You are on page 1of 44

SHULE KUU YA SAYANSI ZA JAMII

IDARA YA LUGHA NA INSIA


MSIMBO WA KOZI: MLA 5107
MADA YA KOZI: Mikabala ya Nadharia za Kiisimu (Trends in Linguistic Theory)
SAA: 42
MADHUMUNI YA KOZI

1 Kuwawezesha wanafunzi kuwa na ufahamu wa nadharia ambazo ziliweka misingi


ya uchanganuzi wa lugha, maendeleo ya nadharia hizi na jinsi zilivyozuana na
kufanikisha kuwepo kwa mikondo mingi ya nadharia iliyopo nyanjani.

2 Kutanguliza mikabala ya kinadharia inayoweza kutumiwa kujadili na kuchanganua


miundo ya sintaksia katika viwango vya juu.

3 Kutambua viunzi vya nadharia mbalimbali na jinsi ya kuvitumia katika uchanganuzi


wa miundo.

4 Kubainisha uhusiano uliopo baina ya nadharia hizi na mchango wake katika vima
mbalimbali vya lugha

MATARAJIO BAADA YA KOZI HII

Kufikia mwisho wa kozi hii, wanafunzi wanatarajiwa:

c) Kuelezea historia ya nadharia mbalimbali

d) Kubainisha jinsi zilivyozuana

e) Kulinganua viunzi na mbinu mbalimbali zinazotumiwa na nadharia hizi katika


uchanganuzi

f) Kufafanua udhaifu uliopelekea kuibuka kwa mikondo tofauti

g) Kuelekeza wanafunzi kutumikiza nadharia hizi kuchanganua lugha ya Kiswahili na


lugha zingine.

1
YALIYOMO

Wiki Mada Mada Ndogo Saa


Wiki 1 Utangulizi  Kijelezi cha dhana ‘Nadharia’ 3
Maana ya Nadharia  Sababu za matumizi ya nadharia katika
Nadharia na usomi wa kisayansi usomi

Lugha kama somo la kisayansi  Sifa kuu za sayansi – uwazi, mpango na


uyakinifu
 Jinsi lugha inaafiki usayansi
Wiki 2 Historia ya matumizi ya nadharia  Utangulizi wa Nadharia ya 3
katika uchanganuzi wa lugha Wanamapokeo
 Viunzi vya Nadharia ya Wanamapokeo
Wiki 3 (endelea)  Nguvu na udhaifu wa Nadharia ya 3
Wanamapokeo
Nguvu na udhaifu wa nadharia
ya wanamapokeo  Mchango wa Nadharia ya Wanamapokeo
katika uchanganuzi wa lugha.
 Vima vya lugha vilivyochangiwa na
Nadharia ya Wanamapokeo.
Wiki 4 Nadharia ya Wanamiundo  Viunzi vya Wanamiundo 3
 Masuala yaliyoigwa na Nadharia ya
Wanamiundo kutokana Nadharia ya
Wanamapokeo
Wiki 5 Nguvu za Nadharia ya  Nguvu za Nadharia ya Wanamiundo 3
Wanamiundo
 Matumizi ya data ya lugha asilia kama
nguvu za nadharia ya wanamiundo
 Udhaifu wa Nadharia ya Wanamiundo
 Matapo ya Wanamiundo
 Mikabala ya kina Bloomfield na
wanaisimu wenzake kuhusiana na dhana
za umuundo na uchanganuzi wa miundo.
Wiki 6 (endelea)  Tofauti za Wanamiundo na 3
Wanamapokeo
 Mchango wa Wanamiundo katika ngazi
ya Mofolojia

2
Wiki Mada Mada Ndogo Saa
 Mchango wa Wanamiundo katika ngazi
ya Sintaksia
Wiki 7 (endelea)  Mchango wa Wanamiundo katika miundo 3
ya kimofemiki
 Mchango wa Wanamiundo na uibukaji wa
Sarufi Mpango/Msonge
 Mtazamo wa Halliday na wenzake
kuhusiana na miundo ya lugha
Wiki 8 Nadharia ya Sarufi Geuza Umbo  Historia ya Nadharia ya Sarufi Geuza 3
Zalishi Umbo Zalishi
 Mwasisi wake na maendeleo yake
 Viunzi vya Nadharia ya SGUZ
Wiki 9 Upya ulioletwa na Nadharia ya  Dhana ya uzalishaji 3
SGUZ
 Umuhimu wa muundo wan je na muundo
wa ndani
 Mchango wa Nadharia ya SGUZ, katika
taaluma ya Fonolojia, Mofolojia, Sintaksia
na Semantiki
Wiki Maendeleo ya Nadharia ya SGUZ  Jinsi Chomsky alivyopanua Nadharia ya 3
10 SGUZ – Nadharia pana sanifu (Extended
Standard Theory)
 Matumizi ya data ya lugha na
ulinganishaji wa miundo mbalimbali ya
ulimwengu.
Wiki (Endelea)  Nadharia ya Miundo Virai; 3
11
 Uibukaji wa Nadharia ya Sarufi bia
Wiki Fonolojia zalishi kama utanzu wa  Fonolojia Asilia 3
12 Nadharia ya SGUZ
 Fonolojia Leksishi
 Fonolojia Arudhi
 Fonolojia ya Vipande Sauti
 Semantiki Zalishi
 Miundo ya sintaksia kwa misingi ya
nadharia ya miundo virai

3
Wiki Mada Mada Ndogo Saa
Wiki Mikondo mingine ya  Uchanganuzi wa sentensi kwa kuzingatia 3
13 uchanganuzi isiyozingatia neno kuu
miundo ya virai
 Semantiki ya sintaksia
Wiki Udurusu na maandalizi ya 3
14 mitihani

Mbinu za Kufundishia:

Mihadhara mkondoni itatumika pamoja na majopo ya utafiti ya kuendeleza mijadala


darasani; kuwapa wanafunzi mijarabu.

Shughuli za Wanafunzi Darasani

Maswali na majibu, kuwasililisha insha za kiutafiti , kuendeleza mijadala, kujibu


maswali ya mazoezi darasani

Vifaa vya kutumika Darasani:

Mawasilisho mtandaoni, makala, madaftari, vitabu vya marejeleo vilivyochapishwa


kuhusiana na taaluma (tazama marejeleo).

Utahini

Mijarabu na Insha za Utafiti kwa 40%


Mtihani kamili 60%
Jumla 100%

Mitihani itafanywa wiki ya 15 na 16

Ili mzamili afaulu kozi hii, ni sharti apate asilimia 50 ya alama zote.

MAREJELEO MAALUMU

Borsley, R. (1999). Syntactic Theory: A Unified Approach 2nd Edition. London: Edward
Arnold.

Carnie, A. (2013). Syntax: A Generative Introduction 3rd Edition. West Sussex: Blackwell.
Chomsky, N. and Halle, M. (1968). The Sound Pattern of English. New York: Harper and
Row.

Chomsky, N. na Halle, M. (1995). The Minimalist Program. Cambridge, MA: MIT Press.

Cook, V.J. na Mark, N. (1996). Chomsky’s Universal Grammar: An Introduction. 2nd ed.
Oxford B: Blackwell Publishers Ltd

4
Crosft, D.A. (2004). Cognitive Linguistics. Cambridge: Cambridge University Press.

Culicover, P.W. (1997). Principles and Parameters: An Introduction to Syntactic Theory.


Oxford: Oxford University Press.

Evans, V. and Melanie, G. (2007). Cognitive Linguistics: An Introduction. Routledge.

Geeraerts, D. na Cuyckens, H. (2007). The Oxford Handbook of Cognitive Linguistics.


London: Cambridge University Press.

Goldsmith, J.A. (1990). Autosegmental and Metrical Phonology. Cambridge, Mass: Basil
Blackwell.

Goldsmith, J.A. (1995). The Handbook of Phonological Theory. Blackwell.

Gussenhoven, C. na Haile, J. (2005). Understanding Phonology 2nd ed. Arnoid.


Gussmann, E. (2002). Phonology, Analysis and Theory. Cambridge: Cambridge University
Press.

Haegeman, L. (1994). Government and Binding Theory 2nd Edition. Oxford: Blackwell.

Halliday, M.A.K. and Christian, M. (2004). An Introduction to Functional Grammar 3rd


Edition. New York: Oxford University Press.

Jackendoff, R. (2002). Foundations of Language: Brain, Meaning, Grammar, Evolution. New


York: Oxford University Press.

Katamba, F. (1989). An Introduction to Phonology. London: Longman.

Katamba, F. (1993). Morphology. New York: St. Martin's Press.

Katamba, F. and Stonham, J. (1986). Morpholology 2nd Edition. London: Palgrave.

Lee, D. (2001). Cognitive Linguistics: An Introduction. New York: Oxford University Press.

Lyons, I. (1968). Introduction to Theoretical Linguistics. Cambridge: Cambridge University


Press.

Massamba, D.P.B. (1996). Phonological Theory: History and Development. Dar es Salaam
University Press.

Massamba, D.P.B. (2011). Maendeleo katika Nadharia ya Fonolojia. Dar es Salaam: TATAKI.

Mathews, P. (1993). Grammatical Theory in the United States from Bloomfied to Chomsky.
Melbourne: Cambridge University Press.

Poole, G. (2011). Syntactic Theory Second Edition. Hampshire: Palgrave.

5
Radford, A. (1988). Transformational Grammar A First Course. Melbourne: Cambridge
University Press.

Radford, A. (1997). Syntax: A Minimalist Introduction. Melbourne: Cambridge University


Press.

Radford, A. (2004). Minimalist Syntax Exploring the Structure of English. New York:
Cambridge University Press.

Sampson, G. (1980). Schools of Linguistics: Competition and Evolution. London: Hutchinson.

Seuren, P.A.M. (2004). Chomsky’s Minimalism. New York: Oxford University Press.

Spencer, A. and Zwicky, A.M. (wah.) (2001). The Handbook of Morphology. John Wiley &
Sons.

Ungerer, F. na Schmid, H. (2006). An Introduction to Cognitive Linguistics Second Edition.


Harlow: Pearson Longman.

Webelhuth, G. (mh.) (1995). Government and Binding Theory and the Minimalist Program.
Blackwell.

IDHINI

Mwongozo wa Kozi Umeidhinishwa na:

Dr.StanleyAdikaKevogo 04/08/2022
Mhadhiri: ............................................................Saini: ............................... Tarehe: ..................
Mudiri (COD): ....................................................... Saini: ............................. Tarehe: ..................

Amidi (DEAN): ...................................................... Saini: .............................. Tarehe: ..................

6
UTANGULIZI

Maana ya Isimu

Wanaisimu wameeleza maana ya isimu kwa njia tofauti. Hata hivyo, wote wanaelekea
kukubaliana kuwa Isimu ni taaluma inayochunguza lugha ya mwanadamu kisayansi.
Kwa mujibu wa Hartman (1972) Isimu ni eneo maalumu la mtalaa ambalo lengo lake ni
kuchunguza lugha. Nao Richards na wenzie (1985) wanaifasili Isimu kuwa ni mtalaa
ambao huchunguza lugha kama mfumo wa mawasiliano ya wanadamu. Besha (1994)
anaeleza Isimu kuwa ni taaluma inayochunguza na kuweka wazi kanuni ambazo ndizo
msingi wa kila lugha. Nayo Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili (1990) inaeleza Isimu
kuwa ni sayansi ya lugha.

Fasili hizi zina maelezo yanayofanana kwa kiasi kikubwa. Jambo linalosisitizwa hapa ni
kwamba Isimu hushughulikia uchunguzi wa lugha mbalimbali kwa kutumia misingi ya
kisayansi. Kwa hivyo, tunaweza kuhitimisha kuwa Isimu ni taaluma inayohakiki lugha
kisayansi. Isimu ni sayansi ya matamshi, maumbo, miundo, maana na matumizi ya
lugha. Isimu inatumia mtazamo wa kisayansi kuchambua lugha kinyume na ilivyokuwa
hapo zamani ambapo watafiti waliathiriwa na hisia na mielekeo yao.

Usayansi wa Isimu

Lengo la isimu ni kuchinguza, kuchambua na kufafanua lugha kisayansi. Verma na


Krishnaswamy (1997:26) wanashikilia kuwa Isimu ni sayansi kwa sababu hufuata mbinu
za kimsingi za utafiti wa kisayansi. Mbinu hizi huhusisha hatua zifuatazo:

i). Uchunguzi uliodhibitiwa.


ii). Uundaji wa nadhariatete.
iii). Uchanganuzi
iv). Ujumlishi
v). Utabiri
vi). Majaribio na uthibitishaji
vii). Urekebishaji au ukataaji wa nadhariatete.

Hili ni kusema kuwa Isimu haichunguzi lugha kiholela bali kwa utaratibu na mwelekeo
maalumu. Katika kuchunguza lugha, wanaisimu hutumia misingi ya kisayansi kama
zinavyofanya sayansi zingine kama vile Fizikia, Kemia na Bayolojia. Zipo sifa nne kuu za
uchambuzi wowote wa kisayansi. Sifa hizo ni pamaoja na:

a) Uwazi na Ukamilifu

Dhana hii ina maana kuwa masuala katika Isimu huelezwa kwa udhahiri usio na utata.
Hoja huelezwa bila shaka yoyote kimaana. Ni sifa inayomtaka mwanaisimu kujiwekea
lengo la kupima kwa uangalifu kila analofanya na kuhakikisha kuwa hoja zote anazotoa
ili kutegemeza nadharia zake au mahitimisho yake ni wazi na zinatokana na utafiti wake.

7
Wakati uchunguzi unapofanywa huwa kuna machukulio. Machukulio haya hubainishwa
wazi. Kwa mfano, mwanaisimu anaweza kuchunguza jinsi watu hujifunza lugha za pili
na matatizo ambayo huwakumba. Machukulio ya utafiti kama huo ni kuwa hawa watu
wana bongo imara na razini. Hili inabidi mchunguzi aweze kulibainisha.

