja aliinuka na kwenda nyumbani (uk. 59).

50
Na katika riwaya ya Rosa Mistika, Mungu amesawiriwa kama hakimu wa kibinadamu

aliyechanganyikiwa na kesi ambayo imemkabili.

Mungu: Rosa kwa nini umejiua?

Rosa: Eee Mungu wangu, haya yote yametokea kwa sababu ya baba yangu.

Mungu: Zakaria, unasema nini?

Zakaria: Haya yote yametokea kwa udhaifu wake mwenyewe.

Mungu: Rosa, una ushahidi?

Rosa: Ndiyo ulimwengu mzima bwana Mungu.

Mungu: Na Zakaria?

Zakaria: Ulimwengu mzima bwana Mungu.

(Mungu anaamka. Anatoa miwani yake. Anafikiri anamwonyesha Rosa kwa

mkono).

Mungu: Vere tu Rosa mistica es!

Kweli wewe ni ua la waridi lenye fumbo, Homines interrogabo!

Nitawauliwa watu (Anatoka na radi kubwa inasikika).

Maigizo ya aina hii yanaweza kutoka tu katika akili ya mwandishi mwenye mawazo asi kuhusu

suala la kuwepo kwa Mungu.

Mfano Mwingine

Mashairi yanayopatikana katika diwani za Kichomi (1974) na Karibu Ndani (1988) pia

yanasisitiza mwelekeo wa kitamaushi kwa upande wa mwandishi. Shairi kama ‘Kisu Mkononi’.

51
(Kichomi) linasawiri chagizo, ukosefu wa hakika na hatimaye kujiamulia kwa mshairi kutenda

anavyotaka kabla ya kunaswa na faradhi ya mauti.

Wakati miaka inaibwa mmoja mmoja


Kurudi nyuma, kusimama, kupunguza mwendo
Siwezi, kama gurudumu nitajiviringisha
Mteremko mkali huu
Lini na wapi mwisho sijui

Mbele chui mweusi, nyuma mwanga


Nionako vifurishi maelefu ya dhambi
Kisu, maisha kafiri haya
Kama kutazama nyuma au mbele
Ni kufa moyo mzima!

Sasa kama simba mtu, shauri nimekata


Ya nyuma sasa nisijali, ya mbele sana niyakabili
Kwa ujasiri na uangalifu nitazunguka
Kama ng’ombe aliyefungwa
Kila mpigo wa moyo wangu
Huu mpiga muziki wa maisha (uk. 13)

Mambo matatu muhimu yanayojitokeza katika mtiririko wa shairi hili. (i) mshairi hajui

anakokwenda wala anakotoka (ii) hatari nyingi zimemzunguka mtunzi (iii) kuna azimio la

kujiamulia anavyotaka mshairi.

Ubeti wa tatu unazungumzia mtu aliyekata tamaa. Jazanda ya ‘chui mweusi’ imetumiwa

kuashiria giza na hatari ambayo iko karibu kumpata mtunzi. Na ingawa tumeelezwa kwamba

nyuma kuna mwanga, mwanga huu hauonyeshi matumaini, bali ‘vifurushi maelfu vya dhambi’.

Mtungaji ametumbukizwa bila utashi wake katika dunia iliyochelea kumpa tumani na tamanio.

Kile tunachajulishwa ni kuwa maisha hayana maana kivyake na kipekee. Kwa hivyo, inambidi

mwanadamu anayejikuta katika ajali mbaya ya kuishi kujitafutia maana ya maisha kibinafsi.

52
Msemaji anadai kwamba maisha ni kafiri. Ni kafiri kwa sababu hakuna maadili ambayo

yanaweza kuchotwa kutokana nayo. Hii ndiyo sababu inayomfanya kukaribia kujiua kabla ya

kujiamulia jinsi ya kukabiliana na ulimwengu uliojaa maudhiko.

Uamuzi huu unafanywa kwa matumizi ya tamathali nzito na yenye kuonyesha ari ya

kutoshindwa na maisha. Anasema ‘Sasa kama simba-mtu’. Ukweli ni kwamba hii ni njonzi tupu.

Hata hivyo anajiaminisha kwamba anao uwezo wa kuutawala ulimwengu.

Tamathali ya ‘sima-mtu’inakanushwa na nyingine, ile ya kuwa ‘kama ng’ombe aliyefungwa’.

Kiuyakinifu, ng’ombe wa aina hii hajiwezi katika ngazi zote za maisha. Hana uhuru kwenda

anakotaka. Kuna utata hapa vilevile, pengine ng’ombe huyu amefungwa ili achinjiwe. Katika

muktadha wa hali ya mshairi, jambo hili linamaanisha kuwa mshairi hawezi kuhepa tanzia

iliyomkabili. Mshairi amefungamanishwa na mauti mithili ya ng’ombe aliyefungwa kwamba

tayari kukabiliana na makali ya machinjioni. Lakini kabla kitendo hiki kutokea, mshairi

anapaswa kutekelezea kiwiliwili chake mahitaji yote. Kwa kifupi, shairi la ‘Kisu Mkononi’ ni

mfano mfano mwafaka unaoonyesha namna utamaushi unavyojidhihirisha katika kazi za

Kezilahabi.

Mihimili

1. Kazi ya fasihi inasawiri ukengeushi kiwahusika na kimtindo

2. Wahusika waliokosa tumaini

3. Maswali ya kimsingi yanayosaili nguvu zozote za kibinadamu na za kiroho

zinazojaribu kuudhibiti uhuru wa mwanadamu kutenda anavyotaka.

4. Ufinyu wa maisha ya binadamu

53
5. Jazanda zinazoashiria kiungulia, uchovu, pekecho na kiwewe zinatumika kusawiria

hali ya binadamu.

6. Kusisitiza kwamba mwisho wa juhudi zote za binadamu ni mauti.

7. Kuabudu mahitaji ya kimwili.

Marejeleo

Esslin, Martin. The Theatre of the Absurd. London: Methuen, 1974.

Macquarrie, John. Existentialism. London: Hurtchinson of London, 1972.

Wafula, R. M. ‘Mtindo wa Majaribio katika Amezidi’, Uhakiki wa Tamthilia: Historia na

Maendeleo Yake. Nairobi: Jomo Kenyatta Foundation, 1999.

54
MHADHARA WA TISA

UFEMINISTI
Malengo

(a) Mshiriki anapaswa kueleza historia fupi ya ufeministi baada ya mhadhara huu.

(b) Baada ya mhadhara, mshiriki anatazamiwa kuainisha mikondo ya kifeministi kimaeneo.

(c) Baada ya mhadhara huu, mshiriki anatarajiwa kuainisha mihimili ya ufeministi kwa

ujumla.

(d) Baada ya mhadhara mwanafunzi anapaswa kufanya utafiti mdogo na atofautishe kati ya

maswala ya kifeministi na maswala ya kijinsia.

Utangulizi

Katika sura hii tunachunguza ufeministi. Hii ni nadharia inayoyaangalia na kujaribu kutatua

matatizo yanayowakabili wanawake katika jamii inayotawaliwa na wanaume. Matatizo ya

wanawake yanahusiana na yanasababishwa na jinsia. Hii ina maana kwamba shida nyingi

zinazowakumba wanawake zimengeka kwenye misingi ya uana wao. Kwa sababu ya uana,

mwanamke amewekwa katika kitengo maalumu cha jamii. Nadharia inayohusu masuala ya

wanawake inajaribu kufichua yawapatayo wanawake kama tabaka la kiuchumi na pia kama

wanawake.