Lugha ya taaluma ya isimu pia ina dhana mbalimbali kama vile ‘sentensi’, ‘neno’, ‘foni’,
‘fonimu’ na ‘mofimu’. Zinapotumika, dhana hizo huelezwa na mtafiti ili kupatikane
uwazi katika utafiti wake.

b) Utaratibu/Upangilifu

Utaratibu ni kufanya mambo kwa mpangilio mzuri wenye kubainika. Utaratibu unaweza
kuhusisha wakati, idadi, umuhimu na hata ukubwa. Kwa mujibu wa sifa hii, hoja za
kisayansi zinapaswa kupangwa vizuri. Taaluma yoyote ya kisayansi hufuata utaratibu
maalum na mambo yake huendeshwa hatua kwa hatua. Wanaisimu huichunguza lugha
kwa utaratibu maalumu, si kiholela.

Mwanaisimu hatakiwi kuchunguza muundo wa lugha kiholela, kushughulikia sehemu


tu ya mada, kutumia istilahi kwa njia isiyowiana, kutotumia taratibu zilizowekwa au
kukosa kurejelea yaliyokwisha kufanywa kuhusu mada fulani. Kwa mfano, katika
kufafanua muundo wa lugha lazima mwanaisimu aamue ataanza na muundo gani (sauti,
maneno au maana), na kwa mfuatano gani.

Wanaisimu wamejaribu kuweka mpangilio wa kufuata katika uchunguzi wa lugha.


Mpangilio huu hurahisisha kazi inayowakabili. Mpangilio huu unajitokeza katika hatua
zifuatazo:

a) Kutambua tatizo linalohitaji uchunguzi


b) Kuunda nadhariatete1

1 Nadhariatete pia huitwa Haipothesia. Nadhariatete ni makisio au taarifa inayotabiri uhusiano baina ya vipengele
(vibadiliki) viwili katika utafiti. Inaonesha uhusiano ambao unaweza ukathibitishwa au ukakosolewa. Kwa mfano,
‘Kuna tofauti za kiisimu kati ya sarufi ya Kiswahili sanifu na sarufi ya Kimaasai’ au ‘Lugha ya Kiswahili ni ya
Kibantu’.

h) Kuchagua nadharia ya kuongoza utafiti


i) Kukusanya data
j) Kuchanganua data

Kwa mfano, ikiwa mwanaisimu ameamua kufanya utafiti juu ya fonolojia ya lugha
fulani, atakuwa tayari na makisio (nadhariatete) ambayo atajaribu kuthibitisha kwa
kutoa data yake katika mawasiliano ya kila siku ya wanadamu wanaozungumza lugha
hiyo. Kisha data itakayokusanywa itachunguzwa kwa kutumia misingi maalumu ya
kinadharia ili kufikia uamuzi kuhusu nadhariatete.

8
Nadharia ni msingi au msimamo wa kuchunguza matukio fulani katika maisha ambao
unaratibu namna jambo linatakiwa kufanywa. Kupitia kwa nadharia, matokeo ya
uchunguzi huhimiliwa na ithibati tosha. Nadharia hutupa mkondo wa fikra, hutumulikia
mambo na kutuwezesha kusaili, inaupa uchunguzi misingi thabiti na inatusaidia kuona
ukweli ili tutoe fasili ifaayo. Nadharia ndiyo huongoza utafiti ikiwa inafafanua mawanda
na kutoa mwelekeo wa kufuata katika utafiti. Kuna nadharia mbalimbali za kiisimu
kama vile: Umuundo, Uchanganuzi makosa, Uchanganuzi Linganuzi, n.k.

Kufuata utaratibu maalumu katika utafiti kuna umuhimu ufuatao:

i) Uamuzi huu utamsaidia mtafiti asijirudierudie, na hoja zake zitakuwa na


mfuatano wa kimantiki. Kwa hali hiyo mtafiti hatapoteza muda mwingi.
ii) Uwezekano wa kukosa kuona uhusiano baina ya vipengele mbalimbali vya lugha
utaondolewa.

c) Urazini/Uhoromo/Uhakikifu

Sifa hii pia inajulikana kama utonafsi au kutopendelea. Huku ni kutazama mambo
yalivyo bila kushawishiwa na hisia. Katika kuzingatia sifa hii, mwanaisimu anapaswa
kuhakikisha kuwa yale anayoyasema, pamoja na mahitimisho anayoyafikia, yanatokana
na data zilizo wazi na ambazo zinaweza kuchunguzika. Tamko lolote la kisayansi lazima
liweze kuthibitishwa na hoja.

Umuhimu wa sifa hii ni kuhakikisha kwamba wanaisimu hawatoi matamko ya juujuu,


ambayo hayawezi kuthibitishwa. Tazama madai kama haya ambayo yamewahi kutolewa
kuhusu lugha:

*Lugha ni bora kuliko lahaja.


*Lugha ya Kilatini ndiyo iliyo na sarufi bora ya kuigwa.
*Lugha za Afrika ni duni kuliko za Ulaya.
*Mwanaisimu ni mtu anayejua lugha nyingi.

Matamko kama haya yalitokana na fikra za kibinafsi na hayakuegemezwa kwenye hoja


zinazoweza kuthibitishwa. Mwanaisimu anatakiwa kuchunguza lugha zote katika
viwango sawa.

Urazini ni sifa kuu ya sifa za usayansi. Inamaanisha kuwa wanaisimu wawe tayari
kupokea mawazo au mashauri mapya katika uchunguzi. Waiwekee nadhariatete shaka
hadi pale ushahidi kamili utakapopatikana. Wanaisimu wajitahidi kuepuka kutilia
mkazo wazo fulani kabla halijakamilika. Inawapasa kila mara kufikiria juu ya mwafaka
badalia wa tatizo hilo au hata kuwapa wenzao kazi zao wazisome na wazikosoe. Kusudi
la sifa hii ni kuondoa ubinafsi katika utafiti.

Maswali yanayoulizwa, uamuzi unaofikiwa na ushahidi unaotolewa sharti uweze


kuonekana hadharani na kuchunguzwa. Matokeo yanayokubaliwa ni yale yenye sifa

9
jarabati, yaani ya kutegemea majaribio, si ya kubahatisha. Sharti matokeo yaweze
kuthibitika. Pia inamaanisha kutumia taratibu zinazokubalika na takribani wanaisimu
wote. Hili linawezekana ikiwa wanaisimu watatumia mbinu zinazokubalika katika Isimu
kama vile jozi milinganuo finyu katika fonolojia. Hii ni mbinu inayotumiwa na
wanaisimu wanapotaka kufahamu mfumo-sauti wa lugha ngeni.

d) Iktisadi

Iktisadi ni sifa ya sayansi inayohitaji uchanganuzi ulenge katika kutumia vipashio


vichache zaidi kadri iwezekanavyo. Inaeleza kwamba taarifu fupi ni bora kuliko sentensi
ndefu ndefu. Imekuwa kawaida kwa sayansi kutumia fomula na kanuni zilizoandikwa
kwa ufupi ili kueleza mambo kwa usahihi bila kutumia maneno mengi. Kwa mfano,
katika somo la Kemia fomula H2O inarejelea ‘maji’. Tutatoa mfano mmoja mmoja kutoka
kwa fonolojia na sintaksia.

a) Fonolojia

/b/  z -i
v

Maelezo yake: konsonanti /b/ hubadilika na kuwa /z/ au /v/ katika mazingira ya
kutangulia /i/. Kwa mfano, iba mwibi mwizi / mwivi.

b) Sintaksia

Juma alikula mkate wa mtoto.

SKN+KT

Maelezo yake: sentensi hii imeundwa kwa Kundi Nomino (KN) na Kundi Tenzi (KT).

Juma/alikula mkate wa mtoto.

KN/KT

Msingi katika Ujuzi wa Kiisimu

Yeyote anayedai kuwa anafahamu lugha lazima awe na uwezo wa kusema na kueleweka
na wale wanaofahau lugha hiyo. Hii ina maana kuwa, mtu anaweza kutoa sauti
zinazoashiria maana fulani, na kuelewa sauti hizo, na kuzifafanua. Miongoni mwa
misingi ya kiisimu kuhusu ujuzi wa lugha ni kama ifuatayo:

a) Mfumo wa Sauti

Ni bayana kuwa kufahamu lugha ni sawa na kuhfahamu sauti zinazopatikana katika


lugha hiyo. Sauti hizo huwa ni muhimu katika kuunda maneno. Aidha, watu wasio
wazungumzaji asilia wa lugha inayohusika hutatizika kutamka sauti zake.

b) Maana ya Maneno

10
Kujua sauti na mfumo wa sauti ni kipengele kimoja tu cha ujuzi wa lugha. Sauti za lugha
sharti ziashirie dhana au maana fulani. Kwa mfano, neno ‘kalamu’ katika mfumo wa
Kiswahili lina maana tofauti na neno ‘karamu’.

Kwa hivyo, ujuzi wa kiisimu humwezesha mtu kutambua namna ambavyo sauti
huhusishwa na maana. Ni lazima mtu ataje na kujifunza sauti zinazowakilishwa na
herufi ili kuwasilisha dhana inayozungumziwa. Sauti katika maneno hupewa maana
katika mfumo wa lugha inamopatikana.

Kawaida, hakuna uhusiano wowote kati ya umbo la kitajwa na maana inayoashiriwa.


Hata hivyo, kuna zile ishara za sauti ambazo hujenga neno kwa kuiga sauti au mlio wa
kitu kama vile maneno ya kitanakali au maneno yanayoeleza hisia.

c) Ubunifu

Ubunifu humwezesha mtu kuweka pamoja sauti ili kuunda neno. Maneno nayo
huwekwa pamoja kuunda sentensi au tungo mbalimbali. Mwanadamu ana uwezo wa
kutaja, kubuni na kutunga sentensi tofauti tofauti kulingana na jinsi anavyotangamana
na mazingira yake.

d) Usahihi wa Sentensi

Sentensi katika lugha huundwa kutokana na mkusanyiko wa maneno ambayo


hupangwa kwa utaratibu. Zipo kanuni ambazo huwa ni za kimsingi katika uundaji wa
sentensi. Kwa hivyo, mjuzi wa lugha fulani anafaa kutunga sentensi sahihi kwa mujibu
wa kanuni za sarufi ya lugha inayohusika.

e) Ujuzi wa Lugha na Utendaji

Ujuzi wa kiisimu wa mzungumzaji humwezesha kutunga sentensi ndefu ambazo


zinaweza kutokana na kufunganishwa kwa mafungu ili kuwa na sentensi ndefu kadri
iwezekanavyo. Hata hivyo, kuna uwezekano kuwa kuna tofauti kati ya ujuzi
unaomwezesha kuzalisha sentensi na utekelezwaji wa sentensi hizo. Hali hiyo
husababisha ‘umilisi’ na ‘utendaji’.

Umilisi ni uwezo wa msemaji kuelewa lugha na kuwa uwezo wa kuzalisha sentensi


nyingi kwa kuzingatia kanuni zake. Utendaji nao hutegemea masuala fulani ya
kimaumbile na yale kisaikolojia ambayo huweza kumzuia mtu kujieleza kikamilifu
anapojaribu kuakisi yaliyo akilini mwake.

Kwa ujumla, ujuzi wa kiisimu ni kuufamu mfumo wa kijumla wa kiisimu katika


kufahamu vipashio vyote vya lugha kama vile sauti, miundo, maana, maneno na sheria
ambazo humilikiwa na mzungumzaji bila yeye kujua jinsi ambavyo mwanadamu
humiliki sheria zozote za kimaumbile ambazo huwezesha watu kusimama, kutembea na
hata kuruka.

Maana ya Nadharia

Richards na wenzie (1985) wanafasili nadharia kuwa ni taarifa ya utaratibu wa kijumla


uliojikita katika mawazo yaliyothibitishwa na kuungwa mkono na ushahidi uliolengwa
katika kueleza jambo fulani. Hii ina maana kuwa nadharia ni seti ya sheria au utaratibu

11
wa kushughulikia somo au taaluma fulani. Kimsingi, nadharia ni mitazamo mbalimbali
kuhusu jambo fulani.

Watu huona jambo kwa mitazamo au mikabala tofauti. Mikabala hiyo sharti iweze
kuthibitishwa kiutafiti. Kwa mfano, wataalamu wanaochunguza masuala ya kiisimu
hutofautiana kimtazamo kwa mujibu wa misingi yao ya kinadharia. Kwa hali hiyo,
nadhari husaidia katika kueleza jambo kwa urahisi.

Aina za Nadharia

Uainishaji wa nadharia unategemea jinsi nadharia hizo zilivyoundwa. Kwa mfano:

Nadharia Asilia

Nadharia asilia inajitosheleza na haina uhusiano wa moja kwa moja na nadharia


nyingine. Nadharia za aina hii zinazingatia hali za mwanzo na hazitokani na nadharia
nyingine. Kwa mfano urasimi, uhalisia na ulimbwende.

Nadharia Nyambuaji

Ni nadharia ambayo imetokana na unyambuaji wa nadharia iliyokuwepo awali. Kwa


hiyo, nadharia ya aina hii ni kimelea cha nadharia iliyotangulia. Kwa mfano nadharia ya

urasimi wa kimagharibi ilitokana na nadharia ya wigo nayo nadharia ya urasimi mpya ni


kimelea cha urasimi mkongwe.

Nadharia Changamano

Nadharia changamano imeundwa kutokana na nadharia mbili au zaidi. Kwa mfano


nadharia ya uhalisia wa kijamaa inatokana na nadharia ya uhalisia na ile ya ujamaa.
Uhalisia ni nadharia ya kutunga na kuhakiki kazi za fasihi inayonuia kuonesha jamii
katika uyakinifu wake. Kwa upande mwingine ujamaa ni mfumo unaolenga
kusawazisha kwa kiwango kikubwa, walimwengu katika mahusiano yao na njia za
kuzalisha mali.

Vipengele vya Nadharia

Nadharia hujumuisha vipengele vifuatavyo:

a) Nadharia sharti iwe tabirifu, yaani inapaswa kutabiri maana fulani. Kwa mfano,
katika mfumo wa Kiswahili, maneno yanafaa kuwa na muundo fulani. Lazima
nadharia iwe na uwezo wa kutenga vipashio katika kategoria mbalimbali kama vile
nomino, vitenzi, viwakilishi, vielezi, viunganishi, vihusishi, n.k.

b) Nadharia lazima ibadilike kila uchao hasa unapopatikana ushahidi mpya.

c) Nadharia huwa na falsafa yake. Hii ina maana kuwa lazima iwe na mtazamo fulani
wa kuelezea kile inachokieleza.

d) Nadharia huwa na ishara na lugha yake maalumu

12
e) Nadharia inapaswa kueleza mambo yaliyozidi data yake. Yaani, maelezo ya nadharia
yaweze kutumika kufafanua data nyinginezo.

Nadharia na Usomi wa Kisayansi

a) Nadharia inahitajika ili kumsaidia na kumwelekeza mtafiti kuweka kadhia


anayoitafiti katika utaratibu maalumu unaoeleweka na watafiti wenzake. Nadharia
kwa hiyo hutoa hatua muhimu za kuzingatia au kufuata wakati wa utafiti.

b) Nadharia hutoa mwongozo kwa mtafiti kueleza vipengele mbalimbali vya fasihi ili
afanye uamuzi wa kutegemewa kuhusu kazi anayoitafiti. Nadharia itamwongoza
mtafiti kuratibu uchunguzi wake katika harakati ya kuzua, kuchuja na kuweka
mikakati ya kutafitia fasihi.

c) Nadharia hutusaidia kulishughulikia somo la fasihi kitaaluma ili lifasiriwe kwa njia
mwafaka. Hii ni kwa sababu fasihi humwathiri msomaji kisaikolojia na umuhimu
wake hauwezi kupuuzwa, kuepukika wala kukwepwa.

Nadharia za Uchanganuzi wa Lugha

Uchambuzi wa lugha umepitia mikondo mitatu mikuu ya uchambuzi. Katika mikondo


hii, misimamo tofauti ya wanaisimu kuhusu lugha imesababisha kuzuka kwa nadharia
tofauti za sarufi ya lugha kwa kila mkondo. Nadharia hizi ni:

a) Sarufi Mapokeo (Traditional Grammar)


b) Sarufi Miundo au Maumbo (Structural Grammar)
c) Sarufi Miundo Virai (Phrase Structure Grammar)
d) Sarufi Zalishi (Generative Grammar)
e) Sarufi Geuzamaumbo Zalishi (Transformational Generative Grammar)

13
SARUFI MAPOKEO

Utangulizi

Dhana ya sarufi mapokeo inatokana na ujumlishaji wa mawazo, mbinu na kaida


zilizohusishwa na wachunguzi wa lugha katika kipindi kirefu kilichoanza K5 Kabla ya
Kristo hadi karne ya 19. Sarufi mapokeo siyo nadharia mahsusi ya wanaisimu kwani si
mkondo mmoja wa mawazo ya kitaaluma uliokuwepo katika kipindi mahsusi cha
maendeleo ya taaluma ya Isimu (Crystal & Davy, 1971).

Wengi kati ya wataalamu wa jadi hawakujihusisha na sarufi au lugha pekee. Ingawa


walijihusisha na masuala ya maumbile ya lugha walijihusisha pia na taaluma nyingine
kama vile falsafa, mantiki, balagha, uhakiki, dini n.k. Kwa hakika, wanazingatiwa katika
sarufi mapokeo kwa namna ambavyo walihusisha lugha na taaluma hizi nyingine.
Miongoni mwa waasisi wa taaluma hizi ni pamoja na Plato, Priscian, Aristotle na
Dionysus Thrax. Mkabala wa sarufi mapokeo unakisiwa kuanzia huko Ugiriki mnamo
karne ya 5KK na ulishikiliwa hadi mwishoni mwa karne ya 18.

Historia ya Sarufi Mapokeo

Istilahi Sarufi Mapokeo inarejelea jumla ya mikabala mbalimbali iliyokuwa ikitumiwa


jadi kuelezea miundo na mifumo ya lugha. Mikabala ya aina hii ilikuwa imekitwa
kwenye kiunzi cha sarufi za zamani za Kilatini na Kigiriki.Mtazamo wa awali zaidi
ambao ulishughulikia lugha ulikuwa wa kifalsafa.

Sarufi mapokeo iliasisiwa na wanafalsafa wa Ulaya hasa Uyunani. Wanafasafa hao


walishughulikia lugha kuanzia karne ya 13. Wakati huo, lugha iliangaliwa kama kipengele
kimoja cha uchunguzi wa taaluma nyingine (za falsafa) kama historia, fasihi, dini, mantiki na
baalagha. Kule Uyunani, kipengele cha lugha kilishughulikiwa katika taaluma ya falsafa.
Wachunguzi hodari wa falsafa ya kigiriki walikuwa Aristotle na Plato.

Plato ndiye anayechukuliwa kuwa mwanasarufi wa kwanza alipotoa mchango wake


kwamba sentensi inaweza kugawanywa katika sehemu mbili kuu yaani mtenda na
mtendwa. Baadaye Aristlotle aliendeleza mawazo ya mwalimu wake Plato na kuigawa
sentensi katika sehemu tatu ambazo ni nomino, kivumishi na kitenzi. Baadaye
Wanastoiki walitenganisha sarufi na falsafa wakaunda tawi huru la Filolojia. Wanastoiki
walibainisha kitenzi kuwa kina sehemu zifuatazo: njeo, kauli, dhamira, uhusika na hali.

Sarufi ya awali zaidi ilitungwa katika kipindi cha mbabe Alexander na Myunani
aliyeitwa Dionysus Thrax. Sarufi hiyo iliitwa Techne Grammatike (The Art of Grammar).
Baadaye Warumi walitumia mfumo wa kisarufi wa Wayunani katika lugha ya Kilatini
bila mabadiliko mengi. Kati ya karne ya 12 hadi ya 14 kikundi cha wasomi kilichoitwa

14
Modistae kilitoa kazi mbalimbali zilizojikita katika sarufi ya makisio. Mtazamo wao wa
kisarufi ulikuwa ukiitwa Grammatica Speculativa. Waliamini kulikuwepo sarufi bia moja
inayohimiliwa na uhalisia na urazini wa binadamu. Kufikia karne 17, maoni tofauti ya
kisarufi yaliendelezwa. Kufikia mwaka wa 1700, sarufi za lugha 61 zilikuwa zimeandikwa
zikiwemo zile za Kiingereza, Kifaransa, Kiarabu na Kiitaliano. Sarufi nyingi za mwanzo
ziliandikiwa kwa makusudi ya kufundishia. Pia, walitaka kuzisanifisha kupitia maandishi.
Katika kipindi hicho cha maendeleo ya sarufi, wataalamu waligawanyika kimaoni wengine
wakipendekeza sarufi fafanuzi na wengine sarufi elekezi.

Kwa ujumla, sarufi mapokeo ilisababisha kuzuka kwa makundi mawili ya wasomi.
Kundi la kwanza ni lile linalowahusu wanafalsafa na la pili ni la wanaisimu. Kimsingi,
mtazamo huu ulizingatia lugha katika mikondo na mikabala ya jadi. Inadaiwa kwamba
Plato ndiye aliyekuwa mtu wa kwanza kutafiti lugha na baadaye akafuatwa na Aristotle
aliyekuwa mwanafunzi wake. Wanaisimu watatu waliokuwa kwenye mstari wa mbele
kutafiti lugha mbalimbali ulimwenguni walikuwa wafuatao:

5 Jacob Green aliyetafiti lugha ya Kijerumani


6 Rasmus Rasak wa Denmark alityeafiti kwa undani lugha yake
7 Thrax aliyekuwa Myunani

Wataalamu hao walitumia mbinu ambazo kwa pamoja zilifanana, kwa mfano:

k) Kubanisha maumbo ya lugha au maneno yanayounda lugha hiyo.

l) Kutumia taratibu za kihistoria kuchunguza mabadiliko ambayo yanahusu


kulinganisha maneno wakati wa sasa na wakati uliopita kwa mfano:

cow (sasa) bovine (hapo awali )


ugali (sasa) sembe (hapo awali)

b Kutumia taratibu za uchanganuzi linganishi ambapo walilinganisha lugha mbili


ili kubainisha uhusiano wa maumbo yake (contrastive analysis) na pia kuchunguza
taratibu za kukopa. Kwa mfano:

Ugonjwa wa Kimeta (Asili yake ni Kimaasai)


Sungura (Kiswahili) Kitungule (Kimvita)

Kwa mujibu wa Sarufi Mapokeo, wataalamu walichunguzi lugha wakiongozwa na


uelewa hisi (intuition). Wataalamu hawa hawakuzingatia mambo yaliyohusiana na
muktadha na badala yake walizingatia maneno bila kuangalia matumizi yake katika
muktadha.

Sifa za Sarufi Mapokeo

d) Wanasarufi mapokeo walichukulia uchambuzi wa kisarufi kuwa sehemu ya


uchunguzi wa kifalsafa.

15
f) Walishikilia kuwa kulikuwepo na uhusiano wa moja kwa moja kati ya neno na kile
kilichowakilishwa na neno hilo. Huu ulikuwa mtizamo wa kiuasilia, ambao pia
huitwa mtizamo wa kionamatopea. Kwa wanamapokeo, huo ndio msingi wa lugha
yoyote.

g) Walishikilia mtizamo wa Isimu Elekezi. Uchunguzi wao ulizingatia matumizi halisi ya


lugha bali siyo ufafanuzi wa lugha husika. Wao walitafuta ni lugha ipi iliyokuwa bora
na ipi isiyokuwa bora.

h) Wanamapokeo waliegemea lugha andishi huku wakipuuza lugha ya kuzungumzwa


katika uchanganuzi wao. Plato na Aristotle walidai kuwa lugha iliyoandikwa ilikuwa
bora. Miongoni mwa lugha walizozingatia wakati huo zilikuwa pamoja na Kigriki,
Kilatini na Kisanskriti.

i) Walifafanua kwamba kila lugha ina kategoria za kisarufi na kileksia kama vile
nomino, vielezi, vitenzi n.k.

j) Kwa wanamapokeo sarufi ilionekana kuwa nyenzo ya kusaidia ufahamu wa sarufi ya


Kigriki. Plato na Aristotle walijihusisha na aina za maneno na muundo wa sentensi.
Plato alibainisha kati ya Kundi Nomino (KN) na Kundi Tenzi (KT). Aliliita Kundi
Nomino Onama nalo Kundi Tenzi akaliita rhema. Aristotle naye aliendeleza ufafanuzi
wa Plato kwa kufafanua kategoria za kisarufi na aina za maneno. Mathalan,
alibainisha kategoria za idadi, wakati (njeo), jinsia na uhusika.

k) Desturi hii ya uainishaji wa maneno na kategoria za kisarufi inashikiliwa hadi sasa na


wanaisimu wanaozingatia uchanganuzi wa maneno katika lugha.

Dhana za Sarufi Mapokeo

Dhana za sarufi mapokeo zinazofafanuliwa katika kijisehemu hiki ni: neno, sentensi,
kishazi na kirai.

Dhana ya Neno

Kwa mtazamo wa kimapokeo, neno ni kipengele cha msingi. Neno linafafanuliwa kuwa
ni kipengele cha lugha ambacho ni kidogo na huru kinachoweza kutamkika pekee yake
(Bloomfield, 1933). Maelezo haya, hata hivyo, yana upungufu. Hii ni kwa sababu
wanamapokeo waliegemea kwa lugha andishi katika fasiri yao. Ni rahisi kulitambua
neno katika muktadha wa maandishi. Kwa kuangalia nafasi kati ya neno moja hadi
lingine, ni rahisi kutambua neno katika maandishi. Hili linawezekana kwa kuangalia
nafasi inayotenganisha kipashio kimoja na kingine. Ikiwa ipo nafasi kati ya vipashio
viwili basi kila kipashio kinachukuliwa kuwa neno. Kwa mfano:

Jumba//hili//ni//zuri.

16
Katika lugha ya mazungumzo, nafasi hizi zinafikiriwa kuwa zinasimamiwa na kituo au
mtuo. Hata hivyo, ukweli ni kwamba, hatutui baada ya kutamka kila neno moja.
Tunaposikiliza lugha tusiyoielewa, hatuwezi kusema kwa uhakika ni wapi maneno
yanapoishia. Ni sawa na kusema kuwa lugha ya mazungumzo hutokea katika mfululizo
wowote bila kutua. Ijapokuwa wanasarufi mapokeo walitumia neno bila kutoa fasili
toshelevu, ukweli ni kwamba dhana hiyo ipo na inaendelea kutumiwa katika
uchanganuzi wa sarufi.

Aina za Maneno

Wanasarufi mapokeo waliainisha maneno katika kategoria mbalimbali. Katika uainishaji


wao, walitambua aina nane, ambapo walitoa ufafanuzi wa kisemantiki kuhusu dhana
hizo. Aina walizoainisha ni pamoja na: Nomino, Vivumishi, Vitenzi, Viwakilishi, Vielezi,
Viunganishi, Vihusishi na Vihisishi.