Wanawake wamekuwa wakipigania hazi zao katika kipindi chote ambacho binadamu ameitawala

sayari hii. Kinadharia, masuala yameanza kutia fora tangu miaka 70 iliyopita ambapo,

wanawake, hasa wanawake wa kizungu walianza kuzungumza juu ya matatizo yao kwa

utaratibu, yaani katika machapisho.

55
Matapo katika Nadharia Inayohusu Masiala ya Wanawake

Tangu nadharia hii ilipochipuka, matapo yapatayo manne yamejitokeza:

 Kifaransa  Kiingerza

 Kimarekani  Kiafrika

(a) Wafaransa

Wanawake wa Kifaransa wanatilia mkazo juu ya lugha. Utafiti wao unalenga katika kufafanua

namna lugha inavyomtolea maana mtumiaji wake. Wanadai kwamba lugha kama inavyotumika

ni zao la taasubi ya kiume. Inampendelea mwanaume zaidi kuliko mwanamke. Jazanda zenye

kuelezea uwezo, nguvu na mamlaka ni za kiume na ilhali zile zenye kusawiria ulegevu na

kutoweza ni za kike.

(b) Wamerekani

Wanakubaliana na Wafaransa kuhusu lugha. Wanaongezea kwamba wanawake wana namna yao

na ya kipekee ya kuandika na kujieleza. Pia, wanasema kwamba kuna dhamira

zinazorudiwarudiwa katika tungo za wanawake. Wanashughulikia na kazi za fasihi zilizotungwa

na wanawake kwa wanaume maadamu zinaongea ju ya wanawake.

(c) Waingereza

Wanaiona dhima yao kuwa ya kisiasa. Wanafikiria kwamba wenzao wa Kimarekani

wanazunguzia zaidi masuala ya kihisia na kisanaa na kusahau historia na siasa. Kwao, mambo ya

historia na siasa ndiyo huathiri matendo ya wanawake.

56
(d) Waafrika

Wanawake wa Kiafrika wanasisitiza zaidi upinzani dhidi ya utamaduni unayomnyima

mwanamke nafasi ya kutekeleza malengo yake.

Mihimili ya Nadharia

Kutokana na matapo ambayo yamezungumziwa hapo juu, sifa kadhaa na za kijumla zinajitokeza.

(a) Ni nadharia inayotumia fasihi kama jukwaa la kuelezea kwa uyakinifu hali aliyomo

mwanamke ili kumsaidia mtu yeyote kuielewa hali hiyo.

(b) Nadharia hii inanuia kuwasawazisha wanadamu kwa upande wa utamaduni na uana.

Inapigani jamii mpya yenye msingi katika amali za kibinadamu. Baadhi ya amali ni za kike

na za kijadi na ambazo zinadharauliwa katika jamii ya sasa.

(c) Mtazamo huu vile vile unajaribu kuhamasisha utungaji wa kai za sanaa zenye wahusika wa

kike wanaoweza kuigwa, wanawake ambao hawawategemei wanaume ili wajiambulishe.

(d) Ni nadharia inayokuza na kuendeleza hisia za umoja wa wanawake kama kundi

linalodhulumiwa.

(e) Pia, nadharia hii hunuia kuzindua mwamko kwa upande wa wanawake jinsi wanavyojiona,

na uhusiano wao na watu wengine.

(f) Hatimaye, lengo muhimu la nadharia hii ni kuvumbua na kuziweka wazi kazi za fasihi

zilizotungwa na wanawake na ambazo zimepuuzwa kwa sababu ya utamaduni

unaompendelea mwanamume.

Ni mihimili ipi ya ufeministi inafaa katika kuishughulikia fasihi ya Kiswahili?

57
Masuala ya Wanawake na Fasihi ya Kiswahili

Wanawake kwa wanaume wamezungumzia masuala ya wanawake. Baadhi ya watunzi hawa

wameshambulia utamaduni unaomfinya mwanamke. Mifano ya watunzi hawa ni Ari Katini

Mwachofi (1987), Alamin Mazrui (1982) na P. O. Mlama (1978), Clara Momanyi (2006).

Kwa ujumla, watunzi wanaozungumza juu ya masuala ya wanawake wameyatetea b ya

wanawake. Wamepigania usawa kati ya mume na mke katika asasi mbalimbali za maisha.

Tamthilia ya Ari Katini Mwachofi ya Mama Ee imekusudiwa umma mkubwa wa wanawake

wanaonyanyaswa. Mwachofi anaipiga vita jamii inayomwekea mwanamke ada nyingi

zinazompinga kujiendeleza katika nyanja nyingi za maisha.

Manufaa muhimu ya nadharia inayozungumzia masuala ya wanawake ni kwamba inapigania

usawa kati ya wanadamu. Inatetea uhuru wa mwanamke kwa kudai kwamba yeye si kibaraka cha

mwanamume.

Soma Tamthilia ya Mama Ee (A. K. Mwachofi) na riwaya ya Nakuruto (Clara Momanyi).


Jadili baadhi ya matatizo yanayowakabili wanawake. Juhudi gani zinafanywa kutatua baadhi
Marejeleo
ya matatizo hayo.
Wafula, R. M. ‘Sauti ya Kike Katika Mama Ee’, Uhakiki wa Tamthilia: Historia na Maendeleo

58
MHADHARA WA KUMI

NADHARIA ZINAZOHUSIANA NA MTINDO WA FASIHI


Malengo

(a) Baada ya mhadhara huu, mtahiniwa anatarajiwa kutambua baadhi ya mikondo ya nadharia

ya kimtindo.

(b) Juu ya haya, baada ya mhadhara huu, mtahiniwa anatazamiwa kubainisha mihimili ya

mikondo mbalimbali ya nadharia ya kimtindo kivyake.

Katika mhadhara huu tutazungumzia nadharia zinazohusiana na mtindo wa fasihi. Nadharia hizi

zinajaribu kufafanua jinsi lugha ya fasihi livyo. Nazo ni: umuundo, umaumbo na miongozi

mingine ya kiisimu juu ya fasihi. Hizi ni nadharia zinazoingiliana na kutegemeana katika

mitazamo yake kuhusu fasihi. Zote zinatokana na isimu muundo.

Umuundo

Umuundo ni nadharia ya kwanza tutakayoshughulikia. Umuundo unapinga wazo la kijadi

linalodai kwamba fasihi ni tokeo la mchango wa maudhui na fani. Dhana ya kimapokeo kuhusu

fasihi inasema kwamba fasihi ni umbo lenye viungo viwili, maudhui na fani ni kwamba viungo

hivi vyaweza kutenganishwa. Hapa, muundo unafananishwa na mtindo ukimaanisha kwamba ni

lugha inayotumika katika maandishi au mazungumzo ya kifasihi.

Kifasihi, mtindo huelezwa kwa kuainishwa na madhumuni ya msanii. Madhumuni ni dhamira na

mtindo ni jinsi dhamira zinavyowasilishwa. Kauli hii inachukulia kwamba wao kwanza huota

59
katika fikra za mwanasanaa au msemaji yeyote wa kifasihi. Wadhifa wa mwanasanaa ni

kuainisha na kutumia lugha inayofaa kulieleza wazo hilo.

Moja kati ya masomo walilofundishwa watoto wa Kiyunani lilikuwa jinsi kujieleza vyema.

Wayunani walitenganisha jambo lililosemwa na jinsi lilivyosemwa, lugha ikachukuliwa kuwa

‘vazi’ la fikra. Fikra na dhana zilikuwepo, lakini zilienea angani bila umbo au muundo wowote.

Ilibidi fikra ‘zivalishwe nguo’. Yaani, zielewe kimaneno ili zipate sura maalumu. Imain hii

ilichukuliwa wazi kwamba kuna maudhui na mtindo, na kwamba maudhui yanapaswa

kuwasilishwa katika mtindo unaofikiana nayo. Jambo hili lilisisitizwa hasa katika kipindi cha

urasimi na urasimi mpya wa fasihi.

Siku hizi, mbali na maoni haya ya Kirasimi, kuna wataalamu wanaofikiria kwamba madhumuni

ya msanii hayawezi kutenganishwa na jinsi msanii huyo anavyoiwasilisha kazi yake. Kadairi

mwanafasihi anavyowaza ndivyo vipengele mbalimbali vya kuwazia vinapomjia. Msingi wa

maoni haya unapatikana katika falsafa ya umuundo.

Umuundo unashikilia kwamba dunia ni umbo lisiloweza kugawika. Dunia haikuundwa kwa

viungo vinavyoweza kutenganishwa na kujisimamia imeundwa kutokana na mahusiano ya

miundo. Hii miundo inapaswa kufikiriana kijumla.

60
Ferdinand de Saussure

Kabla ya umuundo kutumiwa katika fasihi, ulijaribiwa kwa mafanikio makubwa na mwanaisimu

Ferdinand de Saussure. Katika kuzungumzia muundo wa lugha, De Saussure aliona kuwa lugha

ina sehemu mbili zinazojidhihirisha katika usemaji:

(i) Kuna lug inayojikita katika maongezi ya kila siku – lugha dhahiri.

(ii) Sehemu ya pili ya lugha ni dhahania

Lugha ya kudhaniwa – ambayo daima haibainiki wazi, ijapokuwa baadhi ya kanuni zake

hudhibitika katika maongezi ya kila siku.

Kutokana na fikra hii, Saussure alihitamidi kwamba lugha dhahiri au lugha tumikizi huonyeshwa

katika uwezo wa mtu wa kuunda idadi ya sentensi kadiri anavyotaka. Hata hivyo, mtu hawezi

kutunga sentensi zote zinazoweza kutungwa kwa sababu jambo hili haliwezekani.

Pili, mwanaisimu huyu aliona kwamba licha ya kuwa si rahisi kufahamu tabia ya lugha kwa

ujumla, maongezi ya kawaida yanategemea miundo na tabia za lugha. Yaani lugha ni mfano wa

muundo unaojitosheleza na unaojieleza. Matawi mbalimbali ya lugha hayawezi kutafsiliwa nje

ya mipaka ya muundo huu. Dhima ya kila tawi inatokana na kutegemea kuwepo kwa matawi

mengine. Neno ‘matawi’ limetumiwa hapa kumaanisha viwango tofauti tofauti

vinavyoonyeshwa na lugha kama mfumo wa ishara – sauti za nasibu ambao umekubalikwa

kutumiwa na jamii fulani kuwasiliana na kuelewana. Viwango hivi ni:

61
(i) Fonetiki – kiwango cha lugha kinachoshughulika na ishara – sauti zinazopatikana katika

lugha. Fonetiki huainisha viungo vinavyotumiwa kutamka na mawimbi yanayotumiwa na

matamshi mbalimbali. Fonetiki pia hulenga kuonyesha namna sauti zinavyowasilishwa

kutoka katika sikio moja hadi sikio jingine. Hatimaye, lengo la fonetiki ni kuainisha

mazungumzo bila utata. Tahajia za maneno mengi zinatofautiana na matamshi yake.

Pengine tatizo hili halipatikani katika lugha ya Kiswahili. Lakini lugha zingine kama

Kiingereza zinalo. Katika maneno ‘Sit’, ‘women’ na ‘enough’ sauti (1) inawakilishwa na

herufi tofuati tofauti ambazo ni ‘I’, ‘O’, ‘E’. Katika hali kama hii ambapo utamkaji wa

herufi haubashiriki, ishara za kiisimu zitasuluhisha tatizo hili.

(ii) Fonolojia- kama ningekuwa nikizungumza katika lugha ya Kiswahili, na nikiwa katikati

ya mazungumzo yangu, nipige chafya au nikohoe, yawezekana kwamba mtu asiyefahamu

lugha ya Kiswahili atafikiria kikohozi ni sehemu ya lugha ya Kiswahili. Baada ya kujua

fonolojia ya Kiswahili msikilizaji wangu atadhihirikiwa kwamba kikohozi si sehemu ya

mfumo wa lugha ya Kiswahili.

Fonolojia ni kiwango cha isimu kinachoshughulikiwa ishara – sauti za lugha fulani.

Fonolojia humwezesha mtumiaji wa lugha kuainisha sauti za lugha inayohusika.

(iii) Mofolojia – Hii ni tawi la isimu linalochunguza maneno na aina ya maneno. Pia

ni shabaha ya mofolojia kuchunguza viungo vya maneno na kuonyesha jinsi viungo

hivyo vinavyoambatana kuunda maneno mapya.

(iv) Sintaksi – Hii ni dhana ya isimu inayotumiwa kuelezea utaratibu unaofuatwa katika

ujenzi wa sentensi na miundo yake. Pia, sintaksi inaweza kuchukuliwa kama tawi la

62
sarufi linalochanganua mpangilio wa vipashio katika sentensi.

(v) Semantiki – Ni taaluma inayohusu maana ya maneno na sentensi. Kama ilivyotajwa hapo

awali, uhusiano kati ya neno na maana yake ni wa kunasibisha. Kama neno lingesadifu

maana yake, basi pangekuwa na lugha moja tu ulimwenguni.

Maana ni za aina mbili:

 Maana dhahania - Hii ni maana halisi kwa ambavyo inavyojaribu kuzingatia sifa za

kati za neno na kuzieleza. Maana halisi ya ‘Jipu’ itakuwa ‘Uvimbe unaotuna usaha’.

 Maana husishi – ni maana inayotokana na uhusiano wa maneno katika muktadha

maalumu. ‘Jipu’ laweza kumaanisha hali iliyopea inayopaswa kutumbuliwa.

Matayarisho ya mapigano makali ni ‘jipu’.

(vi) Pragmatiki – Kuna vipengele vya maana ya lugha visivyoweza kufahamika kutokana na

maneno kama yalivyo. Taaluma inayoviteua na kuvichambua vipengele hivi ni

pragmatiki. Pragmatiki huchangamua lugha kulingana na mazoea, mila na maoni ya

mtumiaji.

De Saussure hakuzungumzia viwango vyote vya lugha kwa tafsili. Hata hivyo maoni

yake kwamba viwango hivyo vinachangiana na kutegemeana yamethibitishwa kwa

majaribio ya baadaye. Viwango vya kiisimu vya lugha vinaweza kubadilishwa na kuwa

mihimili ya nadharia ya kimtindo yenye mwelekeo wa kiisimu.

Mihimili

Isimu inaweza kumsaidia mhakiki wa fasihi kwa njia mbili kuu:

63
(a) Fasihi inaweza kuangaliwa kama mfumo mdogo ndani ya mfumo mkubwa wa lugha.

Hapa, lugha ya fasihi inakuwa ni matumizi ya kilugha maalumu katika mfumo mpana wa lugha

kama inavyoeleweka na wanaisimu.