Dhana ya Sentensi

Kwa mujibu wa wanamapokeo, sentensi ni tamko lenye fikra kamili. Maaelezo haya hata
hivyo yanadhihirisha upungufu. Kwanza, ‘fikra kamili’ ni nini? Pili, tutaitambuaje fikra
kamili na ni ipi isiyo kamili? Zaidi ya haya, hatuwezi kutambua ikiwa neno ni tamko au
kama kifungu cha maneno ni sentensi. Isitoshe, wanamapokeo hawakufafanua tofauti
iliyopo baina ya sentensi sahili, ambatani na changamani.

Njia mwafaka ya kuifafanua sentensi ni kwa kuchunguza muundo wake. Kila sentensi
huundwa kwa vipashio maalumu vilivyopangwa kwa utaratibu maalumu. Kwa kutumia
muundo wa vipshio, tunaweza kuonyesha kipashio kinachoweza au kisichoweza kuitwa
sentensi. Kwa kutumia muundo kama kigezo cha kuifafanua sentensi, sentensi basi
inakuwa kipashio kikubwa zaidi ambacho kinaweza kuwa na muundo wa kisarufi. Kwa
mfano:

Mbu / wamemng’ata mtoto.


N1 T N2

Kila kipashio katika sentensi huchukua nafasi yake wala hakiwezi kuchukua nafasi ya
kipashio kingine bila kuathiri maana ya sentensi inayohusika.

Kirai

Katika sentensi, mnapatikana maneno yaliyo na dhima sawa. Maneno haya yanaweza
kuchukuliwa kama kipashio kimoja. Kwa mfano:

([Mti mrefu]/ [umeanguka] [mara moja sasa hivi])


N V T E E

Vipashio vya aina hii vinaweza kuitwa virai, vikundi au vifungu. Vinapatikana kama
sehemu moja ya sentensi. Virai haviwezi kujisimamia. Kwa mfano;

17
Mti mrefu; Mtoto mzuri; Kwao nyumbani; Mara tano; n.k

Kila sentensi huwa na vikundi viwili vikuu vinavyoiunda. Hivi ni: KIRAI NOMINO na KIRAI
KITENZI. Virai hivi huchukua nafasi maalumu katika sentensi. Kila kirai lazima kiwe na
neno kuu linaloongoza mengine. KN huungozwa na nomino, ilhali KT huongozwa na
kitenzi.

Kishazi

Virai vinapoungana, huunda vishazi. Kishazi ni kipashio ambacho ni kikubwa kuliko


kirai lakini kidogo kuliko sentensi. Kimuundo, kishazi kiweza kuwa na muundo wa
kiima na kiarifu (kishazi huru) au kiwe na muundo wa kishazi kinachotegemea kingine
ili kikamilike kimaana. Miundo hii inapelekea kuwepo kwa vishazi vya aina mbili -
Kishazi Huru na Kishazi Tegemezi.

Kishazi huru kinajisimamia kimaana huku kishazi tegemezi kikitegemea muundo wa


kile ambacho ni huru. Kutokana na miundo hii ya vishazi, aina mbalimbali za sentensi
zinaweza kuainishwa:

d) Sentensi sahili ambayo inao muundo wa kishazi huru.


e) Sentensi ambatani ambayo ina muungano wa vishazi huru viwili kwa kutumia
kiunganishi.
f) Sentensi changamani ambayo ni sentensi iliyo na kishazi tegemezi, k.v. Mtoto
aliyeiba nguo jana amekamatwa na polisi.

Misingi ya Nadharia ya Sarufi Mapokeo

Mkabala wa Sarufi Mapokeo una misingi yake katika sifa maalumu zinazoibainisha
sarufi hii. Nadharia ya sarufi mapokeo inajikita katika misingi ifuatayo:

f) Lugha iliyochukuliwa kuwa msingi wa sarufi ilikuwa Kilatini. Hii ni kwa sababu mambo
mengi ya kitaaluma wakati huo yalichunguzwa na kuandikwa kwa Kilatini. Lugha
ya Kilatini ilikuwa mojawapo ya lugha awali sana kuwa na maandishi. Lugha zote
zilichunguzwa kwa misingi ya Kilatini. Lugha zote ulimwenguni zilichukuliwa kuwa
na sarufi moja. Kwa muda mrefu lugha ya Kilatini ilichukuliwa kama kielelezo cha
matumizi ya kiwango cha juu kabisa cha lugha. Kwa hivyo, wanamapokeo,
walichunguza na kuishia na kanuni na sheria zilizoeleza matumizi yake. Kanuni hizo
zilichukuliwa kama kigezo cha kuchambulia lugha nyingine za ulimwengu – hata
Kiingereza. Kwa mfano, Kilatini kina sifa ya kunyambulika kwa maneno. Kwa
kutumia kigezo hiki Wanamapokeo walikiona Kiingereza kuwa na chembe za sarufi
kwani hakina sifa hii sana kikilinganishwa na Kilatini ilhali Kichina ambacho hakina
tabia hii kilisemekana kuwa hakina sarufi.

g) Sarufi mapokeo ilipendekeza kanuni za lugha. Sarufi mapokeo ilieleza kwa jinsi ambavyo
mtu anatakiwa kuongea na kuandika. Kulikuwa na kanuni ambazo zilipasa kufuatwa

18
katika kutumia lugha kwa njia sahihi. Wanamapokeo walitoa sheria zilizoelekeza
namna ya kutumia lugha.

3) Kazi za kisanaa zilihusishwa na falsafa. Kazi mbalimbali za wasomi mashuhuri wakati


huo zilichukuliwa kuwa ndizo zilizotumia lugha kwa njia sahihi zaidi. Matumizi ya
lugha nje ya ilivyotumika katika kazi hizo yalichukuliwa kuwa ni makosa. Kwa hali
hiyo, mtazamo wa lugha ukawa kuwa mabadiliko ya lugha yalikuwa ya kuharibu na
kwamba hatua ya awali ya lugha fulani ilikuwa bora na sahihi zaidi kuliko hatua ya
baadaye. Vitabu vya sarufi vilivyoonyesha kanuni za utumiaji sahili wa lugha.

4) Walionelea lugha kuwa ni ya kionomatopea. Wanamapokeo walionelea kwamba


kulikuwa na uhusiano wa moja kwa moja kati ya neno na kile kinachorejelewa na
neno hilo. Maneno kama kengele, tingatinga na pikipiki – yanatokana na sauti
inayotolewa na vyombo hivi.

5) Walijishughulisha na kueleza kategoria za sarufi. Kwa mfano, nomino na vitenzi.


Wanamapokeo walihakiki sentensi kwa kutambua vipashio vyake mbalimbali.
Waliangalia jinsi vipengele hivi vilivyotumiwa – vizuri au kimakosa katika sentensi,
pia walijaribu kuvieleza vijisehemu hivi na kuvitolea maana. Walipanga vipashio vya
lugha katika makundi pia.

6) Walionelea kwamba lugha ya maandishi ilikuwa bora kuliko lugha ya mazungumzo. Kwa
wanamapokeo, lugha ilikuwa ile iliyoandikwa. Maoni haya yalishikiliwa sana na
Wagiriki. Maoni yao yanafungamana na neno la Kigiriki grammar yaani sarufi
linalotokana na neno la Kigiriki grammatike linalotumiwa kwa maana ya 'kuandikwa'.
Kutokana na neno hili basi wanamapokeo wakachukulia kwamba lugha yoyote
ambayo haikuwa imeandikwa au kuandikiwa sarufi haikuwa lugha kamwe. Lugha
ya Kilatini ndiyo iliyokuwa imeandikwa wakati huo. Sarufi za lugha zote za
ulimwengu ziliegemezwa kwa lugha ya Kilatini ambayo ilikuwa lugha ya wasomi
wakati huu na tena iliyoandikwa.

Umuhimu wa Sarufi Mapokeo

Pamoja na kwamba mtazamo wa kimapokeo unaweza kutolewa tathmini ya udhaifu


wake, lakini pia una umuhimu wake katika historia ya taaluma ya isimu.

a) Wanamapokeo waliasisi dhana za kisarufi ambazo hadi leo zinatumika katika


uchanganuzi wa lugha. Dhana kama vile neno, kishazi, kirai, nomino, kitenzi, n.k
zingali zinatumiwa na wanaisimu kufafanua lugha zote.

b) Kuibuka kwa taaluma ya isimu ni zao la mwamko ulioletwa na wanamapokeo.


Kutokana na kazi zao, walianzisha mwamko wa kuichanganua lugha. Mwamko huo
uliwafanya watafiti wengine kuishughulikia lugha.

19
c) Istilahi zilizobuniwa na wanamapokeo zinaendelea kutumiwa na kupanuliwa huku
zikipewa mitizamo mipya ili ziweze kutumika katika lugha nyingi iwezekanavyo.

d) Utangulizi uliofanywa na wanamapokeo ulikuwa kichocheo na kitangulizi cha


kuanzishwa kwa nadharia za kuifafanua sarufi.

Tathmini ya Sarufi Mapokeo

Wanamapokeo waliamini kwamba msingi wa sarufi ulikuwa lugha ya Kilatini. Hili


lilitokana na sababu kwamba kwa wakati huo, shughuli nyingi za kitaaluma
ziliendeshwa na kuandikwa kwa Kilatini. Aidha, lugha ya Kilatini ndiyo iliyokuwa ya
awali kuwa na maandishi. Kwa sababu hiyo, wanamapokeo walichukulia lugha zote
kuwa na sarufi sawa. Kanuni za lugha ya Kilatini zilichukuliwa kuwa kigezo cha
kuchanganua lugha nyingine za ulimwengu.

1. Kwa kutumia kanuni za Kilatini kuwa kigezo cha uchanganuzi wa lugha, mtizamo
huu ulibainisha udhaifu kwani kila lugha ina fonimu zake mahsusi, muundo wa
maneno na sarufi ya kipekee. Takriban lugha zote duniani zinatofautiana kwa njia
mbalimbali, siyo katika kiwango cha leksia, fonolojia, sintaksia n.k. kwa mfano,
katika Kiswahili sentensi:

Utalala? Ni swali. Lakini pia, inaweza kuwa kauli au taarifa: Utalala.

Ikitafsiriwa katika Kiingeza, mfumo wote wa uwasilishaji unabadilika.

Will you sleep?---------- Swali


You will sleep.----------- Taarifa

Aidha, dhana ya wingi huwasilishwa kwa mifumo tofauti. Katika Kiswahili kwa
mfano, kuna matumizi ya viambishi vya wingi kama vile katika msichana -
wasichana. Katika Kiingereza, girl - girls.

2. Wanasarufi mapokeo walidai kwamba Kigriki kilikuwa na hadhi ya juu kuliko lugha
nyingine za ulimwengu. Maoni haya yana udhaifu kwa kuwa lugha zote ni sawa
kihadhi. Haipo lugha inayojivunia kuwa na hadhi kiisimu kuliko lugha nyingine. Hii
ni kwa sababu kila lugha inatimiza malengo ya wazungumzaji wake kijamii na
kwamba kila lugha inajitosheleza. Kila lugha ina msamiati unaoweza kutosheleza
shughuli za maisha ya kawaida ya jamii inayohusika. Lugha inapokosa msamiati wa
kurejelea dhana zisizopatikana katika muktadha wake, si ishara kwamba lugha hiyo
ni dhaifu. Lugha zote zina uwezo wa kusharabu na kuunda misamiati mipya ili
kufidia upungufu huo.

3. Sarufi Mapokeo hupendekeza kanuni za lugha. Sarufi hii ilielekeza jinsi ambavyo
mtu alihitaji kuzungumza na kuandika lugha. Zilikuwepo kanuni zilizopaswa
kufuatwa katika matumizi ya lugha kwa njia sanifu. Msimamo huu hata hivyo

20
unadhihirisha udhaifu kwani, sarufi haipaswi kulazimishwa au kuelekezwa. Sarufi
inapaswa kuelezwa (kufafanuliwa). Wanamapokeo walisahau kuwa sarufi inastahili
kuangalia lugha jinsi ilivyo na kuieleza na siyo kuilazimisha kufuata kanuni. Istoshe,
wazungumzaji wa lugha hawatungiwi kanuni za jinsi ya kuiongea lugha yao kwani
kila mzawa wa lugha fulani anazifahamu kanuni za lugha yake pasi na kuandikiwa
kanuni.

4. Wanamapokeo walikosea kuchukulia uchunguzi wa lugha kuwa sehemu ya


uchunguzi wa kifalsafa. Kitendo hicho huichukulia lugha kuwa kitu kisichokua.
Hata hivyo, lugha, ina uhai na inakua katika viwango vyake vyote. Lugha haipaswi
kufungamanishwa na falsafa kwa kuwa inaweza kutumiwa katika nyanja
mbalimbali za jamii, bali si kwa shughuli za wasomi na hususani falsafa pekee.

5. Kwa wanamapokeo, lugha ilichukuliwa kuwa ya kionamatopea. Udhaifu uliopo na


msimamo huu ni kwamba katika lugha nyingi duniani, yapo maneno machache tu
ambayo yanaweza kuhusishwa moja kwa milio au vifaa vinavyorejelewa. Hakuna
uhusiano wowote kwa mfano, kati ya maneno: ‘kiti’, ‘ubao’, ‘nguo’ na vifaa
vinavyohusika.

6. Sarufi mapokeo ilisisitiza kuwa lugha andishi ilikuwa bora zaidi kuliko lugha
zungumzwa. Walieleza kuwa lugha yoyote ambayo haikuwa imeandikiwa sarufi
haikuwa lugha kamwe. Ni lugha ya Kilatini pekee iliyokuwa imeandikwa kwa
wakati huo. Msimamo huu unadhihirisha udhaifu. Ni dhahiri kuwa lugha
zungumzwa ni kongwe kuliko lugha andishi kwani maandishi yalibuniwa baadaye
tu. Mawasiliano kupitia mazungumzo yalikuwepo kabla ya maandishi. Kuandikwa
kwa lugha ni njia mojawapo tu ya kuhifadhi lugha, wala maandishi si lugha tofauti.