Vilevile, tanzu za fasihi zinaweza kuhakikiwa kwa kufuata mwelekeo huu. Uhusiano uliopo kati

ya dhana ya riwaya na riwaya maalumu iliyochapishwa unashabihiana na uhusiano uliopo kati ya

lugha dhahania na lugha dhahiri.

(b) Baadhi sifa na viwango vya lugha kiisimu vyaweza kumsaidia mhakiki kuichambua kazi

ya fasihi. Kwa kuzingatia jinsi fonetiki, fonemiki, mofolojia, sintakisia, semantiki na pragmatiki

vinavyochangiana na kutegemeana mhakiki anaweza kuisoma kazi ya fasihi kimfumo.

(c) Imetajwa kitambo kwa lugha ni mfumo wa sauti – ishara. Lugha zote zina sifa

zinazozifananisha. Baadhi ya sifa bia hizi humsaidia mhakiki. Moja kati ya sifa bia za lugha ni

utata. Jambo linaweza kuelezwa katika namna nyingi. Kiisimu, kuwepo kwa sanaa ni ushahidi

unaonyesha kwamba lugha inaweza kuvyaziwa miundo mingi kadiri mtumiaji wake anvyotaka.

Lugha ina uwezo wa kuvuka vizingiti vingi kimaana.

Dhima kubwa ya washairi, watunzi w riwaya na wahakiki ni kubainisha na kuchanganua utata

kama kipengele kinachomwezesha mwanasanaa kutumia maneno machache kuwasilisha dhana

pana au kutumia maneno mengi kuwasilisha maana ndogo.

64
Sifa nyingine ya lugha inahusiana na unasibu wa maneno. Uhusiano kati ya neno na maana yake

ni wa kunasibisha. Matumizi ya lugha hudhihirika katika muktadha maalumu. Lugha ya kifasihi

hutilia maanani muktadha kila wakati.

(d) Fonolojia, mofolojia, sintaksia na semantiki pia vyaweza kumwauni mwanafasihi.

Kutokana na fonolojia, mofolojia na sintaksi, washairi, waandishi wa tamthilia na riwaya hujnga

vina, mizani na mitiririko maalum katika kazi zao. Shadda na kidatu pia huweza kuyapa

matamshi maana ya kifasihi. Semantiki huhusu maana. Maana nyingi ni za aina mbili. Kuna

maana dhahania na maana husishi. Kifasihi maana hizi zinaweza kufasiliwa kama maana dhahiri

na maana ya kitamathali. Ujuzi wa semantiki unapaswa kutumiwa kufasiri lugha ya kimafumbo

– kama ile inayotunika katika riwaya ya Mafuta Kusadikika na Walenisi. Semantiki hutuwezesha

kufahamu jinsi lugha isiyokuwa ya kimafumbo hugeuka ikawa ya kimafumbo. Pragmatiki –

inashughulikia matumizi ya lugha yanayotegemea vikwazo anavyokabiliana navyo mtumiaji wa

lugha. Fasihi inahusu uchanganuzi, uteuzi na matumizi ya maneno kwa uangalifu. Hivyo

inapaswa kutii mikatale ya jamii na kutumia lugha kulingana na miktadha mbalimbali.

Kwa ujumla, kama ambavyo muundo wa lugha ni mfumo, muundo wa fasihi una vipengele

vinavyotegemeana na vianvyoelezwa katika muktadha wa vipengele vingine. Katika kazi ya

fasihi kuna vitengo vya kisanaa kama yaliyomo, ploti, wahusika na lugha. Hakuna kipengele cha

fasihi kati ya hivi kitakachoelezwa vizuri katika upekee wake. lazima kielezwe kwa kuzingatia

kuwep kwa kazi za vipengele vingine. Katika kuzungumzia wahusika, ploti, wahusika

watashirikishwa.

65
Nadharia ya umuundo husisitiza vipengele vya kazi ya sanaa, jinsi vianvyohusiana hadi

kuikamilisha kazi hiyo. Huangalia namna sehemu mbalimbali za kazi ya sanaa zimefungamana.

Riwaya, kwa mfano, huangaliwa kama zao linalojitosheleza. Riwaya ina msuko, wahusika na

mbinu mbalimbali za kusimulia ambazo huingiliana na kuchangiana. Mambo haya ndio huifanya

riwaya kuwa muundo unaojitosheleza.

Umaumbo

Nadharia ya umaumbo na ya ummundo zinafanana kwa jambo moja – nalo ni kwamba zote

zinapinga wazo la kimapokeo juu ya fasihi. Wazo la kimapokeo juu ya fasihi ni kwamba fasihi

ina vitengo viwili, Maudhui (yaliyomo) na mtindo (jinsi yaliyomo yanavyowasilishwa). Hata

hivyo, kila mojawapo ya nadharia hizi inapinga dhana ya kimapokeo kivyake pia, msisitizo ni

tofauti. Umuundo hujaribu kuonyesha uhusiano uliopo kati ya ishara na vipashio mbalimbali

vinavyopatikana katika kazi ya sanaa. Kwa upande mwingine, umaumbo hulenga kuainisha sifa

za kisanaa zinazopatikana katika fasihi kama taaluma.

Umaumbo ulianzishwa mnamo mwaka wa 1904 huko urusi. Mwasisi wa nadharia hii alikuwa

Viktor Shklovsky. Aliandika makala ‘ufufuo wa neno’. Katika haya makala Shklovsky

alizungumzia umuhimu wa lugha katika kuelezea maana ya fasihi.

Katika mwaka wa 1919, chama cha waitifaki wa Shlovsky kiliundwa kwa shabaha ya kuelezea

na kuchanganua lugha ya ushairi. Chama hicho kuliwashirikisha Boris Tomashevsky, Viktor

Zhirmunsky, Boris Elkhebaum na Roman Jakobson. Wahakiki hawa walidai kwamba kazi ya

fasihi hujitosheleza – yaani kazi ya sanaa inapaswa kuelezwa – kwa kutumia kanuni za kisanaa.

66
Wanasema kwamba hapo zamani fasihi ilifanuliwa kwa kurejelea masomo mengine. Jambo hili

lilifanya fasihi kutokuwa somo huru. Ili liwe huru hapana haja ya kurejelea masomo mengine

kama historia, sisiolojia na saikolojia ili kuelezea fasihi. Kwake Shklovsky, fasihi ni tungo

zilizotungwa kwa kutumia mbinu za kipekee za kisanii ili zionekane sanifu kadiri zinavyoweza.

Roman Jakobson naye anasema kwamba lengo la fasihi ni kubainisha usanaa katika sanaa ya

maneno. Usanaa unamaanisha sifa zianzouainisha utunzi hadi kiwango cha kuweza kuitwa kazi

ya fasihi. Kwa ujumla wanaumaumbo wanadai kwamba fasihi inajijua na hujitangaza yenyewe

kwa kuweza hadharani sifa zake za kati.

Kwa mfano, shabaha muhimu ya riwaya ni kusimulia hadithi. Kila kiungo cha kusimulia kipo ili

kuiwezesha riwaya kuwepo. Maudhui yni sehemu ya hayo masimulizi. Jambo hili ni kinyume na

imani ya kimapokeo kwamba maudhui na mtindo ni mambo yanayoweza kutengeka.

Wajibu wa mhakiki anayetumia nadharia ya umaumbo ni kutambua mbinu za kusimulia (kama

taharuki, sadifa, mtiririko, ploti na muwala) na kuonyesa dhima ya mbinu hizo katika kufanikish

mazimulizi.

Mambo haya yanaweza kubainika katika kazi yoyote ya fasihi. Kutokana na utumiaji wa mbinu

ya sadifa katika riwaya ya Utubora Mkulima, utubora anakutana na wahusika mbalimbali. Kuna

wale anaokubaliana nao kama Radhia na wengine ambao hakubaliani nao kama Sheha na

Makuu. Kutokana na Sadifa hii, masimulizi ya utubora yanafaulishwa.

67
Kwa upande mwingine lengo la utungo wa kishairi ni kudhihirisha mbinu zinazolifanya shairi

kuwa na mvuto wa kishairi kadiri linavyoweza. Ni mbinu gani zimeajiriwa na mshairi kufaulisha

shairi hili:

Wakati ni kitu chema, ukujiyapo na heri


Hukupambiya neema, kwa laili na nahari
Ukafurahi mtima, na uso ukanawiri
Lakini ni mdawari, ugeukapo wakati

Wakati hutukukuza, ukafanywa mashuhuri


Wendapo ukapendeza, kama anga la gamari
Huzagaa penye giza, kwa nuru kutanawiri
Lakini ni mdawari, ugeukapo wakati
(Nassir, 1970: 102)

Ukariri wa maneno ‘wakati’ na ‘lakini’ unalizidishia shairi hili sifa za kishairi pia. Mtunzi

ametumia vina na mizani maalumu. Hali ya ukinzani vilevile inaufanya utungo huu kuwa wa

kishairi.

Mihimili

1. Kazi za fasihi hasa za kishairi zinapaswa kutumia vipengele mahsusi vya takriri.

2. Kazi za fasihi zinapaswa kutumia vipengele mahsusi vya uchimuzi

3. Kazi ya fasihi itumie vipengele vyovyote maadamu vimeiwezesha kujirejelea.

Orodhesha sifa nyingine za kishairi zinazopatikana katika kipande cha shairi kilichonukuliwa hapo
juu

68
MHADHARA WA KUMI NA MOJA

UJENGUZI, USEMEZANO NA UHALISIAJABU


Malengo

Baada ya mhadhara huu, mshiriki anapaswa:

(a) Kueleza sifa bainifu za nadharia za kisasa leo.

(b) Kutoa mifano ya nadharia za kisasa leo.

(c) Kutaja baadhi ya mihimili ya (i) ujenguzi (ii) usemazano na (iii) uhalisiajabu.

Utangulizi

Nadharia za hapo awali zilitia maanani sana mantiki ya usomaji. Kazi ya sanaa ilitarajiwa kuwa

na mashikanamo ambao ungeiwezesha kujitawala yenyewe. Hivyo ndivyo mambo yalivyo katika

uhalisia, umuundo na umaumbo miongoni mwa nadharia nyinginezo. Kinyume na haya,

nadharia tutakazozungumzia hivi punde zinapuuza mihimili ya kimapokeo kuhusu kazi ya fasihi.

Ujenguzi, usemezano na uhalisiajabu zinaonyesha kwamba muwala au mshikamano wa kazi ya

fasihi kama ilivyozewewa na mapokeo si muhimu tena. Nadharia hizi zinashikilia kwamba kazi

ya fasihi hujengwa kutokana na mchangamano wa tajriba. Baadhi ya tajriba hizi zinapatikana

katika kazi inayosomwa. Nyingine zinapatikana nje ya kazi hiyo.

(a) Ujenguzi

Ujenguzi au ujenguaji unapingana moja kwa moja na umuundo na mitazamo mengine

inayoichukulia lugha na fasihi kuwa miundo inayojitawala. Waitifaki wa ujenguzi wanaamini

kwamba muundo wa lugha na fasihi huendelea kubadilika. Kwa upande wa fasihi hii ina maana

69
kwamba kila usomaji wa kazi ya sanaa ni toleo jipya la kazi hiyo. Uhakiki hujaribu kuiweka kazi

ya fasihi katika miundo inayofahamika na mchambuzi wake.

Kutokana na madai ya ujenguzi, hakuna toleo la mwisho la kazi ya fasihi. Hii ndio sababu

inayowafanya wahakiki kutoa fasiri tofauti za jambo moja baadhi yazo zinazopingana, maadamu

wana ushahidi wa kutosha. Mwasisi wa nadharia hii alikuwa Mfaransa Jacquies Derrida. Derride

aliamini kwamba neno liliopo huendelea kuahirisha maana yake ya mwisho. Jambo hili huifanya

maana kukosa utengamano. Waitifaki wa ujenguzi kama J. Hills Miller wanasema kwamba

ujenguzi hauivunji kazi ya fasihi vipande vipande. Kinyume na haya, ni nadharia inayosawiri

kwamba kitambo kazi ya fasihi imejivunja yenyewe.

(b) Usemezano

Hii ni dhana inayotokana na kiarifa kusemezana. Mwasisi wa usemezano (dialogism) alikuwa

mwanaisimu na mhakiki wa fasihi Mrusi Mikhail B. Bakhtin. Bakhtin aliishi kati ya mwaka wa

1895 – 1975. Kwake Bakhtin kazi ya fasihi ni uwanja ambao una mwingiliano wa matini. Katika

kazi ya fasihi, sauti mbalimbali zinaingiliana na kupiga mwangwi katika kazi nyinginezo

zilizotangulia, zilizopo au zitakazokuja baadaye. Mwingiliano huu unashirikisha pia

mazungumzo ya kila siku yanayotokea kando ya matini zilizorasimishwa. Kutokana na maoni ya

Bakhtini hakuna matini iliyo asilia zaidi. Kila matini inarejelea matini nyinginezo. Uhusiano

uliopo kati ya hadithi kama Adili na Nduguze na Alfu-Lela Ulela. Kitabu cha kwanza

unathibitisha hoja ya Bakhtin. Kuna mwangwi wa Alfu-Lela Ulela. Kitabu cha kwanza

unathibitisha hoja ya Bakhtin. Kuna mwangwi wa Alfu-Lela katika Adili na Nduguze.

Onyesha sifa linganisha ujenguzi, usemezano na uhalisiajabu.


Soma Alfu-Lela Ulela Kitabu cha kwanza na Adili na Nduguze: Jadili jinsi kazi hizi
zinavyofanana na kutofautiana. 70
(c) Uhalisiajabu

Ni nadharia ambayo inakiuka sifa za uhalisia kama zilivyozoelewa na waandishi wa karne ya

kumi na tisa na ishirini. Katika uhalisiajabu, matukio yasiyoaminika (ya kifantasia) husawiriwa.

Mambo ya kiajabu yanaelezwa kwa namna ya moja kwa moja na kuonekana kuwa ya kawaida.

Hali za kushangaza na kuogofya huwasilishwa kama kwamba ni ya kawaida. Katika uhalisiajabu

ndoto na uhalisi vinachanganywa. Pamoja na haya, mipaka yote huvunjwa. Hata wakati nao pia

hausongi kwa njia ya wendo. Riwaya ya W. K. Wamitila ya Binadamu! na ya S. A. Mohamed ya

Babu Alipofufuka ni mifano mwafaka ya kazi za kihalisiajabu. Vilevile riwaya za S. A.

Mohamed Dunia Yao (2006) na Mhanga Nafsi Yangu (2011) ni mifano ya kazi za sanaa

zinazoweza kuhakikiwa kwa kutumia uhalisiajabu.