Aidha, zipo lugha nyingi tu duniani ambazo hazijaandikiwa sarufi. Pia zipo lugha
ambazo zinatumia tu ishara, na hati za uandishi za lugha zingine. Maandishi
yanawakilisha sehemu ndogo tu ya ukwasi wa lugha kwani hatuwezi kuhifadhi
sentensi zote za lugha katika maandishi. Mazungumzo ya watu hubadilika kila mara
na kwa mpito wa wakati. Kwa mfano, matumizi ya Kingereza nyakati za Shakespear
yalikuwa tofauti na ya nyakati hizi. Pia, lugha zungumzwa iko hai, ina ishara na
inadhihirisha hisia mbalimbali, bali ile ya kuandikwa ni kavu na haina mvuto
wowote.

7. Wanapokeo waliainisha kategoria za maneno na wakazitolea ufafanuzi wa


kisemantiki. Huu ni udhaifu. Kwa kuwa dhana hizi ni za kisintaksia, zilipaswa
kupewa ufafanuzi wa kisintaksia; kwa jinsi zinavyotumika kisintaksia. Hakuna sifa
yoyote ya kisemantiki inayoweza kuhusishwa na nomino au kitenzi ama aina
nyingine ya maneno peke yake bila kuhusishwa na dhana hizo nyingine.

Kwa hivyo, katika sintaksia, hatuna budi kutumia sifa za kimsambao katika
kufafanua aina za maneno. Msambao hurejea nafasi mbalimbali ambazo elementi za

kiisimu zinaweza kukalia katika tungo iliyoandikwa vizuri (kisarufi). Kwa mfano,
‘Nomino’ inafafanuliwa kuwa kategoria inayoungana na Vivumishi ili kuunda Kundi

21
Nomino. Pia inaweza kufafanuliwa kama neno linaloungana na kitenzi ili kuunda
Kundi Tenzi. Kwa mfano:

Mama yule//amempiga mtoto.

Vihusishi aghalabu hutangulia nomino katika ujenzi wa Vikundi Vihusishi kama vile:

katika runinga
hadi Namanga

Kwa hali hiyo, hatuwezi basi kutoa ufafanuzi wa aina yoyote ya neno bila kugusia
aina nyingine au dhana nyinginezo za kisintaksia.

Hitimisho

Somo hili limeeleza nadharia ya Sarufi Mapokeo. Historia yake, sifa zake, dhana zake,
umuhimu na udhaifu wake. Tumeeleza kwamba licha ya udhaifu uliojitokeza katika
mkabala huu wa sarufi, bado una umuhimu katika kuzifafanua sarufi mbalimbali za
lugha za ulimwengu.

22
SARUFI MIUNDO

Utangulizi

Sarufi mapokeo ilitumia mtazamo wa uelekezaji. Walieleza matumizi ya lugha katika


mkabala wa matumizi bora. Wanamapokeo waliegemeza uchanganuzi wao katika sheria
au kanuni zilizopaswa kufuatwa ili usemi usiwe na makosa. Hata hivyo, baada ya muda
mrefu baadhi ya wanasarufi walianza kuhisi kwamba mtazamo huo ulikuwa na
upungufu mkubwa. Walihisi kwamba kanuni zilizoainishwa na wanamapokeo
hazikuwa na uwezo wowote wa kupimia matumizi ya lugha. Yaani, hauziwezi kutumika
kama kigezo cha kuainisha matumizi bora na yale yasiyo bora. Mwanaisimu Sweet
(1891)1 anapinga kanuni za Sarufi Mapokeo kwa kusema yafuatayo:
“kanuni za kisarufi hazina thamani yoyote kwani zinaarifu kuhusu hali maalumu.
Matumizi yoyote ya lugha yana usarufi endapo yanatumika kwa ujumla na watu.”

Sweet alidhamiria kuchambua lugha kwa mtazamo wa kisayansi. Sarufi ilichukuliwa


kama sayansi kwa kufuata mbinu au njia za kisayansi za uchanganuzi wa mambo. Kwa
hali hiyo, Sarufi Miundo huchukuliwa kama mwanzo wa uchambuzi wa lugha kisayansi.

Kwa mujibu wa TUKI (1990) muundo umeelezwa kuwa mpangilio wa vipashio mbalimbali
katika lugha. Nayo Kamusi ya Kiswahili Sanifu (2004) imeueleza muundo kuwa ni:

“Umbo la kitu kutokana na jinsi kilivyoundwa au kilivyotengenezwa. Ni namna ya


utengenezaji wa kitu.”

Kwa mujibu wa wanamiundo, lugha inachukuliwa kuwa ni mfumo uliojengeka kwa


mpangilio maalumu. Wao walichunguza jinsi vipashio vya lugha katika sentensi
vilivyopangwa na kujengeka. Mfumo huo una miundo inayodhihirisha mawazo
maalumu yanayorudiwarudiwa.

Kwa hivyo, uchambuzi wa lugha hujikita katika uelezaji wa ruwaza hizo. Hata hivyo,
maelezo ya Sweet hayakutiliwa maanani hadi 1914 ambapo wanaisimu kama vile
Leonard Bloomfield2 waliyatetea katika kazi zao. Hii leo, kazi hizi za awali za Bloomfield
zinachukuliwa kama msingi wa Sarufi Miundo huko Marekani.

Nadharia ya isimu iliendelezwa sana Marekani kuliko Ulaya. Pande za Ulaya Sarufi
Miundo iliendelezwa na mwanaisimu wa Kiswisi Ferdinand de Saussure. Wanaisimu

8 Sweet, H. (1891). A New English Grammar toleo la kwanza uk. 5


m) Tazama Bloomfield, L. (1914). Introduction to the Study of Language. Kitabu ambacho baadaye
kilipanuliwa na kuitwa Language mnamo mwaka wa 1933.

23
wengine ni Franz Boas na Edward Sapir. Kazi ya de Saussure imekusanywa katika
kitabu: A Course in General Linguistics kilicholewa kwa mara ya kwanza mnamo mwaka
wa 1915. Mambo muhimu yanayoifanisha kazi yake ni kule kutenga lugha katika vitengo
maalumu yaani – langage (lugha), langue (mfumolugha) na parole (utendaji).

c Langage

Langage ni jumla ya ishara zinazotumika na wanadamu. Kwa mujibu wa Saussure,


ujumla huu wa lugha haungeweza kufanyiwa utafiti na mwanaisimu.

e) Langue

Langue ni lugha kama inavyojulikana na watumiaji fulani. Mfumolugha huelezwa kama


lugha inayotumika na jamii fulani na hurithishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine.
Lugha hii ni mali bia ya watu wenye utamaduni fulani. Lugha hii isingeweza kumilikiwa
na mtu mmoja. Langue inazo sifa zifuatazo:

l) Ina sheria za kisarufi


m) Ni mfumo wa ishara
n) Ni kipengele cha jamii fulani
o) Ni dhahania
p) Si tumikizi
q) Haibadiliki kutegemea matumizi

Kwa hivyo, langue ni jumla ya sarufi, msamiati, sheria za utamkaji, pamoja na sheria za
uundaji maneno. Langue iliweza kutumiwa na mtu binafsi kama parole.

g) Parole

Parole ina ubinafsi wa yule anayeitumia katika hali halisi. Utendaji ni usemaji wa lugha
katika miktadha halisi. Ni lugha tumikizi inayotokana na sheria za jamii za langue. Kwa
mujibu wa De Saussure lugha hii ina makosa na haipaswi kutumiwa kama data ya
uchunguzi wa kiisimu.

De Saussure aliitenga isimu katika mawanda mawili:

h) Isimu Mamboleo au Isimu Sinkronia (synchronic Linguistics): ni utafiti wa lugha


katika kipindi kimoja maalumu. Ni isimu ambayo huangalia jinsi lugha ilivyo sasa
bila kuchunguza mabadiliko yoyote kwa mujibu wa mpito wa wakati.

i) Isimu Historia au Isimu Daikronia (Diachronic Linguistics): huchunguza jinsi lugha


inavyobadilika kwa mpito wa vipindi vya historia. Kwa mfano, Kiswahili kilipoteza
vokali mbili zikabaki kuwa tano. Aidha, badhi ya maneno yalidondosha sauti kama
vile ‘lola’ na kuwa ‘oa’. Kutokana na mpito wa wakati, baadhi ya lugha kama vile
Kiswahili zimepoteza mfumo wa toni unaopatikana katika lugha nyingine za
Kibantu.

24
Kutokana na kuvuma kwa kazi yake, wanafunzi wake waliweka misuada yake pamoja
na kukichapisha kitabu chake baada ya kufa kwake. De Saussure alieleza umbo la lugha
na muundo wake na kuonyesha kwamba vipengele vya lugha vinahusiana. Ili
kuendeleza wazo hili alitumia mfano wake maarufu wa kulinganisha vipengele vya
lugha na mchezo wa chess. Ili wachezaji wa chess wafanikishe mchezo huo, hawana budi
kusaidiana na kushirikiana.

Wengine waliochangia nadharia hii ni pamoja na Daniel Jonnes, Eugene Naida na C.


Hockett.

Misingi ya Nadharia ya Sarufi Miundo

Nadhari ya Sarufi Miundo imejikita katika misingi ifuatayo:

7) Hujaribu kueleza na kufafanua lugha. Kwa hivyo, Sarufi Miundo huitwa – fafanuzi
au elezi.

8) Hueleza lugha jinsi inavyotumiwa bila kurejelea ukamilifu wake kwa kutegemea
kanuni fulani fulani kama walivyofanya wanamapokeo.

9) Wanamiundo hueleza matumizi yote ya jinsi lugha ilivyo bila kujikita kwenye
matumizi bora, safi au kufuata sheria zilizowekwa.

10) Wao hutegemea miundo au maumbo ya lugha yanayoonekana – yale ya nje (surface
structures). Haya ni yale maumbo tunayoyaona katika maandishi au kuyasikia katika
mazungumzo.

11) Kiini cha uchanganuzi wao ni muundo au umbo la lugha lakini siyo maana ya
vipengele vya lugha (kinyume na wanamapokeo: nomino nk). Walichunguza
vipengele vya isimu kutokana na data (kusanyiko la sentensi).

12) Walieleza muundo kama mpangilio wa ruwaza zinazojirudiarudia ambazo zina


nafasi zilizojazwa na vipengele vya kisarufi.

13) Kwao, muundo wa vipashio ni kitu cha kidhahania ambacho huonyesha kazi ya
kipashio iliyobuniwa ili kusaidia kutoa maelezo ya kile kiwezacho kusemwa au
kuandikwa katika msonge (hierachy) wa vipashio. Kwa mfano,

Sentensi ----> Kishazi ----> Kirai ----> Neno ----> Mofimu

c) Kwa mujibu wa Wanamiundo, lugha hujengwa kwa mofu, mofu ikiwa ndiyo
kipashio kidogo chenye maana katika neno. Walichunguza jinsi vipashio mbalimbali
vinavyojenga tungo.

d) Wanamiundo walichunguza vipashio vinavyojenga tungo kwa kutumia mtindo wa


kuzigawa sentensi ili kuweza kuzichanganua. Wanamapokeo walifafanua dhana zao

3
AdikaStanley Kevogo,Shule Kuu yaSayansi zaJamii,Chuo KikuuchaMount Kenya

25
katika mkabala wa maana. Wanamiundo nao walikopa dhana hizo na kuzifafanua
upya. Wanamiundo walizichukulia istilahi hizo kama vipashio vya lugha
vinavyotenda kazi kwa namna maalumu.

e) Kwa mujibu wa wanamiundo, utendakazi (function/role) ndicho kigezo cha kuanzia


kufafanua dhana au istilahi mbalimbali. Wanamiundo walieleza maumbo ya
vipashio pamoja na uhusiano wake pamoja na vipashio vingine katika sentensi. Hata
hivyo, walishirikisha kigezo cha maana kwa kuangalia uhusiano wa vipashio na
vingine. Kwa mfano, wanamapokeo walieleza nomino kama jina la mtu, kitu au
mahali. Wanamiundo nao wanaangalia nomino kama neno linalofanya kazi fulani au
kwa namna fulani yaani, walitizama utendakazi wa kipashio. Wanamiundo
huliangalia nomino kama neno linalolazimisha au kuleta ukubaliano wa kisarufi
katika maneno mengine ya sentensi kama vielezi, vitenzi, vivumishi n.k. Kwa mfano:

Mtoto mrefu alikuja nyumbani.

2. Uhusiano wa vipashio ndio unaounda msingi wa uchanganuzi wa nadharia hii.


Wanaisimu walioiendeleza ni pamoja na Charles Carpenter Fries katika kitabu The
Structure of English. Ameeleza kwamba maneno yanaunda sentensi kulingana na jinsi
yanavyohusiana katika ruwaza maalumu. Fries anasema kwamba maana ya sentensi
ni zao la muundo wake. Anafafanua kwamba, katika kila sentensi, kuna maana ya
kimuundo inayosimamiwa na muundo wa tungo hiyo. Maana hii ni tofauti na
maana za leksia zinazounda sentensi kama zinavyopatikana katika kamusi. Tunajua
kwamba maana ya sentensi siyo jumla ya maana za maneno yanayoiunda. Fries
anaainisha aina mbili za maana:

Maana ya kimuundo inayosimamiwa na vipashio vya kisarufi.


Maana ya kisemantiki au ya kileksia - yaani, maana ya neno likiwa peke yake au
maana tunayoipata katika kamusi.