Soma Bin-Adam! (Wamitila) au Babu Alipofufuka au Mhanga Nafsi Yangu(S. A.


Mohamed). Bainisha mihimili ya uhalisiajabu katika kazi hizi.

Marejeleo

Bakhtin Mikhail. The Dialogic Imagination. Austin: University of Texas Press, 1981.

Allen, Graham. Intertextuality. London & New York: Routledge, 2000.

Gromov, M. ‘Postmodernistic Elements in Recent Swahili Novels’, Nairobi, 2002.

(Haijachapishwa).

Cooper, B. Magical Realism in West African Fiction. New York: Routledge, 1998.

Derrida, Jacques. Of Grammatology. Baltimore: Johns Hopkins University Press, 1967.

71
MHADHARA WA KUMI NA MBILI

UJUMI-MWEUSI
Malengo

(a) Kueleza maana na usuli wa nadharia ya ujumi-mweusi.

(b) Kufafanua hoja kuu za waasisi wa ujumi-mweusi.

(c) Kuainisha matapo ya ujumi-mweusi.

(d) Kuorodhesha mihimili ya ujumi mweusi na kuonyesha utendakazi wake katika kuhakiki

kazi za fasihi.

Kwa mujibu wa maelezo ya Pio Zirimu (1971), Ujumi ni vigezo vinavyotumiwa kuuanisha

urembo wa sanaa. Vigezo vinavyofaa kutumiwa kuainisha kadhia zenye kuthaminiwa vinatokana

na hali halisi ya jamii inayohusika. Zirimu anasema kwamba jamii mbalimbali zina aina

mbalimbali za ujumi. Jamii za kijamaa zina ujumi wa kijamaa; nazo jamii za kitabaka

hujishughulisha zaidi na kadhia zinazothaminiwa na tabaka tawala. Kwa vyovyote vile, ujumi na

thamani zake hutokana na jamii fulani.

Kulingana na maoni ya Zirimu, wahakiki wanaotumia mbinu za kigeni kuihakiki fasihi ya

Kiafrika si wahakiki halisi, ni waigaji tu. Uhakiki unaofaa, anaendelea kusema Zirimu, ni ule

unaoibuka kutokana na jamii nayochambuliwa.

Kosa la Mwafrika ni kule kufikiria kwake kwamba Uyunani ndicho kitovu cha kila tulichonacho.

Kuiga kwa mawazo ya Wagiriki hutokea ijapokuwa mawazo hayo yamechafuliwa na wasomi wa

kimagharibi. Maoni ya Zirimu ni kwamba ujumi mweusi unapaswa kutokana na mazingira

wanayopatikana watu weusi.


72
Kwa nini Ujumi Mweusi?

Ili kufahamu sababu zilizowafanya watu weusi popote pale walipokuwa kuanza kushughulikia

urembo wa utamaduni wao, historia yao yapaswa kueleweka. Tangu Mwafrika aanze

kukurubiana na wageni, amekabiliwa na matusi na kashfa za aina nyingi. Ithibati kutokana na

vitabu vya kimagharibi vya historia, falsafa vinamsawiri kama kiumbe ambaye hawezi kurithi

chochote kutoka ardhini kwa sababu yeye ni mshenzi kupita kiasi au yeye amelaaniwa kuwa

mtumwa wa watu wa rangi nyingine tangu aumbwe.

Kuna hadithi moja katika Biblia inayosimulia juu ya laana iliyowekwa juu ya mmojawapo wa

watoto wa Nuhu kwa kumchekelea babake. Ham alilaaniwa kwa sababu alithubute kuona uchi

wa babake. Kulingana na wageni wengi, kisasili hiki ndicho kitovu cha maumbile ya Mwafrike

na tajriba ngumu alizozipitia. Utumwa mwa Mwafrika, weusi wake na nywele zake ngumu ni

baadhi ya matokeo ya laana ya Nuhu juu ya mwanawe. Hatimaye, Mwafrika anatokana na kizazi

cha Ham. Watoto wengine wa Nuhu walibarikiwa kutegemea kiasi cha fadhila waliyomtendea

baba yao (Mwanzo, 9/21-29).

Hadithi kama hizi zilipokelewa na waandishi na wanafalsafa wa Kimagharibi na kutumiwa kama

sababu za kumweka Mwafrika nyuma katika harakati za binadamu za kustaarabika. Alipokuwa

akiandika falsafa ya historia, Hegel alitongoa kauli zifuatazo kuhusu Afrika:

Afrika halisi (Afrika Kusini ya jangwa la sahara) haijaingiliana wala kuhusiana na jamii

nyingine za ulimwengu. Afrika ni kama nyumba iliyojifunga kwa ndani na kujihusilisha

kusijulikane chochote kilichomo. Afrika ni eneo lililozaliwa juzijuzi, linalobarizi nje ya mipaka

73
ya historia inayofahamiwa na kujulikana. Ni eneo ambalo limefunikwa gubigubi kwa utandu wa

giza totoro, giza la usiku. Ijapokuwa Mwafrika bado anaishi porini na hawezi kamwe kuguwa,

anasawiri kwa ishara za mbali sifa za kibinadamu kama tunavyozifahamu. Hata hivyo, huwezi

kutarajia ustaarabu wa aina yoyote kutokana na kiumbe cha aina hii. Kwa hayo, tunaliacha eneo

la Afrika na hatutalitaja tena daima dawamu. Afrika si sehemu ya ulimwengu kihistoria.

Mizunguko na alama za kihistoira zinazopatikana katika sehemu ya kaskazini ya Afrika ni

matokeo ya matendo ya Waasia na Wazungu. Kile tunachokifahamu kuwa Afrika ni roho

ambayo ni mtovu wa historia, iliyokwama katika tope las uasili wake na ambayo haijabadilika

wala kukua tangu hapo na kuota kwake. Tumegusia kwa kifupi sura ya ulimwengu ulivyokuwa

kwa jumla kabla ya taathira zozote za kihistoria kutokea. Historia ya ulimwengu husoma ikitokea

mashariki ikieleka magharibi. Uropa ni hatima ya historia, Asia chanzo chake. (Sehemu hii

imedondolewa kutoka Zirimu, 178-179).

Wakoloni, wamisieni na walanguzi wengine na Kizungu waliyjua mambo haya hata kabla ya

kuja barani Afrika. Walipofika, mawazo yao juu ya Mwafrika yalikuwa kitambo yameimarika.

Taasubi ya wageni, pamoja na ukosefu wao wa kuzielewa jamii za Kiafrika katika mising yake

ya kipekee uliwafanya kukubaliana na maoni kama haya. Katika mshabaha huu, kanisa

haikukuwa taasisi iliyowaongoa ‘washenzi’ kutokana na dhambi zao na kuwaleta karibu Mungu;

Kanisa ilikuwa taasisi iliyotumiwa kumleta Mwafrika karibu na utamaduni na ustaarabu wa mtu

mweupe (Fanon).

David Hume anaelezea vingine kuhusu ukosefu wa sayansi na sanaa barani Afrika. Anaamini

kwamba wanadamu wa rangi mbalimbali wanatokana na wazazi wa mwanzo tofauti tofauti.

74
Baadhi ya wazazi hawa wa mwanzo walikuwa wajinga, wengine walikuwa werevu. Wajinga

walizaa wajinga na werevu wakazaa werevu. Kwa maoni yake Hume, Waafrika ni wajinga kwa

sababu wazazi wao wa mwanzo walikuwa wajinga. Ananukuliwa na P. D. Curtin (1964)

akisema:

Hakujakuwepo na taifa lililostaarabika isipokuwa la watu wenye umbo jeupe. Hata watu
binafsi wenye vipawa vya kutafakari na kuunda ni weupe. Watu wasiokuwa weupe
hawaonyeshi uvumbuzi unaobainisha umakinifu wa kufikiria miongoni mwao; hawana
sayansi wala sanaa. Tofauti hizi sare hazingetokea katika mataifa mengi ya nyakati
nyingi kama watu hao hawangekuwa tofauti tangu hapo na uumbaji (uk. 14).

Maoni kama haya yalipalilia na kukuza falsafa ya kikoloni na utumwa. Nia ya falsafa hii ilikuwa

kumwonyesha Mwafrika kimatendo na kimatamshi kuwa alikuwa kiumbe duni. Akizungumza

kuhusu ulimwengu wa kikoloni, Frantz Fanon anasema:

Ulimwengu wa kikoloni una falsafa kuwa kila kitu kilichomo duniani hutokana na
mwangaza au giza, ama hutokana na kitovu cha halali au cha haramu. Ni dunia
iliyojengeka kwenye nguzo kwamba mtu huzaliwa kitambo akiwa amemarikiwa au
kuharamishwa. Ni dunia iliyojengeka kwenye nguzo kwamba mtu huzaliwa kitambo
akiwa amebarikiwa au kulaaniwa. Mkoloni haridhishwi na kumwaangamiza kiwiliwili
mateke wa utawala wake kwa huduma za jeshi au sakri tu; mkoloni vile vile humhujumu
mtawaliwa kihisia na kinafsi. Mbali na kuonyesha kwamba hakuna thamani zozote
zinazopatikana katika utamaduni wa watawaliwa, au hazikuwemo katika jamii ya
mtawaliwa, yeye mtawaliwa huchukuliwa kuwa mtove wa utamaduni. Pamoja na haya,
mtawaliwa anasawiriwa kuwa pingamizi na hata kile cha kinyume cha utamaduni huo
wenyewe. (Uk. 41).

Hii haikosi kuwa ndiyo sababu mkoloni kufikiria kwamba ingechukua muda mrefu sana kwa

Mwafrika kuzingatia mbinu za usanii wa fasihi. Maoni ya wakoloni ndio yamemsukuma

Mwafrika kuutetea utu wake, utamaduni wake na sanaa yake.

Ujumi mweusi umetokana na mazingira yaliyoshuhudia kukandamizwa kwa Mwafrika katika

nyanja zote za maisha. Ni upinzani dhidi ya hujuma zilizofanywa na wakoloni dhidi ya heshima

yake. Hata katika zama hizi, rangi nyeusi, katika falsafa za Kimagharibi ni ishara ya mauti na

75
kuzimu; ni ishara ya milki ya shetani. Juu ya kuitetea heshima ya Mwafrika moja kwa moja,

baadhi ya Waafrika wameunda istilahi zinazoonyesha ustaarabu na urembo wa uafrika. Baadhi

ya istilahi hizi ni kama: Wamerikani Weusi, Waislamu Weusi, Nguvu Nyeusi n.k. Hizi istilahi

zimedhamiriwa kuonyeshwa kwamba Mwafrika ana fahari juu ya utu wake, range yake na hata

matendo yake.

Ujumi Mweusi – Mitazama ya Waasisi na Waitifaki

Kwa mujibu wa maelezo ya Lepold Sedar Senghor, Ujumi Mweusi ni ‘jumla ya ustaarabu na

mapokezi mengine yanayothaminiwa na ulimwengu wa Kiafrika’. Waandishi kama Senghor,

Okot P’Bitek na Chinua Achebe wameusifu utamaduni wa Kiafrika. Achebe amesema bila

kuficha kuwa yeye ni mwamini wa mizimu na miungu wa Kiafrika. Riwaya zake za mwanzo

zina nia ya kudhihirisha kwamba Waafrika walikuwa na utamaduni wao. Achebe amenukuliwa

akisema:

Nitaridhishwa vya kutosha iwapo riwaya zangu (hasa zile zinazosawiri mandhari ya

zamani) hazitekelezi lolote lile isipokuwa kuwafundisha wasomaji wake kwamba zamani

zao hazikukuwa usiku mmoja mrefu wa ushenzi waliozinduliwa kutokana nao na

wamisheni wa kwanza.

Linganisha na uchanganue mawazo ya Cesaire na Senghor

Tafsiri yetu kutoka ‘The Novelist as Teacher’, katika African Writers on African Writing (ed. G.

D. Killam) uk. 4.

76
Waandishi wengine kama vile Ferdinand Oyono (Boi) na Okot P’Bitek Wimbo wa Lawino

(wimbo) wamesuta Waafrika wanaoiga utamaduni wa kigeni bila kuuchambua. Akiwa

amekasirika, P’Bitek anawatukana Waafrika walioelimika akisema wao ni waigaji kwa kiasi cha

kupotosha yale yanayoigwa. Katika riwaya ya Boi, Oyono anaonyesha ni kwa kiasi gani

mwafrika mwenyewe amekubali kwa hiari yake, kujiweka chini ya himaya ya wakoloni.

Ujumi Mweusi – Matapo Yake

Matapo mawili ya ujumi mweusi yalijitokeza katika miaka ya 50 na 60. Moja ni lile la Leopold

Senghor na jingine ni la Aime Cesaire. Kama tulivyotangulia kusema, Senghor, alieleza ujumi

mweusi kuwa ujumla wa mambo yanayojenga ustaarabu wa ulimwengu wa Kiafrika. Kiini cha

mambo haya kilisawiriwa katika weusi wa Mwafrika. Kwa kuwa Mwafrika ni mweusi, ana mila

na mapokezi ya kipekee yanayomwainisha kutokana na watu wa rangi nyingine. Tapo hili

lilipinga vielelezo vilivyotumiwa na wazungu kuwachora Waafrika na ulimwengu wao. Juu ya

haya, Senghor na wale waliofuata mitindo yake aliyachukua mambo yale yale yaliyolundikwa

kashfa na wazungu na kuyapa maana ya heshima, kuyavaa majoho ya taadhima.

Hata hivyo, Senghor na wenzake walishindwa kabisa kuzungumzia maswala ya ubaguzi wa

rangi na ukoloni, na kuyapa maswala hao majawabu yanayoyasadifu. Akina Senghor

hawakupendelea maongozi ya Ufaransa. Maongozi ya Ufaransa yalikusudia kuikata mizizi ya

Mwafrika na kumfanya Mwafrika huyo ajihisi kuwa Mwafrika-Mzungu. Katika tungo zake za

ushairi. Senghor alichora bara la Afrika katika taswira za kilimbwende. Alilionyesha bara hili

kuwa na urembo asili na roho tajiri isiyokuwa na uchoyo (Reed, Uk. 50). Mashairi ya Senghor

yanaonyesha maisha ya Kiafrika yakiwa na ufungamano mkubwa na mazingira asili

77
anamopatikana Mwafrika. Jazanda anazotumia mshairi zinaonyesha hali hii. Ushairi wake

unasifu urembo mweusi, na unalingana sana na jinsi Mulokozi anavyomsifu Mtage katika

tamthilia ya Mukwava wa Uhehe (1979). Kile anachokifanya Senghor ni kuzigeuza kichwa

mgomba taswira alizopewa Mwafrika na mtu mweupe. Badala ya kutumia tamathali zinachukiza

kumsawiri Mwafrika, Senghor alichagua lugha inayompa hadhi Mwafrika badala ya

kumdhalilisha.