Katika lugha ya Kiswahili, vipashio vingi vya kisarufi ni mofu tegemezi. Hatuwezi
kueleza maana ya sentensi kwa kutegemea maana ya maneno peke yake kama:

a-li-m-tembe-lea

Hatuna budi kuelewa utendakazi wake wa kisarufi. Kwake Fries, sentensi si kundi la
maneno tu, bali ni ruwaza ya muundo. Ruwaza hii imeundwa kwa kategoria za
maneno ambazo zinaweza kutambuliwa kwa maumbo yake pamoja na nafasi zake
katika ruwaza. Nafasi hizo ndizo hudhihirisha maana ya kimuundo ya sentensi.
Mpangilio wa maneno katika sentensi ni njia mwafaka zaidi ya kueleza au kutambua
kategoria za maneno. Maneno yanayopatikana katika nafasi sawa na yanayohusiana
na mengine kwa namna sawa yanaweza kuelezwa kuwa yanaunda kategoria moja
ya maneno. Kwa mfano:

26
Nomino Kitenzi Yambwa Kivumishi

Juma alikula chakula kitamu.

Kijana alicheza mpira.

Kitabu kiliibwa.

Ng’ombe alimeza sabuni.

4. Kwa jumla, mtindo wa wanamiundo wa kugawa tungo kwa kuangalia vipashio


uliitwa mtindo au mbinu ya Uchanganuzi wa Kiviambajengo Ambatani (Immediate
Constituent Analysis - ICA). Hii ni mbinu ya uchanganuzi wa sentensi au maneno kwa
kuyagawanya katika viambajengo vyake.

Dhana za Sarufi Miundo

Nadharia ya Sarufi Miundo ni zao la Isimu Fafanuzi iliyoshamiri sana kunako karne ya
8. Nadharia hii ilianza baada ya kuchapishwa kwa kitabu: A Course in General Linguistics
chake mwanaisimu Mswizi, Ferdinand de Saussure mnano mwaka wa 1916. Kitabu
hicho ni zao la uratibishaji wa mihadhara aliyoitoa de Saussure kabla ya kifo chake.

Saussure anaaminika kuwa mwanaisimu wa kwanza kuipa isimu mwelekeo wa kisasa.


Katika kitabu hiki, alipinga dhana za usawa wa lugha alipofafanua uhuru wa kila lugha
kwa kuibua dhana ya langue (mfumolugha) na kufafanua utumiaji wa kila mzungumzaji
au mwandishi kwa kutumia dhana ya parole (utendaji).

Langue

Kwa mujibu wa Saussure, langue ni mfumo ambao kila mtumiaji wa lugha anaurejelea
katika usemaji au uandishi wake. Ni mfumo unaoigwa na kila mtu. Anaeleza kwamba
kila lugha ni mfumo ulio huru, na kwamba kutokana na hiyo langue kuna wasemaji
wengi. Aidha, langue ni mfumo ulio na kanuni zinazohusu lugha fulani, na kila lugha ni
langue kwa maana kwamba ni mfumo unaomilikiwa na wanajamii na kutokana na
mfumo huo wa kijamii wasemaji binafsi huchota na kutenda. Tunaweza kuchukulia
mfumo huo kama jumla ya kanuni na kaida zote zinazotawala au kupatikana katika
lugha fulani. Kila tunapoongea lugha, tunawajibika kuzitii kaida na kanuni za lugha
hiyo.

Parole

Katika langue kuna parole nyingi kadiri walivyo wasemaji wa lugha inayohusika.
Saussure alifafanua parole kuwa ni utendaji wa mtu binafsi katika jamii. Yaani ni upekee
wa matumizi ya lugha ya mzungumzaji wa lugha fulani. Hii inahusisha lafudhi ya
mzungumzaji wa lugha inayohusika.

27
Signife na Signifiant

Kwa mujibu wa Saussure, lugha ni mfumo wa ishara za kiisimu na kwa hivyo ni


kipengele muhimu cha semiolojia. Ishara za kiisimu zina sifa mbili:

a) Kiashiria (Signife) - Sifa hii inatokana na kile kinachoeleweka, yaani, kilichochorwa


au picha inayoonyeshwa.

b) Kiashiriwa (Signifiant) - Sifa hii inatokana na kile kinachomaanishwa na ile ishara.

Saussure pia alifafanua kwamba ishara zote ni nasibu na ni za kikaida. Katika ishara za
kiisimu isimu, signife inawakilishwa na tamko au ishara za kigrafolojia. Signifiant nayo
huwakilishwa na kile kinacho maanishwa na lile tamko ua ishara ya kigrafolojia.

Mahusiano ya Vipashio vya Sentensi

Sarufi Miundo pia inaeleza kwamba sentensi ni mwambatano wa ishara zenye


mahusiano ya aina mbili:

i) Uhusiano wa Silisila

Uhusiano Silisila au uhusiano muktadha ulalo (syntagmatic relationship) ni mfuatano wa


ishara katika mpangilio wa kiulalo (uhusiano muktadha ulalo). Huu ni uhusiano wa
kiulalo wa vipashio vya tungo, kwa mfano:

(a) Yohana + anaimba + wimbo


(b) *Musa + anasoma + shamba

Katika mifano hii, sentensi (a) ni sahihi kwa sababu ishara ‘anaimba’ inaendana na
‘wimbo’ katika uhusiano wa kimlalo, lakini katika mfano wa (b), ishara ‘anasoma’ haina
uhusiano wa silisila na ‘shamba’. Hii ina maana kwamba ishara hizi mbili hazina
uhusiaono silisila kwa sababu haziwezi kubadilishana nafasi katika sentensi hizi.

ii) Uhusiano Muktadha Wima

Uhusiano muktadha wima (paradigmatic/associative relationship) ni mfuatano wa ishara


katika mpangilio wa kusimama. Ni ruwaza ya mpangilio wa vipengele vya kiisimu
vyenye kuonyesha uhusiano wima baina ya kipashio kimoja na vipashio vingine katika
muktadha maalumu. Huu ni uhusiano wa ishara iliyoko kwenye sentensi na nyingine
isiyo kuwepo katika sentensi hiyo. Uhusiano wima ndio unaotuonyesha maana. Kwa
mfano,

(a) Huyu msichana anapendwa sana.


(b) Yule msichana amenikosea.

28
Neno ‘huyu’ na ‘yule’ ni paradimu kwa sababu yanaweza kubadilishana katika maana au
muktadha. ‘Huyu’ linaweza kuchukua nafasi ya ‘yule’, kutokana na hali kwamba neno
‘msichana’ ni sintajimu (syntagm).

Sentensi

Kwa mujibu wa Saussure, sentensi ni mwandamano wa ishara na kila ishara inachangia


maana ya tamko kamili, na kila mojawapo ikifuatana na ishara zote zingine katika lugha.
Kwa hivyo, alibainisha kwamba kipashio chochote cha kiisimu kama vile fonimu,
mofimu, maneno na sentensi katika muktadha mahususi, kinaingia katika uhusiano wa
aina mbili:

a) Uhusiano uliopo baina ya kipashio fulani na vipashio vyote vingine vinavyoweza


kutokea katika nafasi sawa, vina uhusiano wima.

b) Maneno yanayotangulia au kufuatana katika kikundi au sentensi, yanayo


uhusiano mlalo.

Kwa hivyo, sentensi ni zao la uteuzi, na uteuzi katika mahusiano hayo mawili hufanyika
sambamba.

Dhana hizi mbili husaidia katika kuchanganua nomino, vitenzi, n.k. ili tupate kwa
mfano, nomino hisivu na nomino ziso hisivu, vitenzi vielekezi na vitenzi visivyoelekeza,
n.k. Uhusiano wa kisilisila huonyesha namna vipashio vinavyopangwa katika uundaji
wa sentensi. Kuna uhusiano wa maneno yanayofuatana, ndiposa siyo kila neno linaweza
kuchukua nafasi yoyote. Uhusiano wima ni ule wa kutofautisha. Kila ishara ni zao la
uteuzi. Unapoteua kutumia ishara fulani katika nafasi fulani, unaleta tofauti za kimaana.
Kwa hivyo, uhusiano wima unadhihirisha maana katika sentensi.

Sinkronia na Daikronia

Sarufi Miundo, kwa mujibu wa Saussure, ilitenga dhana mbili muhimu katika
kuichunguza lugha kwa kurejelea wakati. Dhana hizo ni Sinkronia (Isimu Mamboleo) na
Daikronia (Isimu Historia) (Habwe & Karanja, 2004:145). Sinkronia ni utafiti wa lugha
katika kipindi kimoja maalumu. Katika mtizamo huu, lugha inafafaniliwa wakati
wowote bila kutazama historia yake. Isimu kisinkronia huiuona lugha kama kitu kilicho
kamilika katika kipindi fulani mahsusi. Kwa hivyo, sinkronia huzingatia muundo wa
lugha katika kipindi mahsusi cha wakati.

Kwa upande mwingine, daikronia ni utafiti wa lugha kwa kuzingatia vipindi tofauti
tofauti. Mtizamo huu huiona lugha kama kitu kinachobadilika kila wakati.

29
Kiambajengo Jirani

Sarufi Muundo pia huchanganua sentensi kwa mujibu wa kiambajengo jirani/ambatani


(immediate constituent). Sentensi zilichanganuliwa kwa mujibu wa ujirani wa
viambajengo. Katika kufanya hivi, walitumia njia tofauti. Kwa mfano:

(a) Juma mfupi ameiba kikapu.


(b) Mwana wake si mwema.

Neno ‘Juma’ liko jirani na neno ‘mfupi’ kuliko ‘kikapu’. Hivyo neno ‘ameiba’ liko jirani
na ‘kikapu’ kukiko lilivyo na ‘mfupi’. Kwa sababu hii, maneno ‘Juma’ na ‘mfupi’
hujumuika kujenga kiima huku maneno ‘ameiiba’ na ‘kikapu’ ni viambajengo
vinavyojumuika kuunda kiarifa.

Uchanganuzi Kiuambajengo

Fries alieleza aina za maneno kwa kutumia istilahi ya makundi ya maumbo (form classes)
kulingana na mahusiano yake na maneno mengine katika sentensi. Uchanganuzi
kiuambajengo ulitumiwa mwanzo katika mofolojia. Mofu hufuatana kwa namna au
ruwaza maalumu katika uundaji wa maneno. Ruwaza hizo huitwa muundo ambajengo.
Kwa mfano:

a – li – kamat – w - a

Neno lenye umbo tata linaweza kugawanywa katika viambajengo vifuasi (immediate
constituents) yaani linaweza kugawika katika viambajengo viwili hadi kufikia mofu au
viambajengo ambavyo haviwezi kugawanywa tena. Hivi vinaitwa viambajengo tamati.
Kwa mfano, neno:

kupigana ku – pig – an - a (viambajengo tamati)

Uchanganuzi huu ulitumiwa katika sintaksia katika kugawa maneno na makundi ya


maneno. Jambo kuu lililoongoza uchanganuzi huu ni kwamba baadhi ya maneno katika
sentensi yana uhusiano zaidi kuliko mengine. Kwa mfano,

Kitabu cheusi kilipotea jana.

yanahusiana zaidi yanahusiana zaidi

Msingi wa uchanganuzi kiumbajengo umejikita katika suala la ubadilishaji (substitution)


yaani, kila kiambajengo kilichochanganuliwa kinaweza kubadilishwa na kingine katika
nafasi au mazingira yale yale. Hivi tunaweza kuelewa ni vipi aina za maneno
zimetawanyika katika tungo. Pamoja na ubadilishaji, wanamiundo walitumia msambao
kama msingi wa uchanganuzi. Uchanganuzi kuiambajengo ni mbinu ya uchanganuzi
iliyodhihirisha uhusiano hasa wa KN na KT pamoja na viambajengo vyao. Aina za
maneno zinaweza kutambulika kwa kutegemea jinsi zilizosambaa na kuhusiana katika

30
tungo. Wanamiundo hawakutolea viambajengo majina, bali waligawa tu sentensi bila
kutoa sababu au kueleza.

Uhusiano wa Karibu

Sentensi siyo mfululizo wa maneno. Inaelezwa kama viwango vya viambajengo. Hivyo
basi, upo uwezekano wa kuigawa sentensi hadi vipashio vya chini zaidi. Kwa
wazungumzaji asilia wa lugha fulani, ni dhahiri kuwa, maneno fulani ya lugha
yanauhusiano wa karibu kuliko yalivyo na mengine katika sentensi. Kwa mujibu wa
wanamiundo, sentensi imegawika kulingana na dhana hii ya uhusiano wa karibu. Kwa
mfano,

Paka walikamata panya.


Paka + wa + li + kamat + a + panya

Dhana ya wingi katika sentensi ina uhusiano wa karibu na nomino paka kuliko ilivyo na
viambajengo vingine. Dhana ya wakati, -li- inahusiana sana na kitenzi. Katika tungo za
Kiswahili, ni dhahiri kuwa wingi au uchache unahusiana na nomino, ilhali, hali na
wakati unahusiana na kitenzi. Kwa mfano:

Mtoto a-li-enda shuleni.


Watoto wa-li-enda shuleni.

Maneno mengine yanayohusiana na nomino ni vionyeshi na vivumishi. Vielezi vina


uhusiano wa karibu na vitenzi.

Upambanuzi wa sentensi ulifanywa bila kuzipa sehemu au vipengele tofauti majina.


Wanamiundo waliendelea kuzipanga na kuzipanua mradi zilionyesha uwiano katika
ruwaza yake kwa mfano:

Juma anaenda.
Juma anaenda sokoni.
Juma anaenda sokoni kununua matunda.
Juma anaenda sokoni kununua matunda aliyotumwa na shangazi.