Senghor aliishia katika kusifu baadhi ya upungufu wa Mwafrika. Pamoja na haya ushairi mwingi

wa Senghor unadhilisha mwito wa usemehevu. Mshairi anamwomba Moja awasamehu Wazungu

kwa kuwatendea Wafrika nuksani zisizostahili. Kejeli ni kwamba wakati alikokuwa akiandika

Senghor ulikuwa muhula wa utetezi mkali wa kisiasa, ambapo Waafrika katika sehemu nyingi za

bara waliwajibika kutumia silaha kujikomboa kutokana na mikatale ya ukoloni. Ni ajabu

kwamba Senghor angeweza kuzungumzia usamehevu katika mazingira haya.

Waaidha Senghor aliisifu Ufaransa kwa kumfundisha utamaduni mzuri. Pia, Senghor alimwona

Mwafrika kuwa kiumbe anayehisi zaidi kuliko kufikiria. Naye Mzungu alionekana kuwa kiumbe

anayetafakari, anayechambua na mwenye kuimiliki taaluma ya kisayansi. Mshairi huyu alifikiria

kwamba ndoa baina ya tabia za kipekee na kizungu kama vile kutafakari na tabia za kipekee za

Kiafrika kama kuhisi ingezalisha utamaduni mwafaka ambao ungekubalika duniani kote. Bila

kufahamu, Senghor alidhahililisha hadhi ya Mwafrika. Inafahamika ni akina nani walikuwa na

ustarabu wa hali ya juu. Pili, na pengine hili ndilo jambo muhimu zaidi, Senghor

hakujishughulisha na uchumi wa Afrika katika falsafa yake ilhali utamaduni wa watu

unategemea uchumi wao.

78
Amie Cesaire anawakilisha tapo lingine la ujumi-mweusi. Tungo zake zinabainisha kwamba

hapawezi kuwa na uhusiano wa kidugu baina ya Mwafrika na Mzungu ... Anashughulikia sana

taasubi inayomfanya Mzungu kujifikiria kuwa yu bora kuliko Mwafrika. Picha anazotumia

kusawiria dhamira zake zinaonyesha uchungu alionao juu ya madhambi aliyotendewa Mwafrika.

Yeye ni mtetezi wa wala njaa na hafichi chuki yake juu ya mnyanyasaji na mnonyaji wa

Mwafrika. Kwake, vita vya wanaoteswa dhidi ya watesaji wao ni mithili ya mashua inayoelea

kwenye bahari ya mawimbi mengi. Imani ya Cesaire ni kwamba lich ya udhaifu wa

wadhuhimiwa, ushindi na haki viko upande wao.

Kwa hivyo, Cesaire anamsuta Mzungu akitumia kauli wanazotumia Wazungu kujisifu nazo.

Anasema kwa mfano kwamba ijapokuwa Wazungu wanajisifu kuwa ni wao walioleta ustaarabu,

huo ustaarabu umeletwa kwa kuwatumikisha watu wengine na hana hofu nao.

Ujumi mweusi kama tulivyotangulia kusema ni nadharia iliyozuka katika mazingira ya ubaguzi

wa rangi na ukoloni. Nadharia hii imejizatiti kumrudishia Mwafrika hadhi yake, adi

iliyobomolewa na Wazungu. Imeonyesha kwamba falsafa zilizokuwa zikitumiwa na Wazungu

kuwatawala Waafrika zilikuwa za uongo.

Ujumi-Mweusi – Mihimili Yake

(i) Nyimbo zinazousifu uafrika na kutilia mkazo usawa wa watu wote weupe kwa weusi.

79
(ii) Majasiri wa Kiafrika kuonyeshwa katika kazi za sanaa.

(iii) Utumiaji wa lugha za Kiafrika katika uandishi.

(iv) Okot P’Bitek

(v) Ngugi wa Thiong’o (Gikuyu na Kiswahili)

(vi) Matumizi ya mbinu zinazofungamana na Uafrika au mazingira ya Kiafrika (Taswira na

misimbo).

 Mibuyu – hali inayotatanisha

 Mikuyu – kikale – kinachowakilisha utamaduni wa Mwafrika. Hii ni tashira ya

kile kinachowafungamanisha Waafrika pamoja. Katika tamthilia ya Wingu Jeusi,

waahusika wenye nia ya kuutetea utu wa Wachinato wanaombea chini ya mikuyu.

 Mbinu nyingine ni istiara – hurafa au harafa

 Maudhui ya Kiafrika

Soma tamthilia ya Wingu Jeusi (1987) na Sumu ya Bafe (2006) (C. N. Chacha). Ainisha na
ujadili sifa za kisanaa zinazotokana na utamaduni wa Mwafrika.

Unafikiria kuna hatari gani zinazoweza kutokana kutumia ujumi mweusi kiholela?

Marejeleo

Achebe, Chinua. ‘The Novelist as Teacher’ African Writers on African Writing. (G. D. Killam).

London. Heinemann, 1973.

Cesaire Aime. Notebook of a Return of the Native Land. Middletown, Connecticut Wesleyan

University Pres,s 2001.

80
Senghor, Leopold Sedar ‘Negritude’ A Humanism of the Twentieth Centyury’, Colonial

Discourse and Post Colonial Theory: A Reader. Ed. Patrick William and Laura Chrisman.

New York: Harvester/Wheatsheef, 1993.

Wafula, R. M. ‘Jazanda na Istiara katika Tamthilia’, Uhakiki wa Tamthilia: Historia na

Maendeleo yake. Nairobi. Jomo Kenyatta Foundation, 1999.

Zirimu, P. O. et. al. Black Aesthetics: Papers from a Colloquim held at the University of Nairobi.

Nairobi: East African Literature Bureau.

Hitimisho

Katika kazi hii tumejaribu kuainisha baadhi ya nadharia za uhakiki wa fasihi. Pia, tumeonyesha

jinsi zinavyoweza kutumika kuzifahamu kazi tofauti tofauti za fasihi. Soma kazi ambazo

zimetajwa katika mwongozo huu pia ili ufaidike zaidi. Kumbuka kwa kwamba ni kupitia katika

usomaji wa kinadharia ndipo utakavyoweza kujifunza usomaji wenye misingi ya kitaalamu. Hizi

ni baadhi ya Nadharia tu . Utafaidika zaidi ikiwa utarutubisha usomaji wako kwa kusoma vitabu

muhimu kama:

Marejeleo:

Njogu Kimani & Chimerah Rocha. Ufundishaji wa Fasihi: Nadharia na Mbinu

Nairobi: Jomo Kenyatta Foundation, 1999.

Senkoro, Fikeni. Fasihi na Jamii. Dar es Salaam: Press & Publicity centre, 1987.

Wafula, R.M. Nadharia za Uhakiki wa Fasihi

Nairobi: Jomo Kenyatta Foundation, 2007 ( toleo la 2013)

Wafula, R.M. Uhakiki wa Tamthilia: Historia na Maendeleo yake. Nairobi: Jomo Kenyatta

Foundation, 2003.

81
Wamitila, K.W. Uhakiki wa Fasihi. Nairobi: Phoenix, 2002.

Wamitila, K.W. Kanzi ya Fasihi. Nairobi: Vide~muwa, 2008.

KILA LA HERI

82

You might also like