Je, walijua watakatia wapi sentensi kwa kuangalia ruwaza kama hii? Hata hivyo,
ijapokuwa vipashio hivi havikupewa majina, hadhi ya vipashio ilionekana kuchukua
hatua hizi:

Sentensi (ambacho ndicho kipashio kikuu)


Kishazi
Neno Ngazi ya vipashio
Mofimu (kipashio cha chini)

31
Tathmini ya Nadhari ya Sarufi Miundo

Umuhimu wa Sarufi Miundo

a) Viambajengo huonyesha mpangilio wa kimstari au mfuatano wa maneno na vijenzi


vingine katika sentensi.

b) Mtindo huu huonyesha hadhi ya viambajengi hadi kufikia kile cha hadhi ya chini
kabisa.

c) Kwa kiasi, mbinu hii ilikumbana na tatizo la utata wa kimuundo katika umbo la
sentensi (structural ambiguity). Kwa mfano:

Baba/ Juma amewasili au Baba Juma/ amewasili.

d) Ilikuwa ni njia ya kimsingi au ya kuendelea kuchanganua sentensi katika kujenga


viwango vya vipashio. Mbinu hii ilipisha mbinu zingine zilizofana zaidi.

Udhaifu wa Sarufi Miundo

a) Mtindo wa viambajengo ulichukulia kwamba sentensi imeundwa kwa mfululizo wa


maneno yaliyopangwa katika mstari au kwa mfuatano, lakini ina udhaifu kwani
kuna maneno mengine katika sentensi yasiyojitokeza katika ruwaza ya aina hii. Kwa
mfano:

She made the whole story up.


She made up the whole story.

b) Vijisehemu au vipashio mbalimbali havikupewa majina.

c) Mtindo huu haungeeleza baadhi ya utata katika sentensi - jambo ambalo


lingewezekana iwapo vipashio vingepewa majina. Kwa mfano:

Baba Juma /amefika

d) Hawakuonyesha jinsi ya kuzua au kuzalisha sentensi mpya au zaidi isipokuwa zile


zilizopatikana katika data.

e) Kigezo cha kugawa hakikuonyeshwa vilivyo.

f) Uchanganuzi kiuambajengo ulishindwa kutumika kwa baadhi ya sentensi ambapo


viambajengo vikuu havikudhihirika kwa urahisi. Kwa mfano:

Je, mzazi wangu aliitwa na mwalimu mkuu.

Vipashio vilivyopigiwa msitari havikuelezwa.

32
g) Walishindwa pia kudhihirisha mahusiano muhimu kati ya sentensi za kimsingi
(basic) na zile zilizozalishwa (derived). Tazama uhusiano uliopo baina ya ile
inayoonyesha kauli tendi na ile ya kauli tendwa.

Juma alimpiga mtoto – tendi (active)


Mtoto alipigwa na Juma – tendwa (passive)

Sentensi ya pili ni zalishwa.

h) Uchanganuzi huu ulijikita kwenye semi maalum – yaani zilizorekodiwa, zinazoitwa


kongoo. Unafuata mtazamo elezi unaoishia kuorodhesha data. Sarufi iliyokamilika
sharti iweze kueleza sentensi au semi zilizotolewa na mzungumzaji asilia wa lugha
pamoja na zile ambazo bado hazijatolewa. Lazima ieleze uwezo wa mzungumzaji
asilia wa lugha. Inapaswa kutilia maanani data zilizorekodiwa na zile
zisizorekodiwa. Sarifi miundo inashindwa kutekeleza haya.

Hitimisho

Somo hili limejadili dhana za kimsingi na misingi ya Nadharia ya Sarufi Miundo.


Tumehitimisha kwa kuitathmini nadhari ya Sarufi Miundo. Tumeangazia umuhimu na
udhaifu wake katika uchambuzi na uchanganuzi wa kiisimu.

Maswali ya Marudio

1. Tofautisha baina ya Wanamiundo na Wanamapokeo.


2. Jadili mchango wa Wanamiundo katika ngazi za isimu zifuatazo:
a) Mofolojia
b) Sintaksia
c) Miundo ya Kimofemiki
3. Jadili mchango wa Wanamiundo kwa uibukaji wa Sarufi Mpango/Msonge

33
SARUFI MIUNDO VIRAI

Utangulizi

Sarufi Miundo Virai (Phrase Structure Grammar) ni mkabala wa uchunganuzi wa sarufi


miundo ambao umekitwa katika matumizi ya virai kama msingi wa uchanganuzi wa
vipengele mbalimbali vya tungo. Hii ni mojawapo ya nadharia za Sarufi Miundo ambayo
imeendelezwa zaidi (Chomsky, 1957; Fromkin, Rodman & Hyams, 2011). Mtazamo huu
uliasisiwa na mwanasarufi miundo wa kimarekani, Leonard Bloomfield (1933). Nadharia
yenyewe inaeleza kuhusu namna ya kuunda na kuzichambua sentensi kwa kutegemea
kanuni muundo kirai.

Nadharia ya sarufi miundo virai iliasisiwa kutokana na mbinu ya uchambuzi wa sentensi


aliyoanzisha Bloomfield na akapendekeza kuitwa Uchambuzi wa Kiuambajengo. Katika
mbinu hii, Bloomfield alibainisha jinsi kila sentensi inavyoweza kugawika katika
viambajengo vifuasi viwili na kisha kugawa viambajengo vifuasi hivyo katika
viambajengo vingine hadi kiwango ambacho hakiwezi kugawika zaidi. Alidhihirisha
kuwa sentensi haiundwi kwa mwandamano wa maneno tu kama vile:

(a + b+ c+ d+... n)

bali inaundwa kwa mpangilio wa vipashio vinavyopishana katika safu/ngazi yenye


ruwaza mahsusi, yaani:

(A B) + (C D)… n

Kisha, (AB) inagawika zaidi katika viambajengo vifuasi viwili:

AB A + B ilhali kiambajengo (C D) kinagawika zaidi katika C+ D. Kwa hivyo,


kwa pamoja inakuwa,

S (A + B) + (C + D), ambapo S => Sentensi

Sarufi Miundo Virai (SMK) ni njia mbadala ya kuwasilisha sentensi zilizo kwenye
vielelezo tungo kwa njia ya kutumia ‘kanuni za kuandika upya.’ Katika mfumo huu,
mwanaisimu huifafanua sarufi kwa kutumia kanuni zalishi ambazo huunda muundo
sahihi wa sentensi.

Sarufi ya aina hii, mbali na kuonyesha viambajengo tamati vya sentensi kiusilisila, pia
huonyesha visehemu vidogo vidogo na viwango vya uhusiano wa vipashio. Katika
nadharia hii, mwanaismu hujishughulisha na masuala yafuatayo:

a) Ruwaza zinazopatikana katika sentensi.

34
9 Vipashio vya kisintaksia vinavyoziunga sentensi pamoja na njia ambazo vipashio au
sehemu tofauti za sentensi huhusiana.

Kwa mujibu wa nadharia hii, Kanuni Muundo Kirai ni nyingi na zisizo na ukomo. Hii
ina maana kwamba ni vigumu mno kwa mtu kuweza kutunga kanuni muundo virai kwa
siku za maisha yake. Hata hivyo, kauli hii inadhihirisha upungufu. Mtoto anapofikia
umri wa miaka 3 au 4, huwa ameishajifunza lugha. Hali hii inatupelekea kuamini
kwamba kanuni hizi si nyingi bali zina ukomo. Kanuni muundo virai za sarufi zalishi ni
kusanyiko la uhusiano wa kiima - kiarifu na uchanganuzi wa kimapokeo wa
viambajengo vifuasi wa wanamiundo. Kanuni hizi zinafafanua uhusiano wa kimsingi
unaohusika katika umbo la ndani. Aidha, zinabainisha ni kipashio kipi kinachokitawala
kingine.

Mchoro matawi kama kielelezo cha muundo kirai wa sentensi huitwa kielelezo tungo
(phrase marker). Lengo lake ni kudhihirisha viambajengo vifuasi vilivyoiunda sentensi.
Mahali ambapo matawi mawili hukutana huitwa kifundo (node). Isipokuwa katika vistari
vya mwisho (tamati), kila kifundo huwakilisha kiambajengo ambacho kinasimamiwa na
alama kama vile: KN, KT, KH, KV n.k. na ambacho kinamiliki au kukiongoza hicho
kinachotokea chini yake.

S kifundo

KN KT kifundo

N V T E

n) Humiliki vipashio KN na KT

KN Kinamiliki vipashio N na V

KT Kinamiliki vipashio T na E

Uhusiano huu wa umiliki wa vipashio unadhihirisha vile kiambajengo kinavyoweza


kuundwa kwa viambajengo vidogo. Aidha, kielelezo tungo kinatuwezesha kutambua
mfuatano wa viambajengo katika sentensi.

Inabainika kwamba KN hutangulia na kufuatwa na KT. Nacho kipashio KT kinaweza


kufuatwa na ama KN, KE, KH au vyote katika sentensi. kwa mfano:

35
Baba yake ameingia ndani ya nyumba yao.

KN KT

N V T KH

H KN

N V

Baba yake ameingia ndani ya nyumba yao

Vielelezo tungo vya miundo virai vinatupa maelezo kuhusu muundo wa sentensi. Hata
hivyo, havina uwezo wa kueleza ni kwa njia gani tunaweza kuzalisha sentenzi mpya.
Hili linawezekana tu kupitia Kanuni Miundo Virai.

Kanuni Miundo Virai

Kanuni Miundo Virai, zinatumika katika kueleza na kuonyesha viambajengo katika


sentensi. Kanuni hizi pia hufafanua muundo wa ndani (maana) wa sentensi. Ndizo
zinazounda Sarufi Miundo Virai. Kupitia kwa kanuni hizi, vijisehemu tofauti vya
sentensi vinaweza kupewa majina na pia kuelezwa kisarufi. Jambo hili halingewezekana
kupitia uchanganuzi wa wanasarufi miundo.

Kanuni Miundo Virai ni kanuni zinazowezesha kuandikwa upya kwa sehemu zote za
sentensi hadi kufikia kiwango tamati cha mofimu. Kwa mfano katika:

Juma aliwasili jana.

S KN+KT
KN N
N Juma
KT T+E
T aliwasili
E jana

36
Kanuni muundo kirai huwa na ishara moja kwa upande wa kushoto na ishara moja au
zaidi kwa upande wa kulia, unaoonyeshwa na mshale.

X YZ

Kanuni hizi hufasiriwa kama maelezo ya jinsi ya kupanua au kuandika upya ishara iliyo
katika upande wa kulia wa mshale. Kwa mfano,

Kanuni X Y Z inafafanuliwa kuwa ishara X ina sehemu mbili ambazo ni


Y na Z. Kwa hivyo, X Y Z ni sawa na kusema:

d KN+KT

Umuhimu wa Kanuni Miundo Virai

f) Kanuni Miundo Virai zina uwezo wa kuzalisha sentensi zote za kisarufi za lugha
inayohusika.

g) Huonyesha mpangilio wa viambajengo katika sentensi na jinsi viambajengo hivyo


hufuatana katika sentensi.

h) Huonyesha baadhi ya vipashio hadi kufikia kiambajengo tamati. Kwa mfano:


anasoma kitabu.

a – na – som – a ki – tabu

d) Huonyesha majina ya vipashio na uhusiano wake katika sentensi. kwa mfano:

Mti mrefu ulianguka jana


N V T E

Ili kuweza kutumia Kanuni Miundo Virai ipasavyo, mwanasarufi hana budi kuwa na
ufahamu wa upeo wa juu wa kategoria za kileksika za lugha inayohusika. Kiswahili
hutumia alama zifuatazo ili kutambua kategoria mbalimbali.

N ------------ Nomino k.v baba, nchi, Jumatatu


V ------------ Kivumishi k.v hodari, baya, zuri
T ------------ Kitenzi k.v alicheza, ni, aliomba
E ------------ Kielezi k.v haraka, jana, sasa, kinyama
W ----------- Kiwakilishi kv Mimi, yeye, Wao
U ----------- Kiunganishi k.v na, hata hivyo, lakini
H ----------- Kihusishi k.v na, kando ya, hadi, mpaka
I ------------ Kihisishi k.v Lo! Lahaula! Ohh!

37
Mifano ya Kanuni Miundo Virai na Matumizi yake

Kanuni Miundo Virai zinaweza kuwasilishwa kwa njia mbalimbali kulingana na


muundo wa sentensi. Ifuatayo ni mifano ya kanuni hizo na matumizi yake:

1. S Ø+KT Njoo
2. S KN+KT Baba analala
3. KN N +V Mbwa mwitu
4. KN N+V+V Mwalimu wetu mzuri
5. KT t + KV (Mtoto huyu) ni mziri
6. KT T+KE anaimba vizuri
7. KT T+KN alimpiga mtoto
8. KT T+KH+KN alilala juu ya kitanda
9. KT Ts + T + KN alikuwa akisoma kitabu
10. KT T+KN+N+V alimpa mwanawe adhabu kali

Udhaifu wa Sarufi Muundo Kirai

r) Nadharia hii huonyesha tu uchanganuzi wa tungo za mtindo mmoja. Kwa mfano:


Rukia analima, Musa analima. Ukitizama tungo zifuatazo, zina maana moja lakini
umbo tofauti:

Rukia analima.
Analima Rukia.

Kwa kutumia nadharia hii, inatubidi tutumie kanuni tofauti kuzifafanua licha ya
kuwa zina maana moja. Uchanganuzi wa miundo virai hauonyeshi kwamba tungo
hizi zina uhusiano wowote. Zinastahili kuchanganuliwa kama tungo mbili tofauti
ilhali tungo ya pili ni muundo mbadala wa ile ya kwanza.

h) Uchanganuzi huu wa sarufi hauonyeshi ni kwa nini karibu katika lugha zote duniani
KN hujitokeza katika nafasi sawa hivi kwamba sentensi inafafanuliwa kama:

S KN + KT na wala siyo S KT + KN

j) Uchanganuzi wa sarufi hii hauwezi kueleza na kuchanganua tungo zisizo na ruwaza


ya moja kwa moja.

k) Katika uchanganuzi huu, tunaweza tu kupanua kanuni moja baada ya nyingine.


Uchanganuzi wa kiisimu hulenga katika kutumia kanuni au vipashio vichache kadri
iwezekanavyo. Mtindo wa uchanganuzi wa Sarufi Miundo Virai haulengi kufanya
hivi kwani hautumii iktisadi.

l) Inaonekana kwamba katika uchanganuzi, lazima viambajengo vifanane kwa kiasi


fulani.

38
Hitimisho

Sarufi Miundo Virai ililenga kufafanua makundi ya kisarufi kwa kuonyesha uhusiano
kati yake. Hata hivyo, nadharia hii ilishindwa kuonyesha uhusiano uliopo kati ya
sentensi mbili tofauti katika umbo la nje lakini zilizo na umbo sawa la ndani, kwa kuwa
na maana sawa. Kwa mfano katika sentensi:

14) Mwajuma alimpiga mtoto.


15) Mtoto alipigwa na Mwajuma.

Kwa mujibu wa Sarufi Miundo Virai, sentensi hizi zingechanganuliwa kila moja
ikijisimamia kwa upekee wake. Matatizo kama haya ndiyo yaliyopelekea kuasisiwa kwa
nadharia ya Sarufi Geuzamaumbo Zalishi na Chomsky mnamo mwaka wa 1957.

39
SARUFI ZALISHI

Utangulizi

Sarufi Zalishi (Generative Grammar) ilizuka kutokana na kushindwa kwa wanamiundo


kutatua matatizo ya kuchanganua lugha hususan, kushindwa kwa Sarufi Miundo Virai
kuonyesha uhusiano uliopo baina ya sentensi (relatedness of sentences). Mwasisi wake ni
Noam Chomsky, ambaye ameifafanua katika vitabu vyake: Syntactic Structures (1957) na
Aspects of the Theory of Syntax (1965). Ameandika vitabu zaidi kuiboresha nadharia hii.

Chomsky alieleza upya umuhimu wa kazi ya sarufi na pia umbo na muundo mpya
ambao sarufi ingechukua. Alipendekeza kwamba sarufi iangaliwe kama nadharia
inayoeleza jinsi lugha inavyotumika. Sarufi hiyo mpya lazima iwe chombo cha kuunda
na kuzalisha miundo ya kisarufi ya lugha inayohusika na pia ile miundo isiyo ya
kisarufi. Alipendekeza kuwa jukumu la wanaisimu liwe ni kuunda sarufi kama hii na
kuibua njia ambazo zingetumiwa kupima na kuitathmini sarufi hii. Kabla ya sarufi hii,
wanaisimu walikuwa wakikusanya data kutoka kwa wahojiwa na baadaye kubuni sarufi
ya kisayansi iliyoandikwa kwa kutalii miundo yake bila kuzingatia maana yake. Kufikia
kipindi cha sasa, aina nyingi za Sarufi Zalishi zimefafanuliwa na kuendelezwa. Sarufi
hizo ni pamoja na:

10 Sarufi Geuzamaumbo (Transformational Grammar)


11 Sarufi Geuzamaumbo Zalishi (Transformational Generative Grammar)
12 Sarufi Amilifu (Functional Grammar) inayozingatia utekelezaji (uwezo) wa sarufi.
13 Sarufi Kanuni na Kaida (Government and Binding Theory)
14 Minimalist Theory
15 Nadharia ya eksiba (X-bar Theory)

Mtindo wa Sarufi Zalishi ulioasisiwa na Chomsky umepitia mikondo tofauti na kwa


upande mwingine umeshtumiwa vikali na wanaisimu, wakisema kwamba madai yake
kuhusu sarufi hayana uhalisia au yana nguvu sana.

Sifa za Sarufi Zalishi

Kwa mujibu wa Noam Chomsky, sifa zifuatazo huibainisha Sarufi Zalishi:

o) Sarufi zalishi hunuia kueleza uwezo wa mzungumzaji wa lugha (mzawa wa lugha),


lakini sio utendaji wake. Inaeleza tungo zote zinazoweza kuzalishwa katika lugha
fulani.

p) Inachunguza na kuchanganua tungo hizi na kisha kuzitolea maelezo mwafaka.


Inatolea tungo maelezo ya kifonetiki (phonetic description) na pia maana yake.

40
e Sarufi hii hueleza sentensi ambazo ni sahihi na zile ambazo si sahihi katika lugha
inayohusika. Aidha, hueleza sentensi ambazo zina mantiki na usarufi. Sentensi hizi
hujieleza kwa uwazi kupitia sheria hivi kwamba msomaji wa sarufi hii hapaswi
kutumia makisio na ujuzi wowote kujaribu kubaini yanayoelezwa na sarufi hii.

f Sheria za Sarufi Zalishi ni kielelezo. Maagizo yake ni kama yanayopewa kompyuta.


Maagizo haya hayaelezwi wala kukisiwa kwani yanajieleza na ni ya moja kwa moja.
Kwa mfano, maagizo yanayosema kwamba sentensi inaelezwa kama:

S KN+KT

i) Kwa mujibu wa Chomsky Sarufi Zalishi inaweza kutabiri. Hailezi tu tungo ambazo
tayari zimetungwa. Inaweza kubuni kwa kutabiri tungo zote zinazowezekana
kutolewa katika lugha inayohusika, au pengine sentensi ambazo hazijawahi
kutolewa kamwe.

j) Sarufi Zalishi hujisimamia. Ina mtindo wa utaratibu mwafaka wa kuunda sentensi


ambazo si za kulazimishwa wala kusukumizwa. Sarufi ya aina hii inawezesha
uzalishaji (generativity).

Dhana za Sarufi Zalishi

Umilisi

Umilisi wa kiisimu (linguistic competence) ni ule ujuzi wa mzungumzaji asilia wa lugha


katika kuzungumza lugha yake. Kwa mjibu wa Chomsky (1957) uwezo huo umeelezwa
kama ule ujuzi wa mzungumzaji asilia wa kuweza kuimudu lugha yake. Ujuzi huo si
tokeo la kufundishwa darasani. Ni ujuzi wa kindani ambao hauelezeki wala
kudhihirishwa kimaandishi. Ujuzi huu unahusu uwezo wa kuweza kutumia lugha
inayohusika, kuielewa, kutoa na kuzua tungo, maneno, msamiati, n.k. kochokocho
kutoka lugha asilia. Chomsky anashikilia kwamba mwanasarufi ana jukumu la kujaribu
kueleza ujuzi huu, kuuelewa na kujaribu kudhihirisha sheria za lugha inayohusika ili
aweze kueleza ujuzi huo wa mzungumzaji asilia wa lugha inayohusika.

Kupitia kwa uwezo, mzungumzaji asilia wa lugha anaweza kudondoa sentensi zilizo
sahihi na zile zisizo za kisarufi. Pia, anaweza kutoa sentensi zinazowezekana kutolewa
katika lugha yake. Aidha, anaweza kutambua zile ambazo haziwezekani kutolewa, au
anaweza kutambua sentensi ambazo hajawahi kuzisikia hapo awali. Isitoshe, anaweza
kuzalisha sentensi zisizo na kipimo. Anaweza kutambua maumbo na miundo tofauti ya
tungo moja. Kwa mfano:

s) Analima Juma.
t) Juma analima.

41
Hii ni miundo tofauti ya tungo moja kwani maana ni moja, “Juma analima”. Pia mzawa
wa lugha ataweza kutambua utata wa kimuundo au wa kimaana katika sentensi.

Utendaji

Chomsky anaueleza utendaji (performance) kuwa ni yale matumizi ya lugha katika


miktadha halisi. Ni utumiaji wa ule uwezo wa kiisimu (umilisi) katika muktadha
mahususi unaomwezesha mzungumzaji asilia kubadilisha maneno na tungo na
kuzitumia vilivyo kutoka mtindo mmoja hadi mwingine. Kwa hivyo, wanaisimu
wanapaswa kutafiti umilisi kwa sababu utendaji aghalabu huwa na makosa mengi
yanayoonyesha hali halisi ya lugha na huathiriwa na uchovu, maradhi, woga, hasira, n.k.

Umbo Ndani na Umbo Nje

Dhana hizi ni za kimsingi katika uchanganuzi wa Sarufi Zalishi. Zinaeleza viwango


viwili vya sentensi vinavyojitokeza kama umbo la ndani na umbo la nje. Viwango hivi
humwezesha mwanaisimu kueleza:

i) Kwa nini sentensi mbili zinazotofautiana kijujuu (katika muundo) huwa na uhusiano
wa ndani (kimaana), kama vile katika:

Otieno alivunja kioo.


Kioo kilivunjwa na Otieno.

b) Kwa nini sentensi hizi zinazofanana zinatofautiana kindani. Tazama mfano:

Alipatikana akila rushwa. (semi)


Alipatikana akila mkate. (kitendo cha kula)

Umbo Ndani

Umbo Ndani (Deep Structure) ni muundo wa kidhahania wa sentensi. Hii ni maana


kamili ya sentensi ambayo hudhihirika kupitia muundo ndani. Katika umbo ndani,
viambajengo vyote vya sentensi vinaonyeshwa. Hii ni kwa sababu sentensi ikiwa katika
hali ya umbo ndani, hakuna ugeuzaji wowote ambao umefanyika. Ugeuzaji unaweza
kufanyiwa tungo ikiwa tu katika hali hii (ya umbo ndani). Ugeuzaji haufanyiwi umbo
nje.

Umbo ndani huwakilisha maana ya sentensi. Umbo ndani hudhirika katika umbo nje
kupitia kwa kanuni za ugeuzaji. Katika Sarufi Zalishi kuna uwezekano wa kubadili
viambajengo kutoka nafasi moja hadi nyingine. Kwa mfano:

Rukia analima. (1)


Analima Rukia. (2)

42
Tazama uhusiano uliopo kati ya kauli tendi (active) na kauli tendwa (passive) katika
tungo. Tungo katika kauli tendi huchukuliwa kuwa ya kimsingi ilihali ya kauli tendwa
imezalishwa na hiyo kauli tendi. Tazama mifano ifuatayo:

Amina aliosha gari. - Kauli tendi


Gari lilioshwa na Amina. - kauli tendwa

Umbo la sentensi katika kauli tendi ni:

S --> KN1 + T (tendi) + KN2

Kihusishi {na} kimeongezwa kupitia sheria ya ugeuzaji inayoruhusu kuongezwa kwa


vipengele.

S --> KN2 + T (tendwa) + na + KN1

Umbo Nje

Umbo Nje (Surface Structure) muundo wa sentensi unaodhihirika kihalisia kupitia kwa
sauti zinazotamkwa. Umbo Nje linadhihirika tunaposema, tunapoandika au tunaposikia.
Ni umbo ambalo tayari limepitia ugeuzaji. Ni hali ya mwisho ya tungo baada ya ugeuzi
kufanywa.

Umbo Ndani

Kanuni za Ugeuzaji
Umbo Nje

Umbo nje haliwezi kufanyiwa ugeuzaji. Dhana za umbo nje na la ndani husaidia kutatua
matatizo ya utata katika sentensi. Pia hutumiwa kuhusisha sentensi mbili ambazo
pengine zingechanganuliwa kama sentensi tofauti kabisa. Uchambuaji wa Ugeuzaji
(Transformation Analysis) hujikita kwenye wazo kwamba baadhi ya tungo katika lugha ni
za msingi (Basic Sentences) ilhali zingine zote huzalishwa kutokana na hizo za kimsingi
kwa kuptia kanuni za ugeuzi.

Sentensi za msingi ni chache na ndizo msingi wa miundo yote sentensi zinazoweza


kuzalishwa na mnenaji wa lugha inayohusika. Miundo yake huwa na sehemu mbili kuu:
KN na KT. Katika Sarufi Geuzamaumbo, kila sentensi huwa na maumbo mawili: umbo la
ndani na muundo wa umbo la nje. Ugeuzaji hufikiwa kupitia sheria tofauti za ugeuzaji
(kanuni geuzi). Kwa mfano:

Nyumba iliyokuwa imezeeka imeanguka. (Umbo Nje)

Nyumba ilikuwa imezeeka.


Nyumba ilianguka. Umbo la Ndani

43
Sheria ya ugeuzaji inaweza kutumiwa kuzalisha sentensi hii. Tazama mfano ufuatao:

[Nyumba [Nyumba ilikuwa imezeeka] ilianguka] -----------------Umbo Ndani

Ugeuzaji ---------------- (Kanuni za Ugeuzi)

[Nyumba iliyokuwa imezeeka ilianguka] -------------------Umbo Nje

Kanuni hizi zimeruhusu matumizi ya kirejeshi (-yo-). Pia, zimeruhusu udondoshaji wa


nomino moja, ambayo ilikuwa inarudiwa. Ugeuzaji wa aina zaidi ya moja unaweza
kutokea ili kufikia umbo nje.

Tanbihi: Hatuongei tukitumia umbo ndani bali umbo la nje. Zingatia mfano ufuatao:

Mitihani ilifanywa.

Sentensi hii ikichanganuliwa inakuwa:

Umbo nje -> Mitihani ilifanywa.

Ugeuzaji

Umbo ndani -> [wingi + mitihani + kiw + wkt +mzizi + kauli + kiishio]
{i} {li} {fany} {w} {a}

Hata hivyo, umbo ndani ndilo hutupa maana kamili ya tungo. Katika muundo wa ndani,
viambajengo havijabadilishwa, kudondoshwa wala kuongezwa. Umbo la nje huonyesha
tu mpangilio wa vipashio na vipengele mbalimbali vya kusintaksia kupitia sauti za lugha
zinazotuwezesha kuwasiliana kwa ujumla.

MAKALA YAMEANDALIWA NA Dkt. Stanley Adika Kevoko

44

You might also like